Asante sana Mhe. Spika kwa fursa hii. Kwa kweli tumesubiri Ripoti hii kwa muda mrefu. Siku ya leo imewadia. Kitu ambacho wananchi wa Taita Taveta wanaomba ni kwamba haki itendeke. Ripoti inataka kuwe na uchunguzi wa kubaini kama haki ilitendeka kwa wananchi wa Taita Taveta katika kila mashamba ambayo walikuwa wanagawanyiwa kuanzia shamba la Criticos ili tujue waliofaidika ni kina nani. Tunataka kujua kama waliofaidika ni wananchi ambao walikuwa hawana mashamba ama ni watu wengine. Kwa hivyo Ripoti inavyosema ni kwamba tuweze kuhakikisha ya kwamba tunajua mahali ukweli upo kwa sababu mambo ya mashamba yakiwachwa vile yako huwa yanaleta shida. Yanaleta umwagaji damu na wananchi wanaanza kukosana wenyewe kwa wenyewe. Saa zingine inaweza kuwa kila kitu kimefanyika kihalali lakini kwa sababu wananchi hawajaelezewa hawawezi wakajua mahali ukweli upo. Kwa hivyo ni vizuri kama kuna ukweli kisheria kuhusu chochote ambacho kilitendeka tuwakalishe wananchi chini ili waweze kujua sheria na haki zilitendeka wapi. Vile vile tukigusia mambo ya mashamba upande wa Mwatate katika shamba la makonge limekua na utetezi kwa miaka mingi. Kumekuwa na wananchi ambao wamelia miaka mingi kwa sababu ya kunyanyaswa wakisema ya kwamba shamba hili la huyu bwenyenye ambaye analima makonge pale ameingilia baadhi ya mashamba ya wananchi. Wamezunguka miaka mingi na ninakumbuka wako na kesi kortini hadi leo. Wamejitolea kuhakikisha ya kwamba haki imepatikana kutokana na kesi hii lakini nguvu za wananchi ni chache kuliko za aliye na pesa nyingi. Akienda kortini kuna njia anazotumia kuhakikisha haki ya wananchi haitendeki. Kulingana na Ripoti iliyosomwa mbele yetu kuna barabara ambazo zimefungwa ili wananchi wasitumie ilhali ni za umma. Kisheria and hata kikatiba hawa wananchi wa Taita Taveta upande wa Mwatate wamenyanyasika kwa miaka mingi. Hili ni jambo ambalo lazima liangaliwe. Vile vile Ripoti hii imegusia kuwa mwaka wa 1991 kulikua na wakati ambapo watu wa makonge walivamia mashamba wakakata mimea na chakula chote ambacho kilikua shambani. Huo mwaka wananchi hawakupata fidia yoyote. Ni vizuri tuangalie hiyo fidia ili wananchi walipwe kwa sababu ni haki yao. Kama walikua wamelima chakula najua mwaka huo walikaa njaa kwa sababu chakula chao kilikatwa. Vile vile lazima tuangalie katika Mwatate Settlement Scheme wapatiwe hati miliki kwa sababu wamekaa bila hati miliki kwa miaka mingi na hawajui kwamba kupata kile cheti ni utajiri wao. Hii ni kwasababu ukiambiwa una shamba lakini hauna cheti cha kuweza kumiliki basi hautakuwa na ule utajiri ambao unaweza kujivunia. Pia kuna wananchi walioumia wakati walikuwa wanapigania mashamba. Walisema kuna wale waliumizwa na wengine wakaumwa na nyoka kwa sababu mahali yale makonge yamefika ni karibu na wananchi na yanaficha nyoka mle ndani. Wananchi wengi waliumwa na nyoka na wengine wakafariki. Kwa hivyo ni vizuri kuhakikisha kuwa haki za hizi familia zimetendeka. Vile vile Mhe. Spika ulivyosema kuwe na kamati ya kuhakikisha kwamba jambo hili ambalo limetoka katika Kamati ya Mashamba limefuatiliwa kuhakikisha ukweli umetendeka na haki imefanyika kwa wananchi wa Taita Taveta. Ahsante Mhe. Spika.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunikumbuka ili nipate nafasi kuchangia Hoja hii muhimu sana. Wakicheka wanafikiria sielewi Kiswahili. Sehemu ninayowakilisha Bungeni inanibidi nijue Kiswahili kwa sababu kule ni uso wa Kenya. Kabila zote ziko hapo na mimi ndiye mkubwa wao. Sasa niko nao. Nakupongeza sana. Vile walisema ama kutaja hapo mbeleni ningetaka iwe lazima tuwe na siku fulani ambayo tunachangia kwa Kiswahili kila wiki ili watu waongee kwa lugha ya Kiswahili kwa sababu hii ni lugha ya taifa. Tena tumepata nafasi ya kugundua wale walitumia njia ya mkato kufika Bungeni. Ni sharti mtu aelewe Kiswahili na Kizungu lakini kuna watu hapa ambao hawakijui Kiswahili. Tunaanza kujiuliza jinsi walipata kuingia katika Bunge. Haya ni eno ya Kiswahili. Walipita namna gani na hawaelewi Kiswahili vizuri? Chief Whip wangu haelewi Kiswahili vizuri.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii nichangie Mswada huu muhimu. Mengi yamezungumzwa na viongozi Wabunge kuhusu suala hili ambalo ni muhimu sana. Limewaumiza Wabunge wa zai wale waliotoa huduma katika Bunge hili. Walihudumia Wakenya katika nyanja tofauti tofauti. Kama tujuavyo Mbunge akishatoka katika Bunge hili kwa njia moja au nyingine ni vigumu kuajiriwa katika shirika lolote. Hata hivyo tunashukuru korti zetu kwa kupitisha juzi ile sheria kwamba unaruhusiwa kuajiriwa au kupata kazi katika kamisheni ambazo ziko katika Jamuhuri ya Kenya hata kama mtu ni Mbunge. Hilo limesaidia kwa kiwango kikubwa. Hata hivyo jambo muhimu ni kwamba sisi ndio adui wa Wabunge kwa sababu sisi ndio tunatengeneza sheria lakini sheria hizi zinakuja kutuumiza. Hii ni kwa sababu jambo kama hili lilistahili kuwa limeshughulikiwa miaka mingi iliyopita. Lakini leo sisi ambao tumekuja katika Bunge hili la Kumi na Mbili ndio tumepata fursa ya kulishughulikia. Nawaomba Wabunge wenzangu kwa sababu kama tulivyoambiwa ukiona mwenzako amenyolewa tia kichwa chako maji. Kwa hivyo na sisi siku moja tutakuwa Wabunge wa zai. Tutaitwa Wabune wa zai pale nje. Tunavyojua Mbung ni kama askari mwalimu na daktari. Ukishakuwa Mbunge wewe ni Mbunge mpaka siku utakapotiwa kaburini. Majukumu hayakukimbii. Majukumu yanabaki palepale. Utakuwa unaalikwa na wakazi uliowahudumia kule mashinani na nyanjani kila wakati. Wao wanakutambua kama kiongozi: kukiwa na mazishi utaalikwa; kukiwa na mchango wa kanisa utaalikwa; kukiwa na mchango wa mambo ya masomo utaalikwa. Wale waliokupigia kura au uliowahudumia hawajui kama wewe huna uwezo kama uliokuwa nao wakati ulipokua Mbunge. Kwa hivyo wanatazamia kila wakati unapohitajika utafika pale kuwahudumia. Hesabu imefanywa hapa. Tumeambiwa Wabunge wa zai ni kama 200. Ikiwa kila Mbunge atapewa shilingi 100000 kwa mwezi ni shilingi 20000000 kwa mwaka mmoja. Hizi ni pesa kidogo sana tukiangalia hali ya jinamizi la corruption ambalo linaendelea katika Jamuhuri ya Kenya. Pesa nyingi sana zimeibwa; pesa nyingi sana zinaliwa kila siku. Ikiwa pesa hizi zitatengwa kuwahudumia Wabunge wa zai zitawasaidia katika njia moja au nyingine. Tumekuwa na Wabunge wengi ambao wamepitia pale ninakotoka katika eneo la Kisauni. Wengi wamehudumu muhula mmoja. Wengi wako kule nyanjani. Kuna Mbunge ambaye ilifikia wakati hawezi kulipa kodi yake ya mwezi na ikawa ni aibu alipokuwa anatolewa na mwenye nyumba alimokuwa anaishi. Haya ni mambo ambayo ni lazima tuyahudumie. Nawaomba Wabunge wenzangu tuipitishe hii Hoja ambayo imeletwa mbele yetu kwa kishindo kikubwa. Hii Hoja si kuhusu wewe. Hoja hii si kuhusu yule Mbunge wa zai. Hoja hii ni ya kuendelea kwa sababu sisi tutaondoka kesho na watakuja Wabunge wengine. Ni muhimu Wabunge wale waweze kuishi maisha mazuri watakapotoka katika Bunge hili wakati Mwenyezi Mungu atawajalia kwenda pale nje. Kwa hivyo naunga Hoja hii mkono kikamilifu.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii ya kuchangia Hoja hii muhimu. Nimesimama kupinga Hoja hii kwa sababu ukiangalia mataifa jirani kama Uganda na Rwanda hayana muda maalum wa viongozi wa mataifa hayo kuhudumu. Sisi tuna miaka mitano maalum lakini wao hawana. Ni hatari sana kuungana nao kijeshi ama kiusalama. Wanaweza kutuambukiza ugonjwa huo huku kwetu. Ukiangalia viongozi wa upinzani katika mataifa hayo wanaishi jela na wengine kupoteza maisha yao. Hapa kwetu tuna demokrasia. Ni vyema tuungane na wao kiuchumi lakini tusiungane nao kiusalama. Kwa hivyo mimi nimesimama hapa kupinga Hoja hii kwa sababu taifa letu lina demokrasia. Sitaki kuona mataifa mengine yakiingilia kwetu ili tufuate mfumo wao. Je ikiwa tumeungana nao katika usalama na kuwe na matatizo hapa wakati wa uchaguzi hilo jeshi ambalo litakuwako litatumika kuja kuharibu kabisa taifa letu ambalo ni zuri huru na liko na ai? Kwa hivyo nimesimama kupinga Hoja hili. Naomba Wabunge wenzangu watafakari kwa makini jambo hili kabla ya kulipitisha.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii. Kulingana na ratiba ya Bunge baada ya kuchaguliwa ratiba iko sambamba. Ni bayana kwamba tunapokuja Bunge kuna masharti yake. Mhe. Jirani wangu Wamalwa ambaye namuombea Mungu miaka ijayo sijui kama atakuwa gavana wangu ana tajriba yake ndani ya Bunge. Kuhusu hoja ya nidhamu
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii. Kwanza nasimama kupinga uteuzi huu kwa sababu zifuatazo: Kenya si taifa changa kwa sababu lina miaka 57. Ni mtazamo wa sisi sote ambao tuko katika nchi hii ya kuwa ni lazima tujue kuwa sisi ni Wakenya na usawa tunaozungumza kwenye mikutano yetu ya BBI uko dhahiri. Ukiangalia haya majina ikiwa tuna makabila 43 katika nchi yetu ya Kenya na uone majina ya sehemu moja ni mengi ilhali sehemu nyingine hazipo kabisa je ni kwa nini tuunge mkono uteuzi huu? Sioni muislamu hata mmoja kwenye uteuzi huu ilhali tuna karibu asilimia 40 ya waislamu. Tunazungumzia kuhusu watu kushirikiana na kutangaa lakini leo mabalozi 14 wanachaguliwa na hakuna hata muislamu mmoja. Ninashangaa sana kwa nini wenzangu wanaunga uteuzi huu mkono. Tunaunga nini mkono? Tuna Wahindi Waarabu na makabila tofauti kwa nini hawako hapa? Sisi sote ni Wakenya. Ni wakati tunataka kuona kuwa katika uteuzi wa aina yeyote Wahindi Waarabu na makabila mengine yanatambuliwa ili watu wote wajisikie na kujivunia kuwa Wakenya. Tunavyozungumza tunajiona sisi ni wageni hatuna haki na hakuna usawa katika hii nchi. Nitakukumbusha tu siku za Hayati Moi ambapo baada ya uchaguzi tulikuwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ardhi kutoka Pwani lakini hayo hayafanyiki hivi leo. Tunapewa tu nafasi moja ya Wizara ya Utalii na ni kwa mtu ambaye hana uhusiano na watu; ni yeye peke yake na Baraza la Mawaziri. Nawaomba Wajumbe wenzangu kuipinga Ripoti hii. Mhe. Spika Mombasa ni kitovu cha Taifa letu na hakuna jambo litafanyika bila kuihusisha na kuunga mkono lakini leo hii tunatumiwa tu. Hatufaidi hata kwenye uteuzi kwenye mashirika yaliyo Mombasa. Hivi majuzi Katibu Mkuu ambaye amelelewa Mombasa alikuja na kututusi kuwa watu wa Pwani hawapati kazi kwa sababu hawajui Kiingereza. Ni nani alikwambia Kiingereza tu ndio lugha ya kufanyia kazi? Wachina hii leo wanajenga mabarara ilhali hawajui Kiingereza. Hivi majuzi uteuzi wa Mkurugenzi wa Kenya Maritime Authority ulifanyika na kijana kutoka Mombasa ambaye ni wakili akaachwa.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii. Nina Mswada ambao nimeushughulikia kwa muda wa miaka mitatu na hadi sasa haujaisha. Ni jambo la busara kwa Kamati husika na Wabunge wote kuhakikisha kwamba kazi iliyofanyika kwa miaka mitatu haitapotea. Kama unavyojua Mswada wangu umekuwa hapa na ni vyema ikiwa utahifadhiwa mpaka upitishwe na Bunge hili kuwa sheria ili uweze kuwanufaisha watu wa Matuga na Wakenya wote kwa jumla. Asante sana na naunga mkono pendekezo hili.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipa fursa nitoe mchango wangu. Moja kwa moja nakupa kongole kwa kuwa wa kwanza kuleta tafi ambazo zitakuwa njema zaidi katika Bunge letu. Kwa miaka mingi kutoka mwaka wa 1974 ambapo Bunge hili lilianza kutumia lugha ya Kiswahili rasmi Kanuni za Bunge zingali katika lugha ya Kiingereza. Kupitia kwako wema wako na Kamati ambayo unaongoza na mimi ni mmoja wa Wabunge tumeweza kuleta tafi za Kanuni za Kudumu za Bunge hili. Hii imetupa historia nzuri zaidi. Najua itakuwa changamoto kuu lakini naomba tutafute mikakati ili tuwe na tafi ya Kanuni za Kudumu za Bunge kwa Kiswahili.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii ili nichangia Hoja hii. Ijapokuwa taarifa ya Kamati iko sawa nina wasiwasi moyoni mwangu. Hii ni kwa sababu wahenga walinena: "Pema usijapo pema ukipema si pema tena." Mhe. Spika ikiwa wataka kumpiga risasi mwizi kwanza hutamlenga kichwani. Utapiga risasi juu akishtuka ndipo umlenge kichwani. Wasiwasi yangu ni kwamba tunaweza kuitumia ripoti hii kutoa ama kufungua mlango wa wale wanyanyasaji na wanyakuzi wa mashamba wakaweza kuiingia ndani. Huo ndio wasiwasi wangu. Mhe. Spika kufikia hivi sasa kazi inaendelea kuteleza kwa binadamu. Kufanya kosa si kosa kurudia kosa ndio kosa. Mhe. Spika kazi inayoendelea kwa wakati huu ni kazi ambayo inaridhisha. Wengi wetu tulikuwa hatujajua rangi ya cheti cha kumiliki shamba. Lakini imefikia wakati yale mashamba ambayo yalikuwa yamekaliwa miaka na miaka kupatiwa wenyewe. Kuna wengine hapa Kibera tu. Kulikuwa na shamba la Wanubi ambalo limekaa miaka na miaka. Kila mwaka lakatwa kipande mpaka sasa limebakia ekari 400. Nakumbuka siku moja Waziri alikuja akatuambia kwamba atafanya juu chini kuhakikisha kwamba Wanubi wanapata ardhi hiyo hata kama itabidi kuuma risasi. Hiyo ni ishara ya kwamba alikuwa amejitolea kufanya kazi kisawa sawa ili kwamba mambo yaweze kuwa mazuri kwa wale Wakenya wanyonge zaidi. Mhe. Spika pale alipoingia katika jengo la Ardhi House ni shimo la tewa. Unaweza ukatafuta hati ya kumiliki ardhi miaka na miaka. Lakini mwenye hela akiingia pale kwa wiki moja atatoka na hati ya kumiliki ardhi. Hiyo ndio kazi huyu mama amejitolea kufanya na kulisafisha lile jumba. Lakini hilo halionekani. Mhe. Spika tusipokuwa waangalifu tutaiangamiza nchi hii. Kwa hakika twendeni mbele tukiangalia tunapotoka. Wengi wamekalia Wizara hiyo lakini hatujaona ufaa ila wakati huu. Si kwamba napinga ripoti hii la hasha! Nina heshima na naipa sifa zote kamati inayosimamia mambo ya ardhi kwa kufanya kazi yake vizuri. Ikiwa lengo la kupitisha ripoti hii ni kumwondoa Waziri huyu ninaapa hapa kwamba sitakuwa pamoja na huyo atakayeleta Mswada wa kumwondoa. Kwa ndani watu wanacheka na kufurahia kwa sababu wanajua wamemshika Waziri. Tutayafanya yote hayo lakini ikiwa ni ya kugandamiza wanyonge hatutakuwa pamoja hata kidogo. Kwa hakika yote na yawe. Ijapokuwa sina tashwishi na ripoti hii lakini litakuwa jambo nadra kuiunga mkono. Asante mhe. Spika.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii kuchangia Hoja hii. Kwanza mimi pia naungana na wenzangu kukupa pongezi nyingi sana kwa namna ambavyo umetuelekeza katika Bunge hili. Haikuwa rahisi. Kama vile ndugu yangu Mhe. Mwanyoha alivyosema Bunge hili liko na wanaume. Vile vile naongezea sisi kule Pwani twasema liko na nyangumi na papa ambao wanaweza kutafuna mtu akifanya mchezo. Kwa hivyo tunashukuru kuona kuwa mawimbi yale umeweza kuenda nayo na kutupeleka kwa njia ya sawasawa. Pili nakupongeza kwa busara yako. Nimekuja ofisini kwako mara kwa mara nikitaka kufafanuliwa vipengele vya sheria na umenieleza namna ya kufanya kazi ambayo nimepewa na watu wangu katika Bunge hili. Vile vile nimesikia wenzangu wakisema ulikuwa unalinda mayatima. Lakini kati ya wale mayatima unaowalinda nataka kuzungumza kama Naibu Katibu Mtendaji wa chama cha Wiper Democratic Movement of Kenya - ndungu yetu Mhe. Munuve hajakuwa yatima. Yatima ni yule ambaye amefiwa na baba na mama. Baba Kalonzo bado yuko na analinda watoto wake. Mhe. Munuve ni mtoto mpotevu sio mtoto ambaye ameachwa na baba. Ni lazima tuhakikishe sheria tunazounda zitafaa wananchi wetu ambao wametutuma hapa kuwawakilisha. Shida za Wakenya nyingi sana ni umasikini ukosefu wa elimu na ajira. Ndio maana ikifika wakati wa uchaguzi tunaona fujo nyingi zinatokea na watu kutumiwa. Asilimia kubwa ya wananchi wetu wangelikuwa na ajira na elimu ya kutosha hawangeliweza kupelekwa kwa njia ambayo sio sawasawa. Kwa hivyo ni wakati wa Serikali kuweka mikakati muafaka ambayo itahakikisha kuwa watoto wetu na jamii zetu wanaweza kusoma na kuwapatia ajira kwa wingi. Nimesikia Mbunge mwenzangu akizumgumza kuhusu kufurahishwa na vile uhusiano umeimarika kati ya Turkana na Pokot na akasema kuwa atachukua fursa hii kuona kuwa wakirudi pale nyumbani watashikana ili wazungumze na wananchi wao. Sisi kule Pwani ambapo matatizo kama haya hayajatupata sana kama Wabunge marafiki watataka kuzungumza na ndugu zao pale tuko tayari kujitolea pia ili kuzungumza na jamii ili sote tushikane tuonyeshane ile ishara ya udugu. Tuonyeshe kuwa tunaweza toka hapa na kuhubiri ai katika sehemu mbalimbali za nchi hii. Natoa pongezi nyingi sana kwetu kwa kupitisha ule Mswada wa riba ya mikopo ya benki. Pia ningependa kukushukuru sana kwa sababu wakati wa kujadili Mswada huo nilipata nafasi ya kuchangia. Kabla Mswada huo kupitishwa watu waliishi katika hali ya ate ate na maisha yakawa segemnege. Kama halingepitishwa basi maisha ya watu yangelikuwa ni hali Waswahili wanasema kiriba na kiriba goji'. Yaani ni pale pale ambapo sisi tunarudi. Mhe. Spika nafikiri tulifanya kazi nzuri sana. Tunakupongeza kwa kuongoza mijadala yetu na kuhakikisha kwamba tumepitisha sheria kwa njia nzuri ambayo itawafurahisha Wakenya. Mwisho nawatakia wabunge wenzangu likizo njema. Tushikane mikono pamoja. Mungu atujalie turudi Bunge tena na tufanye kazi kama ndugu ili tuwasaidie wananchi waliotuchagua.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii pia nichangia Hoja hii. Ninaungana na wenzangu kukupatia kongole kwa kuturuhusu kujadiliana Hoja katika Bunge hili letu. Ninataka kusema Kiswahili katika nchi yetu ya Kenya kilianzia mbali kwa sababu mahali penye nimezaliwa tulikuwa na makabila mengi sana na haikuwa rahisi kuwasiliana na wengine ndiposa tukapata wasomi waliokuja hapo katikati wakatufanya tukifahamu Kiswahili na tukaanza kuongea na wengine. Wengi wamesema kwamba sio rahisi. Ni kweli Kiswahili sio rahisi. Lakini kwa wale wamejitolea kama wenzetu katika kamati hii kwa kutafi Hoja hii wamefanya jambo nzuri sana. Katika michezo ya Afrika Mashariki inawachukua Waganda muda mrefu sana kuwasiliana na Wakenya ama Watanzania kwa lugha ya Kiswahili. Itakuwa vyema sisi tukijifunza katika Bunge letu kuongea lugha ya Kiswahili kwa sababu wananchi wanatuelewa kwa ufaa ya Bunge letu. Mhe. Millie amesema kwamba tujifunze Kiswahili na tulete Sheng . Hatutaongea Sheng na Kiswahili. Tukifanya hivyo tutakuwa tunachanganya wananchi kwa sababu kama tunaenda kujifunza Kiswahili katika Bunge letu ni vizujri kiwe Kiswahili sanifu ili tuwasaidie wananfunzi. Tunaenda kwa kongao nyingi na ni vizuri tuwe tunajua kuongea Kiswahili kimombo au lugha ya ishara. Itatuwezesha kuwasiliana na watu vizuri. Ukikuja kule Trans Nzoia kwa sababu ya makabila megi tunatumia Kiswahili. Nikimalizia ninamshukuru Naibu wako kwa sababu anatupa ufahamu. Mheshimiwa Chris Wamalwa ameongea kuhusu matunda lakini tunaidhinisha Kanuni hizi za kutusaidia katika Bunge letu ili tuweze kutafsri kwa lugha ya Kiswahili. Ninakushuru Mhe. Spika. Asante sana. Mimi pamoja na Wakenya wote na watu kutoka Trans Nzoia County tunakupa kongole. Ubarikiwe sana.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii. Naanza kwa kuunga mkono Hoja hii. Kama mmoja wa wanakamati wa Kamati ya Bajeti naipongeza Kamati hii ikiongozwa na Mhe. Ichung'wah kwa sababu tunapitia nyakati ngumu na tumefanya bajeti hii kwa mazingira ambayo ni magumu sana. Pia nashukuru Wenyeviti wa Kamati zote za Bunge ambazo zilikuja mbele yetu zikatukabidhi mapendekezo yao. Ulikuwa wakati mgumu lakini tunashukuru kwa sababu tumefika. Nyakati tunazopitia kama nchi ni ngumu. Dunia nzima inapambana na kirusi ambacho vile wengine wamesema hatuwezi kukitambua. Kimekuja tuko nacho na hatujui kitaondoka lini. Wakati wa kufanya bajeti ilitubidi tuangalie kwa makini mapendekezo yaliyotoka katika Hazina kuu ya Kitaifa. Mara ya kwanza tulipoletewa makadirio na Hazina kuu ya Kitaifa tuliketi tukakataa mapendekezo yao maanake hawakuwa wameangazia mambo ya kuinua uchumi tena baada ya COVID-19 na hawakuwa wameangazia pesa ambazo zinatakikana ziende kwa idara ya afya ya kuinua hospitali zetu na kuona kwamba tuko tayari kama nchi kupigana na janga la Corona. Tulipokataa mapendekezo yao ya kwanza ilikuwa ni fursa nzuri kwenda kuketi na kutathmini yale tuliyoyapendekeza. Kwa mfano tulitaka kujua ndani ya bajeti hii ya kiwango cha Kshs2.7 trilioni ni pesa ngapi zingeenda kupigana na janga hili. Waliporudi walikuja na Kshs53 bilioni wakatuambia wamezipanga kulingana na vile tuliona inastahili. Mojawapo ya mambo waliyoyasema ni kuwa kuna pesa walitenga kwa kazi mitaani. Ni tumaini la wengi kama Wabunge kazi hizi ziende kwa vijana wetu ambao hawana ajira na zifanywe sawa kwa nchi nzima. Mara ya kwanza ilikuwa ziende kwa miji mikuu. Lakini tunavyojua hakuna mahali nchini hakujapata shida hii. Kwa hivyo tunatazamia kwamba kazi mitaani zitaenda kila eneo la wakilishi Bunge ili vijana wetu wapate ajira. Jambo lingine ningetaka kusema sana na ambalo ningetaka liingie katika datari za Bunge ni kuwa raslimali za Kenya mara nyingi zinalenga maeneo fulani. Bajeti hii ina pesa nyingi ambazo zimekadiriwa. Lakini tukiangalia miradi ambayo imewekwa na imetiliwa maanani kuna sehemu fulani zinapata mgao mkubwa. Kwa mfano katika sekta ya barabara mwaka huu nilidhani kwamba maeneo ambayo hayana barabara za lami yangewekwa ndani ya bajeti hii. Aya 16 imetaja Wundanyi kama mojawapo ya maeneo Bunge ambayo hayana barabara ya lami. Kwa sababu ya COVID-19 nilikubali kuwa mwaka huu tutakosa lami. Lakini naomba Bunge hili litilie maanani sehemu ambazo zimebaki nyuma sana kimaendeleo sana sana katika miundomisingi ya barabara. Jambo ambalo lilinitia kiwewe sana ni kwamba mwaka huu pia nilitarajia mradi wa Mzima II utatengewa pesa. Lakini Waziri alinihakikishia kwamba kwa wiki mbili zijazo kuna makubaliano yanayoendelea kati ya Wizara na wafadhili kutoka China na kwamba mradi huo utapata ufadhili. Haya ni mambo mazito. Wacha kila sehemu ya Kenya ipate kuwa sawa na nyingine ili kila Mkenya ambaye analipa kodi ajihisi kuwa anafaidika kutoka kwa kodi. Namaliza kwa kusema kwamba ni lazima miundomisingi ya afya izidi kutiliwa mkazo.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia fursa hii ili niunge mkono kutoa rambirambi. Kwa niaba yangu familia yangu wananchi wa Lungalunga na Kaunti ya Kwale ninatoa rambirambi zangu. Ninamkumbuka Mhe. marehemu Rais Moi wakati alipokuwa akija Mombasa ama Pwani. Nilikuwa mmoja wa wale walikuwa wakimwimbia kwa vigelegele. Kila wakati tulipokuwa tukimwimbia alikuwa lazima aache mambo mazuri nyuma. Kusema kweli tumeachwa na pengo. Mwenyezi Mungu amrehemu na afadhili familia iliyobaki nyuma. Asante sana.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia fursa hii ili niweze kuongea juu ya mwandishi mkuu wa vyama vya kisiasa hapa nchini. Kwanza nimefurahi kwa sababu Mhe. Rais ametuletea majina hapa. Alikuwa ameleta majina mawili ya wanawake na mawili ya wamaume. Hivyo nampongeza sana Mhe. Rais kwa kuwa aliona kuwe na usawa katika ugawaji wa kazi hii ambayo iko katika afisi ya watu wanne. Mhe. Spika tuko katikati ya maswala ya jinsia na nataka kumpogeza Rais kwa kufanya huo uamuzi. Kwa ufupi ningependa kusema katika hao wote wane Ann Nderitu na Florence Birya ni akina dada ambao nawafahamu. Nafahamu kazi zao na kwa muda mrefu niko na ii kuwa wataweza kazi hii. Kulingana na kubobea kwa kazi ya Ann Nderitu ni sawa amepatiwa kuwa mwandishi mkuu wa kusimamia vyama vya kisiasa hapa nchini. Florence Birya pia namfahamu na najua anaweza kazi na bila shaka atafanya kazi nzuri. Kwa uchache tu ningependa kuzungumzia juu ya kijana huyu. Kusema kweli nafikiria Mhe. Rais alikuwa ameamua kupeana kazi kwa mlemavu na pia awe kijana. Ningependa kusema kuwa kijana huyu ambaye ni mlemavu Mhe. Rais alimchagua kwa nia safi. Isipokua ukiangalia sheria vile ilivyo ni kuwa hakutoshea na hakubobea kuwa kwenye nafasi hiyo. Kuna umuhimu kuwa kijana huanza kwa kutambaa ndio aweze kukimbia. Mimi ningependelea kama walemavu na jamii ndogo kama Wakuria pia wangepatiwa nafasi. Hii ni kwa sababu ni haki yao kupatiwa nafasi. Lakini isiwe mtu anapewa kazi kama hajafanya kazi kwa muda unaofaa ama mrefu. Pia kwa umri wake kazi kama hii ni nzito si nyepesi. Nakubaliana na taarifa hii iliyotolewa na kamati hii kuwa hawa watatu wapatiwe kazi na huyu mmoja anzishwe kutambaa kwanza kabla hajafika kwenye kazi ya afisi kubwa kama hii. Natoa shukran kwa kamati kwa kazi waliofanya. Nikimalizia ni kumrudishia Mhe. Rais shukran kuwa ametupatia nafasi mbili kwa akina mama kati ya nafasi nne. Hili ni jambo limenifurahisha. Saa hizi ni nafasi mbili kati ya nafasi tatu. Hivyo basi thuluthi mbili zimeangaliwa na Mhe. Rais. Asante sana.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia fursa hii nichangia Hotuba ya Rais. Kwanza ninawapongeza wanajeshi wetu wa Kenya ambao wako Somalia wakifanya kazi na kuona kuwa nchi hiyo imetulia kama nchi yetu ya Kenya. Kabla ya kuchangia yale ambayo Rais alisema juzi ningependa kurudi nyuma kidogo katika hotuba ambayo aliitoa mwaka jana akisema kuwa ataweka Kshs10 bilioni kuwalipa watu ambao walifanyiwa dhuluma za kihistoria. Ninakumbuka mwaka huo tulichangia Hotuba ya Rais na tukasema kuwa jambo hilo halitawezekana. Nilipata fursa ya kuzungumza na kusema kuwa badala ya kuweka Kshs10 bilioni kwa watu ambao wamedhulumiwa kihistoria afadhali pesa hizo zingewekewa mabalozi wetu ambao wako kule mitaani wakifanya kazi ngumu. Mabalozi hawakupata kitu na pia wale waliopata dhuluma za kihistoria hawakupata kitu. Katika Hotuba yake Rais amezungumzia kuhusu mradi mkubwa wa Standard Gauge Railway. Mradi huu unapita katika eneo langu la Miritini. Miradi hii lazima ije na faida. Faida kubwa inapaswa kumgusa yule mwananchi ambaye yuko pale chini. Katika eneo la Maganda ambapo mradi huo unapita kuna mtu anaitwa Mzee Sombo ambaye mpaka sasa hajalipwa pesa zake. Pia Salim Said katika eneo la Maganda hajalipwa pesa zake mpaka sasa. Watu ambao wanalipwa kutokana na mradi huu wanapigiwa hesabu ya nyumba lakini hawapigiwi hesabu ya ardhi. Kama ilivyozungumzwa na Rais mradi huu utaleta faida lakini wakazi hawajaona faida yake katika makazi ambayo wananchi wanaishi. Watu hawa wamekuwa wakiishi pale wakijua kuwa kuja kwa mradi huu kutawasaidia. Kwa hivyo tunataka tuangalie mambo kama haya. Serikali ya Kenya inapaswa kujua kuwa watu ambao walikuwa wanaishi pale miaka yote ni wananchi ambao lazima maslahi yao yaangaliwe ili waishi maisha mazuri zaidi kushinda yale ambayo walikuwa wanaishi mwanzo. Katika mradi wa LAPSSET imezungumzwa kwamba Berth 1 2 na 3 zimetengenezwa. Katika Bandari ya Mombasa Berth 19 pia imetengenezwa. Rais aliongea mambo yaya haya mwaka jana na mwaka huu pia amezungumza zaidi. Mpango mzima wa ajira kwa watoto na watu wetu katika sehemu hizo za Bandari bado haujazungumziwa. Tukiangalia zaidi Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Kenya Ports Authority (KPA) Catherine Muturi yuko pale mpaka saa hii lakini hajathibitishwa kamili kama Mkurugenzi Mkuu wa Bandari zetu. Hatuwezi kama binadamu ama viongozi kuzungumza yote mabaya. Kama Upinzani yale mabaya tutasema ni mabaya na yale mazuri tutasema ni mazuri. Ninapongeza Serikali hii kwa kuweka stima katika shule nyingi hapa nchini. Kwa mfano kule Mombasa ninakotoka kuna taa za barabarani katika maeneo mengi na uhalifu umeshuka chini. Hili tumeliona ni jambo nzuri. Ni muhimi tupongeze Serikali kwa jambo kama hili. Hatuwezi kupinga kila kitu. La mwisho kabisa mabenki yanaanguka. Ni lazima Serikali hii iangalie vile Imperial Bank Dubai Bank na Chase Bank zilivyoanguka. Wananchi wadogo wadogo wanaofanya kazi na kuweka pesa zao pale sasa hawana faida ya kuendelea mbele katika maisha yao kwa sababu wanatarajia kupata mikopo. Kwa hayo machache ninakushukuru Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii kuchangia Hotuba ya Rais. Asante sana.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia fursa hii niungane na wenzangu. Kwa niaba yangu na kwa niaba ya wananchi wote wa Jomvu ningependa kutoa rambirambi zangu kwa wakaazi wa Kibra na Kaunti ya Bomet kwa kuwapoteza viongozi wao. Nataka kuzungumza juu ya Mhe. Ken Okoth ambaye alikuwa mtu mzuri sana. Binafsi nilifanya kazi naye katika Bunge la 11. Mhe. Ken Okoth alikuja Jomvu kufungua madarasa huko Bangaladesh Mikindani. Kwa hivyo alikuwa rafiki mzuri. Mimi ni mwanakamati wa Bajeti. Miezi miwili iliyopita tulienda kushirikisha umma katika masuala ya Bajeti kule Bomet. Nilikuwa na mwenzangu Mhe. Nyamita. Marehemu Mhe. Laboso alikuwa amekwenda hospitali. Tuliomba Mungu tukijua atampa uhai. Ingawa haya yametukia tunasema ni kazi ya Mungu ambayo haina makosa. Kwa niaba yangu familia yangu na wananchi wa Jomvu natoa rambirambi kwa wananchi wa Bomet na Kibra. Naomba Serikali ya Kenya itangaze saratani kuwa janga la kitaifa. Aidha ni muhimu tuwe na hospitali za kupima saratani katika kila kaunti nchini. Nachukua nafasi hii kukushukuru Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii kutoa rambimbi zangu kwa familia za ndugu zetu ambao wametuacha. Asante na Mwenyezi Mungu atubariki.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia fursa hii ya kuongeza sauti yangu katika kuunga mkono huu mpango wa kuidhinisha fursa ya lugha ya Kiswahili katika Bunge hili. Hii ni fursa ambayo tumeingoja kwa muda mrefu. Hayati Mzee Jomo Kenyatta ambaye alikuwa Rais wa Kwanza wa Kenya; hayati Kwame Nkrumah hayati Julius Nyerere na viongozi wengine wa Afrika waliunga mkono Kiswahili kiwe lugha ya Afrika. Ni lugha ambayo ilizaliwa katika Bara la Afrika. Ni fursa muhimu sana tukijadiliana katika Bunge la Taifa kwa lugha ya Kiswahili. Kwa hakika Hoja hii itabadilisha mambo mengi. Wananchi wa Kenya wanazungumza kwa lugha ya Kiswahili. Tukitumia Kiswahili wataelewa ni mipango gani tunafanya katika Bunge kila siku. Kwa hivyo itakuwa ni fursa nzuri sana kwa Wakenya wote wakisikia kila neno ambalo linasemwa Bungeni linasikika kila mahali. Kila Mkenya ataelewa kabisa. Kwa hayo machache ninaunga mkono Hoja hii.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia fursa hii. Kwa niaba yangu na watu wa Eneo Bunge la Kisauni ninachukua fursa hii kutoa rambirambi zangu kwa hayati Mzee Moi. Tunasema pole kwa familia. Asante.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia hii fursa. Nawakilisha watu wa Garsen. Kwa maoni yao kitu cha kwanza kule Garsen kuna shida ya stima. Naona bajeti ya stima imeondolewa yote. Kitu kingine ni mambo ya Equalisation Fund ambayo iko katika Katiba ya Kenya. Inafaidi watu wa sehemu kame. Inaoneka ni kama imeondolewa. Kama watu wa sehemu kame tunafaidika kutokana na Equalisation Fund pamoja na stima na Hazina ya Kitaifa ya Maendeleo ya Maeneo Bunge (NG-CDF). Ukienda shule katika maeneo wakilishi Bunge yote Kenya NG-CDF ndio inajenga shule na kambi za machifu na vituo vya polisi. Hiyo yote imeondolewa. Imepunguzwa kumaanisha pesa zimeondolewa. Mhe. Spika pia mawaziri wako na magari ya msafara. Sijui wamechaguliwa na nani ama wako na maadui wa aina gani ndio inawalazimu kutembea na magari kwa msafara. Kwa hivyo napinga Bajeti hii vile imewasilishwa kwa ajili tunataka stima na Equalisation Fund kwa sehemu zetu kame. Ahsante sana Mhe. Spika.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia hii nafasi ili nami niweze kuchangia hii Hoja kwa kupitisha Ripoti ya Kamati ya Uteuzi. Kwanza ninaunga mkono tupitishe hii Ripoti. Pili ninaomba tusibadilishe hata koma bali tuipitishe tu vile ilivyo. Mhe. Spika ukiangalia historia ya nchi ya Kenya mipaka yake ilikuwa na usalama na imara zaidi wakati Waziri wa Mambo ya Usalama wa Nchi za Nje Mhe. Njenga Karume alikuwa kwenye usukani. Wapo wale wanaosema kuwa masomo ya Mhe. Njenga Karume alipata kwa kukaa na wasomi tofauti kwa sababu sio lazima uende shuleni ili upate masomo ama tajriba ya kuendesha mipango nyingi ya Serikali. Unaweza kukaa na daktari na uanze kufikiria kama daktari na pengine huenda ukapata ujuzi wake. Unaweza kukaa na mawakili na uwe na ujuzi wa kuelewa sheria za barabara na sheria zingine tofauti zilizoko katika nchi ya Kenya. Kwa hivyo ninaunga mkono hayo majina. Ningeomba wapewe nafasi ili waendeshe shughuli zao kama Mawaziri. Vile vile ningependa kushukuru Kamati ya Uteuzi ambayo iliwapiga msasa. Ni Kamati ambayo ilikuwa na watu wenye tajriba tofauti. Wapo wale waliohusika na kutengeneza sera za Serikali ya Jubilee kwa nyanja tofauti na walikuwa wanawahoji wale kutaka kujua kama wanaelewa ama hawaelewi mipango ya Serikali. Wapo Wakenya wengi sana ambao hivi sasa wanaishi na matumaini kwa kufuatia uteuzi wa Rashid Echesa Muhamed kwa sababu wanafikiria kwamba hata kama unatoka katika familia maskini ama isiyojiweza familia ambayo wazazi wako hawajulikani angalau tu na chifu wa eneo lako ama mtaa ambao nyinyi mnatoka unaweza kuwa Rais Waziri wa nchi ama mtu ambaye utakuwa na umaarufu zaidi na kujenga jina hilo. Ningependa kuambia marafiki zangu wa mrengo wa Upinzani kuwa sasa hivi kuna mwamko mpya katika nchi ya Kenya kwa sababu vijana wale hawakuwa wanajulikana kwa jina wameweza kufika hata wameweza kuwa Mawaziri. Wale watu ambao familia zao hazijulikani kabisa kunaye mmoja ameweza kuwa Naibu wa Rais wa nchi ya Kenya kama Mhe. William Ruto. Ninafikiri utuezi wa Rashid Echesa Muhamed umeleta mwanga unaoashiria kuwa Kenya lazima ijitayirishe. Mwaka wa 2022 tuwe tayari kuongozwa na Mkenya mwingine kijana ambaye amekuwa akiuza mayai kwa jina la William Samoei Ruto kama Rais wa Kenya. Kwa hivi sasa kila sehemu ya nchi ya Kenya inasubiri kuanza kuona utendakazi kwa hao wanawake na wanaume ambao wameteuliwa kama Mawaziri. Nasi kama Bunge lazima tuwape nafasi kwa sababu Rais anayeongoza Serikali katika nchi ya Kenya ni Uhuru Kenyatta. Yeye anajua nani anafaa kumsaidia ili atimize ndoto yake ama ahadi yake ambayo alipea Wakenya. Kwa hivyo ningependa ndugu zangu wa mrengo wa Upinzani watulie. Kuna wengi wa mrengo wa Upinzani ambao wake zao hawajafika hata kidato cha tatu ama darasa la nane lakini walilipa mahari na wanaishi sawasawa. Hata ukiangalia uongozi wa Upinzani wenyewe utakuta kwamba Naibu wa Kiranja wa Bunge wa Chama cha Wachache Mhe. Chris Wamalwa ni msomi maarufu maana alienda shule ya Havard na pia ako na uzamifu. Mkubwa wake kwa upande mwingine masomo yake nimeangalia hajafika darasa la tatu lakini yeye ni mkubwa. Kwa hivyo hao ndio walioanza mfano mzuri kwamba sio masomo ya darasa inayopeleka watu mbele bali ni masomo ambayo unajifundisha kila siku na hiyo ndio ya muhimu sana. Mhe. Spika ninaunga mkono hii Hoja na ningependa kukomea hapo. Asante sana.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia hii nafasi ili niunge mkono Ombi la Lentoimaga. Kuna maana ya Mhe. Lentoimaga kuandika Ombi hili. Nafikiri tuko na shida kubwa sana kuhusu haya mambo ya wizi wa mifugo. Sijui kwa nini inaitwa wizi wa mifugo ilhali ni kitu inaua wananchi katika pembe zote. Vita vilivyoko Baragoi ni mbaya zaidi. Ninaomba Kamati ya Usalama ichukue hatua na ihakikishe Waziri wa Usalama awe hapa ili wakutane. Shida kubwa iko kwenye hii ofisi. Watu wanauawa na inaporipotiwa hakuna mtu anayejitokeza kuwa ni kweli watu wameuawa. Mali inaenda na watu wanaachwa bila chochote. Hakuna mtu anaangalia kwa nini hii mali inaenda. Hatupigani na watu wa kutoka mbali. Hivi ni vita vinavyotoka Kaunti ya Samburu. Naomba Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama na wenzake wachukue Ombi hili la Mhe. Lentoimaga na kulitilia maanani; walichukulie kuwa ni la ukweli na ni kitu kimeangamiza watu kwa muda mrefu. Miaka nenda miaka rudi watu wamekuwa maskini na wengine kuuliwa. Hata sasa tuko na watu karibu wanne ambao wako hospitalini Nakuru. Wamevunjika miguu na hakuna mtu anayewashughulikia. Wanapigana na kuuana tu ilhali Serikali iko kila mahali. Ng'ombe wanapita tu wakiangaliwa. Pia wao wanauliwa na hakuna hatua inayochukuliwa. Ninaunga mkono Kamati ya Usalama ichukulie maanani Ombi hili. Ni suala ambalo halina mchezo. Asante Bwana Spika kwa kunipatia hii nafasi.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia mwanya huu nichangie jambo muhimu sana katika nchi yetu ya Kenya. La muhimu ambalo umefanya ni kutumia ujai na hekima yako kuleta maendeleo ya Kenya hasa kwa uwiano na uasiliano wa wakenya. Nchi nyingi duniani zimekua na misimamo yao mizito. Lakini katika Afrika tumeshindwa kuwa na misimamo mizito. Kati ya misimamo hii ni lugha tunayotumia kuwasiliana sisi wenyewe. Kama vile waliongea mbele yangu walisema wakati umefika wa Wafrika hasa Wakenya kujiamini na kuheshimu lugha za mawasiliano. Wakenya wengi ni wakulima. Lugha ambayo inatumika mashambani na viwandani ni lugha ya Kiswahili. Lakini hapa Bungeni Kiswahili kinaonekana kuwa cha walio wadhoefu na Kizungu kinakaa kama cha wasomi. Mhe. Spika umesimama nasi na kukubali tuwe na maendeleo ya Kiswahili hasa katika Kanuni za Kudumu za Bunge kwa lugha ya Kiswahili. Hili ni jambo la kujivunia. Nimefurahi kwa sababu waliokua wanatumia lugha ya Kiswahili Bungeni walikua wachache sana. Umesimama nasi na ombi langu ni utenge muda maalum kila siku au kila wakati ambao Wabunge watakua wakitumia lugha ya Kiswahili ili Wabunge wote wakichukulie kama njia moja ya kuwasiliana katika Bunge na hata kule nje. Tukifanya hivyo Kenya itatambulika. Kama tuvyojua hata viongozi wetu hasa kiongozi wa nchi Uhuru Muigai Kenyatta wakati anataka kuwasiliana na Wakenya anatumia lugha ya Kiswahili. Kwa nini sisi Wabunge tusiige huo mfano kwa kuendeleza Kiswahili kiwe njia moja ya mawasiliano hapa Kenya? Mengi yatasemwa lakini nakupongeza Mhe. Spika na nakuombea uendelee kuweka uzito kwa yale mema yatapatikana tukitumia lugha ya Kiswahili. Sitasema mengi ili nipatie mwanya wengime ambao wangependa kuchangia kama mimi. Asante Mhe. Spika.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii ili nitoe rambirambi zangu za familia yangu na baba yangu ambaye ni mwandani sana wa Rais aliyetuacha. Mwaka wa 1950 baba yangu Zakayo Cheruiyot na watu wengine walienda kumtoa darasani akachaguliwa kuwa kiongozi ambaye alikuja Legislative Council (Legco). Rais wetu ambaye ametuacha alianza historia yake kubwa katika jamii ya Nandi masomo yake na vilevile kazi ya siasa. Kama mtoto wa mzee nilipata nafasi ya kufanya kazi na yeye. Miaka 32 iliyopita nilijuana na yeye nikiwa katika Rift Valley Institute of Science and Technology mahali ambapo tulikaribiana sana. Baadaye tulifanya kazi pamoja na ninamshukuru kwa sababu alitujenga kama watoto wake na vilevile kuweka msingi katika nchi hii.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii ili nizungumzie taarifa hii kutoka Kamati ya kusimamia Pesa za Hazina Maalum hapa nchini. Kama kuna jambo ambalo Bunge la 12 limeweza kufanya ni kuwa na kamati hii ambayo inaangalia matumizi ya fedha zilizomo kwenye Hazina Maalum humu nchini. Kazi ya Hazina ya Pesa ya Maeneo Bunge ilianza miaka kadhaa iliyopita. Wakati wa Bunge la Tisa tulipata kima cha Ksh6 milioni. Tangu wakati huo hadi sasa tumerekebisha sheria mpaka sasa inaambatana na Katiba ambayo ilianza kutumika mwaka wa 2010 mwezi wa nane. Pesa za hazina hii zinatumika kimaendeleo. Tulipoaanza kuzitumia maeneo mengi hayakuwa na shule maabara na zahanati za kusaidia wananchi. Pesa hizi zimewaezesha wengi kuona maendeleo mashinani. Zimewawezesha wananchi kusomesha watoto wao. Nampongeza mwenyekiti kwa kazi nzuri ambayo amefanya kwenye Taarifa hii. Tangu hazina hiyo ianzishwe kamati iliyowekwa na Bunge la 12 ni muhimu. Lakini juu ya hapo ningetaka kutoa taarifa kwamba kuna umuhimu wa Serikali kuu kutengeneza jinsi hazina hiyo itaweza kuangalia maeneo yote ya Bunge hapa nchini. Kama unavyofahamu maeneo ni 290 na sio rahisi kwa kila mtu kwenda kila mahali wakati wowote. Pesa za ugatuzi zingelifuata namna pesa hizi za hazina za maeneo Bunge zinavyotumika bila shaka tungeona faida yake. Pesa za ugatuzi zimekuwa zikifujwa na huu ulikuwa mfano wa kugatua pesa kutoka Serikali kuu kushuka nchini lakini sasa hivi tunaona kuwa ni malalamishi kila pahali tunapopita. Sina mengi ya kusema isipokuwa tuzidi kuangalia jinsi tutakavyoboresha matumizi ya pesa hizi na kuweza kusimamia na kuhakikisha kuwa pesa hizo zinatumika vile ambavyo ilivyotengwa kwa mujibu wa sheria ya pesa za hazina za mashinani. Naunga mkono taarifa hii.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii kulizungumzia hili lalamiko ambalo limeletwa kwa Bunge hili kuhusu afisa ambaye alikuwa anafanya kazi kwa jeshi la Kenya. Mimi kama mwanakamati wa Kamati ya Ulinzi na Mswala ya Nje ningefurahia kama ungemwambia mwenyekiti wetu amwalike Mkuu wa Majeshi ya Kenya na wahusika wake ili walete ushahidi na tujadiliane mambo kuhusu haki za Bwana Mbaabu aliyedhulumiwa. Namshukuru Mbunge wa Igembe Kaskazini kwa kufanya kazi nzuri ya kumtetea ndugu wetu na kuleta haya mambo kwa Bunge hili. Kwa kweli wanajeshi na polisi wa Kenya wana shida na lazima tujaribu kuzitatua. Namuunga mkono Mhe. wa Igembe Kaskazini na natarajia kwamba itawezekana hivi karibuni kujadiliana hili jambo. Najua si hili tu. Kuna dhuluma nyingi sana ambazo wafanyikazi wa Serikali hupitia na pia ukiukaji wa haki zao za kibinadamu.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii nichangie mjadala wa Kanuni za Kudumu kwa lugha ya Kiswahili. Hii ni Hoja muhimu sana kwa sababu kulingana na Katiba yetu tuko na lugha tatu za kitaifa kama Kizungu Kiswahili na Lugha ya Ishara ya Kenya. Ni vizuri tutumie lugha zote hasa Bungeni ambapo mambo yote ya kitaifa yanajadiliwa. Tuko kwa Jumuia ya Afrika Mashariki na hatuwezi kusema kuwa hatuwezi kutumia lugha hizi. Tukienda kwa Bunge la Afrika Mashariki ni lazima tutumie lugha ya Kiswahili. Sio hapo peke yake. Shuleni watoto wanafunzwa Kiswahili. Sio vyema kutumia pesa kukifunza Kiswahili ilihali hatukitumii Bungeni. Ni muhimu tufanye mazoezi ya kutumia lugha ya Kiswahili ili tuzoee kuitumia. Nchi zingine kama Korea Japan ama Uchina wanatumia lugha zao kwa sayansi. Kwa hivyo ni lazima tukikuze Kiswahili hata tuandike vitabu vya sayansi ama vya uuguzi kwa lugha ya Kiswahili. Hivyo tutaendelea. Siku ya leo ni muhimu sana kwa kuidhinisha Kanunu za Kudumu kwa Lugha ya Kiswahili. Mhe. Spika tuchape vitabu vingi kwa lugha ya Kiswahili. Kama vile Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni amesema kila Mbunge apewe Kamusi ili tujifunze na tuendelee kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili Bungeni na shuleni. Tutakuza Kiswahili hivyo ili tukitumie kama lugha yetu ya taifa. Asante sana Mhe. Spika. Ninaunga Hoja hii mkono.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii nichangie Mswada huu. Mojawapo ya njia za kuhakikisha kwamba Wakenya wanapata huduma bora katika sekta tofauti ni kubadilisha sheria katika sehemu ambazo zinalenga kuboresha huduma kwa wananchi. Hata hivyo nimepitia Mswada na nangojea wakati ufaao ili nilete mapendekezo ya marekebisho zaidi kuboresha sheria hizi. Nawaomba Wabunge kwa sababu mrengo wa Upinzani wa kuangalia masuala haya wanaoketi upande wa kushoto wa Bunge wameungana na sisi kusonga mbele. Nawahimiza sote kama Wabunge tupitie sheria hizi ili wakati wa kuzipika zaidi tuwape Wakenya sheria ambazo zinawanufaisha wote. Tumekuwa na mazoea hasa katika kurekebisha sheria hizi. Kuna marekebisho ya moja kwa moja na tunaweza kuwa na watu wanaoweza kutumia njia fiche kuhalalisha mipango yao kwa kugeuza hizi sheria. Nimezipitia na nimeona ziko na dosari kidogo hasa sehemu inayosema kutakuwepo na mfuko maalum wa pesa. Ni lazima tujue mfuko huu rasmi wa pesa utaendeshwa vipi na isiwe ni njia ya kuvuja pesa ya wanachama. Vile vile inapendekeza kuwa kutakuwa na kamati maalum ya uegezaji ambayo wanachama wake ni lazima wawe na shahada ya digri. Vile vile inapendekeza si lazima wawe wanachama wa chama wanachowakilisha. Naona hiyo ni dosari kidogo ambayo ni lazima tuiangalie na tuzungumze na wadadisi wa masuala ya uendeshaji shughuli ya vyama vya ushirika tuone kuwa marekebisho tutakayopendekeza yawe yanalenga kuboresha sheria hizi zaidi na wala sio zile ambazo zinaendesha shughuli za vyama vya ushirika tofauti tofauti. Naunga mkono ijapokuwa nangoja wakati ufaao nilete marekebisho ya kuboresha zaidi. Asante sana Mhe. Spika.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii nitoe pole zangu na za familia yangu na Kaunti ya Samburu kwa baba yetu Moi. Tunamkumbuka Baba Moi kwa mengi sana. Kile amefanyia Kaunti ya Samburu hatuwezi kusahau. Tunaamini yeye ndiye mtu wa kwanza kuanzisha shule ya upili ya wasichana katika Kaunti ya Samburu. Hatuwezi kusahau hata kidogo. Kila Mkenya anakumbuka kwamba Baba Moi hakuwa rais wa kuchezewa. Alikuwa rais wa kuheshimiwa zaidi. Ukiangalia kati yake na rais wa sasa unaona kuna tofauti kubwa sana.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii. Kwa niaba ya wananchi wa Eneo Bunge la Mosop na Kaunti ya Nandi kwa jumla napeana risala za rambirambi kwa familia za Mbunge Ken Okoth na Gavana wetu Daktari Laboso. Wiki moja iliyopita mimi Mhe. Serem na Mhe. Keter tulipata nafasi ya kuwazuru wakiwa hospitalini hapa Nairobi. Tulipata Mhe. Okoth na mke wake hospitalini. Tulijumuika pamoja tukiona hali ambayo alikuwa akipitia kwa uchungu wote kupitia ugonjwa huu wa saratani. Baada ya hapo tulipata nafasi ya kumuona Gavana ambaye ametuwacha Dr. Laboso. Sisi sote tulishtuka kuskia kwamba ametuwacha na alikuwa na ii ya kupata dawa na kupona ili arudi kufanya kazi yake ya ugavana katika kaunti ya Bomet. Lakini ya Mungu ni mengi tumewapoteza hawa wote. Jambo la dharura ni kwamba sisi wote kama viongozi na Serikali tuchukulie saratani kama janga la kitaifa na tuweke pesa na mikakati na kutafuta mbinu na maarifa ambayo tunaweza kutumia kusaidia watu wetu. Kwa hayo machache natoa rambirambi zangu kwa niaba yangu familia yangu na wananchi wa Eneo Bunge la Mosop. Poleni sana.
Asante sana mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza ningetaka kumpongeza mhe. Odanga kwa kuleta kilio hiki. Hoja hii ni kilio kile ambacho Wabunge wengi wamekuwa wakilalamika juu ya Mawaziri ambao wamekua na matatizo. Nataka kusema kuwa Prof. Kaimenyi alikuwa mwalimu wangu wa shahada ya udaktari wa meno. Bila yeye leo hii singesimama hapa kama daktari. Kwa vile alikuwa mwalimu wangu nafikiri namwelewa zaidi. Kuna umuhimu wa sisi kuelewa kuwa kila mtu ana maumbile yake. Inachukua muda kwa mtu ambaye amepata shahada hiyo ya uprofesa kufanya kazi kwa urahisi na watu ambao wamechaguliwa. Tatizo lipo. Tunakubali kuwa tatizo lipo. Mimi kama mwanafunzi wake ningechukua nafasi hii kuwaomba wenzangu kwa kuwanyenyekea tafadhali nawaomba mwalimu wangu mpatieni nafasi aweze kufanya kazi. Sio rahisi kwa Prof. Kaimenyi kuweza kufanya kazi wakati kila kukicha Sossion amemlemea kwenye koo. Nilimsikia mhe. Mwandeghu akiongea. Ni kweli kuwa ya mgambo ikilia kuna jambo. Jambo lenyewe ni sasa hivi tuweze kulitatua tuone njia ambayo tutaweza kufanya kazi na Prof. Kaimenyi. Anataka kuwezesha elimu iendelee mbele. Lakini mzigo ambao ameubeba umemkalia kooni na ni mzito. Sisi kama Wabunge wa Bunge hili la Kumi na Moja
Asante sana mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii. Nafikiri mambo kuhusu gavana ninaona kwamba ni sheria ambayo haikuwekwa sawa sawa. Kwa ukweli kila mtu anafikiria ni kwake pekee kuna shida lakini ni kila pahali. Kitu cha kwanza tuna First mmoja tu; Uhuru Kenyatta. Lakini kule ukikuta gavana anasema "First wangu yuko hapa" sijui nani wangu ako hapa! Kwa hivyo ningeomba tujaribu tuangalie sheria ile inaweza kusaidia Kenya yetu. Kama Katiba haikuangalia pande zote ni afadhali iletwe Bunge tupitishe yale mambo yatasaidia Kenya. Mambo kuhusu gavana ni taabu. Tunajua Rais ni mmoja na First ni mmoja hatujui mwingine.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii. Ya kwanza ninashukuru Majority Leader Duale kwa njia ambayo ametuonyesha. Tulikuwa hapa wakati huu Mswada ulipoletwa. Ninashukuru Wabunge wenzangu wote kwa sababu ile sura wametuonyesha ni mbili. Kuna sura ya raha wanatupatia meno na ndani ya roho hatujui kama wako nasi. Ni lazima tufuate Katiba yetu. Ningeomba kusema kusongesha sio kuanguasha. Tujadiliane kama watu wa tumbo moja na watu wanaopendana. Mhe. Spika kuna tatizo kidogo kwa ile njia ambayo wanasema turekebishe ndio tuwe kitu kimoja. Kwa sababu kile wanaongea nasiwezi kusema hapa sio ile njia ambayo tunata ka kwa sababu huu Mswada ukipita haupiti kwa sababu ya akina mama peke yake. Utapita kwa sababu ya sisi wote kama Wakenya. Tunaulizwa na kila Mkenya kama Mswada huu utapita. Kwa kila eneo Bunge kila mama anafaa kumshika Mbunge wake ili kama anang'etang'eta tutajua ni yeye ametuangusha. Ni lazima tujitokeze. Kila mtu amshike Mbunge wake na tuwe kitu kimoja. Kwa ukweli lazima tutii sheria ya Katiba yetu. Ninaomba mkienda nyumbani kila moja avae hii badge na msiitoe. Tukirudi turudi nayo. Ukiamka amka nayo ili tujue tuko pamoja. Asante. Ninaunga mkono.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi nami pia kwa niaba yanguchama changu watu wa Kitutu Chache North na watu wa Kisii County nitume rambirambi zetu kwa jamaa na marafiki wa hayati Senator Kajwang'. Hayati Senator Kajwang' alikuwa rafiki wangu wa dhati. Kitu kimoja ambacho kilikuwa kinatushikanisha sisi wawili ni kwamba miaka kumi hapo mbeleni nilikuwa nimefukuzwa Chuo Kikuu cha Nairobi (UON) nikipigania maendeleo ya wanafunzi. Naye miaka kumi baadaye alifukuzwa viyo hivyo. Kwa hivyo tulikuwa na shida moja. Kitu cha pili alikuwa shujaa wa Kenya kwa kutatua matatizo ya Kenya akiimba "Wakenya msilale lale lale; Wakenya msilale laleee ".
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi niunge mkono mambo ya utumizi wa Kiswahili katika Bunge la 12. Nashukuru sana kwa sababu itatupatia nafasi sisi kama Wabunge wa Bunge hili tuelewe sana kuongea Kiswahili na hata kuandika. Nimekuwa nikijua ya kwamba Kiswahili siyo lugha rahisi sana. Kuongea Kiswahili sanifu ni kazi ngumu sana. Kukubali kama taifa la Kenya kutumia Kiswahili katika Bunge letu ni kwa maana sana sio kwa Wabunge peke yao lakini kwa wale wote waliotuchagua kule nyumbani. Unaelewa kwamba wengi ambao walituchagua ni zaidi ya asilimia 90 ama 80. Kwa hivyo tukianza kutumia Kiswahili ndani ya Bunge watafurahi sana na watakuwa wakitenga wakati kusikiza kwa umakini ni nini tunaongea. Mambo ambayo tunaongea mara nyingi ni yale yanayohusu wananchi wa Kenya na wengi wao hutumia Kiswahili. Mhe. Spika nimefurahi sana kwa kuanza kutumia Kiswahili. Tunakupongeza. Ninampongeza Mhe. Naibu Spika ambaye alijaribu sana kuitetea Hoja hii wakati aliposimama kuongea kuhusu kuzinduliwa kwa matumizi ya Kiswahili katika Bunge hili. Nawapongeza sana. Nampongeza Mhe. Millie sana kwa sababu alijaribu sana kuongea kwa lugha ya Kiswahili. Kama ulivyosema ni heri tupatiwe nafasi tuchanganye lugha ya Kiswahili na Kiingereza wakati huu tunapoanza. Ikiwa huwezi kutamka neno fulani kwa Kiswahili unaweza pia kulitamka kwa Kiingereza. Tutaendelea kujua kuzungumza Kiswahili. Kama leo nimejua maana ya neno "dondoo". Kwa hivyo kutumika kwa hii lugha katika Bunge letu ni bora sana. Nafurahi na ninajua tutajifunza sisi sote. Unaelewa kwamba kuna sehemu fulani humu nchini ambako watu hawakujifunza Kiswahili darasani. Nilipata bahati kwa sababu kwetu tulikuwa tukifunzwa Kiswahili kutoka darasa la kwanza hadi darasa la saba. Kuna watu wengine ambao hawakujifunza na hii itakuwa ni nafasi yao ya kujifunza ili twende mbele pamoja. Lugha ya Kiswahili ni lugha ya maana sana kwa sababu akina mama kule nyumbani wataelewa ni nini tunazungumzia hapa Bungeni. Wengi wao hawaelewi Kiingereza. Kwa hivyo nakupongeza wewe pamoja na team yako kwa sababu ya kufikiria tuanze kuongea Kiswahili katika Bunge la Taifa la 12. Kwa hayo machache Mhe. Spika ninaamini tutaendelea kutumia lugha ya Kiswahili kwa kutenga siku maalum ambayo tutaongea kwa lugha ya Kiswahili tuwe kama Watanzania. Asante sana.
Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi ya kuchangia mjadala huu kuhusu Hoja hii muhimu. Kwanza nakushukuru wewe na kikao chako cha maspika kwa jinsi ulivyoonyesha uongozi katika Bunge hili kama tu ulivyochangia jambo la Mhe. Nyikal. Uko na hekima. Mambo yako ni machache lakini uko na hekima na unajua sheria. Pili nawashukuru watu wa Eneo Bunge la Turkana ya Kati kwa kunichagua kuwa Mbunge wao. Nimejifunza mambo mengi tangu nilipokuja katika Bunge hili. Nimewakuta wazee wenye hekima na nimejifunza kuwa mvumilivu. Pia nimejifunza jinsi ya kujadili mambo yanayowaathiri watu wangu. Ningependa pia kuwashukuru Wabunge kwani tumefanya kazi pamoja. Licha ya kuwa na mgawanyiko katika hali ya vyama tumedumisha heshima. Tumeheshimiana bila kujali vyama ama kabila. Ningependa pia kukushukuru kwa sababu ya sheria ya riba ambayo tulipitisha katika Bunge hili. Wananchi kule nje wanashukuru sana kwa sababu benki nyingi zilikuwa zikitoza riba za juu na wananchi walikuwa wakiumia na kulalamika kwa sababu ya kulipa riba za juu. Rais alipoweka sahihi katika Mswada huo na ukawa sheria Kenya nzima ilishangilia na hiyo yote ilikuwa kazi ya Wabunge ambao wako mahali hapa. Nashukuru kwa nafasi hii ya kwenda likizoni ili tupate nafasi ya kutangaa na watu wetu na pia kuwaelimisha kuhusu sheria ambazo tumetunga hapa ili wajue na wasitumbukie katika mtego wa sheria. Hiyo ni kazi yetu kama Wabunge. Tukienda kule kutangaa na hawa tutawaeleza kuwa tumepitisha hii. Mheshimiwa Spika ni nafasi ya kwenda kuwa na watu wetu kujadili juu ya miradi ambayo tunataka ihifadhiwe mwaka huu. Tujue kutoka kwa hao na tusikie miradi ambayo wanahitaji ili tutakapokuja mahali hapa kupitia Fedha za Eneo Bunge tuone ya kuwa miradi ambayo wananchi wametaka imetimika na imetendeka kama vile wananchi walivyokusudia. Mheshimiwa Spika ningependa kukushukuru kwa sababu ni wakati mwingine ambao tungependa kwenda kupumuzika ili tukija mahali hapa tuwe na nguvu ya kuendesha kazi. Mwisho ningependa kuwaambia Wabunge wenzangu tutakapokutana katika mikutano ya siasa hapa na pale tudumishe heshima na ule urafiki wetu maana wakati mwingine tukifika mahali pale unapata ya kwamba tunatupiana eno makali na mambo ambayo si mazuri mbele ya wananchi tunapoteza heshima ya Bunge hili. Kwa hiyvo ninaomba tuendelee na ile heshima tuliyokuwa nayo mahali hapa. Hata kama hao ni wa kikundi ama chama kingine tukikutana tujue ya kwamba sisi ni Wabunge na tutarudi kwenye Bunge na tuendelee kuheshimiana. Hilo ndilo ambalo ningependa kuwaambia Wabunge. Ninajitayarisha kuenda kukaa na wananchi wangu. Mungu awabariki wote asanteni.
Asante sana Mhe. Spika kwa lugha ya Kiswahili "Kinara" kwa kunipa nafasi pia nichangie katika wazo hili ambalo ni la muhimu sana kwa watu wetu na nchi yetu kwa jumla. Hongera mwenzangu mheshimiwa Jicho Pevu kwa wazo ambalo umelifikiria na kufanya utafiti ambao umeuchukulia kimaanani kwa kutoa maelezo ambayo ni ya kweli. Jambo ambalo ningependa kushukuru ni kwamba tuko na hospitali mbili za rufaa hapa nchini ambazo ni Kenyatta na Eldoret. Lakini hospitali hizi ziko na shida: wagonjwa ambao wanaletwa pale ni wengi zaidi ya uwezo wa hospitali hizo. Kwa mfano Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi - Eldoret imekuwa hospital ya pekee; inapokea wagonjwa kutoka sehemu zote hata kutoka nchi jirani yetu za Uganda Sudan Somalia na sehemu zote ambazo zinakaribiana kwa sababu tuko na uwanja wa ndege pale. Jambo ambalo ni nzito ni idadi ya wagonjwa wanaoletwa pale ambao wangepaswa kutibiwa na mahospitali yaliyo karibu. Kwa hivyo hospitali yenyewe imekosa ule umuhimu wake wa kuwa hospitali ya rufaa. Imekuwa hospitali ya kutibu magonjwa madogo madogo ambayo yangepasa kutibiwa na hospitali zile zingine za kaunti za Kiwango cha 3 au 2 kule nyuma. Ya pili ni kwamba tuko na tatizo katika jamii kwamba mtu anakuwa mgonjwa zaidi ikifika kiwango fulani anakimbizwa pale wakati imekuwa kero. Sisi pia kama wananchi tuko na shida. Sisi viongozi ambao tuko hapa tunajua ya kwamba kila wikendi kila kuchao sisi ndio tunaitwa kwa michango na matibabu. Nashukuru kwamba afya kwa wote imezingatiwa katika yale mawazo ne ya Rais. Naona itatusaidia zaidi iwapo sisi sote kama vingozi tutaweza kupitisha Mswada na pesa ambazo zitatekeleza wajibu huu wa kupea wananchi wetu afya bora. Cha muhimu ni kwamba ni kweli kwamba tuko na madaktari. Ni kweli kwamba tunaongoza katika eneo hili la Afrika Mashariki kwa upande wa matibabu. Cha muhimu ni kwamba usimamizi wa hospitali zetu na viongozi ambao wameteuliwa kama Mawaziri na makatibu kusimamia kiungo hiki hawajawajibika. Kuna hofu kuhusu dawa ambazo zinaletwa nchini. Madaktari husema kuwa dawa nyingine ambazo zinatumika hazipitii barabara nzuri kwa udhibiti; inachangia wazo la kuongezea magonjwa mengine kama saratani kwa sababu dawa zinaozoingia humu nchini hazipitii utaratibu unaofaa. Inafaa wakati tunaenda kuyapitisha mambo haya tuyachunguze na kuona ya kwamba kila kitu ambacho tunala kiwe kimepitishwa katika mpangilio ambao utatuepusha na magonjwa. Vile mheshimiwa mwenzangu amesema hapa maji tunayotumia yana madini ambayo yanasababisha magonjwa mengine. Hili ni jambo ambalo lazima tuliangalie kama viongozi na nchi. La nne ni kwamba lazima tujiulize tunataka nini kama viongozi. Kila kiongozi anayekuwa Rais angependa kuwacha mambo fulani ambayo atakumbukwa kwayo. Namshukuru mstaafu Rais Moi kwa sababu wazo hili la kuweka Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi mjini Eldoret ni lake wakati wake ule. Tunamshukuru sana. Mungu amusaidie apate ubora wa afya anapozeeka. Hii ni ili sisi sote tujue kwamba ni muhimu tupitishe Hoja hii kwa haraka. Ni jambo ambalo limefanyika jana kwamba hata yeye mwenyewe mstaafu Rais amepelekwa kule atibiwe na hali tuko na uwezo tumesoma na tuko na rasilimali ambazo tunaweza kutumia kuyakuza mambo haya. Ya mwisho ni kwamba tulivyo kama nchi wananchi wakiwa wagonjwa ama wageni wetu wanapozuru nchi cha muhimu wanachoangalia ni: "Je nikienda nchi ya Kenya nipate matatizo ya matibabu nitapata hospitali ambayo inaweza kunitibu?" Lazima tuwe watu wanapanga mambo yao mbele ili tupate kuimarisha utalii na vile tupunguze gharama ambazo nchi hii inapitia kwa kuwapeleka wagonjwa wetu nje kwa matibabu. Naunga mkono wazo la kusema kwamba wale wanasimamia hospitali zetu haswa za saratani wapeane nafasi kwa nchi nyingine zijenge hospitali hapa; hospitali ambazo zitakuwa nafuu kwetu kwa kutumia teknolojia yao. Nchi ya India iko na matibabu ya gharama ya chini na ya njia bora kuliko nchi zingine ulimwenguni kama Marekani na Ulaya. Nikifunga hospitlai hizi mbili ambazo tunasema ni za rufaa haziko katika kiwango kimoja. Kuna tofauti kubwa sana kati ya mishahara ya wafanyakazi wa Kenyatta wa na rufaa ya Eldoret. Daktari wa Kenyatta National Hospital na daktari wa Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi kule Eldoret wana tofauti ya mishahara ya Kshs100000 na zote ni hospitali za rufaa. Kama hospitali hizi mbili ni za rufaa lazima mishahara yao isawazishwe kwa sababu inachangia madaktari kutoka kwa hospitali moja kwenda kwa nyingine. Msimamizi wa Kenyatta anashinda msimamizi wa Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi ya Eldoret kwa zaidi ya Kshs200000 kwa mshahara. Hilo ni jambo la kushangaza sana. Juzi Waziri wa Hazina ya Taifa ambaye anatakiwa kuangalia jambo hili anakalia sana pesa za kupeana huduma za hopitali hizi. Utakuta kwamba hata huduma ya kutolewa kwa hospitali hizi zina shida. Ukiangalia bajeti ya KNH na ya Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi - Eldoret kuna shida kubwa sana. Ni ombi langu kwa Wizara ya Fedha kuwa pesa za hospitali zitolewe kwa haraka bila kuchelewa ili kupunguza shida ambazo tunapata. Kwa hayo machache nashukuru.
Asante sana Mhe. Spika kwa nafasi hii. Kwa niaba ya wakaazi wa Eneo Bunge la Rabai na wakaazi wa Kilifi napeana rambirambi zetu kwa familia ikiongozwa na Raymond na Gideon ambao ni Waheshimiwa wenzetu. Pia nasema pole kwa Wakenya wote. Naomba tu viongozi wa nchi hii hasa wale wanaoshikilia hatamu za kuongoza nchi ya Kenya waige mfano wa Rais Moi. Nasema hivyo kwa sababu juu ya yote ulikuwa ukiangalia Baraza la Mawaziri la Moi unaona sura ya Kenya. Siku hizi mambo ni tofauti. Kwa hivyo viongozi wanaoongoza Kenya hii waige mfano wa Moi na waweke ai na upendo mbele.
Asante sana Mhe. Spika kwa uongozi wako. Vile nimesema naunga mkono wote waliochaguliwa kwa sababu wanauzoefu wa kazi na wataendelea na kazi kwa ule muda mfupi ambao umebaki hapa Bungeni. Ni heri wamalize kipindi. Mwaka huu una mambo mengi. Kwa hivyo ningeomba IEBC ijaribu kuangalia mahali kuna tatizo na kujaribu kutafuta suluhu kama vile jana tulikua tunajaribu na mmoja wa wanaeneo Bunge langu vitambulisho vya watu waliofariki. Alipojaribu kuviweka katika zile mashini alipata bado majina yapo kwa orodha. Ni vyema IEBC iondoe majina ya watu waliofariki kutoka orodha ya wapiga kura. Mhe. Spika asante sana kwa kunipa fursa hii.
Asante sana Mhe. Spika wa Muda kwa kunilinda. Nilikuwa naongea kuhusu ile miraa ambayo tunakuza. Ni kilimo ambacho kama Serikali ingekitilia maanani na waitafutie soko kule tungekuwa tunapata hela nyingi. Nchi ya Israeli imeanza kununua ile miraa kutoka mwezi huu. Hizo ni pesa ambazo zitafaidi Serikali kwa njia kubwa. Ukiona zile bidhaa ambazo tunaagiza kutoka nje ni bidhaa za hela nyingi ukilinganisha na zile ambazo sisi tunauza kule nje. Kwa hivyo kama Serikali ingetilia mkazo wakulima wa hapa nchini nadhani zile pesa ambazo tungekuwa tunaomba kutoka kule nje zingekuwa chache na mwananchi hangefinyiliwa na Serikali kwa kulipa kodi. Kwa hivyo kile ambacho kinafanya wananchi walipe kodi ya juu ni Serikali imefeli kutekeleza yale ambayo yanaweza kumsaidia mwananchi katika kukuza bidhaa hapa ili tupate pesa nyingi. Wakati ambapo hii Hoja itapita ni vizuri Serikali iangalie mwananchi kwanza halafu yule ambaye tunanunua kutoka kwake awe wa pili. Hili litasaidia nchi kupata pesa kwa wingi. Sio vizuri wakati ambapo tuko na bidhaa ambazo tunaweza kuziekeza na zitoe pesa nyingi za kusaidia nchi tunaweka mtu wa kutoka nje katika mstari wa mbele na kusahau watu wetu. Ni vizuri Serikali imshughulikie mwananchi wake kwanza kwa kuyashughulikia yale ambayo yanaweza kumsaidia kuzalisha fedha zaidi kushinda zile ambazo tunazipokea kutoka kule nje. Kwa hayo machache naomba kuunga mkono. Asante.
Asante sana mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Mswada huu. Mambo ambayo yako mbele yetu ni muhimu sana kwa kila binadamu. Kama tunavyojua kwa kila mtu maji yakitajwa anahisi kwamba ni kitu ambacho anahitaji. Tukiendelea kuangalia mambo kuhusu maji ninajua kila mmoja katika eneo la uwakilishi Bungeni la Ruiru anaangalia aone ni kitu gani nitasema kuhusu maji. Lakini shida ya maji iko katika Kenya nzima. Ningependa kuongea kidogo kuhusu akina mama ambao wanasumbuka zaidi na jambo hili la maji. Hata kama tutakuwa tukiyashughulikia mambo haya katika kaunti ninahuzunika zaidi ni kikumbuka kwamba ukifika katika maeneo ya Ruiru Mwiki Githurai na Mwihoko utakuta akina mama wanachota maji kwa mitungi. Kwa hivyo masaa mengi yanapotezwa na akina mama wakitafuta maji. Pesa nyingi zinatumika katika mipango hiyo na ni shida kubwa sana pesa hizo kufikia mwananchi wa kawaida. Ninasema kwamba ni vizuri tuwe na wataalamu ambao watasomesha watu kuhusu njia nzuri za kuhifadhi maji hata kama ni maji ya mvua. Mhe. Naibu Spika wa muda ninaomba kwa heshima Mwenzangu mhe. Millie Adhiambo-Mabona ameongea mbele yangu lakini mimi sio yeye. Naomba kwamba tafadhali hatutaki mipango hii Kuna watu ambao tunawahitaji sana sisi ambao tuko karibu hapa; kuna kampuni ya maji ya Nairobi. Kitu ambacho tunacho ni huzuni kwa sababu majina ni makubwa lakini kazi ni kidogo. Mhe. Naibu Spika wa Muda ni jambo la kuhuzunisha sana tukisema kwamba tunataka kupitisha Mswada hapa na wale tunaowapitishia ambao ni wananchi wa kawaida hata hawafikiwi na maji. Naomba hata kama tunasema maji yatakuwa yakisimamiwa na kampuni ya maji ya Nairobi ni vizuri tujue kwamba huko tunakosimamia kunaenda maji kwa mwananchi wa kawaida. Tuweza kuwa na maji katika miji na tunapatiwa maji. Kuna yule ambaye yuko pale mashinani hata akisikia mkiongea kuhusu maji machozi yanamtiririka kwa sababu kuyapata maji ni vigumu. Ule mpango utakaopangwa usipangiwe tu kwa wale watu ambao wanaonekana mijini lakini tuangalie hata wale ambao wako mashinani ndio waweze kufikiwa na maji. Pia tuangalie wakati tunapanga mipango hiyo isitumie pesa nyingi hata watu wetu wakakosa maji. Sipingi Kampuni ya maji ya Nairobi lakini nauliza kazi yao katika eneo Bunge la Ruiru ni ipi? Watu wametaabika na kubeba maji machafu. Watu wengine wameenda kwa mashimo ya mijengo kuchota maji kwa sababu wana shida. Tafadhali nikiunga mkono Mswada huu nawaomba washughulikie suala hilo na wajue kwamba mwananchi wa kawaida analia usiku na mchana kwa sababu ya maji. Akina mama wameumia na migongo yao inauma kwa sababu ya kubeba maji. Tafadhali tuongee hapa Bungeni na pia tufikishe maji pale mashinani. Asante mhe. Naibu Spika wa Muda; ninaunga mkono Mswada huu.
Asante sana Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangie hii Hoja. Kabla sijachangia nataka kutoa shukrani kwa Rais wetu kwa kuapishwa jana. Alifurahisha dunia yote kwa kuapishwa kwake. Hata sisi tumefurahi sana. Pia natoa shukrani kwa Wakenya wote bila kujali vyama vya kisiasa. Wakenya wote walishuhudia kuapishwa kwa Rais wetu bila kujali kabila ama chama cha kisiasa. Wakenya wote walikuwa huko. Tunashukuru sana. Hiyo ni kujenga nchi yetu bila kufuata mambo ya siasa. Pia tunafurahi sana kwa sababu hatuna Kenya mbili mbali ni hii moja. Kiti cha Rais ama Mbunge hakikaliwi na watu wawili. Ni mtu mmoja tu. Kwa hivyo wote tunafurahi. Naambia wenzangu wote viongozi ya kwamba ni muhimu tushikane wote tuone kile kitu kitasaidia Wakenya. Ni kweli tumeona vile huyo mtoto amepigwa risasi. Kama mama na sisi kama viongozi tufikirie sana. Ukiangalia hayo mambo kwa runinga ni kama kuna watu wameanza kuvaa sare ya polisi. Ukiangalia hao polisi unaweza kufikiria hawajapata mafunzo. Kwa hivyo naomba Serikali iingilie kati hayo mambo ya sare za polisi kwa sababu watu wameanza kuzivaa. Nikirudi kwa Hoja ya kutenga njia za gari za dharura nakushuru kwa hii Hoja kwa sababu tunafaa kuangalia kila barabara. Kwa ukweli kuna culvert zingine ambazo zimetengenezwa kwa njia nzuri lakini kuna zile zinakaa kama milima. Hata ukiwa na mgonjwa anaumia akirushwa kwa hizo culvert . Sisi ndio tunapitisha bajeti katika hili Bunge. Ningeomba pia tuangalie bajeti ya barabara maji na hospitali ili tukipitisha wizara zipate pesa. Wakati mwingine pesa zinapitishwa na wizara hazipati hizo pesa. Ninatoka Samburu County ambayo ina shida kubwa sana. Mvua ikinyesha barabara zote zinapasuka na watu hawawezi kwenda upande ule mwingine hata kwa hospitali na hawawezi kufanya chochote. Kwa hivyo ningeomba kuwa mambo ya barabara yanafaa yaangaliwe zaidi. Tukichangia mambo ya magari ya dharura pia tuangalie mambo ya boda boda . Hapa Nairobi nusu saa haipiti bila ya mtu wa boda boda kugongwa na gari kwa sababu hawana barabara za kupitia. Watu ambao wanasafiri kwa boda boda wanapita mbele ya magari. Inafaa tuangalie mahali boda boda zitapita kwa sababu watu wanaumia katikati ya magari. Kwangu tuna shida ya barabara. Ningependa kusema tuangalie sana katika wizara ambazo zina cartels ambazo zinapewa kazi ya kutengeneza barabara. Mtu anaweza kuchukua kampuni yake hapa ipitishwe na apewe kazi ya kujenga barabara. Ningependekeza waanze kuzungumza na viongozi wa eneo Bunge wakati wanapeana hizo kandarasi ili wajue ni barabara gani zinatengenezwa na kwa namna gani. Unakuta kandarasi imepeanwa Nairobi na mtu anaenda Samburu na kiongozi hajui. Kwa hivyo inafaa viongozi wahusishwe kwa yale mambo yanafanywa ndiyo tushirikiane pamoja tuone yamefanywa kwa njia inayotakikana. Unakuta vitu vingine vinaenda kombo kwa sababu viongozi hawaelezwi. Naunga mkono Hoja hii. Lazima tuangalie vitu vingine ili tusaidike. Naomba ndugu zangu wa National Super Alliance (NASA) tuwe pamoja. Tumechaguliwa ili tushirikiane pamoja kama viongozi. Tunafaa kushirikiana na kufanye kazi ya wananchi. Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii.
Asante sana Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangie Mswada wa Mamlaka ya Kitaifa wa Usimamizi wa Majanga. Nimefurahia sana Mswada huu ambao utasaidia Kenya nzima. Unalenga mambo mengi kama moto na mafuriko hata kule kwetu kwenye bahari. Ningependa kiwango fulani cha mgao kutoka Serikali kuu kiwekwe hapo kama asilimia 10 au 20. Itasaidia Kenya pakubwa na tutasonga mbele kimaendeleo. Kwa hakika kuna majanga ambayo hutokea baada ya muda na bado hatujitayarishi wala kusoma. Kwa mfano mafuriko. Tunajua miezi fulani huwa na mafuriko lakini huwa hatujitayarishi. Kuna sehemu za Lamu tunajua miezi fulani bahari inakua chafu sana na majanga hutokea hata tsunami. Maji hupanda hadi kwa nyumba za watu. Tunajua linajiregelea lakini huwa hatujitayarishi. Mswada huu utatoa suluhisho kwa majanga kama hayo. Cha kusikitisha ni kwamba ikiwa kuna kampuni kubwa au mradi mkubwa katika sehemu kwa mfano Lamu Port South Sudan Ethiopia Transport corridor (LAPSSET) katika mambo ya bahari inafaa yajitolee kabla kuanza mradi waweke kitengo cha kusimamia majanga ambacho kitakuwa kikisaidia majanga yakitokea. Lakini hakuna hata moja ingawa ni rahisi kwao kufanya kitu kama hicho. Watu wanakufa wakati huo wanapata shida ama wanakataa kwenda kwa bahari lakini kama kungekua na njia ya kuwasaidia wangekuwa wanaendelea na maisha yao ya kawaida. Watu wanaenda baharini wanapotea na majanga ya kila aina yanatokea lakini kampuni kubwa kama hizo hazitusaidii. Mswada huu utasaidia sana. Mafuriko na majanga mengine pia yako kwa Kaunti ya Lamu. Hata janga la ugaidi lipo. Watu wanahamishwa makwao haswa Wadi ya Basubwa lakini inajirejerea. Tunashukuru Mwenyezi Mungu iko vizuri wakati huu. Ukienda upande wa Bara katika Wadi ya Wito huwa na mafuriko kila mwaka. Siku zote sisi huteta na KenGen. Lakini tunashukuru Mwenyezi Mungu siku hizi wanaingilia vizuri. Ukame pia upo. Haya majanga yako mengi na yanajirejerea na huwa kama aibu. Ni kitu ambacho kinarejelea na tunajua hatuchukui hatua yoyote. Kwa hivyo Mswada huu utasaidia pakubwa na tunaunga mkono sana angalau watu wetu wapate kusaidika. Asante sana Bi Naibu Spika wa Muda.
Asante sana Mhe. Spika wa Muda. Ninaunga mkono Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi ya kwamba Kipenglele cha 6 kiondolewe kwenye Ripoti hii kwa sababu Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi ijapokuwa kwa upande wao walijaribu kupigana na suala hili hawakuwa na nguvu ya kusimamisha pesa sizipeanwe katika njia ile iliyotumika. Vile vile sababu yangu nyingine ni kuwa suala hili la Tume ya Maadili na Kupambana dhidhi ya Ufisadi hapa nchini tumeibaidilisha mara nyingi kwa sababu hatujafurahia kazi ambayo imekuwa ikiendelea. Lakini Tume ya sasa imejaribu. Watu wakijaribu tusiwapatie adhabu kwa kujaribu kazi ambayo wamefanya. Kwa hivyo wakati tanapoendelea kuzungumzia Ripoti hii itakuwa ni vizuri kulirudia tena jambo la pesa za mwananchi kutumika vizuri na kama hazijatumika vizuri Kamati ifuatilie masuala hayo yote vilivyo. Asante sana naunga mkono.
Asante sana Mhe. Spika wa Muda. Ningependa kuungana na wenzangu kuunga mkono marekebisho haya ya Mswada huu kuhusu serikali za kaunti. Tunapaswa kama Wakenya kujipongeza wenyewe na kuipongeza nchi hii kwa Katiba tuliyopitisha kuhusiana na mambo mengi mojawapo ikiwa suala la serikali za kaunti. Leo marekebisho tunayofanya hapa ni kutokana na hofu kubwa kuwa serikali za kaunti kuonekana namna zitakavyojiendeleza na namna zitakavyodumu katika kuendeleza mambo yao. Ndiposa mwongozo huu tuko nao leo waonyesha hofu iliyokuwapo ni kwamba serikali 47 za kaunti huenda zizifanye vyema ama kutokuwa na usawa. Ndiyo sababu kukawekwa mikakati kama hii ili mambo haya yatakapojitokeza ifahamike ni vipi yatarekebishwa. Ukweli ni kwamba ningependa kuzipongeza serikali za kaunti takriban zote. Kutoka zianze masuala haya hakuna kaunti imepitia changamoto hizi isipokuwa tu kaunti moja. Imetajwa na wenzangu hapa lakini vile vile haikufika kiwango cha hofu iliyokuwepo kwa Wakenya wakati walipokuwa wakipanga Katiba hii. Lazima tukubali pakubwa fikra ya kuwa na serikali za kaunti imechangia pakubwa maendeleo ya nchi hii. Tumeshuhudia mambo mengi yamebadilika na maendeleo yamekuwapo katika sehemu mbali mbali katika nchi hii. Ingawaje hakuna jambo ambalo halina changamoto lakini ukweli ni kwamba tunashukuru Mwenyezi Mungu kutokana na serikali za kaunti kuonyesha mabadiliko makubwa. Kumekuwa na tofauti kubwa katika nyanja tofauti tofauti. Ingawaje ni vizuri kuendelea kuhakikisha kwamba zimepigwa darubini ama kuhakikisha kwamba zitadumu na kufuata sheria na utaratibu unaotakikana. Naunga mkono Mswada huu nikiamini pakubwa haya yote ambayo tumeyaweka wazi hapa yatakuwa ndio mwongozo na uangalifu wa serikali za kaunti. Tuhakikishe kwamba panapotokezea matatizo tuna mwongozo kamili wa kuhakikisha kwamba matizo hayaleti athari ama hayatatanishi utaratibu ambao unaendelea hivi sasa wa kisheria. Naunga mkono na naungana na wenzangu kwa kupendekeza na kuhakikisha ya kwamba haya mambo na utaratibu huu umepitishwa. Ningependa kukomea hapa. Asante.
Asante sana Mhe. Spika wa Muda. Ningetaka kuwakumbusha wenzetu ya kuwa tunaanza kuzungumza kuwa Kenya ni yetu sote. Mambo ni namna hii. Lazima wengine kutoka Pwani wazungumze. Nataka kuwakumbukusha wenzangu hivyo hususan wale kutoka sehemu za mimea ya sukari. Wanasema kule kwetu hakuna sukari lakini iko katika Ramisi. Pili nataka kutoa mfano wa mtu anayetumia kapu lililotengenezwa na miyaa kuti ama pakacha na kila siku kwenda katika kisima na kujaribu kuchota maji hayataweza kuchoteka na mwisho wale wenye kuhitaji yale maji wataja kujigundua. Ndipo tunaingia sisi kama Wapwani. Kila mwaka sekta hizi zinazidi kupatiwa fedha. Wakulima wanaambiwa hawawezi kupatiwa aa hizi. Katika sekta hii deni zote zinakaribia takriban Kshs 12-15 billion. Deni ya viwanda vyote vya umma ni Ksh 12 - 15 billion. Ikiwa tutahitaji hivi viwanda vijiendeleze tena basi itabidi mifuko ya Wakenya itapike tena Ksh 12-15 billion. Nataka kutofautiana na wenzangu. Suluhisho ni kupatia viwanda hivi watu ambao wako na uwezo wa kuendesha kazi hii. Serikali haiwezi kufanya kila kitu. Jukumu la Serikali ni kupitisha sheria na kanuni zitakazofaa ili wenye kustahili ambao ni wenye viwanda nchini wapewe nafasi. Kwa mfano thai ya kampuni ya Safaricom ni mabilioni ya pesa. Ilipozaliwa ilikuwa inamilikiwa na serikali. Baadaye ilibinafsishwa. Leo nataka tujiulize swali katika Bunge hili na tulijibu kiukweli ndani ya nafsi yetu: lau Safaricom ingekuwa bado ni mali ya umma kisha tungojee Rais achague mkurugenzi wake je tungekuwa tunailipia madeni na kusema wafanyikazi wake walipwe mishahara? Nia na madhumuni yangu ni kuwasihi wenzangu tusiwe tukiangalia na kusema kila siku Serikali ifanye jambo hili ama lile ama itoe aa. Hata sisi kule Pwani tunayo sekta ya uvuvi na korosho lakini hatujaona Serikali hii ilioko na zile zilizopita zikitufanyia jambo lolote. Tunayo vilevile sekta ya chumvi. Hakuna yeyote anayeweza kuishi bila chumvi. Lakini hatujaona yeyote ambaye amefanya jambo lolote kuhusu sekta hiyo. Kwa nini? Ni kwa sababu kuna watu binafsi wanaoweza kufanya hiyo kazi sawa sawa. Pesa zetu hazitaliwa kiholela. Ahsante sana Mhe. Spika.
Asante sana Mhe. Spika. Hakuna mtu yeyote ambaye anadhalilisha mtu sababu ya umri. Lakini kama mtu amestaafu ni vyema yule ambaye hajapata kazi apate nafasi hiyo ya kazi kwa sababu ni wengi ambao wanatafuta hii kazi na hawawezi kupata hiyo kazi. Sana sana namba iliyo juu ni vijana wengi ambao hawana kazi kwa sasa. Kwa hayo machache naomba kuunga. Asante.
Asante sana Mhe. Spika. Jambo hili kama vile tulivyozungumzia ni la uwazi. Sisi kama waheshimiwa tuko kama vinara wa CDF. Kazi yote hufanyika kupitia hizi kamati. Ninaunga mkono. Ninaomba sisi sote tuipitishe Hoja hii. Hata zile pesa tulizozizungumzia zikitoka kwenye Hazina ya Taifa ikiwa bado Kamati kwenye sehemu za uwakilishi bungeni hazijakuwa tayari wananchi hawatanufaika. Kwa hayo machache ninaiunga mkono Hoja hii.
Asante sana Mhe. Spika. Kupitia Kanuni za Kudumu Nambari 44(2)(c) naomba kuuliza na kusisitiza tena kupitia Kamati ya Uchukuzi Kazi za Umma na Nyumba kuhusu ulazimishaji wa kusafirisha mizigo kupitia reli maarufu Standard Gauge Railway (SGR). Tarehe 2 Juni 2020 nilileta ombi hili kuhusu ulazimishaji wa kusafirisha mizigo kutumia SGR. Ilipofika tarehe 16 Juni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchukuzi Kazi za Umma na Nyumba akaleta Ripoti ambayo inatofauti kubwa na vile hali ilivyo mashinani. Alisema huu ni mpangilio wa Marais wa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki ya tarehe 12 May 2020. Alisema kwamba mizigo yote ya nchi za nje lazima itumie reli kwa sababu ya kuzuia mripuko na mchipuko wa maradhi ya Korona. Jawabu lake likaendelea kusema kwamba Mawaziri wa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki wamepatiwa amri kutekeleza agizo hilo. Ripoti ambazo ziko zinaonyesha kuwa nchi ya Uganda imekataa ulazimishaji wa kutumia reli. Pili gharama alizozitaja Waziri za usafirishaji wa mizigo hazilingani na zinatofauti kubwa mno na zile wahusika wanazolipa na kutumia. Tatu Waziri anasema kutumia SGR ni jambo ambalo nchi zote zimekubaliana kuwa litazuia uenezaji wa Korona. Nchi jirani ya Uganda imekataa jambo hilo. Nne kusema kuwa Naivasha Inland Container Depot (ICD) iko tayari inaenda kinyume na ripoti ambayo iliwekwa sahihi na nchi ya Uganda Rwanda na Sudan Kusini ya tarehe 22 May. Hakuna utafiti wowote ambao umefanywa wa athari ya kiuchumi kwa watu wetu wa Mombasa na wanaofanya kazi na kuishi kwa njia ya reli. Bw. Spika kupitia hayo ningeomba uweze kutoa amri kwa Kamati husika walete ripoti ya undani na ukamilifu ikizingatia yafuatayo - (i) Ni sababu ipi imemlazimisha Waziri kutoa amri hii bila ya idhini ya Bunge wala ufuataji wa sheria? (ii) Tukisubiri ripoti hiyo kutolewe amri kwamba Bunge lisimamishe agizo hili mara moja mpaka watu waweze kuwasiliana na hususan waliohadhirika. (iii) Ripoti hiyo ieleze kinagaubaga adhari za hali ya kiuchumi ya watu wa Mombasa na wale wengine wanaoishi na kufanya kazi katika njia ambayo mizigo hii hupitia ikiwa mpangilio huu utaendelea. Ahsante Bw. Spika.
Asante sana Mhe. Spika. Kusema kweli kama wananchi wa Kwale na Pwani kwa jumla tumesikitishwa sana na kifo cha mwendazake Mheshimiwa Sulei Dori ambaye alikuwa ni mpenda kazi mpenda wenzake na mpenda nchi yake. Mheshimiwa Sulei Dori licha ya kuwa alikuwa Mbunge wa Msambweni alikuwa rafiki wangu wa karibu. Tulizungumza mengi kuhusu maendeleo na kuhusu kazi yetu tunayoifanya na amesaidia sana Wabunge wengi wa kutoka Pwani kwa kuwaonyesha jinsi ambavyo watajifundisha maswala ya Bunge ili waweze kusaidia jamii kwa ujumla. Nataka niwashukuru sana viongozi wote walioweza kufika jana kwa mazishi ijapokuwa muda ulikuwa mfupi. Familia imeshukuru sana kwa sababu mwanzo hawakutazamia kwamba watapata idadi kubwa ya Wabunge kuja kumsindikiza marehemu Sulei Dori. Kwa niaba ya familia yangu na wananchi wote wa Kwale kwa jumla nataka niiambie familia pole. Mwenyezi Mungu awape subira na heri wakati huu mgumu na Mwenyezi Mungi ailaze roho ya marehemu Sulei Dori mahali pema panapo lala wema Asante sana.
Asante sana Mhe. Spika. Kwa niaba ya watu wa Kabete familia yangu na mimi mwenyewe naleta ujumbe wangu wa rambirambi kwa familia ya Mzee Moi. Twakumbuka Mzee Moi kwa mambo kadha wa kadha kukiwemo ukarimu wake na maziwa ya watoto wa Nyayo. Pia twamkumbuka kwa kuleta ai undugu na upendo. Twamkumbuka kwa unyenyekevu wake aliponyenyekea na kuomba msamaha. Mwisho twamkumbuka kwa kupeana uhuru wa kuabudu.
Asante sana Mhe. Spika. Kwa niaba yangu familia yangu na Kaunti ya Lamu kwa jumla natoa rambirambi zetu kwa familia ya Rais wa Pili nakwa mwenzetu Gideon. Tutamkumbuka baba yetu kwa mambo mengi. Moja ni kuleta Wakenya pamoja na yale maziwa ya Nyayo tuliyokunywa. Pia alianzishia watu wa Lamu bursary ya Ksh.10 milioni na watoto wengi wakafaidika kwa masomo. Pia alitupatia Naibu Wa Waziri ndugu yetu Mohamed Hashim na nyumba kuu hapa ikakuwa rahisi kufikia. Kulikuwa na wazee walioheshimika sana na wakipiga simu inashikwa. Pia tunakumbuka wazee wetu kama marehemu Maharus. Tutamkumbuka baba kwa mambo mengi. La muhimu ni sisi viongozi.
Asante sana Mhe. Spika. Kwanza ningependa kumshukuru Mungu kwa ajili ya nafasi ambayo amenipa kuwakilisha watu wangu wa eneo Bunge la Kuria East. Hongera nyote ambao mmechaguliwa kuwakilisha watu kutoka maeneo ambayo mmetoka. Mhe Spika hongera kwa ajili ya kuchaguliwa vilevile. Vilevile nachukua nafasi hii kushukuru Mungu kwa sababu ya Rais wetu. Tabia ambayo ameonyesha utu ambao ameonyesha tangia mambo haya yamefanyika imetutia sisi moyo sana. Kulingana na Hotuba ambayo Rais alitoa jana kipengele kile ambacho alizungumzia kuhusu mambo ya ugatuzi. Sisi ambao tunatoka sehemu ya Kuria na maeneo mengine yenye makabila madogo madogo jambo hili la ugatuzi... Aliposema kwamba Bunge la Kumi lilifanya kazi nzuri kuzalisha Katiba mpya Bunge la Kumi na Moja likafanya kazi nzuri ya kulea Katiba hii mahali ambapo alitaja kwamba Bunge hili litaendeleze demokrasia yetu hapo ndipo ningependa kulenga. Ingependeza sana kwamba Bunge hili tuangazie zaidi jinsi ambavyo tutafanya ugatuzi endelezi. Jinsi ilivyo sasa ni kwamba gatuzi nyingi zimeshikwa mateka na wale ambao tumewapa mamlaka ya kuendeleza ugatuzi. Magavana wengi sisi wote tunajua baada ya kupata mamlaka wameachia palepale. Hakuna ugatuzi unaendelea zaidi ya makao makuu. Hotuba ya Rais kwamba Bunge hili liendeleze utaratibu wa kupanua nafasi ambayo inajumuisha hata jamii zile ambazo ziko katika maeneo ambayo hayawezi kupata haki kwa sababu ya uchache kama vile Wateso Wakuria na sehemu zingine kama Mlima Elgon kuna haja ya Katiba hii nikitumia eno ya Rais " we should revisit ." Kuna mambo ya kurejelea. Wakati ambapo tulikuwa tunajadili Katiba hii tulisema kwamba asilimia theini ni nzuri lakini asilimia ishirini ina matatizo. Katika hiyo asilimia ishirini napendekeza kwamba Bunge hili tupate nafasi nzuri ya kuendeleza ugatuzi huu ili hiyo asilimia iliyobaki ikiwemo kuweka sheria ambazo zitahakikisha kwamba kuna kuendelea kugatua hata zaidi ili watu ambao wanatoka katika jamii ndogo wapate haki yao. Ningependa kutoa mfano. Juzi katika uchaguzi wa Spika kule Migori County Mkuria alipata kiti halafu akapigwa akanyang'anywa na hakuwa na mtu wa kumtetea. Jambo kama hili litakaporuhusiwa kuendelea basi itakuwa hakuna haki tutapata sisi ambao tunatoka katika jamii ndogo. Kwa hivyo Hotuba hii ya Rais haswa ikilenga suala hili la ugatuzi ilinisisimua sana na nikajua kwamba hili Bunge litawaokoa wale ambao sehemu zao hazisikiki kwa sababu ya jinsi ambavyo mfumo huu wa ugatuzi ulivyo. Nisingependa kusema eno mengi kwa sababu najua wengine watachangia. Ni vizuri kwamba tumepata nafasi hii ya kuwaakilisha watu wetu. Asanteni sana watu wa Kuria East kwa kunichagua. Naamini kwamba nitawatumukieni kwa njia iliyo bora. Naomba Mwenyezi Mungu atusaidie. Asanteni kwa kunisikiza.
Asante sana Mhe. Spika. Mimi mwenyewe na familia yangu na wananchi wa Lamu Magharibi ambao ninawaakilisha tunatoa risala za rambirambi kwa marehemu Seneta Kajwang'. Mungu amuweke mahali pema peponi. Pia ni vizuri tulichukue jambo hili na tujue kwamba mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe kama vile Seneta Otieno Kajwang' amekaa na ndugu yake Raila Odinga mpaka kifo chake kilipofika. Asante sana Mhe. Spika.
Asante sana Mhe. Spika. Mimi ni Mhe. Lodepe Nakara Mbunge wa Turkana ya Kati. Nimesimama kuunga mkono Hoja hii lakini ningependa kusema kwamba siyo lazima tuongee Kiswahili sanifu. Iliyo muhimu ni kuwasiliana. Kwa hivyo nawatia Waheshimiwa moyo. Tunapoongea tujulikane tunawasilisha ujumbe fulani. Haijalishi lugha ambayo unatumia kwa maana yule mtu anayekutazama angependa kuelewa. Pili tutakuwa tunatia watu wetu morale ya kutazama runinga waone vile ambavyo tunaongea. Watu wetu watakuwa wakitazama runinga nyumbani waone vile waheshimiwa wanajadili mambo ya taifa kwa sababu wengine hawajui Kiingereza. Tutakapokuwa na siku moja ya kujadili Hoja zetu kwa lugha ya Kiswahili tutawapatia watu wetu morale ya kutazama runinga ili wafurahi. Naona ya kwamba jambo hili ni nzuri. Mhe. Spika kama walivyosema wenzangu jina lako litaingia kwenye vitabu vya kumbukumbu kama mmoja wa Waheshimiwa Spika katika Bara la Afrika waliotafi Kanuni za Kudumu za Bunge la Taifa kwa lugha ya Kiswahili. Kwa hayo machache ninaiunga Hoja hii mkono.
Asante sana Mhe. Spika. Mwenzangu Mbunge wa Gatundu Kusini ametatizika sana kwa sababu ya hali ya usalama hapa nchini na umuhimu wa kuwa na maafisa wa usalama kwenda kwenye mafunzo ili waweze kufanya kazi kama vile Serikali ya Jubilee ilivyoahidi. Ijapokuwa ni hivyo na haswa sisi wenye kutoka maeneo ya mpakani tunapendelea sana kuwa maafisa hawa waende mafunzoni haraka iwezekanavyo ili waje wafanye kazi ya kuwalinda Wakenya haswa wakati huu ambapo tumekuwa na matatizo mengi hapa Kenya. Kulingana na kanuni za Bunge hili Mbunge huyu wa Gatundu Kusini ambaye bado ni mgeni hajaelewa sana kanuni zinavyosema na kwa hivyo ni vizuri Wabunge wenzangu wamuelewe. Sisi sote tunaumwa na roho kuwa maafisa hawa hawajaenda bado kwenye mafunzo hayo lakini vile vile ni muhimu tukumbuke kwamba ni lazima tugawanyane majukumu mahakama wafanye kazi yao na sisi Wabunge pia tufanye kazi yetu. Kitu ningeomba ni mahakama iharakishe ili wale waliochaguliwa kwenda kwenye mafunzo waweze kwenda haraka iwezekanavyo. Vile vile Mhe. Spika wewe kama Spika wetu umekuwa ukiheshimu kanuni za Bunge na sheria za nchi hii kwa hivyo hakuna sababu ya mtu yeyote kusimama kukulenga na kukurushia eno ambayo si ya haki na ambayo ni bughudha. Mhe. Spika ninaomba wenzangu tutulie tumuelewe mwenzetu na tutulize zile duku duku tulizo nazo kuhusu maafisa hawa. Asante sana.
Asante sana Mhe. Spika. Na mimi pia nasimama kuunga mkono wenzangu na kukubaliana kuwa kuna umuhumu wa sisi kijadiliana kuhusu sheria hii ambayo tunaenda kupitisha ya ugawaji wa pesa kulingana na Katiba ambayo ilipitishwa 2010. Katiba hii imetupatia nafasi ya kuwa na serikali za ugatuzi na vile vile serikali ya juu. Bila shaka Wakenya sasa hivi watakuwa na hali ya wasiwasi na hali ya kuhangaika mpaka tuzoee kuwa kuna serikali za aina mbili; serikali ya kitaifa na serikali ya ugatizi ambayo iko mashinani. Kitu ambacho kinanifurahisha zaidi ni kuwa pia katika maeneo yale ambayo yamebaki nyuma yaliyo duni kimaendeleo kuna pesa ambazo ni za kusawazisha hazina ambayo imewekwa ya kuweza kusawazisha maeneo yale kimaendeleo ili tuweze kukimbizana na maeneo yale ambayo yako mbele kimaendeleo. Kwa sasa hivi pesa ambazo watu walikuwa wamezitarajia ni nyingi lakini yote hayo ni kwa sababu hakuna mtu anayefikiria kuwa hesabu itakayotumika itakuwa ya mwaka gani. Tuko mwaka wa 2012/2013 na zile pesa zinazotumika ni zile zilikuwa zimetafutwa Serikalini mwaka wa 2011/2012. Wote wanaangalia kuona vile tutaanza shughuli hizi. Ninakubaliana na wenzangu kwamba tukianza shughuli hizi za kuhakikisha kwamba ugawaji wa pesa unatekelezwa sawa sawa kutakuwa na migongano na malalamishi kati ya tume ambayo inasimamia ugavi wa pesa Serikali ya Kitaifa na serikali za ugatuzi. Tume hii ambayo inashughulikia masuala hayo lazima itagongana kidogo na Wizara ya Fedha kwa sababu hawajafanya kazi pamoja. Hii ndio sababu kipengele cha 199 cha Katiba kinasema watu wajadiliane na wazungumze ili wasikosane. Kulitalajiwa kwamba wakati wa kuanzisha masuala haya ni lazima kutakuwa na hali ya wasiwasi. Mheshimiwa Spika kazi na majukumu ya Serikali ya Kitaifa yamewekwa katika Fourth Schedule ya Katiba. Pia kazi na majukumu ya serikali za ugatuzi yameonyeshwa. Inafaa magavana waelewe majukumu yao na yale ya Serikali ya Kitaifa. Haya ni maswala mapya ambayo yameanza wakati huu. Kwa hivyo ningependa kuomba Wabunge wa Bunge la Kumi na Moja tukae pamoja tujadiliane na tuwaruhusu wananchi watuelezee mambo ambayo wanataka tuyatekeleze katika Bunge hili. Jambo la kusikitisha sana ni kwamba katika serikali ya ugatizu kuna bunge la kauti. Hili bunge linaweza kupatiwa makadirio yao ili kila atakayeangalia ajue kwamba bunge lile lina uhuru na haki ya kufanya shughuli zake bila kusumbuliwa na wale wanaosimamia serikali ya ugatuzi. Sisi ambao tuko katika upande wa Serikali tungependelea kufanya kazi na wenzetu ambao wako katika upande mwingine. Sisi wote ni Wabunge. Wale walio wengi na wale walio wachache ni wanachama wa Bunge hili la Kumi na Moja. Kuna umuhimu wa sisi kufanya kazi pamoja. Tumechelewa sasa hivi kwa sababu Kamati ambayo ingeangalia masuala haya bado haijaundwa. Ningependa kuwaomba wenzangu tuungane ili tuangalie masuala haya yanayohusu shughuli hizi ambazo zitawezesha si tu Serikali ya Kitaifa bali serikali za ugatuzi kutekeleza majukumu yao bila shida yoyote. Mwanzo huwa mgumu lakini watu wakifanya kazi pamoja inakuwa rahisi. Hii ni kwa sababu hili ni jambo geni. Ni hivi majuzi magavana Wabunge na wawakilishi wa kauti walichaguliwa kwa mara ya kwanza katika nchi yetu. Hili si jambo la kawaida.
Asante sana Mhe. Spika. Nami pia najiunga na wenzangu kupinga Mswada huu ambao unarekebisha Kipengele cha 81 cha Katiba. Si utani kuwa Kipengele cha 81 kiko pale si utani kuwa Kipengele cha 27 kiko ndani ya Katiba haswa kwenye ukurasa wa masuala ya haki za kibinadamu. Hakuna uwezekano kuwa Wakenya wataweza kufanya shughuli za kimaendeleo na uongozi bila kuhusisha akina mama walemavu ama wale ambao ni wanyonge katika jamii na ulimwenguni ili kupata suluhu kwa masuala mengi yanayowakabili Wakenya. La kusikitisha ni kwamba wengi wetu tumeongea mara kwa mara kuhusu jambo hili ambalo linahusu Wakenya wote na hata ulimwengu mzima. Ni suala ambao limeleta kero kwa wale wengi ambao wameachwa nje bila kuhusika kwenye masuala ya uongozi nchini. Mhe. Spika ni wazi kwamba Katiba hii ambayo tulipata mwaka wa 2010 iliongeza idadi ya akina mama Bungeni. Haikuongeza idadi inavyotakikana lakini mabunge ya magatuzi yameweza kupata idadi ya akina mama inavyostahili. Katika Bunge la taifa na Bunge la Seneti tunasikitika kuwa idadi ya jinsia moja haikufika theluthi moja ambayo imetajwa katika Katiba. Ninayosema si utani. Wakenya walifanya uamuzi. Wakati huo nilikuwa na wasiwasi sana kuwa hatukuweka kipengele cha kutuonyesha jinsi idadi hii itafikiwa. Niliona kama kungekuwa na tatizo. Ukweli ni kwamba tatizo hilo tunalo sasa. Tuna wasiwasi kuwa mahakama yetu huenda yakaamua kwamba Bunge hili halijaridhia haja za Katiba yetu. Wakati ule nilikataa kuafikiana na kielelezo cha Katiba kwa sababu nilifikiri tutapata matatizo makubwa kupata suluhu. Niliona ingekuwa vigumu kupata nafasi zaidi za wanyonge katika Bunge hili. Idadi ya akina mama Bungeni yafaa kuongezwa kwa sababu wananchi ndio walifanya uamuzi. Ninayo furaha kuwa sasa hivi kuna akina mama 47 ambao wamekuja hapa kwa kupitia kipengele maalum ili waweze kuchukua viti ambavyo wao wenyewe wanapigania katika kusimamia uongozi. La kusikitisha ni kuwa bado Wakenya hawajaamua kuchagua akina mama wa kutosha. Kwa sababu ya masikitiko hayo niliyonayo ninawaomba ndugu zangu katika Bunge hili tushikane mikono pamoja ili tutafute suluhisho la tatizo hili. Mswada huu ulioko mbele yetu sasa hivi hautupatii suluhisho bali unatuweka kwenye matatizo. Mswada huu unanuia kwamba tatizo hili lishughulikiwe siku za baadaye. Hakuna Bunge lingine ambalo lingeweza kutatua tatizo hili. Hii ni kwa sababu Bunge hili hivi maajuzi karibu lipitishe idadi inayostahili ya theluthi moja tunayoulizia kikatiba. Theluthi moja siyo kubwa sana. Hivyo basi ninatumaini kuwa Mswada huu kama tutakubaliana uwekwe kando ili tuweze kupata Mswada wa kuleta sheria ambayo itatupatia suluhisho na idadi iweze kutimia. Hata kama tutakubaliana kusonga mbele pole pole basi Mswada huu usongezwe mbele baada ya sisi kupitisha idadi jinsi inavyotakikana katika Katiba. Haijalishi hata kama itakuwa ni asilimia 30 au 40. Hivyo tutakuwa tunakaribia kufikia kiwango hicho. Lakini kwa sasa hivi tukiacha mambo yabaki yalivyo itakuwa kama kwamba tunafunga mlango. Sisi hatutakubaliana kama Bunge la 11 kuwa hii ni sawa. Walemavu bado wako nje. Idadi yao haijatimia. Aidha idadi ya vijana haijatimia. Ninapinga Mswada huu nikiwaomba ndugu zangu haswa wale wa jinsia ya kiume tushikane pamoja tuweze kutekeleza suala hili na kupata suluhisho bila sisi kukosana. Sisi ni watu wa umoja na tuko Bunge la 11 siyo tu kwa bahati na sibu. Wananchi walituchagua na kutupatia nafasi hii ya kuwawakilisha katika Bunge hili. Naomba kupinga Mswada huu.
Asante sana Mhe. Spika. Nami pia nataka kutoa risala zangu za rambirambi kwa jamii ya Senator Otieno Kajwang' seneta wa Homa Bay kwa jamii yake pamoja na watu wote wa Homa Bay na Wakenya kwa ujumla. Risala zangu za rambirambi si zangu tu bali ni za eneo Bunge la Taveta na watu wake ambao pia wanamfahamu Senator Otieno Kajwang'. Alipokuwa Waziri wa maswala ya uamiaji alikuja mpaka kwetu Taveta mara kadhaa ili kutuwezesha kuwa na ofisi iliyofaa pale mpakani. Senator Kajwang' alikuwa ni mtu wa kupenda utani. Ijapokuwa alikuwa anapenda utani alikuwa ni mtu aliyechukulia kazi yake kwa bidii sana. Hivyo basi nataka kuunga mkono wenzangu kwamba Mwenyezi Mungu amweke pahali pema peponi na pale alipoenda afahamu kuwa ametuacha bado na mapambano ya kimaisha. Yeye ameenda mbele ya haki na ametutangulia ili kututengenezea njia.
Asante sana Mhe. Spika. Nami pia ningependa kuunga mkono wenzangu wengi ambao wameongea kuhusu Mswada huu. Kutoka mwanzo mimi niko hapa kupinga vikali sana Mswada huu ambao umeletwa na Mhe. Chepkong'a. Napinga Mswada huu kwa sababu umeletwa eti utekeleze matakwa ya Katiba. Wakati Katiba ilikuwa ikitengezwa maoni yalitolewa na Wakenya wengi. Kwa wakati huo tulisema kuwa "Wanjiku Kadzo Anyango Chebet Kibet na Onyango wameongea. Haikuwa ni eno ya Wabunge zaidi ya 300 ambao tuko katika Bunge hili la taifa. Wakenya walifikiria kuwa hapo awali kulikuwa na dhuluma za kihistoria katika mambo ya uongozi. Tunajua akina mama wamenyanyaswa kwa misingi ya desturi zetu tamaduni zetu na hata dini zingine ambazo zinasema kuwa kazi ya mama ni ya nyumbani kama vile kupika kufua na pengine kumstarehesha mzee. Kweli tunakubali kwamba kuna zile kazi ambazo ni mwafaka kwa kina mama kuzifanya. Lakini wakati huu nchi yetu katika Riwaza 2030 ilizungumzia kuwa akina mama ni lazima wajenge uwezo kisiasa kijamii na pia kiuchumi. Iwapo tutapitisha Mswada ambao unasema eti tutatekeleza sheria hii ya Katiba pole pole pasina kutueleza kinaga ubaga njia mwafaka itakayotumika watueleze ni kwa muda gani tutatekeleza na ni idadi ya asimilia ngapi ambayo itaweza kuwekwa kuhakikisha kwamba zaidi ya thuluthi mbili haitakuwa ya jinsia moja. Tunawapenda sana ndugu zangu Wabunge wanaume. Nataka niwaambie kwamba Mswada huu ni wa akina mama. Ni Mswada wa jinsia kumaanisha kwamba itafika wakati ambapo nyinyi pia mtahitaji kusaidika na Mswada huu. Kwa hivyo unapochimba kisima usije ukaingia wewe mwenyewe. Sura ya 27(8) inazungumzia kuwa Serikali iweke mikakati na sera zitakazohakikisha kwamba makundi ambayo yalikuwa yametengwa katika jamii ambayo tunaita kwa Kiingereza affirmative groups yatafikia uongozi na kuwa sawa na zile jinsia zote. Iwapo sisi ni wakweli kama watunzi wa sheria katika Jamhuri yetu ya Kenya lazima tuweke sheria za ukweli. Tusiweke sheria tu ati kwa sababu tumesikia Bunge litavunjwa iwapo hatutaweka sheria hii. Mahakama Kuu tunayoiita kwa Kiingereza Supreme Court ilitupatia mawaidha na kusema tutengeneze sheria mwafaka itakayotupatia njia sahihi ya kueleweka na kuhakikisha kwamba sheria ambayo iko katika Sura 81 imetekelezwa. Kwa hivyo tukisema tunapitisha Mswada huu bado hatujafanya jambo lolote. Bado tutarudi nyumbani hivyo hivyo. Sasa tunasikia kuwa kuna kesi. Kama tutaendelea kwenda hivi basi sisi tutakuwa mashakani sana kuweza kuhakikisha kuwa ukweli umepatikana. Tuna mifano mingi. Mhe. Rais alimteua Mama Amina Mohamed katika Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje. Leo hii alijengeka uwezo mpaka sasa anataka kupigania kiti kikubwa katika Umoja wa Mataifa ya Africa nzima. Kama hangeteuliwa na kupewa kiti kama kile angepata nguvu gani za kumwezesha kusimama? Mifano tunayo. Mhe. Cecily Mbarire kwanza aliteuliwa kisha akaweza kusimama na sasa atakwenda kupigania kiti cha ugavana. Hiyo ndio njia. Mimi mwenyewe nimechaguliwa kama mwakilishi wa akina mama. Nimepata nguvu nimejenga uwezo na sasa nitapambana na yule Mbunge wa Eneo Bunge la Likoni. Najua nitaweza na nitakuja katika Bunge hili kama Mbunge wa Likoni. Kwa hivyo ndugu zangu akina baba hamuoni raha nyinyi tukiwa hapa Bunge tumekaa sako kwa bako mama hapa na baba pale? Sasa hivi mumeniona nimekaa hapa na Mhe. Bedzimba yupo karibu na mimi. Hata wakati anachangia ana raha kwa sababu Waingereza walisema " unlike poles attract like poles repel" . Haya si eno ya kuzungumza tu ya sayansi. Ni lazima jinsia zikiwa pamoja mambo huenda sambamba na tukaweza kujenga nchi yetu.
Asante sana Mhe. Spika. Naomba kuunga mkono Kamati hii ya Haki na Sheria ambayo kusema ukweli ilikuwa hapo awali lakini kwa sababu moja au nyingine ikabidi wanakamati wa CORD watolewa kwa muda. Tuliyaweka na kuyachukulia maanani maamuzi yako. Wakati mwingine lazima tupewe mwelekeo. Tumekubali hawa wanakamati wajiunge na wenzao wa upande ule mwingine ili wapate kutimiza majukumu yao. Kamati hii naiona ni ya wasomi kwa maana wengi wao ni wana sheria. Nina ii kwa sababu itakuwa ikiangalia mswala kadhaa ya sheria. Kama ujuavyo sheria inavipengele vyake ambavyo mtu asipo vitafi vizuri vinaweza kutuletea sisi Wabunge shida. Tumejaribu tuwezavyo na ni ombi langu kuwa kamati hii itaendelea na kazi yake mahali ilipokuwa imefikisha. Hivi sasa kuna kazi muhimu ya kuangalia mambo ambayo yasipoangalia vizuri yanaweza kuelekeza nchi hii vibaya. Kamati hii kwangu ni ya umuhimu sana. Naomba mwenyeketi wake Mhe. Chepkong'a awakubali wenzake waendelee na kazi. Awajibike ya kutosha kuwaelezea yale walitimiza wakati walikuwa nje kidogo ili washike dau pamoja na kumaliza kazi bila shida yoyote. Mhe. Spika naomba kuunga mkono.
Asante sana Mhe. Spika. Nashukuru kwanza kwa mwelekezo wako kuhusiana na karatasi hii. Pili hii karatasi hawakutupatia sisi tulipokuwa katika kikao cha Bunge. Tulikuwa tumeitwa kama Wajumbe wa Pwani. Katika hali ya kuuliza hii karatasi waliitoa pale. Sio kuwa tumeitoa katika kamati. Tatu nasisitiza tena ya kuwa lao nia na madhumuni yao ni kuhusiana na mambo ya wafanyikazi. Kwa nini yale maswali yote ambayo tumeyauliza si mara mora si mara mbili bali mara tatu majibu ambayo yameletwa katika Bunge hili wakakubali ya kuwa kuna matatizo na wakasisitiza ya kuwa watabadilisha sheria? Mpaka leo hawajafanya jambo hilo. Licha ya hayo wamejaribu kupenyeza mambo kwa njia ambayo sio mwafaka. Asante sana Bw. Spika.
Asante sana Mhe. Spika. Nasimama kuunga mkono Hoja hii moyo wangu ukiwa na uzito na roho yangu ikiwa na wasiwasi. Hatuwezi kufanya kazi katika Bunge hili kama wanasarakasi badala ya kama Wabunge. Sheria zetu katika Katiba zinaonyesha mujibu au kazi ya Wabunge. Tuko hapa kwa sababu Wakenya wametupatia fursa ya kuwafanyia kazi si kwa kubahatisha. Katika hali yetu ya utendakazi kuwa Mwanakamati ni haki ya Mbunge na ni haki ya yule anayewakilisha Wakenya ili kufanya kazi iliyopo hapa. Si sawa kuwa tunafanya kazi zetu kwa kufuatilia njia za vitendawili sarakasi na vitimbi tukifikiria kuwa hiyo ndiyo kazi iliyotuleta hapa Bungeni. Ninastaajibika sana kuwa viongozi wa waliowachache Bungeni walitatizika sana wakiona kuwa kuna Wabunge waliochukua msimamo wa kuendelea kukaa kwenye vikao vya Kamati inayoshughulika maswala ya kisheria kwenye Bunge la Kumi na Moja na wakaanza kuwafurusha wenzao. Hivyo basi kuna umuhimu wa viongozi wa waliowachache na waliowengi Bungeni kujua kustahamili na kujua kuwa kila mahali kuna upinzani. Hata katika jamii zetu huwa kuna upinzani. Lakini bali na upinzani ni vizuri kukaa na wenzetu na kuweza kuzungumza nao ili watu wafanye kazi pamoja na waakilishe wenzao. Nastaajibika kwamba suala la Mbunge ambaye alikuwa amekosea na kuondolewa hapa Bungeni mmelituma kwenye Kamati ya kusimamia nidhamu ya Wabunge hapa Bungeni. Hivyo basi Wabunge wale wale ambao ni viongozi wa waliowachache wamepiga debe na vigelegele na kuwa na furaha kwa sababu Bunge hili linalazimishwa kufanya kosa la kukubaliana na mtu ambaye alifanya makosa na katika hali ya kuadhibika amerudishwa na korti ile. Sio kawaida kwa Wabunge wote kukimbia kortini kuwezeshwa kutekeleza kazi zao kwa niaba ya wale waliowaakilisha hapa Bungeni na kuhakikisha kuwa Wabunge watatekeleza masuala yaliyowaleta hapa kwa muhula huu ambao ni muda wa miaka mitano. Nakubaliana kuwa si sawa kwa sisi watu wa upande wa Jubilee peke yetu kutekeleza kazi za Kamati ile kama wenzetu hawapo. Nimefurahia kuwa wanarudi kwenye kazi lakini juu ya hayo ningeomba viongozi wa waliowachache Bungeni wajue kustahamili uvumilivu na wajue uongozi ni kuweza kuzungumza na wenzi wao kuhakikisha kuwa Wabunge wote wanafanya kazi. Mnavyojaribu kupigia debe suala hili la yule Mbunge aliyeadhibiwa ningependa hata nyinyi mkumbuke wale Wabunge mliowacha nje kwenye Kamati muwape nafasi wafanye kazi ili watekeleze majukumu yaliyowaleta hapa Bungeni. Naunga mkono Hoja hii.
Asante sana mhe. Spika. Nasimama kuunga mkono suala hili la kuongeza muda ili kesho tuweze kupata kikao haswa kufuatia kanuni za Bunge hili; tutatumia Kanuni ya 30(3)(b) ili tuweze kuzungumza na kuhakikisha kwamba kazi ambazo zimetuleta hapa zinamalizika kabla ya kwenda likizo. Masuala ambayo Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni ameyataja ni muhimu na itakapofika kesho jioni wakati tunaenda kusherehekea pasaka tujue kuwa tutarudi katika muda ambao umefaa; inafaa tuwe tumemaliza masuala yote ambayo yatakuwa kwenye kamati na hatua ya tatu. Tunataka tuende tukiwa katika hali ya utulivu na kuweza kuzungumza na waliotuleta kwenye Bunge hili bila wasiwasi. Asante sana mhe. Spika na naunga mkono.
Asante sana Mhe. Spika. Nataka kujiunga na wenzangu kutuma risala za rambirambi kwa jamii na marafiki wa marehemu Seneta Otieno Kajwang'. Niligadhabishwa na kifo chake punde tu nilipofungua runinga asubuhi na kupata matangazo hayo. Alikuwa mcheshi mpenda watu mtu wa watu na hakika wengi watamkosa. Wafuasi wa ODM katika eneo bunge langu watamkosa marehemu Mhe. Seneta Otieno Kajwang'. Naomba Mwenyezi Mungu akalijalie kaburi lake kuwa bustani katika mabustani Amina.
Asante sana Mhe. Spika. Nataka nijulishe Nyumba hii kwamba Mjumbe ambaye ametumwa na akaleta stakabadhi za wenye kutaka kufanya hiyo konferensi hapa. Naomba Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni anizikilize.
Asante sana Mhe. Spika. Nataka pia kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Kamati ya Kiidara ya Utawala na Usalama wa Kitaifa. Ni dhahiri ya kwamba Meja Mstaafu Shadrack Muiu Mutia amefanya kazi nzuri hapa nchini. Lakini kama tunavyosema; maisha ya binadamu hubadilika kila siku. Kuna wakati ambao utakuwa mzima na wakati ambao utakuwa na shida na hutaweza kutekeleza majukumu yako. Hakuna aliyetaja kuwa Meja Mstaafu Shadrack Muiu Mutia hajafanya kazi yake vizuri kwa utendakazi wake. Lakini maisha ya mwanadamu yanazidi kubadilika Katika Katiba yetu Kipengele cha 251 kimetaja uwazi kwamba atakaposhindwa kutekeleza majukumu ya kufanya kazi hana budi kustaafu. Ninaunga mkono Ripoti hii kwa udhaifu na kuwaomba wenzangu kwa unyenyekefu kwamba tukiangalia Kipengele kile na kazi nzuri Meja Mstaafu Shadrack Muiu alifanya Kamishna wa Tume ya Kitaifa ya Kuwaajiri Polisi amefanya kazi nzuri katika utenda kazi wake. Kimaumbile Meja Mstaafu Shadrack Muiu Mutia hawezi kuendelea kufanya ile kazi sasa hivi. Kamati ilijaribu sana kumtafuta ili aje ajieleze. Lakini Mwenyekiti wa Kamati kwenye masuala kama haya mkiambiwa mtu ni mgonjwa ingelikuwa ni vizuri pia kama mngekwenda kumsalimia nyumbani ili mjue ako hali gani na katika hali ya kiutu na kibinadamu bwana huyu ana tatizo kubwa kiasi gani. Nafikiria hakuna Kanuni za Bunge hili yaani Standing Orders ambazo zinawaruhusu kwenda mpaka nyumbani kwa mtu kuangalia ni shida gani iliyomfanya bwana au mfanyakazi huyu kukosa kuja hapa Bungeni katika utenda kazi wake. Hivyo basi kama wangelipata habari kwamba yuko hospitalini wangekwenda pale. Kuna umuhimu kwamba Kanuni za Bunge hili zibadilishwe kuwaruhusu Wabunge wanakamati fulani kuwatembelea wafanyakazi kama hawa ili tuwezekujua mbivu na mbichi. Nimemsikia ndugu ya Kiongozi wa Wachache Bungeni Mhe. Nyenze akilalamika. Lakini juu ya kulalamika ni kwamba kazi lazima itendwe na ifanyike vilivyo. Roho yangu ikiwa nzito ningependa kumwambia kaka yangu ndugu yangu kiongoze Mhe. Nyenze kwamba ni lazima kazi ifanywe hata tukilalamika vipi. Mhe. Spika tulimpoteza Kamishna Esther Colombini aliyekuwa mama mchapa kazi. Alivyofariki mtu mwingine hajapatiwa jukumu la kutenda kazi ile. Amekwenda mbele ya haki Vile vile ilimbidi dada yetu Naibu Kamishna wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi Bi. Grace Kahindi kustaafu. Kusema kweli Tume hii inashindwa kufanya kazi. Hivyo basi hatuna budi kuunga mkono mapendekezo ya Kamati hii tukiomba kwamba hatuna njia nyingine ila kuhakikisha kuwa majukumu ya kufnaya kazi lazima yatendeke na kazi itendeke. Mhe. Spika hatuna njia nyingine ila kumwoomba Mhe. Rais aunde tume itakayoangalia matatizo haya na kupendekeza njia ya kumsaidia na vile vile kumpatia Mkenya mwingine nafasi ya kufanya hii kazi. Kwa masuala ya Kaunti ya Makueni hivi juzi tulisikia Mhe. Rais akisema kwamba haoni kama hiyo ndiyo njia ya kuisaidia Makueni. Vile vile kwa tume itakayotengenezwa kuangalia masuala haya ya Meja Mstaafu Shadrack Muiu wakipata habari kwamba anaendelea vizuri basi Mhe. Rais ataamua. Mhe. Spika ninaomba wenzangu wote tuunge mkono Hoja hii ya kumuruhusu Meja Mstaafu Shadrack Muiu
Asante sana mhe. Spika. Nataka pia nichukue nafasi hii nikupongeze kwa kuchaguliwa kama Spika wa Bunge hili. Vile vile ningependa kuchukua nafasi hii kuwashukuru watu wa Kilifi Kaskazini kwa kunipatia nafasi kuwa mbunge wao wa kwanza katika eneo hilo jipya la Bunge. Mhe. Spika katika kuchangia Hotuba ya Rais ningependa kutilia mkazo jambo ambalo ndugu yangu Aburi amelizungumzia; hasa upeanaji wa tarakirishi kwa watoto wa darasa la kwanza katika shule zetu za msingi. Nafikiri ijapokuwa Rais ana maono mema katika kuanzisha mradi huu wa tarakirishi kwa watoto wetu wa darasa la kwanza ingekuwa vyema ikiwa Rais badala ya kuwapatia wanafunzi wa darasa la kwanza tarakirishi hizo ambazo zinaweza kuhatarisha usalama wa watoto wetu wadogo badaye Kwa sababu watu watajaribu kuwapokonya. Hata zinaweza kuibiwa zikiwa nyumbani. Watu wanafikiria ni vifaa ambavyo vinaweza kuwasaidia kwa njia nyingi. Serikali ingejenga mahabara katika shule zetu zote za msingi ile watoto wetu wa kutoka darasa la kwanza hadi la nane waweze kufaidika kutokana na mradi huu wa tarakirishi. Vile vile mhe. Spika ningetaka kuzungumzia kuhusu Hotuba ya Rais hasa kuhusu swala la ardhi. Sisi watu wa Pwani swala la ardhi ni swala nyeti sana. Watu wa Pwani wamekuwa maskwota tangu wakati wa uhuru wa nchi hii. Swala la ardhi katika
Asante sana Mhe. Spika. Naunga mkono Ombi hili kuhusu mateso ambayo wakulima wetu wanapitia. Ni kweli mkulima wetu anapitia mateso mengi kwa sababu unapolima shamba lako unatarajia kupata mavuno kama vile sisi tunavyokuja Bunge tunatarajia tupate mshahara wetu. Wakulima wa Kenya wanaendelea kupata mateso awe ni mkulima wa miwa au wa mahindi kwa sababu hapati mavuno ambayo anatarajia. Hili ni jambo ambalo tunafaa kulichukulia maanani kwa sababu mkulima akilima shamba lake anategemea mazao hayo kufanya kazi kwa mfano kulipia watoto wake karo ya shule na kulima shamba tena arudishe mazao ndani. Si vyema Serikali tukufu iwache wakulima kama hao wateseke. Kwa mfano tulikuwa sehemu ya Eldoret mwezi wa tatu mwaka huu na kusema kweli tulipata wakulima wakiwa na malalamiko ya kutolipwa na huo ndio wakati walikuwa wanajitayarisha kulima tena mashamba yao. Ingawaje Serikali ilitoa pesa kwa kiwango kikubwa na ikaongeza bei ya mahindi unapata kwamba anayenufaika kwa kupata mapato kutoka kwa malipo haya si mkulima wa kawaida. Unakuta kwamba ni watu wengine waliagiza mahindi kutoka nje ya nchi hii ndio waliopeleka mazao hayo kwa stoo hizi na wakanufaika badala ya mkulima wa kawaida. Hili si jambo zuri na ninawaomba Wabunge wenzangu wachukulie jambo hili kwa hali ambayo inatakikana ili mkulima asiendelee kupitia mateso anayoyapitia. Kwa mfano wakati huu tunapoongea sio mkulima wa mahindi tu anayeteseka peke yake lakini hata mkulima wa miwa pia anateseka. Unakuta kuwa hata viwanda vyetu vinaanguka kwa sababu ya hali hii na si vyema.
Asante sana mhe. Spika. Ndugu yangu mhe. Aburi ameongea mambo mazito. Kwa sababu ametumia lugha ya taifa ingekuwa vizuri nami nimfuatilie kuongea kwa lugha hiyo. Jambo la kwanza ambalo ningependa kusema ni kwamba nakubaliana na Hotuba ambayo Rais Uhuru Kenyatta alitoa hivi majuzi alipohutubia Bunge hili. Ukiangalia kwa makini shida zilizoko humu nchini zimeambatana na kuunganishwa na ufisadi. Nakubaliana naye kwa sababu ukiangalia sababu inayofanya idara ya polisi kutofanya kazi utagundua kwamba polisi wanakula mulungula njiani. Ukienda katika shule ambazo zina shida ya mtihani na ambako wanafunzi hawajapewa vyeti vyao utagundua kwamba sababu ni mtu fulani alikuwa anangojea apewe pesa ndio atoe vyeti hivyo kwa sababu ni lazima ale mulungula. Rais Uhuru Kenyatta amesema kwamba ni lazima uchumi wa Kenya uendelee kukua. Shida za uchumi wa Kenya haziwezi kutatuliwa bila ya kupambana na ufisadi. Sababu za msongao wa magari jijini Nairobi ni kwamba wale ambao walikuwa na jukumu la kutengeneza barabara miaka 30 iliyopita walipora hela na barabara hazikutengenezwa. Mhe. Spika nikija kwangu binafsi nina kesi kortini. Kesi hiyo inasema kwamba nimefuja Kshs132 milioni. Inasemekana kwamba pesa hizo zilitoka katika Hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge (CDF). Ninataka wale wanaohusika na kuchambua mambo ya ufisadi serikalini wanisikize kwa sababu kisheria siwezi kuongea yaliyo kortini. Nitaongea yale yaliyofanywa na Tume ya kupambana na ufisadi ambayo ilivunjwa. Jambo la kwanza wanalosema ni kwamba katika mwaka wa 2008 nilikuwa Bungeni miezi mitatu. Wanasema kwamba wakati huo nilichukua Kshs132 milioni nikaenda kununua sukari ambayo mimi nilitumia. Ningependa kusema kwamba wakati huo pesa nilizopata katika akaunti ya CDF ya Kitutu Chache zilikuwa Kshs24 milioni tu. Huo ulikuwa mwaka wa kifedha wa 2008/2009. Wanaendelea kusema kwamba nilifuja pesa hizo kutoka Agosti 2008 hadi 2009. Hela ambazo CDF yangu ilipata katika mwaka wa 2009/2010 ni Kshs54 milioni. Ukijumlisha hazifiki Kshs132 milioni. Jambo la pili ambalo ningependa kuzungumzia ni kwamba wale wanaotuchunguza katika ufisadi ni lazima wafuate sheria na wahakikishe kwamba kuna ukweli. Pia ni lazima wajue kwamba mimi simhalifu hadi korti itakaponipata na hatia. Ni lazima wahakikishe kwamba wamepata ukweli wa mambo. Nawaomba wale ambao wana Ripoti iliyoletwa hapa Bungeni leo waangalie ukurasa wa tatu. Inasema kuwa nilifuja fedha za eneo Bunge la Kitutu Chache ambazo zilikuwa Kshs132 milioni. Hiyo ndiyo sababu walinipeleka kortini. Ukienda katika ukurasa wa 43 wa Ripoti hii wanasema-
Asante sana Mhe. Spika. Ni heshima kusikiza Mzee Angwenyi akizungumza katika Bunge hili kwa sababu ni mzee tunayemheshimu sana. Mimi binafsi ni mzee ambaye nimemjua na nimefanya kazi naye. Ningependa kusema kuwa ametupatia busara na masuala ambayo ameyazungumzia ni ya kiheshima. Jambo la kwanza ningependa kusema ni kwamba waandishi wa magazeti nchini Kenya wamechukua liwe jukumu lao kila wakati kuzungumzia mambo ya Bunge hili lakini wakiandika habari kuhusu Bunge hili zinakuwa za kupotosha kila wakati. Nafurahi kwa sababu ndugu zangu ambao wamezungumza wamesema kuwa tungependa waandishi wa magazeti wakiandika kama ni hela ambazo tunapewa kununua nyumba waseme kuwa nyumba hiyo ni lazima tuilipie kwa miaka mitano na ni pesa ambazo zinachukuliwa kutoka kwa mshahara wangu. Mshahara wangu ni Kshs640000 lakini pesa za kulipia nyumba hii ni Kshs600000. Kila Mbunge lazima atoe mshahara wake wote ndio anunue nyumba. Sisi tunasema tungependa tulipiwe mahali ambapo tunaishi. Kwa kizungu tunaita house allowance . Kama mfanyakazi wa serikali yoyote sisi tuwe na uwezo wa kuishi. Jambo la pili nitakalosema ni ukiangalia Tume ya Huduma za Mahakama (JSC) jaji anapewa nyumba gari na bima. Tungependa kusihi kuwa nasi pia masuala haya yaangaliwe. Kumalizia ningependa kumsifu ndugu yangu Mhe Junet Mohamed ambaye ameleta jambo hili tunalolizungumzia. Ningependa kumsifu ndugu yangu Mhe. John Mbadi ambaye amelizungumzia jambo hili. Ningependa kusema kuwa sisi tungependa kufanya kazi nzuri hapa Bungeni na tungependa kutimiza kazi kuhakikisha kuwa tumefanyia Wakenya kazi nzuri. Inatuhitaji tubadilishe sheria ili Bunge letu liwe na nguvu ya kufanya kazi. Kwa hayo machache nasema asante sana.
Asante sana Mhe. Spika. Ni masikitiko sana kwamba tunaregesha tena kuzungumzia suala ambalo sheria ina mkondo wake. Mfumo na ufunuzi wa kutengeza bajeti upo. Kuna kuchukuliwa kwa maoni. Inakaliwa na kamati husika katika Bunge. Mswada unaletwa hapa Makadirio ya Taifa yanajadiliwa mwisho yanaidhinishwa. Kila kitengo kwa taifa kinapata kitita chake. Baada ya hiyo ni matumizi. Kwa Waziri kutoa nakala yake ni udhofu wa nidhamu. Ni kuzembea kwa kazi. Haki ya Mkenya kwa leo inapatikana kortini. Sisi sote tukiwa na tatizo lolote tunaenda kortini. Hatua ya kujaribu kupunguza fedha waliotengewa korti ni kuhujumu mahakama kutoa haki kwa Wakenya. Mhe. Spika umesema kwamba tunapozungumza tutafute suluhu. Kuna Kamati husika ndani ya Bunge hili. Wamwite waziri wamuulize hatua yake inalingana na sheria ipi. Sisi viongozi ndani ya Serikali hatuwezi kukosana. Ni kama meno ya mbwa. Tuko marafiki kufa kuzikana lakini ikifika hatua zingine tunaona kwamba wanahujumu utendakazi na upeanaji wa haki katika taifa la Kenya. Kwa hivyo ningependa kamati husika kumwita Waziri na kumuuliza maswali. Hoja ambayo inaibuka ni kwamba kiranja wa mahakama ametoa ilani kwamba kutasitishwa kesi zingine ama mahakama haitajadili masuala fulani. Wana haki? Sisi kama Bunge wakati kitita chetu kinaingiliwa na Serikali huwa tunafanya maandao. Taifa lolote haliwezi kuruhusu kitengo cha usalama na kitengo cha korti kikome kwa sababu itahujumu haki ya taifa. Sheria ni lazima ifuatwe. Tuliidhinisha pesa hizi na hata sheria ya matumizi inayojulikana kwa lugha ya kimombo kama "Appropriations Bill" ilipitishwa na hakuna kitengo ambacho kina uwezo wa kukiuka na kupindua isipokuwa Bunge hili. Yeyote anajaribu kufanya yale anavunja sheria. Mimi ninaunga Serikali mkono. Hiyo inajulikana wazi na sihitaji kuipigia sifa lakini inafika wakati lazima haki itendeke katika taifa la Kenya. Ndio sasa inanileta katika jambo lingine la kuzungumzia. Katiba tuliyonayo ambayo inalimbikiza mamlaka kwa kitengo kimoja cha taifa ni Katiba ambayo tunahitaji kama taifa ambalo linapiga hatua kuipiga msasa. Ninaweza kuzungumza kama mtu aliye na tajriba ya Bunge la Kumi ambapo mawaziri walikuwa ndani ya Bunge. Imefika wakati ambao ni lazima tuangalie Katiba tuliyo nayo - mawaziri watoke ndani ya Bunge kwa kuwa wao ndio wanajua matatizo ya wananchi. Kwa hivyo tusikejeliane hapa. Tuzungumze na tuseme waziri aitwe na kamati husika na hatua ichukuliwe mara moja ili mahakama ipate kitita chake. Asante.
Asante sana mhe. Spika. Nilikuwa nafikiria kwamba ni jamii ya Wameru tu imeumia. Hiki ni kitu cha kushitua sana. Ukweli wa mambo ni kwamba mwaka wa 2018 hakuna Mheshimiwa atarudi hapa. Ikiendelea vile ilivyo hata Rais wetu Uhuru Kenyatta hapati kura. Ni kwa nini? Juzi nilisikia sauti kwa kipasa sauti ikisema "Mhe. Rais karibu Rais wetu mpendwa". Nikashituka na nikajiuliza: "Kwani Uhuru amekuja kwangu bila kunijulisha?" Mhe. Spika kama nitakuita Rais Uhuru Muigai Kenyatta akija kwangu nitamwita nani? Ninaomba kama inawezekana kwa sababu Bunge ndio ngao ya nchi yetu hayo mamlaka ya gavana ni kama side mirror. Tutasema tuendeshe gari bila side mirror? Kwa nini ninasema hivyo? Ukiangalia zile pesa ambazo wamepewa ni kama kuchukuwa mtoto mdogo na umshindilie ugali na maharagwe hiyo ni kumpasua. Hizo pesa ni shida. Huko kwetu Meru ukikutana na gavana mtasimamisha magari kwa muda wa masaa mawili mpaka apite. Tukiuliza ni nani anakuja tunambiwa ni gavana! Bw. Spika tuna taabu ya kutosha. Wakati Wambunge walisimama kuomba kura kama Kabando wa Kabando alienda kule akasema "mkinichagua nitawaletea maji nitatengeneza barabara ile mali ambayo imevunja akina mama mgongo nitaleta hapa ile hospitali ambayo haina dawa na ile zahanati nitaleta hapa
Asante sana Mhe. Spika. Nilikuwa nimevunjika moyo nikifikiria labda Mhe. Spika anafikiria mimi ni marembo ya Bunge hili kwa sababu kila nikiinuka nanoa. Kwa hivyo ninakushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii kuzungumza machache kuhusu Marehemu Mutula Kilonzo. Mutula hawezi kusahaulika kwa sababu ya shughuli ambazo alikuwa akifanya. Mimi binafsi ningetaka kupeleka rambirambi zangu kwa sehemu yake ya uwakilishi Bungeni na pia kwa familia yake. Mhe. Mutula alikuwa rafiki yangu na hata aliwahi kuwa wakili wangu nilipokuwa nimedhulumiwa katika uchaguzi kule Matuga. Ni matumaini yangu kwamba watu watakuwa wastahimilivu na wanyenyekevu kwa sababu Mungu amesema wazi wazi katika Koran na Bibilia kwamba vyovyote vilivyo siku moja mtu atakufa. Mara nyingi sisi wanadamu hasa mtu anapokufa tunasahau kabisa kwamba amri ya Mungu inasema hivyo. Ni matumaini yangu kwamba familia yake marafiki zake na watu waliofanya kazi naye watamuombea ili aweze kuenda mahali pema peponi. Lakini mbali na hayo ninaunga mkono kwamba Serikali ihakikishe kwamba imejitoa wazi wazi na wale waliowekwa kuchunguza watatoa ushahidi wa
Asante sana Mhe. Spika. Ninakushukuru kwa kunipatia nafasi hii ili niongee machache. Ninawashukuru watu wa Matuga kwa kunipatia kipindi cha miaka minne na miezi miwili kuwatumikia. Ni ii yangu kwamba kutokana na kazi ilivyofanyika tutakuwa pamoja tena hapa mimi na wewe kwani nina ii pia kwamba wewe utarudi na kumbuka kwamba kura yangu ni yako. Kwa hivyo tutakuwa pamoja hapa mara tu baada ya uchaguzi. Mhe. Spika safari yangu ya kuja Bunge hili ilikuwa ndefu sana. Ilianza mwaka wa 2002 nikipelekwa huku na huku nikiibiwa hapa na pale na nikienda kortini na hakimu akiniambia kwamba mjadala wangu ulikuwa mzuri na kamili lakini mwisho uamuzi wake ni kwamba kila mtu arudi afanye kazi yake. Muda huo kazi yangu ilikuwa ni kukanyaga lami kwa sababu mwenzangu alikuwa Mbunge. Sikujua kwa nini mahakimu hao walitoa uamuzi huo. Mhe. Spika ninataka nikariri eno yangu niliyoyazungumza miezi minne iliyopita. Nilikwambia kwamba wewe ni dume kwa sababu kazi uliyoifanya ilikuwa kazi ngumu. Bunge hili katika Afrika nzima ndilo Bunge ambalo lilikuwa na madume na kama ungalikuwa kiongozi legelege wewe hata ungalijiuzulu kwa sababu Bunge hili lilikuwa na watu wakali mno lakini uliwahimili na ukatuongoza mpaka wakati huu. Kongole kwa shughuli zako nzuri. Mwisho ninawaombea wenzangu wote ambao wamekata shauri kurudia viti vyao. Ninaomba wafaulu. Nilipoingia hapa nilikuwa na hofu huenda watu wakapigana ndani ya nyumba hii. Kumbe ilikuwa hali ya kujuana vizuri na kutengeneza urafiki. Hivi sasa nina marafiki mia tatu na arubaini na nane ndani ya nyumba hii baada ya kukaa kwa huo muda wote. Mheshimiwa Spika ninataka nikushukuru kwa kazi nzuri uliyoifanya na Mungu atubariki sote.
Asante sana mhe. Spika. Ningependa kuunga mkono Hoja hii ilioko mbele ya Bunge hili letu kama kijana wa miaka 31 ambaye anajivunia kuwa kijana ambaye anahisi kudhulumiwa. Tumefanya kazi kubwa kuhakikisha kwamba kuna halmashauri ya kitaifa kuhusu vijana ambayo tulianza kuitetea tangu mwaka wa 2004 na ambayo ilipitishwa miaka minane baadaye; na haijawahi kupatiwa pesa na Serikali tukufu. Mhe. Spika hili ni jambo la kushangaza kwa sababu ni jana tu Bunge hili liliweza kupitisha makadirio ya Serikali ya mwaka wa 2013/2014. Na hii halmashauri ni mojawapo ya taasisi za Serikali. Mhe. Spika vijana walirauka na kupigania nafasi za uongozi kutoka mashinani hadi kiwango cha taifa wakati wa uchaguzi wa halmashauri hii. Uchaguzi ulipoitishwa na Waziri aliyekuwemo kulikuwa na tetezi kubwa sana; kulikuwa na makabiliano. Kuwapatia vijana nafasi ilikuwa ni njia moja ya kuwahusisha katika siasa lakini wakaonekana kama watu mboga uongozini. Lakini siyo hivyo. Hii halmashauri ya Kitaifa ya Vijana ni kama ile Maendeleo ya Wanawake. Inawapa vijana wasia mwafaka kujionyesha kwamba wao wana demokrasia na wanaweza kuwa na viongozi ambao watazungumza kwa niaba yao kwa sababu wamechaguliwa na vijana kama wao. Bw. Spika kipengele cha nne cha sheria ambayo imetengeneza hili baraza imesema kinaga ubaga yale mambo ambayo litafanya. Kwa mfano inasema kwamba baraza hili litakuwa likihusika katika kushirikisha miradi na mikakati ya kitaifa kwa vijana. Hili ni jambo muhimu kwa sababu watu wengi wamekuwa wakijaribu kuwasaidia vijana wetu lakini hata Serikali haijui ni nani anayefanya lipi na wapi. Kwa hivyo baraza hili litaweza kuwa na orodha ya miradi na mikakati na hata fedha ambazo zimetengewa vijana ndio tuwe na uiano kwamba tunaweza kuwasaidia vijana kama taifa.
Asante sana Mhe. Spika. Pia mimi sina budi kujiunga na wenzangu kuwapongeza kwanza kwa kuchaguliwa kwenye Bunge hili la 12 baada ya kinyang'anyiro kilichokuwa kigumu. Nataka pia kuchukua nafasi na fursa hii kumpongeza Mhe. Rais kwa msimamo wake wa dhati na kwa upendo wa nchi yetu na kutuliza wananchi kuwa kuna umuhimu wa watu kudumisha ai wakati huu tunavyoelekea kwenye uchaguzi wa tarehe 17 Oktoba. Wakenya wengi walipigwa na butwaa tarehe 1 Septemba wakati uamuzi ulipofanywa. Ulikuwa uamuzi wa kuridhisha. Uamuzi wa Mahakama ya Juu haukueleza kwa nini walifanya uamuzi ule. Wakenya wengi wamejiuliza maswali. Nashangaa nikisikia watu wanashangaa kuwa tunashangaa. Ukweli ni kwamba ukifanya uamuzi kama ule kuna umuhimu wa kueleza sababu. Wakenya walitoka kwa wingi tarehe nane mwezi wa nane kwenda kupiga kura ili kuchagua viongozi wao. Sisi ambao tuko hapa tuko kwa njia iliyo halali na tunaambiwa kwamba uchaguzi wa urais ulikuwa hauna uhalali. Vipengele kadhaa katika katiba yetu vimempatia mwananchi nafasi na fursa ya kuchagua viongozi wake. Si sawa kwa uamuzi kama ule kufanywa na tusiambiwe ni kwa nini. Mhe. Spika vile vile Wabunge waliochaguliwa katika Bunge hili la 12 wakumbuke kwamba wana jukumu walilopatiwa na wananchi wao ambao walitumia haki yao ya kidemokrasia kuwachagua kuja hapa. Bunge letu la kitaifa lina Wabunge wa pande zote mbili upande wa walio wengi na upande wa walio wachache. Kawaida kwa sasa hivi walio wachache ni wale ambao wako katika Upinzani. Jai muangalie msigeuzwe mkawa wanasarakasi ama wanavitimbi kwa sababu upande wa Bunge la Senate wenzenu wamekwenda wamechagua Spika. Wamerudi leo wamemchagua Naibu wa Spika lakini nyinyi mnaambiwa msifanye masuala yaliyowaleta hapa na haki yenu iliyowaleta hapa na msifanye kazi za wananchi waliowatuma hapa. Wanaowatuma wamewaona nyinyi kama watoto wadogo na hamjui mlilokuja kufanya hapa Bungeni. Ninawaomba ndugu zangu mkumbuke umuhimu wa uchaguzi uliotokea na kuwa wananchi waliwapatia nafasi. Mkumbuke kuwa mlipovyokuwa katika kile kinyang'anyiro kulikuwa na wengine pia ambao walikuwa wanastahili kupatiwa nafasi. Wewe ulibahatika kuwa Mbunge wa eneo lako kwa kuweza kuwawakilisha wananchi wako. Nitashangaa sana Wabunge hawa wakienda kwenye vikao vyao kwenye vyama wanashindwa kuwaambia wakubwa wao ukweli uliopo ya kwamba mmetumwa hapa na wananchi waliowachagua. Nawaomba ndugu zangu mkumbuke kuwa Rais Uhuru Kenyatta yuko kwenye kiti kihakika na ndio maanake Wabunge wa Senate wamekwenda kufanya vile wanavyotakikana kufanya. Nyinyi hapa ambao mko wengi kushinda wale mnashindwa nguvu na wachache. Wanawachezea kizungumkuti na mnakubali kuchezewa. Mhe. Spika ulimwengu una mambo mengi. Unaambiwa unavyozidi kukua ndivyo unavyoona mengi. Kuishi kwingi ndio kuona mengi. Nimechaguliwa sasa kwa mara ya nne na ninajua ya kwamba Mhe. Uhuru Kenyatta mpaka tarehe 17 mwezi wa 10 yuko kwenye kiti kwa njia ya halali na baada ya tarehe 17 tutakuwa tumepatiwa nafasi nyingine ya kuwa na rais ambaye atakalia kile kiti. Nina ii kuwa rais huyo sio mwingine bali ni Uhuru Kenyatta. Naunga mkono masuala yote ambayo rais aliyazungumzia haswa suala la ai suala la uchaguzi na kuwapongeza kina mama na nikimalizia kumpongeza dadangu Mhe. Teyiaa kwa kupatiwa nafasi ya kuwa Mbunge katika kaunti ya Kajiado. Mungu awabariki. Tufanye kazi iliyotuleta hapa. Asante sana Mhe. Spika.
Asante sana Mhe. Spika. Pia namshukuru rafiki yangu Pukose. Naomboleza kifo cha rafiki yangu. Tulikuwa na urafiki mkubwa. Alitoka katika Jimbo la Kiambu na watu wa Jimbo la Kiambu wako na machozi. Tukikumbuka vile alivyouliwa hapa katikati ya Nairobi ni jambo baya sana. Watu walishangaa kwa sababu alipigwa risasi akiwa pamoja na walinzi na dereva wake. Kabla ya kifo cha Mhe. Muchai alikuwa ameongea wazi kabisa kwamba kuna watu ambao walikuwa wakimfuata na walikuwa wakitaka kumuua. Hilo limesemekana. Alipouliwa ilisemekana kuwa alikuwa na sanduku ambalo walikimbilia kutoa kwa gari lake. Juzi nilimwona mhe. Muchai kwa runinga akiongea ukweli; alisema kuwa alikokuwa akifanya kazi yaani katika COTU kulikuwa na watu ambao walikuwa wanataka kumuua. Sisi kama Bunge la 11 hatutafanya kazi kama wakenya wanauwawa na hakuna kitu ambacho kinafanyika.
