Mswada huu ni muhimu kwa sababu unapendekeza utaratibu ambao utatuwezesha kurejelea mfumo wa kuorodhesha wanafunzi na shule mbalimbali katika mitihani ya kitaifa. Ni lazima tukubali ya kwamba kuorodheshwa ni suala ambalo linapatikana katika kila nyanja. Hata sisi kama Wabunge tunajua kwamba ukitazama ule utaratibu na utamaduni kwenye Jumuiya ya Madola utapata ya kwamba hata Wabunge kama sisi huorodheshwa kwenye viwango mbalimbali na kuna utaratibu wa utamaduni huo. Kwa mfano ikiwa ni lazima utoe nafasi katika mjadala kati ya Mbunge wa kawaida au Mbunge ambaye anashikilia wadhifa fulani katika uongozi wa Bunge hili utatoa nafasi ya kwanza kwa yule Mbunge anayeshikilia wadhifa fulani ama kwa yule Mbunge ambaye amekuwa hapa kwa muda fulani. Huo ni utaratibu ambao umekubalika katika utamaduni wa Bunge za Jumuiya ya Madola. Utaratibu huu wa kuorodhesha uko hata mbinguni. Kule mbinguni hata malaika wameorodheshwa. Kuna malaika mkuu ambaye ukifika kule mbinguni atakufungulia mlango. Hilo ni suala ambalo sisi Wakristo tunalijua sana. Utaratibu huu wa kuorodheshwa tumekuwa nao kwa muda mrefu hapa nchini. Mwenyekiti wangu wa Kamati ya Bajeti anajua suala hili la orodha kule mbinguni. Hili si suala geni katika taifa hili. Tumekuwa na utaratibu huu wa kuorodhesha shule na wanafunzi katika mitihani ya kitaifa lakini suala hili lilikumbwa na matatizo kwa sababu ya udanganyifu katika mitihani na mashindano yasiyostahili. Shule nyingi ziliiga mtindo ambao mashindano yalifikia kiwango ambacho kilikuwa kufa na kupona. Shule kadhaa zilianza kutumia mbinu potovu ambazo zilipelekea aliyekuwa Waziri wa Elimu Sayansi na Tekinolojia Jacob Kaimenyi kufutilia mbali utaratibu huu wa kuorodhesha shule na wanafunzi. Lakini mimi ningependa kumkosoa Kaimenyi kwa sababu matatizo hayakuwa katika kuorodhesha. Matatizo yalikuwa katika usimamizi wa mitihani jinsi Wizara ya Elimu Sayansi na Tekinolojia inavyosimamia secta hii ya Elimu na jinsi tunavyosambaza rasilmali katika shule mbalimbali katika sehemu tofauti za taifa. Haya ni masuala ambayo Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Tekinolojia inastahili kuyashuhulikia. Lazima tuwe na usimamizi bora wa mitihani. Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) lazima lifanyiwe mabadiliko makubwa ili kuhakikisha kwamba linasimamia mitihani kwa njia inayostahili. Sasa tumeingia kwenye mfumo wa ugatuzi. Nimewasikia wenzangu wakichangia Mswada huu. Wameleta tetesi kwamba itakuwa vigumu kuorodhesha shule ilhali kuna hali tofauti katika sehemu mbalimbali za taifa letu. Wamesema kwamba hatuwezi kuorodhesha shule za kaunti kama vile Wajir sambamba na shule katika kaunti kama Nairobi ama Nakuru. Suala hilo la viwango tofauti ni nyeti na sugu na lazima lishughulikiwe. Ni mojawapo ya sababu ambazo zilitufanya kubuni mfumo wa ugatuzi. Sasa tuna nafasi ya kuhakikisha kwamba shule katika sehemu zote za taifa hili zinapata rasilmali tosha. Ndio sababu tumetenga pesa maalum kwenda katika maeneo ambayo kihistoria yamebaki nyuma kusahaulika ama hayajapata rasilmali za kutosha. Kwa hivyo suala hilo lisitutie wasiwasi tena kwa sababu tayari limeshughulikiwa na linaendelea kushughulikiwa. Wabunge kutoka maeneo kama hayo wanastahili kuunga mkono Mswada huu kwa sababu utabuni utaratibu ambao utawezesha shughuli ya kuorodhesha shule kufanywa kwa viwango mbalimbali. Kwa mfano shule katika kaunti kama Wajir Tana River ama Kwale zitaorodheshwa kwa njia ya kutufahamisha tujue hali ya kila shule katika maeneo hayo na hali hiyo inachangia vipi matokeo katika shule hiyo. Kwa hivyo tuorodheshe shule katika kila kaunti ili tujue shule shupavu katika kila kaunti. Tuorodheshe shule katika maeneo shule za kitaifa na katika viwango vingine vya shule kwa mfano shule za kaunti ili tujue shule za kiwango cha kaunti ambazo zimefanya mtihani kwa njia bora zaidi. Tuorodheshe shule kwa kiwango cha shule za kitaifa kwa sababu tuna shule za kitaifa katika kila kaunti. Kila kaunti sasa imepata shule ya kitaifa. Tuorodheshe shule katika kiwango hicho cha kitaifa. Kwa hivyo Mswada huu unatupatia nafasi ya kubuni utaritibu maalum. Hapo mbeleni shule ziliorodheshwa bila utaratibu. Zimeorodheshwa kiholela. Sheria hii itabuni utaratibu wa kutuwezesha kufanya shughuli hii kwa njia ya utaratibu ambayo ninaamini itazuia udanganyifu. Ni lazima sisi kama Wabunge tuunge mkono hatua hizi hasa hatua ambazo lengo lake ni kuhakikisha kwamba tunaondoa kila aina ya udanganyifu katika mitihani. Ndio sababu nachukua fursa hii kumpongeza Waziri wa Elimu Bw. Fred Matiang'i kwa hatua ambazo amechukua kujaribu kuimarisha hali ya wizara na kurejesha heshima katika usimamizi wa mitihani ingawa sikubaliani naye katika maamuzi yake ya hivi punde ambayo yanaondoa maombi kwa wanafunzi ambao wanajitayarisha kufanya mitihani yao ya mwisho shuleni. Ametangaza kwamba tufutilie mbali wanafunzi kutembelewa na wazazi wao wakati wa muhula wa tatu. Sioni jinsi maombi ya kuombea wanafunzi wanaojitayarisha kufanya mitihani yanavyoweza kuchangia wanafunzi kudanganya katika mitihani. Sioni njia ambayo wanafunzi kutembelewa na wazazi wao inaweza kupelekea udanganyifu katika mitihani. Na ukisema kwamba utafutilia mbali wanafunzi kutembelewa na wazazi wao je utafanya vipi kwa wale wanafunzi ambao wanasoma kwenye shule ambazo wanarejea nyumbani kila siku? Je utajenga ukuta wa China kati ya wanafunzi hawa na wazazi wao au na famillia zao? Uamuzi huo wa Bw. Matiang'i ni uamuzi potovu ambao hauwezi kuchangia hata kidogo kuimarisha hali ya mitihani. Ningependa Bw. Matiang'i achukue hatua za kutosha za kuhakikisha kwamba KNEC inasimamia mitihani kwa njia inayostahili. Vile vile ningependa kuona sheria ikiletwa hapa Bungeni ya
Nashukuru. Imeeleweka na inajulikana ni hivyo. Lakini ninakubaliana na vile ulivyomesema. I respect the . Ukishatoa mwelekeo ni lazima tuufuate. Ndiyo ninamshauri mwenzangu awache kuzungumzia siasa za Bahati. Tuzungumzie mambo ambayo yako mbele yetu. Ndugu yangu tuheshimiane. Tuangalie tutafanya nini ili tuweze kuiendeleza nchi hii tukiwa pamoja. Ahsante sana.
Ningependa kuchukua nafasi hii ili niungane na wenzangu kuunga mkono hii Hoja. Uchunguzi kuhusu aliyeteuliwa umefanywa vilivyo na kamati husika. Jina lake limepitishwa na kamati ambayo imeona kwamba yeye anafaa. Sitaki kurudia yale ambayo yamesemwa na wenzangu. Ni muhimu tuwe na balozi katika nchi ya Somalia ili tuweze kufanya kazi ambayo iko mbele yetu na tusaidie wananchi wetu. Itakuwa bora ikiwa Wakenya watafanya kazi pamoja na wananchi wa Somalia. Naunga mkono.
Ningependa kusema machache kwamba niko katika Kamati hii ambayo inashughulikia mambo ya ardhi. Tulichunguza vile Mwenyekiti amesema na tulizunguka sana. Ni kweli hawa watu walikuwa ni waadhiriwa kama vile Mwenyekiti amesema. Hao watu walitoka upande wa Rift Valley ambapo kulikuwa na ghasia baada ya uchaguzi ambao kila mtu anajua katika mwaka wa 1992. Hawa ni watu ambao walikuwa na shida nyingi. Mambo mengine hayakufanywa walipopata pahali pa kukaa. Serikali ilichelewa kuwapa vibali vyote. Watu wachache walipata vibali. Vile Mwenyekiti amesema kuna. Hao watu walipelekwa pale na Shirika la Kuhifadhi Misitu mwaka wa 1992 na kupewa ruhusa ya kujenga mashule. Pia walionyeshwa mahali pa kuzika watu waliokufa. Idara ya Utawala pia ilikubali kuwa watu hao wasipopewa vyeti vya kumiliki mashamba kwa njia ya kisheria kutakuwa na shida. Kwa hivyo ninaunga mkono Ripoti hii. Ninaomba kuafiki. Asante sana.
asante sana kwa kunipatia fursa hii nami niweze kuichangia Hoja. Yale yaliyotokea yametuumiza mioyo sana. Naibu Spika wa Muda kwa niaba ya wakaazi wa Taita Taveta natoa rambirambi kwa familia ya Mariam na mtoto Mutheu ambao walipoteza maisha katika mkasa huo. Hili ni jambo la aibu sana na la kusikitisha katika karne hii. Wakenya wanapoteza maisha kwa mambo ambayo yanaweza kuzuilika. Kuna utepetevu fulani na uzembe mkubwa katika shirika la huduma za feri. Ni lazima watu wawajibike kwa kazi ambazo wamepewa kuhudumia wananchi. Wakenya na viongozi pia ni lazima tutafakari ni vipi tumejiandaa kukabiliana na majanga kama haya yanapotokea. Majanga aina tofauti tofauti yanaweza kutokea na ni vipi tumejitayarisha kukabiliana nayo? Nikimalizia naendelea kutoa pole zangu. Hili liwe janga la mwisho na kila mmoja wetu aweze kuwajibika katika majukumu ambayo amepewa - ayafanye vyema ili tusipate mikasa kama hiyo siku zijazo. Asante sana Naibu Spika wa Muda.
Ningependa nizungumze kwa Kiswahili Pole kwa kuanza kuzungumza kwa Kiingereza Ningependa kusema kuwa Mzee Nyachae ni mzee ambaye anaheshimika kwa jamii ya Mkisii Mzee Nyachae alifanya kazi na hayati Mzee Moi na bahati yangu ni kuwa Mzee Nyachae alifanya kazi pia na baba yangu ambaye alikuwa Mbunge hapa; Mzee Dkt Zachary Onyonka Wakati mke wa Mzee Nyachae alifariki mwaka uliopita niliona ni heshima kubwa kwenda pale nimzungumzie huyu mzee Hii ni kwa sababu nilikuwa sijamzungumzia tangu miaka kumi na mitano iliyopita Nilipoenda kumzungumzia kabla ya mazishi aliniambia kuwa: "Unajua mimi na baba yako tulikuwa na mvutano wa vuta nikuvute lakini ule ulikuwa ni mvutano wa kiume lakini wa kiheshima Hatukuwa na matusi Tulikuwa na njia na fikira tofauti vile Kenya inafaa kuendelea ama hata jamii ya Mkisii Lakini heshima nilimpa baba yako naye alinipa heshima ijapokuwa tulikuwa wapinzani" Mhe Spika juzi nilikuwa na furaha yule mzee kuniambia kuwa kwa maisha yake ya mwisho hakuwa na shida na familia ya Mhe Dkt Onyonka Kwa hivyo ningependa kusema hapa katika hili jumba ya kwamba Mzee Nyachae aliheshimika Kenya nzima Ninyi viongozi mlioko hapa haswa wakati huu ambapo nchi yetu inahitaji watu ambao wana roho safi akili timamu na wana nia njema kwa nchi yetu tujaribu kujadiliana na kuzungumza kati yetu ili tusije tukasukuma nchi yetu ikaenda mrama Ningependa kusema kuwa Mungu amuweke mahali pema peponi huyu Mzee Tutaiombea familia yake Tunatarajia kuwa hata kama watakuwa na mambo fulani mazito mazito mzee alikuwa na marafiki chungu nzima Kwa hivyo familia yake waendelee kuzungumza wakubaliane kwa sababu jina la Mzee Nyachae lataka liachwe kule juu ambako mashujaa wa nchi ya Kenya
Spika nashukuru kwa kunipatia fursa hii kuchangia mjadala wa lala salama tukielekea kwa likizo. Leo ni siku kubwa zaidi kwani tumepitisha Miswada mitatu muhimu zaidi katika Kenya yetu. Miswada hii ni muhimu zaidi kwa sababu tumekuwa na Miswada mingine mizuri lakini hatujapitisha Miswada kama hii inayohusu uchaguzi na kuhamahama vyama. Tungepoteza mwelekeo wakati sisi sote tulikuwa tumekataa lakini kwa kuwa na uongozi mwema ambao uko katika Kenya tukihusisha Rais wetu naibu wake na kinara wa upande ule wa wasio wengi tumefanya vyema. Pengine hatutajua matunda ambayo tumevuna leo lakini tunajua ya kwamba tuna matunda ambayo tutaona yakivunwa. Huu ni wakati wa kurekebesha vile vyama vimekuwa vingi zaidi na viliyvo na watu wachache zaidi. Kazi ya hivyo vyama vidogo ni kutafuta fedha na kupoteza kura na kutoonyesha Kenya kama tunaendelea kukomaa. Sasa tumechukuwa mwelekeo ambao tutaonyesha kukomaa. Leo tumepitisha Mswada ambao ni wa ushirikiano wa Wakenya na baina ya Serikali ya Uingereza. Ushirikiano huu ni wa kusaidia kustawisha usalama katika nchi hii yetu na wao. Mimi nikiwa nimetoka Laikipia tulifurahi zaidi kwa sababu ya kudumisha uhusiano huo. Sisi tumefaidika kutokana na uhusiano huo. Askari ambao wametoka Uingereza wamekuwa wakitusaidia katika mambo yetu ya kawaida kama vile kujenga barabara kujenga viwanja na hata kuwapatia vijana wetu kazi. Vijana kutoka Laikipia wamefaidika kwa kupata kazi na tumefurahi zaidi kwa sababu ya kuidhinisha huo uhusiano. Ikiwa kuna Wabunge ambao wamesema huu uhusiano si mzuri sisi tuna wakati wa kurekebisha. Tukisema hivyo tunajua hapo mbeleni Kenya ililipwa ridhaa na Uingereza. Watu kutoka Samburu na Laikipia walifaidika na wamefurahi sana. Baina ya wale waliofaidika waliondoka vijijini na kuelekea mijini kustarehe. Leo hawana chochote na bado wana maumivu yaliyolipiwa ridhaa.