Asante sana Mhe. Spika. Pia nimesimama kuwapa kongole wale wote wameunga Hoja hii mkono ambayo kupitia naibu wako imetufanya tuzungumze kwa lugha ya Kiswahili. Naibu wako anataka Kanuni za Kudumu za Bunge zizinduliwe kwa lugha ya Kiswahili. Anaposema kwamba tunamshukuru Rais wa kwanza wa Kenya ambaye alitoa amri iwe haki ya wananchi kuongea kwa lugha ya Kiswahili Bungeni ni vyema pia kukumbuka kwamba Rais wa pili wa nchi ya Kenya Rais Daniel arap Moi pia aliendeleza Kiswahili na akakifanya mashuhuri. Sikumbuki siku moja alipoongea lugha ya mama katika kazi yake. Alikuwa na huo moyo. Tunampongeza katika hiyo hali.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika . Kwanza nataka kumtangaza Mheshimiwa Joyce kama mtu mwenye maono ya hali ya juu sana kwa sababu jambo hili lilikuwa linatakikana liletwe mapema.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika kwa fursa hii. Ninasimama kupinga Hoja hii kwa sababu kubwa ukiangalia Hoja hii haitoi mwongozo thabiti. Hoja hii inasema mashirika ya kiserikali yanapata mali kwa watu wanaoishi katika kaunti. Kitungo chochote kikiwa ni cha kawi au uchukuzi hata kile kiwanda kinachotengeneza risasi huko Eldoret kinatoka katika kaunti. Ni kitengo kipi cha uzalishi hakitoki kaunti? Hili ni swali la kwanza. Swali la pili ukisoma Hoja inasema hawa wanatoa mali gafi lakini hawapati faida kabisa. Kama kweli hawapati faida anavyodai aliyoileta Hoja ni kwa nini uhamishe upeleka mashinani shida hizi? Mhe. Naibu Spika jambo la tatu ambalo linanipa matatizo kuelewa ni kuwa anasema Serikali ya ugatuzi haina uwezo wa kiuchumi kisha anataka tuchukue mashirika ya kiserikali na tuyapeleka kule. Hapa anatuchanganya. Hoja hii haitoi mwongozo na nitaipinga. Miaka ya theini Benki ya Dunia ilitoa sera ya Structural Adjustment Programme ambayo imetunyanganya na kudhalilisha mashirika yote katika nchi hii. Leo mashirika haya yameanza kufufuka na tunataka kuyapeleka mashinani. Katika Serikali ya ugatuzi malalamiko ni mengi kama vile maswala ya fedha na sera. Ni vipi tutapeleka mashirika haya? Je tutakapokosa suluhisho kwa matatizo yanayotukumba njia rahisi ni kuyasukuma mashinani? Iwapo kuna matatizo ya kiuchumi tunastahili kutafuta suluhisho kama Serikali kuu. Utajiuliza mada ya Serikali kukuja na mashiriki ya Serikali ni nini. Kila shirika ambalo liko hapa lina lengo mada na maudhui.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika kwa hii fursa. Kwanza kabisa naunga mkono hii Hoja. Madhumuni malengo nia shabaha na mawazo tangu miaka ya 1960 1970 1980 1990 na kuenda mbele yamekuwa yakibadilika. Maanake mbeleni mfumo wetu wa elimu ulikuwa 7-4-2-3. Ukabadilika ukawa 8-4-4. Vilevile ardhi haijawachwa kwa maana wakati mfumo wa elimu unabadilishwa lazima pia ardhi iwe tofauti. Ni vyema Serikali kutunga sheria na vilevile mwongozo mwafaka na thabiti ambao unaweza kusaidia zile shule ambazo miaka ya 1960 1970 1980 na 1990 idadi ya watu ilikuwa chini. Sasa hivi idadi hiyo imeongezeka. Yafaa Serikali itenge hela za kununua ardhi ya kupanua hizi shule badala ya kujenga shule nyingi. Zile shule za zai zikipanuliwa zitaweza kuwa na watoto wengi kuliko hapo mbeleni. Hoja hii imeletwa wakati mwafaka kwa maana kuna mambo mengi sana ambayo yamebadilika. Ni vyema kuwe na sheria na mwongozo kwa hizi shule na tujue mpangilio. Mwongozo utolewe kwamba shule ya msingi iwe na kiasi fulani cha ardhi shule ya upili iwe na kiasi fulani cha ardhi. Juzi kulikuwa na matapeli wengine kule Mwatate ambao walisema wanataka kutujengea chuo kikuu kutoka Amerika kumbe wameshikana wanataka kuchukua ardhi. Walikuwa wanahitaji ekari 1000. Uzuri tuligundua hivyo. Ingekuwa vizuri wizara husika kutunga sheria kuhusu kiwango cha ardhi shule ya msingi shule ya upili ama chuo kikuu zinahitaji. Vilevile waangalie sana. Tukisema kuwa tuchukue ardhi yote kwa sababu ya mashule tukumbuke pia kuna zahanati na mambo mengine mengi yanayotakikana. Lazima tubadilishe mtindo. Kama tunajenga shule tufikirie kuzijenga kama ghorofa ili shule zisichukue ardhi yote. Mhe. Naibu Spika wenzangu wameongea mengi. Naunga mkono Hoja hii. Ahsante.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuongelea juu y hii ripoti kutoka kwa kamati ya mazingira katika Bunge letu. Ninaungana na wenzangu kushukuru kamati hii. Imekuwa muda haya mambo ya mabwawa yameleta utata mno. Isingelikuwa ni hii kamati imechukua hiyo nafasi hatungejua kinachoendelea kuhusu mabwawa haya. Nataka kuungana na wale wamesema kwamba haya mambo ya mabwawa yalikuwa chini ya Kamati ya Kilimo. Ni ukweli hatungejua ni nini kinaendelea. Namshukuru Mwenyekiti na timu yake kwa kutambua kwamba hizi shida zenye Wabunge wametambua katika Bunge hili ni kweli ni shida zile ziko kule chini na haikuwa ni makosa ya wale walikuwa wanauliza bali ni makosa ya mipangilio sambamba kuhusu haya mambo ya mabwawa. Umesikia kule Budalang'i vile wamesema. Ni ukweli tusipo kuwa na wataalamu wakutambua kwamba hili bwawa linatakikana litoke wapi na liende wapi tutakuwa tunamaliza wakati wetu an hizo pesa zinatakikana kutolewa na serikali zitakuwa zinaangulia patupu. Ukiona sehemu za Turkana mahali ambapo wanasema ni sehemu kame... Iwapo mtu atapewa kandarasi ya kuchimba kisima au bwawa katika eneo hilo pasipo na ujuzi tutakuwa tunamaliza wakati wetu. Ninamushukuru Mhe. Chachu. Amesema hapa kwamba kuna wale ambao walikuwa wamepewa fedha za kutengeneza bwawa. Unaona mtu akikula karibu asilimia sabini bila kufanya kazi. Ndiyo naunga mkono hii Kamati na kusema kwamba Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikari achukue hatua na kuhakikisha kwamba mtu akipewa kazi lazima aikamilishe. Hatuwezi kusema kwamba wananchi hawajajitokeza. Wananchi wako tayari katika sehemu zao. Wabunge kama waakilishi wao wakiona bwawa litajengwa katika sehemu yao wana nafasi ya kuongea na wananchi na kuhakikisha kwamba bwawa nzuri limejengwa. Hatuwezi kuwa tunasema waziri fulani ama kandarasi inatolewe na mtu fulani. Hii ni kwa sababu hawa ni wale watu tu wanaotafuta kazi za maji na wakitoka hapo wanaenda hospitalini ilikujinufaisha wao binafsi. Sio kwamba wanawanufaisha wananchi ambao wanangojea huduma zao kama Wabunge. Kulingana na kazi ya Kamati ni vizuri tuwe na mipangilio ya kuhakikisha kwamba serikali za kaunti kwa sababu ndio zinasimamia mambo ya maji ziko na mipangilio mizuri na kwamba wananchi wanapata haki zao. Wajengewe mabwawa ya kuwasaidia kwa ajili ya kilimo na ufaa yao. Kwa hayo machache nasema asante na kuunga mkono Kamati.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii hata mimi nichangie Hoja hii ambayo ni ya muhimu sana kwetu sisi haswa akina mama. Zoezi hili la kutafuta vyeti vya kuzaliwa vinatuhusu sana. Nachukua fursa hii kumpongeza Mhe. Martha kwa kuifikiria Hoja hii na kuileta hapa Bungeni ili tuweze kuijadili. Ni kweli mambo ya kutafuta vyeti vya kuzaliwa vimekuwa kero kwa wananchi wote wa Kenya. Ni shida sana. Wananchi wanasafiri mbali wanaenda wakirudishwa wanatumia pesa nyingi na kila wakifika pale wanaambiwa warudi siku inayofuatia. Hivi majuzi kule kwetu Taita Taveta hata yale makaratasi ya kuchapisha vyeti hivyo hayakuwepo. Kwa hivyo ilikuwa ni usumbufu mtupu wa kungoja. Pia watoto wakienda shuleni wanaambiwa ni lazima wapeleke vyeti hivyo. Imekuwa ni kero sana ake vyeti ni muhimu. Huwezi kupata pasi ya kusafiri mpaka uwe na cheti cha kuzaliwa. Kwa hivyo naunga mkono kwamba Hoja hii ni muhimu na tunaomba vyeti hivi viweze kupatikana kwa urahisi. Tunaomba huduma hii ya kutoa vyeti vya kuzaliwa iweze kuboreshwa na iwe rahisi kwa wananchi kuvipata vyeti hivi. Kama vinaweza kuletwa kwa ward level itakuwa vizuri zaidi. Nazidi kumpongeza dadangu Martha kwa kuileta Hoja hii Bungeni ili tuweze kuwasaidia wananchi kule mashinani.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Mswada huu unaohusu akina mama. Vile wenzangu wamezungumza ni kweli. Akina mama ndio wanaofanya kazi yote. Kila kazi katika pembe zote za Kenya zinahusu akina mama. Naunga mkono Mswada huu ambao umeletwa Bungeni. Uwezo wa kuwa kiongozi unatoka kwa Mungu. Hatujui ni kwa nini kina mama wanakatazwa kuwa viongozi. Katika Jimbo la Samburu mama alikuwa amewekwa nyumbani kuchunga nyumba na kufanya kazi zote za nyumbani. Kenya nzima kuna wazee ambao wanajijengea nyumba. Kwetu mama huwa anajijengea nyumba. Kama huna nyumba bwana hataishi nawe. Lazima ujenge nyumba hiyo ili mzee huyo aje. Nilipigania kuwa kiongozi kwa sababu nilipendezwa sana kuwa kiongozi. Ningeenda kwa mkutano ya Wasamburu na ningefukuzwa kama mbwa. Wangeuliza: Mwanamke huyu anataka nini? Nashukuru Mungu kwa sababu wakati walinipatia nafasi ya kuwa kiongozi walijua kuwa mwanamke anaweza kuwa kiongozi bora hata kumshinda mwanamume. Nashukuru kwa sababu akina mama katika Jimbo la Samburu wamejitokeza kuwa viongozi. Nashukuru pia kuwa katika sheria zetu kuna kipengele cha uteuzi. Kipengele hicho kinawafungua akili akina mama. Nilikuwa diwani mteule kisha nikawa Mbunge mteule mwishowe nikapigania kiti cha ubunge. Kama ningetaka kiti cha gavana wa Samburu au Seneta wa Samburu ningekichukua. Kwa nini nasema hivyo? Hakuna mmoja wao alifikia zile kura nilipewa. Kama ningetaka kiti chochote ningekipata. Akina mama wanatusiwa kwa wingi wanapopigania viti. Wengi wanashtuliwa na matusi hayo. Ningependa kuwaambia akina mama katika Kenya hii kuwa wasijali matusi hayo. Wapiganie haki ya watu wao. Lazima upiganie haki yako na wenzako. Usishtuliwe na matusi. Wakati huu katika Jimbo la Samburu Seneta Naisula anapigania kiti cha ubunge cha Samburu West. Nina uhakika kuwa atapata kiti hicho kwa sababu yale matusi anayopata wakati huu si madogo. Matusi ambayo napata wakati huu yanainua gredi zangu zote kwa sababu ya kazi ninafanya. Mhe. Naibu Spika wa Muda tunaunga mkono. Nashukuru Wabunge wetu wote na wanaume wale wako hapa kwa kuunga mkono huu Mswada kwa sababu kazi inahitaji kusaidiana. Hakuna mwanamume hapa hamwambii mkewe aangalie kama anapigwa. Anamwambia atembee amutafutie kura akijua anaweza. Nina hakika kina mama tutapigania viti. Kama kwetu Kaunti ya Samburu hatukupata kiti cha kuchaguliwa cha waakilishi wa kaunti lakini kwa sababu ya kuteuliwa tulipata kina mama kumi. Kwa hivyo naunga mkono uteuzi ili usaidie wengine. Naunga mkono. Asante.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii nichangie Hotuba ya Rais. Haikuwa mbaya ilikuwa hotuba nzuri. Lakini kuna yale yaliyonivutia kutokana na hiyo Hotuba. La kwanza ni swala la ufisadi. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa sababu anang'ang'ana sana kupigana na ufisadi. Lakini wale wanaomwakilisha kutekeleza masuala ya ufisadi hawawajibiki vilivyo. Naona wamechukua mikondo ya siasa. Huwa watu wanafuatiliwa kwa mirengo. Naona siasa zimeanza mapema. Kama wewe si wa mrengo fulani basi wewe ndio utaandamwa. Lakini kama wewe ni wa mrengo fulani basi uko huru kufanya utakavyo. Kwa hivyo naomba wahusika wamuunge mkono Mheshimiwa Rais kupigana na ufisadi bila ubaguzi. Mfisadi ni mfisadi. Hana ukubwa wala udogo. Suala lingine ni kuhusu maendeleo yale ametufanyia haswa kwa masuala ya barabara. Tumeona anawajibika sana. Huzuni yangu ni kuwa naona barabara nzuri katika miji mikuu ndizo zinaangaliwa zaidi. Huko barabara zaongezwa zikiongezwa. Kuna sehemu ambazo hali ya usafiri iko na shida mpaka sasa. Tafadhali wale ambao wanawakilisha ofisi ya Rais wamepatiwa majukumu wajue kuna wengine bado wanateseka. Nimefurahi leo kwa sababu mwenzangu amesifu zile kilomita za barabara wamepata kwao. Mimi sina la kujivunia kama mama wa Kaunti ya Tana River kwa sababu barabara ya kwangu mpaka sasa ni mbaya. Hata tone la mvua likianguka hivi usafiri kwangu Tana River ni shida. Kwa hivyo wale mnaotumwa msitubague. Mfanye Rais awache legacy yake nzuri. Ninataka kuzungumzia suala la BBI. Siyo hoja mbaya kurekebisha Katiba. Tangu mwanzo wakati Katiba ya 2010 ililetwa tayari ilikuwa na matatizo. Watu walilalamika na wakasema ilikuwa na shida. Wakasema tuipitishe halafu tutarekebisha. Watu wanalalamika. Wanasema kuna matatizo katika Ripoti ya BBI. Wacheni tusuluhishe ndiyo tuepuke kurekebisha Katiba mara kwa mara. Tusipitishe halafu tuje turekebishe tena. Turekebishe sasa. Pia haina haja ya kupoteza pesa. Hili ni suala la sisi Wakenya. Tunaweza kukaa tujadiliane na pesa hizo ziende kwa maendeleo mengine. Kenya ni yetu na ni kubwa kushinda watu wote. Pia katika hilo suala la BBI sioni kama mwanamke anatendewa haki. Ile nafasi ya wanawake 47 ambao ni wawakilishi wa kaunti ibaki katika Bunge la Kitaifa na watupatie wawakilishi wengine kutoka Bunge la Seneti. Wale wengine ambao wanapanga twende tukapambane na wanaume nguvu tunajua idadi tunayo na tutapambana. Hatusemi ile nafasi ambayo tuko nayo tunyang'anywe. Tuachie na tuongezwe zingine. Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili nami nijiunge na wenzangu kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa Hotuba yake aliyotoa hivi jusi. Ufisadi ni ugonjwa mgumu sana na mbovu kushinda saratani kwa maana ni ugonjwa ambao utamaliza nchi yetu kama hatutasikiza vile Mheshimiwa Rais amesema. Amezungumzia sana kuwa kuna umuhimu wa kupigana na ufisadi maanake ni janga ambalo linatumaliza sisi sote na pia mwananchi. Janga hili la ufisadi ni janga ambalo linahitaji Wakenya wote waungane na Mheshimiwa Rais tuwe kama jeshi lake kuweza kupigana na huu ufisadi. Kina mama wakienda kujifungua hospitalini wanakosa dawa ama vifaa vya kuwasaidia na mama anapata dhiki ya kupata mtoto afariki au yeye apate matatizo na kufariki. Mhe. Naibu Spika wa Muda ufisadi unatumalizia wananchi wetu na kutuletea balaa hapa nchini. Sio wote kule mashinani wanaweza kwenda kwa hospitali ambazo ni za kibinafsi. Watu wengi huenda hospitali za umma ili kuweza kuwezeshwa. Hata Mhe. Rais aliposema anazungumzia ajenda zake nne moja ni kuhusu habari za kuwawezesha Wakenya kupata huduma ya afya kwa njia inayofaa na mwafaka. Kule mashinani watu hutembea kilomita nyingi kutafuta maji. Pesa zinazofujwa kwenye ufisadi zinafanya wananchi kuteseka na kukosa maji ya kutumia. Kama inavyosemekana maji ni uhai. Maswala mengi na haswa sakata kubwa zilizoko ni kuhusu maswala ya kuhusiana na maji. Ufisadi hauwezi kuendeleza nchi na itakuwa sababu kubwa ya nchi hii kudidimia chini kama hatutamsikiliza Mhe. Rais anavyosema. Ningependa sana kumpongeza Raisi haswa kwenye maswala ya kimaendeleo reli ya kisasa inavyotutoa Mombasa ikitufikisha hapa sasa hivi inaelekea kumalizika kuelekea Naivasha halafu kuendelea mbele. Tunajua kwamba ameenda nchi ya Uchina kuhakikisha ya kwamba ameweza kumalizia maswala ya kupata fedha za kumalizia kazi hii. Wakenya wengi wana kilio lakini dawa ya kilio chenyewe ni moja tu kuhakikisha kuwa ajenda hizo nne za Raisi zinaweza kutimizwa na yeye kabla hajafika kustaafu mwaka wa 2022. Kwa hivyo ni lazima sisi wote tumuunga mkono tumwombee afya nzuri na vile vile pia tumwombee hata Naibu wake afya nzuri ili wote waweze kufanya kazi na kutekeleza majukumu walioambia Wakenya. Mhe. Naibu Spika wa Muda naunga mkono Hotuba hii na wale wote ambao wanasimama kidete kuweza kuhakikisha kuwa Wakenya wataweza kupata maendeleo kulingana na vile Mhe. Rais alivyoitakia Serikali yake. Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili niafiki Hoja hii ambayo imeletwa na rafiki yangu Mheshimiwa wa Nyali Mohamed Ali ambaye tunamjua sana kwa jina "Jicho Pevu". Tunafurahia kwa sababu Hoja ambayo amewasilisha hapa ni muhimu sana na yale aliyoyaangazia ni mambo ambayo yanaathiri watu wetu kila uchao. Lakini wakati Mhe. Ali jana alipokuwa anatoa Hoja hii angetoa ilani kwa Wabunge kwamba leo tutakuwa tunaongea kwa Kiswahili ndiyo watu waweze kubeba kamusi. Nimeona sana wakati Mheshimiwa alikuwa anaendeleza Hoja hii wengi walikuwa wameachwa vinywa wazi. Hawakuwa wanaelewa hasa sisi ambao tumetoka bara. Lakini nitajaribu nione kama nitaweza kuiafiki Hoja hii kulingana na matarajio ya Mhe. Mohamed Ali. Tutakumbuka kwamba wakati tulipoanzisha serikali za ugatuzi mwaka wa 2013 tuliona sana magavana wengi wa nchi hii wakikimbia kununua magari ya kusafirisha wagonjwa yanayojulikana kwa kimombo kama ambulance . Walikuwa wanazinunua ili wakipata wagonjwa katika sehemu zao waweze kusafirishwa mpaka kwenye hospitali kuu hapa Nairobi na kule Eldoret. Kuhusu uzima wa mwili yani health kwa maoni yangu tulikosea kidogo wakati tulipoigatua sekta hiyo. Labda sekta hiyo ingeshikiliwa na Serikali ya kitaifa haswa tukizingatia kwamba kila kuchao sisi kama Wabunge tunaitwa kushirika kwenye mikutano ya kuchangisha pesa. Hizo fedha tunachanga kila siku ni za kupeleka wagonjwa hospitali ama ni za kugharamia kuzikwa kwa maiti? Vifo vingi vinavyotokea katika taifa hili husababishwa na magonjwa ambayo yanaweza kutibiwa ama kuhudumiwa kabla ya kusababisha vifo. Haya magojwa yatatibiwa namna gani ilihali hatuna hata zahanati? Yatatibiwaaje kama hatuna madaktari na waauguzi? Yatatibiwaaje kama madaktari tulionao nchini... Tuna madaktari ambao wanahitimu kila mwaka kutoka vyuo vikuu. Lakini wakihitimu hawakai humu nchini. Wanahamia nchi za kigeni.Wanahamia nchi jirani na wengine nchi za Ulaya kwa sababu wanapata lishe bora huko. Mhe.Naibu Spika wa Muda naomba sisi kamaWabunge lazima tufanye kazi yetu sawasawa na tuhakikishe kwamba waliotuchagua walituchagua tuwashughulikie kiafya ajira na mengine. Mhe. Mohamed Ali alisema hospitali za rufaa ni muhimu sana. Tuko na mbili moja hapa Nairobi na ingine kule Eldoret. Tukiangazia maeneo ya uwakilishi Bunge hasa nikitoa eneo langu la Bunge kama mfano hatuna hospitali ya kiwango cha 4 hata hospitali ya kiwango cha 5. Tuko na zahanati peke yake. Wagonjwa kutoka eneo langu la uwakilishi Bunge wanasafirishwa zaidi ya kilomita 200 ili wapate huduma za afya. Lazima tuimarishe zahanati tulizonazo kule mashinani ili zile za kiwango cha 4 ama kiwango cha 5 zihudumie wagonjwa ambao hawapati huduma kule mashinani. Hili si jambo la mzaha. Ni jambo tunapasa kuangazia sisi sote pamoja na magavana. Naomba ya kwamba Hoja kama hii iwasilishwe katika gatuzi zote za taifa hili. Ni jukumu la serikali yoyote kuhakikisha kwamba wananchi wake wote wako na afya njema. Uzima wa kimwili ni jukumu la ugatuzi. Tukiwa na hospitali ya kiwango cha 6 katika kila gatuzi... Hospitali ya Rufaaa Kenyatta imekuwa na changamoto juzi. Wakati mwingine huwezi kulaumu madaktari kwa sababu kila siku wanafanya oparesheni nyingi kwa sababu wagojwa ni wengi na hatuna hospitali za kutosha. Tukiwa na hospitali za kiwango cha 6 kule Homa Bay Nyeri ama Mombasa ama kwa gatuzi zote 47 nchini tutakuwa tumewashughulikia wananchi. Sitaki kupitisha hapo. Kama Wabunge tuko na bahati maanake tuko na bima ya afya. Inatushughulikia kwa kutuwezesha kuenda kutibiwa kule ng'ambo. Lakini walalahoi wa kule mashinani wakigojeka ama wakipata magojwa ambayo hayawezi kutibiwa humu nchini watafanya nini? Naiafiki Hoja hii. Haitakuwa Hoja tu tutahakikisha imetimizwa na Serikali ya Kitaifa na pia serikali gatuzi. Kwa hayo machache naomba niketi. Asante sana.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi ili pia nichangie Mswada ambao uko mbele yetu. Ninashukuru Mheshimiwa ambaye aliketi na akawaza na akaleta Mswada ambao tunaongea juu yake. Sisi wengine tumetembea na tumeona mengi. Ninatoka Kapenguria. Ukisikia Kapenguria kuna wale wanaongea kuhusu "Kapenguria Sita". Wakati niliingia katika Bunge la Nane nilipata Mzee Mheshimiwa Paul Ngei akiwa anazunguka hapa akiwa kwa ile baiskeli ya kuzungushwa. Wakati unamtazama na ukiangalia historia ya Kenya kuhusu wale ambao walipambana mpaka wakafika pale alikua mmoja wao. Baadaye nikaona Mheshimiwa Ochieng Oneko na Hayati Kenyatta. Ni jamii moja inayojulikana lakini wale wengine watano hakuna mtu anayetaka kuongea juu yao. Kwa hivyo miongoni mwetu kuna wale ambao hawajui bei ya petroli kwa sababu wanabebwa kila mahali na wengine. Wengine wetu hapa wanafanya biashara na Serikali na kuna wale ambao wanatoka hapa na kuenda kuhudumia watu wao. Sasa tusifike mahali pa kusema kwamba mtu aende ajitengenezee kwa sababu wengine tumefika hapa hivi. Kusema hivyo kwa njia nyingine ni matusi. Hivyo basi ninataka kuunga mkono na kusema kwamba wenzetu ambao wamekuwa hapa wamekuja kutusikiliza. Mimi nilikuja hapa katika Bunge la Nane na mshahara ambao nilianzia kulipwa ulikuwa Kshs150000. Wengine waliniambia kuwa nilikuwa na bahati kwa sababu mshahara ulikuwa umeongezeka. Watu walikuwa wamefurahi sana. Ukitaka kuchukua mkopo hata wa kununua gari au kujijenga au kusaidia familia yako ama waliokuchagua ilikuwa ngumu. Sisi kama Wajumbe ambao tuko hapa Mungu ametupenda na akatuleta hapa na watu wetu pia Mungu akawasababisha kutuchagua tusije tukaweka wenzetu vibaya. Leo ni wao na kesho atakuwa mwingine hapa hivi. Mimi pia wakati mmoja sikuchaguliwa Bungeni. Nilikuja mara mbili halafu nikabaki nje. Niliona kwamba kubaki nyumbani ni shida. Wakati watu wanaongea wengine hawaelewi na hawajaonja shida ya kuwa nje na wananchi hawajali. Wanafikiri kuwa wewe bado uko sawa. Mwingine anasema wewe ni wetu. Nafupisha kusema kuwa niko katika Kamati ya Huduma ya Wabunge. Nimeenda India na ufikapo huko yule Mjumbe wa zai anapewa tikiti mara nne kwa mwaka ya kusafiri mahali ambapo anataka akitumia ndege. Anapewa karibu mara kumi na tano kwa kusafiri kwa reli. Pia anapewa matibabu kwa jamii yake. Sijui ni nini inayofanya tusiwaangalie wenzetu jambo hili linafanyika kwengine. Nimeenda karibu nchi tatu na wanajali wenzao waliotumikia watu mbeleni. Wanasema kuwa yule ambaye amechaguliwa na amekuwa mwanasiasa hakuna kampuni itamuajiri. Wakati umetoka Bungeni unashukiwa sana na hivyo ndivyo ilivyo hapa Kenya. Kwa hayo ninaunga mkono. Kwa hivyo tuunge mkono na tulete amendments nzuri ambazo zitasaidia wenzetu na jamii zao. Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi kuchangia Hoja hii. Naunga mkono Ripoti ya Kamati ya Bajeti na Makadirio. Licha ya changamoto zilizotajwa na Wabunge wenzangu nafurahi sana kwa sababu wafanyakazi katika sekta ya afya nchini wamepewa fedha za kununua vifaa vya kujikinga kutokana na maradhi ya Korona. Vile vile wameongezewa marupurupu kuwasaidia kupigana na changamoto za kibinafsi zinazowakumba kwa sababu ya kupigana na ugonjwa huu wa Korona. Nimejua zaidi na nimeleta Hoja tofauti Bungeni kuhusiana na masuala ya afya na Wakenya wa kawaida wanavyoteseka kwa kuwa sekta hii ya afya haiendeshwi vizuri katika kaunti tofauti. Nasikitika kusema kuwa hivi majuzi kakangu ambaye ni daktari katika hospitali Kuu ya Pwani alishikwa na ugonjwa wa Korona. Aliugua na nashukuru alipona na hakuhitaji kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi. Hivi sasa anasubiri kupimwa tena kuhakikisha kuwa hana ugonjwa huo. Ni muhimu kuangalia masuala ya wafanyikazi wa afya nchini kwa sababu wanaumia pamoja na familia zao kwa kutuhudumia sisi Wakenya wengine na kuhakikisha kuwa maradhi haya hayasambai kote nchini. Nimefurahishwa na Rais kutoa mgao huo. Ningependa kusisitiza Kamati ya Afya hapa Bungeni na kule Seneti kuhakikisha kuwa hizi fedha zinafika kule zilikolengwa na ziziharibiwe vile zimekuwa zikiharibiwa. Kama muda utaniruhusu nataka kumuunga mkono dadangu Mhe. Gladwell kutoka Baringo alivyosema kuwa mara nyingi Serikalini tunazungumzia shilingi bilioni moja kama pesa kidogo sana. Nafahamu kuwa Mheshimiwa Ichung'wah alijaribu kumrekebisha. Nataka kukubaliana na Mhe. Gladwel kuwa kwa Mkenya wa kawaida kwa shilingi bilioni moja akitoa shilingi elfu moja kila siku atatumia hiyo pesa kwa miaka 2739. Kwa hivyo ni pesa nyingi. Naomba tujizatiti kama Bunge kuhakikisha kuwa hizi fedha zinafika kule zinakostahili. Ahsante.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi ya kuchangia Hoja hii iliyoletwa na Mbunge mwenzetu Ali Mohamed. Namshukuru sana kwa Hoja hii. Imekuja wakati mzuri kwa sababu maeneo ambayo baadhi yetu tunatoka watu wanaumia sana. Mwenzangu Oluoch alichangia na kusema kwamba kulikuwa na hospitali moja katika eneo langu kule Trans Nzoia Crystal Hospital iliyomtoza ada mtu ambaye alikuwa ameumia katika sehemu hizo Ksh200000. Kijana huyo anayeitwa Wanjala alikuwa anaishi maisha ya umasikini na upweke. Hakika hangeweza kulipa hiyo ada na ndiposa inatulazimu sisi kama viongozi kutafuta marafiki wenzetu na tuungane pamoja kuhakikisha kwamba tunamchangia pesa za kumsaidia. Sio yeye peke yake katika hospitali hiyo walikuwa wengi mno. Kuna mama kutoka sehemu yangu aliyekuwa anaugua ugonjwa wa saratani na familia yake ikatozwa Ksh674000 lakini alipoteza maisha yake. Sisi kama viongozi ama wenyeji katika sehemu hizo hatuwezi kujimudu kutoa hizo pesa kumsaidia mama huyo. Ndiposa namshukuru Mhe. Ali kwa kuleta Hoja hii ili tuichangie. Tuna uhakika kwamba wale wanaohusika na mambo ya afya katika nchi yetu wanatusikiza. Mwaka uliopita nilileta Hoja kuhusu akina mama wenzetu ambao baada ya kupata mimba ya mapema ama kujifungua huwa wanaathirika na ugonjwa unaoitwa fistula. Nashukuru sana kwa sababu Mama Margaret alishikilia mara moja na saa hii watu wanapata matibabu katika nchi yetu. Vile vile tunapoijadili Hoja hii katika Bunge hili nina ii kwamba Waziri anayehusika na mambo ya afya atahakikisha kwamba amesaidia Wakenya wasiojiweza kwa kulipa ada hiyo wakifariki. Hata kama wengine hawajafariki lakini hawajimudu kimaisha ahakikishe kwamba ada hiyo imeondolewa mbali. Hivi juzi kulikuwa na janga la magaidi pale Riverside. Kuna watu ambao hawangeweza kujimudu hata kulipa ada katika hospitali na ikamulazimu Seneta wa Kaunti ya Nairobi kutoa pesa zake katika mfuko wake kumlipia yule aliyekuwa ameathirika. Kuna wengi ambao hawawezi kutufikia sisi viongozi. Vile ambavyo wengine wamechangia hapa kuna walemavu miongoni mwao. Kuna wale wametoka katika maisha ya upweke na hawawezi kutufikia sisi viongozi kuwasaidia na senti kidogo kuhakikisha kwamba wanapata matibabu kama watu wengine. Nawaunga wenzangu mkono kwa sababu wakati tunapewa nafasi hii kama viongozi katika Bunge hili haiishi kwamba sisi ni matajiri. Sisi pia tumetoka katika maisha ya upweke. Wengine tumepoteza wapendwa na hatuwezi kujimudu kama viongozi. Tunawapatia watu mwelekeo katika maisha yao na wale wananchi ambao wametupa kura kama viongozi wao. Kuna wenzetu ambao wamekuwa katika Bunge hili ambao kule nje wanapata taabu sana. Upande wa magharibi ya Kenya huwa wanategemea kilimo cha miwa. Lakini wakati huu wakulima kutoka eneo hilo hawana lao la kusema kwamba wanajivunia. Hawana senti za kupeleka wagonjwa wao hospitalini. Katika Bonde la Ufa wengi wanategema mahindi yao. Wakiwa na wagonjwa ama wapoteze wapendwa wao na watoto wao katika eneo hilo tegemeo lao lilikuwa ni mahindi. Tutoe senti wapi kwa sababu watu hawajimudu? Ndiposa namuunga mkono mwenzangu Ali. Nawashukuru watu wa Nyali kwa kukupa nafasi hii kuja katika Bunge hili kuleta Hoja kama hii. Tunatarajia kwamba Kamati ya Bunge hili ya Utekelezaji itahakikisha kwamba imetenda vilivyo. Sisi tutafurahi. Tunawahimiza wale wanaoshikilia Bajeti katika Bunge letu wakipata kama mambo ya afya. Yule gavana katika kaunti yangu hajawahi kuja katika Bunge hili. Huenda ikawa alipewa nafasi katika kaunti hiyo kwa sababu ya mrengo ama bahati yake. Licha ya kupata fedha nyingi watu hawa huwa hawaangalii masilahi ya wale masikini walio huko chini. Ni sisi katika Bunge hili tunaofanya hivyo kwa sababu tunapoongea watu wanasikiza. Tutekeleze mambo mengine katika Serikali ya kitaifa na tuhakikishe tunapopeleka ujumbe kule mashinani tunaongea na watu walio na afya nzuri. Katika eneo langu la Trans Nzoia kuna squatters wengi sana. Hawana lao. Ukisema mtu aende hospitalini hana chochote. Asubuhi akiamka aje kwangu hatafika kwa sababu hana pesa ya kupanda ile pikipiki ama kutumia baiskeli mpaka kwangu. Iwapo ni mgonjwa mtu huyu atasaidika namna gani? Vyumba vya kuhifadhia maiti vimejaa kwa sababu ya mgomo wa madaktari katika nchi yetu. Kama viongozi tunataka tushikilie msimamo wa kuhakikisha kwamba masuala ya madaktari yameshughulikiwa. Ninamsihi Rais. Licha ya kusema kwamba ametoa amri awe na mikakati mwafaka ya kuhakikisha kwamba ile amri anatoa anielekeza panapotarajiwa. Tunapoteza wapendwa hapa nchini. Kila Jumamosi watu hututumia ujumbe kwamba wamepoteza wapendwa wao. Tutoe wapi fedha? Sisi hatuna pesa za kutosha. Nawaomba wenzangu waunge mkono Hoja hii. Mwenzetu Ali alete Mswada katika Bunge hili ili tutenge pesa za kuhakikisha kwamba tunawasaidia wale ambao wamekuwa na shida kama hii. Kuna wale wameumia kama yule kijana Boniface. Nawashukuru wasamaria wema waliojitolea kuhakikisha maisha ya kijana huyo yataendelea mbele. Naunga mkono Hoja hii.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia mwanya wa kuweza kuunga mkono mjadala huu ulio na uzito mkuu katika Kenya yetu tupendayo. Kenya inasemekana kuwa ni eneo la ukulima. Lakini ukiangalia orodha ya madini yaliyo katika Kenya yetu ni mengi kuliko ule ukulima tunafanya. Ukianzia na theluji petroli ambayo imepatikana juzi dhahabu iko titanium iko hewa ya uwekezaji na vile vile mvuke katika eneo la Bonde la Ufa umechangia pakubwa sana kwa umeme. Ombi langu ni wakati tunajaribu kujadili na kutilia uzito mikakati hii mwafaka itakayotumika katika Kenya yetu mpya ni vizuri vile vile tuzingatie uzito wa uchimbaji wa madini kama jambo kubwa la kuleta mapato katika Kenya yetu. Maeneo au nchi zile zimeendelea zaidi ni zile zimetilia uzito katika uchimbaji wa madini kama petroli. Ukiangalia upande wa uarabu utakuta hawana chochote kingine ila madini na yameweza kutumika na kufanya maeneo hayo yatambulike duniani kote. Lakini la muhimu hata kama tutatia uzito katika sekta ya uchimbaji wa madini ningeomba vile vile wapangaji waangalie kiini hasa kile kinachangia sababu ya watu wanaoishi pahali kuna madini mengi kuwa wanyonge sana. Ndio tusije tukaingia katika hilo shimo. Tutengeneze mjadala wetu na kuhusisha wale watu ambao wako kule mashinani kama vile wale walioongea mbele yangu wamesema. Ni vizuri wale matajiri wanapotajirika nalo eneo lile limefanya watajirike litajirike. Lakini ukitafuta usawa wa pahali madini yametoka na pahali yanaenda kuendeleza hakuna uhusiano kamwe. Ombi la watu wote wale wako maeneo ya madini haya ni kuwa ni vizuri wahusishwe kabla hata madini hayajaanza kuchimbwa. Tukifanya hivyo Kenya yetu itakuwa ya kuheshimika. Itakuwa katika mrengo wa mbele wa dunia pahali madini yamekuwa ya kuleta utajiri lakini si umasikini na vita. Ninaunga mkono Hoja hii.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nami nichangie Mswada huu. Kwanza ningependa kushukuru Mswada huu kutoka Bunge la Seneti. Ni Mswada mzuri kwa sababu watoto wengi hukosa elimu kwa sababu ya kukosa msingi bora. Niseme kwamba tumeanza kuona matunda ya Mswada huu. Kwa mfano pale Jomvu eneo Bunge langu ipo shule ya msingi ya Jomvu ambayo inayo shule ya chekechea. Mheshimiwa Ali Hassan Joho Gavana wa Mombasa aliona umuhimu kuhakikisha kwamba shule za chekechea zina ufanisi na zinajengwa kwa muundo wa kileo. Ninayo ii kwamba haya anayofanya Gavana Joho atayafanya vile vile katika nchi nzima kwa maana tunamtarajia kuwa rais wetu katika siku zijazo. Ni muhimu Serikali itoe pesa kwa wingi kugharamia shule hizi za chekechea ili wazazi wasitozwe ada kubwa. Ni muhimu kwa Serikali kutuma pesa kwa wingi ili wazazi wasilipe kwa sababu tunaona watu wengi hulipa pesa za Parents Teachers Association (PTA) kuwezesha malipo ya walimu hawa. Pia ni muhimu kwa Serikali kuona kuwa tunafanya juhudu kutuma pesa hizi kwa kaunti ili walimu wa chekechea waandikwe kwa wingi ili kukimu mahitaji ya idadi ya watoto ambao wanaingia katika shule hizo za chekechea. Mswada huu wa Elimu ya Chekechea kwa Kaunti ni mzuri kwa sababu zai watoto wengi katika misingi yao ya kuanza kusoma walisomea chini ya miti. Wengine wanasomea katika majumba ya matope. Kuja kwa Mswada huu kutaonyesha msingi bora kwa kuwa watoto wanatakikana kuwa na msingi dhabiti kwa safari yao katika elimu. Kwa hivyo tumeona mifano. Shule za chekechea katika Bara Ulaya zinachukuliwa kuwa muhimu sana kwa sababu ndizo msingi wa kumuweka mtoto aonekane kweli anaweza kuwa na taaluma fulani. Pia ni muhimu kuwa na mpango kabambe kwa sababu tunaona watoto wengi sana wanatoka katika hali ya maisha ya mabanda na wengi hawajiwezi katika sehemu nyingi tunazotoka. Kwa hivyo kupitia mfumo wa elimu ya bure ambayo iko sasa watoto wengi wanaenda shule. Ni bora kuangalia katika Serikali Kuu na katika serikali za kaunti kuona kuwa kutakuwa na lishe kwa shule zote za chekechea katika nchi nzima ya Kenya ili hao wanafunzi wanaoenda katika sehemu hizi wasome kwa njia nzuri. Elimu ni chombo muhimu sana katika maisha. Ninasema hivyo kwa sababu watoto ambao hawakusoma hufanyiwa kejeli wanapocheza na watoto wenzao. Unaona mtoto anakaa pale na kwa vile mmoja alienda shule humuuliza yule hajasoma maana ya "debe tupu". Kwa Kiswahili sanifu tunasema "haliachi kelele". Lakini kwa yule hajasoma akiulizwa "debe tupu" atasema "lijaze kitu ili lijae". Kwa hivyo hiyo ni njia moja inayomfanya asizungumze sawa na wenzake. Nikiwa Mbunge wa Jomvu nimeupongeza sana Mswada huu. Nimeupongeza kwa ajili ya kunifaidi katika eneo Bunge langu. Shule ya chekechea ambayo imejengwa watoto wataendelea kusoma na wataonekana kwa fikra zao kuwa wanasomea mahali ambapo ni pazuri. Mswada huu umezungumza kuhusu shahada ya diploma kwa wale watasomesha shule za chekechea. Tumeona kuwa watu wengi wamesoma kozi za elimu ya msingi ya watoto katika vyuo tofauti tofauti. Ni jukumu letu sasa kuangalia katika serikali za kaunti na Serikali Kuu tuone kuna mpango mzuri ili walimu waandikwe kwa wingi na watoto wetu wapate elimu hii. Kwa hayo machache Mswada huu umenifurahisha. Ninaona watoto wetu watakuwa na elimu bora na sio bora elimu. Asante na Mwenyezi Mungu atubariki.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kuchangia Hoja hii ilioletwa na ndugu yangu Mhe. Sherrif Nas Nataka kuipinga vikali sana ile amri inayosema kuwa makasha yote yanayotoka katika bandari ya Mombasa yabebwe kupitia SGR hadi Embakasi. Kenya ni nchi huru na kila mfanyibiashara ana haki ya kuamua makasha yake yachukuliwe barabarani ama kwenye reli kupitia SGR. Kitu ambacho ninazungumzia ni muhimu sana. Serikali ya Kenya lazima iweze kusawazisha. Kuja kwa mradi wa SGR kusiwe ndio kifo cha makampuni yetu pale Pwani. Mwenzetu moja amezungumza hapa akasema kuwa kuna mkopo kutoka China. Ikiwa Serikali ya Kenya inataka kulipa mkopo huu wa SGR basi sharti itambue kwamba SGR si ya watu wa Pwani pekee. Ni ya Kenya nzima. Haifai kugandamiza wafanyibiashara wa Mombasa ama Pwani kwa jumla kwa sababu ya kulipa mkopo. Amri iliyotolewa itafanya makampuni mengi yafungwe. Kule Jomvu kuna makampuni kama vile Roadtainers Crown Petroluem Bayussuf na mengineyo. Bayussuf ni moja ya makampuni mashuhuri nchini. Hata Mhe. Kalembe Ndile alifanya kazi katika Kampuni ya Bayussuf. Kama kampuni hiyo ingekuwa imekufa hatungeweza kumuona Kalembe Ndile kama tunavyomuona leo. Tukilazimisha makasha yabebwe na SGR pekee baadaye wale wanaotumia mabasi wataambiwa waanze kutumia SGR na sio mabasi. Hakika wauzaji mafuta vipuli na wengineo wataharibiwa biashara zao. Matokeo ni kwamba miji mingi ikiwemo Jomvu Changamwe na Mlolongo yatakufa. Kwa hivyo nachukua fursa hii kupinga amri hii vikali.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nizungumze juu ya Ripoti hii ambayo imeletwa na Kamati ya kusimamia Masuala ya Wanajeshi pamoja na Masuala ya Mambo ya Nje. Suala la ardhi ni jambo ambalo huleta hisia mbaya. Ni jambo ambalo limefanya watu kupigana ndugu kwa ndugu kuumizana kuuana na umwagikaji wa damu kwa sababu wenyeji wa kawaida wasipohusishwa vizuri bila shaka ni jambo ambalo linaweza kuleta utata mkubwa sana. Nikiangalia Ripoti hii Kamati imefanya kazi lakini sioni kama wameimaliza kazi yenyewe vizuri. Wangehusisha viongozi wote kama viongozi wa kaunti na wa Bunge ili waafikiane na wananchi kuhusu njia mwafaka ya kufanya kazi hii. Jambo ambalo ni wazi ni kuwa Wizara ya Ulinzi wa Nchi inayosimamia masuala ya wanajeshi hapa nchini inahitaji ardhi upande wa Narok. Lakini juu ya kuhitaji ardhi upande wa Narok ni lazima waipate kwa njia ambayo ni sawa na ya uwazi. Nikiangalia mapendekezo ya Kamati hii pale mwisho yananitatiza mno. Hii ni kwa sababu waliolalamika walipoona kuwa tangu pale mwanzo kulikuwa na mchezo fulani uliochezwa basi wangependekeza kuwa Tume ya Kusimamia Masuala Ya Ufisadi na yule anayesimamia suala la uhalifu hapa nchini haswa Director of Criminal Investigations (DCI) waangalie ni jambo gani lililoendelea. Lakini kabla wafikie hapo nina ii kuwa wangekuwa wamezungumza na viongozi wote kwa jumla na kuhakikisha kuwa wananchi ambao ni wahusika kwenye kipande hiki cha ardhi wacha hawa wa 570 peke yake mbali wote wa 5000 wamehusishwa. Kufikia hapo wangekuwa wamepata habari kamili kuwa aliyepata ardhi hii na anayetajwa sana hapa kushinda wenzake aliipata vipi na kama aliipata kwa hali ya usawa ama kwa kununua kutoka kwa majirani zake. Basi iwe watu wamekubaliana kweli labda wao ndio walikosea walipomuuzia wakati aliuliza kupata vipande hivi vya ardhi. Ukweli ni kwamba sioni kama Ripoti hii iko kikamilifu hapa mbele ya Bunge la Kitaifa. Mwenye Kiti na Wabunge wa Kamati wamejaribu sana kuangalia jambo hili. Ninajua wanaangalia kuwa Wizara inayosimamia masuala ya wanajeshi inataka kufanya hii shughuli na hivyo basi wana hiyo haraka. Wahenga wanasema "Haraka haraka haina baraka." Hivyo basi ninapendekeza warudi wahusishe wahusika na washika dau wote na bila shaka watapata mwelekeo bora. Ninapendekeza kuwa suala hili lirudishwe kwa Kamati na wahusishe watu hao ili waweze kupata mwelekeo ambao utafurahisha kila mtu. Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kuniruhusu kuzungumzia swala hili la shahada. Ni jambo ambalo limetatiza kila mtu.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa nafasi ambayo umenipa ya kuchangia mjadala ambao unahusu vijana ambao hawajafanikiwa kuenda mbele sana na masomo. Kwanza ni kumpongeza Mheshimiwa Kanyi Njagua kwa kuleta hii Hoja. Tuna vijana wengi sana Kenya ambao wana ujuzi wamefundishwa na mababu zao wazazi na wajomba. Ukiangalia kazi ya ujenzi uashi useremela na kazi ya mifereji vijana hao wana ujuzi mzuri sana. Ukienda mashinani utakuta vijana wanakosa kujiendeleza katika maisha yao. Mafundi wengi wanatajika katika vijiji lakini wakija kutafuta kandarasi katika vitengo kama vya kaunti na vya NG-CDF inakuwa vigumu kwa sababu hawana vyeti. Hoja inahimiza kwamba sehemu zitengwe za kufanya majaribio kwa vijana hawa ambao wako na ujuzi tayari. Juzi wakati shirika la reli nchini lilipokuwa linachukua vijana kwa kazi ya Standard Gauge Railway wengi waliulizwa kama wako na vyeti fulani vya kuonyesha ujuzi. Ikawa hawana vyeti vyovyote. Ni mafundi ambao wanatajika kwa jina vijijini lakini wakienda kujitafutia nafasi ya kujiendeleza wanakuta hawawezi pata nafasi. Tunajua nchi yetu sana imekumbwa na umaskini watu wetu mashinani wanachangamoto nyingi. Wengi katika vile vituo ambavyo vinaitwa TVET vilikuwa vimedharaulika sana mbeleni kwamba ni wale tu ambao wanakosa kufanikwa kuenda shule za upili lakini mafundi wengi tunaowajua hawana vyeti. Kwa hivyo Hoja hii imekuja wakati sawa ili vijana wetu wapate kujiendeleza mafundi wapate kujiendeleza kwa hali zao za maisha maanake ufundi wako nao. Nasimama kuunga mkono Hoja hii. Asante.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda Mimi nimesimama kupinga kwa dhati huu Mswada Nataka niseme kwamba Naomba uniruhusu nitoe mask Nataka nianze kwa kuliweka vizuri suala la mchakato mzima kutoka mwanzo wake mpaka hapa tulipofikia Utaratibu ambao ulitumika kufikia hapa tulipokuwa na Mswada ripoti zimekuwa katika hali ya kukanganyana kutoka Bomas 1 KICC na Bomas 2 Ripoti zote zilikuwa zinakanganya Tumesikia kwamba Mswada ambao ulipelekwa katika County Assemblies yaani mabunge ya kaunti ili kuzungumziwa Asante
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Hakuna haja ya kujibu swali hilo kwa sababu hivyo ndivyo Wakenya wote walichukulia tabia yao. Hakuna haja ya kujibishana. Tunamshukuru Rais kwa Hotuba yake. Tutampa mkono kwa njia yoyote ile inayotakikana.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Huwa tunafuraha sana kuona vizazi vinavyokuja vikiweza kuja katika Bunge na kuona yale mambo yaliyofanywa na wale waliopita na yale yanayohitajika kufanyika hivi sasa ili wao wahakikishe wasifanye makosa yale yale. Nikimalizia nilikuwa nazungumza kuhusiana na maswala ya ardhi katika eneo Bunge langu la Mvita. Mabwenyenye walioridhi ardhi wanasemekana ni wenye ardhi zile licha ya kuwa hawaonekani. Kuna watu wamekuwa wakilipa ada na kodi za ardhi kwa muda wa miaka na ikipigwa hesabu ya kodi ambazo wameweza kulipa pale na dhai waliyoweza kuiweka katika ardhi ile hivi sasa itakuwa ile ardhi kisawasawa inastahili kuwa ni yao. Nashukuru Mungu ya kuwa tume inayosimamia mambo ya mashamba imekubali kuja katika eneo Bunge la Mvita na kuweza kukaa chini pamoja na kila mitaa na watu waweze kuwaelezea shida za ardhi ambazo zinawakumba. Ningeomba maeneo mengine yaweze kuiga mfano ili historia iweze kutuhukumu ya kuwa Bunge hili ndilo ambalo limeweza kutatua lile donda sugu la ardhi. Asante sana na ningependa kusisitiza yakuwa naipongeza na kuiunga mkono Ripoti hii kuhusiana na maswala ya ardhi.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Kwanza ni kuwapongeza Wabunge wa Kamati kwa kazi nzuri ile ambayo wamefanya. Ni kazi ambayo sio nyepesi na wameweza kuifanya wakifuata wananchi kule waliko mashinani ili kuweza kupatiwa habari zile zinazoendelea mashinani. Swala la ardhi hapa nchini ni kidonda sugu ambacho sio rahisi kukitibu. Nataka kuwaunga mkono kwa hii kazi ambayo waliofanya ambayo sio nyepesi. Vile vile natumaini kuwa wataweza kusaidia Serikali kwa kuitumia Ripoti kama hizi ili Serikali iweze kuhakikisha ya kwamba wataweza kurekebisha matatizo yaliyoko hapa nchini. Kenya hii wananchi wamekuwa wakipigana na kugombana kwa sababu ya swala hili ambalo limetatiza Wakenya sana. Baada ya Katiba iliyopitishwa mwaka wa 2010 haswa wale ambao walikuwa na matatizo ya kihistoria kama yale maeneo tunayotoka sisi sasa hivi tutapata afueni kama Kamati ya Bunge ya Ardhi itaendelea na kazi hii ambayo imekuwa ikifanya. Huku nchini kuna watu ambao kazi zao nyingi haswa nikiangalia upande wa Taita Taveta ni kupita wakidanganya wananchi ili kuwakoroga akili na hata ile kazi ambayo inafanyika inakuwa shida sana kuweza kutekelezwa. Hivyo basi Wabunge viongozi ambao wamechaguliwa mashinani wakitekeleza majukumu yao namna hii tutaweza kuyamaliza matatizo ambayo yanatukabili hapa nchini haswa maswala ya ardhi. Mheshimiwa Spika wa Muda wananchi wanaokaa upande wa Mwatate wameteseka sana. Ukiangalia utaona kuwa wamepandiwa makonge hadi mlangoni. Kwenye Ripoti hii Wanakamati wamesema kuwa masoroveya waenda waangalie kama maeneo yale yako kwenye shamba au nje ya shamba. Yakionekana kuwa nje ya shamba wananchi wagawanyiwe sehemu zao. Kama haitawezekana ikiwa wako ndani ya shamba Serikali ijitolee kuhakikisha ya kwamba wananchi wamepatiwa sehemu zile kutoka kwa bwana mwenye shamba ili wakae kwa hali ya kutulia wakijua kuwa wako nyumbani kwao. Vile vile nikitaja maswali ya Taveta ninataka kutoa shukrani kwa Serikali ya Kenya kwa kutoa ekari 5000 ili Wakenya wanaoishi Taveta haswa Wataveta wapewe maeneo yale. Ni kweli kuwa wananchi pale walitarajia kuwa zile jamii mbili au tatu ambazo zinaishi pale ndio pekee wangepatiwa shamba lile. Lakini tukiangalia sheria ilifuatwa na tukahakikisha kuwa wote hata wale ambao walikuwa kwenye vijiji kwenye hilo shamba wamepatiwa mashamba na haswa wakapatiwa vyeti vya kumiliki ardhi isipokuwa wengi wao walidanganywa hata wakauza mashamba yao kwa sababu waliambiwa kuwa vyeti hivi si vya ukweli. Hiyo yote ni ile propaganda iliyopitishwa pale na wale ambao wameendelea kufanya hivyo. Wabunge walipoenda kule waliambiwa kuwa hata wale ambao walikuwa na malalamishi walipatiwa vyeti vyao vya kumiliki ardhi. Hivyo basi bila shaka sina wasiwasi kuwa Tume ya Ardhi nchini ikifika pale itaona kuwa kila kitu kimefanywa sawa. Ningetaka pia kuishukuru Tume ya Ardhi kwa sababu tayari walikuwa wametembea Taveta na bado watarudi ili kuhakikisha kuwa wananchi wameingia kwa mashamba yao. Ninaunga mkono Ripoti hii.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Maswala ya ardhi kama nilivyosema yameweza kumwaga damu katika sehemu nyingi za Kenya. Kenya iliweza kupata Uhuru wake na jambo kubwa zaidi lilikuwa ni kuhusiana na maswala ya ardhi. Idadi ya Wakenya sasa hivi inazidi na kiwango cha ardhi ni kile kile. Dhuluma ambazo ziliweza kufanywa katika kihistoria hususan sisi kama watu wa Pwani tusipoweza kuanza kuzitatua sasa hiviKarne hii isipoweza kuwa ndio ya kutatua shida za ardhi zilizokuwa ziko basi hatari yake itakuwa ni kubwa zaidi. Ningetaka kutoa mfano. Leo hii katika eneo Bunge langu la Mvita ambalo ni eneo linalojulikana ni eneo la kimji matatizo ambayo yako na shida ambazo ziko pale zikiwemo watu wanaojiita mabwenyenye wa ardhi na wao wenyewe hawapo katika ardhi ile
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Mimi nami nataka kuchukua fursa hii kuunga mkono kuwa kanuni hizi za kusimamia masuala ya Tume ya Wafanyikazi waUmma hapa nchini zitupiliwe mbali kwa sababu hawakufuata mwafaka ambao unatakikana. Vipengele katika Katiba yetu vinaelezea wazi umuhimu wa kuhusisha umma kwenye masuala yote ambayo yanahusu wananchi na haswa masuala ya huduma kwa wananchi. Ukweli ni kwamba saa nyingine utakuta wafanyikazi wa umma kwenye Serikali wanafanya kama utani kuwa wananchi hawatakikani kuhusishwa. Hivyo basi Kamati hii imefanya kazi nzuri ya kuhakikisha kuwa suala hili linatupiliwa mbali. Vile vile ningependa kusema nimekuwa na wasiwasi. Tume hii ya kusimamia wafanyikazi wa umma inatakikana kusimamia wafanyikazi wote kwa ujumla. Tunajua kuna ngazi mbili hapa nchini. Kuna ngazi ya juu ambayo ni ya kitaifa na ngazi ya pili ni ile ya ugatuzi. Lakini wameshindwa kuangalia jinsi wataweza kuhakikisha kuwa wafanyikazi wa umma wote wanaangaliwa kupitia tume hii ambayo kwa kweli ni ya kitaifa. Hayo ndiyo masikitiko yangu makubwa lakini naunga mkono ripoti ya Kamati hii.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Mimi pia ninaunga mkono Hoja hii. Nchini Kenya tuna shida ya huo ugonjwa unaoitwa nasur kwa lugha ya mama. Ninaunga mkono ili tupate madaktari mashinani. Mambo haya ni mabaya zaidi kule mashinani kwa sababu ya ukosefu wa hospitali na madaktari wa kuhudumia akina mama ambao wako na shida hiyo. Hii ni shida kubwa kila mahali haswa miongoni mwa jamii za wafugaji. Inakuwa aibu kubwa mpaka unaona wasichana hawaendi shuleni. Tunapochunguza tunapata wako na hiyo shida. Vile vile akina mama wanapojifungua hujipata kwenye hali hii. Unapata mama amekiti na mkojo unatoka. Unapojaribu kuuliza unapata hakuna daktari ambaye anaelewa ni kitu gani kinaendelea. Kwa hivyo mimi pia naunga mkono ili jambo hili liweze kuangaziwa kwa kina kwa sababu ni jambo linalowaumiza akina mama. Limenyamaziwa kwa muda mrefu. Akina mama wengi wanaona aibu kusema wako na shida hiyo. Watu wanaogopa. Tunaomba tuwe na madaktari mashinani. Tunawashukuru madaktari ambao Serikali imewaleta kutoka nje. Tunaona sasa wanaelekea mashinani kwenda kutibu magonjwa tofauti. Ninaomba huo pia uwe ugonjwa mojawapo wanaenda kuangalia na kushughulikia hasa huu ugonjwa unaitwa saratani. Madaktari wanarudi mashinani kwenda kutibu magonjwa. Naunga mkono na kusema madaktari hawa wanaotembea mashinani pia waende na wajaribu kuuliza kina mama ile shida wanapata kwa sababu shida hii iko hasa kwa kina mama wanaojifungua mara ya kwanza. Ninaunga mkono Hoja hii na ninamshukuru dadangu kwa kuileta na tutazingatia kuwaelimisha kina mama wetu na wasichana ili mtu akiwa na shida hiyo afike hospitalini kwa haraka ili shida yake ipate kujulikana na kutatuliwa mara moja. Asante na ninaunga mkono.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuchangia Hoja hii. Kiswahili ni lugha ya taifa na ni muhimu tuelewe kwamba sio Wakenya wote wanaofahamu Kizungu. Kusudi sote tuweze kuwa na usawa ni muhimu sheria ya nchi ichapishwe kwa lugha ya taifa. Tuna watu wengi ambao wangependa kujua na kujisomea sheria. Ili tuwezeshe hawa Wakenya wenzetu kufaidika ni lazima tuchapishe sheria kwa lugha iwezayo kueleweka kwa urahisi ambayo ni lugha ya taifa. Ili tuweze kujivunia uhuru wetu ni muhimu tuchapishe sheria kwa lugha ya Kiswahili tunayojivunia. Ni lazima tujikomboe na tuchapishe sheria kwa lugha ya taifa. Naunga Hoja hii mkono. Asante sana.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuiunga mkono Hoja hii kama ilivyobadilishwa na kumrudishia shukrani Mheshimiwa Joyce Lay kwa kuileta Hoja hii. Ni jambo nzuri. Nataka pia kumshukuru Mheshimiwa Mwaura na Mheshimiwa Wario kwa ufasaha wao wa lugha na utamkaji mwema wa eno usiokuwa na athari za lugha ya mama. Ninawavulia kofia. Vile vile nitawaomba kwa heshima na unyenyekevu wakipata nafasi wanifunze Kiswahili pia nami niweze kukifahamu kama wanavyokifahamu. Lakini ninawatolea tahadhari wasinifunze kupitia kwa mtandao au kwa kutumia arafa fupi maanake mimi sijaimarika kidijitali. Kiswahili kimetiliwa mkazo sana na ni lazima tukitilie mkazo jinsi Katiba ilivyokitilia mkazo kuliko lugha nyingine zozote. Ukitazama vyuo vikuu vya Amerika Mexico na Japan na hata nchi zinginezo duniani wameanza kufunza Kiswahili katika vyuo vyao. Kwa hivyo ni vyema pia sisi hapa nyumbani tukichukue Kiswahili kuwa lugha muhimu. Mara nyingi Kiswahili kimechukuliwa kama lugha ya watu hohehahe maskini na wa chini kabisa. Sasa ni lazima tuipatie umuhimu maana ni lugha kama zile nyingine. Lazima tujivunie kama Wakenya. Hii ni lugha yetu. Kama watu wa Afrika mashariki nasi pia lazima tujivunie kwamba ni lugha yetu vile vile. Ningeomba pia katika Bunge ni lazima tuweke mfano mzuri tupitishe kuwa tunapopiga chapa hizi Hoja na nakala zingine ziwe zinachapishwa kwa lugha ya Kiswahili. Hatuwezi kuziambia idara zingine umuhimu wa Kiswahili ilhali sisi wenyewe hapa Bungeni hatuyafuati hayo maadili. Ninajua mawakili wengi sana wakiwa pale kortini huwa wamebobea katika lugha za kikoloni lakini inapofika wakati wa kuzitafi kwa lugha ya Kiswahili huwa wanapata shida. Hapa namuona Mheshimiwa Gs ambaye pia ni wakili lakini ninajua akiambiwa atafi kwa lugha ya Kiswahili atakuwa na changamoto. Kwa hivyo katika mambo ya sheria ni vigumu zaidi. Ukiangalia mambo ya kesi inavyoripotiwa ama kuchukuliwa pale tunasema statement mara nyingi inakuwa katika lugha ya Kiingereza. Hapo ndipo pana shida maanake mshatikwa mara nyingi anasomewa na kuambiwa "hii ndio taarifa uliyosema." Kwa vile hana ule uelewaji wa lugha inakuwa ni tatizo kwake na hata akienda kortini anakumbwa na changamoto. Hii lugha yetu ni lazima tuijivunie na tuonyeshe umuhimu wake. Mambo ya kubuni sheria na kuziandika ina shida. Katiba inatuambia Kiswahili ni muhimu. Mambo mengi katika majarida yaliyoko yameandikwa kwa Kiingereza na wakati mwingine watu hawawezi kuelewa. Naiunga mkono Hoja hii. Asante.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii iliyoletwa ni dadangu Mheshimiwa Joyce Lay. Kwanza nataka kusema ikiwa Kiswahili ni lugha rasmi na ya kitaifa ni lazima tuitukuze na kuienzi kwa mahaba kama tunavyoipenda lugha ya Kiingereza ambayo tuliletewa na wakoloni. Nataka kusema kuwa Katiba yetu ya sasa ni sheria mama na ndiyo inasimamia utawala wa nchi yetu. Vipi Katiba hii itakuwa haijatafiwa kwa Kiswahili? Hili ni suala ambalo lazima sisi watungasheria katika Bunge hili tunafaa tuliangalie kwa undani sana. Katika utekelezaji wa sheria lazima washikadau husika wahusishwe katika mambo ya sheria. Kwa mfano mshikadau ambaye ni mahakama; ambayo inatoa hukumu kwa wale ambao wamekiuka sheria ni lazima aelewe sheria hii. Wenye kutunga sheria kama sisi Wabunge katika Bunge hili ni lazima tuzielewe sheria ili tuweze kufanya utekelezaji. Pia Wakenya ni lazima wazielewe sheria hizo kinaga ubaga ili waweze kuzifuata na kuepuka kufanya maovu kinyume na sheria hizo. Mhe. Naibu Spika wa Muda katika barabara zetu hapa Kenya tunaona kwamba kuna sheria ambazo zimewekwa. Kwenye kibao utaona kumeandikwa "Keep Left" kwa Kiingereza ama "Keep Right". Kwa Mkenya ambaye hajui lugha ya Kiingereza huoni kwamba anaweza kufanya ajali kwa sababu ya kutoijua lugha iliyotumiwa kwenye alama ile? Akina mama wengi na mabanti wetu wadogo ambao wanabakwa wanaelewa Kiswahili. Wanapokwenda kwenye afisi za wahusika wa kisheria kuandikisha taarifa kuhusu dhuluma ambayo wamefanyiwa wengi wao hawawezi kuandikisha taarifa kwa Kiingereza. Hivyo basi mhaiwa anapoandikisha taarifa yake kwa Kiswahili afisa wa polisi anamwambia: "Dada ninaweza kukutafia taarifa hii kwa lugha ya Kiingereza." Je banati huyu ambaye ni mchanga wa umri na ambaye hafahamu sheria zetu atawezaje kujua kwamba taarifa yake imeandikwa kwa lugha inayofaa na kwa yale malengo yanayohusu dhulma aliyofanyiwa? Hata katika jela zetu
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Hotuba ya Rais kwa ukweli na haki na kwa njia yote kwa sababu kile amenena Wakenya wote wamefurahia. Katika Hotuba yake Rais amenena zaidi kwa kila kitu na wenzangu wote wamezungumza.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Mswada huu kwani ikija masuala ya bahati nasibu ni masuala ambayo yanaenda kinyume na maadili ya ufanyi kazi. Mambo ya bahati nasibu ni kwamba watu milioni moja wanachanga shilingi kumi kumi na inakuwa milioni mia moja lakini unachukua milioni moja unampatia mtu mmoja. Kwa kifupi bahati nasibu ni kama wizi. Unanyang'anya wengi mara milioni moja halafu unampatia mtu mmoja. Kwa hivyo zingeongezwa kiasi cha kwamba watu wasiwe na moyo wa kufanya huu mchezo wa bahati nasibu. Kwa masuala ya utozaji ushuru ningetaka kuchangia kwamba kuna wakati ambao vijana wengi waliambiwa kwamba wanahitajika wawe na PIN. Bila kujua kwa hari ya kuwa labda wapatiwa mikopo na vitu kama hivyo wakachukua PIN . La kushangaza baada ya miaka mitano ukitaka kuwasaidia hao vijana kwa kuwapatia kwa mfano zabuni wakienda Halmashauri ya Ukusanyaji Ushuru (KRA) kutafuta yale makaratasi yanahoyohitajika wanaambiwa walipe faini takriban elfu sitini kwa sababu walichukua PIN lakini hawakufuatilia. Kama mtu yuko kijijini ni vigumu apeleke yale makaratasi yanayohitajika hata kama ni kila mwaka. Kwa hivyo katika masuala ya utoaji wa ushuru na faini ninaona kwamba mambo kama haya yangeangaliwa hasa kwa wale vijana ambao walipata PIN na hawajapata ajira yoyote wala hawajafanya biashara. Jambo lingine ambalo ningetaka kuongeza ni kuhusu hii Big Four Agenda za Mheshimiwa Rais. Mojawapo ni usambazaji wa nyumba ambazo zitaweza kufaidi wananchi. Hapo ningeomba ushuru kwa upande wa mbao zinazoletwa kutoka nchi za nje zizitozwe ushuru ziziwekewe vyeti kwa sababu zikiwekewa hapa Kenya tunajua kwamba tumepiga marufuku ukataji wa miti naona moja kwa moja kutachangia ajenda isiweze kutimia ilhali ni ajenda ya ufaa kwa wananchi. La mwisho ni suala la madawa na ule ushuru ambao umewekwa. Tunajua kwamba mara nyingi wale ambao wana pesa huenda India kwa matibabu. Lakini wananchi wengi hawana huo uwezo. Upande wa kule Pwani utakuta wengi wanategemea sana madaktari wa miti shamba. Utaona mtu anajiita daktari lakini huyu ni daktari wa miti shamba si daktari halisi. Hii ni kwa sababu ya bei ya madawa ambayo wengi hawawezi kujihimidi. Ikizidi tunajua wengi kwa upande wa Pwani wanalazimika kuvuka mpaka kuenda nchi jirani ambayo matibabu iko chini. Kwa hivyo moja kwa moja naunga mkono huu Mswada lakini kwa upande wa madawa na matibabu lazima tuingalie upya. Hata tukisema tutapeana ule mradi wa kila mwananchi aweze kujisajili kwa NHIF najua itachukua muda mrefu. Sioni kama mwananchi anastahili kuumia wakati tukingojea ile miradi ya Serikali ambayo itafuatilia. Kwa hayo machache ninaunga mkono nikiongeza maoni ambayo nimetanguliza hapo mbeleni. Asante.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Ninamuunga mkono Mbunge ambaye alikuwa mgeni wangu wa heshima. Si mara ya kwanza Mhe. Sankok amekwenda kwenye eneo Bunge langu na kufanya kazi nzuri. Alikuwa mgeni wangu wa heshima nilipokuwa nikizindua kitabu kuhusu muhula wangu wa pili. Kama alivyosema ni kweli kwamba hazina ya NG-CDF inaweza kufanya kazi vizuri sana iwapo itakua na mikakati ambayo inatakikana. Ninamshukuru kwa kuitikia mwito wa kuwa mgeni wangu wa heshima. Alikuja wakati mlemavu mmoja ambaye alikuwa mwalimu alikuwa amekatazwa kushikilia kuwa mkubwa wa shule kwa sababu yeye ni kiwete na akamtetea. Kwa hiyvo namshukuru. Yeye ni rafiki yangu wa karibu katika kazi ambayo ninafanya. Kuna mambo nyeti yanapaswa kuangaliwa tukizungumzia mambo ya NG-CDF. Tunapaswa kuangalia shinda nyingi zinatoka wapi. Serikali kuu lazima ielewe kitu kimoja: Waziri anasema ni lazima kila mtoto aende shule. Ni kweli na ni haki kwa kila mtoto kuenda shule lakini wakisema hivyo wajiulize huyu mtoto ataenda darasa gani ataketi kwa kiti gani na ni walimu wagani watamsomesha. Haya ndiyo mambo nyeti wanahitaji kuangalia. Lakini sikusema tu ni lazima watoto wote wawe darasani. Kazi ya Wabunge ni mambo mawili: Kuangalia usalama na elimu. Mambo haya yasiwe yakusukumia Wabunge ili waonekane hawafanyi kazi. Kwanza tukirudi kwa hospitali ni lazima tuchunge mambo ya Serikali kuu. Serikali kuu imesema kuwa maternity nursery primary na elimu ya secondary itakuwa ya bure na ukiingia university unapewa pesa. Sasa kazi ya mzazi itakuwa ni nini? Board ya shule haiwezi kusema kuwa hata choo ikianguka na NG-CDF haina pesa haiwezi kuwaambia wazazi wachange pesa kwa sababu wameambiwa elimu ni ya bure. Kwani mtoto ni wa Serikali? Mzazi pia ana jukumu la kuangalia mambo nyeti katika shule ili asaidie. Lakini tumeweka ugonjwa wa kusema kila kitu ni bure. Kwa kweli hakuna kitu cha bure. Wanasema maternity ni bure lakini juzi tumeona mtu akimtoa mtoto wake kwa Hospitali ya Kenyatta kwa i kwa kukosa kulipa ada ya hospitali. Kama maternity ni ya bure kwa nini huyo mtu alienda kumtoa mtoto wake kwa hospitali kama amejificha? Si ukweli eti kila kitu ni cha bure. Mtoto hawezi kuwa darasani bila kuchanga pesa yoyote. Kwa hivyo ningetaka kuomba Serikali yetu ichunguze na Waziri akisema jambo fulani litakuwa la bure inatupasa kuangalia jambo hilo ili wasije wakawawekelea Wabunge mzigo ambao hawawezi. Katika maeneo mengine watoto wanasimama darasani kwa sababu hawana viti. Hawana mahali pa kuketi na hata mawe hayapatikani bure. Yananunuliwa na hiyo pesa ya kununua hakuna. Haya ni mambo nyeti ambayo yanapaswa kuangaliwa. Kuma mambo ambayo tunahitaji kuangalia na kuiambia Serikali kuu ili wakisema kitu wawahusishe Wabunge. Wabunge wako na mzigo mkubwa sana. Ni muhimu kwa kila mtoto kuenda shule lakini ukiangalia mikakati ambayo imewekwa hairuhusu kila mtoto kuwa shuleni. Hakuna madarasa mijengo na barabara za kuingia shuleni. Kwa hivyo kuna mambo nyeti mengi. Pia naunga mkono mazungumzo haya ya NG-CDF kwa sababu inasaidia sana. Nakubaliana na ndugu yangu Mhe. Sankok. Katika eneo Bunge langu ninajenga madarasa kama vile alivyosema nikitumia Kshs800000. Haya madarasa yako na tiles key ceiling na kila kitu. Nitaongeza iwe Kshs1 milioni ili nikipatiana darasa liwe na kila kitu. Hii ni kwa sababu unapata hakuna viti na wazazi hawawezi kuitishwa pesa za viti. Kwa hivyo inabidi tuongeze pesa kutoka kwa NG-CDF. Wakati huu tunazungumzia Bajeti ambayo inakuja. Bajeti tuliyopitisha tumebakisha miezi minne ili tupitishe nyingine na hizo pesa mpaka sasa hazijatoka. Unapata watoto wanasukumwa huko kwa sababu pesa hazijatoka. Tukipitisha Bajeti inayokuja itakuwa ya mwaka mwingine na itapitana na ya mwaka jana kama pesa hazitatoka. Hili ni jambo nyeti. Serikali inapaswa kuangalia mambo gani yanapaswa kupewa kipao mbele ili Mbunge aweze kusaidia. Kwa mfano ukiangalia katika maeneo bunge Wabunge wamefanya kila kitu. Wamejenga madarasa laboratories na kila kitu kinaendelea. Ukienda kwa magavana wanatumia Kshs1.5 milion kujenga darasa moja na hata hilo darasa likitingizwa na upepo litaanguka. Sitaki kuwatetea MCAs lakini nataka kusema kuwa wangepewa pesa kama Wabunge kwa sababu sisi tuko hapo kwa sababu ya public participation lakini pesa iko na fundager na accountant . Hata kama tunataka kuwasaidia MCAs kuna constituency na wardadministrator s ambao hatujui wanafanya nini. Wanapaswa kupatiwa hizo pesa ili MCAs wawe patron kama Wabunge ili tuone kazi ambayo hizo pesa zinafanya. Lakini pesa inatumiwa huko juu inakuliwa na kuibiwa na MCAs wanabebeshwa mzigo kwa sababu hawana kitu cha kuonyesha kazi ambayo wamefanya. Nimesikia kutoka kwa Wabunge wengi kuwa mwelekeo na maoni yao ni kurekebisha mambo yanayosumbua. Wabunge wanafaa kuongea ukweli. Unajua hii mambo ya handshake tulifikiria watawatetea wananchi kwa sababu wako minority . I am happy I can see what the party and the Opposition are doing. Theyare still playing their role kusaidia kupigania haki. Ningetaka kusema kuwa nchi hii kama haina minority ni majority pekee pesa za umma zitaibiwa na kila kitu kitakwisha. Ninafurahi kwa kazi ambayo wanafanya kutetea mambo mabaya ambayo Serikali inaweza kufanya. Nimeona ndani ya Bunge hili tuko pamoja. Wakati mwingine tulikuwa tunapigana kisiasi lakini jukumu letu sisi wote ni kutetea mwananchi na kusikizana kwa mambo yaliyo mbele yetu. Hakuna Mbunge wa minority au majority. Kazi yetu na shida zetu zote ni sawa. Nashukuru wale Wabunge ambao wameunga mkono jambo hili ili turekebisha mambo ambayo tunaona yatatusumbua ili tufikishe maendeleo mashinani. Lakini Serikali kuu haipaswi kusema kila kitu ni cha bure kwa sababu italeta shida. Hata mama akijaribu kusema jambo fulani mzee anasema kila kitu ni cha bure na kwa hivyo waendelee. Tukiendelea hivyo bila mpango tutakuwa na shida ya kuzaliwa kwa watoto wengi. Kwa hayo machache nashukuru.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Ninatoa shukrani zangu kwa ndugu yangu Wario kwa kunipatia fursa hii. Kwanza watu wetu ndio wamedhulumiwa na serikali bali sisi ni Wakenya. Sehemu ambayo ametaja Kalalani imekuwa hata kabla huyu Mhe. azaliwe. Kwa hivyo akidai Kalalani iko kwake anatushangaza. Huko Tana River tuko na game reserves nyingi sana kama nusu ya Tsavo National Park Kora National Reserve Tana Primate Reserve na Kipini Conservancy . Tuko na game reserves na conservancies zaidi ya nusu ya Tana River. Sisi tunaishi vizuri na majirani wetu. Hata ndiyo maana mara nyinyi Tana River humpigia Kalonzo Musyoka kura kwa sababu ni jirani wetu. Sasa Mhe. Nyamai IG Mutyambai ambaye ametoka hiyo sehemu pamoja na Governor Charity wamechukua nafasi hii kuwadhulumu watu wa Tana River. Mama anafaa kuwa na huruma lakini huyu ameonyesha wazi hana huruma. Saa hii wamama wenzake na watoto wao wako kwa baridi. Lakini yeye anaongea hapa kama wale ndio wauaji. Je watu wa Kalalani ama Inyali ni wauaji? Watu wa Tana River ni wakarimu sana. Lakini huu ukarimu wetu usichukuliwe kuwa uoga. Sisi tunasema kwamba Serikali ichukue hatua na Mutyambai ajiiuzulu kwa sababu hafai kuwa Inspector-General wa Polisi. Ametakesides. Kwa vile Mhe. Nyamai na Mhe. Charity wanatoka kwa jamii yake wameshirikiana kukandamiza watu wa Tana River. Kwa hivyo Mutyambai kwanza ajiuzulu na Serikali ichukue hatua dhidi yake. Asante sana.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua fursa hii kupongeza Ripoti hii na kusihi wenzetu kutoka sehemu tofauti za Kenya waweze kuikubali. Maswala ya ardhi ni yenye chembechembe za historia kali katika Kenya. Pengine ungeweza kunisaidia na kikundi cha ndugu zetu walioko pale nyuma ambao wanaozungumza lugha ya short wave kidogo.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Pia nami naunga mkono Hoja hii. Natoa shukrani kwa wenzangu kwa ile kazi nzuri wamefanya mwaka huu. Vile vile Kenya imepata majanga; kumekuwa na shida Garissa ambapo tulipoteza wanafunzi wengi. Kenya pia imekuwa na matatizo mengine mengi. Lakini juu ya hapo mwaka huu tumepata baraka. Tumepata Rais Obama pamoja na Baba Mtakatifu wa Kikatoliki aliyekuja nchi yetu. Nataka kuwaombea Wakenya heri njema ya Krismasi na Mwaka Mpya ulio na mafanikio. Vile vile nawaomba wenzangu wanapokwenda waeneze habari njema ya upendo na umoja. Tusimame kidete kama Wakenya tukifurahia nchi yetu. Asante sana.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Sheria za Bunge zinasema kwamba ukianza na lugha moja utaendelea nayo. Mheshimiwa M'eruaki alianza kwa Kiswahili. Kwa hivyo aendelee nacho.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Vile ambavyo mwenzangu amesema ni kweli kabisa. Mimi ninawakilisha wananchi na ni lazima tuangalie vile hawa
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Wenzangu wa upande ule wa pili walikuwa wananiita niende upande ule lakini Wakenya wangeona nimewasaliti na ikawa ni bora nikae huku. Ninakubaliana na utaratibu wa mwendo ambao umeletwa kwa lugha maarufu ya Kiingereza " Procedural Motion" ili kuweka muda wa ambao utahakikisha kila mmoja ananafasi ya kujadili na kutoa maoni yake katika maswala haya. Hili ni jambo ambalo halitasaidia Bunge hili peke yake lakini pia litaweza kusaidia Wabunge wajao watakaokaa katika viti vivi hivi na watakaozingirwa na kuta zizi hizi. Wengi wameyazungumzia mambo haya. Ninaomba unipatie fursa na wenzangu wanipatie fursa nitaje hili swala. Kila mmoja wetu alipokuwa anaomba kura na kuzungumza katika mashinani tulikuwa tuna mrengo fulani ambao tulikuwa tunafuata. Sisi wana CORD tunaamini ule mrengo ndio njia mwafaka ya kuendesha hii nchi. Yamezungumzwa mengi kuwa watu wakiwa wametolewa katika kamati fulani itakuwa wamefanyiwa dhambi. Lakini lile tunalisahau ni kwa njia ile dhambi inavyofanyiwa wale Wakenya wote wengine waliobaki. Hii ni kwa sababu ikiwa utakuwa ni mwenye kuingia katika kamati fulani na mawazo yako na maoni yako hayalingani na yale matakwa ya Wakenya waliokupigia kura Hii ni kwa sababu waliokupigia kura walifanya hivyo kwa minajili ya ile ifesto ambayo uliitoa wakati ule ulikuwa unaomba kura. Japo tunazungumza na ninaskitika kuwa tumelifanya hili jambo likawa ni la kubinafsishwa kwamba mtu fulani ametolewa katika kamati wale wengine watakaoingia katika zile kamati hawawezi kulifanya lile jambo. Kuna tatizo gani ikiwa wataweza kulifanya na waifanye ile kazi kwa njia mwafaka na inayofaa. Ninajua wenzangu hapa hupenda sana kwenda nyuma ya zile kanuni na sharia za Bunge wakiona fikira na akili zimewashinda. Hupenda kuenda nyuma na kuyatumia yale maswala ya nidhamu na mambo mengine kama vile anavyofanya. Inafaa tuwe ni wenye kuhoji kwa akili. Tukiwa tunazungumza kuwa tuna njia na tunataka watu wawe katika kamati waweze kupendekeza matakwa ya wakenya tuachieni kwa sababu sisi ni sauti ya wakenya. Hatuko hapa kuzungumza sauti ya mtu mmoja bali ni sauti ya wakenya ndio inazungumzwa hapa.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika. Najua Mheshimiwa Junet hakifahamu Kiswahili vizuri. Neno "petishoni" liko katika kamusi ya Kiswahili. Naunga mkono kwamba swala hili liangaliwe kwa kina.
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika. Naunga mkono Mswada huu. Mambo ya wanyama wetu ni mengi. Niko katika Kamati ya Ukulima. Kila wakati huwa tunajiuliza ni kwa nini wafugaji wetu hawana njia yoyote ya kufaidika kutokana na wanyama wao. Sababu ya kutofaidika ni kwamba hawana soko lolote la kuuza wanyama. Hawana mahali pa kuchinjia wanyama. Katika Kenya nzima hakuna mtu anayeweza kula chakula bila nyama. Unapokula nyama ndipo unahisi umekula chakula. Wanaofuga wanyama huwa wanaumia sana kwa sababu wakati wa ukame wanyama wote wanakufa kwa sababu hakuna mahali pa kuwauza. Wakati mvua inaponyesha na wanyama wanapopata nguvu wafugaji wanakosa mahali pa kuwauza. Ni muhimu kwangu kuunga wenzangu mkono kusema kuwa tuwe na bodi ya kushughulikia mambo ya wanyama. Ni muhimu kwa sababu wafugaji wa wanyama wanaumia kwa sababu hawana njia yoyote ya kufaidika au kusaidia familia zao kutokana na wanyama wao. Wale wanaokuza miwa majani na kahawa wako na njia zote za kujisaidia. Wana soko. Kwa mfano kuna soko la Kahawa ya Kenya katika kila nchi. Tukipata bodi inayoweza kuwasaidia wafugaji wa wanyama watapata njia za kufaidika. Tunajua vizuri sana kwamba wafugaji wa wanyama humu nchini hawana njia yoyote ya kujifaidisha isipokuwa kutokana na hao wanyama. Kule Samburu ninakotoka na katika sehemu nyingine kama Laikipia Turkana na Pokot utaona wanyama wanapigwa risasi kama wanyamapori. Kwa sababu hakuna nyasi huwa wanauliwa kama wanyama wa mwituni. Hata wanyamapori hawauliwi jinsi wanyama wetu wanavyouliwa wakati wa ukame. Tukipata bodi inaweza kutusaidia kujua ni njia gani mfugaji anaweza kujisaidia nayo kutokana na wanyama anaofuga. Wafugaji hawana shamba lingine. Shamba lao ni hao wanyama wao. Kunapaswa kuwa na vichinjio katika kaunti zao ili wapate mahali pa kusafirisha nyama. Hata wakiwa na maziwa hawana mahali pa kuyasafirisha. Itakuwa muhimu sana tukiwa na bodi hiyo kwa sababu itatusaidia na kuwasaidia wafugaji. Inafaa Serikali ianze kutafuta soko la kusaidia wafugaji wapate mahali pa kuuzia wanyama wao. Masoko yanapatikana kila mahali mnyama yuko lakini wanajinunulia wenyewe tu. Hakuna mahali pa kuuza wanyama wao na wapate pesa nzuri. Kenya Meat Commission ilikufa kitambo. Haina mahali popote. Hata wanyama wakipelekwa huko watu wanaweza kukaa hata miezi sita au mwaka mmoja bila kulipwa. Zile kilo za nyama wanapeleka KMC ni za kuumiza. Kuna wafugaji wengine Wazungu kule Laikipia. Wakipeleka ng'ombe wao huwa wanatoa kilo 500 au 600 na wetu wanatoa kilo 200. Hatuna njia ya kuwafunza wafugaji wetu jinsi ya kuwalisha ng'ombe wao ili wapate kilo hizo. Kwa hivyo wafugaji wanaumia. Vita tunavyopigana kuhusu wanyama wanaoibiwa ni kwa sababu ya umaskini. Una mali - ng'ombe na mbuzi - lakini huna mahali pa kuwauza. Huna mahali unaweza kujisaidia. Ingekuwa vizuri tupate bodi hiyo ili izingatie mambo ya wanyama kwa sababu ni muhimu sana wafugaji wafaidike. Naunga mkono Mswada huu.
Asante sana Mheshimiwa Naibu wa Spika wa Muda. Hata mimi ninaunga mkono mjadala na kutuma risala za rambi rambi kwa wakaazi wa West Pokot. Pia ningependa kuongeza sauti wakati jambo kama hili la huzuni limetokezea na kuwaomba Waheshimiwa wenzangu tusiwakejeli wenzetu. Wakati wenzetu wamepoteza watu wao na wanahuzunika sisi huku tunakuja kulifanya jambo la siasa hapa. Wengine bado hawajapata watu wao wala kuwazika na sisi hapa tunafanya siasa nyingi badala ya kutafuta suluhu ya kudumu ya hiyo shida. Mimi pia watu wangu wa Tana River tunavyozungumza kuanzia hapa Ziwani karibu na Garissa na Garseni sehemu ya Tana Delta watu wamepoteza makaazi mimea na hata mifugo yao. Hawana mahali pa kulala. Mimi pia ningeomba Serikali iwasaidie. Ile idara ambayo iko kwa kaunti hata kwa Serikali bado ipo. Kwa hivyo ninaomba Serikali iwasaidie wale walioadhirika na mafuriko na malazi chakula na hata madawa. Wakati wa mafuriko magonjwa mengi yanatokea. Mimi pia ningeomba suluhu ya kuduma ipatikane hasa kwa hili janga la mafuriko la Tana Delta. Wakati Tana and Athi Rivers Development Authority (TARDA) ilikuwa inaanza ule mradi wa kunyunyizia mchele maji waliweka ukuta mkubwa ambao waliuita band. Ile ni kama imeteremka kidogo. Ninaomba watu wa TARDA wauinue ule ukuta ili wazuie maji yasiingie kwa mashamba na majumba ya watu. Sehemu ya Ziwani maji yakifurika hata kidogo yanapenya na kuingia kwa mji. Pia ningeomba Serikali ijaribu kuziba hiyo barabara ya maji ambayo inapitisha maji saa zote kutoka kwa mto na yanaingia kwa eneo la Ziwani Bakuyu mpaka Garissa. Ninaomba tunapozungumza hapa tuwe tunachangia kutafuta suluhu lakini si malumbano. Asante.
Asante sana Mheshimiwa Spika kwa kunipa fursa hii kuliwaza familia ya marehemu aliyekuwa Mtukufu Rais wa pili Daniel Toroitich arap Moi. Namkumbuka marehemu kwa mambo matatu. La kwanza nilifaidika na maziwa ya bure. Pili wakati nilikuwa katika shule ya upili alipitia shuleni kwetu na tulipoenda kumwimbia alinipa kifurushi cha pesa ambacho nilipeleka shuleni tukachinjiwa ng'ombe na tukanywa soda. Hayo mambo yalinifanya nimpende sana Rais Moi na kumkumbuka siku nyingi kwa sababu wakati huo shule nzima ilinisalimia ili wasikie mguzo wa mkono wa Rais.
Asante sana Mheshimiwa Spika kwa kunipatia fursa hii. Vile vile watu wa Taita County haswa Mwatate wanaunga mkono malalamishi na kilio kuhusu wanyama pori haswa vile wanaharibu mimea na kuua watu lakini hakuna malipo yoyote. Kitu ambacho kimetushangaza zaidi ni kwamba watu wanabebeshwa mizigo juu ya mingine. Ndovu wanatolewa Laikipia na kupelekwa Mbuga ya Wanyama Pori ya Tsavo. Badala ya kumaliza hiyo taabu kule Laikipia wanatupelekea hiyo taabu kule Taita. Tafadhali tunaomba wakati mnaanaglia hili suala la malalamishi jaribuni kuliangalia vyema. Tayari ukiangalia orodha ya malipo ya fidia Kenya nzima wakazi wa Taita Taveta County ndio wanaodai hela nyingi zaidi. Sasa ndovu wanatolewa kwingineko na kupelekwa kule kwetu. Ni kilio kikubwa tumepoteza watu wengi. Hivi sasa twafa njaa kwa sababu ya uharibifu wa mimea uliotekelezwa na wanyama pori. Hivi juzi niliwaelezea watu wangu kule Mwatate kwamba Katiba inaruhusu wakati mumevamiwa na wanyama tafadhali muleni ndiyo pengine KWS wataamka kidogo. Mheshimiwa Spika ninashukuru sana kwa fursa hii.
Asante sana Mheshimiwa Spika Kwa niaba ya wananchi na wapiga kura wote wa Mosop wamenia
Asante Sana Mheshimiwa Spika Nami nataka kuunga mkono Maombi yaliyoletwa na wakaazi wa Makueni Ni kweli Mheshimiwa Spika mwenzangu wa Taita Taveta ameongea na mimi nitasema kwa uchache sana kwamba kilichobaki sasa si mazungumzo tu Tumeongea na KWS kwa muda mrefu Tumeongea na Wizara kwa muda mrefu lakini muda wote huo hatujapata nafuu ama afueni katika maswala haya Tumeona ni watu ambao wanasema mambo ambayo hawatekelezi Kule kwangu Wundanyi kuna sehemu inaitwa Kishushe Wiki iliyopita shule sita zilivamiwa na ndovu matanki ambayo tumenunua na pesa za NG-CDF yakabomolewa Jana nilikuwa kwa Ofisi ya PS kumuliza ni vipi wanaweza angalau kufidia matanki yale maanake shule zimefunguliwa na ndio wazazi hawajaruhusu watoto wao kwenda shuleni kwa uoga wa ndovu Mheshimiwa Spika Ndovu wa siku hizi ni kama kidogo nao pia wamepiga hatua ya Karne ya 21 Kwasababu gani? Kule kwangu wanakunywa maji kwa matanki kwa juu halafu maji yakipungua na mikono yao haifiki kwa maji wanayabomoa ndiyo wayafikie hayo maji Utakuta kwamba nina matanki karibu sita Ijumaa iliyopita nilikuwa kule Sasa wamefika mahali ambapo wanatoboa mabati ya nyumba ili wachungulie ndani ama waingize mikono waangalie kama kuna chakula ama chochote Mheshimiwa Spika tuna tatizo na mimi naomba hivi: Tunapoangazia maswala ya wanyamapori kuvamia mashamba na mifugo na maisha ya wananchi tusiangalie sana tu ndovu ama simba Mwenzangu amesema kwake ni ndege Sasa kuna tatizo lingine sugu Nilileta Swali ambalo lilijibiwa na Waziri lakini halikujibiwa mwafaka Mheshimiwa Spika kuna tumbiri kwangu milii ambao wanasumbua na huku chini ni ndovu Sasa tunaomba tu Wizara ichukulie mambo haya kwa uzito Mwisho kila mara wanasema hawana pesa za kufidia lakini wakati SGR ikijengwa KWS ilifidiwa karibu Kshs6 bilioni Pesa zile wao wakatumia kwa mambo yao badala ya kufidia wananchi Kwa hivyo Mheshimiwa Spika swala hili ni la msingi na ni zito ambalo nchi hii yatakana iangazie Asante Mheshimiwa Spika
Asante sana Mheshimiwa Spika. Hii Ripoti inaonyesha wazi kuwa watu hutumia sukari kufanya mifuko yao iwe mitamu. Ninataka kuwakumbusha kwamba kuna baadhi ya Wabunge walitaja kuwa mambo ya sukari ni ya kwao lakini kwa hekima za wakoloni kiwanda cha kwanza kilianzishwa Kenya mnamo mwaka wa 1922 katika sehemu ya Miwani. Kiwanda cha pili kilikuwa Pwani mnamo mwaka wa 1927 kule Ramisi. Serikali zote ambazo zimepita zimedharau sekta hii. Ni hamu yetu kuwa tutaweza kuiinua sekta hii. Hii Ripoti ililetwa katika Bunge mwezi wa Machi mwaka wa 2015. Ilipoletwa Kenya ilikuwa na pazia ya kujisitiri na sheria za COMESA. Hizo sheria zikawa zinasitiri Wakenya kuwa hakuna sukari itakayoingia mpaka mwezi wa Februari mwaka wa 2016 na tayari tumeipita. Ndiyo maana kila siku mimi husema kwamba kuna haja ya kila tunachokizungumzia ama tunachokifanya tuangalie na tujue kwamba kuna wenzetu katika sehemu nyingine ulimwenguni ambao wanafanya mambo yao pia. Tunajadili Ripoti hizi zikiwa zimepitwa na wakati. Ninawaomba Wabunge wenzangu waniazime maskio yao. Mwaka wa 2015 Baraza la Mawaziri liliidhinisha ubinafsishaji wa viwanda vyote vitano vya sukari ambavyo vinamilikiwa na Serikali ya Kenya. Mimi ni Mwanachama wa Kamati inayohusika na masuala ya fedha. Katika mwezi wa Aprili 2005 Bunge hili lilipitisha Hoja ambayo ilisema kwamba kabla ya viwanda hivyo kubinafsishwa ni lazima Serikali ilete Miswada ya uwiano na serikali za Kaunti ili tujue kwamba tunaweza kubinafsisha viwanda hivyo bila wakulima kupoteza raslimali zao. Simuoni Mwenyekiti wa Kamati inayohusika na masuala ya kilimo ufugaji na uvuvi. Sitaki kuifanya hii kuwa hoja lakini ninawaomba wahusika waangalie iwapo kulikuwa na makosa walipokuwa wakichapisha Ripoti hii. Wao wameandika kwamba Bunge hili lilipitisha Mswada huu Februari 2013 lakini Hoja hiyo ilipitishwa katika Bunge na Kamati inayohusika na Fedha ambayo mimi ni mmoja wao mnamo Aprili 2015. Ninaomba Mhe. Spika ukumbuke jambo hili. Tunapojikumbusha pia tunaikumbusha Serikali umuhimu wa sekta ya sukari. Miwa nchini Kenya inakuzwa kwenye ardhi ya hektari 2000. Zaidi ya wakenya laki tatu ni wakulima wa miwa. Sekta ya sukari kwa njia moja au nyingine inatoa ajira kwa Wakenya milioni sita. Idadi hii ni asilimia 16 ya Wakenya wote. Hii si idadi ndogo. Sekta ya sukari inachangia uchumi wa Kenya kwa kiasi cha asilimia 7.5. Ndio maana tunasisitiza kwamba Serikali ilete sheria inayoambatana na Hoja iliyoletwa hapa na Kamati inayohusika na masuala ya fedha na kupitishwa na Bunge hili. Tunataka sheria ipitishwe na Bunge hili ili wakulima wasidhoofike. Tunayaomba mashirika husika yachunguze ni kwa nini hektari moja ya miwa nchini Colombia inaweza kutoa tani 115 za sukari ilhali nchini Kenya hektari moja ya miwa inatoa tani 60.5 za sukari pekee. Ni lazima pia tujiulize ni kwa nini gharama ya kukuza miwa nchini Kenya ni US$2.5 kwa kila tani ya sukari ilhali katika nchi jirani gharama hiyo ni US$13 pekee kwa kila tani ya sukari. Ni lazima pia tujue ni kwa nini gharama ya kusaga sukari nchini Kenya ni US$700 kwa kila tani kwa mkulima ambaye hakuchukua mkopo kutoka kwa benki na US$870 kwa kila tani kwa mkulima ambaye amechukua mkopo kutoka kwa benki ilhali nchini Malawi gharama hiyo ni US$350 kwa kila tani nchini Zambia ni US$400 na nchini Brazil ni US$300 pekee. Mambo haya hayawezi kufanywa na mtu binafsi awe ni Mbunge ama mtu mwingine yeyote. Serikali ndiyo yenye uwezo na wadhifa wa kuangazia masuala hayo. Ningependa kuelezea tena umuhimu wa Serikali kuwa na mshikao. Kuna ripoti ambayo ilichapishwa katika mwaka wa 2013/2014. Kila mtu anaweza kuipata na kuisoma ripoti hiyo. Kulingana na ripoti hiyo tani 15140.4 ziliingizwa humu nchini na kutumiwa na wakenya. Sukari hiyo ililetwa kutoka sehemu tofauti za ulimwengu. Bodi ya Sukari Nchini (KSB) haikuidhinisha kuingizwa kwa sukari hiyo nchini Kenya. Wamiliki wa kampuni tano pekee ndio walionufaika kutokana na mauzo ya sukari hiyo ilhali Wakenya wengine wakilalamika tu na kuishi katika hali ya uchungu kama shubiri. Hadi leo hakuna mtu hata mmoja katika halmashauri ya ushuru nchini ambaye amechukuliwa hatua ya kisheria na kupelekwa mahakai kwa sababu ya sakata hiyo. Hili suala liliangaziwa na Kamati hii. Suala hilo lilijadiliwa kwa kina na ushahidi kwamba tani 15140.4 za sukari ziliingizwa humu nchini katika mwaka wa 2013/2014. Ningependa kuipongeza Kamati yetu inayohusika na ukulima kwa kazi njema waliofanya. Ninaomba tena upande wa Serikali uwe mchangamfu. Suluhisho la kuboresha sekta ya sukari nchini si kufurahisha Wabunge ama watu wengine kwa kusema kuwa watatoa billioni moja kwa kiwanda kinachoanguka. Suluhisho ni kuangalia mambo haya ili kesho tuudie kusema kwamba Wakenya wanapoteza pesa zao. Hilo ndilo suluhisho na haya ndio matakwa ya Wakenya ambayo tunafaa kuyazungumzia hapa Bungeni.
Asante sana Mheshimiwa Spika. Kuna mtu hapa analia akisema umenihurumia zaidi kwa sababu yeye amebonyeza mbele yangu. Hata hivyo achana naye. Nataka kuchukua nafasi hii nikushukuru kwa kunipatia wakati huu. Ni fikra yangu kwamba walioleta Mswada huu hawajui wanakoelekea. Mimi naupinga kikamilifu. Mtindo wa Harambee ambao umeletwa na mwanzilishi wa taifa hili Mzee Jomo Kenyatta uungwe mkono mia kwa mia na watu waendelee na shughuli hizo kila uchao. Mheshimiwa Spika wengi hapa hawataki kujieleza lakini tunajua kwamba wamesomeshwa kwa njia ya Harambee. Hata nakumbuka siku moja nilienda Harambee ya Mheshimiwa Duale tukamchangia kwa sababu hili ni jambo ambalo ni muhimu sana. Kwa hivyo ikiwa kiongozi wa walio wengi alifanyiwa Harambee mwingine nani ambaye anaweza kusema ya kwamba Harambee hazifai? Mheshimiwa Spika ingawa rafiki yangu hapa pia amesema kwamba kuwe na marekebisho ili mradi ambao umefanywa kupitia kwa NG-CDF usifanyiwe Harambee mimi nataka kumwambia kwamba hata kama mradi umegharamiwa na NG-CDF lakini umekwama bado Harambee ni muhimu. Ningependa kumfahamisha ndugu yangu ya kwambe pesa ya NG-CDF haitoshi kabisa kumaliza tatizo la uhaba wa mijengo katika nchi hii. Mimi naunga mkono kauli kwamba Harambee ziendelee haswa nikijua ya kwamba Serikali haitii mkono wake katika masuala ya makanisa na miskiti. Mambo ya Harambee kama alivyozungumza mwenzangu ndiyo yamefanya wagonjwa wengi waweze kupata tiba nje ya nchi hii. Kwa hivyo yeyote anayepinga suala hili basi ana kichaa fulani ama ana upungufu ambao yeye mwenyewe hajijui. Asante Mheshimiwa Spika na mimi ninapinga.
Asante sana Mheshimiwa Spika. Kwa kweli ule wembe Mheshimiwa Jessica Mbalu anapitia ndio huo huo ambao unatunyonga katika sehemu za Taita Taveta. Hata akitaja Mtito Andei mimi nafahamu kuwa Mtito Andei iko Taita Taveta. Kwa kweli nimelalamikia sana hili suala la wanyama. Masuala ya kutatua hili tatizo.
Asante sana Mheshimiwa Spika. Kwanza jambo la kusikitisha ni kuwa ukiangalia sababu ya wao kutoweza kulitoa lile gari pale lilipozama ni kwa sababu wameshindwa kupeana hewa ya kununua ambayo itakwenda mita 60 chini. Hewa walionayo ni ile ambayo inaweza kwenda mita 30 chini. Kule sehemu tunazotoka kama Vanga kuna vijana ambao ni wenyeji wazoefu na wanaweza kwenda mita kama 60 chini na wakakaa kama masaa mawili bila kuwa na oxygen ya kununua. Sababu ya mambo kama haya kutokea ni pengine wale wanaoajiriwa pengine wana uzoefu wa kuogolea kwenye mabwawa au swimming pool lakini hawana uzoefu wa kuogelea kwenye maji. Mbali na hivyo ile sehemu ya Likoni ambayo tunaizungumzia ni sehemu ambayo ina papa. Nafikiri kila mmoja ana utamu wa roho yake. Ikiwa umekuzwa katika hali ya kuwa uko ndani ya bahari kila siku basi nina ii ni sawa na maasai ambaye yuko kichakani. Maasai anaweza kuwa amesimama hapa simba yuko pale na hana wasiwasi. Mimi na wewe ambao hatujazoea tukiwa ndani ya gari na simba yuko nje tuko na wasiwasi. Ni kama yule diver ambaye amezoea na hakusoma kufika Form Four lakini ana uwezo wa kuingia pale ndani akasaidia janga kama lile. Ni muhimu sana tulipatie nafasi jioni ili tulizungumzie kindani na liweze kueleweka.
Asante sana Mheshimiwa Spika. Mimi naungana na viongozi wenzangu siku hii ya leo kwa niaba yangu mwenyewe na familia yangu na kwa niaba ya wananchi wangu wote wa eneo Bunge la Jomvu kutoa rambirambi kwa kifo cha Mheshimiwa Otieno Kajwang'. Leo ni siku ya huzuni sana katika nchi yetu ya Kenya. Nikisema hivyo nachukua yale ambaye niko nayo mimi mwenyewe binafsi juu ya Mheshimiwa Otieno Kajwang'. Miaka mitatu iliyopita nilikuwa kinara wa chama cha ODM katika eneo Bunge la Changamwe. Wakati huo tulifanya kazi pamoja tukishirikiana sote pamoja na vile vile katika uchaguzi uliopita hivi punde. Yale ambayo yaliweza kutokea kwangu mimi mwenyewe binafsi katika watu ambao waliniita na kuniambia "pambana endelea mbele na usife moyo" mmoja ni Mheshimiwa Otieno Kajwang'. Leo ninasema kuwa hii ni funzo kubwa katika ulimwengu kwa ajili jana mwenzetu kiongozi alikuwa mzima na leo hii tunazungumza akiwa yuko mahali pengine. Kwa hivyo mimi mwenyewe binafsi na familia yangu na eneo Bunge langu la Jomvu nasema kuwa tunaomboleza pamoja na watu wote na familia zao ili Mungu aweze kumweka mahali pema peponi. Shukrani sana na Mwenyezi Mungu amweke mahali pema.
Asante sana Mheshimiwa Spika. Nami pia naunga mkono wenzangu ndugu Raymond and ndugu Gideon na jamii yote ya Mzee Moi pamoja na jamii ya Wakenya wote kwa ujumla kutoa risala zangu za rambirambi kwa niaba yangu na jamii yangu na watu wote wa Taveta kupeana pole kwa jamii ya mwendazake. Ni wazi kuwa Mzee Moi alikuwa mcha Mungu aliyefuata maadili ya Mwenyezi Mungu. Alikuwa mzee wa heshima ambaye aliheshimiwa katika Kenya na ulimwengu mzima kwa ujumla. Naomba Wakenya wenzangu wampe Mzee heshima yake kwa sababu heshima si utumwa. Mola amweke pahali pema peponi.
Asante sana Mheshimiwa Spika. Nimesimama kuhusu orodha kamili ya majina yaliyotolewa ambayo yanawakilisha mrengo wa NASA kwenye uongozi wa Bunge hili. Msimamo wangu ni kwamba ninaupinga moja kwa moja. Kwanza suala la jinsia halikuzingatiwa kabisa. Pili hii imeashiria wazi kwamba uongozi wa chama umeelekezwa Nyanza pekee na sehemu nyingine zote zimeachwa nje. Hali hii inatuonyesha wazi kwamba uongozi wa muungana wa NASA unapopangwa ni lazima wanachama waitwe kwenye kikao. Ni wazi kwamba taratibu inayotakikana ifuatwe wakati kunapangwa uongonzi haikufuatwa. Nilazima wanachama waitwe kuhudhuria kikao kwa lugha ya kimombo cha Parliamentary Group (PG). Na hii haikufanyika. Kwa hivyo mimi kama mwenyekiti wa wabunge wa Pwani hili swala tunalipinga kwa sababu sisi kama Wapwani tumechangia sana mlengo wa NASA. Mhe Spika hii ni wazi kwamba sisi kama Wapwani na watu wa sehemu zingine hatutambuliwi katika hii chama. Tunasema wazi kwamba kama Wapwani tunayapinga haya majina kikamilifu na tutasimama kuyapinga na hatuyatambui tuta resist kama vile wao wana resist . Asante sana.
Asante sana Naibu Mhe. Spika Wa Muda. Mimi pia napata nafasi hii kuweza kuzungumzia Hotuba ya Mheshimiwa Rais na niseme ilikuwa ya kizalendo sana. Alizungumzia mambo mengi sana. Nimeskia Waheshimiwa wenzangu wakizungumzia janga la Corona. Jai hakuna ambaye hakumwona Mheshimiwa Rais aking'ang'ana wakati tulipata kesi ya kwanza ya Corona. Hata viongozi wengine tukiwemo sisi wenyewe tulisema ya kwamba Corona ni uongo na ni jambo la kutengenezea watu pesa na ni mambo ya propaganda . Kwa hivyo mimi nataka niseme kuwa wakati tunazungumzia ufisadi katika mambo ya Corona sisi Wabunge tuna jukumu la kuangazia mambo ambayo yalifanyika katika taifa letu la Kenya. Hata Bunge la Seneti lina nguvu ya kuangalia mambo ya afya katika kaunti zetu. Afya imegatuliwa na iko mashinani. Ningetaka kumwambia Mhe. Rais katika juhudi zake alizofanya kupigana na janga hili aongeze nguvu zaidi ili tuweze kupata vifaa na wahudumu wa afya zaidi na bima ya afya ya kitaifa ya kuweza kuangalia Wakenya kwa sababu ya janga hili. Vile vile Mhe. Rais alizungumzia kuhusu kujenga ajira laki moja ya vijana wetu. Nataka kushukuru mpango wa Kazi Mtaani . Huu mpango umeweza kuchukua vijana 26000 katika kauti 34. Kwa sababu janga la Corona linaendelea vijana waweze kuendelea na huu mpango na uweze kuangalia vijana wote katika kaunti zetu 47. Pia yale mapato wanapata yaweze kuangaziwa. Namshukuru Mhe. Rais kwa kutujengea daraja katika Eneo Bunge langu likishikana na Eneo Bunge la Mvita. Kwa sababu ya mambo ya Corona watu wa Likoni walikuwa na changamoto kubwa sana kujikinga na janga hili. Hivyo basi daraja hili litaweza kutusaidia kwa ule msongao na tuweze kusafiri na kuendelea na shughuli zetu. Pia Mhe. Rais alizungumzia ule mpango wa mambo ya boda boda. Hii ni njia moja ambayo itaweza kujenga ajira zaidi kwa vijana wetu kule nyanjani. Basi mpango kama huu uweze kusambaswa kule mashinani katika maeneo Bunge yetu na kauti zetu ili kujenga ajira. Mhe. Raisi alisema kuwa vijana wajitokeze ili waweze kupate mshahara na kuwa wamiliki wa fedha. Kwa hivyo ni lazima wajenge uwezo katika kupata zabuni kama za madeski za kufanya kazi ya kuleta vifaa vya kupigana na Corona na za ule mpango wa kutengeneza nyumba za kisasa katika makazi duni. Hii ni kwa sababu tunataka kuweka Wakenya katika hali nzuri. Mhe. Rais pia alizungumzia mambo ya mkusanyiko wa digiti au ditigisation ya mambo ya mashamba ama ardhi. Mimi ni mwanakamati wa Kamati ya Ardhi na tumeweza kutenga pesa na sasa hivi kuna kaunti ambazo tayari wameweza kuitumia. Kwa hivyo namuunga mkono Mhe. Rais kwa jambo kama hili. Pia mambo ya mafunzo ya vijana kuongeza madarasa madawati vifaa na waalimu ili ule mpito wa watoto kusoma kutoka shule ya msingi hadi shule ya upili uweze kupatikana ndiposa watoto wetu waweze kuwa na elimu. Mhe. Rais alivyozungumzia kuhusu watoto kurudi shuleni kufikia Januari mwaka ujao alisema kuwa mikakati iwekwe ili wazazi wasihangaishwe na mambo ya karo. Janga la Corona limerudisha nyuma uchumi wetu. Wazazi wapewe nafasi waweze kulipa kwa njia watakayoweza ili kusomesha watoto wao. Naunga mkono Mhe. Rais kwa mambo ambayo amefanya kama kutengeneza magari hapa Kenya. Yamekuwa assembled hapa na vijana walipata ajira. Pia mambo mengine kama kuweze kujenga viwanda katika taifa letu la Kenya kama sampuli iliyofanyika ili watoto wetu waweze kupata ajira.
Asante sana Naibu Mwenyekiti wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Kwanza ninashangaa ni kwa nini wenzangu wanafikiria kuwa sehemu hii iondolewe ili tuhakikishe kuwa mafuta na gesi zikipatikana basi watu wawili mwanakandarasi na waziri wakishakubaliana yameisha halafu ndio baadaye iletwe Bungeni. Kama kuna njia moja mbaya ya kuleta
Asante sana Naibu Mwenyekiti wa Muda. Nataka kupinga mabadiliko ambayo yamewekwa hapa kwa sababu ukiangalia hali ya mtoto msichana katika nchi yetu ya Kenya wakati wa kutumia zile sodo inakuwa ni shida. Kwa hivyo kama tutaangalia ushuru huu kama utalipiwa kule juu itamaanisha ya kwamba tutazuia wale ambao wanatengeza hizi sodo katika nchi hii kwa sababu bei ya sodo itapanda juu zaidi na mtoto msichana hataweza kupata nafasi kununua ile sodo wakati anataka kuitumia. Kwa hivyo napinga mabadiliko ambayo yamewekwa katika Mswada huu. Asante.
Asante sana Naibu Mwenyekiti wa Muda. Nataka kusema kwamba kuna umuhimu wa kuhakikisha kwamba kazi ya tume inayosimamia maswala ya askari inaendelea vizuri. Wafanyakazi hao wa usalama wako na jukumu kubwa; lakini juu ya hapo kukifanywa uamuzi kama wenye kuwasimamia katika zile kazi hawatakuwapo kutakuwa na matatizo. Kwa hivyo ninaunga mkono mabadiliko haya ambayo mwenyekiti wa Kamati hii amependekeza ili wale wajipange vizuri ili waweze kufanya kazi. Maanake wakikosa kufanya kazi watakuwa wamekosea Wakenya. Kwa hivyo kuna umuhimu wa kuwa watu sita wafanye kazi hiyo. Asante.
Asante sana Naibu Mwenyekiti wa Muda. Ninataka kumpongeza Mwenyekiti Chepkong'a kwa kufikiri kuwa kuna umuhimu wa jambo hili. Tangu Katiba mpya iwepo hapa nchini mwaka wa 2010 Wakenya wengi wamejitokeza wakikimbilia kortini hata bila sababu. Hivyo basi kipengele hiki kitamwezesha Spika wetu kufanya kazi bila hali ya wasiwasi. Asante sana.
Asante sana Naibu Spika kwa kunipa fursa hii nichangie Hoja hili ambayo inatushangaza kwamba tarehe 22.9.2017 watu 10 walipoteza maisha yao kwa kioja ambacho hakieleweki. Ni jambo la kushangaza kwamba kwa karne hili sisi wote tulioko hapa kama Wakenya tunaona maisha ya binadamu yakipotezwa ovyo ovyo. Tumepoteza familia hizi kwa sababu ya kuawa kwa mfanyibiashara mmoja. Hili ni jambo la kutushangaza wote kama taifa. Kama mtu mmoja amefanya uhalifu kwa kumuua mfanyibiashara itakuwaje jambo la kijamii? Ni jambo la kushangaza nilipowasikia Waheshimiwa wa Emurua Dikirr na Kilgoris wakiongea. Ni jukumu letu kuhakikisha kwamba sisi wote tukiwa viongozi na wafanyikazi wa Serikali lazima tuajibike. Jambo kama hili haliwezi kuchukuliwa kimzaha hivi. Watoto wamebaki yatima wamama wajane na mwenye biashara amepoteza mali yake na kiini na sababu ya haya yote ni uhalifu. Je sisi kama Wakenya Wakristo na jamii inayoishi sehemu hiyo jukumu letu ni nini katika hali ya kudumisha ai na sheria? Tunaambia pole Wabunge wa Emurua Dikirr na Kilgoris. Sisi kama viongozi lazima tuone ni sababu gani hali hiyo imetokea na tunaomba mtusaidie kabisa. Ninachukua nafasi hii kuwaomba wananchi wote wa Transmara ambapo mimi hupitia kila mara na nimetembea pale kwa minajili ya harambee za kuchangia maendeleo ya nchi hii wadumishe ai. Niliwapata wakiishi kwa ai. Tangu jadi hata kimila mavazi na matendo yao yanafanana. Ningewaomba kwamba jambo likifanyika wawachie vyombo vya usalama vifanye kazi ili watekeleze wajibu wao. Ningewaomba wasichukulie sheria mikononi mwao. Hasara ambayo tumepata kwa kitendo cha uhalifu imechukua maisha ya watu 10. Tunasema pole sana na ninachukua nafasi hii kwa niamba ya wananchi wa Mosop kusema pole. Pia ninatoa rambirambi zangu kwa familia zote ambazo zimepoteza jamii zao. Tutaungana na jamii hizi kesho kwa maombi ya wafu ili tupate kuwaambia wananchi kwamba ai ni muhimu kuliko chochote. Mwisho vyombo vya usalama viko katika kila kijiji. Silaha ziko miongoni mwetu. Silaha iliyotumika kumuua mfanyabiashara huyo ilikuwa bunduki. Je tutaishi vipi kama bunduki hazijasakwa? Ninaomba viongozi wote na vyombo vya usalama waajibike kwa kuona kwamba silaha haramu zilizoko miongoni mwa wananchi zimetolewe na sheria imechukuliwa kwa wakati unaofaa. Nikimalizia sisi pia kama viongozi tunafaa kuajibika. Sisi ndio tunatakiwa kuunda sheria zitakazodumisha ai na utengao miongoni mwa jamii zetu. Tunafaa tuangalie shida zinazohusu wafugaji. Ni sababu gani mambo kama hayo yanatokea? Kama ni mambo ya kuimarisha utendakazi wa usalama na kitega uchumi basi inafaa tufanye hivyo ili tuone kwamba wananchi wetu wameweza kuishi kwa ai. Kwa hayo machache asante Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii. Pia nachukua nafasi hii tena kuwapa Mhe. Ng'eno na Mhe. Konchella rambirambi zangu.
Asante sana Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii. Jambo la muhimu ambalo limetajwa na wenzangu wote ni kwamba kazi yetu ni kutengeneza sheria. Lakini juu ya hayo sheria huwa imetengenezwa kwenye vipengele. Ukimpelekea vipengele fulani na hakubaliani navyo yeye pia ana haki kuwarudishia akisema hivyo. Hawezi kuleta hapa insha kwa sababu kazi yetu si kuangalia insha. Kazi yetu ni kuangalia vipengele vya sheria. Hivyo basi ukiangalia Kipengele 115(4) cha Katiba utaona kinasema kwamba akiwa hajakubaliana na sisi atarudisha hiyo sheria hapa na akiirudisha hapa baada ya sisi kuangalia mapendekezo yake tutapiga kura. Haikusema ni lazima watu wawe asilimia sitini na saba wakati tunaangalia mapendekezo. Kwa hivyo tunataka Wakenya wote waelewe kwamba Katiba hii ilipopitishwa katika Mwaka wa 2010 Bunge lilikuwa na haki ya kurekebisha yale maswala ambayo yalikuwa yakitutatiza. Tulikataa kufanya hivyo and tukaamua kufanya sarakasi tukisema kwamba
Asante sana Naibu Spika wa Muda and Mhe. Melly. Nimesimama kuunga mkono Hoja hii. Kabla sijazungumzia barabara zetu ningependa kujiunga na wanawake wenzangu kutoka Tana River kwa sababu ya visa vya ubakaji ambavyo vimezidi. Nikiwa hapa ningependa kusema County Commissioner awajibike ili wanaohusika wachukuliwa hatua kwa sababu tumepoteza mtoto kwa sababu ya ubakaji. Mwingine alipata mimba akajiuwa. Mambo haya yamekua zaidi kwa watu wa Tana River. Nikiunga mkono Hoja hii ningependa kusema kuwa kabla hatujafikiria service lanes mnazozungumzia barabara yetu kuu ishughulikiwe. Nikiunga mkono Hoja hii ya barabara ningependa kusema kuwa sisi katika Tana River kabla hatujafikia hizo service lanes mnazozungumzia barabara yenyewe ishughulikiwe. Isikuwe ndio imekaa kama kitega uchumi kila saa inafanyiwa ukarabati. Tunataka tujengewe barabara nzuri kama wenzetu. Kwa upande wa barabara za magari ya dharura ninaunga mkono kwa sababu ya boda boda na hao wengine.
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa jicho lako la ujai kwa kuniona na kunipatia mwanya wa kuchangia mjadala huu ulio na uzito mkali kama vile ulitangulia kusema pale mwanzo. Kila mtu hapa ameguzwa kwa njia moja ama nyingine na masuala ya kiafya. Si mzaha kusikia joto kali kutokana na usemi wa kiongozi wetu kutoka Mombasa "Jicho Pevu". Na ni jicho pevu halisi. Ni vizuri kutilia uzito mkuu masuala ya afya kuliko mambo mengine yoyote yale. Ni afya njema imetuwezesha kuja hapa na hata kutupatia nguvu ya kucheka. Langu ni kuwakumbusha Wabunge na Wakenya kwa jumla kuwa Kenya iko na maeneo matatu makubwa: Nairobi Mombasa na Kisumu. Eneo la Mombasa ni njia moja ya kuingia katika nchi yetu. Kuna njia tatu za usafiri: anga ardhi na maji. Mombasa ndiyo eneo kubwa sana la kuingiza mizigo katika nchi yetu. Tumepata gari moshi la kasi hivi juzi. Ingekuwa bora ikiwa tungepata mambo mengine kwa mwendo wa haraka kwa mfano mambo ya kudumisha afya njema. Kama vile mwenzangu amenena hapo mbeleni Mombasa inaathiri maeneo mengi. Ni vizuri tuwe na hospitali kubwa ya rufaa katika eneo la kisiwa cha Mombasa. Kuna wengine walichangia hapa kuwa katika vyuo vikuu hapa nchini tunafunza madaktari wengi sana lakini wakimaliza masomo yao hawafanyi kazi hapa kwetu. Ni vizuri sisi Wabunge tujiulize kwa nini watu wetu wanasoma na hawatuhudumii. Wengi wameenda kufanya kazi ughaibuni. Je huko ughaibuni kuna nini ambacho hatuna hapa? Kwa nini sisi tukaachwa nyuma? Sisi Wabunge inastahili kutenga hela za kuziimarisha hospitali zetu. Na kama vile wengine wamesema kama tumepata ugatuzi kwa nini tusipate ugatuzi rasmi kwa mambo yote hasa kiafya? Nimetoka Ruiru si Mombasa. Eneo langu liko na watu 600000. Katika hospitali kuu hapo Ruiru akina mama hujifungua watoto 26 kila siku. Hata leo watapatikana. Vitanda vya watoto ni 12. Vitanda vya wanaume ni saba peke yake. Je hayo ni maendeleo kweli? Sharti turudi nyuma kidogo tuchunguze ni wapi tulipotea na kuacha kuzingatia masuala ya afya katika nchi yetu. Hakuna mtetezi wa wanyonge! Asante sana ndugu yangu Mhe. Mohamed Ali Mohamed kwa kujitokeza kuwatetea wanyonge. Wale watu maskini waliotupatia kura tukajipata hapa Bungeni ndio wasioweza kujitetea. Wacha tuchukue fursa hii tuwatetee ndio wapate mwanya wa kuishi maisha mazuri kama sisi. Hiyo itapatikana tukiunga mkono mjadala huu kwa kishindo ili mambo mazuri yapatikane kwa hawa wanyonge. Nilikuwa na hofu kidogo wakati tumekaa hapa Bungeni tukiongea kuhusu mijadala muhimu iliyo na maendeleo mwafaka katika nchi yetu. Kulikuwa na upinzani kidogo hapa. Hapa tumepata mwanya mzuri sana wa kufanya kazi kama kikundi kimoja. Kwa vile upande wa Upinzani na sisi katika upande huu mwingine tunaongea kwa lugha moja kuhusu maendeleo basi mimi naona hata hii hospitali itajengwa haraka hata kuliko anavyotarajia ndugu yangu. Hilo likifanyika basi litakuwa limeambatana na zile ajenda nne zilizopendekezwa na kiongozi wetu wa Jubilee Uhuru Kenyatta. Sitasahau kuwakumbusha kwamba hata katika zile hospitali chache za rufaa tulizonazo vifaa vya matibabu havipo. Ndiyo maana unaona watu wengi bado wanaenda ng'ambo. Hata kama tutachangia na kujenga hospitali za rufaa itabidi sisi Wabunge tutenge fedha zitakazotumiwa katika utafiti wa magonjwa hasa yale yanayotuathiri. Kenya ni nchi ambayo imeendelea kama mnavyojua. Sijui ni nini twakosa hata tukashindwa kujimudu kimaisha hasa kiafya? Kama mnavyojua Wakenya wote wanatuangalia sisi Wabunge wao. Kwa hivyo si King'ara hapa peke yake - Hata wewe pahali popote pale uwakilishapo mwananchi anakuangalia na afya yake iko mikononi mwako. Hii ni kwa sababu wewe ndiwe umehitimu kuwatetea na kuleta mijadala kama hii ambayo itawapatia afya njema kule mashinani na mijini. Sitasema mengi kwa vile nataka kuwapa muda wengine ambao wamekuwa wakingojea tangu asubuhi kama mimi. Naunga mkono Hoja hii na kushukuru sana kwa vile upande wa Upinzani umetuunga mkono kufanya kazi pamoja kama Wakenya.
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili nichangie Mswada huu wa Narcotic Drugs and Psychotropic Substances Mswada huu umekuja wakati ambao unafaa Naunga mkono Mswada huu mia kwa mia Vizazi vyetu viko mashakani kwa sababu ya dawa za kulevya pombe ikiwa moja zao Watu ambao wamejaribu kutusaidia ni kama Mheshimiwa "Jicho Pevu" ambaye kwa hilo jicho pevu aliweza kutuelezea kwa kina wale watu ambao wanauza madawa katika nchi yetu ijapokuwa vitengo ambavyo vinatakiwa kuwakamata na kuwapeleka kortini vilishindwa na ikabidi nchi za ng'ambo ziwashike wale Akasha brothers Sisi kama walemavu hatujaangaziwa sana katika Mswada huu Kwa sababu hiyo nitaongea na rafiki yangu Mwenyekiti wa Kamati hii Bwana Koinange ili tuweze kuangazia eno ya walemavu Nambari yetu inaongezeka kila kuchao kwa sababu watu wengine wanavuta bhangi wanaharibika kiakili wanatumia dawa kama heroine na kuwa walemavu Wengine wanatumia dawa za kulevya wakiwa na mimba halafu baadaye watoto wanazaliwa wakiwa walemavu wa kiakili Kwa hivyo tunaongezeka ilhali kilabu chetu huwa kimejaa Hatutaki kuongeza watu wengine kwa sababu yale ufaa ambayo tumepewa na Serikali hayatutoshi sisi wenyewe sembuse wale watakaongezeka kushindania hayo ufaa Tumeangazia sana kuhusu watu ambao wanauza dawa za kulevya lakini hatujaangazia mambo ya jamii ambayo inachangia sana kwa utumizi wa hizo dawa za kulevya Hatujaangazia mambo ya shuleni ambapo walimu wengine hawafunzi watoto wetu wakati wako nao ili wajikinge kutokana na dawa za kulevya Sababu nyingine ni jamii ambayo haina kiongozi Nasihi akina dada kuwa wakati mwingine hata kama dada hajaolewa atafute mjomba ili ahakikishe kuwa watoto wake wamelelewa kwa njia inayofaa Wakiwa na tabia nzuri ama wamelelewa vizuri watakuwa wazuri wangwana na watakataa hata hizo dawa za kulevya wakiletewa Wakikataa hiyo biashara ya dawa za kulevya itakufia hapo Nasihi akina dada Bibilia inasema kuwa mama aolewe na mzee mmoja Tamaduni zetu pia zinasema hivyo Lakini wakati ambapo unachanganya kana kwamba hapa uko na mtoto ambaye amezaliwa na Mkisii mwingine na Mmasaai mwingine na Mjaluo huo mchanganyiko maalumu ndio huleta confusion na shida wakati mwingine Jambo hilo husababisha watoto kutoroka na kupatwa na watu hao wanaouza dawa za kulevya Hata kama jamii haina baba tafuta mjomba ili awaelezee watoto njia ambayo wanatakiwa kuchukua
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia Hoja hii. Kwanza kabisa ningependa kutoa shukurani na kumshabikia Mhe. Owen Baya na kumpa kongole kwa kuja na wazo hili. Hili ni jambo ambalo linajulikana kuwa mmea wa mnazi mbali na kuwa una faida yake ya kindani ukiangalia dhari yake inarembesha sehemu iliyopandwa. Iwapo mnazi utapatiwa nguvu ya kupandwa kwa teknolojia ya kisasa - na nikisema hivyo ninamaanisha Serikali iwekeze kwa mmea huu - basi katika kuchangia katika uchumi wa Kenya itakuwa ni nguvu moja. Mbali na kuwa sasa hivi ni mmea unaomea katika sehemu ambayo tumekuwa na umaskini muda mrefu pengine kwa sababu nyingi mbalimbali za uongozi kusahauliwa ukame... Hivi vyote vinachangia kuathiri uchumi. Sasa hivi katika hali ile mnazi unachangia karibu Kshs3.2 bilioni lakini ukipatiwa nguvu za kiteknolojia na utafiti unaweza kutoa zaidi ya Kshs13 bilioni. Ikiwa Pwani peke yake itaweza kuchangia katika suala kama hilo kuwa uchumi unachangiwa kwa mwaka na Kshs13 bilioni basi hiyo ni moja kati ya sehemu ambazo Serikali inapaswa kuwekeza. Sisi kila siku kama jamii ya Wakenya tunapigana na janga la ukosefu wa kazi. Na moja kati ya shughuli ambazo ukitembea Pwani utakuta vijana wetu na akina mama wetu wakifanya ni kuuza madafu na nazi. Kwa hivyo inapeana ajira. Na hii ni ajira ambayo iko lakini haijategwa na Serikali. Iwapo Serikali itaingilia na itege ni kumaanisha tutapata ajira za viwanda; watoto wetu watafanya kazi kwa viwanda kutoa mafuta kama vile dada Mbeyu alivyosema. Sasa hivi Tanzania wanachukua nazi yetu na kutega lile tui linafanywa kavu na kuuzwa. Linatengenezwa halafu linauzwa Kenya. Iwapo Serikali ya Kenya itawekeza kuhakikisha safari hii tumepata kiwanda cha kutega mti wa mnazi basi nina hakika mpaka wakulima watakuwa na motisha ya kupanda zaidi. Ajenda moja ya Serikali ni kuhakikisha watu wote wamepata kazi. Na mnazi ni njia moja ambayo tutaweza kupata kazi. Kijiti kinachotumiwa kutolea nyama kwenye meno chatoka kwenye mnazi. Kapeti hii ambayo tumekanyaga yatoka kwenye mnazi. Makuti yale ambayo yako katika dhara ama hoteli nzuri nzuri yatoka kwenye mnazi. Chakula tunachopikiwa Pwani kama samaki wa mipako ama wali wa nazi kinatoka kwenye mnazi. Mmea ule ule mti wake hutumika kama mbao. Kwa hivyo ziko faida zaidi katika mnazi. Ningependa Serikali iupatie nguvu katika Pwani. Kuhusu suala hili la kazi ningependa kukujuza kuwa katika shughuli zetu zote tunakwenda mbio kuhakikisha tumepata viwanda katika sehemu zetu. Lakini unakuta sasa Kwale tuko na kiwanda cha sukari lakini kimefungwa na hakiwezi kufanya kazi kwa sababu ya yale matatizo yaliyotoka juzi. Tuliingilia kama Wabunge tukafanya utafiti na ripoti ikaja. Ni mwezi wa pili Kwale Sugar Company imefungwa na watu wetu wanapata taabu. Kile kiwanda kimeandika watu zaidi ya elfu tatu. Ikifika wiki ijayo nafikiri watafunga kwa sababu mbali na kuwa wanadaiwa pia watu wetu.
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kutoa usemi wangu kuhusu Ripoti zetu za Mahakama. Kusema ukweli ni jambo la kusikitisha na kutamausha kumwona Rais wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Kenya akiongea mbele ya wananchi akilalamika anavyonyanyaswa anavyoonewa na anavyodhulumiwa. Hii haitoi taswira nzuri kwa Jamhuri ya Kenya kwa sababu Rais wa Mahakama ni mtu mkubwa sana katika Jamhuri yetu. Nakumbuka vizuri sana hivi majuzi tulipokuwa na sherehe ya kitaifa ya Mashujaa Day katika Kaunti ya Mombasa. Rais wa Mahakama Kuu alilalamika sana akisema hakutambuliwa wakati alifika katika sherehe kubwa za Serikali kama ile. Ikiwa tunashindwa kumtambua Rais wa Mahakama je kweli tutaheshimu uamuzi wa mahakama? Yeye ndiye Rais wa mahakama zile. Ni lazima tufikirie jambo hilo kama Bunge tuone vile tunaweza kusaidia mahakama zetu na kuzipa nguvu zinapofanya uamuzi wao. Maamuzi mengi yametolewa na mahakama zetu lakini hayasikizwi wala kutekelezwa. Jambo hilo linaonyesha madharau makubwa sana katika Jamhuri ya Kenya. Yale yanayofanywa na mahakama yanaonekana katika ulimwengu mzima. Uamuzi uliotolewa na mahakama unasikiza ulimwengu mzima. Ikiwa uamuzi ule hauwezi kutekelezwa ni kuuisha kuwa hata wale waekezaji walioko nje ya Jamhuri ya Kenya wanahofia kuja kuekeza katika Jamhuri ya Kenya kwa sababu wanajua kesho wakiwa na shida wapelekwe katika mahakama na uamuzi utolewe uamuzi ule hautatekelezwa. Jambo hilo linaonyesha picha mbaya sana ya Jamhuri yetu ya Kenya. Kuna kiongozi hapa ameongea Mjumbe wa kule Bura akisema kuwa siku hizi ikifika siku ya Ijumaa watu wanakamatwa. Inaitwa kamata kamata. Kamata kamata ni kule kushikwa siku ya Ijumaa. Kuna jaji alitoa hukumu juzi akisema hiyo ni dhuluma. Lakini kusema kweli nani atasikiza dhuluma kama ile? Ijumaa itafika kesho kutwa na utasikia mtu fulani amekamatwa na awekwe rude kuanzia Ijumaa hadi Jumapili kwa sababu siku hizo hakuna mahakama inafanya kazi katika Jamhuri ya Kenya. Atafikishwa mahakai siku ya Jumatatu. Mahakama za Kenya zinapigwa vita kila upande. Zinapigwa vita na Bunge la Kitaifa lenyewe kwa sababu sisi ndio tuna uamuzi wa mwisho katika kupitisha bajeti. Leo Mahakama isipocheza vile tunavyotaka tunasema kuwa kama hawawezi kufanya yale yanatakikana basi bajeti yao itakatwa. Naongea kama Mjumbe wa Kisauni. Sisi watu wa Kisauni Mombasa na Pwani kwa jumla tumeumizwa sana na kesi za mashamba. Leo ukienda katika mahakama zetu kule Bura Garsen Malindi Kilifi Mombasa Kwale na Taita utapata kuna kesi zaidi ya elfu sita zimerundikana pale kuhusu masuala ya mashamba. Yote hayo yameletwa na ukosefu na uchache wa majaji na mahakimu. Kama tulivyosikia mara ya mwisho mahakimu waliajiriwa ilikuwa ni katika mwaka wa 2011. Miaka tisa baadaye hakuna hakimu yeyote ameajiriwa kupunguza ule mrundikano wa kesi katika korti zetu. Ndio maana tumesema leo korti zetu zimepata picha mbaya. Korti zinatambulika kuwa na sheria mbili. Kuna sheria ya matajiri na sheria ya masikini. Ukiwa masikini kesi yako inaweza kuenda miaka mitano au sita mpaka ukashindwa njiani na ukaachana na kesi ile. Kwa sababu gani? Labda korti iko kilomita 300 kutoka pale ulipo na unatakikana ufike pale utoe ushahidi. Lakini kwa sababu huna uwezo utakwenda mara ya kwanza na mara ya pili mwishowe unaachana na kesi kama ile. Uamuzi unatolewa. Mambo hayo yameleta picha ambayo inaonyesha mahakama zetu zinapendelea upande fulani. Lakini ukweli ni kuwa mahakama zetu hazipati fedha za kutosha za kuendeleza kazi zao. Juzi juzi tuliona mahakama nyingi zilisimamisha kazi zao kwa sababu hawakuweza kupata pesa za kulipia mafuta ya majaji kuenda kusikiza kesi kama zile. Hii ilionekana katika Jamhuri yote ya Kenya. Tuliona Malindi walifunga korti. Huku pande ya Kiambu korti ilifungwa kutokana na ukosefu wa hela ili mahakama zitimize wajibu wao wa kikatiba. Nilisikia ikitangazwa juzi kuwa mwaka jana Mahakama ilikusanya ushuru wa Ksh700 milioni. Lakini leo unapata kuwa pesa wanazogawiwa kila mwaka zinazidi kupungua. Hatujui ni kwa nini zinazidi kupunguzwa. Tunajua kuna mikakati imewekwa kwa sababu uchumi haufanyi vizuri na tumepunguza hapa na pale lakini tunajua umuhimu wa mahakama zetu katika Jamhuri ya Kenya. Ni lazima kila Mkenya kuanzia Rais mpaka mtu wa kawaida aheshimu hukumu na uamuzi wa korti zetu za Kenya. Ukikumbuka mwaka wa 2017 Mahakama ya Upeo ilitoa uamuzi wakati wa kura ya urais kati ya Mheshimiwa Raila Amolo Odinga na Mheshimiwa Uhuru Kenyatta. Uamuzi ulitolewa kuwa ni lazima kura ile irejelewe kwa sababu kulikuwa na makosa fulani hapa na pale. Lakini viongozi wote - Mheshimiwa Raila Odinga na Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta - waliheshimu uamuzi wa korti kura ikarejelewa na mshindi akapatikana. Leo tuko na Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta kama Rais wa Jamhuri ya Kenya. Ikiwa tulisikiza na kutii uamuzi ule mkubwa ambao ulikuwa ni wa Jamhuri nzima ya Kenya kwa nini hatuwezi kusikiza haya maamuzi madogo madogo ambayo yanatolewa na kuhakikisha yametimia? Hiyo inaonyesha kuwa hatuko tayari kuitambua Mahakama kama kiungo muhimu. Huwa tunasema kuna viungo vitatu katika Jamhuri ya Kenya lakini kiungo cha Mahakama ni kiungo dhaifu. Kiko tu pale na watu fulani wanakichezea vile wanavyotaka. Lakini umefika wakati ni lazima tukubali kuwa mahakama lazima zisaidiwe na tuhakikishe zimejengwa kila sehemu ya Jamhuri ya Kenya. Leo Mombasa tunajenga mahakama nyingine. Ujenzi wa mahakama ile umesimama kwa sababu hakuna pesa ya kuendelea kujenga. Hii ni kumaanisha kutakuwa na mrundiko wa makesi kwa sababu mahakama hazitoshi. Tumesikia Mbunge wa Bura akisema mtu anatoka Mbalambala anasafiri kilomita 400 kuenda Garsen. Hiyo ndio korti iliyo katika eneo la ugatuzi la Tana River nzima. Eneo nzima liko na korti moja. Niambie kama mtu ataweza kufanya safari hiyo ya kilomita 400 afike mahakai. Naunga mkono Ripoti hii. Lakini sisi kama Wajumbe tuna kazi kubwa ya kufanya ya kuhakikisha Mahakama yetu imepewa uhuru wa kufanya kazi zake kisawasawa bila kuingiliwa na upande wowote - sio Bunge wala upande ule mwingine. Naunga mkono Ripoti hii kikamilifu.
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii nichangie hotuba ya Rais wa Tanzania Wakati niliposikia hotuba yake ilikuwa ya kuwawezesha Watanzania waingie Kenya kwa wingi jinsi Wakenya wameingia Tanzania na kupeleka biashara huko Aliseme kwamba ile pesa wanabiashara wamepeleka Tanzania ni nyingi sana kushinda ile Watanzania wameleta Kenya Kwa hivyo alikuja kuongea na Rais wetu wa Kenya kusaidia Watazania pia hao waweze kuweka pesa zao hapa Kenya Pia aliongea kuhusu barabara na umeme ambayo ni miradi Tanzania na Kenya wanafanya pamoja Alifurahia kwamba
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii pia nami nichangie huu mjadala Kwanza kabisa nigependa kumpongeza Rais wetu mpendwa kwa kumwalika Rais Suluhu Hassan na yeye pia kukubali kuja hapa na kuhudhuria kikao cha Bunge zote mbili Pia ningetaka kuwashukuru maspika wetu wote wawili kwa hiyo hatua walichukua kutuita sisi sote tuje kuhudhuria hotuba ya Rais wa Tanzania Katika hotuba yake sana sana alilenga uhusiano mzuri ama mwema kati ya Tanzania na Kenya Vile vile alisema kuwa unaeza kuchagua marafiki lakini huwezi kuchagua jirani
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili nami niweze kuchangia Hoja hii. Kwanza ningependa kumshukuru mhe. Lay kwa kuleta Hoja hii Bungeni na kuitanguliza.Vile vile ningependa kumshukuru mhe. Mbadi kwa kuifanyia marekebisho kusudi sisi tunapoichangia iambatane na mahitaji yetu kama taifa. Ingawa tumeitambua lugha ya Kiswahili kama lugha ya taifa na vile vile kama lugha yetu katika Afrika ya Mashariki katika matumizi yake hatujaboresha lugha hii iwe kama lugha ya Kiingereza. Masikitiko yangu ni kwamba hata mwenye kuileta Hoja hii Bungeni na mwenye kuifanyia marekebisho wote wawili walitumia lugha ya Kimombo. Ningefurahi sana kama wangeitumia lugha ya Kiswahili kusudi sisi sote tuendeshe mambo yetu katika lugha ya Kiswahili ili kuimarisha lugha hiyo. Nitaongea kwa ufupi kwa sababu kuna wenzangu ambao vile vile nao wangependa kuchangia Hoja hii. Jambo langu kuu ni kwamba Kenya na dunia nzima inapiga hatua sana katika nyanja ya sayansi teknolojia na mawasiliano. Maendeleo hayo hayatakuwa na ufaa kwetu na kwa watu wetu ikiwa hatutatumia lugha ambayo watu wetu wanaelewa. Vile vile ningependa kituo hiki cha kunakili na kupasha habari kuhusu sheria zetu kipewe nguvu ili kufanya kazi kana kwamba mawasiliano yote ya umma sio sheria peke yake yaweze kutafiwa kwa lugha ya Kiswahili kusudi watu wetu waweze kuelewa mambo ambayo yanaendelea katika nchi yetu. Naunga mkono Hoja hii. Namsihi mhe. Lay vile vile alete mswada Bungeni kusudi tutengeneze sheria. Ahsante.
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia mjadala huu muhimu ambao unaangazia masuala ya afya ya Wakenya.
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuuchangia Mswada huu. Ni wakati mwafaka wa kuwashughulikia wazee. Wakati mwingine wazee hutafuta haki kwenye mahakama yetu lakini hawapati. Ni kana kwamba hawana haki kwa ajili ya umri wao mkubwa. Huu Mswada utawasaidia sana wazee kwa maana unajali maslahi yao. Kuna pendekezo limetolewa kwenye Mswada huu linaloashiria kuwa Kaunti ziweze kutengeneza orodha ya wazee na kuwasajili. Hivyo basi kila familia iliyo na mzee itajulikana. Kwa jinsi hiyo Serikali itajua wazee walio kwenye familia hizo. Afya ni kitu cha muhimu lakini wazee hawawezi kupata bima ya afya. Kwa kuwaorodhesha Serikali itajua ni familia zipi zilizo na wazee na hata kujua hali yao ya kiafya. Itaweza kuwashughulikia kwa njia nzuri. Wazee wengi wanaaga dunia kwa sababu hakuna watu wanaojali hali yao. Katika familia nyingi vijana wamewageuka wazee kiasi cha kuwachapa kwa ajili ya mashamba. Kuna ugomvi mwingi kuhusu mashamba na vijana wanawafurusha wazee kutoka kwenye mashamba yao. Mswada huu utawapa wazee nafuu kwa sababu shida zao zitashughulikiwa. Hata wakipeleka lalama zao mahakai watasikilizwa. Kesi kuhusu mashamba yao zitaamuliwa. Wazee hawana nguvu ya kupigana na vijana wao. Hii sheria ikipitishwa itawashughulikia na hakuna mtu ataingilia maslahi yao. Kuna wale wazee ambao wako na miaka sitini kuenda juu ilhali hawana vitambulisho. Wengine wanahitaji kusafiri lakini hawana vyeti vya kusafiri. Wapo ambao hawana vyeti vya kuzaliwa. Hii sheria itawasaidia sana kupata stakabadhi hizo. Kule vijijini tunakotoka wako wazee ambao kwa kweli hawana stakabadhi nilizozitaja. Hata wale ambao walipigania uhuru wa taifa hili hawana stakabadhi hizo. Kuna bima ya kuwakinga wazee. Kaunti itakuwa na jukumu kubwa ya kuwasajili wale ambao hawako kwenye orodha ya Serikali Kuu. Kwa sasa kuna wale wanaolipwa na Serikali kuu na wale ambao hawalipwi. Ile njia ilitumika kupata yale majina ninaitilia shaka. Katika eneo-Bunge langu sio wengi wanaofaidika. Lakini kwa ajili ya hii sheria watafaidika. Hii ni kwa sababu watakuwa wamesajiliwa na kujulikana wako wapi. Vipo vikundi vya kuwasaidia wazee kujimudu kimaisha katika jamii zetu. Wazee watakuwa na uhuru wa kujiunga na hivyo vikundi na vitawasaidia kutafuta hela za kujikimu na kujiendeleza kimaisha. Sisi huwasikiliza na kuwauliza mawaidha wazee. Watakuwa na mahali pa kukutana na kuzungumza. Aidha maoni yao yatasikilizwa na serikali za kaunti. Huu Mswada unanuia kuwasaidia wazee ambao hawana mbele wala nyuma. Ni wengi ambao hawana mtu wa kuwasaidia. Wazee watajua kwamba wako na haki ya kufanya chochote kwa sababu hili taifa ni lao pia. Naunga Mswada huu mkono. Naomba tuupitishe haraka ili wazee wapate haki zao.
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia Mswada huu. Nataka kuunga sana mkono Mswada huu mwanzo kama mwakilishi wa vijana katika Bunge kwa sababu Mswada huu utawasaidia wale ambao ni wanyonge zaidi katika jamii kama wanawake vijana na walemavu. Mswada huu unaruhusu wananchi kuomba mikopo kutoka kwa benki za kawaida kwa njia ambayo ni rahisi. Kawaida wananchi wakiwa wanataka senti ama mikopo inabidi waende kwenye vyama vidogo vidogo vinavyoitwa microfinance katika lugha ya Kiingereza ambavyo wakati mwingine vinalipisha faida kubwa sana ama interest . Kitu kingine ni kuwa kwa sababu katika Serikali hivi sasa hatuna mambo ya elimu bure mpaka shule za upili na kadhalika na kwa sababu pia mambo ya afya yamekuwa ghali sana unapata inawabidi wananchi waende kwa watu wa rehani kuweka mali yao ili waweze kupata mikopo. Watu wa rehani huwa wanalipisha faida nyingi sana na badala ya kumsaidia mwananchi inamweka kwenye umaskini zaidi. Mswada huu unaruhusu watu wapate mikopo kwa benki na si lazima watumie ardhi na nyumba kama tunavyojua. Tunajua kuwa katika nchi yetu ya Kenya kupata cheti cha ardhi au title deed huchukua muda mrefu na mara nyingi huwa ni pesa nyingi kwa mwananchi wa kawaida kutafuta kwa sababu ya kufanya mambo ya usoroveya na kadhalika. Wakati mwingine kuna wafanyikazi wa Serikali wenye kulipisha hongo kubwa. Kwa hivyo sheria hii itaruhusu mwananchi wa kawaida kutoa vyombo vyake vyovyote vidogovidogo viwe kama garantii ya mkopo. Hivi ni vitu kama piki piki na mitambo. Uzuri wa sheria kama hii hususan kwa Kaunti ya Kwale inaruhusu mifugo watumike kama garantii ya wananchi kuweza kupata mikopo. Naunga mkono sheria hii. Kwa kweli itasaidia wananchi walala hoi ijapokuwa si ruhusa kwa Serikali kuaacha mamlaka yake ya kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea na maisha yao na wanagharamikiwa kwa mambo ya kawaida kama elimu na afya. Kwa hayo machache asante.
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi ili nichangie Hoja hii. Kwanza ningependa kumshukuru Mhe. Mohamed Ali Mohamed kwa kuwasilisha Hoja hii. Hii Hoja ni muhimu sana kwa sababu tuko na hospitali za rufaa mbili Kenya nzima. Tuko na Hospitali ya Rufaa ya Mafunzo ya Moi ambayo inasaidia watu wakutoka eneo la Magharibi na eneo la Nyanza. Vile vile tuko na Hospitali ya Rufaa ya Kenyatta.
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili nichangie Mswada huu ulio muhimu sana Ninampongeza Mhe Rehema Jaldesa kwa kulifikiria hili jambo na kulileta hapa ili tulijadili Ni kweli kumekuwa na ukame Hata tunahofia kwamba tutaanza kupoteza watu wetu na mifugo kwa ajili ya njaa Katika kaunti yangu ya Taita Taveta pia kuna ukame sampuli mbili Sampuli ya kwanza inasabibishwa na ukosefu wa mvua na maji Sampuli ya pili inasababishwa na wanyamapori Hii ni kwa sababu tumezungukwa na mbuga ya wanyama pori Katika zile sehemu chache ambako mvua imenyesha na watu wamepanda mimea wanyamapori wanavamia na kula kila kitu na wananchi wanabaki bila Swala hilo linatupa hofu kubwa kwa sababu ikiendelea hivyo basi wanyama pori watatoka porini na wakikuta kumekauka namna hiyo watawavamia binadamu na watu watapoteza maisha Tayari tushaona ndovu wakitoka na kuelekea mahali wananchi wako Wameanza tabia ya kupasua matangi ya maji Hii ni kwa sababu ya ukame Wakikosa chakula na maji kwenye mbuga wanavamia makazi ya binadamu na kupasua matangi ili wapate maji ya kunywa Itakuwa vyema nikiwaunga mkono wenzangu waliotangulia kuongea ili tulitaje hili kama janga la kitaifa ili liweze kuchukuliwa kwa uzito unaostahili na liweze kushughulikiwa ili tusiendelee kupoteza maisha Tayari tumeshapoteza wapendwa wetu wengi kupitia hili janga la Korona na hatutaki kuwapoteza watu zaidi kwa sababu ya mambo ambayo tunaweza kuyafanyia kazi Asante
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii kuchangia Hoja hii ambayo inaangazia walioteuliwa kwenye Tume hii. Kuna jambo ambalo limenifurahisha zaidi kutoka kwa mwanakamati ambaye amezungumza sasa hivi. Amesema waliangazia hawa wote ambao waliomba kazi hii na wakawaona ni watu wa tajriba kubwa. Hakika wanaweza kufanya kazi nzuri ili kutoa mchango mkubwa katika Serikali yetu ya Kenya. Nimeiona kazi ambayo dada Charity alishiriki wakati wa nyuma. Tuliona akifanya kazi kwa njia nzuri. Vile Balozi Salma alikuwa akifanya kazi kama balozi. Tumeiona kazi yake. Alitoa mchango mkubwa sana katika nchi hii ya Kenya. Kwa hivyo naunga mkono Hoja hii na kupongeza Kamati hii. Tutapitisha wale ambao wamefanyiwa vetting ili waanze kazi na kutoa mchango katika Serikali yetu ya Kenya. Asante sana Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili nichangie katika mambo haya. Narudia kusema kuwa ni lazima Kamati iangalie vigezo fulani ambavyo vimetajwa. Waheshimiwa wenzangu wanaweze kuangalia hali ya vijana na walemavu. Pia nasihi vijana na walemavu watume maombi wakati nafasi kama hizi zinapotangazwa. Sharti maombi yao yaambatane na zile kanuni ambazo zitahitajika. Kwa hayo machache nashukuru kwa kunipatia fursa hii. Naunga mkono hawa ambao wamewekwa hapa wachaguliwe. Asante Mhe. Spika wa Muda.
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii nami pia nizungumzie swala hili nyeti. Hii ni Hoja inayoleta taarifa kuhusu makadirio ya pesa iliyopeanwa kutoka wizara tofauti tofauti. Vile vile Kamati ya Bunge itueleze kuhusika kwenye makadirio ya kuhakikisha kuwa zile pesa tulizokuwa tumekadiria tuliweza kuzibadilisha zitumike kwenye janga hili. Sio i kwamba kuna utukutu mwingi katika nchi hii. Wafanyibiashara wasiokuwa na nia nzuri walitumia janga hili kujinufaisha. Kamati ya Bunge inayosimamia masuala ya afya imezungumza kinaganaga juu ya matatizo yaliyoko haswa zile pesa zilizofujwa badala ya kutumika vile ilivyotakikana. Ni dhahiri kwamba wale waliofanya biashara na KEMSA hawakujua Wakenya wanahitaji usaidizi kwenye janga hili. Wahudumu wa afya wanajikaza ili Wakenya wapate huduma. Eneo langu la uwakilishi Bungeni liko mpakani. Tuko na shida ya Coronavirus kutoka nchi jirani na pia kwetu kwenyewe. Tumepigika sana. Ni shida kubwa iliyoko kule kwa sababu mtu akija hospitali akose kivuta pumzi hata kama haugui Coronavirus hawezi kusaidika maanake hawawezi kupata njia ya kupata hewa ya haraka ili atibiwe. Wakenya wako na shida kubwa sana. Ninashangaa kuwa mtu anaweza kulala usingizi akijua amechukua pesa amezifuja kwa ufisadi na kuweka mfukoni na kulala akifikiri ametajirika ama akitarajia kuwa wanawe wanatakikana kuishi vizuri kuliko Wakenya wengine. Ni jambo la aibu na la kusikitisha. Ninatumai kufikia sasa watu waliohusika wangekuwa wakichezea jela kama kweli kuna vita dhidi ya ufisadi humu nchini. Ni laana na dhambi. Nilimuona aliyekuwa Katibu wa Kudumu tuliyefanya kazi naye Dr. Nyikal na ambaye pia ni daktari akibubujikwa na machozi. Watu wengine walifikiri ni utani. Jambo hili si la utani. Ni la ukweli. Alizungumza kwa uchungu. Na hayo ndio machungu yanayokumba Wakenya wengi haswa tukiwa viongozi tukijua kuwa mikono yetu imefungika. Tunashindwa vile tutawasaidia wananchi haswa kwa sababu Mhe. Nyikal mwenyewe ni daktari. Yeye alizidiwa zaidi kwa sababu ya ule uzito na shida aliyoiona na kutokuwepo na uwezo wa hao watu kusaidika. Vifaa ambavyo wafanyikazi wa Afya wangetumia kujikinga havijatumika. Wauguzi wanakufa kama nzige. Hili ni jambo la kusikitisha sana. Ninaunga mkono taarifa hii lakini juu ya hapo wacha nimalizie kwa kusema kuwa ni lazima watu waadhibiwe. Asante.
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia hii fursa na pia mimi niweze kuchangia suala hili ambalo linahusu mambo ya usawa wa jinsia na maendeleo. Tunaongea kuhusu jinsia ya kiume na kike. Tunaongea kuhusu maendeleo afya ugavi wa kazi elimu na masuala mengineyo ya kuboresha maisha ya jamii nzima. Tumeona mara nyingi kina mama wakienda barabarani kuitisha haki zao hapa na pale. Tumeona vijana na vile vile watu wanaoishi na ulemavu wakiwa barabarani wakisema 'Haki yetu haki yetu!' Haki hii haifai kuombwa bali ni vile wanajisikia wakiwa wamenyanyasika na hawapati hiyo haki yao. Kwa hivyo kama Hoja hii itaboresha mambo na kuleta mwafaka basi mimi naunga mkono. Kuna suala la BBI ambalo limetajwa. Mimi bado niko pale pa kusoma. Naendelea kusoma lakini ni huzuni kwamba nafasi hii ya kiti cha Mwakilishi wa Wanawake ambacho kilinileta hapa Bungeni naona kama tutaenda kukikosa kupitia hii BBI. Bado naendelea kusoma. Asante kwa hii fursa.
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia hii nafasi nichangie Hoja hii. Kwa kweli kuna mambo ambayo watu wanaona ni magumu kwa kila Mkenya. Kulingana na hii Ripoti Maj. (Rtd.) Muiu ingekuwa muhimu ikiwa mtu amekuwa mgonjwa Huwezi kujiletea ugonjwa. Hakuna mtu anajua ugonjwa unaweza kuingia mwilini mwake siku gani lakini wakati unawahudumia Wakenya na uwe mgonjwa ni muhimu utambuliwe kama shujaa wa Kenya na ukiondoka kazini uondoke inavyostahili. Tume hii inawatatiza watu wengi. Ninashukuru Kamati ya Masuala ya Usalama na Utawala. Kuna mambo yanaendelea kwa wafanyikazi wa Serikali ambao ni polisi. Kama juzi tuliona mengi kwa gazeti. Maafisa wa Serikali walisimamishwa na wengine 70 walifutwa. Ingekuwa muhimu pia kuangalia kwa undani kwa sababu ukiambiwa watu 70 wamefutwa kazi ama wameondoka sijui kama wote ni wabaya ama wote wataenda na malipo yao ya uzeeni ama wataenda kwa njia gani. Kwa hivyo ninaunga mkono Kamati ya Masuala ya Usalama na Utawala. Waendelee kuangalia hayo mambo kwa sababu tukizungumzia kustaafu kwa Maj. (Rtd.) Muiu pengine kesho utapata kesi nyingine. Kamati ya Masuala ya Usalama na utawala inafaa kuangalia kindani ni nini kinachoendelea kwa sababu ukiangalia hata saa hii utapata tunayo shida kupigana na utovu wa usalama. Hujui kama ni kwa sababu ya haya mambo yote wanafanyiwa yanamfanya ashindwe kufanya kazi au ni mambo mengine. Pengine hajui atatoka kesho na atatokaje. Ninaunga mkono hii Ripoti ya Kamati lakini ni vizuri waangalie idara ya polisi. Tuna shida kubwa katika idara ya polisi. Jambo hili linapaswa kuangaliwa kwa kina. Asante Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii.
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Hoja hii inayohusu ulazimishaji wa shule na wananchi kupanda miti. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda mwanzo ningependa kumpongeza aliyeleta Hoja hii Mhe. Chepkut. Kaunti ya Kwale pia imeadhirika sana. Kuna watu kama wawili katika kila eneo letu la Bunge ambao wamekuwa wakipata shida ya njaa. Kukata miti kunapoteza maji maana mizizi ya miti haiwezi kuweka maji kwa muda mrefu. Ukosefu wa maji unasababisha ukosefu wa chakula. Mwaka uliopita kuna sehemu zilikuwa na njaa. Ukosefu wa maji pia unasababisha upungufu wa miti shamba inayotumika kwa kutengenezea dawa ya kienyeji. Hii ni dawa ambayo wananchi na madaktari wamekuwa wakitumia tangu enzi. Ukosefu wa mvua umesababisha upungufu wa aina hii ya miti inayotumika kutengeneza hizo dawa. Iwapo upungufu wa maji utazidi itakuwa vigumu kuregesha miti ya aina.
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kuchangia Hoja hii. Kwanza ningependa kumpongeza Mhe. Alfred Keter kwa kuileta. Lamu County iko na tatizo hili. Wabunge wakisimama wanataja Tana River Garissa na sehemu nyingine lakini hawataji Lamu. Kuna miji mitatu pia ambayo inafurika kule Lamu; Moa Chalaluma na Dide Waride. Kama majirani wa Tana River Kaunti wakipata tatizo inabidi waje Lamu. Kwa hivyoWizara ikifanya mipango yoyote wajue kuna Lamu County. Tunashukuru Red Cross kwa usaidizi wao kwa wananchi. Kuna wanyama kama ng'ombe na hata binadamu ambao walikua wamefungiwa na maji imebidi watolewe. Mashamba yameharibika na maji yamefika kwa yumba. Kuna watu wanatolewa sasa hivi wamepewa ilani watoke maeneo yao na waende maeneo mengine. Serikali kupitia kwa Wizara ya Special Planning inafanya kazi nzuri. Wizara inayohusika na usalama ni kubwa sana ikipewa majukumu kama haya yatapotelea humo. Ningeomba Wizara ya Special Planning ipate kusaidia watu wetu. Watu wana shida watoto hawaendi shuleni watu wana njaa kuna shida ya mbu na tunahitaji neti na chakula pia. Naunga mkono Hoja hii. Asante.
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii kuchangia kuhusu hii sheria ambayo itaweza kuwasaidia maskini kupata msaada wa mawakili wa Serikali. Hii sheria ingepitishwa kama juzi. Kwa hakika ni miaka 50 tangu tupate Uhuru. Pia ni vizuri kuwa tumeweza kufungua macho yetu kwa wakati huu kuweza kuleta sheria kama hii humu chini. Kwa mfano hata leo nimepigiwa simu na mama mmoja kutoka Kaunti ya Kwale ambaye mtoto wake amebakwa. Kijana mshukiwa alishikwa kisha akawachiliwa. Kesi ni kesho na haelewi atafanya nini ama ataenda vipi kumsaidia mtoto wake na yeye mwenyewe waweze kupata haki. Kwa hivyo tukiwa na mawakili ambao wanalipwa na Serikali itawasaidia sana wale walalahoi nchini kwetu ili kupata msaada hususan wale ambao wanadhulumiwa kiasi kama hicho na zaidi. Kwa mfano pia kuna wanawake wengi Kwale ambao mara kwa mara wanakuja kwa sisi viongozi wakitaka msaada kuwatoa vijana wao ambao wameshikwa na wamefungwa gerezani na hawajui vipi watawatetea watoto wao. Wengi ambao wanashikwa huwa ni vijana wa kiume kwa bahati mbaya na afisa wetu wa polisi kwa maswala ambayo hayaeleweki mara nyingi katika mambo ambayo tunayaita misako. Maafisa wa polisi wakimpata kijana anatembea tu wanamshika. Wakati mwingine wanamua kwa muda kushika watu ama kuingia kwa nyumba za watu na kushika vijana bila hatia yoyote. Halafu kina mama ndio wanaumia kwa sababu hawawezi kuwatetea vijana wao. Kitu ambacho nitaomba kibadilishwe na pamoja na wenzangu tutaleta mabadilisho ni Ibara 9(a) ambayo inasema kuwa Rais aweze kuandika mkurugezi wa bodi ambayo itasimamia sheria hii. Tunaona ni afadhali Jaji Mkuu aweze kumchagua atakayesimamia bodi kama hii. Pia tunaona kuwa Wakili Mkuu wa Serikali amewekwa hapa pamoja na Wizara ya Haki ambayo hivi sasa hatuna. Kwa hivyo pengine angewachwa mmoja peke yake. Kuna jambo lingine ambalo limenifurahisha sana. Huko Kwale tuna kabila linaloitwa Makonde. Makonde ni watu ambao wanatoka Mozambique ambao walikuwa hapo miaka na mikaka. Wamezaliwa hapo na wanaishi hapo. Jambo la kusikitisha ni kuwa Serikali ya Kenya bado haijaamua kuwatambua watu hawa ijapokuwa hivi sasa tuko kwenye harakati za kuwasaidia watambulike kama Wakenya. Karibu wote hawajui vile watarudi. Hawana mtu wanaomjua huko na nchi yao ni Kenya. Hivi sasa hawana vitambulisho na hawatambuliki kabisa. Jambo nzuri katika sheria hii ni kuwa watu ambao hawana nchi ama kwa Kiingereza "stateless persons" wataweza kupata msaada wa mawakili ili kusaidika katika kesi zao tofauti tofauti. Pia ingekuwa vizuri kama wangeweza kupata msaada ili kuwatetea pia wao waweze kutambulika kama Wakenya. Makonde hapa nchini wako kama 10000 watu wengi sana ambao wanaumia na wameoana na Wakenya hapa nchini. Watoto wao wanapata shida wakitaka kuandika karatasi za usajili wa kuzaliwa kupata vitambulisho au hati za kusafiria kwa sababu pengine mzazi wao mmoja hatambuliki kama Mkenya. Kabla sijaketi ningetaka kuiomba kwa sababu nina hakika hii sheria itapita katika muda usio mwingi Serikali ifuate maelezo ya sheria hii ili isiwe kama ile Sheria ya Baraza la Vijana la Kitaifa ambayo Serikali imekataa kutaimbua na kuwapatia vijana pesa ili waweze kuendeleza maswala yao kama vile walivyoruhusiwa na Sheria ya Baraza la Vijana la Kitaifa ya 2009. Kwa hayo machache nasema shukrani.
Asante Sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangie mema na mazuri ambayo yanatuleta sote katika eneo la Afrika Mashariki Mwaliko wa Rais wa Tanzania Bi Samia Suluhu ulifanywa na kiongozi mwenye hekima Rais Uhuru Muigai Kenyatta Ninawapongeza wote wawili kwa kutumia njia hiyo kama nafasi ya kuleta uwiano katika maendeleo ya Afrika Mashariki Kuna Nchi sita zinazoshirikiana katika Afrika Mashariki Tukianza na Tanzania ambayo ni nchi kubwa kuliko nyingine kwa ukubwa wa ardhi ninaona maisha yakiwa mazuri Alinivutia pia wakati marais wote wawili walipoangazia vile tutafungua mipaka yetu Mipaka kati ya Kenya na Tanzani ni mingi Mifano ni Naga Lunga Lunga Isebania na are Wafanyabiashara wetu wamekuwa na shida sana katika shughuli zao za biashara pale katia mipaka Viongozi hao walipokutana walijaribu kulainisha vile biashara inaweza kunoga kati ya nchi hizi mbili na kuonyesha maendeleo yatapatikana Pia waliongea kuhusu usalama Hapa kwetu tumekuwa na shida ya usalama hapa na pale Nchi zote mbili zikiungana na haswa zikileta nchi nyingine kwenye muungano huu hali ya usalama itakuwa nzuri Akigusia masuala ya utalii katika nchi zote mbili Rais Suluhu alisema kwamba kulikuwa na changamoto kwa vile Wakenya na Watanzania hawakuwa wakifanya biashara bila ya matatizo katika maeneo ya hifadhi za wanyamapori za Serengeti upande wa Tanzania na Maasai Mara upande wa Kenya
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia Hoja hii. Mwanzo nataka kulalamika kidogo. Karatasi za kueleza Hoja hii hazikuwa zinapatikana katika Chumba No.8 hapa Bungeni. Kwa hivyo tumelazimishwa kutafuta njia nyingine kujua Hoja hii inaomba nini.
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ya kuchangia Hotuba ya kiongozi wa nchi. Kwanza ni kumshukuru kwa sababu aliheshimu Bunge kama eneo la kutafuta uwiano wa kimaendeleo katika Kenya yetu tuipendayo. Mengi yametajwa na Wabunge wakichangia Hoja hii ambayo nimesimama kuunga mkono. La muhimu ni kujua hata kama Kenya inaonekana iko na shida kuna mengi yamepewa kibao mbele na kuhitimu hasa ile ya uwiano. Najua kama vile wengi wamechangia nchi yetu ilipitia wingu mbaya sana na likaleta utengano kati ya Wakenya. Wakati viongozi hasa Rais Uhuru Kenyatta na Mhe. Raila Odinga waliketi na kukubaliana kuleta uwiano katika maendeleo tulipata nafasi ya kuendelea vyema. Kwa hivyo tunawashukuru. Ni vizuri sisi viongozi tuwaige ndiyo Kenya yetu iweze kupiga hatua za haraka kimaendeleo. Lingine la kuvutia ni wakati kiongozi wa nchi aligusia pendekezo la viongozi kuunga mkono ugatuzi. Nchi yetu imeenda njia ya ugatuzi. Nakumbuka alisema ya kwamba kiwango kikubwa cha pesa cha Ksh372milioni kilitengwa cha kuleta usawa kwa ugatuzi katika kaunti ambazo zimewachwa nyuma. Hilo ni jambo la kuonyesha kwamba kiongozi wa nchi anapenda Kenya iendelee katika maeneo yote. Kiongozi wa nchi hakuacha nyuma magonjwa yanayotukumba. Kama vile mnakumbuka alisema kwamba ugonjwa wa malaria ni janga ambalo lilikuwa linaumiza Wakenya sana. Serikali imechukua hatua na kuona hilo limepungua. Vile vile aliongea juu ya akina mama kujifungua bure. Alitaja kuwa kiasi cha Ksh5.2bilioni kilitumika na kitaendelea kutumika kuona akina mama wanajifungua bure. Hilo ni jambo la busara hasa kwa wanasiasa kwa sababu tunapenda wapiga kura. Kama hatushughulikii wapiga kura basi tutaumia. Wakati afya ya wapiga kura inadumishwa ni jambo la kuvutia na kupewa kipaumbele. Nakumbuka kiongozi wa nchi aliongea juu ya barabara. Alitaja kuwa Serikali imetenga kiwango cha pesa cha kutengeneza kilomita 10000 ya barabara. Alisimama mbele yetu akasema tayari wamekamilisha kilomita 3000. La kuvutia ni wakati aliongea juu ya barabara kutoka Isiolo na kuunganisha nchi yetu na Ethiopia. Kama vile mwenzangu Mhe. Jonah Mburu kutoka Lari ametaja kuna umuhimu mkuu wa kuona nchi ya Kenya inaungana na maeneo mengine ya Africa ndiyo maendeleo hasa ya biashara na uchumi yaweze kuenea na kuchukua nafasi iliyochukuliwa na ulimwengu wote. Ni vizuri kukumbuka kwamba kiongozi wa nchi alitaja eno yanayohusu utalii. Mungu anapenda Kenya yetu kwa vile hata kama tumeumia kisiasa alisema tumepiga hatua asilimia 20 kiutalii na inaonekana tukichukua huo mwelekeo wa kuwa na uwiano na kushikaa tutaenda mbele haraka. Sitasahau kutamatisha kwa kusema ufisadi uliingia katika Hotuba ya Rais. Alisema asilimia kumi ya pesa imerudishwa na itaendelea kurudishwa tukiiga mwigo wa kupigana na ufisadi. Nashukuru na naunga mkono Hotuba ya Rais.
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa nafasi hii. Ninaunga mkono Hoja hii kwa sababu wafanyikazi wengi wa Serikali na nyanja tofauti wamekuwa wakipata shida sana kuhusiana na pesa zao za uzeeni. Shida hiyo imewafanya kuwa maskini wakati ambapo wanahitaji hizo pesa na wamezeeka. Wamekuwa wakiekeza pesa zao katika mijengo mashamba na mambo kama hayo. Kuna shida ukiwekeza huko. Juzi kule Kaunti ya Kwale kuna mzee mmoja aliyestaafu na ana shamba lake kule sehemu ya Kanana Lungalunga. Matingatinga yakaja kwa msaada wa baadhi ya watu katika Serikali na kung'oa miti na kutishia kung'oa nyumba. Tunashukuru kuwa Bwana Matiang'i alisimamisha kazi hiyo. Huo ni mfano mmoja. Kuna wengine ambao wanaibiwa ardhi na mali zao bila kuhimili. Ukiwa na malipo ya uzeeni ambayo yanasimamiwa inavyostahili kama vile Mheshimiwa anavyopendekeza kusikuwe na shida kama hizo. Maisha ya mtu anapostaafu yatakuwa na nafuu kwa sababu kuna senti ambazo atakuwa anategemea mara kwa mara kuliko hivi sasa ambapo watu wanastaafu na kungoja kwa miaka mingi sana bila kuona senti zozote na wanahangaika uzeeni. Ninamshukuru sana Mheshimiwa kwa kuleta Hoja hii muhimu. Ninamuunga mkono na ninashukuru sana kwa nafasi hii kwa mara ya pili.
Asante sana Naibu Spika wa Muda Mheshimiwa Rais Samia Suluhu alisema kwamba uongozi ni kuoyesha njia na sio kufunga njia Nafikiri ni somo kubwa sote viongozi Pili sasa nimekuwa na moyo kuwa shida za biashara kubwa na ndogo ndogo kama za boda boda katika mpaka wetu wa Horo Horo ulioko Kaunti ya Kwale zitaisha Alisema tushikane na tuungane naye ili tuweze kupitisha yale maswala aliyotuambia ya kusaidia nchi zetu mbili katika biashara na utalii Asante sana
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Haiwi haiwi leo imefika. Baada ya muda mrefu huyu Daktari Lydia Nzomo ambaye ndiye alikuwa anafaa kupatiwa kazi hii tangu Bunge la Kumi sasa hivi wakati umefika. Imesemekana kuwa akisema atakubariki hakuna atakayezuia. Wakati ni sasa. Daktari Lydia Nzomo angekuwa amefanya kazi nyingi sana. Ukiangalia watu wengi walikuwa wamenyemelea nafasi hii. Wangeipata na Lydia Nzomo angebaki bila kazi hii ambayo amehitimu kufanya na ambayo ni muhimu sana. Tuko na hakika kuwa anaweza kuitekeleza kwa haraka na pia kuhakikisha kuwa walimu na wanafunzi wamepata haki yao. Tume ya Walimu si tume ya mchezo. Wahenga walisema kuwa bahati ya mwenzio usilalie mlango wazi. Daktari Lydia Nzomo akipatiwa kazi hii ataitekeleza. Ukiangalia historia yake amefanya kazi kubwa sana kwenye Tume hii ya Walimu. Baada ya huu muda wote akipatiwa kazi hii ataitekeleza vilivyo. Lydia Nzomo anaelewa matatizo ya walimu. Amekuwa mwalimu na anaelewa shughuli za Tume ya Walimu. Alifikia kuwa Naibu wa Katibu Mkuu wa Tume ya Walimu. Kwa hivyo tunamtakia kila la heri atakapokwenda kuitekeleza kazi hii. Naunga mkono Daktari Lydia Nzomo aanze kazi haraka iwezekanavyo.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Hata mimi nasimama kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Mbunge mwenzangu kutoka Mvita kuzungumzia mambo ya uchukuzi wa shehena ama makasha katika bandari yetu ya Mombasa. Nazungumzia suala hili kwa sababu agizo hili ambalo limetolewa kwamba kila kasha shehena ama mizigo ambayo itaingia poti itumie reli ni jambo ambalo litaathiri uchumi haswa wa sehemu ya Mombasa Pwani na hata Kenya kwa jumla. Tunajua kwamba wakati wafanyibiashara wanaleta mizigo ama mali kutoka sehemu tofauti tofauti mali hii huwa si ya Nairobi peke yake. Mali nyingine ni ya Mombasa nyingine ni ya Voi na sehemu zingine za nchi yetu ya Kenya kabla kufika Nairobi. Kwa hivyo iwapo mtu atalazimishwa mizigo ifike Nairobi tena irudi Mombasa hizo ni gharama mara ya pili. Jambo la pili tunazungumzia kujenga ajira. Agizo hili linazungumzia kumaliza ajira zilizoko hivi sasa. Tunajua mambo ya uchukuzi yamejenga ajira kwa vijana wengi sana. Mambo ya CFSs ya clearing and forwarding na mambo mengi ambayo yanafanyika katika bandari yetu yanapeana ajira nyingi sana kwa vijana wetu. Itakuwaje tunazungumzia kujenga ajira na huku tunavunja ajira zilizoko? Vilevile tuulize SGR iliyoko ina uwezo wa kubeba ile mizigo ama yale makasha yote yanayoingia katika bandari ya Mombasa kwa wakati unaofaa? Ni lazima tuangalie wakati katika biashara. Wakati ukipotea uchumi unapoteza na pia faida nyingi imepotea. Kwa hivyo iwapo tunataka kutengeneza maamuzi ya kutoa agizo lolote lazima kwanza tuangalie faida na hasara zake ni gani. Tunajua kuna changamoto katika mambo ya SGR. Iwapo changamoto hii itafanyika au kutatuliwa kwa njia ya kuumiza Wakenya wengi hili ni jambo ambalo halifai. Kwa hivyo agizo hilo si sawa na hatutaliunga mkono. Sisi viongozi tunakemea sana agizo hili. Kwa sababu soko la Kenya ni soko huru tunataka uamuzi.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Hili swala ambalo limeletwa na Mhe. Jessica Mbalu limenifurahisha kwa sababu limekuja kwa wakati mzuri. Hili swala la wanyama wa pori kuvamia binadamu mifugo na wanaopakana na Hifadhi ya Tsavo Mashariki na Tsavo Magharibi ni swala nyeti. Juzi nilimsikia Katibu Mkuu wa Wizara husika akisema wanahitaji Ksh15 billion ili waweze kufidia wale wote ambao wana malalamishi kuhusu kuvamiwa na wanyama pori. Swala hili ni nzito sana. Kule Taita Taveta Wundanyi ninakotoka na kule mwenzangu wa Mwatate anakotoka umasikini umechangiwa na kuvamiwa na wanyama pori. Hadi leo ni miaka karibu minne au mitano tangu tuahidiwe kulipwa fidia kwa wale waliovamiwa na wanyama pori na kuawa au mali yao kuharibiwa. Mwezi hata haujaisha simba wamevamia watu kwa milima. Babu zetu wanatuambia tangu walipozaliwa hawajawahi kuona simba wakifika kule Wundanyi kwa milima na kule Mwatate Chawia. Leo hii simba wako kule juu. Hili ni swala ambalo Bunge lazima litilie maanani sana na Kamati ya Mazingira haina budi ila kuleta Ripoti ya kueleweka Bungeni.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Huu ni mjadala muhimu. Kwanza ningependa kutuma rambirambi zangu za dhati kwa familia ambazo zimepoteza wapendwa wao. Ni jambo la kusikitisha mno kwa sababu hivi juzi tulikuwa tunajadili kuhusu vile tunavyoweza kupanua barabara zetu. Sehemu hii ya Sachangwan ni sehemu ambayo wananchi watukufu wa Kenya wamepoteza maisha yao kwa muda. Lazima Bunge hili lichukulie hili jambo kwa uzito kwa sababu si vyema tunavyoendelea kupoteza watu wetu muhimu katika nchi hii. Sehemu hii ya Kamukuywa ninapokumbuka ni sehemu ambayo nimesomea. Ni sehemu ambayo watu wengi wamepoteza maisha yao. Si jambo geni kwa Serikali kuu. Lazima kuna mtu ama watu ambao wamelala katika kazi yao. Kama vile wenzangu wamesema tunapitisha sheria hapa tunakaa muda mrefu tukijadili juu ya sheria lakini sheria hii haifuatiliwi na wale wanaohusika. Kwa hivyo ni wakati ambapo lazima wale wanaohusika wafuatilie na kuhakikisha ya kwamba sheria inapopitishwa inafanya kazi na waamuke kutoka kwa usingizi. Si vyema kupitisha sheria ambayo haifanyi kazi na haisaidii Mkenya wa kawaida. Ni jambo la kusikitisha. Sehemu hii ya Sachangwan imekuwa kwa mazungumzo kila siku. Siku moja kufuatilia nyingine lazima kuwe na ripoti ya kwamba kuna ajali katika sehemu hii. Ni wakati ambapo lazima Serikali ama wanaohusika waamke kwa usingizi kwa kazi yao. Wanafaa wafanye kazi vile ambavyo inahitajika. Shirika la NTSA ni lazima lifanye kazi vile ambavyo inahitajika. Nilisikitika kusikia kwa runinga ikitangazwa yakwamba ajali iliyotokea ni kwa sababu maafisa wa NTSA walikuwa wakifuata hilo gari. Ni lazima yule aliyehusika awekwe korokoroni mara moja. Ninaunga mkono ndugu yangu Mhe. Wanyonyi. Asante sana kwa Hoja njema kwa wananchi wa nchi hii. Asante sana Mhe. Spika wa Muda.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Kifungu 136 kinazungumza kuhusu kuchaguliwa kwa Rais. Kifungu cha 102 kinazungumza kuhusu kuchaguliwa kwa Wabunge na Kifungu cha 77 kinazungumza kuhusu kuchaguliwa kwa mbunge wa ugatuzi. Huu uchaguzi ulifanywa siku moja. Ni vipi MCA atakuwa na miaka mitano kamili na Rais kipindi chake hakiko wazi? Kipindi cha Wabunge hakiko wazi na Katiba inazungumza juu ya katikati ya miaka mitano. Ili turekebishe tatizo kama hili ni vizuri tuje na sheria kama hii ili tuweze kutatua wasiwasi ulioko kisheria. Kwa nini tuna wasiwasi juu ya uchaguzi kufanyika mwezi wa Agosti? Kwanza mimi ninawakilisha watu wengi ambao wanaishi katika mbinu ya maisha ya ufugaji. Wakati wa ukame hawa watu wanahama kutoka sehemu moja kuelekea sehemu nyingine kutafuta malisho na maji. Huu ni wakati mgumu kwa wafugaji. Utakapoleta uchaguzi katika Agosti wengi wa wafugaji hawataweza kupiga kura. Hiyo itatuadhiri sisi kama watu wanaopigania viti. Bajeti ya taifa siku hizi ni mchakato ambao unaanza katika mwezi wa pili unainuka katika mwezi wa nne na unaelekea kuisha katika mwezi wa tisa. Unapoweka uchaguzi Agosti utavuruga mchakato wa Bajeti ya taifa. Pia watoto wetu wako shuleni. Muhula unaanza Agosti na unamalizika na mitihani ya kitaifa. Katika eneo langu waalimu wengi ndio presiding officers . Je ni vipi wale waalimu watawacha shule waende wakafanye kazi ya uchaguzi? Kwa minajili ya hizi vurugu ninasimama kuunga mkono sheria hii ili tulete mwongozo kwa taifa la Kenya. Najua kuwa baada ya Mswada huu kupita tutatukanwa. Kwa wanaotusifu na wanaotutukana wajibu wa kutunga sheria ni wetu.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Kwanza kwa niaba yangu kama kiongozi wa CORD Wilaya ya Kwale nzima na kwa niaba ya watu wangu ninaomba kupeleka rambirambi zangu kwa familia na marafiki wa kiongozi wa mapambano ambaye ametuwacha. Nikirudi upande wa Hoja tulionayo ninataka kumshukuru kisawasawa aliyeleta Hoja hii. Jambo hili litakapofanyika litaondoa madhara mengi sana. Ni jambo la kusikitisha kwamba kutoka hapa mpaka Embakasi ambapo mtu anaweza kusafiri kwa gari kwa muda wa dakika kumi na tano kama nilivyofanya jana usiku kama saa tano watu wanachukua muda mrefu sana. Leo asubuhi nimelala nikifikiria kwamba hali itakuwa ile ile lakini nilipopata teksi kuja hapa imenichukuaa masaa matatu na nusu. Nilipochukua taxi kuja huku nilichukua masaa matatu na nusu; jambo ambalo limenisikitisha sana. Kwa hivyo Hoja hii haihitaji mjadala kwa sababu ni Hoja ya maana. Ni jambo ambalo linafaa kushughulikiwa na Serikali haraka sana ili tuhakikishe kwamba barabara hiyo imepanuliwa na kuondoa madhara mengi. Kwenye msongao watu wanabakurwa vipochi. Wengine wanavutwa skati zao zinatolewa kwa sababu mhalifu amejificha mahali penye watu wengi ambao wamesongaa mahali pamoja. Mtu huyo anapenya bila kuonekana. Jambo hili likitekelezwa madhara haya yote yatakwisha. Pia jambo hilo lisitekelezwe hapa Nairobi tu kwa namna imezungumziwa na mheshimiwa. Inaonekana kwamba idadi ya watu inaongezeka maradufu kila kukicha. Kwa hivyo kuna haja ya Serikali kuelekeza juhudi hii kwengineko kama vile Kwale ninakotoka; kule Malindi kulikotajwa na mhe. Gunga Ukunda Msambweni Rabai na kwengineko ambako idadi ya watu imeongezeka maradufu. Hali tunayoishuhudia katika barabara ya Jogoo itashuhudiwa katika sehemu nilizozitaja baada ya muda mfupi. Ni maoni yangu kwamba Bunge hili liiunge mkono Hoja hii ili tuweze kupata nafasi ya kusafiri kwa urahisi na kufika tunakoenda kwa haraka. Kwa hayo machache ninaiunga mkono Hoja hii.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Kwanza ninataka kumpatia kongole Mhe. Mwaura kwa kuileta Hoja hii ambayo ni muhimu sana katika maisha ya ndugu zetu walemavu. Walemavu katika nchi yetu ya Kenya ni takriban asilimia 15. Hawa wanaishi na ulemavu tofauti tofauti. Pia tuzingatie ya kwamba ulemavu ni kwa njia nyingi. Wengine wana ulemavu wa macho wengine wana ulemavu wa masikio na wengine wana ulemavu wa vyungo tofauti tofauti. Katika Katiba yetu ya Kenya katika kifungu cha 54(c) kinazungumzia umuhimu wa kuwezesha walemavu waweze kutembelea maeneo tofauti tofauti bila matatizo waweze kupata usafiri bila kuwa na matatizo na pia waweze kupata habari au kupashwa habari bila kuwa na matatizo. Jambo hili haswa la habari naona ni changamoto kubwa sana. Lakini najua Mhe. Mwaura pia ana Mswada ambao haujafika Bunge hili lakini utafuka ambao utazungumzia hasa masuala ya upasaji habari kwa sababu mpaka sasa tunaona vyombo vyetu vya habari havijatimiza sheria ya kushirikiana na walemavu kupata habari kimwafaka. Pia nataka kusema ya kwamba ndugu zetu wengi walemavu katika taifa hili la Kenya ni masikini. Umasikini huu umesababishwa na yale maumbile walio nayo. Wengi wameshindwa kwenda shule au kwenda kwa taasisi za masomo kwa sababu ya kukosa vifaa vinavyohusika kuweza kuwasomesha wapate taaluma. Hivyo basi wamekuwa wakiishi katika maisha ya uchochole. Vile vile Katiba yetu inazungumzia zile sheria ama haki za kimsingi. Imezungumzia kuwa mtu hatabaguliwa kwa rangi kabila dini na pia ikasema walemavu pia hawatabaguliwa. Hivyo basi tunaona mpaka sasa walemavu katika taifa letu wamebaguliwa. Tukiangalia majengo yetu mengi haswa ya umma hayajazingatia suala kama hili. Katika benki zetu hospitali na mahoteli yahajazingatia haya. Hivi karibuni nilikuwa na Mhe. Sen. Godliver katika warsha ya Kamati ya Bunge. Tulipelekwa kwa hoteli moja ambayo inaitwa Medina. Ilibidi tukose kufanya warsha ile kwa siku ya kwanza kwa sababu ukumbi wa mazungumzo ulikuwa umewekwa katika gorofa nambari nne na ilikuwa ni ngazi pekee na kulikuwa hakuna lifti. Basi ilibidi Seneta aweze kuteta sana mpaka ikabidi tuache kufanya warsha hiyo tukasema tuifanye siku ya pili. Ilitubidi tuifanyie nje ya hoteli. Hatukuifanyia kwa ukumbi wowote. Hivo basi hata sisi katika Bunge hili wakati tunaenda kupanga mikutano ya Wabunge lazima tujue tuna Wabunge wenzetu na Maseneta wenzetu ambao wana hali ya ulemavu. Mbali na mijengo tunaona walemavu ambao wanatumia yale magari yao ambayo imetengenezwa kuwabeba lakini hakuna pahali pa kuegesha magari kama haya. Wakati wanataka kuegesha vigari vyao kunakuwa ni hali ngumu sana. Hivyo basi swala hili ni lazima lizingatiwe. Taasisi ya ujenzi ya kitaifa tunayoita kwa lugha ya Kiingereza "National Construction Authority" inatakikana iweke mikakati na sera mwafaka za kuhakikisha ya kwamba majengo yalioko sasa na majengo ambayo yatajengwa yaweze kufanyiwa ukarabati ama yafanyiwe miundo msingi ambayo itawezesha ndugu zetu waweze kutumia njia hizo pasipokuwa na matatizo. Najua Kenya imeingia katika mikataba mingi sana ya kiulimwengu katika kutetea haki za walemavu lakini shida ni kwamba hatujazingatia na hatujaweka mikakati na kanuni mwafaka za kuhakikisha sheria hizi tumezifuata kulingana na mikataba na pia kulingana na Katiba yetu. Ikiwa sheria hizi hazikufuatwa ama mtu amezigeuka basi kutakuwa na sheria gani ama kutakuwa na hatua gani ya kumwadhibu mtu huyu ama shirika lolote ambalo litakuwa limekiuka mikataba kama hii? Itakuwa vizuri sana washikadau wote kama vile lile shirika la walemavu la nchi yetu kwa jumla wale wanaangalia mipango ya miundo misingi ya nchi yetu ya Kenya wale wanaoshughulika katika mambo ya uchoraji kutoa mapu zile za kutengeneza mijengo katika nchi yetu wakihusishwa. Washikadau hawa wote kabla hawajatekeleza mambo yao katika bajeti zao ni lazima wafikirie kwamba tuna walemavu hapa Kenya takribani asilimia 15. Hawa tu ndio wataweza kutusaidia sisi kama Wakenya na kuwezesha watoto wetu kupata haki zao za kimsingi. Watoto wetu wengi haswa wale ambao hawasikii na wale walemavu wa macho wameshindwa kuona alama za barabara na kwenye majengo. Kunatumika alama za kuonyesha ya kwamba ikiwa unaenda huku unafuata upande fulani. Wakati alama na ishara hizo zinatengezwa hutambulika ya kwamba kuna wenzetu walemavu ambao hawataweza kusoma ama kuzitambua kama vile sisi tunavyoweza kuzitambua. Tunajua tumepata majanga mengi sana hapa nchini kwetu Kenya kutokana na matatizo haya ya kuwa tumeacha kuzingatia walemavu. Walemavu wengi huishia katika majengo ambayo pengine kumetokea moto. Anataka kukimbia atetee roho yake lakini unapata kwamba kutokana na majengo yalivyojengwa mlemavu kama huyu atabakia pale kwenye kiti chake ama pengine yule ambaye anatumia magongo abaki kwenye magongo yake na apatikane na athari kama hiyo. Tujitayarishe kwa haya mambo ya majanga kama Wakenya ili yanapotokea tujue watu walioko pale jinsi watakavyoweza kusaidika. Tuweke katika akili zetu na tutie maanani kwamba kila mahali katika umma kuna walemavu ambao wanatembea mahali pale na chochote kinaweza kutokea na wakati kimetokea je hao watasaidika kwa njia gani? Sisi kama viongozi wa taifa hili la Kenya tunataka tuwe msitari wa mbele kuhakikisha kwamba sheria hizi kweli zimetekelezwa kwa sababu mara nyingi sheria tunazitunga na zinakuwa pale tu kama sheria. Mtekelezaji ni nani na ni nani atakayehimiza sheria zitekelezwe ikiwa kutakuwa hakuna watu wa kuhimiza sheria na kuweka msukumo thabiti wa kuhakikisha kwamba walemavu wana haki kama Mkenya mwingine yeyote? Walemavu hawatachukuliwa tu kwa sababu tumeingia katika mikataba ya kiulimwengu ama kwa sababu Katiba imependekeza hivyo basi sisi tunafanya tu kama kuonyesha. Ni lazima iwe ni haki yao ya kimsingi na ni jambo ambalo litafanywa kwa mikataba vile inavyotakikana. Iwapo yeyote atakiuka sheria lazima itamfuata. Kwa hayo mengi ama machache nataka kutoa kongole tena kwa Hoja hii. Ninamhimiza Mhe. Mwaura alete Mswada Bungeni ili tuuchangia na tuwe na sheria kabambe na mwafaka ya kuwalinda ndugu zetu walemavu. Asante Mhe. Naibu wa Muda.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Langu ni kuipongeza Kamati hii kwa utafiti katika ofisi za ubalozi za nchi ya Kenya zilizoko maeneo yale waliweza kupitia. Ukweli ni kwamba masuala yaliyotajwa hapa ndivyo mambo yalivyo. Matatizo yako katika kila ofisi zetu za ubalozi kule nje. Tatizo linalowakumba mabalozi wetu walioko kule na wafanyikazi wao ambao pia ni mabalozi wasaidizi wakimsaidia balozi mwenyewe ni kwamba pesa zile ambazo wanapatiwa hazitoshi miaka nenda miaka rudi. Ukiangalia Bajeti inavyopitishwa ofisi ya ubalozi bado inapatiwa pesa kidogo kulingana na muda ambao umepita. Ukiangalia hesabu inayofanywa hawajabadilisha pesa walizopeana miaka kadhaa iliyopita mpaka sasa hivi ilhali hela yetu ya Kenya imeshuka nguvu kufananisha na pesa za nje. Hivyo basi inaonekana kuwa kuna upungufu mkubwa sana wa pesa za kufanya kazi ile ambayo waliotumwa kule nje. Suala la pahali ambapo ofisi zetu za ubalozi zipo pamoja na pale wafanyikazi wetu wanapokaa huko nchi za kigeni limekuwa suala nyeti na limezungumziwa kwa muda mrefu. Kuna wakati nakumbuka nikiwa waziri waziri mwenzangu alifanya uamuzi wa kuuza sehemu fulani ambapo tulitakikana kujenga maeneo ya ubalozi na ikatutatiza sana wakati huo. Tulifikiria kuwa tungetafuta pesa kwenye Bajeti za kusaidia kujenga maeneo yale ili ubalozi wa Kenya uwe pahali pa hakika. Vile vile ukiangalia maeneo mengine ambapo tunafanya shughuli nyingi kama vile nchi ya Uchina ukienda kule mara nyingi Wakenya wengi wanafanya shughuli zao haswa za kibiashara upande wa Guangzhou lakini hawana ofisi ama ubalozi ambapo wanaweza kwenda kupata usaidizi. Vile vile mara nyingi eneo lile ambalo watu wanaweza kutumwa kushughulikia chochote kuna umbali kana kwamba hata ukisafiri na ndege ni masaa matatu na nusu mpaka Beijing ambapo ofisi zetu zipo. Hivyo basi nakubaliana na Kamati hii kuwa kuna umuhimu wa Serikali yetu kufungua ofisi ya ubalozi mara moja katika eneo la Guangzhou ili Wakenya walioko kule waweze kupata huduma na pia uhusiano wetu na nchi ile uimarike. Vile vile ukienda kwenye ofisi za ubalozi utakuta wana matatizo makubwa sana haswa kwenye masuala ya magari. Mara nyingi inawabidi watafute magari ya kukodisha. Magari ya kukodisha huwa ya bei ya juu. Kwa kifupi sana ningependa kuzungumzia swala hili la sisi kulipa kodi ya nyumba kwenye maeneo yale. Bei ya kulipa iko juu hata kushinda bei ya kulipa deni kama tutakuwa tumechukua deni kwa uhusiano wetu na zile nchi na haswa benki zile ziko kule ili kuweza kujenga ubalozi kule nchi za nje. Ingekuwa ni rahisi sana kwa sababu wale wengi waliojenga kwa mfano nchi ya Uganda na nchi zingine ambazo zina majumba maeneo yale kama upande wa New York na London utaona wanapata hela nyingi kiuchumi na zinatumika kwenye wizara ya kusimamia masuala ya nje ili kuimarisha shughuli za ubalozini. Maeneo yale ambayo yanahitaji ubalozi mdogo haswa maeneo kama yale niliyotaja kwa mfano Uchina na nchi zinginezo pahali ambapo Wizara hii imeona kuna umuhimu wa kufungua maeneo yale kuna umuhimu wa Bunge hili na haswa Kamati inayohusika kushikana na kuzungumza na wizara pamoja na Rais wetu na Naibu wake ili kuhakikisha ya kwamba maeneo yale yanaweza kupatiwa ubalozi huu haraka iwezekanavyo. Mhe. Naibu Spika wa Muda naunga mkono kazi hii ambayo imefanywa na Kamati hii lakini wasiiachie hapo. Waendelee na kuhakikisha ya kwamba masuala hayo waliyoyataja hapa ambayo ni muhimu yametekelezwa mara moja. Tunapokwenda kwenye mwaka ujao wa kutengeneza Bajeti inayokuja tuangalie umuhimu wa kupatia pesa za kutosha masuala yaliyotajwa hapa na haswa tuangalie kama hela hizo zinatosha ama hazitoshi kwa shughuli zile zinazoendelea na kuita wawekezaji. Ubalozi ndio unaweza kutuunganisha na nchi za nje ili kuhakikisha kuwa wawekezaji wamekuja kwa nchi yetu kwa wingi kufanya biashara huku na kufungua makampuni ambayo yatawapatia kazi watu wetu na haswa vijana. Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa eno hayo machache naomba kuunga mkono.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Mhe. anatoka eneo la Pwani na Kiswahili chake ni cha kiwango cha cha juu kidogo. Lakini tutajikakamua tukinene. Leo tutaongea Kiswahili. Naunga mkono Hoja hii ambayo imewasilishwa na Mhe. Ali ambaye pia tunamjua kama "Jicho Pevu". Hoja hii ambayo ameleta Bungeni tutaiunga mkono kama Wabunge na pia Wakenya wote. Hoja yenyewe inazungumzia shida ambayo imekuwa ikitukabili kama nchi. Ni shida ya afya yetu. Kama nchi hatuwezi kuchezea afya yetu. Ni lazima tuhakikishe kuwa fedha za kutosha zimetengwa ili isiwe Hoja zinaletwa Bungeni na baada ya kuzijadili na kuafikiana kama Wabunge zinakufia hapa; baada ya miezi ama miaka kadhaa hatuoni yale tumepitisha kama Wabunge. Hongera Mhe. Ali. Hili ni tatizo kubwa sana. Kenya nzima ina hospitali mbili peke yake za rufaa ambazo ziko mbali kutoka nyingine. Watu kutoka Pwani huja hadi Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta. Inawachukua muda na watu wetu wanaaga njiani wakati wanasafirishwa. Hii ni shida kubwa sana. Hoja ya Mhe. Ali inafaa itiliwe maanani kabisa ili tuwe na hospitali ya rufaa Pwani. Lakini isiwe Pwani peke yake. Upande wa Kaskazini mwa Kenya pia inahitaji hospitali ya rufaa kwa sababu ni mbali. Watu wa eneo hilo hawawezi kusafiri kuenda Eldoret kwa urahisi. Ni mbali pia kwao kuja Nairobi. Hata tukiwa na Hospitali ya rufaa huko Pwani itakuwa mbali kwa watu wa kaskazini mwa Kenya. Tuko na shida pia ya migomo ya madaktari. Hawagomi bure. Madaktari sio kama wafanyikazi wengine wa Serikali. Wanafanya kazi masaa 24. Wanaitwa usiku wa ane kwa mfano kushughulikia mgonjwa ambaye labda walimtibu mchana lakini hakupata nafuu na anataka kuonana na daktari aliyemtibu wakati wa mchana. Inabidi daktari huyo amke ili aende kazini. Tunapoteza madaktari kwa sababu nchi jirani wanalipa madaktari vizuri kuliko Kenya. Kwa hivyo inatakikana pia tufikirie tutambue shida yetu. Tunatoa mafunzo kwa madaktari wengi katika vyuo vikuu. Siku hizi Chuo Kikuu cha Kenyatta na kile cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta vimeanzisha mafunzo ya udaktari. Pia tuko na wauguzi wanaosomea vyuo vya mafunzo ya uuguzi. Lakini ukitembelea hospitali zetu za Serikali unapata hao madaktari hawafanyi kazi huko. Wengi wao wamefungua hospitali za kibinafsi kwa sababu ladba wanapata pesa. Wengine wamehamia nchi za kigeni. Inabidi tuhakikishe madaktari wanahudumu kwa hospitali zetu za serikali. Watu wote hawana uwezo wa kuenda kwenye hospitali za kibinafsi kwa sababu ya gharama ya juu. Ni uchungu sana ukiona mama akibeba mtoto afikishe kwa hospitali lakini daktari hawezi kumsaidia kwa sababu hana dawa. Ikiwa kuna vifaa ambavyo havipatikani kwenye hiyo hospitali daktari anamtuma huyo mama anunue hivyo vifaa ama dawa kwenye maduka ya madawa lakini huyo mama hana uwezo. Daktari anaangaliana na mama mpaka mtoto anakufa mkononi mwa mama kwa sababu ya ukosefu wa vifaa katika hospitali zetu. Ni uchungu mkubwa. Sisi ambao tunatunga sheria tuko na uwezo wa kupelekwa ng'ambo tunapokua wagonjwa. Tumeona watu ambao wamepelekwa ng'ambo kuwekwa bandeji pekee wakigongwa kidogo na mawe. Kuna wenzetu ambao wanakufa kwa ugonjwa ambao unatibika. Katika karne hii ugonjwa wa malaria unaua watu humu nchini licha ya kwamba tuko na aina zote za dawa za malaria. Unakuta ugonjwa wa pnuemonia unaua watoto nchini Kenya ilhali tuna dawa za kukabiliana na magonjwa kama hayo. Kwa vile madawa hayo hayapatikani kwa urahisi katika hospitali za umma matibabu yanakuwa ni kwa watu walio na pesa. Kulingana na Kifungu 43 cha Katiba yetu afya bora ni haki ya kila Mkenya. Siku hizi afya bora ni haki ya walio na pesa na siyo haki kwa wasio na pesa. Ni lazima tulitilie maanani na tulizingatie suala zima la afya. Ninataka pia kumwambia Mhe. Ali kuwa tukishaipitisha Hoja hii afuatilie kuona kuwa imetekelezwa. Ikibidi urudi Bungeni ili tuweze kutoa maagizo afanye hivyo ndiyo masuala yanayoshughulikiwa na Hoja hii yasiishie hapa Bungeni. Hii itatuwezesha kuhakikisha maombi yote tunayoyapitisha hapa Bungeni yametekelezwa iliWakenya wote waweze kupata matibabu. Hata kama nimeongea Kiswahili ambacho kidogo kinatatiza ninajua kwamba nimejikakamua. Mhe. Omollo ahsante kwa kuja kutuunga mkono. Umemaliza kazi yako. Sasa nitakuwa nikipambambana na nani? Sasa kazi yangu imeisha. Hiyo handshake imemaliza kazi yangu.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Nashukuru sana kwa nafasi hii umenipa nichangie na kuzungumzia suala hili la mazingira. Kwanza nitachukua fursa hii kukashifu Serikali kwa jinsi ilivyofurusha watu ambao ni akina yahe kwa makazi yao. Nitasema kwa nini ni makazi yao. Wale watu wameishi pale. Kule Mau ndio kwao. Sio kwao kimakosa. Serikali kuwa na tabia ya ndumakuwili ndiyo imenipatia nafasi hii kuikashifu licha ya kuwa mwanachama wa Serikali hii. Wamama wameumia. Wakongwe wamenyeshewa. Watoto zaidi ya 4000 wameachwa bila masomo. Shule zaidi ya sabini zimebomolewa. Watu wamekosa maji safi. Wale wagonjwa wamekosa dawa. Swali ambalo ningependa kuuliza ndani ya Bunge ni kwamba tangu tukio hili la watu kufurushwa Mau litokee hatujaona Waziri wa Mazingira na Misitu akitembea kule. Hatujaona Waziri wa Maji Waziri wa Ardhi ama Waziri ambaye anashughulikia majanga akitembea kule. Swali kuu ni: Kenya ni upande upi? Mbona wananchi wanyonge wanakandamizwa? Mimi nilifanya siasa. Nilikuwa katika Bunge la Kumi na tulizungumzia suala hili. Nataka kusema ya kwamba kitumbua cha Raila kiliingia mchanga aliposhika suala hili la Mau. Nataka kueleza Serikali hii kwamba kimo chao kitakuwa motoni wasiposhughulikia suala la Mau kwa namna ambayo itapendeza. Kile ambacho tunataka kusema ni kwamba hatupingi mazingira kuhifadhiwa lakini tunataka ifanywe kisheria. Pale Mau kuna laini mbili. Kuna laini ya kwanza ambayo Mhe. Raila Odinga aliibuni wakati alikuwa Waziri Mkuu. Kuna laini nyingine iliyobuniwa na Rais Uhuru Kenyatta aliposhika usukani. Serikali ambayo iko mamlakani ni ya Uhuru Kenyatta. Tunasimama na uamuzi wa Rais Uhuru Kenyatta kwamba mpaka ndio huu. Kwa hivyo tunataka kuuliza ni nani huyo ameenda kinyume na msimamo wake Rais Uhuru Kenyatta akafurusha watu. Wale watu wanaofurushwa hawako ndani ya msitu. Wako kwa makazi yao na inajulikana. Kuna kitu ambacho kinaitwa kwa kimombo cutline . Kwa hivyo mimi ningependa Bunge lizungumzie suala hili kimakini. Nimesikia hapa kila Mhe. anaisifu Kamati ambayo imefanya kazi. Mgala muue lakini haki yake umpatie. Kamati haijazingatia matatizo ya wale watu ambao walifurushwa. Watapelekwa wapi? Je watapewa sehemu badala? Hilo ndilo jambo ambalo linatukera sisi. Mimi ni kati ya Wabunge ambao wanatoka maeneo ambayo chemichemi ya maji katika taifa la Kenya ipo. Huko ni mlima wa Cherangany. Mmoja wa wanakamati amesema kwamba walitembea katika kila msitu Kenya nzima lakini hawakufika kwetu. Kamati hii haikutembea Kenya nzima. Walienda sehemu mmoja na wakatengeneza Ripoti kulingana na fikra zao. Hawakutembelea Wakenya wote. Kwa hivyo Kamati hii haijafanya kazi bora. Kile ambacho nataka kusisitiza ni kwamba hatuzungumzi mambo ya kuhifadhi misitu kwa mara ya kwanza leo. Misitu ipo. Tukielezwa kwamba kuna mito ambayo inanyauka Aberdare ama Mkoa wa Kati katika Taifa la Kenya ina uhusiano ngani na Mau? Hilo ndilo swali. Mto wa Nairobi hapa ukikauka una uhusiano ngani na Mau? Tukiambiwa mito inakauka kule Kisumu ambapo hata Waheshimiwa hawajapanda miti hata siku moja inauhusiano ngani na Mau? Nilitembea kule na nikaona ni jangwa. Kunakatwa miti kila siku. Sisi tunahifadhi mazingira lakini tunapata faida gani? Tunapigwa na kufurushwa. Kuna Mhe. ambaye ana hoja ya nidhamu. Mpatie nafasi. Labda Mhe. Spika wa Muda hajamuona. Mhe. makinika.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Nasimama hapa kuunga mkono Ripoti hii ya Kamati. Ukuta huu utasaidia sana. Tuulizeni sisi watu wa Lamu kwa sababu tuliumwa. Sasa tunajua umuhimu wa ukuta huu lakini tunazungumzia ukuta sio fence . Jana nilikuwa Ishakani na Kiunga. Niliona kontrakta anatengeza miti yani poles . Sikuona kama wanatengeneza ukuta. Ni vile wenzangu walivyozungumza kwamba si ukuta ni fence . Pia naomba ikiwa watajenga ukuta na Mwenyekiti wa Kamati alijitetea kwamba kwingine kutakuwa ni ukuta na kwingine ni waya kuhakikishwe kwamba jamii ya Wabajun kwenye mpaka ishughulikiwe. Kuna Wabajun wa Somalia na wa Kenya. Waweke zile nafasi ambazo wataweza kupita ili wahamiaji ama wasafiri wasikatazwe ila waweze kuja. Hizi ni jamii ambazo ziligawanywa. Nataka kuzungumzia zaidi hii Southern Sector - Libat-Kiunga ambayo ni kilomita 105. Ni muhimu iwekwe ukuta sawa sawa. Ukuta huo utasaidia sana kwa sababu kule Boni kuna mambo huwa yanatokea. Kulingana na Kamati ukuta huo ulikuwa uwe tayari. Ni matarajio yetu kwamba utakuwa tayari mwaka huu. Unafaa uwe umemalizika mwaka huu. Unafaa uwe umemalizika kitambo kwa sababu zile shida tunazozipata sisi watu wa Lamu zinatufanya sisi viongozi wakati mwingine hatuwezi kufanya kazi yetu. Kamati ya Regional Integration ya Bunge ilienda ikakatazwa kufika Kiunga. Saa hii shule tano za Basuba Ward zimefungwa. Hakuna shule. Hiyo jamii mpaka sasa hawana hata mtu mmoja ambaye amemaliza chuo kikuu. Ikiwa shule tano zitafungwa basi sisi tutakataa ukuta? Tutofautishe wale wahalifu wa kutumia pesa hiyo vibaya na ukuta. Hiyo ni kesi tofauti. Wale wahalifu wasisababishe mambo mazuri kutofanyika. Kama kuna uhalifu ni jukumu la Bunge hili lihakikishe hao wahalifu wameshikwa lakini ukuta uwekwe. Nimependa mapendekezo mengine ya Kamati hii. Kamati imesema ule uwanja wa ndege uondolewe Kiunga uwekwe mwingine. Ni matarajio yetu kwamba wataujenga uwanja mzuri lakini Kamati imesema kwamba itahusisha viongozi. Mimi ni kiongozi wa Lamu lakini bado sijahusishwa. Sijui ni viongozi gani wanahusishwa. Pendekezo lingine ni kwamba barabara ya Hindi-Bodhei-Kiunga iwekwe lami. Ni muhimu ikiwekwa lami kwa sababu asilimia 10 ya uhalifu utapungua. Kabla lami iwekwe angalau wangefyeka pande zote mbili za barabara ili wale wahalifu wakitokezea waonekane. Tumetoa maoni hayo mara nyingi. Lakini sijui kwa nini ukiwaambia wafyeke hawafanyi hivyo bali wanaenda kugusagusa kidogo na hawamalizi kazi hiyo. Nashangaa anasema kwamba ameenda dera. Kamati itueleze zaidi kwa nini hawakuanza na Lamu na wanajua sisi ndio tunapata matatizo zaidi. Mbona wasianze Lamu? Naomba Kamati hii ije Lamu ione. Iende Kiunga na Ishakani. Kamati imependekeza kwamba kontrakta watajwe kwa sababu nimeenda Ishakani na hawana maji ilhali kontrakta ako pale anajenga mambo yake. Si ubinadamu. Huyo kontrakta angesaidia ile jamii angalau na gari moja ya maji kwa wiki. Kontrakta anajenga pale na watu wanaumia na hawezi hata rejesha maji kwa jamii. Kama ni mtu wa pale pale tumjue na kama ni mwingine tumjue mkandarasi ni nani ili awasaidie wale wananchi. Kama nilivyotangulia ni changamoto kwa sisi viongozi pia. Kuna sehemu Lamu hatuwezi fika kwa sababu ya utovu wa usalama. Mimi nashangaa watu wakisema ukuta usiwekwe. Ukuta uwekwe lakini wahalifu washikwe. Mhe. Naibu Spika wa Muda naona niachie hapo. Naunga mkono Kamati na pia naunga mkono kuwa ukuta ujengwe sio fensi ya waya.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Nasimama pia kuunga mkono mapendekezo ambayo Mwenyekiti wa Kamati yetu ya Uchukuzi ameleta mbele ya Bunge hili kuhusu Ripoti ya matumizi ya Standard Gauge Railway (SGR) katika taifa letu la Kenya. Mapendekezo ambayo yamekuja mbele ya Bunge hili ni kutokana na hali ambayo ilitokea na mtafaruku uliopatikana baada ya Serikali kushurutisha kuwa makasha na mizigo yote yabebwe na SGR. Jambo moja ambalo tumejifunza katika mtafaruku huu ni kuwa Serikali na raia wake wakifanya kazi pamoja matatizo makubwa yanaweza kusuluhishwa bila kuwa na vurugu. Pia imetuonyesha kuwa ni vizuri kuwa na miradi mikubwa kama hii ya SGR. Lakini kabla haijatekelezwa pengine watu washirikishwe na watoe maoni yao ili inapotekelezwa watu wote washatoa mawazo yao na kuondoa zile hofu ambazo zingeleta mtafaruku siku za baadaye. Hiyo imeonekana wazi. Baada ya watu kutoa maoni kukawa na masikizano. Jambo lingine ni kwamba Ripoti hii imewafanya Wabunge kufikiria kitaifa. Haikupendeza kuwa ilisemekana kuwa mambo haya yanadhuru sehemu za Pwani peke yake. The coastal regionis part of the nation . Ikiwa tatizo lagusa sehemu moja latakiwa liguse nchi nzima. Sisi ni Wabunge wakitaifa. Nilifurahishwa kuwa ingawaje ilikuja polepole mwishowe tulipata usaidizi kwa sababu SGR ingeathiri sehemu kubwa sana ya nchi yetu. Si Pwani peke yake. Kando ya vile alivyoeleza Mwenyekiti wetu tuliona kuwa katika usafirishaji wa haya makasha badala ya kasha kuletwa mpaka Nairobi ilikuwa kuna wale ambao wanachukua makasha hayo nakuyaregeza kwenye Port . Kwa sababu ya kuzuia msongao kule Port hao walikuwa na ahadi zao wakiwekeza. Baadaye meli ikiwa tayari wanayachukuwa na kuyaweka ndani ya meli na kuyapeleka ambako wanayapeleka. Hapo kulikuwa kuna nafasi nyingi za kazi zilizotokea kutokana na hali kama hii tunayozungumzia. Ilipokuwa ni lazima SGR ibebe mizigo hiyo na baadaye iregeshe ikawa kuwa kila mtu atafutwa kazi kwa sababu huwezi kumlipa mfanyakazi ambaye hafanyi kazi nawe hupati pesa pia. Tumejifunza ni lazima tutumie hizi universities zetu kufanya utafiti katika mambo yote ambayo tunataka kufanya kama nchi. Vile vile kila jambo linalofanywa lihusishe raia kwa ukubwa na upana kwa sababu ni raia ndio watakaoathirika ama watakaotumia zile services . SGR inakuja na kubeba watu lakini inawaangusha katika zile sehemu za Syokimau. Mtu anapaswa apande teksi aje mpaka mjini. Ulimwenguni mzima huwa tunaona train services zinaishia ndani ya mji. Mtu anashuka na kutembea kwa mguu hadi ofisini. Kwa hayo machache naunga mkono mapendekezo hayo na kuomba ndugu zangu pia waunge mkono.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Ni jambo la kusikitisha kuwa hii Serikali inafanya mambo yale yale ambayo yalifanywa na Serikali zilizopita. Tunachukua kizibo cha mraba nia na madhumuni ikiwa ni kuhifadhi pengo la mduara. Hii si mara ya kwanza ambapo tunaongea kuhusu jambo hili. Mwaka uliopita wakati shirika la KQ lilipotangaza hasara ya mabilioni Bunge hili lilikaa chini tukazungumza na kuliwaza jambo hilo. Mwishowe watu walitoa hisia zao na kila mmoja akatoa duku duku lililokuwa kwa roho yake. Lakini suala ni lile lililofuata baada ya pale. Serikali ya Jubilee iliamua kuipatia KQ billion inne. Kwanza hizi fedha hazikuidhinishwa na Bunge ili shirika hili lipewe. Makosa haya haya tunayoyafanya katika shirika hili yamefanywa katika mashirika kama vile Mumias Sugar. Tukiangalia historia ya Kenya mashirika yaliyopewa kipao mbele kuleta fedha katika nchi hii ikiwemo Nzoia Sugar Telkom Kenya Kenya Railways yamedidimia na ukiangalia hata kwa akili za mtoto mchanga hii ni mipangilio ya watu ya kuvuja pesa za umma na tunayaregerea. Tuna baadhi ya watu ambao tuko katika Kamati ya Fedha Mipango na Biashara. Nakumbuka KQ ilileta ombi ili wahifadhiwe wasilipe ushuru wa VAT. Wengine wawe wanalipa lakini wao wasilipe. Shirika hili lilipewa jawabu na Bunge kupitia Kamati ya Fedha Mipango na Biashara ambayo mimi ni mmoja wa wanakamati kuwa jambo hilo haliwezi kukubalika. Walielezea Kamati kuwa kuna dalili mbaya zaidi kuwa pesa zitapotea na ninasisitiza jambo hili. Nawaomba wenzetu kama hawana suluhisho la kutatua hili donda sugu la uvujaji wa pesa za umma waachie watu ambao wataweza kuiendeleza na watu ambao watahakikisha kuwa pesa za umma hazivujwi au kupotea kiholela holela. Historia itatuhukumu. Historia italihukumu Bunge hili. Nawaomba wenzangu katika pande zote tusiliangalie jambo hili kwa minajili na tusiwe wenye kusifu kupiga kelele na duru huku tukiwa na nia na madhumuni ya masuala ya vyama. Tuangalie nchi na maslahi ya wananchi kabla ya mambo mengine yote. Asante sana Mhe. Spika Naibu wa Muda.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Nilikuwa namalizia kwa kusema kuwa namshukuru Mwenyekiti na Wanakamati. Tulipoanza jambo hili kulikuwa na mvutano na bugudha sana. Nawasihi ndugu zangu wanaopendelea " bonga points " za mitaani kwa kuzungumza tu na kutoa kashfa ambazo hazina ukweli kuwa leo pengine iwe funzo tunawapa jinsi sheria zinatungwa. Tumefaulu leo na nina ii kila mmoja amekubaliana na kauli yetu kuwa ni lazima SGR isiwe ya kulazimishiwa mtu bali iwe hiari kwa sababu wanaona inafaa. Asante sana Naibu Spika wa Muda.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kuunga mkono kuondolewa kwa kipengele cha sita cha Ripoti hii kinachohusisha EACC. Sababu yake ni ukizingatia mambo mengi yamezungumziwa humu Bungeni tumeona EACC ndio shirika ambalo tutahitaji kufanya upelelezi na utafiti wa mwisho wa ile Ripoti tumeleta Bungeni. Vile vile wakati tulikuwa tunaandika Ripoti tulipata hawakuwa na uwezo wa kusimamisha malipo ya pesa kwa sababu hilo si jukumu lao. Na kama tungependa kuendelea ni vizuri tuangalie ni akina nani wamehusika na tuone ni akina nani wanaweza kutusaidia kutafuta mwelekeo wa wale wamehusika. Kwa hivyo nimeunga mkono kuondolewa kwa kipengele hicho ndio tukamilishe Ripoti hii muhimu ambayo nchi yetu ya Kenya huenda ikapoteza pesa nyingi. Asante sana. Naunga mkono.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kuunga mkono Mswada huu wa marekebisho. Ni wajibu wa kila mmoja kuwa katika uongozi. Akina mama wameshindwa kufika kwenye Bunge la kitaifa na kwenye mabunge mengine kule nyanjani kwa sababu ya ukosefu na udhaifu wa kiraslimali. Kwa hayo machache naunga mkono.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kuunga mkono Ripoti hii kwa sababu ya madhara mengi ambayo yameangaziwa hapa. Madhara ni mengi wakati ambapo msichana ama mtoto wa kike anapitia hali hii ya ukeketaji. Katika hali hii tumesikia kwamba wakati mtu anapitia haya huvuja damu nyingi ambayo inasababisha hali mbaya ya afya na pia wakati ambapo mtu ni mja mzito saa zingine huwa anaavya mimba. Kwa hivyo wakati ambapo sheria hii tunayoitengeneza ni vizuri Serikali itilie hili jambo maanani na kuharamisha tendo hili. Kwa hivyo yule ambaye anatekeleza tendo hili aweze kuchukuliwa hatua kali sababu wakati ambapo tendo hili linamfanyikia yule mtoto wa kike wengi huacha shule kwa sababu ya jambo hili. Vile vile wakati ambapo unapitia mahali unasikia watu wakizungumza wakati mwingine unakosa raha ya kukaa na wao kwa ajili ya mambo ambayo wanayasema halafu wanajitenga kwa kufikiri kuwa wanaonewa. Kwa hivyo ni vizuri katika zile jamii ambazo zinaendelea kutekeleza haya mambo Wizara ya Jinsia ichukue nafasi hii kuelimisha zile jamii ili waweze kuyashika na kujua ya kwamba wakati wanatekeleza tendo hili yule ambaye anatendewa anaweza umia sana. Hii ni kwa sababu tumesikia madaktari hapa wakisema kwamba wakati wa hedhi damu inarudi ndani ya tumbo na kuharibu nyumba ya mtoto . Hili ni jambo ambalo tunafaa kulichukulia maanani sana. Wakati ambapo jambo kama hili linatekelezwa kule mashinani kule ambako wakati mwingine Serikali hufikiria kuwa hakuna watu ambao wanafika kule ni vizuri wakati ambapo tuko na machifu wanaoongoza kule vijijini pia watwikwe jukumu hili ili waweze kutekeleza wajibu wao kuhakikisha kwamba ukeketaji umekomeshwa. Ni kwa sababu ni vibaya sana wakati ambapo umeolewa halafu wakati wa kupata mtoto njia ya uzazi iwe imefungwa . Basi ni jambo ambalo lafaa kuchukuliwa kwa uzito sana. Wakati tunapitisha hii sheria isiwe tu ni kupitisha bali inafaa ianze kufanya kazi ili yule ambaye anafanya jambo hili achukuliwe hatua kali. Hii ni sababu sio vyema kuangalia tu wasichana wakati ambapo wanafanyiwa tendo hili la kinyama. Kwa hayo machache ninaunga mkono Hoja hii. Asante.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kwa jambo la nidhamu. Kwa ajili ya umuhimu wa Hoja hii ambayo inaendelea kuzungumzwa ningeomba tupunguze muda. Badala ya kuwa dakika kumi ziwe angalau dakika tano ili kila mmoja aweze kuzungumza. Asante.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingara na Rasilimali kwa kuleta Hoja hii. Ikiwa Serikali itafuata Hoja hii inavyotakikana itakuwa ya maana sana. Watu wa Pwani kwa mfano Mombasa na Kwale wamekuwa wakisumbuka na kuteseka sana kwa sababu ya hali ya kutoweza kumudu shughuli zao. Serikali ilikuwa inawaachilia watu kuingililia Mwambao wa Pwani bure tu na kuvuruga mambo. Nina ii kwamba kutokana na Hoja hii mambo yatakuwa sawasawa. Naiomba Serikali ifuatilie mambo haya baada ya hapa. Kama vile Mheshimiwa alivyozungumza miradi mingine kama ule wa kuchimba makaa ya mawe kule Lamu ni miradi ambayo ni haki kabisa izuiliwe mapema. Tatizo ni kwamba shughuli za Katiba ziko wazi watu wanapitisha sheria lakini mambo yanafanywa kimabavu na kunatokea mambo ambayo hayastahili. Kwa mfano kule Mwambao wa Pwani katika Kaunti ya Kwale kuna uvuvi ambao unapaswa ufanyike vizuri. Lakini utaona kwamba kwa sababu hakuna ushirikiano uelewano na umoja kati ya Serikali ya kitaifa serikali ya kaunti na wananchi miradi inayofanywa pale si miradi mizuri na inafanywa kwa kutumia nguvu. Juzi halmashauri ya Bandari ya Mombasa walichimba mchanga kule na kuvuruga kila kitu kwa sababu hakuna usimamizi bora. Ikawa wananchi wanakosa kufanya shughuli zao za uvuvi kwa muda mrefu na samaki wakapotea kwa sababu ya uchimbaji wa mchanga ambao haukuwa sawa. Naunga mkono kikamilifu Hoja hii. Lakini naomba Serikali ifuatilie na ifanye vile ambavyo Bunge hili la Kenya ambalo ni tukufu na linakubalika litakuwa limepitisha.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuyaunga mkono mapendekezo haya kutoka Bunge la Seneti. Hivi vipengele vinaleta mambo mazuri kwa wasee wa nchi hii. Hii hali ya kukosa maji na kuwa na ukame ni kitu tunafaa kufikiria sana sisi kama wasee wa Bunge kwa sababu kuna vijana wengi sana wanakosa doo
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Ningependa kwanza kumshabikia Mhe. Keynan kwa kuuleta Mswada huu. Ningependa kusema kuwa kule nje ni kubaya. Kwa wakati ule mdogo ambao nilipelekwa kwa uchaguzi mdogo niliona kama ndoto. Ukiwapigia simu wenzako hawashiki. Kwa hivyo huu Mswada utawasaidia wengi. Kwa upande wa bima wengi wa wabunge ambao wamekuwa katika viti ningependa kutoa mifano lakini sio kwa majina wale wa kutoka Pwani ukiangalia hali zao sasa hivi za kiafya zimekwenda chini kwa sababu ya kukosa matibabu. Kwa hivyo ninaunga mkono Mswada huu ambao umeletwa Bungeni wakati ufaao.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Ningetaka pia kuchangia mjadala kuhusu hii Ripoti ambayo Rais wa Kenya aliweza kutupatia kuhusu hali ya usalama katika hii nchi. Ijapokuwa hii Ripoti ilikuwa ya miezi kadhaa ambayo imepita nimeiangalia na ninaona bado mambo yale ambayo imeangalia ni yale ambayo yako. Hakuna kitu kimefanyika kutoka mwezi wa tatu na wa nne mwaka huu ambacho kimebadilisha sababu za ukosefu wa usalama katika hii nchi na pia hakuna mambo ambayo yamebadilika. Yale majadiliano yalikuwa na pia suluhisho ambazo Ripoti hii imetoa bado ni zile zile. Kwa hivyo hakuna mabadiliko ambayo yamefanyika. Naibu Spika wa Muda ningetaka kusema kuwa polisi lazima sasa waanze kuangalia hali ya masomo ya wale wananchi ambao wanaajiriwa katika kikosi ya polisi. Haya mambo ya kuwachukua kutoka mahali ambapo wamelelewa na wamesomea na kuwapeleka hapa Kiganjo ama Embakasi na baada ya hapo wanatumwa Baragoi Lamu na dera mahali ambapo kuna vita kabisa lazima yabadilishwe. Lazima kuwe na sehemu ya mafunzo yao ambayo inawapeleka Baragoi na kule kwa kichaka dera ili haya mambo ya ukora ijulikane. Polisi ambao wanatumwa hapo ni wale ambao wameajiriwa hivi juzi. Wale ambao wamekuwa wakikula mshahara na wana uzoevu wa kazi hawatumwi kule kwa sababu wanaweza kuhongana waweze kukaa hapa Nairobi ama sehemu zile ambazo zina usalama. Vijana wetu wa miaka 21 ndio wanatumwa waende kule. Hawa wengine ambao wamepata vitambi hawawezi hata kuenda kufanya kazi hapo. Kwa hivyo ni muhimu sana mambo ya masomo yabadilishwe. Pili kwa hili jambo la ukosefu wa kazi kwa vijana tusiliangalie tuseme eti polisi ndio wataleta suluhisho katika hii nchi. Lazima tutafutie vijana wetu kazi. Huu uamuzi wa Serikali kuwa watu waendelee kufanya kazi na wastaafu baada ya miaka 60 lazima ubadilishwe. Tupatie vijana wetu nafasi ya kufanya kazi. Lazima wananachi wastaafu wakiwa na miaka 55 kama ilivyokuwa. Jambo la mtu kupata mshahara kwa muda wa zaidi ya miaka 30 lazima likome. Vijana wetu watafutiwe kazi. Tatu ukosefu wa usalama umechangiwa na jambo la ufisadi. Sisi wote tunafahamu vyema kuwa wakora wengi ambao wanaingia humu nchini wamepatiwa vibali katika mipaka yetu hapa Nairobi na kwingineko na maofisa wa idara kadha wa kadha ambazo zinahusiana na upeanaji vibali. Hao ndio wanasababisha ukosefu wa usalama katika nchi hii. Naibu Spika wa Muda hatuwezi kuboresha usalama katika nchi hii kama tunafikiria polisi ndio wataleta usalama. Lazima viongozi wote na wananchi wote wa Kenya wakubali vile Rais alisema jana kwamba usalama katika nchi hii ni jukumu lako na langu. Sisi ambao tuna watoto ni filimu gani ambazo tunanunulia watoto wetu waangalie? Ni zile ambazo zina bunduki ambazo watoto wanajifunza nazo? Ukienda kuwanunulia vitu vya kuchezea unawanunulia bunduki ya maji? Sisi wenyewe ndio tunaleta ukosefu wa usalama katika nchi hii na ni jukumu letu kuhakikisha hayo yanafanyika pia. Naibu Spika wa Muda ni muhimu pia tuanze kuangalia mambo ya polisi ili tuhakikisha kwamba wako na vifaa vya kutosha.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Niunga mkona Hoja hii ambayo imeletwa na Mhe. Mohamed Ali ya kufutilia mbali ada za matibabu katika hospitali za rufaa pindi mtu anapofariki. Jana kulikua na taarifa katika runinga nchini kuhusu kijana mmoja ambaye anaitwa Boniface Murage Wangeci ambaye anatoka. Nilikuwa nikisema kulikuwa na kijana mmoja ambaye aliambia mke wake aende hospitali KNH. Baadaye alishindwa kulipa Kshs56000 ambayo ilikua ada ya hospitali. Kijana huyu ambaye anatoka Eneo Bunge langu la Kajiado Kaskazini aliona ni heri aweke mtoto wake kwenye mfuko ili watoroke hospitalini. Alishikwa na kupelekwa mahakai lakini wasamaria wema walichangia na akawa huru. Hii ni kusema ya kwamba alifikiria hivi kwa sababu hakuweza kulipa ada hiyo. Hili ni jambo ambalo hutendeka kila wakati. Wabunge wote watakuambia kuwa wakienda mashinani huwa wanapata shida hizi. Kesho nikienda ofisini kwangu sitakosa mtu ambaye ataniambia ya kwamba kuna maiti hospitalini ambayo imezuiliwa kwa sababu hawawezi kulipa ada ya hospitali. Mtu akifariki amefarika. Familia yake imepoteza. Wakifuatiliwa zaidi wanaendelea kupoteza zaidi. Ni muhimu tujaribu vile tunaweza kuchangia hata ikiwa ni wakati wa Bajeti tuone vile hosipitali zinapatiwa kiwango fulani cha kuhudumia mtu akifariki. Wakati mtu amefiwa na anaendelea kuwekewa maiti hospitalini ni kama kwamba kifo hicho kinaendelea. Matatizo yale yanaendelea. Ni kama kupoteza mara mbili. Wakati mwingine inaonekana kama Serikali imechangia kwa sababu anapelekwa hospitalini na wakati mwingine hakuna dawa. Wakati mwinigine kuna migomo ya wauguzi na wagonjwa hawahudumiwi vizuri na hiyo inasababisha kifo. Wagonjwa wakifariki Serikali inafaa kungana na familia zao. Pia kuna magonjwa mengine kama saratani ama ajali za barabara ambazo hupatikana wakati watu hawatarajii. kwa hivyo ni muhimu tuangalie chanzo cha vifo hivi. Kuna mjadala unaosema kuwa wananchi wawe na kadi ya NHIF. Si watu wengi wana uwezo wa kugharamia kadi hizi. Mia tano kwa mwezi ni pesa nyingi kwa wakenya maskini na ingekua ni vizuri tujaribu juu chini tuhakikishe kwamba tumepunguza ada ya hospitali. Siyo tu miili ambayo inazuiliwa hospitalini mtu akitibiwa na hana uwezo wa kulipa ada hakuna haja aendelee kuzuiliwa hospitalini na familia yake haiwezi kulipa hiyo gharama. Mtu akifariki familia inauza shamba ama wanaitisha harambee ili kulipa ada ya hospitali. Katika eneo Bunge langu kuna kijiji kinaitwa Majengo ambako mama mmoja alipoteza mtoto wake. Huyu mama akawa na deni ya Kshs500000. Familia ikafikiria kufanya mchango na wakapata Kshs20000. Ikawa hawajafanya kitu. Ilibidi waje kwangu. Tukamwandikia social worker ili tuangalie kama hiyo maiti ingeweza kuondolewa KNH. Tulifanya hivyo kwa sababu waliandaa harambee nne na hawakuweza kupata pesa za kulipa ile ada ili wapate ule mwili. Nikimalizia ni vizuri tuangalie ile ahadi tuliwapa Wakenya ya kwamba kutakuwa na matibabu ya bure haswa kwa ngazi ya pili na tatu. Lakini unakuta matibabu ni duni na inabidi wagonjwa wahamishwe katika hospitali zingine. Wanafariki kwa sababu wamezidiwa sana. Wale ambao wanahamishiwa wana mapato ya chini na wakifariki familia zao zinashindwa kuchukua miili yao ili kuizika. Ninaunga mkono Hoja hii. Huu ni mjadala mzuri sana. Hoja hii ikipita Waheshimiwa wengi wakirudi ofisini zao na kuona watu wamepanga laini haitakuwa ni kwa sababu ya mambo ya maiti zilizozuiliwa hospitalini. Pia katika hospitali za umma kama Mama Lucy Hospital gharama iko juu sana na inafika haka kiwango cha Kshs2 milioni. Familia zinashindwa kulipa ada hizo na hawana njia nyingine. Hospitali zinazuilia miili ya wafu na familia zinawasumbua Waheshimiwa na hatuna pesa za jambo hilo. Asante. Ninaunga mkono.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Pia nami naunga mkono na kuwapongeza wale wote ambao tumewachagua siku ya leo kujiunga na viongozi wengine katika Bunge la Afrika Mashariki. Ni kweli kwamba hivi majuzi tulipokuwa katika Michezo ya Afrika Mashariki tulipata kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki ilikuwa inangoja viongozi hawa wateuliwe na naona kwamba azma yao na matarajio yao yametimika siku ya leo. Nawapongeza watu wa Mosop na nawatakia kila la heri katika msimu huu wa Krismasi. Naomba madereva nchini waendeshe magari kwa njia iliyo safi ili tupate kuchunga usalama wetu katika barabara zetu. La mwisho ni kwamba nawatakia wenzangu Wabunge nafasi nzuri na kuwaombea dua tukutane Januari ili tuendeleze kazi nzuri. Nawatakia Wakenya umoja na mambo yote ambayo yanahusiana na umoja na ujenzi wa taifa letu yawe msingi wa kujenga nchi hii. Katika uchaguzi wa viongozi wa leo vijana wawili wamechaguliwa. Hii imedhihirisha ya kwamba vijana wako na haki katika uongozi na wao wenyewe wanautafuta uongozi na kuupata. Wabunge leo wamedhihirisha ya kwamba chochote ambacho unakitaka utakipata ukitia bidii. Kwa hayo machache Naibu Spika wa Muda nakushukuru nakupongeza na kukutakia kila la heri na wale wote ambao walikuteua kutoka pale Kibwezi.
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Usalama umekuwa suala gumu. Ni suala ambalo bila vitengo vya usalama kukaa sawasawa na kubuni mipango mipya ambayo itaweza kuboresha usalama tutakuwa kati ya wale wanaopata hasara. Ninapozungumuzia haya ninatoa mfano wa kitegauchumi kule kwetu Kwale. Pwani kwa jumlatumekuwa katika hali yakutoelewa kwa nini uchumi wetu unashuka. Ukiangalia sekta ya utalii kati ya wale wanaofaidika ni sisi watu wa Pwani. Sasa hivi asilimia theini ya wale ambao walikuwa wakifanya kazi kwenye hoteli hawana kazi. Kina mama ambao walikuwa wakishona viondo na vijana ambao walikuwa na lugha tofauti ya kujieleza kupitia kwa watalii wote wamekosa kazi. Kwa hivyo ni suala ambalo mpaka sasa hatujui ni mipango gani Serikali imetuwekea ili kuhakikisha utalii umerudi jinsi ulivyokuwa zai. Pia ukiangalia tatizo lililopo ni rasilimali zetu za Pwani kushuka bei. Ukiangalia nyumba ambazo watu walikuwa wakilipa Kshs.30000 ili waishi kwa sasa hata ukiuliza Kshs.5000 huwezi kupata. Usalama umechangia watu wa Pwani kutofaidika kiuchumi. Vile vile ukiangalia usalama sasa hivi nchi nzima kuna matatizo ya usalama. Kwa mfano juzi watu waliuliwa kule dera. Pwani kumekuwa na suala hili kwa muda mrefu. Viongozi wetu wakidini wamekuwa wakiuawa mmoja mmoja bila sisi viongozi kuletewa ripoti ya sababu za viongozi hao kuuliwa. Hadi leo hatujapata sababu wala wale waliohusika katika mipango hiyo. Hatujaambiwa kuwa wameshikwa. Ni suala ambalo limesababishwa na mambo mengi. Mojawapo ya sababu zilozofanya usalama kudorora ni ajira kama vile alivyotanguliza Rais katika Ripoti yake. Suala la ajira ni suala ambalo lina changamoto kubwa. Sisi wananchi wa Pwani tumelia na kuzungumza kuhusu sehemu ambayo ilikuwa ikiwasaidia vijana wetu kupata ajira. Hizi ni sehemu kama Halmashuhuri ya Bandari ya Mombasa (KPA). Shirika hili ni la awali kabla uongozi huu haujaingia. Ni shirika ambalo lilikuwa linapeana kazi kwa vijana. Kazi hizo zilikuwa zikiwasaidia kuwapa mapato na chakula katika maisha yao. Lakini kwa sasa hivi miaka karibu saba imepita hakujaajiriwa vijana. Hili ni suala ambalo tumelizungumzia sana lakini mpaka leo hatujapata suluhusho. Ndiposa sisi viongozi wa Pwani tunasema hizi Halmashauri zirejeshwe kwa kaunti ili tuziendeshe wenyewe na zitufaidishe kama wakazi wa sehemu hizo. Katika sehemu ya mpaka niko na changamoto kubwa sana na hii changamoto nimeizungumzia muda mrefu. Sisi hatuna vifaa kama sehemu ya Lungalunga. Washikadao wa usalama na wao vile vile wanashindwa kuwafikia wakubwa wao. Hatuna magari hadi wakati huu na ukiangalia maafisa wetu ni wachache sana. Wale wanaofanya nchi yetu kutopata usalama wanapitia kwa ile mipaka na sisi kama viongozi tumelizungumzia jambo hili sana. Ni jambo la kuhuzunisha kwamba hadi wakati huu hatujaona hatua ikichukuliwa kuhusu jambo hili.
Asante sana Naibu Spika was Bunge. Nasimama kuunga mkono Hoja hii na kumpongeza mhe. Njenga kwa kuileta Hoja hii. Hii ni Hoja nzuri. Ni vizuri tuondoe vyombo ambavyo vinatumika kuweka pombe ili watoto wetu na watu wengine wasifikiwe navyo. Inafaa tuchunguze kama tumeipa halmashauri ya NACADA pesa za kutosha za kutekeleza majukumu yake. Aidha sharti tuchunguze sheria ya pombe humu nchini ili tujue kama tunatastahili kuibadilisha. Muhimu ni kuhakikisha kwamba majukumu ya NACADA ya kushughulikia zile shida zinazotokana na ulevi wa pombe na madawa mengine yametimizwa. Juzi wakati tulikutana na mwenyekiti wa hiyo halmashauri alilia akisema kwamba bajeti yake ni ndogo na kwa hivyo kuna mambo mengi ambayo hawezi kufanya. Tuangalie vile kampuni za soda kama vile Coca Cola huwa zinatumia chupa. Huwa zinarudia matumizi ya chupa. Labda tutapata mfano mzuri kuhusu kile ambacho tunafaa tufanye tunapozidiwa na chupa za pombe. Kampuni ya East African Breweries vile vile ina matumizi mazuri ya chupa za pombe. Sioni kama hili ni jambo gumu lakini huenda Hoja hii pekee isisaidie.Ni muhimu tubadilishe sheria kwa kuweka hatua za kinidhamu na kuhakikisha kuwa watu wametii sheria hiyo. Ni kweli kuwa NACADA haijaweza kufikia kila sehemu ya nchi. Kwa hivyo mambo ya ulevi na upikaji wa pombe haramu bado unaendelea. Watu wengi siku hizi wanaokota chupa za kuweka pombe. Wanaweka chochote ambacho wanataka hata kama ni chang'aa ambayo imepikwa kando ya mto katika njia chafu. Wengine wao huongeza kemikali kwenye pombe hiyo. Wateja hudanganywa kuwa wanachonunua ni pombe ambayo wamezoea. Kule River Road na eneo la Gikomba kunazo nyumba ambazo hutumika kuweke kemikali katika chupa za pombe. Nakubaliana na mhe. Njenga kuwa hatua inastahili kuchukuliwa kwa watu kama hao. Nitashirikiana naye na nitauunga mkono Mswada utakaoletwa wa kusaidia hali hii mbaya. Hii ni Hoja nzuri na tunaomba Serikali ichukue hatua. Sisi kama watunga sheria twastahili kupandisha hii Hoja hadhi ili iwe Mswada. Tukifanya hivyo tutalishughulikia jambo hili vema. Ukiongea na wataalamu katika hii sekta ya pombe watakuambia kwamba hii nchi inapoteza pesa nyingi sana kwa magonjwa yale ambayo inatubidi kutibu kwa sababu ya ulevi. Shule nyingi zinakuwa na migomo kwa sababu ya wanafunzi kunywa pombe. Walimu na wataalamu wengine humu nchini wameathirika kwa ajili ya pombe haramu. Hii imeathiri uchumi wa nchi yetu. Ni ombi langu kuwa huo Mswada uletwe hapa haraka iwezekanavyo. Ningemsihi mhe. Njenga na wahusika wengine waangalie zile sheria zinazohusiana na suala la pombe. Ningependa mhe. Njenga apanue hii Hoja yake ili iweze kubadilisha sheria hizo zote ndiposa tuweze kushughulikia yale ambayo yamelengwa na hii Hoja. Ninaunga mkono.
Asante sana Naibu Spika. Kulingana na Standing Orders za Bunge hili ningeomba kwa sababu.
Asante sana Naibu Spika. Naomba kuendeleza Hoja ifuatayo: KWAMBA tukitambua kuwa Ibara ya 43 ya Katiba imebainisha kuwa kila mtu ana haki ya kupata kiwango bora zaidi cha afya kinachojumuisha haki ya kupata matunzo ya kiafya na kutonyimwa matibabu ya dharura; aidha ikifahamika kwamba gharama za matunzo ya kitabibu katika taasisi za kiafya za kibinafsi zingali ghali mno hivyo kuwalazimu Wakenya wengi kupendelea kusaka huduma hizo kwa hospitali za umma; tukizingatia kwambalicha ya bei nafuu ya matibabu katika hospitali za umma ikilinganishwa na hospitali za kibinafsi bado Wakenya wengi hawamudu na hivyo basi kutumbukia kwenye madeni ufukara na dhiki wanaposhindwa kulipa malimbikizi ya gharama za matibabu yao na ya wapendwa wao; Bunge hili linahimiza Serikali ya Kitaifa kufutilia mbali gharama zote za matibabu ya wagonjwa wote wanaofariki wakipokea matibabu katika hospitali za umma na za rufaa. Nitaanza mjadala wangu kwa kulitaka Bunge hili kuweza kutunga sheria ya kufutilia mbali ada dhidi ya maiti. Hii ni kwa sababu tunajua wazi ya kwamba huwezi dai maiti. Kwa nini nasema tuweze kufutilia mbali ada hizi? Nina sababu zangu ambazo niliweza kupata baada ya kuzunguka mashinani na kuzungumza na wananchi wapendwa wa Jamhuri ya Kenya. Waliweza kunipatia malalamiko yao kuhusiana na maiti kuzuiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti. Sababu za vifo kwanza tunasema kila nafsi itaonja mauti kwa sababu ni Mwenyezi Mungu hupeana na pia ni yeye huchukua. Lakini kuna kuonja maiti kwa sababu ya udhalimu wa serikali iliyo mamlakani ambayo haitaki kuangalia maslahi ya mwananchi wa kawaida. Sababu ya kwanza inayosababisha vifo katika hospitali za umma humu nchini ni usimamizi mbovu wa visa vya maradhi. Kwa mfano mwaka uliopita niliweza kuleta mjadala katika Bunge hili nikiitaka Serikali iweze kujenga hospitali moja ya rufaa katika kaunti zote 47 humu nchini. Tunaposema visa vya maradhi vinatokana na usimami mbovu utaona maskini ambao ni asilimia kubwa nchini Kenya wanapokuwa wagonjwa wanakimbilia mambo ya ajabu ajabu. Kwa mfano maskini akiwa mgonjwa na hawezi kupata pesa za kukimbia hospitalini yeye atakimbia kwa waganga ajaribu kugangwa kule ili apate matibabu kwa sababu hana pesa za kwenda hospitalini. Pili madaktari wa kienyeji - tunawaita madaktari miti shamba - asilimia kubwa inaamini ya kwamba wanaweza kupambana na visa mbali mbali vya kiafia. Tatu kuna madaktari gushi. Tunaona katika vyombo vya habari na kushuhudia ya kwamba kuna madaktari gushi ambao hawajasomea taaluma hiyo na wanaenda mitaani na kufungua kliniki ovyo ovyo na kutibu watu bila ya leseni inayotakikana. Lingine ni kwamba maskini huashiria kujitibu maskini labda ana saratani na hajui. Lakini anaona dawa yake ya kipekee ya kupona ni kununua tembe ya Panadol ajigange polepole nyumbani kwa sababu hana nguvu za kufikia hospitali. Mwisho nyingine nitazungumzia ni viongozi wa dini. Siku hizi tumekuwa na viongozi ambao badala ya kuhubiri neno wanahubiri meno. Kazi yao sasa ni kudaganya wananchi na kuwapa ii ya kwamba wanaweza watibu na hivyo basi kuwachezea. Ukosefu wa taaluma ndiyo umetuletea matatizo haya yote. Ndiyo unaosababisha maafa mengi katika hospitali na uhaba wa vifaa vya matibabu. Mwaka uliyopita niliweza kusimama ndani ya Bunge hili na kusema maswala mengi kuhusiana na madaktari magonjwa na vile vile uhaba mkubwa wa madaktari nchini Kenya. Pia nilisimama katika Bunge hili na kusema ya kwamba saratani ambayo ni ya tatu nchini Kenya kusababisha vifo hadi wa leo hatujafikiria kuweza kupambana nayo. Hii ni kwa sababu sisi tuna madaktari 23 wa saratani Kenya nzima kwa Wakenya milioni 45. Kila siku katika kila mwaka tunapata visa 38 vya saratani. Upasuaji ni jambo lingine ambalo nilizungumzia. Tuna madaktari 18 wa upasuaji ambao hawawezi kujimudu. Madaktari wa figo ni 16. Hatuna maabara. Ikiwa leo mtu ni mgonjwa na hakuna maabara ya figo inakuwa matatizo. Huyo mtu anafariki kwa sababu Serikali imeshindwa kusaidia wananchi wa Jamhuri ya Kenya kwa kuekeza katika afya. Juzi nimeona kuna mgomo wa nesi. Wamesema kwamba hawalipwi vizuri na wataendelea kugoma. Mimi nawaunga mkono. Endeleeni kugoma mpaka siku ile mtaheshimiwa na muweze kuangaliwa ili Wakenya waweze kuhudumiwa. Tangu hao esi waanze kugoma watu wengi wamefariki hospitalini. Hii si makosa ya mwanachi wa kawaida. Ni makosa ya Serikali. Madaktari Kenya nzima ni 11000 kwa Wakenya milioni 45.
Asante sana Naibu Spika. Ninasimama kuunga mkono mjadala huu na kumpongeza mhe. Sakaja. Ni matakwa ya Wakenya na sisi viongozi kuona kwamba vijana wetu na akina mama wamepata uwezo wa kujiendeleza kimaisha. Lakini nikiunga mkono Mswada huu kuna vikwazo ambavyo ni lazima tuvitilie maanani. Kwanza ni kuhusu kusajili kampuni ambako kunahitajika pesa nyingi sana. Tukiangalia vijana na akina mama hawajaanza kufanya kazi hizo pesa watatoa wapi? Naibu Spika tumejitolea sisi viongozi tuwafanyie usajilishaji wa kampuni vijana na akina mama lakini bado kuna vikwazo vingine. Kwa mfano kwenye shirika letu la ujenzi; National Construction Authority ukiaangalia kuna vikwazo vingi. Kuna malipo ya Kshs10000 ambayo inatozwa. Je hawa vijana ikiwa hawajafanya hata kazi hiyo watatoa pesa wapi? Kwa hivyo ninapendekeza kwamba yale mashirika yanayohusika ya Serikali yafikirie kwanza kuyaondoa hayo malipo kwa miaka miwili ili hawa vijana na akina mama wajisajilishe. Baada ya miaka miwili wataweza kulipa kwa sababu watakuwa na pesa. Kama si hivyo vijana na akina mama hawatazipata hizi kazi hata kidogo. Mhe. Naibu Spika kuna kile kiwango kingine ambacho ni cha fomu ya CR12. Nacho pia kinahitaji malipo ya juu. Pia tunapendekeza malipo hayo yaondolewe kwa miaka miwili. Baadaye wataweza kuanza kulipia sababu bila kufanya hivyo hizi kazi zote hawatazipata. Wanahitajika wawe na vyeti lakini hawana kwa sababu hawawezi kuvilipia. Kwa hayo machache ninaunga mkono Mswada huu. Asante sana.
Asante sana Naibu Spika. Ninaunga mkono wenzangu kuhusu hii Ripoti. Tungezungumzia kitu ambacho kinaweza kuwasaidia Wakenya kuliko kuongea kuhusu kitu ambacho hakiwezi kusaidia Mkenya. Naibu Spika ningezungumza kuhusu usalama ambalo ni jambo tunaweza kulitafuta katika Kenya yetu kwa njia yoyote ile. Hii ni kwa sababu tumepoteza wananchi katika kila pembe ya nchi. Kile kinachonishangaza mimi Leshoomo ni mambo ya AlShabaab . Ni nani anitwa Al Shabaab na ana sura gani? Ninauliza swali hili kwa sababu hajulikani. Kama kuna wale wanafahamu Al Shabaab ni vizuri wajitokeze watuambie sura ya AlShabaab ni hii ili Wakenya wajue. Mtu yeyote akibeba bunduki anaitwa Al Shabaab . Ninasema hivyo kwa sababu nilikuwa katika kamati ya usalama katika Bunge la Kumi watoto wetu walichukuliwa na kwenda kufunzwa Tulitoka hapa tukaelekea Voi na tukapata watoto zaidi ya 600 wanafunzwa pale. Siku hiyo walitoka watoto kama Tafadhali nipe nafasi. Naibu Spika nisaidie. Nafikiri ninaongea jambo muhimu na tuelewe ni kitu gani kinasumbua Kenya yetu. Tulienda na tukatoa watoto karibu 300 na wote ni Wakenya. Wote wako na vitambulisho vya Kenya na walikuwa wanafunzwa huko Voi. Kama ni hao ndio wamekuja kuwa Al Shabaab ni muhimu tutafute njia ya kumaliza shida hii. Naibu Spika kuhusu mambo ya Westgate ninashukuru hao watu waliofanya upelelezi. Walipeana Ripoti yao. Zaidi ya hayo kila mtu hapa ni mupelelezi. Hata huyo ambaye anatembea bila viatu kwa barabara ana umuhimu. Wale watu ambao wanaitwa majasusi hawapati eno kutoka mbinguni ama chini. Wanapata eno kutoka wale masikini ambao wanatembea kwa barabara. Ni hao ndio wanapeana hizo ripoti. Tungesema kama viongozi kwamba tutachukua njia gani ndio hii ripoti ijulikane na ifanyike kwa njia inayotakikana? Nilisema mambo ya kaunti yangu ya Baragoi hapa. Watu arobaini walikufa. Waliuawa na Al Shabaab? Kwa hivyo nasema tutafute njia ya kumaliza usalama katika Kenya yetu. Tukiongea mambo ya usalama tusiiweke kama mashindano. Tujue tutamaliza namna gani hii mambo ya usalama ili tusipoteze Mkenya tena kwa sababu ya mtu mungine. Naibu Spika yangu ni hayo na ningesema sisi viongozi tusiweke mambo ya usalama katika Kenya kama mashindano siasa ama kichama. Tushikane tujue tutaimaliza namna gani kwa sababu tunaumia. Tusipendeze fulani lakini tutajaribu tuweke njia ya kusaidia Mkenya. Naunga mkono hii Ripoti na Kamati warudi waitengeneze.
Asante sana Naibu Spika. Ningependa kuunga mkono swala hii. Kwa kweli mambo ya wanyama na wananchi imekuwa kali kwa muda mrefu. Bado haijajulikana sababu ya wanyama wa msituni kuua watu na bado kuna shida ya malipo. Kule ninakotoka watu wanaoishi karibu na wanyama wanateseka sana haswa wakati wa ukame. Wakati huo utapata wanyama wa msituni wanang'ang'ania maji ng'ombe na wanaua watu na bado walioathirika hawajalipwa hadi sasa. Ningeomba ijulikane kuwa kuna shida katika Wizara hiyo na Serikali inafaa kutatua shida hiyo.
Asante sana Naibu wa Spika kwa kunipatia hii nafasi ili name nichangie Hoja hii. Nashukuru mheshimiwa Musimba kwa kunipatia hii nafasi ijapokuwa napinga hii Hoja. Kwa ukweli sisi sote ni viongozi. Ni sisi tulimchagua huyu Spika. Sisi wenyewe inatupasa tujiheshimu kwanza kabla ya kwanza kumtaja Spika. Kufuatana na yale ambayo tumekuwa tukiona sidhani tumeonyesha Wakenya heshima katika Bunge hili. Kile ambacho tumeonyesha ni kibaya. Tumejikosesha adabu sana. Tumeona wenzetu wakichukuwa chupa na kumwagia Naibu Spika maji usoni mwake. Kwa hivyo sisi kama viongozi tujiheshimu kwa vile tumechaguliwa na wananchi ambao wanatuheshimu. Kuhusu hii Hoja Mheshimiwa Musimba angechukua nafasi ya kukaa chini na kupendekeza Kamukunji ili tuwasiliane na tujadiliane kuhusu makosa tunayofanya humu Bungeni. Ukweli ni kwamba sisi tumefanya makosa makubwa sana na inabidi tuyarekebishe. Mimi ninapinga hii Hoja. Ninaopose hiyo kitu.
Asante sana ndugu Spika kwa kunipa fursa nichangie jambo hili kwa dakika mbili tu.
Asante sana. Jambo lingine ni kwamba kaunti wamesema watachimba yale madimbwi ya maji lakini mpaka sasa kuna madimbwi mengi kama huko Kaunti ya Kwale ambayo hayajachimbwa. Unajua mchanga huo unarudi ndani na hawajakuja kuutoa katika miaka minne na wala hawajachimba lile dimbwi likawa linaweza kubeba maji mengi kusaidia watu. Jambo lingine nataka kutumia hii nafasi kuwaeleza wananchi kuwa huu ndio wakati wa kujua kiongozi anayekujali maanake hakuna kiongozi mzuri ambaye atakubali watu wake wafe rasilmali zao zife ama ziharibike na watu waishi kwa dhiki kama hiyo ya kuwa hakuna chakula na hivi sasa pia hakuna maji ya kunywa. Nataka kuomba Serikali kuu na ile ya kaunti kama wamekuwa wamezembea kazini
Asante sana. Kama anataka nizungumzie pesa ya ufisadi nitampatia. Shilingi bilioni moja nukta nane iliweza kutolewa kununua feri mpya mbili. Hizo pesa hatujui zimeenda wapi. Ferry mpya hatujapata mpaka sasa. Shilingi milioni 78 zilitolewa kwa Kenya Ferry Services iweze kuweka camera za CCTV ili wale ambao wanakaa mahala na kuangalia matukio yote yanayotokea wakiona shida yeyote wanaweza kuwafikia wananchi kwa haraka. Hizi ndizo pesa ninauliza ziko wapi na zinafanya nini? Nilikuwa ninazungumzia kujiuzulu au kuwachishwa kazi kwa wahusika wote wakuu kama nilivyokuwa nimewataja hapo awali. Pia nitazungumzia masuala ya kazi. Vijana wengi wa Pwani hawapewi kazi. Inapofika ni wakati wa kuandika wanajeshi wa maji vijana wengi walio na ujuzi hawapewi nafasi. Inakuwa ni kupeana kazi kwa kujuana. Bahari ina wenyewe na wenye bahari wanafaa wapewe kazi hii. Pia ningependa kuzungumzia katika siku za usoni waanze kufanya mikakati ya kuhakikisha kwamba wameweka kivukio cha daraja ili kuhepusha majanga kama haya. Mhe. Naibu Spika wa Muda ninasema kwamba leo ninaomba Mariam Kighenda na Ada Mutheu watusamehe kwa sababu tumefeli kama nchi na tutarekebisha tuweze kuhakikisha kwamba matukio kama haya hayatatokea tena katika siku za usoni. Mungu alaze mioyo yao mahali pema panapo lazwa wema. Asante.
Asante sana. Kuna lugha ambayo mmoja alitumia kwamba key population. Miaka minane iliyopita nilibahatika kwa sababu ya kazi ambayo nilikuwa naifanya dhidi ya wanaotumia madawa ya kulevya na nikapata safari ya kwenda nchi ya India. Nilipofika pale kati ya wale waliofika huko ni watu wa NACADA. Nakumbuka nikiwapa kauli yangu. Tulipofika pale key population iliozungumziwa tuliona misago na maghanithi katika sehemu ya India. Kwa hivyo naomba tusifikirie kamwe kuleta watu ambao nia na madhumuni yao ni kuzungumza mambo ambayo ni ya kushusha hadhi. Watu kutoka nje ya nchi hii kuja kuzungumza mambo ya kipuuzi yenye ni kinyume na sheria ya Kenya na kinyume ya Katiba ya Kenya na muhimu zaidi mambo ambayo ni kinyume na maadili yetu tunayoamini kama jamii na uaminifu wetu kama nchi na wananchi ni dhambi kwa Mwenyezi Mungu. Ahsante sana Mhe. Spika.
Asante sana. Kwanza ningependa kumpongeza Mhe. Ali kwa sababu Hoja yake ni nzuri. Hoja hii itafanya sisi wengine ambao tunatoka sehemu za kaskazini magharibi mwa Kenya pia tunufaike kwa kupata hospitali ya Level 6. Itakuwa vizuri kama Hoja hii baada ya kupitishwa ifuatiliwe ili ifanye kazi mara moja. Kuna sehemu zilipata hospitali za viwango vingine kama Level 4 au Level 5 na hazijawahi kupatiwa huduma nzuri. Kuziorodhesha hospitali hizo katika viwango hivyo haikuweza kuzisaidia. Muda wangu umeisha. Ahsante.
Asante sana. Mimi pia nataka kuchukua fursa hii kumushukuru dada yangu Mheshimiwa Joyce Lay kwa ajili ya Hoja hii. Tunapotafi Katiba yetu katika lugha ya Kiswahili itatupa nafasi nzuri ya kuelimisha watu wetu hasa kuhusu mambo ya ndoa na jinsia katika nchi yetu ya Kenya. Vile wenzangu wamesema hata mkiwaona vijana wetu wanaoendesha pikipiki ama bodaboda unajua hawaelewi Katiba yetu. Itakuwa ni vyema kuona kwamba Katiba yetu imetafiwa katika lugha ya Kiswahili na hiyo itatupa nafasi nzuri sana. Ninamshukuru dada yangu Mheshimiwa Joyce Lay kwa kuleta Hoja kama hii katika Bunge. Ahsante sana.
Asante sana. Najua rafiki yangu anapenda sana kutetateta. Ameteta kutoka asubuhi mpaka saa hii hajanyamaza. Kwa hivyo tutaendelea tu. Tumemzoea lakini hata mimi utanizoea na hiki Kiswahili changu cha kule Nyandarua. Najua naongea vilivyo. Hata rafiki yangu Mhe. Mohamed Ali ananiyoshea kidole kwa sababu naongea lugha sanifu kabisa. Naomba kuunga mkono Hoja hii. Lazima hospitali zetu ziache eno haya ya kufungia miili mwaka mmoja au miezi kadhaa kwa sababu ada hazijalipwa. Kama Mheshimiwa alivyosema madaktari wetu watakuwa wakiwatibu watu haraka kwa sababu wasipowatibu na mtu afe katika hospitali yake hatalipwa pesa yake kama daktari. Naunga mkono pendekezo hilo kwa sababu sasa madaktari watakuwa wanatia makini kutibu watu kwa sababu watu wengi wanakuwa misdiagnosed. Hiyo sijui ni nini kwa Kiswahili. Wanakuwa misdiagnosed na wanatibiwa magonjwa hawako nayo kama kifua kikuu au saratani. Hata saratani ingeitwa shetani kwa sababu huo ndio ugonjwa ambao unamaliza watu nchini. Kama kwetu Nyandarua kila siku unasikia kuna mtu anaugua ugonjwa wa saratani. Watoto wengi wako hospitali ya Kenyatta. Sio eti unashika tu wazee. Siku hizi unashika hata watoto wa miezi miwili au tisa. Juzi tulizika mmoja wa miaka tisa ambaye ugonjwa huu ulimshika mdomoni. Lazima eno yote yaangaliwe. Watu wengi wamezuiliwa katika vyumba vya kuhifadhi maiti. Serikali lazima kutoka kesho iwaachilie. Asante sana. Naunga mkono Hoja hii.
Asante sana. Nasema kwamba ni lazima wanafunzi wawe na stakabadhi hii ndio waweze kuendelea na mitihani yao katika zile shule zetu hapa nchini. Vilevile wakati unataka stakabadhi ya kusafiri ni lazima upate stakabadhi hii kwanza hata kabla hujapeana hiki kitambulisho ambacho pia ni stakabadhi muhimu katika Taifa letu la Kenya. Ukifika katika ofisi zile kwanza utaulizwa utoe stakabadhi hii ya birth certificate. Nataka niseme imekuwa ni changamoto kwa sababu si wazazi wote ambao wanajifungua ama wanazalia katika hospitali zetu ambapo watapata kile cheti kiitwacho birth notification. Wazazi wengi ama akina mama wengi wanaweza kujifungua kupitia wakunga kule yumbani ama kule nyanjani. Hivyo inakuwa changamoto kuweka zile takwimu ama mawasiliano katika zile asasi zetu muhimu ili zinukuliwe na kupata takwimu za mtoto yule ili aweze kupata stakabadhi kama hii. Nasema kwamba huu ni wakati mwafaka ambapo teknolojia imebobea. Wakati teknolojia imebobea lazima pia twende na muondoko huo huo wa kwamba hata sisi pia tumebobea katika teknolojia. Hivyo basi kuwa na ile centre ambayo tunasema ni database centre mahali ambapo mawasiliano yote ama zile takwimu zote zinazohusu stakabadhi nyeti na muhimu kama hizi zitakuwa pahali pamoja na kugatuliwa kule chini mashinani. Juzi tulifungua ile tunaita Huduma Centre mahali ambapo tunaweza kupata huduma tofauti tofauti ikiwemo stakabadhi hii tunayoizungumzia sasa. Lakini tunaona kwamba hizi Huduma Centre zimewekwa katika sehemu za mijini ama ile miji mikubwa. Pia inakuwa changamoto kwa wazazi ama Wakenya wengi kuweza kufika pale ili kupata stakabadhi kama hizi. Iwapo tutaweza kupata hizi database ambazo zitakuwa kule nyanjani katika yale maeneo ya uwakilizi katika bunge letu ama kwa Kingereza our sub-counties itakuwa ni sehemu ambayo hakuna Mkenya atakuwa na matatizo kupata stakabadhi kama hizi. Pia tumekuwa na changamoto kwa sababu utapata watu ambao sio wakenya wanataka kupata stakabadhi za Kenya kupitia njia za ufisadi. Tukiwa na hifadhi ya data kama hii mambo hayo yatachujwa ili kuhakikisha kwamba watu ambao wanapata stakabadhi hii ni walengwa wahusika na watu ambao wamezaliwa katika taifa letu la Kenya. Tukitimiza Hoja kama hii.
Asante sana. Nimejaribu kutafuta nafasi kuweka ishara ya nidhamu. Hata kama ametuchekesha namuomba atembelee Lamu hasa visiwa vya Shella na Pate ajionee warembo kisha tuone kama atasema kwamba Kenya hawajazaliwa bado. Kenya wamezaliwa. Hata sisi ukituangalia utajua kwamba wakati wetu tungekuwa nasi cabin crew nafikiri angefurahia huduma yetu. Kwa hivyo wasichana wetu Wakenya ni warembo. Hakuna nchi hapa Afrika Mashariki inatuweza kwa urembo.
Asante sanaNaibu Spika wa Muda. Mimi pia ninaunga mkono kuongezwa kwa muda kwa sababu tunawahitaji sana hawa Mawaziri. Kuna kazi nyingi ambazo tunatarajia watazifanya na kuzikamilisha baada ya kuapishwa. Watu wamezungumzia siku ya kupendana kwa umaarafu Valentine's Day .
Asante.
Asante. Jambo hili la karantini kama walivyozungumza wenzetu ndugu yetu Mhesimiwa Junet Duale na wengineo huwezi kuchukua Mkenya ambaye hana hatia yeyote na bila ya kutaka kwake na kumlazimisha kukaa katika karantini. Na baadaye unamwambia alipe Ksh2000 kwa siku. Kando na hilo tunazungumza kuwa wale ambao watakaopelekwa karantini lazima Serikali kama ilivyo katika nchi zingine zote duniani watu ambao wanaweza kukaa katika Nyumba zao waweze kukubaliwa. Hili ni jambo ambalo limezungumziwa na Wizara ya Afya na ambalo tumeweza kulijadili na Serikali za Kaunti. Hivi leo ni aibu yakuwa watu wanazuiliwa kutoka katika zile karantini kisa na sababu hamna. Mwisho Bw. Spika wa Muda.
Asante. Kama alivyosema Mheshimiwa Nakara inafaa tuwachunge vijana. Isiwe vijana wanashughulikiwa na ikifika wakati wa kufaidika wazee wanapata na vijana wanakosa. Kwa hivyo tusikose mwelekeo. Vijana pekee ndio wanapaswa kufaidika. Asante sana.
Asante. Mhe. Naibu Spika wa Muda tumechangia sana. Ningependa kuchukua nafasi hii pia kupongeza KCAA. Nimetoka hapo nje kupiga simu kwa marubani kadhaa kuwauliza kama pengine kuna shida zaidi kwa sababu mimi sijarusha ndege kwa miaka kama miwili. Wameniambia saa hii KCAA wanafanya kazi nzuri na kwamba wamefunga ukanda. Zaidi ni kwamba kutoka tupate ile safari ya kwenda Amerika wamejaribu zaidi. Sehemu nyingi wameziba mashimo. Hiyo ni kazi nzuri. Nawapongeza sana KCAA. Tukizungumzia mambo ya ndege na viwanda itakuwa si vyema watu wa Lamu wakiniangalia nikiyazungumzia hayo. Katika Kaunti ya Lamu kiwanja cha ndege ni kimoja. Kitambo ungeweza kutoka nchi za nje na uingie humu nchini kupitia Lamu. Saa hii hauwezi kwa sababu ya mambo ya usalama. Tunaomba Kamati hii izingatie jambo hili. Wacha niseme kwa kimombo ili mwenyekiti aelewe. Wakati wa nyuma Lamu ilikuwa entry and exit point. Saa hii hatuna hilo na tumeendea mambo ya kaunti. Inafaa kaunti zote 47 ziwe na viwanja vya ndege vya kimataifa. Kuna visiwa upande wa Lamu Mashariki. Katika nchi nyingine utapata kila kisiwa kina kiwanja cha ndege. Ni masikitiko kwamba Lamu tuna visiwa 11 na havina viwanja vya ndege. Wakati wa nyuma visiwa vya Pate Ndau and Kiwayu vyote vilikuwa na viwanja vya ndege. Saa hii vyote havina viwanja vya ndege. Saa hii kukitokea mgonjwa usiku na bahari ni chafu au mgonjwa akitakikana kuletwa Nairobi kwa ndege. Sehemu kama vile Maasai Mara kunawekwa mataa ili ndege zishuke kumchukuwa mgonjwa ambaye anatakikana kusafirishwa hadi Nairobi. Lamu hilo haliwezekani hata tukitaka. Ni mpaka mtu apitie bahari chafu na shida nyingi. Naomba Kamati hii izingatie mambo hayo. Haiwezekani kuwa na kisiwa ambacho kina watu zaidi ya 18000 na kiwe hakina kiwanja kidogo cha ndege ambapo ndege ndogo ndogo zinaweza kutoa mtu wakati wa dharura. Hata kuhusu usalama najua eneo la Lamu lilivyo. Itawasaidia sana watu wa Lamu kama kutakuwa na viwanja vya ndege hata huko mainland . Vitasaidia watu kusafiri na kufika kwa haraka. Kwa mfano kama mtu amechukuliwa au imetokea dharura yoyote ya usalama wataruka kwa haraka na wafike. Naomba sana hilo lifanyike. Naona mwenyekiti yuko hapa. Namuomba jambo hili alitilie mkazo. Kisiwa chochote. Hata kule Kisumu inafaa kuwe na airport moja. Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Asante. Nashangaa nikiona Mhe. akiuliza mambo haya na sisi tunaumia. Kwani anaunga mkono ulanguzi wa dawa za kulevya?
Asante. Ningependa kuchukua fursa hii kuunga mkono Mswada huu na vilevile kumpongeza pakubwa Mbunge aliyeuleta hapa kwa sababu suala la ajira ni suala nyeti. Aliyeuleta Mswada huu amelenga masuala ya akina mama wanaofanya kazi haswa wakati wanapojifungua na namna watakavyopata nafasi ya kupumzika watakapokuwa wakiwalea watoto wao. Ukweli ni kwamba Waheshimiwa wengi wanaposimama kuchangia Mswada huu wanazungumzia neno "ajira" kwa ujumla katika nchi hii. Ukweli ni kwamba ile hali ya ajira katika nchi hii ni hali ambayo inahitaji kupewa kipaumbele tunapojadili kuhusu suala hili. Mzazi anapojifungua mtoto ina maana ya kwamba mtoto yule ameanza maisha yake. Malengo ni kwamba mtoto yule atalewa na mwishowe atahitaji kazi. Tunajua vizuri namna nchi yetu ilivyo. Mheshimiwa aliyeuleta Mswada huu ametambua kwamba kuna dharura ya kuwapatia akina mama wanaofanya kazi muda wa kutosha wanapojifungua ili wajipange namna watakavyowaelekeza watoto hao. Naamini kwamba muda ambao wamepewa ni wa takribani miezi mitatu. Ningependa vilevile akina mama hao baada ya kupewa miezi hiyo mitatu kuwe na namna ambayo watakuwa wanasaidika kikamilifu katika kuliangazia suala hili la watoto. Hii ni kwa sababu utotoni mwa kila mtu ni wakati muhimu sana katika malezi. Hivi sasa vijana wengi wako katika hali ya sintofahamu; hawajitambui ama kujielewa. Vijana hao pengine wametupwa na mama zao ama hawajui wazazi wao. Siku hizi idadi ya vijana ambao hawana kazi imekuwa kubwa zaidi kwa sababu ya tatizo hili ambalo lilianza hapo awali na kwa sababu ya makosa ambayo hufanyika wakati mtoto anapozaliwa. Kwa hivyo kuna dharura katika nchi hii ya kuwepo kwa mwongozo kamili wa kujua idadi kamili ya vijana wanaozaliwa wanaoinuka wanaosoma na hata wale ambao hawana kazi. Sielewi ni kwa sababu gani nchi hii haina watu wengi. Tukiangazia idadi ya wanaoishi katika nchi hii ambao wamefikia kiwango cha kuwa na kazi zao ni takribani milioni 40 hivi lakini idadi ya wale ambao hawana kazi ni wengi sana. Hali hii pengine imesababishwa na kutokuweko kwa takwimu kamili ya kuonyesha ni vijana wapi. Ningependa kusema kwamba serikali zote za kaunti 47 ni vizuri ziwe na data ya kuonyesha ni vijana wangapi hawana kazi na wanaohitaji kazi na kiwango chao cha masomo ili nchi hii iwe na mwongozo mwema. Itakuwa vyema wakati kila jambo linaanza liwe na utaratibu. Linapoanza na makosa basi hata huko mbele mambo mengi yataenda mrama. Ni dharura kubwa kwa nchi hii kuangazia mwelekeo na mwongozo wa wananchi wake hususan vijana hapa nchini kwa sababu namna inavyoenda ni kwamba wengi wamekosa ii kabisa na nchi yao. Unapata wengine wanafanya mambo ambayo hayastahili wengine wanajiingiza katika mambo mabaya na tabia ambazo si njema katika jamii. Kwa hivyo kuna dharura kubwa hapa nchini ya kuweza kuangazia na kuwa na mipangilio kamilifu katika suala hili kwa wananchi na jamii. Kwa hayo machache naunga mkono Mswada huu. Asante.
Ashante sana Mhe. Bowen kwa fursa hii. Ningependa kuunga mkono Hoja hii kwa sababu ni Hoja ambayo imekuwa mara kwa mara katika Serikali ya Kenya tukiangalia Shirika la Kenya Power likiwa na uzembe wa kupeleka huduma zao kwa wananchi. Kulingana na mfumo wa kibiashara lazima kuwe na mashindano. Yakiwemo mashindano nina hakika yale malipo ambayo wananchi wanatakikana kulipa yatashuka. Mwezi huu wa Ramadhani sisi Waislamu tunatumia wakati wa usiku kupeleka maombi yetu kukaa vizuri na kuomba Mungu ili atusamehe makosa na dhambi zetu. Kwa hivyo ninaomba Kenya Power wapunguze visa vya kukata stima wakati wa usiku kwa sababu tuko katika harakati za kuomba Mungu wetu wakati huu wa mwezi wa Ramadhani. Vile vile tukiwa Vanga tunatumia stima kutoka Tanzania. Sasa hivi Tanzania pia wanatukatia stima. Sisi Wakenya tuko katika mpaka wa Kenya na Tanzania. Shirika la Kenya Power limeshindwa kufikisha stima kwetu ndio sababu tunatumia stima kutoka Tanzania. Kwa hivyo tunaomba shirika la Kenya Power lihakikishe kupitia kwa Rural Electrification Authority (REA) kwamba tunapata umeme. Kwa sababu ya huu mradi wa Serikali unaokuja naona kila mahali stima itasambazwa itapenya katika shule. Kwa hivyo ninaomba kwamba REA ambao wanafanya kazi nzuri wahakikishe kwamba stima inafika katika maeneo wananchi wanamoishi. Kwa hayo machache naunga mkono Hoja hii na kumshukuru mhe. Bowen.
Ashante sana Naibu Spika. Hata mimi ninaunga mkono Hoja hii kuhusu Bw. Kimemia. Kwa kweli mimi sijui ni watu gani katika Kenya tunataka! Ukiangalia ile kazi Bw. Kimemia amefanya katika nchi hii nafikiri ni mtu ambaye anastahili kupatiwa kazi hii. Badala ya kuongea mengi tungepitisha Hoja kwa sababu naona kila mtu hapa ni rafiki ya Bw. Kimemia. Yafaa tuseme kwamba tunajua kazi yake. Kwa kweli ni mtu mwenye roho safi; hata ukiwa na shida kama sisi ambao tuna shida ya usalama na umpigie simu saa tisa usiku atachakua. Ukimweleza shida zako atafanya kile wakenya wanataka. Kwa hivyo ninaonelea kwamba badala kukaa hadi saa nne au saa tano tukijadiri Hoja hii kuhusu Bw. Kimemia kila mtu ni rafiki yake hapa na wengi wanampenda na kazi yake iko sawa. Naona mhe. Ababu anacheka pale; pia kuna rafiki yangu pale anaitwa Midiwo. Ningeomba tuweke sahihi na kumaliza jambo hili. Ninaunga mkono.
Ath (Lamu East JP): Asante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Ningependa kumpongeza ndugu yetu ambaye ameleta Hoja hii Bungeni. Vile vile niwapongeze Wabunge ambao wameweza kuchangia Hoja hii. La muhimu kwanza ni lazima kufahamu kama viongozi malengo na umuhimu wa Hoja hii ni nini. Tunaweza kuzungumza na kujadili lakini mwishowe ikawa umuhimu wake usipatikane kwa jamii. Kama tunavyofahamu ulimwengu wa leo umebadilika kwa namna nyingi sana ndiposa fikira hii imefika mahali pa kwamba ni muhimu sana kwa Serikali kuhakikisha kwamba wameweza kulitekeleza jambo hili punde tu tutakapolipitisha hapa Bungeni. Leo hii mambo mengi yanavyoendeshwa ulimwenguni kwa ujumla yanatumia mitandao katika kupata zile habari ama kutuma habari zozote zinazohusiana na mambo ya kileo. Lakini kwa masikitiko makubwa katika sehemu nyingi sana katika nchi hii utapata kwamba mambo kama haya hayapatikani. Utapata sehemu nyingi sana wanatumia zile teknolojia za zai katika kuwasiliana na mambo mengi sana ama kuweza kufanya zile shughuli zao za kileo. Ukweli ni kwamba sio kwamba vijana pekee watafaidi katika Hoja hii wao tu ni miongoni mwa wale watakaofaidi sana. Lakini ni jambo litakaloinua uchumi wetu na kuendesha harakati za mambo yetu kama vile nchi nyingine zinafanya. Walimu wanahitaji kutumia huduma kama hizi katika sehemu za mashinani lakini hazipatikani. Inawabidi kusafiri kwenda sehemu nyingine ambazo kuna huduma hizi ama kugharamika pakubwa katika kuzipata huduma hizi. Ningependa kuunga mkono na kuhimiza ya kuwa lifanyiwe haraka jambo hili na litekelezwe kikamilifu. Jambo ambalo singependa lipatikane ni kwamba watashirikishwa waezekaji wa kibinafsi. Kama tutafanya hivyo basi itakuwa bado hatujasonga mbele. Leo hii waekezaji wa kibinafsi wanaweza kufanya huduma hii katika sehemu ambazo hamna lakini tunapolijadili hapa huwa tunapendekeza Serikali ichukue majukumu haya kwa sababu matatizo yale ambayo tunayahofia sasa hivi walioko mashinani hawapati huduma hizi. Hata kesho zikifika huduma hizi na ikiwa wameshirikishwa hawa waekezaji wa kibinafsi gharama zitakuwa vile vile. Kwa hivyo ningependa Serikali iingilie kikamilifu na kuhakikisha wametekeleza huduma hii kwa Wakenya wengi. Asante.
Bi Naibu Mwenyekiti wa Muda kuna umuhimu mawaziri waruhusiwe na wapatiwe nafasi ya kupeperusha bendera katika haki zao za kufanya kazi. Hii ni kwa sababu Baraza la Mawaziri ni chombo chenye umuhimu nchini. Vile vile ikiwa mabalozi walioko chini ya mawaziri wataruhusiwa kupeperusha bendera basi kuna umuhimu mawaziri pia wapewe nafasi ya kupeperusha bendera ya nchi.
Bi Naibu Mwenyekiti wa Muda nasimama kupinga haya mabadiliko. Ikiwa tumewanyima magavana ambao wamechaguliwa na wananchi kwa kura hatuwezi kumpatia mtu ambaye ameteuliwa. Kwa hivyo napinga.
Bi Naibu Spika ningependa kumshukuru Mungu kwa kunijalia kuwa mwakilishi wa watu wa Bura. Nachukua nafasi niseme kongole kwako na pia kwa Spika wa Bunge Rais na Naibu wa Rais mliochaguliwa katika nyadhifa mpya katika nchi ya Kenya. Nikizungumzia juu ya Hotuba ya Rais inaotoa mwangaza juu ya sera ya Serikali yake Rais amegusia swala la ufisadi na uwazi. Kama Bunge tuna furaha kumuunga mkono kumsaidia kupambana na ufisadi. Swali ni kwamba vipi tutafaulu katika hivi vita? Mashirika ambayo si ya kiserikali na ya kiserikali yameungana mkono kudhalilisha waajibu wa Bunge katika nchi ya Kenya. Iwapo Bunge haliwezi kufanya kazi yake ya kuchunguza rasilimali ya Serikali inavyotumika vipi tutapambana na kushinda ufisadi? Hili ni swali kwake. Ninafuraha kwamba Rais amezungumzia ugatuzi. Ninajua kuna dukuduku juu ya magavana wanaotaka bendera ofisi kubwa na pesa nyingi. Lakini watu wetu wako katika hali mbaya. Kumenyesha mvua ya gharika na magavana wetu hawana mikakati sera sheria ama maono juu ya vipi wataendeleza kazi na kuboresha hali ya maisha ya watu wetu. Kila kukicha ni bendera na wanataka ofisi kubwa kubwa. Tunazungumzia karakana kwa sababu katika Hotuba ya Rais alisema kwamba ataboresha karakana. Kati ya Bura na Garissa zaidi ya magari 100 yamelala siku 20 njiani. Kama kweli mtaboresha karakana halahala boresheni hali ya barabara inayounganisha Mombasa na Garissa. Nina furaha wakati Rais anazungumzia nafasi ya kazi kwa vijana. Kwa nini nina furaha? Asilimia 70 ya watoto wa Kenya licha ya kufanya vizuri katika vyuo vikuu ajira ndilo tatizo kubwa. Mazungumzo yale yananifurahisha sana. Namwambia Rais kwamba haya mazungumzo yakifika ofisini utekelezaji utakuwa ni tatizo kubwa. Nitamuunga mkono lakini atupe hakikisho. Katika Hotuba yake Rais hakuzungumza juu ya janga linaloadhiri Wakenya; hili janga la kiasili likiwemo mvua ya gharika inayoendelea sasa. Ni lazima Serikali iwe na mikakati maalum. Ni lazima Serikali iwe na rasilimali maalum. Ni lazima Serikali iwe na mfuko ambao kutakapo tokea dharura itakimbia mara moja kuokoa watu. Angalia hali ya Mororo leo katika sehemu ninayowakilisha. Angalia hali ya Madogo na Bilbil. Ukame umefagia miji watu hawana chakula na makao. Ukienda ofisini unaambiwa rudi siku nyingine maana wanalishughilikia tatizo lako. Hio siku itafika lini? Rais pia alizungumzia kawi. Tangu Mungu aumbe dunia na akamleta mtume Adam mji wa Bangal haujapata stima. Nina furaha kusikia kutaletwa kawi ya solar lakini tangu Mungu kuumba dunia mji wa Bangal haujakuwa na umeme hata siku moja. Hii ni habari nataka kumpa Rais wangu atembee Bangal ajionee mwenyewe kwamba tangu Mungu aumbe dunia hata siku moja stima haijawaka kule. Nikimaliza nina furaha kwamba Rais aligusia swala la elimu. Ningemwomba asome Omingo Report ya 1973 inayosema kuhusu watoto wa wafugaji. Ningemwomba asome KoechReport ya 1990s inayosema kuhusu watoto wa wafugaji. Ningemwomba asome Report ya UNDP. Mtoto wa mfugaji hali yake ya elimu
Bi Naibu Spika wa Muda ninamalizia. Ninaunga mkono iwapo Hoja hii itakuwa na marekebisho yaliyopendekezwa na Daktari Mhe. Nyikal. Itakuwa Hoja itakayotimiza malengo yetu. Tunapozungumzia hii Hoja lazima tujue tutatumia lugha aina gani itakayotuwezesha kutekeleza mapendekezo ambayo tumeyazungumzia. Ninaunga Mkono.
Bi Naibu Spika wa Muda ningependa kuchukua nafasi hii kuunga mkono Mswada huu wa utawala wa mikoa. Tunahitaji utawala wa mikoa ili tuweze kuhakikisha kwamba kuna usalama wa kutosha mashinani. Vile vile tunahitaji utawala kama huu kwa sababu majirani wetu kwa mfano huko Uganda wana watu wanaoitwa ResidentCommissioners. Kuna watu kama hawa wa utawala katika Zimbabwe. Ufaransa kuna utaratibu ambao unaitwa prefecture. Kwa hivyo ni vizuri sisi kama viongozi wa nchi hii kuunga mkono huu Mswada. Sisi sote tunajua kwamba machifu wanafanya kazi nzuri kuhakikisha kwamba kuna usalama katika vijiji vyote nchini. Wanafanya kazi ambazo polisi wa kawaida hawawezi kufanya. Kuna mizozo ambayo hutokea mashinani ambayo hutatuliwa na machifu na aibu wao. Kwa vile Waziri yuko hapa na kwa sababu mimi pia zai nilifanya kazi katika utawala wa mikoa ningependa kutaja vifaa vinavyohitajika. Kwa mfano machifu wanahitaji pikipiki. Mimi mwenyewe kupitia CDF nilipatiana pikipiki kumi katika eneo langu. Ikiwa inawezekana ningependa kila chifu na mdogo wa kata wapatiwe pikipiki ili waweze kutekeleza kazi yao inavyotakikana. Kwa hayo machache naunga mkono kwa nguvu zote.
Bi. Mwenyekiti pia mimi ninasimama kuunga mkono. Liseni ya utafiti ni mojawapo ya njia ambazo zitaleta mapato. Ijapokuwa tutakuwa tukitegemea madini pia tutapata mapato kutokana na kuuza leseni ambazo zitasimamia kazi kutoka mwanzo. Ninaunga mkono.
Bi. Naibu Spika wa Muda ahsante sana kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia suala la vitambulisho. Kwanza kabisa ningependa kuchukua fursa hii kusema kwamba ninaunga mkono suala hili. Pili ningependa kupeana shukrani kwa mhe. Diriye Mohamed ambaye ameileta Hoja hii Bungeni. Ukweli ni kwamba suala la vitambulisho ni muhimu. Kama Hoja inavyosema usipokuwa na kitambulisho kuna mambo mengi ambayo huwezi kuyafanya. Kwa hivyo kuna haja ya Serikali kuhakikisha kwamba vitambulisho vimewafikia watu wote kote nchini. Kuna haja ya kuhakikisha kwamba wasajili wamepelekwa katika sehemu ambako usajili unafaa kufanyika. Kuna baadhi ya maeneo humu nchini ambako mpaka sasa hakuna wasajili. Ni muhimu wasajili wapelekwe huko mara moja ili waweze kuzingatia suala hili na Wakenya wapate vitambulisho. Tunapopeleka wasajili katika sehemu hizo ni lazima pia tukumbuke kwamba sehemu nyingi humu nchini hazina magari. Mara nyingi tunaona watu wanafuatilia vitambulisho kutoka makao makuu ya wilaya. Kwa hivyo Serikali inapaswa kujizatiti vilivyo na kuhakisha kwamba imepeana magari na mafuta ya kutosha ili kuwawezesha wasajili kusafiri hadi kwenye kata ndogo ndipo wananchi waweze kupata vitambulisho. Bi. Naibu Spika wa Muda tukiendelea kuzungumzia suala la vitambulisho ni lazima tukumbuke kwamba kuna kamati ambazo huteuliwa kuchuja na kuona iwapo watu fulani wanastahili kupewa vitambulisho. Ni maoni yangu kwamba kamati hizo zinafaa kukaguliwa kwa kina. Inafaa wanakamati wenyewe wawe wamechujwa kuhakikisha kwamba wanaweza kuchuja wenzao kwa uadilifu. Katika sehemu ninayowakilisha Bungeni ya Kaloleni kuna wananchi wanaoishi sehemu kama vile Mariakani ambao mara kwa mara hubaguliwa vitambulisho vinapotolewa. Sababu za wao kubaguliwa si za msingi. Hili ni jambo ambalo hata sisi tukiwa viongozi tunashindwa kulielewa. Ni muhimu tukubali kwamba wale wanaofanya kazi ya kuwakagua na kuwachuja wengine pia ni binadamu. Kwa hivyo wanakuwa na vikao na wasajili na wana mahitaji kama binadamu wengine. Kuna umuhimu wa kuzingatia maslahi ya watu hao ndipo wanapokuwa na vikao pia waweze kupata kiinua mgongo. Kitambulisho ni stakabadhi muhimu sana. Tunazungumzia ugatuzi na sielewi ni kwa nini bado Wakenya waendelee kusafiri mwendo mrefu kufuatilia vitambulisho vyao. Inafaa Serikali iweke mikakati ya kuhakikisha kwamba watu wanafuatwa kusajiliwa mashinani ili kila mtu aweze kupata kitambulisho chake katika shule ya msingi ama katika zahanati. Tukifanya hivyo tutarahisisha maisha ya Wakenya. Wananchi pia watakuwa wanaona faida ya ugatuzi. Kwa hayo machache ninaiunga mkono Hoja hii.
Bi. Naibu Spika wa Muda mimi pia nataka kuunga Mswada huu mkono kwa dhati. Afisi ya chifu ni muhimu sana katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali mashinani. Katiba ya Kenya ambayo ilipitishwa na wananchi wa Kenya haikupiga marufuku ofisi ya chifu. Ilisema marekebisho yafanywe katika ofisi ya chifu na ya mkuu wa wilaya ili zifanye kazi sambamba na serikali ya kaunti. Kwa hivyo Mswada huu unaidhinisha msimamo wa Katiba ya Kenya juu ya ofisi hizi. Machifu na wenzao wanaofanya kazi katika Serikali ya Wilaya wasiwe na wasiwasi wowote. Kazi yao imejikita katika Katiba ya nchi hii. Wataendelea kutekeleza majukumu yao na kupata mishahara na marupurupu mengine. Huduma zao ni muhimu kwa wananchi wote. Ofisi hizi ni nguzo muhimu katika utawala wa nchi hii. Lakini ya muhimu ni kwamba maafisa wa kaunti watakaokuwa wakifanyia wananchi kazi uko mashinani watafanya pamoja na machifu na viongozi wengine wa kimkoa. Hakutakuwa na vita baina yao. La muhimu kwetu ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma. Sisi sote tukifanya kazi pamoja tutaweza kuwahudumia wananchi wote.
Bi. Naibu Spika wa Muda ningependa kumwunga mkono Waziri wa Fedha na kumwambia ahsante kwa yale aliyoyafanya katika Mswada huu. Yeye ametulia na kuvumilia. Amesikia maoni ya Wabunge na kwa hivyo tunaunga mkono.
Bi. Naibu wa Spika kwa idhini ya Kipengele 44(2)(c) cha kanuni za Bunge ningependa kuomba taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa Kamati ya Usalama kuhusu kuzorota kwa usalama katika eneo la Samburu. Wizi wa mifugo umezidi huko Samburu. Watu wameuawa kwa njia isiyoeleweka. Hali ya usalama imezorota huko Samburu kwa sababu ya wizi wa ng'ombe na hii imechangiwa na biashara haramu ya hao mifugo. Kwa mfano tarehe 26 Oktoba 2013 ng'ombe 23 walipatikana wakiwa wamebebwa kwenye lori. Mifugo hao walikuwa wakienda kuuzwa. Suala hili lilihusisha maafisa wa usalama. Katika taarifa hiyo ningependa nielezwe yafuatayo:- (i) mpango gani Serikali iko nao ili kumaliza huu wizi wa mifugo; (ii) ni lini mifugo hao watarudishwa kwa wenyewe; (iii) ni hatua gani itachukuliwa kwa wale wanaofanya biashara hiyo haramu; (iv) uchunguzi wa mauaji ya kijana na afisa wa usalama utafanywa lini; na (v) afisa mkuu wa Idara ya Polisi katika eneo hilo na kada wa stesheni husika wataondolewa lini katika sehemu hizo ama watachukuliwa hatua gani.
Bi. Naibu wa Spika nimesikia lakini neno kilema na walemavu lina maana sawia. Sidhani kama mhe. Mwaura anaweza kunifunza Kiswahili.
Bi. Naibu wa Spika ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Ninaiunga mkono Hoja hii kwa sababu ni ya muhimu sana. Nimesikia kuna mtu ambaye aliandikia Bunge barua kuhusu suala la IDPs. Kuhusu suala hili ningependa kusema kwamba nimeshughulika sana na masuala ya IDPs. Ninathibitisha kwamba kama kuna mtu ambaye aliwasadia sana IDPs kwa kuwapa makao; ni Bw. Kimemia. Mimi na mkazi wa Nakuruna ninajua shida tulizokuwa nazo kuhusu IDPs lakini Bw. Kimemia alisaidia sana kwa kusikiliza maoni na hata kwenda kuangalia maslahi ya IDPS walipokuwa wakipewa makao. Kwa hivyo ninaomba kwa sababu tumelizungumzia jambo hili kwa kirefu: Sisi sote tuko pamoja. Kwa hivyo tuchukue fursa hii tuseme tumekubaliana na Kamati ambayo imeleta pendekezo hili Bungeni. Kamati hii imefanya kazi nzuri sana. Kama alivyosema mheshimiwa fulani tunamuheshimu sana Bw. Kimemia kwa jinsi alivyoweza kutuambia mambo yake yote kumhusu. Ninaiunga mkono Hoja hii. Kwa hivyo tuipitishe kwa kauli moja ili tushughulikie jambo lingine. Tumeizungumzia Hoja hii kwa masaa mengi sana kwa sababu ya heshima. Kwa hivyo tuipitishe. Bi. Naibu wa Spika kwa hayo machache ninakuomba uulize Swali tuipitishe Hoja hii.
Bi. Naibu wa Spika silipotoshi taifa. Prof. Anyang-Nyongo hatoki eneo la Pwani. Mhe. James Orengo hatoki eneo la Kaskazini Mashariki. Mimi sipotoshi Bunge. Nazungumza nikijua kilichotokea. Kwa hivyo nataka kumuomba mheshimiwa aangalie idadi ya Mawaziri
Bi. Naibu wa Spika Wabunge wanatakiwa kuwa katika Ikulu kesho saa kumi jioni. Siku ya Alhamisi kila Mbunge na kila mwananchi amealikwa ahudhurie ibada ya misa ambayo itaandaliwa na kusomwa na Baba Mtakatifu. Wabunge wamepatiwa mwaliko na vibali vya kuingia. Ninawaomba Wabunge wanisikize kwa makini. Kitu cha kwanza magari hayatakubaliwa katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Nairobi. Kwa hivyo waalikwa watapitia barabara ya Uhuru Highway mpaka karibu na mzunguko wa Museum Hill na kuacha magari hapo na kuelekea kwa miguu kwenye uwanja. Kwenye lango la kuingia kutakuwa na wafanyikazi wa Bunge ambao watawaonyesha mahali pa kukaa. Tumeomba tufanye mawili. Kwanza ile kadi ya mwaliko ambayo umepatiwa imetumwa na askofu Philip Anyolo ambaye ni Mwenyekiti wa Maaskofu wote Kenya. Ziko hapa sebuleni. Kila Mbunge anaombwa achukue yake. Pili kila Mbunge ana kitambulisho chake cha kuonyesha kuwa yeye ni Mbunge. Mnaombwa ili kurahisisha kazi na kwa sababu ya usalama kila Mbunge abebe kitambulisho chake ili iwe rahisi kwa Wabunge kutambulika ndiyo msije mkasumbuliwa na walinda usalama. Tunaomba hafla hii iwe ya kufana ili kila mtu apate baraka za Baba Mtakatifu. Ninatumai nimejieleza vilivyo. Nitaomba ruhusa nikimaliza tangazo hili niende kwa Ofisi ya Rais kwa sababu kuna tatizo ambalo limetokea kwa wake na mabwana wa Wabunge. Tuliwakilisha majina ya wake na mabwana zetu lakini bado kuna tashwishi ambayo ninaenda kuimaliza. Bila shaka nitapata wasaa wa kuwasiliana na Wabunge kabla ya muda kuisha.
Bi. Spika wa Muda Serikali ya siku ilikuwa imepanga kufanya kazi kidijitali. Vile vile Mswada huu unaangazia jinsi ambavyo vile wahudumu wa afya wanaweza kupata mafunzo ama matibabu kutoka hospitali zingine ama kutoka kwa watafiti wengine walio na ujuzi zaidi. Wakati ambapo vipimo vilivyochukulia kutoka hospitali moja vimetumwa kule hakutakuwa na haja ya mtu kutembea kuenda hospitali nyingine iliyo mbali ilhali anaeza kupokea matibabu mahali alipo. Katika nchi yetu watu wengi wanaugua Saratani na ikiwa Serikali itasisitiza jambo hili liweze kufanyika watu hawa wataweza kupata matibabu. Naomba.
Bunge hili huwa na matatizo wakati Mwanyoha anazugumza. Watu hutoa eno ili wakati wangu uishe. Mhe. Naibu Spika wa Muda nashukuru kwa kunitetea; uendelee namna hiyo. Nataka sasa niongee kuhusu nambari ya wale ambao wanahitajika kupiga kura katika kituo. Mara kwa mara kuna watu wengi sana mpaka watu wengine huja saa kumi na mbili za asubuhi. Lakini ikifika saa kumi na mbili za jioni wanaambia wakati umeisha na wanaachwa nje. Naomba kuwe na marekebisho ili badala ya kuwa na watu 1000 wawe 500 kwa kila kituo. Vituo viweze kuongezwa ili kuwe na muda mrefu na kila mtu aweze kupiga kura.Kwa hivyo naomba Serikali ihakikishe kwamba itaongeza vituo na nambari ya kila kituo iwe ndogo. Nikirudi kwa uteuzi wa wale Wabunge ama madiwani ambao wanataka kuchaguliwa au kuteuliwa hii iwe baada ya uchaguzi ili tuweze kuangalia ni nani alikuwa anafanya kazi nzuri wakati wa kampeini na nani alikuwa goigoi. Kwa sababu wengine huketi bure na mwisho huchaguliwa bila kuangalia na wengine wanaenda kiasi cha kuchagua wapenzi wao. Kwa hivyo mimi naomba hii ifanywe sawa. Asante sana. Hiyo ni kuonyesha eno haya ni kabambe. Kwa hivyo naomba ya kwamba uteuzi ufanywe baada ya uchaguzi na tuhakikishe kwamba mambo yamekuwa sawa sawa. Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Naunga mkono.
Bw Spika naunga mkono Bw. Ababu Namwamba. Mimi nilianza na chama cha ODM kutoka 1991 na mpaka sasa nasukua na hawa watu lakini hawa watu wamekuwa wakora wasioshiba. Wanafaa kuongezwa kaquarter ka matumbo ndio wasisikie njaa tena. Mimi si mtu wa kufungiwa nje. Mimi ni mtu wa kuwafungia nyinyi nje. Ki kitendo
Bw. Naibu Spika kwanza nitasema kwamba nimenukuu yale ambayo yalikuwa yamesemwa na Sen. Orengo kwamba hili si jambo la kisheria peke yake bali ni la kisiasa. Kwa hivyo hawa ni watu ambao wana usemi mkubwa sana kisiasa. Licha ya haya yote ikiwa kulikuwa na na Kamukunji wakati mmoja ningepeka kukumbushwa yaliyoajiri katika mkutano huo.
Bw. Naibu Spika na kama nilisema ni ufisadi basi niliacha neno "kama". Lakini nilikuwa ninamaanisha kwamba tukiipitisha vile ilivyo itakuwa ni kama ufisadi.
Bw. Naibu Spika nilikuwa ninasema ninapinga kuundwa kwa kamati hii. Hii ni kwa sababu itakuwa ikifanya kazi kama ile inayofanywa na kamati ya Maswala ya Kikatiba na Haki za Binadamu. Ni Maseneta wachache ambao wameongezewa katika orodha hii. Ikiwezekana ni vyema kubadilisha mwenyekiti wa kamati hii tunayoipendekeza. Kamati ya Sen. Wako inawajumuisha wanasheria wengi kama vile Sen. Mutula Kilonzo Jnr. Sen. Kiraitu Murungi na wengine ambao wanaweza kuongoza kamati kama hii. Kwa hivyo hata kama Seneti itapitisha Hoja hii naona kuwa kamati hiyo haitakuwa na ufaa yoyote wala haitaongeza lolote katika Seneti hii. Kama ingewezekana kamati hii ingekuwa na nyuso geni kabisa ili tuweze kubadilisha yale ambayo tunafikiria yamekuwa yakikwama katika mambo ya kisheria. Kwa hivyo machache ninapinga Hoja hii. Pia ninapinga mwenyekiti anayependekezwa hapa. Asante sana Bw. Naibu Spika.
Bw. Naibu Spika nimesema kwamba tukiipitisha Hoja hii kama vile ilivyo tutakuwa tukisema Kamati hii ilianza kazi tarehe 2.09.2014. Hii itakuwa ni kama tumefanya ufisadi.
Bw. Naibu Spika ningetaka nikumbushwe yale mambo ambayo yalitajwa katika Kamukunji wakati mmoja na ambayo hayatakiwi kuhusishwa wakati huu ambao tunajadili Hoja hii. Hapa Kamati hii inasemakana ilianza kazi kutoka 2.09.2014. Ikiwa tutaipitisha Hoja hii itakuwa ni ufisadi wa hali ya juu. Ningetaka kusema bila kutaja mambao yaliyojadiliwa katika Kamukunji
Bw. Naibu Spika wa Muda ahsante kwa kunipa nafasi hii ya kuunga mkono Hoja hii. Kwanza nachukua nafasi hii kumshukuru Bwana Mola Subhana Huwata'ala kwa kunijalia kuwa ndani ya Bunge la Kumi na Moja
Bw. Naibu Spika wa Muda asante sana kwa kunipa muda huu ili niweze kuunga mkono Mswada huu. Tangu mimi niwe Mbunge miaka kumi iliyopita sijawahi kuongea kwa Kiswahili. Kwa hivyo ningependa kufanya historia kwa kuzungumza katika lugha hii. Bw. Naibu Spika wa Muda ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu machifu wako na kazi muhimu sana nchini Kenya. Kazi hiyo ni kazi ya usalama. Serikali kuanzia kwa Rais mpaka chini kwa county commissioner ward coordinator chifu na naibu wa chifu ni sehemu moja ambayo ina maana sana kwa nchi yetu. Mswada huu unasema kwamba Serikali ya kaunti haisikii kamwe usalama wa nchi. Ni Serikali kuu ambayo inahusika. Hapo ndipo tumeleta Mswada huu ili tupate nguzo kamili kiusalama nchini.
Bw. Naibu Spika wa Muda haijalishi kama nitaongea mambo ya ukweli kama ninavyoyafahamu. Sisi tumechaguliwa hapa tumekuja kisiasa. Na tulichaguana kisiasa. Kwa hivyo tukizungumza mambo yale yanayofaa na kuyasuluhisha kisiasa nafikiri ni kweli. Tuzungumzie suluhisho tunaloweza kupata. Tunahitajika kukaa chini pamoja tuangalie ni jambo gani linalohitaji kurekebishwa kwenye huu Mswada. Tuzungumze ukweli. Kama kuna pahali ambapo kuna shida ama kama Mswada huu ulipitishwa kwa njia mbaya niko tayari kulizungumzia jambo hili ili tuone ukweli uko wapi. Sisemi hivyo kwa sababu ya siasa. Ninasema hivyo kwa sababu ya jukumu letu. Sisi tukiwa hapa kama Wabunge tunahitaji kuweka tofauti zetu kando na tukumbuke kwamba tulichaguliwa tutatue matatizo ya wananchi. Kama kuna jambo lolote lenye utata tulijadili kwa uzuri. Tuwaweke Uhuru Muigai Kenyatta na Raila Odinga nje tuzingatie jukumu letu la kutafuta suluhisho. Ni jukumu letu. Tumechaguliwa na wananchi kuwatetea. Tukianza kutoka nje ya upeo huo mimi nitakataa. Ndiyo maana ninakataa. Ninawaomba wenzangu tukae tuliangalie jambo hili. Kama kuna shida ambayo inaonekana nitakubali. Kama jambo lolote linahitaji majadiliano tukubaliane ili tuweze kuisaidia nchi hii. Hakuna Upinzani na Serikali tukiwa kwenye Bunge hili. Kazi yetu ni kujadiliana na kulinda haki ya mwananchi tukitafuta namna ya kumsaidia. Kama mwananchi anaumia tuzungumze kuhusu jinsi tutakavyomsaidia. Kama bei ya kitu fulani iko juu zaidi tuizungumzie. Hivyo ndivyo ninavyosema. Sisemi hivyo kwa sababu niko upande ya Jubilee. Mimi niko hapa kuwatetea watu wa Bahati. Kazi yangu nzuri ndiyo iliwafanya watu wa Bahati wanirudishe Bungeni kwa muhula mwingine ili niendelee kuwahudumia. Hii ni kwa sababu mimi huwatetea kwa njia ya haki. Kwa hivyo ninaomba tuendelee na utaratibu wa kuangalia jambo nyeti ni gani. Na hilo jambo nyetu tulizungumzie kwa utaratibu. Lakini tukianza kuingilia mambo mengine
Bw. Naibu Spika wa Muda mhe. Mwaura aliuliza kuhusu uhusiano kati ya utetezi wa kisiasa na lile janga lililotokea kule Mpeketoni. Pia alitakata kujua sababu gani waathariwa walilipwa Kshs50000 na Serikali ya Kitaifa na akalinganisha pesa hizi na zile pesa ambazo serikali ya kaunti iliwalipa ambazo zilikuwa Kshs100000. Alitaka pia kujua ni hatua gani imechukuliwa kwa maafisa wa polisi ambao walizembea katika kazi yao. Nafikiri nilisema hatua ambayo imechukuliwa na Serikali; nilikuwa nimejibu swali hili awali. Kuhusu pesa ningependa kueleza mhe. Mwaura kwamba Serikali ya kitaifa ina pesa za dharura na mara nyingi hizi pesa zinasaidia waathiriwa katika Kenya nzima. Kwa hivyo zile pesa Serikali ilionelea ni vizuri zitolewe ni Kshs50000. Kuna pesa nyingine ambazo zinawekwa ili janga lingine likitokea waathiriwa waweze kusaidiwa. Bw. Naibu Spika wa Muda kuhusu utetezi wa kisiasa nilikuwa nimjibu hili. Mbunge wa Samburu Mashariki mhe. Letimalo alisema kwamba Mpeketoni ni eneo la watu tofaouti tofauti yaani cosmopolitan area. Nakubaliana naye. Mhe. Nas alitaka ufafanuzi kuhusu kuchelewa kwa
Bw. Naibu Spika wa Muda nachukua nafasi hii hata mimi kuzungumzia Hotuba iliyotolewa na Rais. Ningependa kuzungumzia vipengele kadhaa ambavyo alivizungumzia katika Hotuba yake. Kwanza kabisa nataka kupongeza habari za kawi ambazo amezungumzia kwamba tutaweza kuwa na megawatts 5000 ambazo zitatuwezesha kupata umeme kwa asimilia 80 ya jamii. Swala la umeme limetupa shida sana kama Wakenya. Tumekuwa tukipimiwa umeme na kuukosa katika nyakati nyingi. Hivyo basi Wizara husika inahitajika kueneza huu mradi vilivyo. Jambo la pili ningezungumzia swala la usalama ambao kwa sasa katika nchi yetu umedorora sana. Ni swala ambalo Serikali na zile Wizara husika inatakikana iangalie kwa upeo mwingine wa ndani sana. Kwanza haswa chanzo cha kukosa usalama katika nchi ya Kenya ni nini? Sababu ya Kenya kila wakati kuwa na uvamizi na visa vya kigaidi Tunaona wachungaji wa makanisa wakiuawa. Tunawaona pia masheikh wa Kiislamu wakiuawa. Ni sababu gani husika haswa ambayo inafanya usalama kudorora katika nchi yetu? Pia tusisahau kuangalia kuelewa kwamba kumekuwa na biashara ya silaha ndogo ndogo katika mipaka yetu. Je vitengo vyetu vya kiusalama vimeangalia swala hili? Ni vipi Wakenya wengi wanaweza kupata silaha na kuweza kuathiri maisha ya Wakenya? Tunasikitika pia kuona kwamba vyombo vya usalama wakati kumetokea matukio kama ya Likoni Kuna wakati ambapo Makamu wa Rais alisema vijana wawili kati wale walioingia katika kanisa lile na kufanya visa vile walikuwa wameuawa. Lakini je kama Wakenya tumeambiwa ni kina nani na wametoka sehemu gani? Tunapopata habari kama hii ndio tutaweza kujua kabisa watu hao walitoka upande gani. Kwa hivyo tunaomba Serikali ituambie ni kina nani na walitoka wapi na ni watu wa aina gani. Jambo lingine ambalo nataka kuzungumzia ni kwamba Rais alizungumzia kwamba mahakama zimekuwa zikisaidia kuhakikisha kwamba taasisi zetu zimekuwa na usawa wa kijinsia. Hivyo basi napenda kuwaambia Wabunge wenzangu haswa wale ambao wanataka kuleta Mswada wa kuondoa zile nafasi za akina mama 47 wakati watafanya hivyo watakuwa hawafuati ile falsafa ya vyama vyao na pia Katiba. Kama tunafuata Katiba lazima tuangalie kwa undani mambo ya usawa wa jinsia. Jambo la tatu napenda kuzungumzia ni mradi wa reli na upanuzi wa bandari ya Mombasa ambayo Rais amezungumzia. Iwapo jambo hili litatekelezwa kwa haraka na zile Wizara husika basi tutaweza kupata ajira nyingi kwa vijana wetu na kuboresha utendaji kazi katika bandari ya Mombasa; hivyo basi uchumi wetu utaweza kukua zaidi. Jambo lingine ambalo Rais hakulizungumzia na ni swala nyeti sana ni kuhusu ajira. Nilitarajia Rais azungumzie vipi tutaweza kufufua viwanda ambavyo vimedorora na vingine hata kufungwa. Viwanda kama vya Bixa korosho makonge na pamba vinahitaji kuboreshwa ili tuweze kupata ajira kwa vijana wetu. Pia inafaa tuboreshe sekta ya jua kali ili tuweze kuwa na ajira zaidi. Jambo la mwisho ambalo ningependa sana kuzungumzia kuhusiana na Hotua ya Rais ni bei za vyakula. Bei imepanda sana na Wakenya wengi wameshindwa hata kujimudu kimaisha katika upande wa chakula na mambo mengine. Ningependa kusema Serikali hii na sisi tukiwa ndani kama Wabunge tuweze kuangalia mambo ya kulipa ushuru wa VAT
Bw. Naibu Spika wa Muda nasema labda Mhe. Ngong'o hana laini nzuri ya kufikia mkubwa wake; kwa hivyo nitaendelea kusema kwamba kile kitu Rais aligusia na naona kitasaidia Kenya ni wajibu wa kuhakikisha kwamba wawindaji haramu wamekamatwa na kufungwa. Leo tukizungumza kila mtu anaelewa kwamba wawindaji haramu wameuwa ndovu wetu na vifaru. Kwa hivyo kulingana na zile sera Serikali imeweka sina wasiwasi kabisa kwamba tutaweza kukamata wale wakora na wale watu ambao wanaharibu nchi yetu. La mwisho ni kwamba ile asilimia 30 ambayo imepewa vijana akina mama na walemavu kuna sheria nyingi zimewekwa na Wizara ya Ugatuzi na Mipango. Kwa hivyo ninaomba hiyo Wizara iangalie na iache kuitisha vyeti vya kuonyesha kama umelipa kodi ama ushuru. Kwa hivyo haya mambo yote yakiangaliwa nchi yetu itaendelea kuimarika.
Bw. Naibu Spika wa Muda nimesimama kupinga Hoja hii kwa sababu Serikali ama chama kilio na wengi ama wachache kina nafasi ya kuleta miswada na ajenda zao Bungeni June Jumatano saa nane na pia Alhamisi. Wabunge wengi wana miswada tofauti ambayo wangependa kupendekeza. Kutokana na Katiba mpya Bunge hili halifai tu kupatiwa ajenda na upande wa Serikali. Tunafaa kuwa na nafasi ya kuweza kuwasilisha matakwa na jumbe kutoka kwa wale ambao tunawaakilisha na Jumatano asubuhi tunakuwa na mwanya mwafaka. Ninapenda kupinga kwa sababu wakati huu ndio tunapata nafasi ya kuzungumza kwa sababu mara nyingi wakati ule mwingine hatupati nafasi. Utakuta kwamba ni Mkuu wa Wengi na wengineo ambao wanazungumza. Kwa hivyo ninafikiri muda huu unafaa kutengwa tuweze kujieleza na kuwashawishi Wabunge wenzetu ndiposa ajenda zetu pia ziwe na nafasi katika Bunge hili. Ninapinga.
Bw. Naibu Spika wa Muda nimesimama kuupinga Mswada huu kwa sababu ingawaje ni Mswada mzuri unatashiwishi. Waswahili wanasema hata unapopika mchuzi wako mzuri unapoingia jongoo hauwezi kuwa mzuri. Kama Wakenya tunatambua kwamba tumekuwa katika mapambano makali sana kuhakikisha kwamba kumekuwa na uhuru wa habari na kuvipatia vyombo vya habari uhuru na kupata uhuru wa kujieleza. Katiba yetu katika Sura ya Nne Vipengele 33 34 na 35 inazungumzia jinsi tulivyopata uhuru wa kujieleza uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kupata habari katika nchi yetu. Kwenye Mswada huu kuna Kipengele kinachosema kwamba kutakuwa na Tume itakayopokea malalamiko. Tume hiyo imepewa nguvu nyingi ambazo zinaweza kumfanya mwanahabari asiweze kufanya kazi yake.
Bw. Naibu Spika wa Muda vile ndugu yangu alivyosema katika kumalizia ningependa kusema kwamba hela ambazo zimegawiwa maeneo ya uwakilishi Bungeni ambazo ni za CDF ni lazima Bunge hili lihakikishe kwamba hela hizo haziondolewi kamwe. Hizo hela zinasaidia wananchi; sisi ndio tunajenga shule na barabara. Hayo ndio maendeleo wananchi wanatarajia mashinani. Jambo lingine ambalo linaleta shida ni kuwa kama gavana hataweza kuleta maendeleo yale tunayotarajia katika maeneo ya uwakilishi Bungeni katika sehemu za kaunti tutafanya nini? Hapo ndipo CDF itasaidia. Kwa kumalizia ninaunga mkono Mswada huu na ninatoa hisia zangu kwa hisani. Ningependa kutoa hisia kwamba tuhakikishe tumalize na kupitisha huu Mswada ili kaunti ziendelee na wananchi wa Kenya wahisi vizuri na maendeleo kupatikana mashinani.
Bw. Naibu Spika wakati nimesema naipinga Hoja hii pamoja na majina katika orodha hii hapa pengine liwe ni jambo la ubaguzi ambalo linaweza kuwa katika hii Seneti kwa sababu mimi si pekee yaka ambaye ametaja mambo ya ufisadi katika Hoja hii. Leo pia kuna Seneta ambaye pia ametaja jambo hilo la ufisadi. Sikusikia wenzangu wakisimama kwa hoja ya nidhamu. Ikiwa mimi ninahisi na naona jambo tofauti na ninafikiria Hoja hii imewasilishwa hapa ili tuijadili
Bw. Spika Alhamisi wiki jana niliamua kuonyesha uzoefu wangu wa lugha yetu ya taifa; Kiswahili. Lakini kuna Wabunge kama Mhe. Millie Odhiambo waliolalamika kuwa nilikuwa ninawatesa kwa kuongea kwa lugha ya Kiswahili. Kwa sababu hiyo nimeamua kuwa leo nitaonyesha uzoefu wangu kwa lugha ya Kiingereza. Bw. Spika ukiamua naweza kuendelea kwa Kiswahili.
Bw. Spika alichosema ni jambo la kutia kidonda chumvi. Kusema mlevu atawakilishwa. Akishawakilishwa
Bw. Spika kwa majina naitwa Zena Chidzuga na nawakilisha wananchi wa Kwale. Nimesimama kuchangia Hoja hii kwa sababu sehemu ninayotoka ni kame. Wanyama wetu wamekufa; wanyama wetu hawafi tu kwa sababu ya mafuriko bali pia kwa sababu ya njaa na maradhi. Tegemeo langu katika kuunga mkono Hoja hii si tu ili wafugaji wapate bima lakini naomba Hoja hii ifanyiwe ukarabati ili kuwe na unyunyuziaji maji maeneo kame. Hili likifanyika watu wetu watakuwa na nyasi za kutosha kulisha mifugo yao. Wafugaji wenzetu walio katika sehemu za Kasikazini Mashariki mwa nchi huishia kuja sehemu zetu kwa sababu kwetu nyasi huchukua muda kukauka. Kule kuja kwao huchangia ukosefu wa usalama. Wakati mwingine wakija hata hawaombi ruhusa kulisha mifugo wao huko kwetu. Wao huleta wanyama wao na kuwaingiza katika mashamba ya watu kisha fujo hutokea. Kwa hivyo inafaa Hoja hii irekebishwe kuitaka Serikali itoe pesa za kutosha kujenga mabwawa katika kila sehemu yenye wanyama kwa wingi. Mabwawa haya hayatamsaidia tu mfugaji bali yatawasaidia wananchi wengine kupata chakula kwa kunyunyuzia mashamba yao maji. Kwa njia hiyo tutakuwa tumeua ndege kumi kwa jiwe moja.
Bw. Spika mheshimiwa anasema hanielewi. Nitamufafanulia jioni tukikutana baada ya futari yake. Kwa sasa ninaomba aniache niyaseme. Aelewe asielewe hiyo ni shida yake. Mhe. Spika ninawomba Wabunge watafakari iwapo wanataka Prof. Kaimenyi aendelee na kazi ama aondoke. Hoja hii inasema tuangalie kama tunaweza kumptatia nafasi nyingine ama la lakini tumeambiwa kwamba Bunge hili litateua kamati maalum kuangalia jinsi anavyofanya kazi; na kwamba kwa sasa tuendelee mbele ili tuipatie kamati hiyo nafasi ya kuifanya shughuli hiyo. Maoni yangu ni kwamba sidhani kama Prof. Kaimenyi anaweza kuyatekeleza majukumu kwenye kitengo cha elimu. Matatizo aliyonayo ni mengi. Kama angeliweza kuketi chini na kuzungumza na wenzake katika sekta ya elimu - wakiwemo waalimu Wabunge na hata wazee wa Njuri Ncheke - ili aweze kuridhiana nao matatizo yake yangekuwa haba. Imebidi alazimishwe ndiyo atoe ng'ombe kwa sababu ya ujeuri na ubambe ninaozungumzia. Yeye ni mpaka asukumwe ndiyo aweze kuitikia mwito.
Bw. Spika nakushukuru kwa kunipa fursa hii. Ningependa kumpongeza Naibu Rais wetu na pia Sen. Musila kwa kuleta Hoja hii. Nafikiri Wakenya wengi wamepata matatizo kwa kukosa kupata vyeti vyao vya shule kwa sababu vyeti hivyo vimetiwa "mbaroni" na waalimu. Hii ni fursa muhimu sana kwa wanafunzi waliokosa vyeti vyao kwa muda mrefu. Kwa hivyo langu ni shukrani na pongezi kwa Naibu Rais na Serikali ya Jubilee. Asante.
Bw. Spika namshukuru Waziri Msaidizi kwa sababu amesema alichelewa kuja Bungeni kwa sababu ya msongao wa magari pale Kibarani. Nataka kumuuliza ni mikakati gani anayo ya kuhakikisha kwamba gari la moshi linafanya kazi kuanzia Mariakani Mombasa Uwanja wa Ndege wa Moi na kutoka Mombasa hadi Malindi?
Bw. Spika naomba kukueleza kwamba nilileta Petition Bungeni mwezi wa September 2014 kuomba ardhi ya Serikali kwa sababu ya sehemu ya uwakilishi Bungeni ya Changamwe lakini mpaka sasa Kamati ya Ardhi haijatoa jibu. Zaidi ya miezi mitatu imeshapita sasa. Kwa hivyo nakuomba uishurutishe Kamati ya Ardhi iwajibike na kuwatendea haki wakazi wa Changamwe. Ahsante Bw. Spika.
Bw. Spika nayaheshimu maoni ya mheshimiwa aliyezungumza lakini ukweli ni kwamba sisi kama Wabunge wa Bunge la Kumi na Moja hatutaki kurudi kule ambako tumetoka kama nchi. Tunataka tuwe nchi ambayo kabila zote zimeshikana pamoja ili tulijenge taifa hili. Kwa ufupi tusiwe na machungu tunapozungumza ukweli. Ni lazima tukubali ukweli. Mkuu wa Wengi ako hapa na ni lazima amshauri Rais wetu. Wabunge wanamuuliza awe kiongozi wa kitaifa kama vile Wakenya walivyomchagua. Kwa ufupi tunamheshimu. Naunga mkono kuteuliwa kwa Njee Muturi lakini ni lazima uteuzi wote utakaofanyika kuanzia sasa ufanywe kutoka taifa nzima.
Bw. Spika ni lazima nisikike kwa sababu mimi ni mmoja wa hili Bunge. Kuna mwendo ambao umeanza na unaendelea. Ni juzi tu ambapo Baraza la Elimu ambalo linachagua orodha ya Halmashauri ya Elimu nchini Na nitaitisha habari hiyo Mungu akipenda wiki ijao
Bw. Spika nilikuwa mbele ya mheshimiwa kuingia katika Bunge hili. Kwa hivyo si mara yangu ya kwanza na hawezi kunifundisha Standing Orders . Nimesimama kupinga Hoja hii. Sipingi kwa sababu ninaunga mkono ufisadi au ninataka NCPB ikufe. Ninapinga kwa sababu shida ambayo imepatikana imetokana na NCPB ambayo imesimamia zabuni. Wao ndio wametoa kadarasi. Wakati wamezozana na Erad Erad wemeenda kortini NCPB hawajakata rufani hata mara moja mpaka leo.
Bw. Spika nilipoleta hoja ya nidhamu niliitwa majina mengi ikiwemo kusemekana kuwa nimeleta hoja kupinga moja kwa sababu ya ufisadi na pili kwa sababu ya ukabila. Mimi nimetoka Mkoa wa Pwani kisha Pwani barani si baharini kule. Katika hiyo bara cheo kubwa kabisa tulichonacho katika Serikali ni DC. Ukabila hautanipeleka mahali. Mimi ni kiongozi na ninatoka Bura ambapo kumetoka makabila 42 ya nchi ya Kenya. Siwezi kuleta hoja kwa ajili ya ukabila. Pendekezo la 13 katika ripoti iliyo mbele yetu linasema uchunguzi ufanywe kwa sababu ukame ambao umetangazwa haufai kutangazwa saa hii. Wajibu wa kutangaza ukame kama janga la kitaifa ni wa nani? Miaka tisa iliyopita Bunge lilikuwa wapi? Ule ukame uliotangazwa miaka tisa iliyopita uchunguzi uanze? Tunatumia cheo na mamlaka vibaya.
Bw. Spika ningependa kukushukuru kwa kunipa nafasi hii. Kwanza ningependa kuipinga Hoja hii. Licha ya mjadala huu kuwa mzuri kuweka kando walemavu ambao walichaguliwa kwenye kaunti ni dhuluma na ubaguzi wa hali ya juu. Bodi hii itakapokuwa inakaa walemavu watakuwa wakiwakilishwa na kina nani? Hii ni bodi ya kaunti ambayo itakuwa ikijihusisha na mambo ya maendeleo. Ikiwa katiba ilipiganiwa na ikapita na tukapewa nafasi hizi sielewi kwa nini Seneti na NationalAssembly zilifikiria kutunyima nafasi hizo. Ingekuwa afadhali kama tungewaweka walemavu katika Bodi hiyo badala ya kuwaacha nje.
Bw. Spika ningependa kumwambia Bw. Mung'aro kwamba Wizara ina mipango kambambe ya kuweza kuboresha hali ya uchukuzi hapa jijini na Mombasa ambako msongamo wa magari umenifanya nichelewe kufika hapa Bungeni leo. Kuna mipango ya kaunti tofauti na Mombasa ni moja ambayo tunaiangalia kuona kwamba tunaweza kuhamisha hata shughuli nyingi za kibandari katika maeneo ya Mariakani na kwingineko. Kwa hivyo hali italazimisha kwamba tuwe na uwezo wa kuwezesha usafiri wa reli kutoka Mombasa na vitongoji vyake. Kwa hivyo kuna mipango maalum ya kuona doto hii imetimilika kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo au ifikiapo 2015.
Bw. Spika swali la uchafu halikuwa limeulizwa katika lile swali ambalo lilifika kwa Kamati. Kwa hivyo ningemuomba Mhe. Kombe aulize swali la uchafu ili niweze kuelezea eno ya uchafu na vile ambavyo tunaweza kusafisha Jumbe la Ardhi.
Bw. Spika wa Muda kuna maswala ambayo ni muhimu sana. Nimeweza kuzungumza na nikataja. Ndugu zangu lugha ya Kiswahili ni lugha yetu. Bw. Spika wa Muda nitadai dakika zangu. Tayari nimeweza kusema kuwa kama ilivyoorodheshwa.
Bwana Naibu Spika Mhe. Arati anaposema masomo yangu na yake haiyatoshani... Bwana Arati ni mtu sidhani kama amefika chuo kikuu. Mimi ni daktari na niko na Masters degree . Mimi ni daktari wa upasuaji. Siwezi lingana na Bwana Arati kwa masomo!
Bwana Naibu Spika wa Muda nilikuwa nataka kuchangia lile suala la Lamu wala si hili.
Bwana Naibu Spika wa Muda ningetaka kuomba msamaha na kuondoa yale ambayo nimesema. Hili ni Bunge la heshima na ni lazima tudhihirishe heshima ya Bunge hili. Ninashukuru na kusema kwamba tuendelee kuwa wangwana.
Bwana Naibu Spika wa Muda ningetaka kusema kwamba sikufanya jambo hili makusudi.
Bwana Naibu Spika wa Muda yangu ni kupeana pole kwa familia za wenzetu ambao waliuliwa kule dera.
Bwana Naibu Spika wa Muda yangu nikuongeze kwamba tukisema Jogoo Road iongezwe kutoka kwa shamba ambalo liko Kenya Railways hatuishi hiyo sehemu ya chini. Hatuwezi kung'oa stesheni ya mafuta na kituo cha reli ambavyo viko karibu ili tusukume soko la Muthurwa chini. Hili si jambo zuri. Jambo hili linahitaji mpangilio na watu wanafaa kuketi wapange pamoja. Sitaki kurudia mambo ya (word expunged ). Huo ni mdomo uliteguka na nimeomba msamaha. Lakini ukiwachunguza watu ambao wameileta Hoja hii katika Bunge kuhusu shamba la KRC utapata kuwa kuna kitu ambacho kinaendelea nyuma yake. Nyuma yake utasikia kuwa Mhe. Aburi alisimama Bunge na akasema kuwa kuna kitu ambacho kinaendelea. Bw. Naibu Spika kwa mfano katika eneo la Tigania East niko na mipango yangu. Kwanza lazima uniulize; "Bw. Aburi lile daraja likoje?" Ndio maana Mhe. Kada amesimama akasema kwamba shamba hilo halitoshi kwake. Shamba lililoko pale kwangu ni ekari 35 na lote liko na nyumba ndogo ndogo kama zile za zai. Bw. Naibu Spika wa Muda inamaanisha kwamba kile kikundi ambacho kinataka kuleta hayo mambo ni kikundi ambacho kina mpango wa kubomoa zile nyumba halafu hiyo mada iletwa Bunge tena ili tuanze kupiga kelele katika Bunge kwamba nyumba za Shirika la Reli zimebomolewa. Kwa hayo machache Bw. Naibu Spika wa Muda kamwe siungi mkono Hoja hii. Asante.
Bwana Naibu wa Spika nashukuru kwa kunipa fursa hii. Nataka kumshukuru Mwenyekiti Mhe. Koinange kwa yale mambo ambayo amesema. Jambo kubwa katika ugavi wa chakula tunachosema ni relief food nikuwasaidia wanaoumia. Ninataka kujiunga na mwenzangu kutoka Trans-Nzoia Mhe. Chris Wamalwa kwamba sisi tuko na shida kwa sababu kile chakula kililetwa kule hata tunapoongea sasa hivi Mhe. Koinange tunaambiwa mafuta iliibiwa - ile ilipelekwa katika Kaunti ya Trans-Nzoia. Na hadi sasa haijapatikana. Chakula cha msaada kinapotolewa tumeweka mikakati ipi kuhakikisha kwamba hicho chakula kinafikia wale ambao wanakihitaji? Tuhakikishe kwamba kila mtu ambaye ameathirika anaweza kushughulikiwa vilivyo. Ninajua watu watajaribu kusema pengine tupeane pesa wengine wanaweza kuchukua pesa hizo na wakafanyia jambo ambalo sio sawa. Wanaweza kutumia hizo pesa kwa kununua pombe. Wengine watachukua hizo pesa na zisifikie watoto na akina mama. Kwa hivyo tunapopeana hiki chakula ni lazima tuhakikishe ya kwamba kinafikia wale ambao wameathiriwa kweli. Kwa hivyo Mhe. Koinange ningependa kuomba muhakikishe ya kwamba wale wanaohusika na kupeana chakula cha msaada wanawajibika. Na wengine pia wasitumie chakula cha msaada kwa mambo ya kisiasa. Tupeane chakula kwa wale ambao wameathirika siasa itakuja baadaye. Nashukuru Mhe. Naibu wa Spika.
Bwana Naibu wa Spika nimetafuta Katiba ya Kiswahili lakini nimekosa. Katiba ambayo nimepata ni ya Kiingereza.
Bwana Spika hii ni nyumba ambayo inaangaliwa na Wakenya wote wakubwa kwa wadogo na watoto kwa wazee. Tegemeo lao ni sheria tunazotunga hapa. Bila usawa na haki hadhi ya nyumba hii itateremka. Kuna pendekezo moja kwamba Serikali itoe ruzuku kwa NCPB ili iweze kusimama. Mimi nitaunga hilo mkono ikiwa viongozi wa NCPB watabadilishwa. Baada ya hukumu kutolewa wale waliokuwepo hawakwenda kukata rufaa. Hawakumjulisha Mkuu wa Sheria kwamba kuna tatizo kama hili. Kwa sababu gani? Ni kwa sababu wao pia wana mikono yao ndani ya suala hili. Ikiwa Erad imepoteza robo ya mali ya umma NCPB itapoteza theluthi tatu ya mali ya umma. Kwa sababu ya NCPB ninapinga ripoti iliyomo ndani ya Bunge hili.
Bwana Spika naona kwamba pia wewe unafurahia haya mambo. Ni shwari kwamba ni mambo ambayo yanatuguza sisi sote. Wale wanawake ambao wamekeketwa - ingawaje sio wote ambao watakubali - huwa wanasema kuwa ukikatwa unakosa " network" . Hiyo " network " inahitajika. Kazi ya wanaume ni kutunyanyasa. Wao wanapata " network" lakini sisi hatuipati. Tunafananisha kiungo hicho na aerial ya Safaricom. Katika hali hiyo hata afya ya wanawake inadhulumiwa kwa sababu kitendo cha ndoa kinakuwa ni kama kulazimishwa. Wakati wa kuzaa wanatuambia kuwa uchungu ni mwingi sana ilhali tunaendelea kuwalazimisha kukeketwa. Tunawaomba wanaume waje mbele tupigane vita hivi pamoja. Watueleze gani ndio bora kuliko nyingine.
Bwana Spika nilitumwa na watu wa Muhoroni kuja kumpigia Bwana Raila Odinga na Uhuru Kenyatta kura Kwa hivyo napiga ndio
Bwana Spika pendekezo la 13 linasema kwamba uchunguzi ufanywe katika Wizara ya Miradi Spesheli na Wizara ya Kilimo kwa kutangaza ukame. Miaka tisa imepita sasa. Kwa nini ukame ulitangazwa kuwa janga la kitaifa? Wajibu wa kufanya hivyo ni wajibu wa Baraza la Mawaziri na Rais. Kwa nini ripoti haijaletwa hapa? Ripoti hi inatupatia ukweli nusu na uongo nusu. Hatujaambiwa fedha ni za nani. Tumechukua kampuni moja na kujaribu kuihalalisha kwa sababu tunataka kuwaambia Wakenya kwamba hawa ndio wabaya zaidi. Je wale waliochukuwa zabuni ya kuleta tani zaidi ya 110 wako wapi? Wamefanya nini? Wamelipwa pesa ngapi? Ripoti hii haituelezi hayo. Kwa sababu kuna Erad tutaonyeshwa hiyo Erad na ukweli mwingine ufichwe. Tutapitisha hii ripoti kwa ajili ya kufurahisha watu fulani. Tuelezeni Purma ni ya nani? Tueleze Freba ni ya nani? Tueleze Euro Commodities ni ya nani? Wamelipwa hela ngapi? Ukifanya hivyo mimi nitakuamini kisha nikuunge mkono. Bunge hili linapaswa kutoa ukweli na haki kwa Wakenya wote.
Bwana Spika sijui itabidi tutafute askari ili tuje nao ndani ya Chamber kwa maana tunasikia kuna immunity hapa. Ili wengine watunyamazishe wanataka kutupiga kwani hawajui kwamba wanawake hawapigwi. Especially sisi wanawake wa Coast wanaume huwa wanatubembeleza. Sisi tunapigwa na leso. Wanatuletea vitu na si kutupiga. Sijui ni tabia gani hii ya kupiga wanawake. Imetoka wapi? Mimi sijaona kwa hizo field zingine.
Bwana Spika tumekuwa na Rais Suluhu jana Kwa hivyo wacha nijaribu Kiswahili Mimi Ahmed Kolosh Mohamed Mjumbe wa Wajir Magharibi kwa niaba ya watu wangu napiga ndio
Dakika zako zimeisha Mhe. Aisha. Dakika yako moja imeisha.
Eeh ni lazima niongee kwa Kiswahili? Bw. Spika nimesikiza ndugu yangu Mhe. Olago Aluoch kwa makini akiongea kwa Kiswahili na kusema neno 'sambamba' kwa mara ya kwanza. Nilikuwa nafikiri ni yule comedian ndiye anayejua neno 'sambamba' peke yake. Kwa kuwa najua anaongea kuhusu eneo bunge lake je ako na hakika wameelewa eno ambayo amesema? Mahali ambako tunatoka watu huongea kwa Kiingereza. Kiswahili si mdomo yetu. Sisi tunaongea kwa Kiingereza. Si hii ni torture ?
Haijatosha. Lamu imeathirika pakubwa na ni muhimu kamati husika iangalie mambo haya na hatua ya haraka ichukuliwe.
Hata juzi nimemwambia President ya kwamba zile mashine alikuwa amenunua kupeleka kwa kaunti na zikakataliwa zipelekwe kwa lazima.
Hatutaomba msaada kwa Tume ya Sarah Serem kutusaidia kama Wabunge kututungia Katiba ambaye haiambatani na vifungu vya Sheria ya nchi hii.
Haya dakika yako imekwisha Mhe. Dukicha tafadhali.
Hilo ndilo swali ambalo nauliza. Nipe nafasi hata kama ni dakika mbili peke yake. Kwa hivyo niendelee?
Hiyo ni hoja ya nidhamu ya kweli Tusichanganye mambo ya ukabila na mambo ya kukosa nidhamu na mwelekeo katika maisha Mhe Sankok fafanua zaidi hilo jambo na kama hauwezi itabidi uliondoe
Hoja haijawasilishwa kikamilifu katika ule mnyambuliko ambao Mheshimiwa amesema. Unapokuwa na Hoja ni lazima useme "I beg to move " yani "nasongesha". Lakini labda mwenzetu amesahau sheria na tamaduni za Bunge. Ukileta Hoja ni lazima "usongeshe". Mwenzagu amesahau "kusongesha". Lazima "asongeshe".
Hoja hii imechangiwa na watu wengi sana. Kulingana na Standing Order No.95 naomba mwenye Hoja ajibu ili tuendelee na mambo mengine tafadhali.
Hoja iliyotolewa na Mhe. Ali kulingana na vile Kiongozi wa Walio Wengi alisema inakejeli Katiba. Mambo ya huduma ya afya imegawanyika kati ya Serikali Kuu na serikali ya ugatuzi. Itakuwa fursa nzuri kufanya marekebisho kwa sababu tayari ametoa Hoja yake. Kiongozi wa Walio Wengi alisema ni bure kwa sababu haitaweza kuleta ufaa kwa wakenya. Kwa sababu ni Hoja nzuri tunafaa kutumia fursa hii kufanya marekebisho ili isikejeli Katiba.
Hoja ya nidhamu Mhe Naibu Spika Asante sana kwa kunipatia fursa hii kuchangia hili jambo
Hoja ya nidhamu Mhe Naibu Spika Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi amesema kwamba angependa tujionyeshe Afafanue vile tutajionyesha ili tupate kujua kama ni Kiswahili sanifu kimemshinda
Hoja ya nidhamu Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kuna ile hoja ya nidhamu ambayo ililetwa ya kupunguza muda wa kuongea kuwa dakika tatu.
Hoja ya nidhamu Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninashangaa kusikia kuwa mwenzangu anaongea kuhusu mambo ambayo hayako mbele yetu wakati huu. Hatuongei kuhusu vyama au kuwaondoa watu kwa Kamati. Tunajadili Hoja ambayo iko mbele yetu na tunahitajika kuiunga mkono. Mimi ninasema kuwa Hoja hii ni muhimu sana. Tuko wengi sana katika Bunge na tunataka kila mtu apate nafasi ya kuongea. Hii si nafasi ya kuzungumzia mambo ya chama au kuhusu Wabunge ambao walitolewa kwa Kamati. Mhe. Nas hafuatilii mikakati ambayo tuko nayo wakati huu. Mambo anayozungumzia yako inje ya utaratibu wa mambo tunayozungumzia wakati huu.
Hoja ya nidhamu Mhe. Naibu Spika Wa Muda. Ningependa kusema jambo kuhusu nidhamu katika Jumba hili. Wakati ulikuwa unazungumza Mhe. Sankok alikuwa anachukua video . Ningetaka kujua kama hii iko katika Kanuni za Kudumu. Nimeona hili si jambo nzuri. Kwa hivyo ni vizuri aseme nia ya kuchukua hiyo video
Hoja ya nidhamu Mhe. Naibu Spika. Mhe. amesema anatoa kongole kwa walioongea. Sisi hatujui maana ya kongole. Tafadhali atuambie ni nini pengine ni matusi. Atufafanulie maana yake.
Hoja ya nidhamu mhe. Spika. Kufuatana na Kanuni No.44 ningetaka kuguzia swala ambalo limekuwa katika vichwa vya habari na katika magazeti kuhusu hali yangu ambayo imesemwa nina bunduki. Inadaiwa kwamba nilitoa bunduki na kutaka kumpiga risasi mfanyabiashara mmoja. Nataka kusema kwamba huo ni uongo mtupu. Mimi sijawahi kuwa na bunduki. Sijawahi kupewa leseni ya kubeba bunduki na sijui kutumia bunduki. Nataka niseme kwamba haya yamefanyika katika eneo la Bunge langu ambapo kumekuwa na mzozo wa ardhi ambayo Marehemu Wangari Maathai alikuwa amesimamisha ujenzi wake. Tarehe 11th May nikiwa na Mbunge Mutemi tukiwa kule Dagoretti niliitwa kwa sababu lile shamba lilikuwa limeingiwa na vijana kutoka eneo langu la Bunge. Walikuwa kadiri ya vijana kumi. Nilipoingia pale wale niliwakuta pale wawili wa vijana hao walitoa bunduki na alipotaka kunipiga risasi yule mlinzi wangu aliingilia kati. Alitoa bunduki yake na kukawa na sitofahamu hadi yule mtu akarudisha bunduki yake mfukoni. Huyo mfanyabiashara anadai kwamba analindwa na polisi na akataja majina ya wakubwa. Alimtaja mkubwa wa CID ambaye nilienda kumwona. Mkubwa wa CID Bw. Muhoro akakataa. Akasema mtu yeyote ambaye ni mwarifu lazima akamatwe na ashtakiwe. Gazeti la Nation - na hii si mara ya kwanza - limekuwa na nia ya kuniharibia jina. Leo hii maisha yangu naambiwa kwamba yamo hatarini. Nataka niombe Kwa sababu ni kawaida ikiwepo kwamba ni Mbunge anatajwa kwa kitu chochote kile inakuwa kwamba ni hali ya kutengeneza pesa kupitia kwa gazeti. Mimi nikiwa hapa nahuzunika sana! Mimi ni baba; ni bwana na ni Mheshimiwa wa eneo langu la uwakilishi Bungeni la Dagoretti North. Gazeti limekuwa ndilo askari mahakama ya kutuma watu katika jela. Naomba kwamba hili Bunge - na ninaongea Kiswahili kwa sababu nataka watu wangu wanielewe Kumekuwa na hali ya taharuki kule Dagoretti. Wanasema Mheshimiwa anataka kuuawa ama yeye ndiye anataka kuuwa mtu. Naomba kuuliza haya maswali kwa sababu kulikuwa na vyombo vingine ambavyo vilishika hayo mambo na vikanunuliwa lakini nilipata ile clip kuonyesha vile alivyotoa bunduki na ku cock - karibu kunipiga risasi. Ningeuawa siku hiyo singekuwa katika Bunge hili. Nashukuru Mungu kwa sababu siku yangu haikuwa imefika. Mhe. Spika huyo mtu anasema kwamba yeye amepewa walinzi wawili na hakuna mtu atakayemshitua na anatembea Jiji hili lote. Kwa vile hili ni Bunge la kutengeza sheria ninaomba lisaidie Wakenya wengine. Mimi nitajitetetea leo katika Bunge hili. Lakini itakuwaje kwa yule ambaye hawezi kujitetea katika Bunge hili ama kwingine? Nimesikia kwamba mfanyabiashara anayeitwa Ashok Shah ametajwa kwingi. Naomba kwamba sheria ichukue mkondo wake. Naomba pia Mkuu wa Mashtaka ya Umma afanye kazi yake kwa sababu tangu tarehe 11 mwezi wa tano mpaka leo hakuna kitu ambacho kimefanyika. Mhe. Spika kwa vile inawezekana ikawa leo ni mimi na kesho ni mwingine aliye hapa naomba Bunge hili lichukue hatua. Nataka kuwaonya wale watangazaji wa NationNewspaper kwamba nitachukua hatua thabiti kuhakikisha kwamba haki imetendeka. Ahsante.
Hoja ya nidhamu Naibu Spika wa Muda. Mimi nimekuja hapa kitambo sana ilhali huyu mheshimiwa ambaye yuko kwenye jukwaa
Huo ni ufisadi. Ni ufisadi kuambia watu kuwa SGR lazima ibebe makasha peke yake. Bado niko katika mada ya Mswada huu nikizungumza mambo ya ufisadi. Ni ufisadi mkubwa kuambia watu wapakie makasha katika SGR na si malori. Leo ninasema tunajitayarisha kushtaki Serikali ya Kenya katika Korti ya Afrika Mashariki mpaka tukomboe watu wa Mombasa. Ahsante na Mungu atubariki.
Iko sehemu mbili. Nadhani anafahamu. Mhe. Naibu Spika wa Muda ninaomba dakika zangu ambazo zimechukuliwa Karani ahakikishe nimezipata ili watu wa Mvita wawakilishwe sawasawa. Kwanza nimezungumza kuhusiana na aa ya karantina. Si sawa Wakenya kuchukuliwa na kuambiwa walipe ile aa. Pili nimezungumzia wale ambao wako na nafasi ndani ya nyumba zao wakubaliwe kufanya karantina nyumbani mwao. Hilo ni jambo ambalo Wizara ya Afya na serikali za kaunti wamekubali. Ni aibu kwamba Serikali ya Kaunti ya Mombasa imeshatumia zaidi ya Ksh20 milioni kuwalipia watu ambao walikua wamezuiliwa kwenye makazi ya karantina. Nawasihi nawarai na kuwaomba kwa unyenyekevu kila Mkenya anayetusikiza kama Mhe. Duale alivyosema wenye kuhusika na mambo ya lockdown na mambo ya cessation of movement..
Jambo hili ni la muhimu katika elimu yetu hapa nchini Kenya. Lakini ningependa kumsihi yule ambaye ameleta Ombi hili hapa Bungeni Dkt. Chris Wamalwa kuwa ingekuwa vizuri tuhakikishe kuwa hili jambo lililetwe kwa Kamati ya Bunge inayohusika na mambo ya elimu ili tumwite Waziri wa Elimu aje atuelezee ni sababu gani iliyomfanya aamue hivyo. Jambo la mwisho ni kuhusu vile ambavyo Mhe. Dadangu alisema hapa kuwa Waziri Matiang'i ni mzee wa Kanisa la SDA. Ni mzee ambaye anaheshimika na ni Waziri wakati huu. Si vyema kusema kuwa yeye hajui kumwomba ama kuswali kwa Mwenyezi Mungu. Ingekuwa vizuri tumpe nafasi wakati Kamati itakavyoketi atueleze ni nini kilichomfanya akaamua hivyo.
Jambo la Nidhamu Bw Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuelewa kwa nini mwenzetu anawataja Waislamu. Inaonekana kwamba Waislamu ndio ambao wameleta haya maafaa. Hili jambo si la Waislamu kwa sababu katika dini ya Kiislamu hakuna mahali ambapo kuna mambo ya kuuana.
Jambo la nidhamu Bw. Naibu Spika wa Muda. Tangu tulipoingia wanaoongea ni wanaume peke yake. Tunaomba wanawake nao waongee tafadhali.
Jambo la nidhamu Bw. Spika. Kuna kitendo kimetokea cha kuwapiga akina mama na kimeanzia hapa Bungeni. Ninaomba utusaidie. Hapa Bungeni tuliambiwa sisi ni endangered species. Leo kuna kitendo kimetokea Bungeni ambapo Wajir County Wo Representative Fatuma Gedi amepigwa na mwanamume mwingine. Kama kitendo hiki hakikanywi vikali sisi wengine tutapigwa.
Jambo la nidhamu Bw. Spika. Yangu ni machache. Tukiwa katika Bungewatu wanauliza maswali na yanajibiwa. Hayo ni maswali yanayohusu nchi yetu ya Kenya. Lakini mtu kama Mhe Duale alisema kwamba bomu sizilipuliwe kule Eastleigh lakini zilipuliwe kule Machakos; nataka kumuuliza kama Machakos haina watu? Nataka afahamu kwamba ina watu! Ni lazima asimame atueleze ile bomu alisema igonge Machakos
Jambo la nidhamu mhe Naibu Spika. Niliuliza taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi. Kwa muda mrefu hajakuwepo. Hivi leo nimemwona. Ni matumaini yangu kwamba nitapata taarifa hiyo mapema iwezakanavyo kesho. Hii ni kwa sababu najua huenda pengine akawa bado ana maruweruwe ya kule alikotoka.
Jambo la nidhamu Mhe. Naibu Spika. Ningependa kukuelezea kuhusu kitu ambacho kinaniwasha sana.
Jambo la nidhamu mhe. Spika. ingawa wamenipatia wadhifa wa Kiranja hapa Bungeni siwezi kuwa Kiranja na nikubali matamshi ambayo hayawezi kuthibitishwa. Wataita wameonewa hata wakati huu. Siwezi kuunga mkono hata mtu mmoja kwa sababu hakuna Mtaita hata mmoja ambaye amepewa wadhifa. Kwa hivyo siwezi kuunga mkono na hamna
Jambo la nidhamu Mhe. Spika. Kuna mpangilio ambao haueleweki vizuri katika Bunge hili kwa sababu unatoa fursa ya kuzungumza kwa Wabunge wa mrengo wa Jubilee upande huo na upande huu. Baadhi ya Wabunge wa mrengo wa Jubilee wakiona umetoa fursa upande huo huvuka upande huu ili waweze kupata fursa ya kuzungumza. Tafadhali lishughulikie suala hili.
Jambo la nidhamu mhe. Spika. Nimesimama nikukumbushe tu kwamba ndani ya Bunge hili kuna wabunge akina mama maanake tumeona mtiririko wa wabunge wenzetu; kufikia sasa kama kumi wameongea na akina mama tumebonyeza lakini hatujapata nafasi. Asante.
Jambo la Nidhamu mhe. Spika. Ningependa kuwajulisha kwamba hata ukienda katika nyumba za kuhifadhia maiti utaona ni watu wapi wamekufa wengi leo. Pia ukienda jela utaona ni nani wako wengi. Hata ukiangalia wezi utaona ni akina nani wako wengi. Ukiangalia hata kanisani utaona ni akina nani wako wengi. Kwa hivyo sio kupenda kwetu mtuwie radhi.
Jambo la nidhamu Naibu Spika wa Muda. Kulingana na wakati inaonekana ya kwamba wengi wetu hatutapata fursa ya kuchambua Hoja hii. Ningeomba dakika zipunguzwe mpaka dakika tatu.
Jicho la Spika sasa limemuangazia Mhe. Mohamed. Wakati ni wako Mhe. Mohamed.
k Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Vile nilivyotangulia kusema ningetai sana nione ile nguvu wenzetu wa Seneti waliitumia kwa kujadili Kshs316 bilioni na vile zitagawanywa katika kaunti zetu. Wangetumia nguvu hizo kupigana na ufisadi ambao unaendelea katika magatuzi yetu. Walitumia nguvu nyingi sana lakini wenzangu wengi wameongea kwamba wakati mwingi kuna ufujaji wa pesa sana katika magatuzi yetu. Wenzetu wa Seneti hawajatumia nguvu ile kuangalia na kutilia maanani kwamba pesa zinazoenda kwa magatuzi zimetumika vyema. Kwa haraka tu ningependa kusema hivi. CRA ambayo imeleta formula hii ambayo ilipelekwa kwa Seneti na leo hii Seneti wakajadili ikaja kwetu imeongea juu ya mambo ya kilimo. Hizi takwimu za mambo ya kilimo zinasukuma nje sana serikali gatuzi ambazo hazijabobea kwa mambo ya kilimo. Kama vile wenzangu wamesema kuna serikali gatuzi ambazo zinategemea uvuvi wa samaki. Kuna serikali gatuzi pia kama Taita Taveta kule nitokako ambako hatuwezi kilimo kwa sababu ya shida tulizonazo dhidi ya wananchi na wanyama wa pori. Wakati wanaweka takwimu ya juu kwa mambo ya kilimo sisi ambao hatuwezi kufanya kilimo kwa sababu ya shida hizi za wanyama wa pori inatudhulumu. Pili sisi ambao tunakaa mahali ambapo maji haijatajwa katika takwimu hii tunaumia. Sababu ya kutokuwa na maji ndio inafanya wengine wetu ama wale tunatoka kwa kimombo ASAL tunashindwa kufanya kilimo ama maendeleo mengine. Kwa hivyo Seneti na CRA ingetilia mkazo mambo ya maji kuliko kilimo. La mwisho ni mambo ya afya. Wengine wetu tunajua kwamba kuna zahanati za afya ambazo zimebobea sana katika serikali gatuzi nyingi. Kuna serikali gatuzi ambazo ningetaka kusema kama mahali Mhe. Shaban anatoka wananchi wengi hawaendi hospitalini kwa sababu hazina vifaa madawa na miundo msingi mhimu ya kusaidia watu wetu. Inabidi wavuke waende nchi jirani. Wakisema idadi ya watu wanaotembelea zahanati watu wengi ambao wanatoka nchini kwenda nchi jirani hawachukuliwi maanani. Tunapoteza idadi ya watu ambao wanatembelea zahanati kule nyanjani. Watu wengi hawaendi hospitali zetu. Kwa hivyo fomula hii iliyotumika inadhalilisha maeneo ambayo yamebaki nyuma miaka nenda miaka rudi. Kama tunaunga mkono ni vizuri ziende katika kumbukumbu za Bunge kuwa CRA ikishirikiana na Bunge la Seneti ni muhumi wachangamkie takwimu walizozitumia. Nyingi kati yazo si takwimu ambazo zina uhakika. Mfano ni wakati CRA ilileta fomula ya mambo ya kutengwa. Walitumia takwimu ambazo nilipinga na nikaketi na Commissioners wa CRA na wakaona takwimu hizo walizotumia si nzuri ama hazikua sawa. Waliweka maeneo mengine kuwa yalikua yamebobea. Ilibidi watembee kudhibitisha kuwa hawakutumia takwimu sawa. Naunga mkono lakini nitasema ni vizuri tuchunguze kwa undani takwimu zinazotumiwa kwa sababu tukiendelea hivi nchi yetu itabaki kuwa kwingine kutaendelea na kwingine kunabaki nyuma. Najua saa zimeisha lakini kuna pesa nyingi ambazo zinabaki katika Serikali kuu. Ni vyema kama Bunge la Kitaifa tunapojadili Bajeti ama Bajeti-nyongeza itakapoletwa iletwe hesabu ya kweli kuonyesha pesa zinazobaki katika serikali za kitaifa zinatumika vipi. Kuna miradi mingi katika maeneo fulani na maeneo mengine yanabaki kuwa maskini. Naunga mkono. Ahsante sana Naibu Spika wa Muda.
Kabla hujaniambia mambo ya leadership kutoka jana mpaka leo hii kadi yangu imekuwa ikiwaka na hali sijapewa nafasi ya kuongea. Nitapewa lini mimi nafasi ya kuongea ndani ya Bunge hili?
Kabla sijatamatisha asante sana Mambo ya jinsia ni ya maana sana Wakati kutakuwa na usawa katika utekelezaji wa mambo haswa ya kiserikali hilo naunga mkono Wakati Katiba hii imesema tukumbuke akina mama wetu au jinsia hiyo naunga mkono Haya ni eno ambayo yataleta maendeleo Hata kama huenda Katiba isiwe mia kwa mia kwa nini tusiiunge mkono kama imefika tisini kwa mia au sabini kwa mia? Mimi naunga mkono
Kama hatutawalipia watu hao gharama za matibabu katika hospitali za umma za rufaa watazidi kukaa katika vyumba vya kuhifadhia maiti. Kama nchi ya Kenya tutazidi kujenga vyumba vya kuhifadhia maiti na hatutakuwa nchi tukufu. Kwa hivyo tunataka kufanya yale mambo ambayo yanatakikana katika Hoja hii. Namshukuru Mhe. Mohamed Ali kwa kuileta Hoja hii. Sisi sote tunaunga mkono kwa sababu tunataka kuwasaidia watu wetu. Asante Mhe. Naibu Spika.
Kama nilivyokuwa naelezea swala lililoko mbele yetu ni la vijana na akina mama. Kwa hivyo kuna umuhimu vijana kuwa wengi katika hizo kamati kinyume na vile ilivyokuwa wakati wa mipango ya kamati za wanaoishi na virushi vya ukimwi. Utakuta wanaoshiriki katika swala hilo la wanaoishi na virushi vya ukimwi katika kamati hizo zote hakuna hata mmoja anaugua ukimwi. Ni jambo la kusikitisha. Lisiwe hivyo basi.
Kama utaniruhusu ningependa kutoa rambirambi zangu kwa jamaa na marafiki wa Gavana wa Nyeri. Mimi na watu wa Kaunti ya Lamu tunasema pole. Pia Lamu tumekuwa na mkasa mdogo na ningependa kutoa rambirambi zangu. Kuna mgonjwa wa akili aliyekuwa anatembea msituni. Maafisa wa KDF walimpiga risasi kisha wakaandika wameua gaidi wa Al-Shaabab . Tunatoa pole na tunaomba wahusika waombe msamaha kwa sababu familia ina uchungu sana na sisi kama viongozi wa Lamu tunajaribu kuweka jamii na maafisa wa usalama wawe karibu na wasiwe mbali sana ili wakiona mtu anapita ambaye hawamjui wapeleke habari. Hata hivyo mambo haya yakiendelea kwamba watu ambao hawana hatia wanauawa hiyo chuki inaendelea na hata wakiona wahalifu hawawezi kusema. Haya mambo ya pension in mazuri na itasaidia maana hata tunaogopa. Kila anayesimama anatupatia mfano wa kusema wale waliokuwa hapa na sisi ni wageni tumeingia. Tunaogopa na tumeingiwa na uoga tusije tukatoka hivi hivi na ukiona mambo yanavyoendelea hali saa hii ni ngumu na mishahara imekatwa. Tunafikiria kwenda kuvaa badge turudi kwa kurusha ndege au kufanya kazi zingine. Hata hivyo naona muda hautoshi. Tunafaa tuhudumie jamii. Kwa hivyo mimi ninaunga mkono sana mambo haya ya pension . Sijui pension kwa Kiswahili. Asante.
Kassim (Matuga ANC): Asante sana Bw Mnenaji kwa sababu katika Kiswahili sanifu Spika anaitwa mnenaji Kwanza natoa pongezi kwa Mhe King'ara kwa kuleta Mswada huu ambao utaweza kusawazisha donda sugu hasa kwa mimi Mbunge wa Matuga Ni wiki iliyopita tu ambapo niliitwa katika shule moja inayoitwa Bombo pale Kiteje Kuna bwenyenye mmoja ambaye alikuwa ameweka ua kwenye afisi ya mwalimu mkuu akidai kuwa iko kwenye shamba lake Hii ni shule ambayo imekuwa pale kwa zaidi ya miaka 30 Hali kadhalika imenibidi kutoa pesa za National Government-Constituency Development kujenga afisi ya Chifu Kwambani ambayo imekaa pale kwa zaidi ya miaka 20 lakini sasa hivi kuna bwenyenye amekuja na kuweka ua pale akidai ile ardhi ni yake kibinasfi Natoa pongezi Mswada huu uungwe mkono na upitishwe ili mali ya Umma ipate kutetewa vilivyo Asante sana
Katika historia ya Mhe Millie Odhiambo nakumbuka wakati alitembea bila viatu Mhe Naibu Spika wa Muda kuna ushahidi katika Chuo Kikuu cha Maasai Mara ya kwamba kile chakula kinaitwa ngumu ama KDF kinawekwa dawa za kulevya na bhangi na kinauziwa watoto pale mitaani Ndio sababu nilikuwa nikisema kuwa saa zingine wale walio chini wanafanya watu wakuwe waraibu wa kutumia ngumu na KDF Wanaendelea kuwa wachochole kwa sababu wanafanya kazi kidogo na ile pesa kidogo wanapata wanaitumia kununua dawa za kulevya Watoto wa matajiri ndio wako na pesa ya kununua dawa za kulevya za bei ya juu na ndio wanaumia zaidi Ndio sababu sisi wote kama wananchi wa Kenya na Wabunge ambao ni wawakilishi wa watu wote tunaunga mkono huu Mswada Asante sana Mhe Naibu Spika wa Muda
Kiongozi wa Wachache Bungeni anaongea kuhusu nzige lakini ameendelea kuongea kuhusu ya afisi ya Naibu wa Rais. Sioni vile hao nzige wanahusiana na afisi ya pili.
Kisha kejeli ya Katiba kama alivyosema mwenzangu hatujakejeli Katiba kwa sababu tuko katika Jumba hili kutunga sheria na wakati mwingini huandikwa hufutiliwa mbali na kuandikwa tena upya kwa ufaa ya wananchi wa Jamhuri ya Kenya. Sera za afya nchini Kenya ni za kitaifa.
ko (Wundanyi WDM-K): Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Sitasema mambo mengi leo kwa sababu mengi yamesemwa. Nina mambo kama matatu hivi ambayo ningetaka kusema. Kwanza naunga mkono mjadala huu kwamba sheria ya tatu ambayo imepitishwa na Seneti tuiunge mkono kama Bunge la Taifa. Haya yaliyojadiliwa ndani ya Seneti kwa muda mrefu yalitatiza sana shughuli katika kaunti nyingi hapa Kenya. Nilitai sana nguvu ile wenzetu wa Seneti...
Kuaga dunia ama kuachana na sisi tukiwa hapa dunia. Wakiaga dunia inakuwa gharama kubwa sana kupeleka miili yao kuzikwa. Tunaomba Serikali kwa sababu sisi ni mali yake itushughulikie wafutilie mbali ada hii ili itusaidie kupeleka watu wetu kuzikwa. Nilikuwa na hayo. Tunaomba turuhusiwe tuongee Kizungu.
Kulingana na mnyambuliko wa vitenzi yeye ameongea Kiswahili sanifu. Kufanya is a synonym . Yaani alisomea halafu akahitimu na akapata alama ya "A" katika somo la Kiswahili.
Kumalizia ninaomba kuunga mkono huu Mswada na yale yote tuliyoyazungumza hapa ama tuliyojadili yaweze kutiliwa maanani. Kwa wale ambao wanahusika pia waweze kuyasikia na kuyatilia maanani tuone vile ambavyo tunaweza kuokoa maisha ama pia kuokoa vijana wetu katika ajali zile ambazo zinaendelea katika barabara zetu. Naunga mkono huu mjadala. .
Kumbe imekuwa NASA sio CORD. Ningesema hivi ni muhimu tuangalie kile kitu ambacho kitawasaidia wananchi wa Kenya. Mhe. Wamalwa amesema kwamba kuna temperature. Nani amepima akatuambia temperature inapimwa namna gani? Pili sijui kama yeye ni daktari. Ni vizuri mnisikize. Hiyo temperature kama iko Kenya inaletwa na NASA. Kila mtu anajua hivyo. Kwa hivyo wakitaka wateremshe hiyo temperature kwa sababu wao ndio wanaoleta temperature humu nchini.
Kuna haja ya sisi kama Wakenya na Serikali kujifunza kutoa shukrani kwa watu ambao wamefanya kazi na watu ambao wanasaidia kwa hali kubwa kuhakikisha na kuendeleza maswala ya maendeleo kwa Jamhuri ya Kenya. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa hayo eno machache ningependa kuunga mkono Hoja hii. Asante.
Kupitia kwa Kanuni za Kudumu Nambari 44(2)(c) naomba Jawabu kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira kuhusiana na mjengo unaondelea sehemu ya Forodhani Old Town na majengo ya maghorofa yanayokusudiwa katika eneo la Buxton yote yakiwa katika eneo la Mvita Kipengele cha Tano cha Kanuni ya 12 katika Ratiba ya Tatu ya Sheria za shirika la National Environment agement Authority (NEMA) kinakubali ripoti ya athari ya mazingira kwa jambo lolote linaloathiri mazingira na binadamu Kwa sasa mipangilio hii inaathiri wakaazi wa maeneo hayo ikiwemo ugurushaji na majumba jirani kuathirika Kupitia hayo ningeomba masuala matatu: (1) Je ripoti hii ya NEMA ilifanywa kweli katika sehemu hizi? (2) Je wakazi walijulishwa wakati NEMA ilipokuwa inafanya ripoti hii na ni lini maana wakaazi wenyewe hawakuhusishwa katika eneo la Old Town wala Buxton? (3) Je Wizara itachukua hatua gani kwa wale maafisa husika ambao hawakufuata sheria kutoka shirika la NEMA?
Kwa haraka nitapitia suala la Katiba. Sio wengi walipata kuifahamu Katiba. Kwa haraka tuliipitia na kuipitisha. Laiti wangejua yale madhara ambayo yangewakumba kama yanavyotukumba siku ya leo Katiba hatungeipitisha kamwe. Tungeisimamisha tuirekebishe kisha tuipitishe. Miezi michache iliyopita katika sehemu za magharibi ya nchi hii kuna bunge lililopitisha kwamba watu ambao wamefuga kuku na paka watozwe ushuru. Watu walilalamika ilhali wao walikuwa wanatekeleza yaliyomo katika Katiba. Vile vile walipitisha Katiba bila kufahamu kwamba nyumba wanazolala ndani zitatozwa kodi. Hilo likitendeka nina hakika Wakenya wote watalalamika. Hivyo basi kuna umuhimu sana wa kuhakikisha kwamba Katiba na sheria zote za nchi zinatafiwa kwa lugha ya Kiswahili na kwa lugha nyepesi. Nikiwa mtaalamu wa lugha hii ya Kiswahili niko tayari kushughulika katika harakati hiyo ya kutafi Katiba na pia sheria za nchi. Naunga mkono.
Kwa hayo machache ninaiunga mkono Hoja hii ili masuala ya usalama yaweze kupewa uzito unaostahili.
Kwa heshima nimeondoa hiyo Mhe Naibu Spika wa Muda kwa sababu uko hapo Ya mwisho wale ambao wameumia sana na hizi dawa za kulevya sio matajiri ni wale ambao tunaita hustlers ambao ni watoto wa maskini Mhe Naibu Spika wa muda nilinde kutoka kwa Mhe Ichung'wah
Kwa hivyo ninaunga mkono na ningeomba kwamba baada ya kupitisha Hoja hii basi kila kitu ndani ya Bunge hili kitafiwe kwa lugha ya Kiswahili. Vile vile Serikali ihakikishe ya kwamba inapeleka walimu katika kila kijiji na iwe ni lazima kila mtu afundishwe Kiswahili. Jambo hili litafanya watu kujua haki zao na kujitetea
Kwa hivyo unakosa kuelewa vile Mheshimiwa anataka kujieleza. Mhe. Wairimu nafikiri ako sawa.
Kwa hoja ya nidhamu Bw. Spika. Ningependa kuzungumza kwa lugha ya taifa ambayo ndugu yangu mhe. Wario ametumia. Katika mjadala wake ambao anaouzungumzia kwanza ni kuwa lawama haiko kwa Erad lakini kwa NCPB. Ile hisia ambayo anaileta kwa Bunge hili na katika Kenya nzima ni kuwa ripoti hii inaisafisha NCPB ambayo sio ukweli wa eno. Katika eno yake ambayo nimemkatiza sasa hivi
Kwa Hoja ya Nidhamu Mhe. Naibu Spika wa Muda. Tukizungumzia suala la maji kwanza ningependa kusaidia Wamaasai
Kwa kusema ukweli Mhe Tandaza Sawa ametandaza habari za mrangi huu kweli kweli
Kwa majina naitwa Captain Ruweida Mohamed Mbunge wa Kike was Kaunti ya Lamu Kwa sababu tunaongezwa milioni 400 hizo pia ni pesa Kwa niaba ya watu wangu wa Lamu Rais wetu mpendwa Uhuru Muigai Kenyatta na Gideon Moi napiga kura ya ndio
Kwa majina ninaitwa Zainabu Chadzuga kutoka Jimbo la Kwale. Sijazungumza kuhusu Hotuba ya Rais!
Kwa mfano ardhi ya Kaya . Kwa hivyo ninayapinga vikali mabadiliko haya.
Kwa niaba ya watu wa Balambala napiga kura yangu ya ndio
Kwa niaba yangu na watu wa Kilifi South nachukua nafasi hii kutoa rambirambi zangu za dhati kwa jamaa na marafiki wa mwenda zake Rais Moi. Ninakumbuka msemo mmoja wa mzungumzaji Albert Einstein. Alisema kwamba mtu ambaye hajafanya kosa ni yule hajajaribu kufanya kitu chochote. Kwa hivyo katika mazungumzo yake mheshimiwa aliyeenda zake alisema yuko tayari kusamehe mtu yeyote aliyemkosea na yeye pia akaomba msamaha kwa aliowakosea. Nina ii maombi hayo yametufikia. La mwisho ni kwamba Rais wetu ameenda akiwa na ndoto ambayo haijatimia. Alianzisha mpango wa kutengeneza gari. Ameenda kama ndoto ile haijatimia. Tusipate laana wala dua tuhakikishe Wakenya tunaendeleza ndoto hiyo.
Kwa niamba ya watu wa Kinango na Kwale kwa jumla napiga kura ya ndio
Kwa sababu nazungumzia jambo nyeti. Itakuwa bora tukipitisha sheria kuwa pesa zote zinazokusanywa katika makaunti ziwe zikiwekwa na Serikali mahali fulani. Hizo pesa zitakuwa ni zao tu lakini tujue zile wataongezewa na zile wamekusanya ni ngapi. Bila kufanya hivyo tutazungumza mengi na tutaendelea kuwa na shida kubwa. Kwa hivyo ninaunga mkono huu Mswada lakini tuweke mikakati ya kutosha ili tuweze kujua pesa ambazo zinatozwa ushuru ni ngapi. Tunasikia kwamba hata zingine haziwekwi kwenye akaunti ya kaunti. Hizo pesa zinapatiwa mawakala ambao wanakusanya hizo pesa. Baadaye hizo pesa hazirudi kwa wananchi hata kidogo. Hayo ndiyo maoni yangu na ninashukuru kwa kuniongezea muda.
Kwa sasa nimesema ninakubaliana ikiwa taratibu zitafuatwa. Wakienda kinyume nimeikataa hiyo otomatiki juu kwa juu.