Ahsante Bw. Spika. Kwa majina ninaitwa Zainab Chizuga muwakilishi wa akina mama katika kaunti ya Kwale. Ningependa kukupongeza sana kwa kuchaguliwa kuwa Spika wetu pamoja na naibu wako akiwa mama. Kwanza nimesimama kuiunga mkono Hoja hii kama ilivyo kwa sababu muhimu ni lile ambalo unalizungumza na uzito wake; siyo eno matupu. Pili ningependa kuwapongeza Wabunge wote walioteuliwa. Tatu ninawaomba Wabunge wasichukulie kwamba sisi akina mama tulio hapa tumekuja kuteta. Tumekuja hapa kuungana na kushirikiana ili tulijenge taifa la Kenya. Ahsante Bw. Spika.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunitetea. Nikimalizia uteuzi huu umezingatia kanuni za Katiba zinazoangazia usawa wa jinsia. Mheshimiwa Rais na naibu wake wameangalia sana suala hilo na wamewapa nyadhifa kina mama ambao wana uwezo kama sisi katika utenda-kazi. Kwa hayo
Mhe. Naibu Spika mimi ni mheshimiwa Aisha kutoka Kilifi. Kwa vile ni mara yangu ya kwanza naomba uniruhusu niwapongeze watu wa Kilifi kwa kunichagua ili niwaakilishe katika Bunge hili la Kumi na Moja. Nimesimama kuunga mkono orodha ya majina. Nimeipitia Ripoti hii kwa uchache na nikaona kwamba walioteuliwa wana tajriba na taaluma ya kutosha kuendesha Wizara walizotengewa. Kuhusu suala la ukabila nafikiri Katiba imeangazia hilo jambo katika Kipengele cha 152 (d); kwamba si chini ya Mawaziri 14 na si zaidi ya 22. Katika taifa letu tuna makabila 42. Wenzangu waliozungumza awali wametaja kwamba kuna ugumu fulani unaojitokeza. Hata ikiwa Rais angeamua kuwepo na Wizara 22 bado haingeweza kufikia idadi ya makabila tuliyonayo katika taifa hili. Mimi naona kwamba hakuwachagua kwa kuzingatia kabila ila ametumia misingi ya elimu na tajriba waliyonayo ili watumikie Wakenya wala siyo makabila yao. Mimi naamini kwamba wanao uwezo
Asante sana Bw. Spika. Ninaitwa Mishi Juma na ni muwakilishi wa akina mama katika kaunti ya Mombasa. Kwanza kabisa napenda kukupa pongezi nyingi kwa kuchaguliwa katika kiti chako hicho; pia nataka kutoa pongezi kwa Hotuba ya Mtukufu Rais Uhuru Kenyatta. Nina machache ya kuzungumzia katika ajenda zake alizozungumzia kuhusu ya nchi yetu ya Kenya. Bw. Spika ajenda ya kwanza ni ardhi. Mheshimiwa Rais alisema kwamba ardhi ni katika vigezo ambavyo vinaleta mapato ama kwa Kiingereza factor of production. Mimi nasema ardhi si tena kigezo cha kuweza kuzalisha. Ardhi ni kitu ambacho kimeleta tetesi na vita katika Jamhuri yetu ya Kenya tukiangalia Rift Valley ama Bonde la Ufa na Pwani. Sasa hivi pia tunashukuru ndugu zetu wa kutoka Mkoa wa Kati na Bonde la Ufa. Walipiga kura pamoja. Hivyo basi hakuna tetesi nyingi na shida ambazo tumeziona. Tunashukuru Mwenyezi Mungu lakini kitu ambacho tunasema ni kwamba ni lazima viongozi tuwe wa kweli. Tulikuwa na tume ambayo ilituletea ripoti ya Ndungu; pia tuna Tume ya TJRC ambayo ni ya kuleta ukweli haki na maridhiano. Tume hizi zote zimetupatia ripoti na zikatueleza madhambi na mambo ambayo yamefanyika kuhusiana na mashamba; ajabu ni kwamba Ndungu Report inaoza katika makabati ya Serikali. Jambo hili pia limezungumuziwa na tume ya ukweli na maridhiano. Je hii tume ya ardhi itaweza kupatiwa nguvu za kisiasa na tutaweza kuwa Wakenya wa dhati ili Wakenya ambao ni maskwota Wakenya ambao ni wakimbizi wa ndani ambao tunawaita IDPs waweze kupata mashamba? Katika Katiba yetu sura ya tano inazungumzia swala la ardhi; inasema kuna ardhi ya kiserikali ardhi ya kijamii na ardhi ya watu binafsi; katika mapendekezo mengi yalitolewa ni kwamba katika ardhi za kibinafsi viongozi wengi tukiwemo sisi wa kisiasa tumenyakua ardhi ya kiserikali. Tumenyakua ardhi za kijamii. Ni wakati wetu sisi kuwa mbele katika kuregesha ardhi hizo hata kama tuko katika nafasi kuu katika Jamhuri yetu ya Kenya. Tuwe wa ukweli katika swala la ardhi. Tunataka akina mama tupate haki zetu za kumiliki ardhi na najua katika Miswada mitatu ambayo imetolewa na ile tume ya ardhi itaweza kufanya kazi; hii inamaanisha sisi viongozi tuwe wa ukweli. Bw. Spika jambo la pili ni swala hili la kutolipa ada wakati wa kuzaa. Mimi namshukuru Mheshimiwa kwa jambo hili lakini nataka kusema kwamba hatukuelezewa kinagaubaga pesa hizi zitatoka wapi. Nahofia kwamba Wakenya watatozwa ushuru kuweza kufidia jambo kama hili kwa sababu mahali ninapotoka katika kaunti ya Mombasa Coast General Hospital sasa hivi tunalipishwa Kshs1800 kwa kujifungua kikawaida. Ukizaa kwa kupasuliwa unalipa Kshs7500
Shukrani Mhe. Spikar. Ni pongezi kwako kwa kuchaguliwa kama Spika wetu. Nikiongezea ningependa kusema kwamba nilikuwa afisa wa uhusiano mwema na ndio sababu hakukuwa na fujo yoyote wakati ulichaguliwa. Nasema ahsante pia kwa wabunge wenzangu. Kulingana na ile Hotuba ya Rais nasema hongera. Ilikuwa Hotuba nzuri sana lakini nataka tupige hatua katika mambo ya ulinzi na usalama katika sehemu ambayo nimetoka. Kabla zijasema hivyo ningependa kutoa hongera kwa watu wa Laikipia kwa kuchagua huyu mama ambaye anaitwa Jane Machira. Niliapa mbele ya Bunge hili kwamba nitawatumikia wote. Tukiangazia ulinzi na usalama Kenya ilifanya vizuri sana wakati ilielekea Somalia na kuhakikisha ai katika nchi hiyo. Lakini sisi wenyewe tunaweza kuwa tunakunywa maji ili hali majirani wetu wanakunywa pombe za kifahari. Katika sehemu ya Laikipia majirani wetu wamekuwa wakipigwa na kukipigana wenyewe kwa wenyewe na hata kuuana kwa ajili ya mifugo. Juzi tu katika sehemu ya Kamwenje huko Laikipia baba mmoja na mtoto walipoteza maisha yao. Pia katika Kaunti ya Baringo ambayo ni jirani yetu ilipoteza mtu mmoja na kijana wa shule. Pole kwa hayo yote. Mungu aweke roho zao mapahali pema peponi. Nataja tupige hatua ambayo Rais alizungumzia kuhusu ulinzi. Hatua ya kwanza inahusu watu ambao wameuliwa. Itakuwaje ikiwa jamii zao hawatapatiwa ridhaa? Tunataka watu hao wawe wakipatiwa ridhaa kwa sababu ikiwa mama amewachwa bila mzee wake na watoto bado wanasoma anapata shida kubwa sana katika maisha yake. Kwa hivyo katika Bunge hili tungetenga kiazi fulani cha fedha za kuwalipa ridhaa waliofiwa na kuwa wajane. Tukiwa bado katika masuala ya ulinzi na usalama kuna wazee ambao wanafanya kazi ya uhusiano mwema na kulinda usalama katika sehemu Fulani fulani. Tunawaamini sana. Lingekuwa ni jambo la busara kuwatengea fedha kidogo za malipo. Tunawaita wazee wa mitaani na wanasaidia jamii zinazoishi Laikipia. Jambo la tatu ni kuwa kuna tatizo la wanyama wa pori kuzurura huko Laikipia. Hao wanyama wa pori wemawatatiza wananchi wa Laikipia. Watoto wetu siyo kama
Mheshimiwa Naibu Spika ningetaka kuendelea na maoni yangu kuhusu aliyoyanena Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni. Tulikotoka waliotuchagua wanaangalia yale yote ambayo tunanena katika Bunge hili. Haitakuwa jambo la busara kwetu sisi kuamka alfajiri kuja hapa tu kuzungumza eno ambayo hayatafika pahali popote. Nikitamatisha nimesalimu amri yako na nimeomba msamaha kwa yale niliyoyanena. Lakini waweza kumtoa mtu katika soko lakini huwezi kutoa yake.
Nimesalimu amri. Namuunga mkono Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni kwa maoni yake kuhusu mijadala ambayo tumekuwa nayo katika Bunge hili.
Shukrani Mheshimiwa Naibu Spika. Nitazungumza kwa Kiswahili ili mwenzangu Mheshimiwa aweze kuninukuu vizuri maanake walipotoka katika mabaraza ya ispaa wengi walikuwa wanazungumza kwa lugha ya mama. Nataka kumuunga??

Asante sana Mheshimiwa Spika ama kweli Kiswahili kitukuzwe. Ninachukua nafasi hii kwanza kumpongeza sana Mheshimiwa Owen ambaye ameileta Hoja hii. Ukulima wa korosho na mkorosho kwa jumla ni mmea wa kitaifa. Kwa sababu hiyo upandaji wa mmea huu wa korosho na mazao yake hasa yanapatikana katika ukanda wa Pwani. Mhe. Spika wa Muda ninataka niseme kwamba kiwanda cha korosho kilichokuwa na sifa mwaka wa 1974 hadi mwaka wa 1992 kilikuwa kinaitwa Cashew Nuts?? Kilikuwa maeneo ya Kaunti ya kilifi. Ninataka nichukue nafasi hii kwanza niwajuze kwamba kauli ya Rais wa Jamhuri yetu ya Kenya Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta Mhe. William Samoei Ruto Chama cha Jubilee kwa jumla na sisi ambao tuko ndani ya Chama hicho hivi sasa ni kwamba kuna Agenda Nne Kuu. Moja yapo katika zile Agenda Kuu Nne ambazo Mhe. Rais amezipigia mbiu sana ni uboreshaji na ubunifu wa viwanda katika Jamhuri yetu ya Kenya. Ni jambo ambalo analitilia mkazo sana. Ninataka kuliunga mkono kwa dhati nikiwa na tamaa yote kama mkaazi wa kutoka Pwani Kaunti ya Kilifi na Mkenya kwa jumla. Kiwanda hiki cha korosho ambacho tumekikosa kwa muda kilikuwa kikileta ufaa mengi ya kiuchumi katika maeneo ya ukanda wa Pwani na taifa nzima kitapewa kipaumbele na kitaanzishwa upya. Kwanza kitabuni nafasi za kazi na vile vile kuleta mapato katika kapu la kitaifa ambalo ni mapato yetu katika taifa nzima. Zai tulikuwa tunaona kwamba linachangiwa kabisa. Asilimia nne ya mapato katika mradi mzima wa korosho ama viwanda vyote vitano vilikuwa vimeboreshwa katika taifa letu la Kenya. Kiwanda hiki kitabuni nafasi za kazi. Kule ambapo tunatoka sehemu ya Kilifi Pwani na Kenya nzima kwa ujumla. Viwanda hivi vimesomesha watoto wetu na kukuza jamii bila shida yoyote. Hivi sasa kuna shughuli nyingi ambazo zinatukumba na moja yapo ni njaa. Ukizungumzia kuhusu njaa katika taifa hili utakuta kwamba Kaunti ya Kilifi haiwezi kuachwa nyuma. Kwa hivyo mimi nina ii kwamba kiwanda hiki kikirudi nafasi za kazi zitabuniwa tutapata nafasi za kuajiri watu wetu kusomesha watoto wetu na kuwalisha bila kuwa na shida za utapia mlo katika taifa letu la Kenya. Nikimalizia ninataka kusema kwamba wakulima zaidi ya 50000 katika kanda la Pwani na Kenya wameathirika pakubwa. Urudishaji ama kuanzwa tena upya kwa kiwanda cha korosho katika sehemu hii yetu ya pwani hasa Kaunti ya Kilifi kutabuni nafasi za kazi kuanzia 4000 hadi 50000. Tukiangalia suala la kiwanda iwe basi ni mchakato mzima kutoka upandaji ukuzaji na pia katika hali za kuliboresha zao hilo la mkorosho. Muda wangu haujaisha. Kwa hayo mengi Mhe. Spika wa Muda ninaunga mkono kwa dhati kiwanda hiki cha korosho hasa katika upande wa pwani na Kaunti ya Kilifi. Kiwanda hiki kikipewa nafasi Mhe. Rais atakuwa ametupa nafasi kubwa sana kiuchumi katika maeneo yetu ya Kilifi. Asante sana.
Mhe. Leshoomo atuambie kama anazungumza kama mwanakamati wa BBI au kama mama wa Samburu.
Seme ODM Asante sana Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii nichangie kwa kuondolewa kwa kipengele cha 6 katika maamuzi ambayo tulikuja nayo. Sababu yetu kama Kamati kuchukua msimamo huo ilikuwa ni tulipowaita EACC kuwauliza maswali kuhusu swala hili walituambia kuwa kwa sababu ni suala ambalo lina umuhimu ni lazima masuala mengine yafichwe.
Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia swala hili ambalo ni muhimu kabisa na nampongeza Mhe. Swarup Mishra kwa kuleta swala hili wakati sawa kabisa. Tunajua ni kweli Mhe. Naibu Spika wa Muda ya kwamba Wakenya wengi sana wanasafiri kwenda nchi za nje kwa ajili ya kutafuta matibabu. Ni wakati sasa karne hii hata hapa nchini Kenya tuweze kubadilisha hilo. Tunajua linawezekana kwa sababu hili suala la matibabu ya nje ya nchi limekuwa kama biashara sasa. Wakenya wanatumwa kutibiwa nje mwa nchi mara kwa mara na wakati mwingine haijalishi kama wana uwezo ama hawana. Hilo limetubidi kupata matatizo ya kuwa kwa michango mara nyingi sana kwa ajili ya kuwafanyia michango ilhali maswala mengine ni yale ambayo yanaweza kutibiwa humu humu nchini. Tumeona vyema wakati huu wa janga hili la Coronavirus ya kwamba watu wengi ambao walipaswa kwenda nchi za nje kutibiwa hawakuweza kwenda na wengine wao walitibiwa humu humu nchini na wakapata afueni. Kwa hivyo inaonekana kuwa mengine yanaweza kufanyika humu nchini. Naunga mkono Mswada huu. Ni vyema kuwa sasa tuwe na mwongozo dhabiti kama nchi zingine ambazo zinatusaidia kwa masuala haya ya matibabu
Asante sana Mheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi hii pia kuzungumzia suala hili ambalo ni la kikatiba na ambalo tayari limeweka nchi hii kwenye hali ya wasiwasi. Katiba ya mwaka wa 2010 - Katiba yetu mpya- ilivyokuwa inatengenezwa ilikuwa kwa sababu ya matatizo yale ambayo tulikuwa tumeyapata wakati watu walikosana. Pia vile wananchi mara nyingi walisema kuwa kwa sababu ya yale makosa yaliyokuwemo ni vizuri kuwa na Katiba mpya. Mheshimiwa Spika Wakenya wengi walitaka kuwa Katiba mpya ije ili mamlaka mengine yapunguzwe yaende kwenye ugatuzi ili hapa juu tubaki tukiangalia maswala ambayo yanaweza kuendeleza nchi hii mbele wakati ugatuzi nao pia unaendeleza kaunti zetu mbele. Mheshimiwa Spika nilikuwa Waziri wa Jinsia baada ya Katiba hii kupitishwa mwaka wa 2010 mwezi wa Agosti. Mheshimiwa Spika swala hili la Kipengele cha 27 (8) limetutatiza mno maanake tayari kiko kwenye ukurasa wa haki zetu na vile ni kuwa huwezi kukigusa kipengele hiki kama hutarudi kwenye kielelezo yani referendum. Mheshimiwa Spika jambo linalonisikitisha ni kuwa mtu akipatiwa kazi ya uongozi kuna umuhimu wa huyo mtu kufahamu kuwa Kenya si ya mtu mmoja ama watu wawili bali Kenya ni watu karibu milioni hamsini. Mheshimiwa Spika Kipengele hiki cha 27 (8) ambacho kinatumika kinahakikisha kwamba Bunge hili la kitaifa halina watu wa jinsia moja haswa wanawake. Tungependa kuona wanawake wakichaguliwa nchi hii lakini Wakenya wana haki- kama vile mwenzangu alivyotaja Mheshimiwa Olago Aluoch- kuchagua katika kipengele cha 38. Wana haki ya kuchagua mtu yeyote aliye jinsia ya kike ama ya kiume katika maeneo bunge 290. Mheshimiwa Spika hatuko hapa kubahatisha. Wakenya waliamua kutuleta hapa na walivyotuleta sisi hawakujua kuwa eti kuna wanawake na wanaume hapa nchini. Mara kwa mara mimi husikia watu wakiuliza ni kwa nini hatufanani na Rwanda ama Afrika Kusini. Mheshimiwa Spika haiwezekani kwa sababu wale wanachaguliwa kupitia orodha ya vyama vya kisiasa. Sisi hapa Kenya kuna tofauti kubwa sana. Kupitia Kipengele cha 38 Wakenya hupiga kura kuamua ni nani atakayewawakilisha hapa Bungeni. Mheshimiwa Spika nilivokuwa Waziri wa Jinsia tulijaribu tukaongea na Mheshimiwa Rais akamtuma Mkuu wa Sheria kwenye Mahakama Kuu ili tuweze kupata njia mwafaka vile tutaweza kuongeza idadi ya kina mama hapa nchini. Wakatuelezea kuwa wanatupatia miaka mitano ili tuweze kupata njia mwafaka lakini Mahakama Kuu haikusema kinaga-ubaga swala hili litatatuliwa vipi. Walitaja kuwa swala hili ni lazima lipatiwe muda hadi hapo tutakapofikia idadi ya kina mama jinsi inavyotakikana. Mheshimiwa Spika mwenzetu Mheshimiwa Otiende Amollo alikuwa na bahati ya kuwa kwenye wale ambao walikuwa wataalam wa kuandika Katiba. Jambo ambalo hawataki kusema wazi ni kuwa waliangalia wakajua kuwa katika Bunge la Kitaifa ukisema utaongezea idadi jinsi wanavyofikiria haitawezekana. Ndio ukaona kuwa kwenye Kipengele cha 177- kwa ugatuzi kwenye Bunge za Ugatuzi- waliamua kuweka kipengele ambacho kitaweza kuongezea jinsia hiyo nyingine. Waliiweka bayana na kila mtu akisoma anajua kuwa wanapatikana vipi. Japo kuwa vile ningependa kusema kuwa walivyokiweka kile kipengele kimechezewa. Huwezi kuwa maeneo yetu ya Bunge za Ugatuzi ni 1450 lakini wanaochaguliwa kupitia njia ile wanafika nafikiria Wabunge 800. Mheshimiwa Spika ukiangalia hesabu tayari inakuchanganya. Bila shaka Bunge la Senate waliona kuwa walipatie Kipengele cha 98 kinachoeleza akina mama ama wabunge wa jinsia nyingine watapatikana vipi lakini kwenye Bunge la Kitaifa ilishindikana. Mheshimiwa Spika Kipengele cha 27 (8) kinasema kuwa watu wote ambao ni Wakenya haswa wale ambao wamepatiwa nafasi za uongozi hapa nchini na sio Wabunge peke yake ndio wako na nafasi ya uongozi. Uongozi upo katika mahakama na hata Ofisi ya Rais kupitia kwa Baraza lake la Mawaziri. Nafasi hizo ziko. Kipengele cha 27 kinataja kuwa sio wenye kuchaguliwa peke yake kwenye Bunge la Kenya ndio lazima wawe thuluthi zisizo pita mbili katika jinsia moja. Inataja hata wale wanaopatiwa kazi upande huo mwingine kwa hiyo mikono miwili ya kiserikali wawe pia wana idadi ya kutosha ambayo haitapita thuluthi mbili. Mheshimiwa Spika kwa nini liwe Bunge ndilo litabeba kashfa hii ambayo inatakikana kubebwa na Kenya nzima? Inatakikana kubebwa na uongozi wote hapa nchini. Nilikuwa na wasiwasi ya kwamba siku moja tutakuja kuwa na Jaji Mkuu ambaye atafanya vitu bila kuuliza na kuweza kuzungumza na washikadau wote ili kuweza kutatua tatizo hili. Mheshimiwa Spika Bunge la Kumi na Moja lilijaribu sana. Bunge hili limejaribu kufikiria kuwa sheria hii tutaileta vipi na sio rahisi ake huwezi kulazimisha mtu kupiga kura kwa njia fulani. Halafu isitoshe hupigi kura tu. Ni lazima tufikirie upigaji wetu kura hapa je unaleta faida gani ama unaleta nini hapa nchini. Kwa mfano ikiwa tutaongezea Wabunge 80 je watakaa wapi? Huo ndio ukweli wa eno jai na mficha uchi hazai! Napenda kusema wazi kuwa hayo yote tumeyafikiria. Ndio ningependa kuona wanawake wanaongezeka. Ningependa tutafute njia ya kuleta akina mama zaidi lakini je Wakenya wenyewe watatupatia hiyo njia? Tunashukuru kuwa Katiba hiyo imetupatia akina mama 47 kupitia njia ya Wawakilishi wa Kina Mama. Lakini juu ya hapo tukumbuke hata Bunge la Seneti la Kwanza hakuna mama hata mmoja alikuwa amechaguliwa. Sasa hivi Wakenya wamejaribu wakaleta akina mama watatu. Wakichanganya na wale 20 ambao wako pale unakuta Bunge la Seneti tayari limefikisha idadi inayohitajika. Shida kubwa tuliyoko nayo ni hapa kwenye Bunge la Kitaifa. Nataka kina mama waongezeke lakini je tutaongeza kupita kinyume na vile wananchi wanavyotaka? Tutaongeza bila kurudi kwa wananchi kuwauliza? Mheshimiwa Spika Kipengele cha 27 (8) huwezi kukigusa bila kurudi kwa Wananchi. Tuuseme ukweli wa mambo. Naomba Mwenyezi Mungu amguse Mheshimiwa Rais asikubaliane na Jaji Mkuu kwa jambo hilo ambalo litakaloleta mtafaruku kwa nchi yetu hii tukufu. Asante sana Mheshmiwa Spika.
Asante sana Mheshimiwa Spika. Nasimama kulingana na Kanuni ya Kudumu ya 95 ya Bunge hili kumwomba Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi ambaye ameleta mjadala wa Ripoti hii ya ardhi inayozungumzia cheti cha kumilika ardhi Nambari 7879/4 asimame amalize mjadala huu ili tuweze kusonga mbele.
Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangie mjadala huu ambao umeletwa na Mhe. Didmus Mbunge wa Kimilili. Ningetaka kushirikiana na wenzangu ambao wanaunga mkono mjadala huu kuhusu nauli zinazolipishwa watu kwenye barabara zetu hasa sekta ya uchukuzi katika nchi yetu ya Kenya. Vile Mhe. Dennitah Ghati ameongea hapa kuhusu walemavu kutumia usafiri huu hapa nchini Kenya ni kweli kabisa. Baadhi ya hawa watu hupata shida sana. Hii ni kwa sababu hawana nafasi ya kusimama ama kuongea na amba wa matatu na kusema wangependa nauli iteremshwe ama wanatoka pahali fulani wakielekea pahali pengine. Inakuwa ni huzuni kuona walemavu katika nchi hii wakiumia sana. Hasa ofisini zetu na wakisafiri kwenda mashinani kwenye kaunti zetu huwa wanapata shida sana. Wenzangu hapa wameongea kuhusu washikadau katika sekta hii. Ndiposa mimi nakushukuru kwa kusema kwamba Mwenyekiti wa Kamati ya Uchukuzi katika Bunge hili akae hapa ili tuone pengo ambalo tunaweza kuziba katika kuhakikisha kwamba tumekuwa na usafiri bora nchini mwetu Kenya. Katika eneo la huko kwangu Trans Nzoia utaona kwamba watu wenye matatu hawana nafasi hata ya kuegesha magari yao. Kaunti zetu hazijakuwa na mikakati mwafaka au jopokazi la kuhakikisha kwamba watu wa matatu wamepata nafasi zao licha ya kusema kwamba wanaweza kuwabeba wasafiri kutoka eneo moja kueleka maeneo mengine. Ndiposa mimi ninazisihi serikali zetu za kaunti na serikali kuu zihakikishe kwamba tumeweka mikakati mwafaka kuhakikisha kwamba wasafiri wamepata nafuu katika nchi yetu ya Kenya. Naweza kumnukuu Rais akisema kule Bomas of Kenya kwamba mambo ya ufisadi katika nchi yetu ya Kenya yamekita mizizi. Ndiposa unaona hata wahudumu na wenye matatu wana vyeo vikubwa serikalini na wengine ni askari. Uamuzi wa kusema nauli itakuwa namna gani ni wa mwenye matatu. Iwapo mwenye matatu ni askari mwananchi wa kawaida atapata namna gani nafuu ya kuhakikisha kwamba anaweza kusimama mahali na aongee mambo ya nauli katika nchi yetu ya Kenya. Sisi kama viongozi katika Bunge hili hatujakuja hapa ili kuzozana kama nilivyowaona wenzangu wakifanya. Baada ya mmoja kuongea mwingine anamrushia matusi. Sisi sote tulikuja hapa sio kwa sababu tunafaa bali ni kwa mambo yake Mwenyezi Mungu kupitia kwa wapigakura kule mashinani kuhakikisha kwamba tuko hapa tukifanyia kazi wananchi waliotutuma katika Bunge hili. Mimi humpa kongole Rais mstaafu Moi ambaye alikuwa rais wetu kwa miaka 24 kwa sababu hawakusema alikuwa amehitimu kiwango fulani. Uongozi unamfaa mtu mwenye hekima zake za kuhakikisha kwamba anakuwa rais kiongozi au katibu katika nchi yetu ya Kenya. Tukiwa katika Bunge hili tumetumwa na Hoja hii ambayo imeletwa na Mhe. Didmus ni jukumu letu sisi kwa sababu tunapotoka mashinani tunaona watu wakiumia sana. Ukija katika eneo la Trans Nzoia kwa sababu ya uchumi na umaskini wa watu wa Trans Nzoia utawaona wengi wakitumia pikipiki. Saa hii ninapoongea wiki iliyopita mwalimu pamoja na wanafunzi wake waliokuwa wakisafiri kutumia pikipiki waligongwa na gari la serikali. Ndiposa ninasema lazima tuwe na mikakati mwafaka na hata jopokazi la kuhakikisha kwamba usalama na usafiri katika nchi yetu ya Kenya uko sambamba. Watoto wetu hutaka kusafiri kwenda shule au wanapofunga shule zao. Uliona hivi juzi kule Bungoma watoto wetu wakitumia matatu moja kutoka Bungoma kuelekea shuleni baada ya kutoka nyumbani na wakapata ajali katika barabara zetu na kupoteza maisha yao. Ndio tunasema huenda ikawa nauli iliteremka au ilipanda ndiposa watoto hao wakaamua kutumia gari moja. Ndio maana ninasema wacha tuwe na mikakati mwafaka ya kuhakikisha kwamba uchukuzi katika nchi yetu ya Kenya umeimarishwa. Naunga mkono wenzangu walioongea kuhusu barabara zetu. Hiyo ni kweli kwa sababu tunapoenda huko nje tunapata kwamba barabara zao zimetengenezwa sambamba. Ziko sawa. Lakini ukija katika nchi yetu ya Kenya wale ambao wamepewa nafasi ya kuhakikisha kwamba barabara zetu ni nzuri hawatumii nafasi hiyo vilivyo. Ndiposa unaona Wabunge wenzangu wakipigana katika Bunge hili wakisema hata Hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge ipewe hawa kwa sababu wanajua ni barabara zipi zina shida katika sehemu wanazotoka. Ndiposa nashukuru na kusihi magavana wanaochaguliwa katika serikali za kaunti wahakikishe kwamba wanaelewa masilahi ya watu wanaowashughulikia katika sehemu hizo. Namuunga mwenzangu aliyesema kwamba Mheshimiwa Didmus aje na Mswada katika Bunge hili. Akija na Mswada huo itakuwa rahisi sana kwa sababu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchukuzi yuko hapa. Itakuwa rahisi sana kuangalia mapengo hayo ili tuhakikishe kwamba usafiri uko sambamba. Mheshimiwa mwenzangu ameongea kuhusu matapeli. Hapakosi matapeli katika kila sekta. Sio sekta hii peke yake ndiyo ina matapeli. Wanapatikana kila mahali katika nchi yetu ya Kenya. Lazima tuwe na mikakati ya kuzuia watu kama hawa katika nchi yetu ya Kenya kwa sababu tunataka kuendelea mbele. Namshukuru Mheshimiwa Didmus. Nampongeza sana kwa kuleta mjadala huu katika Bunge hili ndiposa tuuchangie. Naunga mkono Hoja hii.