Kwa unyenyekevu muda wangu umeliwa kidogo Naomba dakika mbili niweze kutamatisha
Kwanza nataka kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipatia uongozi kwa sababu kiongozi anatoka kwake. Pili nataka kuwashukuru wananchi wa Tana River kwa kunichagua kuwawakilisha. Kweli hayo mashindano yalikuwa magumu sana hasa kwangu mimi ambaye natoka jamii ndogo ambayo inaitwa Wailwana. Ninajua hata hamjawahi kusikia jina kama hilo; ni mara yenu ya kwanza. Namshukuru Mhe. Raisi kwa sababu alitupatia nambari yake wakati alipokuwa akisajili Wamakonde ingawa hatukuwa kwenye gazeti la Serikali. Hatukujiona. Namwomba bado ajaribu kufuatilia hilo jambo ili nasi tupate hiyo nambari ndiyo tuweze kutambulika. Pia namshukuru Rais kutokana na Hotuba yake ya jana. Nimeona hakika tuko na Rais ambaye anapenda wananchi wa Kenya. Wakati uamuzi ulipokuwa ukisomwa nilijifungia nyumbani na nikaanza kuomba 'Yarabi Mungu tusaidie yasije tena yaliyopita.' Kwa hivyo nimeona huyu Rais wetu ni mpenda wananchi wake kwa sababu si rahisi uwe mshindi kisha uambiwe eti wewe si mshindi. Nilikuwa nimeona vita mimi. Nilisema 'Haya tutapigana tena!' Lakini Mungu aliyasikia maombi yetu maana nina uhakika Wakenya wengi waliomba na Mungu akawasikiza. Kutokana na hiyo Hotuba ya Rais ya jana hata mimi nataka kurudia alichosema Mhe. Ali Wario. Kuna mambo tuliyoahidiwa hata nilitarajia pengine angeyataja lakini sikuyasikia. Mimi nitarudia jambo la ukame. Sisi tuko na mto lakini umekauka. Wananchi wengi saa hii wanakufa kutokana na njaa na kiu. Hata niliona jambo la kusitikisha. Kwangu ni Madogo. Ninaposafiri kuja Nairobi sehemu ya Banga ninawapata watoto wadogo wakiwa na chupa ndogo ndogo wakiomba maji njiani. Wanaomba watu ambao hawajui maji ya kunywa. Wale watoto wako katika hatari kwa sababu wanaweza kutiliwa madawa ya kulevya kwenye yale maji kwa sababu huwezi ukajua adui wako ni nani. Mimi bado naomba na kutilia mkazo ili Rais atakapokaa akipanga mambo yake asisahau wananchi wa Tana River. Tuko na shida na tunahitaji maji tena kwa haraka iwezekanavyo. Kulingana na Hotuba hiyo wengine waliotangulia waliuliza ni kwa nini Mheshimiwa Rais hakusema maendeleo aliyotupangia. Wakati uko kwa vita huwezi kukumbuka kupanga. Unakumbuka tu kupanga silaha utakayopigana nayo. Kwa hivyo wananchi wa Kenya ni lazima tumuelewe Mheshimiwa Rais. Ako na vita. Saa hizi anajipanga kwa sababu ya vita kwa sababu ni lazima Mungu akipenda tarehe 17 Oktoba ashinde. Na sisi tutamuunga mkono kuhakikisha ameshinda na atuongoze alivyotuongoza hii miaka mingine iliyopita. Kwa kuongezea tupende kudumisha ai. Vita havitusaidii. Tuwe watu wa kukubali ushindi. Utakaposhindwa kubali. Kenya ni muhimu kuliko mimi na wewe. Ahsanteni.
Labda tama ndio itakuwa nzuri na Bunge la Kumi na Moja nitakuwa hapa Inshallah. Bw. Naibu Spika wa Muda napenda kuichukia nafasi hii kukishukuru chama cha National Muslim Leaders Forum (NAMLEF) wakishiriana na Council of Imams and Preachers of Kenya (CIPK) kwa kuniwezesha kuchaguliwa au kuteuliwa kwenye Bunge
Lakini maadamu utafanya maamuzi nitaangalia kwenye televisheni hivyo hivyo mwenzangu amenieleza. Nawasihi wabunge wenzangu waangalie kwa kikamilifu jambo hili. Sheria hazibadilishwi tu ili kupendekeza majina fulani. Chama cha ODM vile ninavvojua kitaendelea kusisitiza kuwa majina haya haya ndiyo yatakayoletwa tena. La mwisho hatujui ni akina nani watarudi kushughulikia haya mambo. Nakubaliana na Mheshimiwa Duale kuwa kuanzia kesho masilahi yake yatakuwa kuangalia kuwa amerudi hapa. Haya mengine kwake ni mzigo ambao hataki kubebana nao. Naomba nikunje jamvi kwa kusema hivi: tusigeuze sheria ili kubinafsisha watu fulani. Labda wengine wenu mnataka tuzigeuze ili msipo bahatika kurudi basi majina yenu yaingizwe. Hata mimi naambiwa labda huenda nataka hivyo hivyo. Lakini kauli yangu nishaiweka wazi kuwa nagombea kiti cha gavana na wenzangu wananitakia kila la heri. Hata Mheshimiwa Duale amenitumia ujumbe akisema ananitakia mema. Anasema eti angekuwa mpigaji kura katika kaunti yangu angenipigia kura. Kwa hivyo sikubaliani na hii ripoti ya kamati. Ni ombi langu kuwa Bunge lisiikubali. Ahsante Mheshimiwa Spika.
Langu ni kupongeza Mheshimiwa wa Nyali Mhe. Mohamed Ali kwa kuleta Hoja hii Bungeni. Ningependa pia kukosoa kidogo.
Leo tuna changamoto ya vipasa sauti. Utatumia kipasa sauti ambacho kiko mbele yangu.
Mama Rais Suluhu ni mama aliye na unyenyekevu na ni mwakishi kwa wamama wote ambao ni viongozi katika Afrika Mashariki na dunia nzima Tunampa pongezi Nimefurahia sana Na tunaomba arudi tena Mwisho tunampatia Rais wetu mpendwa Uhuru Kenyatta hongera kwa kumpokea jirani Rais Bi Suluhu Asante sana
Mambo mengine ni yangu mwenyewe. Mambo mengine hata nikisema ni ya undani ni yangu mwenyewe na ni i yangu. Lakini ni mtu namjua ako na uzoefu wa kazi hana shaka kwa kazi ya Serikali na hata kazi zinginezo. Kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu katika Bandari ya Mombasa. Anatuwakilisha vilivyo bila tashwishi. Kwa hivyo naona ametosha kuwa katika Tume hii. Naiunga mkono Riporti hii.
Messrs Gethenji Baiya Abass Abdinoor Aden Farah Nooru Oyugi Dido Wario; Chae; Lentoimaga; B.N. Nyaga; Messrs Shinali Kitungi Ganya Njagagua Nakuleu Wambugu Anyango Gikaria Bowen Losiakou; Ghati; Messrs J.K. Chege Ngare; F.I. Ali; F.K. Wanyonyi; Kajuju; Messrs Njenga Ogalo; Duri; Messrs Os Kiptanui Rop Ekomwa Murgor; Teiya; Messrs Omagwa Kihagi Serut Waiganjo Sakaja M'uthari je; Dr.Laboso; Messrs Kemei KabandowaKabando Murungi Okoth A.B. Duale Sang Muluvi; Otucho; Mbugua; Seneta; Munene; Onyura; Odhiambo-Mabona; Messrs Huka Mohamed Abdi Lessonet; Dr.ShabanKoinange; Tobiko; Messrs Mwangi Shehe; R.K. Nyamai; Shebesh; Amolo; Letimalo; Changorok; Dr.Pukose; Mumo; Messrs Bunyasi Chepkong`a Ndiritu Anami Karani Mule; Chebet; Musyoka; Boe; T.G. Ali; Messrs Kisang Cheruiyot; Kering; Juma; Muia; Muhia; Messrs Mirenga Nakara; Korere; Messrs Alfred Keter Serem; Ngeny; C.M. Nyamai.
Messrs Odanga Midiwo Rai Mwamkale Kombe Mwanyoha Wakhungu Robi Maweu Mustafa Mwaura M.D. Duale J.O. Omondi Wandayi; Tuya; Messrs Injendi J.K. Bett Chea Nanok; Eng. Gumbo; Messrs ole Ntutu Wangamati; Prof.Nyikal; Messrs Katoo Opiyo Mwadime Rotino Akujah Kipyegon Karithi Kimaru Simba Koyi Makenga Tongi Mbui Lagat Tonui Lempurkel ole Kenta Mwaita Magwanga Gichigi Andayi Onyango Mulu Kangara Ababu Kajwang Abongotum Mwadeghu Nderitu Wetangula B.K. Bett; Dr.Munyaka; Messrs Wamunyinyi Korir Keynan Ichung'wah H.K. Njuguna Moi Kaluma Mwashetani Lomunokol
Messrs. Elmi Midiwo Katoo ole Kenta Gethenji Baiya J.O. Omondi P.E.O. Anyanga Wandayi A.B. Duale Dido A.T. Anyanga Washiali Otsiula Bowen Ochieng J.K. Chege Ngare Waititu Ferdinard Nderitu Njenga Outa Ogalo Kiptanui Teiya Messrs Olum Kihagi Kariuki Ndirangu Koyi je Magwanga Njomo Kanini Kega Murungi Mohamed Abdi Cheboi Musyimi Eng. Gumbo Messrs. Letimalo Mwaita Ndiritu Karani Mwadeghu Boe Dr. Otichilo and Opore. Dr. Simiyu Messrs Elmi Katoo K.K. Kinyanjui Lati Gethenji Baiya A.O Ahmed A. B. Duale Dido Abdalla Messrs Kangara Wambugu Karithi Wekesa F.I. Ali Messrs Dukicha Banticha Teiya Omagwa Dr. Laboso Messrs Nuh Keynan M.D. Duale Mohamed Abdi Dr.Shaban Kanyua Shebesh Duba Dr. Pukose Messrs Gichigi Gure Messrs oti Wetangula and Opore Dr. Simiyu Messrs Elmi Katoo K.K. Kinyanjui Lati Gethenji Baiya A.O Ahmed Nooru A. B. Duale Dido Abdalla Messrs Kimaru Kangara Wambugu Wekesa F.I. Ali Messrs Dukicha Banticha Teiya Omagwa Dr. Laboso Messrs Nuh Keynan M.D. Duale Mohamed Abdi Dr.Shaban Messrs. Ole Ntutu Kanyua Shebesh Duba Dr. Pukose Messrs Gichigi Isaack Gure Messrs oti T. G. Ali Messrs Opore
Messrs. Njagagua Mukwe Prof. Nyikal Machira Wanyama Messrs. Gimose Wakhungu Omagwa Katana Dr. Simiyu Abdalla Messrs Wekesa Were Moindi Wangwe Wa Kabando Mohamed Abass Moyi Muluvi Lomunokol Onyura F.K. Wanyonyi Shinali Injendi Mati Mwamkale Gaichuhie Nyenze Aluoch Musimba Wangamati Tobiko R.K. Nyamai Bishop R. Mutua Messrs. Otaalo Oyugi Kinoti Theuri Mule Kariuki Stephen Chebet Messrs. Chea Dukicha T. G. Ali Wamunyinyi Chepkwony Messrs. Kisang Chanzu Chidzuga and Mustafa. Wahome Messrs Kilonzo Nderitu Nyenze Ogalo G.W. Omondi Kariuki Stephen Mungaro Kipchoim Messrs Oyoo Simba Murgor Prof. Nyikal B.N. Nyaga Opiyo Mbalu Messrs Mulu Kipyegon J.M. Nyaga Koyi Mlolwa J.K. Ng'ang'a Oyugi Magwanga B.K. Bett Kinoti Wa Kabando Mbarire Sang Keraa Messrs Onyura Kisoi Linturi Njagagua Wakhungu ole Sakuda Ombaka Eng. Gumbo Dr. Oginga Messrs Musimba ole Ntutu Omulele R.K. Nyamai Messrs Alfred Keter Otaalo Anyango Bowen Nyamunga Messrs Sambu Ochieng Ndiritu Losiakou Ogari Mule Midiwo Kaluma Mwadeghu Boe J.K. Chege Dr. Munyaka Dr. Ottichilo W.K. Njuguna Cheruiyot Ngeny and Kering. Messrs Nderitu Messrs Kilonzo Nyenze Ogalo G.W. Omondi Kariuki Stephen Mungaro Kipchoim Messrs Mwanyoha Midiwo Oyugi Murgor Oyoo Simba Murgor Prof. Nyikal Machira Messrs Simba Opiyo Mbalu B.N. Nyaga Messrs Kipyegon Waluke Mlolwa Messrs J.K. Ng'ang'a je Magwanga Mulu Alfred Keter Wa Kabando B.K. Bett Sang Keraa Munene Messrs Onyura Kisoi Odhiambo- Mabona Messrs Linturi Kinoti Mbarire Messrs Ole Sakuda Njagagua Eng. Gumbo Dr. Oginga Musimba Wakhungu Ombaka R.K. Nyamai Messrs Omulele Otaalo Sambu Anyango Nyamunga Messrs Bowen Ochieng Losiakou Ogari Mule Eng. Kiragu Kaluma Mwadeghu Boe Ngeny Wahome Dr. Munyaka Dr. Ottichilo M.W. Njuguna Cheruiyot Kering.
Messrs. ole Metito KK. Kinyanjui ole Kenta Gethenji Abdinoor Farah Nooru A.B. Duale and Dido Wahome Messrs. Letoiga Odera Shill Langat Mutura Gikaria Bowen Pkosing Wekesa and Waweru Dr. Laboso Messrs. Busienei Nderitu Waititu and Rai Kipchoim Kiptui Messrs. Dukicha Kiptanui Rop Murgor and Kamau Teiyaa Messrs. Kipyegon Kihagi Njoroge Nyaga Melly Abongotum and Kanini Kega Korere Messrs. Robi Huka and Mohamed Haji ole Sakuda Cheboi Njuki Letimalo Koech Mwaita Gichigi Tiren and Karani Sunjeev Messrs. Kipkemoi Cheptumo Sang Serem Gitari Gathecha Wanyama and Changorok Order.
Messrs. S.A. Ali Midiwo ole Metito Kosgey Lati ole Kenta Gethenji and Baiya Mwendwa Messrs. Omondi Wandayi and Kaluma Tuya Messrs. Mohamed Abbass Abdinoor Aden A.O. Ahmed Dawood Farah Nas A.B. Duale Oyugi A. Keter Masadia Sambu and Dido Wahome Messrs. Letoimaga Abdalla Messrs. Mwadime and Toboso Nyokabi Messrs. Simba Savula and Shill Nyaga Messrs. Moyi Shinali Washiali Langat Mutura Kitungi Bett and Bishop Mutua Mbarire Ganya Gimose Wamalwa and Nakuleu Ombaka Omulele Cpt. Wambugu Messrs. Serem Iringo Anyango Kazungu Maanzo Bowen Karithi Kiaraho Ochieng Pkosing Wekesa Were and Waweru Ghati Dr. Laboso Messrs. Lagat Wangwe Busienei Kiragu Ngare and E. Keter Mathenge Ngeny F.I. Ali Wanyonyi Mutua Kajuju Messrs. Nderitu Nyenze Waititu Odanga Ogalo G.W. Omondi Muchai Theuri Kariuki Irea Konchella Mungaro and Ochanda Wanga Rai Kipchoim Duri Messrs. Kombe Mwanyoha Os Chepkwony Saney Abass Sane Mwaura Kiptanui Rop and Macharia Banticha Messrs. Gakuya and Mukwe Dr. Gesami Kimaru Dr. Nyikal Teiyaa Opiyo Mbalu Messrs. Angwenyi Olum Kipyegon Serut Waiganjo Kobado Ndirangu Njoroge Nyaga Waluke Sakaja and Mlolwe Maj-Gen. Nkaissery Messrs. Gitari Kiuna Lekuton Limo Lomwa je Magwanga Obiero and Aduma Lay Messrs. Njomo Melly Nuh Kemei Abongotum Mbiuki Obura Okoth Keynan Njuguna Moi Bitok and ole Lemein Korere Messrs. Aramat and Sang Fathia Kada Leshoomo Messrs. Nyamweya Muluvi and Lomunokol Keraa Mbugua Seneta Messrs. Robi Kyengo Onyura and Kisoi Odhiambo-Mabona Messrs. Linturi Huka and Mohamed Haji Eng. Mahamud Messrs. Cheboi Injendi Lessonet Kuria Aburi Mati Musyimi and Chea Ibren Ngikor Eng. Gumbo Messrs. Barua Aluoch Ngunjiri Njuki Otuoma Makau ole Ntutu Koinange Kinyua Mwangi Shehe and Rotino Kanyua Akujah Nyamai Messrs. Letimalo and Otaalo Muia Wanyonyi Messrs. Makenga and Mbui Dr. Pukose Tonui Mitaru Mumo Messrs. Bunyasi Koech Mwaita Gichigi Arama Moroto Isaack ga S.S. Ali Tiren Osele Anami Ogari Karani Mule oti and Murunga Sunjeev Chebet Musyoka Messrs. Wetangula and Ngahu Dr. Munyaka Wamunyinyi Muhia Korir Dr. Ottichilo Messrs. Cheptumo and Kipkemoi Chidzuga Kering and Juma. Messrs. Gathenji and S.A. Ali Mwendwa Messrs. Omondi Wandayi and Kaluma Tuya Messrs. Mohamed Abbass Abdinoor Aden A.O. Ahmed Dawood Farah Nas A.B. Duale Oyugi A. Keter Masadia Sambu and Dido Wahome Messrs. Letoimaga Midiwo Mwadime and Toboso Nyokabi Messrs. Simba Savula and Shill Nyaga Messrs. Moyi Shinali Washiali Langat Mulu Mutura Kitungi Bett and Bishop Mutua Kinoti Mbarire Ganya Gimose Wamalwa and Nakuleu Ombaka Omulele Capt. Wambugu Messrs. Serem Iringo Anyango Maanzo Bowen Kiaraho Ochieng Pkosing Wekesa Were and Waweru Ghati Dr. Laboso Messrs. Moindi Lagat Busienei Wangwe Eng. Kiragu Ngare and E. Keter Mathenge Ngeny F.I. Ali Wanyonyi Mutua Kajuju Messrs. Nderitu Nyenze Waititu Odanga Ogalo G.W. Omondi Muchai Theuri Kariuki Irea Konchella Mungaro and Ochanda Wanga Rai Kipchoim Duri Messrs. Kombe Mwanyoha Os Chepkwony Saney Abass Sane Ole Metito Kiptanui Rop and Macharia Banticha Messrs. Gakuya and Mukwe Dr. Gesami Kimaru Murgor Dr. Nyikal Wanyama Teiyaa Messrs. Opiyo Angwenyi Olum Kipyegon Serut Waiganjo Kobado Ndirangu Njoroge Nyaga Sakaja and Mlolwa Maj-Gen. Nkaissery Messrs. Gitari Kiuna Lekuton Limo Lomwa je Magwanga Obiero and Aduma Lay Messrs. Njomo Melly Nuh Kemei Abongotum Mbiuki Obura Okoth Keynan Njuguna Moi Bitok and ole Lemein Korere Messrs. Aramat and Sang Fathia Kada Leshoomo Messrs. Nyamweya Muluvi and Lomunokol Keraa Mbugua Seneta Messrs. Robi Lati Onyura and Kisoi Odhiambo-Mabona Messrs. Linturi Huka and Mohamed Haji Eng. Mahamud Sumra Messrs. Cheboi Injendi Lessonet Kuria Aburi Munuve Musyimi and Chea Ibren Ngikor Eng. Gumbo Messrs. Barua Aluoch Ngunjiri Njuki Otuoma Makau ole Ntutu Biii Koinange Kinyua Gitau Mwangi Shehe and Rotino Kanyua Akujah Nyamai Shebesh Messrs. Letimalo and Otaalo Muia Wanyonyi Messrs. Makenga and Mbui Ole Kenta Tonui Mitaru Mumo Messrs. Bunyasi Koech Mwaita Gichigi Arama Moroto Isaack ga S.S. Ahmed Tiren Osele Anami Ogari Karani Mule oti and Murunga Sunjeev Chebet Musyoka Messrs. Wetangula and Ngahu Dr. Munyaka Wamunyinyi Muhia Korir Dr. Ottichilo Messrs. Cheptumo Kipkemoi Chanzu Chidzuga Kering and Ababu. Messrs. S.A. Ali Midiwo ole Metito K.K. Kinyanjui Lempurkel Lati ole Kenta Gethenji and Baiya Omondi Wandayi and Kaluma; Tuya; Messrs. Abdinoor Aden A.O. Ahmed Dawood Farah Nas A.B. Duale Oyugi Alfred Keter Sambu and Dido; Wahome; Lentoimaga; Abdalla; Messrs. Mwadime Toboso; Gethecha; Simba; Nyaga; Messrs. Shinali Washiali Langat Mbai Mutura Kitungi Bett; Bishop Mutua; Kinoti; Mbarire; Messrs. Ganya Geni and Gimose; (Dr.) Wakhungu; Nakuleu; Ombaka; Omulele; Cpt. Wambugu Messrs. Iringo Anyango Kazungu Maanzo Bowen Karithi Kiaraho Ochieng Pkosing Wekesa Were and Waweru Lagat Businei; Eng. Kiragu; Eng. Ngare; Eric Keter; Gathogo Mathenge; Ngeny; F.I. Ali; Wanyonyi; Mutua Kajuju; Messrs. Kilonzo Nderitu Waititu Outa Odanga Ogalo G.W. Omondi Muchai Theuri Irea Konchella Mungaro and Ochanda Rai; Kipchoim; Messrs. Chea Kombe Mwanyoha and Os; Chepkwony Sambili; Messrs. Saney Abass Sane Mustafa Kiptanui and Rop; Banticha; Mukwe; Dr. Gesami; Messrs. Kimaru and Murgor; Dr. Nyikal; Kamau; Wanyama Teiyaa; Opiyo; Mbalu Messrs. Olum Kipyegon Serut Waiganjo Kobado Nakara Ndirangu Njoroge Nyaga Waluke Sakaja and Mlolwe; Maj-Gen. Nkaissery Messrs. Gitari Kiuna Lekuton Limo Lomwa je Magwanga and Aduma; Lay Messrs. Njomo Melly Nuh Kemei Abongotum Obura Okoth Keynan Njuguna Moi Bitok and ole Lemein; Korere; Messrs. Aramat Sang Kada Mulu Muluvi and Lomunokol; Keraa Mbugua Seneta; Messrs. Robi Kyengo Onyura and Kisoi; Odhiambo-Mabona; Messrs. Linturi Huka and Mohamed Haji Eng. Mahamud Messrs. Ole Sakuda Cheboi Injendi Lessonet Kuria Mati Musyimi and Ngikor; Eng. Gumbo; Messrs. Barua Aluoch Shimbwa Ngunjiri Njuki Otuoma Makau ole Ntutu Bii Koinange Kinyua Gitau Mwangi Shehe and Rotino; Kanyua; Akujah; Nyamai; Shebesh; Bedzimba Muia Nyeris Wanyonyi; Messrs. Otaalo Makenga and Mbui; Dr. Pukose; Tonui; Mitaru Mumo Messrs. Bunyasi Koech Mwaita Gichigi Moroto Isaack ga S.S. Ali Tiren Osele Ogari Karani Mule oti and Kariuki; Sunjeev Chebet Musyoka; Messrs. Wetangula and Ngahu; Dr. Munyaka; Muhia; Dr. Ottichilo; Messrs. Chanzu Cheptumo Korir Kipkemoi and Opore; Chidzuga Kering Juma and Dr. Laboso.
Messrs. Washiali Oyoo Mulu Mwaura A. Keter Gimose Mukwe and Mongare Dr. Ombaka Wanyama and Anyango Mbalu Messrs. Maanzo Agoi Serut Waiganjo Kobado Wndayi Ochieng Sakaja and Mlolwe Maj-Gen. Nkaissery Messrs. je and Magwanga Lay Chae Messrs. Midiwo Obura Okoth Aden Nyamweya and Muluvi Keraa Munene Kedogo Odhiambo-Mabona Messrs. Lagat Mwadime Wangwe Eng. Kiragu Eng. Gumbo Messrs. Barua and Shimbwa Mutua Messrs. Otuoma and Wangamati Tobiko Messrs. Simba Otaalo Makenga Nyenze Baiya Ogalo G. W. Omondi Ndiritu Chumel Muchai Osele Anami Ogari Ochanda Mule and oti Wanga Musyoka Boe Muhia Messrs. J.O Omondi Mwanyoha and Gure.
Mhe Bi Naibu Spika wa Muda utaniongezea muda wangu kwa sababu amenikatiza kwa njia isiyo halali Tunahitaji kuthibitisha kama kweli ni maji ama ni kitu kingine Nilikuwa nasema kwamba niko na furaha sana kama mama kiongozi; mama ambaye ako na watoto wa kike ambao ndio viongozi wa kesho Hatua ambayo wamechukua Watanzania ingawaje uongozi wa Rais Suluhu ulikuja kwa njia ya kipekee ambayo ni ya kusikitisha akiwa mama kiongozi ambaye anaona mwanga mpya ambao unaangazia uongozi wa kina mama nina furaha sana Unaposoma vichwa vya habari kuhusu uhusiano mwema Afrika Mashariki kwenye mambo ya uwekezaji maendeleo na biashara tangu Rais Suluhu kushika usukani umekuwa ni muda mfupi sana lakini tayari tumeshaanza kuona anga mpya na mwamko mpya katika uhusiano mwema kati ya Kenya na Tanzania Uhusiano huu pengine utafungua nafasi nyingi za kuweza kuendeleza uwekezaji na ujirani mwema Haya ni eno ambayo yataleta mambo mazuri na yanapitia katika uongozi wa mama Uongozi wa Rais Suluhu Hassan unatuonyesha kwamba wakati wa akina mama umefika Kwa lugha ya Kimombo tunasema " We should rise to the occasion We should wake up and smell the coffee " kwa sababu wakati wa kina mama umefika Nikiangazia nyanja mbali mbali leo asubuhi tuliweza kumkagua aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya Jaji Mkuu wa Mahakama ya Kenya Hili ni jambo ambalo halijasikika kihistoria katika nchi hii yetu Hata katika nyadhifa nyingine nyingi tunaona nafasi ya kina mama inazidi kupanuka na kuongezeka Rais Suluhu alizuru nchini Kenya ikiwa ziara yake rasmi ya kwanza tangu achukue hatamu za uongozi nchini Tanzania Hiyo ni heshima kubwa sana kwa Kenya na shukrani kwa Mhe Rais Uhuru Kenyatta kwa kumpa fursa hiyo Hii ni njia moja ya kuonyesha kwamba Kenya tunatambua uongozi wa kina mama na tunajua wanaweza Na wale ambao wanaendeleza mijadala na fikira za kusema kwamba kina mama hawawezi nafikiri wanaendelea kuota ndoto ya mchana Nawasihi Wakenya wote Wanaafrika Mashariki Wanaafrika na dunia nzima; tuwape kina mama uhuru wa kuweza kuingia katika nyanja zote za uongozi kwa sababu wanaweza na tutakuwa na matumaini Hata watoto tunaolea watajua kwamba ndoto zao ni halali bila kujali kama yeye ni msichana au mvulana Asante sana Bi Naibu Spika wa Muda
Mhe Naibu Mwenye Kiti wa Muda nilitaka tu kuunga mkono Kuna umuhimu wa washika dau pamoja na umma kuhusishwa kwenye shughuli hizi ili wawe wanaelewa kinachoendelea wakati sheria zinapotengenezwa Naam Clause 25
Mhe Naibu Spika hata maseneta sasa hivi watakuwa na uwezo wa kuangazia zile fedha ambazo zimekusanywa na kaunti na si zile tu ambazo zimetoka katika ngazi ya kitaifa Vilevile watu watateuliwa baada ya kura kupigwa na watu kuchaguliwa Watakaoteuliwa ni wale ambao pia wamegombea na kung'ang'ana katika uchaguzi na pengine kwa bahati mbaya au nzuri wakaanguka Wao ndio watapatiwa nafasi Mhe Spika naunga mkono Mswada huu kwa sababu ni Mswada ambao utaleta maridhiano na maelewano katika taifa Mambo ya uchaguzi yatakuwa na ii na kutakuwa na ai katika taifa letu la Kenya Asante Mhe Spika
Mhe Naibu Spika naomba kutoa Arifa ya Hoja ifuatayo: KWAMBA kwa mujibu wa Kanuni ya 25 (Mgeni Mashuhuri) Shukrani za Bunge la Taifa zinakiliwe kwa ajili ya Hotuba ya Mhe Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyotolewa katika Kikao Cha Pamoja cha Bunge la Jamhuri ya Kenya mnamo Jumatano tarehe 5 Mei 2021 Asante Mhe Naibu wa Spika
Mhe Naibu Spika pengine huna habari kwamba nilisomea shule ya upili iliyoko huko Mombasa Kwa hivyo naelewa Kiswahili Tukifika jioni watu wajionyeshe vile wanaelewa
Mhe Naibu Spika wa Muda kwanza kabisa wacha nikushukuru kwa kunipa nafasi hii niweze kuongeza sauti yangu katika Hoja hii ya mjadala huhusu hotuba ya Mhe Suluhu ambaye ni Rais wa Tanzania aliyoitoa hapa Bungeni kwetu Kuja kwa Mhe Suluhu katika Jengo hili ni kuonyesha heshima kubwa sana kwa Wabunge wa Taifa la Kenya Tunamshukuru kwa kupata nafasi ya kuja kwetu kututembelea na kuzungumza eno ambayo yana uzito katika uboreshaji wa maswala ya uchumi elimu mambo ya barabara na mengineyo Sisi kama Wakenya ambao Mwenyezi Mungu ametupa nafasi kuwa hapa Bungeni tunasema asante sana Tuligundua kwamba Mhe Suluhu ndiye Rais wa pili kuzungumza katika Jengo hili baada ya Rais wao wa awali Mhe Jakaya Kikwete pia kupata nafasi mwafaka kama hiyo na kuzungumza nasi hapa nchini Kenya Nchi zetu zimepakana na ni dhihirisho ya kufanana kwa utamaduni wetu kama ndugu na dada Alizungumza eno mengi sana juu ya undugu wetu Tusionyeshe undugu huo tu kwa mambo ya Kenya na Tanzania lakini kwa bara la Afrika nzima na hata ikiwezekana tuionyeshe katika dunia nzima Akina mama wamekuwa na vita vikali sana dhidi ya kutopanda ngazi Katika Karne hii ya 21 bado tunatatizwa na akina mama kutopanda nyadhifa za uongozi Sasa tunasema kwamba Mhe Suluhu kule Tanzania ametuonyesha kwamba akina mama wanaweza na kama Mungu atatujalia kwa huu wakati bado tunapumua hapa duniani hata Kenya wakati fulani tupate mama atuongoze huku Hii ni kwa sababu wameonyesha kwamba wanawake wanaweza Juzi kule Ujerui tuliona wakati aliyekuwa Chancellor wao Angela Merkel alipomaliza kutoa hotuba yake ya kustaafu kila mmoja alisimama na kumpigia makofi kwa dakika sita kwa kazi nzuri ambayo aliwafanyia Hapa Kenya pia tuwape wanawake nafasi kutuongoza na tuwapigie makofi vile tuliona kule Ujerui Tukiwa hapa Bungeni na Mhe Suluhu tulichekeshwa Kulikuwa na mbwembwe na nderemo alipotaja kwamba wanyama wa pori kule Tanzania huwa wanakuja Kenya kutiwa mimba na kurudi kule Tanzania kuzaa Sasa kazi ya wanyama wetu hapa nyumbani ni rahisi aje? Kazi yao ni kutia tu mimba wanyama wa kike kutoka kule Tanzania na kurudi kuzaa Sasa hiyo mzigo tunapeleka Tanzania Tulikuwa na vichekesho sana hapa wakati Mhe Suluhu alitutembelea Tumekuwa na changamoto kadhaa katika uwekezaji wa mali na jinsi ya kufanya biashara hapa na kule Tanzania Kila mtu anatambua kuwa cheti au kibali cha kufanya kazi kule Tanzania kimekuwa kizungumkuti na alisema kwamba atafanya chochote anachoweza kuondoa kizingiti chochote ili tukae kama ndugu Pia kama kibali kinatakikana na Mkenya kufanya kazi Tanzania anafaa kupewa na vilevile Watanzania pia wakitaka kibali kufanya kazi Kenya wapewe kwa sababu sisi ni majirani ndugu na jamii moja Asante sana Mhe Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi Naona light yangu is blinking
Mhe Naibu Spika wa Muda Mhe Kii Ichung'wah amekuchukua kama Kiongozi wa Waliowengi Hukuelewa vizuri vile nilikuwa nasema Nilisema ya kwamba kuna boma ambayo iko na watoto ambao wako na baba tofauti Kuna huo mchanganyiko maalum katika hiyo boma Nitatoa mfano Tuseme hii boma iko na bwawa ambalo ng'ombe anakunywa maji Uko na mtoto wa Mjaluo Maasai na Mhindi Huyu wa Maasai analeta ng'ombe akunywe yale maji na huyu wa Mkikuyu anataka kupanda nyanya zake hapo karibu anyunyizie maji Sasa hawa watu wanapigana Yule mtoto wa Mhindi anataka kutoa mineral water ndio auze Yule mtoto wa Mjaluo anataka kuweka samaki Huyu mtoto wa Maasai analeta ng'ombe 1000 ambao wanakojolea maji na wanaua wale samaki kwa sababu ya gasidi Watoto wanapigana kwa boma halafu wanatoka nje Katika ile boma ambayo iko na utaratibu mmoja
Mhe Naibu Spika wa Muda mimi najua Kiswahili sanifu. Ningependa kupongeza Mheshimiwa mwenzangu. Je ni halali kwa Mheshimwa mwenzangu kusema ya kwamba yule aliyekua upande wa Jubilee kuruka upande mwingine hastahili kushutumu mabaya yanayotendeka katika nchi? Ni lazima ninyamaze wakati ambao watu wangu kule Turkana wanakufa njaa ama hawapati chochote? Hata kama niko Jubilee lazima nishutumu maana Serikali iliyoko sasa ni ya Uhuru Kenyatta na yeye ndiye anashikilia uongozi na siyo Raila. Makosa yote yanaenda kwa yule anayeongoza. Asante Mhe Naibu Spika wa Muda.
Mhe Naibu Spika wa Muda naomba kuwashukuru Wabunge wenzangu wote waliochangia Hoja hii na kwa eno yote mazuri wamezungumza kuhusu Rais Samia Suluhu Hassan safari yake na hotuba aliyotoa katika Bunge hili Ninashukuru kwa vile alivyojitolea kuboresha uhusiano baina ya nchi zetu mbili na kama nilivyosema ni kupapalia magugu yote ambayo yamekua na kuanza ukurasa mpya katika uwiano wa nchi zetu mbili na hasa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa jumla Pia ikiwa hiki ni kikao cha mwisho kabla ya kwenda kwenye likizo fupi ningetaka kuwatakia Wabunge wote likizo yenye mafanikio na Mungu awalinde wote Tuonane tena panapo majaliwa na kila mtu akumbuke kujikinga kutokana na janga la corona ambalo liko hapa na liko na sisi Tukiweza kurudi hapa tutamshukuru Mungu kwamba tumeenda kutenda yale tunayotenda kwa wananchi tunaowahudumia na tumerudi hapa kuendelea na huduma tunazotoa katika Bunge tukiwa Wabunge ambao wameteuliwa kuwahudumia wananchi Kwa hayo machache naomba kuhitimisha
Mhe Naibu Spika wa muda naomba uniruhusu nitoe barakoa ili niweze kuongea vizuri Nataka nichukue fursa ili niunge mkono Hoja hii ya maana kwa Bunge hili na taifa kwa jumla Ni wazi ya kwamba kuchaguliwa kwa Mhe Rais wa Tanzania Samia Suluhu ni jambo la kihistoria Yeye ndiye Rais wa kwanza mama kuchagulia katika eneo hili la Afrika Mashariki Pongezi kubwa kwake na wananchi wa Tanzania Kenya na Tanzania wana uhusiano wa muda mrefu sana uliyoanza hata kabla ya nchi hizi mbili kujinyakulia uhuru Huo uhusiano umekuwa ukiendelea ingawa hapo awali ulikuwa na tashwishi kidogo Kwa hivyo kuchukua usukani kwa Rais Suluhu ni jambo la kufurahia Tumepata nafasi ya kufufua na kuimarisha huo uhusiano Nikimpongeza Rais Suluhu ni lazima nipongeze pia Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta Hakupoteza wakati hata kidogo Alichukua hatua haraka kuhakikisha ya kwamba tumetengeneza urafiki na Rais mpya wa Tanzania Samia Suluhu Hakuna nchi yoyote katika dunia nzima ambayo inaweza kuendesha shughuli zake kivyake Nchi zinahitaji ushirikiano katika mambo ya uchumi jamii na kadhalika Hakuna nchi hata moja inaweza kuwa kama Island
Mhe Naibu Spika wa Muda ninakushukuru kwa kunipatia hii fursa ili nichangie Hoja hii kuhusu Hotuba ya Rais wa Muungano Tanzania Ninatangulia kwa kumshukuru Rais wetu kwa kumpa mwaliko Mama Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Pia nampongeza Mama Suluhu kwa kukubali mwaliko huo na kuifanya Kenya nchi yake ya kwanza kuzuru rasmi akiwa kama Rais Leo hii tunamshukuru Hotuba ya Mama Rais Suluhu ilikuwa ya kufana sana Nilivutiwa na hekima yake Pia nilipendezwa na umakini wake kila alipokuwa akijieleza Nilifurahishwa na jinsi alivyotilia mkazo jambo la umoja na undugu wetu haswa aliposema kuwa hili ni jambo ambalo limekuwa tangu mwanzo akieleza kwamba tangu jadi Watanzania na Wakenya waliishi kama ndugu Nilifurahi kuona kwamba anataka kufufua uhusiano wetu wa tangu mwanzoni Ndugu ni kufaana sio kufanana Nchi za Kenya na Tanzania na haswa Gatuzi la Taita Taveta Eneo Bunge la Taveta ni jirani wa Tanzania na tumekuwa tukifaana na ndugu zetu wa Tanzania kwa mambo mengi sana
Mhe Naibu Spika wa Muda ningependa kuchukua fursa hii kuunga mkono Hoja hii. Nampa shukrani zangu mheshimiwa Kigo Njenga kwa kuleta masuala haya. Kinachonivutia zaidi katika Hoja hii ni kwamba inapendekeza tuanzie mashinani. Hoja hii imezungumza hasa kuhusu watoto wetu wa shule. Hii ni ishara kwamba tunaenda kuambatana na yale wahenga walisema kwamba ni lazima samaki tumkunje angali mbichi. Tunazungumza kuhusu masuala ya pombe hasa pombe ambayo haijahalalishwa na sheria. Sijui kama mheshimiwa Kigo alikosea lakini alisema kwamba pombe ya mnazi ni baadhi ya zile pombe haramu. Nataka kusawazisha maoni haya. Mnazi si haramu. Pombe hii inatoka kwenye mti aina ya mnazi na haina matatizo yoyote. Ningependa kusema kwamba unywaji pombe hasa miongoni mwa vijana umedidimiza uchumi sana. Vijana wanapoingilia unywaji pombe wanakosa kujihulisha na masuala ya maendeleo. Hivyo basi ni kweli kwamba kuna haja ya NACADA kujizatiti zaidi kwa kuibua mbinu mwafaka ambazo zitahakikisha suala hili linashughulikiwa vilivyo. Tatizo hili halihitaji tu suluhu kutoka kwa Serikali peke yake. Hili tatizo ambalo linatuhitaji sisi viongozi na wazazi kulitilia maanani. Hoja hii inazungumzia hasa matumizi ya pombe haramu katika miji yetu. Sharti tukubali kwamba jinsi tunavyoishi makwetu ni muhimu. Kwa mfano si vema kuwatuma watoto wadogo dukani kununua pombe. Wazazi wakome kufanya hivyo. Sharti tuhakikishe tumewaonyesha watoto wetu mienendo mizuri. Ni muhimu walimu wetu wachangie katika kukuza watoto wetu kwa njia nzuri. Najua haya masuala yako kwenye syllabus ambazo walimu wanafuata. Ningependekeza kwamba washikadau wote wahusike katika kutatua tatizo hili. Lazima wahusike kwa njia nzuri kwa sababu kama suala hili halitaangaziwa vyema huenda ikawa tumefungua nafasi ya baadhi ya watu kuleta ufisadi. Mimi ninaamini kunazo sheria ambazo zinadhibiti unywaji pombe. Ni sheria ambazo zikifuatwa kwa njia nzuri basi hatutakuwa na matatizo kama yale yamezungumziwa na wanenaji wenzangu. Kwa hivyo ninaiunga mkono Hoja hii. Ningependa kwa mara ya pili kumshukuru mhe. Kigo kwa kuileta Hoja hii. Ninaiunga mkono.
Mhe Naibu Spika wa Muda niwie radhi nitoe barakoa kidogo ndio niweze kupumua vizuri
Mhe Naibu Spika wa Muda sijasema hivyo Itabidi unilinde kutoka kwa Mhe Millie Odhiambo Unajua historia yake Unajua eno yake ni makali Nimesema ya kwamba wale ambao wanaumia sana na wanauziwa dawa za kulevya
Mhe Spika asante sana kwa fursa hii ambayo umetupa kujadili jambo hili la kushtua Linashangaza sana kwamba Kiongozi wa Waliowengi anahitaji wiki mbili kupata jibu ambalo ni rahisi Leo tumejadili ule Mswada wa kuangalia mambo ya pesa katika Wizara ya Masuala ya Nje na tumegundua kwamba suala hili limejadiliwa Wiki mbili ni mbali sana Kama ingewezekana tupate jibu kwa wiki moja Ni hatia kwa nchi na vilevile kibalozi ulimwenguni kwa Balozi kupokelewa kwa nchi nyingine bila nyaraka ambazo zimeidhinishwa rasmi na Bunge Hili ni jambo ambalo litatupa sura mbaya kama nchi iwapo mabalozi watachaguliwa kwa njia ambayo haifai Ni ombi langu kuwa jambo hili lipewe muda mfupi ili tumalize mambo haya kwa wakati huu
Mhe Spika asante sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia Hoja ya Mhe John Ngongo. Pia nataka kuchukua nafasi hii kutoa hotuba yangu ya kwanza; katika siku za nyuma sikupata nafasi kamili ya kupeana hotuba yangu ya kwanza Bungeni. Ninaitwa Mishonari Lodepe Nakara Mbunge wa Turkana ya Kati. Ningependa kuchukua nafasi hii kushukuru watu wa Turkana ya Kati kwa kunichagua na kunifanya kuwa Mbunge wao wa kwanza chini ya Katiba mpya.Turkana ya Kati ni moja ya maeneo ya Bunge ambayo yako katika kaunti ya Turkana na ni moja ya maeneo ya Bunge ambayo yamekuwako tangu Kenya ipate Uhuru; nawashukuru wananchi wa Turkana ya Kati kwa kunichagua kuwawakilisha katika Bunge hili la Kumi na Moja. Nikichangia Hoja ambayo iko mbele yetu ningependa kusema kwamba kama kuna wavuvi ambao wanaumia ama wanateseka sana katika nchi ya Kenya ni wavuvi wa Ziwa Turkana; shida yao ni mambo yafuatayo kwanza ni barabara. Barabara inayoelekea Ziwa la Turkana ambalo kubwa katika nchi hii ni barabara ambayo ni kama inayoenda mbinguni. Ina shida nyingi. Magari yanaharibika. Kuna mashimo mengi barabarani. Usalama ni mbaya na umefanya wavuvi wasiweze kupeleka mazao yao katika miji iliyo karibu na Ziwa la Turkana ili kupata soko. Hilo ni tatizo moja ambalo wavuvi wa Turkana wanapata. Bw. Spika tatizo la pili ni soko. Nilishangaa juzi nilipoenda kwenye hoteli moja hapa Nairobi na kuagiza nipewe samaki. Samaki niliyoletewa kule kwetu Turkana inauzwa Kshs20. Hapa niliuziwa Kshs200. Nilishangaa sana. Nilisema kama tungekuwa na soko kama hiyo samaki ambao tunauza Kshs20 huko Turkana hata tukiiuza Kshs50 itakuwa ni faida kwa watu wa Turkana. Naiomba Serikali iangalie jinsi ambavyo wavuvi wa Turkana wanaweza kuleta samaki katika mji wa Nairobi ili wapate soko nzuri. Bw. Naibu Spika wa Muda shida nyingine ambayo wavuvi wa Turkana wanapata ni mambo ya kuvua samaki kwenye ziwa. Wanatumia teknolojia ya zai na jambo la kushangaza ni kwamba wakati upepo unapokuja unasukuma hawa wavuvi mpaka katikati ya ziwa. Wanapofika katikati ya bahari wanashikwa na Kenya Wildlife Service (KWS) ama na Marine forces na kupelekwa Marsabit. Mimi nauliza sasa hawa watu ambao wamesukumwa na upepo kwa nini washikwe? Si kupenda kwao kuingia kwenye sehemu ambayo hawastahili kuwa lakini upepo unasukuma hadi mahali anaposhikiwa. Baada ya kushikwa badala ya kuletwa Turkana na kushtakiwa pale wanapelekwa Marsabit na kushtakiwa. Sasa tunatumia nauli kubwa ya kwenda mpaka Marsabit kutoa hao wavuvi kwenye jela na tena kuwarudisha mpaka Turkana. Hii ni shida kubwa sana. Hii ndio
Mhe Spika japo wengi wamekutolea kongole katika lugha ya Kingereza ningependa kuongeza sauti yangu nikisema kwamba nakupa pongezi kwa niaba ya watu wangu wa Shinyalu na kongole kwa wewe kutunukiwa nafasi hiyo ambayo ni muhimu katika jamii zetu Suala la muhimu ni unavyotukalia hapa kama Kinara unafanya kazi yako sawasawa Wewe una maingiliano mazuri na Wabunge hawa Mimi kama Mbunge ambaye amekuwepo hapo awali pia nimeona Spika wengi wakikalia mahali ulipo Lakini kwa sasa wewe ndiye mufti na bora zaidi Ni kwa sababu umeweza kutoa ule ubabe pale Kuna wale wengine ambao wanakaa pale na ubabe Wewe umekuwa ni mtu mvumilivu mzuri mwenye maingiliano mazuri na Wabunge na pia tunakaa mahali pamoja tunakula pamoja na tunazungumza pamoja Hilo ndilo suala ambalo nakuambia kwamba huo ndio uongozi Suala hilo ndilo limekupa kipaumbele na watu wa kwenu wakaona kwamba watosha Nami najua kwamba hata sisi katika Mkoa wa Magharibi tunakutambua Umefanya kazi kwingi katika ule uitifaki wako wa kutarazaki katika masuala ya kisheria Kule kwetu tumeona umefanya kazi nzuri japo kama ilivyosemekana kule labda mambo yapo Lakini tunajua kwamba pia wewe si mchache katika maingiliano na watu Kwa hivyo tunakusifu na tunakutakia kila la heri kwa sababu watu wa upande ule wa mlima hawakukosea Wewe umejaa tajriba na vilevile una ukiritimba mkubwa sana katika masuala ya kisheria masuala ya mambo haya ya Kanuni za Kudumu na kadhalika Tukirudi katika Bunge wewe umeleta mabadiliko mengi sana katika Bunge hili Tumeona Kanuni za Kudumu zimekuja katika Kiswahili Tunaweza kuzungumza kwenye Bunge katika Kiswahili Hata tumewapiku wale wenzetu wa Tanzania Kama unavyojua Kiswahili cha Kenya ndicho cha ustandadi mkubwa Wewe umetusaidia sana hapo na tumefurahia kwa sababu tuna ule ustandadi sasa Tunaweza kuzungumza Kiswahili hapa Tunaweza kusoma mambo mengi katika Kanuni za Kudumu Kwa hivyo nasema heko na kongole Hata nikienda kule kwetu nitaweza kuwauliza wale wengine ambao ni wenzetu waige mfano wako Nasi tukija jaribu zile za mlimamlima tutaweza kuja kule tumuambie Baba wa kwetu ambaye tunamjua ndiye kiongozi wetu Tutamuambia "ukienda kule ujue kwamba kuna kigogo na kigogo huyo anaitwa Bwana Muturi"
Mhe Spika kauli mbiu ya mimi kuzungumza ni kusema kwamba Bunge hili la 12 limedharauliwa sana kiasi cha kwamba hata sheria zikiundwa humu hazifuatiliwi wala kutekelezwa Tunaloliuliza ni kwamba iwapo Mbunge yeyote atauliza maswali yake kuhusiana na eneo lake ama suala lolote linalohusu nchi hii ni sharti mawaziri waheshimu Bunge hili Shukrani sana Mhe Spika
Mhe Spika kivyangu nasema sijui ni nani aliyeyatoa malalamishi hayo Kwa hivyo sijui nitamjibu kivipi Kivyangu nasema ni mambo ambayo yamepitwa na wakati na tuendelee mbele Mimi sijui nani amenishtaki na amenishtaki katika misingi ipi
Mhe Spika kwa rekodi ya hili Bunge sidhani kama nimetaja jambo kama hilo hapa
Mhe Spika mimi Faisal Badir Salim Mbunge wa Msambweni kwa niaba ya watu wangwana wa Msambweni napiga kura ya ndio
Mhe Spika naomba Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama atakapozungumza na wizara husika aweze kuwaambia wazi kwamba wakija wasituambie ilikuwa ni mambo ya wizi kwa sababu duka la M-PESA ambalo liko pale ni dogo sana na hakuna chochote kilichoibiwa Kwa hivyo waje watuambie kulingana na uchunguzi uliofanywa ni kwa nini walifanya jambo hili Kama wanatuambia ni masuala yanayohitaji wiki mbili tutalikubali hilo ili wasiwe na sababu ya kuwa wiki mbili waliitisha na tukataka muda mfupi zaidi
Mhe Spika nashukuru kwa nafasi hii Ni furaha mpwitompwito kama mtu aliyepata mwana kwa fursa hii kusimama hapa mbele kwa niaba ya wakaaji ninaowaakilisha wa Bunge la Cherengany Kama Naibu Mkuu wa chama tawala cha Jubilee na mkereketwa ambaye amepata ufaa kupata maeneo Bunge mawili kaskazini na kusini Cherengany napiga kura ya ndio bila kulalamika
Mhe Spika nasimama kuunga mkono Hoja hii. Tukizingatia umuhimu wa Kamati hii na umuhimu wa kuwa na Baraza la Mawaziri wakati unaofaa sioni kama inafaa hata kwa mmoja wetu kusimama kupinga Hoja hii. Hata kama ingewezekana ingekuwa pengine watu wawili tu wazungumze kuhusu Hoja hii ili tuipitishe; inafaa tutoe nafasi kwa haraka kwa Baraza ili mawaziri wateuliwa katika wakati unaofaa. Mhe. Spika katika wizara zilizobuniwa ni kama kuna vitengo vingine ambavyo vimeachwa nje. Mfano ni kitengo kile cha jinsia. Haijajulikana kitakuwa katika Wizara gani. Hivyo basi inafaa kamati hii ijitwike wadhifa wa kuweza kuwashauri viongozi wahusika Mheshimiwa Rais na Mheshimiwa naibu wake ili kitengo cha jinsia kiwekwe katika Wizara ambayo itatekeleza majukumu kama vile ilivyokuwa katika siku za nyuma. Mhe. Spika pia katika harakati hizo za kubuni Baraza la Mawaziri ningeuliza tena wahusika waangalie maeneo yote ya nchi ili yapate kuwakilishwa katika Baraza hilo. Hiyo itawafurahisha wananchi wa Jamhuri ya Kenya; wataona kwamba kila sehemu inawakilishwa katika Baraza hilo. Mhe. Spika nina mengi lakini kufikia hapo nasema ninaunga mkono kwamba Hoja hii ipitishwe pasipo kusitasita. Asante Mhe. Spika.
Mhe Spika nataka nichukue nafasi hii kuchangia katika hii Petition kwa sababu inagusa Wakenya ambao wanafanya biashara ndogo sana Nimeishi katika Jiji la Mombasa Ninaelewa yale Mhe Abdullswamad ameongea kuhusu Nilijivinjari katika Light House na Mama Ngina Drive Wakazi wengi wa Mombasa ambao huenda kujivinjari huko ni Wakenya wa mapato ya chini Wafanyi biashara wanapata fursa ya kutafuta riziki yao ya siku ili watoto wao wapate chakula kwa meza Niliona hii amri ambayo ilitolewa na Wizara ya utalii Waziri wa Utalii ni mkazi wa Jiji la Mombasa Alikuwa Meya wa Jiji hilo Ni mtu ambaye anaelewa sana wafanyi biashara hawa katika eneo hizo mbili Nitafurahi sana Kamati husika ikifika katika hayo maeneo kwa haraka ili waongee na hawa Wakenya ambao wameathirika kibiashara Pia walete taarifa ambayo itawasaidia Asante Mhe Spika
Mhe Spika natoa kongole na kukubaliana na mwenzangu Mhe Tandaza Kama walivyozungumza Wajumbe kadhaa masuala ya ardhi ni tetesi hususan huko kwetu maeneo ya Pwani Nataka kutoa mfano wa eneo lile natoka mimi la Mvita Kihistoria kuna baadhi ya watu waliopatiwa ardhi hizi sio kwa sababu nyingine lakini walipatiwa kwa niaba ya wakaazi wa Mvita na Mombasa kwa jumla Na hii ilikuwa kabla Kenya kupata uhuru Ardhi hizi walipatiwa watu waliokuwa wanaitwa sultan kwa sababu walikuwa na mamlaka ya maeneo yale Wakati wa aliyekuwa Mbunge wa Mvita marehemu Shariff Nas Mungu amuweke pema palipo na wema alihakikisha Wizara ya Ardhi ilienda katika maeneo yale na Rais Mstaafu ambaye pia ameenda mbele ya haki Daniel arap Moi alitoa amri ya kuwa ardhi za mbele za eneo hili watu walipe Sh30000 na za nyuma Sh15000 kwa sababu ya ile historia Nakumbuka ya kuwa baadhi ya watu walilipa na baadhi wakapewa stakabadhi zao Huu wakati wangu mimi niliweza kuenda na National Land Commission ambayo ni kamisheni inayotambulika kikatiba Walitoa amri kwa zile ardhi kwa saabu ya historia ya mahali pale watu walipe Sh400000 na Sh500000 ili wapatiwe ardhi zao Mpaka sasa hivi kuna wengine wanaona kuwa watu wazima wanaweza kutishwa Mwingi West Nguna yaani bado wanataka kutisha watu eti watawabumburusha kutoka kwenye ardhi zile Wanasahau tuko na nchi iliyo na sheria Ninakubaliana na ardhilhali hii Ninaomba National Land Commission kuwa ikishatoa amri ifuatilie Tusiwe ni wenye kukaa tu na hali watu wetu wanateseka Kuna wale ambao wametumia viongozi wao na mambo yakatekelezwa Nimewasiliana na mwenyekiti husika wa ardhi Haya mambo kuhusu Mvita nitayapeleka kwake ili aweze kufuatilia Ahsante sana
Mhe Spika niko relevant sana kwa sababu hakuna mwanamke amebeba fedheha katika hii Kenya kama Mhe Martha Wangari Maathai na ndio nauliza
Mhe Spika nilijaribu kwa muda kupata jicho lako Nataka kujulisha Jumba hili ya kwamba tarehe 8 Juni nilileta ardhilhali kuhusu wachuuzi ambao wako katika eneo la Mama Ngina Drive Kumetokea matokeo kadhaa Ni muhimu kupata mwelekeo wako Kamati iliyopelekewa ni ya Idara ya Uchukuzi lakini Kamata inayohusika na utalii waliwasiliana na Wizara ya Utalii na Wizara ikafungua rasmi lakini ufunguzi wake sio vile unavyotakikana Nahofia isije ikaonekana tumeridhika kwa vile imefunguliwa lakini kiasi Masuali yalioko bado yanaleta kero kwa sababu huwezi kufungulia watu kwa ubaguzi wengine wanakubaliwa kufanya biashara lakini mwenye ushanga ama mwenye biashara ndogo ndogo hakubaliwi Mhe Spika tupatia mwelekeo kama kinara wetu Njia mwafaka itakuwa ipi ili watu wetu wa Mombasa ambao wameumia tayari kila mmoja wao licha ya hali yoyote bila ubaguzi waendelee na biashara zao?
Mhe Spika nitajaribu. Nasemba kwamba kama Bunge na nchi ni lazima tuone kuwa Wakenya wamepata haki. Tutakifanyia mabadiliko kikosi chetu cha polisi. Wakati wa polisi kuwapiga watu ili kuwalazimisha watoe habari
Mhe Spika sahai Tuko katika masuala ya mtandao na watu wanaweza kuangalia mahali popote walipo vile mambo yalivyoendelea
Mhe Spika wa Muda eno yako ni kuntu Mhe Naibu Spika wa Muda nilitunga sheria hii kwa sababu tulikuwa tumeona yaliyoko kuwa hakuna hesabu zinazowekwa katika mambo ya waqf Tuliona yale yaliyoko Ni mikakati gani zitatumika kuchagua makamishna? Nilipoleta sheria hiyo Serikali kupitia kwa aliyekuwa Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi katika Bunge Mhe Aden Duale aliniambia kuwa kuna sheria nyingine tayari inajadiliwa kwa hivyo ili tusishindane nikubali yangu iwe nyuma Nakubaliana na vinara wote walioko katika Bunge na nafurahi Hata juzi tulikuwa Mombasa tukihudhuria sherehe fulani ya Idd pamoja na Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi na akaahidi atahakikisha kuwa hii sheria imepewa kipaumbele na ninashukuru Kwa hivyo nawasihi wenzangu waangalie hii sheria ili vizazi vijavyo viweze kufaidika kutokana na yale vizazi vilivyopita vilijaribu kufanya Asante sana Mhe Naibu Spika wa Muda
Mhe Spika wa Muda mimi ndio Mhe wa Suba North sio Mhe Opiyo Wandayi
Mhe Spika wakati unang'ang'ana kumuamsha Mhe Sunkuyia labda uangalie watu wote kama wamepiga kura haswa wale wamekua macho kabla hawajalala
Mhe Spika wewe ni Spika wa wanawake na wanaume Pia wewe umezaa wasichana ambao kesho watasimama kuwa marais Safari ni ile ile ya wanawake kukimbizwa Sisi kama wanawake wa hili Bunge tunazidi kusema Mhe Wangari Maathai viva W anawake tusimame kidete Naye Minister ambaye anahusika na eno ya usalama wacha kutuma askari kusukuma wanawake hasa wanawake wale ambao wanatafuta viti Sisi wanawake tunajivunia Wangari Maathai Mhe Spika Mhe David ole Sankok amevaa rangi ya chama Furusha yeye avae nguo ambazo zinafaa Bungeni maanake hizo amevaa ni uniform ya chama Ahsante
Mhe. Aburi huo ni mchango na wala si dosari katika utaratibu.
Mhe. Baya nitakuelekeza. Wewe ndiye umekosa nidhamu kwa sababu haujasoma Kanuni za Bunge. Yule wa kuchangia ndiye anachugua lugha ya kutumia. Ukianza kwa Kiswahili utamalizia kwa Kiswahili na ukianza kwa Kiingereza utamalizia kwa Kiingereza. Kwa hivyo Mhe. Oluoch ako sawa katika mchango wake.
Mhe. Bi. Mwenyekiti wa Muda naomba kuweka hii chini. Sijui tuseme nini. Baba amekwisha soma na amesema ni mzuri. Mimi sitaki amendment tena. Nimeweka chini.
Mhe. Gikaria ingekuwa vyema kama ungekuwa mwenye kutoa mfano mwema kwa huo utoaji wa damu. Ungekuwa unatuelezea hapa kwenye sebule ya Bunge kwamba wewe umeweza kutoa damu mara ngapi ili sisi tuweze kufuata huo mfano wako mwema. Kwa sasa nitampatia nafasi Mhe. Mwambire Ngumbao Mheshimiwa wa Ganze.
Mhe. Kolosh ulikuwa umemkashifu Mhe. Kassait. Ulisema ya kwamba alikuwa amekuhujumu kwa njia nyingine. Lakini nimeona sasa umegundua kwamba baniani mbaya lakini kiatu chake dawa. Wamalwa.
Mhe. Leshoomo tafadhali tumefika wakati wa kukomesha. Uko na dakika nane za kuongea na kwa hivyo utakuwa wa kwanza wakati hii Hoja italetwa tena.
Mhe. Mwenyekiti ningependa kusema vile Mhe. Shebesh amesema. Tafadhali tuangalie kuwa ingekuwa vizuri tujielewe kwa sababu wananchi kule nje wanatuangalia na vile mnavyoona runinga inaonesha tunazungumza nini hapa. Tangu jana tumekuwa tukijishughulisha na mambo kuhusu mishahara yetu pesa ambazo
Mhe. Mwenyekiti wa Muda biashara ya kamari inafaida watu wengi sana. Pia ina hasara kwa Wakenya wengi sana mpaka watoto wetu. Majumba mengi yameadhirika kwa sababu ya biashara ya kamari. Hii Kshs20 milioni ni sawa.
Mhe. Mwenyekiti wa Muda mambo yanayozungumzwa hapa ni muhimu sana. Yanahitaji watu wa kutosha kwa sababu Wakenya wote wanaangalia siku ya leo. Nikiangalia watu hawajatosha; hakuna quorum kamili ya kuendelea na eno haya. Kwa hivyo ifungike na watu wangoje mengine kwa sababu pana klabu hapa ambayo imejipanga makusudi kuhujumu eno ambayo yametengenezwa na Wakenya wote. Asante Mhe. Mwenykiti wa Muda.
Mhe. Mwenzangu anaongea vizuri lakini ni vizuri kusema kwamba wale wanabeba wateja kwa pikipiki wanakunywa bhang na pombe? Uko na uhakika kwamba wanakunywa pombe?
Mhe. Mwirigi mchango wako umekuwa wa ufaa sana. Ningependa tu kuelewa jambo moja. Unaposema kuwa hawana mbele wala nyuma unamaanisha vipi? Ni sawa lakini! Tutakuwa na mchango kutoka kwa Mhe. Oduol Adhiambo. Tafadhali chukua usukani.
Mhe. Naib Spika wa Muda ningependa kuunga mkono Hoja ya Mhe. Odhiambo-Mabona ya kubadilisha kidogo tu Hoja ya Mhe. Ngongo. Nitaanza kwanza kwa kuwakumbusha Wabunge na Wakenya wote kwamba uvuvi unachangia pakubwa katika uchumi wa Taifa hili. Ninaposema hivyo nasema mchango kwenye viwango mbalimbali. Kuna viwango vya wale ambao wanategea uvuvi moja kwa moja kama wavuvi katika pembe zote za taifa letu kutoka Bahari ya Hindi hadi Ziwa Victoria. Pia samaki hupatikana katika mito mbalimbali kama vile Mto Tana Mto Nzoia na mito mingine kwenye taifa letu. Pia hupatikana katika maziwa mengine kama vile Ziwa Turkana na Ziwa Naivasha. Kuna Wakenya wengi ambao wanaishi katika maeneo haya ambao tegemeo lao kuu katika maisha yao ni uvuvi. Vile vile kuna Wakenya wengine ambao wanategemea uvuvi katika hali zingine. Kuna wafanya biashara na wachuuzi wa samaki katika sehemu mbalimbali za taifa letu wanaofanya biashara katika viwanda ambavyo biashara yao ni samaki katika sehemu mbalimbali za taifa hili iwe ni Kisumu Thika au Mombasa. Kuna wale ambao wako kwenye biashara ya kuuza samaki kwenye mataifa ya nje hasa katika Muungano wa Mataifa ya Ulaya (European Union). Kwa hivyo uvuvi ni msingi mkubwa kwenye uchumi wetu kama taifa. Lakini kidogo kumekuwa na upungufu mkubwa kutoka kwa Serikali tunapozungumzia misaada kwenye sekta ya uvuvi. Tayari wenzangu waliozungumza hapo mbeleni wametaja msaada mkubwa ambao wakulima wa kawaida wamepata kutoka kwa Serikali. Tumeshuhudia hapo mbeleni Serikali ikifutilia mbali madeni makubwa mabilioni ya fedha katika sekta kama vile kahawa mpunga sukari lakini hatujashuhudia hatua yoyote kama hii kwenye
Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda Mheshimiwa Gathogo amesema aliumwa na kitu. Inawezakuwa kitu ambacho kinaambukiza? Ninataka kujua aliumwa na nini. Kama ni kitu ambacho kinaambukiza ni vizuri tupate kinga.
Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda nakubaliana na Mhe. (Dkt.) Ottichilo kuwa ni muhimu kuwe na sheria wazi wazi bila tashwishi yoyote. Wenye kufanya shughuli hizi ni lazima wawe wamesomea masuala haya na haswa wawe wamesomea muda ambao sio mrefu kutoka wakati wanapolipa ada yao.
Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda nilikuwa najipanga kutoa maoni yangu kuhusiana na kipengele kinachofuata. Ninaunga mkono kipengele hiki. Clause 70
Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda ninaunga mkono. Wakati mwingi Tafadhali tuachane na mambo ya nguo. Mara nyingi tunaongea mambo ya vijana lakini ikifika wakati wa kufaidika wazee wanafaidika na vijana wanakosa.
Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda unajua ninataka nimwambie Mhe. Mwadeghu kwamba hoja tunayoijadili ni Memoranda. Lakini tangu walipokua kwa mazishi ya mamake ndugu yangu Mbadi wanachama wa Coalition for Reforms and Democracy (CORD) wanaongea tu juu ya Duale. Wana kasumba na Duale?
Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda wakati tunaongea mambo haya ni lazima tukumbuke nyumbani kwa sababu ndio imetuleta hapa. Kama sio wale watu wa Meru ama watu wa Tigania Mashariki ambao walinipigia kura singeweza kuja katika Bunge hili. Wakati ninaongea akili yangu hainionyeshi Kenya nzima bali inanionyesha Watigania na jamii ya Wameru. Ndivyo ninasema Wakenya wajue ya kwamba pesa zote ambazo zinaenda kwa afya zinapitia katika Bunge letu ambapo Mhe. Kajuju yuko na wewe ukiwa Naibu Mwenyekiti wa Muda. Sikumaanisha ya kwamba ni gavana analeta pesa. Tunazipitisha zinapelekwa Kericho Kilifi Mombasa na Meru. Zikifika kule Meru zinakuwa za mtu mmoja. Naiunga mkono Serikali lakini imekuwa na ukora mwingi ambao haufai. Naunga mkono.
Mhe. Naibu Spika ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ili niwafahamishe Wabunge wenzangu kuhusu ziara ya Baba Mtakatifu ambaye atakuwa humu nchini kuanzia kesho. Wabunge waheshimiwa mpangilio ambao umewekwa
Mhe. Naibu Spika ahsante sana kwa kunipatia fursa hii. Namshukuru na kumpongeza Rais wa nchi ya Kenya kwa hotuba yake kwa taifa wiki iliyopita. Nilisikiliza na kufuatilia kwa makini hotuba ya Mhe. Rais. Kwa kweli alizungumzia masuala nyeti na muhimu haswa wakati huu nchi ya Kenya na dunia nzima inapitia magumu na makali kutokana na majanga kama vile virusi hatari vya Korona na uvamizi wa nzige katika baadhi ya maeneo ya nchi hii na kwingineko katika Afrika. Nikimnukuu Mhe. Rais alizungumzia yale waliweza kufanya kama Serikali ili kupunguza makali ambayo Wakenya wanapitia kwa sababu ya hali ya uchumi na ukosefu wa biashara. Baadhi ya kodi ambazo zimepunguzwa ili kukabiliana na makali ya virusi vya Korona ni dhibitisho tosha kwamba Mhe. Rais anajali taifa la Kenya wachuuzi na wafanyi biashara wadogo. Nitazungumzia kuhusu virusi vya Korona. Tumeona kwamba Mhe. Rais amefanya mengi na yote ambayo anaweza. Pia ninapongeza Bunge hili kwa sababu waliketi chini kwa dharura haswa Kamati ya Bajeti na Kamati ya Afya. Lakini inasikitisha kwamba baada ya Wabunge kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha kwamba Wakenya wako salama na sekta ya afya iko sawa kuna wale ambao waliona nafasi ya kujitajirisha kwa kuiba fedha. Inahuzunisha sana kwamba tunavyozungumza sasa hivi sio Wakenya wa kawaida peke yao wanaokufa; madaktari pia wanaangamia. Mhe. Naibu Spika nilibahatika kuwa katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Afya jana ambapo madaktari waliwasilisha malalamishi yao. Inasikitisha kwamba katika Bunge hili kila mmoja wetu hapa anajua rafiki ndugu au jamii ambaye ameangamia kutokana na makali ya virusi vya Korona. Hata kuna wenzetu katika Bunge hili ambao wameangamia. Tulivyo keti hivi tunaangaliana kama "marehemu watarajiwa" ake hatujui nani atafuata. Najua Wabunge wanasikitika na kushtuka sana ninaposema sisi ni "marehemu watarajiwa" lakini Waswahili husema ukiona mwenzako ananyolewa tia chako maji. Rais amefanya yote awezayo. Ni muhimi Waheshimiwa katika Bunge hili kumuunga Rais mkono haswa katika vita dhidi ya ufisadi. Mhe. Naibu Spika ninaona muda wangu umeisha lakini sitakosa kuongea kuhusu usalama wa nchi hii. Kweli nchi yetu ni salama kutokana na hatari za nje lakini nchi yetu si salama kutokana na hatari ya sisi kwa sisi. Nitokako mimi kuna ujambazi ambao umekita mizizi haswa wizi wa mifugo na uvamizi. Kule kwetu watu hawaogopi virusi vya Korona. Wanaogopa wezi wa mifugo. Nashangaa kwamba askari ambao wanafanya kazi katika eneo gumu kama hilo ni wale wa ziada kwa kimombo wanaoitwa Kenya Police Reservists (KPR). Lakini baada ya miezi michache.
Mhe. Naibu Spika hata kama hatuelewi Kiswahili sana hatusemi "esi" au "anasi". Wanaitwa wauguzi. Kwa hivyo ataje inavyofaa.
Mhe. Naibu Spika jambo la nidhamu la mhe Wamunyinyi imenipoteza kidogo maanake halikunihusu. Nikimaliza iwapo polisi wanasema wanataka kufanya uchunguzi wa kiafya kwanza ama kutumia mbio kama mbinu inayoonyesha ni kurutu gani bora katika Bura daktari ni mmoja na ndiye anakagua makurutu 100. Je tutazuiaje ufisadi? Nikimaliza Bw. Kavuludi alisema yeyote mwenye malalamishi ampelekee lakini karani akasema kwamba mwenyekiti hachukui malalamishi yoyote. Tunataka mbinu badala ya kupeleka malalamishi kwa sababu kuna mchezo wa paka na panya. Inafaa kuwe na tume huru ambayo itachunguza jambo hili. Wale wanaoajiri ni tume ya Kavuludi. Itajichunguza vipi? Afadhali malalamishi yaende kwa Kamati ya Bunge maanake walipokuwa wakiajiri walisema hawataki maoni ya wanasiasa. Kwa vile ufisadi umedhihirika wacha wanasiasa wauchunguze.
Mhe. Naibu Spika je ni haki kwa Kiongozi wa Walio Wengi kutumia nafasi yake siku zote hapa kwa Bunge kutishia akina mama? Siku zote anatishia maisha ya akina mama. Kila kitu kinachofanywa anatishia wanawake. Akisema is indigenous species yeye kama Kiongozi wa Walio Wengi anafanya nini? Ikiwa kuna indigenous species tunajua Serikali huchukua hatua kuwalinda sio kuwatishia. Yeye anafanya nini? Amezoea. Wakati nilipoenda na Atwoli alinitishia; saa hii anatutishia. Mara anatuita flower girls. Ni haki hiyo?
Mhe. Naibu Spika kama kuna masahihisho yoyote ambayo yanahitajika ni jambo la kawaida watu kusahihishana. Ninaomba niwafahamishe Wabunge kuwa Baba Mtakatifu atawasili kesho. Wabunge wamealikwa na Serikali waende Ikulu kesho wawe pamoja na Rais akimpokea na kumkaribisha Baba Mtakatifu katika Ikulu hapo kesho. Kila Mbunge amepatiwa cheti cha mwaliko. Iwapa kuna Mbunge ambaye hajakipata cheti hicho ninamshauri aende kule sebuleni akakichukue. Pia kuna pasi ya gari. Hapo awali tulifikiria tutapata basi ili tuende pamoja lakini imeamuliwa kuwa kila Mbunge yuko huru kutumia usafiri wake binafsi mradi tu aweke kibandiko ambacho kinamruhusu kuingia huko Ikulu. Munaelewa kwamba mpangilio huo umezingatia masuala ya usalama. La pili kuna ibada ya misa siku ya Alhamisi kuanzia saa kumi
Mhe. Naibu Spika Kipengele cha saba cha Katiba ya Kenya na Kanuni za Kudumu 77 zinatambua Kiswahili kama lugha ya taifa. Tunaomba Bunge litafi Kanuni za Kudumu kwa Kiswahili maana wanaozungumza Kiswahili wanatatizika kutafi kutoka Kiingereza hadi Kiswahili. Hii ni kwa sababu Bunge limetunyima fursa. Naunga mkono mpaka Bunge litakapotupatia kanuni kamili.
Mhe. Naibu Spika kwa niaba yangu na kwa niaba ya watu wa Bomet na Bonde la Ufa kwa jumla ningependa kumuomboleza Mhe. Kipchoim na wenzangu. Nawashukuru watu wa Baringo kwa kumchagua hata wakati alikuwa hajaelekea pale kufanya siasa zake.
Mhe. Naibu Spika kwa sababu naona muda wangu umeenda sana mara nyingi twarejelea lugha yetu ya Kiswahili kwa sababu wahenga walisema kuwa "mwenda tesi na omo marejeo ni ngai". Kwa sababu muda hauniruhusu na Waswahili husema "ana eno mengi kama chiriku aliye kunywa maji ya chooni". Mimi sijayanywa na ninaunga mkono Hoja hii.
Mhe. Naibu Spika kwa unyenyekevu ningependa kumkosoa rafiki yangu kuwa Bunge hili ndilo linalotengeneza bajeti ya nchi. Liko na wajibu wa kujua pesa zitakazoenda kwa afya na kwa NYS. Tusiweke mambo hayo kwa Serikali. Serikali inaweza kuleta mapendekezo yake lakini ni wajibu wa Bunge hili kutengeneza bajeti ya nchi na kutoa pesa kwa NYS na kuweka pesa kwa afya kama Bunge hili linaona ni sawa.
Mhe. Naibu Spika Mhe. wa Kiharu anataka kupotosha Bunge. Ukija katika kaunti yetu ya Taita Taveta utapata watu wanapata fedha kwa kuhifadhi miti. Kwa hivyo kutojua kwake na kutoelewa kwake kusije kukajumuishwa kuwa nchi yote ya Kenya haina ufahamu kama yeye. Ninaomba Mhe. wa Kiharu asipotoshe Bunge kwa kutojua yaliyoko nchini.
Mhe. Naibu Spika mimi nilikuwa ninataka maelekezo kutoka kwako kuhusiana na wafanyikazi wetu kwa sababu hawajalipwa tangu Julai. Ningetaka unipe maelezo kwa sababu wana matatizo mengi sana kule ofisini.
Mhe. Naibu Spika nachukua nafasi hii kwanza kukushukuru kwa kunipa nafasi hii niweze kuchangia mjadala huu. Mjadala huu kusema ukweli ni mjadala ambao unagusa roho ya uchumi kule nyanjani. Mhe. Naibu Spika wa Muda vijana wa boda boda ni fungu ambalo tunaweza kusema linasaidia katika ajira mashinani lakini ni sehemu ya uchumi ambayo haijatiliwa maanani kuboreshwa. Ninampongeza Mheshimiwa kwa kuuleta huu mjadala na ningeomba badala ya Hoja hii alete Mswada wa sheria ili tuweke sheria mwaafaka ambazo zitaweza kusimamia sekta hii. Kama walivyozungumza wenzangu vijana wa boda boda wana mengi ambayo wanastahili kufanyiwa. Utapata Waheshimiwa mara nyingi ndio ambao wamesimamia yale matatizo ambayo yanawakumba hao vijana; kwamba mtu akiumia na ile pikipiki Mheshimiwa ndiye anampeleka hospitali. Kama ni leseni ni Mheshimiwa anashughulikia. Lakini kuna njia ambazo Serikali kupitia kwa hili Bunge inaweza kuboresha biashara hii iwe ya ufaa zaidi. Kwanza utakuta kwa mfano kama kule kwetu Kaunti ya Kwale hao vijana kupata leseni ni lazima waende Mombasa. Ingekuwa bora ikiwa kupitia kwa wizara inayohusika na usafiri kungekuwa na shule maalum ya kuwapatia watoto hao mafunzo. Wakimaliza mafunzo yao wapewe vifaa viwili au vitatu kama vile kofia ambayo ni lazima wawe nayo wakati wa kuendesha pikipiki. Pia abiria lazima awe nayo. Kwa nini ninapendekeza hivyo? Ukiangalia yule kijana wa boda boda kwanza yeye hana ajira. Kwa hivyo hana pesa za kununua vifaa vinavyohitajika. Wakipatiwa yale mafunzo na wakimaliza wapatiwe zile kofia. Itakuwa pia tumewapunguzia ule mzigo ambao wako nao wa kuendesha pikipiki wakiwa na usalama wa miili yao na abiria wao. Lingine wizara hii inapaswa kushughulikia ni barabara zetu. Kusema kweli barabara zetu zimechangia yale matatizo ambayo tuko nayo kutokana na uendeshaji wa pikipiki. Barabara zetu ni nyembamba na kwa hivyo inamlazimu mwenye pikipiki aingiliane katikati na magari. Barabara zingine hasa kule mashinani ukiangalia vile zilitengenezwa ni nyembamba na ni kama zina milima katikati. Kwa hivyo yule mwenye pikipiki inamlazimu apitie katikati ya barabara na kama kuna magari pande zote za barabara kuzihepa inakuwa ni shida na mwishowe pikipiki inapinduka na kuleta hatari ya mtu kuumia ama kufariki. Kwenye hospitali nyingi kuna vyumba vya malazi vinavyoitwa " Boda Boda Ward". Hiyo ni kwa sababu watu wote wanaolazwa kwenye vyumba hivyo wanaathirika kwenye ajali za pikipiki. Tukiangazia usalama pikipiki zinafaa kuwekewa kifaa aina ya "Track It" kama magari kwa sababu baadhi ya pikipiki zinatumiwa na wahalifu. Juma lililopita kule kwetu Kwale kuna mzee aliyeuawa na majambazi waliokuwa kwenye pikipiki. Hiyo siyo mara ya kwanza kisa kama hicho kutokea. Visa kama hivyo vimekuwa vikitokea mara kwa mara katika sehemu hiyo. Kukiwa na kifaa cha "Track It" kwenye pikipiki itakuwa rahisi kujua pikipiki hiyo iko wapi ni ya nani na ilikuwa na nani wakati uhalifu ulipotekelezwa. Mwendo wa pikipiki hiyo utafuatiliwa kupitia mahali maalum pa kuangalia pikipiki zinatembea katika sehemu gani. Kama walivyosema wenzangu inafaa tuwe na hazina itakayotengwa na Bunge hili ili vijana waweze kuwa na pesa zao. Pesa zilizotengewa vijana kupitia Uwezo Fund ni ndogo mno na hazitawafikia watu wote. Kukiwa na fedha maalumu zitakazoelekezwa upande wa matatu na pikipiki hazitaweza kuchukuliwa na watu wengine isipokuwa washikadau kwenye sekta hizo. Watapewa mikopo nafuu itakayowawezesha kufaidika na kujisimamia. Wataweza kununua vipuri vyao ama kuwa na maduka ambayo yatakuwa yakiuza vipuri vyao badala ya kufanya safari ndefu. Kwa mfano kule kwetu Kwale kununua vipuri ni lazima mwenye pikipiki atoke aende Mombasa kutafuta vipuri vya pikipiki. Pia watakuwa wanaweza kujifundisha mambo ya biashara na kuzipanua zile biashara zao. Naunga mkono mjadala huu na ni mjadala ambao una ufaa kwa vijana wetu na pia ukipanuliwa zaidi kulingana na mipangilio ambayo ipo ya Serikali utaweza kuwa wa ufaa na kuinua uchumi wa nchi hii ama kwa kaunti zetu kwa jumla. Tutaweza kuondoa ule upungufu wa ajira miongoni mwa vijana wetu. Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hii.
Mhe. Naibu Spika nakushukuru kwa nafasi hii. Nilitaka kusimama kwa Hoja ya Nidhamu na sikupata nafasi hiyo wakati Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni alipokuwa akiongea. Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni alisema Hoja hii ambayo Mhe. Ali alitoa ni bure kabisa. Huo ni upotevu wa nidhamu na lugha hii haikubaliki katika Bunge letu.
Mhe. Naibu Spika nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii. Imekuwa kazi ngumu sana. Niliomba kura kwa wiki tatu na nikapata kura 50000. Lakini
Mhe. Naibu Spika naomba kutoa taarifa ya Hoja ifuatayo: KWAMBA tukitambua kuwa Ibara ya 43 ya Katiba imebainisha kuwa kila mtu ana haki ya kupata kiwango bora zaidi cha afya kinachojumuisha haki ya kupata matunzo ya kiafya na kutonyimwa matibabu ya dharura; aidha ikifahamika kwamba gharama za matunzo ya kitabibu katika taasisi za kiafya za kibinafsu zingali ghali mno hivyo kuwalazimu Wakenya wengi kupendelea kusaka huduma hizo kwa hospitali za umma; tukizingatia kwamba licha ya bei nafuu ya matibabu katika hospitali za umma ikilinganishwa na hospitali za kibinafsi bado Wakenya wengi hawamudu hivyo basi kutumbukia kwenye madeni ufukara na dhiki wanaposhindwa kulipa malimbikizi ya gharama za matibabu yao na ya wapendwa wao; Bunge hili linahimiza Serikali ya kitaifa kufutilia mbali gharama zote za matibabu ya wagonjwa wote wanaofariki wakipokea matibabu katika hospitali za umma. Asante Mhe. Naibu Spika.
Mhe. Naibu Spika naomba nichukue nafasi hii nichangie Mswada huu ambao umeletwa Bungeni kuhusu Mkaguzi Mkuu. Niko na mambo matano au sita ambayo ningeomba niyaangazie ili tupate mwelekeo unaofaa kuhusu Mswada huu ambao umeletwa Bungeni. Kitu cha kwanza ni uhuru wa Mkaguzi Mkuu. Mkaguzi Mkuu ambaye anahusika na ukaguzi wa vitabu vyote au hesabu zote za Serikali pamoja na mashirika ya Serikali anahitaji kuwa na uhuru wa kuajiri wafanyikazi wake. Tukiangalia kipengele kimoja Tume ya Uajiri wa Umma kwa kimombo "Public Service Commission" ndio inatakiwa kuajiri wafanyi kazi wa Mkaguzi Mkuu. Utakubaliana na mimi kuwa tukifuata mwenendo na mtindo huo tutakuwa tunamnyima Mkaguzi Mkuu wa Serikali na mashirika yake uhuru wa kuwachagua wafanyikazi ambao anahitaji kulingana na vyeo majukumu na sifa zao. Kama vitengo vingine vya Serikali vinaajiri watu wake vyenyewe kwa nini tumnyime Mkaguzi Mkuu wa Serikali uwezo huo? Maoni yangu ni kuwa apatiwe uhuru wa kuwaajiri wafanyikazi wake kulingana na uwajibikaji wa ofisi yake. La pili ni kiapo. Mkaguzi Mkuu anahitajika kula kiapo mbele ya Mkuu wa Sheria. Kwa nini aapishwe mbele ya Mkuu wa Sheria? Kwa nini asiapishwe mbele ya Rais? Haieleweki ni kwa nini aapishwe huko. Kwa nini asikichukue kiapo chake mbele ya Rais? Naomba tuyachunguze mambo haya ili tuone ni vipi tunavyoweza kumfanya Mkaguzi Mkuu awe na uhuru aonekane kuifanya kazi yake bila upendeleo na bila kufuatiliwa ama kuwa na uoga. Jambo lingine ambalo ningeomba kuangazia ni makadirio. Hivi sasa inabainika wazi kuwa inambidi Mkaguzi Mkuu kupeleka makadirio yake kwa afisa anayehusika na fedha kwenye Hazina ya Kitaifa. Kwa nini ayapeleke huko? Kwa nini haya makadirio yasiletwe Bungeni kama ana uhuru wake? Hii itampatia Mkaguzi Mkuu nafasi ya kufanya makadirio yake kuyaleta Bungeni kama vile sisi tunayafanya yetu na kama vile wanasheria wanaleta yao wenyewe. Kwa nini alazimishwe kuyapeleka makadirio yake kwa kitengo cha fedha ambacho yeye mwenyewe ndiye anakikagua? Inabainika wazi wazi mara nyingi kuwa akiomba kuongezewa fedha fedha zake zinapunguzwa ili asije akawa na nafasi ya kuchunguza mashirika yote pamoja na Hazina ya Kitaifa. Kila wakati Hazina ya Kitaifa inapunguza fedha za Mkaguzi Mkuu ili isipate nafasi ya kufanya ukaguzi wa kutosha. Kama itawezekana Niko na ii itawezekana kwa sababu nimemsikia mwenyekiti wa kamati ambayo inahusika na jambo hili mhe. Langat ambaye alikuwa hapa akisema kuwa atapokea na atakubali mapendekezo ambayo yatatoka kwa umma pamoja na sisi Wabunge ambayo yatapendekeza kuwa Mkaguzi Mkuu apatiwe uhuru wa kutekeleza wajibu wake kama vile Katiba inavyomhitaji. Jambo lingine ambalo ningependa kuchangia ni kuhusu majukumu ya Mkaguzi Mkuu. Majukumu haya yameongezeka. Hivi sasa tuna Serikali za ugatuzi 47 na zote zinahitaji kuangaliwa na Mkaguzii Mkuu. Fedha ambazo amepatiwa ni zile zile alizokuwa akipatiwa wakati hatukuwa na Serikali za ugatuzi. Tuulizane wazi: Je hiyo ni haki? Hawezi kuifanya hii kazi kama ana fedha zile zile ambazo alikuwa nazo wakati ambapo hatukuwa na Serikali za ugatuzi. Kuna mashirika mengi ambayo yameundwa. Kuna ile hazina ya maeneo ya uwakilisha Bungeni ambayo tunaiita CDF. Mkaguzi Mkuu anahitajika kufanya ukaguzi huko na fedha ambazo anazo ni zile zile ambazo alipangiwa. Tumeunda mashirika mengi na yote yanahitaji ukaguzi wa vitabu kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Hataweza kuifanya kazi hii kama hataongezewa fedha. Kama makadirio yake yatapitia katika Hazina ya Kitaifa ninasikitika na nina uoga na wasiwasi kuwa hatapatiwa fedha ambazo ataomba. Makadirio yake na ombi lake yanafaa kuja moja kwa moja Bungeni ili yashughulikiwe na Bunge. Yeye atakuwa na uhuru wake na sisi tutapata muda wa kuchangia na kumuuliza "Hizi fedha unazoziomba ni za kufanya kazi again?" Yeye ataijibu kamati ya Bunge na kuieleza vile anavyotaka kuutekeleza wajibu wake. Hapo tutamsaidia na kumpatia peza za kutosha ili kuwajibika. Lakini ikiwa ni lazima apitie katika Hazina ya Kitaifa ninasikitika kwamba hataweza kupata kile atakachohitaji. Nikiongea kuhusu usalama mara nyingi tumeambiwa Mkaguzi Mkuu hawezi kukagua vitu ambavyo vinanunuliwa na ambavyo vinahusu usalama wa nchi. Hapo ndipo kuna ufisadi wa hali ya juu. Pendekezo langu ni kuwa aruhusiwe kukagua na akitoa ukaguzi wake si lazima huo ukaguzi uchambuliwe ama uwekwe hadharani. Unaweza kupelekwa kwa Rais kwa sababu hata Rais angependa kujua ni mambo gani ambayo yanatokea katika mashirika hasa katika mashirika ambayo yanahusika na usalama. Kwa mfano jeshi letu linanunua vifaa ambavyo vinahitajika. Lakini tukiangalia vile Mswada huu umeletwa kuna pahali ambapo wanataka kujikinga kabisa na vitabu vyao visichunguzwe. Je nani atagundua kama kuna ufisadi kama hatutamtarajia Mkaguzi Mkuu aangalie hivyo vitabu na angalie fedha za umma zimetumiwa namna gani? La mwisho ni sikitiko kuona kuwa kila mwaka na kila muhula Mkaguzi Mkuu akitoa ripoti yake inaletwa Bungeni. Inaenda kwa Kamati mbalimbali wanazijadili na kisha wanatoa maoni yao na wanapitisha maamuzi. Maamuzi haya yakipitishwa hayatekelezwi. Utaona kwamba wanaohusika wanaachwa na wanaofanya wizi wanawachwa. Hawashughulikiwi. Wakati huu kwa sababu tunakuja na sera na uwajibikaji mpya wa ukaguzi ripoti yoyote ya Mkaguzi Mkuu ikiletwa Bungeni tukiipitisha wale ambao hawajatekeleza majukumu yao kulingana na ripoti ya Mkaguzi Mkuu basi wachukuliwe hatua. Wasiachwe waendelee hivi hivi. Inaonekana ni fedheha. Mwaka baada ya mwaka ripoti zinakuja hapa Bungeni tunazichangia tunazizungumzia tunatoa mapendekezo yetu na baada ha hapo mambo yanakwisha. Ripoti inawekwa kwa kabati inaokota vumbi inaliwa na panya na kombamwiko wanailalia. Tunafaa kusisitiza na kuweka wazi kuwa wakati huu ripoti ya Mkaguzi Mkuu ikipitia Bungeni itatekelezwa.
Mhe. Naibu Spika nasimama kwa hoja ya nidhamu nikitaka kujua kama Mhe. Simba Arati ako sawa kutuonyesha kidole na kutuambia kwamba chetu kiko motoni na kutumia vitisho kwenye hotuba yake kuhusu kupunguza muda wa kuchapisha Mswada kutoka siku 14 hadi moja. Hilo jambo linastahili sisi kutishwa? Ni jamaa ambaye anauza mboga Kawangware na mimi ni daktari!
Mhe. Naibu Spika nilikuwa nimeguzwa sana kwa sababu mhe. Mbunge amesema anapoitisha gari anaambiwa hakuna mafuta. Kwa hivyo tuangalie hilo na tena kuweka maafisa wa usalama ndio waweze kumsaidia; hili pia lifanyike katika maeneo mengine ambapo watu wanalia kama yeye.
Mhe. Naibu Spika niliuliza taarifa kutoka kwa Mwenyekiti anayesimamia Kamati kuhushu Ardhi. Hajakuwepo Bungeni kwa muda mrefu. Leo nimemuona. Ni matumaini yangu kwamba nitaweza kupata taarifa hiyo sasa hivi maana alikuwa amenidokezea kwamba yuko tayari na anangoja tu kuulizwa aitoe taarifa yake.
Mhe. Naibu Spika nimemaliza. Kazi zote za akina mama zinafanywa na sisi. Kila kitu kinafanywa na wamama. Hata nyumba ikiwa baridi wewe huwezi kuingia. Kwa hivyo tunaomba Kenya nzima ituunge mkono. Saa hii ninashangaa kila Mjumbe anatoka nje. Katika Bunge la Kumi na la Kumi na Moja tulipigania Mswada huu na ninaomba tuupitishe. Ninaunga mkono na ninawaomba magavana wetu mahali popote wanapotusikiza watuunge mkono. Wawakilishi wetu wote wa kaunti pia watuunge mkono.
Mhe. Naibu Spika nimesikia Mhe. Richard Onyonka akikuita Mama Spika. Najua hakuna Mama Spika ama Baba Spika katika Bunge hili. Spika ni Spika. Kwa hivyo anapaswa kurekebisha akuite jina linalofaa unapoketi katika Kiti hicho. Akina mama wako nyumbani!
Mhe. Naibu Spika nimesimama kulipinga tengenezo badilisho hili ambalo Mhe. Korir amependekeza. Nalipinga kwa sababu hatutaki kuwa tunakaa tukingoja maafa yatokee ili tuyashughulikie. Tunataka tuzuie maafa. Kama itakuwa silaha zifuatiliwe popote zilipo ni lazima kuwe kumewekwa mikakati. Polisi jeshi ama kitengo chochote kile cha usalama kinapaswa kuwa na mikakati ya kufuatilia mahali ambako silaha ziko. Hatutaki kungojea mpaka shida itokee ndiyo tuanze kutapatapa. Nina ii kwamba tukiingiza pesa katika hali ambayo imepangiwa na kusitokee mambo ya ufisadi tutaweza kuokoa maisha ya Wakenya mahali popote walipo kuliko vile ambavyo hali iko. Hivi sasa pesa zinatumika lakini haieleweki zinatufaidi vipi ilhali watu wanapoteza maisha yao. Katika maeneo ya ufugaji kila asubuhi kuna watu ambao hujitengenezea bunduki. Je bunduki hizo nazo tuziache? Ni lazima kuwe na mikakati ambayo itatumika kuzitafuta na kutambua mahali ziko. Kama mtu ana bunduki ambayo haikuandikishwa na kujumuishwa kwenye mpangilio huo ichukuliwe kwamba yeye ni mhalifu. Tusipitishe tengenezo badilisho ambalo litabadilisha sheria ambayo itatusaidia kuzuia maafa. Tupitishe tengenezo badilisho la kutumika wakati ambapo maafa yametokea. Tukizingatia hali tuliyo nayo katika nchi hii ni lazima tusimame kidete kama Waheshimiwa tutunge sheria ambazo zitamuokoa mwananchi awe salama pahali popote alipo.
Mhe. Naibu Spika nimesimama kwa hoja ya nidhamu kuulizia Swali niliuliza hapa Bungeni kuhusu. Hii ni ngumu.
Mhe. Naibu Spika ninakubali kuwa huyu shangazi anatoka Embu. Lakini tukubaliane kwamba Embu iko katika Mkoa wa Kati. Ngoja nimalize. Watu wa Embu Mkoa wa Kati na hata Mkoa wa Mashariki ni sawa na hawana tofauti. Wakati wa kura wanasema wako pamoja lakini ikiwa ni kugawanya vitu inakuwa wako tofauti. Ninatumai wakati umefika tuambiane ukweli na ukweli usemwe. Ningependa kusema kwamba ninaiheshimu na nitaendelea kuiheshimu Tume ya Mishahara na Marupurupu. Ningependa kutamatishia hapo. Mhe. Naibu Spika siungi mkono uteuzi wa mama huyu.
Mhe. Naibu Spika ninakushukuru kwa kunipatia nafasi hii. Nikianza ningependa kumwambia Mhe. Cecil Mbarire ajue tofauti kati ya chuo kikuu na college . Ninamwomba ajue jambo hili. Yangu ni kumwambia tu kuwa watu ambao walienda college hawakuenda chuo kikuu. Kwa hivyo Mhe. Mbarire
Mhe. Naibu Spika ninaomba niheshimu uamuzi wako na mwelekeo wako kwa Bunge. Hata hivyo mimi ni mwanachama wa Kamati ya Ardhi. Matamshi yangu hayamaanishi kwamba ninaupinga uamuzi wako. Wakati tulipotoa uamuzi wetu kama Kamati hatukuwa tumeipata barua uliyoinakili hapa. Kama tungekuwa tumeipata labda uamuzi wetu ungekuwa tofauti. Kutokana na uamuzi wako inabainika kwamba Kamati ya Bunge ilienda kinyume na kanuni na sheria za Bunge kwa kuzungumzia suala hilo kwa vyombo vya habari. Kamati ya Bunge haikuwa na habari kabisa kuhusu waraka huo. Ndiyo maana Kamati ya Bunge imetoa mwelekeo mwingine. Je hiyo barua ilikuwa wapi? Hayo ndiyo mambo ambayo ningependa yawekwe wazi. Ndiyo maana Kamati ya Ardhi inafikiria kwamba labda kuna udanganyifu fulani ama kuna mambo fulani ambayo yanatokea bila ya kuwepo kwa uwazi. Kama tungekuwa tumeipata barua hiyo bila shaka uamuzi wetu ungekuwa tofauti. Ninaomba nieleweke na wenzangu kuwa Kamati haikuwa imeipata barua hiyo. Ahsante.
Mhe. Naibu Spika ningependa kukushukuru kwa kunipa nafasi hii ili nami nichangie Hotuba ya Rais kwa Taifa. Kwanza ningependa kumshukuru Rais kwa Hotuba yake kwa taifa ili tujue mafanikio changamoto na mambo ya usoni katika nchi hii. Rais ametimiza ahadi ambazo alitoa katika ifesto yake ya Jubilee. Jambo la kwanza alituahidi kwamba atafufua uchumi wa nchi hii. Kwa kweli uchumi wa nchi hii umefikia asilimia sita. Hiyo ni maendeleo. Aliahidi kwamba kila shule ya msingi ya umma itawekwa stima. Kati ya shule 20500 shule 18400 zimewekwa stima. Ingawa tunafurahia hayo katika kaunti ninayotoka ya Turkana watu wangu wa Mji wa Lodwar hawajapata stima kwa wiki nzima. Wafanyabiashara wamepata hasara. Wenye maduka wamepoteza vitu ambavyo vinahifadhiwa kwa kutumia stima. Hoteli zimeenda hasara kwa sababu ya kutokuwa na stima. Ingawa Rais alikuwa ameweka mkazo kwa mambo ya stima naomba stima ya Lodwar iwe inatoka Turkwel kuliko kutumia jenereta ambayo imechangia hasara katika kaunti ya Turkana. Rais pia alitoa miradi ambayo ameibuni kwa ajili ya kuinua maisha ya Wakenya kwa mfano kunyunyizia mashamba maji. Ikiwa nchi hii itaelekea katika njia hiyo hata kaunti ya Turkana ambayo haina ardhi nzuri ya ukulima ikipata maji na kunyunyizia kwenye mashamba shida moja itakuwa imetatuliwa. Tutapata chakula katika udongo wetu. Rais pia aliongea juu ya ujenzi wa reli ya kisasa. Hiyo reli itabuni nafasi nyingi za kazi kwa vijana na itafanya uchumi wetu kuinuka. Tunakubaliana na Rais ya kwamba mradi wa LAPSSET pia unaweza kuchangia nafasi za kazi kwa vijana wetu katika nchi hii. Rais alichangia mambo ya ujenzi wa barabara lakini kuna shida. Katika Kaunti ya Turkana tumepoteza maisha ya watu wengi. Biashara kati ya Turkana na sehemu zingine za Kenya haiendi vizuri. Ukijaribu kupitia barabara kutoka Kitale hadi Lodwar ni kama unaenda mbinguni. Barabara ni mbovu katika Kenya nzima. Hakuna barabara iliyo mbaya zaidi katika nchi ya Kenya kwa Karne hii ya 21 kama barabara ya Turkana. Tunaomba Rais aangalie mambo ya barabara za Kaunti ya Turkana. Katika sekta ya usalama tunashukuru mahali ambapo Serikali imefanya vizuri. Lakini kila wiki katika Kaunti ya Turkana tunazika mtu ambaye ameuliwa barabarani ama kwa sababu ya kuchunga mbuzi wake. Hakuna wiki inapita katika Kaunti ya Turkana bila kuzika mtu aliyeuliwa. Kama vile Mheshimiwa Cheptumo alisema tunaomba Serikali iangalie hali ya usalama ambayo imezorota kati ya Turkana Pokot na Baringo. Watu wetu hawalali na hawana wakati wa kwenda shule kwa sababu ya hali ya usalama. Nikimalizia tunaunga mkono msimamo wa Rais juu ya ufisadi. Watu wengine wanasema kwamba Naibu wa Rais William Ruto ndiye amepoteza zaidi na pengine kabila lake halisikii vizuri. Sisi kama Wakenya tunasema msimamo wa Naibu wa Rais William Ruto kukubali marafiki wake na watu ambao wako karibu na yeye kuondoka afisini kwa muda ni ishara ya kwamba yeye ni kiongozi anayetaka mabadiliko katika nchi ya Kenya hasa kwa mambo ya ufisadi. Watu wetu wanasema kwamba hao wakae kando na wafanyiwe uchunguzi.
Mhe. Naibu Spika ningependa kusimama kuunga mkono Mswada huu. Kwanza ningependa kusema kwamba ukitathmini na kuangalia hii sheria na ulinganishe na ile tuliokuwa nayo mwaka jana ni ishara kwamba kumekuwa na mabadiliko. Kumekuwa na uwiano wa mambo ambayo tunafaa kuyaafikia kama Taifa la Kenya. Inasemekana kwamba hii sheria itazungumziwa na Bunge zote mbili - Bunge la Seneti na Bunge la Kitaifa. Ukikumbuka kulikuwa na tashwishi na watu wakakimbia kwa Mahakama Kuu ili ieleweke ni vipi ambavyo tutaweza kuangazia swala hili. Pia tumeona wakati uliopita kwamba kumekuwa na malumbano kati ya yale maamuzi ambayo yanafanyika kutoka katika korti zetu na kuendelea kwa Taifa. Kwa hivyo tunafurahi kwamba Mswada huu unapendekeza ya kwamba kabla ya kukimbia kortini watu waketi chini na kuangazia maswala tata na kuyashughulikia badala ya kwenda kortini. Pia kipengele hicho kinasema hususan kwamba ikiwa kuna afisa yeyote wa umma ambaye atafanya Serikali gatuzi ipate gharama ya kwenda kortini basi achukuliwe hatua yeye mwenyewe kama mtu binafsi. Pia ukiangalia asilimia ya hela ambazo zimewekwa kufikia mashinani kupitia serikali za ugatuzi ni kweli kwamba zimeongezeka kwa kiasa cha asilimia 43. Lakini pia tumekuwa na mazungumzo kama Kamati ya Bajeti na Makadirio kwamba kulikuwa na kiwango ambacho kilikuwa kimependekezwa na ile Tume ya Ugavi wa Rasilmali cha Kshs279 bilioni. Tulitoka pale hadi Kshs238 bilioni. Kwa hivyo huu mchakato lazima uendelee kwa sababu sijui kana kwamba kupunguza kule ni kutokana na majukumu ambayo yamezidi katika Serikali ya Kitaifa. Pia ukiangalia zaidi nafikiri Wakenya wamekuwa na mwito wa kuhakikisha kwamba hakuna rushwa ambayo inajikidhiri katika maeneo ya mashinani kupitia mifumo ya serikali za ugatuzi. Lakini pia tujue kwamba vile ambavyo tunapiga msasa serikali za ugatuzi ndivyo ambavyo tunatazamiwa pia kupiga msasa Serikali ya Kitaifa. Kuna mwandishi mmoja ambaye anaitwa John C. Maxwell ambaye anasema kwamba ndiposa ufaulu ni lazima ufanye makosa. Nafikiri mwaka huu ni wa kwanza. Kwa kweli tumeona kwamba serikali za ugatuzi zimefanya makosa na kutoka hapa kusonga mbele kutakuwa na mwito mpya kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma. Wananchi wanapata dhaa ya zile hela ambazo zinapelekwa katika serikali za ugatuzi. Ukiangalia Mswada huu unaelezea kinaga ubaga jinsi ambavyo pesa zilizotengwa zitatumika. Jambo ambalo linanifurahisha ni kuona ya kwamba tumepatiana hela za kuboresha polytechnics katika kila kaunti ya nchi hii. Pia kuna hela za kuboresha mahospitali. Mhe. Naibu Spika mwaka jana kulikuwa na tetezi kwamba Kshs16.6 bilioni zilikuwa zimewekwa ili ziweze kutumiwa na serikali za ugatuzi kama masharti fulani yangeweza kufuatwa. Kwa lugha ya Kimombo ukipenda "Conditional Allocations". Kwa hivyo katika masuala ya elimu kuhakikisha kwamba wale ambao hawajahitimu kujiunga na shule za upili wanapata nafasi ya kupata taaluma ili waweze kujikimu katika maisha na kusaidia jamii ndiposa tuweze kuafikia Ruwaza Ya 2030 ninafikiri ni jambo la kutajiwa. Pia kumekuwa na tetesi kuhusu masuala ya usalama na nafikiri jambo hili linaweza kuangaziwa ili vijana wetu waweze kupata ajira na riziki ya kila siku. Mhe.Naibu Spika piani jambo la kutajika kuona kwamba kuna hela ambazo zimetengwa za kuinua miradi ambayo inafaa kusaidia uchumi wetu uweze kukua kwa kiwango ambacho kinafaa. Jambo la kusikitisha ni kwamba Kenya inaorodheshwa kufikia mwezi wa Septemba kuwa na uchumi ambao ni wa nne bora zaidi katika ukanda wa Afrika. Lakini jambo ambalo tunafaa kuangazia ni ni vipi tutaweza kuweka pesa mashinani ambazo zitawasaidia wananchi kupata ajira? Hii ni kwa sababu ukuaji wa uchumi pasipo na ajira si jambo ambalo linasaidia kwa sababu linafanya maskini wawe maskini zaidi na mabwenyenye waendelee kuwa mabwenyenye na matajiri zaidi. Kwa hivyo ni jambo ambalo tunafaa kuangazia ili tuweke masharti ya utumizi wa pesa kuhakikisha kwamba hela ambazo zinafika mashinani zinasaidia kuleta ajira na kuinua kiwango cha uchumi hususani katika familia. Pia katika kiwango cha kitaifa tumekuwa na mwito mpya kama Kamati ya Bajeti na Makadirio kwamba tunaangalia takwimu ama unapatiwa hela ambazo unahitaji lakini lazima uwe ni miradi ambayo unaonyesha kweli kwamba Wakenya wataweza kufaidika. Tungependa Bunge la Seneti liweze kuangalia jambo hili baada ya Mswada huu na ule Mswada mwingine ambao unapatiana hela katika kila kaunti ili wasisitize miradi ambayo kila kaunti inaonyesha ndiposa wasipatiane hela kwa sababu watu wanasema kwamba wametengwa kwa muda mrefu ama watu wanasema kwamba hawajawahi kuangaziwa na Serikali. Mhe. Naibu Spika pia ningependa kusema kwamba ni muhimu katika hiyo miradi kuhakikisha ya kwamba asilimia ya watu walemavu ambao wanaishi mashinani ni 79. Kwa hivyo ni muhimu katika kila kaunti kuwe na hela ambazo zimetengwa ili kuwasaidia kuenda shule na kuhamasisha jamii kuhusu madhara ya kuwatenga watu walemavu na kujua ni vipi wataweza kuhusishwa. Hii ni kwa sababu wakati huu tunaona kwamba pesa nyingi zimewekwa tu katika Baraza la Kitaifa kuhusuWatuWalemavu. Lakini kama ambavyo imesemekana Bodi ya Baraza hilo haijateuliwa karibu mwaka mzima sasa. Hili Bunge lilipeana Kshs1.3 bilioni mwisho wa makadirio ya matumizi ya Serikali na hizo hela hasijatumika. Masuala ya watu walemavu si tu masuala ya Serikali ya Kitaifa bali ni masuala ya serikali za ugatuzi. Kwa hivyo ni lazima magavana na bunge za kaunti tofauti ziweze kuweka pesa ambazo zitasaidia watu walemavu. Ukiangalia deni la nchi utaona kwamba kiasi kikubwa kinatumika. Tumeongeza matumizi yetu kulipa deni kwa Kshs34 bilioni na Kshs60 bilioni zinatumika kulipa malipo ya uzeeni. Vile miaka inavyosonga kutakuwa na watu wengi ambao watakuwa wanastaafu lakini kuna kasumba ya rushwa ambayo inafanya pesa hizo kutowekwa vizuri ndiposa ziwafaidi wale ambao wanastaafu. Kama nchi inatumia Kshs414 bilioni katika masuala haya ni viema tujiulize ni vipi tutahakikisha kwamba tunapata
Mhe. Naibu Spika si nia yangu kutusi ama kushusha hadhi ya kiti cha Naibu Spika lakini ninaomba kama wewe pia ulienda huko ukubali maoni yangu kuwa sikubaliani na Mhe. Mbarire kuwa kilikuwa chuo kikuu. Wakati huo kilikua college. Kwa hivyo wote walioenda huko wakati huo walienda college. Mhe. Naibu Spika ninaomba nitoe mwongozo wangu. Wewe hukusoma huko lakini ulikuwa unafundisha. Hivi sasa tunakubali huyu mama Anne Gitau apatiwe kazi hii. Ninaomba tuulizane maswala kadha wa kadha. Ningependa tuangalie Katiba inasema nini. Katiba inaongea kuhusu usawa wa nchi. Kwa nini kila wakati majina yakiletwa hapa yanaletwa ya maeneo mawili tu? Majina yanatoka Bonde la Ufa ama eneo la Kati. Nikisema hivi si eti ninamchukia mtu. Mimi simchukii mtu. Bi. Gitau amehitimu na ana kila kitu lakini ningependa kusema kwamba wako Wakenya wengine. Mimi sina shida na huyu shangazi. Ninamheshimu amehitimu ana sifa ana elimu na ameenda college Egerton. Kwa hivyo sikatai lakini kama tunataka usawa katika nchi hii lazima tujue kwamba majina mengine yako pia. Wataita Waluhya Wakamba Wasomali Wadorobo na Waogiek wako. Hawa watu wameachwa wapi? Kila wakati majina yanayoletwa hapa ni ya makabila mawili. Kwa nini? Hata Mwenyekiti wa Tume hii anatoka Bonde la Ufa. Mimi sitamuunga mkono leo kesho au kesho kutwa na si kwa sababu hahitimu. Ningependa kusema hivi
Mhe. Naibu Spika siasa ni nyumbani. Niliahidi watu wangu na nilipata target ya Kshs10.7million ya akina mama wa Lamu for the firsttime.
Mhe. Naibu Spika sijui kama umesema ni ni nini lakini ninataka nihakikishe kwamba yale kiongozi amesema ni ya kweli. Tulizungumzia haya eno na tukaamua tupewe mwenye Hoja. Huyo ni Mhe. Ali. Yeye ndiye atapendekeza marekebisho ili hii Hoja ilingane na Katiba ya nchi yetu. Asante sana Mhe. Naibu Spika. Wakati wa kuchangia hii Hoja ukifika hapo ndipo tutajua ni akina nani wako na uwezo wa kuongea Kiswahili sanifu. Mimi nilifanya Kiswahili na nikapita. Namaanisha nilifanya Kiswahili katika mtihani na nikapita. Lazima ufanye mtihani. Unajua unaweza kusoma Kiswahili lakini hukitumii. Nilisoma nikafanya na nikapita mitihani. Naona hata Mhe. Sankok ambaye hawezi kuongea Kiswahili sanifu anapiga kelele nyingi. Asante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii.
Mhe. Naibu Spika sisi wote ambao tuko hapa hata kama tuko literate ama illiterate tulichaguliwa na watu. Mtu akiwa Kiongozi wa Wachache asifikirie amesoma kuliko wengine. Hata sisi tumesoma rafiki yangu. Tulichaguliwa na watu ambao walituleta hapa. Hauna cheo cha kuongea vibaya kuhusu Wabunge wengine ambao walichaguliwa kama wewe. Kwa hivyo is it in order kwa Mbunge kama mimi kuongea vibaya kuhusu mwenzetu ambaye ako hapa?
Mhe. Naibu Spika ufafanuzi ninaomba ni kwamba wakati kulitangazwa kuwa kulikuwa na kazi kulikuwa na pendekezo katika gazeti kwamba wanasiasa wasitoe mapendekezo. Nataka sababu ya hili jambo kwa misingi ya kisheria; kwa nini mwanasiasa asitoe mapendekezo? Pili makurutu waliambiwa wakimbie. Huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhan. Ikiwa hii ndio mbinu inatumika kujua kurutu bora na hali wengine walikuwa wamefunga; je walikimbia sawa na wale ambao hawakuwa wamefunga? Je hii si ilikuwa dhulma kwa Waislamu?
Mhe. Naibu Spika umesikia Mhe. Mohamed Ali akisema "ikiwa Nyumba itapasisha". Hicho si Kiswahili sanifu. Anapaswa aseme "ikiwa Nyumba itakubaliana naye ama kupitisha". Yeye ameleta kile Kiswahili cha sheng eti "itapasisha". Nataka umwambie aondoe neno hilo kutoka rekodi ya Bunge.
Mhe. Naibu Spika utumizi wa neno "kupasishwa" au neno "kupitisha" utategemea lugha unayoitumia. Unaweza kuzungumza Kiswahili cha Mvita au cha Kenya. Kwa hivyo kuna tofauti lakini yote ni moja. Hoja inapitishwa katika Bunge na Wabunge.
Mhe. Naibu Spika wa Muda asante sana kwa kunipatia fursa hii. Ningetaka tu kuipongeza Kamati hii kwa kazi nzuri iliyofanya nakuipongeza bodi yenyewe pia ilivyofanya kazi nzuri hadi Waziri akaona ampatie Bw. Yusuf Mbuno kazi hii ya kusimamaia Hazina hii ya maendeleo katika Maeneo Bunge. La muhimu ni kujua kuwa Yusuf Mbuno amezoea kazi ameiva na kubobea kwenye kazi na sasa ndio ataweza kutufanyia kazi kisawa sawa humu nchini kuhakikisha kwamba hazina hii inatumika kisawa sawa. Naunga mkono uamuzi huu.
Mhe. Naibu Spika wa Muda asante sana kwa kunipatia nafasi hii niweze kuchangia huu mkasa uliotokea katika eneo letu la Mombasa Kaunti ya Mombasa. Kwanza ninatoa pole zangu kwa jamii ya marehemu Mariam na mtoto Ada na kujulisha Bunge hili ijapokuwa walifariki katika kivuko cha Likoni ni wakazi kutoka eneo la Bunge langu la Kisauni na hivi tunavyozungumza tumeanza mipango ya kuchanga pesa katika kusaidia mazishi. Kwa hivyo ninaomba Wabunge wenzangu pia tuweze kusaidiana kwa njia moja au nyingine. Wale wataweza kuchanga tutashukuru zaidi ili tuweze kufikisha msaada ule kwa jamii ambayo imepata mkasa huu. Kwanza kabisa hili ni janga la kitaifa. Ni janga ambalo limeonyesha udhaifu mkubwa kwa taifa la Kenya. Ni aibu ikiwa mkasa huu ulitokea siku ya Jumapili jioni na mpaka leo mili haijatolewa. Jumapili ilikuwa ni tarehe 29 mwezi wa tisa leo tumefika tarehe mbili mwezi wa kumi siku tatu na mpaka sasa tunavoongea hakuna kitu ambacho kimepatikana. Imetuonyesha udhaifu kuwa kama taifa hatuko tayari kupambana na majanga kama haya. Ijapokuwa wakati tokeo la kihuni la wale magaidi litakapotokea katika sehemu hiyo tutaona vitengo vya usalama vinavyohusika kupambana na magaidi vinavyojitahidi. Lakini leo jeshi letu la wanamaji limeonyesha udhaifu mkubwa. Wamefundishwa na wanaujuzi wa kushugulikia maswala ya ndani ya maji. Lakini kwa siku tatu wameshindwa kuokoa wale maiti ambao wako pale ndani na kutoa gari iliyozama katika kivuko cha Likoni. Kama Taifa hii imetuonyesha hatuko tayari kabisa. Kivuko kile cha Likoni kinavukisha magari elfu sita na watu zaidi ya laki tatu kwa siku. Je ingekuwaje kama kwa bahati mbaya feri ile ingezama? Ikiwa tukio la mtu mmoja limetushinda. Je kama feri ile ambayo inabeba watu elfu nne mia tano wakati inavukisha kwa safari moja ingezama? Je tuko tayari kwa swala kama hilo? Hatuko tayari. Hii imetuonyesha tuko na kazi ya kufanya na kama taifa ni lazima watu wawajibike. Ningekuwa Waziri anayehusika na maswala ya usafiri ningekuwa nimewacha kazi kuonyesha imenishinda. Mkurungezi mkuu wa Kenya Ferry Bw. Bakari Gowa angekuwa tayari ameenda nyumbani na yuko korokoroni. Haya ndio mambo yanayofanyika katika nchi zilizoendelea. Maisha ya Mkenya mmoja ni sawa na kupoteza umma mzima. Huyu ni mama na mtoto wake. Ukiangalia mwaka wa 1994 katika kivuko cha Mtongwe tulipoteza maisha ya Wakenya 272 na kivukio kile kiko mita 40 kutoka kambi ya wanajeshi wa maji. Hiyo feri ilikuwa imebeba watu 400. Watu 128 waliokolewa na wavuvi na wapiga mbizi wa mtaani. Lakini kikosi cha Kenya Navy kilishindwa kuokoa maisha. Leo imetuonyesha vilevile udhaifu walionao. Mashirika ya Kenya Ports Authority (KPA) Kenya Maritime Authority (KMA) na Kenya Coast Guard Services (KCGS) ni vitengo tunapatia pesa nyingi. Tunajua pesa tunazopitisha katika maswala yetu ya bajeti katika mambo ya usalama. Ni pesa chungu nzima tunazopatia pande lile. Lakini leo wameshindwa kuokoa gari moja na maiti zilizo ndani kwa siku tatu mfululizo. Hili ni jambo ambalo linatusikitisha sana kama watu wa Pwani Mombasa na Jamhuri ya Kenya. Tukiangalia yale ambayo yametokea ninafikiri kuna umuhimu ile Kamati ya Usafiri iweze kushugulikia swala hili na kulete ripoti hapa katika Bunge la Kitaifa ili tupate kujua kiini cha kilichotokea na kusababisha ajali ile. Pia kitu gani kitafanywa kwenda mbele ili tusije kupata madhara makubwa. Kitu ambacho tunaangalia sasa ni kwamba tutakuja kupata majanga makubwa ambayo tutashindwa kujiondoa kama taifa. Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Mhe. Naibu Spika wa Muda historia ya watu wetu kunyang'anywa mashamba imekithiri. Zaidi ya mara tatu tumeihusisha Tume ya Ardhi kwenye masuala ya mashamba ambayo yamechukuliwa. Lakini Tume hiyo bado haijatupatia mwelekeo wowote. Hivi sasa hata wakazi wangu wa Lunga Lunga wanaoishi kwenye kipande cha ardhi chenye ekari 1083 wanaondolewa. Nyumba zao zimeharibiwa na wataondolewa wakati wowote kutoka kwa mashamba hayo. Mamlaka ya Kukusanya Ushuru (KRA) hukusanya fedha ambazo hutumika kutekeleza miradi ya Serikali. Kupitia Kamati ya Fedha Mipango na Biashara nilitaka kujua viwango vya ushuru wa VAT wanaotozwa wanabiashara wanaoingiza magari humu nchini na jinsi ushuru huo unavyokusanywa. Lakini mpaka sasa sijapata ripoti yoyote. Mwaka umepita sasa tangu nilipowasilisha ombi hilo. Kila siku nikiuliza swali hilo napelekwa huku na kule. Kwa hayo machache naiunga mkono Hotuba ya Rais na kumpongeza kwa sababu maandalizi ya safari ya kesho huanza leo.
Mhe. Naibu Spika wa Muda Hoja yangu ya nidhamu ni kwa mama Leshoomo ambaye namheshimu sana. Labda katika hizo dakika nane amebakisha ningetaka akizungumza katika hii Nyumba atuambie kama anazungumza kama mama ambaye ametembea Samburu ama aliyekuwa katika Kamati ya BBI. Hii ni kwa sababu vile wananchi walisema. Wenzetu wamezungumza kwa niaba ya wananchi na amesahau walitumwa na wao. Kwa hivyo katika hizo dakika zingine nane ahimize anazungumza vile alisikia kutoka kwa wananchi kwa sababu wako na nguvu na walituchagua na kutupatia Katiba ya Kenya 2010. Pia ametupatia.
Mhe. Naibu Spika wa Muda inaonekana kuna njama ya kuukatakata muda wangu. Ninasema hivyo kwa sababu hoja zote za nidhamu zilizotolewa hazina maana. Kwa hivyo ninawaomba Wabunge wenzangu waache kutoa hoja za nidhamu ambazo haziwezi zikatusaidia. Kwa hivyo
Mhe. Naibu Spika wa Muda kama ingekuwa wakati wa siasa ningesema kwamba kuna mtu amenikanyangia. Lakini nataka kuongea kuhusu barabara ambayo imetoka Ruiru na kupitia maeneo matatu ya uwakilishi Bunge. Barabara hiyo imetuletea aibu sana sisi Wabunge watatu wa Kaunti ya Kiambu. Hii ni kwa sababu kila wakati ndizi hupandwa katika barabara hiyo kana kwamba ni shamba. Ninashukuru kwa Kshs5 milioni ambazo zimetolewa. Walakini hii ni madharau.Tunaomba barabara hiyo ambayo inatoka Ruiru hadi Githunguri na inaguza eneo la Mburu Kahangara iweze kupewa pesa yakutosha ili iweze kujengwa vizuri na watu wetu wafurahie. Mtu anaweza kuitumia hiyo barabara kutoka Ruiru akielekewa town. Lakini sasa inabidi mtu atumie njia refu kwa sababu barabara hiyo haipitiki. Ningependa warudi wachore tena na wapatie Barabara ya Ruiru kuelekea Githunguri na Lari pesa ya kutosha ili itengenezwe kama barabara zingine. Hatuna furaha kwa sababu hatutaki viraka katika hiyo barabara. Tunataka barabara itengenezwe vizuri ili tusiaibike kutokana na barabara hiyo kupandwa ndizi. Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Mhe. Naibu Spika wa Muda kama nilivyosema naunga mkono marekebisho machache ambayo Daktari Nyikal amependekeza kwa Hoja hii. Ni muhimu tuweke mikakati ambayo itawezesha mapendekezo tunayowasilisha kutekelezwa. Hivyo basi lazima tuonyeshe njia ya mikakati ambayo itawekwa ili mapendekezo yetu yachukuliwe kwa umuhimu sana na kuweka programmes mahususi za kuhakikisha mapendekezo yamefanyika. Naunga mkono.
Mhe. Naibu Spika wa Muda kama nilivyosema ni masikitiko makubwa kwa sababu nilitarajia Kamati hii ichukue majina ya Wakenya wote waliorudishwa nchini wakiwa wameathirika kwa kudhulumia na kuteswa halafu waende kule wakafanye uchunguzi kuhusu waathiriwa hao. Mwisho ninaamini kuwa kweli watu wengi wanapenda kuenda Saudi Arabia kufanya kazi kwa sababu ya hali ya kiuchumi nchini mwetu.
Mhe. Naibu Spika wa Muda kawaida huwa tunapitisha majina yakiwa pamoja sio moja moja vile Mhe. Mbadi amesema. Kwa hivyo naunga tupitishe wote pamoja.
Mhe. Naibu Spika wa Muda kongole zangu kwa Mhe. Wanga kwa kujaribu kunena Kiswahili ambacho tunakitazamia. Ningetaka kumalizia kwa kusema kuwa katika jamii zetu swala la watu kusoma Kiswahili limekua shida sana. Kuna watu wengi sana ambao Kiswahili hawakielewi. Kwa hivyo ningetaka kuungana na wanenaji wenzangu ambao wamesema kuwa kuna haja ya kuhakikisha kwamba ile elimu ya watu wazima ambayo imekuwa ikitolewa imeregeshwa ndio watu waweze kurudi shule ili wapate mafunzo na wahakikishe wameelewa maswala haya.
Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa sababu upinzani wangu wa Mswada huu unapingwa tutakapoenda likizoni watu wote wajiulize; tukiwapatia maadui nchi hii wataiongoza jinsi wanavyoongoza maandao dhidi ya Tume ya Uchaguzi? Hii ni iwapo tutapeana nchi hii kwao.
Mhe. Naibu Spika wa Muda kwanza kabisa nimesimama kuunga Mswada huu mkono. Pia nachukua fursa hii kushukuru Kiongozi wa Wengi Bungeni kwa kuleta Mswada huu ambao ni muhimu kwa taifa na watu wa Kenya kwa jumla. Sheria iliyo mbele yetu ina vifungu 64 sehemu nane na ratiba ama schedule nne. Lengo na maudhui ya sheria hii ni nini? Ni kwa sababu tunataka kufuta Kifungu 208 yaani National Youth Service (NYS) Act tuibadilishe ili tulete sheria ambayo inaambatana na Katiba 2010 na inaweza tatua matatizo yanayokumba taasisi ama shirika la NYS. Historia ya taasisi ya NYS inasikitisha. Watu wachache wameshirikiana kuwa wafisadi na kudhulumu vijana ambao tumewatuma wasome. Wameenda kuiba pesa. Hii ni hali ambayo imeleta huzuni na kueleweka vibaya kwa NYS katika taifa la Kenya na wananchi kwa jumla. Hali hii imeadhiri utendakazi hadhi na jina la NYS. Tutafanya nini kama Bunge na taifa ili hadhi heshima na jina la NYS lirudi pale lilipokuwa zai? Mwizi ni nani? Ni nani ameiba pesa za umma? Je ni watoto 15000 tuliowatuma kujifunza? La sio wao. Mara hii hatua imechukuliwa kwa waliohusika kuiba pesa za umma. Nashukuru kwa sababu wako mahakai. Kwa hivyo hakustahili kuuwawa kwa taasisi ya NYS kwa sababu ya makosa ya watu wachache. Wale watoto ambao wanaenda kupata mafunzo hawana hatia. Wanafanya juhudi na wajibu wa kujenga taifa la Kenya. Hawastahili kubeba mzigo wa wale walioenda kuiba pesa za NYS. Katika hii sheria lengo kubwa ni kubadilisha muundo ili mara hii kuwe na baraza. Alivyosema Kiongozi wa Wengi Bungeni ni ukweli kwa sababu NYS ilikuwa inaanza na Director-General na inaisha na yeye pia. Tunaleta baraza leo ambalo litaangalia hali ya utendakazi wa NYS. Kama kuna ufisadi baraza lile litakuwa la kwanza kupiga parapanda na kuita Wakenya na kuwajulisha ya kwamba hali haiko sawa huko. Kwa hivyo tumesema tubadilishe muundo wa NYS. Pili kwa furaha kubwa nafurahi na kumpongeza Rais kwa kuleta mabadiliko katika uongozi wa NYS. Moja ameleta Principal Secretary Owino ambaye ametoka mashinani. Alikuwa kama ofisa wa tarafa. Amepanda mpaka mahali ako leo. Ni mtu ana ujuzi na ii kuona kwamba shirika la NYS linaenda mbali. Bwana Matilda Sakwa ambaye ni Director- General wa NYS ni mtu amesimamia taasisi ya umma kwa muda mrefu. Kwa hivyo tukibadilisha viongozi wa taasisi hii na tuwe na sheria mpya kwa hakika lengo la kuwa na taasisi ya NYS inayotoa mafunzo kwa watoto wetu tutaifikia karibuni. Vijana 15000 walimaliza masomo katika NYS juzi. Kwa sababu ya ufisadi katika NYS Kamati ya Bajeti imepunguza zaidi ya Ksh.6milioni ya shirika hiyo. Wale watoto wanaoenda pale kusoma wanataka chakula matibabu na rasilimali. Pesa ile imetolewa imepelekwa kwa barabara. Hii si haki wala si sawa. Kwa mujibu wa Kifungu 118 cha Katiba 2010 na Kifungu 127 cha Kanuni za Bunge tulialika Wakenya kwa jumla. Walikuja wananchi wa tabaka na taasisi mbalimbali ikiwemo Kenya Law Reforms na wizara wakatoa rai zao ambazo tumeweka katika Ripoti. Mtasoma ili ituwezesha kurekebisha sheria iliyo mbele yetu kwa ufaa ya taasisi vijana na taifa la Kenya kwa jumla. Kabla sijasahau ningependa kuchukua fursa hii kushukuru Kamati ya Kazi na Maslahi ya Jamii. Wamechukua muda mrefu kupitia Vipengele 64 moja baada ya nyingine. Tulizungumza mpaka saa zingine tukachoka tukijadili ili kuweza kuafikiana na kutoa sheria kwa taifa la Kenya. Naomba Waheshimiwa Wabunge kwamba NYS sio wezi wezi ni watu ambao wameenda pale na wameshirikiana na viongozi wa hiyo taasisi ili kudhulumu watoto wetu. Ni haki tubadilishe sheria ili vijana wapate mafunzo pale ili wahudumie taifa la Kenya. Ombi langu kwa Waheshimiwa Wabunge ni wapitishe hii sheria ili tuweze kuhudimia Wakenya. Kwa hayo machache Mhe. Spika wa Muda naunga mkono sheria hii. Asante.
Mhe. Naibu Spika wa Muda labda wakati wanasajili hawa maajuza pia ndugu wetu anaweza kuwa ni baadhi ya wale ambao watafaidika na hizi fedha. Tukiangalia masuala ya usalama ni Ksh6.9 bilioni imepewa kwa wizara hii. Tunavyoangalia hali ilivyo sasa hivi tunavyoangalia jinsi utangao wa Wakenya ulivyo kwa sababu ya hii marudio ya uchaguzi inahitajika kwamba Katiba ya Kenya inaruhusu kuhakikisha kila Mkenya kwamba serikali itashughulikia usalama wao na usalama wa mali yao. Na hii haiwezi kufanyika iwapo idara ya kusimamia usalama haitapewa fedha jinsi wanavyohitaji. La muhimu zaidi pia tukizingatia hali ya anga ilivyo nchini sasa hivi tunagundua kwamba baadhi ya maeneo ama majimbo ya nchi hii yamekumbwa na janga baya sana la njaa. Na baadhi ya maeneo hayo ni kama vile pahali ninakotoka. Inahitajika hatua za dharura ili kutatua ama kushughulikia wananchi ambao wanaangamia kwa sababu ya janga la njaa. Haswa maeneo ambayo yamekumbwa zaidi ni pahali ambapo wafugaji wanatoka. Wafugaji wengi ambao wameketi hapa wanaotoka Wajir dera Marsabit Moyale na kule kwingine kama Narok Kajiado na mahala pengi hata mifugo yao sasa imeangamia. Ukitazama chini ya idara ya kilimo utagundua kwamba Ksh950 milioni ambayo kwa malengo yangu ni kidogo itashughulikia kununua wale mifugo kabla ya wao kuangamia ili ipee afueni wale wafugaji ambao kwa sasa hivi hawana la kufanya na hawa mifugo ambao lishe imewaishia maji hamna na wamekuwa hohehahe wasiwe na mbele wala nyuma. Ninapotia tamati baadhi ya fedha hizi zimewekwa ili kushughulikia usambazaji wa umeme na kununua gesi ya kupika. Tunapozungumza uhifadhi wa misitu ni muhimu katika nchi hii yetu ili tupate maji na kwa mifugo yetu. Tusiposhughulikia uhifadhi wa misitu labda itakuwa vigumu kidogo kwa nchi. Kwa hivyo ningeomba Bunge hili Waheshimiwa walioko hapa na hata wale ambao wataingia kwa muda usio mrefu waunge mkono makadirio ya matumizi ya Bajeti wa mwaka 2017/2018 ili tuendeleze nchi yetu mbele na kuhakikishia wananchi kwamba kazi muhimu ambayo walitupatia ya kuwawakilisha kwa kweli tumeifanya. Nikitia tamati ningependa pia kuchukua nafasi hii kuwashukuru wanalaikipia hasa kutoka Laikipia Kaskazini kwa kunipa muda wa kuwashughulikia kama Mbunge mteule na wala sio Mbunge maalum tena. Shukrani Mhe. Nibu Spika wa Muda.
Mhe. Naibu Spika wa Muda mazingira yameharibika. Ile mvua tulikuwa tunapata zai haipo tena. Mtu anapoongea juu ya unyunyizaji maji wa mashamba huo ni mwelekeo mwema. Mwenyezi Mungu kabla hajatuumba sisi binadamu alitupatia maji hewa na chakula. Vitu vingine kama vile nguo na usalama yalikuja baadaye. Ukimpa binadamu chakula utakuwa umempa maendeleo. Ukifananisha nchi yetu ya Kenya na nchi zingine utakuta kwamba Mwenyezi Mungu alitupa ardhi nzuri ambayo ina rotuba nyingi. Shida ni kwamba mipangilio yetu haiko sawa sawa. Yule aliyeleta huu Mswada kuhusu unyunyizaji maji sharti tumpe kongole. Kule kwangu katika Kaunti ya Taita Eneo Bunge la Mwatate kuna milima mingi. Mikondo ya maji pia ni mingi. Kila wakati maji ya mvua yanabomoa nyumba za watu. Maji hayo huwa mengi kiasi cha kuathiri wananchi. Tungekuwa tunatengeneza mabwawa ama c heckdams basi tungewasaidia wananchi pakubwa sana. Hayo maji yaliyohifadhiwa yanaweza kutumika na wafugaji kwa mifugo yao na hata yakanywiwa na watu. Aidha yatatumika katika unyunyizaji maji kwa mashamba na mambo mengine mengi. Rotuba ya Taita Taveta na Mwatate kwa ujumla ikipata maji inaweza kulisha Kenya nzima. Maji tu ndiyo tatizo kubwa. Wananchi sasa hivi wanashindana na wanyama kwa sababu ya maji. Nakumbuka mwaka juzi Februari tulipoteza watu kumi na wanane kwa sababu ya kutumia maji yaliyokuwa na madhara. Kule kuna madini. Ukichimba kisima utagundua kwamba maji yake yana madini. Baada ya muda mrefu wananchi wanaokunywa hayo maji hupatikana na matatizo. Mabwawa yakitengenezwa yatasaidia sana. Yale maji ambayo huelekea baharini tutayahifadhi. Lakini yakizuiliwa itakuwa vizuri. Kama unavyofahamu kule kwetu Taita Taveta ndiyo eneo pekee hapa Kenya ambayo ni disease free zone . Hata watu ambao wanalisha ng'ombe wakitaka kuziuza wanazileta huko kwetu. Lakini maji ni tatizo kwetu. Tukiwa na mabawa jimbo letu litakuwa na maendeleo mengi na kwa jumla litasaidia Kenya nzima. Makazi yamekuwa ni taabu. Hapa nchini Kenya wananchi wengi ni wakulima. Kwa kweli Serikali yetu inapaswa kutenga pesa za kutosha ili kujenga mabawa. Tunapaswa kuwa na mpangilio sawasawa ndio tuzidi kuenda mbele. Wahenga walisema kwamba 'panapo hela basi hapo hela zitaongezeka.' Pia vile vile panapo maji pia maji yataongezeka. Hii ni kumaanisha haya mabawa yakijengwa basi watu wataanza kupanda miti ambayo italeta mvua. Pia mzingara yatakuwa kama yalivyokuwa hapo awali. Mbunge ambaye ameleta Mswada huu amefikiria wakati mwafaka. Basi tunapaswa kuunga mkono na kuhakikisha kwamba umetekelezwa. Wenzangu wameongea mengi na singependa kurejelea yale wameongea. Nashukuru kwa kupatiwa fursa hii. Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Mhe. Naibu Spika wa Muda mimi ni mama na ninaumwa na hali yetu. Waheshimiwa wakienda kule wataona hali yetu. Ninataka kupongeza Serikali kwa yale inafanya saa hii. Inafaa msako uhakikishe walanguzi wa dawa za kulevya katika Lamu wameshikwa. Ninataka kumuunga mkono Rais. Inafaa ahakikishe amemaliza dawa za kulevya ufisadi na alete watu pamoja. Mhe. Naibu Spika wa Muda ninaona taa imewaka na dakika zangu zimechukuliwa. Ninaomba nipewe nafasi zaidi. Vifo vingi vinatokea Lamu. Msichana mdogo wa miaka 23 ameuawa kwa kukatwa na panga kwa sababu ya ulanguzi wa dawa za kulevya. Ninaomba Serikali ihurumie watu wa Lamu kwa sababu tunamalizwa na ulanguzi wa dawa za kulevya. Ninaomba Rais asikie kilio cha watu wa Lamu. Tumeisha hasa Wabajuni. Kule dawa zimetumaliza. Msichana mdogo na akinamama.
Mhe. Naibu Spika wa Muda mimi sikutaja jina la mtu yeyote lakini kama mtu anajijue ni haki yake ajijue. Hakuna haja ya kupongeza Serikali wakati ulikuwa upande huu halafu baada ya mchujo uanze kuongea ubaya wa Serikali. Hivyo ni kukosa msimamo. Mambo yaliyo mbele yetu tunahitaji kuyaangalia. Sisi ndio tunatengeneza sheria. Kama tunatengeneza sheria tuwache kupiga kelele. Tuseme yale mambo ambayo tunaweza kutatua. Kama kuna shida ya jambo fulani tuipendekeze tuizungumzie na tuone mwelekeo ni upi. Lakini tukifanya mambo ambayo inatuhusu kama Wabunge ni lazima tujue kwamba sheria ya nchi hii haitengenezwi na Uhuru Muigai Kenyatta ama Raila. Ni sisi Wabunge! Kwa hivyo tunahitaji ushirikiano mzuri wa kuangalia ni shida gani ili tuweze kujua ni jambo gani tunaweza kufanya kutatua jambo hili. Mambo haya yote yamefanyika tukiwa kwa hili Bunge. Na kama tulikuwa kwa hili Bunge
Mhe. Naibu Spika wa Muda muda wangu unamalizwa bure na watu ambao wana njama fulani. Nakuomba uniongezee dakika kadha kwa sababu muda wangu umepotezwa na watu ambao wameleta hoja zisizo na msingi. Ninaunga mkono kikamilifu kwamba stakabadhi ambazo zinatolewa zitumike kikamilifu kwa kila jambo ambalo mtu anahitaji
Mhe. Naibu Spika wa Muda nachukua hii nafasi kumpongeza Mhe. Njenga kwa kuleta Hoja hii. Hoja hii imekuja kwa wakati unaofaa hasa tukiangalia kule mashinani kati ya vijana wetu. Kusema kweli vijana wanastahili kutengewa pesa za kutosha katika Bajeti ya Kenya kinyume na vile ilivyo leo kwa sababu kwanza wao ni wengi na pili mahitaji yao yamekuwa zaidi haswa kwa wale ambao wametoka mashule kabla ya kumaliza elimu kwa sababu ya ukosefu wa pesa. Wameshindwa kuendeleza masomo yao. Kwa hivyo nafikiri hizo pesa zikitengwa zitasiadia. Nawaomba Waheshimiwa wenzangu kuwa kila wanapozungumza wale ambao wanashikilia constituencies hujitaja wao peke yao na wanatusahau sisi ambao constituency zetu ni lile jimbo. Tunaomba hizo pesa zipatikane lakini hata na sisi tupate
Mhe. Naibu Spika wa Muda nadhani tetesi hapa... Ninaomba wenzangu waweze kunisikiza. Kuna hoja mbili ambazo nimeleta. Ya kwanza ni kuhusiana na fedha za National Government - Constituency Development Fund (NG-CDF). Ninavyoona ninafikiri ni hisia za wenzangu hiyo ya NG-CDF ningeomba iteremshwe na isiwe katika orodha. Pili ni jambo kila mmoja wetu analifahamu nina Ii kwamba hakuna yeyote hapa atakayeweza kukubali Mkenya alipishwe aa ambayo hana hatia yoyote. Nimezungumzia hili kwa lugha inayofahamika. Nikimalizia ninataka kutoa usisitizo kwa unyenyekevu kama vile anavyozungumza Mhe. Aden Duale kuwa hakuna yeyote katika hili Bunge pamoja na magavana ambaye ana ruhusa ya kusema kwamba hakuna watu kutembea kuhusiana na lockdown ." Kwa hivyo nawasihi wenzangu wote tuchunge hali zilivyo.
Mhe. Naibu Spika wa Muda nafikiria ni nidhamu ya Bunge kwamba kama Hoja imeandikwa kwa lugha fulani iendelezwe mpaka iishe katika ile lugha. Hii Hoja imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Ibara ya hapa Bunge inasema kwamba Hoja indelezwe kaika ile lugha imeandikwa.
Mhe. Naibu Spika wa Muda nakamilisha kwa kusema kwamba naunga mkono ombi la kwamba badala ya Serikali kutoa mikopo iwe ni msaada maalum - yaani grant pesa ambazo zitawasaidia wavuvi kuweza kujimudu na wapate nguvu ndipo wawe kwenye hali ambao wanaweza kuchukua na kulipa mikopo. Bw. Naibu Spika wa Muda naunga mkono.
Mhe. Naibu Spika wa Muda nakushukuru kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa nimesimama kuunga mkono Mswada huu. Kifungu cha 94(1) na (3) kinapeana wajibu wa utunzi na urekebishaji wa sheria kwa Bunge la taifa. Wale wenye dhana kwamba Wabunge wana nia ya kujiongezea muda na wanataka kuzua pesa hii ni dhana isiyokuwa na msingi wa kisheria. Tuna wajibu. Wakitusifu au watutusi tuna wajibu wa kuirekebisha sheria. Swala nyeti ni je Mswada ulioko mbele yetu unataka kura ya maoni? Kifungu cha 255 ni wazi kuhusu ni nini kinachofaa kupigiwa kura ya maoni na ni nini hakifai. Kwa hivyo Kifungu 259 kinatupa sisi fursa ya kutunga sheria kama hii ili kuweka wazi siku ya uchaguzi itakuwa lini ndio Wakenya waweze kujipanga kimbele.
Mhe. Naibu Spika wa Muda nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii. Ningependa kutoa shukrani zangu kwa mhe. Zuleikha kwa kunipa dakika mbili za muda wake ili niweze kuchangia Hoja hii. Ningependa kusema kwamba Hoja hii ni nzuri kwa sababu katika taifa letu la Kenya tumeona mara nyingi masuala ya vijana ambayo ni muhimu sana kwa taifa hili yakiwekwa nyuma. Kwa hivyo ningependa kuiunga mkono Hoja hii kwa dhati kwa sababu ninafahamu kwamba iwapo vijana watapata fedha watapata nafasi ya kujiendeleza na kuleta maendeleo katika taifa hili. Ni kweli kwamba suala la kusema vijana ni viongozi wa kesho limepitwa na wakati. Naamini kwamba tukitoa fedha kwa vijana na wapewe nafasi ya kuzitumia vizuri fedha hizo zitaendeleza mipango ya vijana humu nchini. Hatutaki kusikia tena vijana wakijiingiza kwenye shida za mihadarati ama wakiwekwa katika ngazi ya chini. Mara nyingi vijana huchukuliwa kuwa watu wa kuendesha pikipiki za boda boda kufanya kazi duni na kutumiwa vibaya haswa wakati wa kampeini za kisiasa. Sheria inasema kwamba ni lazima pesa hizo zitolewe kwa vijana ili vijana waweze kuendeleza miradi yao ndiyo tuweze kupata maendeleo katika nchi hii. Kwa hayo eno machache naunga mkono Hoja hii.
Mhe. Naibu Spika wa Muda naomba kuunga mkono Mswada huu na kuiombea kuwa sheria. Sisi ambao tumetoka eneo kame na mahali ambapo maji ni shida hatukuwahi kuiona kiliniki. Tuliishi kutumia madawa ya kienyeji. Hivi sasa wanatekinolojia wanaona kwamba ni vyema kuwa na kituo kama hicho ambacho kinaweza kuleta utafiti na kuboresha mambo kama haya ili yaweze kunawiri. Ningependa kulipongeza suala hilo kwa sababu enzi zile za nyuma tulikuwa tukitegemea mavi ya ndovu kutibu homa. Yalikuwa yakiwekwa kwenye makaa na tungewekwa karibu na ule moshi. Tulinawiri na tumefika pahali ambapo tumefika. Tumeharibiwa masuala mengi na mzungu aliyetutawala pia kiakili. Imefika mahali ambapo tunaona kuwa kila kitu kitokacho ardhi ya Mwafrika hakiwezi kuwa cha msaada. Kituo kama hicho kitakapoanzishwa na kutambua mbegu na mimea inayoweza kuwa ya faida katika nchi hii kitasaidia Wakenya au Waafrika kuliko sisi kutegemea kwamba mpaka twende Uchina tupewe nyasi na tukubali kuwa ni dawa na labda nyasi zile zinapatikana nchini. Ukweli ni kwamba tunavidharau vitu vyetu lakini tukipata mwelekeo wa kuviboresha ni suala ambalo tunaweza kujivunia ili tukatambue tunakotoka na tunakokwenda. Nina ii kuwa jinsi Mswada huu unavyoungwa mkono hata ijapo mapendekezo madogo madogo yatakayofanyiwa ukarabati kwenye Kamati huenda ukawa nguzo ya kutegemea na kuhakikisha kwamba nchi hii inarudi katika barabara ya kujitambua. Ni rahisi kwa binadamu kusema kwamba amejitoa katika minyororo ya wakoloni lakini ukoloni unaendelea kumsumbua akilini. Katika Vitabu vya Mwenyezi Mungu Biblia na Quran tuliwahi kuambiwa kuwa miti mingi ni dawa. Zama zile tulipokumbana na nyoka hatukupelekwa hospitalini kwa sababu nyoka angesemewa na kusikia na sumu ingesimama mahali ilipokuwa. Uwezo huo ulikuweko na labda utafiti wa kuboresha hali hiyo unakosekana. Naunga mkono kwamba kituo hicho kitakapoanzishwa kipewe pesa kwa sababu kuna vitu viwili. Tupitishe na kiwe kituo cha kufanya utafiti lakini tukikosa kukipa pesa itakuwa tumejenga nyumba ambayo haina wanadamu ndani. Naunga mkono na kutia sauti kwa wale wengi ambao walikuwa tayari wameunga mkono Mswada huu. Tunaweza kufanya utafiti wa miti mbegu na miche yetu na kujua ni ipi yenye faida na yenye haina faida. Tunaweza kutilia maanani yaliyo na nguvu. Hapo awali hatukuwa tunaenda hospitali tukipata maradhi kama msukumo wa damu. Tulikuwa tunatumia mbegu na madawa ya kienyeji na tulikuwa tukipona. Lakini kutokana na haya makubwa tuliyoletewa na mkoloni hata mtoto mchanga anaugua saratani kwa sababu ya mafuta tunayotumia. Tunaambiwa kwamba kuna madawa ambayo yanaweza kuregesha saratani chini. Lakini kinachohitajika ni kuboresha mimea ama dawa ili kuhakikisha kwamba tunapata lishe bora. Mswada huu unahitaji kuboreshwa katika Kamati ya Bunge nzima ili kuhakikisha kwamba umeweza kuyalenga yale yote ambayo yanaweza kumnufaisha mwanadamu. Mhe. Naibu Spika wa Muda naomba kuunga mkono.
Mhe. Naibu Spika wa Muda naomba kuwasilisha Hoja ifuatayo: KWAMBA tukifahamu Kifungu cha 43 cha Katiba ya Kenya kimeweka wazi kwamba kila Mkenya ana haki ya kuwa na kiwango bora cha afya kinachojumuisha afya bora ya uzazi; aidha katika utaratibu wa Ajenda ya Maendeleo ya baada ya Mwaka wa 2015 dunia imewajibikia Afya kwa Wote na kutimiza Lengo Endelevu la Maendeleo la tatu (SDG-3) kuhakikisha na kuendeleza maisha na afya bora kwa wote; tukiafiki uwekezaji katika sekta bora ya afya ni muhimu kuhakikisha kila mtu anapata huduma za kimsingi za afya bila kuzingatia eneo analotoka au hali yake ya kiuchumi; tukitambua asilimia 80 hutegemea huduma ya afya ya umma ilihali kuna hospitali mbili pekee za rufaa nchini ambazo ni Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta - Nairobi na Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Moi - Eldoret; tukizingatia Kifungu cha ishirini na tano (25) kikiambatanishwa na Mpangilio wa Kwanza wa Sheria ya Afya 2017 kinasema kutakuwa na hospitali ya kitaifa ya rufaa katika kila gatuzi (Level 6); Bunge hili linahimiza Serikali kuharakisha kuwepo Hospitali ya Rufaa ya Kitaifa katika Kaunti ya Mombasa ili kufanikisha huduma zote za afya zinazohitajika eneo hilo zitumiazo teknolojia pevu na wataalamu wa hali ya juu pamoja na kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya kabla na baada ya kuhitimu. Mhe. Naibu Spika wa Muda hili ni wazo ambalo liliwahi kuletwa na Rais Uhuru Kenyatta Juni mwaka uliopita. Rais alipendekeza kwamba katika kila kaunti kuwe na hospitali ya rufaa. Ningependa kutoa utaratibu wa mambo fulani ambayo yanachangia kuwepo kwa hospitali hizi kwa sababu asilimia 80 ya Wakenya ni wale ambao hawawezi kufikia huduma hizi za afya. Nitaanza kwa kutoa mifano ambayo imesalia katika historia ya Kenya. Nitaanza na kwangu nyumbani kule Mombasa. Kuna mtoto mdogo kwa jina la Satrin Osinya au Baby Osinya aliyepigwa risasi na akakaa na risasi kichwani kwa takriban siku nne kabla ya kuletwa Nairobi ili afanyiwe upasuaji. Hii inamaanisha nini? Inamaanisha kwamba iwapo hatutakuwa na huduma za afya katika kila kaunti basi tutakuwa katika hali mbaya sana. Hospitali ya Coast General iliyoko Mombasa inahudumia kaunti sita ambazo zinajumuisha Taita Taveta Tana River Kwale na Kilifi. Hizi ni baadhi ya kaunti ambazo zinategemea hospitali hii katika huduma za rufaa. Shirika la Afya Duniani (WHO) lina mapendekezo yake ambayo yanasema kwamba daktari mmoja anafaa ahudumie wagonjwa elfu moja lakini hapa nchini Kenya daktari mmoja anahudumia wagonjwa elfu kumi. Hili ni jambo ambalo haliwezekani si la msingi na haliingii akilini. Tangu tupate Uhuru miaka 55 iliyopita tuna hospitali mbili peke yake ambazo ni hospitali ya kitaifa ya Kenyatta na ile ya rufaa ya Eldoret. Leo napendekeza na kusema kwamba kila kaunti ipewe hospitali yake ya rufaa ili mwananchi wa kawaida aweze kufikiwa. Si kusema tu zijengwe bali pia nasema zile zilizopo hapo zinaweza boreshwa zaidi na kuwekwa katika kiwango cha Level 6 ambayo itaweza hudumia mwananchi wa kawaida aliye na matatizo chungu nzima. Hospitali ambazo ningelipenda zianze kufanyiwa ukarabarati wa hali ya juu na kuanza kufikia wananchi kufika ile kiwango ya Level 6 ni Meru Embu Mombasa Kakamega Busia Jaramogi Garissa na Kisii ambazo ni Level 5. Mhe. Spika wa Muda nadhani utashangaa nikikwambia ya kwamba taifa hili lina madaktari wa kutibu saratani yani oncologists kwa lugha ya kimombo wanaohudumia Wakenya takriban 45 milioni madaktari 23 peke yake. Hawa madaktari ni wa kibinafsi. Namaanisha nini? Wanahudumu katika hospitali ambazo ni za wale ambao wana nguvu kama Aga Khan University Hospital na Nairobi Hospital. Mkenya wa kawaida hawezi kuenda kutibiwa ugonjwa wa saratani katika hospitali hizo. Miaka 55 imepita tangu Kenya ipate Uhuru na tunajipiga kifua tukisema tumeendelea na ilhali tuna madaktari wa upasuaji yaani neurosurgeon 18. Hii ni aibu iwapo tuna madaktari 18 Kenya nzima. Leo tunajipiga kifua na kusema ya kwamba tuna madaktari tosha ambao ni wa figo kwa lugha ya kimombo tunawaita nephrologists. Hawa ni 16 peke yake. Mombasa tuna wawili pekee. Ni nani atawafikia hawa maskini? Leo Mbunge katika Bunge hili akisikia anasokotwa na tumbo kidogo tu yeye ana daktari wake wa kipekee. Yeye ana nguvu za kwenda katika hospitali na kuhudumiwa mara ya kwanza. Kule mashinani kuna watu ambao tumbo zao zinanguruma kama mitambo ya kuchapia mahindi lakini hawajui wataenda wapi kwa sababu hawana daktari wa kibinafsi hospitali haziko karibu na iliyoko karibu iko katika kaunti nyingine. Haya ndiyo mambo ambayo nataka tuangalie. Kwa mfano Kenya nzima madaktari waliosomea taaluma mbalimbali ambazo nimezitaja kama vile saratani upasuaji na figo ni 425. Nitakupatia utaratibu tu wa kukuonyesha athari ambazo zinaweza kutupata iwapo hatutaweza kushughulikia janga hili na kupitisha Hoja hii na kuhakikisha kwamba hospitali zimeweza kufika katika kaunti. Nitakupa mfano wa kaunti ya Mombasa ambayo idadi yake ni watu 939370. Madaktari wanaohudumia watu hawa takriban milioni moja ni 198. Katika kaunti ya Kwale watu 649331 wanahudumiwa na madaktari 65. Hawa ni watu takriban 700000. Sehemu kama Nyeri ambayo ina watu takriban 700000 wanahudumiwa na madaktari 143. Kiambu ambayo ina watu takriban 1.6 milioni wanahudumiwa na madaktari 278. Kisumu ambayo idadi yake inakaribia milioni moja wanahudumiwa na madaktari 163. Ukiangalia kaunti ya Kisii ambao ina idadi ya 1.2 milioni wana madaktari 163 utaona ya kwamba wanahitaji madaktari 989 zaidi. Kisumu wanahitaji madaktari 800. Kiambu wanahitaji madaktari 1343. Hizi tu ni baadhi ya sehemu ambazo zinaathiriwa sana. Hii ndiyo sababu ambayo imetuleta katika Bunge hili. Tulienda kupiga kampeini na tukawaahidi wananchi ya kwamba tutakuwa sauti yao katika Bunge hili. Tulitoa ahadi zote. Nadhani ahadi ambayo tutaitoa kwa Wakenya na ambayo itasalia mioyoni mwao ni ya kuhakikisha katika kila kaunti katika taifa hili kuna hospitali ya rufaa na mwananchi wa kawaida ataweza kuhudumiwa. Madaktari waliosajiliwa na Serikali na ambao wanajulikana Kenya nzima ni 11000. Hawa wanahudumia Wakenya 45 milioni. Kati ya hawa madaktari 11000 wanaofanya kazi practising kwa lugha ya kimombo ni 6000 peke yake. Hivi sasa tunapozungumza kuna wale ambao ni watahiniwa tunawaita interns kwa lugha ya kimombo ni 1000. Wakimaliza kusoma hawana mahala pa kuenda. Watajiunga na wenzao 1200 ambao hawana kazi na wako nje. Kwa ufupi nasema taifa hili linahitaji madaktari 34445. Nitaendelea bado kwa kueleza ni kwa nini hasa tunataka hizi hospitali ziweze kuhudumia wananchi. Nitaanza na masuala ya rufaa. Leo mgonjwa akiwa Nyeri Kiambu Mombasa ama Turkana ataenda katika hospitali iliyoko hapo. Hospitali za maskini ni hospitali za Panadol dawa ya maumivu tu maana hawana dawa zingine. Wakienda katika hizi hospitali iwapo wana kesi nyeti ni lazima waletwe Nairobi. Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta ina madaktari 264. Wale ambao wanasimama pale casualty kwa matibabu ya dharura ni sita. Kwa mfano Hospitali ya Coast General inapokea zaidi ya watu 50 kwa siku moja kutoka kaunti mbalimbali waliotumwa kwa sababu vifaa ama huduma inapatikana huko. Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta inapokea kati ya watu 200 na 300 kila siku kutoka sehemu mbalimbali sawia na ile ya Eldoret. Mwaka wa 2015/2016 Serikali ya Kenya ilitumia Kshs.38bilioni kwa mashine za kisasa katika hospitali lakini kwa sasa hazifanyi kazi kwa sababu hatuna madaktari wanaopata mafunzo ya kuzitumia. Mwaka uliopita 2015/2016 iliangaziwa katika vyombo vya habari ya kwamba mashine za kisasa za saratani na figo zimekuja. Watu walifurahi na wakasema kweli ugatuzi umezaa matunda. Ugatuzi wakuleta mashine bila daktari wa kujua kuzitumia nikutia gunia upepo kwa maana haina faida. Ninaposema kutia gunia upepo na maanisha ya kwamba unatia gunia upepo lakini linatoa. Kwa hivyo haujazi. Inakuwa ni kazi ya bure. Je kujenga hospitali moja ya rufaa katika kaunti moja itagharimu Serikali pesa ngapi? Itagharimu takriban Kshs3bilioni. Tukisema tuboreshe zile zilizopo ambazo nimezitaja kutoka Level 5 hadi Level 6 tunaweza tumia Kshs2bilioni. Sasa wacha nikupe mfano tufanye hesabu. Kujenga hospitali moja ni Kshs3bilioni. Kuboresha hospitali iliyoko ni takriban Ksh2bilioni. Idadi ya Wakenya wanaondoka nchini kuenda kutafuta matibabu nje hususan taifa la India kila mwaka wanatumia Kshs10bilioni. Ni jambo linaweza kufanyika. Idadi ya watu wanaokufa inazidi kuongezeka. Mungu ametujalia tumeletwa katika Bunge hili kujadili na kutunga sheria lakini hatutungi sheria ambazo zitatulinda pia sisi tukitoka maana hakuna mtu atakayeishi hapa milele. Tukitoka hapa vizazi vyetu hatujui kama vitakuwa vya ubunge kula madawa ya kulevya ama kuiba. Watakuwa ni miongoni mwa wale ambao watapata matatizo ambayo sisi tunasuluhu sasa hivi. Nitakupa mifano nikianzia na mgomo uliofanyika miezi minane iliyopita wakati madaktari waligoma. Nitakupa tu mifano na kaunti kadhaa kama Kaunti ya Kilifi. Kaunti ya Kilifi ina madaktrari wa upasuaji wa caesarean section 18. Ina madaktari wa upasuaji 18 peke yake. Idadi ya vitanda ni 610. Wagonjwa wanaokwenda kutibiwa kila siku ni zaidi ya 10852. Watu wanaokufa ni 1410. Wanakufa kwa sababu ya magonjwa ya kiajabuajabu. Magonjwa yanayo tiba lakini tunayachukulia mzaha mzaha. Leo Mombasa tunakufa kwa sababu ya Chikungunya; eti ukiumwa na mbu wewe kwisha. Hatuna wataalamu wa kupambana na magonjwa. Maradhi ya ajabuajabu yanatokea na hatuwezi saidika. Asilimia kubwa ya Wakenya hata hawana ile Bima ya Afya ya Kitaifa. Hawawezi kujitetea na hawajui la kufanya. Angalia Kaunti ya Mombasa. Idadi ya wanaokufa ni 1272. Katika miaka ya 2014 na 2015 Kilifi ilifanyia upasuaji wagonjwa 2668. Waliokufa ni 1553. Haikubaliwi. Inasemekana kwamba kila nafsi itaonja mauti lakini suala la kuonja mauti kwa sababu ya udhalimu na uzembe wetu sisi Wabunge halikubaliki. Sisi ni wasomi ambao tuko na Bachelor's Degree na Master's Degree lakini tumeamua kuweka makaratasi yetu kwenye mifuko na kushabikia ukiritimba. Hili leo nalipite ili tuweze kupata hospitali katika kila kaunti Kenya nzima. Bado nitaendelea kulilia hili suala kwa sababu linahusu mwananchi wa kawaida. Nitazungumzia hospitali na vile vile madaktari wenyewe. Katika Kenya ya sasa madaktari ambao tunawategemea wanalipwa mishahara ambayo haiingii akilini. Nitaanza na ile wanaita entry level ambayo ni hatua ya kwanza ya daktari kuingia. Mshahara wao wa kwanza wakimaliza mafunzo ni Kshs44000. Daktari aliyekaa katika taaluma hiyo kwa muda wa kati ya miaka 10 na 15 - daktari ambaye anakuangalia tu hivi na anajua dawa yako - analipwa Kshs114000 katika Kenya ya sasa. Ndio unaona tumekuwa na uhaba wa madaktari. Wengi wao wanakimbia kwenda kufanya kazi nje. Wengi wanafungua hospitali zao za kibinafsi ambazo haziwezi kufikiwa. Daktari aliye na uzoefu wa zaidi ya miaka 15 analipwa takriban Ksh200000. Watu wanaumia na wanakufa. Sisi tuna uwezo. Mungu hatusamehi sisi Wabunge kwa sababu tukiwa wagonjwa tuna suluhu. Sisi tunaenda katika mahospitali ya kifahari. Tunapanda ndege na kuenda Ulaya kutafuta matibabu lakini Mungu anaturegesha katika majeneza na masunduku hadi nchini Kenya. Kisha tunaanza kupiga kelele na kusema kwamba ni vipi Mbunge fulani alipelekwa nje aende apate matibabu amerudi akiwa maiti? Ni aibu. Hatuwezi kutunga sheria za kuleta hospitali usawa na haki? Leo sisi tunasikia uchungu mmoja wetu akituondokea kwa sababu tumejaribu kila tuwezacho. Tumetumia pesa tumemwaza Nairobi Hospital Aga Khan Hospital tumempandisha ndege ameenda Uingereza na Marekani lakini hivyo hivyo amerudi akiwa maiti ndani ya sanduku. Yule mama anayeuza mboga kule Kaloleni Giriama; yule mama anayeuza viazi kule Nyeri; yule mzee ambaye anakaa kule mashinani Turkana na Pokot; ni nani anayempeleka katika hizi hospitali? Ni nani anayemkatia nauli ya kupanda ndege na kuenda Ulaya? Hakuna? Atakayefanya hiyo kuhakikisha ya kwamba watu hawa hawatapata haya matatizo ni sisi Wabunge wote. Kwa kauli moja tukubaliane ya kwamba hii ina umuhimu zaidi na ni ya Wakenya asilimia 80 ambao hawana huduma za afya. Leo nchini Kenya miaka 55 baada ya kupata Uhuru mama anajifungua ndani ya nyumba. Jamani hatuoni haya? Jamani hatuogopi Mungu? Mama anakufa akijifungua mimba kwa sababu hawezi kufikia hospitali. Mfano ni katika Eneo Bunge la Nyali ninakotoka. Linaonekana kama eneo Bunge tajiri kwa sababu ukisema unaenda Nyali watu wanajua ni Eneo Bunge tajiri. Lakini utashangaa nikikuambia kwamba Mungu anajalia akina mama wetu kupata mimba ndani ya Nyali lakini wanajifungua katika Eneo Bunge la Mvita. Hali hii haikubaliki. Jameni hili si jambo la kuchekea wala kushabikia. Watu wanakufa. Leo maradhi madogo madogo yanatusumbua. Nimekupa mfano wakati nilipoanza mjadala wangu. Naona muda unanipa kisogo. Ningelipenda kusoma na kuelezea mengi zaidi lakini kwa hayo machache naomba ya kwamba haya yamewaingia Wabunge. Naomba kuwasilisha Hoja hii na atakaye afiki yani Seconder ni Mheshimiwa Kanini Kega.
Mhe. Naibu Spika wa Muda nashukuru kwa fursa hii. Naamka kuunga mkono Mswada huu. Kwa kweli kudhibiti mwendo wa kasi kwa magari ni jambo mwafaka kabisa maanake ajali nchini mwetu zimekuwa nyingi mno. Ukiangalia ulimwengu mzima kwa sasa hivi tuko nambari 22 kwa nchi zenye ajali nyingi ilihali tukiangalia idadi yetu yote ni watu kama 40 milioni na China ina watu zaidi ya 1.5 bilioni lakini ajali zao ni kidogo sana. Nampongeza Lekuton kwa kuleta huu Mswada na ingekuwa vyema pia katika shule zetu na taasisi za Serikali waweke matatu kwa barabara ambazo zinaweza kudhibiti mwendo wa kasi. Vile vile wangeweka vivukio kwa shule zetu hasa za msingi maanake ajali hapa nchini zimeongezeka sana. Watu wengi wamechangia huu Mswada na ninaona yale waliochangia yanaambatana na singependelea kuyarejelea. Nasimama tena kuunga mkono huu Mswada.
Mhe. Naibu Spika wa Muda nashukuru kwa nafasi hii ambayo umenipatia nimpongeze mhe. (Bi.) Joyce Lay kwa Hoja hii ambayo ameileta Bungeni asubuhi ya leo. Naomba pia nitumie nafasi hii kumshukuru.
Mhe. Naibu Spika wa Muda nashukuru kwa nafasi hii. Nasimama kuunga mkono Mswada huu ulioletwa na mwenzetu Mhe. Nyoro kuwa hukumu na faini inayotolewa kwa wafisadi ipate kuongezeka maradufu. Kila mara tunapokaa katika Bunge hili na kuongea juu ya masuala ya ufisadi nafikiri nchi nzima huwa inatuangazia sana kama viongozi. Ni jambo la kusikitisha sana kuwa nchi hii ambayo inajulikana katika Afrika na ulimwengu mzima kuwa ni nchi ambayo inastawi tunajulikana kwa masuala ya ufisadi. Tumewekwa katika jedwali katika nchi za Afrika na inaonekana kuwa Kenya imestawi sana na mambo ya ufisadi. Leo hii wanariadha wetu kule Doha wanaleta sifa nyingi kwa nchi yetu. Lakini vilevile mara nyingine wakati tunapeleka wanariadha kule kushindana duniani bado masuala ya ufisadi yanaingia ndani. Tunakumbuka yale yaliyotendeka miaka miwili au mitatu iliyopita wakati tulipeleka timu ya nchi lakini ufisadi ukaingia sana. Leo Wakenya wanalia. Wengi wao wako katika hali ya umaskini kwa sababu wale waliopewa nyadhifa za uongozi miaka ya mbele wengine hata walipewa urais kila mmoja kutoka juu mpaka chini kwa yule askari anayechunga mlango wa hospitali wanajitafutia mafanikio kupitia njia ya ufisadi. Rais alitangaza vita vikali sana dhidi ya ufisadi. Aliwapa nyadhifa za kazi Mawaziri na tukadhani kwamba kipindi hiki tutaona kweli watu wakihukumiwa. Tulidhani kwamba tutaona watu wakipigwa faini kubwa ili Wakenya wazidi kuwa na ii kuwa ufisadi kweli tunapigana nao. Nadhani kuwa Bunge hili sasa limepata nafasi ya kutoa maoni yake kwa uzito kabisa. Maoni yetu tutatoa kivipi? Kupitia sheria kama hii. Sheria hii ni nzuri. Lazima sauti yetu ya kupigana na ufisadi izidi kuenda juu. Itaenda juu wakati tunasema kwamba ukiiba pesa ya umma. Hesabu inafanywa na Mkaguzi wa Vitabu Vya Serikali na inakuja katika kamati yetu ya masuala ya pesa na tunajadili. Tunajua kwamba kwa kaunti fulani gavana fulani eneo Bunge fulani au wizara fulani pesa zimepotea lakini hakuna atakayepelekwa mahakai. Wakati Mkaguzi wa Vitabu vya Serikali amesema pesa fulani imepotea katika eneo Bunge langu ama katika ofisi fulani ya Serikali wacha yule atakayepatikana na makosa yale arudishe ile pesa mara mbili inavyoandikwa katika sheria hii. Tukifanya hivyo huenda tukapunguza tamaa ambayo watu wengi wanaopata nafasi za Serikali wako nayo. Ni vibaya sana kwamba wale wanaolala korokoroni wale waliohukumiwa wengi ni kwa makosa madogo madogo ambayo yanadhuru mtu mmoja ama wawili. Lakini makosa makubwa hufanyika wakati watu wanakufa mahospitalini kwa mfano katika Hospitali Kuu ya Kenyatta. Watu wanakufa hospitalini lakini wale waliopora pesa ya madawa wanapopelekwa kortini mara nyingi kesi haina ushahidi ama hata ikiwa na ushahidi wale wanaohukumiwa ni watu wa chini tu kuliko wale waliotia sahihi stakabadhi fulani. Lakini wale mabwenyenye ambao wanafaidika kutoka na ile pesa ya ufisadi wengi wako huru hata wengi wako katika hili Bunge. Ni jambo la kusikitisha sana. Kwa hivyo wakati tunapojadili suala hili kama Waheshimiwa ni vizuri itoke wazi. Hata kama nakubaliana na Mheshimiwa aliyesema kuwa tupatie mahakama uhuru wa kuamua ni vipi kesi iko namna gani hili ni jambo zuri katika sheria. Lakini mahali nchi hii imefika tunajua ufisadi unatendeka hata ndani ya mahakama. Kwa hivyo tukizidi kupatia wahukumu wetu uhuru wa kuamua ni nani atafungwa miaka kumi au mmoja bado ufisadi utaingia maeneo yale. Ndiposa nakubaliana na Hoja hii kwamba tuwache mambo ya ufisadi. Maanake hata kwa mahakama upo. Wacha tutoe huo uamuzi kama Bunge na tuseme kuwa ukipatikana umeiba pesa za umma utarudisha mara mbili na ufungwe miaka isiopungua kumi kwa sababu vizazi vinavyokua vitatuhukumu vibaya sana kwa maana hawatapata kitu katika nchi hii. Juzi kulitendeka kisa kibaya sana pale Mombasa Ferry. Kwa kusema ukweli kama si ufisadi hakuna vile wananchi maelfu na maelfu wanavuka katika kivuko kile lakini kunakosekana hata mpiga mbizi mmoja ndani ya Ferry. Mpiga mbizi ambaye angalau anatakikana aangalie wakati kumetendeka jambo kama lile. Mama yule na mtoto wake wamepoteza maisha yao kwa sababu ya ufisadi. Kama si ufisadi yule mama hangekufa maanake wale wanaosimamia Ferry wamejitwika jukumu la kuangalia makandarasi pekee - Kutafuta njia ya kula pesa. Mara wanatengeneza Ferry lakini haitengenezwi vizuri. Ferry inakosa vitu muhimu vya msingi vya kulinda maisha ya wanadamu kwa sababu watu waliamua kufuja pesa ya Serikali. Jambo hili ni nzito. Hili ni jambo ambalo kama viongozi tukuchukue nafasi yetu tupitishe Mswada kwa sababu Wakenya wanaumia. Wanapoteza maisha kila kukicha. Asante kwa fursa hii na ninasimama kwa vikali sana kuunga mkono sheria hii ambayo imependekezwa na Mheshimiwa Ndindi Nyoro. Asante
Mhe. Naibu Spika wa Muda nasimama kuunga mkono hii sheria ambayo itabadilisha mjadala huu kwa sababu ni muhimu sana. Watu wengi wameumia kwa miaka mingi. Kwa hivyo ninaunga mkono kwa kusema marekebisho haya ni ya maana na ninamshukuru mwenye kuipendekeza. Wananchi wameumia hata sisi tumekuwa kwa kampuni ambazo zimekuwa na shida kwa sababu liquidators hawaji kusaidia. Wanakuja kuzimaliza kabisa na kuumiiza. Kwa hivyo naunga mkono marekebisho ya siku ya leo. Yataleta mambo mazuri ya kubadilisha mjadala huu ili watu wengi waweze kupata njia ya kurekebisha hata wakiwa na deni. Kutapatikana njia ya kulipa madeni na kubaki kwa njia inayotakikana. Nashukuru na ninaunga mkono sana. Nakushukuru pia kwa sababu ya kunipa nafasi hii. Jambo hilo limenikera kwa siku nyingi lakini imekuwa wakati wake mzuri wa kuletwa Bungeni ingawa nilikuwa mbali. Ningekuwa na mambo mengi ya kusema lakini nafasi imekuwa ndogo. Naona ndugu zangu hapa wengine na ningetaka pia wachangie. Asante sana Mhe. Spika wa Muda.
Mhe. Naibu Spika wa Muda nasimama kwa Hoja ya Nidhamu ni kitaka kuuliza: Je ni lugha safi ya Bunge kwa Mhe. Mpuru kuita Wabunge wengine wanaounga mkono Hoja hii wa mashamba ilihali yeye mwenyewe tunamjua kuwa wa kwanza wa mashamba?
Mhe. Naibu Spika wa Muda nataka kuunga mkono Hoja hii iliyoletwa na Mhe. Ali. Tunajua kwamba Kipengele cha 25 cha Katiba ya Kenya na Kipengele cha kwanza cha Sheria ya Afya vinasema kwamba tutaweka hospitali ya rufaa katika kila jimbo. Nataka kusema kwamba watu wanakufa wengi sana kwa sababu hawana dawa na vifaa ambavyo vinafaa katika hospitali zetu. Hoja hii itawasaidia Wakenya sana. Sisi Wabunge tunaitwa kila wiki kushughulikia watu wengi ambao wako na shida. Tuko na magonjwa mengi kama ugonjwa wa saratani ugonjwa wa figo na watu wameuza mashamba wakabaki hohehahe. Hawawezi kuwapeleka watoto wao shuleni kwa sababu wanalazimika kwenda kupata huduma kwenye hospitali za kibinafsi na kulipa Kshs4 milioni. Inabidi mtu auze shamba lake la ekari tano ili apatiwe dawa zinazofaa. Tunajua kwamba tuko na hospitali mbili za rufaa. Tuko na moja kule Eldoret na pia tuko na ile ya Kitaifa ya Kenyatta. Tunajua kwamba hospitali ya Mombasa inahudumia kaunti sita. Tumeona kuwa watu wa Mombasa wanataabika sana na tunaiunga mkono Hoja hii. Tunajua kwamba kama kuna shida katika hospitali wanaoteseka ni kina mama. Kwa nini ninasema kina mama wanateseka? Kina mama wako na kazi nyingi kule nyumbani. Baba wa nyumba akiwa mgonjwa mama wa nyumba huacha kila kitu kuhakikisha kwamba watoto wameenda shuleni. Tunajua kwamba katika hospitali zetu za kaunti hakuna dawa wala mitambo ya kuwashughulikia watu wanaougua ugonjwa wa figo. Hatuna mashine za kuwashughulikia watu wenye ugonjwa wa saratani. Tunaweka hii iwe priority number one katika nchi yetu ya Kenya. Tunajua Serikali ya Jubilee iko na ajenda nne. Moja ya hizo ni kupatia kila mmoja matibabu ya kufaa. Tukitaka kuendeleza hii ajenda tuanzishe hospitali za rufaa katika kaunti zote. Tangu tulipopata Uhuru mwaka wa 1963 tuliapa kwamba tutaangamiza matatizo ya ugonjwa upumbavu na umaskini. Lakini umaskini unachangiwa na kutokuwa na hospitali za rufaa. Hali hiyo inasababisha watu kuuza ardhi yao ili waweze kupata huduma katika hospitali za kibinafsi. Hakuna Mbunge ambaye halii. Mimi kama mama kaunti wa Nandi ninaitiwa harambee ishirini kila mwishoni mwa wiki. Tunaomba Serikali itusaidie kwa sababu kupeana dawa na kila kitu ni kazi ya Serikali. Mshahara mdogo tunaolipwa hautoshi kisimamia harambee ya kuchangia watu. Hii ni kwa sababu ya magonjwa kuchangia watoto wa shule na kila kitu. Utaona Mbunge akijiongelesha peke yake kwa sababu hawezi kupata pesa za kumchangia mtu aliyelazwa hospitali. Ninaomba tuweke maanani afya ya watu wetu. Tupitishe yale Mhe. Ali amesema. Na haitakuwa Mombasa peke yake kwa sababu watu wetu wanakufa sana. Tuwe na hospitali za rufaa katika kila kaunti na tuweze kutimiza ajenda moja ya Serikali ya Jubilee. Asante.
Mhe. Naibu Spika wa Muda naweza kuondoa hiyo sehemu ya mazungumzo yangu na niseme: "Halikuwa jambo nzuri kukataa kuja kusikiliza Hotuba ya Rais." wakati kama ule nchi yetu ilikuwa kwenye majaribio. Ningewaomba Waheshimiwa wakati mwingine waweke siasa kando kidogo. Hata jana nilisema kwamba wakati kuna mambo ambayo yanawafaidi Wakenya ni heri sisi sote tuungane pamoja. Isiwe upande tunaoketi unatuletea shida ili ifike kiwango ambacho hatuwezi kuwahudumia watu wetu. Kwa hayo machache naunga mkono Hoja hii. Ahsante.
Mhe. Naibu Spika wa Muda ni "Lamu East" na si "Amu". Kwanza ningependa kumpongeza Mhe. Osoro kwa kuleta Hoja hii hapa Bungeni. Kwa kweli suala la barabara ni suala nyeti sana. Tunazungumzia uchumi nzima wa nchi. Kwa masikitiko makubwa barabara zetu za Kenya. Kwanza kabla hatujaingia katika suala la namna tutakavyo fundisha vijana wetu wakiwa shule barabara zetu ni tofauti na za nchi zingine. Kwa hivyo hata unapomfundisha mtu kuhusu barabara zile barabara anazofundishwa na zile anaenda kukumbana nazo ni tofauti. Kitu muhimu ni Serikali kupitia wizara ihakikishe kwamba barabara zetu zimejengwa kulingana na mwelekeo na mwongozo unaotakikakana. Utapata mambo mengi ambayo yanahitajika kuwe na barabara. Udhaifu na makosa makubwa yanapatikana katika barabara zetu. Hii ndio sababu utapata ajali na matatizo mengi yanapatikana katika barabara zetu. Swala la vijana kufundishwa maswala ya usalama ya barabara wakiwa shuleni ni jambo la muhimu na linahitaji kuangaziwa pakubwa. Kama nilivyosema barabara nikipengele muhimu katika uchumi wetu ambao unatumika hapa nchini. Unapotembea mahali popote katika nchi hii lazima utatembea katika barabara zetu. Ni muhimu vijana hawa wakiwa shuleni wafunzwe ili waelewe jinsi barabara zetu zilivyo na vile wanavyotakikana kutembea katika barabara zetu wakiwa wachanga na hata watakapokuwa wakubwa. Leo watoto wadogo wakiwa katika shule za chekechea wanatumia barabara hizi kwenda shuleni. Utapata kwamba ikiwa vijana hawa hawatakuwa na elimu ama na ujuzi kamili kuhusu barabara hizi matatizo mengi yanachipuka. Itakuwa vyema vijana hawa wakiwa na ujuzi na uelewaji kuhusu barabara zetu. Jambo hili litasaidia pakubwa katika kupunguza maafa mengi ambayo yanatokea. Kwa hayo machache ahsante.
Mhe. Naibu Spika wa Muda nikimkumbuka Rais wa Tanzania mhe. Julius Kabarage Nyerere ambaye alikitafi kitabu chake cha Uhuru WaWatumwa natumaini kwamba tunaelekea kupata uhuru wetu. Sheria za nchi yetu zimeandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Hoja hii inaomba wanaohusika watafi sheria zetu zote pamoja na Katiba kwa lugha ya Kiswahili; ambayo ndiyo lugha inayoeleweka na wengi. Tukiangalia ule udhalimu waliofanyiwa Wakenya utaona kwamba mara nyingi waadhiriwa wanashindwa kueleza kwa lugha ya Kiingereza kwa sababu lugha ambayo wanaifahamu ni Kiswahili. Mara nyingi washukiwa wanapopelekwa mahakai wakalii ambao wameajiriwa kutafi lugha ya Kiingereza mara nyingi huwapotosha washtakiwa. Mhe. Spika tulipoipitisha Katiba mwaka wa 2010 tukaingia katika sera ya ugatuzi moja ya vipengele ambavyo vinahusika ni makadirio ya fedha za kaunti. Makadirio hayo huandikwa kwa lugha ya Kiingereza na watu hawaelewi. Utakuta fedha ambazo zinaombwa na kaunti zimeandikwa kwa Kiingereza na wananchi wanashindwa watajikwamua namna gani kutoka kwa hali hiyo ili wapate kuyaelewa makadirio hayo. Wakitaka kuyapitisha mara nyingi wanayapitisha kwa sababu ya maelezo wanayopata kutoka kwa wahusika ambao huwadanganya wananchi kua wamefanya marekebisho kwa sababu ya shida ya lugha. Mazungumzo yetu ya kawaida hufanywa kwa Kiswahili. Ninapochangia Hoja na Miswada hapa Bungeni mara nyingi mimi hutumia lugha ya Kiswahili. Namshukuru mhe. Lay kwa kuileta Hoja hii Bungeni kuwashinikiza wanaohusika kuzitafi sheria zetu kwa lugha ya Kiswahili. Tukubaliane kwamba vituo vingi vya redio vinavyotumia masafa marefu ambavyo hupeperusha vipindi vyao kwa lugha ya Kiswahili vina wafuasi wengi ambao wanavifurahia kuliko vituo ambavyo hupeperusha vipindi vyao kwa Kiingereza. Wakati umefika wa kuchapisha matangazo ya kandarasi za Serikali magazetini kwa lugha ya Kiswahili ndiyo wananchi wapate kujua ni nini kinahitajika kutoka kwao. Nikimalizia hata Bibilia na Kuruani zimetafiwa kwa lugha ya Kiswahili. Itakuaje Katiba yetu ambayo imebana humu nchini ibaki kwa kugha ya kigeni pekee? Ndiyo maana Hoja hii ni muhimu sana. Ninawaomba Wabunge wenzangu waiunge mkono Hoja hii na watilie mkazo ili kila kitu chetu kipate kutafiwa kwa lugha ya Kiswahili. Kwa haya machache ninaaunga mkono.
Mhe. Naibu Spika wa Muda nilisikiza vizuri Mhe. Mohamed Ali alipokuwa akichangia. Kwanza kabisa alitambua Ibara ya 43 ya Katiba ambayo inasisitiza umuhimu wa kupata matibabu ya bure. Ibara ya 43 ya Katiba inazingatia umuhimu wa kupata matibabu ya bure. Hiyo ni haki. Ningesisitiza kwa Kamati ya Afya kuwe na sheria ambazo zinazingatia umuhimu wa kupata matibabu ya bure katika hospitali za umma zote. Nilisoma juzi ya kwamba kaunti ya Lamu iliita madaktari kutoka Uspania ambao walikuwa wanapeana matibabu ya bure. Kwa wiki tatu kulikuwa na watu kama 400 ambao walijitokeza ili wapate matibabu ya bure. Hiyo ni ishara ya kwamba kama tungekuwa na sheria ama kama tungekuwa tunatibiwa katika hospitali za umma bila kulipa pesa zozote tungekuwa tunazuia vifo. Mtu anapata maumivu kwa mwili na anaogopa kwenda hospitali kwa sababu hana pesa. Anaenda kwa duka ananunua dawa na anajitibu. Kama hakuna pesa ambazo mtu analipa akienda hospitali wakati tu amepata maumivu anaenda hospitali na anapata matibabu angezuia kifo. Tunaona wakati mwingi watu wanaenda hospitali wakati wamepata maumivu kabisa ndio wanafanya mchango. Juzi nilikua na kesi ya mgonjwa fulani kutoka eneo langu la Tetu. Aligonjeka akapelekwa Hospitali ya Kenyatta halafu akaaga dunia. Alikua na ada ya Kshs800000. Nilichanga pesa kidogo lakini maiti ilikaa kwa chumba cha kuhifadhi maiti kwa zaidi ya mwezi mmoja. Juzi tu ndio tulipata pesa na tukaweza kuzika maiti. Uingereza ni mfano mwema wa nchi ambayo imeendelea. Wananchi wa Uingereza wanapata matibabu ya bure na kila mtu ako na dakitari wake. Najua sisi kama Wabunge tunaweza kuunda sheria. Tunaweza kuwa na sheria zitakaoifanya iwe ni lazima kila mtu apate matibabu ya bure. Tukipata matibabu ya bure idadi ya watu wanaoaga dunia itakuwa ya chini. Piamtu akipata matibabu ya bure na kwa bahati mbaya aage dunia inastahili asilipe pesa yoyote hata ada ya chumba cha kuhifadhi maiti. Tukifanya hivyo kama Wabunge tutakuwa tunaiunga Serikali mkono. Tutakua tumesaidia wananchi ambao wametuchagua. Jambo muhimu ni kuwa na afya njema. Ndiposa imeekwa kwa Katibu kama haki ya binadamu. Kwa hivyo mimi ni mmoja wa wale wanaunga mkono Hoja ya kufutilia mbali ada za matibabu katika hospitali zote za umma. Tukifanya hivyo tutaona ya kwamba Kenya yetu itaendelea vizuri. Kwa hayo machache naunga mkono. Asante.
Mhe. Naibu Spika wa Muda nimesema tatizo sio idadi. Tatizo ni mchakato. Kwa mchakato Wakenya 41 walipoomba nafasi utawanyamazisha vipi na kuleta majina ne? Wakati muungano wa vyama vya Jubilee umepewa nafasi tano kwa kila nafasi umeleta nafasi tatu ili Bunge lifanye uchaguzi. Ukileta majina ne hiyo ni uteuzi ama uchaguzi? Na ukizoea kudhulumu Wakenya usilazimishe Bunge likuunge mkono katika dhuluma zako. Wengine wanasema tunatumia nambari kudhulumu upande wa CORD. Kama tungedhulumu upande wa CORD hatungepeana muda zaidi. Ukiangalia pendekezo la tano limepeana nafasi kwa CORD kuleta majina masaba zaidi. Kama ni tyranny of numbers vile wanavyosema kweli tungewapatia nafasi walete majina zaidi? Tusingefanya hivyo. Kamati yetu imefanya haki. Kamati imeambia CORD kwa sababu imeleta majina matano leteni majina mengine masaba wawe 12. Utakapoleta majina hayo katika Bunge Bunge litaweza kuchagua majina kadhaa. Usitupee majina ya watoto ambao baba yao ni mwaniaji mwenza. Wako Wakenya wengine ambao wana haki. Walete hapa tuwachague. Sisi hatuko hapa kufanya uteuzi. Tuko hapa kufanya uchaguzi.
Mhe. Naibu Spika Wa Muda ninajiunga na wenzangu kusema kuwa kuna umuhimu wa sheria hii. Hata ingawa ilichelewa kidogo lakini sasa hivi muda umefika. Sheria hii ikipitishwa itasaidia kurekebisha matatizo ambayo askari gongo wa hapa nchini wamekuwa wakipata. Kuwapatia bunduki lingekuwa janga nchini. Kwa hivyo sheria hii ikipita itawawezesha kupata mishahara inayofaa ili waweze kujimudu kimaisha. Ukweli ni kwamba askari gongo wana firimbi na Wabunge walisahau kuwa wao ni Wabunge na wakafanya tabia kama za askari gongo. Ninaunga mkono.
Mhe. Naibu Spika wa Muda ninakubaliana lakini pengine unaweza kutupatia mwelekeo wa lugha mwafaka inayofaa kutumika kwa sababu "huelewanga" ama lugha kama hii sijui kama ni Kiswahili. Tuzungumzeni Kiingereza au Kiswahili. Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Mhe. Naibu Spika wa Muda ninamwomba kwa heshima kuwa nikitoka nje aniulize yale eno. Wakati mwingi Nilinde Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninafikiri hilo jambo limewafurahisha sana. Wengi wamesoma na wanajua kuhusu mimea ambayo tuko nayo. Kile kitu tunakosa ni watu wa kueleza wananchi wa kawaida kuhusu yale maoni ama masomo ambayo wamesoma. Saa zingine tunaidharau hiyo mimea kwa sababu tunaona kama mimea ya kiasili imeisha. Ningeomba kila mtu atilie maanani hiyo mimea na tuilinde ndiposa tuweze kuendelea. Wakati mwingi hata ukiwa na ugonjwa unaambiwa ukichemsha majani haya na unywe maji yake labda utakuwa sawa. Wengine hasa mimi saa zingine tunaambiwa kwamba tumbo zetu ni kubwa na kwa hivyo tunywe maji ya majani fulani na hayo majani yametoka ugenini. Labda yalitoka kwetu yakapelekwa ugenini na kurudi. Kwa hivyo ni vizuri hata sisi tuheshimu mimea ambayo iko hapa nchini ndiposa tukifanya kitu hata sisi tunajivunia kuwa na mimea ambayo inatusaidia. Tunaweza kuhifadhi hata wakati kuna njaa na hatutakimbia hapa na pale tukiomba mbegu za kupanda na chakula cha kula. Ni vyema tuwe nazo ili tuweze kuzilinda na kuzihifadhi. Mheshimiwa ninaomba unione nikitoka nje.
Mhe. Naibu Spika wa Muda ninaomba dakika moja. Asante sana. Tulikuwa na kizaazaa wakati tulipoenda katika ukaguzi kule chooni. Ilisemekana Wabunge wanawake hawafungi milango yao wakienda chooni na hili ni jambo ambalo hatukuweza kulithibitisha kwa sababu hatungeweza kwenda chooni wakati wako pale. Kwa hivyo pengine tungefanya utafiti zaidi kuhusu Wabunge akina mama ili watueleze kama wakienda chooni huwa wanaacha milango yao wazi. Hili ni tatizo kubwa sana ambalo Kamati yetu ilipata. Kwa hayo naunga mkono Kamati hii na vile vile Ripoti hii.
Mhe. Naibu Spika wa Muda ninaomba kuchukua nafasi hii kukushukuru na kumshukuru aliyeleta Hoja hii. Ni wakati mwafaka kwa sababu baada ya miaka 50 tangu tupate Uhuru itakuwa ni jambo bora kama tungeanza kuangazia masuala ya afya kuwa muhimu sana katika maisha ya jamii. Kadri tunavyoendelea kumuunga mkono Mhe. Wanga kwa sababu ya Hoja hii lingekuwa pia wazo bora kama pengine baada ya haya yote ya kuwatuma wataalam kwenda kusomea na kuja kuleta mwelekeo bora ingekuwa bora kujua baadhi ya wataalam fulani kielimu ili kuhakikisha kwamba masuala ya elimu katika jamii yameaangaziwa. Hii ni kwa sababu punde saratani inapomkumba mwanadamu huwa maisha yamekwisha. Nimewahi kumpoteza mzazi wangu kutokana na saratani na rafiki yangu moja wa karibu aliyekuwa akiitwa Prof. Juma Lugogo. Ninakumbuka kabla Prof. Lugogo kuondoka duniani aliinita hospitalini na kuniambia:- "Nimepigana na matatizo ya saratani kwa muda wa mwaka moja na nusu na hivi sasa nimefika kiwango ninainua mikono kwa sababu ninajua kwamba mambo yameshindikana na inalazimika niondoke duniani." Alisema kitu ambacho kinaniumiza mpaka sasa kwamba: "Mimi ninaondoka na niliweza kuhimili kupigana vita hivi vya saratani kwa muda wa mwaka mmoja na nusu. Je mtu yule wa kawaida ambaye yuko kule mashambani ataweza kuishi muda ambao nimeishi kwa sababu mimi nilikuwa ninajiweza na ninaweza kufanya mambo fulani yanayoniwezesha kuishi na kupata matibabu yanayotarajiwa?" Hili ni suala nyeti kwa sababu zai ugonjwa wa kifua kikuu zai kilikuwa kikitisha watu. Sasa kifua kikuu kinaweza kupata tiba hospitali fulani na hatimaye ukarejeshwa nyumbani ili uendelee kupewa dawa ukiwa huko. Saratani imefika kiwango ambacho kinachukua watu wiki baada ya wiki lakini miaka 15 ijayo huenda tukawa tulikuwa tunamsubiri Yesu Kristo kuja duniani kumbe saratani ndiyo itakuwa kiama cha mwanadamu kupoteza ama kuangamiza maisha yake katika ulimwengu huu. Unapoambiwa kuwa saratani imepatikana katika mwili wako mara nyingi kinachokuja ni kwamba umebakisha kama miezi minne ama sita kuondoka duniani. Sisi kama viongozi ama kama watu tuliopewa majukumu na hasa zaidi kwa sababu ya utafiti ambao umefanywa na Mhe.Wanga nina ii kwamba takrimu hizi ambazo zimewekwa wazi kwetu Iko haja baada ya kupitisha Hoja hii kuifuatilia kwa karibu sana ili kuona kwamba matokeo yake yamesaidia jamii ya Wakenya na kuleta afueni katika maisha ya mwanadamu. Kimekuwa kitu cha kawaida pengine tumwuulize Mhe. Wanga ilimchukua muda gani kufikiria suala hili na hasa baada ya suala kumalizika pengine aangazie pia kufanya utafiti. Hii "saratani" ya ufisadi ataweza kuitumia tiba gani ama kuiletea Hoja gani kwa sababu pasipo sisi kupata suluhisho la kudumu Mara nyingi suala linaloulizwa ni kwamba wakati tunapohitaji msaada wa aina yoyote huambiwa kwamba Serikali haina pesa. Lakini haijapata jibu la wale watu wanaopoteza pesa za Umma kwa sababu anayekula pesa nyingi mara nyingi huambiwa bondi yake ni shilingi 500000. Mwenye kula shilingi kumi bondi yake ni shilingi milioni mbili. Kwa hivyo ninamwomba Mhe. Wanga arudi tena kizimbani afanye utafiti wa kutosha ili ajue kwamba hawa wafisadi atawapatia adhabu gani ili tupate kujua kwamba mwisho utakuwa nini kwa sababu masuala ya saratani kama tutayapitisha jinsi yalivyopendekezwa huenda tukapata afueni. Kwa hayo machache ama mengi ninaunga mkono. Mungu atubariki.
Mhe. Naibu Spika wa Muda ninaomba nimuulize mwenzagu wa upande ule mwingine Mheshimiwa Chepkong'a kama kweli ana uwezo na mamlaka ya kuachia mtu mwingine nafasi yake ya uanachama kwenye kamati ya Bunge. Uwezo huo ameutoa wapi? Hana uwezo wa kufanya hivyo kwa sababu huo uwezo uko Bungeni. Kwa hivyo asijitwike mamlaka ambayo hana. Amejibandikia mamlaka ambayo si yake. Watu hao wanaitwa kwa lugha ya mtaani wezi. Hawezi wala hana huo uwezo na hatakuwa na huo uwezo kwa sababu uwezo huo ni wa Bunge hili.
Mhe. Naibu Spika wa Muda ninashukuru kwa kunipatia nafasi hii. Nitachangia Hoja hii kwa ufupi. Kwanza ningependa kuishukuru Kamati ya Mhe. Gumbo kwa kuleta Ripoti hii wakati huu. Imechukua muda sana. Ningependa kusema kwamba ni lazima tutunze na tutumie rasilimali ya Kenya vizuri. Hilo ni jambo ambalo linajulikana na kila mtu katika nchi hii. Mmoja wa wananchi ambaye anaweka mkazo katika kutunza rasilimali ya nchi hii ni Naibu wa Rais. Kila mara akitumia chochote katika nchi hii anakitumia kwa njia iliyo safi na kwa njia ya heshima. Jambo hili lilileta joto jingi katika nchi hii ya Kenya kisiasa kwa sababu lilichukua mkondo ambao haukuwa unatakikana. Sababu ni kwamba tumekuwa na tabia au mazoea kwamba jambo fulani likitendeka tunalichukua na kulifanya kuwa la kisiasa. Kabla hata jambo hili halijachunguzwa na Kamati ya Bunge tayari lilikuwa limeenea kwamba Naibu wa Rais alitumia rasilimali vibaya na kwamba alibeba abiria wengi. Jambo hili pia liliharibu heshima ya ofisi hiyo na pia familia kwa jumla. Jambo la kwanza ni kwamba waliokuwa kwenye ndege hiyo walikuwa Waheshimiwa katika Bunge hili. Mimi pia nilikuwa mmoja wao. Tulienda kuiwakilisha Kenya katika mikutano. Tulipoenda Kinshasa tuliiwakilisha Kenya. Tulipeana hoja zetu na tukapendekeza mambo mazuri. Tulitoka mahali hapo na tukaenda Nigeria ambako tuliiwakilisha Kenya katika sherehe iliyokuwa huko. Naibu wa Rais alipata nafasi ya kutangaza nchi huko na hata kuwaambia wawekezaji waje upande huu. Hiyo yote inachangia faida katika nchi hii. Wakati tunaleta jambo kama hili mbele ya wananchi lazima kuwe na ukweli na mambo yawe yamethibitishwa. Lazima tuheshimu ofisi na hata jina la mtu. Tunapochukua kila jambo katika hali ya kisiasa tunaharibu sifa ya Bunge hili na pia tunaharibu heshima ya ofisi kwa sababu ofisi iliyoko sasa haiko mikononi mwa mtu fulani. Utafika wakati ambapo wananchi wataingia ndani. Nikimalizia jambo lingine ni kwamba wakati tunafanya uchunguzi lazima tujue kiini cha jambo hilo na tujue kama safari hiyo ina faida katika nchi au la. Tunaishukuru kamati inayochunguza matumizi ya pesa za umma ambayo inaongozwa na Mhe. Gumbo kwa sababu sasa imeweka wazi Ripoti hii na iko mbele yetu. Tunaomba siku nyingine tusitangulie kuharibu jina la mtu ama kuharibu ofisi ya mtu kabla hatujafanya uchunguzi. Kwa hayo ninaunga mkono Ripoti hii. Asante.
Mhe. Naibu Spika wa Muda ninashukuru. Yangu yatakuwa machache kwa sababu mimi ni mwanachama wa Kamati ya Ardhi. Ningependa kumshukuru Mwenyekiti wangu kwa kazi nzuri ambayo amefanya kwa Kamati yetu. Kamati ya Ardhi inafanya mambo yote ambayo inaweza kufanya kuhakikisha kwamba mjadala kama huu kuhusu shamba la Muri umetimia na mambo haya yamemalizikika. Lakini ningetaka kuweka wazi ili kila mtu aelewe na Serikali ielewe kuwa baada ya Kamati ya Ardhi kumaliza mambo haya yote shida nyingi zinatokea baada ya sisi kutoa maoni yetu. Shida hutokea baada ya kuanza kuwapatia cheti cha mashamba yao. Hapo ndio watu huingilia na kuuharibu mpangilio ambao umepangwa na Serikali. Ningewaomba wale ambao watahusika baada ya Bunge kutoa muongozo wake waangalie kwa makini sana ili tuudi kwa shida baada ya kusema kuwa tunataka kuyamaliza mambo haya. Wale ambao hawana mashamba wanafaa kupata mahali pa kukaa. Ukiangalia shamba hili ambalo tunazungumzia utakuta kuwa vitukuu vinaendelea kuwa na vizazi na maskwota wanaendelea kuongezeka usiku na mchana. Tukitatua jambo hili haraka iwezekanavyo tutapunguza umaskini. Hawa watu wakipata vyeti vya kumilika mashamba watasaidika kwa njia zingine kama vile kujaribu kupata mashamba mengine madogo kwa familia. Ni lazima tujue kuwa kuna shida. Tukimaliza mambo ya mipangilio ni lazima tuhakikishe kuwa wale ambao wanahusika kama vile Tume ya Ardhi au Wizara ya Ardhi inafanya mambo haya kwa uwazi. Wakati tulikuwa na shida ya IDPs watu wengi ambao walipewa makao sio wale ambao walikuwa IDPs. Baada ya Serikali kutoa shamba ya kuwapa IDPs mambo mengi yalitokea badaye. Ningetaka kuambia maofisa wa Serikali wanapowapatia watu mashamba wanafaa kuangalia kwa makini sana ili wasilete orodha zingine ambazo si za watu ambao wanafaa kupewa hayo mashamba. Hiyo italeta shida juu ya shida. Kwa hivyo Kamati yetu inafanya iwezavyo chini ya uongozi wa Mwenyekiti wetu Mhe. Mwiru ambaye anafanya kazi nzuri. Ninashukuru kusikia Wabunge wanaunga mkono jambo hili. Wanaiunga mkono Kamati ya Ardhi kwa kazi ambayo tunayoifanya. Tuko na mengi ambayo tumetayarisha kuleta Bungeni. Tukiwachia Wizara ya Ardhi na Tume ya Ardhi jambo la kufuatilia utaratibu wa mipangilio ya mashamba tungetaka waifuatilie ili isilete aibu tena au isisemekane kuwa wale ambao tulipendekeza wapewe mashamba sio wao walipewa na watu wengine walipewa. Jambo hili linaleta shida sana. Ninamshukuru Mwenyekiti wetu kwa kazi nzuri. Ninamshukuru Mbunge wa eneo hilo kwa sababu alitupeleka kwa shamba hili na tukaona vile liko. Ningetaka mambo haya yafuatiliwe bila kupita njia nyingine kwa sababu Kamati ya Ardhi katika Bunge iko na haki ya kuyamaliza mambo haya ambayo yaliletwa Bungeni. Kwa hivyo ninashukuru Bunge kwa kutuunga mkono. Tuendelee hivyo hivyo na tutapata nguvu.
Mhe. Naibu Spika wa Muda ninataka niseme kwamba tukiangalia Ibara ya Nne kwa wale hawatafahamu "Ibara" ni nini ni ile " FourthSchedule ". Ibara hiyo imezungumzia haswa zile kazi ambazo zinahusu Bunge la Seneti kama kilimo afya usafiri katika kaunti na mambo mengi sana ambayo wenzangu waliotangulia wameyazungumzia. Vilevile Ibara ya Nne imezungumzia yale majukumu ya kitaifa ambayo yanafanywa na Bunge la Taifa. Iwapo Katiba imezungumzia mambo haya kinagaubaga kwa nini tuwe na sitofahamu? Kwa nini tuwe tunarudiarudia ama ile tunasema duplication wakati tunafanya kazi zetu kama Wabunge? Wakati mwingi sana kuna suala limeangaziwa na Bunge la Seneti na Bunge la Taifa. Ripoti zinazokuja huwa tofauti na zinazoleta mg'ang'ano na tunakosa kupata mwelekeo. Ni wakati muafaka tujue sisi viongozi wa Taifa ambao tunajua majukumu yetu tujue kamati zile zitatengenezwa katika Seneti ziwe ni kulingana na majukumu nguvu na kazi zao. Zile zitatengenezwa katika Bunge la Taifa hili la National Assembly iwe ni kulingana na majukumu na nguvu ambazo tumepewa na Katiba ya Kenya pasi na kwenda kinyume chake. Katika Kifungu cha 94 tunaona kwamba Bunge zote mbili zinahitajika kukubali na kulinda Katiba yetu. Katika Kifungu cha 3 cha Katiba Mkenya anahitajika kukubali na kuilinda Katiba. Kuilinda Katiba ni kuilinda kwa kufanya zile kazi ambazo Katiba imetupa sisi kama Wabunge katika Bunge la Taifa na lile la Seneti. Katika Kifungu cha 110(3) Spika wetu na yule was Seneti kila wakati wanahitajika kuangalia suala la kujua Miswada ni ya kaunti au ni inayosimamia kupitia Bunge la Taifa. Kwa hivyo sijui tunavurutania nini kwa haya mambo kila saa. Mambo ya kukagua walioteuliwa na Rais tumeona ni jukumu la Bunge la Taifa linaloitwa National Assembly kulingana na Katiba. Kipengee cha 132(2) kinasema kwamba Rais atateua na sisi kama Bunge tutakagua iwapo aliyeteuliwa anaweza kufanya kazi ile. Lakini tunaona hata Seneti wamekagua yule tunamuita Inspector General of Police (IG) juzi. Hapo tunaona tunaleta utata na sitofahamu katika mambo yetu kama watu moja. Je sisi kama Wakenya tunaweza kuyapata mambo ya ugatuzi ambayo tuliweza kuwa na Seneti ambalo jukumu lake kubwa ni kuangalia mambo ya kaunti 47? Kuna changamoto gani na tutaweza kuangalia nini? Kwa hivyo mambo ambayo tunazungumzia kwa mfano kilimo makavazi tunayoita Museums leseni za pombe wanyama na cemetery tusiyaone kuwa ni mambo madogo. Haya ni mambo ambayo yanamdhuru mwananchi kila kuchao na anapata changamoto nyingi. Kwa hivyo ni lazima tujue kamati tutakazotengeza zitakuwa ni kamati kulingana na majukumu yetu ya kikatiba kwa mujibu wa vifungu 95 na 96 vya Katiba. Iwapo tutaenda kinyume na hayo itakuwa si sawa. Wizara kama ile ya Defence ni wizara inayoangalia mambo ya kitaifa tu. Haiangalii mambo ya kaunti. Wizara ya Interior inaangalia mambo ya usalama wa kitaifa. Wizara ya Foreign Affairs inaangalia mambo ya kimataifa. Kwa hivyo hizi wizara ambazo hazina mambo ya ugatuzi sioni ni kwa nini Mawaziri wake waitwe Seneti kuzungumzia mambo ambayo ni ya kitaifa na si ya ugatuzi. Lazima tujue mipaka yetu ni ipi. Hapa hakuna cha Bunge kubwa wala Bunge ndogo. Hapa ni Katiba inasema nini imetupatia nguvu gani imetupatia majukumu gani na mipaka yetu itakuwa gani?
Mhe. Naibu Spika wa Muda ningeomba hii iwe kama mazungumzo yangu ya kwanza katika Bunge. Nilisimama tu kuunga mkono Hoja nilipopata nafasi. Nashukuru Mwenyezi Mungu amekuwezesha kuniona. Nimekuwa nikisimama nikikaa hapa tangu nije. Nikianza na Hoja hii ninaunga mkono vilivyo kwa sababu wazee si watu wa kutupwa. Wazee wamefanyia mengi taifa hili ambalo linahitaji kuangaliwa kwa uangalifu zaidi. Wazee wa miaka 60 na zaidi wengi wao hawana ajira. Wengi wao wamestaafu na wengine hawajawahi kuajiriwa kabisa kwa sababu ya kujitegemea wenyewe kwa kazi zao za kibinafsi. Wazee hao wamekuwa mizigo kwa vijana wetu. Imekuwa wazee wanawategemea vijana na ilhali hali ya vijana ni ngumu kimaisha hata ajira hawana. Hata sasa unakuta vijana wanaanza kukosana na wazee wao. Hata sehemu nyingi wanawaita wazee wao wachawi. Hata inafikia wakati wanaanza kuwaua. Sio kwamba wale wazee wameroga watoto. Wale watoto wanafahamu vyema kwamba hawa wazee wamewalea tangu utotoni itakuaje hivi sasa wamekuwa wachawi? Kama wangekuwa na malengo mabaya wangeyatimiza wakiwa wachanga. Lakini kwa sababu ya hali ngumu ya maisha wanaona njia rahisi ya kuondoa mzigo huo ni kusema kwamba hawa wazee ni wachawi. Hii Serikali ninaweza kusema kwamba imepuuza wazee wetu. Hata mikasa mingi ambayo tunapata katika taifa nzima ni kwa sababu ya wazee. Kwa roho zao hawana raha. Kwa mfano ukosefu wa usalama katika taifa mafuriko na mambo mengi mazito yanatokana na kwamba wazee wetu hawana raha na wanaona kama wametengwa. Nikikupa habari kuna wazee wamekuwa katika nyumba ya muwajiri wao miaka miwili sasa katika hoteli za African Safari Club wakidai malipo yao. Wazee wale walikuja katika Bunge la Kumi hapa wakazungumza na kamati husika lakini hadi wakati huu shida yao haijasuluhishwa. Wale wazee wana
Mhe. Naibu Spika wa Muda ningeomba tu kutaja ya kwamba tusije tukawa kama pwagu na pwaguzi ambapo ndugu akifanya hili wewe unafanya lingine ili kuonyesha kuwa sisi si watu wa moja. Bunge la Kenya kazi yake ni kutengeneza sheria. Hivyo basi huu upwagu na upwaguzi ni lazima uwachwe ili tuweze kusongeza mambo mbele. Masuala ya ardhi haswa hapa nchini ni maswala yenye kuchukuliwa na kuleta hisia mbalimabli na hisia hizo zimewafanya watu wengi Wakenya kuumizana kwa sababu ya masuala haya. Kwa hivyo kwenye mipangilio ya ardhi zetu hatutaki utani. Asante sana.
Mhe. Naibu Spika wa Muda ningependa kuichukua fursa hii kukushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia Mswada huu. Nitaanza kwa kumshukuru Mhe. Lekuton ambaye kwa wazo lake la burasa ameuleta Mswada huu. Mswada huu unaelekea hasa kuangalia maswala ya usalama wa watoto wa shule. Ukiangalia baadhi ya mambo ambayo yamezungumziwa Mswada huu unaangalia usalama wa baadhi ya watumiaji wa mahala tofauti tofauti Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda haswa ukiangalia Mswada wenyewe unahimiza kuweko kwa baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kutusaidia kupunguza maswala ya ajali. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda Mswada huu ukiwa utapita - na ni matumaini yangu kwamba utapita - utaweza kutusaidia sisi kwanza kama wakaazi wa Kaloleni. Ukiangalia katika eneo ambalo ninawakilisha bali tu na zile barabara zingine kuna barabara mbili muhimu. Ya kwanza ikiwa ni ile ya kutoka maeneo ya Mariakani kuelekea Kaloleni ambapo karibu shule tano ziko karibu na barabara. Barabara hii ni muhimu sana kwa sababu inatumiwa na magari mengine ambayo hayawezi kuenda Mombasa ili kuepuka msongao wa magari. Ukiangalia pia kuna baadhi ya makampuni ambayo yamejenga na yana magari makubwa sana. Tena kuna shule na ajali pia zimekuwa nyingi sana. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa hivyo ningependa kusema kwamba Mswada huu ni muhimu sana. Kuna baadhi ya mambo ambayo lazima tuyaangalie. Jambo la kwanza ambalo lazima tutazame ni mafunzo ya madereva. Utakuta kwamba asilimia 90 ya zile shule ambazo ni za kufundisha watu wetu jinsi ya kupeleka magari yameandika kwa lugha ya Kimombo "guaranteed pass." Hii ni kuonyesha kwamba katika shule hizo hakuna hata mtu moja ambayo ataanguka mtihani wa kuendesha gari. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda pia ukiangalia sana utakuta kwamba kitu ambacho kinahitajika kwa mtu kuweza kupeleka gari ni kitambulisho chake cha kitaifa. Hakuna maswala ya kiwango cha elimu; ni kitambulisho cha taifa peke yake kinachohitajika. Unaanza kusoma na baada ya wiki tatu umehitimu kuwa dereva. Cha kushangaza ni kwamba hakuna nafasi ya watu kuweza kupewa mafunzo mara kwa mara ndio waweze kukumbushwa baadhi ya yale mambo ambayo waliyasoma wakiwa shule. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa hivyo nasisitiza kwamba tukiangalia marekebisho ambayo yatafanywa kwa hiyo sheria ya trafiki ni muhimu pia kuangalia maswala ya mafunzo ya madereva. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda jambo lingine ambalo ningependa pia kuliangazia ni kuhusu wale ambao wanahusika ama washikadau katika maswala ya trafiki. Kuna baadhi ya madereva ambao leo hii wanapeleka magari katika barabara zetu na baadhi yao labda kwa kupitia amri za mahakama walipigwa marufuku miaka kadhaa kupeleka magari. Leo watu hao wamepata zile tunaita copy za zile leseni zao na wako kwa barabara zetu na wanapeleka magari na watu hawajali. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa hivyo kuna haja ya kwamba wale ambao wanahusika haswa askari wanaohusika katika maswala ya trafiki waangalie swala hili. Katika kuangalia ulinzi wa watoto wetu shuleni haswa kwa magari ya shule ni muhimu pia zile shule ambazo huajiri madereva zikae chini na kukagua stakabadhi zao. Sio eti kwa sababu mimi nikiwa Mheshimiwa ama labda mwalimu mkuu wa shule amefanya mpango akapata gari basi mtu yeyote anaweza kuajiriwa kuwa dereva hivyo sio vizuri. Ni lazima kamati ambayo inahusika na mahojiano wahusishe idara inayohusika na usafiri ili wakague madereva hao. Wafanyiwe mtihani vizuri kabla ya kuruhusiwa kuendsha watoto wetu. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda ikiwa mambo haya yote yataweza kuzingatiwa utaona kwamba usalama wa watoto wetu kwa usafiri utaimarika. Kwa hayo eno mengi ningependa kuunga mkono Mswada huu.
Mhe. Naibu Spika wa Muda ningependa Mhe. T.G. Ali ajue kwamba hiyo ndiyo sababu ya kuibadilisha sheria hiyo. Nilipokuwa kule Malindi nilifuatwa na vijana wanaofika 2000 wakiwa na maua yao wakipiga kelele; wakifikiria kwamba mimi ni mfuasi wa KADU Asili rafiki yangu Mhe. Gunga. Inaonekana kwamba kama vijana wale wangelipata ruhusa ya kupiga kura - wale wakiwa vijana kutoka Jilore peke yake hatujui Malindi nzima kulikuwa na vijana wangapi waliokuwa na kadi za aina ile - nina hakika kwamba badala ya Jubilee nambari kuwa ya pilli ingekuwa KADU Asili. Lakini kwa sababu haki haikuzingatiwa wale vijana hawakupiga kura.
Mhe. Naibu Spika wa Muda shukrani sana. Naomba nianze kwa kusema kuwa naunga mkono Hoja hii kuhusu maafisa wa polisi. Sharti masuala yao yaungwe mkono. Nitaanza kwa kusema kuwa dunia nzima imewekeza vilivyo katika usalama wa taifa lakini hapa nchini Kenya sisi tumewekeza katika uhalifu wa kujitakia kwa sababu hatufuatilii utaratibu na kanuni zinazohitajika kuhakikisha kwamba usalama wa taifa unapatikana. Polisi ni mwananchi. Pia ni raia wa kawaida kama Mkenya mwingine. Kwa hivyo polisi wanahitaji kuangaliwa vilivyo ili waweze kutulinda sisi Wakenya. Pia nitazungumzia masuala kama vile bima yao vifaa wanavyotumia nyumba wanamoishi mishahara yao pamoja na marupurupu wanayopata. Maafisa wa polisi wanalipwa vibaya mno. Hata askari gongo analipwa zaidi ya afisa wa polisi. Ndio maana unaona nchi hii haisongi mbele kwa sababu hatuekezi katika usalama wa taifa. Ningelipenda kutoa mifano ambayo ni ya muhimu zaidi hususa katika vituo vya polisi au kambi za polisi. Vile maafisa wa polisi wanavyoishi ni jambo la kuchukiza mno. Vyumba wanavyotumia ni vyumba ambavyo aliyeoa na asiyeoa wanaishi pamoja. Huyu ambaye ameoa akitumwa safari ya mbali kwenda kuhudumia taifa kuna mtu anajenga nyumba yake. Ataregea kwa haa na kufanya mambo ya ajabu ajabu kama kuua au kufanya mambo mengine kisha tutaanza kupiga kelele na kusema kuwa maafisa wa polisi hawafanyi kazi inavyotakikana. Sisi Wabunge twapaswa kuweka mfano bora katika Bunge hili na kuhakikisha kwamba Hoja hii imepita na maafisa wa polisi wameanza kulipwa kama maafisa wengine. Tuweke mfano bora kwa maafisa wa polisi wanaotulinda ambao wanakaa hapa nje na ambao kunyeshewa au kuwe na jua kali wanasimama tu hapa nje wala hawana mahala hata pa kujizuia. Tuanze kwa kuweka mfano bora na watu kama hawa. Kuna maafisa chapakazi walioumia kwa ajili ya taifa hili. Namkumbuka afisa wa polisi Erastus Kirui Chemorei aliyepigwa risasi 21 kule Kitale na ambaye hadi sasa amezikwa katika kaburi kama mhalifu ilhali yeye si mhalifu. Ni mtu aliyekuwa akilinda maslahi ya Wakenya. Namkumbuka afisa wa polisi aliyemuangamiza jambazi sugu zaidi aliyeitwa Rasta. Yuko Eldoret hadi sasa hivi. Ana risasi mwilini mwake. Hadi wa leo hajapewa heshima wala matibabu ya kutolewa risasi hiyo kwa kazi aliyowafanyia Wakenya. Ni nani atakayezungumza kuhusu maafisa wa polisi 40 waliouawa kule Baragoi? Nilikuwa pale kama mwanahabari kuangazia masahibu ya maafisa wa polisi. Waliuawa kinyama. Hakuna mtu yeyote anayewazungumzia kuhusu maafisa wengine 29 waliouawa kule Kasarani Turkana. Hawa ni watu wa kawaida. Hawa ni Wakenya na ni binadamu. Watu hawa wana familia. Hatutakaa tukiimba kila siku kuanzia Januari hadi Disemba tukizungumzia masuala ya nyongeza ya mshahara ya maafisa wa polisi. Haifai. Haikubaliki. Hawa ni binadamu ambao wana uzito wa kutulinda sisi na taifa nzima. Leo afisa wa polisi analipwa kati ya Ksh15000 na Ksh21000. Ukiweka zote kwa pamoja - Ksh15 000 au Ksh21 000 - atapeleka wapi? Hi ni kama chakula chako cha mchana. Ana watoto na bibi. Hawajui watoto wao wataenda shule gani. Katika kambi za jeshi angalau wamejaribu kuekeza katika elimu na kujenga shule zao. Kambi za jeshi zina shule. Polisi hawana. Watoto wa polisi wataenda wapi? Leo bibi wa polisi akipachikwa mimba atajisaidia wapi? Hana bima. Ndio maana polisi anarudi katika ile kauli mbiu yake ya bima yake: "toa kitu kidogo". Kwa sababu sisi tumeshindwa kutunga sheria ya kuwafikia hao watu. Wakati ambapo polisi ni mtu wa maana katika taifa hili ni wakati ambapo kuna uvamizi Kenya. Katika shambulio la kigaidi kule Westgate maafisa wa polisi walijizatiti wakahakikisha ya kwamba wamelinda maslahi ya Wakenya. Maafisa wale wote waliopigana pale katika jumba la Westgate bado wana makovu ya upweke bado hawajalipwa na bado wanatembea na machungu kwa sababu hawawezi fikia hospitali. Afisa ambaye amepigwa risasi akipambana na mhalifu anaambiwa ajipeleke katika Hospitali ya Kenyatta. Hapewi heshima ya afisa wa polisi. Ni kwa sababu sisi hatutaki kutunga hizo sheria. Lau kama tungetunga sheria za kuleta mambo ya anasa duniani tungelikuwa wa kwanza kuzipitisha haraka haraka. Lakini sheria ambazo zinahusu maisha ya watu hawa hatufanyi. Naomba tuweke mfano na hawa wanaotulinda. Naomba tuwajengee mahala ambapo watakaa kwenye kivuli ili mvua ikinyesha wanaweza kujistiri mahali wakitusubiri. Ni lazima tutoe mfano kwa watu hawa. Leo wafisadi wakubwa na wabakaji wa demokrasia ni sisi Wabunge Mawaziri na viongozi wengine wakubwa wakubwa. Lakini leo afisa wa polisi wa barabarani akishikwa kama amechukua Ksh200 inakuwa ni habari ya dunia. Tunaacha wale walioiba mamilioni ya pesa; waliobeba na gunia wakabeba; waliobeba na mabegi wakabeba; lakini afisa wa polisi anayeiba Ksh200 tu inakuwa ni taarifa za dunia. Kuna sababu ya yeye kuchukua Ksh200. Kwa sababu wewe huwezi kuishi Kenya sasa na mshahara wa Ksh15000 au Ksh21000 una bibi na watoto na unataka wawe na maisha kama ya Wakenya wengine. Hili ni jambo ambalo tunafaa tulifikirie zaidi na tulipitishe kwa haraka bila wasiwasi wowote. Kuna kitu wanaita Harambee SACCO. Hii si SACCO ya maafisa wa polisi; ni SACCO ya matapeli. Maafisa wa polisi wanaekeza pale lakini hizo pesa zinakuwa ni za kushurutishwa na zinatumiwa na baadhi ya maafisa wakuu wa polisi wanaowanyanyasa maafisa wadogo wa polisi. Hawapati marupurupu ya kazi ngumu au hardship allowance ambayo wanapaswa kulipwa wakienda katika sehemu mbalimbali hatari kwa usalama. Afisa atapelekwa sehemu kama dera au Kainuk kule Turkana na zile pesa ambazo anafaa alipwe kwa siku hawezi kupewa kwa sababu zinaingia katika mfuko wa afisa mmoja ambaye anajiona yeye ndiye simba kati ya maafisa wengine. Naomba kupendekeza Hoja hii ipitishwe. Angalau nina furaha kama Mkenya kwa sababu tumeweza kufika kiwango cha dunia cha afisa mmoja kwa Wakenya 400 ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambayo hatukuweza kufika kiwango hiki. Kwa hivi sasa Kenya nzima ina maafisa 80 000 ambao wanalinda Wakenya milioni 45. Kuwapa motisha ni kuhakikisha kwamba wanapata mshahara wa kutosha ili waweze kujimudu wao na familia zao ili waweze kutuhudumia sisi Wakenya. Mvua inanyesha kila siku jua ni kali lakini ukipita katika mabarabara yetu utapata maafisa wamesimama kwa mvua. Hata Kitengo cha Usalama hakiwezi kuwapatia hawa watu mwavuli au majaketi ya kuzuia baridi. Ni laana na jambo la kuaibisha na kusikitisha. Nasimama na kusema kuwa wakati umefika wa Bunge hili la 12 kuhakikisha kwamba Hoja hii imepita na maafisa wa polisi wamehudumiwa. Tume ya Kavuludi isiwe tu ya vyombo vya habari. Iwe ni tume ya kuhakikisha ya kwamba hawa watu wamesikizwa na kulipwa ipasavyo. Hawa watu na ni binadamu. Hawana bima. Lazima washughulikiwe ipasavyo ili tuweze kuunda taifa nzuri ya usalama na kuekeza katika usalama kama nchi zingine. Dunia inaekeza katika usalama ilhali sisi tunaekeza katika ujinga. Leo tunavamiwa kiholelaholela. Leo utampa polisi bunduki aina ya bastola ambayo ina risasi 12 na jambazi ana bunduki aina ya AK47 na amejihami na risasi za kisasa. Leo unawatuma maafisa kama hao wapambane na wahalifu wakubwa. Wapeeni silaha vifaa mshahara na mambo yatakuwa mazuri.
Mhe. Naibu Spika wa Muda singependa kuzuia mwenzangu kuongea lakini anasema Serikali iliwatoa Wasabaoti. Si Wasabaoti ndugu yangu. Hiyo ni Sabaot Land Defense Force (SLDF). Ukisema wasabaoti unanikosea hapa na mwenzangu Serut na wengine kutoka kwa jamii ya Sabaot. Namuomba atupilie mbali mambo hayo na kuomba msamaha. Ameze mate Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Mhe. Naibu Spika wa Muda sio kwa sababu napenda watu wa boda boda sana kwa sababu mimi ni mama wa boda boda . Wakati mwingi mtu wa boda boda akiendesha boda boda hawezi kupiga mtu risasi. Mtu aliye na bunduki ndiye atamkodisha. Tafadhali sio mwendeshaji ndio anapiga risasi na sisemi hivyo kwa sababu mimi ni rafiki wa watu wa boda boda . Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Mhe. Naibu Spika wa Muda tukizungumzia habari ya stima ambayo Mhe. Rais alizungumzia sasa shule nyingi zinakatiwa stima zinakuwa kwa giza. Anasema kwamba yeye ameweka stima lakini shule nyingi zimeshindwa kulipa gharama ya stima. Shule nyingi zimerudi gizani. Hapo hajafuatilizia kujua hali halisi ilivyo. Akizungumzia kuhusu suala la barabara sisi kwetu Mombasa tunasema hata kama watu wanaona ni uchungu hakuna barabara hata kilomita moja ama mbili ambayo imejengwa na pesa ambazo tunalipa kama kodi. Barabara zinajengwa kule karibu zote ni zile ambazo tunapata misaada na mikopo kutoka Benki ya Dunia ama Uingereza. Sasa hapo ndio anasema ametengeneza barabara lakini kwetu kaunti ya Mombasa hatuoni. Hata mimi wakati moja tulikaa na Mhe Rais na Naibu wake tukazungumzia barabara ya Mwakirunge. Hata mimi katika pesa zangu za NG-CDF nilitaka kuanza kutengeza nusunusu wakaniambia "Usitengeneze. Tutatengeneza sisi kama Serikali kuu." Hakuna kitu ambacho wamefanya. Kwa hivyo sioni kama amezungumzia mambo ya maana sana. Kuhusu reli alisema tarehe moja Juni twende tukapande reli tukuje. Reli ile ni kuukuu. Ile ni reli ambayo ni second-hand sio ile wananchi walikuwa wanataka - ile ya kuenda mbio. Ile ni kama ya zai tu imepakwa rangi.
Mhe. Naibu Spika wa Muda ukiangalia gazeti la leo la The Standard katika ukurasa wa tatu utapata "mizigo" ya mwanaume. Unaelewa "mizigo" ya mwanaume. Hatuwezi kuitaja lakini kila mtu anaielewa. Wanawake wa Nyeri wakifanya harusi baada ya kupewa vyeti wanangoja wakati wanaume wamelewa pombe ama wamelala kisha wanakuja na kisu na kung'oa kila kitu. Sisi wanaume tumechokeshwa na hawa akina mama. Ndio maana nasema hata ni shida kuunganishwa katika ndoa. Mimi natetea wanaume kwa sababu wanawake wamekuwa shida kwetu. Lazima tuende polepole na tuelewane na akina mama kwamba "Mimi nimekuoa uwe bibi yangu. Nimeunganishwa na wewe na kuwekwa pete na nitakaa pamoja na wewe." Hakuna maana ya mama kutoheshimu bwana yake. Lazima uniheshimu na mimi nikuheshimu ndio tuweze kukaa pamoja. Hata tukienda kuunganishwawakati mwingine kuna wale wakora. Unaunganishwa nao lakini yeye analenga ile mali ambayo unayo kama magari na nyumba. Akiingia kwa nyumba anakuwa simba; huwezi hata kuongea wala kuinuka. Hilo ni jambo baya sana. Sisi wanaume tunasema kwamba kile kitendo kilitendeka Nyeri kwa Wakikuyu si kizuri. Ni kitendo kibaya sana kung'oa mwanaume "mizigo" yake. Wewe mama unang'oa mali ya mwanaume na hiyo mali ndio inakufurahisha ! Ni vibaya sana. Mimi ninaunga mkono Hoja hii lakini hilo jambo la kung'oa vitu vya wanaume sitaki.
Mhe. Naibu Spika Wa Muda ukweli ni kwamba kipengele cha 147 cha Katiba yetu ya Kenya kinahusisha binadamu wa maumbile yote na binadamu wa jinsia zote kwenye maswala ya ugatuzi hasa kwa maswala ya bunge za kaunti. Ninatoa pongezi zangu kwa Seneta Martha Wangari kwa kutukumbusha kwamba bunge za maeneo ya ugatuzi haswa kaunti zetu humu nchini zilivyoanza kazi wakati huu uliopita hazikua na wanachama vile instahili kulingana na kipengele hicho cha Katiba. Ni tatizo kubwa sana kuwa bunge hizi za ugatuzi zilianza kazi kabla ya kina mama na haswa walemavu kuweko katika bunge hizo ili kuchagua spika pamoja na wale wengine ambao wanasimamia kamati tofauti tofauti. Jambo la kusikitisha ni kuwa ikifikia swala la wanawake ama swala la kuhusisha vijana ama walemavu watu wanataka kuangalia ikiwa mtu huyu amesoma kiasi gani ama unasikia watu wanaongea kama Wakenya wote hawana haki ya kuhusishwa kwenye maswala ya kutengeneza sheria hasa kwa maswala ya ugatuzi ambayo ni maswala mapya na ni maswala ambayo yanatakikana kuangaliwa kwa uangalifu ukihusisha wananchi wote wa Kenya. Jambo la kusikitisha ni kuwa wakati huu makosa yalifanyika kwa sababu ni mara ya kwanza. Lakini tunavyoelekea mbele ni lazima tuangalie kuwa bunge zimebeba jinsia zote na kujumuisha wananchi wote ili waweze kufanya kazi pamoja. Tume ya Sarah Serem imefanya mambo ambayo yanalenga sana na kutenga wale ambao walikuwa washughulishwe tangu mwanzo kuwa wanachama wa bunge za ugatuzi. Kuna pesa zingine wenzao wanalipwa na wao hawalipwi. Kwa mfano wenzao wanarudishiwa ridhaa wakati wa usafiri mileage claim lakini wale ambao wamewekwa kwa orodha hii maluum ya wabunge wa kaunti wamenyimwa. Akina mama walemavu pamoja na vijana wamenyimwa wakiambiwa hawastahili kupatiwa. Hutoka maeneo walipochaguliwa kutoka kwenye wadi zao kuletwa kwenye bunge lile. Maswala hayo yote ni lazima sasa hivi tuyarekebishe ili tuhakikishe kwamba tunapokwenda kwenye uchaguzi ujao kusiwe na makosa yale yaliyotokea pale mwanzo. Kwa hivyo ninaunga mkono na ninatoa pongezi zangu mara nyingine tena kwa Seneta Martha Wangari kuhakikisha kuwa tunavyoenda mbele Kenya inaweze kujumuisha wananchi wote kwa maswala ya ugatuzi kwenye bunge za kaunti.
Mhe. Naibu Spika wa muda vile vile nasimama kuunga mkono Hoja hii. Hoja hii inalingana na jukumu la Bunge kuwa itaweza kujadili na kutatua matatizo ambayo yanahusiana na wananchi kama inavyosema Katika katiba Kifungo cha 95(2). Pia naunga mkono Hoja hii ambayo inaungwa mkono na Katiba katika Kifungo cha 19(2) na 20(2) ambayo imezungumzia kuhusu haki za raia ambazo zatakiwa watu wafaidike kwa kikamilifu. Tukiangalia katika Kifungo cha 43(1)(a) ambacho kinazungumzia haki za afya za wananchi yatakiwa wananchi wapate huduma kwa hali ya juu kabisa. Tukimalizia watu wazima ama wale ambao ni wazee Katiba vile vile katika Kifungo cha 57(b) inasema wanatakiwa wapate huduma bora kutoka kwa watu wao na Serikali. Tukiangalia hayo yote tunaona Katiba ya nchi yetu inatilia mkazo mambo ya afya. Tukiangalia katika historia nchi yetu ya Kenya iko nyuma katika mambo yote yalioahidiwa wananchi wakati wa Uhuru. Kwa ufupi tungependelea hata ikiwa hili Bunge linaweza kukubali mambo ya laptop na maziwa ya bure yaondolewe ili tuweze kuhudumia wananchi wetu katika mambo muhimu ya elimu afya na mishahara ya waalimu ili tusiwe na mizozo siku za karibuni wananchi waalimu na madaktari wakiomba mishahara na tushindwe kuwahudumia wananchi wetu. Kwa hivyo kwa ufupi hata mimi ningeongezea kusema kwamba community health workers wafikiriwe kwa maana wanafanya kazi muhimu katika jamii zetu. Mwisho kuna mahosipitali ambayo yako kwenye barabara zetu muhimu kama vile Voi na zinginezo. Zingefaa zipatiwe wahudumu wengi kwa sababu ajali nyingi zikitokea kupeleka watu Mombasa ama Nairobi huwa inapoteza wakati mwingi na wengi wanakufa kwa sababu ya ukosefu wa huduma za haraka. Kwa hayo machache naunga mkono.
Mhe. Naibu Spika wa Muda wale wazee ambao wako pale ni miaka miwili sasa; wanakufa mmoja mmoja na sasa wanaona kwamba wanaanza kulaumu Serikali na kuilaani na ndio sababu tunapata mambo mengi na maafa. Ningeomba wazee wetu waangaliwe ili tuzuie laana kwa taifa letu. Kuhusu usalama wa kitaifa uko katika majaribio. Mavamizi katika sehemu za magharibi; magengi katika sehemu za dera na sehemu nyingi za taifa hata sehemu za Pwani imekuwa shida kubwa. Kila siku kuna vikundi vipya vimejiunda na wanakula
Mhe. Naibu Spika wa muda yangu nikushukuru Rais kwa ile kazi amefanyia Wakenya. Ya pili ni kile kitendo ambacho alifanya kabla hajaenda ng'ambo kumwaachia Mhe. Samoei Ruto Serikali. Si wengi wanaweza kufanya hivyo. Hata wewe ukiwa mhe. huwezi kuwacha kiti chako na kwenda ng'ambo. Hiyo ni kuonyesha kwamba yeye ni mtu wa watu; hana mtoto wa mgongo wala wa tumbo; hana mtoto aliye na kamasi wala mate. Watoto wote wa Kenya ni wake. Jambo la tatu aliingia gari bila walinda usalama na kupitia ule mlango ambao tunapitia tukienda ng'ambo. La nne alirudi Kenya bila walinda usalama wowote mpaka akaingia Ikulu. Hii ni kuonyesha kwamba vita vya 2008 havikuwa vya Uhuru Kenyatta William Ruto ama Raila; vilikuwa ni vita vya PNU na ODM. Alionyesha kwamba mkubwa wa Electoral Commission of Kenya (ECK) alitangaza ODM ilikuwa imeshinda uchaguzi na wakaanza kuimba wimbo lakini baadaye akatangaza kuwa PNU walikuwa wameshinda nao wakaanza kuimba wimbo; baadaye walikutana na wakaanza kupigana. Walipoanza kupigana Uhuru Kenyatta hakuweko William Ruto hakuweko na wengine pia hawakuweko; baadaye hatukusikia kuwa kile kikundi chote kingepelekwa The Hague. Wale walipelekwa Hague ni William Ruto na Uhuru Kenyatta. Hii Ndio sababu tunasema kama Wakenya tumekataa kutawaliwa vibya na wakoloni Waafrika wenye ngozi nyeusi. Wakati umefika sisi Wakenya tuweke ukenya wetu chini na tuseme sisi ni binadamu na tushirikiane na watu wetu. Watu wanaona Uhuru Kenyatta akiitwa kule The Hague na wengine wanapiga makofi na kusema kwamba anaenda kufungwa ili wachukue Serikali. Serikali haichukuliwi ovyo ovyo. Serikali huchungwa. Serikali ni kama mtoto mdogo. Uliona kitendo ambacho alifanya kilishtua Kenya yote. Kuna wengine wangeachiwa mamlaka vile Ruto aliachiwa wangesema eti Uhuru asikanyage uwanja wa ndege; Serikali yake ingepinduliwa. Lakini hiki ni kitendo cha maana na nikiwa katika CORD naunga Serikali mkono. Kwa nini? Kwa sababu wameweza kuinua Wakenya na kutoa vitu vyote mezani. Kuna wengine wangechukua Serikali na kazi yao ingekuwa ni kufanya mambo chini ya meza. Lakini kwa sasa Jubilee inafanya mipango yake juu ya meza. Kwa njia gani? Angalia mambo ya pesa za kaunti. Kwa sasa Meru County ina Kshs5 billion; Kisumu ambao hawakumpigia kura wana Kshs6 billion; Ukambani hawakumpigia kura na wana Kshs7 billion; Mombasa hawakumpigia kura na wana Kshs4 billion na yote ni Uhuru Kenyatta na William Ruto wameweka mezani. Lakini utasikia watu wakisema kwamba hakuna kitu Jubilee imefanya. Hakuna kwa nini? Eti kwa sababu wakati nyumba inajengwa wakati msingi unachimbwa watu wengi hua hawajui kama ile nyumba itainuka. Wakati nyumba inaanza kuwekwa mawe na chuma na kuanza kuinuka ndipo watu wanakubali kuwa kuna nyumba inayojengwa. Jubilee ilikuwa ikijenga nyumba; Ilikuwa ikichimba msingi. Sasa nyumba imeanza kuinuka na kuonyesha kwamba Uhuru Kenyatta anaweza kupeana Serikali. Anaweza kwenda bila walinda usalama. Hii ndio maana namwambia mheshimiwa asiseme Nyanza hawajafanyiwa kitu. Juzi wamepelekewa kshs7.6 billion na badala yao kupokea Rais kwa mikono miwili kama mtoto mdogo kwa sababu amewaletea pesa walimpokea kwa viatu. Ndio maana ninasema hata wasingepewa hizo pesa. Zingekuja upande wa Meru ambako tuna taabu. Tuna taabu ya barabara chakula na biashara ya miraa imefungwa kule ng'ambo. Tuna taabu ya vitu vingi. Kwa hivyo nina ii na Rais wetu mpendwa ambaye anatawala nchi hii na ninawaambia kwamba hakuna maana ya kubembeleza kile kikundi. Hakuna haja ya kumbembeleza punda kwa mteremko mwachilie ateremke ukambembelezee kule chini.
Mhe. Naibu Spika wakati mwingine uangalie watu wengine ili waweze kusema neno hata moja. Tangu tuingie hapa wengine wetu hatujapata nafasi. Haya mambo ya miraa yanadhuru kila mahali.
Mhe. Naibu wa Muda ningependa tu kutoa shukrani na kuwajulisha wenzangu ya kuwa ifikapo 6.00 p.m. na hatujaweza kumaliza nataka kufafanua ili wenzangu wafahamu kwa nini tunakata mazungumzo. Ni kwa sababu Mhe. K'oyoo alikuwa ameomba ikifika 6.00 p.m. Bunge lisimamishwe lizungumzie swala la maafa ya mafuriko. Kwa hiyvo mimi natoa shukrani na sasa tunaacha jukumu hili kwa Kenya Ferry Services Kenya Maritime Authority na Wizara. Kama Wajumbe tumefanya kazi yetu; tumeweza kumaliza; na mimi natoa shukrani kwa kila aliyehusika: Wajumbe wenzangu wafanyikazi wa Bunge wakiwemo makarani afisi ya Spika na afisi ya Karani Mkuu. Ahsante sana nawatakia likizo yenye heri na fanaka.
Mhe. Naibu wa Spika nataka kuwafahamisha Wabunge wenzangu kwamba nimezoea kelele hata nilikotoka lakini mimi husema ninayotaka kusema. Nasikitika kwa sababu leo nimeketi upande mbaya wa Jumba hili lakini nitaendelea.
Mhe. Naibu wa Spika wa Muda asante sana kwa kunipatia nafasi hii. Ningependa kusema kuwa Mwenyekiti wa Kamati hii ya kukagua kazi za Serikali haswa vile Serikali imetumia pesa na kama pesa zimefujwa ama zimetumika sawasawa amefanya kazi nzuri. Mhe. Keynan na wenzake wamefanya kazi nzuri. Chuo hiki ni cha muhimu sana. Lakini juu ya hapo ni jambo la muhimu kuwa Wakenya wafahamu kuwa haiwezekani kuwa tunajenga chuo miaka nenda miaka rudi na hakiishi. Kama chuo kilichorwa na mipangilio ilikuwa kuwa awamu ya kwanza ijengwe kwa kutumia pesa taslimu karibu bilioni mbili basi wangekuwa wamemalizia awamu hiyo ya kwanza. Halafu kama kuna chochote cha kuongezewa kiongezewe baadaye. Lakini kwa sasa hivi miaka imesonga mbele. Hata reli kutoka Mombasa hadi Nairobi ilijengwa kwa miaka mitatu. Ulimwengu mzima tunapongezwa kuwa hakuna pahali pengine reli inajengwa kwa kasi namna hiyo. Chuo hiki kingekuwa kinawafaa watoto wetu hapa nchini Kenya na haswa sisi wapwani ambao swala la utalii ni la muhimu sana kwetu na Wakenya wote kwa jumla. Mpaka sana watu wanakizungumzia kuwa kimetumia pesa mara tano ya kiasi kile ambacho kilikuwa kimetarajiwa kutumika. Na hata leo tunavyozungumza chuo bado hakijakamilika. Ni mambo ya kustaajabisha sana. Ni lazima ufujaji wa pesa Kenya hii ukome. Katika uchaguzi unaokuja wananchi watafanya uamuzi kuwa ufujaji wa pesa lazima ukome. Katika hali ya ugatuzi vyombo vya ugatuzi na kazi za ugatuzi unaona kuwa ufujaji unaendelea. Tunaomba kuwa Wakenya wafanye uamuzi wachague viongozi ambao wataweza kutumia pesa vizuri na vile vile chuo hiki kiweze kukamilika. Mhe. Rais anataka chuo hiki kikamilike maanake anajua faida na hali ya uchumi ambapo utalii unasaidia. Tunaomba chuo hiki kimalizike mara moja. Lakini juu ya hapo ufujaji wa pesa lazima uchungwe na ulindwe ili chuo hiki kiweze kutekeleza matarajio ambayo kilitarajio kutekeleza. Nikimalizia nawaunga mkono wenzangu kwa yote waliyosema na kwa wote waliotoa mapendekezo. Tunaomba chuo hiki kikamilike.
Mhe. Ndugu Spika ninakubaliana nawe. Ni kama amri kwamba niwape nafasi Wabunge kama wawili. Ninajua kuna Mbunge wa Lamu ambaye alitusaidia sana na ninampatia dakika moja pamoja na Mhe. K'Oyoo na akiharibu lugha polisi wanaweza kumshika. Halafu Mheshimiwa ambaye pia yuko kwa hiyo kamati ambaye tulikuwa naye hapo jana kutoka Baringo. Wanne dakika moja kila mmoja.
Mhe. Ngunjiri nafikiri itakuwa vyema kama tutaweza kuangalia ule Mswada ambao uko mbele yetu badala ya kuzungumzia siasa. Najua yapo eno mengi yanayofanyika kule nje lakini kwa sasa hivi kazi yetu ni kuangalia Mswada ulioko hapa ambao ni Finance Bill 2017. Tuangalie vipengele hivyo na tusizungumzie mambo mengine. Tusiende kwa siasa tafadhali kwa sababu naona kuna hoja za nidhami nyingi. Itafanya mchango wako kuwa bila ladha. Kwa hivyo jaribu kuzingatia Mswada.
Mhe. Richard Onyonka nataka kukukumbusha kwamba uko na dakika mbili kabla tumwite mwenye Hoja kujibu.
Mhe. Sankok umempatia Mhe. Mohamed Ali wa Nyali sifa chungu nzima na hii ni sawa. Changamoto ni kwako kwa sababu umesema hili ni Jumba ambalo linaunda Bajeti. Kwa hivyo katika Mswada wa kuunda Bajeti tutakutegemea wewe uweze kuleta mchango wako na marekebisho ya kuweka haya mawazo ya mwenzetu Mhe. Mohamed ili watu wetu waweze kuondolewa huo mzigo. Kwa wakati huu nitampatia nafasi Mbunge wa Kauti ya Kilifi aweze kupeana mchango wake.
Mhe. Spika aisifuye mvua imemnyeshea. Kama huyu shangazi amependezwa na Duale na ubabe wake ni sawa; sina shida naye.
Mhe. Spika asante kwa fursa. Namshukuru Mwenyezi Mungu kupata fursa kuchangia Hoja ya kihistoria katika Taifa la Kenya. Kwa nini ninasema ni Hoja ya kihistoria? Ukisoma kifungo cha sheria 152(2) inatoa uwezo kwa mara ya kwanza katika Taifa Bunge kama taasisi kupitisha pendekezo lililotolewa na Rais wa Taifa. Hii ni historia kubwa. Ukisoma kifungo cha 152(3) kinasema Bunge lisihusike katika kuteuliwa kwa mawaziri watakao endesha shughuli ya kitaifa. Hii ni historia kubwa ambayo ninafuraha nikisimama hapa leo kuchangia Hoja hii. Bi. Naibu wa Spika hii ni heshima kubwa kwa taasisi ya Bunge na Wabunge. Mawazo ni tofauti. Baadhi yetu wanasema kwamba asilimia fulani ya Mawaziri wateule wanatoka mkoa fulani na asilimia fulani wanatoka mkoa mwingine. Lengo na maudhui ya kubuni Serikali ni kuhudumia wananchi. Inafaa wale wanaoleta hoja hii wakumbuke kwamba Serikali iliyopita ilikuwa ya sehemu mbili za nchi hii. Zaidi ya asilimia 50 ya Mawaziri wa Chama cha ODM walitoka Mkoa wa Nyanza. Kwa nini wakati huo wenzetu hawakushangaa? Mbona leo wanaona ajabu?
Mhe. Spika asante sana. Hii ni barua iliyoandikwa kwa Karani Mkuu wa Bunge. Haya si eno yangu mimi. Kwa ruhusa yako Bwana Spika ningeomba niiweke katika meza waweze kuikubali ama kuikataa karatasi hii.
Mhe. Spika asante sana. Naunga mkono mjadala huu ambao ni muhimu sana. Pili unapomsikia Mhe. Naomi Shaban akizungumza Kiswahili na akikiboronga sawasawa unapata uchu kidogo nawe pia ukizungumze Kiswahili. Nimemuona ni mkiritimba na mtu ambaye ana ujuzi mwingi sana na ubabe katika lugha hiyo. Mimi kama Mjumbe wa Shinyalu nasimama hapa kumuunga mkono Bi. Ann Nderitu. Ni afisa ambaye ninavyomjua ana ujuzi mzuri na pia ana mahusiano mazuri na watu. Vilevile ana hulka na tabia nzuri. Tunaona kwamba anafaa sana kushikilia wadhifa huo katika kuendeleza gurudumu hili ambalo ni telezi. Kama mnavyojua mara nyingi tumewajua wale waliokuwa pale mbeleni. Kuna Lucy Ndung'u ambaye pia alifanya kazi nzuri lakini ujue ukiwa kaimu inakuwa vigumu sana wewe kutekeleza na kushikilia vizuri kwa sababu hujui kesho au siku utakayotolewa. Ningependa kumshukuru Rais kwa kumchagua yule mtu anafaa zaidi na pia kuzingatia majadiliano yaliyofanywa na shirika la kuajiri. Hiyo ni heko kwake. Ningependa kumwambia Nderitu akae ange kwa sababu inafika wakati ambapo tutakuwa na mambo mengi ya kudafilisha na kuchanganyachanganya. Kama mnavyojua kuweka shajara mara nyingi huwa kuna mushikili kidogo. Unaweza kujikuta umo kwenye chama kingine ambacho si chako. Nakumbuka wakati nikitafuta uchaguzi wangu hasa baada ya kuteuliwa kama mgombea wa chama cha ODM nilipelekwa kortini nikajikuta kwamba nimo katika chama cha ANC. Msajili anayesimamia alikuwa amesema mimi ni mwanachama wa ANC na hakuna hata wakati mmoja niliwahi kuwa kule lakini ukiangalia kwenye sajili zinasema kwamba Mhe. Kizito ni mwanachama wa ANC. Kwa hivyo niliweza kurudi tena kwa uchaguzi kwa sababu hiyo. Lazima akae ange angaalie rekodi hizo sawasawa ili tusije tukawa na balaa na belua kama hiyo. Kama unavyojua sisi wanasiasa mara nyingi tunakuwa na mambo yetu ya kisiasa ambayo si ya kanisa bali ya kaisari. Kwa hivyo sisi lazima tuachiwe njia yetu pia tufanye vile tunavyotaka lakini naye pia awe ange ili tuweze kushirikiana vizuri. Nikirejelea suala la yule bwana aliyebanduliwa nje ningependa kumuunga mkoni sana Mhe. Dennitah kwamba kweli kijana yule amefanya bidii na ameonyesha kwamba yeye ni shujaa. Ningependa kumtolea kongole na nimpatie heko kubwa kabisa kwa kuwa ni swala nzuri kujaribu. Ningependa kumkumbusha kijana yule kuwa ameshinda kwa sababu amefika kiwango cha Rais wa nchi hii. Amri Jeshi Mkuu kuweza kuweka kidole kuwa anafaa lakini wale wahitifadhi wakutarazaki wenye ujuzi akina Otiende waliingilia pale wakaweza kuona kwamba yeye hatoshi. Tumpee moyo siku nyingine atapata. Nampa kongole kwa sababu amefanya bidii sana. Lakini kwa mujibu wa taharudhi na kanuni zinazosimamia mambo hayo hangeweza kupata fursa hiyo. Nampa kongole. Labda niseme tunastahili tutafute namna ya kuweza kuwapatia nafasi vijana wetu tukiangalia sheria zetu tulegeze mahali fulani kwa sababu ya vijana kwa sababu tukitafuta ujuzi ama tajiriba fulani atakuwa amepata wapi? Labda ni mtu amesoma ametoka tu shuleni lakini sasa tunaangalia ujuzi tajiriba miaka mingapi na amesomea nini. Swala hilo huwa linachanganya na linaweza tuweka mahali pabaya sana. Kwa hivyo ningependa kuomba nchi hii iweze kuwaangalia hawa watu kwa sababu unaweza kumpata mzee wa miaka 50 lakini ana akili kidogo kuliko kijana ama unaweza mpata kijana aliye na akili nyingi kuliko mzee. Kwa hivyo swala la umri lisiwe kikwazo. Isiwe tu ni tajiriba. Inaweza kuwa ni tajiriba mbaya ya wizi tu. Ujuzi wako mwingi miaka arubaini lakini ni wizi tu.
Mhe. Spika hata wewe unataja masuala ya jinsia ambayo ni muhimu kwa Wakenya wote haswa kwa vile tumepata Wizara ya kusimamia masuala ya jinsia. Vile vile Waziri Willy Bett ambaye amapatiwa kazi hii atawaze kufanya kazi kwa Wizara ya Kilimo. Yeye pia ana shahada tofauti tofauti na utendaji kazi wake unafahamika. Ukweli ni kwamba Waswahili husema sikio la kufa halisikii dawa. Tunavyokuja hapa leo kuzungumzia masuala haya tukumbuke kwamba sisi ni Wakenya na nchi yetu ni moja. Hakuna yule aliye Serikalini na yule aliye Upinzani ambaye atasema hiyo ni Kenya yenu na hiyo sio Kenya yetu. Kuna umuhimu kwa Wakenya kuwa kitu kimoja na kufanya kazi pamoja. Naunga mkono. Ahsante sana.
Mhe. Spika haya mapendekezo ambayo yameletwa na Serikali ya Jubilee; ni mapendekezo gani ambayo yameletwa katika Bunge hili na ule upande ambayo yamepingwa na Serikali ya Jubilee? Hakuna mapendekezo ambayo yameletwa na Upinzani.
Mhe. Spika inakubalika katika Kanuni za Kudumu za Bunge la Taifa kuangalia yale umeyaandika ukiongea na wenzako katika Bunge hili. Lakini bahali yake huyu mtu ni kusumbua watu. Bahali yake huyu Mheshimiwa wa Endebess ni mtu wa matata. Mimi nataka nipongeze na nishukuru Katibu wa Bunge la Kitaifa na lile Jopo ambalo lilitayarisha Kanuni hizi. Hii ni hatua muhimu sana katika historia ya Bunge hili na katika historia ya nchi yetu. Tutakumbukwa kama Wabunge waliowezesha kuwepo kwa Kanuni za Kudumu kwa Kiswahili. Na wewe pia utakumbukwa na Bunge la 12 litakumbukwa. Ni mara ya kwanza katika historia. Ningependa kuwaomba ndugu zetu Watanzania kama wanatusikiliza na kufuatilia mjadala huu kwenye runinga watusamehe. Huu ndio mwanzo wetu. Kadri tunavyoendelea tutakuwa tumejua ufasaha wa lugha ya Kiswahili zaidi. Waheshimiwa wenzangu Kiswahili ni sehemu ya maisha na utamaduni wa kila Mkenya.
Mhe. Spika jambo la pili ni kuwa huenda kuna mapendekezo ambayo yanatashwishi hapa. Ni nani amekatazwa kuleta mabadiliko ili kubadilisha na kutengeneza hii sheria wakati ufaao? Hakuna mtu ambaye amejaribu kufanya hivi. Wale ambao wanapinga haya mapendekezo wameguzia vifungu kama vitatu. Kwa kweli tumesikia maoni yao. Mwenyekiti wa kamati ya Utawala wa Mikoa na Usalama wa Ndani amesikia. Ataangalia kuhusu mambo ya mikutano kama hiyo ambayo iko na shida na kutaletwa mapendekezo ya kubadilisha mambo haya. Kwa hivyo ninawaomba wenzangu wote tushikane ili tuyashughulikie mambo ya usalama katika nchi hii. Mwaka jana tuliipatia Serikali pesa nyingi sana kwa upande wa usalama lakini tumeona kuwa hazitumiwi vyema hata kidogo. Kama afisa ambaye anahusika na mambo ya mipaka anamruhusu mtu kuja hapa nchini baada ya kupewa hongo anastahili kufungwa. Hivi majuzi nilikua Mombasa nikaongea na jamaa mmoja akaniambia ametoka Rwanda lakini akatoa kitambulisho akaniambia alikinunua hicho kitambulisho kwa Kshs10000 pekee. Mnasema yule ofisa ambaye alipeana kitambulisho tusimhukumu? Mnasema huyo mtu mwenye kitambulisho hicho tusimnyang'anye? Hizi sheria ambazo ziko hapa ni muhimu sana. Tupatie Rais na askari wetu uwezo wa kushughulikia hawa maharamia. Wacha wamalizwe kabisa. Hivyo ndivyo ninasema.
Mhe. Spika jina langu ni Onesmas Kii Ngunjiri kutoka sehemu ya uwakilishi ya Bahati. Kwanza ningependa kuwashukuru wakazi wa Bahati kwa kunichagua na kuweka rekodi. Kutoka mwaka wa 1963 Mbunge aliyechaguliwa kwa kura nyingi zaidi katika eneo Bunge hilo ni mimi Kii Ngunjiri. Kwa hivyo ninawashukuru sana watu wa Bahati. Pia ningependa kukupongeza mhe. Spika kwa kuteuliwa kuwa Spika wetu. Pili ningependa kuichangia Hoja tunayoizungumzia leo kuhusu Hotuba ya Rais wetu. Mara nyingi ndoto humsumbua mwenye kuota lakini siyo mwenye kutafiwa. Rais wetu anajua anachozungumzia. Sidhani kama kuna rais aliyechaguliwa na kura
Mhe. Spika katika Jumba hili kama kuna watu ambao wanajulikana kwa hekima zao wewe ni mmoja wao na utaingia kwenye kumbukumbu za historia kwa sababu ya hekima ambayo umeweza kuitumia hususa hivi sasa. Mmeweza kueleza lugha ya kisheria. Ningetaka tuzungumze lugha ya mtaani. Mpuuzi mpe sifa. Baadaya yote yale hili Jumba ni Jumba ambalo rekodi zote zinawekwa. Inajulikana wazi ni nani anayeleta masuala yakutetea watu zaidi ya yeyote mwingine. Historia ipo katika Hansard iliyo hapa. Inajulikana wazi ni nani. Lakini leo nakumbuka eno ya marehemu Mzee wangu akiniambia usihofie.Nakumbuka kauli ya kuwa pale unapoona ya kuwa ghafla mawe yanaanza kutupwa kwa kiwewe. Ile lugha yakunikashifu mimi familia yangu mpaka marehemu baba yangu aliyoko chini kwenye kaburi kwa sababu ya kauli za jana nawaambia tu kama vile ulivyozungumza wewe Bwana Spika namsamehe. Leo kuna Wabunge watakaopoteza viti vyao kwa sababu Mahakama imewahukumu. Ikiwa kuna jambo lolote ambalo Abdullswamad Sheriff Nas kama Mjumbe wa Mvita alikeuka na kuchukua kandarasi yoyote ya haramu basi naomba afuate njia mwafaka ili jina langu litolewe kuwa sifai kuwa kiongozi. Hivi si vita vya sasa. Vita vinapangwa kwa sababu ya mwaka wa 2022. Lakini Jumba hili halidanganyi. Inajulikana wazi tetesi za mambo ya Poti ni nani aliyozungumzia tangu mambo ya CT2 Privatisation . Ina julikana ni nani alipitisha Mswada huo. Hili Jumba halidanganyi. Inajulikana ni nani aliyehakikisha kuwa Waziri aliregea nyuma kauli yake ya kwanza kuhusu mambo ya Standard Gauge Railway (SGR). Hili Jumba halidanganyi kuhusu yale yote tuliwafanyia wafanyi kazi wa Poti. Inajulikana wazi ni nani aliyewatetea. Siku zote hizo nilikuwa sijapewa kandarasi. Lakini mnasema nimepewa kandarasi kwa sababu sitaki kukubaliana na mambo ambayo ni ya upotofu wa sheria na naona wazi kuwa njia unayokwenda wewe ni njia ya kutanga tanga kisiasa. Nitaendelea kuhudumia watu wangu wale wale. Naomba kwa unyenyekevu kuwa uwaambie wengine ambao unaketi nao katika lile gumzo la baraza kuwa mazungumzo yote pale yasife. Wayachukue wayapeleke katika Mahakama. Hiyo ndiyo njia mwafaka na kisa sawa cha kusema kuwa Abdullswamad Sheriff Nas hafai. Historia na rekodi inaonyesha wazi msimamo wangu uko vipi. Leo wengine wanasema ni kwa sababu ya Baba ndio nakataa. Siku zote nilipokuwa ninapinga mbona sikuambiwa kuwa Baba alinikataza? Vile wamemtaja maheremu baba yangu nitamalizia na kauli yake. Wapende wasipende tutaifanyakazi hii vile inavyotakikana. : Basi tutie kikomo hapo . Tutilie kikomo hapo hayo eno .

Mhe. Spika kwa hadhi na taadhimu kuu Kiongozi wa Walio Wengi anasoma badala ya kujadila Hoja hii. Nafikiri hiyo sio sawa.
Mhe. Spika kwa heshima na taadhima kwa sababu kiongozi wangu amenitaja kwa jina hapa ningependa tu kumweleza kwamba sina haja na nafasi yake. Ukiona niko na "Baba" ujue mapenzi yetu yalitoka kabla ya wewe. Na ule msimamo wetu ni kabla ya wewe. Haya mengine tutayatatua yatakavyokuja. Mimi ningeomba uwaachie wengine waingize jina la "Baba". Wewe uko hapa kuhakikisha kwamba unalitetea sio kuliingiza. Ahsante sana.
Mhe. Spika kwa niaba yangu na familia natoa rambirambi zangu kwa familia ya hayati Mzee Rais Daniel arap Moi. Niliwahi kutumikia Bunge hili kwa miaka 10 akiwa rais wa Jamhuri ya Kenya. Wakati huo eneo langu lilikuwa linaitwa Ntonyiri. Tulifanikiwa kwa kujengewa barabara ya Maili Tatu-Lare-Mutuati na nyingine kutoka Meru National Park. Kwa hiyo natoa shukrani nyingi. Watu wanaomboleza kwa dhati kifo cha Mzee Rais Moi. Asante.
Mhe. Spika leo ni siku ya furaha kwa hakika. Kwa heshima na taadhima kubwa nachukua fursa hii kushukuru uongozi wa Nyumba haswa akiwemo wewe Katibu wa Kudumu wa Bunge na wafanyikazi wa Bunge kwa sababu leo wametupa tunu wametupa zawadi wametupa kitabu ambacho kwa mtazamo wa juu ukiangalia watu watasema ni kitabu tu kama vitabu vingine. Lakini ili tutambue maana halisi ya kanuni za Bunge hili Kifungu cha Saba cha Katiba na Kipengele 77 cha Kanuni za Bunge zinatambua Kiswahili kama lugha rasmi na lugha ya kitaifa katika nchi ya Kenya. Wengine tumeanza msafara mbali. Miaka 16 leo utakapokwenda kwa kumbukumbu za Bunge la Taifa utapata ni barua ngapi nimeandika ni siku ngapi nimesimama ndani ya Nyumba nikidai na kuomba lini tutapata Kanuni. Kwa nini tunaomba Kanuni. Kwa uchache nikiguzia tu Mau Mau walisema Mzungu aende Ulaya Mwafrika apate Uhuru uhuru wetu utabaki kamili lini wakati tunatumia lugha ya kigeni?
Mhe. Spika Mbunge wa kule Migori ni mtu wa matata. Naomba unilinde kutokana naye ili niweze kuongea Kiswahili sanifu kwa vile leo nimepewa Kamusi na ndugu Naibu Spika na Mwenye Kiti wa Kamati ambaye inawakilisha wanakamati wengine Bungeni. Mhe. Spika ni furaha yangu na ninaamini kwamba pia ni furaha yetu sote kama viongozi kuona wananchi wakishiriki katika mjadala wa uongozi. Huu ndio uwezo na uwajibikaji wetu tukiwa wananchi wazalendo na viongozi.Vile vile hii itasaidia kustawisha Jumuia ya Afrika Mashariki na Afrika nzima. Kiswahili ni kiungo cha kuwaunganisha Wakenya Wafrika na mataifa mengine ulimwengu kote.
Mhe. Spika Mbunge wa Suna hakusoma Kanuni ya 80 vilivyo na kikamilifu. Kanuni ya 80 Ibara ya (2) inasema kwamba Spika wa Bunge mara kwa mara kulingana na jinsi ambayo hoja iko - na kwa vile leo ni siku ya kwanza - anaweza kukubali. Nikimsomea inasema "Spika anaweza kumruhusu Mbunge kusoma Mchango ikiwa Spika ameridhika kwamba kufanya hivyo ni muhimu katika kufafanua jambo." Kwa hivyo namuomba Mbunge wa Suna aridhike kwa sababu anafanya ubaguzi. Naibu wa Spika pia alisoma. Niacheni nimalize tafadhalini!
Mhe. Spika Mhe. Amina alikuwa anasema kuwa ninawatisha Wabunge. Naomba nirudie yale niliyoyasema hapo jana. Ninarudia Mhe. Amina na si kwa ubaya vile ulivyokuwa umesisitiza kuwa tusitishie Wabunge. Theluthi theini kulingana na stakabadhi na vile tunavyoelewa wengine wenu hamtarudi hapa. Kwa hivyo tafadhali wakati umefika
Mhe. Spika mimi naunga mkono maombi ya Meja Mstaafu. Natumai kwamba Kamati itakapoangalia masuala haya muhimu ambayo yamegusiwa Wakenya watapata changamoto ili waendelee kupanda miti katika mashamba yao. Hii ni kwa sababu hakuna haja Mkenya kukosa makao kama kuna mahali pamoja ambapo msitu uko wa ekari nyingi zaidi. Inafaa tuangalie vile tunaweza kuwasaidia Wakenya watumie yale mashamba pasipo kuingilia na kuchafua mazingira. Kwa hivyo naunga mkono maombi haya. Asante Mhe.Spika.
Mhe. Spika mimi ni Mheshimiwa aliyeshindwa mara saba na ya nane akachaguliwa kuja hapa ndani. Natoa shukrani kubwa sana kwa wewe kupata hicho kiti. Najua wewe ni kiongozi ambaye atatuongoza tukiwa pamoja. Natoa pia shukrani kwa Mwenyezi Mungu kunileta hapa na watu wa Tigania Mashariki. Pia nimekutana na ndugu yangu Mhe. Kabando wa Kabando tuliyekuwa naye 1992 na Mhe. Chris Bichage ambaye pia tulikuwa naye tukipigania haki. Kutoka wakati huo sijawahi kupumzika hadi sasa niko Bunge. Kwa hivyo nasema ahsante kwa Mwenyezi Mungu na kwa watu wa Tigania Mashariki kwa kunileta Bungeni. Hotuba ya Rais ilikuwa nzuri sana. Sisi watu wa Upinzani wa chama cha ODM hatufai kuwa tunapingana na kila kitu. Saa zingine tuseme kingine ni kizuri. Hotuba ya Rais aliyoisoma katika Bunge hili ilikuwa nzuri sana. Ukiingia Tigania Mashariki kuna mahali panaitwa Amgaa Ngutu na Kunati. Ukiingia zaidi magharibi sehemu ya Ndia barabara imekatika na hakuna daraja. Zile shule ambazo zitapelekewa laptops mahali pengine watoto wanasomea chini ya miti. Hivi sasa ukimpelekea mtoto laptop akiwa chini ya mti na mvua inyeshe laptop hiyo itaharibika. Kwanza tunataka shule zijengwe halafu laptops zifuate. Katika sehemu ya Tigania Mashariki hakuna hospitali ilihali inapakana na Igembe ya Kati na Igembe Kusini. Watu wa Tigania Kusini wa kutoka upande wa Ngutu na wale wanaotoka Kunati wana hospitali. Lakini sisi hatuna chochote. Inaonekana ni mahali hapawezi kupata uhuru lakini kwa sababu Mhe. Kenyatta amepata Serikali na watu wa Tigania Mashariki walimpigia kura na kunipigia mimi ni lazima afike kule aone wale ni wazalendo Waafrika awapiganie. Hawa ni wazalendo wa Afrika ambao walipigania uhuru na wakapata. Ningependa kuzungumzia masuala yanayohusu kahawa. Eneo letu la Tigania Mashariki lilikuwa nambari moja katika kilimo cha kahawa. Lakini kahawa iliharibiwa na ikachafuka. Wakulima wa eneo la Tigania Mashariki walingoa kahawa wakapanda miraa . Naomba Serikali inayoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta na Bw. Ruto - kwa sababu wako pamoja - waunganishe watu wa Tigania Mashariki ili waweze kupanda kahawa. Kahawa ilisaidia sana kuimarisha elimu katika eneo la Tigania Mashariki. Mhe. Spika Jumapili nilitembea katika Mkoa wa Kati na rafiki yangu mmoja hapa ambaye sitaki kumtaja. Tulienda kanisani na yeye na akaniuliza: Mhe. Aburi nitatoa nini? Na mimi nikamuuliza: Kwa nini unaniuliza hivyo? Akajibu: Mshahara
Mhe. Spika mimi ni mwanachama wa Kamati ya Uchukuzi na Ujenzi na Makazi. Jana tulikuwa na kikao na Waziri anayehusika na masuala hayo. Kilichoibukwa kwenye kikao hicho ni kwamba hakuna sheria inayomuruhusu kuchukua pesa za barabara na kuzipeleka kwa serekiali za kaunti. Kwa hivyo kama Kamati tuliketi na kulizungumzia jambo hilo. Waziri aliomba muda. Kufikia Jumatatu ijayo ataleta jawabu lakini hakikisho ni kwamba ni kinyume cha sheria kupeleka pesa za barabara kwa magavana mpaka Bunge litakapobatilisha sheria iliyopo. Sheria ya Roads Levy Fund bado inatumika. Hadi sheria hiyo itakapobatilishwa ni lazima pesa za barabara ziende kwa maeneo Bunge. Ahsante mhe. Spika.
Mhe. Spika muongozo utatoka kwako tu Spika mwenyewe. Wale Wabunge tutakuwa chini hapa itakuwa ni kufuata amri. Kwa hivyo ndugu yetu ambaye ni msemaji sana kwa lugha ya Kiswahili angojee. Hapa ilikuwa ni practise kwa wale ambao. Ni mazoezi kwa wale kama K'Oyoo ambao hawaelewi Kiswahili vizuri. Nikimalizia ni shukrani sana kwa Wabunge ambao wamechangia na wale pia wameketi hapa kusikiza. Sio kawaida Wabunge kukaa na kufuatilia Hoja mpaka dakika kama hii. Nashukuru afisi ya Spika. Pia nashukuru afisi ya Karani wetu wa Bunge. Kazi ambayo wameiweka hapa ni ya maana sana. Naomba kuhitimisha. Asante sana Mhe. Spika.
Mhe. Spika mwisho kuna mzozo kati ya NCPB na Erad mbele ya Bunge la Kenya na Bunge haliwezi kuangalia sehemu moja. Mahakama inaangalia haki ya Erad na NCPB. Lakini hapa tunapewa mwongozo. Jiulize swali moja. Kampuni ambazo zimeletwa mbele yetu ni saba. Hizi kampuni zingine ni za nani? Tumeambiwa Erad ni ya nani kwa sababu wenyewe wametajwa. Mahindi yaliyoletwa ni metric tonne 70000 na LC imetiwa sahihi. Saa hii hatutaki kusema kwamba tunaweka hii chini. Tunambiwa shetani mkubwa ni Erad. Bunge lina haki kuangalia haki ya kila Mkenya. Wajibu wa kuangalia haki ya Erad na NCPB ni wa mahakama na si Bunge. PIC isitufanye sisi hapa kuwa korti ndogo. Kwa hayo nasimama kupinga mapendekezo haya.
Mhe. Spika nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu. Nakushukuru wewe pia. Natoa kongole kwako na kwa naibu wako. Lakini kwa vile uko hapo leo wacha niseme kongole kwako kwanza. Mhe.Spika nachukua fursa hii kumpongeza Mhe. Koinange kwa kufikiria na kulete Hoja kama hii. Lakini mimi nina tatizo na Hoja hii vile ilivyoandikwa. Ni muhimu kuanzisha matibabu ya dharura kwa Wakenya hasa wale wanaotoka katika sehemu kame katika nchi hii. Lakini matibabu ya dharura yanaambatana na vitu viwili. Moja ni uchukuzi. Kuna uchukuzi wa ubinafsi na uchukuzi wa umma. Uchukuzi wa umma unaopatikana katika matibabu ya dharura ni ambulensi zinazotolewa naSerikali. Hizo ambulensi hupati bure. Mpaka uzilipie.Utaangalia uchukuzi wa umma na uchukue teksi. Kwa sababu ni haki ya kikatiba tutasema Beba mgonjwa hapa upeleke hospitali bure kwa sababu ni haki ya kikatiba? Hayo yanawezekana? Hayawezekani. Haki ya kikatiba siyo tukio la siku moja. Haki ya Katiba ni mchakato. Ni lazima tupige hatua ake kuna haki nyingi katika Katiba yetu. Hatuwezi kuamka kesho asuhuhi na sote tupige laini tuseme: Twataka haki zetu! Haiwezekani. Sisi kama viongozi ni lazima tuwaeleze Wakenya ukweli. Yale yanayowezekana yatekelezwe kwa mipangilio. Hoja hii inakosa nini Mhe.Spika? Miaka 50 ya Uhuru nikizungumzia sehemu ninayowakilisha Bungeni ya Bura ambayo ina eneo la kilomita 16000 mraba kuna hospitali moja tu.Ukienda kwa hiyo hospitali utapata dawa aina tatu kila siku nazo ni panadol asprin na ORS. Hauwezi ukayapata madawa mengine. Tuliunda CDF na tukajenga zaidi ya hospitali kumi. Wacha hata dawa kupata daktari hata leo ni ndoto. Zimebaki tupu na zinaishi popo. Sasa tutakapokuja na fikra zakusema tutoe huduma za dharura bure ikiwa tumeshindwa kwanza na zile hospitali ziko je tunazungumza ukweli? Utekelezaji wake uko? Ningemuomba aliyeileta Hoja hii- -- Mhe. Spika hiki kidude nikama kimeletwa kutoka Korea. Mtu mrefu kama mimi ni lazima ainame sana. Sijui warefu kama mimi tutapata fursa vipi tupate vyombo ambavyo vitatoa sauti yetu bila kuinama. Nikirudi kwa Hoja kinachokosekana ni bima ya kitaifa. Bima ambayo kila Mkenya popote alipo akiwa mashambani au mji mkuu ataipata. Serikali itakapotoa bima hiyo itatoa kwa uchukuzi na matibabu. Lakini hivi hivi hoja hii haiwezi ikatekelezwa. Ndiyo ni ya kimsingi na ni ya haki ya kikatiba lakini haki hiyo haina mbinu ya vile tutaitekeleza. Kwa hayo machache nasikitika kuipinga. Ahsante.
Mhe. Spika nadhani kila Mbunge amesikia. Hii Hoja itasaidia Wakenya kwa ujumla maanake watu husafiri kutoka maeneo mbalimbali. Tukiangalia hali ya mfuko kwa kila mtu kwa kweli haiendi sambamba. Kifungu 43 cha Katiba kinaambatana pia na kile cha ugatuzi. Kinasema kwamba ikiwezekana hela izidi kusukumwa kwa wingi kule mashinani. Najua kuna changamoto maanake ugatuzi ulianza juzi. Wakipelekewa pesa kwa wingi nafahamu kaunti zetu zitatatua hili tatizo la magonjwa. Vile vile kupata dawa limekuwa tatizo katika hospitali ya Serikali. Hii Hoja ikitekelezwa najua itapunguza taabu kwa wingi. Kwa sababu wenzangu wameongea sana na nikiongea nitakuwa narejelea yale natoa shukrani kwa kunipa hii fursa. Asante sana Mhe. Spika wa Muda.
Mhe. Spika nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Kwa niaba ya watu wa Kipkelion Mashariki na Kericho County nzima nachukua fursa hii kusema pole sana kwa familia ya Mzee Moi. Mzee Moi alijulikana sana kwa mambo mengi ya maendeleo. Pia alikua mtu wa kuchunga saa. Alitufunza kuchunga masaa. Hakuna wakati alichelewa kwenda kanisa. Kwa niaba ya Wakenya wote tunasema poleni sana. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Asante sana.
Mhe. Spika nakushukuru kwa kunipatia nafasi hii. Ni heshima kubwa. Bunge la 12 litakumbukwa na Wakenya kwa kuidhinisha Kiswahili. Najua wengi wetu tunaogopa kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili kwa sababu ya kuathiriwa na lugha ya mama. Ninaunga mkono Mheshimiwa kutoka Ruiru aliyesema kuwa itakuwa vizuri tukitenga siku moja ili tuzungumze kwa lugha ya Kiswahili ili tupate mazoea ya kuizungumza. Tunajua kwamba tunaruhusiwa kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili wakati wowote lakini tukijua siku kama ya leo tunafaa kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili wengi wetu watajitahidi na tukienda pale nje tutazungumza Kiswahili sanifu. Kwa sasa ninasema hongera Bw. Spika na tuendelee kutukuza Kiswahili.
Mhe. Spika nakushukuru kwa muda ambao umenipatia niwasiliane na wenzangu katika Ukumbi huu. Kama Mhe. Duale haelewi Kiswahili basi niko radhi nimpatie masomo ya bure wala sitamlipisha chochote.
Mhe. Spika nakushukuru. Ningependa kulifahamisha Bunge hili kwamba hatuongei kama watu wa CORD wala sisi hatuna ukabila tunawawakilisha Wakenya. Tukiona sehemu ambazo tunazotoka haziangaliwi na tumepewa ahadi na Makamu wa Rais kuwa baada ya kura hakuna tena mambo ya CORD wala Jubilee ni lazima tuongee.
Mhe. Spika namuomba Mheshimiwa mwenzangu aweze kufuatilia yale ambayo yanazungumziwa Bungeni. Ripoti ambayo anadai kwamba Kamati yangu haijaweza kuifanya tayari tumeiwasilisha katika Meza ya Bunge hili.
Mhe. Spika naomba nitoe mchango wangu kuhusu Hoja hii. Kitu cha kwanza hata huenda ikawa wengi wa Wabunge ambao wako hapa walisoma kupitia michango ya harambee. Ninajua kwamba ndugu yangu Chris Wamalwa alisomeshwa kwa Harambee. Hata ndani ya hili Bunge leo tuna wageni ambao ni wanafunzi. Nimewaona huko juu kwa gallery ; wengi wao wanasomeshwa na fedha za Harambee. Wabunge wamejitoa muhanga ili kusomesha ndugu zao watoto wa dada zao ama kaka zao. Kwa hivyo kusema kuwa kuweko kwa Harambee kunaua ule moyo wa kutoa wa wananchi wetu si sawa; ninakubaliana na msemaji wa hapo awali. Alisema hata juu ya kichwa chako kuna neno "Harambee". Sisi ni nani tuanze kusema hatutaki Harambee? Ningeomba niisome hiyo barua kwa kina na niielewe. Inasema tusitoe Harambee ama tusiombe pesa za kutoa katika Harambee? Vile nimeielewa anaomba tusiende kutafuta hela huko nje za kutoa kwenye michango; lakini kama mimi binafsi nina hela zangu nina nia ya kumsaidia mtu fulani nani hapa nchini anaweza kunizuia kumsaidia mtu fulani? Hata Jumapili ijayo Rais atakuwa katika sehemu yangu ya uwakilishi Bungeni na atakuwa anachangisha pesa. Mnataka kuniambia nisiende nikachangie shule? Mimi naye tutapelekwa kortini? Kama vile mwenzangu amesema ni kweli kuwa hiyo barua ina ubaguzi. Imelenga Wabunge peke yao; imeacha watu wengine. Naomba tuangalie hilo jambo vizuri; ikiwa Wabunge wamejitolea kutoa mchango wao kusaidia wagonjwa shule na kadhalika wasiwekewe vikwazo na mtu yeyote. Naomba ndugu yetu wakati huu aanze kufikiria mwenzake. Alianza kuzozana na Wabunge katika Bunge la Kumi na kilichompata kilikuwa ni kuondolewa kutoka kazi yake. Singependa twende njia hiyo; inafaa tuwe na tahadhari.
Mhe. Spika nashukuru kupata nafasi hii kutoa wasia wangu wakati nakunja jamvi kuagana na wenzangu - kuhusu Ripoti hii na kuhusu Bunge la Afrika mashariki. Si sahihi kwa hii Ripoti kunakili katika ukurasa wa 17 kuwa Chama cha ODM kilipeana majina matano. Mimi mwenyewe ndiye nilipeleka haya majina. Majina yalikuwa ne. Kwa hivyo hii Ripoti imechangia kwa undani sana kuleta mambo ambayo hayakuweko. Nashangaa kwa nini kama tuna wafanyikazi ambao wanatakiwa kunakili kwa ufasaha yale ambayo yametokea kuletea Bunge maandishi ambayo si sahihi. Kipengele cha 6(a)(i) kinasema kuwa kila chama kiko na nafasi ya kuleta watu ambao wamepatiwa. Hivi sasa tunataka tukigeuze ili tutimize matakwa ya wenzetu. Huwezi kugeuza sheria ili kutimiza yale unataka. Wazungu wanasema: " The law cannot be applied retrospectively." Mheshimiwa Spika ni wasia wangu tusikimbizane na muda. Kama itabidi basi tungoje Hoja hii ipitishwe na Bunge la kumi na mbili. Hatuwezi kuketi hapa kusema eti lazima chama kilete majina kadha wa kadha. Nakubalina na Bunge jinsi ilivyopitisha jambo hili kwa kauli moja. Kwa minajili hiyo chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kimeleta majina matatu nacho chama cha Wiper jina moja kwa mujibu wa sheria. Sudan Kusini nayo imekumbwa na tatizo ikabidi iende mahakai. Nakubali kwamba nasi pia tumechangia vilivyo kukwama kwa shughuli katika Bunge la Afrika Mashariki. Ingawa hivyo iwapo tungekuwa na nia moja sisi sote basi hili janga halingetupata. Kilichopo ni kwamba sote tuliangalia sheria tofauti tofauti tukazinakili tofauti tofuati. Chama cha Jubilee kikaleta majina kulingana na vile kilivyofikiria. Chama cha CORD nacho kikaleta majina jinsi kilivyotafi hiyo sheria. Ndiyo maana Mheshimiwa ole Metito anapendekeza kwamba tugeuze hicho kipengele ili kusiwe na tafi mbali mbali za hiyo sheria. Lakini huwezi kugeuza hiyo sheria sasa hivi kwa sababu ya haya majina tuliyoorodhesha! Hali ilivyo sitakuwa kwenye Bunge la kumi na mbili. Laiti ningekuwepo.
Mhe. Spika nashukuru kwa kunipatia nafasi ya kuchangia Mswada huu ambao umechukua muda. Hata hivyo tungependa kulishukuru Bunge la Seneti kwa kuuleta kwa wakati unaofaa. Nazishukuru bunge za kaunti kwa sababu miaka hii matatu zimekuwa zikifanya kazi bila mwongozo wala mwelekeo. Wamejaribu sana. Hatungependa kuwalaumu sana kwa sababu walianza juzi juzi. Hatuwezi kuzilingalisha bunge za kaunti na Bunge la Kitaifa maana hili limekaa miaka mingi. Nawashukuru wawakilishi wa kaunti kwa bidii ambayo wamefanya ili kufikisha serikali za kaunti mahali zimefika. Jambo la kwanza ambalo ningependa kuzungumzia ni Mswada huu unatusaidia kuwapa wawakilishi wa kaunti majukumu ili wajue jinsi wanavyoweza kufanya kazi yao wakiwa na mwongozo wa kisheria na pia wakiwa na uwezo na mamlaka waliyopewa kisheria ili mtu yeyote atakayepinga uteuzi huo aweze kusimama katika sheria waliyopewa. Bunge za kaunti zinahitaji mwongozo huu ili wanapoteua watu katika nyadhifa mbalimbali wafuate mpangilio uliowekwa kisheria na mtu yeyote atakayepinga ataweza kwenda kortini na kutumia sheria hii kujipatia mamlaka. Kuna mambo ambayo ningependa kuchangia kwa ufupi. Jambo la kwanza ni kuhusu kuwajulisha wateuliwa wakati wa mchujo. Watu wengi wanaopata mwaliko kwenda mbele ya kamati za bunge la kaunti hawajui wakati wanaostahili kufika mahali pale. Lazima watu hao wajulishwe kupitia magazeti ya kitaifa ambayo yanasambazwa nchi nzima ili wajue ni lini wanatakikana kwenda mbele ya kamati za bunge la kaunti. Pia wanapaswa kujulishwa kuhusu vitu ambavyo wanapaswa kuwa navyo wakati wa mchujo. Wakati mwingine mteuliwa anaenda pale bila kubeba vitu vyote anavyostahili kuwa navyo kwa sababu hajajulishwa mapema kuhusu vitu anavyofaa kubeba. Ili kuwasilisha habari hizi bunge za kaunti zinaweza kuandika barua pepe au kumpigia simu. Pia wanaweza kumwandikia barua ili kama mtu huyo hayuko katika sehemu yenye mtandao wa rununu au redio aweze kupata habari kupitia kwa watu wengine. Tumeona kaunti nyingi zikipoteza watu ambao wanastahili kwenda kwa mchujo kwa sababu njia za kupeana habari au za kuwafikia ni ngumu. Jambo lingine ambalo Mswada huu umetusaidia ni kuupa umma nafasi ya kuwakagua wateuliwa. Umma ndio unawajua watu kuliko maandishi. Mswada huu umeupatia umma nafasi ya kukagua watu na kupeana nafasi kwa mtu yeyote kutoa sababu za kueleza kwa nini mtu hafai kuteuliwa. Tukifanya hivi tutapata watu ambao wanaheshimika ambao wana sifa nzuri na ambao wanakubalika. Hata wanapopewa kazi umma utasema ulichangia. Wakati huu ambao tuko habari hizi lazima zifikie umma kwa njia ya magazeti ya kitaifa ili wajue wakati wanaoweza kwenda. Wakati umma unamkagua mtu lazima pia upeane ushahidi wa ukweli kwa sababu tusipowalinda wateuliwa na kuachia umma nafasi ya kuwakagua bila ukweli au ushahidi kamili tutapoteza watu wengi kwa njia isiyo bora. Kwa mfano kama nilikosana na wewe au nilikushinda mahali fulani utatumia njia hiyo ya kunipinga na kupeleka habari za uongo kwamba mimi ni mbaya. Kwa hivyo ni lazima pia tuweke sheria kwamba shahidi yeyote ambaye anaenda kuwakilisha umma lazima awe na ushahidi wa ukweli na kama hatapeana ushahidi wa ukweli basi sheria imchukulie hatua ili tupunguze mashahidi ambao wanatoa mambo ya uongo kuhusu mtu aliyeteuliwa. Ni vizuri tuwalinde walioteuliwa kwa sababu tukiuacha umma upeane ushahidi wa uongo tutakuwa tunawapoteza wateuliwa wazuri. Mambo ambayo yanatumika kuwateuwa watu lazima pia yawekwe hadharani. Kwa mfano kama wateuliwa ni wengi ni kitu gani kilichowafanya wateuliwe? Lazima waseme ili mtu yeyote akiwa na pingamizi aonyeshe kwamba mtu huyo alikuwa na uwezo kuwashinda wengine. Mtu anaweza kuwashinda wenzake kikatiba kama vile kutumia kitengo cha jinsia hata kama hana kisomo cha juu. Kwa hivyo ningependa jambo hilo lisaidie katika mwongozo wa kuwachagua wafanyikazi. Jambo lingine ni kuhusu wakati wa kupeana ripoti kuhusu mteuliwa. Inachukua muda kwa mteuliwa kujua kwamba amekubalika. Huenda ameteuliwa kwa wadhifa fulani lakini hajapata ripoti. Utapata mtu ameteuliwa lakini yule mwingine hajaambiwa kwamba hakufaulu katika mchujo. Ni vizuri pia kwa wale ambao hawakubahatika kuteuliwa waambiwe sababu ambazo ziliwafanya wasiteuliwe na kamati ya bunge la kaunti. Akiambiwa sababu ya kuteuliwa kwake mtu ataridhika. Sisi sote tunahitaji kuambiwa sababu ya kutoteuliwa kwa mtu Fulani. I lazima mtu aridhike ya kwamba hakuteuliwa kwa sababu ya jambo moja au lingine. Jambo lingine ni lile la kukataliwa kwa wateuliwa. Mswada huu unatusaidia kusema kuwa mtu yeyote ambaye anakataliwa ni sharti apewe sababu ya kukataliwa. Nikimalizia tunafaa kuchunga Bunge la Seneti wasichanganye wateuliwa. Kuna watu ambao wameajiriwa na lazima waendelee kufanya kazi katika kaunti. Kuna watu ambao waliajiriwa kwa muda fulani lakini kuna sheria ambayo Seneti inataka kuleta kusema kuwa baada ya miaka mitano tunaondoa walioajiriwa na gavana fulani. Tukifanya hivyo itakuwa siasa tutaharibu rasilimali ya Serikali tupoteze wakati na uwajibikaji hautapatikana. Lazima tujue kuwa magavana wamepewa mamlaka na Katiba.
Mhe. Spika nashukuru kwa nafasi hii umenipatia nitoe mchango wangu kulingana na Ripoti hii ambayo tumepatiwa ili kueleza mwelekeo wa makadirio ambayo yatakuja mwaka wa 2016. Mwelekeo huu umepeanwa na Kamati ya Ratiba ambayo imeongozwa na Naibu Spika Mhe. Laboso. La kushangaza ni kuwa wenyeviti wa Kamati hizi hivi wangekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wanachangia kikamilifu kutetea Ripoti hii ili nasi tuwaunge mkono. Wakati mwingine mambo kama haya yanafadhaisha kwani ingekuwa bora zaidi wao wawe kipau mbele. Naomba niwapongeze kwa kazi hii njema ambayo wameifanya. Wakati mwingine jambo linaweza kutokea na ukaliona labda si la faida lakini labda ile shida iliyotokea na Kamati ya Bajeti na Makadirio ambayo ilitufanya twende kwenye hii Kamati ya Ratiba naona matunda yake. Huenda ikawa Mungu alituongoza mambo kama haya yatokee ili tupate matunda haya. Nina ii tutafikia kiwango tunachotarajia kufika. Mhe. Spika nina machache ambayo ningependa niangazie nikianza na Jopo la Ardhi. Jopo hili la Ardhi limepewa majukumu ya kuhakikisha kuwa kesi zote ambazo bado hazijakamilishwa zimekamilishwa na vipande vya ardhi ambavyo vina utata vimeratibiwa. Zaidi ya hivyo tunafaa kuhakikisha kuwa majukumu ya Jopo hili yametimizwa kabla muda wao haujaisha. Nashukuru Kamati ya Ardhi kwa kuondoa yale mapendekezo ambayo walikuwa nayo ya kubadilisha fedha ambazo zilikuwa zimepatiwa kitengo hiki kwa sababu imebainika wazi kuwa mara nyingi kitengo hiki kinanyimwa fedha ndio maana kinashindwa kutekeleza wajibu wake. Vile Mhe. Amina amesema alivyokuwa akichangia naomba nimuunge mkono kwa dhati alivyosema kuwa katika nchi hii ya Kenya madini yameanza kuleta faida na kuchangia katika kuzalisha fedha ambazo zinahitajika nchini. Lakini ni vizuri tuangalie fedha ambazo Wizara zinazohusika na madini zinapewa. Wakati mwingine waliomba shilingi bilioni nne na wakapewa chini ya bilioni moja. Wakati huu tunaomba angalau wapewe bilioni mbili lakini pia hilo linaleta shida. Wakati umefika nchi hii ijue rasilimali yake ambayo iko chini ya ardhi. Ukiuliza Mkenya kiasi cha madini ambacho kipo chini ya ardhi hawezi kusema kwa sababu vifaa ambavyo vinahitajika kutupatia utaratibu wa kujua kiasi cha mali chini ya ardhi havijanunuliwa. Nchi hii inaelekea wapi? Iwapo tunajua tuna rasilimali na madini kwa nini tungojee watu watoke nje waje na vifaa vyao na kupima na kujua kiasi cha madini chini ya ardhi na waanze kuyachimbua wakati nchi imenyamaza? Wakati umefika tuhakikishe kuwa vitengo ambavyo vinaweza kuzalisha fedha nchi hii vimepewa pesa ya kutosha. Madini yapatiwe vifaa ambavyo vinafaa kupewa watu ambao wanavihitaji na upimaji uwe ni wa kutosha. Kila mtu ambaye anataka kuingia katika sekta hii ya madini apewe nafasi ili kutoa mchango wake wa kuzalisha mali. Ningependa kuongea kuhusu suala la maji. Kama tunavyojua wakati wa ugatuzi sekta ya maji imegatuliwa lakini tuna Wizara ya Maji. Vile tujuavyo katika Bunge la Kumi tulichukua mkopo kutoka China wa kutengeneza bomba la pili kutoka Mzima kuenda Mombasa. Nini imefanyika na hizo fedha? Wenzangu ambao tulikuwa nao katika Bunge la Kumi tukipitisha huo mkopo na sote tulikuwa hapa wakati huo Waziri alikuwa Mhe. Charity Ngilu. Alikuja hapa akatueleza wazi wazi kuwa fedha hizo za kwanza zingetumiwa kurekebisha bomba na katika awamu ya pili ya kuleta bomba la pili kutoka Mzima kwenda Mombasa watu wa Taita ambao wako hapo katikati wawe na maji ya kutosha. Watu wa Voi Mbololo Kishushe na Mwakitau wawe na maji ya kutosha. Nini kimetokea? Fedha hizo zijui nazo pia zimeingia katika lile kapu ambalo tunalijua siku hizi la kuingia lakini kutoka ni shida. Mhe. Spika naomba wakati utaratibu utakuwa umeanza wa kuhakikisha kuwa makadirio ya fedha za mwaka 2016/2017 tuambiwe fedha hizo ziko wapi na tuambiwe zimefanya nini na kwa nini hazijatumiwa. Jambo lingine ambalo ningependa kuangazia ambalo limezungumziwa na wenzangu ni kuhusu fedha za wazee. Wazee wamelalamika. Tunasema tunaongeza hizi fedha lakini nikiangalia hapa hazijaongezwa. Zimebanwa. Tunasema kuwa zitakuja kuongezwa mwaka mwingine. Ni nini kimetokea na hawa wazee wetu bado nao wamejitoa mhanga kuhakikisha kuwa taifa linakuwa? Wamejibidiisha vile wawezavyo kushikilia taifa lakini tukifika wakati wa kuhakikisha wamepata kitu angalau kabla maisha yao hayajafika kikomo tunawanyima fedha. Ni ombi langu kuwa wakati makadirio yatakuwa yamefikishwa hapa fedha ambazo zinahitajika ziwekwa ndani sawa sawa. Fedha za walimu zimewekwa kama fedheha. Kila mtu amepiga kelele kuhusu walimu. Wakati umefika katika nchi hii tuangalie haya makadirio kuwa yamewekwa sawa sawa na walimu wamepewa haki yao. Nimekubaliana na wewe. Umesema kuwa katika orodha yetu ya leo Orodha No.13 tunatakiwa tuangalie sheria hii ambayo inatupatia viwango na vipimo ambavyo hatuwezi kupitisha.
Mhe. Spika nashukuru wenzangu leo wamemuweka sahihi huyu ndugu na rafiki yangu mkubwa wa upande wa walio wengi. Lakini huenda ikawa alikuwa amefikiria Mhe. Benjamin amehama chama chao. Kwa hivyo anaweza kuchukua mamlaka yake. Kwa hivyo nashukuru Mhe. Benjamin Langat amekuja akasema wazi kuwa bado yuko na anaendelea. Wakati umefika wa kuambiana ukweli na ukweli ujitoe wazi. Tukiwa tunaleta mabadiliko katika Hoja yoyote Bungeni hasa ambayo inahusu fedha ni lazima na ni muhimu vipengele vyote vya sheria vifuatwe. Kama tutakaa hapa na watu watumie mamlaka ambayo hawana na yakubalike kuwa sheria ipitishwe kiholela tutakuwa tumehujumu nchi yetu na tutaepuka mamlaka tuliyopewa na wananchi. Nikimalizia nasema hivi: Wakati huu tufuate sheria vile ilivyo. Kama Waziri ambaye anahusika na mambo na fedha hakuhusishwa kulingana na sheria tunaomba ahusishwe kikamilifu na iletwe tena na ijadiliwe vile inavyotakikana. Wale ambao wamejitwika mzigo wa kubeba mamlaka ambayo si yao wakome. Tuelezane wazi wazi. Kwa haya machache kama ujuavyo hivi nakunja jamvi langu. Labda haya yatakuwa mazungumzo yangu ya mwisho mbele ya Wabunge wenzangu. Naomba Bunge liendelee kuheshimu Katiba na sheria zake. Ahsante.
Mhe. Spika nasimama kuunga mkono Hoja hii ya Bunge kuridhia kwamba Kanuni za Kudumu zitafiwe kutoka Kiingereza hadi Kiswahili. Jambo la pili ni kwamba nilikuwa nimekosea hapo mbeleni. Nilisema kwamba kurefer ni kuchungulia. Ni kusoma dondoo. Nimegundua saa hii. Nilikuwa nimesema kurefer ni kuchungulia. Kumbe kuchungulia ni mambo mengine. Sasa ni kusoma dondoo. Kurejelea ni kurudia. Mimi siwezi kuongea zaidi ya dakika mbili. Sitaki kukudanganya. Kiswahili changu hakiwezi kupita dakika mbili. Siwezi kukuambia ati nitaongea dakika tano. Nitakuwa nakudanganya. Nitaongea dakika mbili peke yake. Jambo la kwanza ni kushukuru Bunge kwa kutafi Kanuni hizi kwa Kiswahili. Namshukuru pia Naibu Spika. Neno "Spika" ni la Kiingereza. Nimewazia jinsi linaweza kugeuzwa kuwa Kiswahili. Sijui kama nitakosea kwa kusema liwe 'Mstahiki Mkurugenzi wa Bunge'. Nataka neno hilo liwekwe kwenye gazeti kama watu watakubali. Naishukuru Bunge kwa sababu hili ni jambo muhimu sana. Kuna wakati nilimsikia Mbunge mwenzangu akisema kuwa kuna wale wanaoongea Kiingereza kingi huko Bunge. Sasa watu waje waongee Kiswahili kingi hapa Bunge. Hakuna haja ya Kiingereza. Lugha hii siyo vile tunavyofikiria. Wakati unapoongea katika matanga ama rally unaongea Kiswahili lakini hujui unasema nini. Kumbe kuongea lugha hii hapa na huko nje ni tofauti. Kuna eno muhimu ambayo lazima uzungumze. Jambo hili limechelewa. Lilifaa lije zai. Unapaswa uangalie vile wanavyozungumza katika Bunge la Tanzania. Hapa Bungeni kuna aina tofauti tofauti za watu. Kuna wasomi wale wamesoma sheria madaktari na wakulima. Sasa wakulima na wezi wa ng'ombe wanaweza kuongea Kiswahili. Naunga mkono Hoja hii. Hili ni jambo la maana sana ambalo limefanyika katika Bunge. Kama vile wenzangu wamesema tuwe tukizunguma Kiswahili siku moja kwa mfano Jumatano asubuhi. Hakuna haja ya wewe kuvurutana na Kiingereza. Naunga mkono Hoja hii. Nimesindikiza Hoja hii vibaya sana.
Mhe. Spika nasimama kuunga mkono Hoja hii. Kama tulivyosikia ni Ripoti inayohusu Kanuni za Kudumu za Kiswahili. Shukrani na heko zangu kwa Kamati ya Utaratibu na Masharti ya Bunge kwa kuleta Hoja hii. Namshukuru Katibu wa Bunge na Jopo lililotayarisha Kanuni hizi. Hii ni hatua muhimu sana.
Mhe. Spika nasimama kwa Hoja ya Nidhamu kwa sababu nilipoingia Bungeni... Afternoon inaitwa nini? Nilipoingia Bungeni alai ya leo nilimpata Mhe. Mjumbe wa Kaunti ya Murang'a akiwa ameketi katika kile kiti changu rasmi. Kwa kuwa ninaheshimu sana viongozi wa kike ndiposa nikaamua nikae kwenye kiti kilicho karibu. Nataka nikujulishe kuwa nimepata chombo ambacho sielewi katika hiki kiti na hakiko katika viti vingine.
Mhe. Spika nataka kurudia mambo ambayo ni muhimu sana kwa sababu ya ile nyumba ambayo kamisheni inatumia. Mimi mwenyewe ndio nilioyaleta yale katika ule mkutano. Kwa hivyo nikiongea naelewa vizuri kwamba yale ninayogusia ni kwa sababu yanamgusa moja kwa moja mwenyekiti wa ile kamati. Nataka nikueleze kwamba mwenyekiti wa ile kamati amehusika kwa njia moja ama nyingine kuhakikisha kwamba wale makamishina Mmoja ni kamishina Keino ambaye aliweza kupatiana ripoti pale kwamba mhe. mwenyekiti wa kamati
Mhe. Spika nataka kwanza mwelekeo kutoka kwako. Mwelekeo ambao nautaka ni kwamba mwenyekiti wa kamati ya Justice and Legal Affairs Mhe Chepkong'a amekuwa hapa Bungeni lakini ameachia makamu wake kuisoma ile Ripoti. Najua kwamba hii inakubalika katika sheria zetu. Mhe Spika nataka nikueleze leo hii kwamba nilipata nafasi nzuri ya kuingia katika ile kamati kama rafiki wa kamati.
Mhe. Spika naungana na wenzangu pia kuhusu Harambee. Kwa kweli Harambee zinasaidia Wakenya ambao hawajiwezi. Hii ni kwa sababu sisi kina mama wa kaunti tunatumia mifuko yetu. Hatuna ndururu katika CDF ama pesa za kaunti; kwa hivyo Harambee ziendelee ndipo kile kidogo tulicho nacho kisaidie wale ambao hawajiwezi. Tuna watoto mayatima; tuna watoto hawajiwezi; tuna watoto wanafukuzwa shuleni. Kwa hivyo nimeungana na wenzangu kusema ni muhimu tuendelee na Harambee. Kwa kweli pesa ambazo zinatoka CDF kama bursary na za kaunti hazitoshi. Hospitali zina wagonjwa na hawana pa kuelekea na ni lazima wawe na Harambee. Tukifunga Harambee hao wagonjwa watasaidikaje? Watoto ambao hawajiwezi wataenda wapi? Kama kuna njia ya kuwa na sheria ya kuwasaidia wasiojiweza Harambeee iondolewe. Ninasema Harambee itaendelea. Kama kuna sheria nyingine wale wasiojiweza pia watafutiwe njia ya kujisaidia. Kuna mambo mengi. Kuna mwenzangu ambaye ameongea kuhusu "Pesa Mashinani" na sahihi za watu; haiwezekani kuhusisha Harambee na hizi sahihi. Hakuna haja ya kuongea kuhusu jambo lililopita kitambo na kulihusisha na Harambee.
Mhe. Spika ni tatizo kubwa sana kwa sisi ambao tumebaleghe katika lugha kuona watu wananajisi lugha hapa. Nimebonyeza dude hapa tena kwa muda mrefu sana nikitaka kutoa muongozo. Ni hoja ya nidhamu.
Mhe. Spika nikimsikiza dada yangu kutoka huko Suba Mhe. Millie Odhiambo alikosea usanifu wa Kiswahili kwa sababu anasema kuwa lile neno Mhe. Olago amelitamka ni neno ambalo linatamkwa na comedian . Nafikiri ingekuwa hoja ukubalie Mhe. Millie Odhiambo alitoe kutoka kwa orodha ya kitabu sahihi cha historia ya Bunge ili miaka ijayo kumbukumbu ya Bunge hili ikisomwa isimnukuu vibaya. Ahsante Bw. Spika.
Mhe. Spika niko na Kamusi nyingine ambayo nitampelekea ndugu yangu Kiongozi wa Walio Wachache Bungeni. Nachukua nafasi hii kuwashukuru wale walio jumuika katika kazi hii. Ni kazi iliyofanywa kwa miezi sita. Kuna wafanyikazi wetu hapa waliofanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kwamba shughuli hii inafaulu. Pia nashukuru Ofisi yako Bw. Spika kwa sababu wewe ndiye uliyetenga rasilimali za kuhakikisha kwamba tutakuwa Bunge la pili duniani kuwa na Kanuni za Kudumu zilizotafiwa kwa lugha ya Kiswahili. Wafanyikazi hawa waliweza kutembelea Bunge la Taifa jirani la Tanzania ambalo lina Kanuni za Kudumu kwa lugha ya Kiswahili. Ni wao peke yao waliokuwa na kanuni hizo kwa lugha ya Kiswahili duniani. Kwa hivyo tutakuwa taifa la pili lenye Kanuni za Kudumu katika lugha ya Kiswahili Tumegundua kuwa Kiswahili cha Watanzania na chetu kina tofauti kiasi. Hii ndio sababu tumeamua kuwa hatutatumia kanuni hizi mara moja. Ni lazima zipigwe msasa. Najua wengi hawaelewi msasa ni nini. Ndugu yangu Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni atawaambia baadaye. Ni vyema tuwe na Kiswahili chetu cha hapa nchini. Tutahakikisha kuwa tumepeleka kanuni zetu katika vyuo vyetu vikuu hapa nchini kama Chuo Kikuu cha Nairobi ili wataalamu wa lugha wazipitie na kutupa nakala itakayokuwa ya hapa nyumbani. Kiswahili ni lugha maskini. Kwa mfano jina tunalitoa na kuliita "Spika" badala ya kutafuta neno la Kiswahili litakalotoa tafi ya moja kwa moja.
Mhe. Spika niko na shangwe na furaha mpwitompwito kama tasa aliyepata mwana. Ni mimi ambaye alizindua ndoto hii ambayo imetimia. Punde tu baada ya uchaguzi nilisema hadharani kwamba itakuwa muhimu Rais Uhuru Kenyatta ambaye alikuwa ameshinda uchaguzi na Mhe. Raila Odinga ambaye alikuwa hakupoteza bali mambo yalikuwa yamemwendea mrama kushirikiana. Nilisema kitumbua cha Mhe. Raila kilikua kimeingia mchanga kidogo na hivyo basi akae na Rais Uhuru Kenyatta wawaunganishe Wakenya. Mhe. Raila ana sifa zake. Ni lazima tumheshimu. Ni kigogo na uti wa mgongo wa siasa za taifa la Kenya. Hakuna jinsi Rais Uhuru angefanya kazi bila kuungana na Mhe. Raila. Hii inatufunza nini? Inatufunza kwamba ukipenda usipende sana na ukichukia usichukie sana. Usitusi wakunga kama uzazi ungalipo.
Mhe. Spika nilikuwa nataka kuzungumzia jambo hapo awali lakini kwa vile muhula uliisha ningependa kusema sina jambo la kusema.
Mhe. Spika nimesimama kwa jambo la nidhamu. Kulingana na Kanuni ya 80 unaruhusuhiwa kuangalia kile ambacho umeandika lakini hufai kusoma. Ni lazima uifanye hiyo Kanuni itumike. Inaonekana Kiongozi wa Wengi Bungeni anasoma taarifa. Kanuni ya 80 ya Bunge la Taifa inasema kwamba tunaweza kuchungulia stakabadhi za maandalizi yetu na wala sio kusoma. Mhe. Spika ni lazima tufuate Kanuni za Bunge hili. Kanuni zetu zishageuzwa kwa Kiswahili. Ni lazima tufuate Kanuni ya 80 ambayo inaturuhusu kuchungulia maandishi yetu ya matayarisho. Mtu hafai kusoma kana kwamba anatoa hotuba. Kiongozi wa Wengi anatoa hotuba ndani ya Bunge. Inafaa azungumze bila kusoma. Anastahili kuchungulia tuu maandishi yake ndiyo yaweze kumsaidia kidogo.
Mhe. Spika nimesimama leo kumuunga mkono mwenzangu Owen Baya kwa hili ombi ambalo ameleta hapa Bungeni. Mimi mwenyewe ninafahamu sana watu ambao hawana ukoo nchini. Tumekaa na watu hao kwa miaka miwili tukizungumza wakitueleza shida ambazo wanapatana nazo. Walipoona Rais akipeana vyeti vya kukaa kwa Wanamakonde hawa wa Kibera pia waliona kuwa wana uwezo. Saa zile Washona walikuja hapa Bunge kutuletea ombi lao walisema kuwa Rais wa kwanza Mhe. Jomo Kenyatta aliwatambua na kama angekuwa amebarikiwa na maisha ya mbeleni zaidi angekuwa ameshawatimizia ombi lao la kuonekana na kujulikana kama Wakenya. Washona wenyewe walipewa shamba karibu na Chuo kikuu cha Daystar ambako walijenga kanisa lao. Ni watu ambao wana maombi na wanakaa na ukweli na undugu na Wakenya. Hawajui nchi nyingine. Wakoloni walipokuwa hapa walileta watu kutoka Afrika nzima. Tuko na watu kutoka Rwanda Zimbabwe Pemba na Tanzania. Hao watu wote waliletwa hapa kukaa na sisi na kufanya kazi kama kujenga reli. Lakini sasa wako na shida sana. Hawatambuliwi. Tukiwa na hii Huduma Namba watakuwa na shida zaidi. Hata kama tunataka kuwatambua kama Wakenya ni lazima pia tuwasamehe kwa sababu kuna mambo waliyofanya ambayo si ya haki - kama kwenda kuchukua vitambulisho ama kuwaandikisha watoto wao kuwa wamezaliwa Kenya ili waweze kwenda shule au hospitali. Kuna familia nyingine tunazozitambua ambazo watoto wao wamezaliwa huku lakini wazazi hawatambuliki. Kuna wengine wamemaliza masomo ya O-Level lakini mpaka sasa hawawezi kujiunga na vyuo vikuu. Mhe. Spika sisi kama Wabunge tulikuomba tuwe na caucus ya kuangalia hao watu ambao hawana jinsi ya kujulikana ama kutambulika kama Wakenya. Tuko na wengi na si community moja. Katiba yetu inasema kuwa haifai watu wengine wapate na wengine wakose. Sisi sote kama Wabunge tunajua kuwa hao watu ambao wako nchini mwetu na wameishi na sisi wanafaa watambulike kama Wakenya. Kwa hivyo naunga mkono hilo ombi la watu wa Pemba na watu wote wengine kama vile Washona na wale wa Rwanda ambao wameishi na sisi kama Wakenya ili watambulike kama Wakenya. Ahsante Mh. Spika.
Mhe. Spika nimeyaelewa mambo ambayo ndugu yangu amesema. Mhe. Chepkong'a ni mtu ambaye ninamheshimu sana lakini hapa hatuzungumzi kuhusu ng'ombe wa Wakalenjin; tunazungumza kuhusu ng'ombe wa Njuri Ncheke kule Meru. Mhe. Spika naomba tu nimalize kwa kusema kuwa tukubaliane kuwa Kipengele cha 10 cha Katiba kinasema yeyote anaweza kufai Katiba. Nimeisoma. Mtu yeyote anaweza kufai Katiba. Vile tumeifai tunaomba Bunge lionyeshe huu uwe ni mfano kwa wenzetu ambao wamepewa nafasi za kuhudumia nchi hii. Kama hawaendi kulingana na matakwa ya wananchi basi Bunge litoe nafasi ya kumuita Kaimenyi aje aangaliwe. Natumai mnaelewa na yale ninasema. Nasema Bunge litoe nafasi Kaimenyi aitwe aje aeleze upande wake maana lazima apewe nafasi. Ndio tunasema kuwa hiyo kamati ikiundwa impe nafasi ajieleze. Kama atapatikana na makosa ataadhibiwa. Kwa sasa naomba tukubaliane tuipitishe hii Hoja ili Kaimenyi apewe nafasi ya kujisafisha. Kwa hayo mengi mhe. Spika naomba kuunga mkono Hoja hii. Asante.
Mhe. Spika ninakubali muongozo wako na ninaomba nimaliza kwa kuwaomba wenzetu tuelewane. Msichukue ujumbe wetu vibaya. Ninaomba muelewe ujumbe wetu vizuri kuwa kongao hili ambalo ni la Bunge hatukulidharau wala hatujalidharau. Kongao hili la Bunge ni la muhimu wala hatukusema halina umuhimu. Kitu tunasema ni kuwa wakati huu ambao kuna mambo mengi ambayo yanakumba nchi hii kwa maoni yetu tumeona si vizuri upande wetu kushiriki kikamilifu kwa wakati huu. Lakini haiishi mtu akitaka kwenda atafungiwa. Ndio maana Mhe. Midiwo amesema yeye ataelekea. Lakini ninaomba tuheshimiane. Kama upande wetu umeonelea ndio hivyo basi uwachwe ufikirie uone kwa nini umeonelea hivyo. Kwa sababu Bunge linahitaji nieleze na ndio maana ninaeleza upande wetu umeonelea wakati huu mambo mengi ambayo yanaendelea na kuna malumbano huko nje huenda tukaenda chini tukaongeza malumbano. Itakuwa badala ya kurekebisha yale tunatakiwa kurekebisha huenda tukaenda tukachangia matatizo mengi maana utaenda na watu wataanza kuzungumziana yale yako moyoni mwao; yale yako katika fikra yao katika hali hii ya kisiasa. Kwa hivyo maoni yetu yangekuwa labda lingekuwa jambo la busara tuwe tumejadiliana mambo haya hapa kwanza ndio tukiwa tunaenda tunaenda tukiwa tumewasiliana tumeafikiana kuwa jai tunaenda kufanya hili na lile. Lakini wasiwasi wetu ni kuwa tunaweza kwenda huko tukaenda tukaanza malumbano kwa sababu kila upande una mambo yake. Hivi sasa unaona mambo ya kisiasa yalivyo; tunazozana kisiasa kwa mambo ya ufisadi. Mara yanatoka upande ule yanarudi upande huu. Kwa hivyo hakukuwa na mazungumzo. Hata hapa Bungeni hatukuwa na mazungumzo na tukajadiliana kuwa jai tunaenda kufanya abcd na haya ndiyo mambo tunaenda kusema Kwa hivyo Mhe. Spika ninaomba unielewe.
Mhe. Spika ninaomba kumfahamisha mwenzangu kwamba ukizoea wa nazi wa samli huuwezi. Mhe. Spika ninamheshimu sana ndugu yangu Kaimenyi kwa sababu ametimiza majukumu yake lakini kuna mambo ambayo yamemlemea. Hadi sasa shule hazina bodi. Tukiliangazia suala hilo mutakubaliana nami kwamba huyu bwana amelemewa na majukumu yake. Sina shaka kwamba ndugu yangu Kaimenyi ni msomi. Ana sifa za usomi lakini tusipotoke kwamba mtu anaweza kutekeleza majukumu kwa sababu ya usomi. La! Majukumu mengine yanamshinda licha ya kwamba ni majukumu ya elimu. Tukiangalia jinsi nchi hii inavyoendelea na tukimwacha ndugu yetu Kaimenyi aendelee
Mhe. Spika ninaomba mwongozo kutoka kwako. Wakati Mbunge mpya anapolishwa kiapo cha ofisi tunalazimika kusimama. Kanuni za Bunge Vipengele vya 3 na 104 havisemi kwamba ni lazima tusimame wakati Mbunge mpya anapolishwa kiapo. Mwongozi wa sisi kusimama wakati Mbunge mpya analishwa kiapo umetoka wapi? Naomba mwongozo kutoka kwa Mhe. Spika.
Mhe. Spika ninashukuru kwa muda huu ambao umenitunukia nijibu mawili matatu ambayo yameletwa na Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni. Ninamheshimu na nitaendelea kumheshimu. Lakini haimaanishi kuwa ana majukumu ya kutuambia msimamo wetu utakuwa upi kulingana na muongozo wa nchi. Wakati umefika Mhe. Duale aambiwe wazi wazi kwamba hatakuwa akipeleka ubabe wake kila pahali. Pia wakati umefika Duale aambiwe wazi wazi kuwa ana uhuru wake wa kueleza na kutoa maoni kuhusu msimamo wake lakini msimamo wake hauwezi kuwa sawa na wetu. Msimamo wake ni wake na wetu ni wetu. Kitu ambacho tumesema ni kwamba hatuna haja ya uchaguzi wa ugomvi. La! Tunataka ai. Kama kuna watu wanahitaji ai ni sisi. Tunataka uchaguzi wa ai. Haimaanishi tunataka kuchangia uchafu ama machafu nchini tukiamua hatutashiriki katika zoezi lolote. Katika kila kongao na kila upande wa siasa kuna majadiliano. Watu huzungumziana wakaelezana na wakakubaliana. Mhe. Duale amesimama akisema: Mimi kama Kiranja wa Walio Wachache niwache kuchukua muelekeo kutoka kwa viogozi wangu wakubwa wa kisiasa. Ni wapi umeona mambo kama hayo? Hayajaonekana wala hayataonekana. Hata yeye mara nyingi huchukua muelekeo kutoka kwa wakubwa wake. Hata wakati mwingine tunapitisha sheria hapa na kusema hatuzitaki. Mhe. Duale anasimama kusema: "Nimeambiwa yawe haya na haya." Tunakubaliana na muongozo wake. Kwa hivyo hana mamlaka yoyote ya kutuelekeza. La pili ninaomba niweke bayana kwmaba ni kweli wala sitaki kukana kuwa nimetuma huo ujumbe. Nimeuzungusha lakini sikukaa nikautunga. Bila shaka tumekaa tukajadiliana nikatoa muelekeo na nikaupeleka. Umesikia Mhe. Midiwo akisema yeye hajapata huo ujumbe. Kwa hivyo maadamu ameamua anaenda Mombasa anaenda. Hakuna yeyote ameambiwa asiende Mombasa.
Mhe. Spika ninaunga mkono Hoja hii. Tumemsikia Mhe. Gumbo vile alivyotoa maoni yake kuwa inabidi tuweke wasomi katika Kamati hizi. Mhe. Spika nimesikia mara nyingi ukitoa mwongozo hapa Bungeni kuwa Wabunge wote wako sawa mbele ya Bunge wawe wamesoma au bado hawajasoma mradi tu wananchi wameona waje Bungeni. Wana haki yao ya kuwawakilisha watu wao katika sehemu wanayotoka. Ijapokuwa nimemuelewa Mhe. Gumbo yale anayoyasema kuwa angependa kuwaona wasomi peke yake ninamuomba arudi pale tumeanzia. Kama wananchi wataona inafaa walete watu ambao kisomo chao kulingana na Mhe. Gumbo ni hafifu na hakilingani vile Mhe. Gumbo anavyoona basi mimi kama mmoja wa wasomi siwezi kukaa hapa nianze kusema kuwa ninakubaliana na maoni ya Mhe. Gumbo. Tugeuze sheria iseme kuwa yeyote ambaye atakuja Bungeni lazima awe na kiwango fulani cha kisomo. Kwa sasa tunasema lazima mtu awe amefika kidato cha nne. Hicho ni kiwango ambacho tunatarajia kiwekwe ili Mbunge awe amefika kidato cha nne. Lakini ikibainika waziwazi kuwa si muhimu na wananchi wakatae waseme kuwa Mbunge yeyote mradi tu awe ni binadamu mwenye akili timamu ana haki ya kuja Bungeni itakuwa ni uamuzi wa wananchi. Hivi sasa tumefuata mwelekeo uliotupatia kuwa Wabunge wote wana haki sawa na ndio maana tukaleta majina haya. Ninaunga mkono Hoja hii na majina haya.
Mhe. Spika ninawaelewa. Ni vigumu kuelewa lugha ya Kiswahili. Nilivyosema Kiswahili ni lugha maskini. Kuna misamiati ambayo haipatikani kwa Kiswahili. Ni lazima uazime kutoka kwa lugha ya Kiingereza na utoe kwa mfano neno ambalo ni la Kiingereza . Tukitafi kama "Msemaji" huko ni kupotoka; hicho si Kiswahili sanifu. Tukijaribu kutafi tutapata shida kiasi. Kama ujuavyo katika Bunge la Kitaifa tuna Waswahili wa kutosha. Kwa mfano kuna ndugu yangu niliyeketi naye hapa ambaye ninashauriana naye. Anaitwa Mhe. Mwashetani. Kuna Waswahili wazuri Bungeni. Tuko na Mhe. Ali Mjumbe Ali Wario Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni ambaye amejifunza Kiswahili kama wengine na Captain Ruweida. Hili ni jambo la maana. Kuna lahaja za Kiswahili kama vile Kipate na Kiunguja. Kila mmoja wa wazungumzaji wake ana umahiri wa lugha. Naomba Wabunge waipitishe Hoja hii. Sababu ya kazi hii kufanywa haraka ni kuwa siku ya kesho - ambayo ni siku kubwa katika Bunge hili - tutakuwa na mkutano wa kwanza wa kuonyesha kamati za Bunge hufanya nini. Moja ya vitabu tutakavyozindua kesho ni Kanuni za Bunge la Taifa ambazo tunataka kupitisha siku ya leo. Kuna ndugu zangu kama Mhe. Kaluma na wengine ambao wamechoka kwa sababu hawaelewi. Kesho itakuwa siku nzuri. Tutazindua rasmi hizi kanuni. Mhe. Spika utafanya. Nimemshauri ndugu yangu ambaye amekaa karibu na mimi. Nitaomba ulinzi mwafaka kutoka kwako ili ndugu yangu aliye karibu nami anipe nafasi nimalize. Itakuwa vizuri Wabunge waje kwa wingi ili tuweze kuonyesha kama Bunge kuwa tuna kazi kadhaa ambazo sisi hufanya. Tunaongea Kiingereza na lugha ya taifa vizuri. Kuna kazi ambazo sisi hufanya ambazo hatuwezi kujipiga kifua lakini kesho tutapata nafasi ya kueleza kuwa tunafanya kazi hizo. Lazima kesho tuonyeshe kuwa kamati ni za maana kama plenary. Mwenzangu ameniambia kuwa ni "ukumbi" kwa Kiswahili. Kwa hivyo ni kama vile ukumbi wa Bunge unavyofanya kazi. Tuna shida kidogo na ndio sababu ya kuwa na kamusi hapa. Kwa Kiingereza tunasema " The august House ." Nilimuuliza ndugu yangu ikiwa tafi yake tutasema ni "Nyumba ya Mwezi wa Nane" Aliniambia la! Tutaitafi na kusema ni "Nyumba ya maana au ya kifahari" Hivyo ndivyo nitakavyosema. Kuna mambo kadhaa ambayo yataendelea kuwatatiza Wabunge kuyaelewa kikamilifu. Kwa mfano ukiangalia " Petition " kwa kawaida tungesema ni "Ombi" Lakini tafi yake si "Ombi" Nataka nimshukuru Mhe. Millie kwa sababu ameniletea maji. Ameona ninajikaza. Kwa hivyo ni vyema tuipitishe Hoja hii. Nawaomba Wabunge wenzangu kwamba katika hali ya patriotism; samahani katika hali ya uzalendo tuchukue nafasi hii leo na tuipitishe Hoja hii haraka ili tuweze kuwasiliana na Wakenya wenzetu kwa urahisi. Kwa haya Mhe. Spika naomba kuwasilisha hii Hoja na niombe Mhe. Ali Wario awe mwafiki wangu. Ahsante sana Mhe. Spika.
Mhe. Spika ningependa kuungana na wenzangu kutoa pole zangu pamoja na jamii yangu na Wapokot wote kwa jamii ya Mhe. Marehemu Litole. Najua Mhe. Marehemu Litole alihudumia nchi hii katika nyanja mbali mbali ya mwisho katika Bunge la Kumi. Alifanya kazi nyingi zaidi katika Kaunti ya Pokot ambayo amewacha alama. Kwa hivyo natoa pole zangu na Mungu amurehemu.
Mhe. Spika ningependa mheshimiwa atueleze iwapo mapenzi ni ya mwanamke peke yake. Mbona anaelekeza lawama kwa wanawake peke yake na hasemi wanaume pia wajiheshimu?
Mhe. Spika nitaomba uniongezee dakika mbili ambazo zimepotea hapo. Nimesimama kuunga mkono Mswada huu. Huu ni wakati wa kushughulikia mambo ya usalama. Miezi kadhaa iliyopika kunashambulizi ambalo lilitokea kwa matatu katika Barabara ya Thika na miongoni mwa waliokufa ni kijana mmoja aliyekuwa ametoka kwangu. Alikuwa na mke wake ambaye aliumia miguu mpaka sasa hivi hawezi kutembea. Kila siku anaenda hospitali na imetubidi kurudi kwa mifuko yetu ili tumchangie. Amewachwa mjane na mlemavu kwa wakati huu. Juzi tulihudhuria mazishi ya dada huko Kieni ambao waliuawa. Ungekuwa miongoni mwa wale waliohudhuria hayo mazishi haungejaribu kuzipinga sheria hizi. Miezi kadhaa iliyopita Kiongozi wa Upinzani alisema kuwa anataka kuwe na majadiliano kuhusu usalama. Ilisemekana kuwa Serikali imekataa.
Mhe. Spika ombi la Mhe. Junet ni la muhimu. Ni vyema tumalize mjadala huu kwa sababu muda wake ni leo. Kama mnaomba niweke tamati ili wenzangu wapate nafasi ni radhi niweke tamati. Kwa haya mengi naunga mkono.
Mhe. Spika pia mimi ningependa kuchangia kuhusu hili jambo la kufariki kwa Mzee Ngala. Mimi kama mtoto wa mwanasiasa ambaye alikuwa anafanya kazi na mzee Ngala kwa hili Bunge ningependa kutoa rambirambi zangu kama Mbunge wa eneo la Kitutu Chache Kusini. Tena ningependa kutoa rambirambi zangu kutoka kwa familia yangu ya mzee Dr. Zachary Onyonka aliyeaga. Mhe. Ngala ni mzee ambaye aliheshimika. Alifanya kazi kama mzalendo na wale Wakenya ambao wako nchi hii wanakumbuka. Vigogo wa zai walipenda nchi hii waliamini na walitaka iendelee mbele. Anaheshimika kwa sababu alifanya kazi kama mzalendo. Wakenya wanakumbuka wale vigogo wa zai kama wazee walioipenda na kuithamini nchi hii. Walitaka nchi hii iendelee mbele. Ningependa kuwaombea wananchi wa Kitui Mungu awabariki kwa kutupa kiongozi ambaye alikuwa anaheshimika. Ni kiongozi ambaye atakumbukwa nchini milele. Ahsante Mhe. Spika.
Mhe. Spika Shukrani sana kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa ningependa kuweka rekodi sawa kabisa. La kwanza na muhimu zaidi ni kwamba idadi ya Wabunge waliokuwa wakitaka kupiga kura ilikuwa mia asili mia. Ya pili swali likauliza na Wabunge wote kwa kauli moja wakakubaliana na kupinga na kusema ya kwamba hawatakubali kama wanavyotaka ila kama anavyotaka Wanjiku. Hamna mtafaruku wowote ambao umetokea baina yetu. Wakati ambapo Mwenyekiti aliomba tupige kura tulikubaliana kwa kauli moja tuweke foleni lakini baadhi ya viongozi ndani ya Bunge wakiwemo Duale na Mbadi wakaanza kuiingilia na kuzuia upigaji wa kura.
Mhe. Spika sijaiona chombo hiki katika Bunge hili. Nimechungulia viti vya viongozi ambao wako karibu nami na nikapata havina chombo hiki. Kwa hivyo ningeomba uamuru Karani wa Bunge la Kitaifa achunguze kwa haraka kwa nini kiti hiki kina chombo tofauti na vile viti vingine. Pia naomba utoe amri kuwa Mhe. Sabina Chege aondoke kutoka kwenye kiti changu kwa haraka ili nirudi huko kwa usalama wangu binafsi.
Mhe. Spika ukiangalia hali Wabunge walivyo hawana nia ya kuendelea na Hoja kama hii. Najua hii Hoja ni ya mbinu ambazo zinatakiwa kutumiwa. Wabunge wamechoka wamelemewa; wanataka haya mambo yaishe twende tufanye mambo mengine. Lakini ukweli wa mambo ni kuwa hii Hoja ya mbinu imeletwa hapa kwa kutokubaliana kwa Kamati ile iliyokuwa imeundwa; inatuletea shida bure tu. Naomba tuangalie sheria zetu kwa sababu hili Bunge ndilo linatakiwa kutatua hili tatizo vile Mwenyekiti amesema. Kwa hivyo tusianze kuzungushana merry-go-round kila pahali. Naomba tukubaliane huu muda upunguzwe vile tulivyoomba. Tukishamalizana nao ikileta shida hivyo hivyo tuamue kwa hili hili Bunge. Labda Wabunge lazima waweke sahihi kabisa kuwa hili Bunge ndilo linaheshimiwa na litoe muelekeo kwa wenzao. Naomba kuunga mkono.
Mhe. Spika umeona wazi wazi. Makamu wako amempa Kamusi Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni na amemuacha Kiongozi wa Walio Wachache Bungeni. Naona huu ni ubaguzi Bungeni. Huo ni ungwana kweli?
Mhe. Spika unajua Mhe. Duale anatoka sehemu ambayo huwa iko na hatari nyingi. Kwa hivyo akiona chombo kama hicho ningependa nimhakikishie kuwa hicho si kilipuzi. Ningetaka kuwahakikishia kwamba hicho si kilipuzi kwa sababu mnajua natoka sehemu za mlima na tumeona vitu kama vilipuzi. Kwa hivyo hicho si kilipuzi. Atulie kidogo. Asiwe na wasiwasi.
Mhe. Spika unajua raia wako na shida nyingi sana. Ukisoma jumbe tulizonazo kwa simu utapata mtu anakuambiaz: "Mtoto wangu yuko hospitalini." Mwingine anakuambia: "Kuna maiti imekawia kutolewa huko mochari iletwe nyumbani." Hawana pesa. Mwingine anakuambia: "Mtoto wangu amefukuzwa kwa shule. Hana pesa." Mwingine anakuambia: "Bw. Spika wajua sisi hatuna hizo shida kwa sababu tunapata pesa." Kwa nini tunataka kuwa watu ambao hawataki kusaidiana na wengine? Kwa nini tunakuwa wachoyo hadi kutoa ile kandururu kadogo tunako ndio watu wengine wajimudu ni vigumu? Nilifikiria ninatoka familia ya matajiri nikiwa kijana mdogo. Lakini ikafika wakati nilikuwa nataka niende ng'ambo kusoma. Wacha nikuambie! Watu walichanga wakachanga na kuchanga. Wakati nilirudi kuna mzee mmoja alinionyesha mti aliouza alete kwa mchango wangu. Haukuwa umekatwa. Halafu unaniambia nikatazwe kuchanga. Hata kama niko na ndururu ama shilingi kumi pia nitampelekea anayemtuma mtoto ng'ambo. Hatutaki sheria kama hizi. Tuunde sheria inayosaidia Kenya hii. Tunatoka sehemu ambazo watu wanatoa mamilioni ya pesa kila wikendi. Kuna shida gani? Hawa ni watu wameshindwa kufanyia raia kazi. Sisi tumesema: "Kwa sababu wameshindwa kufanyia raia kazi wacha wazilete hizo pessa kwa michango." Hivyo itakuwa tumetumia ile pesa angeleta kufanyia kazi. Napinga hii sheria kabisa. Ningependa hii Nyumba isiwe ya kupitisha sheria mbaya. Tutumie hii Nyumba kujenga nchi yetu. Hakuna hatia kuchanga. Hakuna sheria yoyote kwa hii Nyumba ama kwa Katiba inayokataza na kusema ni hatia kufanya mchango. Uchaguzi unakuja. Utasikia kila hoteli Nairobi hii iwe Inter-Continental au Laico Regency Wajumbe wanaunda michango yao ya kuwasaidia kuwania viti. Hata Marekani wanafanya hivyo. Yaani unataka usaidiwe kuchanga pesa za kwenda kuzunguka kutafuta kiti na hutaki kusaidia mama asiye na hata ndururu ya kupeleka mtoto shule? Najua sheria hii ililetwa kutoka upande ule mwingine. Lakini tuikatae ikifika hapa tafadhalini. Hata rafiki yangu Mwenyekiti wa Kamati ya Kiidara ya Haki na Masuala ya Sheria aliyeleta huu Mswada hapa namuuliza autoe. Mhe. Spika unajua umaskini si kitu unajiitia. Mwenyezi Mungu hajatakia yeyote kuwa maskini. Hakuna mtu Mwenyezi Mungu alimtuma duniani na kumuambia: "Nenda uwe maskini." Umaskini unaletwa na shida. Shida moja ni kutokuwa na rasilimali. Shida ya pili ni viongozi wanaokataza wananchi kupata au kufikia rasilimali za nchi hii. Kwa sababu tunataka michango iendelee ile sheria ambayo labda tungekubali ni inayosema michango ifungwe miezi sita au mitano kabla ya uchaguzi. Saa hii nimechaguliwa na raia. Raia wana shida. Eti naambiwa nisiende kwa michango miezi miwili au sita baada ya kuchaguliwa. Huenda mtoto wa mtu yuko hospitalini. Wengine wanafaa kupelekwa India kwa operesheni halafu tunaambiwa hatuwezi kuwachangia kwa sababu tu Wajumbe! Wewe ni Mjumbe wa nani kama huwezi kusaidia hata mtoto anayepelekwa hospitali? Wewe ni raia aina gani uliye nacho na hutaki kusadia wengine? Napinga. Napinga nikisema lazima turuhusiwe kusaidia watu wetu walio na shida katika nchi hii. Tuko na pesa iitwayo "bursary". Tunajaribu kugawa hiyo pesa. Ukigawa unagawa hadi iishe. Lakini kuna wengine wameshindwa kupata. Wengine wanapata lakini haijatosha kulipia karo. Hapo ndio tunachukua fursa hii tuseme twende tuchangie na kuwalipia. Ningependa niseme napinga huu Mswada. Tunakemea aliyeleta Mswada huu. Atafute Mswada mwingine wa kuleta kwa hii Nyumba. Napinga. Ahsante.
Mhe. Spika wa Muda kwa vile Nyumba ilivyotulivu leo na viwango vya joto vikiwa chini naomba msamaha.
Mhe. Spika wa Muda mimi na Mhe. Njagua tunaenda kuchukua shahada zetu kesho kule Mount Kenya University. Nakuomba kwa unyenyekevu umpatia ruhusa kwa sababu tunaitwa tukachukue vyeti vyetu.
Mhe. Spika wa Muda nakushukuru sana kwa kunipatia hii nafasi nichangie Hoja hii na kuiunga mkono. Ni vizuri kuwa na mpangilio ili tufaidike kutokana na lile tunalotafuata. Mwanzo ningependa kuishukuru ile kampuni ya Zarara ambayo iko Lamu. Wamejitahidi sana. Wanakwenda mashinani kuzungumza na jamii. Kwa hivyo jamii katika Lamu Magharibi na haswa katika Wadi ya Faza wanajua kile kinachoendelea. Naomba pia kampuni zote zinazokuja Lamu kwa chochote wahusishe jamii vizuri. Pia kile kinachopatikana kutokana na kuchimbwa kwa madini kiwe kinafaida jamii maana vitu vingine kama ule mradi wa makaa Lamu umeleta shida sana. Viongozi waliokuweko labda waliwaonyesha ufaa; lakini sisi tulioingia Bungeni tunaomba pia tupitie mpangilio wao watuonyeshe kama huo mradi una ufaa kwa jamii ama hauna. Tunaomba watupatie muda kama viongozi ili tufanye utafiti wetu. Wasitupeleka haraka vile huo mradi unavyoenda. Tunataka viongozi na jamii mashinani wahusishwe vizuri. Ikiwa kitu kinafaida watueleze vyema. Vile vile kama kitu hakina faida tuambiane kinaga ubaga. Asante Mhe. Spika wa Muda.
Mhe. Spika wahenga walisema "Usiache mbachao kwa msala upitao." Maana yake ni kwamba usiache ule mkeka wa zai ukitafuta wa Kizungu. Hiyo ni kusema kwamba msala mbachao ni Kiswahili chetu. Kiswahili ni mbachao wetu. Kiswahili ni lugha yetu na ni sharti tukitukuze na kukienzi kama desturi yetu na pia kwa sababu Katiba yetu imetuamurisha kufanya hivyo. Mhe. Spika watu wengi wako na shida ya lugha ya Kizungu. Hoja hii ya leo itawasaidia. Wale ambao hawajaweza kuongea tangu Bunge la Kenya lilipoanza kwa sababu kuzungumza Kizungu kwao imekuwa shida leo tunawapatia fursa wasome Kanuni za Kudumu za Bunge la Taifa ili waweze kuleta Hoja. Wakitaka kuleta hoja ya kusema kwamba idadi ya Wabunge haijatosha watasema hivyo kulingana ha hoja ya akidi ama " lack of quorum ". Kuna wengine wetu ambao hawajui maana ya " quorum ". Hao watasema "Hoja ya akidi". Wale ambao hawajui " Committee " ni nini watasema "kamati". Taarifa ni "statement". Ukitaka kuleta petition utasema...Ninafundisha akina Mhe. Kaluma Mhe. Mbadi Mhe. T.J. Mhe. Junet Mhe. Millie na wengineo. Kuna wenzetu ambao wanajua Kizungu lakini ikifika kuongea Kiswahili wanazubaa wanabaki mabubu kama watu ambao hawasikii. Kuna wenzetu katika Bunge hili ambao Mhe. Mbadi Mhe. T.J na Mhe. Shollei wanapozungumza Kizungu wanakua mabubu. Sasa kuna fursa ya Bunge hili kujaa. Kila mtu anaweza kuongea Kizungu ama Kiswahili. Tukiendelea mbele tutaleta lugha ya mama pia kwa sababu kuna wenzetu ambao hawajui Kiswahili ama Kizungu. Uongozi si lugha; uongozi ni vitendo. Uongozi si vile unavyoongea katika Bunge hili. Mhe. Spika jina lako litaingia kwenye kumbukumbu za historia. Ni katika enzi yako ambapo tuliweza kupata hiki chombo cha kupigia kura. Leo pia umekalia Kiti cha Spika wakati tunapitisha Hoja hii. Kenya ni nchi ya pili ulimwenguni kupitisha Kanuni za Bunge za Kudumu. Mhe. Spika wengine wetu tutaandika vitabu na tutakupatia sura rasmi yako kama Spika ambaye ameleta mabadiliko muhimu katika Bunge. Wale wa zai hawakufanya hivyo lakini walijaribu. Nikimalizia mimi naunga mkono Hoja hii na nataka Waswahili wapate nafasi ya kuja katika Bunge hili ili wachangie zile Hoja ambazo zitaendelea. Ahsante Mheshimiwa Spika.
Mhe. Spika wajua Kiswahili kilikuja na meli na barabara hadi kwetu. Tungependa Tume hiyo ihakikishe kuwa ile shida ya ardhi katika kila sehemu ya nchi hii imeangaliwa. Ni vyema kama kuna sehemu ambayo hatimiliki zake hazijapeanwa zipeanwe. Kama kuna mahali hakujagawanywa kugawe. Kupitia "petishoni" ya Mhe. Lelelit ningependa kuseme kwamba ninaunga mkono. Asante Mhe. Spika.
Mhe. Spika wakati mwingine kuna watu ambao hawafahamu zile sheria za Bunge wanaona kwa kuita jina lako wao hutukatiza eno. Katika hali yaa kutukatiza eno hatufahamu nia yao ni ipi. Ningemuomba aache niendelee ama umkataze kuendelea kuzungumza.
Mhe. Wa Bahati kila jambo ni bure. Tutapata mchango kutoka kwa Mhe. Ahmed Shabbir wa Kisumu East.
Mhe. Wairimu kidogo tu. Kuna hoja ya nidhamu kutoka kwa Mhe. Sankok.
Mhe. Wairimu umejaribu sana na umefanya vyema. Tunakuunga mkono na kukushukuru. Anayefuata ni Mhe. Mwadime Mbunge wa Mwatate.
Mhe. Wario nimepata raha sana kukusikiza ukitoa hiyo hotuba hapa Bungeni. Kwa sasa hivi tutamskiza Mhe. Osotsi.
Mhe.Naibu Spika naomba kutoa azimio la Hoja ifuatayo: KWAMBA tukitambua kuwa Ibara ya 43 ya Katiba imebainisha kila mtu ana haki ya kupata kiwango bora zaidi cha afya kinachojumuisha haki ya kupata matunzo ya kiafya na kutonyimwa matibabu ya dharura; aidha ikifahamika kwamba gharama za matunzo ya kitabibu katika taasisi za kiafya za kibinafsi zingali ghali mno hivyo kuwalazimu Wakenya wengi kupendelea kusaka huduma hizo kwa hospitali za umma; tukizingatia kwamba licha ya bei nafuu ya matibabu katika hospitali za umma ikilinganishwa na hospitali za kibinafsi bado Wakenya wengi hawamudu hivyo basi kutumbukia kwenye madeni ufukara na dhiki wanaposhindwa kulipa malimbikizi ya gharama za matibabu yao na ya wapendwa wao; Bunge hili linahimiza Serikali ya Kitaifa kufutilia mbali gharama zote za matibabu za wagonjwa wote wanaofariki wakipokea matibabu katika hosptali za umma za rufaa. Asante Mhe. Naibu Spika.
Mheshimiwa
Mheshimiwa Mwadime umeongea kwa utamu katika Hoja hii. Nataka kumpa nafasi hii Mheshimwa Nangabo Janet Mbunge wa Trans Nzoia.
Mheshimiwa Mwinyi hujakosea nidhamu. Kwa hivyo mtanikubalia nisome Hoja ilivyo. Let us have Pukose.
Mheshimiwa Naibu Mwenyekiti wa Muda laiti sheria hizi zingekuwa katika lugha ya Kiswahili mungeelewa kikamilifu kile ambacho Mheshimiwa Mwadime anamaanisha. Lakini kwa sababu tunazitunga sheria hizi kwa lugha ya Kimombo Mheshimiwa Mwadime anapotumia neno " traditional " anamaanisha wenyeji. Tukianza kuingilia suala la wenyeji ndipo haya masuala mengine yanaingilia. Kuna utata kuwa wenyeji ni kina nani na waliokuja ni kina nani? Haki zao zikoje? Je waliokuja wakiwa wengi watawanyima wenyeji haki zao? Natumai haya ndio masuala ambayo Mswada huu ulitakiwa ufafanue ueleze na uweke baana wazi wazi usawa uko wapi. Lakini kwa sababu tunazitunga sheria hizi tukitumia lugha ya Kiingereza inakuwa shida kwa wenzetu kuona kuwa Mheshimiwa Mwadime analenga wenyeji wa taifa ili wasipokonywe ardhi ambayo wanaitumia. Naomba tumuelewe Mheshimiwa Mwadime kikamilifu.
Mheshimiwa Naibu Mwenyekiti wa Muda nakubaliana na marekebisho hayo Hatutaki Serikali kuu ikae ikiotea miradi na kuamua kuwa miradi mikubwa inaweza kuiotea na kuifanya wakati wowote ule ili wananchi na wanauma wote wajue kuwa muradi ule utafanywa na Serikali kuu
Mheshimiwa Naibu Mwenyekiti wa Muda ninayapinga vikali mabadiliko yanayoletwa kwenye sheria hii. Waziri wa Afya na Waziri wa Ardhi wanapewa nguvu ambazo haziko katika Katiba. Ibara ya 67(2) (a) ya Katiba inaeleza kazi ya National Land Commission (NLC). Inasema kuwa NLC inatakikana kusimamia ardhi za umma kwa niaba ya Serikali ya kitaifa na serikali za kaunti. Pia Ibara ya 67(2)(c) ya Katiba inasema kwamba NLC inatakikana kuishauri Serikali ya kitaifa kuhusu masuala ya kuandikisha ardhi. Kwa hivyo mabadiliko yanayoletwa kwenye sheria hii yanampatia Waziri wa Ardhi nguvu ambazo haziko kwenye Katiba ya nchi yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika kuweka wazi wacha tuseme "iwapo Bunge hili litapitisha Hoja hii ambayo tulileta wiki iliyopita". Kwa ufupi Hoja hii itasaidia mwananchi wa kawaida katika masuala ya gharama ya maisha kwa sababu sisi Wabunge hatuna mamlaka dhidi ya mambo fulani yanayotendeka katika taifa hili. Kwa mfano swala la afya liko katika ugatuzi. Ni swala ambalo wahusika wakuu katika kaunti ni magavana ambao wanafaa wasaidie katika mambo haya lakini sio wote. Wengine wamezembea katika majukumu yao hivyo basi kutuletea kazi kubwa zaidi. Wiki iliyopita sikuweza kugusia mambo mawili. Katika Hospitali ya Kitaifa ya Rufaa ya Kenyatta kila wadi ina vitanda vinne. Kwa ujumla hospitali iko na wadi kama 50. Asilimia 78 ya Wakenya hawawezi kulipa kwa sababu katika wadi hizi utapata watu wanalazwa chini hawapati dawa na kuna uhaba wa madaktari. Kwa hivyo chanzo kubwa kabisa kinachosababisha vifo ni uzembe katika Serikali kuboresha sekta ya afya. Kwa mfano Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta pekee inapoteza Kshs600000 kwa siku kwa watu wasioweza kulipa kwa sababu ya maradhi kama vile saratani au figo. Katika mradi wa Linda Mama Serikali inawajibika na kulipia akina mama ada ya Kshs17000. Swali tunalofaa tujiulize ni kwamba katika huu mradi wa Linda Mama je ikizidi Kshs17000.
Mheshimiwa Naibu Spika naelewa mjadala kuhusu kupunguzwa kwa siku 14 hadi siku moja. Ingawa hivyo imenilazimu nizungumze namna hiyo kwa sababu kama usambazaji wa matokeo ndiyo ulileta shida basi tuzungumzie suala hilo. Uchumi umeenda chini kwa sababu ya siasa yetu. Tukae pamoja na tusilete mambo ya NASA ama Jubilee hapa. Sisi tumechaguliwa ili tutengeneze sheria ambayo itatusaidia. Mwisho ingawa unasema nimetoka nje ya mambo tunayojadili ningeomba wana NASA waheshimu akina mama. Ninajua wanatatizo na akina mama hata principal wao mmoja hupigwa na akina mama. Sisi tuna heshima.
Mheshimiwa Naibu Spika nakushukuru kwa kunipatia nafasi hii ili nitoe mchango wangu kwa Mswada huu wa Mapato. Huu ni Mswada muhimu sana kwa nchi yetu na unafaa uangaliwe kwa makini sana. Kila Mbunge anahitajika na anatakiwa atafakari ni wapi Mswada huu unatupeleka na matokeo yake yatakuwa yapi. Nikitoa maoni yangu kuhusu Mswada huu naomba nichukue nafasi hii kwanza kukishukuru chama changu cha Orange Democratic Movement (ODM) na muungano wa CORD kwa ujumla kwa kunitunukia nafasi ya kuwa kiranja wa walio wachache Bungeni na walio wengi nchini. Hii ni kwa sababu sisi ndio tulio wengi nchini lakini hapa Bungeni tuko wachache. Natumaini kwamba ndugu zangu wa muungano wa Jubilee wanaelewa huo msimamo.
Mheshimiwa Naibu Spika naomba kusimama kwa hoja ya nidhamu. Je Mheshimiwa anayezungumza hivi sasa ana haki ya kuzungumza yale anayosema kuwa tunachukua hundi ya Hazina ya Ustawishaji Maeneo Bunge na kuipeleka nyumbani? Nani anapeleka hundi ya Hazina ya Ustawishaji Maeneo Bunge nyumbani? Labda ni maongezi yake ya mwanzo. Naomba afafanue.
Mheshimiwa Naibu Spika nilipopata jawabu hii jana niliwasiliana na familia Nasikitika kuwa dadangu amepewa karatasi asome lakini sivyo ilivyo Kwanza majina yaliyo hapa si yale niliulizia Pili ikiwa ni wizi tujaribu kuwaza Fedha ambazo zinazunguka katika duka lile hazipiti hata Ksh20000 Watu waliingia na AK-47 kuiba kutoka kwa duka ndogo sana la M-PESA Tatu kama ni kweli uchunguzi unafanywa mpaka leo Statement ya Sadat haijachukuliwa Viongozi wa Wizara hawajui kile ambacho wanachokizungumza Wamesema kwamba wale ambao walimiminiwa risasi walipelekwa hospitali ya Coast General ambayo ni uongo Hawakupelekwa huko Mhe Naibu wa Spika Wale waliathirika walipelekwa katika hospitali ya Memon ambayo iko karibu Baada ya hapo walipelekwa katika hospitali ya Aga Khan Wametaja hapa kuwa kuna namba ya Occurrence Book (OB) Lakusikitisha ni kuwa hakuna mmoja wa wale wanafanya kazi katika eneo hilo waliopigwa risasi ama familia zao ambao Statement yao zimechukuliwa Licha ya hivyo walijipeleka kusema kuwa wanataka kupiga ripoti ya masuala haya Waliambiwa kuwa ripoti tayari imepigwa wakae kado Mwishowe nikimalizia kuna huu mwenendo wa Katiba 2010 ambao Waziri anaandika ripoti kisha anampelekea Mjumbe kuisoma Nasikitika itabidi waregeshe tena suala hili ili wajue ukweli Mwisho wamesema post-mortem ilifanywa Hakuna post-mortem yeyote ilifanywa kwa marehemu Kwa hivyo nasikitika kwa sababu itabidi dadangu ambaye yuko katika Kamati ambayo inahusika arejee tena kuambia Serikali kuwa kuna kiwango ambacho watu wanaweza kuhadaiwa
Mheshimiwa Naibu Spika ningependa kuungana na wenzangu ambao wameunga mkono Mjadala huu vilivyo. Sera ni kanuni ambazo zinatusaidia kufanya uamuzi ulio bora. Hatuwezi kuwasaidia wazee wa mtaa kama hakutakuwepo na sera ambazo zitawalinda na kuwafaidi. Ili kuwasaidia wazee ni lazima tuwe na sera ambazo zitakuwa sheria na zitafuatwa kikamilifu ili baada ya Serikali yoyote kuingia ama kutoka tutakuwa tumeweka sera ambazo zitawasaidia wazee. Tunahitaji sera ambazo zitakuwa sheria ili Serikali iwajibike kwa ajili ya wazee. Tusipokuwa na sera itakuwa vigumu kufanya Serikali kuwajibika. Hiyo ndiyo sababu Bunge hili lazima litengenenze sera ili Serikali isipowalipa wazee tunaweza kuipeleka Serikali kortini kwa sababu tutakuwa na sera ambazo tumeziweka. Sera hizi zitashughulikia mahitaji yote ya wazee. Hawa wazee wanafanya kazi kubwa sana katika vijiji vyetu. Hawa wazee ndio hakimu katika vijiji wanatoa uamuzi ulio bora na wanaleta ai katika vijiji. Sera hizi ambazo tunaziweka katika Bunge hii lazima ziwasaidie wazee hao. Sio tu fedha peke yake. Tunataka Serikali iweke sera ambazo zitazawadi wazee hao. Kuna wengine ambao hawajawahi kufanya kazi maisha yao yote na hawana bima ya maisha na pesa za uzeeni. Kwa hivyo tukiajiri hawa wazee itabidi Serikali pia iwazawadi kwa kuwapatia mashamba ili wajijengee nyumba ama Serikali iwajengee ili waishi maisha ambayo ni mazuri. Mhe. Naibu wa Spika wa Muda serikali ya ugatuzi imefanya kazi iwe rahisi kwa sababu imeajiri wawakilishi wa wadi. Kuna wawakilishi wa wadi na hiyo imefanya serikali ya kaunti kuhudumia wananchi. Nina mfano mzuri katika kaunti ya Turkana ambayo imeajiri mwakilishi wa wadi ambaye ni ward administrator . Sasa hivi County assembly imepitisha sheria.
Mheshimiwa Naibu Spika ukiona watu wanapiga kelele basi wana akili ndogo. Aliye na akili kubwa hawezi kupiga kelele ambayo inapigwa sasa hivi. Mimi nataka kusema bila kuogopa kuna nia mbovu ya kupunguza muda wa kuchapisha Miswada hii. Kwa sababu ya hiyo nia mbaya tunawaambia kwamba: Nyinyi mmeanza lakini chuma ki motoni na tutahakikisha kwamba hamna sababu ya mtu yeyote kutufanyisha biashara mbaya. Kwa hivyo ndungu zangu wa Jubilee tunawaonya mapema tu kwamba hamtutishi hatutishiki na hatutakubali. Nataka kuwaonya mapema. Sasa ndio mtajua kwamba kiko motoni na hakuna mchezo. Hatuchezi na nyinyi. Sasa tumeanza. Nchi hii lazima tutailinda kuliko mnavyodhania.
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda Kiswahili kitukuzwe Tumetoka kwenye mapumziko na tukaitwa hususan kwa kikao maalum Kwa hivyo hapo hakuna hoja ambayo inatatiza Labda pia ningekushauri ukapata mafunzo ya darasa la Kiswahili maanake ni lugha ambayo inatambulika na inaeleweka kikatiba Wananchi katika taifa letu wametupa nguvu zao kuweza kuwasemea katika Bunge hili Leo wananchi wanaumia na ugonjwa wa korona na Oxygen katika hospitali zetu hakuna Watu wamechukua loans na wanakufa na depression Watu wana mizigo mikubwa Leo sisi tunakuja hapa kuzungumzia Bill ambayo kwanza inaongezea mzigo Wanjiku ambaye tayari saa hii ana mzigo wa kutulipa mishahara sisi Wabunge 416 Tunazungumzia kumwongezea mzigo wa 650 wa Wabunge Wabunge tunaupata mshahara wetu kikamilifu Lakini walioko kule nje wanaumia Ukiangalia biashara ya utalii na Transport Industry utapata watu ambao wamefinyiliwa Sekta nyingi za watu ambao wanafanya biashara katika nchi hii ya Kenya zimeumia Ni mikakati gani ambayo sisi kama Bunge ama kama taifa kwa niaba ya mwananchi wa chini tumeweka? Ukiangalia hakuna Bibilia inasema katika Kitabu cha Mathayo 6:33 kwamba tuutafute ufalme wa mbinguni na vyote tutaongezewa Lakini katika taifa la Kenya tunasikia kwamba tutafute BBI na mizigo yote tutaongezewa Tutaongezewa ushuru kwa sababu ya kuwalipa Wabunge 650 Tutaongezewa mizigo ya kodi Ni jambo la kusikitisha sana Tunapokaa hapa Waheshimiwa nawaomba tufikirie mwananchi kwanza Mimi naamini kwamba hakuna aliyesema anahitaji Wabunge 650 katika Bunge la Kumi na Tatu linalokuja Ndio maana tunasema Mswada huu au Ripoti hii ni ya kukataliwa Ninaamini Wananchi kule nje wananiona Tukipitisha watakaoumia ni wananchi Sisi tutakuwa starehe hapa hata kama tuko mia saba na watatulipa Kwa hivyo mimi nataka niseme kuwa wananchi kule nje wajipange na wajue kwamba huu ni mzigo wao Sio mzigo wa Wabumge ambao wamekaa starehe ndani ya Bunge hili letu la taifa Kwa hivyo mimi ninataka kusema kuwa jambo hili litawarudia wananchi Ninataka kuongee na taifa kwamba hakuna atakayeweza kuutoa huu mzigo kwa wananchi isipokuwa wao wenyeye
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda Mwenyekiti anaunga huu Mswada mkono au anaupinga? Ni kwa sababu simuelewi.