Asante sana Mhe. Naibu Spika Muda kwa kunipa nafasi hii niweze kusema jambo kuhusu huu mjadala wa walemavu. Nimesikia vile Mhe. Ghati pamoja na Mhe. Sankok wameongea. Kusema kweli walemavu wako na shida mingi. Wengi wao hawana vifaa vya kuwasadia kutembea kama mikogonjo viti vya migurudumu na kadhalika. Ni huzuni kubwa kwa sababu watu wengi huwaficha walemavu. Nimesikia huzuni mingi sana moyoni mwangu kusikia kuna mahali mlemavu alikuwa amefungwa kama mbuzi katika zizi la ng'ombe. Hili si jambo la haki. Mlemavu ni kama binadamu wengine. Wanafaa kulindwa kisheria na kupewa haki zao. Jambo la walemavu si la kuchukuliwa kwa mzaha mbali lina takikana kuchukuliwa kwa makini. Mahitaji yao yanapaswa kuchukuliwa kama ya Wakenya wengine. Kusema ukweli kuna wengine ambao tangu wazaliwe hawajawahi kutembea wengine wakiwa na umri wa miaka 50 ama 60. Wengine wanafaa kupewa nepi. Kusema ukweli huko vijijini vya kwangu kuna wamama ambao hawawezi kununua hizo nepi. Walemavu wanafungwa matambara na vidonda za kitanda zinawashika na wako tu. Kwa hivyo wanahitaji usaidizi unaofaa. Serikali inapaswa kuhudumia ndugu zetu na baba wetu ambao ni walemavu. Nimeona dada yangu Mhe. Ghati ameongea kwa upendo. Tumetembea naye katika mikutano mingi. Naona mama anatetea walemavu na ukiangalia hakuna mtu ambaye angependa kuwa na mlemavu. Yeye ni kiumbe au mtu ambaye Mungu aliumba kama wengine. Wanafaa wapewe mahitaji yao vile wanavyohitaji. Kuna zeruzeru ambao wanahitaji mafuta ya kujipaka ndiyo jua lisichome sana ngozi yao na tena wanahitaji miwani kwa wingi. Nasihi serikali iangalie tuone mahitaji ya hawa ndugu dada na baba zetu wanalindwa katika hii nchi yetu ya Kenya. Na ifanyike haraka tuone kwamba inashughulikiwa vilivyo na walemavu wote katika nchi hii wanashughulikiwa. Nikiongea hivi tumejaribu kununua wheels na hazitoshi. Unajaribu kutoka kwa mfuko wako lakini hazitoshi. Ukienda kwa hafla tofauti unaona mzee au mama anakuja akitambaa chini. Hawa watu wanahitaji waishi maisha ambayo yanafaa katika hii nchi yetu ya Kenya. Kwa hivyo ningependa kuunga mkono Hoja hii na kusema kwamba walemavu wapewe nafasi kimasomo kibiashara na kimaisha. Waishi kama wakenya in a dignified ner. Asante sana Mhe Naibu Spika wa Muda.
Ahsante Bi. Mwenyekiti wa Muda. Nimesimama kupinga pendekezo la Mwenyeketi la kukifanyia mabadiliko Kipengele hiki. Mwanamke anapoolewa huenda ikawa hana ajira lakini inafaa ifahamike kwamba kufagia nyumbani kwake asubuhi na kumchemshia mumewe maji ya kuoga pia ni mchango kwenye ndoa. Mwanamke huyo pia huchangia mengi kwenye ndoa. Kwa hivyo ana haki ya kupata ugavi sawia wa mali yatakayopatikana wakati wa ndoa. Ahsante Bi. Naibu Spika wa Muda.
Ahsante Bi. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Mswada huu. Huu Mswada umekuja wakati unaofaa; wakati ambapo Wakenya tunasherehekea miaka 50 tangu tujikomboe kutoka kwenye minyororo ya wabeberu na kuweza kujitawala kama Wakenya. Mswada huu unatambua na kuteua mashujaa. Wakenya tumekuwa na fikira kwamba mashujaa wa ukombozi wa uhuru wametoka katika jamii fulani ama sehemu fulani humu nchini. Lakini mashujaa wetu wa uhuru wametoka katika Jamhuri yetu yote ya Kenya. Kwa mfano kule kwetu pwani tunaye mama yetu Mekatilili wa Menza. Yeye alikuwa shujaa ambaye alitembea kilomita 1200 kwenda na kurudi ili kuwatetea wakenya dhidi ya dhuluma za wabeberu. Tunao watu kama vile Abdalla Bambaulo na Mfalme wa Digo Kubo. Wao pia walipigania uhuru wetu. Mswada huu utaangalia vigezo na kutengeneza sera ambazo zitaweza kutambua mashujaa ni akina nani. Kuna wale ambao watakuwa mashujaa bandia na hiyo haitakuwa sawa. Iwapo tutakuwa na sera mwafaka basi tutajua shujaa ni nani. Mswada huu pia umezungumzia vitengo mbali mbali vya mashujaa. Mswada huu pia unatambua mashujaa kupitia uvumbuzi. Labda kuna Mkenya fulani ambaye amevumbua jambo ambalo litawasaidia Wakenya kutatua shida fulani. Kuna wale pia watakuwa wameleta maadili fulani katika nchi yetu. Huu Mswada kwa kweli umezungumzia nani ndiye shujaa. Tumekuwa tukifikiria kwamba ushujaa ni wa wale waliopigania uhuru peke yao. Hata hivyo tunaona kwamba mashujaa wako katika nyanja nyingi sana. Tuna mashujaa hata katika mambo ya elimu. Tuna waalimu na maprofesa ambao wamevumbua hali nyingi. Mfano ni maprofesa wa hesabu ambao wamevumbua formula za kutatua matatizo yetu katika nyanja ya hesabu. Vile vile tuna mashujaa katika soka. Wengi pale mashinani wamesahaulika. Tunawataja sana wanasoka wa nchi za nje na tunawasahau wetu. Mswada huu ukipitishwa tutakuwa na miundo misingi wa kuwatambua mashujaa wetu. Nimefurahi kwa sababu Mswada huu umezungumzia hazina ya fedha ambazo zitawasaidia mashujaa ama waliokuwa wakiwategemea mashujaa. Mfano hapa ni Dedan Kimathi na Mekatilili wa Menza. Jamii zao ziko katika hali ya umaskini. Iwapo tutakuwa na hazina hiyo basi itawasaidia wake na watoto wa mashujaa. Lazima pia tuweke vigezo ili tujue fedha hizo zitasaidia kwa njia gani. Tukiacha hazina hii itumike tu wakati shujaa ana mahitaji ya fedha basi tutakuwa tumeacha mwanya mkubwa sana ambao pengine utatuletea matatizo. Lazima tuseme kwamba fedha hizo zitasaidia pengine katika kusaidia jambo fulani. Hivyo hatutatumia vibaya fedha hizo. Mswada huu utawafanya Wakenya wachanga walioko sasa waweze kuona vielelezo vyema katika mashujaa ambao walipigania uhuru wetu ama kutuletea mambo fulani humu nchini. Mswada huu utaangazia vile vile Wakenya ambao wameleta mageuzi Tulikuwa nchi ambayo ilikuwa na chama kimoja cha kisiasa lakini kuna wale ambao walipigania demokrasia. Wengine walipoteza maisha yao na wengine walipigania na kuhakikisha kwamba ni lazima Wakenya wawe katika sera ya vyama tofauti ili tuweze kujieleza kisiasa na kufanya siasa huru. Kuna wengi waliopigania mazingira kama dada yangu marehemu Wangari Maathai. Alipigania sana mambo ya mazingira yetu. Hadi wakati huu tunafuata njia zake ili kuhifadhi mazingira yetu. Watu kama hao ni lazima tujue watakua vipi kielelezo kwa jamii zilioko sasa ili wengi wao waweze kuingia katika mambo kama hayo. Nafurahishwa sana pia na Mswada huu kwa sababu umezungumzia kuhusishwa kwa Wakenya ama jamii katika kutambua mashujaa. Itakuwa vyema zaidi wakati baraza litaundwa ili kuhusisha Wakenya kule mashinani ambao pengine wana historia kuhusu mambo yaliyotokea tulipokuwa tunapigania uhuru wetu. Tunajua pia kuna Wakenya waliochukuliwa wakati wa nyuma katika Vita Vikuu vya Dunia ama World War ambao mpaka sasa hawatajwi na hawajulikani. Lakini ikiwa tutahusisha jamii kwa jumla katika jambo hili itakuwa vizuri. Kwa hakika wale wakongwe wetu kule mashinani wanaijua historia ya nchi yetu ya Kenya vizuri. Nashukuru sana kwa kunipatia nafasi hii. Nawaomba Wakenya wenzangu tuunge mkono Mswada huu ili hata kesho kukiwa kuna haja ya kujitolea mhanga kila Mkenya atajitolea bila kusita. Inafaa kuhakikisha ya kwamba sisi Wakenya tunafikia malengo yetu na azma yetu ili tuwe na nchi ambayo ina mapenzi na maendeleo dhabiti. Kwa hayo mengi nashukuru sana na naunga mkono Mswada huu.
Ahsante Bi. Naibu Spika wa Muda. Ninaiunga mkono Hoja hii. Niko kwenye Kamati ya Utekelezaji wa Katiba ambayo inaangalia mambo yote yanayopitishwa Bungeni ili kuhakikisha kwamba yametekelezwa. Kwanza Hoja hii haihitaji senti ndiyo Mkuu wa Sheria aweze kuitekeleze isipokuwa senti kidogo tu ambazo zitatumika kwa uchapishaji wa sheria. Nilipata nafasi siku moja kuwa katika gereza. Ni kweli kwamba wafungwa wengi wanaumia sana kwa sababu ya kutoelewa sheria ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kizungu. Kwa hivyo kama alivyosema dada yetu sheria zetu zikitafiwa kwa lugha ya Kiswahili utakuwa msada mkubwa sana kwa wale wote ambao wako magerezani. Wale amabo watapelekwa kortini wataweza kutumia sheria ambazo tuko nazo kujitetea. Ni kweli kwamba nchi hii haijafikia kiwango cha kuwa na mawakili ambao wataweza kusaidia watu wanyonge. Kwa hivyo masuala mengi ya kisheria yawekwe kwa Kiswahili. Hata hivyo Kiswahili si lugha rahisi. Ni lugha ambayo ni lazima kila mtu aisome ili aweze kuilewa kwa undani. Mambo mengi ambayo yanaweza kutafiwa kutoka Kiingereza hadi Kiswahili utapata hata Kiswahili ni kigumu zaidi kuliko Kiingereza. Hata hivyo ningetaka kumshukuru dada yangu kwa kuileta Hoja hii na tutaitekeleza zile siku 60 sitakapomalizika.
Ahsante Bi. Naibu wa Spika. Mamlaka ya kuajiri Mawaziri ni mamlaka ya Utawala. Si mamlaka ya Bunge. Kazi yetu ni kuunga mkono ama kukosoa yanayopendekezwa. Nikiendelea kuzungumzia tunayojiuliza leo kwa mara ya kwanza haswa nikizingatia kwamba baadhi yetu wanasoma vipengele fulani vya Katiba kwa sababu vilema hawamo kwenye ratiba ya walioteuliwa; nakiri kwamba kwa sasa vilema hawamo kwenye ratiba ya walioteuliwa kuwa Mawaziri lakini uteuzi huo bado haujakamilika. Hivi sasa tunawakagua wateule 14 lakini Katiba imeruhusu kuteuliwa kwa Mawaziri wasiozidi 22. Kwa hivyo hii ni shughuli ambayo bado inaendelea. Bi. Naibu wa Spika nimefurahi sana kuichangia Hoja hii kama ilivyo kwa sababu
Ahsante Bi. Naibu wa Spika. Nikiendelea lengo letu si kuangalia ni mkoa upi umewakilishwa kwenye Baraza la Mawaziri. Lengo letu ni kuona jinsi huduma ya Serikali itakavyomfikia Mkenya popote alipo bila ya kujali kama anatoka eneo la Tana River Kaskazini Mashariki ama Nyanza. Lengo na maudhui yetu
Ahsante Bi. Naibu wa Spika. Sisemi hivyo kwa sababu ya kuonyesha madharau kwa walemavu. Namuomba msamaha ndungu yangu Mwaura na walemavu wote nchini Kenya. Natumai mhe. Mwaura amefurahi. Bi. Naibu wa Spika nikiendelea lengo na maudhui yetu ya kuangalia uteuzi wa Mawaziri hivi leo ni kutoa huduma kwa nchi ya Kenya. Nimetoka katika sehemu ya Tana River. Tunavyozungumza barabara zimekatika katika sehemu hiyo. Zaidi ya watu 10000 hawana makao. Je tutamkimbilia nani kwenye ofisi ya Wizara husika kuomba usaidizi ili wakazi wa sehemu hiyo wapate huduma? Mizozo imeibuka kwenye kila pembe ya nchi hii. Ni vipi tutapata Waziri haraka atoe huduma inayostahili ili tupunguze ukabila na siasa za vyama? Tunataka tupate Mawaziri ili watoe huduma kwa Wakenya kwa sababu wao hawatakwenda kuuliza ni nani anayetoka Nyanza ama Pwani. Watatoa huduma kwa Wakenya wote kama Mawaziri wa Serikali. Tumeelezwa mengi na Wanakamati wa Kamati ya Uteuzi kuhusu Bi. Kandie. Lakini Wanakamati hao hawakutuambia iwapo mteule huyo hana elimu ya kutosha ama ni mfisadi ama ana matatizo ya kiutu ama ya kitaaluma. Kamati hiyo imetuambia kwamba Bi. Kandie hafai. Je imekuwaje hafai? Niliisoma Katiba na haswa Kifungu husika Kifungu 12(a) na (b). Hadhi ya Kamati ya Bunge ya Uteuzi ni sawa na ile ya Mahakama Kuu. Kamati ya Uteuzi ina uwezo wa kumshurutisha mtu yoyote kuleta habari yoyote inayohitajika kwa shughuli ya Kamati hiyo. Unapokosa kuitumia fursa hiyo na kuleta Bungeni Ripoti ambayo haiambatani na maono yako na kutuambia kwamba Bi. Kandie hafai kuhudumu kama Waziri unatuambia nini? Wakenya wanaliangalia Bunge hili. Si kila mtu ambaye atapata fursa ya kusimama hapa na kuzungumza jinsi ninavyozungumza. Ukipewa wajibu wa kutunga sheria na kuamua ni nani anayefaa kuwa Waziri ni lazima utekeleze wajibu huo kwa haki na uadilifu. Tusizingatie maumbile ya kijinsia ya mtu huyo ama sehemu anakotoka.