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda nami pia nataka kuchukua fursa hii kuwapongeza Mheshimiwa Alex Mwiru pamoja na timu yake ya Kamati ya Ardhi ambao wamefanya kazi nzuri sana na haswa kuweka masaa mengi kuweza kutekeleza kazi hii. Vile vile ningependa kuwapongeza ndugu zangu wote Wabunge kwa ujumla na haswa Wabunge kutoka Pwani ambao pia wamelivalia njuga jambo hili kuhakikisha kuwa wameweza kufanya kazi kwa pamoja na kufikia uwiano na kukubaliana kuwa masuala haya ni mazuri. Tuweze kuyaangalia tukiwa pamoja na tukubaliane. Tunafahamu ya kwamba suala la ardhi ni suala ambalo limekuwa kidonda sugu hapa nchini na haswa maeneo yetu ya Pwani ambapo suala kubwa ambalo limekuwa likikera kila mtu ni suala la mashamba. Ningetoa mfano tu. Katika Katiba ile ya kitambo tuliyoiondoa mwaka wa 2010 wakati huo hata Taita Taveta ilikuwa imetajwa pale kwa masuala haya ya ardhi za kijamii. Tulikuwa na wasiwasi sana kuwa sasa hivi vile jina letu limeondoka kwenye Katiba suala hili litakuwa vipi. Tulivyokuwa Bunge la Kumi tulivyokwenda Mombasa kuweza kukubaliana kama Wabunge hatukuweza kukubaliana maanake kila mtu alikuwa anamuangalia mwenzake na kumuota kidole akiwa na wasiwasi kuwa je hawa wanafikiria nini ama wanatupangia njama gani? Hivyo basi sheria hii ikishakubalika na ninaomba na nitashukuru ya kwamba Bunge la Seneti halitakwenda kubadilisha masuala haya mengi ambayo yamezungumziwa itawezesha Wakenya kusonga mbele na haswa kutuliza kidonda hiki ambacho kimekuwa kikikera Wakenya wengi. Natoa shukrani kwa Wabunge wote kwa kazi nzuri ambayo wamefanya na haswa wewe kwa kuweza kukaa mpaka saa hizi saa za usiku ambapo ungekuwa umeenda nyumbani tayari kufanya shughuli zako zingine kwa sababu jamii pia zinangojea. Ninawashukuru wenzangu wote ambao tumekaa hapa mpaka sasa hii. Sheria hii itatuwezesha kama Wakenya kuweza kusonga mbele. Naunga mkono.
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda naomba kuondoa hoja hiyo lakini kwa wanaoshika ofisi za kikatiba Bunge huwa linapitisha majina matatu na Rais anachagua jina moja miongoni mwa hayo matatu.
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda nashukuru sana kwa nafasi hii ili niunge mkono Hoja hii iliyoletwa hapa na Mhe. George Murugara. Hii ni Hoja ambayo imenifurahisha sana. Kule vijijini tunakotoka watu wanaohakikisha kwamba ai inadumishwa na kuhakikisha kwamba jamaa wetu wanaishi katika hali ya heshima ni wazee wa Nyumba Kumi au liguruu . Tunaunga mkono Hoja hii ili Serikali kuu iwajumuishe kwenya orodha ya wafanyikazi wa umma wanaolipwa mishahara. Niruhusu niseme kwamba hawa watu wetu ni lazima walipwe mishahara kila mwisho wa mwezi. Hii ni kwa sababu kazi ambazo wanafanya pale chini ni kazi ambazo ni za kudhalilishwa tu. Hawa wazee walipwe kila mwezi na tunapoongea juu ya hawa village elders lazima tujue ya kwamba hawa viongozi wetu ambao ni wazee wa Nyumba Kumi wao pia ni wamama wa Nyumba Kumi. Unapoona vile tunaongea tunasema tu juu ya wazee wa Nyuma Kumi na hii ni jinsia moja. Tukiendelea kujadiliana tuhakikishe kwamba hata wamama pale nyumbani wanahusishwa kama viongozi wa Nyumba Kumi ili tuwe na gender balance kwa sababu hii ni kazi muhimu. Leo nimefurahi kwa sababu tunapatia kipao mbele watu ambao kwa muda mrefu hawajashughulikiwa Huwa hatupati nafasi ya kuongea kuhusu watu walio huko chini. Katika kaunti zetu gavana huwa na structure yake ya ward administrator na sub-county administrator lakini wale wako huko chini huwa hawashughulikiwe na kaunti. Kwa hivyo Hoja hii ni muhimu kwa sababu itahakikisha kwamba Serikali kuu itaweza kuwapatia village elders wazee na wamama.
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda nasimama kwa suala la nidhamu. Ile lugha ambayo Mheshimiwa Mwinyi ametumia si lugha ya Bunge. Ni lugha isiyo ya ustaarabu. Amesema kwamba wengine wetu hapa wakiingia chooni hawafungi milango. Hiyo ni aibu kubwa sana. Kama suala hilo lipo katika Ripoti ni sawa. Lakini kama halipo kwenye Ripoti atoe hoja hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda nilikuwa nikizungumzia waendeshaji boda boda. Ni jukumu letu kuhakikisha kwamba sheria za barabarani zinaheshimiwa. Mara nyinyi sisi wananchi tunatazama tu boda boda mmoja akibeba zaidi ya watu watatu wanne ama watano. Ni kweli tunataka vijana wetu wapate pesa lakini polisi wa trafiki nao wanaangalia nini? Ajali inapotokea na watu kufariki unakuta badala ya kufa mmoja ingawa hatuombei wafe watakufa sita na hiyo inatokana na uzembe uliyoko katika upande wetu wa trafiki.
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda ningependa kuchukua nafasi hii kumshukuru Mheshimiwa Wanjiku kwa kuleta Hoja hii. Tunapinga pombe haramu kwa uwezo ambao tulionao na kwa lugha yote tunayoweza. Ningependa kusema mambo mawili. Jambo la kwanza ni kuwa kuna askari ambao wamechukua nafasi hii kunyanyasa wananchi. Wanaenda kushika wenye pombe lakini pia wanawanyanganya pesa na kuwaharibia mali yao. Lazima tuchunge askari kama hao ambao wananyanyasa wananchi. Jambo la pili nikuwa kuna watu wa aina mbili katika jambo hili. Kuna watu ambao wanatengeneza pombe kwasababu ni maskini. Pia kuna watua mbao wanakunywa pombe kwa sababu wana pesa. Ningependa serikali za kaunti na Serikali Kuu zihakikishe kwamba kuna njia ambazo zinasaidia watu ambao wanatengeneza pombe kujimudu kimaisha. Ni njia moja kusimamisha watu wasikunywe ama wasitengeneze pombe lakini ni njia nyingine uchumi wa sehemu hiyo uangaliwe kwasababu kuna watu ambao wanatengeneza pombe kwa sababu ya umaskini. Ni bora serikali za kaunti na Serikali Kuu zijaribu njia za kusaidia watu wa namna hiyo ili wajimudu kimaisha. Nikimalizia ningependa kukubaliana na wengine kwamba hili jambo ni janga. Kwa hivyo ukitoa mtu katika shida lazima pia uwe na njia ya kumsaidia kujimudu kimaisha. Leo huyu mtu ameacha pombe lakini kesho atarudia pombe. Kwa hivyo ni vizuri hao watu wapelekwe katika shule ama mahali pa kupatiwa mawaidha pole pole na waache pombe. Kwa hivyo ninaomba Serikali ifungue vituo vya kuwasaidia hao watu na wapatiwe ushauri ili wawe watu wazuri. Ninaunga mkono Hoja hii. Asante
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda ningependa kukushukuru kwa kunipatia nafasi hii ili niungane na wenzangu kuunga mkono Mswada huu wa barabara. Barabara ni muhimu katika nchi yetu ya Kenya. Maisha ya mwanadamu yanaenda pamoja na barabara. Ninasema hivyo kwa sababu pasipokuwa na barabara nzuri hata ugonjwa ukitokea watu wengi huangamia. Ninaposema hivi asilimia kubwa ya barabara katika nchi hii ziko katika hali mbaya. Tunapoangalia sehemu nyingi katika Kenya tunaona kwamba watu wengi hutatizika na hata vyakula kuharibika wakati wa mvua kwa sababu ya barabara mbaya. Unakumbuka kwamba mara nyingine mitihani inachukua muda na inakosa kufanywa siku ile imepangwa kwa sababu ya kutokuwa na barabara nzuri katika sehemu ile. Kuna barabara nyingi huko Pokot lakini ni barabara moja tu ambayo iliwekwa lami kitambo. Hii barabara inachukua sehemu kubwa ya hiyo nchi. Barabara ya Kitale hadi Lodwar imeharibika sana. Katika Chesegon wale ambao wamepewa kazi ya kujenga barabara hawafanyi kazi vile inavyotakikana. Ninataka niseme kwa ukali kidogo kwa sababu barabara hii ambayo imepewa kandarasi juzi ni muhimu. Inaunganisha Kaunti za Pokot Turkana na Marakwet. Hii barabara inachukua vyakula vingi kutoka Marakwet na Pokot na hata wananchi kutoka Turkana hutumia barabara hii. Tumesikia kwamba kuna wale ambao wamepewa kandarasi ilhali miezi mingi imepita na kazi haijaanza. Tukiangalia mambo ya daraja tunakuta kwamba watu wanafariki nyingine ya mto kwa sababu ya kutokuwa na daraja. Akina mama wengi wamepoteza maisha yao wakati wanajifungua kwa sababu ya barabara mbovu na hawawezi kufikishwa hospitalini. Miezi miwili iliyopita tulipoteza mwalimu wa Shule ya Msingi ya Lomut kwa sababu hawangeweza kumvukisha mto kwa sababu mvua ilinyesha. Kulikuwa na gari upande huo mwingine wa mto lakini mwalimu alifariki kwa sababu gari halingepita. Ningependa kuungana na wenzangu kwamba ni sharti Serikali itilie mkazo barabara ambazo inasimamia na kuzitengeneza. Ningependa kupongeza Kaunti ya Pokot kwa sababu wametengeneza barabara za mashinani. Jambo hili limesaidia kuimarika kwa usalama wa eneo hilo na hivi sasa tuna usalama baina ya Turkana na Pokot. Ninaamini tutapata barabara nyingi zaidi. Ningependa kuzungumzia juu ya wale ambao wanapewa kandarasi. Kazi nyingi zinarudiwa kwa sababu wale ambao wanapewa kandarasi hawafanyi kazi nzuri. Tunaporudia ile kazi tunatumia pesa za Serikali. Inafaa wale ambao wamepata kandarasi watengeneze hizo barabara kwa njia ambayo itafanya barabara zidumu kwa muda. Barabara nyingi hutengenezwa kiholela na mvua inaponyesha zinaharibika na pesa za nchi zinatumika kuzirekebisha. Serikali ya Jubilee imejaribu na ninatumai tutaendelea kufanya kazi nzuri zaidi kuliko ilivyo sasa. Kule Pokot tumeahidiwa kutengenezewa barabara tatu na ninaamini kuwa zitatengenezwa kwa muda mfupi ili zisaidia wananchi kusafirisha vyakula vyao. Katika eneo la Pokot Kusini kuna vyakula vingi haswa maziwa. Maziwa na matunda huharibika kwa urahisi. Barabara inapoharibika na magari yanapokwama vyakula vyote vinaharibika na jambo hili husababisha hasara na uchumi kuharibika. Wananchi wanaumia kwa sababu wanategemea mapato kusomesha watoto wao. Barabara ni maisha ya wananchi na wasipotengenezewa barabara nchi haiwezi kusonga mbele. Wananchi hawawezi kufanya biashara kama barabara ni mbaya. Mhe. Naibu Spika wa Muda ninaunga mkono Mswada huu.
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda ningependa kutoa shukrani kwa wakati huu ambao nimepewa kuunga mkono Mswada huu. Ni maoni yangu kuwa pale ambapo kuna vipengele ambavyo vinahitaji marekebisho vifanyiwe marekebisho ili angalau tupate sheria ambazo zitadumu. Wakati umefika kwa sisi kuangalia kuwa wakati wa uchaguzi wale ambao wanafanya dhambi wakati wa uchaguzi nao pia waadhibiwe vilivyo. Ningependa kuunga Mhe. Millie Odhiambo mkono kuwa lazima tuhakikishe tunapofanya mchujo atakayepewa tiketi ya chama akifanya makosa lazima ahusishwe katika dhuluma ambazo zimetajwa na vipengle hivi ili aadhibiwe kwa mujibu wa sheria.
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda sijaona hizi karatasi kwenye mtandao. Kama utaniruhusu mara nyingi hakuna makaratasi yenye kufai hizi ripoti katika lugha ya Kiswahili. Wengi wa wananchi kule tutokako hawajui Kiingereza. Ningeomba Bunge ifahamu kuwa Kiswahili ni lugha ya taifa na iwe ikitufaia taarifa zote zinazokuja Bungeni. Kama Wabunge wengine ningependa kuiunga mkono Hoja hii kuhusu kuendeleza maswala ya Pwani. Ningependa kuongeza kuwa ni muhimu vyombo tofauti vya Serikali vikija pamoja kuleta miradi vihusishe wananchi katika mambo wanayotaka kufanya na wawe wakiwashauri. Wananchi mara nyingi huamka tu asubuhi na kuona mabadiliko. Hawakuhusishwa katika mabadiliko hayo wala hawajui kitu gani kinaendelea. Naunga mkono Hoja hii kwa sababu maisha ya watu wa Pwani yataendelezwa kwa kufanya miradi tofauti tofauti ya kuleta maendeleo katika sehemu hiyo. Ni aibu kuwa nchi ya Kenya inashindwa na nchi ndogo kama vile Mauritius ambayo imeendelea sana katika maswala ya uvuvi ilhali ni nchi ndogo sana na yenye watu wachache sana; ni lazima tujiendeleze. Pia nimegundua kuwa mara nyingi Serikali haiwaajiri watu wa Pwani wala haihusishi watu wa Pwani katika miradi ya Pwani. Nilienda mkutano kule Mauritius na kati ya Wakenya 11 tuliosafiri mimi pekee ndiye nilikuwa nimetoka Pwani. Sikutoka katika Wizara. Ulikuwa ni mkutano wa Wizara. Yaonekana kuwa kwa sababu watu wa Pwani hawahusishwi sana katika maswala ndio sababu tangu tupate Uhuru maswala ya uvuvi yamekuwa nyuma sana. Hii ndio maana tunapitwa na nchi nyingine kama Norway nchi ndogo sana lakini katika ulimwengu mzima ndio ya pili katika kuuza samaki. Ya kwanza ni nchi ya Uchina. Hapa Kenya tunaweza kupunguza umaskini ikiwa tutazingatia mambo yaliyotajwa katika hii Ripoti. Isiwe tu ni ripoti ambayo itakaa na kupata vumbi lakini iwe Ripoti ambayo mambo yake yatafuatiliwa. Jambo lingine ni kwamba katika bajeti za masuala ya uvuvi na kadhalika pesa nyingi sana huwa zinaenda kwa utafiti. Mwaka baada ya mwaka Bajeti ikitengenezwa hata tukijaribu kushindana pesa nyingi sana zinaelekezwa kwenye utafiti. Saa hii tunataka pesa zielekezwe katika masuala ya maendeleo kwa sababu baada ya miaka hiyo yote hatujaona faida ya huo utafiti. Kitu kingine ni kama alivyozungumza Mhe. Mwanyoha uchimbaji wa mchanga umefukuza samaki na wavuvi hawana njia nyingine ya kupata pesa. Umaskini umezidi sasa. Mashirika ya kusimamia ufuo wa bahari pia yameachwa peke yao. Hawashugulikiwi na Serikali. Pesa haziko ilhali wanafanya kazi nzuri. Kumalizia nashukuru sana Mwenyekiti na wanachama wa Kamati hii kwa kuleta Hoja hii.
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda tulikuwa tunazungumza kuhusu vitambulisho. Namshukuru Mheshimiwa Chris Wamalwa kwa sababu watoto kutoka eneo letu haswa la Trans Nzoia wako na shida sana. Tumeongea kuhusu mambo ya walemavu. Hao walemavu pia hawapati nafasi ya kupata vitambulisho. Tukiwa na ofisi kule mashinani itatusaidia sana ili watu wapate vitambulisho kwa muda unaofaa. Tuna pesa ambazo tumepewa kama akina mama. Akina mama wenzetu hawapati pesa hizo kwa sababu hawana vitambulisho. Vitambulisho vikipeanwa kule mashinani vitawezesha watu hao kupata nafasi na pia kula "keki" ya nchi hii.
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda wacha nione kama ninaweza kufanya vizuri zaidi kuliko Mheshimiwa ambaye ametangulia. Ningependa kutoa maoni yangu kuhusu maswala haya ambayo yametokea kuhusu Makatibu wa Wizara kuja mbele ya Kamati ya Bunge - Kamati ambayo imeteuliwa ili kujihuzisha ama kuwahuzisha Wabunge wote ili waje waelezwe waziwazi yanayojiri katika Wizara zao. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kabla zijaenda mbali naomba kuchukua nafasi hii kwa heshima yako nitoe rambirambi zangu kwa mwanakenya Professa Ali Mazrui ambaye ametuacha akiwa ni mtu mwenye sifa ambaye ameheshimika ulimwengu wote mzima na amepatia nchi hii sifa. Naomba mwenyezi Mungu aiweke roho yake pahali pema peponi. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda Spika ameeleza wazi kuwa kukutana na Makatibu Wakuu hapa hakumaanishi kuwa wanaingia Bungeni. Ni sababu tumekosa sebule kubwa ambapo tunaweza kukutana na wao vile wanavyokutana na kamati kila wakati. Tungekuwa tuko na nafasi kubwa hatungekutana hapa. Tungekutana pahali pengine lakini kwa sababu hiyo imebidi waje hapa. Swala la kushangaza ni huu uoga umetokea wapi? Kama Katibu wa Wizara Mhesimiwa Charity Ngilu amekuja hapa akajieleza na wenzake wawili walionekana hapa basi kilichowafanya watoweke ni nini? Ni uoga ama nikutuheshimu Bunge ama nini kimetokea? Ndio maana nilikuwa naomba Kiranja wa Walio Wengi Bungeni na Walio Wachache Naomba nifafanue sisi mrengo wetu mnatuita wachache hapa Bungeni lakini uko nje ndio tulio wengi. Kwa hivyo Kiranja wa Walio Wengi ndani ya Bunge ningeomba afafanulie Bunge ni nini kimewafanya hawa wenzetu Makatibu wakaondoka bila kuja kufafanulia Bunge yale ambayo walikuwa wameitiwa. Hata kama walikuwa wanaondoka wangeomba radhi. Wangeeleza "mna mambo yametokea dharura na inatubidi tuondoke na tunaomba msamaha ili tuje wakati mwingine tujieleze yale ambayo yametuvika". Wamepotea hivi hivi. Je ni watu wenye nidhamu ama ni watu tuu wanachukulia Bunge kama ni kitu ama ni watu wanakutana tuu kupoteze muda? Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda ni ombi langu kuwa hawa waje tena wajieleze na wachukuliwe sheria za kinidhamu. Mwenzangu Mheshimiwa Nyokabi alisema kuwa Serikali hii ya Jubilee iko katika nguzo za uwajibikaji na uwazi. Nashukuru na ni vizuri. Kama iko katika nguzo za uwajibikaji na uwazi mbona watu wao hivi leo asubuhi wakaogopa kuja mbele ya kamati ya Bunge? Walikuwa wamepata wakati unaofaa waje wajieleze na waonyeshe kuwa Serikali ya Jubilee imefanya hili na inataka kutekeleza haya na hatufichi chochote lakini huu uoga umetokea wapi? Ni nini wanachoficha? Nakubaliana na Mheshimiwa ambaye amesema hata hizi kamati za Bunge ambazo tumeziunda wakati mwingine lazima ziwe zenyewe zina sifa. Wale ambao wamepelekwa kamati fulani kama ni kamati ya sheria je tuko na wanasheria wangapi pale ili waweze kuingia kina cha kisheria na waweze kuwauliza hao maswali? Mara nyingi unakuta tumepeana kamati na yule ambaye amepelekwa kwa kamati fulani hana ufahamu uwezo na majukumu. Anaenda tuu pale kujionyesha kisha anaondoka. Naomba tuchukue nafasi hii hata hizi kamati nazo tuziangalia upya na tuone ni wapi watu wanaweza kuwajibika. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda nashukuru Mheshimiwa Ngilu kwa kuja hapa lakini wakati huo alipokuwa anajibu yale yalikuwa yanakuja kwangu ni "Karen kuna utata". Wao wenyewe wamesema hii ardhi ni ya mtu mwingine. National Land Commission imesema hii ardhi ni ya mtu mwingine. Ukweli uko wapi? Wakati kama huu vile Mheshimiwa amesema ni mchache mno wakuweza kutoa maswala kama haya bayana yakabainika waziwazi kuwa yanaweza kujibiwa. Kwa hivyo tunaomba ijapokuwa muda huu umetolewa kamati pia ziendelee na kazi zao ambazo zinahitajika kufanya. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda tulikuwa na kikao hapa Jumatatu iliyopita ambacho kiliandaliwa na Mheshimiwa Spika. Makatibu wa Wizara wakaja wote na wakaelezwa kwa nini tumebadilisha sheria zetu za Bunge. Wanakuja kwa kamati andalizi ya Wabunge wote ili wajieleze. Wakafafanuliwa kila kitu. Jana na leo katika magazeti tunasoma kuwa mmoja wa Makatibu ambaye ni kinara wa Jubilee anawaomba hawa Makatibu wa Wizara wasije Bungeni. Yeye mwenyewe kwa nini awaelekeze? Kwa hivyo kuna utata mkubwa ambao tungeomba Bunge iutatue. Inafaa wafahamu kuwa wakija hapa ni kujibu maswala ambayo Wabunge wangependa yafafanuliwe. Kwa haya mengi Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda naomba kuweka tamati.
Mheshimiwa Naibu wa Spika wa Muda sisomi lakini kuna vidokezo ambavyo ninatoa. Ni vile nimeshika karatasi mkononi na ukisema niiweke chini nitafanya hivyo lakini inanisaidia. Nataka kusema kamati ya afya katika Bunge hili tafadhali badala kuenda kujifunza mambo ya afya kuzunguka katika hospitali za nchi nyingine kujifunza mambo yanayohusu afya ni muhimu watembee Kenya. Ni aibu sana usikie mwananchi wa Kenya amechukua hatua ya kuiba mtoto wake akitumia mfuko. Hiyo ni aibu kubwa sana sio kwa mzazi pekee bali hata kwa sisi wote viongozi. Kwa hivyo kama tungekuwa na utaratibu wa vile tunaweza kuwa na wanakamati ambao wanaangalia Wakenya ambao hawawezi kulipa ada zao kwa sababu hawana pesa na wamempoteza mgonjwa wao ama mwingine amepona na hawezi kuondoka kwa hospitali kwa kukosa pesa... Kwa hivyo ni jukumu letu sisi wote kuangalia kwamba wakati Hoja kama hii imeletwa katika Bunge hili itekelezwe. Ninaomba Kamati Tekelezi iangalie kwa umakini. Kuongea na kuwakilisha shida za wananchi Bungeni ni tofauti na kutekeleza. Mambo mengi yameongewa na Wabunge wenzangu ambao nataka kuwapongeza sana lakini shida ni vile itatekelezwa. Kwa hivyo Bunge la Taifa tuko na nguvu na uwezo wa kupitisha sheria ambayo inaweza boresha afya katika nchi yetu ya Kenya. Mhe. Naibu Spika wa Muda utakubaliana nami kuwa wananchi wengine hapa Kenya wanaamua kuenda hospitali za kibinafsi na wanalipishwa pesa ambazo zinashangaza. Hawalipishi kwa mashilingi au maelfu wanalipishwa kwa mamillioni. Mtu akikaa kwa wiki moja ama mbili anapelekwa mbio mbio wadi ya mahututi (ICU) na analipishwa pesa nyingi. Mtu akifa anawekwa na mwili hauwachiliwi mpaka pesa zilipwe. Wananchi wa Kenya wanataabika sana. Sisi kama Bunge tuangalie mambo ya afya katika nchi yetu ya Kenya. Serikali ingekuwa na jinsi ya kuweka utaratibu wa mambo ya hospitali za kibinafsi. Kwa sababu wanalipisha pesa nyingi sana ilhali haijulikani wanalipisha nini. Kamati ya Afya katika Bunge hili wanapaswa kuangalia vile hizo hospitali za kibinafsi hulipisha wagonjwa. Hii ni kwa sababu Wakenya wamefinywa sana. Imefika mahali hatuwezi kunyamaza kama Wabunge. Hoja imeletwa hapa na Mbunge ambaye alifikiria vizuri na ninampongeza. Tumefurahi kama Wabunge wenzake na tumechangia. Pia nawapongeza sana wale Wabunge ambao wameongea mbele yangu. Kwa hayo machache Mhe. Naibu Spika wa Muda naunga mkono. Asante sana kwa kunipatia nafasi ya kuchangia hii Hoja.
Mheshimiwa Sonkok or Sankok
Mheshimiwa Spika asante kwa kunipa nafasi hii. Naomba niunge mkono Hoja hii tukiangalia kuwa tarehe 23 mwezi wa Mei itakuwa ni siku muhimu sana kwa Wabunge ama watu wote ambao wanatarajia kuomba viti tofauti tofauti tukianzia na cha ugavana - ambacho nitakuwa nakiomba kwa watu wa Taita Taveta - maseneta wabunge na wabunge wa kaunti. Mhe. Spika ni muhimu tuwapatie Wabunge nafasi wahudhurie vikao hivyo kwa sababu ni mengi yatakuwa yanaelezwa. Wasipopata maelezo sahihi siku hiyo huenda wengine wakashindwa kuwasilisha makaratasi yao ama vyovyote ambavyo vinahitajika na IEBC siku hiyo. Kwa hiyo naomba tukubaliane zote Wabunge kwa kauli moja bila kupinga tusiwe na kikao hapa Bungeni siku hiyo. Tupatiwe nasafi twende mashinani twende kwa kaunti zetu; tuelezwe wazi wazi ni nini kinahitajika. Ukiniambia niwe Bungeni siku hiyo na mimi natarajia kuwa gavana wa Taita Taveta - na wenzangu hawa wote wanatarajia wawe magavana ambao wanastahili - si vyema. Tumekubaliana kuwa hatutaaibisha Bunge hili. Wenzetu Wabunge ambao wanaomba viti vya ugavana watakuwa ni magavana ambao wanaenda kuendesha sera ambazo zimetungwa sahihi na Bunge hili. Tunawahakikishia Wabunge wenzetu hatutawaibisha kwa vyovyote. Mhe. Spika umetuelekeza mpaka sasa tunafikia kukunja jamvi. Sidhani kama kuna yeyote ambaye angependa kwenda nje kukuaibisha. Kwa wale ambao watakuwa wanarudi ni matumaini yangu kuwa nao watakuwa watu wa nidhamu ambao wataendesha shughuli zao bila shida yoyote. Kwa hivyo naomba niunge Hoja hii mkono. Naomba wenzangu pia waiunge mkono. Ahsante Mhe. Spika.
Mheshimiwa Spika asante kwa mwongozo wako. Lakini nilifikiria kwamba nikiongea nafanya hivyo ili tumalize hili suala kwa kikamilifu.
Mheshimiwa Spika Kipengele 86 cha Kanuni za Bunge kinamkataza Mbunge yeyote kuzungumza juu ya suala lililopangwa kuwa mbele ya Kamati. Kipengele hiki kinawazuia Wabunge kuzungumzia kile ambacho kitajadiliwa na wanakamati. Tunayo kamati iliyochaguliwa nayo itazungumza juu ya Mawaziri wateule. Haya tunayozungumza hapa ni mazungumzo ya hiyo Kamati. Naomba kipengele hicho kiongoze ushauri wetu.
Mheshimiwa Spika kwa niaba ya watu wa eneo Bunge la Matayos kura yangu ni ya ndio
Mheshimiwa Spika kwa niaba ya watu wa Magarini na jamii ya Wamijikenda kutoka Jamuhuri yetu ya Kenya napeana pole zangu kwa familia ya mwendazake aliyekuwa Rais wetu wa pili Mzee Daniel Toroitich arap Moi. Mzee Moi anajulikana kwa kuendeleza mwito wa harambee iliyokuwa inahakikisha kwamba watu kutoka jamii maskini wanapata msaada kupitia kwa mwito huo. Kwa hivyo kwa niaba ya jamii ya watu wa Magarini na jamii ya Wapwani nasema Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Mheshimiwa Spika mimi ni Kii Francis Kuria Mbunge wa Eneo Bunge la Molo Nakuru County Napiga kura ya ndio
Mheshimiwa Spika Mjumbe wa Mvita na kiongozi wa kamati ya PIC amesema eno kuhusu vile makampuni tofauti wanamiliki hisa zao. Inawezekana atoe ushahidi ya kutosha kuwa KPA ina hisa za asilimia katika kanuni za Bunge Nambari 91. Kama hana ushahidi basi nitamuuliza ayakanushe matamshi hayo.
Mheshimiwa Spika naomba nikamilishe. Mwenzangu katika hii hoja ya nidhamu aliyosimama kwa maoni yangu anapotosha Bunge kusema kuwa hawa ndugu zetu wako katika hatari kubwa sana ya kufurukushwa kwa chama. Kama wamefuata sheria hakuna mtu yeyote atakayefurukushwa. Lakini kama hawatafuata
Mheshimiwa Spika naomba nitoe mchango wangu kwa Ripoti hii ya Kamati ya Bunge kuhusu Uwekezaji wa Umma ambayo imechambua mambo mengi kuhusu uendeshaji wa mashirika mbali mbali ya nchi hii. Haswa naomba nielekeze mwelekeo wangu kwa Shirika la Reli la Kenya ambalo lilichangia sana kuona kuwa kazi ya uendeshaji wa reli imepeanwa kampuni iliyokuwa mbichi geni mwanamwali na isiyoweza kufanya kazi. Kampuni hii ilikuwa inatoka Afrika Kusini na kazi yake haikuwa imetambulika au kueleweka vizuri. Hata hivyo Mheshimiwa Spika ikabainika wazi kuwa Shirika la Reli la Kenya lilitakikana lipeane kazi hii kwa kampuni hiyo. Wakati mmoja ilibidi wakuu wa Serikali waje waone Kamati ya Bunge kuhusu Uwekezaji wa Umma ili waweze kujieleza kwa sababu Kamati hii ilikuwa imeomba tume ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi ichunguze kwa undani waliokuwa Mawaziri wa Usafirishaji na Fedha tangu hapo awali. Mawaziri hao walikuwa Mhe. Kimunya Mhe. Chirau Ali Mwakwere na Mkuu wa Fedha Joseph Kinyua na Esther Koimett kwa sababu ya yale waliyotenda. Mhe. Spika unakumbuka kuwa haya mambo yalitokea Shirika la Reli la Kenya lilipopeanwa kwa kampuni na kusemekana kuwa kampuni hiyo itaendesha Shirika la Reli lakini ikawa haina ujuzi wala mwelekeo. Mpaka hivi sasa tunaposema hakuna mabehewa yamenunuliwa. Hamna chochote kimetendeka kwa Shirika la Reli. Kwa hivyo Mhe. Spika hii ni moja tu ya Ripoti zilizoko na zilizotakikana kuangaliwa na Bunge la Kumi ama Bunge la muhula ule uliopita. Kamati husika haikuweza kuziangalia na ndio maana imebidi Kamati hii iende mbele sana na kuhakikisha kuwa Ripoti zote zimemalizika na kuletwa kwako ama kwa Bunge ili Bunge liziangalie na kuzipitisha. Hii ni kwa sababu Ripoti kama hii inahusisha mashirika kadha wa kadha na ni mengi. Ripoti hii ina mashirika 20 na vile mwenzangu amesema labda haoni ni vipi Kamati hii ingeweza kuziangalia. Hata hivyo na kama ujuavyo Mhe. Spika tumechukua muda na kuomba ruhusa yako ya kipekee ili Kamati hii ipate kuchunguza Ripoti hizi zote. Kazi ambayo imefanywa na Kamati hii Mhe. Spika inaridhisha na ni ombi langu kuwa Bunge lipitishe na kukubali Ripoti hii ambayo imepeanwa na Kamati ya Bunge kuhusu Uwekezaji wa Umma. Kwa haya machache naomba niunge mkono Ripoti ambayo tumeipeana hapa. Naweka tamati Mhe. Spika.
Mheshimiwa Spika naomba pia mwongozo wako kuhusu hili suala kwa sababu kinara wa walio wengi Bungeni na kiongozi mwenzangu ametoa hoja hapa ya kumaanisha kuwa hawa mabwana waheshimiwa wa Bondo na Kisumu wako katika hatari kubwa ya kufurushwa kwa chama. Suala kama hili naomba nilichangie kwa sababu mimi ni mhusika. Wasiwasi wa hawa ndugu zangu waheshimiwa naomba niutulize. Chama chetu cha Orange Democratic Movement (ODM) si chama cha kuvamia mambo ya kuweza kufukuza wenzetu wa chama kiholela. Kwanza tunaanzia mashinani na katiba ya chama iko. Kama hufuati katiba ya chama na mwongozo wa chama unafanya nini chai? Hilo ndilo suali.
Mheshimiwa Spika naunga mkono haya malalamishi. Tusiongee sana kuhusu masuala ya mpaka lakini inadhihirika hata wakati wa uchaguzi kuwa watu wa Mtito Andei hawampigii kura Mheshimiwa Jessica Mbalu wanampigia kura Mbunge wa Voi anayeitwa Bwana Jones Mlolwa. Tusiendelee kuongea zaidi kuhusu hilo suala maanake kuna makamishna ambao wanahusishwa na hayo. Kwa kweli hili suala la wanyama ni swala tata na sugu. Nimelalamikia suala hili kwa muda mrefu. Nilichangia asilimia kuu katika ile sheria ya kulinda wanyamapori ya mwaka 2016. Lakini ninashangaa kuwa masuala ya kulipa wananchi ambao mimea yao imeharibiwa na wanyama au kujeruhiwa hayajatekelezwa mpaka leo. Ningeomba Kamati yetu Tekelezi ifuatilie hili suala. Kule kwangu Taita Taveta watu wangu wamefukarika kwa sababu ya wanyamapori. Watu wangu wana bidii wanafanya shughuli za ukulima wanafuga wanyama lakini bahati mbaya wakati hao ndovu simba na wanyamapori wengine wakija kwa maeneo ya binadamu wanatufanyia uharibifu mkubwa sana. Mheshimwa Spika kuna wakati hata wewe mwenyewe uliagiza kwamba shughuli hii ifanyike kabla ya siku 60. Nashukuru kuwa KWS ilianza kutengeneza ua ambao ndio suluhu ya kila kitu. Lakini kwa bahati mbaya lile ua walikuwa wanatengeneza lilikuwa linapitia kwa mashamba ya wananchi badala.
Mheshimiwa Spika ninasimama kuunga mkono Hoja hii ya kumwezesha Mhe. Ferdinand Waititu kuingia kwenye Kamati mbili; moja ya kusimamia wafanyakazi na nyingine ya kusimamia mambo ya Bajeti. Kulingana na Kanuni za Bunge hili Kipengele cha 173 Mbunge huyu ambaye alichaguliwa hive majuzi kama Mbunge wa Kabete ana haki ya kuhudumu katika Bunge hili la Kumi na Moja akiwa katika Kamati mbili. Ninaunga mkono Hoja hii.
Mheshimiwa Spika ninasimama kuunga mkono Ombi hili kwani hata mimi sielewi ni kwa sababu gani Waziri alitoa uamuzi kuwa suala la maombi katika shule nchini lipigwe marufuku hasa katika muhula wa tatu. Sioni uhusiano wowote kati ya sala na udanganyifu wakati wa mtihani. Ndugu yangu Mhe. Kamama ninaomba nikujulishe kuwa si vijana ama wanafunzi wanaokaa katika mabweni tu ambao wanaweza kupatikana na hatia kama hiyo. Je itakuwa namna gani kwa wale ambao wanakuja shuleni asubuhi na kwenda nyumbani jioni ambao hawakai katika mabweni? Ikiwa ni suala la udanganyifu wao pia wanaweza kupata hayo makaratasi njiani. Kwa hivyo hiyo si sababu ya kumfanya Waziri kutoa uamuzi bila kuwahusisha wahusika wote. Shida kuu ni kuwa tunatafuta njia ya kusitisha au kuondoa udanganyifu katika masuala ya mitihani kwa kutafuta sababu zingine ambazo hazihusiki na mitihani. Tunamwomba Waziri atafute sababu na njia mwafaka ya kuondoa udanganyifu katika mtihani wetu. Ninakubali kuwa Ombi hili ni la muhimu kwa sababu kuna udanganyifu katika masuala ya mitihani lakini mbinu ambayo imetumiwa na Waziri ya kusitisha maombi haifai. Kama mnavyofahamu sala na maombi wakati wa mtihani inatia wanafunzi mori na kuwafanya wamtegemee Mungu katika mitihani yao. Sina habari kama Waziri anajua maombi ni nini wala sijui kama anajihusisha na maombi. Ninaunga mkono Ombi hili na ninamuunga mkono Mhe. Chris kwa kulileta Bungeni.
Mheshimiwa Wamunyinyi haelewi kuwa "ndugu" ni jina la Kiswahili lenye heshima na hekima. Wakati mwingine nitajaribu kumfunza lugha ya taifa ili aelewe.
Mheshimwa Naibu Mwenyekiti wa Muda nimesimama kuunga mkono mabadiliko haya kusudi yafuatane na yale yote ya awali yaliyokuwa na mabadiliko.
Mheshimwa Naibu Spika wa Muda naomba kutoa mchango wangu kama mwanakamati wa Kamati ya Ardhi. Tumekaa katika vikao na kuchangia itoshavyo. Ni matumaini yangu kuwa Mswada huu utawafaidi watu wa nchi hii ijapokuwa tumekuwa na changamoto nyingi. Nashukuru kwa yale ambayo yamepita kuwa watu wameweza kuridhiana na kukubaliana kuwa yale mapendekezo yote ambayo yaliletwa hasa na ndugu zetu wachungaji na Wabunge wa Pwani yamewekwa ndani na tukakubaliana. Kwa hivyo naunga mkono Mswada huu.
Mimi kama Engineer na coordinator wa BBI Kwale County kwa niamba yangu watu wa Matuga na Kwale kwa jumla ninapiga kura ya ndio
Mimi Mohamed Ali Mohamed kwa niaba ya wakaazi wa Eneo Bunge la Nyali na taifa nzima kwa ujumla napiga kura ya la
Mimi ni Mbajuni. Sisi ni wale waliotengwa na bado tu wachache. Tunawahimiza watu wazaane ili tuwe wengi. Nimeamka kuunga mkono ombi la Mhe. Baya. Ni kweli hao wapendwa wanadhalilishwa hapa Kenya. Kuna mambo mengi hawapati kule Tanzania na huku Kenya pia hawapati. Si wao peke yao. Kuna tatizo zaidi kule kwenye mipaka. Mipaka ilipowekwa Lamu iligawanya jamii. Kuna Bajuni wa Somalia na Bajuni wa Kenya. Bajuni wa Somalia wakakaa kwa maisha. Kuna babu zetu walioa kule na wa kule wakaoa Kenya. Kuna watoto walizaliwa kule na wengine wa kule wakazaliwa huku. Ni ndogo lakini imegawanywa. Kulipotokea shida Somalia na watu wakapigana walikimbilia Kenya kutafuta hifadhi. Hao watu wako Kenya eneo la Kiunga kwa zaidi ya miaka arubaini sasa. Wengine wameolewa huko na wakazaa. Wengine huku wakazaa. Hapa sasa hawana vitambulisho vya Kenya. Kuna mmoja nakumbuka alinililia. Ana miaka karibu arubaini na alisoma Kenya akamaliza kidato cha nne. Kule kwetu Lamu ukipata C+ umepita sana. Ana C+ na hakuweza kuendelea na masomo kwa sababu hana kitambulisho. Imebidi afanye biashara pale. Kwa hivyo hili tatizo liko. Mimi pia ombi langu litakuja kuwatetea watu wangu wa Kiunga. Ahsante Mhe. Spika.
Mimi nimepatwa na saratani na nikasema niko nayo hata kabla ya kwenda kutibiwa. Sababu yangu kwenda kupimwa ni kwa sababu dada yangu mkubwa aliyekuwa anaishi Muchatha Banana alikuwa na saratani na alipozidiwa na ugonjwa alikuja kuishi kwangu Juja. Wakati alipimwa na akapatikana na saratani baada ya hapo alikufa kwa sababu saratani ilikuwa imefika Stage 4 . Alikufa na akapumzika. Wa pili alikuwa ni mama yangu ambaye sasa tunaishi naye. Wakati alipimwa mimi nilikuwa nafanya kampeni. Mama pia alipatikana na saratani. Lakini kwa bahati ya Mwenyezi Mungu ilikuwa ni Stage 2 . Tulimpeleka Aga Khan miezi minane na akapona. Wakati nimemaliza kufanya kampeni nilisema inaweza kuwa familia ina haya mambo ya saratani. Wakati nilienda kupimwa hospitali ya Aga Khan nilipatikana nayo ikiwa Stage 2 . Kwa bahati nilikuwa nimefanyia familia ya Kenyatta kazi kwa miaka mingi miaka 30 kama meneja wao wa kahawa. Nikapelekwa India mbio mbio. Nilipofika pale ndipo tukajua kwamba saratani si vile tunafikiria hapa nchini. Huko India kuna mashine mbili tu ambazo zinapima saratani. Zile mashine zingine 15 ziko Marekani. Wakati unapimwa hivyo virusi vingi vya mwili unaambiwa saratani yako inaweza kuwa ya aina ya virusi maelfu na maelfu ya milioni. Sasa niliulizwa: "Kwa sababu ulichukuliwa picha hiyo bloki iko wapi?" Tulingojea wiki moja ndio ifike kule. Bila hiyo singetibiwa kwa sababu haingewezekana. Ndio tuliona baadhi ya watu 9000 waliokuwa huko 5000 walikuwa wanalala huko nje. Tumewafanyia mchango na wameenda huko kutibiwa lakini hamna kinachoendelea kwa sababu hawana hata pesa ya kukomboa pahali pa malazi ijapokuwa hapa tumefanya mchango. Watu 4000 ndio walikuwa na mahali pa kulala. Kwa hivyo tunauliza Serikali kwa sababu tunajua tutasaidiana.
Misa itaanza saa nne asubuhi siku ya Alhamisi. Mnaombwa tafadhali mhakikishe mko hapo mapema maana milango itafungwa ikifika saa tatu kwa sababu za kiusalama. Hatutaki watu kuzungukazunguka wakati ibaada takatifu inaendelea. Ni vyema kila Mbunge achukue nafasi hii ya kipekee kupata baraka za Baba Mtakatifu. Msiichukue kimzaha. Mmeona watu wameanza kuridhiana. Nchi imeanza kupata angalau heri ya kuwa wanaweza kusameheana. Waheshimiwa chukueni nafasi hii mje nyote. Haijalishi uko dini ipi. Njoni mmekaribishwa. Ninatumai nimejieleza vya kutosha. Labda kuwe na suala la kufafanua niko tayari kuwahudumia Wabunge wenzangu. Mungu awabariki. Asante Mhe. Naibu Spika.
Mkubwa wa ODM si urudi?
Mwisho kabisa ninapongeza Kamati ambayo imefanya kazi hii. Wametutoa katika lindi la shida na waliokuwa wanajiita walala hoi sasa watakuwa walala hai. Kwa hayo machache Mhe. Naibu Spika ninakushukuru kwa kunipatia nafasi hii ambayo ilikuwa imenipita lakini ukanirudisha kwa amri zako nimalize yale ambayo sikuwa nimemaliza jana. Asante Mhe. Naibu Spika.
Na simiti pamoja. Bwana Naibu Spika wa Muda kama alivyosema mhe Kajuju Wameru wanategemea miraa kwa kiwango kikubwa. Wameru wanapokea zaidi ya Ksh20 million kila siku pale Muringene. Miraa nyingine ipo pale Tigania East mahali panaitwa Mlango. Hizo ni pesa nyingi na ndizo zinatumika kusomesha watoto. Hatuna mahali pengine pa kupata pesa. Sisi Wameru hatuna kitu kingine cha kutegemea ila kilimo cha miraa. Tunataka kilimo cha miraa kiwe sawa na kilimo cha mahindi majani chai kahawa ama ndizi. Hii ni kwa sababu miraa ni chakula kama vyakula vingine. Watu waliompigia mhe Wanjohi kura kule Mathare ni wafanyi biashara wa miraa ; walikuwa watu zaidi ya asilimia 80. Pesa zinazoingia katika jimbo la Meru kutoka kwa mhe Wanjohi ni nyingi mno. Mimi naunga mkono kwamba biashara ya miraa iendelee. Wakati wa vita kule Turbo Eldoret na Molo mwaka wa 2007 mlisoma kwenye magazeti kwamba watu waliobebwa na mabasi ya Eldoret Express walimwagwa pale Gakoromone sokoni. Waliingia katika benki ya Equity na wakapewa kila mtu Ksh50000. Vijana wetu Wameru waliokuwa wakifanya hawking walipewa pesa wakanunua nguo na bidhaa nyingine ili wafanye biashara. Je mkipiga miraa marufuku na hali kazi ya hawking miraa ilifungwa
Na tuliongeza mmoja jana ijapokwa sikuwa hapa nchini. Tumeongeza moja kutoka eneo la Uwakilishi Bungeni la Mathare. Nashukuru kila mmoja aliyehusika na shughuli hiyo. Mheshimiwa Naibu Spika naomba nimshukuru aliyekuwa kiranja wa walio wachache Bungeni Mhe. Mung'aro kwa kazi alizozifanya wakati alikuwa katika kiti cha kiranja wa walio wachache Bungeni. Namshukuru kwa kazi zake na namtakia kila la heri. Naomba wenzangu wa muungano wa CORD tushirikiane na tuangalie hawa ndugu zetu wa Muungano wa Jubilee. Tunaenda nao kwa safu moja kwa moja. Pale ambapo hawatekelezi wajibu wao tunawakosoa yakutosha kwa sababu ni wajibu wao. Mara nyingi kuna utelezi na utetezi. Ni wajibu wetu sisi ambao tuku katika upande huu pale ambapo mambo hayakuenda sawa sawa turekebishe. Siyo kwa ubaya wala utata ama ugomvi. Mhe. Naibu Spika naomba tushirikiane na wenzetu kujenga nchi yetu. Tulipitisha Mswada wa ugawaji wa fedha unaoitwa Appropriation Bill; kodi zitakazotumiwa. Ilikuwa tuangalie zitatumiwa namna gani. Ni njia gani tutatafuta mapato na ni mbinu gani tutakazotumia ili nchi iweze kupata mapato ya kutosha. Ni muhimu pia njia hizo ziambatane na uchumi wa nchi. Ni muhimu pia ziangalie kuwa watu wako katika nafasi gani ya kuweza kutoa fedha hizo. Mhe. Naibu Spika utakubaliana nami kwamba si kila wakati ushuru ukichukuliwa ama tukichukuwa nafasi zile zinatumiwa kwa kutafuta ushuru nchi itakuwa nzuri. Tukiangalia hali ilivyo katika nchi ambazo zimeendelea utakuta nchi kama Ujerui Sweden Denmark Uingereza na hata Marekani ushuru wao ni wa hali ya juu mradi tu unatumiwa vyema. Tungeomba kwamba Mswada huu ambao umekuja uangaliwe kwa makini. Hela ama fedha zikitafutwa zinatumiwa kwa njia gani? Mara nyingi utakuta fedha zinatafutwa na watu wanatoa ushuru. Lakini jinsi zinavyotumiwa hazilingani wala hazisaidii nchi. Mara nyingi utakuta kwamba kuna uporaji mwingi sana wa fedha za umma. Utekelezaji wenyewe wa miradi ambayo inafadhiliwa na fedha hizo upo na kasoro nyingi. Watu wakiulizwa waeleze ama waajibike sawa sawa ama wazi wazi mara nyingi wanaona kama wanaonewa. Lakini ukweli ni kwamba watu wengependa watoe ushuru na mapato yaongezeke. Lakini vile fedha zinavyotumiwa hailingani na mahitaji ya watu. Watu wachache ndio wanajinufaisha na fedha hizo. Ni sehemu chache tu za nchi zinapata maendeleo. Mhe. Naibu Spika tukiangalia Mswada huu katika kipengele cha pili hadi cha 24 vipengele hivi vyote vimependekeza mageuzo fulani ya kutafuta ushuru. Mbinu hizi ni muhimu. Hizi mbinu zilingane na mahitaji ya nchi. Hizi mbinu za kutatufa hela ni muhimu. Lazima tuzingatie vile tutakavyoweza kuinua kiwango cha maisha cha watu wetu. Tukiangalia nchi nzima utakuta kwamba mara nyingi usambazaji wa miradi umegemea upande fulani. Tungependa kurekebisha hayo na ndio maana tukaomba ugatuzi katika Kenya. Ijapokuwa ugatuzi umeingia bado kuna changamoto za vile hela zinavyotumiwa mashinani hasa tukiangalia vile magavana wengine wanavyotumia pesa. Hawataki kujibu vile fedha zinavyotumiwa.. Mhe. Naibu Spika singependa kutumia muda mwingi ijapokuwa tu kuzungumzia kwa uchache kuhusu NSSF. Inapendekezwa isimamiwe na RBA kulingani na vile Katibu Mkuu wa COTU alivyotoa maoni yake. Lakini si Serikali ichukue uenezaji na mamlaka ya kuhakikisha kwamba wale watu ambao wanawakilisha wafanyikazi hawapewi nafasi. Mhe. Naibu Spika tusipokuwa waangalifu tutalenga kupandisha ushuru kwa vitu ambavyo vinahitajika na wananchi kila wakati wa maisha yao. Mara nyingi wananchi wanaathirika na hawapati afueni ya kuweza kuhimili maisha. Kwa hivyo ni ombi langu kwamba tunapotoa mapendekezo haya yaweza kubainika wazi kuwa yatakuwa yanafaa nchi na yataweza kusaidia nchi kwa ujumla. Kwa hayo mengi nilikuwa nje ya nchi na nashukuru Mungu nimerudi salama. Nitatekeleza wajibu wangu kulingana na kanuni za nchi na za Bunge na kila mtu aelewe kwamba ukiwa kiranja Bungeni kuna matarajio wenzangu wanatarajia kutoka kwangu. Ningependa kuwahakikishia wenzangu kwamba nitatimiza wajibu wangu kwa mjibu wa sheria. Na yale wanaotarajia kutoka kwangu kama kiranja nitayatimiza. Wasiwe na wasi wasi. Na wenzangu katika upande wa Jubilee mwe sawa sawa kwa sababu tutaonana ana kwa ana! Ahsante.
Nachukua fursa kukushukuru kwa kunipa fursa nichangie Hoja iliyo mbele yetu. Kwanza kabisa msimamo na maamuzi yangu juu ya Hoja hii ni kwamba naiunga mkono. Nimefanya kazi pamoja na Mhe. Chepkong'a katika Bunge la Kumi na Moja kama mwenyekiti mtunzi na mwanasheria. Ninaamini ujuzi aliyokuwa nao kutekeleza wajibu wake kama mbunge na mwenyekiti. Kama kuna taasisi katika taifa la Kenya inayoeleweka vibaya ni taasisi ya Bunge. Pengine ni kwa sababu tunatunga sheria ambazo hazifurahishi wengi ndiposa dunia imekataa kutuelewa na kuchukulia Wabunge vibaya. Mahali ninakaa kama Mbunge ninaamini ni tume inayotoa huduma katika Bunge ndiyo inaweza kutoa fikra za wakenya na inaweza badilisha uso wetu kama viongozi wa taifa ili Wakenya waweze kutuelewa. Kwa hivyo kiongozi kama Chepkong'a alikuwa ndani ya Bunge na anajua Bunge ni nini. Nikiwa mfano najua sehemu mbili za shilingi. Ninajua kupata kiti na kuwakilisha wananchi hapa na pia najua kukosa. Ni muhimu Wakenya waelewa wajibu wa Wabunge wao. Sisi tumepewa wajibu muhimu wa utunzi wa sheria na usimamizi wa utendajikazi wa Serikali. Tumeondolewa wajibu muhimu na sasa tumekua taasisi ya maendeleo. Kukiwa na kifo lazima uwe hapo kukiwa na harusi lazima uwe hapo kuna mgonjwa lazima uwe hapo. Kuna wakati fulani nikiwa Tana River kulikua na mtu mkubwa katika Serikali na wanachi hawakuenda kwake. Matatizo yao yalikua yanaenda kwa Mbunge. Zama zile nilikua nikiongea juu ya Sarah Serem kuwa amevunja sheria kulia kusini kaskazini na kati kwa sababu ya kudhulumu haki ya Wabunge. Mhe. Chepkong'a atakapokuja katika tume hii atajua wajibu wa Wabunge na bila shaka atasimama kutetea haki yetu. Kwa sababu wazungumzaji ni wengi ningependa kufupisha mchango wangu. Nina ombi kwako kwa mwenyekiti wa tume ya huduma ya Bunge. Kipengele cha saba cha Katiba kinatambua Kiswahili kama lugha rasmi na lugha ya taifa. Kipengele 77 cha Kanuni ya Bunge kinatambua Kiswahili kama lugha rasmi na lugha ya taifa. Lakini kanuni ya Bunge imeandikwa kwa kizungu Katiba ya taifa imeandikwa kwa kizungu ratiba ya kikao cha Bunge cha siku imeandikwa kwa kizungu. Inabidi sasa uchukue Katiba Kanuni za Bunge ratiba ya kikao cha Bunge na uanze kutafi kwa lugha ya Kiswahili badala ya kuangalia kipengele na kukizungumzia. Najua katika Bunge la Kumi na Moja na Bunge la Kumi tume inayotoa huduma kwa Bunge imefanya kazi kubwa. Tunawapa kongole tunawapongeza. Lakini lazima tuwe na vyombo vyakutuwezesha kama wazungumzi wa Kiswahili ili tuweze kuchangia mada kikamilifu. Hili ni ombi na ni wajibu kwa commissoners ambao wamechaguliwa. Asante sana Mhe. Spika
Nadhani wananchi wa Lungalunga wamepokea salamu zako.
Naendelea Mhe. Naibu Spika. Unaweza kusikia kuwa kuna polisi mahala fulani ambaye amepigwa na kunyang'anywa bunduki
Nafikiri ni joto mko nalo jingi. Wakati ambapo mna joto mnakunywa maji baridi halafu joto linapoa. Kwa hivyo ninaomba tupunguze hilo joto ndiyo tuone Kenya yetu vile itaendelea. Bw. Naibu Spika ninaomba uwapatie hao nafasi waongee sana ili walitoe hilo joto ndiyo tupige kura tumalize. Kwa sababu hivi sasa tukianza kupiga kura watatoka nje. Ukitoka nje tafadhali ujue kwamba mwananchi amekuchagua uje hapa umuwakilishe; hukuchaguliwa ukae nje ya Bunge. Kwa hivyo Naibu Spika wapatie nafasi waongee sana ili watoe hilo joto. Asante.
Naibu Spika nimesimama kuunga mkono Hoja hii kwa sababu mara nyingi unakuta kwamba watu wakipatikana na mafuriko ama majanga ambayo yamesababishwa na binadamu Serikali huwa wakati mwingi inaanza kutafuta bajeti ya kuhakikisha kwamba lile jambo limesuluhishwa. Utaona kwamba hili linatatiza ile mipango mingine ya kimaendeleo kwa sababu ni lazima Serikali ianze kutafuta pesa za miradi ambayo tayari ilikuwa imeafikiwa. Jambo ambalo pia ni la kushangaza ni kwa sababu wakati kunapotokea mafuriko ama majanga kama mengine watu wengine huchukua nafasi ile kujitajirisha au kutafuta pesa za kuwafaidi wao binafsi. Hii nchi imeweza kushuhudia Kwa mfano wakati tulikuwa na njaa na kulisemekana kwamba kulikuwa na kashfa ya mahindi. Utakumbuka kwamba pia kuna mambo ambayo yametendeka kwa IDPs. Utakuta watu pia katika janga kama lile walichukua ile nafasi kama matapeli kupitia ununuzi wa ardhi. Hii nchi pia inajua vile ambavyo Wakenya wamekuwa wakiiomba Serikali iweze kuwasaidia ili kujikimu katika maisha ya kila siku na katika mambo ambayo wanahitaji kama nyumba chakula na kadhalika. Kwa hivyo shirika hili likibuniwa nafikiri litakuwa ni jambo muhimu sana. Niseme kwamba Hoja hii ingepingwa na wale ambao kila baada ya muda hutaka kujinufaisha kutokana na majanga ya watu. Ni vizuri pia tuwe na hili shirika kwa sababu Wakenya wenyewe hawajaweza kuhamasishwa ni vipi ambavyo wanaweza kujikinga na adhari za majanga ambayo yanatokea. Kwa mfano hata ukiangalia nyumba wanawezaje kujikinga na moto ukitokea? Kwa hivyo nimesimama kuunga mkono. Natumaini kwamba hii Hoja inaweza kuhakikisha kupunguka kwa nafasi ya watu ambao hufaidika kutokana na shida za watu wengine. Kwa hayo machache naunga mkono.
Naibu Spika nina Hoja ya nidhamu. Mheshimiwa amesema kuwa suala hili limejadiliwa hapa lakini Kamati imetaja tu Tana River na Garissa. Nimeisoma Ripoti yao na Lamu haikutajwa popote. Sijui Lamu mwataka twende Somalia; kwani Lamu si Kenya? Katika Ripoti yenu mumeweka only Garissa na Tana River na Lamu kuna mafuriko kila pahali. Hii ni shida kubwa munatuletea. Hamuhesabu Lamu sijui munatupeleka wapi.
Naibu Spika ninaomba nisikizwe. Katika Mwaka wa 2010 tuliposema Naibu Spika unajua sikio la kufa halisikii dawa. Katika Mwaka wa 2010 tuliposema tufanye marekebisho fulani watu hawakutaka kusikiza. Pia Wabunge waliokuwa hapa hawakutaka kusikiza. Tulikuwa na Mbunge kama Jakoyo Midowo hapa na hakutaka kusikia. Sasa hivi kuna matatizo kwa sababu hatufurahii yale yaliyo kwenye Katiba. Kama hatufurahii yale yaliyo kwenye Katiba tuna njia mbili tu. Moja ni kupata kura asilimia sitini na saba kubadilisha vile Mhe. Rais amependekeza. La sivyo turudi kwa wananchi na tuwaambie kwamba kipengele hiki hakitufai.
Naibu Spika wa Muda kabla ya kuendelea nilikuwa nimeomba hoja ya nidhamu kuhusiana na suala hili nzima. Hoja hii inaonekana imetia hamasa wengi na wangependa kuchangia lakini naona muda haupo nasi maana umetupa kisogo. Pengine kupitia utaratabu wa Bunge hili Sheria za Bunge Kifungu Nambari 97(4) ningeomba muda wa kuongea pengine upunguzwe kutoka dakika kumi hadi tano ili wenzetu wengine nao waweze kupata fursa ya kuchangia ikiwa itawezekana. Naibu Spika wa Muda ningependa kumpongeza Mhe. Ali kwa fikira ya kuleta Hoja hii hapa. Vile vile ningependa kumpongeza kwa ule utafiti ameweza kufanya kikamilifu kuhusiana na suala nzima la afya katika nchi yetu ya Kenya. Pengine kadri tunavyoendelea kujadili suala hili ndivyo tutakapoweza kuuliza tatizo liko wapi na limesababishwa na nini. Hii ni kwa sababu linaonekana kama kwamba katika karne hii ambayo tuko wengi wanaochangia swala hili hawajaridhishwa na huduma ya afya nchini Kenya. Vile vile tunajua kuwa ni pesa nyingi ambazo zinatumika katika nyanja hii ya afya hususan baada ya Wakenya kusema kuwa huduma hizi zipelekwe mashinani na zigatuliwe. Ningependa kushukuru wale wahusika mashinani ambao wameweza kushughulikia suala hili kwa namna ambavyo wameweza kufanya. Lakini tatizo hili bado lipo na wakenya wengi wanateseka. Sio kwamba pengine nitazungumzia eneo Bunge langu la mashinani bali hata Nairobi kuna watu wanaoishi humu lakini wakishikwa na homa hawajui waende wapi ama watasaidika namna gani. Kama nilivyosema kuna umuhimu wa kuangalia suala hili na kuliangazia kwa undani kabisa. Tatizo ni nini na limesababishwa na nini? Naibu Spika wa Muda Hospitali ya Mombasa kwa hivi sasa hakuna asiyejua kwamba inapokea wageni kupitia kila sehemu katika masuala ya matibabu. Iwe ni wageni kutoka Lamu Kilifi ama sehemu tofauti wote huenda Hospitali ya Mombasa. La kusikitisha ni kuwa Bunge hili likikaa kugawanya pesa za mashinani ama za kaunti ama kugawanya pesa katika Bajeti yake kila mwaka sijaona mambo haya yakifikiriwa. Jambo ambalo ningependekeza tunaposubiri ujenzi ambao umependekezwa wa hospitali nyingine kule Mombasa tayari hospitali hii inahudumia na kupeana huduma ambayo tuko nayo. Tatizo tu ni kwamba huduma hizi haziwezionekana kukamilika ikiwa Bajeti ya nchi hii haiweki kisawasawa na kusema kwamba kwa sababu fulani tumepea hospitali ya Mombasa bajeti ya ziada ili iweze kujimudu na mambo kama haya huku tukipanga namna jinsi tutakavyojenga hospitali nyingine ya Level 6. Kadri tunavyoendelea kuishi katika nchi hii tukumbuke pia kwamba idadi ya watu inaongezeka. Idadi ya watu ikiongezeka kuna dharura ya mambo yanayoweza kupanuliwa ili yaongezeke. Naibu Spika wa Muda suala lingine lililojadiliwa ni suala la madaktari. Mhe. Ali amepeana idadi ya madaktari walioko Kenya. Pengine tujiulize ni kwa nini madaktari ni wachache hivyo. Pia ni kwa nini hao madaktari hawana ii ya kufanya kazi Kenya hii. Hayo ndiyo mambo tunayotaka kuyajua ili tuyatafutie suluhisho. Madaktari wengi wanaosomea taaluma hii huenda kufanya kazi nchi za nje kwa sababu malipo huku ni duni. Kwa hivyo suala la malipo kwa madaktari ni kitu muhimu sana kitakachofanya madaktari wawe na ii na utulivu wa kufanya kazi hapa Kenya. Vile vile inawagharimu pesa nyingi sana wale wanaosomea udaktari. Hivyo basi ningeomba Serikali iwe na mipangilio maalum ya kuwasomesha takriban vijana 500 wanaotaka kusomea taaluma hii ili idadi ya madaktari iongezeke kadri idadi ya watu inavyoongezeka. Naibu Spika wa Muda matatizo ni mengi. Kuna haja ya kuhakikisha mwananchi wa kawaida amepata huduma hizi. Ingawaje Serikali bado inajitahidi bado kuna tatizo. Tatizo kubwa lipo katika wahusika wakuu ambao wanaendeleza mambo haya. Kama viongozi tunafaa kusimama kidete na kuyaweka mambo kama haya sawasawa. Mambo mengi huzungumzwa hapa lakini ukienda mashinani hakuna hata moja limeweza kufanyika. Kuna dharura ya Wakenya kusaidika kiafya kwa sababu rasilimali ya kiumbe chochote ni afya. Sisi kama binadamu tunafikiria pengine rasilimali zetu kubwa ni masuala ya pesa lakini jambo muhimu sana ni afya ya binadamu. Tunahitaji kuizingatia pakubwa na kuhakikisha tumefuatilia haya na yamekuwa sawa kwa wale wenzetu wanyonge vile ilivyozungumzwa kuhusu wale hawawezi kujimudu kupata matibabu ya gharama za juu. Naibu Spika wa Muda kuna watu ambao hawajielewi katika nchi hii. Mtu anaamka asubui na hajui atajisaidia namna gani na familia yake huku tayari kuna uzito wa magonjwa na kadhalika. Kwa hivyo kama nchi pia tujaribu kuangalia uchumi wa watu wetu ili kuwasaidia kupambana na mambo kama hayo ya magonjwa yanapofika. Ningependa kuunga mkono na ningependa Bunge hili liwe pamoja ili kupitisha Hoja hii. Tuweze kufuatilia jambo hili na kuhakikisha kwamba Mkenya wa kawaida anasaidika na haya tunayozungumzia hapa. Asante.
Naibu Spika wa Muda kwanza ningependa kutoa ahsante zangu kwa Mhe. Richard Makenga ambaye alikuwa mbele yangu katika orodha lakini amenikubalia nizungumze kwa sababu nina mahali ambapo nahitajika baada ya dakika 15. Pia ningependa kutoa asante zangu kwa Mbunge mwenzangu Mhe. Omar Mwinyi kwa sababu Hoja hii ni ya heshima sana. Mambo tunayoyazungumzia ni yale ambayo hayawahusu wananchi ambao hawajiwezi. Ni mambo ambayo saa zingine tunayaangalia na kusema hakuna haja ya kuyashughulikia; tuyaangalie yale mengine makubwa. Jambo la kuwa na hati mtu akiumia ama akipigwa ni muhimu. Lazima mtu aende hospitali achukue ile hati ambayo itatumika kortini kama kuna kesi. Hati hii lazima iandikwe na daktari na itaonyesha vile mtu ameumia. Hili ni jambo muhimu na ni jambo ambalo tumeliachilia kama Wabunge na lilifaa kuangaziwa hapo mbeleni. Hiyo ndiyo sababu ambayo imenifanya nikaseme kuwa ndugu yangu Mhe. Omar Mwinyi amefanya vizuri kuleta Hoja hii ili tuizungumzie na tueleze Wakenya ili waelewe kwamba kuna mambo fulani ambayo imefika wakati lazima tujihusishe nayo na kujaribu kuyarekebisha ama kutoa suluhu. Ni mambo nyeti ambayo yanawasumbua wananchi wa kawaida. Kama vile ndugu zangu wamesema hapa mtu akifariki kupata ile hati ambayo daktari ameandika ili kuwe na upasuaji wa kuonyesha ni nini kilichosababisha mtu huyo kufariki ni ngumu sana. Hati hiyo inaonyesha sababu ambazo zilimuua mtu huyo. Yaweza kuwa aliumia ama alikua mgonjwa ama kwa sababu nyingine. Kazi yetu sisi Wabunge imekuwa ni kuzika watu. Ni shida sana kwa familia masikini kupata Kshs6000 za kulipa daktari ili afanye upasuaje. Upasuaji huu lazima ufanyike kwa sababu hati ya upasuaji huhitajika kabla ya kumzika mtu. Mambo hayo mawili yana uhusiano. Wabunge wenzangu wamesema ukitaka hati ya matibabu kwa hospitali haiuzwi. Ningependa kuwaelezea wenzangu wajue kuwa wakati huu ukienda kwa hospitali utaambiwa kuwa hati hiyo haiuzwi. Ukiwa Mbunge hauwezi kuulizwa pesa hizo.
Naibu Spika wa Muda nafikiria bado tunahitaji mafunzo. Wengine tumekuwa Wabunge kwa muda mrefu na wengine bado tunahitaji mafunzo ili kuweza kuelewa masuala haya. Nataka kumalizia kwa kusema kuwa mimi naunga mkono Hoja hii. Serikali iweze kuhakikisha kuwa sheria zinatafsriwa katika lugha ya Kiswahili. Asante sana.
Naibu Spika Wa Muda nashukuru kwa kunipa hii nafasi. Ningependa kuungana na wenzangu kusema napinga Mswada huu kabisa kwa sababu Wabunge wenzangu wanahitaji kuelewa tumechaguliwa na wananchi kuwasimamia na kuangalia shida zao na masilahi yao. Hatuwezi kuenda kinyume ya wale waliotuchagua kusema mambo yawe yakifanywa na kutoa nguvu zetu katika Bunge na kupeleka nje ya Bunge. Tutakua tukipigana na wananchi waliotuchagua. Lazima tuwe na msimamo kamili kama Wabunge kuweza kujua yale mambo tunayopitisha hapa ama yale tunaangalia. Tunaangalia mambo ambayo yanapelekana na matakwa ya wananchi na kufikiria tunafanya mambo ambayo yanafaa. Ningependa kuwajulisha kuwa tunaendelea kutoa nguvu kwetu tukipeleka kwa watu wengine. Sisi sote tulipitisha mambo ya vyama. Hata miezi sita haijaisha watu wameanza kulia. Tumepeleka nguvu kwa wachache tumesikia wameanza kusema fulani ndio atasimama hapa and fulani ndio anasimama kule. Kwa nini tusisome yale tunayoyaona sisi wenyewe? Mambo haya tuangalie. Ninauliza vile huwa watu wanasema katika Bunge mmeona hata wakiwa wengi Bungeni wanatumia fikira zao kupinga mambo ambayo wanaona hayafai. Mjifunze kutoka kwa mambo hayo. Tuko kwa wale wengi na tunasema huu Mswada si mzuri. Sisi sote tuko hapa tukiwa wakilishi wa wananchi kutoka sehemu zote za Kenya. Kwa hivyo ni muhimu tukiona mambo nyeti tunaangalia kwa makini ili tusije kupitisha mambo ambayo tukikutana na wananchi itakua ni shida kwa sababu walitupa nafasi ya kuwawakilisha. Sisi ndio macho ya wananchi walituchagua kwa kura nyingi na ni vizuri tubebe msalaba wetu na tukifanya makosa tutaadhibiwa kwa sababu ya kazi tulioifanya. Ndugu yangu ameongea juu ya Kenya Railways. Jambo la muhimu ambalo limesaidia nchi hii sana kwa miaka mingi ni sheria zilizokua wakati huo. Tulizivunja tukafanya tulivyofanya ikaenda kwa wengine wachache leo tunatafuta tutakavyofanya kuhusu Kenya Railways. Ni vizuri tusome kwa yale tunayoona yanaharibu nchi hii. Tusichukue mambo haya kama ni ya Upinzani ama ni ya upande ya Jubilee. Ni muhimu tujue tunawajibika wakati tunazungumza mambo ambayo itasaidia wananchi wetu. Napinga Mswada huu kabisa. Tumepitisha mambo mengi na yakaenda kwa wachache ambao wana mpango ya kujitajirisha wao wenyewe na kupora mali ya wananchi. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda najulikana kwa kusema ukweli. Hata nikiwa pale nipo huwa na vita vingi sana kwa sababu mimi ni mtu wa kusema ukweli. Mimi si mtu wa kuambiwa nifanye bila kufikiria. Kuna msemo wa Kiswahili husema akili ni nywele na hakuna asiye na nywele zake kwa kichwa. Umefika wakati sisi watu na nywele zetu kusema tuna fikira zetu kufikiria jambo nzuri na jambo mbaya. Kwa hivyo naipinga na ninasema hata haihitajiki kuizungumzia katika hili Bunge. Kama tungekuwa wengi nafikiri hili ni jambo ungesema uweke swali tu na tujibu. Kuna mambo muhimu yaliyo mbele yetu; kuna mambo ya njaa kuna mambo ya ukame. Tunapoteza wakati kama Wabunge ambao tumechaguliwa kwa mambo ambayo hayaongezi; ni ya kuharibu. Kwa hivyo kama ni fikira zangu isipokuwa siwezi kaa kwa kiti chako kwa kuwa tunakuheshimu kama ningepata nafasi ya kusimama hapo ningeweka swali la kusema tuutupilie mbali ama tuendelee. Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Naibu Spika wa Muda ninajua ulikuwa unashauriana na Kiongozi wa Walio Wengi kwa hivyo labda hukusikia yale ambayo ndugu yangu Mheshimiwa Nominee 001 amesema Amesema kuwa mtoto akichanganyika uzazi awe na baba ambaye ni Mjaluo mwingine sijui amezaliwa na Mkisii na mwingine na kabila lingine hayo ndiyo mambo yanayochangia utumizi wa dawa za kulevya Sijui ni ushahidi gani alio nao wa kuonyesha kuwa ukichanganya uzazi utatumia dawa za kulevya kutokana na uzazi ama mambo ya ukabila Hayo ndiyo mambo tunaomba viongozi kuwa tuwache kuchanganya kila kitu na mambo ya ukabila Hakuna mtoto ambaye huchagua atazaliwa na baba yupi Hata Nominee 001 kuna ushahidi kuwa kuna vile ambavyo anahusiana na Mheshimiwa wa Bahati Kii Ngunjiri ilhali yeye amezaliwa kule Narok Sijui kama ni ushahidi kutokana na utumizi wake mwenyewe ama mambo namna gani Ningeomba afafanue ama atoe matamshi ya kukejeli wale ambao wamezaliwa kutoka kabila tofauti
Naibu Spika wa Muda unatumia mbinu gani kutupatia nafasi? Hii ni kwa sababu unaona mtu amekuja nyuma na anapata nafasi ya kuongea na wewe umekaa hapa kwa muda huo wote. Ni vizuri tuelewe unafuata mtindo gani.
Naibu Spika wa Muda wacha niachie hapo. Lakini huu Mswada ni poa sana na ninauunga mkono. Naupa kidole. Asante.
Nakushukuru Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii ili nami niichangie Hoja hii. Ni wazi kwamba lugha ya Kiswahili inatumika wakati wowote. Inatumika ofisini katika biashara kwa mashule na sehemu zinginezo. Haka kama mtu hakuhitimu kwa masomo bado anaifahamu lugha ya Kiswahili kuliko Kiingereza. Kwa hivyo ni muhimu tuitafi Katiba yetu na sheria zingine ili Wakenya wote wafaidike. Katiba yetu inasema kwamba ni lazima wananchi wahusishwe katika mipango yote ambayo inawahusu. Kwa hivyo Bunge ina sababu ya kuwahusisha wananchi kama tunavyosema katika Kiingereza public participation . Inakuwa muhimu kwa wananchi kutoa maoni yao. Lakini kwa sababu haya yote yameandikwa katika lugha ya Kiingereza inakuwa ni vigumu sana kwa wananchi hata ikiwa wangekuwa na maoni kuyatoa. Ni vyema hasa katika sehemu zingine ambapo masomo yako katika hali ya chini ili wananchi kutoka sehemu hizo wahusishwe. Ukiangalia maadili au sera za Serikali zote zinatoka katika Katiba. Wale ambao wanahusika kama vile maafisa wa Serikali na viongozi wa siasa wanatumia mikutano ya hadhara kuelimisha wananchi. Inakuwa vigumu ikiwa kila kitu kitahitaji kutafiwa ili ilete usawa. Kama Katiba imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili itakuwa rahisi kuwaelimisha wananchi ili waelewe wajibu wao. La mwisho ambalo mara kwa mara linakuwa tatizo na kama vile mwenzangu amesema mshtakiwa anapelekwa kortini mashtaka yote yameandikwa kwa lugha ya Kiingereza na haelewi Kiingereza na wakati mwingine Kiswahili chake ni duni. Inabidi huyo mshtakiwa kufungiwa hadi wakati korti litapata mtu ambaye ataweza kutafi kwa lugha ambayo mshtakiwa anaelewa. Jambo hili hutatiza. Itachukua muda mrefu kwa mshtakiwa kupata haki yake. Ni muhimu Katiba yetu na sheria zote zitafiwe kwa lugha ya Kiswahili ili wananchi wafaidike.
Nakushukuru Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii ili nitoe maoni yangu kuhusu Ombi ambalo limeletwa na Mhe. wa Igembe Kaskazini. Kitengo cha wanyama wa pori kinachoitwa KWS kimekuwa na tabia na uzoefu wa kuingilia ardhi za umma na kusongesha ardhi kiholela.
Nakushukuru Mhe. Naibu Spika kwa mwongozo ambao umetupatia kutokana na ujumbe wa Seneti. Ninamuunga mkono Mhe. Duale kwa mambo ambayo ameyazungumzia hapa Bungeni. Amesema kwamba Bunge hili haliwezi kupitisha suala lolote bila kufuata sheria na sera zilizoko. Naliheshimu Bunge la Seneti na nitaendelea kuliheshimu lakini kuna sheria ambazo zinatakiwa kufuatwa. Imebainika wazi kuwa Wanakamati wetu walioliangalia suala hilo hawakuridhika na mambo ambayo yamefanyika. Ndiposa Bunge la Taifa likaonelea kwamba sheria zilizowekwa kuhusu hundi hii haziambatani na utaratibu unaohusu hazina kuu ya taifa. Sheria hizo haziambatani na mkataba uliowekwa kuhusu usimamizi wa fedha za umma. Kwa hivyo ninamuunga mkono Mhe. Duale. Imebainika wazi kwamba ni lazima tuwachague wenzetu 15 wajiunge na wenzetu kutoka Bunge la Seneti kwenye Kamati ya Pamoja ili walishughulikie jambo hili kikamilifu. Kwa upande wetu ninakubaliana na mwenzangu kwamba wanachama wa Kamati ambayo ilishughulikia jambo hili hapo awali wateuliwe wakajiunge na wenzetu kutoka Bunge la Seneti ili waweze kukishughulikia kikohozi hiki. Mimi niko tayari kutoa majina kutoka upande wetu wa Upinzani ili suala hili liweze kufika katika Bunge siku ya June ili tuweze kulishughulikia haraka iwezekanavyo ndio wenzetu kutoka Bunge la Seneti wasione tunawakanyangia. Ninawaomba Wabunge wenzangu waje tulishughulikie jambo hili. Asante Mhe. Naibu wa Spika.
Nakushukuru Mhe. Naibu Spika kwa nafasi hii ambayo umenipatia. Kitu cha kwanza ni kuwapongeza wenzangu katika Kamati hii ya kuangalia Makadirio ya Fedha kwa kazi ambayo wamefanya ya kuridhisha ijapokuwa mara ya kwanza tulikuwa tumeshikwa na ghadhabu kwa yale waliofanya. Lakini nashukuru Mungu. Wakiongozwa na ndugu yangu Mheshimiwa Mutava Musyimi wamefanya marekebisho ambayo yamekubalika na hivi sasa tuko katika kiwango cha kuangalia ugavi wa fedha za Serikali. Ugavi au ugawaji huu katika wakati huu umechukuwa mwelekeo mpya kwani fedha hizi zimegawanywa kulingana na mipango ya Serikali. Ile miradi ambayo imekubalika ndio itakayofanywa ndipo hapo fedha zimeelekezwa. Ni jukumu la Wabunge kuhakikisha kuwa wanafuatilia kwa uangalifu waone kuwa fedha hizi zinatumika kwa kazi ama mipango ile ambayo imewasilishwa Bungeni. La sivyo itakuwa ni jambo la fedheha sisi kukaa hapa kukubaliana na mipango kadha wa kadha ya Serikali halafu hapo katikati unapata fedha hizo hizo zinabadilishwa na kutumiwa kwa mipango mingine ambayo hatukuidhinisha hapa Bungeni. Bunge lazima liwe macho na liangalie kuwa shughuli hizi zinafanywa kulingana na yale tumekubaliana hapa. Niliposikiza kwa uangalifu Mwenyekiti akitoa taarifa yake alisema kuwa kuna fedha ambazo zimeombwa ili ziongezwe katika Makadirio haya kwa kiwango cha Ksh4 bilioni. Lakini tunakubaliana na Mwenyekiti kuwa tukifanya hivyo tutaongeza gharama kubwa kwa Serikali. Itakuwa na deni kubwa na hatutaweza kulimudu. Itakuwa ni shida kubwa sana kwa Serikali. Ndio maana Mwenyekiti ameomba kuwa hela ambazo zimeombwa zifikiriwe wakati wa Supplementary Budget . Lile ambalo naona bado lina kero ni fedha ambazo zimewekwa katika kitengo cha elimu. Hapo awali tulikuwa tumeweka Ksh11000 kwa kila mwanafunzi kwa mwaka. Sasa zimeongezwa zimefika Ksh13000 kwa mwaka kwa kila mwanafunzi. Lakini tukiangalia Ksh13000 kwa kila mwanafunzi haziwezi kufadhili mwanafunzi kusoma kwa mwaka mzima. Ndio maana katikati unaona kila wakati wanafunzi wanaambiwa warudi nyumbani. Tunatarajia wakati utafika ambapo tutasema kuwa kama elimu ya sekondari inafadhiliwa kikamilifu na Serikali basi iwe kweli inafadhiliwa kikamilifu na Serikali. Fedha zitengwe za kutosha. Wanafunzi wakilipiwa karo basi wajue wanaenda muhula wa kwanza mpaka wamalize muhula wa mwisho bila kuambiwa na walimu warudi nyumbani. Tukiangalia ni kuwa ile hazina ambayo ilikuwa inatolewa kwa wanafunzi wa sekondari katika Makadirio haya imeondolewa. Hiyo najua itakuwa changamoto. Kwa hivyo itabidi kila mzazi aangalie atafanya nini. Bila shaka itatulazimu tuangalie vile Hazina ya Ustawi wa Maeneo Bunge (CDF) itakavyotumika kufadhili wanafunzi hao. Kuna fedha ambazo zimewekwa za kuajiri walimu - Ksh4 bilioni. Tukiangalia hali ya nchi vile ilivyo walimu wanaohitajika ni wengi na sioni kama fedha hizo zitatosha. Ni ombi langu tuanze kufikiria ni wapi tena tutatoa pesa za kufadhili uajiri wa walimu. La sivyo kuna sehemu za nchi ambazo walimu hawatoshi na imebidi wazazi wenyewe wajifunge kibwebwe ili waangalie kuwa walimu wanaajiriwa. Wazazi wenyewe ndio wanaowalipa. Je pale ambapo wazazi hawana uwezo wa kuajiri hao walimu itakuwa namna gani? Nikiangalia kuna Hazina Sawazishi kwa Kiingereza inaitwa Equalisation Fund. Mpaka sasa hizo fedha bado ziko katika Benki Kuu ya Kenya na hazijawahi kutumika tangu tuanze Katiba mpya. Sheria zake bado hazijaletwa hapa Bungeni na najua zina utata. Hazina hiyo ilikuwa imewekwa katika Katiba yetu ili tuangalie sehemu ambazo hazijaendelea au kustawi ili zipewe fedha hizo ili zipate kustawi kama maeneo mengine. Namwomba Mwenyekiti wa Kamati ya Makadirio aangalie kikamilifu hazina hiyo - namtafia kuwa inaitwa Equalisation Fund kwa Kiingereza yaani Hazina Sawazishi. Kwa nini hizo fedha mpaka sasa bado ziko katika Benki Kuu ya Kenya na hazijatumika? Tunaambiwa kuwa hawataki. Ni akina nani ambao hawataki? Kwa mujibu wa Katiba maeneo ambayo hayajastawi kufikia viwango vya maeneo ambayo yamestawi yanastahili kupewa fedha hizo ili nayo yaweze kustawishwa sehemu zao. Tutaendelea hivi hadi lini? Tunaambiwa kwamba tusipokuwa waangalifu Serikali ya kitaifa itazigawa fedha hizo kwa maeneo ambayo inafikiri kwamba yanastahili kufaidika na hazina hiyo. Namuomba Mwenyekiti kwa heshima kuu alizingatie jambo hili ili tuhakikishe kwamba fedha hizo zimegawanyiwa maeneo yanayostahili kufaidika na hazina hiyo. Mhe. Naibu Spika naomba niweke tamati nikiunga mkono ugavi wa fedha hizi. Ni matumaini yangu kwamba Mswada huu utapitishwa na kwamba miradi inayoendelea itatekelezwa vyema na wala haitatekelezwa kiholela kama ilivyofanyika mwaka jana. Kandarasi ya kujenga barabara ya kutoka Voi kwenda Mwatate hadi Wundanyi ilitolewa lakini baadaye Serikali ikakataa kuufadhili mradi huo na mwenye kandarasi akaondoka. Rais alipoenda Taita- Taveta hivi juzi alisema mwenye kandarasi atarudi mwezi wa kwanza na ghafla bin vuu akarudi. Naomba kwamba kwenye miradi inayofadhiliwa na Serikali kusiwe na ukora. Haki ifanywe na fedha zitumike vyema ili miradi yote ikamilike. Kwa hayo mengi naomba kuunga mkono Mswada huu.
Nakushukuru Mhe. Naibu Spika. Nasimama kuchangia Hotuba ya Rais kwa Taifa iliyokuwa ya kufana sana. Mhe. Rais alidhihirisha miundo misingi iliyokuweko nchini wakati wa kubuniwa kwa taifa changa la Kenya mwaka wa 1963 ambayo ni umoja wa Kenya na uwiyano. Hotuba ya Mhe. Rais ilidhihirisha mahali tumetoka na kule tunakoelekea. Wahenga walisema kuwa mwenye macho haambiwi tazama. Tukiangalia upande wa elimu Serikali ya Jubilee imefanya mengi. Kwanza tukiangazia ada ya mitihani iliyokuwa ikitozwa wanafunzi wa Kidato cha Nne na Darasa la Nane imefutuliwa mbali. Pia karibu shule 22000 zimesambaziwa nguvu za umeme chini ya Serikali ya Jubilee. Baadhi ya shule hizo ni zile ambazo ziko mahali hakujawahi onekana umeme. Umeme umeonekana kwenye baadhi ya vijiji ambavyo vilikuwa vimesahaulika kwa miaka na miaka kama kule Doldol ambako natoka. Sitima imefika huko. Tukiangalia upande wa usalama inafaa ifahamike kwamba chini ya Serikali ya Jubilee usalama umeimarika. Serikali ya Jubilee kupitia kwa Wizara ya Usalama na Undani imeweza kudhibiti ugaidi kwa kiwango kikubwa sana. Yafaa ifahamike kwamba ugaidi ni vita vya kidunia si vya Kenya peke yake. Kwa upande wa usalama tumeweza kuona magari ambayo idara za usalama na polisi zimepatiwa. Ninaamini tuko na nguvu za kuwafukuza na kuwakamata magaidi na wataisha. Lakini tisho kubwa la usalama nchini ni baadhi ya matamshi kutoka kwa viongozi wa kisiasa haswa wakiongozwa na vinara wa Upinzani. Upinzani sharti uwe lakini uwe na mwelekeo. Si Upinzani hohehahe. Wakiamka asubuhi ni matamshi mabaya yakupiganisha kabila tofauti matusi na kusuta Serikali yao. Tunapokaribia uchaguzi wa 2017 tumesikia matamshi kutoka kwa baadhi ya viongozi wa Upinzani haswa rafiki wetu ambaye anafahamika kama baba lakini ni babu. Tumeyasikia yale ambayo amesema kwamba asiposhinda hili and lile litafanyika. Ameanza kutia Wakenya kasumba kwamba ni sharti ashinde. Usalama wa nchi hii unaanzia na mimi na wewe. Nikichangia kuhusu ufisadi sijasikia Serikali nyingine ambayo imeweza kupiga kalamu maafisa wa kitengo cha juu kama Mawaziri. Hii ndio Serikali ya kwanza nchini kufanya hivyo. Kwa hivyo vita dhidi ya ufisadi vinaanza na mimi na wewe. Nawashauri Wabunge wenzangu wanaohusika na maswala ya Hazina ya Ustawishaji Maeneo Bunge wakomeshe ufisadi. Mhe. Rais alizungumiza kuhusu pesa za ugatuzi. Ni lazima tuelewe kwamba ugatuzi unakuja na changa moto zake na ni lazima ukweli usemwe.
Nakushukuru mhe. Spika kwa kunipatina nafasi hii. Namshukuru Rais kwa Hotuba aliyotoa hapa Alhamisi wiki jana. Kwanza nina furaha kusema kwamba nimekuwa mashinani leo. Wananchi wamefurahi kwa sababu ya stima iliyowafikia wakati huu ambapo Serikali inalenga shule za msingi. Tunatarajia kwamba kama vile Rais alivyoahidi zile shule ambazo hazijafikiwa zitafikiwa kufikia mwisho wa mwaka huu wa kifedha; yaani mwezi wa sita. Mhe. Spika pia tunaishukuru Serikali kwa kuanza kugharamia malipo ya mitihani katika shule zetu za umma. Kwa niaba ya wananchi na haswa wakazi wa Kipipiri tunashukuru kwa hilo. Pia watu ambao wamefurushwa kutoka sehemu zao na sasa wanaishi na wananchi wengine wanashukuru kwa zile Kshs10 bilioni ambazo zimetengwa kuwasimamia ili waweze kupata mahali pengine pa kuishi. Maisha yao ambayo yamekuwa ya huzuni kubwa yatabadilika. Nikija katika Ripoti ya Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kuna msemo wa kisheria ambao unasema "mshukiwa hana hatia mpaka ithibitishwe kortini kuwa ana hatia". Kwa hivyo hatupaswi kusema kwamba wale watu ambao wametajwa katika Ripoti hii ya EACC wana makosa. Nadhani Rais aliwaagiza mawaziri wake na wafanyakazi wengine wa Serikali wang'atuke afisini mwao ili uchunguzi ukamilike na wasipopatikana na makosa watarudi kazini. Nafikiria hivyo ndivyo alivyomaanisha. Baadhi ya marafiki zetu waandishi wa habari wameripoti kana kwamba watu ambao wametajwa hapa tayari imethibitishwa kwamba ni wafisadi na wameshafanyiwa kesi wamehukumiwa na kupatikana na makosa. Ni muhimu hilo liwekwe wazi. Kuna uwezekano kwamba baadhi ya watu ambao wametoka katika afisi zao watarudi kazini wakipatikana hawana makosa. Ni muhimu sana wananchi wa Kenya wajue kwamba sio kwa sababu eti Serikali haijafanya uchunguzi wake bali ni kwa sababu hawajapatikana na makosa. Pia ningetaka EACC ianze kufanya kazi yake vile inavyofaa. Ni vibaya sana kuanza kutajataja majina ya watu. Ukiangalia katika Ripoti hii ambayo tumepatiwa unakuta mtu anaambiwa "wewe waziri uliunga mkono jambo fulani". Hakuna ushahidi au maelezo yoyote yalitoletwa yanayothibitisha kwamba katika kuunga mkono jambo hilo ulihusika katika ufisadi wowote. Unaambiwa tu kwamba una makosa kwa kuwa uliunga mkono mradi fulani au ulipitia mahali fulani. Ni muhimu sana EACC imshauri Rais katika ombi lake la kupewa Ripoti kuwa kuna watu wamepatikana na makosa na wengine wanaelekea kushtakiwa. Wale ambao wametajwa tu katika malalamiko ya hapa na pale hawafai kuorodheshwa hapa kama watu ambao wanastahili kukaa kando. Sheria inajulikana; ni lazima wapewe nafasi yao ya kujitetea. Nikimalizia kuna ombi ambalo limeletwa hapa Bungeni la kuwataka maafisa wa tume ya kukabiliana na ufisadi ambayo imewafanya mawaziri na maafisa wengine wang'atuke afisini mwao kwenda nyumbani. Kama kuna watu ambao wanastahili kuondoka afisini mwao kabla ya wengine ni makamishna wa EACC. Wanafaa kung'atuka wafanyiwe uchunguzi na Bunge na wakipatikana hawana makosa warudi. Haifai waendelee kufanya kazi katika tume hiyo.
Nakushukuru Mhe. Spika kwa nafasi hii ambayo umenipatia nami niunge mkono ombi ambalo limetolewa na Mhe. Weru. Naomba nichukue nafasi hii kukosoa Kamati ya Kilimo. Tangu tuanze mmeleta ripoti ngapi hapa Bungeni? Nauliza Waheshimiwa hebu tuangalia haya mambo. Mhe. Spika Kamati za Mbunge zimepewa nafasi zijadiliane na ziangalie mambo ambayo yanaletwa kutoka kwa wananchi ili ipate kuyaangaziya na kutoa ripoti Bungeni. Lakini Mhe. Spika nina wasiwasi kwa sababu kuna uzembe ambao hauwezi kukubalika katika Kamati ya Kilimo. Huu uzembe naomba Mhe. Spika ukomeshwe na hii Kamati. Kama hayo unayosema tuko na Ripoti katika Kamati ambayo inahusika na mswala ya ratiba ya Bunge na mimi ni mmoja wao. Sijawahi kusoma ripoti zimekamilishwa nikilinganisha hii Kamati ya Kilimo na zingine. Mhe. Spika wako huru kujitetea lakini kuna uzembe wa hali ya juu na lazima huo uzembe ukomeshwe na uishe. Watu ambao wamepatiwa kazi na wanazembea lazima wabadilishwe katika kamati za Bunge. Kama hamtafanya kazi. Mhe. Spika naomba uchukulie hili jambo kuwa la busara. Kama si hivyo hii Kamati na wenzake wote naomba uwapatie nafasi wajitetee lakini vile ninavyojua waheshimiwa wenzangu hebu niambieni ni ripoti ngapi tumesoma kutoka kamati ya Kilimo? Mambo yao ni mengi. Kuna sukari samaki na leo hii maziwa. Yatakaa siku ngapi kabla hamjaleta ripoti yenu? Naomba Mhe. Spika wawache uzembe na wafanye kazi.
Nakushukuru Mhe. Spika. Mjadala uliopo mbele yetu kwa maoni yangu ungekuwa imefanyika mwaka jana. Hata hivyo ni shukrani maanake leo tumepata kuujadili. Hoja hii ni muhimu sana. Sekta ya boda boda ni sekta ambayo imechangia pakubwa kuinua uchumi wa nchi yetu. Imechangia pakubwa pia kuimarisha uchumi wa jamii na pia imetoa ajira kwa vijana ambao wamekuwa wakitangatanga mitaani bila ajira na imeinua pia mapato ya jamii. Cha kusikitisha ni kwamba vijana hawa wakiwa ni wasichana na wavulana ambao wanaendesha boda boda ni watu ambao hata kupata leseni imekuwa ni shida. Kwa kusema kweli maeneo mengi ambayo sisi wengine tumetoka ni maeneo ambako barabara ni mbovu; ni maeneo ambako hata sisi tukiwa katika Bunge hii Ni mahali ambako inakubidi uache gari lako na kuchukua boda boda ndio uweze kuwafikia wananchi. Kwa hivyo hizi boda boda haziwabebi tu wale watu wa chini. Wabunge watakubaliana nami haswa wale wa kutoka sehemu kavu kwamba mara nyingi sisi tumelazimika kutumia boda boda ili kuwafikia wananchi wetu. Kwa hivyo hizi boda boda zinapofanya ajali hata sisi tukiwa Wabunge mara kwa mara tunapatikana katika hizo ajali. Cha kusitikisha ni kwamba hakuna mipango kabambe ya kutoa mafunzo na leseni kwa waendeshaji boda boda. Iwapo tunawataka hawa vijana wachangie uchumi wa nchi hii ni lazima pia tuangalia maslahi yao. Ni lazima pia tuhakikishe kwamba wana usalama katika uendeshaji wa boda boda. Kwa hivyo ombi langu ni kwamba Wabunge katika Bunge hili la Kitaifa la Kenya na Serikali yetu ambayo imechaguliwa na wananchi waweke mipango kabambe kuhakikisha kwamba haswa utoaji leseni umepelekwa hadi vijijini. Kwa mfano waendeshaji boda boda katika mji maarufu ambao nimetoka unaoitwa Doldol inawabidi kwenda Nyeri ambayo iko katika Mkoa wa Kati kutafuta leseni. Labda ni kijana mmoja au wawili ambao watapata hizo leseni. Vijana wanapokosa hizi leseni inakuwa ni kama kuwapatia polisi fursa ya kupata mapato yao ya kila siku kutoka kwa hawa vijana. Polisi wanapoishiwa na fedha mifukoni mwao wanakumbuka kuna vijana ambao hawana leseni. Wanamwagika kwenya barabara na kuwadhulumu vijana wetu. Iwapo polisi atachukua Kshs500 au Kshs1000 kutoka kwa mwendeshaji boda boda siku hiyo familia ya huyo mwendeshaji boda boda haitapata chakula chake cha kila siku. Ni ombi langu kwamba hili swala tuliitilie maanani tulipitishe na tufuatilie kuona kwamba mafunzo kwa wendeshaji boda boda yametolewa. Pia labda Serikali ilipe kitu kidogo ili gharama ya kupata leseni iwe ni ile ambayo hawa vijana wanaweza kuimudu na kupata leseni. Kwa hayo machache naomba kuunga mkono mjadala huu.
Nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nina furaha tumeweza kuupitisha Mswada huu ulioletwa Bungeni leo kupitia kikao hiki spesheli. Tuna wanariadha au wakimbiaji na wanamichezo wengi kule Kipipiri. Walikuwa wameanza kupata wasiwasi kuwa huenda nchi yetu isipewe nafasi ya kwenda kwa nashindano ya Olimpiki. Tukiangalia yale yamefanyika kuhusiana na hii sheria ni kweli kuwa Kenya inaonewa na mataifa yale makubwa yasiyoamini kuwa nchi ndogo kiuchumi kama Kenya inaweza kuwa ikiongoza katika mashindano. Katika mashindanao ya dunia ya riadha yaliyopita Kenya ilikuwa namba moja. Naona kama shida za Kenya zilianzia hapo. Kwa hivyo tunawaomba World Anti-Doping Agency (WADA) waache kuangalia Kenya kwa sababu ya ushindani wake. Tunastahili kutwikwa zawadi na medali na sio mambo ya kukimbizwa-kimbizwa. Mwishowe inajulikana kuwa Kenya huchukua zaidi ya asilimia kubwa ya medali katika mbio za nyika.
Nakushukuru sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii kuunga mkono uteuzi wa maafisa ambao wamepata nafasi ya kufanya kazi ya muhimu sana katika Kenya hii. Sisi sote twajua kwamba twategemea sekta ya kilimo. Kama tutaweza kupata watu wazuri kusimamia ukulima sisi sote tutafaidika katika Kenya kwa sababu hatujafika kiwango cha kupata chakula cha kutosha. Litakuwa jambo muhimu sana tukiwa na maafisa ambao wataweza kutuongoza kwa njia nzuri ili tuweze kupata chakula cha kutosha. Mimi naunga mkono Hoja hii kwa sababu hiyo. Nashangaa kuwaona Wabunge wengine wakisimama hapa kana kwamba siyo Wakenya. Wanasimama hapa wakitaka kuendeleza ukabila. Wengine wanataka kufanya siasa waonekane wanatetea makabila yao ili wapate kura. Hilo si jawabu. Jawabu letu ni tuwaunge Wakenya mkono. Mtu yeyote anaweza kuisaidia Kenya hii bila kujali ametoka eneo lipi la Kenya. Mtu akichaguliwa huwa ni asaidie nchi. Tunajua kuna wale huwaza kwamba pengine hawawezi kuchaguliwa tena 2017 na kwa hivyo lazima watafute njia ya ukabila ili wakitoka waseme walitetea makabila yao. Hao ni watu wameanguka na ambao hawana sura ya Kenya. Kuna watu ambao wanakaa wakingojea. Ningependa watu waende kwa kitabu cha Mungu. Kuna mtu alikaa kwenye kisima kwa muda wa miaka 38 lakini hakuwa na pesa wala nguvu za kuingia kisii kutibiwa. Kwa sababu ya ii Yesu alimuona na akamwambia:- "Simama na utembee kwa sababu ya ii yako." Wale hatujapata siku moja itafika tutapata kiti. Sisi watu wa Nakuru tuna ii kama ya huyo mtu aliyekaa miaka 38. Hata kama hatujapata tangu 1963 tuna ii kwamba siku moja tutapata na tutaongoza Kenya hii kwa sababu ya ii. Mungu awabariki.
Nakushukuru sana Mhe. Spika. Nikimalizia nachukua nafasi hii kusema asante sana kwa waliochangia. Ni ajabu nimekuwa hapa kwa Bunge hili kwa miaka nyingi na sijapata kuona Hoja ambayo inaungwa mkono asilimia mia kwa mia. Hii ni mojawapo. Wabunge wote ambao wamezungumza hapo mbele wamechangia mambo tofauti lakini wamesema kwamba inabidi tubadilishe kipengele ambacho kinasema umalizie Kiingereza ukianzia Kiingereza. Tunaweza kuchanganya lugha. Ni vizuri lakini pia tuchunge ili tusiweke mix kubwa mpaka tuwe na Sheng na kuileta katika Bunge letu. Hiyo itabidi twende kutafuta Kanuni tofauti za ile Sheng . Kwa hivyo ni lazima tuwe tukiomba neno moja au lingine kutoka ile lugha nyingine ili tuwe na Kiswahili sanifu ambacho wanafunzi wataiga.
Nakushukuru sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Hata mimi sitaki kuachwa nyuma kukupongeza kwa wadhifa huu mpya uliopewa. Naongea kama mtu ambaye amekusikiliza ukihudumu. Najua utaweza hiyo kazi. Nasimama kuunga mkono Hoja hii. Naomba Serikali iangalie haya mambo ya maji vile iliangalia mambo ya stima. Ijapokuwa mradi wa stima ni wa kupeleka umeme kwa kila shule ya upili ya umma kwa karatasi madhumuni ya pili yalikuwa kupelekea wananchi stima. Hii ni kwa sababu kama kila shule ya msingi ya umma inapata stima inawezekana kila sehemu ya nchi itakuwa imepata umeme kufikia sasa. Mradi huu ukichukuliwa hivyo - kuwa kila shule ya msingi ya umma ipelekewe maji - kila sehemu katika nchi hii itapata maji. Kwa hivyo huu mradi hautakuwa wa kunufaisha wanafunzi tu. Utanufaisha maeneo yote ambayo yamezunguka hizo shule za umma. Pili ni kweli huduma ya kusambaza maji ni wajibu wa serikali za ugatuzi. Jukumu la Serikali Kuu ni mabwawa makubwa makubwa na miradi mikubwa mikubwa ya maji na kulinda chemichemi za maji. Tunapoongea kuhusu Hoja hii itakuwa muhimu Serikali iangalie kama kuna uwezekano wa kusambaza maji katika kila mahali. Iwe ni kama vile imefanya mradi huu wa hospitali mbili katika kila kaunti. Ule ni wajibu wa Serikali kuu na sio wa kaunti Serikali Kuu inaweza kupeana hazina kwa serikali za kaunti ziweze kutimiza wajibu wake na Serikali kuu iwe ikifanya wajibu wake. Tunataka kuwe na ushirikiano kwa sababu hatutaki tena ugomvi mkubwa. Jinsi Serikali ilivyofanya ratiba nzuri ya kufadhili hospitali mbili katika kila kaunti inapaswa kufadhili miradi itakayopeleka maji kwa kila shule ya umma. Tukiongea mambo ya maji katika shule za umma kuna shule ambazo zina mashamba makubwa kuliko wanayohitaji kujenga. Pia kuna shule nyingine zenye miradi ya kujiinua kiuchumi kama ukulima. Shule hizo zikipata maji watanyunyizia mimea ambayo inafanya vizuri katika maeneo hayo. Watapata fedha za kufanya mambo mengine badala ya kutegemea Serikali na wazazi kwa pesa ambazo zinatumika katika shule hizo. Nikimalizia nawaomba wote ambao wanasimamia mambo ya maji. Sisi kama Wabunge siku hizi sio wanachama wa Kamati za Hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge lakini tunaweza kuongea na kamati ambazo ziko ili zimulike shule zote kuhakikisha kuwa maji yanafika huku tukingojea Hoja hii ambayo nina hakika tutaipitisha itekelezwe na Serikali. Naomba Kamati ya Utekelezaji katika Bunge hili ichukue Hoja hii itakapopitishwa. Iende haraka haraka kwa wizara zinazohusika na isisitize itekelezwe haraka iwezekanavyo. Naunga mkono.
Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi hii. Nasimama kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Kamati ya Elimu Sayansi na Teknolojia. Sababu zangu za kuiunga mkono ni kama zifuatazo:- Kwanza umuhimu wa hao maafisa kuteuliwa ni waende kazini katika Tume ya Kuajiri Walimu hili iweze kufanya kazi vizuri. Pili ni kwa sababu wametoa mfano mwema kwa kuteua mlemavu ambaye amepewa wajibu na jukumu kubwa katika nchi hii. Kumekuwa na mgogoro huko mashinani kuhusu uwezo na majukumu ya Wizara ya Elimu na Tume hii. Kwa hivyo ni muhimu sana. Sasa ni wengi. Waende watatue matatizo ili kazi iendelee vizuri. Pia waende washughulikie walimu wakuu ambao wanakataa kutii amri ya Wizara kuhusu karo. Vile wanakataa ni kama hizo pesa zinaenda kwa mifuko ya watu. Ni afadhali wangekuwa wakiambia Serikali iweze kusaidia mahali ambapo pana upungufu wa pesa badala ya waendelee kuumiza wazazi na wanafunzi kwa kuitisha karo ya juu zaidi. Ijapokuwa naunga mkono ningetaka kutaja eno kadha. Kwanza kuna shida kidogo kuhusu hawa maafisa ambao wameteuliwa hapa. Tutapitisha Hoja hii na nitaiunga mkono kwa sababu ya wakati na wamehitimu kuchukua nafasi hizo. Lakini ukiangalia wale wote ambao wameteuliwa vile Serikali yetu ya Jubilee na ifesto yake na pia vile Katiba inasema hakuna kijana hata mmoja ambaye amepewa nafasi. Ukiangalia wale wameteuliwa mmoja ni miaka 60 mwingine ni miaka 59 mwingine ni miaka 56 na mwingine ni miaka 62. Sisemi wazee wasifanye kazi lakini ni muhimu pia vijana wa kati ya miaka 30 na 40 wapewe nafasi. Wengi wa walimu ambao wanasimamiwa na hii Tume ni vijana. Kila wakati wakienda kutafuta msaada kwa Tume wanaenda kwa wazee watupu. Hata wale ambao wako kule kwa wakati huu pamoja na Katibu wote miaka yao imesonga. Ni kweli tunataka ile hekima lakini vijana pia wapewe nafasi kwa uteuzi ambao utakuja. Naona kuna umuhimu tubadilishe sera ya elimu ambayo inasema kitambo mtu ateuliwe katika Tume hiyo anastahili kuwa amefanya kazi zaidi ya miaka kumi. Mwalimu akitoka chuo kikuu akiwa na miaka 25 na umpatie miaka 10 atafikisha miaka 35. Kwa hivyo ni muhimu sana vijana wapewe nafasi. Kwa Serikali yetu na hata Rais wetu ningetaka hili jambo la vijana liangaliwe kwa sababu litaleta shida katika hii nchi. Jambo lingine ni kuwa hawa wote ambao wameteuliwa ni walimu ambao wamefanya kazi wakakuwa maafisa wakubwa katika idara mbali mbali. Kwa kweli hii ni Tume ya walimu. Lakini ni makosa Tume yote inasimamiwa na walimu. Wanahitaji pia taaluma zingine kama vile sheria na uhasibu. Vile wako itakuwa ni kama shule itakuwa ikiendelea katika Tume hii. Nikimalizia ni muhimu pia tuangalie mambo ya tume kama hizi. Ni kweli wana uwezo wa kikatiba lakini wote wakumbuke kuwa wako katika Serikali. Vile tume za kikatiba zimekuwa zikifanya ni kukaa kando na kusema zisiambiwe kwa sababu zina uhuru na zitafanya vile zipendavyo. Lakini kila mwisho wa mwaka wanakuja kwa Serikali Kuu kuomba fedha za kugharamiaa bajeti zao. Ni muhimu sana waweze kujua kwamba lazima wafanye kazi na idara zingine za Serikali na tume zingine. Tuko katika Serikali moja. Zote tuko katika basi moja ya kuelekea kuleta maendeleo katika nchi hii yetu. Nashukuru sana Mheshimiwa Spika.
Nakushuru Mhe. Spika wa Muda. Kwanza ninampongeze ndugu yangu Mhe. Mohamed Ali kwa kuleta Hoja hii ya kuanzisha hospitali ya rufaa kule Mombasa. Nasikitika kwamba katika Bunge lililopita tulipitisha Hoja nyingi. Hata mimi nilipitisha Hoja ya kuweka chumba cha wagonjwa mahututi katika kila kaunti na hata kila eneo Bunge kwa Kenya nzima lakini mpaka leo Kamati ya Utekelezaji haijasema ni nini itafanyika. Hoja hili ambayo imeletwa na Mhe. Mohamed Ali ni nzuri hasa mambo ya kuanzisha hospitali ya rufaa Mombasa. Pia zikuwe kila pembe ya nchi yetu ndio tuweze kuangalia mambo ya ugonjwa. Tuna changamoto kwani hatuna madaktari. Hata wakati nilikuwa nikileta Hoja yangu tulikuwa tunasema hatuna madaktari. Mhe. Mohamed Ali ametuambia leo kwamba madaktari wanalipwa pesa kidogo. Lazima tufikirie ni kitu gani tutawafanyia madaktari wetu. Hatutakuwa na madaktari kila siku wanaenda kwa hospitali kisha wakirejea nyumbani hawana pesa kwa mfuko. Wanafanya kazi kutoka asubuhi mpaka usiku na hata ukiwapigia saa nane ya usiku unatarajia wakuwe hospitalini lakini hawana fedha. Tukiwa nchi na Wabunge lazima tufikirie Kenya yetu inaenda vipi. Tunaelekea vizuri ama la? Kama hatuna afya kama Kenya nzima basi hatutaendelea mbele. Nashukuru Mhe. Ali amesema tunaweza kujenga hospitali na Kshd3bilion na tuziboresha zile zilizoko ili ziwe hospitali za rufaa na Kshs2bilioni. Nauliza ni nani anatoa hizo pesa kama sio Bunge kutenga hizo pesa ziende kwa hospitali? Katika Kaunti yangu ya Meru tulikuwa na hospitali ya Level 5. Kwa wakati huu Gavana wetu Kiraitu anaipeleka ikuwe Level 6. Nasikitika miaka 15 iliyopita tulikuwa na mashine ambazo zilitoka Spain lakini hatuna wataalamu wa kuzitumia. Katika Kenya yetu lazima tutafute wataalamu ili mashine zilizoko kwa hospitali ziweze kutumika. Nashukuru Serikali ya India kwa kutupatia mashine ya babatron mwaka uliopita ya kuangalia saratani. Lakini tujiulize kweli kama mashine moja ndiyo itafaa Kenya nzima ambayo ina idadi ya watu 45milioni. Serikali na Bunge lazima tupitishe pesa zile na ziangaliwe zisikuwe na sakata ya ufisadi kama zile za Afya House ambapo tunasikia Kshs5 bilioni zinapotea. Wale wamechukua hizo pesa lazima wachukuliwe hatua na tusiwadhulumu madaktari. Wiki mbili ama tatu zilizopita daktari katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta alifanya upasuaji mtu asiyefaa. Kama angekimya nani angejua amefanya vibaya? Hakuna mtu angejua. Ni vizuri alisema amekosea. Sasa tusiwalaumu hao. Waziri Cecily Kariuki amesema hajafuta kazi yule Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta Lily Koros. Amesema akae kando ndio mambo yaangaliwe kwa sababu Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta ina shida nyingi. Lazima tuone tutakavyofanya. Lakini tukisema kwamba tutampeleka nyumbani kwa sababu ya kumfuta 'mtu wetu'. Kwani nani siyo mtu wetu? Kila mtu Kenya hii ni mtu wetu! Kwa hivyo lazima tujue kwamba ikiwa tunataka kuendesha Kenya lazima tuelewe kuwa sisi ni ndugu hata kama tunatoka makabila tofauti. Ugonjwa haujui ndugu wala dada. Inatupasa kuwa na hospitali za rufaa Kenya nzima. Tutenge pesa kwa ajili ya hospiltali za rufaa. Pia tunapaswa tuhakikishe kuwa hospitali za rufaa zinasimamiwa na Serikali kuu wala siyo za gatuzi. Hii ni kwa sababu magavana hawawezi kutekeleza wajibu wa kuwalipa madaktari na wafanyakazi wengine. Kwa hayo machache naiunga mkono Hoja hii. Ni changamoto kwa Mhe. Ali afuatilie Hoja hii ili tuweze kupata hospitali hii. Tumeshapitisha Hoja kumi na moja humu Bungeni lakini mpaka leo. Mhe. Mwadime amesema kwamba Hoja yake ya maji haijapita na yangu ya hospitali ya intensive care unit (ICU) na blood donor unit sijaiona ilhali tunahitaji vitu hivyo.
Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe Suluhu Hassan Ni baraka kutoka kwa Mungu kuwa na jirani ambaye mnaheshimiana Ni baraka kutoka kwa mungu kuwa na jirani mwema ambaye ako na ufaa mengi sana Jirani mwema akiona unanawiri anafurahia Tulipokuwa shuleni tulikuwa na watu kutoka Tanzania ambao walikuwa mashuhuri Walikuwa wameandika vitabu ambavyo tulikuwa tunavisoma shuleni kama vile Shaaban Robert Kuna wale wanajua kutunga mashairi kwa mfano "Titi la Mama Litamu hata Likiwa la Mbwa'' Pia kuna mwingine mashuhuri anaitwa Ibrahim Hussein ambaye ameandika mchezo wa kuigiza ambao unaitwa Mashetani Kuna msemo ambao naupenda sana na ningependa kuutumia leo: "Mpanda ngazi na mshuka ngazi hawawezi kushikana mikono" Kwa sababu hiyo Rais Suluhu Hassan alipowasili hapa alikuja ili tushikane mikono ndio tuweze kusonga mbele pamoja kiuchumi kimaendeleo na kidiplomasia Vile vile alipotutembelea hapa katika ziara yake nilipata simu nyingi nikiambiwa kwamba Tanzania haina sheria ambazo zinaweza kuharibu biashara nyingi Kuna mumea tunaopanda kule kwetu unaoitwa ' miraa ' ama ' maurungi ' kama unavyojulikana huko Ni vizuri kusema kuwa hapa Kenya mumea huu ni biashara halali Lakini ukivuka mpaka upande wa Tanzania biashara ya miraa ni haramu Mara nyingi nimejaribu kuwatoa vijana jela kule wakiwa wamefungwa maisha kwa sababu ya kujihusisha na biashara ya miraa Tunasema kuwa huu ndio wakati wa kupeleka ujumbe kule pole pole ili tujitetee kidogo tusiwe tunaumia Bi Naibu Spika wa Muda kabla ya kuaga dunia kwa Hayati Rais John Pombe Magufuli hatukuwa tunamfahamu Makamu wa Rais wa Tanzania Alivyochipuka na kuchukua usukani wengi walipomskia waliona ni kiongozi ambaye amejaa taadhima hekima na ni mwerevu wa akili kuliko viongozi wengi tuliowahi kuwasikia Rais Suluhu aliweza kuwasisimua Wakenya kwa njia nyingi Afrika Masharika imepunga hewa tofauti na tunamsifu Mungu kwa kutuletea kiongozi kama huyu kututembelea hapa nchini Kenya Ahsante Bi Naibu Spika wa Muda
Nani CORD? Niko CORD lakini niko CORD ambaye inaelewa inafanya nini katika nchi yetu ya Kenya. Na ndivyo nasema ya kwamba nyinyi mwasema kwamba Serikali haifanyi kazi
Naomba kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili nikiungana na Wabunge ambao wamezungumza mbele yangu. Mmoja wao Mhe. Mishi Mboko ambaye alisema wamama wetu hata wale ambao hawakuingia darasani ni Wakenya wanalipa ushuru na pia tunatembea katika hii safari pamoja na wao. Niruhusu kwa njia ya kipekee niseme asante kwa Mhe. Aden Duale na uongozi wa hii nyumba ya kitaifa. Pia kwa Mhe. Rais Uhuru Muigai Kenyatta kwa kukubaliana na sisi na kuomba Wakenya wote wakubaliane na huu mwito wa Two-Third Gender Bill umefika wakati wa kutekelezwa. Natuma asante zangu pia kwa President Mhe. Raila Odinga Mhe. Kalonzo Musyoka Mhe. Mudavadi na Mhe. Wetangula pamoja na Wizara ya Gender ambao wamesimama na sisi. Pia washikadau wengine ambao wametoa rasilimali zao wamama na viongozi wa kiume ambao wamesimama na sisi kwa kutayarisha huu Mswada ndio ufike hapa. Pia niruhusu niseme kwa njia ya kipekee kwamba Wakenya wako na matarajio mengi sana katika hii Bunge ya 12. Nikisema hivyo najua Wabunge ni wanasiasa. Wanajua zile changamoto ambazo sisi kama viogozi tunapitia. Moja yake ni propaganda ambazo hutumiwa kupiga jambo lolote ambalo Wakenya hukubaliana nalo. Lakini niruhusu tu ni kumbushe wananchi wa Kenya kwamba Mhe. Mwai Kibaki zile enzi wakiwa na Mhe. Raila Amollo Odinga wakati alikuwa Waziri Mkuu waliweza kutembea katika sehemu zote za Kenya wakiuliza Wakenya watoke kwa idadi kuu kupiga kura ya Katiba ya mwaka 2010 na wakafanya hivyo. Hii ndiyo iliweza kutupatia jambo hili ambalo tunazungumzia la thuluthi mbili. Hii thuluthi mbili si ya akina mama peke yao ni ya jinsia zote. Hii imekuwa safari ambayo mwaka mmoja uliopita Bunge la Taifa tulijiahidi kwamba tutaweza kutekeleze huu mjadala na pia kutunga sheria lakini haijawezekana. Tunavyoongea katika mkono ule mwingine wa Serikali ambao tunauita mahakama wako na matarajio na sisi. Tukifanya hivyo tutaokoa pesa ambazo zinaweza kutumika kwa sababu ya mambo ambayo yanaafikiana na kutotii sheria na Katiba ambayo kila mmoja wetu aliapa na kusema atailinda ataihifadhi na kuitunza. Na tuliapa kwa Quran na Bibilia. Nazidi kuomba ndugu zetu wanaume na pia wamama kwamba wiki ijayo tutoke kwa idadi kuu aake tumeongea na mimi najua yule ambaye alitilia maanani lile jambo ambalo tumezungumza siku ya leo. Hakuna kitu kingine kimebaki kwetu kufanya ila kuwaomba tutoke kwa idadi kuu. Nimeona kwa mtandao Mbunge dada yangu Mhe. Gathoni wa Muchomba Gs Wanga na mimi kama tumechorwa sura maridadi lakini mdomo ni wa yule mnyama anaitwa nguruwe. Wabunge wanaitwa Mpigs sijui kama ni jina la Mpesa walikosea. Lakini tunaitwa hivi kwa sababu tunapigania ile thuluthi mbili. Serikali zetu za ugatuzi zimeafikiana na hii thuluthi mbili na zinatumia rasilimali kuu. Tunauliza Wakenya kwa njia ya heshima waturuhusu kwa mara ya kwanza tuweze kuafikiana na Katiba ya kwamba hakutakuwa jinsia moja ambayo itakuwa zaidi ya thuluthi mbili bila kuweka wengine ndani. Nasema hivyo kama mama najua kuna Wabunge wanaume vijana na walemavu. Naomba sisi wote tutembee pamoja. Maanake Mungu alipomuumba Adamu aliumba hata mama. Mama alitolewa kwa mbavu hakutolewa kichwani. Lakini mama akawa improvement kama ile tunaita improved smart phone . Mama amewekwa GB ile iko juu. Sisi tunataka kuwa memory ya ile maafikiano tuliafikiana na Wakenya.
Naomba radhi Mhe. Spika. Waheshimiwa Wabunge naomba tuelewane ili tujue nini tunatakiwa tufanye. Sio eti hamuelewi. Najua mnaelewa lakini naomba tuelewane. Tukishaelewana tutajua upande tutakaoenda. Kitu cha kwanza kuna Hoja iliyoletwa hapa. Hoja ilipoletwa tuliikataa. Hoja ililetwa ili kuona kama tutawakubali hawa wenzetu ambao wameteuliwa kushughulikia mambo ya makadirio ya fedha. Mliwakataa. Sasa ni lipi tutakalofanya? Nikiangalia vile hisia zenu zilivyo inabainika waziwazi kuwa hata wakiletwa hivi sasa mtawakataa tena. Naomba tuelewane. Mhe. Spika tumekubaliana mara nyingi kuwa ni muhimu tuangalie hisia za wengi. Hisia zao zinaonyesha waziwazi kuwa hawangependelea hao waheshimiwa warudishwe. Wanatupatia muda tulete kamati nyingine. Kwa hisani yenu nawaomba tuelewane. Bila shaka itabidi Waheshimiwa waamue kama wanaunga Hoja hii mkono au la. Kama hawaungi mkono basi tujue tutafanya nini. Naomba hili jambo nilirudishe mikononi mwako ili maamuzi yafanywe. Lakini la busara ni kukuomba tusitishe majadiliano. Tusimamishe majadiliano haya ili tupate muda wa kuwasiliana na kuzungumziana. Tusiendelee na mjadala huu leo. Naomba ukubali ombi langu kama kinara wa Bunge. Tusiendelee na mjadala huu. Mhe. Spika narudisha kwako.
Naomba uniongezee dakika zangu Ningependa kumshukuru Rais Uhuru Kenyatta kwa kutuletea Suluhu hapa nchini Kenya Tulipata suluhu ya ng'ombe zetu kutopigwa mnada hata kama zitavuka mpaka bila pasipoti Tulipata suluhu za vifaranga kutoteketezwa hata kama watapatikana nchini Tanzania bila pasipoti Tulipata suluhu ya miundo mbinu za kidiplomasia ushirikiano maendeleo na ai Mhe Suluhu karibu tena nchini kwa sababu nchi hii ina uhuru; uhuru wa kujieleza wa kuabudu kutembea kuishi na kufanya biashara popote nchini na uwezekano wa vipaji Mhe Suhulu vile nyumbu wa Serengeti wanavyovuka mipaka kutungwa mimba Maasai Mara ndivyo Wakenya na Watanzania watavuka mipaka kuekeza na kufanya biashara katika nchi zote mbili Vile nyumbu wa Tanganyika wanavuka mipaka kutafuta mapenzi Maasai Mara bila pasipoti ndivyo Wamaasai wa Kenya watavuka mipaka kutavuta wamaasai wenzao Tanzania bila masharti Vile wanyama wa Serengeti wanatembeleana na wenzao wa Mara bila pasipoti ndivyo waendeshaji wa utalii watatembea kuenda Tanzania bila vikwazo vyovyote ili tuimarishe biashara ya utalii Vile Nyumbu wa Serengeti wanatungwa mimba Maasai Mara na kuzalia Tanzania ndivyo ng'ombe wa wamaasai watatungwa mimba huku Kenya na kuzalia Tanzania bila masharti yoyote Mtukufu Rais Suluhu Hassan ni heshima kubwa sana nikiwa mwakilishi wa wakenya walemavu kuwa mmoja wa Wabunge ambao walisikiza hotuba yako kwa vikao vya pamoja vya Bunge la Seneti na Bunge la Taifa Ilikuwa heshima kubwa sana na nashukuru sana Kuwa mama wa kwanza kuwa Rais Afrika Mashariki ni ishara tosha kuwa watu wetu wanadhamini vikundi maalum vya riba special interest groups kwa kimombo Kwa mapenzi ya Maulana mkenya mlemavu atakuwa rais hivi karibuni Rais Suluhu Hassan nakubaliana nawe kwamba Kiswahili chetu sio murua kama chenu Kiswahili chetu kina vioja na vitimbi Tulipoanzisha rasmi Kiswahili Bungeni mimi Mhe David ole Sankok nilifikiri Standing Orders zinatafiwa kama "Amri ya Kusimama" Naomba msamaha Nimejikakamua tangu tuanzishe Kiswahili Bungeni mpaka sasa at least nimeweza kuongea Kiswahili na nafikiri nitapata alama ya "A" Asante naunga mkono
Nasahihishwa kuwa ni Mhe. wa Igembe ya Kati samahani. Kitengo cha ndugu zetu ambao wanashughulika na wanyama wa pori kinauzoefu wa kujisongeshea ardhi kiholela. Kwa mfano kule Taita kutoka Maungu hadi Voi upande wa chini wa reli katika mwaka wa 2009 KWS ilijisongeshea ardhi ambayo ni ya wananchi. Watu wa sehemu hiyo wamepitisha ombi lao na litakuja kwa Spika. Ukienda Tsavo pale ambapo watu walishambuliwa na Simba wakati wa kujenga reli kuu KWS imefanya dhuluma hizo. Pia imefanya dhuluma katika sehemu za Taveta. Tukienda Kishushe wameweka ua ambalo sila stima lakini wameliingiza ndani ya ardhi ya wananchi. Hawakuweka ua upande wao. Ukiwauliza wanakwambia wameamua. Wakati umefika Bunge liingilie kati lione kuwa ardhi ya wananchi imerudishwa na wanyama wasionekana kama ndio wanahitaji ardhi kuliko wananchi. Haya maombi yote yako jiani. Niko katika Kamati ya Ardhi na nimemsikia Mhe. Makali kuhusi bodi cha mashamba. Tulimuita Waziri ambaye anahusika na shughuli za mashamba na bodi na alituhakikishia kuwa bodi zitarudishwa na Wabunge watahusishwa wakati watu wanapoteuliwa kwa hizo bodi. Namshukuru mwenzangu Mhe. wa Igembe ya Kati kwa kuleta Ombi hili kwa niamba ya watu wake. Ombi langu la Wataita pia liko njiani. Limefika Bungeni na tunatarajia hivi karibuni pia nalo litasomwa.
Nasema "Mhe. Ndugu Spika" kwa sababu hivyo ndivyo inafanywa. Singesema hivyo kwa Kiingereza lakini tunasema "Mhe. Ndugu Spika" kwa Kiswahili na eneo ambapo Kanuni za Kiswahili zinatumika. Mhe. Ndugu Spika naomba kutoa Hoja: KWAMBA Bunge hili liridhie Ripoti ya Tatu ya Kamati ya Utaratibu na Masharti ya Bunge kuhusu utafi wa Kanuni za Kudumu za Bunge la Taifa kwa lugha ya Kiswahili iliyowasilishwa Mezani mwa Bunge la Taifa June tarehe ishirini na tisa Oktoba mwaka huu na kuidhinisha toleo la Kiswahili la Kanuni za Kudumu za Bunge la Taifa na vilevile kuamua kwamba Kanuni za Kudumu za Bunge la Taifa kwa lugha ya Kiswahili zianze kutumika mwanzoni mwa Kipindi cha Nne cha Bunge la Kumi na Mbili. Kanuni za Kudumu ni Standing Orders . Nimesema "Kanuni za Kudumu". Mhe. Spika nimekuja hapa nikiwa nimejihami vilivyo. Niko na Kamusi ya Kiswahili sanifu ambayo naomba nimpe Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni ili ajisaidie nacho nikiendelea na mchango. Najua hatanielewa. Kama Bunge la Taifa tumeamua kwamba itakuwa bora tukianza kutumia Kiswahili na Kanuni zetu ziwe kwa Kiswahili. Itatusaidia kuangalia kwamba mambo yatakayo kuja mbele yetu yatatekelezwa kwa haki.
Nasema Baba Raila Odinga Sijasema Musalia mimi Kwa hivyo wakati ule ukifika tutakuja kule tukuombe na kukuambia tutembee pamoja Tunafurahia kwa sababu tunaona viongozi wanaibuka Wewe ndio wale viongozi wapya na viongozi wanamapinduzi ambao wana mawazo mapya ambayo yanaweza kutusukuma mbele Heko na naunga wote mkono kwamba zaidi Kama kuna nafasi pale mbele usikawie bwana Nenda kule kwa sababu tunajua wewe ni wetu Shukrani
Nashukuru Bw. Naibu Spika wa Muda. Ahsante sana. Ukosefu wa ai katika Kaunti ya Marsabit haujaanza leo. Ulianza kitambo sana kabla ya sisi kuzaliwa. Lakini kila kitu kina kianzilishi. Vita vilivyoko wakati huu vilianzishwa na viongozi. Lazima ukweli usemwe. Viongozi ndio kila kitu. Ndio kiini cha ukosefu wa ai katika Kaunti ya Marsabit. Vita vilianza Moyale na kufika North Horr. Vikaja Saku na sasa viko Laisamis. Mheshimiwa Naibu Spika wa muda kwa miezi mitatu sasa watu wa Moyale hawako Moyale tena. Wako upande wa Ethiopia. Watoroka wote kwa sababu ya ukosefu wa ai. Mheshimiwa Naibu Spika wa muda malori ne yamechomwa na yote yanabeba rasilmali zaidi ya milioni 30 kwa kila lori. Mheshimiwa Naibu Spika wa muda magari aina ya Land Cruiser yanachomwa. Mimi nalilia Serikali. Serikali iko wapi? Mbona Serikali isituangalia kama Wakenya? Kwani sisi siyo Wakenya? Nyumba kadhaa zimechomwa. Akina mama na watoto wamekuwa wakimbizi upande wa Ethiopia. Hili jambo litaendelea mpaka lini? Gari la mwisho kuchomwa lilichomwa wakiwemo askari kadhaa pahali pale. Wale askari wanafanya kazi gani? Serikali lazima itusikie ama itueleze kwamba Marsabit siyo Kenya. Tunataka kujua ukweli wa mambo. Ikiwa kila kiongozi atazungumza na watu wake itakuwa vizuri. Lakini unapata kwamba huyu anajaribu kuchochea na yule anatia chumvi upande ule mwingine. Wale viongozi wanalala vizuri kwao nyumbani. Watoto wao wanaenda shule vizuri. Lakini wananchi wale waliowachagua hawana ai. Watoto wao hawaendi shule. Kule shule kadhaa zimechomwa. Shule ni kabila gani? Watoto wote wanasoma katika shule hizo wawe Waborana Waburji Gari Gabra na Rendile. Kila mtu anasoma katika shule hizo. Shule kama hiyo inachomwa. Ni shule ambayo ina maendeleo zaidi na hufanya vizuri sana katika mitihani ya kitaifa.
Nashukuru Bw. Naibu wa Spika kwa kupata nafasi hii ili niweze kuwashukuru watu wa Kinango kwa kuniweka katika Bunge hili sasa nikitimiza miaka 15. Ninamshukuru Mwenyezi Mungu nikisema asante kwa yale ambayo niliweza kuyafanya kwa kipindi hicho. Ni ii yangu kwamba niliyafanya kwa uwezo wake Mola. Tunapokwenda kufanya sasa maombi yangu ni kwamba Wakenya waiombee nchi hii kwa sababu uchaguzi unafuata si wa kawaida; na kwamba yale yatakayoipata umma tarehe 4.3.2023 tumeze kuyapokea kwa mikono miwili tukiwa na ii kwamba yote yatakuwa kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu. Sisi kazi yetu ni kuomba. Analoitikia Mwenyezi Mungu ndilo litakalo kuwa. Kwa hivyo kwetu ni kumuregeshea Mwenyezi Mungu ahsante. Miaka mitano ni muda mrefu. Kwa sababu bado ninavuta pumzi za uhai ninamatumaini kwamba tarehe 4.3.2013 nitakuwa kwenye kinyang'anyiro ili kuangalia hatima ya maisha yangu ya kisiasa.
Nashukuru Mhe Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa kuchangia hii Bill ya mambo ya finance ambayo ni muhimu ya kukusanya ushuru ili kuweza kuchangia katika Bajeti yetu ya Mwaka 2021/2022 Kwanza nashukuru Kamati ikiongozwa na Mhe (Bi) Gs Wanga kwa kazi nzuri ambayo imefanya Jambo ambalo nimeona la kushukuru na ambalo tutaliunga mkono ni mambo ya kuongeza ushuru kwa mambo ya pikipiki; kwa watu wa boda boda Waziri wa NationalTreasury katika Bajeti yake alipanga kuongeza ushuru kwa mambo ya pikipiki kwa asilimia 15 Kamati imeangalia na sisi kama Wabunge tunaiunga Kamati mkono kwamba huo ushuru utolewe kwa mambo ya pikipiki ili watu wa bodaboda waweze kufanya kazi yao kwa njia nzuri Mhe Naibu Spika wa Muda kama ujuavyo saa hiii tukiwa katika msimu huu wa Coronavirus watu wengi wanafanya biashara ya boda boda Ukiangalia kwa mfano juzi jumamosi katika eneo Bunge langu la Endebess vijana wa boda boda walikuja kwangu wakasema "Mhe saa hii vile lockdown imewekwa sisi kulipia pikipiki ni vigurmu Unajua wengi wanachukua boda boda kwa deni ili wanaposafirisha watu wanatengeneza pesa ili waweze kulipia Kwa sasa kulipia hizo pikipiki ni shida Ikiwa tutaongeza ushuru wa asilimia kumi na tano tutafanya biashara ya boda boda kuwa ngumu sana Hawa ni watu ambao mapato yao ni ya chini na wanatafuta namna ya kuishi Kwa hivyo naunga Kamati mkono asilimia mia inaposema kuwa ushuru kwa boda boda utolewe Jambo lingine ambalo limesemwa na Mheshimiwa KJ Mbunge wa Dagoretti South ni kuwa LPG gas imewekwa ushuru Vile tujuavyo katika nchi yetu wakati huu tunajaribu kuchunga mazingira Tunapochunga mazingira inafaa tuhakikishe kuwa wananchi wanatumia environmental-friendly sources of fuel Nafikiri Waswahili wataitafi vizuri kusema tuchunge mazingira yetu Ili tuchunge mazingira yetu inapaswa tupike chakula kupitia LPG gas Bei ya mafuta taa imeenda juu kwa sababu ya ile tabia ya watu kuchanganya mafuta taa na petroli Kwa hivyo the Ministry ilisema kuwa ni lazima tuweke ushuru wa juu kwa mafuta taa ili wanabiashara wasichanganye na kudhuru magari yetu na kutuletea hasara Tunapohimiza wananchi watumie LPG gas kwa kupika inapaswa tuangalie kuwa ushuru wa LPG gas especially VAT ambayo imewekwa ifanyiwe zero-rating kama tulivyofanya kwa mkate Serikali ilitaka kuongeza ushuru kwa mkate Kamati iliangalia hiyo na kusema hapana Ushuru uliowekwa kwa mkate si sawa kwa sababu mkate ni food security Ni chakula ambacho kinaliwa na watu wengi Kwa hivyo Kamati ilisema ushuru kwa mkate utolewe Mimi na wengine hapa Bunge tunaiunga mkono Kamati kwa sababu wameangalia kuwa wananchi wa kawaida wanakula mkate especially katika institutions nyingi na familia Mkate ni chakula Kwa hivyo tusiweke ushuru kwa chakula kwa sababu tunapofanya hivyo tunaumiza Mkenya wa kawaida Kwa hayo mengi nashukuru na kuunga mkono Kamati katika marekebisho ambayo wataleta ili kuhakikisha kuwa mtu wa kawaida anapata afueni hasa katika bajeti ya mwaka huu Naunga mkono Mswada huu
Nashukuru Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia mwelekeo. Kabla sijatoa mapendekezo yangu wacha nifafanue kuwa niko na nia ya kugombea kiti cha ugavana katika Kaunti ya Taita Taveta 2017 lakini haimaanishi ningependa kupigania kiti cha ugavana wakati huo na sheria mbaya. Singependa niwe gavana na sheria mbaya ambayo itawafanya wafanykazi waendelee na wizi ambao ninauona. Ningependa niwe gavana ambaye atafuata sheria. Ndio maana ninapendekeza sheria hii ibadilishwe ili magavana wasiwe wanaweza kupunja na kutumia fedha za umma kiholela kama vile tunavyoona hivi sasa. Tukiangalia hali ilivyo hivi sasa kuna mambo matatu ambayo ningependa nichangie kwa undani. Kwanza vipengele vya 13 na 14 vinaleta vipengele vipya kabisa katika mwongozo huu wa matumizi ya fedha. Vipengele hivi vinataka Wizara ya Fedha ipewe mamlaka ya kutumia fedha za umma bila idhini ya Bunge. Naomba tukubaliane kuwa Bunge limepewa jukumu la kuidhinisha matumizi ya fedha za umma za Serikali yetu. Tukisema kuwa Wizara ya Fedha ipewe idhini ya kutumia fedha mpaka theluthi hamsini bila kupitia Bungeni nchi hii itajikuta kwa shida. Hii ni kwa sababu italeta uzembe na maafisa wanaohitajika kuwasilisha makadirio ya pesa hawatahusika na watasema kuwa hawawezi kuwasilisha kwa muda unaofaa kwa sababu kulingana na mwongozo wa sheria za matumizi ambazo tutapitisha zinawaruhusu kutumia fedha bila kuidhinishwa na Bunge. Napinga hicho kipengele na naomba kuleta mapendekezo yangu kuhakikisha kuwa idhini kama hiyo haitatolewa. Katika Katiba yetu tuko na Mkaguzi wa Vitabu vya Fedha za Serikali. Ni muhimu apewe nafasi ya kukagua vitabu na kuja na sheria na miongozo ambayo itasaidia fedha za Serikali zisifujwe vile watu wanavyotaka. Tukianza kumwekea vikwazo na kumfunga kamba ya shingo ili tumwelekeze jinsi ya kukagua vitabu kwa mujibu wa sheria ambayo tunaweka tutakua tunamnyima nafasi yake. Si ajabu kuwa hivi vitabu havitakaguliwa na vituo mwafaka ambavyo vinahitajika kuangazia vile pesa zimetumika. Si haki na sheria kumwekea Mkaguzi wa Vitabu vya Fedha za Serikali kitanzi kwani tutakuwa tunamnyima uhuru wake. Mhe. Naibu Spika wa Muda nikikumbuka mwaka jana katika zoezi hili la Mwongozo wa Sheria za Matumizi ya Serikali tuligeuza na kusema kuwa Wizara ya Fedha ina idhini ya kutumia pesa kulipia ada ya mikopo yote kutoka nje. Ilipokuja mambo ya 'Euro Bond' hawa mabwana walihakikisha kuwa zile fedha zilipoingia badala ya kuleta hapa Bungeni vile zilivyo walizitumia kulipa ada zingine huko nje. Walipoulizwa kilichotendeka walisema kuwa wamezitumia. Tulipouliza kwa idhini gani walisema kuwa tulikuwa tumeipitisha sisi wenyewe. Kipengele hicho kiangaliwe na wanyimwe hiyo ruhusa ili wasikope pesa na kuzitumia huko nje. Wenzangu wamechangia kwa undani kuhusu upotovu kukosa nidhamu na jinsi magavana wanavyotumia pesa za umma. Ugatuzi ulikuja ili tuwe na usawa na watu wasaidike mashinani. Lakini yanayotendeka ni kuwa kandarasi zinapeanwa kiholela na hakuna makadirio ambayo yanafuatwa. Ya kusikitisha ni kuwa kuna kodi ambayo ilikuwa inachukuliwa tangu hapo awali tulipokuwa na mabaraza ya miji. Fedha hizi zilikuwa zinaonekana waziwazi. Kwa mfano katika Kaunti ya Taita Taveta tulikuwa tunachukua Ksh140 milioni kutoka Soko la Taveta lakini tangu ugatuzi uingie ada imeshuka hadi Ksh80 milioni. Shiling milioni sitini zimeenda wapi? Wanaajiri wafanyikazi na kuwalipa Kshs18000 kwa mwezi na wanaleta kodi ya Ksh3000. Hiyo kodi ingine haipatikani. Je huo mshahara unaomlipa unatoka wapi? Mhe. Naibu Spika wa Muda upotovu na ukosefu wa nidhamu kama huu umeletea Kaunti ya Taita Taveta matatizo chungu nzima. Wenzangu walikuwa wanazungumza kuhusu akaunti ambazo ziko Banki Kuu ya Kenya. Unakuta kuna hundi ambazo zimetolewa za karo lakini zote zimerudi kwa sababu hakuna fedha. Ni Jambo la kusikitisha kuona kuwa kaunti inaweza kutoa fedha kupatia wanafunzi za kuwasaidia kulipa karo na hizo hundi zote zirudi kwa sababu hakuna pesa kwa akaunti. Ni jambo la kuaibisha na naomba lichukuliwe hatua ambayo inahitajika ili kuwe na nidhamu katika matumizi ya pesa za umma. Tukiwacha hawa magavana waendelee vile wanavyofanya na nchi iendeshwe hivi nchi hii itakwama na kusimama na hakuna lolote litaendelea kufanyika. Tutapatwa na hasara. Nikimalizia ningependa sheria hizi zigeuzwe ili tuhakikishe usawa na haki. Kuna ndeni ambalo litawachwa na magavana wakati huu kwa sababu katika makadirio yao wanaweza kutoa kandarasi lakini hawatailipia. Wataipeleka mbele kwa makadirio ya mwaka ujao. Kwa hivyo kila wakati kuna deni na hili deni linaendelea kukua. Hii nchi itajikuta iko katika matatizo na imejitia kitanzi. Ndiyo maana naunga mkono Mswada huu.
Nashukuru Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa nafasi hii nami nitoe mchango wangu kwa Mswada huu unaotoa mwongozo wa matumizi ya fedha za umma. Ijapokuwa umeshatoa uamuzi kuwa si muhimu tuwe na Ripoti ya Kamati ili kujadili Mswada huu naomba nitoe mapendekezo kuwa lingekuwa jambo la busara sana kama Ripoti ya Kamati ingekuwa imejadiliwa Bungeni ili Wabunge wapate mwongozo na mwelekeo wa kuchangia kwa undani Mswada huu.
Nashukuru Mhe. Naibu Spika wa Muda. Jambo muhimu katika Mswada huu ni kwamba wakati mtu anapofikwa na maafa anahitaji msaada. Ikiwa atafikiwa kwa kuchelewa itakuwa hakuna faida sana. Kwa hivyo namshukuru sana ndugu yangu Mhe. Kii Ichung'wah kwa sababu tuna matatizo mengi. Saa hii kwangu kumechomeka nyumba nne na hakuna mtu anayeangaliwa isipokuwa Mhe. Mbunge. Kwa Hivyo hili ni jambo muhimu sana. Pengine hata moto ambao hutokea mara kwa mara kule Kariako utaweza kuzuiwa kwa sababu hali hiyo itakuwa inaangaziwa. Utafiti utakua umefanywa kubainisha ni sababu gani mambo hayo hutokea. Vile vile ningeomba.
Nashukuru Mhe. Naibu Spika. Nataka niwaambie kwamba ninapoongea lazima nikunje kidole na nifanye hivi kila mahali. Kunielewa pia ni vigumu. Kuelewa ni kipawa. Mimi nataka nipinge kutoka mwanzo kwamba madhumuni ya kupunguza wakati ni mbovu.
Nashukuru Mhe. Naibu wa Spika kwa nafasi hii. Nataka kuwarai Wabunge wenzangu kwamba hili ni Bunge la sheria na utaratibu. Kwa hivyo tufuate utaratibu na sheria ambazo zinaliongoza Bunge hili. Natoa pongezi zangu za dhati kwa Kamati Teule ambayo iliwasilisha Ripoti hii. Nitasema aake ni lazima niseme ninayotaka kusema. Kamati Teule ambayo imewasilisha Ripoti hii iliongozwa na Wabunge ambao tunawaheshimu sana. Wamesifika sana haswa kwa masuala ya kisheria. Kuhusu makamishna ambao wanatarajiwa kuondoka kutoka ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ninaiunga mkono Ripoti hii. Mhe. Naibu wa Spika naomba unilinde dhidi ya hawa mabwenyenye.
Nashukuru Mhe. Spika kwa fursa hii. Ningependa kuchukua fursa hii kwa niaba yangu binafsi na niaba ya watu wa Marsabit na watu wa Mashariki ya juu ya Kenya kwa jumla kutuma rambirambi zangu za kirasmi kwa familia marafiki na watu wa Homa Bay kwa kumpoteza mpendwa wao Senator Kajwang'. Pia ningependa kuambia Waheshimiwa wenzangu wote kwamba maisha sio ya milele. Kwa hivyo tuwafanyie kazi watu waliotuchagua. Tuwawakilishe vizuri katika hili Bunge. Naomba Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.
Nashukuru Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii kutoa rambirambi zangu. Kwa niaba ya watu wa Kisauni nasema pole ndugu jamaa na familia ya Senator Kajwang'. Vilevile nitachukua fursa hii kusema pole kwa familia nne zilizouawa juzi katika eneo Bunge la Kisauni kupitia mikono ya majambazi. Tunawaombea roho zao zilale mahali pema peponi.
Nashukuru Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii niomboleze rafiki yangu wa dhati Mhe. Litole. Nilibahatika kuwa naye katika Bunge la Kumi. Naomba nichukue nafasi hii kutuma rambirambi kwa familia yake na jamii yake kwa ujumla. Nilipata nafasi ya kuandaa naye hadi nyumbani kwake na tukapata nafasi ya kuhudhuria ibada ya misa takatifu pamoja naye. Ni Mbunge niliyemfahamu na nikamjua. Nilipata nafasi ya kumwalika katika eneo langu la Bunge. Akaja hadi Taita na akawajua watu wangu. Nilimjua Litole kama Mbunge aliyeshughulikia watu wake kwa taaluma na azma nzuri. Ningependa kuchukua nafasi hii kuitakia familia yake uponyaji wa kiroho wakati huu wa majonzi. Naomba Mungu ailaze roho yake pahali pema peponi.
Nashukuru Mhe. Spika. Kwa hivyo Kiswahili si lugha geni. Kiswahili ni lugha yetu. Ili uhuru wetu ukamilike mara kwa mara. Kwa ruhusa yako nilikuwa kwa ofisi ya Kirui kujua amefikisha wapi hatua hii. Leo nina furaha kwa sababu ndio chimbukizo kwa utunzi wa sheria na sera kwa nchi nzima. Hivyo basi ili tuweze kutunga sera na sheria kwa mujibu wa Kiswahili ni lazima tuwe na kanuni za kudumu kwa Kiswahili. Tukio la leo ni la kihistoria. Mchakato mzima msafara mzima wa kuleta Kanuni za Kudumu za Bunge la 12 la Kenya unastahili kupewa kongole. Mimi leo kwa sababu ya furaha sitaki kuzungumza kwa upana zaidi. Nimesimama kuafiki Hoja. Na naomba iweze kupitishwa leo ili kesho izinduliwe rasmi. Kwa hayo nimesimama kuafiki. Ahsante.
Nashukuru Mheshimiwa Mwanyoha. Ahsante.
Nashukuru Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa nafasi hii umenipatia nami nitoe mchango wangu.
Nashukuru Mheshimiwa Spika kwa nafasi hii ambayo umenipatia nami nitoe mchango wangu kuhusu hawa ndugu na dada zetu ambao wamependekezwa ili wapewe kibali na Rais tukianzia na Bunge ili nao waingie kazini na kuwapa Wakenya matumaini ya kuwa uchaguzi utakuwa huru na wa haki maana hivi sasa hatuna Tume nzuri. Tunataka kina Hassan waondoke na ni muhimu sisi kama Bunge tumalize zoezi hili ili tuwape Wakenya kwa ujumla nafasi ya kupiga kura ifikapo August. Nikiangalia orodha ile ambayo tumepatiwa hapa Bungeni kuanzia Mwenyekiti na wenzake naona kuna usawa ambao umependekezwa kati ya wanawake na wanaume ili tufuate vile Katiba inavyosema. Mambo ya maadili hayajatolewa wazi wazi. Hamna mtu ambaye ameenda kwa Kamati ambayo ilikuwa inawahoji kuzungumzia kwa undani kuhusu swala la maadili na nidhamu. Kuna mmoja wao ambaye alikuwa ana wasiwasi kuwa maadili ya hawa ambao wamependekezwa kuwa huenda ikawa ni tisho au huenda ikawa inaleta cheche zozote. Bali tukisoma ripoti ya Kamati inaonyesha kuwa wote ambao wamependekezwa walikuwa wamehitimu kitu cha kwanza maadili yao yaliridhisha ya tatu wana uzoefu ijapokuwa pia mna swala ambalo limeandikwa mara kwa mara kuwa labda hawana uzoefu. Lakini inategemea ni uzoefu wa aina gani. Tukiangalia hawa wote tukianzia na Mwenyekiti ni watu wamehitimu wamesoma ni watu ambao wamefanya kazi ni watu mara nyingi wamepewa shughuli kadha wa kadha na wakazifanya wakazitekeleza na wakazitimiza bila shida yoyote. Katika hao wote ambao wamependekezwa naomba niwe wazi kuwa wawili wao ni watu ninawafahamu sana. Nitaanza na Wanjala. Yeye ni binti anayetoka Taita ijapokuwa ni mzaliwa wa Kwale. Babake ametoka Sungululu katika Wilaya yangu pale ambapo mimi mwenyewe nawakilisha kule Wundanyi akahamia Kwale na bintiye akazaliwa lakini amerudi huko Taita. Ni binti ambaye namfahamu na ana uadilifu wa kutosha kwa hivyo hapo sina wasiwasi. Nina ii kuwa atatekeleza wajibu wake na atafanya kazi na ii sawa. Nikiangalia huyu mwingine ambaye watu wanaanza kushangaa ni nani ni dada yetu Consolata Nkatha Bucha Maina. Nimemfahamu akiwa mwanafunzi miaka theini nikiwa wakati huo ni Meneja katika Industrial Development Bank. Nimemfahamu akiwa mtoto mwanafunzi akiomba kazi. Amefanya kazi wakati huo wote hata wakati ameenda Kenya Wildlife Service (KWS) nilikuwa consultant kule na ninafahamu kuwa ana uadilifu. Mara nyingi watu wanaweza kuuliza unawafahamu aje hawa watu? Ninawafahamu kwa sababu ya uzoefu wangu wa kazi. Nikiangalia kama Duale hana uzoefu kama ule nilionao ndio maana wakati mwingine anaanza kutia wasiwasi lakini ule uzoefu nilio nao na umri nilionao nimeona mengi nimekutana na wengi na nimeangazia mengi. Kwa hivyo sina wasiwasi wakati huu kwa kazi ambayo imefanywa na Kamati yetu ya Sheria. Ni kazi ya kuridhisha na watu ambao tumewapatia. Tukiangalia ule muda tulionao hata tukianza kusema kuwa tutafute wengine huo muda tulionao wa kufanya uchaguzi August ni muhimu tumalize hili zoezi ili waingie kazini. Lazima Wakenya tuweze kuwa na ii na Wakenya wenzetu. Kama kila wakati hatutakuwa na ii na Wakenya wenzetu itakuwa inatuletea shida. Labda ni kama haya ambayo yalikuwa yanasemwa hapa wakati tulikuwa tunatoa maamuzi kuhusu Mwenyekiti wa Tume ya Maadili na Ufisadi. Watu wengi walikuwa na wasiwasi. Wasiwasi wangu ni kuwa je tunamjaribu mtu wa Mungu katika kazi ambayo itamletea vishawishi na baadaye tuingize Kanisa katika shida? Huo ndio wasiwasi nilikuwa nao. Mpaka sasa ninao. Lakini kwa hawa ambao wanaenda kuangalia mambo ya usajili wa kura kusimamia uchaguzi na kuhakikisha kuwa nchi hii inafanya uchaguzi wa haki ambao utakubaliwa na kila mtu sina wasiwasi kuwa watatekeleza wajibu wao na wataweza kufikisha nchi mahali iliko. Naomba nichukue nafasi hii pia kuwahimiza Wakenya. Bunge linatimiza wajibu wake. Wakenya nao watimize wajibu wao wa kujitoa waende wajiandikishe wajisajili kuwa wapigaji kura maana haina haja tupitishe hawa sisi kama Bunge tuna ii watafanya kazi na hawatashindwa kujiandikisha wawe ni watu wachache halafu uchaguzi utakuwa umefanywa na idadi ndogo sana ya Wakenya ikilinganishwa na ile inatakikana. Tunaomba Wakenya wakati huu ambao umetolewa na IEBC wachukue wakati huu waende wajiandikishe. Nasi kama Bunge tunakamilisha zoezi hili leo. Nina ii Wabunge wenzangu tutaunga mkono mapendekezo ambayo yameletwa hapa na Kamati hii ya Sheria ili tukamilishe na Rais awapatie kibali waanze kazi hata ikiwezekana kesho kutwa na hao wengine wafunge virago waende. Kwa hayo mengi naomba niunge mkono wote ambao wamependekezwa katika Ripoti hiyo.
Nashukuru Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii na pia nashukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kurudi hapa. Tulikua na muda mzito sana lakini Mwenyezi Mungu ametuwezesha kurudi. Ni jambo nzuri ujiweke kwa Mwenyezi Mungu na tujadiliane vile mambo yalivyo mbele yetu na tusipige kelele. Mtoto anaweza kupiga kelele na hajui kuzungumza na unashindwa anataka nini. Ni peremende unga ama ni nini anataka? Lazima mtu aanze kuongea ndio tuweze kujua. Hatukukuja hapa kuzungumza mambo ya Rais ama Raila. Tumekuja kuzungumza yale mambo yaliyo mbele yetu. Kuna watu wanasema eti Rais ameshindwa. Si Rais. Hatujaona Upinzani ukileta Mswada wowote ambao unaongea juu ya mambo wanayozungumzia. Waseme tumeleta Mswada unaohusu jambo hili na hili. Hakuna. Tunawahitaji sana wasaidie kukosoa na wasaidie kuleta Mswada utakaosaidia. Ni muhimu sana. Kama hawawezi kuleta hiyo ni kelele tu. Nashangaa mmoja ni rafiki yangu. Nashangaa kwa sababu Wabunge huelewa kwamba tuko hapa kutetea nchi hii. Ninaona wengine kwa sababu wameruka kutoka Jubilee na kuenda upande wa Upinzani na ni watu wanahitaji kujua msimamo wao wanaanza kuzungumza mambo ya kushangaza. Pengine wangekua Bishops lakini mtu lazima achunge na ajue Mwenyezi Mungu anatujua. Tuzungumze mambo ya ukweli na si mambo ambayo hayatusaidii.
Nashukuru Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Nimesimama kuunga mkono Mswada huu lakini pia tunayo mambo nyeti ambayo tunahitaji kuangalia sisi kama Wabunge. Kwanza tunajadiliana mambo ambayo hatuna uwezo kuyahusu. Kila mara tunalaumu Serikali ilhali sisi ndio Serikali.Tukiwa hapa tuna mikakati ya kisheria ya kumwita Waziri yeyote ili kuchunguza mambo ambayo tunataka yawe ni kuhusu fedha ama mabadiliko ambayo tunataka. Lakini ninaona tunalia tu bila kuona tuna uwezo wa kufanya hilo jambo. Nakubali kuna mambo nyeti ambayo tunayazungumzia hasa kuhusu serikali za kaunti. Kuna kaunti zimefanya vizuri sana na kuna nyingine ambazo zina shida. Hata hivyo tuna uwezo wa sheria kuchunguza ni nani amekosa kufanya kazi yake. Ndugu zetu katika Seneti mimi naona wana shida. Hii ni kwa sababu wakipendekeza na kupitisha kwamba pesa zipeanwe kwa kaunti sisi hapa tunapitisha hilo. Mwenye kuangalia fedha akitoa ripoti yake kusema pesa zimefujwa sioni Seneti ikifuatilia. Kwa maoni yangu Seneti iweze kusema "tulipendekeza hii na ikapitishwa lakini hii pesa imetumika vibaya." Pengine ni kwa sababu wengi wao wanataka kuchukuwa hivyo viti vya magavana. Nafikiri ndio maana hawataki kuunda sheria itakayochunga hizo pesa. Tunazungumza mambo ya kupatia makaunti pesa lakini hatujadiliani kuhusu ile pesa wanayokusanya. Hatuoni wala hatusikii. Hizo pesa ni zao za kula. Ni pesa za wizi na za kufujwa. Mbeleni kulikuwa na mabaraza ya miji na ispaa . Mfano ni ispaa ya Nakuru ambayo ilikuwa ikijisamamia bila kupewa pesa na Serikali. Wakiongezewa ilikuwa ni pesa kidogo kutoka kwenye hazina ya Local Authority Transfer Fund (LATF). Sasa hii wanapewa pesa nyingi na Serakili lakini Maseneta hawafuatilii pesa ambazo wanatoza watu ushuru. Ni muhimu Seneti ifuatiliie kwamba Kenya Revenue Authority (KRA) iwe ikitoza ushuru.
Nashukuru Naibu Spika. Ni kitu cha maana kwamba katika Mswada huu tumeeleza jinsi ujenzi wa barabara utakavyotekelezwa. Imekuwa taabu kubwa sana hasa kuhusu jinsi ambavyo serikali za kaunti zinajenga barabara. Kwa hivyo nataka kupongeza Kamati iliyowasilisha Mswada huu. Ni matumaini yetu makubwa kwamba mahali kulikosahaulika kutakuwa na mabadiliko hivi karibuni. Nashukuru.
Nashukuru sana Bi. Naibu wa Spika kwa kunipatia hii nafasi. Ningependa kuanza kwa kumpongeza Rais Kenyatta kwa Hotuba yake. Namshukuru kwa kuweza kufika hapa ili kulitangazia taifa yale mambo Serikali ya Jubilee imekuwa ikifanya kwa muda wa mwaka mmoja ambao umepita na yale ambayo Serikali inapanga kufanya kwa kipindi kijacho. Kuhusu maadili ya kitaifa na misingi ya utawala lile ambalo litafanya hii nchi iweze kuendelea ni sisi kuanza kutilia maanani maadili. Kwanza kabisa inatupasa kushikilia uzalendo. Isiwe kwamba kila mtu anajitakia mambo yake binafsi na kusahau mambo ya taifa. Ukienda kwenye barabara kila mmoja anataka kuruka laini ili aweze kufika mbele ya watu wengine na hali wanavunja sheria. Ukienda kwenye biashara hasa na Serikali kila mmoja anajaribu kutoa hongo ili aweze kupitishwa mbele ya wengine ambao wangefaulu zaidi. Kuhusu umoja katika nchi nafikiri kwamba ni muhimu sisi Wabunge tuepuke mizozo. Isiwe kwamba tukija hapa kila wakati tunazozana tukijaribu kuonyesha jinsi sisi tuko upande huu na wale wengine upande ule mwingine. Sisi ni viongozi wa taifa na tunastahili kuiweka hii nchi pamoja pasi na kuleta utengano hasa tukitumia ukabila. Ni muhimu pia tuanze kuwakumbuka na kuwaheshimu mashujaa wetu. Tuna mashujaa wengi sana ambao wamepigania hili taifa tangu enzi za uhuru. Kufikia sasa tunaongea tu wala hatufanyi jambo kuwakumbuka mashujaa wetu. Jambo ambalo ningekumbuka na ninafurahi kwamba Serikali ya Jubilee imelifanya ni kuwakumbuka wanyonge katika jamii. Hili jambo la kuwapatia wazee kiinua mgongo ni bora. Tumewakumbuka mayatima. Tumeongeza zile pesa ambazo huwa wanapatiwa. Wale ambao ni walemavu katika jamii tumeweza kuwaongezea pesa. Haya ni mambo muhimu katika nchi. Serikali ya Kibaki iliwakumbuka wanafunzi wa shule za msingi. Itakuwa muhimu sana basi Serikali hii yetu ya Jubilee iwakumbuke wanafunzi wa shule za upili ili wanafunzi wote kama ambavyo Katiba imenena masomo ya msingi yasikomee Darasa la Nane bali yafike Kidato cha Nne. Hivyo nchi hii itaendelea zaidi. Ni muhimu tuwakumbuke wale ambao hawana kazi. Hata tukiendelea kuajiri polisi wengi katika nchi haitawezekana kuajiri polisi wa kutosha. Ni muhimu tukumbuke wale ambao hawana kazi. Tusipowatafutia kazi hawa vijana na kupeleka raslimali kule mashinani ukweli ni kuwa wakikosa kazi usalama hautakuweko. Tuwakumbuke polisi vile vile ili wasije kulalamika kila wakati juu ya mishahara yao. Namshukuru Rais kwa Hotuba yake.
Nashukuru sana Mhe Spika Ninaongea kwa niaba yangu familia yangu na watu wa Nakuru Town East Constituency na ninaleta rambirambi kwa familia na jamaa za ndugu yangu marehemu Mhe Jakoyo Midiwo ambaye tulijuana katika Bunge la Kumi na Moja Mwendazake Mhe Jakoyo kwa yale mambo alifanya wakati ule alitufunza mengi sana wakati alipokuwa akifanya debate sana sana Marehemu Mhe Jakoyo alikuwa ni mtu aliyekuwa informed sana Tulikuwa tunamheshimu Mhe Aden Duale lakini ile information Mhe Duale alikuwa nayo he had always an answer for that I respected the late Jakoyo Midiwo kwa yale mambo alikuwa akitoa wakati ule ya kuweza kutupatia kama wageni katika Bunge hili kuweza kuweka Miswada Hasa alikuwa akiniambia vile alishiriki katika kupitisha Constitution ya 2010
Nashukuru sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Awali kidogo nilikuwa na wasiwasi kwa sababu nimekitegea sana hiki kidude. Nashukuru kwa fursa umenipa. Wazee wa mtaa ni uti wa mgongo wa taifa. Kwa masuala ya kuunganisha jamii wao ndio uso wa Serikali. Hawa ndio wanashughulikia masuala ya usalama wa kijamii. Matatizo yakiwepo kwa jamii wao ndio huleta watu pamoja. Serikali ilipoanzisha Nyumba Kumi ilikuwa inategemea wazee wa mtaa waishughulikie. Lakini ukiangalia hali yao wamezorota. Ukiangalia jinsi machifu na wakubwa wengine wa Serikali wanashughulikiwa utashangaa jinsi wazee wa mtaa wameachwa bila kushughulikiwa. Wao pia wana watoto wanaowasomesha. Vilevile wana makao lakini ukiangalia makao yao hayastahili watu ambao wanafanya kazi kwa Serikali. Vilevile wana famila za kutunza na kupatia chakula. Afya ya wengi imezorota. Hatua za Serikali za kuimarisha hali yao duni ni kama kusema; "kufa kwa inzi kidondani sio hatia." Hata hii haingekuwa Hoja. Ungekuwa Mswada ili tuitunge sheria kama Bunge kushurutisha Serikali kuwalipa wazee wa vijiji kama wafanyikazi wengine was Serikali. Kwa hivyo naunga mkono wenzangu kwamba Hoja hii tuipigie kura ya upato tukitarajia kwamba Serikali itaitilia maanani. Tatizo ni kwamba Hoja inazungumziwa hapa lakini haishughulikiwi. Kwa hivyo natarajia kitengo husika ndani ya Bunge kitaweza kusukuma Serikali iweze kutilia maanani matakwa ya hawa wazee wa mtaa. Nashukuru.
Nashukuru sana Mhe. Spika. Ningependa kuunga mkono uamuzi wa Kamati iliyoteuliwa kuleta maridhiano kati ya Bunge la Seneti na Bunge la Kitaifa. Ni kweli kwamba kumekuwa na matatizo kuhusu makao makuu ya serikali za ugatuzi. Ni muhimu sheria hii ipitishwe ili kuwe na uwazi na uhakika kuhusu mahali ambapo makao makuu yatajengwa. Sehemu zingine kama katika serikali ya Kaunti ya Nyandarua hatujakuwa na makazi hayo. Tumekuwa tukikodisha ofisi za serikali za Kaunti juu ya maduka. Ni muhimu kuwe na uamuzi wazi kuwa makao makuu ya serikali ya ugatuzi inapatikana mahali fulani. Hii ni kwasababu raslimali zinazotakikana kujenga hayo makao makuu zitumike. Hii itatusaidia kujua kwamba hapa ndipo makao makuu yataendelea kwa muda mrefu na hayatabadilishwa leo au kesho. Pia naunga mkono sheria hii inayosema kuwa wananchi wenyewe wahusishwe katika uamuzi iwapo kutakuwa na pendekezo la kuhamisha makao makuu. Naomba serikali iendelee kusaidia zile kaunti ambazo hazina rasilmali namijengo yakutosha ili kuwa na makao makuu ya kaunti. Asante.
Nashukuru sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Nasimama kuunga mkono Hoja hii. Nina hakika Wabunge wote tutaunga mkono Hoja hii kwa sababu inapendekeza utaratibu mwafaka. Maji ni uhai. Nina hakika wakati tuliamka asubuhi hakuna mtu hakutumia maji. Kwa hivyo maji ni kitu cha muhimu sana. Nakubaliana na wale ambao wamesema kuwa utaratibu wa maji lazima upangwe kwa njia nzuri. Najua tuna maji ya kutosha lakini mikakati ya kuweka maji pamoja sharti iwepo. Sharti wizara mbalimbali ziwekwe pamoja ili zitengeneze utaratibu kuhusu ukusanyaji na matumizi ya maji. Wananchi sharti waelewe kwamba nafasi na maeneo ya kujenga barabara ni wao wanapaswa kutupatia. Wasipotenga ardhi ya kutengenezea barabara hali itakuwa ngumu. Maji ni mengi hasa ya mvua. Tusipoyakusanya tutazidi kuwa na shida ya maji. Maji yamekuweko lakini hatukuweka mikakati ya kuiteka ili itusaidie kesho. Hili ni jambo tunalohitaji kuangazia kwa kina. Tunastahili kushikana sote ili tusaidie watu kwa njia nzuri itakayotusaidia kwa maisha yetu baadaye na ya watoto wetu. Maji inapotea kwa sababu ya kukosa mikakati na sheria. Hii inafanya tupoteze maji kwa wingi. Mvua imenyesha kwa muda mfupi sana na watu wameanza kulia kwamba maji imeharibu mashamba na mabonde mengine. Baada ya wiki mbili mvua ikiisha tunaanza kulia kuna ukame. Hii ni kuonyesha ya kwamba hatujaweka mipangilio na mikakati vile inavyotakikana. Jambo ambalo liko mbele yetu ni la kuweka mikakati sheria za kusaidia na kuleta wadau wa pande zote pamoja ili tupitishe mikakati mizuri kuhusu maji ambayo itasaidia Kenya. Hata imechelewa. Hii Hoja ingeletwa kitambo ili itusaidie sisi wote. Tuko na bwawa moja ambalo limetengenezwa juzi na Serikali. Nimesikia kwamba wanataka kutengeneza mabwawa katika kila eneo bunge. Katika eneo bunge la Bahati tulikuwa na shida ya maji sana. Tuko na mabwawa machache na watu wa Bahati wameanza kusherehekea kwa sababu wataanza kupata maji mazuri. Huko Bahati tuko na mabwawa ambayo yalitengenezwa wakati wa mbeberu karibu miaka sitini iliyopita. Lakini hayo mabwawa hayajaundwa upya ili yaweze kuteka maji mengi kwa sababu watu wameongezeka. Naunga hii Hoja mkono na najua Wakenya watafurahia tukiipitisha na kushirikiana ili tuweke mikakati na sheria nzuri kuhusu maji. Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii.
Nasimama kwa hoja ya nidhamu Bw. Spika wa Muda. Kwa nini Sen. Kisasa anasema kuwa sijui lugha ya Kiswahili ilhali nimekuwa katika siasa kwa miaka 20 sasa?
Natoa rambirambi zangu kwa familia ya Moi. Moi aliimarisha elimu alijenga hospitali. Ndio sababu tuko na Wadi za Nyayo mahali akina mama wanaenda kujifungua. Alipenda akina mama sana. Ndio maana alikuwa ananunua matunda na ndizi njiani. Hakutaka akina mama wateseke. Alikuwa alikuwa mkristo aliyeogopa Mungu ndiposa akakaa madarakani kwa miaka 24. Ni kwa sababu alikuwa mtu wa Mungu. Hapo sisi wanasiasa tujivunie na tujifunze kutoka kwake. Asante.
Natumaini muda wangu unaangaliwa usije ukaisha kwa sababu ya shughuli za kuangalia nani amezungumza na nani hajazungumza. Kisiwa cha Migingo ni sehemu ya Kenya. Mimi ni Mkenya na nawakilisha sehemu ya Wundanyi ya Taita Taveta ambayo ni sehemu ya Kenya. Sehemu yoyote ya Kenya ikiguswa na mtu yeyote nina haki ya kuzungumza kuhusu jambo hilo na kutoa mchango wangu. La pili tumesikia na tumeelezwa kuwa mara nyingi Hoja zimeletwa hapa Bungeni kuhusu Kisiwa cha Migingo lakini hakuna lolote linalofanywa. Watu wanaumia wanauawa wananyang'anywa mali yao na Serikali yetu inaangalia. Kulingana na maoni ambayo yametolewa hapa leo tumeelezwa kuwa kulikuwa na tume ambayo ilienda Uganda ikajadiliana na Serikali ya Uganda na wakakubaliana kuwa masoroveya wapime waangalie wafuate utaratibu na wajue hii sehemu ya Migingo iko sehemu gani. Walikubaliana baadaye kuwa Migingo iko upande wa Kenya. Serikali ya Uganda ikakataa kuweka sahihi makubaliano hayo. Baadaye Serikali ya Kenya ikaanza kuongeza biashara na wao. Ni kwa nini tunabembeleza Uganda? Ni nini wanachotupatia ambacho kinatufanya tubembeleze Serikali ya Uganda? Hata wakati wa hayati Rais Amin mnakumbuka vitisho alivyotupatia lakini Serikali ya Kenya ilitoa ukali ikaiambia kuwa "hebu jaribu na tutaona ni nini kitafanyika". Walipojaribu kuvamia Tanzania Mhe. Mwalimu Kabarage Nyerere alitoa jeshi lake likaenda likakomesha Uganda. Sisi watu wa Kenya tunaendelea kulalia masikio. Hata hivi tulivyo si Migingo peke yake. Hata Somalia imeanza kusema ufuo wa bahari upande wa Lamu kuenda ndani mpaka kilomita 200 ni sehemu yake. Kenya bado inatapatapa. Hatujui kama kesho sehemu ya Tanga upande wa chini wa Mombasa itapeanwa nchi nyingine. Wakati umefika wa Serikali ya Kenya kuamka na kusema waziwazi kuwa hatutavumilia watu wetu waendelee kuteswa kunyanyaswa na kudhulumiwa katika Kenya. Tukiwa na shida kama hizo na Majeshi yanatakiwa yalinde mipaka yetu tunashangaa ni kwa nini tusishugulikie mambo kama hayo ya mipaka badala ya kutuma magari na Wanajeshi kwa uchaguzi mdogo wa Malindi. Hata haya hatuna. Tuko tayari kuzozana sisi wenyewe na kunyang'anya magavana wetu silaha zao ambazo wanazitumia kwa ulinzi wao. Ndio maana tunasema haki ifanyike. Tufanyie watu wa Migingo haki na watu wetu hapa nchini tuwafanyie haki. Mambo kama haya tunayaona ya kina Joho hayaturidhishi yakifanywa humu nchini kwa Wakenya. Kwa hivyo naweka mkazo na nasisitiza kuwa wakati umefika Serikali ichukue hatua kuwalinda watu wa Migingo. Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Ndio Mhe. Spika wa Muda nimekubali anifahamishe mahali ambapo ameona kwamba nahitaji kufahamika.
Ndio naendelea Nitaeleza Katika hali yangu ya kuafiki natoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais wetu Uhuru Kenyatta kwa kumwalika Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Namshukuru haswa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutembele Bunge letu la Kenya Ningependa kusema kuwa ndugu si kufanana tu bali ni kufaana Ndugu wa Kenya na Tanzania ni ndugu ambao wamezaliwa Kama vile Mheshiwa Rais Suluhu Hassan mwenyewe alivyosema kutengana kwetu hakuwezekani kwa sababu sisi ni ndugu wamoja Mimi natoka maeneo ya mpakani Haswa tunapakana pale Taveta na Holili upande wa Tanzania Sisi ni ndugu kwa sababu ndugu zetu wengine wamevuka mpaka wako upande ule mwengine Wengine kutoka Tanzania wako upande wetu Vile vile ndugu wa Kenya wameolewa na wameoa Vile vile ndugu wa Kenya wameolewa na wameoa Tanzania Hivyo basi kama vile Mhe Raisi Samia Suluhu alivyosema mimba yaweza tungiwa Kenya ikazaliwa Tanzania Ukweli wa mambo ni kuwa hospitali ya karibu pahali ambapo huwa tunatuma wagonjwa kukiwa kunahitajika matibabu zaidi ni upande wa Tanzania Kilijaro Christian Medical Center ambayo iko upande ule kwa sababu ndiyo iko karibu kushinda kuenda Voi ambako hutuchukua safari ndefu Katika hali ya kukaa pale mipakani hatuwezi kugawa hali ya uchumi wetu kwa sababu hakuna uchumi wa mpaka huu ama mpaka ule Wakulima wetu wanauza bidhaa zao haswa vyakula wanavyovuna mashambani upande ule mwingine na wale pia wanauza bidhaa zao upande huu Hivyo basi Mhe Rais katika hotuba yake akitaja mpaka wa Taveta na Holili ambako kuna ile inatwa kwa Kingereza one-stop-boarder pahali pamoja pakufanyia shughuli za mipakani kazi zinazoendelea pale zinaleta faida kwa watu wetu kutoka pande zote mbili Ningependa kutaja kuwa sisi tunaotoka mpakani kama Taveta Mwaka wa 2015 nataka kuwakumbusha kuwa Mhe Raisi Uhuru Kenyatta alimualika Mhe Rais Jakaya Kikwete kule Taveta kabla hajamaliza awamu yake Wakati huo wakaanzisha ile barabara inayoelekea upande wa Voi Haya yote yalitendeka kwa sababu ya uhusiano mzuri ulioyoko kati ya Kenya na Tanzania Vile vile namshukuru Mhe Samia Suluhu Hassan kwa sababu mwanzo wa ziara zake ameona kuwa aweke Kenya mbele aipatie nafasi ya awali ili aweze kututembelea Haya yote hayangewezekana kama siyo uhusiano wetu mzuri ambao una mizizi mirefu sana Hata Kanuni za Kudumu za hapa Bungeni zilizinduliwa na Bunge la Muungano wa Tanzania Hatuyachukulii maswala haya kama mchezo Haya ni maswala ya undugu ambayo tutazidi kudumisha Ningependa vile vile kushukuru kuwa Mhe Rais Mwendazake John Pombe Magufuli aliamua kumpatia nafasi mama Rais Samia Suluhu Hassan kuwa naibu wake Sasa hivi ndio amepata nafasi hiyo ya kuwa Rais Alionyesha heshima kubwa kwa akina mama Vile vile ningependa kuwashukuru Watanzania kwa hali ya utulivu waliyokuwa nayo kumpokea Rais Suluhu Hassan Heko kwao Ningependa kuchukua nafasi hii kama Mbunge wa Taveta kutoa pole kwa kumpoteza Rais jirani wetu lakini vile vile kwa sababu nilikua Waziri aliyehusika na mambo ya jinsia kufurahia kuwa Mama Suluhu amepata nafasi hiyo Bila kusema mengi naunga mkono hotuba yake Mhe Rais Samia Suluhu na kumtakia kila la heri katika kazi nzito ambayo Mwenyezi Mungu amemjalia na ametunukiwa na Watanzania Mhe Spika naomba kumalizia hapo kwa hayo machache na kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa Bunge hili limekuja kusalimiwa na mama mmoja ambaye amepata nafasi ya kuwa Rais barani Africa na si Africa tu bali Afrika Mashariki Naafikiana na Kiongozi wa Walio Wengi hapa Bungeni
Ndiposa nimechukua Kipengele cha Saba na Kanuni 77 ya Bunge la Kenya kwamba Kiswahili ni lugha rasmi na ni lugha ya taifa na mimi ninajivunia. Kwa wale wanaodhani ni ujinga samahani. Mhe. Naibu Spika wa Muda chimbuko la ubinafsishaji limetoka wapi? Miaka ya 90 taifa la Kenya lilikuwa maskini. Tulikuwa waombaji. Rais alikuwa anachukua kikapu kwenda kuomba Benki ya Dunia. Waziri wa Fedha alikuwa anaenda na bakuli kwenda kuomba Benki ya Dunia. Wale wenye senti hiyo wakatoa masharti yaitwayo kwa lugha ya Kimombo structural adjustments programmes. Hilo ndilo chimbuko la ubinafsishaji. Kumetokea tukio. Mzungu kaja na mkoba na akatushawishi tuuze reli ya Kenya. Alisema ataleta kampuni kubwa zaidi itakayoshughulikia reli ya Kenya. Tukampa fursa. Akachukua rasilimali yote. Siku ya pili jina alilotuletea alilichukua hapa River Road. Inaitwa Rift Valley Railways. Hizi ndio athari na madhara ya ubinafsishaji wa mali ya umma. Kipengele cha 23 cha Mswada huo kimetoa wajibu kwa Bunge la Taifa kupitisha na kuidhinisha ubinafsishaji wakati unapofanyika kwa mashirika ya serikali. Kifungu cha 5 (1)(d) kinaondoa wajibu wa Bunge na kwenda kwa Baraza la Mawaziri. Hii ni dhuluma kwa Wakenya. Hii ni sheria mbaya. Utakaponiita mjinga au mwerevu hapa nilipo watu wa Bura walionichagua wanajua kwa nini wamenichagua na mimi naweza kujua sheria mbaya na nzuri kwa lugha yoyote ile utaleta. Nimeomba hapa mara nyingi kwamba Mswada unaoletwa hapa utafiwe kwa Kiswahili ili mwananchi pale mashinani wakati tunapochangia ajue sheria hii ni mbaya. Leo ninataka kuwaambia Wakenya kwamba Mswada huu ni mbaya. Ukiletwa na chama changu ni mbaya. Ukiletwa na mtu binafsi ni mbaya na ukiletwa na Upinzani Mswada huu ni mbaya na dawa ya Mswada mbaya ni kuuangusha. Mtoto wangu ataniuliza: "Kwa nini umepitisha sheria kama hii?" Nitakuwa sina jawabu la kujibu mtoto wangu atakaponiuliza swali kama hilo. Ili nilinde haki ya Wakenya na tukio lililotokea Kenya Railways Posta na Telkom lisitokee tena katika taifa la Kenya ninapinga Mswada huu. Wengi wanadhana kwamba ni makosa kwa serikali kufanya biashara. Ikiwa dhana ya kuleta ubinafsishaji ni kutoa Serikali katika biashara mbona Serikali imeshika benki zote hizi. Zaidi ya asilimia 50 ya riba katika National Bank of Kenya na Kenya Commercial Bank ni ya nani? Hospitali Kuu ya Kenyatta ni ya nani? Mbona mwenyekiti kwa mkono mmoja anasema ni vibaya kwa Serikali kufanya biashara na mkono wa pili anaunga mkono Serikali ifanye biashara? Katika mataifa mengi serikali inafanya biashara na inapata faida. Inaboresha ushuru wake. Kwa hayo machache Mswada huu ni mbaya. Nimesimama kuupinga. Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Ndiyo Mhe. Spika. Nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili niweze kutoa mchango kwa Mswada huu ambao umezua hisia tofauti miongoni mwa wananchi na Wabunge. Kama tunavyojua michango imeisaidia nchi hii haswa wanafunzi na wagonjwa. Harambee zimetoa mchango wa kutosha katika nchi hii. Shida inatokea mchango unapochukuliwa kuwa kigezo cha uongozi bora haswa inapodhaniwa kwamba kiongozi ambaye anazunguka nchini akitoa michango mingi ni kiongozi bora kuliko viongozi wengine bila ya watu kufikiria kuhusu mahali ambapo kiongozi huyo anazitoa fedha hizo. Kuna uzuri wa michango. Ningependa kusema wazi kwamba katika eneo la Pwani miradi mingi imefanywa kupitia michango. Shule nyingi zimejengwa kupitia michango. Vile vile watu wamesaidiwa kwenda shule na kufanikisha masomo yao kupitia michango. Watu wamesaidiwa kulipa gharama za matibabu katika hospitali kupitia michango. Hatuwezi tu kuamka leo na kusema kwamba michango haitakuwepo tena. Suala hili ni sharti liangaliwe kwa undani ili tujue linalohitajika kufanyika. Sikatai kwamba kuna watu ambao wametumia michango vibaya. Watu wengine wamefanya michango na kukataa kutoa hesabu. Ni muhimu kuangalia sehemu ya michango inayotumiwa vibaya. Ni muhimu pia tuangalie sheria inayofaa kuwekwa maanani ili ionekane wazi kwamba ikiheshimiwa michango itafanyika kwa njia ya uwazi na wala sio kutapeli. Mhe. Spika mara nyingi watu wametuma jumbe kwenye runinga au kwenye simu za mikono ama kuandika barua wakiomba michango ya watu wagonjwa au wale ambao wamekufa. Baadaye ukifuatilia kwa undani utaona kwamba hayo yote ni utapeli na hamna jambo lolote kama hilo. Tunafaa kuangalia sheria itakayowekwa ili michango isitumiwe vibaya na ili nafasi hii isipotoshe watu na tusinyime wale watu ambao wanahitaji michango nafasi ya kujiendeleza. Mswada huu unafaa kufanyiwa marekebisho kwa kuweka vipengele ambavyo vitahakikisha kwamba wale ambao wataomba michango ni watu ambao wanastahili kupata msaada ili tuhakikishe ya kwamba wanafunzi ambao wanahitaji kusaidika wanasaidika. Tukiwafungia watu wote kwa kupitisha sheria hii basi watu ambao wana nia nzuri ya kusaidiana na kusaidiwa wataathirika. Tutakuwa tumewanyima nafasi nzuri ya kujiendeleza. Ninavyozungumza hivi sasa watu wengi wanahitaji matibabu. Mara nyingi tunapopata maombi ya kuwasaidia wale ambao wameathirika tunakusanyika kama jamii na kuwaita marafiki na kuomba michango kutoka kwao ili tuwasaidie. Mara nyingi watu wanapatwa na ajali za vifo na wanafaa kusafirisha miili ya ndugu zao kutoka Nairobi hadi Mombasa au miji mingine. Mara nyingi tunaitisha michango. Tukiupitisha Mswada huu na kuharamisha michango tutafanya nini? Sio familia zote zina uwezo wa kugharamia au kufidia gharama za matanga na ujenzi wa shule na hospitali. Tukifunga michango kwa sheria basi tutawanyima watu hao nafasi ya kusaidiwa na wale ambao wana uwezo. Mara nyingi watu wanakutana na kuchanga kiasi kidogo cha pesa kwa muda fulani na mwishowe wanaweza kumudu gharama iliyokuwa inawatatiza. Maoni yangu ni kwamba Mswada huu urekebishwe ili watu ambao watachangiwa kwa sababu moja au nyingine waweze kuwajibika na kupeleka ripoti kwa msajili kuonyesha jinsi fedha hizo zilivyotumika kama itakavyopendekezwa ili watu waone kuwa pesa ambazo zimechangishwa zimetumiwa kwa minajili ambayo ilikuwa inahitajika. Kama ni karo basi ijulikane kuwa mwanafunzi amechangiwa kiasi fulani cha fedha na fedha hizo zimetumika kwa njia inayostahili. Iwapo ni gharama ya hospitali basi gharama hizo zigharamiwe na wenyewe watoe stakabadhi za kuonyesha kwamba walichangiwa fedha kiasi fulani na jinsi ambavyo fedha hizo zimetumika. Kama ni fedha za mazishi basi iwe hivyo hivyo. Ninapinga pendekezo la kuondolewa kwa ujumla mambo ya michango. Msimamo wangu ni kuwa michango iendelee. Tunafaa kuifanyia marekebisho sheria husika kwa kuweka vipengele ambavyo vitawashurutisha wale wanaochangiwa - iwe ni wanafunzi wagonjwa au makanisa - kutoa stakabadhi zitakazoonyesha kwamba fedha zilizochangishwa zilitumika kulingana na maombi yao. Kwa hayo mengi naomba kuweka tamati nikiwaomba Wabunge wenzangu waniunge mkono ili tusije tukalazimika kuunda kamati ya uwiano kati ya Bunge la Kitaifa na Bunge la Seneti ili jambo hili lifanyiwe marekebisho. Naomba Mswada huu upitishwe na wenzangu tukizingatia suala la kupendekeza mabadiliko.
Ndiyo. Tukizungumzia suala la maji lazima tuangalie maeneo yote ambayo hayana maji kwa mfano Tharaka na Isiolo.
Ndugu yangu Mheshimwa ananikumbusha kuwa nyege ni kunyegezana. Kunyegezana lazima kuwe na mume na mke. Hakuwezi kuwa na jinsia moja. Kwa hivyo lazima tujue ya kwamba hizi sheria tunazileta kwa sababu tunataka kesho wale akina mama ambao watakuwa wamejengwa uwezo kwa kupitia sheria hii wawe na nguvu na tajiriba ili waweze kushindana na akina baba tuwe tuko sawasawa. Ni aibu sana tukiangalia nchi jirani kama Rwanda Uganda na Tanzania. Akina mama wamejengwa uwezo na wameingia katika viti vile vya kuweka maamuzi katika taasisi za umma katika nchi zao. Sisi Wakenya ambao tumebobea tukienda Tanzania tunaambiwa kuwa tuko juu lakini tunataka kujibwaga kwa sababu ya kuleta sheria ambazo hazieleweki. Sheria ambazo hatuelewi zitatekeleza vipi sheria ambazo zimezungumziwa katika sheria mama inayoitwa Katiba? Lazima tuangalie kule tunakotoka na kule tunakoenda. Leo hii tukisema hatutaweza kutekeleza sheria hii kesho kutwa tutakuwa na Bunge ambalo lina akina mama kumi. Itakuwa ni aibu na fedheha. Lazima pia tuwe tunazingatia nyanja hizo. Leo wewe kama Mbunge mwanaume pengine umejaaliwa watoto wa kike pekee lazima upitishe sheria ambazo haswa zinamlenga mtoto wa kike. Ijapokuwa ni jinsia ukweli ni kwamba mama alikuwa amegandamizwa kihistoria kidesturi kimila na pia katika mambo ya kupigwa na mambo ya kiuchumi. Tulikuwa tumegandamizwa sana. Hatusemi kuwa sisi tunaomba lakini tunataka tuiweke Kenya yetu iwe inapendeza hata miongoni mwa yale mataifa mengine. Pia sisi kama Wakenya tuna sheria kama ile mikataba ya kiulimwengu ambayo tumetia sahihi ya kwamba tutahakikisha haki za akina mama katika kisiasa uchumi na jamii. Leo hii mambo haya yote tunayafahamu lakini tukirudi nyuma tunamwangalia mwanamke kana kwamba ni chombo tu. Mjue akina mama kura tunazo na kura zetu ni nyingi. Tukiamua wakati huu kuwa dawa ya moto ni moto naona wengine watapata shida hapa Bungeni. Maanake tutaongea na hatutanyamaza. Tutaongea kinaga ubaga kwa sababu nipe nikupe ndio biashara iliyoko sasa. Hakuna biashara nyingine. Biashara ni nipe nikupe. Hatutakuwa tunawasaidia. Hapa kulikuwa na Mswada wa mambo ya Hazina ya Kitaifa ya Maeneo Bunge na sisi kama Wawakilishi wa Akina Mama ambao hatuna hiyo Hazina tulisimama kidete tukaunga mkono kwa sababu sisi tuko pamoja na ni wapenzi sako kwa bako tusonge mbele kama Wakenya. Leo hii mbona nyinyi mwatubwaga? Itakuwa si sawa jai. Palipo na wema lazima kurudi wema. Sisi tunapowafanyia wema lazima nanyi mregeshe wema. Kwa hivyo mimi najua hatujachoka. Najua ndugu zangu viongozi wa kiume mnatupenda. Najua hata leo ukipinga Mswada huu na useme tutengeze Mswada mwafaka hata ukifika nyumbani makaribisho yako yatakuwa tofauti. Maanake akina mama watajua kwamba unasimama kidete kuangalia haki zao. Na hata sisi yumbani tutajua lazima ile haki nyingine tuifanye kwa njia sambamba kwa sababu wametupatia nguvu sana. Akina mama tumejaribu sana. Dada yangu Rose Nyamunga amesema kuwa tuliwanunulia dinner . Lakini sisi hatutaki kuwadai. Ile ilikuwa ni mapenzi yetu. Natutaendelea kufanya mengi mazuri ili sisi tuwe kitu kimoja tuwe na upendo na mapenzi jai. Wenzetu hapa Tanzania Makamu wa Rais wao ni mama. Hiyo ndiyo njia ambayo sisi tunastahili kuendelea nayo. Lakini hivi hivi bila kuwajenga kiuwezo akina mama hatutafikia pale. Na kama tunataka kutajika katika ulimwengu kwa mambo ya uongozi lazima tuhakikishe akina mama wako mbele tumewasaidia na wamepata haki yao. Natukifanya hivyo basi Kenya itakuwa miongoni mwa inchi ambazo zimestawi na kubobea kiuchumi mambo ya kijamii na siasa. Kwa hayo mengi ama machache naomba jai mtuunge mkono hata mkibadilisha na kuweka hicho kilma ' progressive '. Lakini kama hamutaweza kugeuza kile Kipengele cha 97 ambacho kinazungumzia muundo wa Bunge utakuwa na akina nani ikiwa hamutakuwa mumezungumza na kutupatia njia mwafaka tutakuwa tumefanya kazi ambayo haitakuwa na mshahara. Kwa hayo mengi ama machache mwendo utakuwa ni ule wa aste aste ama kama ni wa kobe tuungane mikono pamoja Kenya isonge mbele. Asanteni.
Ndugu yangu mpendwa mheshimiwa wa eneo Bunge la Shinyalu anafurahia sana kusikia ni kitu gani kinang'olewa. Ndugu yangu wa Shinyalu hicho kitu ambacho kinang'olewa wewe mwenyewe umekibeba na mheshimiwa Aburi amekibeba. Sikusema ni kigeni. Kwa vile sisi ni familia hatuwezi kukitaja mbele ya Bunge lakini wazee wanajua ni kitu gani kinang'olewa. Ni kweli tunaona kinang'olewa. Tunakiita sehemu nyeti.
Ni kwa sababu ulikuwa unamsikiza Mbunge wa Marakwet Nimesema Mbunge wa Kipipiri ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi katika taarifa yake amesema kwamba angependa tujionyeshe Lakini hajafafanua vipi kama ni kwa vitendo ama mavazi pengine ni Kiswahili kimemchanganya
Ni kweli Bwana Naibu wa Spika. Hata baba alisema Kiswahili kilianza Pate. Akatoa historia yote mpaka kikakufa huko Congo. Lakini kilipata ugonjwa hapa Nairobi. Makala ya 53 (b) ya Katiba inasema ni haki ya kila mtoto kupata elimu ya bure. Makala ya 55 (a) inasema kuwa Serikali ina jukumu la kuhakikisha vijana wapate elimu na ujuzi. Basuba Ward haijakuwa na shule ya chekechea ya msingi au ya sekondari kwa miaka mitano. Huu ni ukweli.
Ni kweli nakubaliana na wewe Mhe. Leshoomo kwa sababu Bunge ni letu sisi wote na ndiyo kazi yetu. Wanjiru for Murang'a what is out of order?
Ni Mhe. Abdisalan. Sijui kama ataongea kwa Kiswahili ama Kiingereza kumkumbusha tu kuwa Kisomali hakikubaliwi Bunge.
Ni wakati wa lala salama. Wengine mnakunja majavi yenu kabisa na wegine wanayakunja nusu na watarudi. Kwa hivyo itategemea uko upande upi. Wengine wetu tumeamua kwa hiyari kwenda kuomba kiti cha ugavana. Wale ambao mmeamua mnarudi hapa wakati ndio huu ambao umebaki mchangie kikamilifu ule wajibu ambao mmepatiwa na umma kushughulika katika utungaji sheria na kuwajibika wakati wa ugawaji wa pesa. La sivyo wengine wenu mtakuwa mnasema mmekaa hapa miaka minne lakina hakuna kitu chochote cha kuonyesha. Lakini wengi wamefanya kazi ya kuridhisha na ninawapongeza. Mhe. Spika kazi ambayo imebaki ni nyingi. Kama tulivyoona leo wakati huu utakuwa mgumu sana kwa viranja kwa sababu mara kwa mara Wabunge watakuwa huko mashinani wakiomba kura. Lakini tumetumia wakati huu vizuri kwa sababu tumejaribu tuwezavyo Ninawapongeza Wabunge wenzangu vile wametumia huu muda. Hata hivyo kwa muda mfupi ambao umebaki itakuwa ni wajibu wa kila Mbunge kuhakikisha ameangalia wastani wa muda wake. Ni muda upi utatumia kwa shughuli za Bunge na ni upi utatumia kuangalia maslahi na miradi yako ambayo imebaki? Kwa haya machache ninaomba kuunga mkono Hoja hii. Asante Mhe. Spika.
Ni. hukrani Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili niweze kuichangia Hoja hii. Kwa kweli Hoja hii imekuja wakati ambao ni muhimu sana kwa sisi kuijadili ili kutoa mwelekeo kulingana na hali ya kiafya ilivyo katika nchi yetu. Bw. Naibu Spika wa Muda Katiba ya Kenya katika Kipengele cha 43 kinasema: "Every person has the right to the highest attainable standard of health which includes the right to healthcare services" Wakenya walipitisha Katiba na ukweli ni kwamba ni haki ya kila mkenya kuhakikishiwa kwamba amepata huduma ya matibabu popote pale alipo; lakini ni masitiko makubwa
Nidhamu! Nidhamu! Mheshimiwa Rais wa nchi jirani ya Tanzania Rais Jakaya Mrisho Kikwete Spika wa Seneti Mheshimiwa Ekwee Ethuro waheshimiwa Wabunge wote ambao mmefika kupata mafunzo kutoka kwa jirani mwema Rais Jakaya Mrisho Kikwete Bunge la Kitaifa litahairishwa kwa muda wa dakika 30. Tutarudia kikao papa hapa.
Nikimalizia Kenya huchukua zaidi ya asilimia 90 ya medali katika ushindani wa mbio za nyika. Hiyo ndiyo inafanya tuonewe. Tunawambia wanariadha wetu wachukue nafasi hii watuletee medali kwa wingi katika kipindi cha mashindano yajayo.
Nikiomboleza na kusikitika na ndugu zangu wa kule Baringo na sehemu za Pokot ni lazima Mhe. Nkaissery apandishe soksi zake na akaze ukanda vizuri atume maofisa na kuweka ai katika sehemu hiyo. Mimi binafsi nikiwa Mbunge wa Jomvu
Nikipewa muda nitakuja na orodha niwaseme. Hata wale wanaosema na waseme - inajulikana wazi kuwa sheria zetu zinasema kama mwanakamati hajaudhuria vikao vitatu aondolewe katika kamati hiyo. Wakati umefika Waheshimiwa tuchukue majukumu yetu sawasawa na sahihi. Kila mtu ashughulike na shughuli za Bunge. Kama umeingia kwa kamati ni muhimu na ni lazima ushughulike. Kwa hayo mengi Mhe.Spika naunga mkono.
Niko hapa mhe. Naibu wa Spika. Kwanza ningependa kukubaliana na mhe. Leshoomo kwamba hali ya usalama katika Wilaya ya Samburu imezorota na haswa katika Wilaya ya Baragoi Kaskazini. Ninafahamu kwamba kuna operesheni inayoendelea katika wilaya hiyo ya kuwanyanganya bunduki watu wanaozimiliki kwa njia haramu. Kuna askari karibu 700 ambao wanafanya kazi hiyo. Kwa hivyo ningependa kumhakikishia mheshimiwa kwamba operesheni hiyo inawalenga wakora. Tunajua kwamba kule Baragoi kuna bunduki zaidi ya 46 zilizoibwa na majambazi askari wetu walipouawa kwenye tukio la hapo awali. Tungependa wale askari wanaofanya operesheni hiyo waokoe bunduki hizo kwanza. Pili kuna operesheni inayowalenga walinzi kutoka kitengo cha KPR. Si jambo la busara kukifutilia mbali kitengo hicho cha walinzi bila ya kuwahakikishia wananchi usalama wa kutosha. Kwa hivyo operesheni ya kwanza inalenga kuziokoa bunduki za serikali zilizoibwa na majambazi. Kuhusu masuala yaliyosalia nitaongea na Katibu anayesimamia masuala ya usalama ili tuweze kupata habari kamili kuhusu OCPD na OCS kwa sababu tunajua kwamba kulikuwa na shida iliyotokea kati ya maafisa hao wawili na wanafunzi. Kuhusu suala la ngo'mbe 26 walioibiwa nitaleta taarifa Bungeni baada ya wiki moja. Ahsante Bi. Naibu wa Spika.
Niko hapo Mhe. Naibu Spika. Nalipinga tengenezo badilisho hili. Utapata askari wa polisi amepigwa na kunyang'anywa bunduki. Je ikiwa bunduki hiyo haitafuatiliwa tutajua pale itakapoangukia? Kwa hivyo ni lazima tuwe na mikakati ya kusuluhisha mambo haya. Kwa hayo machache nalipinga tengenezo badilisho hili.
Niko mbali halafu nabanwa Nashukuru Bi Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili niseme machache tu kuhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Serikali hiyo Bi Suluhu Hassan Kwanza kabisa ningependa kumshukuru Rais wetu wa Kenya Mhe Uhuru Kenyatta kwa sababu ilitokana na ule uhusiano wake mzuri na watu wa Jumuiya hii Nafikiri ndilo lilimfanya Bi Suluhu kuona kwamba ni muhimu aje hapa ili atengeneze uhusiano Kwa hilo ningependa kusema shukrani Kwanza kabisa ningependa kumshukuru huyo Mhe Rais wa Tanzania kwa kubadilisha mwenendo Kama mnavyojua mahusiano kati ya Kenya na Tanzania kutoka mwanzo yalikuwa na mporomoko na mikinzano mingi ikitokana na mambo ya kutoelewana taharuki kuogopana namna hiyo na kusema kwamba Wakenya ndio wajuaji Kwa hiyo ilikuwa ni mambo ambayo hayana msingi Lakini Dkt Bi Suluhu ambaye ndiye Rais wa nchi hiyo amebadilisha na kuleta mwenendo ambao sasa ni sawa kuleta ukuruba kuleta mahusiano mazuri kati yetu na wao ili tuweze kuweka msingi wa undugu ambao utatufaa zaidi katika siku nenda siku rudi daima dawamu Utadumu milele ili kusaidia watu wetu wafanye kazi pamoja kwa sababu ya soko kuu Wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kati wakifanya biashara pamoja tutakuwa na soko kubwa la kazi kuuza mazao yetu na kufanya mambo yetu mengi ambayo yatakuwa yanatufaa sisi haswa katika kuleta vitega- uchumi vitakavyofaa kwa watu wetu Muhimu ni kwamba ulipomuona Mama Suluhu akizungumza hapa alizungumza Kiswahili kizuri sana Kiswahili chenye uletelezi sahili burudani nyingi bashasha vijembe vimejaa mumo kwa ndani Tuliona kwamba Kiswahili hicho kilikuwa kizuri sana kikatuchangamsha Nimeona Kiswahili kimewatia Wabunge wa hapa motisha Naona Wabunge wanazungumza Kiswahili kizuri Nimemuona yule anayetoka kule Nyanza nimemuona dada hapa wa kutoka kule akisema Kiswahili kizuri sana Nawaambia kwamba lugha ya Kiswahili ni nzuri na itatufanya tuwe na mahusiano mazuri sana Tanzania Ningependa kwa vile mama yule ametutia motisha na mshawasha wa kuwa na uchu na tamaa ya kuendeleza lugha hii katika Bunge hili itatufaa sisi pia tupate siku moja au mbili katika zile kaida ama Kanuni zetu ili tuweze kuzungumza Kiswahili kwa lazima Tunapofanya mazoezi pale-hapa tutakuwa tunazungumza sawasawa Nilipomuona Mama Mhe Rais akisema kwamba Kiswahili chetu kinakuwa na vituko na vijembe vinavyowafanya wacheke na kufurahia kinapozunguzwa nafikiri ni sawa Nataka niwaambie Wakenya wajue kwamba taifa letu la Kenya katika ustandadi wa Kiswahili tunaposema waandishi ambao wamekomaa wale gwiji wanaojua lugha ya Kiswahili undani wale wakiritimba ni walewale wanaotoka hapa Ningependa kuwashangaza kuwa yule anayezungumza Kiswahili kizuri zaidi yule gwiji au bingwa mkubwa anatoka Nyanza Anaitwa James Ndeda ama muite Wallah bin Wallah Ndiye muandishi wa mno katika lugha ya Kiswahili Namshukuru Bibiye Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Kenya Nasema asante shukrani naunga mjadala huu mkono wa dhati Asante
Niko na hoja ya nidhamu. Katika Bunge hili ukiongea kwa lugha moja unatumia lugha hiyo pekee lakini mimi nasikia "I am sure." Ninachanganyika kidogo.
Niko tayari Mhe. Spika. (Kinango ODM)
Nilikaika Naibu Spika wa Muda kwa sababu niliweka kadi yangu mbele ya watu wengi zaidi hapa lakini sikupata nafasi Nashukuru pia nimepata nafasi hii kidogo nami niunge mkono Mswada huu kwa sababu hata Pwani kuna sukari Tulikuwa na kiwanda cha Ramisi ambacho kilikuwa kiwanda cha umma na kikafa hadi sasa Ningependa kusema ya kwamba bodi hii ambayo itatengenezwa itaweza kusaidi kuleta soko la sukari yetu hapa Kenya Hivyo basi kuboresha uchumi wetu wa kitaifa na uchumi wa wakulima wetu wa sukari Vile vile wale wenye cartels wanaoleta sukari haramu sukari ambayo itakuwa na madhara ya kiafya katika taifa letu la Kenya wanaweza kudhibitiwa kupitia bodi hii ambayo itakuwa imetengenezwa kuangalia majukumu kama hayo Vile vile katika mambo ya utafiti ni vizuri kwamba tukifanya utafiti ili kuweza kuboresha mazao tuweze kupata mazao zaidi na tupate tofauti nyingi katika huu mmea wa sukari ama wa miwa ili tuweze kupata sukari kwa kiwango cha hali ya juu sana Vile vile wakulima wetu kupata hisa hamsini na moja katika kampuni ambazo ni za watu binafsi na pia katika zile kampuni za kusaga itawapatia nguvu sana wakulima wetu wa miwa Hilo litakuwa ni jambo la kupunguza wale watu ambao wana ubinafsi katika mambo ya uchumi wa sukari Vile vile wakulima wengi hawajalipwa malipo ya fedha zao katika kilimo hiki Hivi sasa kupitia bodi hii ambayo itakuwa imetengezwa na sheria hii ya sukari ambayo inaitwa Sugar Act hayo mambo yote hayatakuwa changamoto bali litakuwa ni jambo la kuboresha mambo hayo Hazina ambayo itakuwa imetengezwa kupitia ule ushuru ambao tunauita levy itaweza kusaidia sana watu kuweza kuchukua mikopo na kufufua vile viwanda ambavyo vimekufa ama vile ambavyo vimedorora katika wakati huu Nataka niseme ya kwamba sukari ni kilimo cha kuweza kuleta uchumi wa kenya kama kilimo cha kahawa na majani chai Kwa hivyo ni kilimo ambacho sisi kama taifa lazima tukichukulie kwa njia ya hali ya juu ili tuweze kujenga ajira pia kwa vijana wetu na kuweza kuboresha uchumi katika county zetu haswa zile ambazo zina kilimo cha sukari ndiyo tuweze kuendeleza nchi yetu kwa pamoja Vile vile ningependa kusema ya kwamba jambo hili limetuwezesha kuzungumzia uchumi wa sukari ambao utaweza kuondoa zile changamoto zote ambazo zilikuwa za mambo ya sera Tutaweza kujua sera mwafaka ambazo zitatuwezesha kuboresha kilimo cha sukari Mhe Naibu Spika wa Muda najua watu ni wengi Namuunga mkono na kumpea kongole Mhe Wamunyinyi Kupitia jambo hili leo tutajivunia kufufua viwanda vyetu vyote ambavyo vilidorora ama vilikuwa vimekufa kwa sababu za kimsingi ama sababu ambazo hatuwezi kuzizungumzia kwa hivi sasa Naunga mkono Mswada huu Ahsante sana Mhe Naibu Spika wa Muda
Nilikuwa nataka kumuunga mkono ndugu yangu Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi kwa kuwakilisha hili jambo ili tuweze kuzungumzia hotuba
Nimeeleza kuwa mambo haya yameisha. Mhe. Spika shida ya Kiswahili ni hio. Hapakuwa na nia yoyote kumuudhi. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
Nimeshukuru Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Hii itakuwa sheria ya kufana sana tukizingatia makosa yanayofanywa na wapiga kura na baadhi ya wagombeaji viti vya uchaguzi. Imebainika kwamba akina dada mara nyingi huwa wanazuiwa kugombea ama kushiriki kwenye chaguzi huru kwa sababu ya makuruhu na dhuluma wanayofanyiwa na baadhi ya wapinzani wao wa kiume. Kifungu cha 16 kinazungumzia ubebaji wa wapiga kura kutoka sehemu moja hadi nyingine na kuwaregesha. Hili limekuwa pigo kubwa sana kwa akina dada wanaogombea viti. Wakati wa kuwasajili wapiga kura wapinzani wengine huwasafirisha wapiga kura kutoka wilaya moja hadi nyingini. Kifungu cha 18 kinaangazia suala la baadhi ya waajiri ambao huwazuia waajiriwa wao kwenda kupiga kura. Ninavyoelewa ni kwamba kuna kampuni ambazo zimeajiri zaidi ya Wakenya 600 ama 1000. Wakenya hao wamekatazwa kuweka vituo vya kupigia kura miongoni mwao. Siku ya kupiga kura wenye kampuni hizo huwazuia wafanyikazi wao kutoka nje ili kwenda kupiga kura. Huo ni unyanyasaji na ukiukaji wa sheria za Kenya. Mengi yamesemwa kuhusu sheria za upigaji kura. Ninataka tu kuchangia kuhusu eno ya kugura vyama vya kisiasa. Kuwakataza wagombeaji kuhama vyama vyao vya kisiasa baada ya uchaguzi wa mchujo ni kuturegesha katika hali ya chama moja. Sisi sote katika Bunge hili tunajiunga na vyama vya kisiasa kwa sababu ya kuamini miundo misingi ya vyama hivyo. Litakuwa jambo la kufana iwapo tutaamini miundo misingi ya vyama hivi na tukae katika vyama na tutafute namna ya kusuluhisha matatizo yote ambayo yatatokea baada ya chaguzi za mchujo. Iwapo mtu anahisi kwamba ana nguvu za kuunda chama chake agure vyama vya kisiasa kabla ya uchaguzi wa mchujo. Katika Bunge hili mimi ni mmoja wa watetezi wa haki za kibinadamu na ukiukaji wa haki za kibinadamu. Mhe. Spika wa Muda sheria hii imezungumzia haswa usawa wa kijinsia baadhi ya wagombeaji na wapiga kura. Ninapoongea kuhusu usawa wa kijinsia tumeongea sana kuhusu uteketaji wa wasichana. Litakuwa ni jambo la maana kutunga sheria ambayo inaidhinisha na kulazimisha kutahiri kwa wanaume katika nchi hii yetu ya Kenya. Mbali na kudhibiti makali ya ugonjwa wa ukimwi imebainika kwamba iko pia na faida ya kusaidia kukomaa ili tusione wanaume wazima wakiketi kwa barabara kulazimisha Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ing'atuke. Tunajua kuna sheria ambayo imetungwa ambayo inasema wazi kuhusu kung'atua Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka.
Nimesikia maamuzi muongozo na mwelekeo wako kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Makadirio Mhe. Spika. Naomba nichukue nafasi hii nitoe masikitiko yangu kwa Kamati ya Pamoja ya Mabunge yote mawili iliyoshindwa kuafikiana kuhusu Mswada huu. Inamaanisha kaunti zetu zitaanza makadirio yao zikiwa zimechelwa hapo mwakani mwezi wa saba kama hatutakuwa waangalifu. Mhe. Spika ni muhimu makadirio haya yafike mapema. Naomba nihimize Mwenyekiti wa Kamati ya Makadirio ahakikishe kuwa wamemaliza haya umeyaagiza wayamalize. Nina ii hatutakuwa na changamoto yoyote hapa Bungeni na Seneti pia haitakuwa na shida ili makadirio haya yafike mapema. Kama ujuavyo wengine wetu tuko katika harakati ya kukunja jamvi kufuatana na haya makadirio huko mbele. Yakichelewa inamaanisha wengine wetu hatutaweza kufanya kazi. Kwa hivyo ni muhimu na ni muhimu. Nasisitiza kuwa makadirio haya yamaliziwe mapema ili tuweze kufanya kazi kwa muda unaofaa. Naomba nihakikishie Bunge hili kuwa wale ambao tuko hapa na tunatarajia kwenda huko kwingine hatutaaibisha hili Bunge. Hatutaaibisha hili Bunge kwa kuwa Magavana wa kuiba ama wakuletwa hapa kwa Seneti. Tunaenda huko kutumikia wananchi. Naliheshimu hili Bunge na nitaendelea kuliheshimu Bunge la Kumi na Moja. Mmenifunza mengi. Sitawaaibisha. Mhe. Spika naomba nitoe mchango wangu kuwa hiyo ndio ilani ninayotoa. Asante Mhe. Spika.
Nimesimama kuunga mkono Mswada huu kuhusu Mahakama ya Madai Madogo ambao umeletwa Bungeni. Kwa haraka nataka kuwajulisha wenzangu na wananchi kuwa haya mahakama ambayo yatatengenezwa baada ya hii sheria si ya jinai au uhalifu bali ni ya mashtaka kati ya watu binafsi. Kwa hivyo wasifikirie kuwa ni polisi watakuwa wakipeleka mashitaka katika hayo mahakama. Pili ni sheria nzuri ambayo inatungwa. Hii ni kwa sababu kwa mara ya kwanza tangu Katiba ipitishwe tuzipa Mahakama za Juu nafasi ya wiki mbili na nyingine miezi sita ili kupeana hukumu wakipelekewa madai ya kuhusu uchaguzi ambao umekumbwa na shida. Kwa mara ya kwanza Mahakama ya Madai Madogo itakuwa na nafasi ya kuamua kesi kwa siku tatu. Hii ni sheria nzuri kabisa. Lingine wananchi wanastahili kujua kuhusu hii sheria ni kuwa mahakama hizi zitakuwa katika kila kaunti na zinahusu kesi ndogo ndogo au madai madogo madogo ambayo hayazidi Ksh100 000. Kwa hivyo kama kesi inazidi Ksh100 000 inabidi mlalamishi aende katika mahakama za kawaida. Lingine muhimu ni hilo la kuwa hakuna wanasheria wanahusishwa hapa. Mimi ni mwanasheria lakini ukweli ni kuwa watu wengi huko nje hutisha wenzao. Ukienda kupeleka madai yako ambayo ni halali kabisa mtu hukutisha kuwa ataajiri wakili na wewe utaona. Hii sheria inasema hakuna mawakili. Watu watakuwa wanatoshana nguvu wakienda mbele ya muamuzi atakayekuwa katika hii sheria. Sheria hii imesema Msajili awe wakili. Nakataa hilo. Ni muhimu tubadilishe sheria hii katika sehemu ya tatu ya upitishaji sheria na tuondoe hili pendekezo kuwa Msajili sharti awe wakili. Mtu yeyote aliye na uwezo wa kusimamia ofisi awe Msajili katika mahakama hii. Hamna haja ya kusema tunapunguza uanasheria mwingi halafu tunaajiri mawakili katika kila sehemu. Mhe. Naibu Spika wa Muda hili jambo la lugha pia ni zuri sana. Kwa mara ya kwanza wananchi wataruhusiwa kuongea lugha ya mama ambayo mtu anajisikia anaweza kuelezea madai yake. Hii ni badala ya lazima ya kuwepo na mtu wa kutafi kila wakati na kila wakati kuulizwa uongee Kiingereza au Kiswahili. Hii sheria itakuruhusu uongee ile lugha ambayo unajisikia uko nyumbani nayo. Kipengele cha 32 kinasema zile sheria ambazo kwa kawaida zinatumika wakati wa kutoa ushahidi zilegezwe. Unaweza kutoa ushahidi hata kwa simu na mahakama inawezatumia karatasi tu. Ile sheria inayokataza watu na kuwaambia "usiseme hivi sema vile" imeondolewa hapa. Haya ni mahakama ambayo inawaruhusu watu ambao hawana mawakili hawana masomo waweze kutoa ushahidi wao haraka haraka. Kipengele ambacho labda nina shaka nacho ni cha 47 ambacho kinasema eti "mtu akipatikana kuwa anastahili kulipa mwingine" usipolipa unawekwa ndani miezi sita. Hiyo ni sheria mbaya kwa sababu haisemi "kama una uwezo wa kulipa na ukatae ndipo unaweza wekwa ndani." Kwa kweli imesema ukishindwa kulipa uwekwe ndani. Hiyo ni sheria mbovu kabisa na lazima tuibadilishe na kusema hatua itachukuliwa mtu ambaye ana uwezo wa kulipa lakini anakataa kulipa. Kipengele cha 48 kinasema kuwa mtu anawezapeleka madai yake madogo kwa mahakama nyingine wakati wowote. Nasema hivi: Haina haja tutengeneze haya mahakama halafu turuhusu watu wapeleke madai haya madogo madogo kwa mahakama zingine. Wacha madai ambayo hayajazidi Kshs100 000 tuyapeleke katika haya mahakama. Sheria hii pia ina shida kidogo. Inasema madai yanayohusiana na kampuni hayawezi kupelekwa katika haya mahakama. Kama madai ni madogo madogo na ni ya chini ya Kshs100 000 kwa nini tusiseme kampuni ambazo zimeenda mashinani kwa sababu ya kandarasi pesa zinazokuja kwa kaunti na kadhalika zisipeleke madai na mashtaka yao katika haya mahakama? Hicho ni kipengele ambacho tunastahili kubadilisha. Naunga mkono.
Nimezema bixa . Kwa kimombo inaitwa hivyo lakini kwa Kiswahili ni mrangi.
Ninakushukuru Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kuchangia hili jambo muhimu sana katika Kenya. Kwanza ninaunga mkono mjadala huu kwa maana ni muhimu sana. Lakini ningependa kurudi nyuma kihistoria ili tuweze kuelewa hili jambo la ajali na sheria za barabara. Ingawa ninaunga mkono kuna mambo machache ninataka kutaja. Nilipata driving licence yangu mwaka wa 1972. Ingawa tunasema watoto wafundishwe sheria za barabara kuna mambo nyeti ninataka kuyataja na ninajua Wabunge wezangu watayaunga mkono. Jambo moja ni kwamba hata kama Ministry ya Matiang'i imeleta jambo hili ijue imefail . Hii ni kwa sababu wakati nilipochukua driving licence traffic officers wakikusimamisha kwa mkono lazima ungesimama. Kabla wafike kwa gari wangekwambia uwashe taa upige dim uweke signal na upige wiper . Akimaliza angeenda nyuma ya gari na kusema ukanyage brakes ili angalie brake lights and parking lights . Tena angekwambia uweke hand brake na atingishe gari. Tunataka kutengeneza sheria mpya lakini zile ziko zikizingatiwa kwa njia nzuri zitareduce accidents katika nchi yetu. Hatujalitilia hili jambo maanani kwa sababu ukiangalia miaka ya 2007 na 2008 wakati wa crashes watu zaidi ya elfu moja walikufa. Na dunia nzima ilisimama to condemn na kusema hayo mambo ni mabaya. Lakini watu zaidi ya elfu tatu wakifa kupitia road accidents hatuwezi kusimama kama Serikali na kuuliza ni kwa sababu gani. Leo ukipata traffic officers barabarani na usimamishwe kitu cha kwanza kuulizwa ni driving licence . Kwa nini? Kwa sababu hiyo ndiyo wanawekewa pesa. Kama dereva anapeleka gari mpaka mahali traffic officer yuko inamaanisha anajua kuendesha gari. Kitu cha kwanza anachopaswa kuangalia ni tyres na stands za gari. Pili aangalie kama hiyo gari iko na shida yoyote halafu aangalie insurance ndio aulize maswali mengine. Wabunge wenzangu hata tukipitisha hii Hoja ambayo ninaiunga mkono kama Matiang'i ambaye anasimamia polisi na traffic officers hatasimama imara ili sheria ambazo ziko ziweze kufuatwa then inaonekana tutazungumza mambo mengi na watu wataendelea kutotii sheria. Kuna mambo nyeti ambayo yanaendelea siku hizi. Tunapitisha sheria lakini watu wa boda boda wanapita right left and any side or corner of the road and can go in any direction . Kama barabara ya mahali fulani ni moja wanatumia wrong side . Hizi sheria zinastahili kufuatwa. Lakini kuhusu traffic rules hatujasimama imara. Tunasikia kuna ufisadi na pesa ambazo zinapatianwa huko chini zinakuja zikitambaa mpaka juu na hii ni unyonge. Lazima tuseme enough is enough na tuchunge watu wetu. Tusiangalie vifo vya watu 3000 kupitia ajali za barabara peke yake kwa sababu inaweza kuwa mzee au mama amewacha familia na watu wengine wanakuwa viwete. This is a big burden for this country . Ninaomba Wajumbe walitilie hili jambo maanani kabisa. Matiang'i anapaswa aje ili atuambie ni nini kinapaswa kufanywa katika barabara zetu ndio sheria zifuatwe. Tusipofanya hivyo kuna effects za vifo vya watu 3000 na tukiangalia vizuri ni kama tumepoteza watu 50000. Hii ni kwa sababu wengine wanameza dawa ama wamevunjika miguu. Na mambo hayo yote yanatumia pesa nyingi za Serikali wakati tunatafuta pesa za kujenga economy . I think kuna shida na ninaomba Wabunge wezangu tujadiliane kwa ukweli na kuuliza shida iko wapi na tutafanya nini. Sisi zote tungependa mambo ya vifo yafike mwisho na watu wafuate sheria. Ahsante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia hii nafasi.
Ninakushukuru Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili nichangie jambo hili nyeti la Hotuba ya Rais wakati alikuwa hapa Bungeni. Ningependa kusema machache. Ninakubaliana na mwenzangu ambaye ameongea sasa hivi. Ni kweli kwamba lazima tujadiliane kuhusu mazungumzo ya Rais. Yale yamefanyika mazuri tuseme yamefanyika vizuri. Kama kuna shida tujue ni sisi tunahitaji kama Bunge kuijadili. Ninashangaa sana kuona kwamba kuna watu ambao hawaoni kitu kizuri kwa Serikali hii. Ni mambo ya kushangaza sana. La pili ningependa kusema kwamba sisi tuna Katiba ambayo tulipea Rais iliyotengenezwa na Wanjiku. Tulimpatia Rais na kumwambia kuwa tunataka afuate Katiba na mikakakati ambayo tumeweka kwa Katiba. Lakini nimeona wapinzani wetu wengine wametengeza Katiba nyingine ya mazishi ambayo wanataka tuitumie kufuta tume ya Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC) na watu wote kazi. Hilo haliko kwa Katiba. Haiwezekani kwa sababu Rais anafuata Katiba ambayo tulimpatia. Hii Katiba ya mazishi inataka tufute IEBC na EACC. Hii Katiba inasema kwamba majaji si wazuri polisi si wazuri mpaka bibi zao si wazuri. We must respect the law ya kusema hii ni nzuri na hii si nzuri. Inafaa tufuate haki. Hatusemi watu wote wa CORD ni wabaya hapana. Watu kama Mhe. Otuoma na wengine we respect them. Wanajua sheria na utaratibu wa kufanya mambo. Wakati tunaongea kuhusu ufisadi ufisadi uko na tunakubali lakini tunataka tuulize Uhuru Muigai Kenyatta alipoingia uongozini alikuja na malaika kutoka mbinguni ama alikuta watu wale wale? Miaka yote wamekuwa hapa kwa ufisadi. Tunahitaji kujua. Hata Wabunge hakukuja nao kutoka mbinguni. Ni wale wale. Lakini hainistaajabishi kwa sababu ninajua kwamba kuna wale waliosema Yesu asulubiwe na mwizi aachiliwe. Ni kama hawa tu tulionao hapa duniani. Kwa hivyo tusijali haya mambo ya kelele. Tufanye kazi ya haki inayotakikana. Nimesikia mwenzangu mmoja akisema hapa kwamba kuna kabila moja linaloajiriwa. Mambo haya si kweli. Hayo ni mambo ya uongo na hatutaongoza nchi hii na uongo ambao unawasilishwa kama ukweli. Uongo unaowasilishwa kama ukweli hautatusaidia katika nchi hii. Lazima tuzungumze ukweli kama viongozi. Tunaposema kabila moja ndilo linaloajiriwa si kweli. Sisi Wabunge tuliona kabila moja na ndugu wawili wanaotoka kaunti moja wakipiga firimbi. Ni kabila moja lilifanya haya mambo yote hapa. Out of 42tribes kabila moja lilifanya haya mambo hapa. Hatuwezi kusema ni Wabunge wa CORD wote walifanya mambo hayo lakini walifanya vibaya kwa kupiga firimbi na hata mimi nilishangaa. Kama unapiga firimbi kama Rais hajaongea inaonyesha wazi kuwa ni mpango uliopangwa na ni vita vya kisiasa. Unahitaji kumusikiliza Rais akiongea kwa sababu tuna muda kama huu kuzungumzia aliyoyasema. Ni vibaya Rais akienda kusimama unapiga firimbi. Wakati chama chenu kitachagua Rais na sisi tukiwa upande wa Jubilee tupige firimbi itakuwaje? Hilo halitatupeleka mahali pazuri. Tunahitaji kuwa na heshima. Nimeona Wabunge wakijadili hapa mambo mengi ambayo yanawahusu. Wao wenyewe wanahitaji kutunga sheria hizo. Ukiangalia mambo ya ufisadi utakuta inakumba pande zote mbili na si upande mmoja. Mwizi ni mwizi. Akiwa Muluhya akiwa Mukikuyu akiwa Mujaluo au Mukisii ni mwizi. Kwa hivyo tusichanganye na kusema ni sehemu moja tu ya Jubilee inayokumbwa na ufisadi. Mwisho katika vituo vya redio wabunge wengi wa CORD walisema jinsi Serikali hii ni mbovu lakini dakika ya mwisho walipoulizwa kama watachaguliwa walisema "ndio". Kwa nini: "Kwa sababu nimejenga barabara nimejenga shule na nimeweka maji" Umeweka na pesa za nani? Hizi ni pesa za Serikali ya Uhuru Muigai Kenyatta zinazokusanywa kama kodi. Usiifiche Serikali kwa kujipeleka mbele na ilihali wewe huna kodi unayokusanya. Ni utawala wa Jubilee unaokusanya hizo pesa. Kwa hivyo tuzungumze ukweli na tujenge nchi hii tukiwa pamoja kama Wakenya.
Ninakushukuru Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi niweze kuchangia suala hili. Ni suala nyeti. Ninataka pia kumpongeza mwenzangu Mbunge wa Turkana Mashariki kwa kuileta Hoja hii. Ninakotoka anakotoka yeye na wanakotoka baadhi yetu hapa wafugaji tumekuwa waathiriwa wakubwa sana katika suala hili la kupokonywa polisi wa ziada almaarufu NPR. Alivyonena yule alitangulia kuwasilisha suala hili ni kwamba wizi wa mifugo katika nchi hii na haswa katika maeneo tunakotoka sisi wafugaji imekuwa biashara ambayo iko na wenyewe. Kila siku tunapojaribu kutatua suala hili majibu tunayopata kutoka kwa wale ambao tumewapatia vifaa vya kulinda usalama wetu ni kwamba wanawajua na watawakamata. Wakati hawakamatwi tunaendelea kupoteza maisha ya binadamu na mali ya wananchi ambao tunawakilisha katika Bunge hili. Tunaendelea kuona shule zikifungwa kwa sababu ya ukosefu wa usalama. Katiba ya nchi hii inasema kwamba usalama wa mali na uhai wa binadamu ni suala la kikatiba. Kwa hivyo tukirejelea masuala hayo wale wananchi wa kaunti za Turkana Laikipia na Baringo haki yao ya kikatiba ya usalama na usalama wa mali yao imekiukwa na Serikali ya nchi hii. Tulipokuwa na Inspekta Mkuu wa Polisi ambaye aliondoka afisi hivi majuzi Bw. Boinnet aliweza kutambua mahali ambapo kulihitajika usalama katika nchi hii na wakaweza kuwahamisha wale askari wa ziada ambao ni vijana kutoka jamii hizo ili waweze kudhibiti wizi wa mifugo na ushambulizi wa majambazi ambao wamejihami kwa silaha hatari. Mimi ni mmoja wa waathiriwa maanake Laikipia Kaskazini tumepoteza mali nyingi sana haswa kuanzia mwaka wa 2013 hadi 2017 wakati tulipewa hawa polisi wa ziada. Wabunge wenzangu watakubaliana na mimi kuwa wakati tulipata hawa askari wa ziada shida zetu zilipungua kwa kiasi cha haja. Awali mali zetu zikiibiwa na hawa majambazi ambao wamejihami kwa silaha hatari polisi wa kawaida. Tunajua na sio i vile uajiri unaendelea katika nchi hii. Unamtoa mtoto Nairobi hajawahi kanyaga Turkana unampeleka kule. Akifuata hiyo mali kilomita moja anarudi kwa kambi. Hawa askari wa ziada wanafuata mali zetu kwenye mabonde na milima mpaka wanahakikisha zimerudi. Pia usalama wa raia wa kawaida unaimarishwa sana wakati wale askari wa ziada wako katika maboma zetu. Baadhi ya visingizio ambavyo tunapewa na wale ambao wanasimamia idara ya usalama ni kwamba kuna baadhi ya wale askari wa ziada ambao wanatumia hizo silaha vibaya. Tunajua kuna polisi wa kawaida ambao wamejiua wakitumia hizo silaha. Wengine wameua wake zao marafiki zao na pia raia. Lakini hatujasikia yule Waziri ambaye anahusika na usalama akisema polisi wote wapokonywe silaha. Kwa hivyo mimi ninarai na kusihi Bunge hili kwamba eno ya watu kukula dazi Nairobi na kutoa amri kwa mahali ambayo hawana.
Ninakushukuru Naibu Spika wa Muda. Ninataka kumpongeza Mhe. Sakaja kwa sababu ya kuuleta Mswada huu katika Bunge ili tuwasaidie vijana wetu. Katika Kamati ya Wafanyikazi na Ustawi wa Jamii tumeongea na Mhe. Sakaja na tumekubaliana kuwa tutafanya mabadiliko kidogo ili tuweke vipengele ambavyo vitashughulikia walemavu pia ili tusiwe na haja ya kuunda shirika lingine la kuwashughulikia walemavu na kina mama. Kwa hivyo tutaurekebisha Mswada huu ili uweze kuwashughulikia hawa watu wote. Pia tunataka kuwashughulikia wafanyakazi katika nchi za ng'ambo ili wasiendelee kuumia.
Ninakushukuru sana kwa kuelewa yale eno ambayo nilikuwa ninayazungumza. Ninaomba kila Mkenya aweze kupata nafasi nzuri anapofikisha umri wa miaka 18 ili apewe nafasi ya kuchukua ile stakabadhi ya kwanza na hiyo iwe inatumika. Sioni haja ya watu kuomba stakabadhi na kusubiri kwa miezi mitatu au minne. Maombi yote ya stakabadhi hiyo yanafaa kushughulikiwa mara moja ili mtu aweze kupata kitambulisho siku ya pili. Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Ninakushukuru sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi kuchangia Hoja hii ya dharura iliyoletwa na Mhe.Aluoch Jambo la kwanza ningependa kutoa rambirambi zangu kama Mbunge wa Turkana ya Kati maana kuna wanafunzi wanaotoka katika eneo langu la Bunge na wanaosomea sehemu hiyo. Ningependa kutuma rambirambi zangu kwa familia ambazo zimepoteza watoto wao. Jambo la pili ni kwamba maisha yaliyopotea ni maisha ambayo yalikuwa na matumaini makubwa katika nchi hii. Wazazi wao na nchi pia ilikuwa imewaangalia kwa njia moja au nyingine kuleta tofauti maendeleo au kuleta elimu yao kubadilisha maisha ya wazazi wao na kutumikia wananchi wa Kenya. Jambo la askari kutumia silaha zaidi ya wale watu ambao wanaenda kukubaliana nao limekuwa jambo ambalo tumerudia mara nyingi. Hao wanafunzi hawakuwa na silaha wala hawakutisha maisha ya askari kiwango cha kutumia risasi kuwaua. Kisheria maisha ya askari pia inalindwa lakini ni lazima pia askari aone adui ama mtu ambaye anakabiliana naye kama yuko na silaha ama hana ili ajue jinsi ya kukabiliana naye. Imefika wakati ambapo lazima askari wetu waende wapate mafunzo na elimu jinsi ya kutumia silaha kwa maana mtu anapoajiriwa katika kazi ya askari wengine wanaishi miaka mingi bila kuenda kwa mafunzo au kwa elimu ya kujua kuendeleza kazi yake mbele. Imefika wakati ambapo askari akiua mtu naye pia lazima aadhibiwe vikali ili iwe mfano kwa wengine. Kila mara askari anapoua mwanafunzi ama mtu yeyote kesi hiyo inaenda polepole mpaka . Hakuna hatua yoyote inayochukuliwa dhidi ya askari huyo. Ningependa kuona kwamba wanaohusika na vifo vya hao wanafunzi wamepatikana na mkono wa sheria ili nao wapitie uchungu ambao wazazi wa hao wanafunzi wanapitia sasa. Licha ya hayo kuna mambo ambayo pia yanachangia mambo hayo kutendeka katika vyuo vyetu. Jambo la kwanza ambalo Mhe. Millie Odhiambo amesema ni ukabila. Ukabila umezidi katika vyuo vyetu vikuu. Utakuta kwamba kuanzia juu mpaka katikati ni kabila moja. Wakati kuna jambo ambalo limetokea katika vyuo utaona kwamba linahusu kabila majo ambalo pengine wanabishana kisiasa na lingine; utaona kabila hili likifukuzwa ndiyo chanzo cha mambo yanayotendeka katika chuo. Tuangalie mambo hayo. Ni lazima makabila yote yawakilishwe katika chuo kikuu kuonyesha sura ya Kenya kwa maana tuna makabila zaidi ya 40. Ni lazima katika vyuo vyote kama mmoja ni wa kabila fulani wa pili awe wa kabila lingine. Kuna siasa kutoka nje ambazo zinaingia kwenye vyuo. Sisi kama wanasiasa tunaleta siasa za vyama na kuziinginza kwa wanafunzi. Hili ni jambo linalochangia wanafunzi kugawanyika na kuwa na ule mtindo wa kuchukiana na kuanza ukabila wakiwa bado shuleni. Naibu Spika wa Muda jambo lingine linalochangia kukosekana kwa nidhamu kwa wanafunzi ni ile hali ya sisi kama wazazi kuwapa fedha zaidi. Wanafunzi wanatumia fedha hizo kwa njia moja au nyingine kuharibu maisha yao. Kwa ufupi ninaunga mkono wale wanaosema hatua ichukuliwe kwa wale askari waliotumia silaha kuangamiza wanafunzi. Ahsante Naibu Spika wa Muda.
Ninamaanisha "wasee" na si "wazee". Ukicheki vile hiki kipengele kimewekwa utaona kwamba
Ninampongeza Mheshimiwa Joyce Wanjalah kwa kuleta Hoja hii. Kenya ni nchi ambayo iko na makabila 42 na mikakati ambayo tumeweka kila wakati haijanufaisha umoja wa Wakenya lakini tukiwa na lugha ambayo inaweza kuzungumzwa kutoka sehemu zote ni njia moja ambayo inaweza kutusaidia kuweka Wakenya pamoja. Kwa hivyo iwe ni lazima kwa shule zetu kufunza kwa lugha ya Kiswahili. Vile vile Kiswahili kifunzwe katika vyuo vya uwalimu ili tuwe na walimu ambao wanaweza kufunza Kiswahili. Kila mikutano ya kisiasa na kokote tuendapo tuwe tukiongea lugha ya Kiswahili ndipo tudumishe lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo ninampongeza Mheshimiwa Joyce Lay.
Ninashukuru Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Hotuba ya Mtukufu Rais kwa taifa tukufu la Kenya. Waswahili husema "aliye na macho haambiwi tazama". Ndiposa nasimama mbele ya Bunge hili nikishangaa sana vile wapinzani wetu wanaongea. Kaka aliyesema mbele yangu amenishangaza kwa sababu anapotoka yeye barabara ya lami ilifika baada ya Serikali ya Jubilee kuchaguliwa. Rais alizungumzia kuhusu vita dhidi ya uraibu wa madawa ya kulevya katika nchi tukufu ya Kenya. Hakuna Serikali nyingine ambayo nimeona ikipigana na janga hili la madawa ya kulevya na uraibu wake jinsi Serikali ya Jubilee ilivyopigana nayo. Vizazi vyetu haswa vijana wanaangamia kwa sababu ya madawa ya kulevya. Cha kushangaza waraibu wakuu na wenye biashara kuu za madawa za kulevya ni watu ambao wana sifa kocho kocho katika nchi hii. Wamesikika na wameshikilia nyadhifa kubwa kubwa katika nchi hii na ni watu ambao wana nia ya kugombea kiti cha Urais katika nchi hii. Ndio maana ningependa kumwambia Rais wangu apigane na vita vya madawa ya kulevya aokoe vizazi vyetu na vijana wa nchi hii. Suala lingine nyeti ambalo Rais alizungumzia katika Bunge hili ni usalama. Yale ambayo tumeona yakifanyika haswa katika baadhi ya kaunti kama vile Laikipia ninakotoka Kaunti ya Baringo hawa ni majambazi ambao ni Wakenya na wanaangamiza wakenya wengine. Hii ndio maana ninataka kumpa heko hata kwa kutuma jeshi kwenda kudhibiti usalama. Rais anapozungumza kuhusu kupatia kazi vijana tunaelewa biashara ambayo sisi Wanalaikipia tunafanya. Biashara ambayo iko Laikipia ni biashara ya utalii. Biashara ya utalii katika Laikipia inaenda kuangamia kwa sababu ya ujambazi na jinsi tulivyoona mahali pa utalii pakiharibiwa. Baadhi ya mambo ambayo yameharibu usalama na kuchangia sekta ya utalii kufa Laikipia ni siasa duni ambayo imechangiwa sana na wapinzani wetu. Hii ndio maana ninasema aliye na macho haambiwi tazama. Iwapo tutaua sekta ya utalii nchini kazi kwa vijana itatoka wapi? Wale wanachangia katika kuua sekta ya utalii nchini wanatarajia kuchaguliwa kesho. Hawa ndio tunawaita mahasidi wasio na mbele wala nyuma. Tukitazama mambo ya ugaidi nchini na mipaka ya Kenya ni sharti tupigane nayo. Jumamosi iliyopita tuliona Rais akitembelea vikosi vyetu vya jeshi kule Somalia. Ningeomba ndugu zangu walio katika Bunge hili kuwa tupigane na ugaidi kwa pamoja na si kuliachia jambo hili Rais ama jeshi pekee. Ninavyoelewa ni kwamba waliochangia pakuu kutuma jeshi letu Somalia mmoja wao ni yule babu ambaye anatarajia kugombea kiti 2017 ambaye ni kinara wa Upinzani ambaye tunamfahamu kama Raila Odinga. Ninaomba ndugu zangu walio Upinzani wasipinge tu kwa sababu Serikali ya Jubilee imefanya lakini wapinge kwa sababu ya kupinga. Ukitazama sekta ya kawi
Ninashukuru Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Mswada huu. Pili ningetaka kumpongeza Mhe. Okoth kwa kuuleta Mswada huu wakati ufaao. Haswa kwa ujuzi ninao kwa mambo nimepitia Mswada huu unahitajika sana na ni muhimu sana sisi kama Wabunge tuuangalie kwa makini. Mara nyingi Miswada huja hapa Bungeni na tunaikimbiza bila kuangalia matokeo yake. Njia za kuwaadhibu washukiwa kama wameshikwa na polisi zimezidi kila mahali. Polisi wanatumia njia nyingi sana. Matusi ambayo wananchi ambao tunaongoza wanatusiwa ni adhabu kubwa sana kabla hawajafikishwa kortini. Wanatusiwa vibaya sana. Polisi wanawatukana wananchi kwa majina ya waheshimiwa na watu wengine wakubwa. Ni kama hawa ndio mwisho. Ukishikwa na polisi ni kama umefika mwisho. Ningetaka kutoa mfano wangu mwenyewe. Wakati tulishikwa ambao tunajulikana kama Pangani 6 kuadhibiwa ambako tuliadhibiwa bila kupelekwa kortini kulikuwa ni kwa hali ya juu zaidi. Kama Mbunge ambaye anaheshimiwa na amechaguliwa na watu anawekwa seli na hawezi kupewa maji anapewa ndoo ya kuenda choo mukiwa na wengine huko ndani huwezi badilisha nguo hii ni adhabu ambayo haitakikani. Ndio ninasema Wabunge wajaribu kuangalia jambo hili sana. Nyinyi Wabunge kwanza ningeomba muanze kuelewa. Uhusiano wenu na polisi uko na shida. Wakiona Mbunge sijui ni kama uliwafanyia kazi gani. Inakuwa matusi ambayo haifai kwa mtu ambaye anaheshimika. Kama Mheshimiwa ataadhibiwa na matusi kama hayo mwananchi wa kawaida wale tunaongoza hali yao itakuwa namna gani? Pia kunyang'anya watu mali yao baada ya kushikwa na kuingizwa seli ni kuadhibu mtu kabla hajafika kortini. Unakuta hata njia ya kupea hawa watu chakula wengi wanaadhibiwa kwa majina ambayo hata siwezi kutaja hapa kwa sababu lugha hiyo ni mbaya kwa Mbunge kutaja. Lakini unakuta wanaadhibiwa vibaya sana. Hata rude zingine ukiingia hali ni mbaya sana. Kwa hivyo lazima tuangaliie mikakati. Nafasi imekuja ya sisi tuangalie huu mjadala na tuangalie ni kitu gani tutaweka kisheria ili kulainisha vifungo ambavyo tunaweza ongezea. Kwanza hasa wakati huu tunaenda kwa siasa. Na ile siasa tunaenda nawahakikishia nyinyi Wabunge polisi wanawangoja. Matusi mtapata na kuadhibiwa na kufungiwa mikutano ovyo ovyo. Hivi vitu viko hapa. Ni kama wakati wa kuvuna mahindi. Wakati wao wanasema umefika. Licha ya hayo kuna polisi tunaheshimu kwa sababu utaratibu wao ni mzuri. Wanaheshima wakitaka kukuletea summon s kuna utaratibu mzuri. Lakini kuna wengi ambao njia zao lazima tuzikatae kama Wabunge na tuweke sheria kali wataadhibiwa namna gani. Tumeona wengi wakifa katika seli; tumeona wengine wakibakwa wakiwa kwa seli; tumeona wengine wakiadhibiwa kwa njia ya matusi; na tumeona wengine wakiadhibiwa kwa kunyang'anywa mali yao. Hayo yote tumeyaona. Wakati umefika. Juzi niliona kwa NTV ulaghai wa polisi wa trafiki. Niliona wakiokota pesa kwa wananchi na nikajiuliza kama huyu mtu amewekwa kuchunga maisha ya raia ama amewekwa hapo Niliona polisi mmoja ambaye kijiti chake kimewekwa Big G upande wa chini ndio noti ikiangushwa chini inachukuliwa kwa hicho kijiti. Mambo haya ndio yako kwa seli na yana madhumuni ya kuadhibu watu wetu. Ni mambo ya aibu. Nauliza Wabunge tuweke mikakati ya kutosha kwa Mswada huu ili tusaidie mwananchi wa kawaida. Kama wewe utaadhibiwa kama Mbunge unafikiriaje mtu yule wa chini? Wengi wanakubali mambo fulani yafikishwe kortini ili waondoke kwa seli. Sio kwa sababu wamekosa lakini wanakubali ili waondoke kwa seli. Afadhali waende kortini ama wapelekwe rude kwa sababu ya ile adhabu iko kwa seli. Kwa hivyo utaratibu wa kujua mtu kama amefanya makosa sio kumwadhibu kumpiga au kumnyang'anya mali yake. Kuna utaratibu ambao unahitaji kufuatiliwa. Jambo muhimu tungeomba Wabunge wenzangu ni tuangalie sana jambo la kutozwa faini au kifungo kwa mtu anayemuumiza Mkenya bila sababu. Kuchukua sheria mikononi mwako Sehemu zingine unawekwa stesheni ya polisi kabla ya kupelekwa kortini na utahukumiwa huko utapigwa faini huko utaachiliwa huko ama utaadhibiwa huko huko ndani. Kwa hivyo ninaunga mkono jambo hili ili tuweke mikakati. Mhe. Okoth Mungu akubariki sana.
Ninashukuru mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa pia kumshukuru Mbunge aliyeweka Hoja hii mbele yetu na kwa busara kubwa ambayo ametumia. Itafahamika kwamba dhuluma waliofanya hao wabeberu kwa nchi hii ni nyingi sana. Tukisema Mau Mau itafahamika kwamba kila kabila la Kenya lilikuwa na Mau Mau yao na inategemea kila kabila liliita Mau Mau yake nini. Waliyoyafanya hao wabeberu katika nchi hii na kuwadhulumu watu wa Kenya yalikuwa mabaya na mengi sana. Kwa mfano waliwafunga mashujaa wetu mmoja wao akiwa ni hayati mwanzilishi wa taifa hili Mzee Jomo Kenyatta. Itafahamika kwamba tukiongea juu ya mashujaa na dhuluma ambazo walifanya wabeberu na tunataka fidia ilipwe ili kufidia wale ambao walipata madhara kutokana na wabeberu na mambo waliyofanya. Itakumbukwa kwamba wanawake wa nchi hii walifanya mambo mengi kupigania uhuru wa Kenya. Lakini mara nyingi wanawake wamesahauliwa katika kufidia mashujaa. Itafahamika kwamba wanawake wengi waliwachwa na mzigo wa kulea familia na baadaye kufanywa wajane baada ya mabwana zao kuuawa. Pia wanawake wengi ambao mabwana zao waliwekwa vizuizini walinajisiwa na maafisa weupe na kubebeshwa watoto weupe ambao leo hii hawana baba; sijui wanaitwa wa nani. Itafahamika kwamba baadhi ya taabu tulizonazo leo katika Kenya ni zile ambazo tumeridhi kutokana na ukoloni wa wabeberu mojawapo ikiwa ni shida ya ardhi. Tukiongea juu ya shida ya ardhi itafahamika kwamba hadi tunapoongea siku ya leo Ukitembea katika eneo la Laikipia utapata kwamba 90 per cent ya ardhi bado inamilikiwa na watoto wajukuu wa waliokuwa wakoloni. Wenyeji wameachwa wakipigania vijipande vidogo sana vya ardhi. Kwa hivyo ni muhimu tutilie mkazo iwapo tunataka haki itendeke. Inatubidi tufahamu yale ambayo yaliaachwa na hawa wabeberu. Zile taabu ambazo tulirithi na tungali tunaishi nazo ziangaliwe. Mashujaa wote wafidiwe bila kujali wametoka sehemu gani. Bi. Naibu Spika wa Muda baadhi ya wale ambao walikuwa askari wa kikoloni yaani British Army walifanya mazoezi katika sehemu tofauti tofauti za nchi hii. Baada ya kutoka katika sehemu hizowaliacha mabomu ambayo mpaka leo yanaendelea kuwaua wenyeji na kuathiri mifugo. Walifanya mambo mengi ambayo ni ya kuvunja moyo sana. Kwa hivyo ningependa kusema kwamba Hoja aliyowasilisha mhe Wangamati ni muhimu sana. Naomba wabunge wenzangu tuunge mkono Hoja hii. Aidha tutilie maanani suala la kuibua njia ambazo zitawafaidi mashujaa hasa wale ambao wangali hai. Tunajua kwamba wengi bado hawajafa. Ni muhimu tuangalie masuala ya ardhi ili kwamba ardhi iliyonyakuliwa irudishiwe wale wanaostahiki kumiliki ardhi hiyo. Bi. Naibu Spika wa Muda naomba kuunga mkono Hoja hii.
Ninashukuru Mhe. Naibu Spika wa Muda. Umeamua na usawa. Ninaomba ieleweke kuwa kama umefuata sheria zifuate mpaka mwisho. Sheria zetu za Bunge zinampatia Kiranja wa Bunge nafasi kama ameagizwa na chama chake kuomuondoa mtu mmoja kutoka kamati. Isije ikawa kuna watu ambao wanataka kupeana adhabu. Ninaunga mkono Hoja hii bila tatizo lo lote.
Ninashukuru Mhe. Spika kwa kunipatia hii nafasi. Nitanena machache tu. Ninaunga mkono hii Ripoti ya Kamati. Nitataja tu kuwa ni jambo la kusikitisha sana kuwa hawa walimu ambao hata sisi wengine wao walitufundisha tunakutana nao kule mashinani wakiumia kwa sababu ya kutolipwa pesa zao baada ya kustaafu. Serikali imechelewa sana kubadilisha mipango ya malipo ya uzeeni kwa sababu hili jambo la kuwa kila mmoja anategemea Serikali kumlipa hayo malipo ni mbaya sana. Ilikuwa ni muhimu na hata sasa nitaomba wale ambao wanahusika katika Wizari mbalimbali za Serikali waweze kutimiza mpango wa malipo ya uzeeni ambao kila mmoja anachangia; mwenye kuajiri anachangia na mwajiriwa pia anachangia. Hatutaki watu wangojee kustaafu ndio ikae kama wanaomba kutoka kwa yule ambaye amewaajiri. Hayo mabadaliko yamechelewa sana katika mipango ya Serikali. Kila wakati tunaona hata Waziri wa Fedha anaweka pesa katika Bajeti kushughulikia hilo jambo lakini baadaye huo mpango hautimizwi. Kwa hivyo ni muhimu sana. Ni vibaya sana kwa sababu hawa waalimu walitimiza wajibu muhimu. Hii nchi haingeweza kufika mahali ilipo kama hawa walimu hawakuwafundisha wanafunzi ambao sasa ni viongozi katika hii nchi. Tatizo lililetwa na mahakama ambayo iliamuru kuwa malipo yapeanwe ambayo ni zaidi ya mishahara walimu hao walikuwa wakipata. Unakuta kuwa Ofisi ya Mkuu wa Sheria inajipata pabaya kwa sababu inaambiwa ishauri Serikali ilipe pesa ambazo kikatiba ziko na shida kidogo. Lakini kwa sababu kuna pesa ambazo zilikuwa zimetengwa na ni zaidi ya Ksh16 bilioni ninaomba wahusika wote wawili; Tume ya Kuwaajiri Walimu na pia hao walimu ambao wamestaafu na
Ninashukuru Mhe. Spika. Ningependa kusema kwamba hii shida si ya Samburu pekee kwa sababu inahusu wananchi wote wa Kenya. Kila sehemu ya Kenya huwa na shida kama hii. Serikali au watumishsi wake wakati mwingine huchukua ardhi ambayo ingetumiwa na wananchi. Wananchi wanaendelea kuumia ilhali Serikali haitumii hiyo ardhi. Tungependa kusema kwamba tunaunga mkono hilo Ombi la Mhe. Lelelit. Tunataka Serikali iamue mara moja ili wananchi wasiendelee kuumia wakati Serikali au jeshi haitumii hiyo ardhi saa hii. Pia ninasihi Tume ya Kitaifa ya Ardhi
Ninashukuru sana kwa sababu nilikuwa ninasikia short wave huko nyuma. Pili wizara husika na Serikali hazijachukua njia mwafaka ya kuangalia shule hususan shule za mabweni. Hapajawekwa njia mwafaka ili walimu wapewe mafunzo ya kuzungumza na wale wanafunzi. Ninataka nichukue mfano wangu mimi pamoja na wabunge 16 wa Seneti na Bunge la Kitaifa. Mhe. Anami alikuwa mwalimu wetu wa muziki. Leo hayuko hapa na sisi. Ninatai kupitia kwako Mhe. Naibu Spika wa Muda sauti ifike kwa wakenya wengine. Tulipokuwa shuleni wakati mmoja wafanyakazi waligoma. Wafanyakazi wote wa shule ya Lenana School ambayo ni ya kitaifa waliamua kugoma lakini kwa sababu ya ukakamavu na urafiki wa walimu na kwamba walimu hawakuwa na ubinafsi hususan mwalimu mkuu tulipanga kujipikia wenyewe. Chai ya asubuhi ilikuwa inapikwa na mwalimu mmoja au wawili lakini waliokuwa wanasimamia walikuwa ni wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha pili. Chakula cha mchana kilikuwa kinapikwa na walimu ilhali cha jioni kilipikwa na watu waliojitolea. Tuliendelea bila shida yoyote kwa muda wa takriban wiki tatu. Hakuna chochote kilichomwa wala hakuna jambo lolote lililotokea. Hii Kenya ni moja. Ninawasihi kuwa lazima turejee katika enzi zile za karne za zai jinsi watu walivyokuwa wanafunzwa katika shule. Wabunge 16 wako hapa na sote tumetoka shule moja. Tuna nidhamu ya hali ya juu. Asante sana.
Ninashukuru sana Mhe. Spika kwa fursa hii ya kuweza kuchangia Mswada huu kuhusiana na shamba za jamii. Kama tujuavyo shida hizi za mashamba zimetukumba haswa sisi wakazi wa Pwani Taita Taveta ikiongoza. Ni vizuri tukiwa na Mswada ambao unaweza kuambatana na Katiba yetu ya mwaka 2010. Lakini vile vile pia tutasubiri wakati ambao utafika wa kuweza kufanya marekebisho kwa sababu kunayo marekebisho mengi ambayo yanastahili kuongezwa kwa Mswada huu. Nikiguzia kipengele cha sita kuhusiana na nyadhifa za serikari ya Kaunti lazima zibainishwe wazi ni vipi. Kwa sababu mashamba haya ya jamii yako chini ya serikari ya kaunti. Kwa hivyo ni vizuri iwe wazi pale je majukumu ya serikali ya kaunti kuhusiana na haya mashamba yatakuwa ni yapi? Vile vile wakati wanashikilia haya mashamba ya jamii itakuwa ni kwa muda ngani? Na kama niwao watakaokuwa wakiweka hazina hiyo ama kuna wakati mwingine ambao kunauwezekano kwamba kamati inaweza tengenezwa ili kwamba mambo yote yanayohusiana na ardhi ya jamii yapitie hiyo kamati. Vile vile lazima iwe wazi kwamba kuna mashamba ya jamii ambayo hayajasajiliwa. Haya mashamba je wakati mtu amekuja kama mwekezaji katika kauti hiyo ni nani ambaye atahusika katika maswala hayo? Ni vizuri kama itakuwa wazi ili mtu yeyote ambaye anakuja kuekeza katika shamba za jamii jamii hizo ziweze kuwakilishwa vilivyo. ake wakati mwingine kuna mambo ya fidia kwa mfano. Lazina tujue hiyo fidia ni nani haswa watakuwa wanaangazia. Tukianganzia pia katika kipengele cha 37 tunaona kinazungumza kuhusu maswala ya ugawaji wa hiyo fidia. Ni vizuri wananchi wenyewe ama jamii ipatiwe nafasi sauti na nguvu ya kuweza kuaamua kwamba ni nini haswa inataka kutoka kwa yule mwekezaji. Hii ni kwa sababu wakati mwingine hata si fedha labda zinatakikana; wanaweza kuamua kwa sababu huyu amekuja kuekeza kwao waweke ombi kwamba awatengenezee barabara au awajengee hospitali. Mambo haya yanaweza kutoka kwa wananchi wenyewe. Vile vile nikiangazia katika kipengele cha 46 kunao watu ambao wameweza kukaa katika mashamba haya ya jamii bila idhini au stakabathi ambazo zinatakikana. Ni vizuri pia tujue kwamba kabla ya huu Mswada haujakuwa sheria je mambo yao yanaweza kuangaziwa ili wasije wakawa hawataweza kufaidika sheria hii ikipita? Vile vile kunao Waingereza ambao waliondoka na kuacha mashamba makubwa makubwa. Haya mashamba ni vizuri tujue kama yatarudishwa kwa jamii ama serikali. Inafaa jambo hili lifanywe wazi. Nikimalizia kunao watu ambao wanakuja kuwekeza kwa mfano viwandani. Ni vizuri wananchi waweze kuelezewa madhara ya kazi hiyo ambayo huyo kama ni mbwenyenye amekuja kufanya. Hii ni kwa sababu tukiwa na uwazi utapata kwamba kukiwa na hatari yoyote ni vizuri hawa wananchi waweze kuelezwa na wao wenyewe wapate nafasi ya kuweza kuamua ni sawa kiwanda kiwekwe hapo au si sawa. Mambo haya yote yakiangaziwa katika huu Mswada wakati utaletwa kwenye Kamati ya Bunge ninafikiri utakuwa wa kufana sana. Asante sana Mhe. Spika.
Ninashukuru sana Mhe. Spika. Hata mimi nachukua fursa hii kupeana rambirambi zangu kwa familia jamaa na marafiki wa Senator Kajwang'. Kwa kweli tumempoteza mtu shupavu mtu mkakamavu mtu ambaye alikuwa hana woga wowote; alizungumza kile ambacho alijua ni cha haki. Kwa kweli tumempoteza mtu aliyekuwa anapendwa na watu wengi. Nakumbuka hata katika mikutano yetu ya CORD akiwa amefika ulipata kwamba kila mtu alimshangilia na huo mkutano hungeisha kabla hajapewa nafasi ya kuzumgumza maanake wananchi wangelazimisha aongee. Katika wimbo wake wa "bado mapambano" lazima kuna kitu ambacho alikuwa anahisi kwamba hatujafikia. Kama ni kuhusu ukombozi alimaanisha hatukuwa tumeupata. Kwa hivyo wimbo huo ametuachia sisi ambao ni wachanga kisiasa tuweze kujua kwamba hatujafika na bado tung'ang'ane ili Kenya iweze kuwa mahali pazuri. Kwa hivyo tunaiombea jamii yake. Tunawaweka katika maombi kwa sababu huu ni wakati mgumu sana na bila nguvu za Mwenyezi Mungu hawataweza. Sisi sote tuweze kusimama na wao kwa maombi. Ninaamini ya kwamba Mungu ataisimamisha familia yake.
Ninasimama kuichangia Hoja hii. Sijaichangia Hoja hii. Nilisimama kwa jambo la nidhamu na nikachangia marekebisho. Ikiwa kusema kwangu kunawadhuru; kama hamfurahii nataka Sikuichangia Hoja hii.
Ninasimama kuunga mkono mjadala huu kuhusu ai. Wakaaji wa eneo langu la Baringo Kusini wamepoteza maisha kwa ajili ya mambo ya wizi wa ng'ombe. Hawa sio wezi wa ng'ombe lakini ukora unaojulikana na biashara kwa wengine. Ninakubaliana na wengine kwamba Serikali inajua wale ambao wanafaidika na biashara ya wizi wa ng'ombe. Wanaelewa kazi yao na kuna ukora. Inaonekana kwamba kuna wafanyakazi wa Serikali ambao wanakulia jambo hili. Huu ni ufisadi mwingine nchini humu na ni mbaya kwa sababu hawa wakora wanawaua watu wetu. Katika eneo langu la Baringo Kusini tumepoteza maisha ya watu 278 kufikia sasa. Mwaka uliopita waliua watoto watano ambao walikuwa wanasoma na wakachukua ng'ombe. Juzi tena wakamuua mwanafunzi. Jumatatu wiki iliyopita tulikuwa kwenye mazishi. Wamechukua ng'ombe katika sehemu za Arabal Mukutani na Rugus. Inajulikana vizuri na ukiuliza Serikali inasema kwamba wanawajua hao. Kama wenye wanafanya biashara hii wanajulikana mbona wasishikwe? Hiyo ni kusema kwamba wale ambao wanawajua hawa ambao ni wa Serikali wanakulia biashara hii. Kwa sababu ni biashara hawawezi kuharibu biashara yao. Kwa nini inachukua muda? Tuko na askari na Serikali. Hii ni nini? Ninamuomba Rais wetu Uhuru ajue kwamba watu wengine tunaishi katika ufukara na umaskini na tunapoteza maisha yetu. Shule 11 zilifungwa katika eneo bunge langu. Hivi majuzi tulifungua shule zingine na zingine bado zinafungwa. Wanaiba mchana kwa sababu bunduki ambazo zilichukuliwa na polisi wa ziada zilirudishwa. Sasa wanakuja saa tisa au saa sita mchana na kuwaua watu wetu. Serikali inajua. Tunaambiwa helicopter inakuja lakini maisha yamepotea. Tumebaki na wale ambao wako hospitalini na tunachanga pesa ili tugharamie malipo ya hospitali. Hili ni jambo mbaya katika nchi hii. Ninaomba yule ambaye alichukua Biblia na kusema kwamba atachunga mali na maisha ya wananchi kwamba hukumu iko mbele yake kwa sababu hatuwezi kuwa tukilia katika nchi hii wakati wengine wanakaa vizuri. Ninashangaa kwamba maeneo bunge saba jirani ya eneo Bunge la Tiaty yanalia kwa ajili ya Tiaty. Yaani hii Tiaty imeshinda nchi hii na Rais wa Kenya? Hii legacy Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta atawacha ya Big Four Agenda ni Big Four Agenda kwa sisi wengine tuuawe? Hii si haki. Tunataka fidia kwa watu wetu. Tunataka shule ziendelee vizuri. Tunataka barabara ziendelee vizuri. Hawa wakora wameingia katika eneo bunge langu wakati huu wa census ambayo inakuja. Ninaomba warudi kwao. Hatutakubaliana na tabia kama hii na hatutaruhusu tabia kama hii na huyu Mheshimiwa kutoka Tiaty ambaye anajifanya yeye ni mzuri. Ni mkaidi mkubwa na ni lazima ijulikane katika nchi hii kwamba huyu ndio mkora mkubwa zaidi. Tumepata shida zaidi wakati alichaguliwa kuliko wakati alikuwa hayuko.
Ninaunga mkono Hoja hii. Lakini kubwa ambalo nataka tuangazie kama viongozi ni kuwajibika kutekelza na kujua kwamba wananchi wa Kenya wanaumia popote walipo kwa ajili ya masuala ya afya. Asante.
Ningependa kumjibu Dadangu Mheshimiwa Mbarire kuwa ukimwita mwanamke "mama" ni kumtunukia heshima kubwa sana. Kwa hivyo katika kutatua shida hii ni kuhakikisha kuwa Wabunge wenzangu kama mama Cecily Mbarire wamefundishwa lugha ya Kiswahili ili lugha yao ijumuike na kuwa safi.
Ningependa kurekebisha Kiongozi wa Walio Wengi kwa kusema kuwa Mheshimiwa Ali ameleta Hoja hii kwa njia inayokiuka Katiba. Kipengele cha 119 kinaruhusu kila mtu kuleta Mswada au marekebisho yoyote ambayo yanagusia sehemu fulani kisheria. Kwa hivyo Hoja hii iko hapa kisheria na iko kwa njia ambayo inastahili. Kwa hivyo Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni anapotosha watu hapa.
Ningependa kusema hivi: Niko kwa Kamati ya Bajeti na Uidhinishaji wa Matumizi Tulimuita Waziri Yatani tukamuelezea hivi Mheshimiwa Wamunyinyi ambaye ndiye Mwenyekiti
Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa kila mmoja aliyechaguliwa kwenye Bunge la 12. Nasikitika kwamba ndugu Duale ambaye ameomba kupunguza siku za kujadili. Mheshimiwa Naibu Spika ningependa kuzungumzia maswala muhimu ambayo lazima tukubaliane kwa sababu lazima tufuatilie sheria ambazo zipo kuhakikisha kwamba ndizo za ukweli. Waheshimiwa wamesema vizuri kwamba kuna joto jingi katika nchi yetu. Nataka tuhakikishiane kwamba joto hilo litakuwa jingi sana. Litakuwa jingi hata wengine wenu mtaruka kupitia madirisha mkielekea nje. Joto hili tutahakikisha kwamba tumelihifadhi kwa kutia kuni nyingi mno. Ni tabia mbovu na nia mbaya kwa watu wenye akili ndogo kutaka kuongoza wenye akili kubwa. Hiyo ndiyo shida iliyopo. Kumbe ndiyo maana wenye akili ndogo ukiwapa nafasi kuongoza wanaharibu nchi.
Ningependa kuzungumzia mambo ya unyakuzi wa mifugo na usalama. Mambo ya usalama ni muhimu sana katika Kenya yetu. Tujue bila usalama hakuna vile tunaweza kuishi. Ningezungumzia kwa upande wa wafugaji. Ningeomba Mheshimiwa Rais aangalie zaidi mambo ya usalama kwa upande wa wafugaji kwa sababu inaonekana kuwa hiyo imekuwa biashara. Vita vile tunapigana pale imekuwa ni biashara ama wizi. Kwa kweli Mheshimiwa Rais amesema kuwa wale wamepata taabu ya vita mbeleni Wafugaji wamepoteza waume wao na mali. Mimi pia ningesema wafugaji walipwe fidia. Tumepoteza watu mali na kila Mkenya anajua kuwa mahali ambapo ninatoka watu wengi wamekufa na hadi wakati huu bado askari wanaendelea kufariki. Inafaa jambo hili liangaliwe kwa makini kwa sababu moto ukichoma pahali pamoja unaenea kote. Mambo haya kila siku yanachukuliwa kama cattle rustling . Ningesema ni vyema ijulikane ni kwa nini shida inatokea katika pande hizo za wafugaji kila wakati. Kuna mambo ya ukame. Ingefaa tuliangalie jambo la ukame kwa sababu ukame uko kila mwaka. Tunategemea mvua ya Mwenyezi Mungu. Ingefaa pia hayo mambo ya ukame yaangaliwe kwa sababu watu wanaenda kuzunguka kutafuta nyasi. Wakati wananchi wanaenda kutafuta nyasi jambo hili linaleta shida. Kwa hiyvo ninaunga mkono. Tunaambia Rais asimame hivyo na aendelee hivyo. Mambo ya ufisadi na wizi yanafaa yaangaliwe zaidi. Ningeomba na kusema ya kwamba tusiyachukue haya kuwa ni mambo ya ukabila. Kama una ufisadi ni afadhali uangaliwe zaidi. Isichukuliwe kama kuna wale wanadhulumiwa. Hakuna mtu anadhulumiwa. Kama mtu ni mfisadi lazima aangaliwe. Wakenya wote wanamuunga mkono Rais. Kwa vituo vya Huduma pia tunashukuru sana. Vituo vya Huduma vinaletea Wakenya ufaa kwa sababu huduma zote ziko karibu. Wale watu hawawezi kufika Nairobi watapata huduma yao karibu.
Ningependa tu kueleza kuwa lau wangekua na nia safi Mswada huu ungeletwa kwa njia yaa kisawasawa sio kwa njia ya Mswada kumba. Huu Mswada Kumba ukiletwa njia na madhumuni na nia ilikuwa ni Mswada kama huu ukiwekwa huwa ni Mkusanyiko wa sheria tofauti tofauti lau kuna mabadiliko ya herufi na mambo madogo madogo ambayo hayana uzito wa maana hivyo. Lakini leo kupeleka Mswada kama huu kwa kupitia njia hii ni njia ya ulaghai ambayo inatumika. Watarejea hapa. Ningependa kulielezea Bunge kupitia kwako wewe Spika kuwa huu Mswada ukibadilishwa njia na madhumuni ni nini? Serikali ya Japan ilitoa bilioni 27 kukajengwa terminal mpya kule Mombasa na kukaandikwa mkataba. Katika ule mkataba walielewana kuwa lau kutakuwa na nia ya kuwa shirika ambalo si KPA kuendesha terminal ile basi kulikuwa kutumike Public Private Participation ile Act iweze kutumika. Leo tunajaribu kuletewa mashirika ambayo niya kibinafsi kutumia njia ambayo si sawa. Lugha watakayotumia ni kuwa njia hii ni kuweza kuleta Kenya National Shipping Line. Mbele yangu kuna stakabadhi ambazo zimeletwa katika kamati tofauti za Bunge; kuna karatasi zenye kuonyesha hii Kenya National Shipping line ni ya nani. Asilimia 74.3 inafaa kuwa ya KPA asilimia12.5 ni ya Unimar na asilimia12.5 nyingine ni ya kampuni DEG. Lakini Serikali wamekubaliana na kabla ya sheria kupitishwa lakini hizo hisa hazijatolewa. Hivi sasa KPA ina asilimia 53 Kampuni ya AON ina asilimia 23 kampuni ya Unimar ina asilimia 7 na Kampuni ya DEG ina asilimia saba. Sasa wanajaribu.
Ningependelea sana na naomba Wajumbe tuweze kujionyesha Hii ni kwa sababu ya changamoto tuliyonayo ndiyo Mhe Rais pia aone Wakenya wamechangamka na wanaweza kujadili kwa Kiswahili kama alivyotuhutubia kwa Kiswahili
Ningetaka kujua kama kuchukua video inakubaliwa maanake si vizuri yeye kukurekodi. Nataka atueleze ako na nia gani na wewe.
Nitauliza kwa Kiswahili kwa kuwa najua Kiswahili sanifu. Mimi hapana. Mimi nimeelewa na nitazungumza Kiswahili sanifu. Mhe. Naibu Spika jana katika mkutano wa kamati ambayo inaratibisha kazi ya Bunge ambayo inaongozwa na Spika wa Bunge tulimuuliza Katibu wa Bunge hili afanye mabadiliko katika hiyo Hoja.
Nyali Independent): Shukrani sana Mhe Naibu Spika wa Muda Kwanza ningependa kuipongeza Kamati ya Utawala na Usalama wa Taifa kwa kazi nzuri waliofanya Labda watu hawajui kwamba mimi ndiye mmiliki wa mapendekezo ya hizi sheria kabla hazijawasilishwa katika Kamati ya Utawala na Usalama wa Taifa Ninawashukuru kwa sababu wamezingatia yale yote tuliyoyasema Nami ninaunga mkono kabisa Tatizo la mihadarati limekuwa donda sugu hususan katika eneo la Pwani Tulipokuwa tukiangalia sheria za hapo awali na hizi mpya kulibaini wazi kuwa sheria zilizokuwa zikitumika hapo awali hazikuwa nzito kiwango cha kuwazuia walanguzi kuleta madawa humu nchini Ningependa kuzizungumzia hizi sheria ambazo zimekuwa kali zaidi Ni sheria ambazo tumeweza kuzigawanya kwenye njia tatu Hapo awali mlanguzi wa madawa ya kulevya na mtumizi walikuwa wakihukumiwa kifungo kimoja hukumu moja Sasa imebainishwa kuwa mtumizi anayeuza na mlanguzi kila mmoja wao yuko na hukumu yake Jambo muhimu katika sheria hii ni kuhakikisha kuwa wale ambao wametumia nguvu za mapeni kuweza kutawala anga na kuhakikisha watoto wetu wanafariki wanachukuliwa hatua kali ya kisheria Hii sheria hakika inaweza kuwalinda Wakenya na watoto wetu kwa jumla Polisi sasa wako na sheria itakayomuadhibu atakaenda kinyume na sheria Walanguzi wa madawa ya kulevya na watumizi wako na sheria yao kila mmoja Labda kulikuwa na mtafaruku hapo awali wa kusema kuwa zile faini zilizowekwa hususan kwa watumizi wa bangi na cocaine ni kana kwamba wamefinyiliwa sana Lakini imepunguzwa kutoka ile pesa ya shilingi milioni ishirini na kifungo cha miaka mitano na kuletwa chini kabisa Katika siku za usoni wanasayansi wanasema kuwa inaweza kutumika kama matibabu ya saratani Ninaunga mkono na ninasema kuwa yeyote atakayepinga swala hili ni adui wa nchi Hii ni kwa sababu watoto wanaumia wanakufa kila kukicha na Serikali sasa imepewa nguvu maradufu ya kuweza kunakili kuingia katika nyumba na kupata ushahidi wa sauti na video na kuutumia katika mahakama Swala la kuwaondoa hapa nchini na kuwapeleka nje ni sawa kabisa Hii ni kwa sababu lau kama tungeeendelea kukaa katika huu uongozi wetu yale yaliyopata Bwana Akasha hayangelimpata Angezidi kuendelea kufanya yale aliyoyafanya humu nchini Kwa hivyo hii sheria ya kuweza kubadilishana kimawazo kama kuna Mkenya anauza madawa ya kulevya hapa nchini Kenya na amepotelea Tanzania ama taifa lingine Serikali ina haki ya kuzungumza na Serikali ya huko na kuhakikisha kuwa ameletwa humu nchini ili aweze kupata adhabu ya kuangamiza watoto wetu Ninafurahia vile Kamati hii ilivyofanya kazi yake Namuona ndugu yangu Mhe Kaluma hapa Wamefanya kazi nzuri na natumai hii sheria itatumika kuhakikisha kwamba matatizo ya dawa za kulevya ambayo yamekuwa donda sugu tangu jadi yamefika mwisho Ukiangalia matatizo ya dawa za kulevya zikiwemo cocaine na heroine yanashuhudiwa Mombasa na katika eneo zima la Pwani kwa jumla Huwezi kupata mteja Nairobi Kisumu Bonde la Ufa ama kwengineko Wote wanaangamia kupitia sehemu ya ukanda wa Pwani Hapo ndipo hizo dawa zinaingilia Vile vile sheria hii itahakikisha kwamba yeyote anayesimamia kwa mfano Bandari ya Pwani ama sehemu zote ambazo ni za kuingia katika Jamhuri ya Kenya yeye binafsi ndiye atakayechukuliwa hatua za kisheria Hii ni kwa sababu wananchi na Serikali ya nchi imeweza kumpa nafasi hiyo kuhakikisha kwamba hizi dawa haziwezi kuingia tena Hizi dawa zikiingia ni sharti kama ni mkurugenzi wa Halmashauri ya Bandari nchini (KPA) ni lazima aeleze zimepita vipi Pwani na kuingia hadi Nairobi ama sehemu nyingine Kama ni katika mipaka yetu kwa mfano Naga na Malaba ni lazima pia aeleze ni vipi dawa hizi zimeingia Vile vile sheria hizi zimewapa polisi nguvu ya kutosha Hapo awali polisi walikuwa wakiwashika walanguzi na kuwafikisha mahakai lakini ilikuwa zile hadithi za lelemama Unafika pale mambo yanapotelea mbali kwa sababu ya nguvu za kazi Serikali sasa inaweza kushikilia mali ya mlanguzi wa dawa za kulevya hadi pale mahakama itakapomtangaza kuwa ni mtu msafi ndiyo arudishiwe mali yake Hii itawazuwia walanguzi wa dawa za kulevya kuwekeza pesa katika biashara Wanawekeza katika mijengo na mataifa ya nje Hii sheria itaipa Serikali nguvu ya kufuata pesa hizo Pia tumependekeza kuwa hizo pesa zikipatikana zitumike kujenga rehabilitation centres ambazo zitakomboa watoto wetu na kuwarudisha katika hali ya kawaida Nitamalizia kwa kusema kuwa yeyote atakayepinga hii sheria mpya ni adui wa taifa na watoto wetu na anafaa azuiliwe katika kila njia kuhakikisha watoto wetu wanapumua na dawa za kulevya hazimo Tunataka kuona Kenya ikiwa kama mataifa mengine kama vile Malaysia na Singapore Ukienda kule na upatikane na gramu hata moja ya dawa za kulevya hukumu ni kifo Serikali za zile nchi zinawekeza katika watoto wao na kuwalinda pia Tunataka kuwa na hizi sheria kali ili tuweze kuwekeza katika afya bora na watoto ambao wako na akili na fikira za kuikomboa nchi hii katika siku za usoni Tusiwekeze kwenye watoto ambao wamegeuzwa na kuwa mazezeta wasiojua mbele wala nyuma Maisha yao yatakuwa vipi kwa sababu ya dawa ya kulevya? Pindi tu hii sheria itakapopita pia tunataka kuona asasi zote za usalama nchini Kenya zikichukua hatua Hapo awali walikuwa wakisema hii sheria sio kali hailindi na inafaa kubadilishwa Sasa hivi Bunge hili kwa heshima ya Kamati ya Utawala na Usalama wa Taifa limeweza kuleta hii sheria ili iweze kupitishwa Sasa tunataka kuona maafisa wa kulinda usalama katika asasi zote wameanza kufanya kazi Hatutaki hao samaki wadogo watumizi tunataka walanguzi wa dawa za kulevya Hapa Kenya hawako wengi Wakati mmoja miaka ya nyuma mambo mengi yalizungumzwa katika Bunge hili Ni sharti Serikali ya hii nchi kupitia asasi za usalama kusimama kidete na kutumia sheria hizi mpya ambazo zimeletwa kukinga watoto wetu na kuhakikisha kwamba kwenye ukanda wa Pwani na Kenya nzima suala la madawa ya kulevya halimo tena Ukiangalia maswala hayo ya madawa ya kulevya yamevuka mpaka sasa Watoto wanakimbilia dawa zingine za kujichanganyishia kama vile codeine Watoto pia wanakula muguka na wanatumia kila aina ya dawa za kulevya Ni lazima katika hii nchi tuwe na utaratibu wa kuwakinga watoto wetu Ni lazima kuwepo na sheria ambazo zitalinda maslahi ya watoto wetu kwa sababu nchi ambayo inazalisha ujinga itatawaliwa na ujinga miaka nenda miaka rudi Lakini nchi ambayo imeekeza katika elimu ya watoto wake na inayowekeza na misingi bora inakuwa kiafya kimiundo misingi na nguvu kazi Kule Mombasa ama katika sehemu za ukanda wa Pwani vijana wote hawana kazi Asilimia kubwa ya vijana wanatumia madawa ya kulevya Ni kwa sababu tumeshindwa kuwapa nafasi ya kuelekeza fikira zao kwenye elimu katika miundo misingi na kwa nguvu kazi Hii sheria ambayo imeletwa ni nzuri sana Itahakikisha hayo yote tunayozungumzia yataisha Nataka kumwona Mhe mwenzangu Kaluma atakapotembea katika sehemu za ukanda wa Pwani awe anaona kuwa mambo ni shwari na sisi sote tutafurahi pamoja na kulinda heshima ya watoto wetu Kwa hayo machache ninaunga mkono Asante sana kwa huu uhusika wote Shukrani Naibu Spika wa Muda
Pongezi. Hicho ni Kiswahili sanifu kutoka kwa Mhe. wa Likoni. Tumsifu sana Mheshimiwa Shariff na Kamati yake kwa sababu wamefanya kazi nzuri kabisa kutuletea Ripoti ya usalama za feri zetu. Hasa sana kulingana na vidokezo ama maswali yaliyoletwa Bungeni kupitia kwa Kamati ya Public Investments Committee (PIC).
Samahani Mhe Spika Nimekuja kuchelewa Nimepewa habari kuhusu hiyo ripoti lakini kwa sasa haijanifikia mkononi
Sawa Mhe. Mishi. Wakati wako umekwisha. Tunampa sasa Mhe. Buyu Akinyi Mbunge wa Kisumu.
Sawa Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kulingana na uwezo wako na kulingana na hali ya Kiswahili nitazungumza Kiswahili adhimu na sitaunganisha lugha nyingine yeyote. Maana ya "in totality" ni kwa jumla. Kwa hivyo nimejirekebisha na kusema "kwa jumla". Neno "James" ni katika lugha ya Kizungu sijui niseme Jemsi Nyikal. Ni yale ambayo Mhe. Nyikal na vile vile Mhe. Millie Odhiambo walipinga. Katika Mswada huu kuna mambo ambayo yananigusa binafsi. Kama Mbunge kutoka kule Mombasa tumempa uwezo mkubwa sana huyu Waziri katika mambo ya bandari. Hali hii itatuumiza sisi kama wakazi wa Mombasa ambako bandari ipo. Hivi sasa mdahalo mkubwa unaoendelea ni kuhusu Kenya National Shipping Line (KNSL) kuungananishwa na Mediterranean Shipping Company (MSC). Jambo hili si la sawasawa kwa sababu hakuna usawa. Katika bandari ya Mombasa hivi sasa kampuni ya Maersk Line ambayo yatoka Uholanzi inabeba shehena asilimia 40 ya shehena za Serikali. Vile vile Pacific International Line (PIL) inabeba takriban asilimia 15. Nashangaa ni kwa nini KNSL isisawazishwe na zile kampuni nyingine. Ni kwa nini MSC inafanya kazi yote? Naona hata ndugu yangu Mbunge wa Mvita Abdullswamad anapiga makofi kunipongeza kwa sababu ni jambo la sawa. Ijapokuwa ni mimi ninayezungumza yeye ana fikra hizo hizo: kwamba ni lazima kuwe na usawa wa mambo haya. Kabla ya kuingia katika siasa nilifanya kazi katika bandari. Ni lazima tuangalie kwa umakini kwa sababu pesa zote ambazo zinaingia kwa MSC zinakwenda katika nchi yao ya Italy. Pesa nyingi ambazo zinaingia katika Maersk Line zinakwenda Uholanzi. Pesa zinazoingia katika kampuni za meli ambazo zimefungua ofisi hapa nyumbani zinapeleka pesa zile katika nchi zao tofauti tofauti. Kenya National Shipping Line iliundwa mwaka 1989. Madhumuni yake ilikuwa kuangalia jinsi tutakavyokuwa na laini yetu ambayo itabeba shehena zetu. Kwa hivi sasa kama alivyosema Mhe. Millie Odhiambo kuna watu watapeli ambao wanataka kuingia pale na kuona jinsi watakavyopata commission na mambo ya tenda. Mediteranian Shipping Company Maersk Line PIL na kampuni kama Global Container Line zipo. Wanafanya kazi kutoka nchi zao na kuja katika bandari yetu ya Mombasa. Nashangaa mpaka sasa hakuna mabaharia ama vijana wetu wowote ambao wameandikwa katika hizo shipping lines ambazo ziko hapo. Ile basi ambayo bandari ya Mombasa inataka kutumia imejengwa kutokana na pesa za ushuru wa mwananchi. Haikujengwa na pesa za ushuru wa mtu mmoja. Haiwezekani kudhaifishwa au kubinafsishwa kwa mtu binafsi akaweza kuifanyia kazi ilhali ni sisi wananchi ndio tunaoilipia kodi. Kwa hivyo ni lazima kuwe na usawa ili sisi watu wa Mombasa tufaidike katika mpango huu. Kulingana na Katiba ya Kenya ni lazima kuwe na public participation yani watu kuhusishwa. Katika mambo haya watu hawajahusishwa kisawasawa. Wasitufanyie ule mzaha ambao kwa Kiswahili unajulikana kama "kiriba goji goji kiriba" - yani kutuzungusha tu hapo hapo kisha baadaye tunakuwa hatuna mbele wala nyuma. Ni mwezi mmoja na nusu uliopita tangu Serikali iamue kwamba watu watapata kipato kutoka kwa Mbuga ya Wanyamapori ya Voi. Tukiangalia katika Maasai Mara watu wanapata kipato kule Kaunti ya Narok. Mpaka leo hakuna chochote ambacho tunapata kutoka bandari yetu ya Mombasa. Watu wetu hawaajiriwi kazi kwa usawa. Nataka kupiga firimbi hapa leo. Hata kama bandari ni rasilimali ya Serikali kuu ni lazima watu wahesabiwe ili waangalie wale ambao ni wenyeji wa pale. Ukiwa Mkamba Mkikuyu Mjaluo ama Msomali na unaishi Mombasa ni lazima upatiwe nafasi ya kwanza katika bandari. Kwa hivyo hivi sasa tunaona kuna watu wengi sana ambao wanaajiriwa katika bandari na kuna watu wetu ambao wamesoma na hawapati nafasi kama hiyo. Kwa hayo machache nashukuru Wabunge wenzangu kwa kukataa Mswada huu kwa sababu utatuumiza. Nikimalizia kwa sababu tunataka kwenda kufuturu baada ya dakika tano nataka kuchukua fursa hii nikiwa Muislamu na Mbunge ambaye anahudumu katika kipindi cha pili cha Bunge hili kuwaombea Waislamu wote popote pale walipo. Nawatakia Ramadan njema. Wafunge kwa kusaidiana baina ya wenyewe kwa wenyewe na kusimamisha dini ya Kiislamu. Asanteni na Mwenyezi Mungu atusaidie. Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Napinga sana Mswada huu kutoka Pwani eneo Bunge la Jomvu Kaunti ya Mombasa.
Sha watu ama wananchi kwa jumla. Kwa sababu najua kuna marekebisho kadhaa ambayo yatakuja na tutayazungumzia hapa na kukubaliana nayo naunga mkono haya mapendekezo. Swala la ardhi ni nyeti na linaguza kila mmoja aliye hapa. Hata wengine wakisema ni maskwota wengine wamenunua mashamba na bado wanachukuliwa kama maskwota. Hiyo ni kwa sababu hili swala halijapatiwa uzito vile linavyostahili. Nikiangalia sehemu ambayo natoka ya Taita ardhi imenyakuliwa na kuchukuliwa. Unapata Wataita wanakaa kwa theruthi moja tuu ya ardhi yao. Hiyo nyingine yote imeenda. Ndiyo maana tulikuwa tunatarajia kwamba tutapata nafasi ya kipekee ya kuleta sheria ambazo zitangalia wale watu walio dhulumiwa na mambo ya ardhi. Kwa sababu ya hekima ambayo hii Kamati iko nayo ilionelea ni jambo la busara zote zishikanishwe ziangaziwe pamoja. Kuna sheria za kufurusha watu sheria za ardhi ya umma na sheria za watu ambao wamehujumiwa. Sheria zote zikusanywe na kuwekwa pahali pamoja ili mtu akitaka kuangalia sheria za ardhi asiwe anaenda kwa kitengo hiki na kile na kuzunguka huku na kule. Atakuja kwa hizi sheria za ardhi ambazo zimeletwa pamoja. Ataziangalia na kuzisoma kuanzia sheria za ardhi zenyewe sheria za mambo ya vile wengine wamefanyiwa tangu hapo awali sheria za kufurushwa kwa watu na sheria za umilikaji. Tukiangalia yale ambayo yanaendelea nchini hivi sasa ule ufisadi uliopo na vile watu wamejipatia stakabadhi na vyeti vya mashamba utapata kuwa moja wa vitu ambavyo sheria hizi zinapaswa kuzingatia ni kuhakikisha kuwa watu hawataendelea kunyanyaswa na kunyang'anywa mali yao.
Sheria za Bunge zinasema niko na uhuru wa kuzungumza lugha ya Kiswahila ama ya Kizungu. Nimeamua nizungumze kwa lugha ya Kiswahili ambayo ni lugha yangu na ninaielewa. Wala ninyi wa upande ule msifikiri kuwa Kizungu sikiwezi. Kizungu ninakiweza lakini nimeamua nitumie Kiswahili. Sasa kitu kinachowawasha ni nini? Mnawashwa na nini? Pilipili usiyoila yakuwashiani? Wachana nayo! Wachana nayo whether umeelewa Kama uko hapa Bungeni unatakiwa uwe unajua Kiswahili. Wewe ni Mkenya na huelewi Kiswahili. Ni Mkenya wa aina gani ambaye haelewi Kiswahili? Jai ninaomba nijieleze na nijifahamishe.
Shukran Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa hii fursa. Mwanzo kabisa kufufua kilimo cha korosho ni kupunguza taabu za Kenya.
Shukran Mhe. Naibu wa Spika. Nasimama kuiunga mkono Hoja hii na kuipongeza Seneti na pia Kamati za Nyumba zote mbili kwa sababu zimeonyesha uwiano. Nina ii kuwa uwiano huu utaendelea katika Miswada yote ili tuonekane kwamba tunafanya kazi kumsimamia mwananchi apate haki yake kwa pande ya Seneti na Bunge la Taifa lenyewe. Hoja hii imefungua mlango wa ajira zaidi kwa vijana kina mama na wenzetu waliozaliwa na ulemavu. Hili limekuwa tatizo sugu katika maeneo yetu ya Bunge. Vijana wetu hawana kazi ilhali kandarasi zinatolewa kwa watu ambao si wenyeji wa lile jimbo na watu wetu wanawachwa bila chochote cha kujishikilia. Mswada huu umekuja kwa wakati unaofaa. Pia utasimamiwa na sheria kwamba haiwezekani kwa kandarasi zote za sehemu hiyo zitolewe bila kuhusisha wenyeji. Pia imefungua njia ambayo itatuwezesha sisi pamoja na wananchi kufuatilia kwa kina zile kazi zinazofanywa kule nyanjani na kuweza kutoa maoni yetu kama kazi haifanyiki kwa njia ya kisawa. Naupongeza huu Mswada na naunga mkono kwamba tunaweza kusonga mbele. Shukrani sana.
Shukran Mhe. Spika. Kwa niaba ya watu wa Turkana Magharibi na mimi mwenyewe ningependa kutoa rambirambi zangu kwa wakenya wote na jamii ya hayati Mzee Moi. Ninamkumbuka binafsi kama aliyesaidika na karo ya shule ambayo yeye mwenyewe alianzisha kule Kabarak. Niliweza kutunukiwa scholarship ya shule hiyo hadi vile nilivyo hivi sasa. Nimefanya kazi kwa sababu ya nafasi aliyotoa. Namuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Shukran Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa nafasi hii. Mwanzo kabisa Hoja hii ni muhimu sana maanake pembe zote za Kenya kwa muda mrefu watu huzungumza kuhusu hawa wazee wetu ambao walipigania Uhuru lakini hakuna mtu ambaye alijitokeza na kuleta hii Hoja Bungeni. Mheshimiwa Wangamati nakupa kongole kwa Mungu kukumulika ili ulete hii Hoja hapa Bungeni. Wakenya ni kitu kimoja. Hata lile neno la umoja liko katika wimbo wetu wa kitaifa na limerejelewa. Hili neno lilitoka kwa sababu ya ule umoja Wakenya walikuwa nao wakipigania Uhuru. Ni vyema kuwafidia Mau Mau lakini pia ingekuwa vyema zaidi kama wale ambao walipigania Uhuru pembe zote za Kenya kufidiwa. Hata kuna wengine ambao walipigana vita vya ulimwengu na wamesahaulika kabisa. Hakuna jambo gumu kama kujitolea mhanga. Kule kwetu Taita Taveta kuna watu kama Mwangeka ambaye alijitolea mhanga. Ni vyema kumtambua kama mmoja wa wapiganiaji Uhuru. Vile vile kuna mapango ambapo hata mwanzilishi wa taifa hili letu la Kenya Mzee Jomo Kenyatta alikuja wakati mapambano yalikuwa moto moto pande hizi. Alikuwa anafichwa kwa hayo mapango. Ni vyema Serikali kutambua mapango hayo na wale ambao walihusika kuwaficha hawa wapiganiaji Uhuru. Kwa upande wa mashamba ni kweli baada ya kupata Uhuru kuna wananchi ambao bado wanatatizika katika mashamba ambayo yalimilikiwa na hao mabeberu. Mwatate ni mojawapo ya mahali ambapo wanasumbua wananchi sana kwa mashamba. Ni vyema baada ya kupitisha hii Hoja tujaribu kuangalia kila mahali na tutengeneze ile kamati ambayo itafuatilizia hii Hoja na itekeleze kila kitu ambacho tunaongea hapa. Ni vyema kutambua yeyote ambaye amefanya kitendo cha ushujaa. Kama vile mwenzangu aliyenitangulia alisema hawa wazee wa "Nyumba Kumi" na vijiji ni watu ambao wamesaidia kwa muda mrefu sana. Wangetambuliwa pia. Hata kule Taita Taveta kulikuwa na sherehe za kumbukumbu za Vita vya Kwanza vya Dunia. Wakati Vita vya Kwanza vya Dunia vilikuwa kule baadhi ya watu ambao walikuwa wanaishi hapo walipelekwa mahali tofauti tofauti. Kwa hivyo ni vyema kutambua watu hao na mahali kama hapo. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda mengi yameongelewa na sitakuwa na mengi ya kuongezea. Ninaunga mkono Hoja hii. Asante sana.
Shukran Naibu Spika wa Muda. Ninaiunga mkono Hoja hii inayogusia maisha ya wananchi wetu kule nyanjani. Wakati umefika wa kutambua haki za binadamu. Ni makosa sana kuwa vijana wetu wanapotaka kujisajili kule nyanjani wanaambiwa hawawezi kujisajili kuwa wapigaji kura kwa sababu hawana vitambulisho bali wana stakabadhi za kungojea vitambulisho. Kuwa na kitambulisho ni haki yetu. Pia kujiandikisha kama mpiga kura ni haki yetu. Ingekuwa bora kama Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka na wizara inayohusika na mambo ya vitambulisho wangeweza kukaa pamoja na kuwa na uwiano kwamba wakati vijana wanapopewa vitambulisho ama stakabadhi za kungojea vitambulisho waweze kujiandikisha kama wapigaji kura. Wakati Serikali ilipoanza kutoa vitambulisho humu nchini hakukuwa na mpangilio mrefu. Mtu alihitajika kujaza fomu zake zote na akimaliza anapigwa picha na kupatiwa kitambulisho chake. Sijui ni makosa gani yalitokea ama ni ufisadi tunaozungumzia ndio maana hakuna mtu anayeweza kuenda katika kituo cha usajili ili apate kitambulisho mara moja. Inachukua hata mwaka mzima kwa mtu kupata kitambulisho chake. Bunge hili lilipitisha sheria kwamba hata hiyo stakabadhi ya kungojea itambuliwe kuwa ni stakabadhi ambayo inaweza kumpa mtu ruhusa ama nafasi ya kuweza kujisajili katika upigaji wa kura. Zaidi ya hayo utakuta kuwa zile herufi zilizoandikwa katika stakabadhi za kungojea vitambulisho ni nyingi na zinachanganya. Mtu anasahau stakabadhi hiyo na inakua vigumu kuikumbuka. Pia wanaoziandikisha waweze kuangalia mbinu mpya za kupunguza herufi zile ndio mtu awe na urahisi wa kukumbuka nambari yake hata kama hajabeba stakabadhi yake na apate huduma mahali popote anapohitaji. Ningependa tume huru ya uchaguzi na mipaka ianze kuwatembelea wanafunzi shuleni kwa sababu wanafunzi hawawezi kuacha masomo na kwenda kwenye afisi ili wasajiliwe. Ninaiunga mkono Hoja hii nikiamini kwamba sheria itaweza kutekelezwa ya kuwawezesha watoto wetu kujisajili kama wapigaji kura. Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Shukran Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuunga mkono makadirio ya bajeti ya matumizi ya fedha ya mwaka 2017/2018. Imesemwa hapa kwamba ni muhimu kuzingatia matukio katika nchi. Ni wajibu wetu kuangalia upya jinsi tutakavyokabiliana na baadhi ya mambo ambayo yametukumba kama nchi. Nikizungumzia juu ya makadirio ya bajeti hii ni wazi kwamba wakati huu ni mgumu kwetu Wakenya. Tunashuhudia ugumu wa uchumi wetu ambao sasa hivi haufanyi vizuri. Bunge hili limepewa jukumu kuunda bajeti. Katika hali hiyo ni muhimu kuzingatia matarajio ambayo wananchi wameonyesha. Upande wa elimu Ksh23 milioni imetengwa kushughulikia elimu ya bure katika shule za sekondari. Fedha hizi zitashughulikia watoto wa Kenya nzima iwe ni kule Bondo Siaya Kisumu kule nitokako ama kwingineko humu nchini. Kwa hivyo ijapokuwa wenzetu wa mrengo wa NASA hawamo Bungeni leo inastahili watupongeze kwa vile tunawafanyia shughuli muhimu ambayo wangekuwa wanafanya wao. Bibilia inasema mtu asipofanya kazi hastahili kula. Nashangaa kwamba wenzetu wanakaa chini ilhali sisi tunawafanyia kazi muhimu na wanategemea kulipwa mshahara wa kazi ambayo hawajafanya. Fedha zingine ambazo imebidi kamati itenge ni zile za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka. Tunafahamu kwamba sasa hivi tunatarajia kurudi kwa uchaguzi mpya tarehe 26 mwezi huu. Tulipoketi kama kamati kushughulikia masuala haya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ilikuja mbele yetu na kutupa mahitaji yao. Ningetaka pia ifahamike na Wakenya kwamba kama uchaguzi utafanyika tarehe 26 mwezi huu ama Novemba ama Januari ama Februari uchaguzi ni lazima ufanyike. Inastahili pia ifahamike na Wakenya kwamba kujiuzulu kwa kinara wa NASA katika kinyang'anyiro hakumaanishi alijiuzulu kama mpiga kura. Yeye bado ni mpiga kura. Shughuli hii imechukua shilingi bilioni kumi. Pia hii inawapatia Wakenya nafasi nzuri ya kuangalia iwapo korti zetu hazingetuingiza katika shughuli za kurudia kura hii. Iwapo huyu babu ambaye analalamika kuanzia asubuhi mpaka jioni hakulalamikia kushindwa ambapo sasa hivi pia amekataa kurudi kwa uchaguzi; pesa hizi zingetumiwa kwa kazi nyingine kama vile kuendeleza miradi ya barabara elimu na shughuli nyinginezo muhimu sana katika nchi hii. Pia katika kamati hii tukaonelea kuna pesa wanapewa wakongwe. Na nikisema wakongwe ifahamike kwamba ni wale maajuza na babu wa miaka 72 kuenda juu. Katika Bibilia inafahamika kwamba mtu ambaye anaishi baada ya miaka 72 anaishi kwa wakati wa kuomba. Kwa hivyo fedha hizi zinashughulikia pia wale watu wamefikisha miaka kama yule babu ambaye ni kinara wa Upinzani.
Shukran sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Pia mimi ningependa kuchangia na kusema kwamba hii ni aibu hapa nchini Kenya iwapo baada ya kutokea kile kisa cha Mtongwe bado hatujajifunza lolote. Ni aibu kubwa iwapo leo Serikali itatangaza na kusema kwamba haina hewa ya kutosha ama gesi ya kuweza kufika kule chini. Leo Kenya hatuna fedha za kununua hewa lakini tuna fedha za kununua vitoa machozi. Leo Kenya hatuna fedha za kununua hewa lakini tuna pesa za kununua makumi ya magari kwa viongozi. Leo hii katika Kenya hatuna pesa ya kununua hewa lakini tuna pesa za ufisadi. Hii ni aibu na ni sharti sheria ichukue mkondo wake na kuhakikisha kwamba wahusika wote ambao wamekaa kimya wakiangalia marehemu Mariam Kighenda na mtoto Ada Mutheu wakiangamia na kufa kifo cha polepole ni sharti wachukuliwe hatua za kisheria. Mhusika mkuu Waziri wa Uchukuzi Bwana Macharia achukuliwe hatua. Mkurugenzi Mkuu wa Kenya Ferry Services Kenya Ports Authority (KPA) Maritime Authority of Kenya na Kenya Coast Guards (KCG) wote wachukuliwe hatua za kisheria maana hii itakuwa ni hekaya za abunwasi. Tutakuwa tunarudia haya miaka nenda miaka rudi. Katika Mtongwe Ferry tulipoteza makumi ya watu na tulidhani labda tutajifunza mengi na kuhakikisha kwamba tumeweza kuwa tayari kwa matukio kama haya.
Shukrani Bi. Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii. Nilikuwa nafanya ushauri wa karibu na mhe Kamoti.
Shukrani Bw. Naibu Spika wa Muda kwa macho yako kunilenga na kunimpa fursa hii. Mimi natoka Mwatate Taita Taveta County ambapo ninapakana na mbuga ya nyama pori ya Tsavo. Kwa kweli nashukuru kwa Hoja hii na ninaiunga mkono lakini nataka iwe na marekebisho. Ukiwauliza watu wa eneo Bunge langu kuhusu kuchagua kati ya kuwachunga na kuwaua ndovu watakuambia hawa wanyama pori wanawasumbua sana. Sisi hatujaona mvua kwa zaidi ya miaka mitatu. Tumeiona mwaka huu lakini mimea yetu imeharibiwa na wanyama pori. Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kweli naunga mkono kuongezwa kwa walinda wanyama pori lakini tuangalie wale ambao wanaishi karibu na maeneo ya mbuga za wanyama pori. Bila hivyo hawataona umuhimu wa kuwachunga wanyama pori; naunga hii Hoja mkono lakini nataka iwe na marekebisho. Nataka tuongeze askari wa kuhifadhi wanyama pori tuhusishe watu ambao wamepakana nai mbuga zetu katika uchungaji wa wanyama pori. Jana usiku katika maeneo ya Mwakitau Sorongo na Mwachapo mimea ya watu iliharibiwa sana na wanyama pori. Hatuwezi kusema watu wa Kenya Wildlife Service (KWS) hawana vifaa. Mwezi jana nilikuwa Voi Safari Lodge na nikawa nauliza: Kwa nini Voi Safari Lodge inalindwa na polisi? Niliambiwa wakati walikuwa wanalindwa na watu wa KWS walikuwa wakiibiwa mara kwa mara na hii ilimaanisha kuna tatizo fulani katika KWS. Mwenye kuleta hii Hoja Bw. Ganya nampongeza lakini yafaa tuijadili kwa upana zaidi. Inahitaji marekebisho mengi sana maanake kuna tatizo kubwa sana.
Shukrani Bw. Naibu Spika wa Muda. Masikitiko makubwa ni kwamba utapata sehemu nyingi za nchi yetu ya Kenya hazipati huduma za afya vile inavyopaswa. Nikizungumzia eneo Bunge langu la Lamu Mashariki licha ya kwamba kupatikana madaktari ni vigumu hata hospitali zenyewe ama hata zahanati zenyewe hazina madawa. Watu huenda na kurudi; hata ingawa hufika huko akiwa mgonjwa anaambiwa kwamba dawa hakuna. Kwa hiyo mara kwa mara watu wamekuwa wakisumbuka au kuteseka. Hata huduma za X-ray hazipatikani. Leo Serikali imesema kwamba wanawake watajifungua bure lakini utapata hakuna sehemu ya akina mama ama akina dada zetu ya kujifungulia katika eneo la Lamu Mashariki. Utapata kwamba madaktari ama wahudumu ambao wako pengine ni mmoja katika zahanati; ama pengine utapata siku ya kazi mtu anapaswa awepo kazini lakini wagonjwa wanaenda hospitalini na kupata kwamba hata yule mmoja ambaye anapaswa awe pale hayupo. Bw. Naibu Spika wa Muda ukweli ni kwamba sisi tunazungumza mambo haya lakini maeneo Bunge mengi yana matatizo hasa mashinani. Mimi naunga mkono Hoja hii na bali na kuiunga mkono ningependa kupendekeza kwamba yote yatakayopitishwa katika Bunge hili kuhakikisha kwamba sio kwamba tumeyazungumza hapa Bungeni kwa sababu ya kuyazungumza ama kwa sababu ni Hoja imeletwa Inafaa tuhakikishe kwamba mambo haya yameweza kuwasaidia ndugu zetu ama jamii ambazo zimeweza kuteseka kwa muda mrefu. Hivi sasa wanahitaji kupata zile huduma ambazo Serikali hii imetuahidi. Tuna ii kubwa kwamba Serikali hii inaweza kuyatekeleza mambo mengi tukiwa tumekuwa kama kitu kimoja na kuwa na ushirikiano katika kuendeleza mambo yetu. Mimi nataka niunge mkono Hoja hii na nashukuru kwa hayo ambayo nimechangia.
Shukrani Bw. Spika kwa kunipatia fursa hii. Mwanzo kabisa kwa upana Hotuba ya Rais ilikuwa ya kufana. Hata asilimia theini kwa mia ninamuunga mkono. Ni maswala tu hapa na pale ambayo alikuwa ayashughulikie halafu angepata alama tisa kwa kumi. Mhe. Spika wengi hapa wanalia kwa ukosefu wa chakula kwa sababu ni taabu kukipata. Lakini Mwenyezi Mungu alitupatia hewa na maji bure. Kule kwangu sehemu ya Mwatate kupata maji ni shida. Kuna matatizo makubwa tunapochimba visima kwa sababu ya ukosefu wa hela kwa vile kaunti yetu ni ndogo. Tunapata maji ya visima yakiwa na madini. Hata watu wengine wanatuambia kwamba tukinyua hayo maji basi baada ya miaka kumi kwenda mbele wakati visasi vyetu vitakuwa vinapata watoto hao watoto watakuwa hawana mapua midomo na kadhalika. Tumejaribu kila namna. Tunapoongea juu ya usawa wa nchi inafaa Rais aangalie pembe zote za Kenya. Inafaa tuangalie wale ambao hawana maji ili wapewe ndio chakula ifuate na maswala mengine. Kule sehemu za Mwakitau kuna ndovu wengi na akinamama hawawezi kwenda kuchota maji ovyo ovyo kwa sababu wengine wameuawa. Kuna matatizo. Ni vyema wakati Rais anaangazia mambo haya anaangazie pande zote. Kamati za Bunge ambazo zinahusika na maji na bajeti zinafaa kuwa makini sana. Kenya ni yetu sote. Ni lazima tuangalie ni wapi hakuna maji ili tuzibe hizo pengo ndio tuje kwa maswala mengine. Sasa hivi ukiniambia juu ya barabara na sina maji hiyo barabara itakuwa haina maana kwangu. Juzi hapa Bungeni wakati Rais aliongea kwa Kiingereza kuna watu ambao walikuwa wanauliza kama tunaelewa. Katika hii Bunge Wabunge zaidi ya asilimia 90 wanaongea Kiingereza na wale ambao wanaongea Kiswahili ni asimilia 10. Lakini ukienda kule nje asilimia 90 ya wananchi wanaelewa Kiswahili na asilimia 10 ndio wanaelewa Kiingereza pekee. Ni vyema sisi kama Waafrika tuangalie na tuangazie lugha zetu bila kuchukua lugha za watu wengine na kujigamba wakati tunaongea lugha hizi mpaka wengine wanaweka vifua vyao mbele. Kwa kweli ni lazima tuangazie suala hili. Kwa kweli mazungumzo ya Rais yalikuwa ya kufana sana kwa sababu aliongea juu ya ufisadi na swala la utangao ili tuwe kitu kimoja. Ni vyema tuwe kitu kimoja kama dugu. Lile swala la ufisadi alilisisitiza sana na sisi tunangojea tuone vitendo. Asubuhi nilimsikia mwenzangu akiongea kuhusu mihadarati. Hili si swala la kuchekesha lakini ni swala mbaya katika pwani haswa Lamu. Hata kule kwetu sehemu ya Voi na kwingine hili ni tatizo. Sasa hivi Rais ameshikana na kinara wetu wa chama cha ODM na kwenda Uchina. Mtu kama mimi ninayetoka kabila ndogo siwezi kwenda Uchina ilhali kule Voi mpaka Taveta reli inatakikana zaidi kwa sababu Arusha iko karibu ndiyo iende mpaka Rwanda. Je nani atatusaidia watu wadogo kama sisi? Ninaomba pia ikiwezekana sisi Wakenya tubadilike. Juzi tumewapigia watu kura. Inafaa tuanze kufikiria kwamba ni bora Rais atoke kabila ndogo kama langu. Ahsante sana Mhe. Spika.
Shukrani Bwana Naibu wa Spika. Huenda nitaomba radhi kwa sababu Swali langu limechapishwa katika lugha ya kimombo. Sasa nitalisoma jinsi ilivyo.
Shukrani kwa kunipa nafasi hii. Mwanzo kabisa ningependa kuiunga mkono Hoja hii. Nikiangalia walioorodheshwa katika ratiba ya leo wote wanauzoefu wa kazi hii. Kabla sijaendelea nawatakia wenzangu mwaka wenye fanaka na vilevile kuomba wafanikiwe kwa shughuli nyingi walizo nazo mbeleni. Najua kwamba Wakenya wote wamejitokeza kujiandikisha kupiga kura. Ningeomba watoke na kujisajirisha kwa wingi. Vile vile Tume ya Uchaguzi na Mipaka au Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC) yafaa ijaribu kuangalia mahali kuna utata. Niliona mtu mmoja wa eneo langu la Uwakilishi Bungeni akijaribu kutumia kadi za watu wake ambao wamefariki na jambo la kushangaza ni kwamba bado hayo majina yamo katika orodha ya wapiga kura.
Shukrani kwa kunipatia dakika moja. Kwa ukweli kama ndugu zetu upande ule mwingine husema: "Kiswahili kilizaliwa kule Tanzania kikaanguliwa Kenya na kikafia kule Uganda." Itakuwa ni dawa ya huu usemi. Vile vile lugha huchangia pakubwa kwa kuboresha madili na mila kwa wale ambao wanaongea hiyo lugha. Ingekuwa ni vyema zaidi kutafi hizi sheria kwa lugha zetu kwa sababu hii itakuwa njia ya kuziboresha pia tutakuwa tunaboresha mila zetu za Kenya. Lugha ya Kiswahili
Shukrani Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Ninaunga mkono huu Mswada kwa hicho kipengele ambacho kimeletwa na Mhe. Eikor kwa sababu tumeonyesha wazi kwamba hili Bunge linasimamia kufadhili Katiba yetu na kukubaliana na yote tuliyopitisha. Lakini pia tutaweza kujitenganisha na wale ambao wanataka kufanya mambo yao wakati sisi tunaendesha mambo yetu katika Bunge hususan kama walivyozungumza Waheshimiwa wenzangu. Wakati ule wa nyuma tuliweza kuona wakituletea nguruwe na hali inajulikana wazi kwamba nguruwe si halali kwa Mwislamu. Walitutia katika hali ambayo haikuturidhisha kama Waislamu katika Bunge na hata Kenya nzima. Kwa hivyo ninaunga mkono.
Shukrani Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii. Kwanza natoa pongezi kwa Kiongozi wa Walio Wengi kwa kutuletea Mswada huu ambao haugusii jinsia moja tu. Kwa sasa inaweza kuonekana kana kwamba tunatetea haki ya wanawake pekee. Lakini tutakuwa tunajitayarisha kwa wakati wowote ikiwa itatokea kuwe na upungufu katika jinsia ya kiume katika mabunge yajayo. Hivyo watakuwa na sheria inayoweza kuwasimamia na kutoa haki katika nyanja mbali mbali katika maeneo tofauti tofauti yanayosimamiwa na mambo yanayotokana na kuchaguliwa. Mswada huu umekuja kwa wakati unaofaa. Hii ni kwa sababu tusipoupitisha tutakuwa tumeenda kinyume na Katiba yetu. Hii inaweza kutuletea matatizo. Bunge hili linaweza kusimamishwa kwa kuhalifu Katiba tuliyoitetea kwa pamoja. Pili katika kutetea Mswada huu itaonyesha wananchi wetu hususani akina mama ambao hujitokeza kwa wingi kutupigia kura kwamba tunawatambua kwa jitihada walizonazo nyanjani wanapotutafutia kura na kutupitisha ili tuwawakilishe katika Bunge hili na lile la Seneti. Kwa hali ya Mswada huu ni wazi kwamba kuna walio na akili potofu kwamba sisi tunajaribu kufungulia akina mama mlango ili watawale waume. Hivyo sivyo. Inatakikana kila mmoja aelewe kila upande wa jinsia una haki ya kutawala kutawalwa na kusimamia katika ngazi yoyote. Tunapoupitisha huu Mswada kwa pamoja hatutakuwa tunafungua mlango kwa wanawake pekee bali kwa jinsia zote. Mswada huu umekuja kwa wakati ufaao kuonyesha ii yetu kwa wenzetu wanaume walio katika Bunge hili. Akina mama tuliochaguliwa katika hili Bunge tumesimama na wenzetu Waheshimiwa wa kiume kupitisha mijadala tofauti tofauti. Safari hii tunaomba mregeshe mkono ili msimame nasi katika vita hivi vya kutetea haki ya akina mama. Si haki ya akina mama tu. Inatakikana ifahamike ya kwamba palipo na mama hata kama ni ndani ya nyumba inayotelekea mama husimama na nyumba ikawa imara. Msimame nasi tuokoe taifa letu kutokana na kutokuwa na usawa wa kijinsia. Sitakuwa na marefu kwa sababu ya hali yangu. Ningetaka nimkosoe dadangu Mheshimiwa Wanga. Tumetoka katika yale mambo ya kutoa tu. Nipe nikupe ndio mtindo wa kisasa. Kwa hivyo hatuko kwa kutoa peke yake. Ni nipe nikupe! Shukrani Mhe. Naibu Spika.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda ingawa nimeketi kwa muda mrefu mno. Nasimama kuunga mkono Hoja hii ambayo imerekebishwa. Hoja hii kwa kweli kabisa inaambatana na Katiba yetu kuhusu ugatuzi. Sisi ambao tuko karibu na mpaka tuna matatizo mengi sana wakati tunatafuta vitambulisho lakini tukipitisha Hoja hii haya matatizo yatapungua. Imekuja wakati mwafaka mzuri na sawa sawa kabisa. Ningependelea ikiwezekana tuweke marekebisho mengine maanake mtoto anapozaliwa anapata cheti cha kuzaliwa na vile vile wakati huo huo akitafutiwa pasi ya kusafiri nje inapatikana. Ingewezekana pia kitambulisho kingepatikana wakati huo huo. Vile vile kuna Cheti cha Tabia Nzuri kutoka kwa maafisa wa usalama kinachoitwa kwa Kiingereza Certificateof Good Conduct ambacho pia kinasumbua sana vijana. Tungesaidika sana ikiwa vyeti hivi vingeshikanishwa vyote kwa pamoja. Pia kuna nambari inayotumika katika National Treasury inayoitwa Integrated Financial agement Information System (IFMIS). Sioni sababu gani vitambulisho visigatuliwe. Vikigatuliwa wananchi wengi wataweza kupata vitambulisho. Kwa sasa hivi kuna wazee kina mama na waume ambao wako zaidi ya umri wa miaka 50 ambao bado hawana vitambulisho kwa sababu ni gharama kubwa kwenda kila saa kwa afisi kuulizia kuhusu hivyo vitambulisho. Wale maafisa hawako kule mashinani. Vitambulisho hivyo vikishapelekwa pale afisini Nairobi kufuatilia inakuwa vigumu kwa sababu hujui ni wakati gani vinatoka. Lakini vikigatuliwa kulingana na Hoja hii Wakenya watasaidika kwa kupunguza gharama muda na zile nguvu ambazo mtu anatumia kuvitafuta vyeti hivi. Wenzangu wameongea mengi. Naunga mkono Hoja hii na hayo marekebisho ambayo yamefanyiwa na Mheshimiwa sasa hivi.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili pia nami niongeze sauti yangu kwa huu mjadala. Hawa wazee wa kijiji ni wananchi wema kwa sababu wanafanya kazi nzuri. Wao ndio husaidia nchi kupokea habari za jambo lolote linapotokea katika eneo lolote nchini. Hili ni jambo ambalo lingefanywa kitambo. Ni wazee ambao hujitolea; hutoka majumbani mwao mapema na kurudi usiku.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia Mswada huu. Mswada huu utaokoa nchi yetu kutokana na walaguzi ambao wametuharibia mimea yetu ama mbegu ambazo zilikuwa tegemeo la mwananchi tangu abu na abu. Maradhi ambayo yanakumba nchi hii hivi sasa ni maradhi ambayo wakati wa wazee wetu hayakuwa. Kwa mfano kuna saratani. Saratani na ugonjwa wa Kifua Kikuu ni maradhi ambayo yalikuwa yakishika milango fulani lakini sasa yamekuwa maradhi ambayo yanashika watu ovyo ovyo. Hii inatokana na yale madawa yanayotumika katika kuchanganya mbegu ambazo zinaletwa na wenzetu ambao wanasema kwamba wameelimika zaidi kushida Waafrika. Mswada huu utalinda mbegu na mimea yetu na kulinda tamaduni na desturi zetu kama Waafrika wa Kenya. Miti na mimea ilikuwa ni ya dawa chakula na kivuli. Hivi sasa ile mimea tunayoletewa kwa kisingizio kwamba ndiyo mimea bora imeharibu mazingira. Kwa mfano huko Kwale katika sehemu ya Marere wakati sisi tulipokuwa wachanga Mto Marere ulikuwa haukauki maji. Lakini wakati ulipopandwa miti iliyoko sasa hivi ilikuwa chanzo cha ule mto kukauka mpaka leo. Kuna shida kubwa ya maji katika maeneo yetu. Mswada huu utatusaidia kuikuza mimea yetu na kuipatia mapato kwa kuwa tutakuwa tunaelewa mmea huu ni wa aina gani na unaweza kutibu nini ama unaweza kuleta lishe ya aina gani. Katika miaka ya sabini kule kwetu Shimba Hills kulikuwa na mzee ambaye alizindua mti ambao ulikuwa ukitibu saratani. Hatukujua ni vipi ilitokea kwa sababu wananchi walishtukia watu wamewasili kwa magari makubwa na kuikata ile miti yote wakaibeba na kuenda nayo. Wakazi wa sehemu hiyo hawajui ilikopelekwa miti ile. Hakuna faida ambayo huyo mzee na Serikali ilipata. Si ajabu kuwa mti huo unatengeneza madawa ambayo tunauziwa kwa bei ghali na ilhali huo mti ulitoka nchini kwetu. Kuna masuala ya vyakula. Ni kweli Serikali yetu kupitia Bunge iliweza kuzuia vile vyakula ambavyo vinatokana na mchanganyiko wa madawa. Ni haki vile vyakula vizuiliwe kwa sababu vimeua hadhi ya vyakula vyetu vya kitamaduni. Ninakumbuka nyanya yangu alifariki akiwa na umri wa miaka 126. Alikuwa anaona na kula nyama na mahindi kwa sababu alikuwa na meno yote. Mtoto wa miaka 35 leo hata meno yameisha mdomoni kwa sababu ya vyakula ambavyo tunakula. Vyakula vyote viko ndani ya mkebe na vina madawa ambayo hatuyaelewi yametokana na nini. Hii ni hatari kubwa kwa afya zetu. Ninaunga mkono Mswada huu kwa maana utalinda hali ya mazingira utamaduni na mimea yetu. Mswada huu utatusaidia kufanya utafiti kwa maana vyuo vyetu vinatumia rasilimali iliyo katika nchi yetu kukuza taaluma katika kitengo cha kilimo na kulinda mazingira. Ninafurahi na kushukuru kwa sababu tumepata Mswada huu ambao utaweza kuokoa nchi yetu. Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia Mswada huu.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Mwanzo kabisa naunga mkono Hoja hii. Sura ya nchi ni lishe bora mazingira bora na matibabu bora. Vilevile kabla sijasahau ni vyema Bunge hili lifikirie sana sheria za nidhamu kwa sababu kuchanganya lugha ya Kiswahili na Kiingereza iko kila mahali. Ndio maana Bunge la Tanzania limechangamka kuliko hili letu kwa sababu Wabunge wengi hawawezi kuongea Kiingereza moja kwa moja na pia hawawezi kuongea Kiswahili moja kwa moja. Hiyo ni changamoto. Kando na changamoto za lishe bora na mazingira bora matibabu nchini yamekuwa kizaazaa kikubwa mno. Sasa hivi Wabunge wengi wanatumia mishahara yao kulipia madawa hospitalini ama kuchangia mazishi. Limekuwa suala nyeti sana hapa nchini. Utapata Jumamosi moja mnazika watu zaidi ya kumi hata mtu anakuwa na wasiwasi ilhali sote ni mali ya Serikali. Kuna Muingereza mmoja ambaye alikuwa anaitwa Maslow aliyeandika kuhusu mahitaji ya binadamu. Aliorodhesha mahitaji madogo madogo hadi mahitaji makubwa makubwa. Matibabu ni katika mahitaji madogo madogo kama vile lishe lakini hapa nchini ninashangaa kwa sababu kodi tunazotoa kwa mwaka zinafikia zaidi ya Sh1000 bilioni tena zaidi ya mara tatu. Ni kwa sababu hakuna mpangilio sawasawa. Kungekuwa na mpangilio sawasawa na ufujaji usiwepo Serikali ingekuwa inaweza kutibu watu wake bila hata kuomba hela za madawa au za matibabu na hata kama unahifadhi mwili mtu anapofariki. Sisi tumelegea katika upande huo. Hela inayohitajika kutibu Wakenya wote haiwezi kuzidi Sh500 bilioni. Haya ni mahitaji ya kila mwananchi. Sasa hivi ukiangalia hospitali zote nchini sio za rufaa tu bali hata zile za umma kule mashinani taabu ni hizo hizo. Kwangu nyumbani niko karibu na zahanati nyingine hapo. Ni kizaazaa. Hamna hata kutulia. Hili ni suala ambalo watu wanafaa kulichukulia kwa undani na walifikirie sawasawa. Nampa Mbunge wa Nyali pongezi kwa kuleta Hoja hii. Ubaya wetu tunatoa Hoja tamu tamu kama hizi lakini kesho kutwa utakuta imepotea. Hakuna mtu ataongezea. Kamati tekelezi haifuatilii. Inakuwa tu tabia ya kuongea masuala mazuri kama haya. Nchi nyingine wanaiga na wanatelekeleza na sisi bado tuko pale pale. Wakenya wanaumia. Ukiwauliza Wabunge wengi hapa hata sasa hivi kuna mmoja hapa alikuwa ananiitisha hela aende tu hapa kwa sababu hana chochote. Najua ni kwa sababu ya masuala kama haya. Kamati ya Bajeti iketi chini na ifikirie suala hili kwa kina na sio kuongea tu na kupata bonga points katika Bunge hili na katika runinga halafu tunaachilia suala hili hivi. Nampongeza sana Mbunge wa Nyali maana ni mbunifu. Ameleta Hoja ambayo inaweza kuwasaidia Wakenya hasa wale ambao hawajiwezi. Singependa kuongea mengi. Shukrani kwa kunipa fursa hii. Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii kuafiki Ripoti hii ya Kamati ya uwezo na kivuli kinachowawezesha Wabunge kuongea na kutekeleza shughuli zao bila kuwekewa vikwazo na sheria. Vilevile tukielewa kwamba sheria zote ambazo tumepewa zina ukingo au limitations sheria inatupatia nafasi kuwa sisi twaweza kusema lolote ambalo twataka kusema lakini sheria hiyo hiyo vilevile imetuwekea ukingo ambao hatuwezi kuvuka. Kwa sauti hiyo tumekuwa na kazi ngumu katika kuangalia suala hili ambapo tulifadhaishwa sana na ripoti ambazo zilikuwa zinaonyeshwa katika magazeti kwamba Wabunge wanachukua hongo Bunge limeoza na masuala kama haya. Hapo ndipo tukasema kulinganisha na uwezo ambao tumepewa kama Kamati tufanye uchunguzi. Katika uchunguzi tuliona kwamba kwasababu ripoti hii ilikuwa inaonyeshwa moja kwa moja katika vyombo vya habari mashahidi wengine pengine waliona kuna hatari na wakija pale katika Kamati wakasema: "Sisi hatukuona na hatukusikia." Sasa kama mtu ashasema hakuona wala hakusikia hakuna mahali ambapo tungeweza kusonga mbele. Vile vile katika Ripoti hii tumeona kwamba iko haja ya Bunge hili lijichukue kama Bunge la kitaifa. Ripoti ambayo inakuja hapa iangaliwe kwa mujibu wakitaifa na tusione kwamba ni Wabunge wa magharibi peke yao ndio wanafaa kuchangia mambo ya sukari na wengine wawe wanapinga. Jambo la haki liwe la haki. Katika Ripoti hii tumeona kwamba kumekuwa na bidii na juhudi za kuwa Hoja hii iangushwe kwa sababu kulikuwa na mawaziri ambao walikuwa lazima wakingwe wasije wakaumia. Nafikiri huu si mwendo ambao Bunge hili lafaa kuchukua. Ikiwa twataka kukomesha ufisadi kila mtu ambaye atakuwa ametajwa apewe nafasi aweze kuulizwa na yeye mwenyewe aweze kujisafisha. Hivyo tungeweza kukomesha mambo ya ufisadi katika nchi yetu. Hata jana katika Bunge la Seneti walikuwa wakijadili mambo ya Ruaraka tuliona bado kuna watu walikuwa wanakingwa katika Ripoti hiyo. Nafikiria mwendo huu ukiendelea itakuwa sisi kama Bunge hatutekelezi kazi yetu sawa sawa. Mwisho napenda kuangazia maombi yetu katika Bunge hili. Kabla hatujaanza kikao chetu huwa tunasema: "Ewe Mwenyezi Mungu ambaye kwa hekima na wema wako umeteua nyadhifa za viongozi na mabunge kwa ustawi wa jamii na utawala wa haki wa wanadamu: twakusi hi ututazame kwa neema nyingi sisi watumishi wako ambao umeridhika kutuita ili tutekeleze shughuli muhimu za Jamhuri hii yetu." Mhe. Naibu Spika wa Muda hili ni moja katika mambo ambayo twatakiwa tuyazingatie. Mwisho kabisa ombi hilo linasema:"Twakuomba ututeremshie Baraka zako sisi tuliokutanika hapa." Kisha inamalizia ikisema: ".ufanisi na heri ya nchi hii yetu na wale ambao haja zao umezikabidhi mikononi mwetu." Ikiwa wananchi wametukabidhi sisi majukumu yakuangalia maslahi yao na mambo yao yaende sawa sawa itakuwa hatutekelezi kazi zetu ikiwa tutaenda kinyume chao.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ya kuongea kuhusu jambo ambalo ni janga la Wakenya wanaoishi karibu na mbuga za wanyama pori. Malalamishi ambayo yamewakilishwa na Mhe. Sara yanawaathiri watu wengi. Wale ambao mipaka yao imeshikana na mbuga za wanyamapori wanaumia haswa katika Eneo Bunge la Mwatate. Baada ya Standard Gauge Railway (SGR) kutengenezwa wanyama wengi kutoka Tanzania hupitia mbuga ya Tsavo West wakitaka kwenda Tsavo East. Wanyama hawa wanazuiwa kupita Tsavo East na wote wanarejea upande wa Mwatate. Kwa sasa jambo hili limekuwa janga kwani chakula cha wananchi kimemalizwa na wanyama hawa. Yale maji tuliyonayo kidogo yamekuwa tatizo. Juzi nimekuwa na wazo kwamba tukichimba mtaro mkubwa kabisa katika mpaka wa Tsavo labda ndovu hawa watatumbukia humo ndani ya mtaro wakati wanajaribu kuvuka na waache kuwasumbua wananchi. Tumelia kwa muda mrefu. Waziri alikuja kule na bado hatujaona chochote ambacho kinaweza kutusaidia. Ninaomba Wizara husika iingilie kati kwani wananchi wanaumia. Ninashukuru sana kwa fursa hii mbayo umenipatia. Malalamishi ya Mhe. Sara yaangaliwe kwa undani maana ni janga la Kenya nzima.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa ili nichangie suala la nzige. Kweli mvua ilinyesha na kawaida mvua ni baraka. Tunajua kama Wakenya tumepitia kipindi kigumu awali cha ukame ambapo ilibidi watu wetu waishi kwa kutegemea chakula cha msaada. Basi wakati mvua ilinyesha watu walijitupa mashambani wakalima kwa bidii. Inaleta wasiwasi sana wakati tunasikia kwamba mazao ambayo tulikua tunatarajia yatavamiwa yataliwa na nzige. Wengine wetu hapa tunatoka sehemu ambayo mvua hiyo ambayo ni baraka iliwadhuru watu kwa sababu kulikuwa na mafuriko na mimea mingi tuliokua tunatarajia ilisombwa. Nikisimama hapa nzige hawajafika Kaunti yangu ya Taita Taveta lakini sipati usingizi kwa sababu tunatarajia chakula kutoka wenzetu ambao wamevamiwa na nzige. Ndiposa tunasema kwamba jambo hili lichukuliwe kwa dharura kubwa sana. Inatakikana suluhu mwafaka ipatikane kusuluhisha jambo hili la nzige. Naunga wenzangu mkono ambao wameongea awali. Huu ni wakati suala la nzige litangazwe kuwa janga la kitaifa nchini Kenya kwa sababu kupitia mifano nimetoa awali vile watu wamekua wakikosa chakula na vile mvua ilinyesha na hakuna suluhu mwafaka basi ni vizuri kama nchi tuseme kwamba ni janga la kitaifa ili idara husika ziweke vichwa pamoja ili tuweze kupata suluhu thabiti la kutusaidia kupambana na janga hili. Asante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili nichangie. Nampongeza mwenzangu ambaye ameleta Hoja hii ili tuijadili.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia hii nafasi. Nitachukua muda mfupi. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu unapatia wanawake wa hii nchi nafasi ya kujumuika na viongozi wengine katika kufanya maamuzi ya maendeleo ya nchi hii. Tunakumbuka Rais Obama wa Marekani alipokuja nchini alitoa hotuba nzuri sana wa kuunga sheria kama hii mkono. Alitukumbusha kuwa tukiacha wanawake nyuma ni kama timu ya mpira inayochezesha wachezaji nusu. Kutengeneza sheria ili wanawake waongezeke hapa Bungeni ni kitu ambacho kitatufanya sisi kama nchi tusonge mbele kwa pamoja. Kitu kingine utaona katika dini mila zetu na eno ya wahenga kuna eno ya kuonyesha kuwa wanawake ni kiungo muhimu katika jamii. Kwa mfano katika Dini ya Kiislamu Mtume Mohammed (Rehema na ai ziwe juu yake) alisema kuwa mama ni madrasa ama shule. Kwa hivyo ukimpatia mwamake nafasi ya kuongeza elimu na kuchangia katika uongozi basi ile familia itaimarika na jamii kwa ujumla itanawiri. Pamoja na hiyo kuna msemo wa Kiingereza unaosema kuwa ukielimisha mwamke mmoja ni kama umeelimisha jamii nzima. Hii inaonyesha umuhimu wa wanawake katika uongozi. Tukiwaacha nyuma tunaacha Kenya nyuma na tutashindwa na nchi zingine. Kitu kizuri kwa huu Mswada ni kusema kuwa wakati wowote kusiwe na zaidi ya theluthi mbili ya jinsia moja katika Bunge la Kitaifa au Seneti. Hii inahakikisha kuwa hakutakuwa wakati ambapo kuna wanaume au wanawake watupu Bungeni kama ilivyokuwa siku zilizopita katika nchi hii. Kitu ambacho nafurahia pia ni kuwa si wanawake tu wamepewa nafasi; ni kwa sababu hivi sasa walioachwa nyuma ni wanawake na sio wanaume. Haitupi tu nafasi ya kuteuliwa kama wanawake watakaochaguliwa lakini pia imetuwekea kiwango cha miaka 20 kutoka sasa. Tunapewa miaka 20 wanawake wateuliwe na kupata uzoefu wa uongozi wa Bunge ili baada ya hapo wafuatilize vile viti vingine vya kuchaguliwa. Kuna mifano michache tu ya haraka ya uzuri wa wanawake kuja Bungeni. Kuna sheria za kuzuia watu kudhulumiwa kimapenzi ambazo zimeletwa hapa na Mbunge wa kitambo ambaye sasa ni Jaji wa Mahaka ya Juu ya Kenya. Kuna sheria zinazopinga vita vya yumbani pia zilipitishwa kwa sababu ya msukumo wa wanawake. Kuna sheria zingine ambazo kwa mfano zimeondoa ushuru kwenye visodo ambavyo wanawake hutumia wakiwa kwenye hada zao za mwezi. Hizo sheria zimepitishwa kwa sababu ya kuwa na wanawake Bungeni. Si masuala hayo peke yake. Ni muhimu kupata maoni ya wanawake katika sheria za nchi hii ili tusonge mbele. Hii ni kwa sababu idadi ya wanaume kwa wanawake ni asilimia sawa. Nawaomba Wabunge wenzangu wahakikishe kuwa vijana wa kike wako katika orodha ya watakaoteuliwa. Isiwe ni wanawake watu wazima pekee ambao watateuliwa. Kwa hayo machache shukrani Naibu Spika wa Muda.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Mheshimiwa usitie wasiwasi. Utapata nafasi maana Kwale na pahali unakotoka ni tofauti. Tena wewe ni mwanaume na mimi ni mwanamke. Kwa hivyo tuko tofauti. Hoja hii imekuja wakati unaofaa lakini kwa wakati ambapo tupo katika mashaka makubwa kumaanisha ingefaa ije mapema zaidi ya hivi. Pia ninampongeza Mhe. Mwadime kwa sababu maji ni uhai. Wakati tunazungumzia maji yaenezwe katika shule zetu pasiwe kwamba ni shule chache. Haya maji yanahitajika sana haswa tukiangalia hali iliyo katika shule zetu na nikizungumzia sehemu za kwetu. Katika sehemu za Kinangop Matuga na Lunga Lunga kuna maeneo yenye ukame kwa sababu mvua haijanyesha mwaka huu. Watu wetu wako katika hali ngumu wakati huu. Watoto ndio wanaoathirika sana. Kwanza asubuhi akiamka mzazi wake hana hata maji ya kumtengenezea kiamsha kinywa wakati anaenda shuleni ambapo anafika akiwa hana maji ya kunywa. Ukiangalia mtoto wa kike ambaye wakati wa hedhi unapofika utakuta kwamba anahitaji maji ya kutumia kwa usafi. Kwa vile hakuna maji yule mtoto haendi shuleni. Kusema kweli sisi kama Bunge tunastahili kuwa na msukumo kuhakikisha maji yamepatikana bila kusema kwamba haya ni majukumu ya serikali ya kaunti. Maji ni uhai na uhai huu hauko kwa kaunti peke yake bali ni kwa nchi nzima. Ni wajibu wetu kama Bunge tuangalie katika makadirio ya ziada tuweke pesa hapo ili wananchi waweze kupatiwa maji katika shule zetu zote. Kwa mfano tuna huu mradi wa NYS mashinani na nikiwa hapa ninaipongeza Serikali kwa huu mradi. Huu ni mradi ambao ungeweza kuokoa pesa kwa sababu vijana watakuwa wakisimamiwa na kufanya mambo tofauti ya ujenzi wa taifa katika maeneo tofauti. Ikiwa hizi pesa zitaekezwa katika NYS zitatumiwa katika uchimbaji wa mabwawa visima na mitaro ya kuweka maji karibu na shule zetu. Tukitumia vijana wa NYS tunaweza kurekebisha paa za shule na kuweka mipangilio ambayo itaweza kukusanya maji kwa kutumia matangi. Katika maeneo yangu shule zote hazijatenga maji ya kusaidia watoto wakati wako shuleni pamoja na walimu wao. Hii pia inachangia zaidi ukosefu wa utulivu wa watoto katika masomo.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ili niweze kuichangia Hoja hii yenye nia ya kuleta usafi kwenya mazingira yetu. Ninaiunga mkono Hoja hii. Kwanza nampongeza sana Mhe. Ottichilo kwa sababu ni mwanamazingira ambaye huzungumza kuhusu mazingira na anataka kuona vitendo ambavyo vitarekebisha hali ilivyo katika nchi yetu. Hoja hii isiwe tu ndani ya Bunge la kitaifa bali iwe ni sheria mwafaka ambayo itaweza kuiokoa nchi hii. Kabla ya kupitisha Katiba ya Kenya 2010 tulikuwa na serikali za mitaa. Wakati huo mazingira yalikuwa na nafuu na usafi. Tunazipatia serikali za kaunti pesa nyingi kupitia kwa magavana lakini yasikitisha kwamba kila unapopita wasikia harufu ya uvundo na waona takataka.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Hawa tunawaelewa. Ni wale ambao wanawapiga akinamama magongo. Kwa hivyo hajali afya ya mama. Ninamshukuru sana Mhe. Ottichilo kwa kuileta Hoja hii. Ni lazima tusimame na afya na mazingira yetu sio kwa kuzungumzia tu bali kwa vitendo pia. Tuitenge siku ambayo itakuwa maalum kwetu sisi sote kwa maana mazingira si jukumu la sehemu moja ama la watu fulani bali ni jukumu letu sisi sote. Katika utamaduni wa Kiafrika mama ndiye anayelinda mazingira kuanzia mzee ndani ya nyumba akioga. Mama ndiye anayehakikisha usafi wa mzee akivaa. Kuna pesa ambazo zimepangiwa kupelekwa kwenye serikali za kaunti kutekeleza majukumu ya usafi wa mazingira na wameshindwa. Ni jukumu letu kama Bunge la kitaifa kuona kwamba pesa hizo zimepatiwa akinamama wawakilishi wa maeneo Bunge. Usafi utaweza kuonekana katika kaunti zetu na kila mahali mtakapopita mtafurahia mazingira mazuri. Kwa mfano mazingira ambayo hayana takataka upandaji wa miti na urembo kama vile kupanda maua katika bustani zetu. Hilo ni jukumu ambalo likiachiwa akinamama mtashangaa vile ambavyo Kenya hii itabadilika. Ninampongeza Rais wetu. Hivi juzi nilikuwa kwenye msafara wake kwenda Ujerui. Alikaa na wafanyibiashara na wawekezaji ambao wengi wao walikuwa wamelenga kuja Kenya kuhifadhi mazingira kupitia shughuli za kuzoa na kubadilisha takataka ziwe mbolea na umeme. Rais amelitilia jambo hilo maanani. Ni kwa nini sisi kama Bunge tusimuunge mkono Rais wetu na tuweke sheria dhidi ya ukiukaji wa sera ya kulinda mazingira ili watu hao wachukuliwe hatua mwafaka? Hiyo itakuwa hukumu ambayo itaweza kuwafunza watu wetu kulinda mazingira. Nilitembelea nchi ya Zimbabwe. Usishangae kwa sababu ukipakuliwa chakula katika barabara za Zimbabwe utakula na hakuna madhara utapata maana kuna usafi wa hali ya juu. Kwa nini Kenya isiwe kama Zimbabwe? Wale ni Wafrika kama sisi. Kwa nini tusiweze kulinda mazingira yetu? Tulipokuwa tukisoma kila siku ya Ijumaa ilikuwa ni siku ya mazingira katika shule. Hayo mambo yote yametupiliwa mbali. Tujiulizeni ni kitu gani tumekosea ili tuweze kurekebisha na kuyalinda mazingira yetu. Mhe. Naibu Spika wa Muda ingia mlango wetu wa Kenya. Nikizungumza hivyo ninamaanisha wakati unapotoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Moi na kuingia Mombasa. Utakutana na uvundo. Kuna maradhi ambayo hizi sasa yameikumba kaunti ya Mombasa. Hii ni kwa sababu hakuna mtu anayeyajali mazingira bali watu wanajali mifuko yao. Twende katika Kaunti ya kwale. Hapo awali kulikuwa kusafi sana. Hivi sasa kila mahali kuna makaratasi na kinyesi. Wakati umefika Bunge la Taifa lisimame kindete kuokoa mazingira afya na nchi yetu kwa jumla bila kujali ni nani; tusimame kwa umoja tuamue. Mhe. Ottichilo tunaunga mkono siku ya Alhamisi itengwe kulinda mazingira. Sisi sote tuingie kiwanjani na mitaani tusafishe mji wetu. Pia tuwape nafasi wawekezaji ambao wako tayari kushirikiana na Wakenya kubadilisha zile taka zote ziwe ni vitu vya ufaa. Tukifanya hivyo tutaleta ajira kwa vijana wetu ambao wanalia hawana kazi. Tukitoa hiyo nafasi bila kuweka vikwazo vingi na kuleta ufisadi tutaweza kuyaokoa mazingira yetu. Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Pongezi kwa Mhe. Ottichilo.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza nataka kukupongeza kwa kazi nzito ambayo umeipata. Naamini unaiweza. Mhe. Spika Naibu wa Muda Hoja hii ni muhimu sana kwa sababu hakuna kitu kinachoweza kufanyika katika kijiji au shuleni bila maji kuwepo. Badala ya umeme kupewa kipaumbele ingefaa maji yapewe umuhimu zaidi kwa sababu maji ni uhai. Hivi sasa watoto wetu katika shule nyingi wanafaidika na mpango wa chakula cha mchana. Ni lazima chakula hicho kipikwe kutumia maji. Watoto wetu wanapitia hali taabani wakitembea mwendo wa kilomita 10 wakitafuta maji. Licha ya masaibu yanayowakumba wanafunzi shuleni kuwepo kwa maji vijijini pia ni muhimu. Watu wengi wanapata magonjwa kwa sababu wanachimba mashimo ili maji yatoke. Wengi wao hunywa maji mitoni - mito ambamo mbuzi na wanyama wengine wameenda haja zao ndani. Hali hiyo huwafanya wananchi kuwa wagonjwa. Ningependa kukuhakikishia kwamba kule nitokako Matuga nyumba zimevunjika kwa sababu ya ukosefu wa maji. Mnajua utamu wa bwana na bibi kitandani ni masaa ya kuanzia saa kumi hadi saa kumi na mbili asubuhi. Wakati huo unapata bibi akiruka kutoka kitandani na akiulizwa anasema anaenda kutafuta maji. Bibi anarauka kwenda kutafuta maji wakati bwana anahitaji kukumbatiwa. Mhe. Naibu Spika wa Muda tungependa kuondoa hali hii kwa sababu miji imebomoka.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza ninampongeza Daktari Susan kwa Hoja hii ambayo ameileta kwa wakati unaofaa. Tukiangalia hali ilivyo nyanjani panapotokea ajali tunakuta ni hali ya kusikitisha sana. Tutafaidika tutakapowapatia vijana wetu elimu maalum inayosimamia mambo ya ajali. Kwa mfano pale kwangu Kwale kulitokea ajali ambapo mama mmoja ambaye alikuwa ameumia uti wa mgongo Kwa vile watu hawakuwa na ujuzi wa kuokoa majeruhi huyo mama mwishowe alipoteza maisha yake. Kwa hivyo hii isiwe tu katika hali ya kuelimisha watu peke yake. Inatakikana tuwe na magari na vifaa vya kuende unyo kwa unyo panapotokea ajali. Pia inafaa tuwe na watu wanaojua kuvitumia vifaa hivyo. Tunatoa heko kwa Mama Margaret Kenyatta. Ametuletea zile kiliniki za rununu au mobile clinics ambazo zina kila kitu ndani. Lakini hakuna watu ambao wanaujuzi wa kuvitumia. Kwa hivyo hayo magari pia yamesimama. Wakati tutaweza kuleta hii elimu na zile ambalanzi tulizo nazo ziweze kuwekwa vifaa maalum mle ndani tutaweza kuwahudumia wagonjwa kabla hawajafika katika hospitali. Ninamshukuru Mhe. Dkt. Susana Musyoka kwa kuileta Hoja hii. Asante.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Mhe. Khamisi bado ni mgeni kwenye Bunge hili. Kwa hivyo tunaweza kuelewa kidogo. Nilikuwa nazungumzia swala la utafiti. Serikali inatumia kiwango kubwa zaidi cha fedha kufanya utafiti katika sekta ya ukulima kwa mfano kupitia mashirika kama vile KARI na mengineo. Lakini hatujaona utafiti wowote ukifanyika ama matunda ya utafiti wowote katika sekta hii ya uvuvi. Mhe. Odhiambo-Mabona ametaja hatua ya kipindi ambacho wavuvi huzuiwa kufanya biashara yao - closed season. Kipindi hicho kifikapo wavuvi wote wanazuiwa kufika katika maeneo ya uvuvi. Kwa muda huo wote inamaanisha kwamba wavuvi wote hawako kwenye kazi yoyote. Kumbuka wavuvi hao wanategemea uvuvi kama chakula chao na kuwaelimisha watoto wao. Katika hali zote za maisha yao wao hutegemea uvuvi huo na kwa hivyo ukiwafungia kazi yao kwa muda wa miezi minne Ikiwa sisi Wabunge tutaambiwa hatutafanya kazi hapa kwa muda wa mieze minne na hakutakuwa na malipo yoyote; hakuna mshahara na hakuna marupurupu kwa muda ambao tunaketi kwenye Bunge hili ama kwa Kamati naamini hakuna Mbunge yeyote atakubali hatua kama hiyo. Sasa wewe tafakari ujiulize: Mvuvi kwenye kijiji cha Mbita Budalangi ama Turkana afungiwe njia yake ya pekee ya kujimudu kwa muda wa miezi minne mfululizo atafanya nini? Jiulize: Mvuvi huyo atajimudu namna gani? Tafakari hayo kwenye Bunge hili la kifahari. Huyo mvuvi atajimudu namna gani? Na wakati wa kipindi hicho cha kufunga uvuvi ni muda ambao huwa ni mgumu sana kwa wavuvi na familia zao.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuchangia Mswada huu ambao ni wa maana sana. Ninalo ombi kwa Waheshimiwa Wabunge kwamba tusikimbie tu kuupitisha Mswada huu bila kurudi nyuma kuufanyia ukarabati kidogo. Kweli tunatetea haki ipatikane upande wetu sisi wanawake lakini ifahamike kwamba hata sisi wanawake tunachangia hizi shida zingine. Ukiangalia mavazi ambayo tunavaa yatamfanya huyo mwanamme agutuke nafsi yake. Je atakuwa amekosea huyo au la? We are provoking proble Kwa hivyo katika hii sheria tuende nayo kwa utaratibu tuweze kurekebisha mpaka katika Katiba. Kwa sababu wakati tunasema mtu anaruhusiwa kuvaa anavyotaka lakini mtu avae nusu uchi uwe unategemea nini? Uwe unategemea ufuatwe kwa macho na kwa vitendo. Kwa hiyvo Mswada huu ni wa maana sana na utaweza kulinda haki zetu pande zote mbili; wanawake na wanaume. Ningependa kusema kuwa hicho kipengele kinachosema kwamba watu wanaweza kujadiliana ili kesi iondolewe ningeomba wakati mwafaka ukifika tukiondoe. Wanaopatikana na hatia wanafaa kuadhibiwa hata kwa adhabu ya kifo kwa sababu watakuwa wamemharibia mtoto maisha yake awe ni wa kike au wa kiume. Shukrani.
Shukrani mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono kwamba CDF ibaki. Ningetaka nikichangia hii Hoja nianze kwa kuwauliza waheshimiwa Wabunge wenzangu maswali. Swali la kwanza je wanaotengeneza sheria ni akina nani? Wanaotengeneza sheria za Kenya ni sisi hapa na sisi ndio tulitengeneza sheria ya CDF na hivyo basi CDF lazima ibaki. Kwa hali na mali CDF ibaki. Hii ni kwa sababu magavana hivi sasa wanazunguka; unasikia wameenda kufungua miradi. Wangefungua nini kama ingekuwa si CDF? CDF imetuwekea mashule. CDF imetuwekea zahanati. CDF imetuwekea wadi za akina mama ambazo magavana wanaenda kufungua. Ingekuwa si CDF wangefungua nini? Hii ni kwa sababu katika hiyo miaka yao mitatu ambayo tumewamiminia pesa chungu nzima hakuna cha kutuonyesha. Pesa zao za bursary pia hatuelewi ziko wapi pesa za bursary ambazo zinatoka CDF wazazi wanazifurahia. Ninaomba CDF ibaki na tuiongeze zaidi na zaidi. Tusiongeze tu CDF bali pia na mfuko ambao tunauita "Social Fund" ambao utasimamiwa na wawakilishi wa wanawake. Zile pesa za magavana zikatwe na ziongezwe kwa hii Social Fund; tufanye kazi pamoja tuinue Kenya yetu. Kuna watu tunaweza kuwaita mabepari ambao bado wanataka kutuwekea ukoloni Kenya na ni hao wanaoitwa World Bank. Wameona kwamba hatutaenda tena kukopa pesa kwa sababu CDF na Social Fund zinashikilia ile nafasi ambayo wao walikuwa wakishikilia. Hatutaki tena madeni. Sisi wenyewe tunaweza kujisimamia na tunajisimamia kupitia Social Fund na CDF. Wabunge wenzangu katika bajeti ya mwaka huu ikiwa hakuna CDF na Social Fund there will be no Budget . Kwanza tupitishe yetu halafu tuangalie hayo mengine. Kwa hayo mengi .