Ahsante Bw Spika kwa kunipa fursa hii Kwa niaba yangu na ile ya watu wa Taita Taveta ninaowaakilisha hapa Bungeni naleta rambirambi zangu kwa watu wa Juja na hata familia ya Mhe Waititu almaharufu Wakapee Nataka kumwomboleza mheshimiwa huyu kama kiongozi shujaa sana Alikuwa mpole na mpenda watu Kipindi kidogo nilichojuana na yeye nilimwona kama mtu aliyekuwa na upendo sana Nilimfahamu pia alipokuwa anafanya uhamasisho wa mambo haya ya saratani Mara kwa mara tukipata fursa ya kukaa na yeye alituongelesha na kutueleza umuhimu wa kuzingatia afya zetu kwa kwenda kupata uchunguzi wa kimatibabu Alitupatia historia ya alivyopata kujua kuwa anaugua ugonjwa huu wa saratani Kwa hivyo tunamwomboleza kama shujaa aliyepigana vita na ugonjwa huu wa saratani na alikuwa na matumaini makubwa ya kushinda vita hivyo Tulikuwa tunakutana na Mhe Wakapee katika ibada zetu za misa za Wakatoliki hapa Bungeni Kama Wakatoliki kipindi hiki cha Kwaresma ni kipindi cha kusali kufunga na kutoa Kama Wakatoliki tutamwombea sana Mungu aipatie familia yake faraja Eh Bwana umpe eh Bwana na Mwanga wa milele umwangazie milele ili apumzike kwa ai Amina Ahsante sana Bw Spika
Ahsante Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili niweze kuichangia Hotuba ya Rais. Ningependa kuchukua fursa hii kumpongeza Rais kwa kutekeleza majukumu yake ya kuja na kutuelezea maendeleo ambayo Serikali yake imefanya katika muda wa mwaka mmoja uliopita. Ni muhimu tufahamu kwamba katika nchi hii tuna matatizo. Ni matatizo ambayo Rais ameyakubali. Ni matatizo ambayo tunakumbana nayo kila siku. Nilifurahi Rais aliposema kwamba barabara ya kutoka Lamu kwenda Turkana kwa sababu ya bandari ya Lamu iko kwenye mipango ya Serikali. Masikitiko makubwa ni kwamba Serikali inazingatia kujenga barabara hiyo huku matatizo yanayowakumba wakazi wa Lamu kuhusiana na bandari hiyo yakipuuzwa. Serikali haijaweza kuyatatua matatizo ambayo yako Lamu. Kuna watu ambao wamefurushwa kutoka ardhi yao lakini mpaka sasa hakuna hata mtu mmoja ambaye amepewa fidia. Watu hao hivi sasa hawajielewi. Hawajui wafanye nini ama waende wapi. Bw. Naibu Spika wa Muda kuhusu masuala ya IDPs ningependa kusema kwamba wakazi wa Lamu ndio walikuwa IDPs wa kwanza katika nchi hii. Kuna watu ambao walikuwa wakiishi katika maeneo ya Rubu na Mwombore. Hivi sasa watu hao wameondoka kutoka maeneo hayo. Wamekuwa IDPs. Mpaka sasa Serikali inazungumzia IDPs wa hivi majuzi bila ya kuwazungumzia IDPs wa kitambo. Kutokana na haya ni lazima Serikali iwajibike na kujua kwamba tuna matatizo na itafute njia mwafaka ya kuyatatua kabla ya kufanya mambo mengine. Tukizunguumzia masuala ya usalama ni wengi waliochangia masuala hayo. Sote tutakubaliana kwamba usalama ni kama mlango wa nchi hii. Bila ya nchi hii kuwa na mlango sidhani kwamba kutakuwa na mwelekeo wowote. Hivi sasa tunaona watu wakiuawa barabarani bila ya sababu zozote. Kuua na kuuawa limekuwa jambo la kawaida ambalo limeingia kwenye nyoyo za watu. Limekuwa jambo la kawaida. Ni masikitiko makubwa kuona kwamba viongozi ama watu mashuhuri katika nchi hii wanaweza kuuawa barabarani huku Serikali ikisema kwamba inafanya uchunguzi bila ya uchunguzi huo kujulikana ulipofikia na bila ya suluhisho lolote kupatikana. Tunaelekea mahali pabaya. Inafaa Serikali iliangazie suala hili na kuchukua hatua kuhakikisha kwamba mambo haya yamewekwa katika uthibiti maalumu ili kuweza kuikomboa na kuitetea nchi hii katika siku za usoni. Mhe Rais na naibu wake wanazungumzia masuala ya uchumi wa nchi hii. Wanasema kwamba wameweza kupiga hatua na kuinua uchumi wa nchi hii. Masikitiko makubwa ni kwamba Wakenya ambao wanaishi katika nchi hii wanaamuka asubuhi wasijue wale nini ama waende wapi. Kwa kweli katika nchi hii bado kuna watu ambao wana matatizo ya kiuchumi na ambao hawajui wafanye nini. Tukizungumzia suala la mataniti mhe. Rais amesema kwamba dada zetu na akina mama wajifungue bure katika hospitali za umma. Sijui kama ameweza kutembelea mataniti kwenye hospitali za umma na kuona jinsi zilivyo. Katika sehemu za mashinani kuna matatizo makubwa. Kwa hivyo haifai kusema tu kwamba umefanya nini. Ni lazima Serikali iwajibike na kufuatilia masuala hayo.
Ahsante Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa hii nafasi. Hakuna mtu aliye na taabu zaidi ya mchungaji. Hawa watu hawavai viatu wala nguo nzuri. Juzi tulikuwa na mkutano mkubwa ambao ulihudhuriwa na Wabunge wa Samburu ya Magharibi Igembe ya Kati na Igembe ya Kusini. Mkutano huo ulikuwa juu ya mifugo. Wananchi wanateseka sana wakati wa kiangazi kwa sababu mifugo hawapati maji. Kila mtu analia kwamba hakuna maziwa na nyama. Wakati wa kiangazi anayefuga hawa wanyama huzidi kutaabika. Serikali ya Jubilee siyo mbaya; ni Serikali nzuri. Watu wetu wa CORD ni lazima tusikizane nao. Ni lazima tupendane katika Bunge hili ili tuwe kitu kimoja. Katika Kimeru husemekana kwamba atakayeoa mamako ndiye babako. Tuachane na mambo ya Jubilee ama CORD. Tuongee juu ya masuala muhimu hapa. Ule ulikuwa ni mpira uwanjani. Tulicheza na CORD ikaingiza kwa mguu nayo Jubilee ikaingiza kwa mkono ikasemekana kwamba muungano wa CORD Sisi lazima tuwe pamoja tupendane na tusikilizane. Zai kulikuwa na cattle dip ambazo zilikuwa zimejengwa na Moi. Cattle dip zingerudi lingekuwa jambo la maana sana. Mimi nafurahia kuwa na Jubilee na CORD. Ahsante.
Ahsante Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa ruhusa ili nami niongee kidogo kuhusu Hotuba ya Rais. Rais Uhuru ametueleza kuhusu mpangilio wake wa kazi ili kutujulisha mambo anayofikiria kuhusu nchi yetu. Rais Uhuru ameshateua watu ambao tunaweza kusema ni watu ambao kazi yao ni ya mkono katika nchi nzima nao ni Mawaziri. Tunaposema kwamba Rais hafanyi kazi labda kuna watu ambao wamesinzia katika nyadhifa zao. Tusitupe mawe kwa Rais tukisema kuwa hajafanya kazi yoyote. Rais alitujulisha mpangilio wake katika usalama. Aliteua nyumba kumi. Hii itatusaidia katika kuimarisha usalama. Huenda katika miji nyumba kumi isifaulu sana lakini mashinani najua zinaweza. Tukisema kwamba Rais hajafanya chochote tukumbuke zile nyadhifa ambazo inambidi kuteua watu ni chache mno. Sisi Wakenya tuna makabila 42 na tusingeweza kupata sote nafasi hizo. Tuangalie mambo ili tuone ile kazi Rais amefanya. Tunampatia hongera Rais. Naunga mkono Hotuba ya Rais.
Ahsante Bw. Naibu Spika wa Muda. Nakushukuru sana kwa sababu hata sisi wengine tumekuwa tukijaribu sana kuzungumza katika Bunge hili lakini hatukupata nafasi. Nilikuwa nimeingiza kadi yangu alafu nikatoka nje. Sasa ndiyo nimerudi. Jopo lililopendekezwa kwenya Mswada huu ili kuangalia nidhamu ya wanahabari ni jopo ambalo nguvu zake ni nyingi mno kiasi cha kwamba mwanahabari anaweza kupokonywa kibali cha kazi yake na taasisi za uanahabari pia kupokonywa vibali vya kufanyia kazi na akaunti zao kwenye mabenki kufungwa na kuambiwa wasiendelee na kazi yao. Hili ni jambo ambalo halitaweza kukubalika. Cha msingi ni kuweza kuangalia na kupima uanahabari ulio na nidhamu na uanahabari usio na nidhamu na wenye kutumia nguvu. Naibu Spika wa Muda pengine ningezungumza kwa Kingereza ili wenzangu ambao hawaelewi lugha sanifu ya Kiswahili waweze kuelewa. We need to address media so that there is a balance between aggressive reporting and responsible journalism. Hilo ndilo jambo ambalo linaleta utata katika Kenya kwa sababu wanahabari wengi ni wale ambao hawana taaluma ya uanahabari mwafaka. Hivyo basi wanatoa habari ambazo zina uchochezi ama zinapita mipaka ya kisheria. Lakini tunapofuata njia sawa tutaweza kuwa na habari sawa. Wakenya wenzangu lazima tutambue kwamba Kenya tuko miongoni mwa nchi ambazo zimesifika kwa kulinda haki za wanahabari. Ndio sababu katika nchi kama Ethiopia na Eritrea kuna wanahabari wengine ambao wamekimbilia Kenya ili kuja mafichoni na kupata afueni. Naibu Spika wa Muda ikiwa tutaweka sheria ambazo tutampatia Waziri nguvu nyingi katika baraza hili la wanahabari basi tutarudi katika zile siku za giza; siku ambazo habari zitakuwa si sawa. Mfano mzuri ni juzi katika nchi yetu ya Kenya. Wanahabari wetu walitupatia matukio muhimu sana; matokeo ya uchaguzi wetu mkubwa matukio ya uvamizi katika soko la Westgate ambayo ni mambo ya kigaidi na pia habari kuhusu kesi inayoendelea katika Korti la Kimataifa ICC. Iwapo jambo hili la wanahabari litakuwa chini ya himaya ya Waziri ambaye amekula kiapo kulinda Serikali yake basi mambo mengi kuhusu kupata habari hayatakuwa sawasawa. Walalahoi Wakenya maskini hawangejua yaliyojiri katika soko la Westgate kama nguvu zote nyingi zitakuwa zimepelekwa katika ofisi ya Waziri. Tunaona hata lile jopo Bw. Waziri ndiye atatengeneza. Naibu Spika wa Muda hata lile jopo la rufaa ambalo kwa Kingereza tunaliita tribunal ni yeye ataliunda. Wakati jopo hili la kuangalia mambo ya utetezi litakuwa limepeleka mapendekezo yake kwa Waziri basi Waziri anaweza kusema kwamba mtu fulani ua mwandishi habari amekosea katika jambo hili. Lazima tujue tutokako ni mbali na tunakofika ni karibu. Iwapo tunataka kubaki pale karibu tulipo na kulinda wanahabari; kuhakikisha Wakenya walalahoi wamepata haki zao za kimsingi ambazo ni Katiba iliowapa haki kama hizo tuwache wanahabari wenyewe watengeze jopo lao ama baraza lao kuu la kuangalia haki za wanahabari. Tunajua kwamba baraza hili bila ya kuwa na hilo tume la malalamiko lina nguvu zaidi. Mswada huu umezungumzia mambo mengi zaidi ambayo yameangazia vile watalinda wanahabari na vile watalinda nchi katika kuangazia habari. Kwa hayo mengi ama machache ninapinga Mswada huu. Ikiwa Mswada huu utaendelea basi Wabunge wenzangu tuweze kuupiga msasa tufanye marekebisho madogo madogo ndipo tuweze kupata Mswada ambao utawapatia hadhi wanahabari na sisi tunaosikiza habari. Asante.
Ahsante Bw. Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kuiunga mkono Hoja hii kwa sababu inaangazia suala muhimu sana. Ni kweli kwamba katika nchi hii kuna uhaba mkubwa wa madaktari na madawa. Uhaba wa madaktari umeathiri sana utoaji wa huduma za matibabu kwa jamii na haswa katika sehemu ninakotoka ya Tana River. Katika sehemu yangu ya uwakilishi Bungeni ya Galole kuna sehemu ambazo ziko umbali wa kilomita 200 kutoka mjini Hola kama vile Waldena Wayu Chifiri na Haroresa. Katika sehemu hizo kuna uhaba mkubwa wa madaktari na hospitali. Hakuna mabarabara katika maeneo hayo. Kukinyesha wagonjwa husafirishwa kwa punda mpaka Hola. Hospital ya Hola ndiyo hospitali kubwa pekee katika kaunti lakini haina vifaa muhimu kama vile chumba cha kuhifadhia maiti na mtambo wa kupigia picha za X-Ray. Madaktari pia ni haba. Madawa na vifaa vingine
Ahsante Bw. Spika kwa kunipa hii nafasi niongee. Nilikuwa nataka kumkosoa dada yangu Mhe. Millie Odhiambo. Hufai kusema: "Unaongea na Kiswahili." Unafaa kusema: "Unaongea kwa Kiswahili." Ahsante.
Ahsante Bw. Spika. Nasimama kuunga mkono Hoja hii baada ya kurekebishwa kwamba mhe. Mututho apewe nafasi ya kufanya kazi ya kupigana na shida hii kubwa humu nchini. Kwetu sisi tunaotoka pwani hili ni suala la kusikitisha. Watoto wetu kule pwani wanazaa watoto kabla watoto hao hawajafika muda wao. Watoto wanazaliwa wakiwa vilema na matatizo kibao kwa sababu ya matumizi ya mihadarati. Ukienda kule Mkoa wa Kati na hata Mkoa wa Pwani utawakuta vijana wakiwa wamelewa mchana na hawana habari kuhusu yanayoendelea. Tunamtaka mtu kama mhe. Mututho apigane na mihadarati na pombe nchini Kenya. Haiwezekani kumkataza kazi na hali tunamsifu kwa kazi nzuri aliyoifanya akiwa Bungeni kupitia sheria aliyoleta dhidi ya shida kubwa iliyotukabili humu nchini. Sisi tumemwona hata kule vijijini akiangalia kunaendelea nini. Ningependa kuwaambia wenzangu kwamba mhe. Mututho hata kabla hajateuliwa kwa wadhifa huu alipitia kule kijijini kwangu Taveta kuangalia ni njia zipi zinatumiwa kupitisha pombe haramu ambayo inaumiza watu. Vile vile anaelewa njia za kupitisha bhangi zi wapi. Kusema ukweli si kawaida mtu kutumia hela zake kufanya kazi zile isipokuwa ni vile yeye anajua vijana wetu maisha yao yataharibika kwa ajili ya kutumia madawa ya kulevya na pombe. Je ikiwa mtu kama Bw. Mututho hawezi kupatiwa hii kazi nani mwingine atapatiwa? Bw. Spika mtu akiwa na kesi kortini isiwe sababu kwa sababu korti itaamua ikiwa mtu anafaa ama hafai. Kwa sasa hivi tumpe Mututho nafasi ili afanye kazi atusaidie hasa sisi wazazi tulio na kilio na uchungu. Naomba kuunga mkono Hoja hii.
Ahsante Bw. Spika. Ningependa kuchangia hili jambo ambalo ni muhimu. Hasa ni kwa sababu wakati wa asubuhi pengine kuna jambo ambalo nilinena ambalo lilikukera kwa sababu nilikuona ukiniangalia kwa jicho kavu. Hata hivyo ndugu Spika ningependa kusema kuwa Bunge hili linaheshimika. Ni Bunge la wawakilishi. Sisi sote tumeteuliwa ili tulete mambo ambayo Wakenya wanatarajia yatatuliwe. Ikiwa tungependa kufanya kazi kwa pamoja na tuheshimiane lazima pawepo mazungumzo ambapo tutakubaliana kuwa kuna mambo makubwa ya kikatiba ambayo yanamkera kila mwananchi humu nchini. Lazima tufanye kazi pamoja. Ingawa kwa upande mwingine mko wengi tungependa wakati mwingine kama jana mtusaidie kupitisha sheria ambazo zitawasaidia wananchi. Kwa upande wetu tungependa kusikia mnayosema ili tuwasaidie kuendeleza Serikali na mshikilie uongozi jinsi mnavyofanya. Hatuna tashwishi kabisa kuwa ninyi ndiyo mlichukuwa kura na kuwa ninyi ndiyo chama kinachotawala na pia mna miaka minne mbele yenu na sharti mtekeleze hili jambo. Lakini lazima pia sisi mtuheshimu kutoka upande huo. Utaniwia radhi ndugu Spika nikisema kwamba wewe kama mwenyekiti wa Bunge hili ningependa kukusihi wewe kama rafiki yangu - tumefanya siasa na wewe hapo mbeleni na tukasoma nawe - uwe mtu ambaye ana roho safi ili uwe unatuangalia. Hata kama utaona tunafanya makosa ndani ya Bunge hili uwe unatuongoza na kutueleza mahali ambapo makosa yamefanyika ili tujirekebishe na tuwe na mijadala ambayo itaheshimika Kenya hii. Ahsante ndugu Spika.
Ahsante Bw. Spika. Nitaiunga mkono Hoja hii nikitumia lugha ya mama ya Kiswahili.
Ahsante Bw. Spika. Tafadhali ndugu zangu muniwie radhi. Tukiikuza lugha yetu ya Kiswahili Kenya itakuwa nchi nzuri zaidi. Bw. Spika kwanza ninaiunga mkono Hoja hii kwa sababu sisi kama wanakamati wa Kamati ya Bajeti ya Bunge tuliketi pamoja tukakubaliana juu ya Ripoti hii. Hakuna mwanakamati hata mmoja aliyepinga masuala ambayo Mwenyekiti wetu ameyaangazia. Kwa hivyo ninawasihi wanasiasa wasilete siasa kwa ugavi wa mali humu nchini na haswa kuhusu masuala ya Bajeti. Kama kuna jambo ambalo walitaka kulizungumzia wangekuja kwenye ile mikutano iliyoandaliwa washikadau kule mashinani. Wangezungumzia mambo hayo wakati huo. Kwa hivyo haifai mtu yeyote kusema kwamba hatukufanya vile walivyotushauri tufanye.
Ahsante Bwana Spika. Nimesimama kuiunga mkono Ripoti hii. Bado napinga wazo la kumtoa huyu dada yetu Ashubwe. Sababu moja ambayo napinga ni kuwa wanadamu kadri tunavyoishi huko nje tuna maadui wengi sana. Hakuna yule ambaye hakutakii mazuri atakaye kuunga mkono. Kwa hivyo katika wale watu wa Central Organisation of Trade Unions (COTU) ambao walipinga uchaguzi wa huyu mama pengine wengine ni watu walikosana naye kwa njia moja ama nyingine. Kwa hivyo mimi sioni kama hiyo ni sababu ambayo inapaswa ichukuliwe kwa uzito kumnyima mama huyu nafasi. Naomba marekebisho yafanyike na mama huyu achukuliwe kuwa mmoja wa Tume hii. Naunga mkono Ripoti hii hasa kwa upande wa Dkt. Ai Yuda Komora. Ni mtu ambaye namjua kwa undani sana na ambaye amefanya kazi sehemu nyingi. Namjua kwa njia zote. Ako na uzoefu wa kazi. Bwana Spika tafadhali naomba unitetee.
Ahsante kwa kunipa fursa hii. Nilikuwa nataka kuipatia kongole Kamati husika na kusema umuhimu wa hizi jahazi kuvukia pale Likoni ni muhimu sana kwa ajili ya usafirisaji wa goods nyingi ambazo zinaingia nchi hii. Kwa hivyo ni muhimu watu watimize majukumu yao.
Ahsante kwa kuniruhusu nichangie Hotuba ya Rais wetu mhe Uhuru Kenyatta. Ningependa kumpongeza kwanza kwa sababu ametuonyesha mfano ambao tunastahili kufuata kama viongozi kwamba sheria iko juu yetu sisi. Yeye alipojitoa mhanga kwenda Hague alikuwa anatuongoza kwa mfano bora. Ninampongeza kwa kitendo hicho. Rais alipomkabadhi msaidizi wake mhe Ruto mamlaka alikuwa anatuonyesha kwamba hana tamaa. Alituonyesha kwamba si lazima abaki kama Rais. Alituonyesha kwamba yuko tayari wakati wowote kutoa nafasi ili mtu mwingine ashike mamlaka. Hii ina maana kwamba hata baada ya wakati wake kuisha hatatuletea matatizo ya kulazimisha kubaki kwenye mamlaka; ataondoka kwenye kiti ili yule ambaye Wakenya watamchagua achukue nafasi. Jingine la kushangaza ni tabia aliyotuonyesha Rais Uhuru Kenyatta. Aliteremsha hadhi yake akawa sawa na mwananchi wa kijijini. Sisi tulioandaa naye kwenda Hague tulijionea kwa macho yetu kwa sababu tuliishi naye katika hoteli duni tukala mtaani na tukatembea kwa miguu. Hiyo ni heshima kubwa sana kwa sababu aliheshimu Umoja wa Afrika na kuonyesha kwamba asingepeleka Kenya kortini ndiposa akaenda kama mtu binafsi. Ninampongeza kwa kitendo hicho. Lingine linalojitokeza hasa kwa wale wanaosema kwamba Rais alihatarisha maisha yake ama wasimamazi wake walihatarisha maisha yake ni kwamba Rais Uhuru anatawala watu anaowaamini. Yeye anaamini hawawezi kumdhuru ndiposa alipowasili kutoka Hague aliingia kwenye gari lake na kupungia wananchi mkono wake. Yeye si Rais wa kimabavu. Hayaanzi sasa haya anayofanya Rais Uhuru. Alituonyesha alipokuja Pwani kwa maana tulienda naye hadi Public Beach kuogelea naye. Hii ina maana kwamba yeye ni Rais ambaye amejitolea ili amsikize mwananchi wa chini. Ukiongoza nchi kwa namna hiyo basi utaelewa wanachotaka wananchi. Katika Hotuba yake amezungumzia pia kuhusu wale walioathirika kwa mfano wale ambao wako kwenye kambi. Kesi haionyeshi kwamba ni ya maana kwa sababu tuliyasikia kwa masikio yetu na tukajionea. La muhimu ni Wakenya wawekwe mahali pamoja ili tuzungumziane na tuelewane ili yule ambaye aliumia apatiwe ridhaa yake kisha tuishi kama tulivyokuwa tukiishi zai. Hizi kesi zikiendelea tutakuwa tunatonesha vidonda. Badala ya vidonda kupoa kila kuchao tutakuwa tunavitonesha. La muhimu hapa ni kuwaita wale ambao waliathirika wazungumziwe na waweze kupatiwa kile kitawawezesha kuendelea na maisha ya kawaida kama ilivyokuwa wakati wa nyuma. Ninampongeza Rais. Akifuata mwenendo aliotuonyesha ni kweli Kenya itasonga mbele na tutadumisha ai yetu. Ahsanteni.
Ahsante Mhe Naibu Spika Ningependa kutumia fursa hii kumpongeza Mhe Kassim Tandaza kwa kuja na Mswada huu Sote tunafahamu kwamba ukulima ndio uti wa mgongo katika maisha ya leo Mmea huu ambao Mhe Kassim Tandaza ameutaja ni mmea ambao unapatikana katika sehemu za Pwani hususan katika maeneo ya Lamu na Kwale Kabla sijazungumzia mmea huu ningependa kuzungumzia swala nzima la ukulima na faida ya ukulima hususan katika nchi hii na eneo la Pwani Mbali na kuwa tunafahamu kwamba ukulima ndio muhimu sana katika uchumi wetu tumeona wazi ya kwamba watu wanategemea ukulima katika mambo mengi Kwa masikitiko makubwa nikizungumzia eneo la Pwani ukulima umefifia sana kwa sababu ya kutotiliwa nguvu na kutosaidiwa na Serikali Ninaamini kwamba Wapwani wanapenda maswala ya ukulima na wanajitahidi sana Lakini katika swala hili Wapwani hawajasaidika na namna ya kujiendeleza na ukulima wao Kwa hivyo Mhe Naibu Spika tunapojadili swala hili ni vyema tufahamu na Serikali ijue ya kwamba Wapwani wanahitaji usaidizi katika kuendeleza ukulima Kuwe kwamba tuko na ardhi za kutosha na mimea ya kutosha Katika hali hii tunaamini ya kwamba angalau tutapata misaada kama vile misaada mingine inavyotolewa katika sehemu nyingine katika nchi hii Tukifanya hivyo Pwani itakuwa na ukulima mwingi na wengi watajiingiza katika jambo hili ili waweze kusaidika na kusaidiwa kuliendeleza jambo hili Vile clienteles ni vyema tufahamu kwamba katika hali ya uchumi wetu hivi sasa ukulima ndio jambo ambalo tunahitaji kulipea kipaumbele Ardhi tuko nazo na wanaohitaji kufanya ukulima tuko nao lakini Serikali lazima ijitokeze kupitia kwa wizara husika kuhakikisha ya kwamba wakulima hawa wamesaidiwa kwa njia zote wanazotaka na kuhamasishwa ili kuhakikisha ya kwamba wameweza kufanya ukulima wao ili kujiendeleza na kujimudu katika maisha ya leo Kwa haya ni wajibu wa Serikali kuhakikisha wakulima wa sehemu zote wamefaidika hususan Wapwani nikiamini pakubwa kwamba wakulima wa Pwani wameachwa nyuma kwa kutosaidiwa na Serikali katika swala nzima la ukulima Ahsante
Ahsante Mhe Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hi Mimi pia najiunga na wenzangu kumpongeza ndugu yetu mhe Tandaza mbunge wa Matuga kwa kuleta Mswada huu ambao unarekebisha sharia za mimea hapa nchini Kwanza ningepende kuto risala zangu za rambi rambi kutoka kwangu pamoja na jamii yangu eneo bunge la Taveta na Taita Taveta kwa ujumla kwa jamii za wabunge waliokufa Bunge hili la kumi na mbili limepata kipigo cha kuwapoteza wabunge wengi Tunawaombea na tunajua wametutangulia mbele ya haki Kule walikokwenda Mwenyezi Mungu aweke roho zao pahali pema peponi Mti huu wa Bixa au mrangi kama unavyoitwa pwani ni mti muhimu sana Mbegu zake ni za muhimu Si bure tu Mhe Tandaza amelivalia njuga jambo hili Eneo lake haswa kule kwale ndiko kiwanda cha Bixa kiliko ambacho inaweza kuhakikisha mmea huu wa Bixa unapatia watu faida Ni sawa ikiwa mmea huu wa Bixa utaorodheshwa pamoja na mimea mingine muhimu hapa nchini Si jambo la kutosha kuorodhesha tu Orodha hizi zikitoka mimea hii lazima ipatiwe kipaumbele Serikali ya taifa na serikali za magatuzi ziangalie kuwa mimea hii inapatiwa umuhimu haswa kwa kuwasaidia wakulima waweze kupata mbegu zinazofaa na kuwafunza ukulima wa kisasa maana yake kule mashinani zaidi wakulima wengine hulima kiholela kwa sababu hawapatiwi mwelekeo wa njia za kulima za kisasa ili wapate haki yao kutokana na jasho lao la ukulima Maeneo mengi yana mimea tofauti tofauti ambayo yana faida hapa nchini Kwa mfano kuna mkorosho mnazi ndizi kutoka maeneo yetu ya Taveta na maeneo mengi hapa nchini vile vile mihogo viazi vitamu ndegu iliyotajwa kuwa inapandwa hapa nchini na mimea mingine mingi ikiwemo kahawa na chai Si i kuwa vitu vyote vinavyopandwa hapa nchini ni vya umuhimu na vinatumika ulimwengu mzima isipokuwa wakulima wasipopatiwa ujuzi wa kuhakikisha kuwa wanaweza kulima kwa njia za kisasa na kuhakikisha mavuno yao yanakuwa ya gredi ya juu itakuwa shida kwa mkulima kupata haki ya jasho lake alilolitoa Ukweli ni kwamba hapa nchini mambo ya kilimo ni ya muhimu Yamewezesha wazazi kujiendeleza na kusomesha watoto na kubadilisha uchumi wa nchi hii Lakini hivi juzi tuliona kuna vitu ambavyo vinaweza kukaa sana na kuna ile mimea ambayo mazao yake hayawezi kukaa kwa muda mrefu Kwa mfano nataka kuzungumzia ndizi ambazo zinatoka kule kwetu Utakuta kuwa ndizi hazikai kwa muda mrefu Ni kati ya ile mimea ambayo tunajua itakuwa na matatizo Tunajua mahindi yanaweza kukaa kwa muda lakini juu ya hiyo mahindi pia lazima yapatiwe bei inayostahili Vilevile Serikali inafaa kuhakikisha kuwa wafanyakazi wa taaluma ya kilimo wanaweza kuwasaidia wakulima kupata haki yao Ukienda nchi za nje utakuta kuwa kahawa na chai nzuri zaidi zinazotumika kule ni zile za kutoka Kenya Saa zingine wanachanganya kahawa yetu na zingine lakini zaidi sana kahawa ya Kenya inasifika kila mahali Ukienda Marekani utakuta ndiyo inasifika; kila mahali duniani Vilevile wamechukua chai yetu wakachanganya na chai zingine ambazo hazina utamu kama ya Kenya Chai yetu inajulikana ulimwengu mzima Swali ni kuwa je wakulima wetu wanapata haki yao? Hilo ndilo swali kubwa ambalo Serikali yetu itatusaidie ili wakulima wetu wapate haki yao sio eti wale wanaofanya biashara ya mimea hii na mavuno haya ya kahawa ndio wanaofaidika peke yao Bixa ama mrangi ni mbegu zinazotumika kutengeneza rangi na hata kwenye chakula na kwa vitu vya urembo vya akina mama Juu ya hapo kitu ambacho kinaweza kutumika kwenye chakula ni kitu ambacho Serikali ingekipatia nguvu sana ili kiwanda kile kijengwe upya ili wakulima wa maeneo hayo na hata wakulima wengine wahimizwe kulima na kuvuna mbegu za mrangi Ni dhahiri kuwa Kenya tumezoea kufanya ukulima wa kutegemea mvua Mvua ikichelewa tu kidogo basi kumeharibikiwa kwote Serikali kuu imekuwa ikiweka mkazo kuhakikisha kuwa imejenga madimbwi ya maji kila mahali Lakini naona kuwa ugawaji wa hayo madimbwi hauendi inavyotakikana Hivyo basi kuna umuhimu wa Serikali kuhakikisha kuwa madimbwi hayo ya maji yanatengenezwa kila maeneo ili wakulima wote hata wenye kutoka maeneo kame waweze kupata maji Mvua ikinyesha tunapata mafuriko ambayo yanaharibu kila kitu - yanaua watu na mifugo na kumaliza mimea Maji haya yakitumika vizuri yataweza kutuletea faida wakati wa ukame Namalizia kwa kumuunga mkono na kumpongeza kaka yangu Mhe Tandaza kwa kuleta Mswada huu ambao utarekebisha orodha ya mimea ambayo imetejwa kwenye sheria ya mimea hapa nchini Naunga mkono