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Mswada huu kuhusu kubadilisha tarehe ya uchaguzi. Bunge hili linatunga sheria na ni lazima tufahamu kwamba sheria inakata mbele na nyuma kama msumeno. Kwa hivyo haiwezekani tuliunda sheria ambayo inasema kwamba MCAs na kila anayechaguliwa awe ni Mbunge Seneta au Rais atatumikia kipindi cha miaka mitano na leo tunataka kuibadilisha. Kwa nini leo iwe hao watu watatu watapunguziwa muda wao na MCAs waachiwe muda wao? Mswada huu unatuletea uwiano ili tuweze kuweka hali ya uchaguzi iwe sawa kwa kila mtu. Pili ikiwa tutakuwa na uchaguzi katika mwezi wa nane kwanza tutakuwa tumeadhiri elimu ya watoto wetu. Mwezi wa nane ni wakati ambapo watoto wetu katika Darasa la Nane wanajitayarisha kwa mtihani wa mwigo. Wale ambao wako katika Kidato cha Nne pia wako katika hali ya matayarisho ya mtihani wa mwisho. Ikiwa uchaguzi utafanyika Agosti tutayaharibu maisha ya watoto wetu ambao ni viongozi wetu wa baadaye. Tutaingilia mambo ya masomo yao. Uchaguzi ukifanywa sio mwisho wa siasa. Baada ya uchaguzi inachukua karibu miezi mitatu kwa nchi kuwa na utulivu wa hali ya kawaida. Kwa hivyo ni vizuri uchaguzi ufanyike katika mwezi wa kumi ma mbili. Kwa mfano kwetu pwani kuna wengi ambao walichukua kura zao katika sehemu za bara kwa sababu bara ndiyo kwao. Decemba huwa wamejipanga kurudi kwao ili wapige kura. Huo ndio wakati ambao wanaweza kupata ruhusa ya kurudi katika maeneo yao na waweze kupigiwa au kupiga kura. Kwa hivyo naunga mkono pendekezo kwamba uchaguzi ufanywa mwezi wa Desemba. Hii haimaanishi kwamba Wabunge watakuwa wameongezewa mshahara. Kusema ukweli tulichaguliwa na sheria inayosema tutatumika kwa miaka mitano. Kwa hivyo tukitumika mpaka mwezi wa nane inamaanisha hata haki yetu itakuwa imekiukwa. Je kwani hiyo haki ni ya wale wako kule nje na siyo sisi katika Bunge hili? Kwa hivyo tunataka kuleta uwiano kupitia huu Mswada wa Mhe. Ochieng. Namuunga mkono na kumpongeza. Ameleta Mswada ambao utaleta uwiano kwa kila mtu. Mwisho inatakikana ifahamike kwa wananchi vizuri. Kuna wenzetu huko nje ambao hupata vipesa vyao sijui kutoka wapi na kazi yao ni kuwadanganya wananchi kwamba Wabunge wanataka kujiongezea muda. Tafadhali wale wanaowafadhili watu hao waangalie vile wanavyowafadhili wasiwe wakawa ni wale ambao wanaoleta uchochezi katika nchi hii na kuifanya isiwe na utulivu. Tunahitaji utulivu ili utalii wetu ufufuke biashara zetu ziendelee na hili Bunge liwe na wakati wa kutosha kutengeneza makadirio ya matumizi ya nchi hii. Ikiwa uchaguzi utafanyika katika Agosti hatutakuwa na muda wa kutengeneza mipangilio na makadirio ya matumizi ya nchi hii. Hii inamaanisha kuwa tutakuwa tumeufungua mlango kwa wale mapapa ambao wanataka kula pesa za Mkenya wapate nafasi ya kufanya hivyo. Hali hiyo italeta janga kubwa katika uchumi wa Kenya. Naunga mkono Mswada huu na kusema kwamba uchaguzi ufanywe katika mwezi wa 12.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Mswada huu na kumpongeza Mhe. Wamalwa kwa sababu umekuja kwa wakati unaofaa tukiwa tumebaki na muda mfupi kwenda kutafuta kura tena. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu hali ilivyo sasa katika kila chama - na nitazungumzia upande wa chama changu ili nisizungumzie wengine - kila mwezi mshahara wetu unakatwa. Zile ofisi ambazo zimewekwa mashinani inambidi Mhe. Mwanyoha atoe pesa mfukoni mwake ili azilipie. Unashangaa hizo pesa ziko wapi. Hata kabla pesa hizo kuzungumziwa zaidi ningetaka Mkaguzi Mkuu wa Fedha ajitokeze waziwazi kukagua matumizi ya pesa hizo kwa sababu hatuelewi. Hakuna wakati ambapo tumeelezwa kuhusu matumizi ya pesa hizo kinagaubaga ili tujue zinatumika kwa njia gani. Kwa sababu hiyo hivi vyama vingine vimeshikiliwa kama vyombo binafsi. Vina ubaguzi na ukabila. Wengine wakizungumza na upande wa pili ni haleluya! Lakini wengine kutoka eneo fulani wakionekana wanashirikiana na upande wa pili hao ni wasaliti na wanafaa kuadhibiwa. Kwa hivyo huu Mswada utatusafishia hali ilivyo katika vyama vya kisiasa kwa wakati huu. Pia itatupatia nafasi tuzidi kuongeza vyama. Vyama vikiongezeka humu nchini demokrasia itaeleweka. Kila mtu atatetea kile chama ambacho anakiona kina msimamo wa kuelekeza mapenzi na uwiano katika jamii zote. Vyama vingi tulivyonavyo leo tukiwa nje vinazungumzia uwiano wa jamii. Lakini vikikaa peke yao vinasema: "Ni sisi kama kabila ama nyumba hii." Hatuwezi kukubaliana na kauli hiyo kwa sababu haielekezi Kenya katika mwelekeo ambao unafaa. Inaelekeza Kenya katika hali ambayo inaleta utata katika jamii. Hizo pesa zikichunguzwa zaidi tutapata ukweli. Ndiyo mwananchi mlipa ushuru aelewe ni kwa nini vyama vinapewa pesa. Lakini kwa sasa wananchi ambao pesa zao zinapewa vyama vya kisiasa hawajui zinafanya kazi gani. Hakuna siku utakuta chama kimemwita yule mwananchi kumweleza: "Pesa yako ikikatwa huwa inafanyiwa kazi hii na hii katika chama." Kwa hivyo naunga mkono Mswada huu. Mhe. Wamalwa ahsante sana.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Natoa sauti yangu kuchangia Hoja iliyo mbele yetu. Ni wazi na imedhihirika kwamba hili baa la njaa limekumba maeneo mengi Kenya nzima. Natoka Laikipia na hali ni hiyo hiyo ya dukuduku na kumekuwa na tahadhari ya binadamu kupoteza maisha na mifugo yao kupitia baa la njaa ambalo limeenea. Yafaa ieleweke kwamba tulipopitisha Katiba na kupigia kura ugatuzi ilikuwa kwa sababu wananchi wapate huduma za karibu. Inasikitisha kwamba huduma ya karibu ambayo wananchi wa majimbo mengi wameweza kupata ni kule kuona magari ya kifahari na makubwa makubwa ambayo mara mingi hupita na kuwachia vumbi wasijue wanakotoka ama wanapokwenda. Laikipia inajulikana kwa umaarufu wake wa kufuga mifugo wa hali ya juu haswa ng'ombe wa nyama. Pia tumejulikana kwa kuhifadhi nyasi na eno yetu mengine. Imekuwa ni kitu cha kusikitisha kwamba sisi tumehifadhi nyasi zetu kupitia conservancies ili tupeleke mifugo wetu pale wakati wa njaa. Lakini hali kule imekuwa ni mwenye nguvu mpishe. Kumekuwa na tatizo kubwa ambapo jirani wetu kutoka anakotoka magu hapa na wengine kutoka Isiolo ni kutumia nguvu kutupokonya zile rasilimali tumeweza kutunza. Mhe. Naibu Spika wa Muda nalilia Wizara ya Usalama ilinde usalama wa watu wa Laikipia. Hii ni kwa sababu kumekuwa na mzozo mkubwa sana wa wafugaji kung'ang'ania rasilimali. Nataka ieleweke kwamba iwapo hautatunza rasilimali zako hizo rasilimali hazitakutunza. Kwa hivyo ni kitu cha kusikitisha sana kwamba ninapozungumza katika Bunge hili leo wawili wa watu kutoka eneo Bunge langu wanazikwa leo hii kwa sababu ya kupigwa risasi na wafugaji wanaotoka kaunti jirani kwa sababu ya kule kutaka kulisha mifugo wao kwa lazima katika maeneno ambayo sisi wenyewe tumehifadhi. Tunapoendelea ni kwamba kaunti jirani pia waketi chini na kujaribu vile watatatua tatizo hili la baa la njaa. Pia naomba na kusema kwa unyenyekevu kwamba Serikali kuu iangazie maeneo kama Samburu Laikipia Isiolo na yale mengine yamekumbwa na hili baa la njaa. Ninapozungumza kuna shule nyingi ambazo huenda zikafungwa kwa sababu ya watoto kukosa kulipa karo. Kama hawalipi karo hawatapata lishe. Jinsi tunavyojua baadhi ya wale wafugaji wanategemea soko la wanyama ili kuuza wanyama wao wakimu mahitaji yao ya maisha kama kulipa karo na kununua chakula. Hivi sasa mifugo hao wamedhoofika sana na hamna soko la kuuza hawa mifugo. Pia tunaomba Kenya Meat Commission (KMC) wanunue hawa mifugo kwa ile inajulikana kama offtake ili wasiangamie bure bilashi. Nashukuru Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nilikuwa nadhani sitapata muda wa kuongea kwa sababu nimengoja sana. Nasimama kuunga mkono Hoja hii. Kwa kweli sheria ilikumbuka wanyama pori ikasahau binadamu. Wanyama pori wamekuwa kero kubwa sana katika eneo la uwakilishi Bungeni la Mwatate na vile vile Jimbo la Kaunti ya Taita Taveta. Wiki mbili zilizopita simba walikula mbuzi zaidi ya kumi na ngombe zaidi ya tano mali ya mkaaji wa eneo la uwakilishi Bungeni la Mwatate. Ni nadra sana mvua kunyesha katika maeneo hayo. Wakaaji wa hayo maeneo wanawategemea tu hao wanyama wa kufuga. Msimu huu uliopita mvua ilinyesha vizuri na watu wakapanda mimea yao sawa sawa. Lakini baada ya muda mfupi ndovu waliharibu hiyo mimea yote. Hata sijui tutafanya nini. Maanake nikiangalia huku mshahara umempunguzwa kidogo na Serem na hatuna hata kiwanda kimoja kule. Kwa jumla wanyama wa pori wameumiza watu wengi. Mzee mmoja aliumizwa na ndovu. Ako na watoto shuleni lakini hawezi kufanya shughuli yoyote kwa sababu amelemaa. Akienda kutafuta fidia kutoka KWS hakuna kitu ambacho kinapatikana. Hoja hii ni nzuri sana na ningeomba tuangalia Mswada ambao utaletwa hapa Bungeni ili tuweze kutatua shida ya wanyama wa pori na binadamu. Tunafaa kuangalia vile binadamu wanavyoweza kufaidika wakati wameumizwa au mimea yao imeharibiwa na wanyama wa pori. Hii inafaa kuwa sambamba kama vile binadamu akiumiza wanyama. Hawa wanyama wameishi na binadamu kwa muda mrefu na sio kuwa wana akili kuliko binadamu. Ninavyoongea sasa wakaazi wa eneo Bunge langu wanauliza watafanya nini kama watu wa KWS hawasikii na watatumia njia gani kuwamaliza wanyama. Kama unavyofahamu njia ni nyingi. Ingawaje tunafahamu kuwa wanyama pori wana faida kwa upande wa utalii hawa watu ambao wanakaa na wanyama pori katika eneo hilo hawafaidiki kwa njia yoyote kutokana na utalii. Kwa jumla kuna matatizo mengi kati ya wanyama pori na binadamu.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kuchangia Hoja hii na kuiunga mkono vile imerekebishwa na Mhe. Pukose. Vile wanenaji wengine wamesema hata Bibilia takatifu katika Zaburi 22:1 inasema kwamba ni bora mtu kuwa na jina zuri kuliko fedha na dhahabu. Kwa hivyo wenzetu walilimbikizia lawama wengine; kwamba walikula rushwa na Kamati ya Bunge ikakaa ikafanya uchungizi na wakatoa mapendekezo yao. Kule nje majina ya wengi wetu yameharibika na tunaonekana kuwa watu waliokuja hapa kula rushwa ya Kshs10000 ama Kshs20000. Kama walivyosema Wabunge wenzangu tungependa pia kuona wenzetu ambao walitoa lawama hii wakisema waliona hiki na kile waende kwa Idara ya Ujajusi ama kwa Tume ya Kupambana na Ufisadi wakatoe ripoti zao huko ili wachunguzwe. Hatutakaa hapa baada ya kupitia hali ngumu katika maisha halafu tuchafuliwe majina na watu ambao wako na eno yao. Nimesoma Ripoti iliyoko mbele yetu na nikaona mheshimiwa mmoja ambaye ametajwa akisema mheshimiwa mwenzake alimlimbikizia lawama kwa sababu walishindania kiti fulani. Sasa ni viti gani vinashindaniwa Bungeni baada ya kuwashinda wapinzani wetu kule nyanjani? Sasa wameleta eno hayo yote na wameharibia jina Bunge nzima. Nawaomba Wabunge waheshimiwa jina "mheshimiwa" lina heshima zake. Wale ambao wameharibu heshima hiyo wakutane na wale wanafanya uchunguzi na wabebe mizigo yao wenyewe. Naunga mkono Ripoti hii.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninachukua fursa hii kuupinga huu Mswada wa rafiki yangu Chepkong'a . Kwanza ninatoa mwito kwa wananchi wa Kenya nikianza na vijana walemavu na akina mama Mswada huu siyo wa mwanamke bali ni wa kutuweka katika hali ya usawa wa kijinsia. Leo ni sisi akina mama ndio tunalia kesho itakuwa wanaume kesho kutwa vijana na walemavu. Kwa hivyo akina mama wa Kenya wanalilia Mswada huu kwa sababu mama ndiye mzazi wa kila mtu. Mhe. Chepkong'a na timu yake wanafaa waelewe kwamba ni huyu mama kijana na mlemavu ndio wamewafanya wachaguliwe kuja hapa Bunge. Walemavu akina mama na vijana wanastahili kupewa nafasi zao kamili ndani ya hili Bunge kama ambavyo Katiba inatarajia. Hili si jambo tunataka eti kwa ajili ya ubinafsi. Ni wanaume hawa walioketi katika Bunge lililopita na kugawanya maeneo bunge. Walijiongezea maeneo bunge. Ni wao waliwatwika mzigo mkubwa wananchi wa Kenya. Kama kweli wao wanazungumzia mzigo tunataka tuwaone wakijitokeza waseme: "Ninatoa eneo langu la uwakilishi Bungeni liunganishwe na lingine ili tutoe nafasi ili Bunge lipunguze uzito." Ni Wabunge hawa hawa wa kiume ambao wamelemaza uchumi wa nchi ya Kenya maana wao ndio wengi hapa. Sisi ni wachache. Ni Wabunge hawa hawa waliopiga kura katika mpangilio wa Bunge wakanyima wawakilishi wa akina mama pesa ya kutosha sawa na National Government Constituencies Development Fund (NG-CDF). Tukapewa chache wakachukua nyingi. Mbona hamkusema kwamba sisi pia tuongezewe pesa tuwe sawa nanyi? Inamaanisha kwamba Waheshimiwa wenzetu wa kiume hawako tayari kuondoa mzigo kwa mwananchi wa Kenya. Wakati ni huu. Tukaeni tuzungumze tutoke kortini tuwe na uwiano. Tuondoe maeneo ya Bunge mengine turejeshe yale ya zai.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninampongeza Rais kwa Hotuba yake iliyokuwa na mwelekeo katika uongozi bora wa nchi yetu. Sisi sote tuko hapa kuwawakilisha wananchi wetu. Ninampongeza kwa sababu Hotuba hii ilizungumzia mambo muhimu katika maisha ya mwananchi kule nyanjani. Kuna watu wachache ambao wanasema barabara hazijaenea. Ningependa kuzungumzia upande wa Kwale. Hata hivi tunavyozungumza barabara ya Lunga Lunga kuanzia Msambweni inarekebishwa. Barabara hii ilizungumziwa na Rais. Kuna zabuni ambazo ziko tayari na mwezi ujao Rais mwenyewe anaenda kuanzisha mradi wetu wa barabara ya Kinango kuelekea Lunga Lunga ambayo itawekwa lami. Kwa hivyo upande wa barabara tunaweza kusema kuwa serikali inatengeneza barabara ili wananchi wawe na usafiri mzuri. Kuhusu mambo ya hospitali Rais wetu ametuonyesha kupitia serikali yake kwamba ametafuta pesa kupitia Bunge hili na tukapata vifaa ambavyo vimeanza kuwekwa katika hospitali zetu ili kusimamia matibabu ya wagonjwa mahututi matibabu ya saratani na magonjwa mengine. Kitu cha kusikitisha ni kwamba mashini hizo hazijafikishwa katika serikali za kaunti hasa Kwale. Mashini zetu hazijafikishwa kwa sababu hakuna mahali pa kuziweka licha ya kwamba hospitali zenyewe ziko. Mashini hizi ni kubwa sana na zina uwezo mkubwa. Hospitali zetu hazina nafasi ilhali tumezipatia kaunti zetu pesa ili zitayarishe hospitali hizo ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi tukishirikiana na serikali kuu. Kwa upande wa elimu Wizara ya Elimu imejaribu kwa sababu tumeona mpangilio mpya wa kubadilisha mfumo wa elimu wa 8-4-4 ili watoto wetu waweze kuwa na elimu ya kuwawezesha kutengeneza au kurekebisha vifaa kinyume na vile ilivyo sasa. Hata hizo mashini ambazo tumeletewa katika hospitali zetu hatuna wataalamu ambao wanaweza kuzirekebisha zinapoharibika. Hii inatokana na elimu ambayo imekuwa ikipatiwa watoto wetu. Kwa hivyo kuna mpangilio mzuri ambao umeelekezwa katika hali ya matibabu. Kuhusu ajira kwa vijana ni vyema ieleweke kwamba si lazima mtu aajiriwe katika afisi ya Serikali. Kupitia kwa mpangilio wa asilimia 30 tumeweza kuwaona vijana na kina mama wetu wakichukua zabuni na kuanza kufanya biashara. Hiyo ni njia moja ya kuongeza ajira katika mpangilio ule ambao ulikuwa umewekwa na Serikali. Ninataka ieleweke kwamba tumeanza mipangilio kupitia katiba mpya ya Kenya. Neno hili haliwezi kuwa asilimia 100. Linaenda kwa mipangilio. Kwa hivyo tuendelee kuiunga mkono Serikali na kama Wabunge tusukume na kusimama kidete kupambana na ufisadi ili yale yote yaliyopangwa yatekelezwe kwa wakati unaofaa. Ninampongeza Rais kwa Hotuba yake na kazi nzuri anayoifanya.
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninasimama kuuzungumzia Mswada huu. Ukiangalia zile hali ambazo tumekuwa nazo wakati wa nyuma kuhusu mambo ya kampuni ambazo zinaweza kupata zabuni tofauti tofauti katika maeneo yetu utakuta kuwa kumekuwa na unyanyasaji mkubwa. Nikizungumzia upande wa akina mama na vijana tukianzia hasa katika hali ya mtu kusajili kampuni yake unakuta kuna sheria nyingi. Ofisi ambazo zinahusika haziko mahali ambapo yule mama ama kijana wa nyanjani anaweza kufika na kupata ile huduma. Pili inabidi upitie mikononi mwa mawakili. Ukiangalia pesa ambazo wanadaiwa kulipa ili watengenezewe zile stakabadhi ambazo zinatakikana inakuwa ni malipo ya hali ya juu sana. Hii ni njia ya unyanyasaji na kumfanya mwenyeji wa nchi hii azidi kubaki maskini. Ikiwa sisi kama Wabunge tunataka kuiondoa shida ambayo imetukabidhi katika nchi hii katika hali ya kuwatayarisha vijana na akina mama waweze kupata ajira bila kutegemea kuajiriwa ni lazima tushuughulikie huu Mswada vilivyo. Tukiushughulikia huu Mswada vilivyo tutaweza kuutoa ule uzito ambao unamkabidhi mwananchi ili aweze kufunga safari kuja Nairobi ili kusajili kampuni. Tutaregesha hivi vituo vya kusajili katika Maeneo Bunge si kaunti pekee lakini yaende katika Maeneo Bunge ndio yule mwananchi au kijana ambaye hana uwezo aweze kuwa na mahala rahisi pa kuenda. Pili tuondoe yale mahitaji ya malipo ambayo yako juu kisheria kwa sababu ikiwa kila kitu lazima kipitie mikononi mwa mwanasheria ndio ile stakabadhi ipatikane je huyu mama na huyu kijana wataweza lini kuwa na kampuni na wapate zabuni ambazo zitaweza kutekeleza ule mwelekeo ambao tulipitisha katika Bunge hili wa kuwezesha asilimia 30 ya zabuni zipatiwe kina mama na vijana? Zaidi ya hayo tukizungumzia upande wa hizi kampuni ambazo zinatoka nje nitawapa mfano wa kampuni ambazo zinashughulikia mambo ya uchimbaji wa madini. Utapata kuwa tuna sheria tuliyoweka kuwa mtu hawezi kuwa na kampuni ikiwa ametoka nje. Ni lazima amhusishe Mkenya. Lakini hatukuweza kuiweka wazi kwamba Mkenya huyu atakuwa yeye mwenyewe ana kiwango gani cha hisa katika ile kampuni? Kwa hivyo unampata mtu anadanganyika anaambiwa aje ajiandikishe na yule mwingine wakubaliane kuwa atapewa shilingi mbili lakini ukiangalia faida kubwa yote inabaki mikononi mwa hizi kampuni ambazo zimetoka nje. Huu ni unyanyasaji wa hali ya juu kwa sababu kile kinachotokona na ule uchimbaji wa yale madini kinabakia mikononi mwa watu wa nje na sisi tunabaki na umaskini. Itakuwa ni vizuri sana ikiwa sisi Waheshimiwa katika Bunge hili ambalo tumelikalia kwa kula kiapo tutaamua kwamba tutasimama na taifa letu na wananchi wetu na kuona ni vipi tutakavyokubaliana na Mswada huu ili uelekeze sheria hizi pale ambapo mwananchi kijana na mama wa kawaida nyanjani ataweza kunufaika kuliko vile ilivyo leo. Ukiangalia mawakili wengi hawafanyi kazi za kortini bali wanatajirika kupitia hali hii ya kutayarisha stakabadhi hizi ambazo zinasimamia mambo ya usajili wa makampuni. Kwa mfano kuisajili kampuni moja ambayo ni ya kiasi inakubidi uwe na takriban kama Ksh25000 ama Ksh45000. Je huyu kijana au mama ambaye anataka kufanya biashara atakuwa amezitoa wapi pesa hizo ikiwa yeye mwenyewe kwanza hata biashara yenyewe hana? Mswada huu pia utaweza kuturahisishia mambo kwa sababu utaweza kutuwekea mipangilio ambayo mtu ama vijana wakipata zabuni benki inaweza kuwasimamia kufanya ile kazi kwa njia ya urahisi kuliko vile ilivyo saa hii. Hata vijana wanapopata hizi zabuni inabidi sisi Waheshimiwa tuanze kuenda juu na chini kuhakikisha hiki kikundi cha kina mama au vijana tumewatafutia pesa ili waweze kufanya ile biashara. Itakapokuwa sisi tumekamilisha huu mwongozo ambao tumeutoa kulingana na Mswada huu tutaweza kuwa tumerahisisha namna ambayo vijana wetu na kina mama watafanya biashara. Hapo tutakuwa tumesaidia vijana wetu kutoka kwa shida hii ya madawa na kuingiliana na mambo ambayo hayalingani na tamaduni zetu na usalama wetu. Mwisho tunaishia kulia na hali sisi wenyewe ndio ambao tunaweza kurekebisha hii sheria na tuweze kusaidia nchi yetu isonge mbele. Nasimama kuunga mkono Mswada huu.
Shukrani Mhe. Naibu Spika. Katika mradi wa Linda Mama Serikali inalipa Kshs17000 lakini hii haimudu kujifungua kwa upasuaji ambao kwa lugha ya kimombo ni Caesarean Section . Je hatima ya mwanamke anayejifungua kwa upasuaji iko vipi? Je hatima ya mtoto ambaye anazaliwa kabla ya siku yake iko vipi? Hivi ndivyo vipengele ambavyo tunaangalia kwa undani na kuhakikisha ya kwamba mwananchi wa kawaida amesaidika. Tutahesabu watu na tutatumia Kshs6 bilioni. Pia kuna kauli mbiu ya kura ya maoni ambapo zaidi ya Ksh18 bilioni itatumika. Hizi pesa zitatumika kwa mambo ambayo hayana uzito kwa mwananchi wa kawaida. Badala hizi pesa zitumike katika afya na ujenzi wa taifa hili zinatumika katika masuala ambayo hayasaidii asimilia kubwa ya Wakenya asilimia 80 ambao ni maskini. Nasimama kuzungumzia fundi wa mbao mfanyikazi wa mjengo mama wa mboga dereva wa matatu kondakta na wafanyikazi wote wa jua kali ambao wanapopoteza wapendwa wao miili yao inazidi kuzuiliwa katika vyumba vya kuhifadhi maiti na baadaye kutupwa. Naomba Bunge hili lipitishe Hoja hii na tuweze kuendelea mbele kujenga Jamhuri ya Kenya. Asante sana.
Shukrani Mhe. Naibu Spika. Nasimama kuunga mkono hili swala. Kwa kweli hawa wazee wa vijiji ni watu muhimu sana aake kawaida viongozi huwatumia hawa watu na baadaye wanawasahau. Ni vyema wangewaangalia kimfuko aake wao kwa upande wa usalama ndio nguzo. Kila mtu anayeingia katika kijiji ndio wanaomfahamu. Ukiangalia maswala mengine kama kesi ndogo ndogo wao ndio hutumika. Ni vyema tuwaangalie vizuri hawa wazee wa vijiji. Naunga mkono kwa dhati kabisa maswala ambayo wenzangu wamezungumzia. Asante Sana Mhe. Naibu Spika.
Shukrani Mhe. Naibu Spika. Nasimama kuunga mkono Ripoti iliyo mbele. Imechangiwa na Kamati ya Pamoja na Uwiano wakiongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mwenyekiti wangu katika Kamati. Ninampongeza. Ni muhimu kuzingatia kwamba katika Kipengele cha 97 wamezungumzia maswala ya jinsi ya kufurusha watu ambao wamekaa kwa ardhi isiyo yao kihalali. Hili limekuwa swala nyeti sana katika nchi ya Kenya tukizingatia matukio ya mara kwa mara ambapo tumeona wananchi wakifurushwa katika sehemu tofauti tofauti Kenya. Tumeshuhudia dhuluma ambayo wananchi wanapitia wakati wanafurushwa kutoka kwa ardhi. Mara kwa mara wanaomiliki ardhi hii huambiwa kuwa si yao. Mara nyingi utapata hii ni ardhi ya babu zao ambayo imenyakuliwa na mabwenyenye. Kwa hivyo wakati tunaweka mikakati kuhusu jinsi watu watakavyofurushwa katika ardhi liwe swala nyeti ili kufurushwa kwao kusiwe na dhuluma na kupoteza maisha yao. Mhe. Naibu Spika ukitazama Ripoti hii ambayo imefanywa na Kamati ya Pamoja utazingatia kwamba wamebainisha wasiwasi majukumu ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi na Wizara ya Ardhi. Kwa wakati uliopita tumeshuhudia mizozo kati ya hizi idara mbili ambayo imeathiri utendakazi wao. Kwa hivyo kupitia Ripoti iliyo mbele yetu ni matumaini yangu makubwa kuwa Wizara ya Ardhi na Tume ya Kitaifa ya Ardhi watatekeleza majukumu yao bila mizozo. Hii Ripoti imengojewa sana na Wakenya hasa tukizingatia ya kwamba jamii nyingi zimengoja kuona vile tutasuluhisha dhuluma za kihistoria ambazo zimewakumba. Katika Kipengele cha 3 wamejumuisha serikali za kaunti katika kutatua maswala ya ardhi. Baadhi ya dhuluma ambazo jamii zimeshuhudia kwa wakati uliopita katika unyakuzi wa ardhi utakuta watu wachache ambao ni mabwenyenye na wanajulikana kuwa na sifa mbaya za unyakuzi wanaketi katika ofisi kubwa hapa Nairobi na kuchora vile watakavyonyakua ardhi ya wananchi ambao hawana habari kuhusu yanayoendelea. Kwa hivyo tukizingatia kwamba ardhi nyingi ambazo labda hazijafanyiwa chochote ni ardhi za jamii serikali za kaunti zinafaa kuhakikisha kuwa jamii ambazo zinamiliki ardhi hizi hazijapokonywa ardhi zao kupitia mlango wa nyuma na mabwenyenye. Kwa hivyo Ripoti hii ni ya kufana sana na itakuwa na ufaa kwa Wakenya wengi. Tunapoelekea katika msimu wa kupiga kura Mwaka 2017 swala la ardhi ni nyeti sana. Ni muhimu tukumbuke kwamba baadhi ya wanasiasa ambao wameishiwa na maarifa na neema watachukua swala la ardhi kuwapiganisha Wakenya. Tukizingatia Ripoti ambazo ziko mbele yetu na Miswada ambayo imepitishwa katika Bunge hili ni matumaini yangu kubwa kwamba hatukakuwa na vurugu wala fitina maanake tutakuwa na sheria ambayo itatoa mwongozo kambambe kuhusu jinsi swala la ardhi ambalo ni nyeti katika taifa letu litatatuliwa. Ninaunga mkono Ripoti hii na kuipongeza Kamati ambayo imeleta.
Shukrani Mhe. Naibu wa Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada huu. Kwa kweli utamaduni ni kitu muhimu. Tujiulize utamaduni ni nini? Ni nini kinachangia utamaduni? Hapo ndipo tutafahamu maana ya vile wahenga walivyosema "Muacha mila ni mtumwa". Hii inaambatana na msemo unaosema "Penye wazee hapaharibiki neno". Ni kwa sababu utamaduni ni mambo ambayo yamechunguzwa na yametokezea kwa muda mrefu yakahifadhiwa mpaka leo hii na tunayatumia kwa mambo mengine. Hapa nchini tumetupa utamaduni kidogo. Nakumbuka kwetu Taita Taveta kulikuwa na utamaduni wa kuhifadhi mazingara. Kulikuwa na mahali wazee walikuwa wanaenda kufanya mazingaombwe yao na kuomba miungu yao. Ikiwa hapakuwa na mvua baada ya maombi hayo mvua ingenyesha. Lakini leo hii hakuna mambo kama hayo na ndiyo maana hakuna mvua kabisa kule kwetu. Vile vile miti ilikuwa inahifadhiwa. Siku hizi hilo halipo. Misitu yote imeharibiwa na hivi karibuni itapotea. Nakumbuka tulipokuwa wadogo tukiwa shule za chekechea tulikuwa tunaongea lugha za kitamaduni. Kuongea peke yake kunachangia pakubwa kuhifadhi utamaduni. Lakini siku hizi tunapenda kuongea Kiingereza ijapokuwa hatuwezi kuongea kama Mwingereza mwenyewe. Nampa kongole yule ambaye ameleta Mswada huu. Ikiwezekana sharti Serikali ihifadhi hela za kutosha ili utamaduni ulindwe. Kwa hayo machache naunga mkono Mswada huu kwa asilimia mia moja. Ahsante sana Mhe. Naibu wa Spika.
Shukrani Mhe. Spika kwa hii fursa ambayo umenipa. Napongeza Kamati ya Bajeti kwa sababu katika wakati huu mgumu wameweza kuja na Bajeti ambayo tumeona angalao kila idara imepata hela kidogo. Ingawaje tukiangalia changamoto tuko nazo nchini kama kazi kwa watu wetu. Ukiangalia Idara ya Viwanda kwa kweli ile hela wamepewa sio eti inawawezesha kutengeneza kampuni nyingi ili vijana wetu wapate kazi. Vile vile kulikuwa na raha na vifijo na nderemo kule kwangu wakati vijijini umeme ulikuwa unawaka hapa na pale lakini nikiangalia bajeti ya idara ya kawi naona imepunguziwa hela kidogo. Sioni kama itaendelea tena kuweka umeme kule vijijini. Kila wakati hata hapa Bungeni huwa tunalia tunasema kwamba wazee wa vijiji wana kazi kubwa. Sasa hivi nimeona Wizara ya Ndani angalau kidogo wameshiba. Basi tunaomba pia wao washibishe wale wazee wa vijiji. Ugavi wa mkate ndio huleta vita malumbano makaikiano na chuki zote kubwa humu duniani. Kwa kweli ukiangalia hii Bajeti na nikiangazia Eneo Bunge langu la Mwatate tumekuwa na kilio kikubwa cha maji. Kuanzia mwaka wa 2014 Serikali imekuwa ikisema kwamba itaweka maji ya Mzima Springs kule kwetu Kaunti ya Taita Taveta na maji mengine yaende Kaunti za Mombasa Kilifi na Kwale lakini nashangaa mpaka leo hii bado katika hii Bajeti hawajaiwekea mgao wa hela. Mimi hulia sana na ndovu na simba. Hata hivi juzi tumekuwa na fisi mla watu haswa wazee. Hata mimi nina wasiwasi na hii Bajeti ya mwaka wa 2020/2021 maana nimelia sana kuhusu ndovu. Nikiangalia Wizara ya Mazingira na Maliasili kwa kweli bajeti yao imepunguzwa na sasa hivi najua hawa wanyama watatusumbua sana. Zile hela walizopata ni za marupurupu yao tu lakini kufanya zile kazi zinatakikani itakuwa vigumu kwao. Nitaongea kuhusu Tume ya Kuajiri Walimu. Kwa kweli naipongeza kamati kwa kuipatia pesa za kutosha ingawaje hela ambazo wametenga za matumizi katika afisi ile wameweka juu sana. Mimi nikiwa mwalimu kwa kweli ile hela ya Kshs7 bilioni iko juu. Namuunga mkono mwenzangu Mhe. Sossion vile alikuwa amesema. Angalau wapunguze hizo hela na wawe na afisi ambayo inaweza kutoa huduma sawasawa kila mahali. Naona muda wangu umekwisha na nilikuwa na mengi ya kuongea. Asante Mhe. Spika.
Shukrani Mhe. Spika kwa hii fursa. Nimesimama kuunga mkono malalamishi haya ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu. Ni leo tu asubuhi mkazi mmoja wa eneo Bunge langu amenitumia barua kwa njia ya nukishi akilalamika kwamba yeye ni mgonjwa na hali yake ni mbaya. Kwa wale ambao hawaelewi nukishi ni fax . Ni kweli kwamba wengi wao ambao walistaafu mwaka wa 1997 walikuwa ni wazee na hela hii imechelewa. Ninaomba Kamati ambayo inashughulikia suala hili iharakishe. Mwaka jana mwezi wa tano tulikutana na wale waliostaafu 1997. Wengi wao wamekomaa na ni wazee. Wanadai hela yao ambayo ni haki yao. Ingekuwa ni vyema hili suala liharakishwe vilivyo. Wengine walikuwa wanalalamika kwamba sehemu nyingine nchini watu wamepata hela zao ilhali wao hawajapata. Naunga mkono kwa dhati kabisa.
Shukrani Mhe. Spika kwa kunipa hii nafasi. Nasimama kuunga mkono Hoja hii. Imekuja kwa wakati ufaao. Shule nyingi haswa za upili wakati huu zilianzishwa kama shule za msingi. Kwa mfano kuna shule moja kutoka kwangu ambayo imeanzishwa kwa ekari moja ya shamba. Ukiangalia mahitaji na majengo ya shule hiyo watoto wanahitaji mahali pa kuchezea. Mahali pa kuchezea kama uwanja wa mpira utachukua kiasi cha ekari moja ya shamba. Kwa hivyo hii ni Hoja iliyokuja kwa wakati unaofaa. Serikali yetu inafaa kuweka sheria kwa sababu ya upanuzi wa shule zetu. Naunga mkono Hoja hii. Ahsante.
Shukrani Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii kama mwakilishi wa Kamati ya Malipo ya Uzeeni. Kwa kweli malalamishi ya wale waliokuwa Bungeni miaka iliyopita yanafaa kushughulikiwa. Kwa kweli Wabunge wastaafu wako na matatizo makubwa. Wengi huja hapa lakini hata hela kidogo za kununulia chakula cha mchana huwa hawana. Hata wakiwa wagonjwa wengi wao hawana uwezo wa kujisaidia. Hilo ni tatizo kuu. Kiongozi ni kiongozi hata kama amesita kuwa Mbunge. Wengi wa Wabunge wastaafu wanalalamika kwamba wakiwa nyumbani kwao wananchi bado huwatembelea lakini hawawezi kuwasaidia. Hata wenyewe wakiwa wagonjwa ni tatizo. Kwa hivyo ningependa Wabunge wenzangu walitazame ombi hili kwa undani kabisa ndio tuone jinsi tutakavyolishughulikia janga hili. Wengi wao huja ofisini kwangu kwa sababu wanajua niko katika Kamati ya Malipo ya Uzeeni. Mimi hushindwa niwambie nini. Asante kwa fursa uliyonipa. Singependa kuzungumza mengi.
Shukrani Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii kuchangia Mswada huu ambao umekuja wakati mzuri. Nasema hivyo kwa sababu utaweza kutufafanulia barabara ambazo zitasimamiwa na Serikali kuu na zile za serikali za kaunti. Hapo awali kumekuwa na mvutano ambao umesababisha madhara. Kwa mfano katika eneo langu la Kwale barabara ni mbovu kabisa. Zaidi ya machungu ni pale ambapo Serikali kuu ilipoamua kutuwekea barabara lami magavana walienda kortini kuzuia barabara hizo ziziwekwe lami. Kama Wabunge Mswada huu utatupa mwangaza kutekeleza majukumu yetu ya kuangalia jinsi hela inatumika pande zote mbili - Serikali kuu na serikali za kaunti - kinyume na vile magavana wanavyofikiria kwamba sisi hatupaswi kuchunguza matumizi ya pesa katika kaunti. Mhe. Spika ni jambo la kusikitisha. Ilifikia kiwango kwamba barabara zetu zilizorota kwa sababu ya mvutano. Tumekuwa tukitetea barabara nyingi zisimamiwe na Wabunge. Kuna mfano mzuri wa matumizi mabaya ya pesa pale ambapo magavana waliamua kuchukua hospitali zote na hivi leo hospitali hazina madawa. Kunguni tele na watu wanalala watano na wengine wanalala chini. Hivi sasa wamepewa nafasi ya kusimamia barabara na sisi pia tuna hofu iwapo wataweza kusimamia vizuri kwa sababu lengo lao sio kumuhudumia mwananchi bali ni kuweka pesa mifukoni. Mhe. Spika kuna tatizo kuu katika Kaunti yetu ya Kwale. Tumekuwa tukiambiwa kuwa Dongo Kundu itajengwa barabara. Ingekuwa imejengwa. Lile tatizo la watu na magari kutumbukia baharini lingekuwa limeepukika. Ule msongao ambao uko katika feri ni kwa sababu Dongo Kundu imekuwa ni nyimbo au hadithi ambayo mpaka leo haijawahi kutekelezwa. Tuna ii kwamba kupitia Mswada huu barabara nyingine kama hiyo ya Dongo Kundu ile iliyoko eneo Bunge la Matuga na ile iliyoko Marere kuzunguka kupitia Shimba Hills hadi Mabungo imewekwa lami kwa wakati unaofaa. Barabara hiyo katika Eneo Bunge la Matuga imesaidia usafiri na ingeweza kusaidia kusafirisha mazao na hata wagonjwa. Hufikia kiwango ikawa barabara hiyo haipitiki. Barabara nyingine ni ile ya Samburu-Kinango-Kwale-Lungalunga kupitia Ndavaya. Hivi sasa magari yote kutoka Tanzania yanatumia barabara hiyo kwa sababu yanapopitia feri inachukua siku tatu au nne ndio gari liweze kuvukishwa. Barabara ya Samburu- Kinango-Lungalunga imerahisisha usafiri. Kwa upande wa utalii barabara hiyo ya Samburu- Kinango-Lungalunga-Kwale inafaa kuwekwa lami wakati huu. Hii ni kwa sababu imekuwa nyimbo tangu enzi ya Rais Mstaafu Daniel Arap Moi. Kila wakati tunaambiwa kwamba lami itawekwa lakini hatujawahi kuiona. Sasa hivi tunategemea barabara hiyo kwa utalii. Ikiwekwa lami itatufungulia utalii ambao umezoroteka katika Kaunti yetu ya Kwale. Barabara iliyo katika eneo la Lungalunga inayoenda Shimoni ni barabara nyingine muhimu. Hivi leo tunataka bandari ijengwe haraka lakini ikiwa barabara kutoka Kanana hadi Shimoni haitawekwa lami basi hakutakuwa na maana. Mvua inaponyesha barabara hiyo haipitiki. Barabara ya kwenda Vanga pia haipitiki mvua inaponyesha. Sehemu hizi ni nzuri sana katika kukuza utalii katika eneo letu la Kwale. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu utatuonyesha mwelekeo ambao utatekeleza mahitaji muhimu ya mwananchi. La ziada ni barabara ambazo zimejengwa kupitia China Road na mashirika tofauti. Wakati umefika upanuzi wa barabara hizo uweke nafasi ya watu wa boda boda . Ajali nyingi za boda boda zimetokana na barabara nyembamba na hawajatengewa sehemu zao za kupita. Magari yetu yana michoro kwa sababu zile pikipiki zikipita zinakwangura gari na ukisema umshtaki utakuwa unamwonea kwa sababu si makosa yake maana anahitaji kutumia barabara hiyo. Mswada huu utatusaidia. Natumai hakutakuwa na ufisadi katika mpangilio wa ujenzi wa hizo barabara. Ufisadi umetuharibia mipangilio mingi ambayo inasimamiwa na Serikali kuu kumwondolea mwananchi tatizo katika usafiri katika nyanja zote. Kwa hayo naunga mkono Mswada huu.
Shukrani Mhe. Spika kwa nafasi ambayo umenipa. Kama Mwenyekiti wa Kamati ya Malipo ya Uzeeni katika Bunge nachukua nafasi hii kutoa rambirambi zangu kwa jamii ya Mhe. Oprong. Kwa kweli viongozi waliokuweko mbele yetu na haswa Wabunge wanaumia sana. Katika Kamati yetu kila siku Wabunge wengi huja ofisini kwangu na wengi wao huwa hawana hata nauli ya kurudi nyumbani. Wana magonjwa lakini kununua madawa ni matatizo. Ni lazima tuliangazie suala hili kwa undani kabisa. Hata wenzangu hapa nawaomba kuwa hoja ikiletwa ya masuala ya malipo ya uzeeni wajaribu kuisikiza na kuiangalia kwa undani kabisa kwa maana tutakachofanya wakati huu kesho kutwa kitatuhusu sisi pia. Ahsante sana Mhe. Spika.
Shukrani Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii. Asante sana. Umenitambua kwa sababu nilikuwa nimekuja mbele kabisa. Bahati mbaya mwenzangu kwa ile shagala bagala ukapitiwa ukashika kadi yangu kwa bega lake basi ikabanduka. Kabla hata sijaongea kwa kweli na dhati kabisa naunga mkono hii Hoja. Kabla sijasahau najua wenzangu hapa wameongea kuhusa masuala ya maji. Nadhani katika awamu ya Bunge la 11 nilipitisha Hoja ya maji na Wabunge hapa waliunga mkono kwa wingi kabisa kuwa kila taasisi ya umma ipate maji. Hiyo Hoja ilipita vizuri lakini kwa sasa hivi mpaka dakika hii hatujui imefiki wapi. Nimejaribu kuifuatilia kila mahali lakini ninatupwa huku na kule. Kwa hivyo Kamati Tekelezi ni vyema ifuatilie hiyo Hoja. Ikiwezekana maji ipatikane kila mahali ndiyo magonjwa mengi yapungue. Kwa sasa hivi mimi kama mwakilishaji wa Eneo Bunge la Mwatate naona saratani inatumaliza. Na ni kweli watu wengi sana wana saratani. Juzi tu nilikuwa na Mbunge wa kwanza ambaye alikuwa anawakilisha Eneo Bunge la Mwatate. Alikuwa anateta na kuuliza kwa nini Bunge isifanye bidii ili kila kaunti angalau ipate mashine ya kuangalia saratani. Mwenzangu wa Nyali Mhe. Ali kwa kweli hii Hoja ameitunga na ikatungika. Tunasema tutaifuatilia ili itekelezwe. Kama vile Mbunge wa Jomvu alivyosema tusikuwe na mambo ya mchezo maanake magonjwa kwa kweli hayataki siasa. Wakenya tutakuwa tumesaidika. Mwanzo tuanze na ile mikoa ya zai nane. Kila mkoa angalau upate hospitali ya rufaa na vile vile tuangazie kila kaunti.
Shukrani Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ya kuchangia Mswada huu ambao umeweza kufika wakati ambao Wakenya wanateseka. Wakenya hukaa wakiwa na vipeni vyao hususan kina mama ambao wameamka na biashara ndogo. Wanatafuta mahali pa kuwekeza vipeni vyao vidogo ili waweze kupata mkopo waendeleze biashara. Lakini unakuta katika zile benki zetu tunazozitegemea za Serikali ni vigumu kupata mkopo kwa sababu wanahitajika udhaa wa hali ya juu. Wanapokimbilia hizi benki ndogo ambazo zinabuniwa za kisasa zenye riba ya chini inafika wakati wanarudi kujuta kama hivi sasa tunalia Chase Bank na Imperial Bank zimefungwa. Katika eneo Bunge langu kuna mwekezaji ambaye alikuwa ameamua kushirikiana na wananchi katika upande wa baharini ili waweze kuanzisha mradi ambao ungekuwa ni historia katika Afrika wa Well Shark ambao kwa Kiswahili tunamwita Papa Shilingi. Pesa ziliwekwa katika Imperial Bank. Leo hatuelewi kama Imperial Bank itaweza kufufuka ama itakuwa ni vipi. Kwa hivyo Mswada huu umeletwa kwa wakati unaofaa lakini tunajiuliza Benki Kuu ya Kenya iko wapi wakati benki hizi zinakuja kutapeli wananchi? Banki kuu ya Kenya ndio macho ya mwananchi na Serikali. Mbona wakuu wa Benki Kuu wamenyamaza wakati watu wanatapeliwa? Hakuna hatua ambayo inachukuliwa kwa wale wanaotapeli wananchi. Kwa hivyo Mswada huu utatusaidia kurekebisha na kuweka sheria mwafaka ambazo zitasimamia haki za mwananchi kupitia maeneo inayohusiana na pesa wanazoweka katika benki zetu. Pia tungependa Bunge hili kupitia Kamati yetu ambayo inahusika na mambo ya fedha ihakikishe kuwa Benki Kuu ya Kenya na Waziri wametuelezea ile pyramid scheme ambayo iliwatapeli Wakenya fedha ilienda wapi. Kule Kwale kina mama na wazee wengi walikufa kwa kiwewe baada ya ile pyramid scheme kuanguka. Tunafaa kujua kufikia leo pesa hizo ziko wapi na ni lini wananchi wetu watarudishiwa pesa zao. Watu walikimbia kuweka pesa kwa wingi kila siku na kila uchao wakifikiria kwamba wakati umefika wa kujinasua katika matatizo waliyo nayo ya kiuchumi. Kumbe walipeleka pesa zao katika midomo ya papa na zilimezwa na mpaka leo hatujui tutaelekea wapi. Huu Mswada umekuja wakati unaofaa. Bunge hili litaweza kuwanasua wananchi wa nchi hii kutokana na hawa matapeli na hizi benki. Tutaweza kusaidia mwananchi kuona benki zetu kwa mfano Kenya Commercial Bank (KCB) Cooperative Bank na National Bank na zitaweka riba sawa. Sijui kama tunaweza kujiuliza ni akina nani ambao huunda zile benki ndio waweze kututapeli. Hili ni swali tunaloliacha mikononi mwa Benki Kuu ya Kenya iweze kutujibu na kuchukua hatua inayofaa ili mwananchi aweze kupata haki yake. Kuna ulanguzi ambao unaendeshwa na zile benki ambazo zinaundwa na zina sauti tamu ya kuwavutia mwananchi ili waende kutapeliwa. Ningeomba kupitia kwako Mhe. Spika wa Muda niweze kutoa hizo dakika zangu mbili or tatu ambazo zimebaki kwa Mhe. Mwanyoha ambaye amekaa sana hapa ndani.
Shukrani Mhe. Spika. Nachukua fursa hi kwanza kumpongeza Rais wetu wa Jamhuri ya Kenya kwa kuona umuhimu wa kumteua mama kuwa Mwenyekiti wa Tume inayosimamia ugavi wa rasilimali. Kusema ukweli hii Kamati ambayo ilimhoji huyu mama waliona ni mama ambaye ana utaalamu na elimu ambayo kati ya wengi na waume walikuwa akaibuka kwamba ndiye mjuzi kushinda wale wengine wote - kielimu na kiutaalamu. Ameweza kutumikia Serikali na jamii ndani na nje ya nchi. Ni mama ambaye katika wadhifa wake atasimamia rasilimali zetu na kuona ugavi wa haki na wa usawa katika nchi nzima. Tukiangalia nchi nzima pia nitoe wito kwake aangalie maeneo ambayo yameathirika zaidi. Yameathirika kimaumbile na sio kwa sababu ya watu kupenda bali ndivyo yalivyoumbwa. Kwa mfano kuna maeneo ya Turkana Isiolo Kaskazini Mashariki sehemu za Pwani ikimewo Kwale. Waangalie vile tutapata mgao wetu kwa wakati unaofaa na utumike kwa njia inayofaa. Katika hali ya akina mama mara nyingi ndio wanaojua jinsi ya kugawa. Natoa wito kwake asiwe kiongozi wa ndani ya ofisi atoke atembee nyanjani atushirikishe sisi viongozi wa mashinani ili tutembee na yeye aweze kujionea mwenyewe ili akitoa uamuzi awe anatoa uamuzi wa kisawasawa ikiwa ni kitu ambacho yeye mwenyewe amejionea kwa macho. Pia nitoe witu kwa Wabunge wenzangu kwamba hii nafasi kwa huyu mama ni nafasi ambayo imekuja kwa wakati unaofaa hasa mkiangalia ile hali tulio nayo ya njaa katika nchi yetu ya Kenya. Saa hii kuna shida nyingi za njaa. Kuna shida kubwa ya maji. Kuna shida kubwa upande wa usalama. Hayo yote yameletwa kwa sababu hakujakuwa na usawa wa ugavi wa rasilimali. Lakini tutakapompa nafasi Daktari nina ii tutakuwa tumejijenga kwa kumtukuza mama ambaye ana ujuzi wa kugawa. Kawaida yetu akina mama hata ukimwachia shilingi hamsini juu ya meza utakwenda uendako halafu ukirudi utapata ugali juu ya meza na watoto watakuwa sawa. Kwa hivyo hii nafasi mkimpatia daktari itabidi tuwe na ii kwamba ugavi utakuwa wa usawa bila upendeleo. Shukrani kwa Rais wetu kwa kuweza kuona mbali na kumpatia mama hii nafasi na sisi Wabunge tunaunga mkono kwa pamoja. Shukrani Bwana Spika.
Shukrani Mhe. Spika. Nasimama kuunga mkono Mswada huu. Nampongeza sana Mhe. Millie kwa kuwa ameweza kuona yale ambayo yanawakumba akina mama haswa wale ambao tunawaita akina mama tasa. Kusema ukweli ninazungumza nikiwa mambo haya yalinikumba kupitia kwa magu nikiwa mimi ni mtoto wa pekee kwa mama. Niliona jinsi ambavyo magu alikuwa anasikitika kwa kuwa alinizaa peke yangu na hakuweza kupata watoto wengine hadi ikafikia kiwango cha kumlazimisha babangu aoe mke mwingine ili aweze kupata watoto na kuwaita watoto wake naye pia. Lakini basi ikiwa tunaunga mkono huu Mswada ni lazima tuangalie sheria kwa makini haswa zile ambazo zitaweza kulinda huyu mtoto atakayezaliwa na mama atakaye kuwa amebeba hiyo mimba inayotokana na mbegu ya mtu mwingine. Tusije kufungua njia ya kuwasaidia wale ambao wameamua kuishi kinyume na maadili ya kibinadamu kinyume na maadili ya dini na nikizungumzia hususan wale ambao tunawaita kwa lugha ya Kimombo gays na wanawake lesbians . Kwa Kiswahili wale wanawake huitwa msago. Tusipokuwa na umakini wa sheria tutawafanya hawa watu kuendeleza hizo tabia zao wakijua kwamba hata mtu asipozaa ana njia ya kupata mtoto na kudai kuwa yule mtoto ni wake. Hii itakuwa imewapa nafasi wale ambao wanataka kuendeleza uchafu huo kuwa wanaweza kuuendeleza na itaambukiza vizazi vingine. Hivyo basi nikiunga mkono sheria hii nampongeza Mhe. Nyikal kwa kutufafanulia zaidi akiwa yeye ni daktari anayeelewa zaidi mambo yanayohusiana na uzazi kupitia teknolojia mpya ambayo tumeweza kuirithi katika ulimwengu huu wa sasa. Katika hali ya kupongeza ningependa pia tuweze kuelewa ya kwamba tutakuwa tumempa mtoto huyu ulimwengu lakini je mtoto huyu atakuwa mwenyewe ni nani? Ataweza kupata haki zake kama mtoto kwa nani? Kwa sababu atakuwa haelewi babake na mamake ni yupi kwa sababu anaambiwa wewe ulizaliwa kupitia mbegu zetu na yule ambaye alimbeba kwa miezi tisa atasema mtoto ni wake. Mwishowe yule mtoto ataishi katika maisha ambayo hajielewi maisha yake iko mikononi mwa nani? Pia tuweze kuangalia kuwa kuna wale ambao watajitolea kutoa mbegu zao na baadaye aje aone kwamba hana haja tena ya kuweza kuwa na yule mtoto. Je na yule aliyebebeshwa ule mzigo ni nani atakayemtunza mpaka atakapozaa yule mtoto? Kwa sababu atakuwa anahitaji kulewa ndio yule mtoto aliye tumboni aweze kukua na aweze kuzaliwa. Katika sheria ambazo tutaweza kuangalia katika Bunge hili ambayo nina ii kuwa vichwa vilivyoko hapa ni vichwa ambavyo vinaelewa kila neno kwa ufasaha tutaweza kutoka na mwelekeo ambao utaweza kusaidia jamii kwa vizazi vijavyo bila kuhitilafiana na dini na bila kuhitilafiana na maadili yetu ya utamaduni wetu. Naomba kukomea hapo. Ninapongeza na hii sheria tuiendeleze tuweze kuchambua zaidi na tupate kitu mwafaka ambacho kitasimamia hili neno bila kuleta utata kati yetu binadamu. Shukrani sana Mhe. Spika.
Shukrani Mhe. Spika. Nasimama kuunga mkono Ripoti hii ambayo imetolewa na Kamati ya Ardhi na pia kuipongeza kwa maana kwa muda tuliokua nao wameweza kuzunguka katika maeneo mengi wakijaribu kutatua haya mambo ya ardhi. Naiunga mkono hii Ripoti kwa sababu ukiangalia kiundani utaona kwamba hili eneo la Taita ni moja kati ya maeneo ya Pwani ambayo yamedhulumika sana na mambo ya ardhi. Ikiwa tutaweza kuyafuatilia unyo unyo kama vile ilivyo saa hizi nina ii tutaweza kuweka roho za wananchi katika hali ya usalama na kuweka roho za wananchi katika ii ya kuamini kwamba walichagua viongozi wanaowajali. Mambo ya ardhi yamekuwa ni donda sugu sana hususan katika eneo letu la Pwani. Unapoliangalia kiundani utakuta wenyeji hawafaidiki bali ni watu wanaokuja kwa juu. Naishukuru Kamati ya Ardhi kwa maana imeweza kufika katika maeneo ya kwetu Kwale na tuna ii hivi karibuni wataweza kutoa Ripoti kulingana na yale ambayo wameweza kupata katika eneo la Kwale. Pia ningependa kuwahimiza viongozi wenzangu katika maeneo ya Pwani tuweze kushikana pamoja na tunapoona matatizo tuyakabili kwa sauti moja ndiposa hii Kamati iweze kuwa na nguvu ya kuweza kuyatatua haya matatizo. Vilevile ningependa kuiomba hii Kamati iweze kuangalia kiundani wakati hii ardhi inagawanywa waweze kujua kama akina mama nao wamepata vipande vya ardhi kwa sababu sisi katika mila za Kiafrika utakuta akina mama hawana kipande cha ardhi ambacho kinahesabika kwa jina la mama. Kwa hivyo hii Kamati iangalie wakati ardhi inagawanywa akina mama pia wapate sehemu za ardhi nao waweze kujivunia kama vile Wakenya wengine wanvyojivunia. Pia Kamati ya Ardhi iangalie kwa kina katika wale ambao wanagawanya ardhi kuna wengine ambao wanatumia ulaghai. Wanajihesabu kuwa wao ni maafisa wanaokuja kusaidia na kumbe palepale wanajikatia visehemu vyao. Tungependa kuona mkono wa sheria ukifanya kazi ili tuweze kuondoa tatizo hili sugu ambalo limetukabili haswa katika maeneo yetu ya Pwani. Tumeumia na mpaka sasa hatuna cha kujivunia. Hii ni hatari kubwa kwa sababu tumewahi kumwaga damu kwa sababu ya mambo ya ardhi. Hatutaki kuona tena nchi yetu ya Kenya tukipigana kwa sababu ya ardhi. Tunataka tupigane na tumbo ukosefu wa kazi na mambo ya usalama lakini siyo kwa mambo ya ardhi. Pia tutakapokuwa tumetatua haya mambo ya ardhi tutaweza kuondoa yale ambayo yamekuwa yakitumiwa na wanasiasa kutafuta kuchaguliwa. Tunataka mambo ya ardhi yatatuliwe ili tuweze kubaki katika maeneo yetu na tufaidike kama Wakenya wengine. Shukrani sana. Ninaunga mkono hii Ripoti.
Shukrani Mhe. Spika. Ninasimama kuunga mkono Ripoti ya hii kamati. Wakati ninaiunga mkono ningetaka kuzungumzia maeneo tofauti ambayo kusema ukweli kutokana na huu mradi ulivyoanza na kule unapotuelekeza ni mradi ambao utaleta mabadiliko makubwa katika uchumi wa nchi hii yetu. Kwanza ninapongeza huu mkataba kwa sababu umetuletea uwiano baina ya nchi yetu ya Kenya na zile nchi nyingine ambazo zimeingia katika mkataba. Hii ina maana kwamba wananchi katika hizi nchi zote nne wataweza kutembeleana kwa wakati wanaotaka bila kuchelewa hapa na pale kwa sababu ya usafiri. Pili mradi huu ukilinganishwa na mingine ambayo Serikali imeanzisha umeweza kukimbizwa kwa haraka. Huu mradi wa reli umetupa tamaa kubwa hata tumeanza kuona mazao ya pesa zetu kwa sababu mradi umeanza na unasonga mbele kwa haraka sana. Tatu mradi huu ukikamilika barabara zetu zitaokoka. Ile hali iliyo katika mabarabara yetu saa hii ni mbaya sana. Kwanza katika usafiri kuna ajali ambazo zinatokana na malori pamoja na mabasi. Mwishowe ni mauti ama majeruhi wengi sana. Lakini tutakapokuwa tunatumia reli usafiri utakuwa na usalama zaidi. Nne usafiri wa reli utatusaidia kwa sababu ukiangalia tabia ambayo inaendelezwa na Shirika la Ndege la Kenya utagundua kwamba shirika hilo halimsaidii mwananchi. Kwa mfano utafika katika kiwanja cha ndege ukijua utaondoka saa fulani. Mtawekwa pale na kile mtakachosikia ni matangazo tu: "Tunawaomba msamaha." Lakini wewe ukichelewa kwa sababu pengine ya msongao wa magari barabarani ukifika pale unatozwa faini. Hii inamaanisha kwamba hili Shirika haliko pale kutusaidia sisi bali wana mambo yao wenyewe ambayo wanayaendeleza. Tano mradi huu utawawezesha wananchi na hata sisi Wabunge kufika katika maeneo yetu ya kazi haraka sana. Kwa mfano nitaweza kulala nyumbani Kwale na niingie pale Samburu kwa sababu nitapata usafiri wangu kwa wakati. Nitaweza kuhudhuria Bunge mapema vilivyo. Hii ni tofauti na kuwa Nairobi ambapo nitakumbwa na msongao wa magari katika barabara kuu ya kuelekea Mombasa kisha nichelewa kufika Bungeni. Mradi huu utaweza kutuondolea ufisadi kwa upande mwingine. Ukiangalia yale yanayotendeka katika maeneo yaliyo na mashine ya kupima mizani ya malori na matrela kusema ukweli Tulizungumzia hili neno wakati ambapo Mhe. Birdi alileta Mswada wake hapa. Mimi binafsi nilipendekeza kwamba tuondoa maofisa wote walioko katika haya maeneo. Hii ni kwa sababu yanayotendeka pale yanatuvunja moyo sisi kama viongozi katika nchi hii ya Kenya. Serikali kupitia kwake Rais inajaribu kupigana na ufisadi lakini yanayotendeka pale ni maajabu. Ikiwa tutaweza kuwaondoa wale watu kule na kuweka watu wapya ambao wana malengo ya kusafisha ufisadi tutaweza kuongoza hii nchi yetu na kupata usafiri ambao hauna matatizo mengi kama vile ilivyo leo. Kwa upande mwingine kidogo kuna tetesi. Sisi viongozi wa Kaunti ya Kwale tumezungumzia hizi tetesi. Hii ni kwa sababu kuna neno ambalo linaendelezwa na wale waliochukua hii kandarasi na ningeomba hili neno liende katika maandishi ya Bunge. Kuna mambo ambayo yanaenda kinyume na mkataba wa hii reli upande wa wale ambao walichukua kwa sababu kumekuwa na uchimbaji wa mchanga katika bahari yetu ya Kwale. Hakuna mahali tuliketi nao wakatueleza ni kiwango gani cha mchanga watachimba na ni faida gani watu wa Kwale ama Kaunti ya Kwale itapata. Hapo mbeleni Kenya Ports Authority (KPA) ilichimba huo mchanga na hakuna kitu mpaka leo ambacho kimeweza kumfaidisha mwananchi wa Kwale licha ya kwamba kulikuwa na maelewano baina ya KPA na wavuvi wetu wa Kwale. Hivi leo wavuvi wa Kwale wanaishi maisha duni kwa sababu walikuwa wakitegemea uvuvi. Uvuvi umekufa kwa sababu maeneo ya samaki yote yaliharibiwa na wale waliokuwa wakichimba huo mchanga. Hakuna lolote ambalo wametufanyia. Tunaiomba Serikali kupitia Wizara zinazohusika; Wizara ya Mazingira na Wizara ya Usafiri ipange mkutano ili tukae pamoja tujue mambo hayo. Tunashukuru kwa sababu mnamo Mwezi wa 11 mwaka jana hiyo meli ilisimamishwa. Lakini hatujui bado kutatokea kitu gani na hali mchanga uliochukuliwa ni raslimali ambayo itamnufaisha mtu wa Kwale ama Kaunti ya Kwale. Kwa hayo mengi ninaipongeza hii kamati ambayo ilitoa hii Ripoti. Pia naipongeza Serikali kwa kufikiria kwamba huu mradi utaweza kusaidia wananchi wa Kenya. Sasa tutakuwa na usafiri ambao si wa gharama ya juu kinyume na vile ilivyo katika usafiri wa ndege. Shukrani.
Shukrani Mhe.Naibu Spika kwa kuniokoa. Naomba kuchangia Hotuba ya Rais kama alivyotupatia wakati wa kufungua Bunge letu. Naipongeza sana hotuba ya Rais wetu kwa sababu iliguzia mambo muhimu; hususan yale yalionileta katika Bunge hili. Kwanza ni kuhusu ada zinazolipiwa na kina mama wakati wa kujifungua. Nashukuru kwamba jambo hilo limeweza kutatuliwa. Na pia ametupatia nafasi hususan sisi watu wa Pwani tuweze kuzaana kwa wingi kwa sababu inaonekana mkiwa wengi ndio mnaweza kupata urais katika hii nchi. Pia itaweza kutusaidia kwa sababu hali ya umaskini imekidhiri sana katika Jimbo letu la Kwale na Pwani kwa ujumla. Kwa upande wa elimu Rais alisema kwamba tarakirishi zitapatikana kwanzia mwaka ujao. Swali langu ni je nani atawafunza watoto hao kutumia tarakirishi-beba? Hata walimu wenyewe hawatoshi katika shule. Hata hawana elimu ya kutumia tarakirishi-beba. Kwa hivyo nilikuwa natarajia kwamba Rais atatupatia ratiba ya kuajiri walimu zaidi katika shule na waanze kupewa elimu kabla ya mwaka ujao. Tukiangazia usalama hatuzungumzii tu kuwa na askari wengi. Nilikuwa natarajia Rais wetu atatueleza vile ataweza kutatua yale madhambi yaliyotendewa watu wa Pwani. Madhambi yaliyotendewa watu wa Pwani ndio chanzo cha kutokuwa na usalama katika eneo letu la Pwani. Tunadai mambo yetu ya ardhi na ajira. Kwa mfano ukiingia katika Wizara ya Fedha kuanzia A hadi Z ni watu wa kabila moja! Rais hakutueleza vile atatatua mambo kama hayo. Tunataka usawa; sio usawa wa jinsia bali usawa katika ugavi wa mamlaka katika kila eneo ili tuweze kuwa na usalama katika nchi hii yetu ya Kenya. Jambo lingine ni kuhusu mambo ya kilimo. Rais alisema kwamba ataweza kuboresha ukulima. Ukulima hauwezi kuboreshwa ikiwa kwanza wenyeji wa zile sehemu zenye utata wa ardhi hawana hata zile sitakabadhi za kumiliki ardhi hizo. Kwa hivyo kwanza Rais atuwezeshe kupata mashamba yetu ndio tuweze kuzungumzia jinsi kilimo kitaboreshwa katika Pwani. Nikimalizia natambua juhudi za Rais kuwasaidia akina mama na vijana ili waweze kujimudu kimaisha. Zile pesa ambazo zimetengwa zije kwetu nilikuwa natarajia Rais ijapokuwa anasema zitelemshwe ziende kwa maeneo ya Bunge lakini angetaja ni nani atakuwa msimamizi. Ningeomba pesa hizo zielekezwe katika majimbo ziweze kuwa katika mikono ya akina mama waakilishi wa majiimbo. Kwa sababu sisi akina mama tumeletwa katika Bunge hili lakini hatukuelezwa tutakuwa tunatumia vyombo gani katika kuendesha mipangalio ya
Shukrani Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa hii nafasi na heshima niliopatiwa na Mheshimiwa Malulu Injendi. Naunga mkono hii Hoja ambayo ni muhimu sana. Mimi mwenyewe nilikuwa nimeandika Hoja kama hii lakini ikawa mwenza amenitangulia. Sina budi bali kumuunga mkono kwa kila namna. Mheshimiwa Naibu wa Spika wa Muda mwanzo kabla hata sijaongea sana hao wazee wa kijiji sio lazima wawe na elimu kiwango fulani bali lazima wawe ni watu tu ambao wamechaguliwa na wananchi kule vijijini. Hao wazee wa vijiji wakiwa wazee kwa wamama hufanya kazi kubwa haswa kwa masuala ya usalama ambalo ni jukumu muhimu sana kwa nchi yetu kwa ujumla. Maanake inachangia kwa masuala ya uchumi kama vile utalii uchumi na kile kitengo kwa ujumla maanake hata ukila Ugali na hakuna usalama huo Ugali hausimami tumboni. Mhe. Naibu Spika wa Muda hawa wazee wa vijiji huchangia sana. Wao hufanya kazi kubwa. Saa zingine wanaamka masaa ya usiku sana na hawana tochi viatu nguo na hawalipwi na ilhali wanachangia pakubwa sana katika shughuli tofauti za nchi yetu kuleta maendeleo kule mashinani. Miaka ya nyuma wazee wa vijiji walikuwa ni watu ambao wamekomaa wamefundisha watoto wao wakamaliza na wengine wamepumzika kule mashinani lakini hali imebadilika. Siku hizi wazee wa vijiji ni vijana ambao wameoa juzi na akina mama pia wako na watoto wanasoma. Nampongeza sana Mhe. Injendi kwa kuleta Hoja hii. Wazee wa vijiji ndio wanafahamu kila kitu ambacho kinaendelea kule vijijini. Tukiwatunza tutatunza nchi yetu kwa kila namna kwa sababu wao huhusishwa kwa masuala ya mashamba malumbano madogo na wakati mama na baba wamekosana kule nyumbani. Wazee wa vijiji hutumiwa na Serikali wakati inataka kufikia malengo yao kule mashinani. Wakati viongozi wote hapa Bungeni wanatafuta kura huwatumia wazee kupiga firimbi hapa na pale ili waonane na wananchi. Watu wamekuwa wakiongea kuhusu suala la wazee kwa muda mrefu lakini halijatekelezwa. Baada ya huu mjadala kuisha naomba ile Kamati ya Utekelezi iende mbio na Hoja hii iwe sheria kwa haraka iwezekanavyo. Wazee wa vijiji wanasikia vile nasema. Naomba waangalie hawa viongozi wote ambao wako hapa Bungeni. Wachukue hatua kwa wale viongozi ambao hawaungi mkono Hoja hii kwa sababu ni muhimu sana. Sitaki kuongea mengi kwa sababu Hoja hii inajielezea. Naunga mkono Hoja hii kwa dhati. Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Shukrani Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa hiyo nafasi ya muda mdogo japo nilikuwa nataka kuwa na muda wa kutosha. Ukweli ni kwamba tungetaka sana kupitisha Mswada huu. Kwa wakati ujao tungetaka tuwekewe sehemu nyingine inayoonyesha kuwa katika majimbo na zile sehemu ambazo pesa zinakusanywa ni kiwango kipi cha pesa kimekusanywa ili wakati wanapewa pesa zingine tuangalie ni vipi tutawapa pesa kwa sababu saa hivi tunatoa pesa ambazo hatuelewi zitatumika vipi. Upande wa unyunyizaji wa maji katika mashamba ningeomba tuweze kusimamia sekta hii iendelee katika Galana kwa sababu ni moja kati ya sehemu ambazo zinaweza kulisha nchi hii.
Shukrani Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Nafikiri sikosei kwa sababu kama Mheshimiwa angekuwa anaelewa Kiswahili vizuri angejua kuwa nimesema chama cha ODM na wala si chama cha ODM pekee ndicho kilitetea ugatuzi. Tulikuwa katika msitari wa mbele katika kutetea ugatuzi. Naomba pia niongezee dakika moja kwa sababu nimekatizwa na haya mambo ni muhimu
Shukrani Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Mswada huu. Ukiangalia hiki kikundi cha watu ni kama asilimia 15. Ni kama watu zaidi ya milioni sita. Ni kikundi ambacho kimepuuzwa - si kwa mahospitali benki shule na makanisa. Naomba Kamati Tekelezi baada ya huu Msada kuwa sheria watekeleze. Wahakikishe kuwa imetekelezwa na hicho kikundi cha walemavu angalau kimesaidika ili wajione wako sawa na Wakenya wote kwa ujumla. Nasimama kuunga huu Msada. Ahsante sana.
Shukrani Mheshimiwa Spika kwa kunipatia nafasi hii. Ningelipenda kwanza nikushukuru wewe kikamilifu kwa sababu ya vle ulivyopambana katika hali ya kudumisha na kuhakikisha kwamba sheria zinafuatwa. Ninakumbuka mwaka wa 1967 marehemu muanzilishi wa taifa hili Hayati Mzee Jomo Kenyatta aliulizwa na rafiki yake Hayati Julius Nyerere: kwa nini wewe unatembea na askari akajibu na askari wengi kwa sababu Tanzania si kama Kenya. Kenya ina ninataka kukuhakikishia umepambana vikali Mheshimiwa Spika kwa sababu Bunge hili lina wanaume kuliko Mabunge yote ulimwengni. Kwa hiyvo umefanya kazi nzuri pamoja na kamati yako na ninakuombea likizo njema ili uweze kutafuta nguvu kwa sababu wanaume wale bado wako na watakuja na wanakungoja uwaongoze kisawasawa. Mheshimiwa Spika nataka kuunga mkono vikamilifu Mswada ambao umeletwa mbele yetu kwa sababu tumefanya kazi nzuri na Kenya nzima ikafurahia. Kenya imefurahia kupitishwa kwa Mswada wa kupunguza riba inayotozwa na benki. Wajua mimi huingia vichochoro vya Nairobi hii. Nimekunywa chai ya watu karibu 20 na nikiuliza kwa nini wananinunulia chai ilhali hawanijui wanasema kwamba wamefurahishwa na kazi nzuri ya kupunguza riba. Kwa hivyo hiyo ni kazi ambayo imeweza kulifanya Bunge hili lipate sifa na sifa ile yote imekuja kwa sababu ya usimamizi wako Mheshimiwa Spika. Nikirudi katika sheria za vyama nataka niunge mkono kikamilifu kwamba watu wauke hapa na pale. Ni lazima kila mtu afanye kazi yake kikamilifu na kama anaunga mkono chama chake kikamilifu basi hapo hawezi kutingishwa na mtu yeyote. Najua kwamba kuna wengi hawakusikia raha kwa sababu pengine wamepitisha Mswada huu kwa sababu baba Rais Mheshimiwa Wetangula au Kalonzo amependa. Wengine wao walikuwa hawapendi lakini wamefanya kwa sababu hiyo. Mimi naomba kila mtu ambaye yuko katika Bunge hili ahakikishe kwamba Mswada huu ameutilia maanani na ameufurahikia kwa sababu huwezi kubwagwa na yeyote wakati wewe unafanya kazi nzuri katika chama chako. Na mimi ninasema wale wanasema kuna mayatima wale si mayatima. Wale wamekata shauri wameondoka kwenye mlo na kuingia katika sehemu ambazo zina giza kidogo. Wale in mashujaa kwa sababu kuacha chakula hapa na kuenda kutafuta mahali pengine huo ni ushujaa mkali na wanastahili sifa badala ya kuitwa mayatima. Kuhusu NGCDF mimi naunga mkono Mswada uliopitishwa lakini pia naomba kuwe na mipango ya haraka haswa kuhusu ili kamati ya Oversight . Hii kamati inaweza kufanya kazi nzuri lakini mpaka sasa nikiangalia hawana chochote wamefanya. Naomba Kamati ya NGCDF ihakikishe kwamba imepangia kamati ya Oversigh t mambo itakayoweza kufanya kwenye shughuli zake kwa sababu kukaa bure bila chochote ni shida. Huko kwangu nilifanya hesabu na kuona watapata 30000 peke yake kila mwaka. Hiyo ni pesa kidogo na lazima kuwe na marekebisho ili waweze kufanya kazi hii kwa juhudi. Hii ni kwa sababu wao ndiyo watafanya ile bodi ifanye kazi kisawasawa bila hivyo mambo yataende segemnege. Nikiketi naunga mkono na kukusifu tena kwa kazi nzuri ambayo umefanya bila ubaguzi. Asante Mhe. Spika.
Shukrani Naibu Spika kwa kunipa nafasi niweze kuuchangia Mswada huu ambao umekuja kwa wakati unaofaa. Itakuwa bora kwa Bunge kuutilia maanani na kuupitisha haraka iwezekanavyo ili mwananchi aweze kuona faida ya utamaduni wake. Ukiangalia maisha ya sasa vile ambavyo vijana wetu wanavyolelewa na vile wanavyoishi utakuta kwamba tumepoteza hadhi zetu kama Waafrika na kama Wakenya. Mambo mengi ya kitamaduni tumeyaacha na hii imetuingiza katika matatizo makubwa haswa katika upande wa mavazi na vyakula. Mababu zetu wameishi maisha marefu zaidi kuliko sisi kwa sababu waliegemea vyakula vya kitamaduni na matibabu ya kitamaduni. Mavazi yetu ya kitamaduni tumeyawacha kiwango cha kwamba hata katika Bunge letu tumeshindwa kujionyesha tumetoka katika asilia gani. Wakati umefika wa Bunge kutenga siku maalum ambayo tunaweza kuvaa kitamaduni ili tuonyeshe vizazi vyetu ni kipi kilicho bora katika utamaduni wetu. Kupitia Mswada huu tutaweza kulinda mazingira ya utamaduni wetu. Tutaweza kuhifadhi utamaduni wetu kuanzia vyombo ambavyo tulikuwa tukitumia kuanzia vyakula mpaka namna ya kutoa utao kwa watoto wetu. Kwa ushirikiano baina ya Serikali Kuu na serikali za majimbo tutaweza kuukuza utamaduni wetu ikiwa sote tutazungumza kwa sauti moja na kushirikiana katika kushauriana. Katika maeneo yetu ya Pwani kuna mavazi ambyo yamepotea. Tulikuwa na hando vazi ambalo lilivaliwa na akina mama. Mama akivaa vazi hilo hata akipita unaona raha anavyotembea. Kuna mavazi ya ushanga ambao tukivaa kiunoni shingoni na mikononi mpaka miguuni mama au msichana anapendeza. Leo hii hayo yote tumeyatupilia mbali na tumeingia katika mavazi yaitwayo tights ambayo yanaonyesha maumbile ya mwamamke ambayo ni kinyume na dini na utamaduni wetu. Tukiyatilia maanani yale yote ambayo yameandikwa katika huu Mswada tutaokoa mambo mengi. Kwa upande wa mapishi vifaa ambayo vilikuwa vikitumiwa na wazee wetu kama vile nyungu na vikaango chakula ulikuwa ukikila unapata radha tamu ya chakula. Ulikuwa unapata ile radha ya ile mboga. Leo kutokana na sufuria ambazo tunatumia saratani ndio hiyo kwa sababu ile sufuria inafikia wakati inaanza kuisha. Haishi kwa sababu imechomeka na moto ni wewe ambao unakula vile vipande vya ile sufuria. Kwa hivyo tukihifadhi utamaduni wetu na kuulinda kisheria tutaweza kuyaokoa maisha yetu pia kulingana na yale ambayo yanatukumba hivi leo. Angalia chombo kinachoitwa uteo. Uteo ni chombo ambacho kimesukwa kupitia mnazi ambacho kinatumiwa na akina mama kudondoa chakula kama vile mchele au maharagwe na kuyatenganisha. Leo tumekimbilia mambo ya blender na vifaa vingine vya kisasa kinyume na utamaduni wetu. Viko wapi vitu vyetu vya zai? Hivi ni vitu ambavyo wazungu wanatoka kule wanakotoka kuja kuvifuata na mwisho wanavinunua na wanaenda navyo na sisi tunabaki bila chochote. Wengine hawanunui wanatumia mbinu zao na wanabeba kwa kisingizio eti ni zawadi lakini akifika kule hiki ni chombo ambacho kina dhai kubwa sana. Kwa hivyo Mswada huu utatusaidia na tutaweza kuwafuatilia wale ambao waliiba utamaduni wetu. Tutadai watulipe kwa kiwango kile ambacho kitakuwa sawa kulingalisha na utamaduni wetu. Ni lazima tuukuze utamaduni wetu na kuulinda. Kule Pwani mti wa mnazi una mazao na mambo mengi lakini umewekwa kando. Tukihifadhi yale yanayotokana na mnazi tutaokoa hata matumizi mabaya yaliyoko leo. Watoto wamepotelea kwa unywaji mbaya wa pombe. Lakini ukiangalia pombe ya mnazi kwa wale wanayoitumia ni kilevyo ambacho hakidhuru kama vile pombe za whisky zinavyodhuru. Tukipata njia ya kuhifadhi vitu kama hivyo kwa njia sawa tutapata ufaa mengi. Kule kwetu kuna ile changa tunaitumia kama yeast kwa mahamri au dazi. Pombe ya mnazi ina dhai zaidi ya vile watu wanavyoifikiria. Iko na mambo mengi sana. Watu wakioza watoto wao ni lazima kinywaji kile kiweko. Je leo tunaambiwa tulete makreti ya Tusker . Huo sio utamaduni. Turudini katika utamaduni wetu na tuyavae mavazi yetu ili na sisi tuhesabike katika ulimwengu kuliko vile ilivyo leo. Mpaka hapa ndani ya Bunge ni lazima ujifunge tai na uvae sketi ndio uhesabike kwamba wewe ni Mbunge. Haifai! Tuukuze utamaduni wetu na turudi katika makavadhi yetu. Kupitia Mswada huu tutaweza kuyalinda yale makaya na kuyakuza mpaka hata watalii wakija waweze kuyatembelea ili waone utamaduni wetu na wauelewe. Pia tutakuwa tunawapatia watoto wetu nafasi ya kupata utao na mwongozo kulingana na utamaduni wetu kinyume na vile ilivyo leo. Watoto wetu wamepotoka kwa sababu ya kufuata tamaduni za kutoka nje. Namshukuru Mheshimiwa ambaye alitayarisha Mswada huu. Tutauunga mkono na kuupitisha haraka iwezekanavyo na tuweke pesa zote hapo kwa sababu tutakuwa tunajiokoa sisi wenyewe.
Shukrani Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii. Nia malengo hata madhumuni ya Hotuba ya Rais ilikuwa nzuri ingawa kuna upungufu fulani. Nimepiga nduru sana. Nikiunganisha eno niliyotumia kupiga nduru yanawezatoka Lunga Lunga hadi Nairobi. Ni nduru ya tatizo la maji wanyama na mengineyo. Wakati huu ukisikia wananchi wanashindania maji na wanyama si sawasawa. Katika Hotuba ya Rais hakutaja mambo ya maji. Kule kwangu eneo Bunge la Mwatate hali ya maji ni mbaya mno. Wananchi wanashindania maji na wanyama. Watoto wa shule saa zingine kwenda shule ni taabu. Akina mama wanaumia pia. Vitabu takatifu Bible na Quran kuna sehemu imetaja kuwa yule ambaye anaweza kumpatia mwenzake maji basi atapata baraka. Tuangalie masuala ya wanyama. Hili limekuwa suala sugu. Katika Hotuba ya Rais hakutaja. Kuna hawa wanyama wanaoharibu mimea ya wananchi lakini bado hawajapatiwa fidia. Na ni jambo ambalo tumeliongea kwa muda mrefu. Mahali pakavu kama kule kwangu Mwatate wakati tumeona mvua kidogomwananchi akipanda mimea yake ikiliwa na wanyama inakuwa ni taabu kubwa. Vile vile ukiangalia katika eneo hili la Kenya kuna mahali ambapo pamebaguliwa ambapo hakuna viwanda wala nini. Siku hizi kupata kazi kama hauna mtu mkubwa katika shirika fulani kuipata ni vigumu. Mahali kama Mwatate kwa kweli Serikali ingefikiria kuweka vitu kama viwanda ama kitu fulani cha kuwezesha wananchi wapate mapato. Kwa sasa hivi kule Mwatate hakuna njia yoyote mwananchi anaweza kujisaidia kupata mapato. Ni taabu moja kwa moja. Kuhusu elimu kuna vyuo vikuu ambavyo viko katika haya maeneo ambayo yaliachwa nyuma. Hawana mafunzo ya ziada kama vile miji mikubwa kama hapa Nairobi na Mombasa. Utakuta kwamba katika hii Bajeti hivi vyuo vikuu vimepatiwa hela kidogo. Inakuwa vigumu sana kwa wale ambao wanaviongoza kuvishughulikia. Hata vingine baada ya muda mfupi labda vitaporomoka. Ile Hotuba ya Rais ingekua ingezingatia masuala yote na kuangalia pembe zote za Kenya maanake ni Rais wetu wa Jamhuri. Angeangalia masuala yote haswa ya maji. Mwenyezi mungu alimpa hewa binadamu halafu ya pili ni maji. Bila maji maisha si sawasawa. Asante kwa kunipa fursa hii kuongea masuala mawili au matatu.
Shukrani Naibu Spika wa Muda. Nilidhani hunioni kumbe waniona! Mhe. Naibu Spika wa Muda mimi nasimama kuunga mkono Hoja hii kwa sababu anayekuja ni mtu mtukufu na hata kama dini ni tofauti zote zaelekea kwa Mungu mmoja. Mimi ni Muislamu na najua kwamba Bunge hili lina Waislamu wa kutosha. Nawauliza Waislamu wenzangu waheshimu Baba Mtakatifu ili tuweze kuhakikisha kwamba tunaenda kukutana na yeye. Baraka hazitoki sehemu moja. Zinatoka sehemu mbalimbali na nina ii kuwa yeye akiwa kiongozi wa ulimwengu atatupatia baraka zake. Langu tu ni kumuuliza Mwenyezi Mungu siku moja Baba Mtakatifu aje awe mtu wa Kenya kama Mhe. Gunga ili tuweze kupata baraka za karibu kuliko kungoja miaka mingi hadi Baba Mtakatifu Francis aje. Tunataka tuwe na mtu karibu sana. Ingawa Mhe. Gunga anakataa ni nafasi ambayo angeitumia. Nataka kutoa shukrani zangu za dhati. Itakua si sawa kwetu kusema kuwa tunabaki hapa ilhali kiongozi mkubwa wa dini ya wenzetu anakuja. Nawaomba Wakatoliki wakumbuke kuwa Uprotestanti pia ni dini na Uislamu pia ni dini. Kiongozi wa Kiislamu pia naye akija siku moja pia nao wavunje kazi zao na waelekee kumuona ili tuweze kuwa kitu kimoja ndani ya nchi hii. Ahsanteni. Mungu atubariki na naunga mkono.
Shukrani Naibu Spika wa Muda. Ningependa pia kumpongeza Mhe. aliyewasilisha Hoja hii Mhe. "Jicho Pevu". Kwa kweli yeye ni jicho pevu mkakamavu. Mhe. Naibu Spika wa Muda ni wazi kwamba jinsi mienendo na mitindo ya kimaisha inavyobadilika kumekuwa na changamoto nyingi sana hasa za kiafya. Kwangu binafsi tungekuwa na uwezo wa kurudisha masaa nyuma tungelipitisha Hoja hii juzi. Waswahili husema kuwa "Hayawi hayawi huwa." Kwa hivyo ninaonelea kuwa ni Hoja ambayo wakati wake ni huu. Mambo kuhusu afya katika nchi yetu ya Kenya yanatatanisha sana. Kama vile walionena mbele yangu walivyonena: Walalahoi afya yao imeachwa mikononi ya Maulana. Pia Mwenyezi Mungu aliweka tofauti kati ya binadamu na ng'ombe kwa kutupa akili kama ya kutibu ili tuitumie kisawasawa. Ni jambo la aibu kwamba Wakenya wengi wanakatika maisha mapema. Maisha ya wale ambao wanalinda familia zao yamekatika kwa ghafla. Wale wanaowategemea huachwa wasiwe na mbele wala nyuma. Hii ni kwa sababu gharama ya matibabu iko juu sana. Watu wanalazimika kuuza mifugo wao na hata mashamba ili kugharamia matibabu. Isitoshe wagonjwa wanapoaga dunia wanaobaki huwa hawana mbele wala nyuma. Wabunge katika Bunge hili watakubaliana nami kuwa kila Ijumaa tunaitwa katika michango hapa na pale kwa ajili ya kuchangia wagonjwa. Kwa hivyo Hoja hii aliyowasilisha Mheshimiwa "Jicho Pevu" ni Hoja ambayo imewasilishwa wakati bora na itatulazimu tuache shughuli nyingine zote ili tuipitishe; kisha tuhakikishe imetekelezwa. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda jimbo la Mombasa anakotoka mwanzilishi wa Hoja hii ni jimbo ambalo linasifika kwa utalii. Watu wengi ambao wanastaafu haswa wale ambao wanastaafu katika nchi nyingine na wanaathiriwa na baridi ya nchi zao huja kupumzika kule Mombasa. Hawa ni watu ambao wako na taaluma tofauti tofauti wakiwemo madaktari. Tutakapokuwa na hospitali ya rufaa kule Mombasa itasaidia pia watalii wagonjwa. Leo hii mtu akitoka Laikipia akitaka kutibiwa anaingia gari la moshi la Standard Gauge Railway (SGR) ambayo ililetwa na Serikali ya Jubilee moja kwa moja mpaka Mombasa kutibiwa. Kwenda Mombasa si kama kwenda India kutafuta matibabu. Cha kutia aibu sana ni kwamba katika Karne ya 21 akina mama wanakufa kwa ajili ya kujifungua. Katika hospitali zetu za majimbo bado hatujajimudu kuhakikisha kwamba akina mama wanapoleta maisha duniani humu hawapotezi maisha yao. Kwa hivyo tunapozungumzia mambo ya afya ni sharti pia tuelewa kwamba taifa lenye afya ni taifa tajiri. Iwapo wale watu ambao sisi tunaongoza watakuwa wana afya njema basi tutaweza kuwaambia vijana wetu wajitafutie riziki. Wataweza kufanya hivyo bila kuhangaishwa na maradhi. Ni jambo la kutia hofu sana kwamba kila mara tunalia nchi haina fedha ilhali fedha nyingi zinapotelea katika miradi isiyofaa na yenye kufaidi watu binafsi. Hiyo ni miradi ya kuendeleza ufisadi. Ninazungumza bila kusita kwa sababu najua tulitenga fedha katika Bunge hili ili zitumike katika ugatuzi kwa kununua vifaa vya hali ya juu vya hospitali. Vifaa hivyo vilinuiwa kusaidia wagonjwa ambao wanalazimika kusafiri hadi Nairobi kupata matibabu. Kwa mfano kusafishwa damu. Magonjwa kama vile kisukari mpigo wa damu na saratani yamekithiri. Kwa hivyo tuansema hivi: Iwapo kuna fedha zitatengewa masuala ya matibabu basi fedha hizo zitumike vilivyo na kikamilifu kama alivyosema mwenye Hoja. Aliongeza kusema kwamba tumekuwa tukitia gunia pumzi. Baadhi ya majimbo tunapozungumza sasa hivi yamehifadhi mashine zilizogharimu mabilioni ya pesa katika mahospitali. Pesa zilizotumika si kwamba zimetoka kwenye mfuko wa mtu binafsi bali ni kodi ambayo wamelipa Wakenya. Kwa hivyo itakuwa ni aibu kubwa sana kama kuna mashine ya kutibu wagonjwa na ambayo imehifadhiwa katika chumba mahali pasipo kutumika. Kwa hivyo ninapotia tamati ninaunga mkono Hoja hii. Shukrani na pongezi tena kwa aliyewasilisha Hoja hii ambayo tungepitisha jana na wala sio leo. Ninapoenda kukaa ningependa ieleweke kwamba mimi sitoki Pwani; ninatoka bara haswa eneo la Laikipia - Mimi ndiye Mdorobo pekee katika Bunge hili. Mwalimu aliyenifunza Kiswahili katika shule ya upili ya Doldol Bwana Mwangi Motisha sasa ni mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Miamoja; abarikiwe sana. Shukrani.
Shukrani Naibu Spika. Nasimama kuunga mkono Ripoti hii ambayo inasimamia umoja wa uti wa uchumi wa Kenya. Tutakapojenga huo mfereji wa kupitisha mafuta hiyo itakuwa ni njia moja ya kuokoa Wakenya kutokana na ajali nyingi ambazo zinatokana na magari ya kusafirisha mafuta. Pia imeonekana wazi kwamba sharti tuweze kufuata mipangilio ya sheria kwa kuhusisha Mkuu wa Sheria katika mipango ya zabuni za Serikali na miradi tofauti tofauti. Tukifanya hivyo miradi haitatugharimu sana. Tutaweza kuepuka ule ufisadi mwingi ambao umeonekana ukiingilia miradi mikubwa ambayo ni ya ufaa kwa nchi hii na kwa mwananchi kwa jumla. Pia kuhusu huu mradi ninaonelea kwamba tungeweza kuhamazishwa zaidi kuhusu faida ambazo zitatokana na huu mradi. Kwa mfano tungeweza kusikia kwamba mradi huu utaweza kushukisha bei ya mafuta. Bei ya mafuta imetuumiza sana hasa tukichukulia kwa mfano uwanja wa ndege. Kila wakati tunapoambiwa bei ya mafuta imeshuka hakuna wakati tunaambiwa kuwa bei ya tikiti ya ndege imeshuka. Badala yake inaongezeka mara dufu. Kwa hivyo katika mradi huu tuzidi kuangazia vile ambavyo tutaweza kuweka mikakati ambayo itafanya bei ya mafuta iache kupanda kila mara. Hata inaposhuka katika soko ya ulimwengu tubaki na ile bei ambayo sisi wenyewe tunaweza kuihimili na inaweza kumsaidia mwanchi wa kawaida. Pia tuwe waangalifu tunapojenga huu mfereji. Je huu mradi wetu ambao ndio mradi mkuu katika eneo letu la Pwani na unasimamia Kenya nzima ambao ni Kenya Refinery ni vipi ambavyo tunaweza kuifufua Kenya Refenery ili iwe ndio chanzo cha kuwa na mahala pa kuweka mafuta yetu kuliko vile ilivyo wakati huu? Ule mradi mkuu wa refinery umekufa na watu wengi wameachishwa kazi. Ninaunga mkono huu mradi wa pipeline uweze kuendeshwa kisheria.
Shukrani sana Bi. Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii. Ningependa mwanzo nitoe shukrani zangu za dhati kwake mhe Wangamati kwa kuleta Hoja hii. Naiunga mkono Hoja hii kwa maana ni nzuri na imeletwa kwa wakati mwafaka. Upiganiaji uhuru katika nchi yetu haukuwa kazi ya mtu mmoja. Kazi hii ilifanywa na watu binafsi jamii na taasisi mbali mbali. Ili tuweze kujua mambo yalivyojiri kuna maswali ambayo lazima tuulize na tupate majibu. Swali la kwanza ni hili: Ni akina nani walipigania uhuru? Pili katika kupiginia uhuru ni yapi mema na mabaya yaliyotokea? Je hali ya maisha ya wapiganiaji huru leo hii iko vipi? Mwisho ni lazima tujadili masuala ya malipo ya wapiganiaji uhuru. Swali la kwanza nimelijibu. Ukweli ni kwamba kuna jamii mbali mbali ambazo zilipigania uhuru wetu. Tulikuwa na kundi la Mau Mau Dini ya Msambwa na makundi mengine kutoka sehemu nyingine humu nchini. Jamii ya Mijikenda inapatikana katika Mkoa wa Pwani. Katika jamii hii kuna watu ambao sisi tunajivunia kwa kuwa walipigania uhuru na wakatuletea mema. Kwa mfano katika jamii ya Wagiriama kulikuwepo na mama shujaa aliyeitwa Mekatilili wa Menza. Yeye sifa zake zilivuma sana. Historia ya Kenya imemrekodi vya kutosha. Alipigania uhuru lakini hali ya maisha ya jamaa zake si nzuri. Katika eneo Bunge langu kuna mama anayeitwa Mepoho. Nimekumbushwa na mheshimiwa mwenzangu kwamba katika maeneo ya Rabai kulikuwa na mama aliyeitwa Mengao Mose ambaye alikuwa mstari wa mbele kupigania uhuru wetu. Mwingine anayejulikana ni Bi. Mtwana. Wote hawa walihusika. Kando na watu waliopigania uhuru zipo taasisi ambazo zilipigania uhuru. Kwa mfano katika jamii zetu zipo zile Kaya. Hizi ndizo baadhi za taasisi ambazo zilikuwa zikitumiwa na watu kuangalia mambo hapa na pale ili kuhakikisha ya kwamba wamepeana habari ya jinsi mkoloni alivyokuwa anapanga kunyanyasa Wakenya. Taasisi hizi zimeachwa nyuma. Wale wazee ambao wanakaa ndani ya zile kaya wanateseka na taasisi hizi pia zimeachwa nyuma. Zingine zinachukuliwa na watu ambao wanachukua ardhi ilhali serikali tofauti tofauti hazijaingilia kati na kuchukua hatua. Ni kweli watu walienda mahakai na kuna malipo ambayo yalitoka na kuna wale ambao walilipwa na wengine hawajalipwa. Kile ambacho ningehimiza ni kwamba mbali na mahakama Serikali yetu ya Kenya ambayo tuko na ii nayo kwa hakika inaweza kufanya jambo fulani kuhakikisha kwamba familia hizi watu hawa na taasisi ambazo zilipigania uhuru huu pia zinaangaliwa. Jambo hilo likifanyika tutakuwa tumeanza safari nzuri. Kwa kumalizia hata tukiangalia swala la wale waliopigania uhuru ambapo sasa tumekaa hapa na tunaendelea kufaidi kuna baadhi ya mambo ambayo pia hukera. Nakumbuka tukiingia Bunge na nimefurahi kuona Mheshimiwa Mustafa Idd alileta Hoja ya baadhi ya watu ambao husaidia Serikali kufanya kazi yake. Huu ulikuwa ni Mswada kuhusu wazee wa vijiji. Hawa ni watu ambao wanafanya kazi ya kusaidia Serikali hasa za utawala kuhakikisha mambo yanaenda sawa.
Shukrani sana Mhe Spika Hili ni Bunge la heshima Ni mahala ambapo sheria ya taifa inaundwa Ukiona Wabunge wakizungumza kwa hamasa na haa ni kwa sababau Bunge hili limeanza kudharauliwa na baadhi ya Mawaziri katika Serikali Nimesikia Wabunge wakisema ya kwamba kila mara wanapoleta masuala yao mbele ya Wizara hawasikizwi kwa sababu tumedharauliwa Wizara mbili zinazo matatizo sana ni ya Usalama wa Ndani na Wizara ya Uchukuzi Jana nimemsikia Waziri wa Usalama wa Ndani Bw Fred Matiang'i akisema ya kwamba mahakama ni sharti ifanye vile wanataka Huyu Matiang'i binafsi amekataa kuheshimu sheria za hii nchi
Shukrani sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipa fursa ya kuchangia hii Hoja ambayo imeletwa mbele ya Bunge na Mheshimiwa Dr. Susan Musyoka. Ningependa kumpongeza kwanza kwa kuileta na kuwa na fikra nzuri kama hii. Suala la afya kwa Jamhuri yetu ya Kenya kama vile wengi tunavyofahamu ni kwamba baada ya kupitisha Katiba yetu mwaka wa 2010 iliweza kuweka uongozi mara mbili kwanza kwa Serikali Kuu na pili kwa serikali ya ugatuzi. Masuala ya kuwafundisha na labda kuwaongeza ujuzi ndio masuala ambayo yamewekwa katika Serikari Kuu. Serikali gatuzi imewekewa yale masuala mengine ikiwa ni hospitali zile zahanati ndogo ndogo na pia yale masuala yanayohusu afya. Katika kuchangia Hoja hii ni kweli kuna masuala mengi sana ya dharura ambayo yanahitaji kuangaliwa kwa kina. Tumeona watu wetu katika Jamhuri ya Kenya wakipoteza maisha yao kwa sababu kwanza ya ukosefu wa vifaa vizuri katika hospitali hizi na pili pia matibabu ambayo yanastahili ndio waweze kuepuka maafa. Nikichangia Hoja hii nitaangalia mambo mawili. Kwanza hata kabla tuzungumze kuhusu kuleta mafunzo kwa wale wahudumu ambao wanastahili kututibu katika hospitali zetu ni lazima tuangalie ikiwa hospitali zetu ziko na vile vifaa ambavyo vinahitajika. Baadhi ya masuala ambayo yanatokezea kwa dharura mashambani utapata kwamba baadhii ya zile hospitali ambazo ziko kule hazina vifaa ambavyo vinastahili na ambavyo vinaweza kushughulikia masuala ya dharura. Ndio maana wakati mtu anapoumia wakati ambao hali za kighafla zinatokea vile wanavyopelekwa ni rahisi kupoteza maisha yao. Nitatoa mfano katika eneo langu la Kaloleni na eneo lile jirani la Rabai. Unakuta wakaazi wa sehemu hizi wanategemea sana ule mti wa mnazi. Wengi wale ambao ni wajuzi wa masuala ya kugema hasa ile pombe ya mnazi kuna wagema wengi sana ambao kila siku wanapoteza maisha yao kwa sababu ya kuanguka kutoka miti hiyo ya minazi. Hata kabla ya masuala ya bodaboda na magari kutokezea miti ya minazi imekuwa ni baadhi ya sababu ambazo zimeacha watu wengi wamepoteza maisha yao. Lakini kinachostaajabisha katika sehemu hizi ni kwamba hospitali zake bado ziko chini. Ikiwa hatutakuwa na vifaa ambavyo vinastahili basi kila siku tutapoteza watu wetu. Ni kweli kama vile Hoja inavyosema kwamba wengi ambao wataenda kwa hospitali hizo kuhudumiwa kwa mara ya kwanza wanapata watu ambao sio wataalamu katika taaluma hiyo. Ikiwa mtu amekuwa mgonjwa kwa mfano amepata ajali na afike apate mtu ambaye si mtaalamu kwa suala fulani ni rahisi kwa mtu huyu kupoteza maisha yake. Ndio maana ningependa kuunga mkono kwamba kuna haja kweli ya kuhakikisha ya kwamba mafunzo maalumu ya afya ya watu wetu itafanyika hasa kwa madaktari na hata watu wengine ambao wanaweza kutusaidia kwa mambo kama hayo. Mambo haya yakifanyika naamini yatasaidia watu wetu na tutaokoa maisha ya binadamu. Kwa hayo eno machache ningependa kuunga mkono Hoja hii. Shukrani.
Shukrani sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii. Naichukua fursa hii kumshukuru Mhe. Joyce Lay kwa kufikiria kuhusu swala hili. Ninaunga mkono Hoja hii. Ningependa kuungana na wenzangu kusema kuwa swala la lugha ya Kiswahili ni muhimu sana. Kama vile ilivyozungumzwa hapo awali Kipengele cha Saba cha Katiba yetu kimekiweka Kiswahili kama moja ya lugha za kitaifa. Pia Kipengele cha 120 cha Katiba yetu kimesema kuwa baadhi ya lugha rasmi za Bunge ni Kiswahili. Kunao umuhimu wa kuhakikisha kwamba lugha ya Kisawahili imetumiwa vyema na hasa kutafi Katiba yetu na sheria zetu ili kuhakikisha kwamba watu wengi wanaelewa mambo haya. Ukiangalia ndani ya Katiba yetu kuna baadhi ya vipengele ambavyo vimesisitizwa kwamba iwapo kuna changamoto ya lugha ni muhimu pia Serikali ihakikishe kwamba imepeana watu ambao wanaweza kutafi ama wakalii hasa mahakai. Wakati wowote mtu anautata kuhusu lugha ambayo angependa kutumia Kipengele cha 50 cha Katiba yetu kimesema kuwa ana haki ya kuhakikisha kwamba kuna mkalii ambaye amelipwa ndio sheria itafiwe kwa ile lugha ambayo anaelewa zaidi. Umuhimu wa kuhakikisha kwamba lugha ya Kiswahili imetumika ni jambo ambalo ni lazima tuliangalie kwa karibu. Kwanza mawasiliano yatakua mema kati ya wale wote ambao wanahusika katika utumizi wa maswala ya kisheria. Mengi yamezungumzwa hapa kuhusu vile mawakili na baadhi ya watu hutumia lugha hii ya Kiswahili kujiletea utajiri. Nikionekana labda natetea mawakili hawa kati ya matawi yote ya kiserikali yakiwemo hasa mahakama na ambayo hasa mara nyingi utata wa lugha hii hutokea kuna umuhimu wa kuhakikisha kwamba mahakimu wetu mara kwa mara wanapelekwa katika warsha ndio waelewe vile maswala kama haya yanaendelea. Kwa hiyo ningependa kusisitiza kwamba kuna haja ya kuhakikisha kuwa hata askari wetu ambao mara nyingi ndio huwa vianzilishi vya kesi hizi wanafahamu lugha hii. Wakati wanapoandika malalamishi ya washukiwa waiandike kwa lugha ya Kiswahili. Ningependa pia kuungana na wenzangu.
Shukrani sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa niungane mkono na wenzangu kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa hapa na Mhe. Njomo. Hoja hii inazungumzia ushawishi katika masuala ya uandikishaji wa kura. Ukipata fursa ya kuisoma utaona kwamba leo inazungumza kuhusu kushawishi watu kuchukua kura na baadaye pia waweze kuhusika katika uchaguzi mkuu bila shaka hapo Agosti mwaka huu. Jinsi tunavyojadili Hoja hii ni lazima tuiangalie mara mbili. Kwanza kwa sasa vile tutazungumza na watu mpaka wachukue kura na bila shaka baadaye njia gani zitatumika ili waweze kuhusika katika uchaguzi mkuu. Ninasema haya kwa sababu nimeona sana wengi wa Waheshimiwa wakizungumza tu juu ya suala la kushawishi watu kuchukua kura. Baadaye ni lazima washawishiwe jinsi gani watakaoweza kupiga kura. Kura kuweza kupigwa ni lazima kuwe na vitambulisho. Na inahuzunisha kwamba mara nyingi katika Jamhuri yetu ya Kenya utoaji na usajili wa vitambulisho umekuwa duni sana. Ni juzi tu Mhe. Rais aliona atafute mbinu ambayo inaweza kufanya jambo hili lifanyike kwa haraka. Ni vyema lakini ilikuwa imechelewa. Kwa hivyo ningependa kutoa mwito kwamba suala la uandikishaji wa vitambulisho liwe linafanywa kila wakati na suala linafanywa bila kuwa na gharama yoyote. Watu wetu wengi hawajachukua vitambulisho hivi kwa sababu mahali vinachukuliwa ni mbali na ni gharama kupata stakabadhi hizi. Baadhi ya vitambulisho hivi pia vimekuwa vikifika katika vituo kwa machifu na mahali kwingine vikiwa na makosa fulani fulani. Ningependa kusema ya kwamba wale ambao wanasajili vitambulisho hivi ni muhimi wawe waangalifu ndio tusiweze kuwa na majina ambayo hayaeleweki wakati watu wanapopewa vitambulisho hivi. Siasa ama upigaji kura ni ushawishi. Kwa hivyo ikiwa Hoja itazungumza kuhusu kuwashawishi watu wachukue kura tunaelekea sawa. Kwa sababu hiyo ni lazima tukubali kwamba jukumu la kushawishi watu wachukue kura ni letu kama wanasiasa hasa Wabunge na ni jukumu la vyama vya kisiasa. Ndio maana mimi nikiwa naongoza chama changu cha KADU- Asili nimekuwa mstari wa mbele kuzungumza na watu kwamba ni muhimu kuchukua kura. Nataka nichukue fursa hii hapa katika Bunge hili la kitaifa niseme kuwa kuna umuhimu watu wachukue kura hususan watu wetu kutoka Mkoa wa Pwani na Kaunti yetu ya Kilifi ndio wafanye uamuzi wa busara. Kumekuwa na changamoto nyingi sana katika masuala haya ya kuchukua kura. Kaunti yetu ya Kilifi kwa mfano imegonga vichwa vya habari kwa suala la baa la njaa. Suala hili la ukosefu wa lishe limechangia kwa kiasi kikubwa watu kutochukua kura katika Kaunti yetu ya Kilifi. Nataka nizungumze tu bila wasiwasi kuwa Serikali iko na jukumu la kuja na mbinu ya kuhakikisha kwamba watu wanaweza kupata lishe. Wakipata lishe wataweza kuhusika katika hali kubwa ya kuweza kuchukua kura hizi. Haimaanishi watakapopewa lishe ndio lazima watapigia kura mrengo fulani. Hayo yatakuwa masuala ya baadaye. Kwa hivyo saa hii ni kuhakikisha kwamba mbinu zimebuniwa watu wachukue kura. Si vyema kweli kuambatanisha huduma ambazo watu wanastahili kupewa na masuala ya kama wako na kadi ya kura ama la. Kifungu Nambari 38 katika Katiba yetu kinazungumza kuhusu watu kusajiliwa kama wapiga kura na hatimaye kupiga kura zao. Ukiangalia Katiba yote kwa ujumla iko na haki nyingi sana za kikatiba. Kwa hivyo kwa mtazamo wangu ninaona ya kuwa tukizungumza kwamba mtu hajapiga kura ikifika masuala ya kuchukuliwa wanajeshi ama watu wanaandikwa kwa ajira fulani eti watu hawa wasiweze kupata fursa hiyo sio sawa. Nasema haya kwa sababu wakati uchaguzi unapofanyika na wakati kura zinapopigwa hali inarudi sawa na Serikali inahitaji kutoa huduma kwa mtu bila kubagua kama alipiga kura ama hakupiga au alikupigia kura ama hakukupigia kura. Ni jukumu lako kama kiongozi kumhudumia kwa njia mwafaka ndio maana yeye ni mwananchi wa Kenya na anaongozwa na Katiba ya Jamhuri ya Kenya. Baadhi ya mikakati imewekwa kuhakikisha kwamba kura zinachukuliwa. Tumekuwa tukisisitiza kwamba ni lazima kura ziandikishwe kila mahali. Tumeona vijana wetu wa boda boda wametia juhudi na nimeona pia baadhi ya watu wanaosajili kura wamejitoa kutoka yale mashule waliokuwa wamekita kambi kuhakikisha ya kwamba wanasajili. Safari hii tunawapata wakiwa katika mahali pa kufanya biashara. Bila wasiwasi Jumapili iliopita mimi pamoja na Mhe. Njomo tulipata fursa ya kwenda katika mazishi ya mamake Mhe. Harry Kombe. Mhe. Njomo atakubaliana nami kuwa katika mazishi haya kulikuwa na sehemu ya kusajili watu kura na watu baada ya kuangalia mwili walikuwa wanaenda kukamata kura jinsi wanavyotaka kujishughulisha katika upigaji kura. Mtu yeyote ambaye atazungumza kuhusu kutolazimisha watu kuchukua kura itakuwa makosa. Sisi kama wakaazi wa Pwani mara nyingi masuala kama haya hayajaenda sawa kwa sababu watu wamesema eti kura zetu ni chache. Ninataka niwahakikishie kuwa safari hii mambo yamegeuka. Watu wataendelea kujiandikisha kura kwa sababu pia nasi tunataka kuongeza uzito wetu katika masuala ya kisiasa ya kitaifa. Kwa hivyo Hoja hii ni muhimu. Kamati ambayo inahusika katika masuala ya kisheria iko na wajibu wa kukaa chini na kuibua mbinu ambazo zitatusaidia kwa muda huu mfupi na nyingine kesho kesho kutwa na kuendelea. Suala la kura sio suala tu la leo. Baada ya uchaguzi labda kutokana na malalamishi ama mambo mengine kuna uwezekano wa kuwa na uchaguzi mdogo. Ikiwa usajili wa kura utakuwa unafanywa mara moja hivyo haitakuwa vyema. Kwa hivyo ninataka niungane mkono na waheshimiwa wengine ambao wamesema kwamba usajili ufanywe kila wakati. Vitambulisho vitolewe kila siku na usajili wa kura uendelee kila siku. Cha msingi tunahitaji kuwaeleza watu wetu umuhimu wa kupiga kura. Mambo yalivyo sasa hivi watu wanazungumzia zaidi kuhusu idadi ya watu wanaosajiliwa. Labada demokrasia yetu pahali ipo inazungumza tu kuhusu idadi ya kura lakini bila shaka kadri miaka inavyosonga tutafika mahali na tutajua ni akina nani wanastahili kupiga kura na wasiostahili kupiga kura. Kwa lugha ya Kiingereza tunataka tufike mahali tutakuwa na quality voting. Hatutaki iwe kwamba kwa sababu lazima ipigwe kura basi watu wapige kura. Mara nyingine watu hupiga kura na hawajui kitu gani ambacho wanatafuta. Kwa hivyo hii ni Hoja muhimu. Ninaiunga mkono na zaidi ya yote nihimize watu wangu waweze kukamata kura ndipo tuweze kuhusika katika uchaguzi mkuu ujao. Kwa hayo machache asante kwa kunipa fursa hii.
Shukrani sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia Hoja hii ambayo imeletwa na Mheshimiwa mwenzetu. Ninampongeza mheshimiwa kwa kuwa hii ni Hoja muhimu kwa maisha ya Mkenya. Ningependa kumpongeza kwa kuwa ametambua kwamba ni wachache wametambulika katika kufidiwa na wakoloni. Kwa kweli upiganiaji wa Uhuru haukuwa katika sehemu moja ya Kenya hii; ulikuwa katika kila pembe za nchi hii. Kwa sababu ya hali ya umaskini uliowakabidhi watu wetu katika maeneo mengine mpaka sasa hawajaweza kwenda kortini ili kutetea haki zao. Ni wajibu wa Serikali kusimama kidete kuwatetea Wakenya. Ninamshukuru mheshimiwa kwa kuwa ameweza kuyataja maeneo husika lakini kwa uchache ningependa pia kuwataja mashujaa kutoka sehemu ya Kwale maana kunao walioweza kujitokeza na kupigania uhuru wa nchi hii; kwa mfano Mzee Bilashaka Mzee Mwamgunga Mzee Mbembe Mzee Bambaulo na nyanya yangu ambaye alikuwa mpishi wa wapiganaji wa Mau Mau . Mababu zangu pia walikuwa wapishi wa wapiganaji wa Mau Mau . Kuna Mzee Munyambu Mbaa Kivanguli kutoka Ukambani ambako ndiko kwenye usuli wangu kwa upande wa babangu. Kuna Mzee Mwamgogo Mzee Jerui na Mama Mekatilili ambaye alitoka sehemu za Ugiriama. Hao ni miongoni mwa wale ambao waliweza kututetea. Wako wengine wengi ambao hatuwajui. Ni wajibu wetu sisi kama Waheshimiwa kwenda mashinani na kuleta rekodi kamili kwa maana kila mmoja wetu anamjua ni nani aliyeweza kusimama kidete katika sehemu yake ya uwakilishi na kutetea haki za Wakenya. Baadaye tunapaswa kuwa na kamati maalumu ambayo itaisukuma Serikali yetu ili iweze kuwatetea watu wetu ili waweze kupata haki yao. Hata kama watu hao wameshakufa wameacha watoto na wajukuu. Hatutakwenda tukamfukue mtu ndiyo aje aseme kwamba aliteswa lakini tunawajua wale ambao waliteseka. Kwa hivyo ni wajibu wetu kama Waheshimiwa kuchukua rekodi na kusimama imara kuwatetea hao ndugu zetu. Kutambuliwa tu kama mashujaa haijatosha. Baadhi yao hawatambuliwi kamwe kama mashujaa. Wapeni kitu familia zao ishikilie na ishukuru Mwenyezi Mungu kwamba kutoka na kizazi chao wameweza kunufaika katika familia yao. Hoja aliyotuletea Bungeni mheshimiwa huyo siyo kana kwamba aliumia peke yake lakini Mwenyezi Mungu amemuwezesha na kumpa moyo ili aweze kuileta Hoja hii Bungeni. Sisi kama Waheshimiwa tunaiunga mkono. Kwa niaba ya watu wa Kwale ninampongeza na kumshukuru. Tuendelee kushikana mpaka Mkenya apate haki yake. Haki bado haijatendeka kwa wale ambao walipigania uhuru wa nchi yetu. Kuongezea kuna maovu yaliyotendwa baada ya wakoloni kuondoka. Tunataka hayo maovu pia yafuatiliwe haswa upande unaohusika na masuala ya ardhi. Suala la ardhi limeumiza watu. Mpaka sasa tunaishi kama maskwota licha ya kwamba tunasema tuko katika Kenya huru. Kwa hivyo tunaiomba Wizara inayohusuka na masuala ya ardhi pamoja na Tume wajikakamue zaidi. Pesa tulipitisha tukawapatia. Tunachotaka ni kuona kwamba ardhi yetu imeregeshwa na ardhi yenye utata ishuhulikiwe ili mwenye ardhi apewe ardhi yake bila kucheleweshwa. Ahsante sana tunaishukuru Serikali yetu na kumshukuru sana mheshimiwa mwenzetu kwa kuileta Hoja hii Bungeni. Kwa hayo machache ninaiunga mkono Hoja hii.
Shukrani sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii. Asante sana Mhe. Mucheke kwa kunipatia pia fursa hii niweke sauti yangu kuhusiana na masuala haya ya saratani. Nitasema kwa ufupi kwamba namshukuru Mhe. (Daktari) Tum kwa kuleta Hoja hii. Huu ndio wakati mwafaka wa kuongelea masuala ya saratani kwa sababu tumepoteza wenzetu kwa sababu ya saratani. Kila mtu apimwe saratani; sio vijana ama wasichana pekee. Hata wazee na akina mama wapimwe pia. Serikali inafaa iwekeze zaidi kwa masuala ya saratani ili tuweze kupata madaktari na wauguzi wenye ufahamu wa mambo ya saratani na tuwe na vifaa thabiti vya kuweza kutusaidia katika matibabu. Pia kutengwe pesa kwa ajili ya.
Shukrani sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza naomba kumpongeza Mheshimiwa Joyce kwa sababu ya hii Hoja aliyoileta. Kusema ukweli shida tuliyonayo Kenya ni kuwa sheria tukonazo nyingi lakini utekelezaji ndio shida. Ikiwa tuliweza kukipitisha Kiswahili kiwe lugha ya Taifa tangu enzi za Raisi aliyestaafu Mheshimiwa Moi na mpaka leo hakijatiliwa maanani tungependa tujiulize: Shida iko wapi? Pia tuangalie jinsi ambavyo tunaweza kuirekebisha shida hiyo ili Kiswahili kiweze kutumika hata kwenye chupa za dawa. Maelezo yawe yameandikwa kwa Kiswahili ndio yule mama kijijini asiweze kumpatia mtoto wake dawa kipimo cha zaidi. Ninaunga mkono Hoja hii kwa sababu mengi tunayoyazungumza hapa Bungeni ni yanayomhusu mwananchi kule nyanjani. Lakini je ni wote wanaoelewa kile ambacho tunakizungumza kwa Kizungu? Hata wakati tunapokwenda kutafuta kura zetu sidhani kwamba tunazitafuta kwa kuzungumza Kiingereza. Tunaomba kura zetu hususan kwa kutumia lugha yetu ya taifa. Kwa hivyo hii Hoja itaweza kutusaidia sio sisi tu kama Wabunge kuweza kueleweka kule nyanjani bali pia wananchi ambao wanajua kukizungumza na kukisoma Kiswahili lakini hawawezi kukitafi Kiingereza kwa lugha ya Kiswahili. Ukiangalia katika korti zetu utakuta mtu amehukumiwa na hajui amehukumiwa kivipi. Hata namna ya kuweza kuibadili ile hukumu anashindwa. Inaishia mtu huyo kutozwa pesa nyingi sana na mawakili bila kujielewa kwa sababu ataelezwa mambo ambayo si ya kweli. Lakini kwa vile anatafuta haki yake anakubali na mwisho inaishia kuwa atafungwa licha ya kwamba ametoa pesa nyingi kwa mawakili waliomwambia kwamba wakibadilisha sehemu fulani watapata haki yake. Kwa hivyo ninaunga mkono Hoja hii na nina ii na Waheshimiwa licha ya kwamba tutaweza kubadilisha mipangilio yetu ya Bunge iweze kuandikwa kwa Kiswahili tuanzie hapo na tuweze kuona pia hata masomo katika shule zetu kama vile Jiografia na Agriculture zimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Hii ni ili tuweze kuelewa lugha hizi zote na tuweze kutumia haki zetu tukiwa tunaelewa haki zetu tunazitumia kwa njia gani. Ningependa nikomee hapo kwa sababu naona muda hauturuhusu kuzungumza sana na kila Mheshimiwa anataka kuchangia Hoja hii. Shukrani.
Shukrani sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Langu ni kuunga mkono Hoja hii na kupendekeza kwamba Wizara ya Elimu. Sayansi na Teknolojia iweze kuhakikisha kwamba walemavu wana nafasi katika taifa hili. Sisi Wabunge tunapata shida sana wakati tunapotembelewa na Wakenya wenzetu ambao ni walemavu katika afisi zetu. Ninakotoka katika Kaunti ya Mombasa kuna visa kama hivyo vingi sana katika afisi yangu. Ni vigumu kuwasaidia kwa sababu Serikali haijaekeza wala kuwafikiria watoto walemavu hasa upande wa kuwapatia elimu bora katika shule za chekechea msingi upili na hata chuo kikuu ili waweze kupigania nafasi zao kama Wakenya wengine. Mighairi na hayo vile vile tunaomba wawe na hospitali zao ambazo zitaweza kukimu mahitaji yao. Kwa sababu ukiwaweka pamoja na Wakenya wengine wa kawaida wasio walemavu patakuwa na matatizo chungu nzima. Shule ambazo zipo nchini kuwahudumia ni chache sana. Mimi ninajua shule mbili pekee. Ile Shule ya Thika ya vipofu na Joy Town ambayo iko Kisumu. Sharti tuwe na shule spesheli katika kila kaunti ili tuweze kusaidia hawa walemavu ambao ni Wakenya wenzetu. Demokrasia tunayopigania ni ya kuleta usawa kwa kila Mkenya. Hizi shule zinahitaji walimu na bajeti. Waalimu ni haba. Ni kweli kwamba waalimu wanaoweza kukidhi mahitaji ya hawa wanafunzi ni wachache mno. Ni lazima Serikali ihakikishe kuna walimu wanapokea mafunzo spesheli ya kuangalia watoto hawa. Ningetaka Serikali itoe bajeti kubwa sana kwa walemavu kwa sababu hawana nguvu kama Wakenya wengine. Wawekewe bajeti ambayo itawafaa. Ninaposema bajeti ninazungumzia suala kama karo na basari ambazo tunapeana kwa shule zetu. Wahakikishiwe kuwa bajeti yao imeongezwa kwa sababu wao ni tofauti kabisa. Vitu ambavyo wanahitaji ni tofauti na vitu ambavyo Mkenya wa kawaida anahitaji. Pia tuwekeze katika mambo ya michezo. Tusiseme tu shule bali tuwekeze katika shule hizi na tuangalie kwamba zinapata vifaa spesheli ambavyo pia Wakenya wengine wanapata katika shule mbalimbali. Wazo langu ni kwamba wakati ambapo shule zinaundwa ni vyema pia wao tuwawekee nafasi ya kuhakikisha wanajihisi kama Wakenya wengine ili waweze kuendelea na maisha kama Wakenya wengine. Naunga mkono Hoja hii na ninaifurahia. Mbunge aliyeileta nampa kongole na kusema kwamba nitasimama na Hoja hii. Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Shukrani sana Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii. Nataka kuunga mkono mapendekezo katika malalamishi haya. Mwanzo kwa sababu katika benki za kiislamu sheria zake huwa ni za kiutu zaidi. Nakubali kuwa baadhi ya senti za Serikali hazitaharibika zikiwekwa katika benki kama hizo. Pesa za Serikali pia hazitaliwa ovyo ovyo na benki zenye kulaghai watu na benki zenye tamaa ya kula pesa za Serikali ambazo zinahitajika kutumika kwa wananchi humu nchini ambao wana shida nyingi. Jambo lingine ambalo nakubaliana nalo ni kuweka vikwazo katika asilimia ya pesa ambazo Serikali kuu inaweza kuchukua kama mkopo kutoka benki zozote. Kiwango cha asilimia tano ya bajeti ya nchi - kama nimeelewa sawa - ni jambo nzuri sana. Hivi sasa tunajua Serikali kuu imechukua madeni makubwa ambayo yatatulemea sisi na vizazi vijavyo. Kwa hivyo kutunga sheria ambayo itaizuia Serikali kuu kukopa kupita kiwango fulani itakuwa jambo la busara. Ahsante.
Shukrani sana Mhe. Spika wa Muda. Labda kwa kuhitimisha katika Hoja hii ya siku ya leo ambayo imechangiwa vilivyo kwanza kabisa nawashukuru Wabunge wenzangu walioweza kuchangia na wale wote ambao walikuwa wanataka kuchangia lakini muda haukuwaruhusu. Ningependa pia kuwaambia kuwa Hoja hii ni ya taifa. Asilimia 80 ya Wakenya wana matatizo ya afya. Hoja hii bila shaka itakapofaulu na kufanywa sheria itaweza kuhakikisha ya kwamba kila kaunti nchini Kenya imepata hospitali ya Level 6 ama hospitali ya rufaa. Tumeweza kutoa takwimu mbalimbali na kuonyesha ni kwa nini tunahitaji hospitali hizi. Rais Uhuru Kenyatta mapema mwaka jana alisema ya kwamba anatoa pendekezo la kujengwa kwa hospitali katika kila kaunti. Kwa wale ambao waliingia wakati ambapo nilikuwa nikiendelea ama walichelewa kuingia niliwapatia mifano mbalimbali na kuwaambia ya kwamba sisi tunaenda kinyume na Shirika la Afya Duniani (WHO). Shirika hilo linasema kuwa daktari mmoja anapaswa kuwashughulikia wagonjwa 1000. Hapa Kenya daktari mmoja anawashughulikia wagonjwa 10000. Watu wanaumia sana. Tunazidi kumaliza kizazi. Tunazidi kuhakikisha ya kwamba watu wetu wanazidi kuumia badala ya kuwawakilisha katika Bunge. Tunawawakilisha katika mambo mengine yasiyo na maana. Naomba Bunge hili liweze kupitisha Hoja hii na kujua ya kwamba tuko tayari kukataa kuongeza majeneza Kenya ili tupunguze mzigo huu. Ningependa kuwapongeza akina mama Wabunge wenzangu ambao mara kwa mara nawaona kwenye runinga wakati ambapo mama amepigwa katika visa vya nyumbani ama amebakwa wanakimbia katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta kusimama naye. Leo nawataka msisimame nyuma ya mama huyo lakini msimame nyuma ya hospitali ili huyo mama asipate shida kutolewa Wajir mpaka Nairobi mbali apate huduma hizo hapo. Kwa hivyo naona muda ndio huo umefikia kikomo. Langu nikusema tu asanteni sana na natumai idadi ya madaktari itaongezeka na hospitali zitajengwa. Kwa Wabunge wote nasema asanteni sana na Mungu awabariki. Shukrani Mhe. Spika wa Muda.
Shukrani sana mhe. Spika. Nasimama kuunga mkono Hoja hii lakini kabla sijaunga mkono ningependa kuhimiza kwamba Hoja hii Katika Kamati hii ambayo itawachunguza Mawaziri tungetaka tuwe na watu ambao hawakukataliwa na wananchi. Wale waliokataliwa na wananchi ni wazi kwamba hawataweza kutekeleza matakwa ya Wakenya. Kwa hivyo mtakapokuwa mnatuletea majina hapa na maoni haya pia yamfikie Mhe Rais wetu tunahitaji wale ambao hawakukataliwa na wananchi; tunataka wapewe nyadhifa za kuweza kutufanyia kazi katika Kenya na sio kuwa Mawaziri peke yake. Tunataka hata katika ubalozi na tume zote tupate watu ambao ni wapya na tuanze nao kazi. Asante sana mhe. Spika. Naunga mkono.
Shukrani sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii kuchangia Hoja hii muhimu sana. Nataka kumshukuru Mheshimiwa Nooru kwa kuleta Hoja hii hapa Bungeni. Hili jambo limenitamausha sasa kwa kiasi cha wiki nzima. Nimehuzunika kusikia na kuona jinsi watu wanavyoteseka katika kaunti yangu ya Kwale. Hili jambo halijaanza jana juzi wala wiki jana. Hii mvua ilipoanza miezi kadhaa iliyopita ilikuwa chache sana na kulikuwepo na dalili ya ukame. Kuna akina nyanya ambao hawajawahi kuenda shule lakini walitabiri kwamba mwaka huu kutakuwepo njaa. Itakuwaje wataalamu ambao wameandikwa kazi na Serikali hawawezi kujua kama huu mwaka kungekuwa na ukame? Hivyo tungejitayarisha mapema kwa chakula na maji. Mimi nimezunguka sehemu za Kaunti ya Kwale. Katika wadi ya Puma nilipata wanawake wakanieleza kuwa kuna njaa. Wao huamka asubuhi lakini hawana chai wala chakula. Wao hushinda hivyo mchana kutwa bila chakula. Ifikapo jioni bado huwa hawajala chochote. Wana watoto wadogo. Ni ajabu kwamba mtoto wa miaka miwili au saba anaishi bila chakula! Saa hizi hamna chakula kwa sababu mvua haikutosha. Mahindi hayakupatikana. Maji hayapo na yakipatikana ni mwendo mrefu sana. Lakini watu wanaenda wakiteka maji ya chini ambayo ni machafu. Hivyo ndivyo wanasukuma gurudumu la maisha. Hivi sasa yale maji ya chini yamekauka kabisa kwa hivyo hawana njia yoyote ya kupata maji safi. Bila shaka kama hakuna mtu ama shirika lolote ambalo limeenda kujua kama kuna watu wamefariki kwa sababu ya hili janga nina hakika watu wamefariki maanake wiki zilizopita nilienda nikaonana na watu wagonjwa wanaomeza dawa lakini hawana chakula. Bila shaka kuna watoto na wengineo ambao wameathirika . Pia nimepata habari kutoka kwa Wadi ya Kasemeni ya kuwa Serikali ya Kaunti imejenga sehemu za akina mama kujifungulia katika zahanati lakini zahanati hazina maji. Hivi sasa nimeambiwa kuna wanawake wanajifungua watoto na hakuna hata maji ya kuosha mtoto. Vile mama alivyojifungua ndio vile anarudi aende mpaka nyumbani kwa sababu hakuna maji. Hivi sasa mifugo; ng'ombe mbuzi na kadhalika wanafariki kitu ambacho ni mali ya hawa watu wa Kwale ambao wanaishi sehemu za Kinango Lunga Lunga na baadhi ya sehemu za Matuga. Hata mvua ikija watakuwa wamepata hasara sana. Ninashangaa kama chama chetu cha ODM kimeweza kutetea ugatuzi ukaja tukafaulu na ukapita kuna shida gani? Pesa zimetolewa na Bunge za Seneti na Taifa na Bunge hili letu wamehakikisha kuwa senti zinafika kaunti lakini miaka mine sasa kaunti hazijaweza kufanya miradi ya kudumu katika hii sehemu. Kuna sehemu zina maji lakini zingine zina ukame zaidi. Ingekuwa vyema hizo kushughulikiwa. Saa zingine wanalaumu kuwa maji ya sehemu ya chini yana chumvi lakini saa hii tunajua ya kuwa kuna tecnolojia za kuweza kutoa chumvi kwenye maji. Hivi sasa afadhali maji ya chumvi kuliko kukosa maji kabisa. Kitu kingine wanachosingizia wanasema pesa nyingi inatumiwa kwa maji ya pipe .
Shukrani sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa nafasi hii. Ningependa kuuliza ikiwa ni haki kweli kwa Mbunge huyu kuita Wabunge wenzake watoto wa darasa la kwanza? Ni haki kweli? Je inaruhusiwa katika Sheria za Bunge?
Shukrani sana Mheshimiwa Spika kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kuunga mkono Mswada huu. Kwenye Mswada huu kuna baadhi ya vipengele ambavyo ni lazima nivisisitize. Katika Kifungu cha 34 inaonekana kwamba lugha ambazo zitatumika katika Mahakama Kuu ni Kiingereza na Kiswahili. Mambo haya pia bila shaka yatakuwa na changamoto zake. Moja ya changamoto hizo ni kwamba miongoni mwa wale watakaotumia mahakama hizo haswa majaji wetu kutakuwa na umuhimu wa kuhakikisha kwamba wanapata mafunzo mwafaka ya lugha yetu ya Kiswahili. Ijapo Kiswahili ni lugha kongwe mara kwa mara mambo hugeuka. Ili kesi ziweze kusikizwa na kutatuliwa vizuri katika mahakama zetu kuna umuhimu wa kuhakikisha kwamba maafisa watakaotekeleza majukumu hayo watapata mafunzo mara kwa mara. Mhe. Spika ni wazi kwamba katika kila kaunti ya Kenya kuna umuhimu wa kuwekwa mahakama. Hii itasaidia wengi haswa waliokuwa wanaenda safari za mbali kutafuta haki. Ikiwa mambo haya yatakuwa na ninaamini yatakuwa kwa sababu tayari tumeona yakitendeka wananchi wetu katika Jamhuri ya Kenya hawatakuwa na matatizo ya kutafuta haki. Jambo lingine ningependa kugusia ni lile ambalo Waheshimiwa wenzangu wamegusia haswa kuhusu utatuzi wa kesi Vile sheria yetu ilivyo na hali ya utatuzi wa kesi katika Kenya ni kwamba yule ambaye atakuwa ameshinda ameshinda na yule ambaye amepoteza kesi huwa ashapoteza. Lakini ikiwa kama vile ambavyo kifungu cha 26 kimezungumzia kwamba kutakuwa na nafasi ya mahakama kuleta mawiano ambapo watu watakaa chini na wazungumze ili waweze kutatua kesi ni mambo ambayo yatasaidia wengi haswa wale wenye matatizo. Kifungu cha 26(3) kimezungumzia utumiaji mbinu ambazo ni za kitamaduni kutatua mizozo. Tunajua wazi kwamba katika Jamhuri yetu ya Kenya katika mahali ambapo watu wanaishi kuna baadhi ya mambo yanaenda kulingana na tamaduni za mahali hapo. Itabidi watu kukaa chini na kuona wale wataalam katika hali hizi wataweza kushughulishwa vipi katika masuala haya ndiyo mizozo iweze kutatuliwa. Hili ni jambo muhimu kwa sababu mara nyingi utaona kwamba kesi zinafika mahakai na kuna vipengele fulani ambavyo hutumiwa na unaona labda mtu amepoteza kesi ilhali mtu yule alikuwa na uhakika fulani. Mhe. Spika jambo lingine ambalo limesumbua hali ya haki katika Jamhuri ya Kenya ni wingi wa kesi. Mara nyingi unapata watu wanaenda mahakai wakitafuta haki lakini kesi zinazidi kuahirishwa mara kwa mara kwa sababu ya ukosefu wa majaji au sababu zingine. Ikiwa leo hii sheria yetu ambayo tuko nayo tunazungumzia kuhusu majaji kama 200 na wasaidizi wa mahakama ambao wanaweza kusaidia katika suala hili ikiwa mambo haya yote yatapita yatatusaidia vilivyo kuhakikisha kwamba haki inapatikana na haki inafaa kupatikana mapema. Sina mengi ya kuzungumza lakini ningependa kusema kwamba huu ni Mswada mzuri. Ni muhimu tuunge mkono upite ndiyo hatimaye wananchi waweze kupata haki zao. Shukrani sana Mhe. Spika.
Shukrani sana Mheshimiwa spika kwa kunipa fursa hii. Ningependa kuwaunga wenzangu mkono na kuungana na taifa nzima kwa ujumla kutoa rambirambi zetu kwa marehemu Mariam Kighenda na mtoto wake Ada. Licha ya hayo umesema ya kwamba utatutengea muda tuzungumzie jambo hili kwa sababu iwapo hakutakuwa na suluhu tutakuwa na matatizo chungu nzima katika siku za usoni. Kwanza kabisa inaelekea kuwa siku ya tatu Serikali ikiwa imenyamaza na kuangalia tu bila usaidizi wowote. Leo Waziri wa Uchukuzi amemuamrisha Katibu wa Kudumu katika wizara afike pale na kusaidia katika shughuli za kupata maiti. Pesa nyingi zimetolewa katika Huduma ya Kenya Ferry . Karibu Ksh78 milioni zimetolewa kuweka CCTV ya kuangalia kwamba iwapo kutatokea janga lolote wao wanakuwa wa kwanza kuona matatizo hayo. Kwa kumalizia safari hii Serikali imefeli. Vifo vya Mariam na mtoto mdogo Ada vimesababishwa na Serikali ya Jamhuri ya Kenya. Ni sharti Serikali ilipe familia ya waathirika na vile vile iwajibike kuhakikisha ya kwamba kivukio cha ferry hakitadhuru mtu yeyote katika siku za usoni. Watu watatu ndio wanafaa waelezee taifa hili jambo hili limetendeka vipi. Wa kwanza ni Bakari Gowa Mkurugenzi Mkuu wa Kenya Ferry Brigadia Mstaafu Vincent Naisho Loonena ambaye ni Director General wa Kenya Coast Guard na Meja Generali Levi Franklin Mghalu Kenya Navy Comder . Hawa ni watu ambao wana uwezo. Walikuwa karibu na wangeokoa mtoto huyo mdogo mwenye miaka minne na mamake. Ilichukua takriban dakika 20 watu hao kutafuta usaidizi pasi na kuupata. Kifo cha Mariam Kighenda na Ada kimesababishwa na Serikali ya taifa na ni sharti walipwe. Shukrani.
Shukrani sana Mheshimiwa Spika. Kwa niaba ya wakaazi wa Eneo Bunge la Nyali familia yangu ninatoa risala za rambirambi kwa familia ya hayati Daniel Toroitich arap Moi. Hakika atakumbukwa kwa mambo mengi mazuri na tunamuomba Mwenyezi Mungu amfutie dhambi zake na hata za i na amlaze pema panapolazwa wema.
Shukrani sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii niweze kuchangia mjadala huu. Kwanza ningependa kumshukuru Mhe. Mohamed Ali kwa kuleta Hoja hii ambayo inamgusa kila mtu. Tukiongea eno ya siha ama afya ni jambo linalomlenga kila mwananchi wa Kenya. Sitaki kurudia eno yaliyosemwa na Wabunge wenzangu lakini kabla sijachangia sana ningependa kumkosoa Mhe. King'ara aliyesema Rais Kenyatta ni Rais wa Jubilee. Rais Kenyatta ni Rais wa Kenya na chama cha Jubilee ndicho kilichompeleka mbele akawa Rais. eno ya chama sasa yameisha na sisi tuliokua upande huu tumekaribiana sasa. Watu wa Jubilee mjue sasa Rais ni wa Kenya. Nikirudia Hoja iliyoko mbele yetu ningependa nikubaliane na Mhe. Ali ila nitapendekeza marekebisho machache. Kwa mfano nitataka arekebishe Hoja kwa kusema 'Hospitali ya Mombasa ya Rufaa na Mafunzo' kwa sababu kuna vyuo vikuu Mombasa ambavyo vinasomesha mafunzo ya afya. Juzi tuliona madaktari wakifanya makosa kwa kumpasua kichwa mtu ambaye hakufaa kupasuliwa. Lazima pia tutilie mkazo masomo ya afya. Haiwezekani kuwepo mafunzo ya afya bila kuwepo maabara na hospitali za mafunzo. Nakubaliana na Hoja hii kwa sababu gharama ya kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi kama vile India Tel Aviv. Tunayo habari kwamba aliyekuwa Rais wetu yuko Tel Aviv. Hivi juzi kiongozi wa chama chetu cha Wiper alikuwa ujerui akakaa kule kwa miezi kadhaa. Tunajua kwamba ni wengi wetu ambao wamekuwa wakienda nchi za nje kutafuta matibabu. Naomba tutengeneze hospitali zetu za rufaa hata kama watalaamu hatuna wengi tuwalete kutoka nchi za nje tuwakodeshe kwa miezi au miaka kama tulivyokodesha vifaa vya kutibia ugonjwa wa saratani. Labda ule muda uliyopeanwa wa kukodi vifaa vile ufupishwe na ukiisha tuangalie namna ya kununua vifaa vyetu. Hii ni kwa sababu nimeelezwa kwamba hata vifaa vidogo vidogo kama makasi sharti tuvinunue sasa. Kwa hivyo ningeomba turekebishe namna ya kukodesha vifaa vya kutibu saratani. La mwisho nimeiskia kutoka kwa wale Wabunge waliokuwa Bunge la 11 kuwa kuna Hoja na sheria nyingi zilipitishwa kama vile Mhe. Mwadime na Mbunge wa Meru walivyosema. Naibu Spika wa Muda ningeomba kama inawezekana uitishe hiyo Miswada ama Hoja ili tuchukue likizo ama nafasi tuzizungumzie na tuipe ile kamati tekelezi jukumu hilo. Mwisho kabisa ningependa kuwashukuru wanafunzi wa Shule ya Upili ya Kamuwongo ambao wametembelea Bunge hili leo. Ni shule katika eneo langu la Bunge. Hao ni viongozi wa kesho watakaokuwa Wabunge kama mimi. Asante sana Naibu Spika wa Muda.
Shukrani sana Naibu Spika wa Muda. Nakushukuru kwa kunipa fursa ili niweze kuchangia swala hili ambalo tunaliongea hapa na ni swala kuhusu Hotuba ya Rais. Ninataka kusema ya kwamba Hotuba ya Rais ilikuwa sawa. Kuna mambo mengi ambayo aliyataja na mojawapo ikiwa ni janga hili la Coronavirus. Mimi nataka kusema hivi: Coronavirus ipo Coronavirus imeuwa Coronavirus imeumiza na inazidi kuumiza Wakenya. Wakenya wanakufa madaktari wanakufa na hata sasa Wabunge na walimu wanakufa. Ni uchungu sana kuona kwamba madaktari ambao tunawategemea kutusaidia wakati huu mgumu hata wao pia wanafariki kwa ajili ya ugonjwa huu. Watu wanaumia mioyo. Watu wanaumia akili. Watu wana uoga mkubwa sana. Ni wakati sasa kama nchi wa kuwajibika bila samahani. Ni wakati wa kuona kwamba hospitali zetu tumeweza kuziboresha kila sehemu ya nchi hii. Swala lingine pia ambalo ningependa kulitaja ambalo lilikuwa kwa Hotuba ya Rais ni jambo la elimu. Nashukuru kwa sababu kulikuwa na maswali mengi ya kwamba watoto wamekaa nyumbani muda mrefu na kunakuwa na sintofahamu ya kuwa ni lini basi watoto hao watarudi shuleni ama itakuwa namna gani kuhusu maswala yetu ya elimu. Napongeza Idara ya Elimu kwa sababu walitoa tarehe ambazo shule zetu zitafunguliwa. Swala kuu kwa wakati huu ni je tumeweka miundo misingi ya kuweza kuwakaribisha watoto wetu ama kuweza kuwarudisha watoto wetu shuleni? Tunayo madarasa ya kutosha? Tunayo madawati? Na je ile ada ya shule itakayolipwa tuko nayo? Tunajua wananchi wengi wamekuwa nyumbani na wengi wamekosa kazi kwa sababu ya hii mambo ya Coronavirus. Hili ni janga. Na hawana fedha sasa. Je watalipa vipi hiyo ada? Tunajua watoto wetu wamekaa nyumbani na wamekuwa wakubwa na hata zile sare zao za shule haziwatoshi sasa. Kwa hivyo itakuwa ni kama mwanzo mpya kupeleka watoto kuanzia sare ya shule kuanzia vitabu na hata ada za shule. Kwa hivyo ni wakati wa kuweza kuangalia hilo swala na kuona ni vipi tutasaidiana na kusaidia jamii itakapofikia kurudisha watoto wetu shuleni. Nikimalizia pia swala lingine ambalo Rais alitaja ni mambo ya BBI. Kuhusu BBI nitasema kama kina mama bado tunahisi tumenyanyaswa na tunasema bado kuwe na muda wa majadiliano. Hii si kwa sababu ya akina mama peke yao ila wadau mbali mbali waweze kuja na kutoa hoja zao pale ili kuwepo na uwiano. Nasema asante sana. Nikimalizia pia niwapongeze kina baba wote walioko hapa na niwapongeze pia kina baba yumbani na kina baba wote wa Kenya wale wanatenda wema kwa sababu leo ni siku ya kina baba; International Men's Day. Asante sana kwa kunipatia hii fursa.
Shukrani sana. Nasimama kuunga mkono Mswada huu. Vile vile nampongeza Mbunge mwenzetu kwa kuleta hisia kama hizi ambazo zitaweza kukuza talanta ya wale wanaohusika na mambo ya kukanda mwili ili kuagua mifupa na mishipa ambayo ina shida. Kamati inayohusika na masuala ya afya yapaswa kujua kwamba kuna watu ambao wamezaliwa na kipawa cha ukandaji. Si kwamba wamekwenda shule kusomea hiyo taaluma lakini wanafanya kazi nzuri sana kule nyanjani. Kwa mfano kuna wakunga ambao walichukuliwa na kuwekwa mahospitalini ili kusaidia akina mama waja wazito. Kuna watu vile vile ambao hawahusiki na mambo ya uzazi lakini wanahusika na mambo ya mifupa; wao hawakusomea hii taaluma shuleni. Napendekeza kwamba wao pia wachukuliwe na wapewe mafunzo zaidi ili waweze kusaidia jamii. Ni watu ambao wanaishi nasi katika jamii na wameweza kuokoa maisha licha ya kwamba hawajawahi kwenda shule. Lingine ni kwamba hili baraza linalonuiwa kuundwa liwafikirie wale ambao hawakusomea hii taaluma shuleni ili nao wawakilishwe katika hilo baraza. Hii ni kwa sababu watu hawa wataleta maarifa wanayoyapata kule nyanjani. Wakenya wenzetu wanaosomea hii taaluma na kufanya kazi katika nchi za nje bado ni watu wetu. Tukifungua mlango ili waweze kurudi nyumbani na kufanya kazi humu nchini itakuwa ni bora kwetu. Tunapoteza pesa nyingi wakati hawa watu wanafanya kazi zao huko nchi za nje. Vile vile tunapoteza pesa nyingi wakati tunawatuma wagonjwa wetu kwenda kupata matibabu nchi za nje. Hawa ambao wana ujuzi pia Serikali iweze kufikiria kupanua zile hospitali ambazo tuko nazo ili wawahusishe. Waweze kupatiwa leseni na kuweza kuondolewa malipo ya KRA ili waweze kuleta mashine zao kutoka nchi za nje. Kwa hayo ninamshukuru Mhe. Sang. Nina ii huu ndio mwanzo wetu sisi kama Bunge hili ili kuweza kumwaangalia huyo mwanachi ambaye anaumia na hana uwezo wa pesa za kwenda kwa matibabu. Hii ni njia moja ambapo itaweza kuwasaidia watu wetu. Asanteni
ShukraniMhe. Naibu Spika. Nimesimama kuunga mkono na kumpongeza Mhe. Waluke kwa kuileta Hoja ambayo inagusia usalama wetu kikamilifu. Serikali huwaajiri watu na kuwapa mafunzo maalum lakini baada ya muda mfupi watu hao wanaacha kazi na kwenda kuhudumu kwingineko. Hali hii imechangia ukosefu wa usalama nchini kwa sababu maafisa wanaobakia kwenye kikosi ni wale ambao hawajapata mafunzo yanayohitajika kwenye vitengo tofauti. Kwa mfano ukiangazia kundi la Recce katika idara ya polisi utaona kwamba ni maafisa wachache sana ambao hupata mafunzo maalumu. Tunapowahitaji inakuwa vigumu kupatikana kwa sababu wako katika kambi moja pekee. Kama mafunzo hayo yangesambazwa kwa kila pembe miongozi mwa kikosi cha polisi na maslahi yao yaangaliwe vilivyo itakuwa vigumu mtu kuacha kazi kwenda kutafuta matunda katika maeneo mengine kinyume na alivyokubaliana na Serikali alipokuwa akiajiriwa kazi. Kwa nini ninasema hali hii inachangia utovu wa usalama? Tumeweza kuona na kusikia kwamba miongoni mwa majambazi wanaokamatwa ni watu ambao walipitia kikosi cha polisi. Baadhi ya maafisa wa usalama hushiriki kwenye uhalifu ili wapate hela za kuwawezesha kujimudu kimaisha. Mhe. Naibu Spika kwenye vikosi vya majeshi yetu kuna mkataba ambao unasema kwamba mtu hawezi kuacha kazi ya jeshi mpaka atakapohudumu kwa miaka fulani. Kwa hivyo kwenye mkataba wa ajira ya askari polisi inafaa tuweke kipengele kama hicho ndiyo isiwe rahisi kwa hao watu kuacha kazi na mtu akiamua kuacha kazi mapema iwe ni sharti alipe ridhaa ya zile pesa ambazo zilitumika wakati alipokuwa akipatiwa mafunzo. Pia tukitekeleza ukarabati ambao umependekezwa na Mhe. Waluke ili kuangalia jinsi tunavyoweza kuwasaidia maafisa wa polisi itawafanya vijana kinyume na jinsi ilivyo sasa wakubali ajira katika kitengo cha polisi. Ukiangalia nyanjani wakati watu wanaambiwa waende wakaombe hizo kazi vijana wengi siku hizi wamevunjika moyo. Hawataki kuenda maana wanasema: "Hata nikienda sina nyumba nzuri wala mshahara wa maana. Mwisho itaishia nishindwe na kazi." Katika kitengo cha polisi miaka ya nyuma Makamu wa Rais akiwa ni Mhe. Moody Awori ilitokea kwamba kutakuwa na usimamizi maalum ambao utaweza kubadilisha maisha ya kitengo cha magereza na hata polisi wa kawaida. Lakini ukiangalia zile nyumba ambazo zilijengwa nyingi ziko Nairobi na miji mikubwa. Kadhalika hazimfaidi anayepaswa. Nyingi zimechukuliwa na wale maafisa walio na mishahara mikubwa na katika ngazi za juu. Ofisa anayetumikia katika ngazi ya chini anakuwa mtu anayenyanyasika kimaisha. Ninaunga mkono Hoja hii ikiwa na ukarabati ambao umeletwa na Mheshimiwa mwenzetu. Shukrani Mhe. Naibu Spika.
Shukurani Mhe. Spika. Nasimama kuunga mkono Ripoti ambayo imeletwa na Kamati hii ambayo inasimamia mambo ya jinsia. Ninawapongeza kwa kuwa Ripoti hii imetuonyesha waziwazi kuwa ni kweli kuna akina mama ambao wamepatiwa nafasi. Hata hivyo kuna watu ambao hawako tayari kuwaona akina mama wakiongoza. Kwa sababu hiyo kwa niaba ya akina mama wenzangu Kenya nzima tunashukuru kwamba Kamati hii imemtoa mama huyu katika dhuluma ambayo alikuwa amepangiwa na wale wachache ambao hawataki kuona akina mama wakisonga mbele katika uongozi. Nawapongeza na naunga mkono Ripoti hii.
Sio pizza ni bixa . Mmea huu unatumika kwote ulimwengu na unatumika kwa chakula. Ni mmea wenye thai. Pia ni jukumu la Serikali kuona kuwa mmea huu unakuzwa na kiwanda kile kinapatiwa nguvu ili kiweze kutoa ajira kwa vijana wetu. Ni jukumu la kila Mkenya hasa kupitia utafiti maana saa hizi watu wakizungumza ni kama wanafikiria labda korosho ziko Pwani peke yake. Tunajua kwamba utafiti uliofanyika hapo nyuma ulidhihirisha kwamba mmea huu wa korosho unaweza kufanya vizuri maeneo mengine ya Kenya hasa maeneo ya kule Tharaka Nithi ambayo ni karibu na Meru. Hali kadhalika suala la mnazi pia limedhihirishwa kwamba sio Pwani peke yake lakini hata maeneo mengine ya Tharaka Nithi na Meru. Kwa hivyo tukizungumzia mmea huu ninawaomba viongozi wenzangu tulitilie mkazo jukumu hili. Tuweze kulipongeza kwani sio suala la watu wa Pwani peke yake lakini ni suala ambalo lina uwezo wa kusaidia nchi nzima na vijana wetu katika lile janga kubwa la kukosa ajira tukiona kwamba ajenda ya viwanda inapewa nguvu kupitia mazao haya. Kwa hayo mengi ninaunga mkono. Nimetanguliza. Siungi mkono peke yake kwa sababu zao hili linaniathiri kwa kiasi kikubwa. Naliunga mkono pamoja na miguu nione kwamba ufufuzi huu unafanyika na wananchi wote wananufaika. Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Sioni kama vile hii mambo inavyoendelea ni sawa. Sisi tumefinya tukitaka kuzungumza
Sisi pia tunataka viti. Sisi hatuna ruhusa ya kuongea na kwa hivyo tunapigwa. Kama ni nguvu hatuwawezi.
So Amisi kwa hivyo unataka kusema Mhe. Kanyi ashavuka border ama bado?
Tafadhali ningependa nijulishwe ni kwa nini mwenzagu hawezi kusimama ilhali wikendi hii alionekana akizungumza jukwaani katika Kaunti ya Kwale.
Tuheshimiane. Mimi niko na bwana. Sikuja hapa kutafuta wanaume. I am a married wo . Sikuja hapa kupendwa. Unaniambia umependa nini? Tuheshimiane. Nimetumwa hapa na kaunti ya Lamu. Namhurumia sana mama na watoto wa marubani wawili walioshikwa South Sudan. Hii siku ya leo watu wanafurahia Valentine's Day ilhali wao wanahuzunika. Ningependa muda uongezwe. Waziri wa masuala za nje na wengine wafuatilie. Waharakishe ili wale marubani wawili walioshikwa kule na waasi baada ya ndege yao kuanguka waachiliwe huru. Marubani wamezuiliwa kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa. Nahurumia sana bibi yake na watoto ambao hawana habari ni lini wataachiliwa. Ningependa pia kuwaeleza Mawaziri waharakishe kwa sababu watu wakisherehekea mambo mengine nimesikia mwenzangu akisema watu huko Lamu wana huzuni. Wakazi katika miji ya Kizingitini Bajumali Chundwa na miji mingine wameambiwa kwamba nyumba zao zitavunjwa lakini hawakupewa ilani. Hawana raha. Hvi saa sisi wakazi wa Lamu Mashariki tunataka hawa Mawaziri waangalie tatizo hilo. Tunataka maendeleo. Barabara yataka kujengwa lakini hiyo barabara ilifuata nyumba. Hakukuwa na rai ya barabara. Kwa hivyo haki za wale watakaoathirika zifuatiliwe. Asanteni.
Tukifanya hivyo tutaweza kuokoa hili Bunge lizifedheheke. Tuepukeni fedheha. Huu Mswada ninaupinga vilivyo. Wakenya waungane na sisi tuupinge pamoja. Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Tulimuuliza Katibu wa Bunge afanyie Hoja hiyo mabadiliko. Hii ni kwa sababu yale ndugu yetu Bw. Ali Mohamed anauliza yanahusu vile vipengele vya Katiba ambavyo vinahusiana na matibabu. Hii ni kwa vile tunajua kuna matibabu ya Serikali kuu na ya serikali za ugatuzi. Mhe. Kiongozi wa Wachache na Mhe. Washiali walikuwa katika huo mkutano. Tulimtaka aulize Serikali kuu na zile za ugatuzi; hospitali nyingi katika nchi yetu ziko chini ya seriakli za ugatuzi. Kabla hajafanya hayo mabadiliko hiyo Hoja yake ni bure kabisa. Ni bure kabisa kulingana na Katiba. Ni kama haiambatani hailingani na haiko sawia na Katiba ya Kenya. Mwenyekiti nakuuliza uulize makarani ambao wamekaa hapa Bungeni kama hiyo Hoja iko sawa. Nitampa Mhe. Mbadi fursa pia aongee Kiswahili ili ahakikishe kwamba yale ninasema ni ya kweli.
Tumesema kwa maoni yetu kongao hili si eti tumelipuuza. Ninaomba tuelewane; hatukulipuuza. Tunasema kwamba wakati huu ambapo kuna mambo mengi ambayo yanatokea hatuoni kama hilo kongao vile limekuja litakuwa na maslahi tulivyokuwa tunatarajia. Kama mheshimiwa mwenzangu alivyoeleza kuna mambo kadha wa kadha ambayo yanatukera na yanakumba nchi hivi sasa. Mambo ya ufisadi yametukera. Yako ndani. Tunauliza kwa nini tusiwe tunazungumzia mambo hayo kwanza ndio twende kwa kongao hilo? Nchi inataka kuzama. Sio CORD inataka kuzamisha nchi. Ni upande huu mwingine wa Jubilee unataka kuzamisha nchi. Na nini? Na wizi. Sasa mnataka mfanye wizi na mnataka mtuhusishe ndani. Tumekataa na tutaendelea kukataa. Tumekataa na tutaendelea kukataa. Ninaomba mnielewe. Ninazungumza Kiswahili lugha ambayo unatakiwa uelewe hata kama wewe ni mbabe wa kivita. Hata kama wewe ni mbabe wa kivita ninaomba mnielewe na ninaomba mnisikize kwa sababu huu ni wakati wangu. Mara nyingi mmenichukulia kwa kero kuwa Mwadeghu ni mpole na mnaweza kumsukuma Mwadeghu mpaka hapa. Hamjui Mwadeghu yule mnazungumza naye. Leo utajua kuwa mimi ninaweza kuwa mbabe. Ninaomba niseme haya. Wacha niwapashe na niwapashe sawasawa maana mna uzoefu mbaya. Mna uzoefu wa kuona kuwa mnaweza kutusukuma
Tunawapongeza. Waendelee na kazi nzuri. Hata mimi nimefunga saumu na nimekaa mpaka dakika hii kwa sababu hii ni kazi nzuri. Tunahimiza Kamati zingine pia katika hili Bunge ziwe na bidii kama Kamati ya Mazingira na Mali Asili. Ahsante sana.
Two minutes each. They are Mwashetani Shariff Nas Eikor Janet Nangabo Wafula Lazaro Bunyasi and Nyiva Mwendwa senior.
Ukichukua mfano wa hospitali ya Hola imeoza haina mochari mahali pa kulala wala chochote. Leo unawaambia eti wachukue hii wapeleke eneo la wakilishi Bungeni.
Umeeleza kwa ufasaha unaofaa. Tunashukuru. Kwa wakati huu tutampatia nafasi Mwakilishi wa eneo bunge la Nyandarua.
Umesema wale Waheshimiwa ambao wamesema ndio wamechukua. Hicho si Kiswahili sanifu. Ungesema wale wamesema ndio wamekubaliana na Bunge.
Unajua tatizo hapa ni kuwa kila mmoja hujifanya kuwa Spika katika Bunge hili. Ningeomba tu niweze kutaja jambo lingine hapa kwa sababu katika hisia ambazo wanajaribu kutumia hawa mabwana; la kwanza na la pili wanasema kutakuwa na nafasi za kazi. Suala lile tunajiuliza sisi hatukatai na hakuna anayepinga ya kuwa ni sawa tuwe na maendeleo na kuwe na usawa katika nchi. Kwa nini iwe ni kampuni moja pekee yake ambayo imepatiwa nafasi hii bila ya kuwa na mkataba wa maana ambao umefuata sheria? Kwa nini ikiwa tunataka kupeana port yetu kwa kampuni kwa sababu KPA imeshindwa kuiendesha kwa nini kusiwe na competitive bidding? Natumia lugha hii ili kuwakumbusha na kuwafahamisha Wakenya. Kwa nini kusiulizwe na kuwekwe makaratasi ya kuambiwa ya kuwa kampuni ambayo inataka kufanya kazi hii lazima ihakikishe imeajiri watu elfu kumi kazi. Jambo la pili tunataka kujua ni mtatoa fedha ngapi kutupatia? Ukitaka kujua ulaghai katika Bunge hili hili kupitia sahihi yako niliuliza swali hapa na ukapeleka suala hili kwa wenye kuhusika ya kuwa kuna mashirika ya nje badili ya kuajiri Wakenya wanaajiri watu ambao sio Wakenya licha ya kuwa Wakenya wana uwezo wa kufanya kazi zile. Majibu tuliyoyapata na niko tayari kwa sababu haya majibu yana muhuri wa Bunge. Majibu ambayo yaliletwa na Waziri husika na aliyekuwa msimamizi wa Kenya Maritime Authority ni kuwa wanakubali kuna tatizo na wakaelezea ya kuwa wako katika hali ya kubadilisha sheria.
Vile vile ningependa kutoa shukrani kwa Rais kwa sababu alizungumza kuhusu elimu bila malipo sio tu katika shule za msingi bali pia katika shule za upili ambako wanafunzi wetu watapata elimu bila kulipa karo. Bei ya stima imeshuka. Kushuka kwenyewe kusiwe tu kwa muda mfupi bali Serikali ya Rais Kenyatta iendelee kuhakikisha kuwa bei ya stima inashuka ili watu wote nchini waweze kupata stima. Pia wawekezaji nchini wawekeze kwa njia rahisi ili bei ya stima isizifanye bidhaa ambazo watakuwa wanatengeza kuwa za bei ya juu. Mhe. Naibu Spika wa Muda si i kuwa shughuli ya mradi wa reli unaendelea. Vile vile shughuli za ujenzi wa barabara zinaendelea. Mojawapo ni barabara ya kwangu nyumbani Taveta hadi Mwatate na kuelekea Voi. Hizo ni shughuli ambazo Rais amezitekeleza. Tunafurahi kwamba kazi hiyo inaendelea kote nchini. Rais aliahidi kutengeneza kilomita 10000 za barabara. Ni kweli kwamba ujenzi wa kilomita 3000 za mwanzo utaanza hivi karibuni. Huwezi kuzungumzia suala la usalama bila kuzungumzia vijana wetu 10000 ambao walikuwa wamepewa nafasi ya kupata mafunzo ya kuimarisha usalama. Kama shughuli hiyo haingesimamishwa hivi sasa tungekuwa tunafanya awamu ya pili - yaani vijana wengine 10000 wangekuwa wanaajiriwa. Jambo hili limekuwa donda ndugu baada ya korti kuisimamisha shughuli hiyo. Ningependa kuzungumza kuhusu vyeti vya kumiliki ardhi. Serikali hii ya Rais Uhuru Kenyatta tayari imetoa vyeti 400000 vya kumiliki ardhi. Makadirio yake ni kwamba itatoa vyeti milioni tatu kufikia mwaka wa 2017 ili watu waweze kuwa na vyeti vya kumiliki ardhi na kukaa bila wasiwasi. Nazidi kumpongeza Rais kwa kulizungumzia suala nyeti ambalo limekuwa donda ndugu na kama saratani inayotumaliza humu nchini. Rais alileta kilio. Kilio chenyewe ni kuhusu ufisadi. Rais amekuja kutuomba msaada. Jambo hili lisichukuliwe kama dhihaka au kama jambo la uzushi. Wanaokwenda kuchunguza masuala haya wasifanyie wananchi uzushi wowote. Mhe. Naibu Spika wa Muda naunga mkono masuala ya Hotuba ya Rais.
Vile vile tuko na Hospitali ya Rufaa ya Kenyatta ambayo inajali masilahi ya wagonjwa kutoka eneo la Kati Nairobi na eneo la Mashariki. Vile vile hii Hoja ya kuwa na Hospitali ya Rufaa ya Kitaifa kule Mombasa itasaidia sana kwa sababu kuna wagonjwa wengi wanaotoka kaunti za Lamu Mombasa Kwale Kilifi na Taita Taveta. Ukiangalia ajenda ya jubilee utapata kwamba matibabu yamepewa kipaumbele. Isitoshe kuhusu Malengo Endelevu ya Maendeleo hasa lengo la tatu (SDG-3) mambo ya universal healthcare yamezingatiwa. Mwenzangu Mohamed Ali ameongea kiswahili mufti. Tulijaribu kumfuatilia ikawa vigumu lakini katika zile pilkapilka za kumuelewa tukagundua kwamba tunaendelea kujifunza kidogo kidogo. Wajua kwamba Kiswahili ni lugha ya taifa. Mimi naomba tutenge angalau siku moja ili Wabunge waongee Kiswahili. Hii ni kwa sababu wakati tunaongea Kiingereza hapa yule nyanyangu aliye nyumbani haelewi tunachosema. Kulingana na Katiba mpya mambo ya Bunge lazima yajadiliwe hadharani ili mwananchi wa kawaida afuatilie na apeane mawaidha yake. Nikimalizia yafaa tutenge pesa katika Bajeti kwa sababu mara kwa mara Hoja nzuri kama hii zinaletwa hapa tunazipitisha lakini hakuna mtu wa kuzifuatilia ili zitekelezwe. Sisi tukiwa Wabunge hatuwezi kupitisha Hoja na hiyo Hoja isitiliwe maanani.Ndiposa nimeangalia humu ndani nikamwona mwenyekiti wa kamati ya utekelezaji. Katika Kiswahili ni "implementshoni" Hii Hoja ikipita yafaa aifuatilie ili tuwe na Hospitali ya Rufaa ya Kitaifa kule Mombasa.Wengine labda wanasema Mombasa si Kenya. Sisi tunajua Pwani ni Kenya. Ni vizuri hospitali iwe hapo karibu ili iwasaidie akina mama watoto na wagonjwa kwa ujumla. Wakenya wanatumia pesa nyingi kuenda ng'ambo kutafuta matibabu. Wengine wanaenda kule India ilhali matibabu wanayotafuta huku yanapatikana hapa nyumbani. Ukienda kule Kenyatta wagonjwa wamejaa sana. Tukitaka hospitali ya Kenyatta isiwe na wagonjwa wengi lazima tuanzishe hospitali nyingine za rufaa. Kule Eldoret kuna Hospitali ya Rufaa na Mafunzo. Tunataka hospitali ya rufaa kule Mombasa ijengwe ili wagonjwa wa saratani waende pale. Vile vile upasuaji utafanywa pale. Mhe. Mbadi amesema kulingana na kule anakotoka hawezi kuongea kiswahili maana ni kigumu sana. Amesema anataka anione nikijetetea kidogo kidogo. Nikiweza ataongea na akiona kinanilemea basi ataondoka. Ninajua watu wangu wa Kiminini wanafurahi kwa sababu wanasikia na wanaelewa Kiswahili. Wale wako nyumbani vile vile wanafurahi wakisikia tunaongea kiswahili. Watu wengi nchini wanaelewa Kiswahili. Tunaiomba ile Kamati yetu ya Bajeti kwamba ikileta Bajeti ya Ziada hapa lazima tutenge pesa ili zitumike katika ujenzi wa hospitali ya rufaa. Hatutaki tupitishe Hoja hii na ikose kutekelezwa.Nilikuwa na mengi ya kusema lakini wacha nikomee hapo ili wengine vile vile waongee. Ninashukuru Mhe. Mohamed Ali kwa kuleta hii Hoja. Ninaunga mkono. Ahsanteni sana.
Wacha kukosea watu hapa heshima!
Wacha nifuate mwelekeo wako Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Yangu ni kusema kwamba nchi nyingi zimegombana na zimefanya watu wakawa maskini haswa wakati mafuta ama gesi imepatikana kwa sababu mikataba inawekwa bila Bunge kuhusishwa. Wakati umefika tukubaliane kama Bunge kuwa mikataba yoyote ambayo itawekwa lazima iletwe Bungeni hasa hii ya mafuta kabla lolote kufanywa ili tujue ni nini iko ndani yake. Tunaweza kuwa tunajitia kitanzi. Mara nyingi tumejitia kitanzi. Mikataba imewekwa na baadaye ikiletwa hapa Bungeni tunajikuta tumejifunga. Hatuna la kufanya na hatuwezi kujitoa kwenye mikataba hiyo. Wakati umefika ikiwa tunatunga sheria tuhakikishe kuwa tumeangalia wale watu wako na hizo rasilmali wasinyanyaswe. Ombi ambalo limeletwa na Mhe. Amina Abdalla na Mhe. Profesa Nyikal ni nzuri. Nawashukuru kwa njia ya kipekee kwa kuona pahali tatizo liko. Naomba Wabunge wenzangu tukubaliane kwa kauli moja. Hata tusibishane. Wakati umefika tuunde hii sheria kuwa mikataba italetwa hapa hasa ya mafuta kabla watu kupanga mikakati yao ya kunyanyasa Wakenya. Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda naunga mikono. Asante.
Waheshimiwa Wabunge tuendelee kusimama. Mheshimiwa Rais wa Tanzania jirani wetu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni mgeni wetu wa heshima Mheshimiwa Spika wa Bunge la Taifa Mheshimiwa Justin Muturi waheshimiwa Wabunge wote wa Bunge la Kenya tumekuwa na mkufunzi na mimi ni mwanafunzi. Waheshimiwa Maseneta Bunge la Seneti litahairishwa kwa muda wa dakika 30 na tutarejea katika makao yetu baada ya muda huo.
Wajua Mhe Spika kile kitu anashuhudia ni yale sisi tumepitia sote Basi ningeomba tu kusema akina mama wapewe ulinzi wa kutosha Ninamwambia mwenzangu ajaribu juu chini kwa sababu hilo ni jambo la maana Hayo si mambo ya kulegea bali ni ya kuendelea Sisi sote tumepitia hayo na ndiposa tuko katika hili Bunge Asante Mhe Spika
Wajua ni muhimu kujitahidi kwa lugha yetu ya kitaifa ili tuendelee mbele. Lakini umuhimu wa hii Ripoti ambayo imependekezwa hapa na Mhe. Abdullswamad inatuelekeza kushugulikia maswala ya usalama kwa kila kipengele ambacho tunashughulikia. Kwa hayo machache nataka niwaunge mkono na kuwapa kongole wanakamati kwa Ripoti ambayo wamefanikisha hapa Bungeni. Ahsante sana.
Watoto wanajua kwamba walizaliwa pia. Maji ni muhimu na tunaiomba Serikali ihakikishe kwamba imechukua jukumu hili kwa dhati zaidi na kulipa umuhimu. Nampongeza Mhe. Mwadime kwa kuuleta Mswada huu Bungeni. Nakupongeza tena Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Ahsante na Mungu atubariki sote. Kwa hayo machache naunga Mkono Hoja huu.
Wauguzi wetu wako katika mgomo. Serikali yetu pamoja na sisi Wabunge kila wakati tuko katika televisheni redio na hakuna ambaye anajitokeza kujaribu kutetea wauguzi ilhali Wakenya wetu wanaumia. Madaktari waligoma kwa siku mia moja na hili Bunge pamoja na Serikali hatukujitokeza kama vile tulivyojitokeza wakati wa migomo ya waalimu. Hatujatilia maanani mambo ya afya na ndio sababu ninamshukuru Mhe. Mohamed Ali kwa kuileta Hoja hii. Sio kawaida mtu kufariki katika hospitali ndogo ama zahanati kwa sababu wagonjwa wanaelekezwa katika hospitali ambazo zina vifaa. Lakini madaktari kwa sababu ya kukosa kulipwa vizuri wanajaribu hivi na vile katika hizo hospitali ndogo mpaka wagonjwa wanaaga dunia. Hoja hii itawafanya madaktari pia wawe waangalifu. Kama mgonjwa akifariki daktari hatalipwa ada ya hospitali yule daktari atajaribu juu chini kuokoa maisha kwa sababu hayo maisha yameshikanishwa na pesa zake za huduma. Iwapo daktari hatalipwa mgonjwa akiaga dunia basi atajaribu vyovyote vile ili aokoe huyu mgonjwa kwa sababu hivyo ni kuokoa pesa zake. Wakati mwingine tukihimiza Serikali katika Miswada ni kama kuomba Serikali itusaidie nao wananchi ambao walijitokeza mapema kutuchagua wakasimama kwa jua mvua vumbi na upepo mwingi wakituomba wanahuzunika tunapokosa kuwahudumia. Ninamuomba Mhe. Ali abadilishe hiyo sentensi iamrishe Serikali. Hii ni kwa sababu Bunge hili linagawa rasilimali za nchi hii. Tunafaa kutoa amri ya kwamba hamna mgonjwa ambaye atalipishwa pesa za hospitali wakati ameaga dunia haswa ada ya hospitali. Sisi hatufai kuomba bali kutoa amri. Sisi ndio tunabeba mfuko wa mali ya pesa ya wananchi. Inasikitisha pia kusikia kwamba mzazi anashindwa kulipa ada ya hospitali ya mtoto wake na inabidi amuibe yule mtoto bila kupenda kwake. Sisi Wabunge na Serikali tulitangaza kwamba matibabu itakuwa bila malipo lakini mgonjwa akifika kule anaambiwa alipe na ikabidi aibe mtoto wake. Hii inahuzunisha sana na ingetakiwa kuamsha kilio cha Bunge hili ili kuamrisha Serikali iweze kulipia watoto ada za hospitali sio tu wale ambao wamekufa lakini hata wale ambao wanaishi. Hivi juzi mama alilazimishwa kubeba maiti ya mtoto wake kwa umbali wa kilometa tano. Hata kama hatuna utu hata kama sisi tumepata nafasi ya kupata mshahara mtoto kuaga kwa mikono yako inaumiza roho. Mama huyo alikuwa katika kilio halafu baadaye anaambiwa aipeleke maiti kwa polisi. Kumpoteza mtoto ni uchungu sana na ukibebeshwa hiyo maiti kwa umbali wa kilometa tano ni uchungu zaidi. Sisi Wabunge na hata Serikali hatujatilia maanani umuhimu wa afya ya wanachi wetu. Kwa hivyo ningesema kwamba huduma ya afya irudishwe kwa Serikali kuu ili tuweze kuwa na msemo kama Bunge la Taifa. Hata tukijaribu kupitisha Hoja kama hii itabidi iende katika Seneti au bunge za kauti ili iweze kupitishwa. Kama afya ingekuwa katika Serikali kuu ingekuwa rahisi kwetu kupitisha Hoja hii. Kwa hayo mengi naunga mkono Hoja hii mia kwa mia ili iweze kuwasaidia wananchi wetu haswa kwa eno ya afya. Pia ningetaka kuwashukuru sana watu wa Nyali kwa sababu inaonekana kwamba ule uchunguzi Mhe. Mohamed Ali alikuwa akifanya katika Jicho Pevu haukuwa wa bure. Amekuwa na jicho pevu la kuangalia maslahi ya Wakenya wote sio watu wa Nyali peke yao. Kwa hivyo na waambia asante sana. Pia ninawahimiza Wakenya kuchagua vijana chupavu kama Mhe. Mohamed Ali ili tuwe na Bunge ambalo litaleta Miswada ya maana ya kuwasaidia wananchi wa taifa la Kenya. Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Well- Waluke.
Wewe kaa chini.
Ya mwisho ni kueleza wananchi wa Kenya na wale tuko nao hapa Bunge kuwa nilirudi juzi. Nikikueleza kuna wengine wamenikuta hapa Bunge 34 na wameniambia niwaonyesha mahali nilikuwa na vile wataenda. Mambo ya saratani isifichwe ndio watu wajue saratani inaweza kutibiwa namna gani. Lakini saratani isipelekwe mashinani kwa kaunti kwa sababu watu wanakufa kila siku juu ya saratani.
Yangu ni kuuliza kwa heshima kubwa Mhe. Naibu Spika wa Muda tupunguze muda wa kuchangia Hoja hii ili kila mtu aweze kupata nafasi. Ni Hoja muhimu sana.
Yangu ni machache sana kwa wenzangu wa chama cha CORD. Kama ningelikuwa nimefanya makosa yoyote kuhusu chama chetu cha CORD mngeniita mnieleze kwamba kama kiongozi kutoka Meru nimewakosea hivi na vile. Haifai mkiingia kwa nyumba na kuota moto mseme kwamba Mhe. Aburi hafai kwa Kamati ya Lands. Mjue kwamba kupata kiti na CORD katika Meru ni kama kutoa nyama kutoka mdomo ya fisi. Nataka tena Melewe kwamba mimi sina vita na nyinyi. Vita yangu ilikuwa kidogo na CORD. Mimi nilikuwa nagombea kiti cha mwenyekiti katika chama cha ODM nchi nzima. Kufika uwanjani pale mimi na watu wangu tulitupwa nje. Mimi niliamua kwamba singekuwa na vita na nyinyi. Lakini mnaaandika mna vita na mimi; hiyo ni kama kuingiza kidole kwa shimo la siafu na siafu ndio hawa; hakuna lingine. Mimi napinga mambo haya. Kama ningelikuwa na makosa Kama mngelikuwa watu wa ukweli ama watu wanaofuata ukweli mngeniita na kuniambia: Mhe. Aburi umekosa hivi na hivi. Mimi sitaki mseme kwamba Mhe. Aburi hatii sheria zetu ama haimbi wimbo wetu ama hatupigii makofi. Siwezi nikakupigia makofi ukiwa na makosa. Ndiposa nimesema kwamba mimi nikiwa kiongozi kutoka Meru simbebelezi punda kwa mteremko. Namachilia ateremke chini; nitampembeleza akipanda. Mimi suingi mkono mambo haya Sikukaa chini na hawa; hawa ni wakora; inafaa waongezwe kokoto kwa tumbo ndio wasisikie njaa tena
Yes Mhe Spika ningeomba nikariri kilio hiki kwa Kiswahili ili tuweze kufahamikiana Niko na Ardhilhali ya umma ambayo kwa lugha maarufu ni Public Petition Nambari 22 ya 2021 Tukitukuze Kiswahili kiongozi wangu ili tufahamikiane hapa na nje ya Bunge pia Ardhilhali Nambari 22 ya mwaka 2021 inayohusu pingamizi za biashara mjini Mombasa Mhe Spika mimi Mhe Abdullswamad Nas Mbunge wa eneo la Mvita kwa niaba ya wafanyibiashara katika Kaunti ya Mombasa na hususan wafanyibiashara wadogo katika Mama Ngina Water Front kwa jina jingine Light House na Jomo Kenyatta Public Beach ama kama inavyojulikana Bamburi Beach nataka kufahamisha Jumba hili mambo yafuatayo: Kwanza Wizara ya Utalii kwa madai inayosemekana ni ilani kutoka kwa Wizara ya Afya waliamrisha kufungwa kwa Mama Ngina Water Front na Jomo Kenyatta Public Beach kwa madai ya maradhi ya coronavirus Mamia ya wafanyibiashara wa maeneo ya Mama Ngina Water Front na Jomo Kenyatta Public Beach kwa sasa wanapoteza mapato yao na familia zao baada ya kuzuiwa kuingia na kufanya biashara katika sehemu hizo Wafanyibiashara hao wameteseka mno Biashara zao ni vitu kwa wale wenye kufahamu kama kachiri madafu mihogo kutembeza watu katika sehemu hizi za utalii kwa maboti wauzaji ushanga na mavazi ya bahari Wafanyibiashara hawa wamekuwa katika sehemu hizi zaidi ya miaka arobaini na hawana pengine pa kwenda Hii inasababisha ufukara kukosa kutazama familia zao kusomesha watoto wao na mwishowe uhalifu utazidi Mhe Spika tunafurahi na kukubali ya kuwa baadhi ya sehemu nyingine ya biashara Kubwa kubwa kuweza kufunguliwa lakini tusiwe ni wenye kusahau ya kuwa tunafungua zile kubwa ilhali wale ambao ni wenye biashara ndogo ndogo wanaumia Wafanyibiashara hawa wamejaribu kila njia kuzungumza na wenye kusimamia maeneo haya na kilio chao kimeenda pahali ambapo hawajaweza kuridhika Nataka kukariri vilevile ya kuwa haya maswala ambayo nimeweza kuyaleta katika bunge hili hayapo mbele ya korti yoyote ya sheria hii Kenya Kwa hivyo Mhe Spika kwa unyenyekevu ombi langu ni kuwa Bunge hili kupitia Kamati ya Biashara Viwanda na Vyama vya Ushirika liingilie kati na liangalie jambo hili haraka iwezekanavyo Watu warejee na wafanye biashara zao katika Mama Ngina Recreation Centre Light House Jomo Kenyatta Public Beach na katika sehemu zingine Mombasa Vilevile ikiwa kutakuwa na maoni yoyote Kamati itazingatia tuko radhi na sawa kuweza kuyafuata Asante sana
Asante Mhe Naibu Spika wa Muda Rais wa Tanzania alituchekesha na utamu wa Kiswahili chake Kwanza nataka kumpongeza Mwenyekiti wa Kamati hii Mhe Kizito kwa kazi safi ambayo ameifanya Mhe Naibu Spika wa Muda mimi pia ni mmoja wa wanakamati ya Utangazaji na Shughuli za Bunge na Maktba Lakini kabla hata nichangie chochote kuna jambo ambalo limekuwa likinivunja moyo sana Sasa ni mwaka wa nne tangu niwe katika Kamati hii Cha kushangaza ni kwamba Kamati hii ambayo kwa sasa imeleta Hoja hii ambayo inapongezwa na kila Mbunge ni Kamati ambayo imechukuliwa kama Kamati hafifu ambayo wanaoadhibiwa na wale ambao wanaonekana kwamba hawafai kuwa katika Kamati kubwa kubwa huletwa upande huu Hata tunapozungumza saa hii ni juzi tu ambapo Wenyekiti wa Kamati kadhaa kwa sababu ya malumbano waliokuwa nayo ndani ya vyama vyao walitolewa kule na kutupwa huku Walikuja na ule msimamo wakifiria kuwa hii ni Kamati ambayo haina mwelekeo Lakini tazama ile kazi ambayo Mhe Kizito na Wabunge wake wameifanya Kusema kweli kabisa sisi sote tunafahamu kuwa Bunge ndio mahali ambapo sheria na mwelekeo wa tasasi za Serikali zote hutoka Iwe ni mahakama au hospitali kila kitu lazima kiweze kutungwa kama sheria kupitia Bunge hili La kushangaza ni kwamba katika yote yanayoshughulikiwa katika Bunge hili hakuna lolote ambalo mwananchi analifahamu Ninapongeza Hoja hii na hatua iliyochukuliwa Kwanza kabisa linalonitia moyo ni mbali na kuwa kazi na jitihada za Wabunge kwenye Kamati na kwenye Bunge pia mwananchi wa kawaida ataweza kuelewa ni kitu kipi kinaendelea Bungeni Mbali na michango yetu mwananchi ataweza kufahamu mambo ambayo yanaendelea Bungeni pia Pili Wabunge wengi wamesema hapa kuwa angalau kazi za Wabunge zitakuwa zinaonekana Lakini mbali na hilo pia hii itapatia mwanachi nafasi ya kuchagua kati ya stesheni zinazotangaza jumbe ni stesheni ipi angetaka kufuatiliza ili kuelewa yanayojiri na yanayoendelea katika taifa hili Mimi na wewe tunafahamu hivo Kuna stesheni zingine ambazo yale wanayopeperusha ni mambo ya aibu ya kuvunja moyo na ambayo huwezi keti na watoto wako kama familia kutazama Lakini hii ni stesheni mmoja ambayo wengi wataitazama Kwa mfano mimi kama Mbunge sasa hivi nafikiria kuwa familia yangu ingetaka kujua ni maswala yapi ambayo nayafuatilia ndani ya Bunge Ingewezekana Mhe Naibu Spika wa Muda ungeniongezea muda ake naona muda wangu umeyoyoma Hata hivyo langu mimi ni kuwaomba na kuwasishi Wabunge kama vile wameunga mkono tafadhali tuzidi kuipatia Kamati hii motisha ili yanayohitajika haswa fedha bajeti inafaa kuanganzia hili ili kuhakisha kwamba kituo hiki kinazinduliwa Kusema ukweli Mhe Kizito ameweza kupiga hatua kubwa sana na ingekuwa bora kama hatua hii