Ahsante Mhe Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii kuchangia huu Mswada kuhusiana na sheria hii ambayo imeletwa na Mhe (Bi) Odhiambo-Mabona ambayo itasaidia watu kupata watoto kwa njia ambazo si za kawaida Mwanzo naunga mkono Mswada huu hususan kwa watu wawili ambao wameoana wanataka kupata watoto na wana shida kwa sababu ya njia moja au nyingine na kuwa madaktari wamesema kuwa bado wanaweza kupata watoto ikiwa watatumia njia hii ya kiteknolojia ambayo inatumiwa pia sehemu zingine ulimwenguni Kuna maswala tofauti katika huu Mswada ambayo ningependa yaweze kuondolewa wakati tutakuja kwenye Kamati kumaliza kazi ya Mswada huu Mwanzo nataka kutaja sehemu ya Katiba ya mwanzo kabisa sentensi ya kwanza ya Katiba yetu inayosema kuwa Wakenya tunatambua ukubwa wa Mwenyezi Mungu na muumba wa viumbe vyote Pia kuna sentensi nyingine hapo mwanzoni ya tano nadhani ambayo inasema kuwa kama Wakenya tumesema kuwa tutakuza na tutalinda hali ya afya ya sisi kama watu binafsi jamii na nchi kwa jumla Kitu cha kwanza ambacho ningependa kisiwe ndani ya sheria hii ni neno katika Mswada huo ambalo linaitwa kwa Kiingereza " donor " ama yule mwanamke ambaye atapeana yai lake ama mwanamume ambaye atapeana mbegu yake Kenya ni nchi ambayo wengi wetu tunafuata dini Kuna Waislamu na Wakristo Tunajua katika malezi yetu kuwa kuna vile tunapenda jamii yetu iwe na tunapenda kuheshimu ndoa kati ya watu wawili mume na mke waliokuja pamoja na kuoana Kwa hivyo naunga mkono kuwa ndoa iwe tu ya watu wawili ambao wamekuja pamoja lakini isiwe ya watu ambao wako nje ya ndoa Tayari katika jamii yetu ni kitu ambacho hatuungi mkono Mara nyingi tunalalamika sana kuwa kuna wazazi ambao wanalea watoto peke yao sana sana wanawake ambao tunaita single mothers Ni jambo ambalo Serikali yetu inatafutia suluhu Kwa hivyo hii pia itakuwa njia ya kuongeza idadi ya single parents ama mzazi mmoja ijapokuwa ni kitu ambacho hatukipendi kwa sababu ya tabia zetu malezi yetu na uzoefu wetu Mengine ni kuwa ile mbegu ambaye baba atatoa inaweza kukaa kwa miaka mingi hata baada ya yeye kufariki Mbegu hiyo inaweza kubaki na kutengeneza mtoto Twawaonea huruma watu ambao hawawezi kupata watoto na ndio maana naunga mkono Mswada huu ila pia wakati mwingine tufikirie mtoto atakayezaliwa Je atahisi vipi kuwa tofauti sana na binadamu wengine? Inawezekana kuwa mzazi wake alikufa miaka mitano iliyopita na baada ya mzazi kufariki ndio anaanza kuumbwa kutumia teknolojia Kwa Kiingereza wanatumia neno " stigm a" Hata kama twataka kupata watoto na tuna uchungu lakini pia tufikirie yule mtoto akishazaliwa maoni yake yatakuwa vipi na pia hatajua mzazi wake Pengine asijue babake ama mamake ni nani Kuna huo uwezekano Nishafuatiliza sana kesi nyingi huko Uingereza ambapo teknolojia hii imetumiwa kwa miaka mingi sana Utaona watoto walioumbwa na teknolojia hii wakitafuta wazazi wao wakifika miaka 20 au 30 Kuna mwingine ambaye alipata ndugu zake wengi Mbegu ya babake ilitumiwa kwa watu wengi sana Akafanya bidii kutafuta ndugu zake wote Kwa hivyo ina machungu fulani Kitu kingine ambacho kinanitia wasiwasi ni Kipengele cha 31 kuhusiana na mwanamke kubeba mtoto ambaye yeye hakuchangia yai na ile mbegu ni ya wazazi wengine yaani surrogacy Yeye peke yake ndiye anabeba mtoto Kuna nchi kadhaa ulimwenguni ambazo zimekataa hiyo kwa sababu tofauti tofauti Mojawapo ni kuwa licha ya kuwa mwanamke anasaidia watu wengine kupata watoto hali yake ya akili na fikira itaathirika kwa sababu anabeba mtoto kisha anapeana Ukibeba mtoto kutoka siku ya kwanza inakuwa ni kama wataka kumlinda Unamwona kama ni mtoto wako na una uhusiano naye ilhali baada ya kuzaa inabidi upeane Ndio maana unaona nchi chache zinakataa hiyo kwa sababu kuna athari Ndio amesaidia watu wapate mtoto lakini je athari kwa yule aliyebeba ni zipi? Kuna jambo lingine ambalo nahofia Pengine Mheshimiwa hakuwa na nia hii na nafahamu hivyo maanake niko naye siku nyingi namsikiza na ni mwalimu wangu kwa mambo mengi ya Bunge Samahani sina neno lingine la kutumia isipokuwa hili lakini kwa Kiswahili linaitwa "ushoga" Kwa Kiingereza ni " homosexuality" Hii inaweza kutumiwa kama njia ya kupata mtoto hapa nchini Kenya kwa watu ambao wameamua kuwa wataoana mwanamume kwa mwanamume ama mwanamke kwa mwanamke kwa sababu bado jamii haijakubali Kwa hivyo hiyo ndio wasiwasi yangu kwamba hiyo itatumiwa kama njia ya watu kama hao kupata mtoto Kwa hayo mengi na machache shukran kwa nafasi hiyo
Ahsante Mhe Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi Naunga mkono Ni vizuri tuwe na wafanyakazi wa kaunti ambao wanastakabadhi zinazohitajika Tunaona mambo mengi katika kaunti yanafanyika kiholelaholela saa zingine Hayafanyiki vizuri Tukipata yule ana hizo qualifications zote hapa zikifuatwa kuanzia huo wosia na hao wengine wote na zichukuliwe hizi sheria zimeandikwa hapa itasaidia sana Utaona mara nyingine kwa mfano saa hii kuna kaunti ambazo zimepata pesa nyingi ambazo zinafaa zizitumie zizimalize na ni mkopo wa Serikali kutoka kwa World Bank Lakini utaona kwa sababu sijui ni wale walioko hawana zile qualification au ni uzembe utaona zile kazi hazifanyiki vizuri Saa zingine mtu anaweza kuwa na qualifications zinazohitajika lakini pia akawa hafanyi kazi vizuri Kwa hivyo utaona saa hii kama sasa wakati huu tumepewa pesa nyingi kama Kaunti ya Lamu na World Bank lakini utaona kwa kaunti zimebakia pesa zaidi ya shillingi millioni mia tatu ambazo hazijatumika na watu wana njaa Kama wangepea women representative pesa kama hizo zingekuwa zimetumika vizuri sana katika vikundi Mhe Naibu Spika wa Muda ule mradi unaitwa Climate Smart imagine mwezi unaokuja ndio mwisho Hizo pesa zitabidi zirejeshwe na Serikali ya Kenya inalipa loan Tukipata wafanyikazi ambao wana qualification s na hizo qualities zote ambazo zimewekwa hapa kama integrity waweke watu wa kutoka jamii mbalimbali kila wadi ipate nafasi yake wale walemavu pia wapate nafasi yao youth na akina mama naona itaweza kusaidia sana Ahsante
Ahsante Mhe Naibu Spika wa Muda Kwanza nataka kumpongeza Mjumbe wa Matuga Mhe Kassim Tandaza kwa kuleta Mswada huu wa mabdiliko Wakati umefika sasa wa Wizara ya Kilimo kufanya utafiti kwa kila mmea katika majimbo yetu ili wajue ni mmea upi waweza kutumika kuzalisha na kuleta mapatao katika maeneo haya na nchi kwa jumla Kwa muda mrefu mimea kama kahawa chai korosho na mnazi zilikuwa zikisifika kwa mazao yao Lakini kwa sasa mimea hizi zimefifia Tunajua kwamba kilimo ni uti wa mgongo wa nchi hii Serikali inatakikana kuweka bajeti kubwa kwa Wizara ya Kilimo ili utafiti ufanywe wa kusaidia wakulima wa mimea hizi Kule pwani tuko na mimea ya mnazi mkorosho na Bixa Mimea hii imekua ikileta mapato lakini tangu viwanda vya mkorosho na Bixa vifungwe hali ya uchumi wa jimbo la pwani imerudi nyuma Ni jambo la aibu kuwa kwa sasa tunaagiza tui la nazi kutoka nchi ya Malaysia ilihali pwani tuna mmea huu ambao unaweza kutumika kutoa zao hilo Vile vile kama Serikali inaweza kufanya utafiti wa mimea hii mitatu pwani inaweza kutoa suluhu la ukosefu wa ajiri katika jimbo la pwani na kenya nzima Kwa muda mrefu ifikapo wakati wa uchaguzi watu wengi huja pwani na kuwahadaa wapwani kwamba watawekeza kwa mnazi na kufufua viwanda vya mkorosho na Bixa lakini ukienda kule baada ya uchaguzi mimea hii haitambuliki Nataka kuunga mkono Mswada huu Bixa Mkorosho na nazi ziletwe kataika ibara ya kwanza ya mimea ambayo inaweza kutumika kuzalisha na kuleta mapato katika taifa letu Mnazi peke yake unaweza kuajiri zaidi ya watu alfu kumi Kwa muda mrefu watu wamekuwa wakiongea kuhusu bidhaa moja ya mnazi ambayo ni pome peke yake Mnazi una Zaidi ya bidhaa kumi na mopja Kwa mfano fuvu la nazi linaweza kutumika kutengeneza vifungo Kwa sababu kilimo kimegatuliwa serikali za kaunti zinaweza kuleta mitambo na kuajiri vijana wengi ili waweze kujikimu kuliko kuwapa maslasha wafyeke na kusafisha mitaro ya maji-taka Pesa zinazotumika kule zinaweza kutumika kuwekeza kwa kilimo Mhe Naibu Spika kama waweza kukumbuka mti wa mnazi katika nchi ya Malaysia umefanya nchi hiyo kukua kiuchumi Serikali haijafanya utafiti muhimu wa kuhakikisha kwamba mti huu unaweza kutupatia pato Wakati huu wa ugonjwa wa COVID-19 ni kilimo peke yake abayo imeweza kusaidia wananchi kujikimu kimaisha Naunga mkono Bixa kuletwa kwa ibara ya kwanza ya mimea Vile vile mnazi na korosho ziwekwe katika ibara ya kwanza ili tupate pesa ya kufanya utafiti na kutafuta masoko nchini na nchi za kigeni Naunga mkono Mswada huu wa mabadiliko Ahsante
Ahsante Mhe Naibu Spika wa Muda Ningependa kuchukua fursa hii kuungana na wenzangu kuunga mkono huu Mswada ambao uko mbele yetu kuhusiana na ugavi wa pesa ambazo zinaenda kwa serikali gatuzi Kwa kweli Wakenya mwaka 2010 walisimama kidete kuhakikisha kuwa wamepitisha Katiba ambayo itakuwa na serikali gatuzi Kutokana na hiyo matarajio ya Wakenya yalikuwa ni mengi sana miongoni mwao ni kuona kwamba huduma zimeweza kuwafikia kule mashinani na kuhakikisha kwamba usawa umepatikana na wakaweze kufurahia zile huduma ambazo zilikuwa ziwafikie katika sehemu 47 zilizogawanywa nchini Vile vile ni jambo muhimu sana na ni jambo linalohitaji kuzingatiwa kwamba zile fedha ambazo zinaenda katika serikali gatuzi ni fedha ambazo zinahitaji kuwahudumia wananchi Lakini kwa masikitiko makubwa tumeweza kushuhudia kwa takriban hivi sasa awamu ya pili kuanzia serikali hizi zianze shughuli zake kwamba kumekuwa na matatizo mengi sana husasan katika zile hali za uongozi ambao unapatikana katika sehemu hizo Mbali na maadhimiyo ya Wakenya kutaka serikali za kaunti ziwe zinafanya kazi katika sehemu 47 zilizopo yale yanayoshuhudiwa hivi sasa yamekuwa ni matatizo mengi sana Ukweli ni kwamba Wakenya wanahitaji huduma lakini zile shida na mateso yanayoonekana hivi sasa yanasikitisha sana Mfano utapata kwamba wakati mwingine inafika hadi miezi mitatu au minne wafanyikazi wa kaunti hawajalipwa mishahara Tatizo hili mara nyingi huwa linaambatana na kuchelewa kulipwa fedha kwa hizo serikali Mbali na hayo tukumbuke kwamba haya yote yalifanyika kwa sababu ya kusawazisha na sababu ya kuweza kuinua na kuendelesha uchumi Hili linapopatikana huwa ni jambo la kusikitisha sana Utapata kwamba kama nilivyosema wafanyikazi wanateseka Utapata mtu amefanya kazi yake ambayo labda pengine amepewa na hizo kaunti na pengine amechukua mkopo katika benki kwa sababu ya kufanya kazi yake Lakini pesa hizo anaweza kuzipata baada ya mwaka moja au miaka miwili Kutokana na hayo ni vyema Bunge hili na Bunge la Seneti na hata wale wajumbe ambao wako kule kaunti kuhakikisha kwamba muongozo huu na mwelekeo huu unaendeshwa kwa namna unavyotakikana na kwa namna Wakenya wanafurahia Vilevile ningependa kuchukua fursa hii kuiambia Serikali ya Kitaifa kuhakikisha kwamba kuchelewesha fedha ambazo zinapangiwa serikali za kaunti hakupo Yanapotokea hayo ndipo yale matatizo yote ambayo tunayoyazungumzia hapa yanatokea Wengi wameweza kuyazungumzia Utapata kwamba uchafu umedorora katika kaunti na huduma nyingi hasipo Hivi sasa kama sijakosea kaunti zimepeana ilani kwamba ifikapo tarehe ishirini na nne mwezi huu basi watasitisha huduma zao zote Hii ni kwa sababu Serikali ya kitaifa bado haijawapelekea ule mgao wao ambao ulikuwa upelekwe katika ile Bajeti ya mwaka 2020 na 2021 Mhe Naibu Spika wa Muda kwa kweli kuna umuhimu mkubwa sana wa kuhakikisha kwamba Wakenya wamefurahia huduma ambazo zinapatikana katika serikali zote mbili Wale wanaoongoza katika serikali hizi mbili wahakikishe kwamba Wakenya wameweza kufurahia huduma hizo wameweza kuwajibika na kazi zao na wameweza kuonyesha uongozi mzuri Haitakuwa jambo la busara tusimame hapa leo tuanze kulaumiana kwa sababu dunia hii hakuna ambaye ni mkamilifu Mkamilifu ni Mwenyezi Mungu peke yake Unapochukua majukumu na kuchukua kiapo cha kuhakikisha kwamba umekubali kuchukua yadhifa unaopewa kama kiongozi basi ni jambo la busara kuhakikisha kwamba umeweza kutekeleza yale ambayo ni ya usawa Matatizo ni mengi ambayo yako katika serikali hizi za kaunti Ukweli ni kwamba kuna dharura na kunahitajika pakubwa kuweza kuyarekebisha matatizo hayo tukianza na kuhakikisha kwamba migao hii ambayo inagawanywa kila mwaka kwa serikali hizi za kaunti imeweza kufikishwa katika kila kaunti kwa wakati unaofaa bila ya kucheleweshwa Vile vile wale wahusika ambao wanasimamia fedha hizi katika sehemu hizo wahakikishe kwamba wameweza kutekeleza zile huduma zinazohitajika kwa namna inayofaa na namna inayotakikana Vile vile swala nzima la siasa katika sehemu hizi utapata kwamba kuna malalamishi pia katika kaunti nyingi Utapata kwamba wale ambao ni wahusika wakuu zaidi wanatembea kisiasa badala ya kutembea kiuongozi Ninavyofahamu ni kwamba yeyote ambaye ametoka katika kaunti ile na anayestahili kupewa kazi ambayo anaweza kuifanya katika sehemu ile haimaanishi kwamba awe ni mtu wako kisiasa La msingi ni ikiwa anastahili kupata kazi ile basi ni sawa wale wahusika waweze kuchukua fursa hii kufanya usawa katika kuendeleza mambo kama haya Kwa hayo machache ningependa kuhimiza Serikali ya kitaifa kuhakikisha kwamba matatizo haya hayapatikani kwa sababu yanapotokea shida nyingi ambazo utaziona zinajitokeza katika kaunti lawama inakuwa nyingi na ule uchumi unaaza kuleta shida katika sehemu zile kwa sababu zile fedha zinapokuwa hazijafika katika sehemu hiyo ni wengi ambao wanapata matatizo na wanapata shida sana kutokana na hali hiyo Kwa hayo machache naunga mkono Mswada huu kuhakikisha kwamba hili limeweza kutekelezwa kwa njia inayostahili Ahsante
Ahsante mhe Naibu Spika wa Muda. Ni kweli jina langu ni Samuel Kamunye Gichigi na ninawakilisha eneo Bunge la Kipipiri. Ninasimama kunga mkono Hoja ambayo imeletwa Bungeni siku ya leo. Kwa miaka 50 ambayo tumekuwa huru hatujakuwa na sheria na utaratibu wa kuwachagua mashujaa wetu ambao tunatunukia tuzo za ushujaa katika nchi hii. Wakati wa siku ya mashujaa mwaka huu niliweza kupata maoni ya wananchi wangu wa Kipipiri kuhusu ni watu gani tunaweza kuita mashujaa katika eneo bunge langu. Kuna watu walitajwa na bila shaka niliona kwamba hatukuwa na utaratibu mzuri wa kuwatambua mashujaa katika nchi yetu. Tangu tupate uhuru tumekuwa na mpango ambapo vibaraka na viongozi wa Serikali zilizopita walitunukiwa tuzo za ushujaa. Wale wananchi wetu ambao walijitolea kutetea haki zetu na kulinda hii nchi na kuleta mema na utukufu kwa nchi hii hawakutambuliwa. Wengi wao walikufa wakiwa na shida nyingi. Hatutasahau mashujaa wetu kama hayati mhe. Shikuku Bildad Kaggia Seroney na wengine wengi ambao sisi kama Wakenya hatukuwatambua. Kwa hivyo hii ni Hoja ambayo imeletwa wakati wake. Katika Hoja hii kuna utaratibu mzuri sana wa kuwatambua mashujaa wetu kutoka sehemu mbalimbali na si mashujaa wa kisiasa peke yake. Tuna mashujaa katika michezo waliopigania uhuru na wengine wengi wa kutambuliwa. Pia ninaunga mkono Hoja hii kwa sababu inatoa nafasi ya kutambua na kuamua ni akina nani watakuwa mashujaa. Kama ilivyosemwa na aliyezungumza mbele yangu umma una uwezo wakukataa mashujaa waliochaguliwa. Wananchi wakipiga kura na kusema kwamba hawamtaki mtu fulani kuwa shujaa kamati ya kuwatambua mashujaa haitakuwa na budi ila kumkataa huyo. Mhe.Naibu Spika wa Muda ninafurahia Hoja hii kwa sababu ina sehemu ambayo inapanga kusaidia mashujaa wetu ambao wana shida mbali mbali. Hoja hii itabuni hazina ambayo inaweza kushughulikia mashujaa wetu na wapendwa wao. Kwa mfano kama shujaa atatuacha tutawasaidia wapendwa wake kifedha. Pia ninaunga mkono Hoja hii kwa sababu kuna sehemu ambayo inaruhusu kuondolewa kwa tuzo ya shujaa ambaye anafanya kinyume na matakwa ya nchi ama anajiingiza katika uhalifu. Tunaweza kusema kwamba yeye si shujaa tena. Kwa hivyo ninaunga mkono Hoja hii nikiwa mwongeaji wa pili. Ahsante mhe. Naibu Spika wa Muda.
Ahsante Mhe Spika kwa kunipatia nafasi hii nitoe risala za rambirambi kwa jamaa na marafiki wa rafiki yangu Mhe Waititu Wingu la sizi limetanda katika taifa letu na kule Juja kwa sababu tumempoteza Mbunge na pia rafiki yetu Nilijuana na Mhe Waititu mwaka wa 2013 tulipokuwa tunafanya kampeni Wetu ulikuwa ni urafiki wa mara ya kwanza kwa sababu yeye ni mcheshi na mpenda watu Kama walivyosema Wabunge wenzangu jina 'Wakapee' linatokana na ule moyo wake wakupeana Tulipokuwa na yeye hapa Bunge mara nyingi tulipokuwa tunakunywa naye chai hakuwa anapatia mtu nafasi ya kulipa Pili kinyume na Wabunge wengi ambao hawaishi katika maeneo bunge ambayo wanawakilisha Mhe Wakapee alikuwa anaishi Juja Kila wakati ukienda huko ulikuwa unapata akijiendesha na kukaa na wananchii Labda hiyo ndio sababu waliweza kumpatia nafasi ya pili kuwahudumia kama Mbunge wao La mwisho nilikuwa mmoja wa wale walienda nyumbani kwake alipokuwa anaugua Kila wakati tulipoenda kumtembelea alikuwa anauliza: "Ile Bill yangu imefika wapi?" Hata kama alikuwa anaugua sana Kwa hivyo ni vizuri Mhe Duale amesema kuwa atachukua Mswada huo Kama kuna kitu kizuri tunaeza patia familia ya mwendazake Mhe Wakapee ni kuhakisha kwamba tumeleta Mswada huo na tumeukamilisha Ugonjwa huu wa saratani umekita mizizi katika kila familia Hakuna familia moja katika Bunge hili ambayo inaweza kuwa haijaathiriwa na ugonjwa huu Tunajua kuwa ugonjwa huu ukigundulia mapema unaweza kutibiwa Kwa hivyo hili ni jukumu tunalopeleka kwa serikali za kaunti kuhakikisha kuwa wako na vituo mbadala vya kuangazia ugonjwa huu Kwa hayo machache ningependa kutoa mkono wa buriani kwa familia ya rafiki yangu mwendazake Wakapee Ahsante Mhe Spika
Ahsante Mhe Spika Nataka nichukue fursa hii kuungana na wenzangu ambao wametangulia kuzungumza kwa kupinga na kukataa marekebisho haya Vile vile nataka niseme kwamba nchi hii inawashukuru pakubwa Mhe Raila Odinga na Mhe Uhuru Kenyatta kwa kunyamazisha fujo iliyokuweko nchini Miongoni mwa fujo hizo tulikuwa sisi viongozi Leo hii nchi inashuhudia kwamba hakuna tena makelele na matusi Tunalolijadili mbele yetu ni suala la uchumi na mazingira ama miundo msingi katika nchi yetu ya Kenya Tunayajadili haya yote yaliyoko mbele yetu kama Wabunge tuliopewa fursa Ni mambo mazuri tunapoyaona na kuyasoma lakini yote yanahitaji kutekelezwa baada ya kupitishwa na Bunge Kwa mtazamo wangu nikiwa kama Mkenya na kiongozi anayeishi katika hii nchi haya yote yatahitaji fedha ili kuendelezwa Kwa mfano iwapo twapanga kuongeza maeneo bunge sabini ni lazima kuwe na fedha zitakazoendesha maeneo bunge hayo Vile vile sote twajua na kufahamu namna uchumi wa nchi hii ulivyo Mwisho wa haya yote mimi na wengine tutalazimika kutoa ushuru wa ziada ilhali tunauelewa uchumi ambao tuko nao Hakuna kiongozi atakayekataa mazuri yaliyoko katika marekebisho haya Hofu yangu kubwa ninayotaka wakenya waifahamu ni utekelezaji wa haya mazuri tunayoyajadili yatakapopitishwa Tunavyojua sasa ni kwamba nchi imekumbwa na madeni chungu nzima Lazima hatua za ziada za kuhakikisha kuwa ushuru umeweza kupatikana ili kuyatekeleza haya Ninasimama kupinga kikamilifu haya marekebisho kwa hofu kwamba huu ni mzigo ambao utaenda kwa wananchi baada ya marekebisho hayo Kwa hayo machache asante
Ahsante Mhe Spika Naunga mkono ombi la Mhe Ali Wario Hili tatizo linafaa lisuluhishwe maana likisuluhishwa hata sisi watu wa Lamu tutafaidi Ahsante
Ahsante Mhe Spika Niruhusu pia nitoe pongezi kwa Mhe Yusuf Hassan Mbunge wa Kamukunji kwa sababu ya kufikiria mambo ya Mhe Wangari Maathai Sisi kama Bunge hatutaki hili Bunge la Kitaifa lifanywe kuwa kama kaunti ambayo sitaki kutaja Kuna watu ambao wanaamka na kufanya mambo bila mipango na kuleta uhasama kati ya jamii Ni lazima iwekwe wazi kwamba kama hatuna sheria ambayo imetungwa ni njia gani itatumika na kamati ili kupitisha mambo ambayo yanahusu kuname kitu kutumia jina la na Kiswahili kidogo lakini nitaendelea Mhe Spika Mhe Wangari Maathai alishafariki Alifanya kazi ngumu na alifurushwa na Serikali ya marehemu Mzee Daniel Moi Yule mama alifedheheshwa alivuliwa nguo alivuliwa hadi uchi na alifanywa kuwa mtu wa kuchekelewa na jamii Yule mama hakufa moyo Niruhusu nitumie hii fursa kuwaambia wanawake tulio ndani ya hili Bunge kuwa safari zetu katika siasa si lazima ziwe ni za shangwe na vigelegele Tutapigwa na teargas tutakimbizwa na polisi na tutatolewa nguo Nauliza wanawake tukae kidete kama Mhe Wangari Maathai Niruhusu niseme kwa sababu kuna watu ambao wako na mazoea mabovu Wakishindwa katika sera ama kufanya kazi wao hukimbiza wanawake wakitumia polisi na teargas Mimi nitauliza
Ahsante Mhe Spika. Kwanza ningependa kuwapongeza wote walioteuliwa. Ninaomba nisisitize kuwa uteuzi huo bado haujaonyesha sura ya nchi. Tunaomba sura ya nchi itolewe na iononekane kwenye uteuzi kama huu. Mkuki ni mtamu kwa nguruwe na chungu kwa binadamu. Mhe. Spika ninawaunga mkono wote walioteuliwa kwa sababu wana sifa na wanaweza kazi wanazopewa. Wao hawana shida bali mteuzi yule ambaye aliwateua ndiye ninataka aangazie uso wa Kenya. Lakini wale walioteuliwa ninawapongeza na kuwatakia kila la heri. Mhe. Spika ninaounga mkono.
Ahsante Mhe. Naibu . Langu ni pendekezo kwa Bodi ambayo inahusika na mikopo kwa wanafunzi. Hii ni kwa sababu tunaona kwa mfano katika sehemu ya Kwale tunaweza kumaliza mihula kama miwili au mitatu na hakuna mtoto hata mmoja ambaye amepata mkopo huo. Hii ni keki ya Wakenya wote na inafaa igawanywe sawasawa ndiyo kila mahali watu wapate. Tungependa tujue ni mikakati ngani ambayo wameiweka ili kila sehemu ya nchi iweze kupata pesa hizo ili watoto wetu waweze kusonga mbele na elimu. Hii ni kwa sababu vyuo vikuu vipo hata sehemu za nyanjani.
Ahsante Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Ninawaomba wenzangu wanawake na pia Wabunge wa kiume tuungane kuhakikisha kuwa pendekezo hili lililoletwa hapa halitapita na tuache pesa hizi ziwe katika Tume ya Jinsia na Usawa ya Kenya. Masuala ya jinsia humu nchini na hususan ya wanawake kila mtu anajua kuwa wamekuwa wakiumia kwa muda mrefu. Watoto wa kisichana wanaumia zaidi kuliko wavulana na ukiangalia takwimu unaona kuwa jinsia hiyo inapata shida zaidi. Wasichana wengi zaidi hawaendi shuleni na kadhalika. Kwa hivyo ninaomba tuunge mkono kuwa Tume hii isikatiwe pesa zake na pesa ziweze kubaki pale pale. Tupinge pendekezo hili.
Ahsante Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Naunga mkono maoni ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maji na Mazingira. Tukisema kuwa wenyekiti watoke kwenye kaunti zinazohusika ni lazima kuwe na uwazi na usawa.
Ahsante Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Nikiwa mmoja wa wanakamati tumezungumzia suala hili tukiulizana maswali mengi ili tuweze kuifanya sheria hii iwe rahisi kueleweka na kila mtu na kusiwe na shida kuitafi. Kwa hivyo ninayaunga mkono mapendekezo ya Mwenyekiti.
Ahsante Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Ninaomba Waheshimiwa tuelewane. Tumesoma Katiba na tumeielewa. Tumeona vile vipengele vinavyompatia Rais nguvu. Hata hivyo lazima tutumie akili zetu. Kuna akili za kuzaliwa na zingine tunazipata shuleni. Hapa tunatakiwa tutumie akili za kuzaliwa. Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda ninaomba nisikizwe. Jogoo likikutana na mwamba halizingatii kuvunja mwamba lakini huwa linazunguka mwamba. Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda ninaomba umfahamishe Mhe. Duale kwamba nasi pia tulienda shule na si yeye pekee alienda shule. Ninataka pia nikuambie avumaye baharini ni papa lakini pia kuna nyangumi. Sio lazima kila wakati yale Duale amesema yachukuliwe kama Bibilia. Wakati umefika Mhe. Duale pia aambiwe kuwa ubabe wake si ule utakua unatupeleka kila mahali. Mhe. Duale ninaomba utulie. Ninasema hivi wakati umefika ambapo wakati hizi sheria zinapopitishwa jai tuangalie tuone kama tunaweza kuahirisha kikao hiki. Kama kinaweza kuahirishwa kiahirishwe ili tupate muda wa kuzingatia haya mambo ili tumalize hii sheria.
Ahsante Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Ninaunga mkono watu wa IPOA wapatiwe pesa hizo lakini ninazungumza kwa masikitiko. Sioni kazi IPOA wanafanya kwa sababu mwaka jana kuna vijana wa kwangu Madogo walidhulumiwa na sijaona wakichukua hatua yoyote. Watu watatu walikufa na kuna kijana wa miaka 20 ambaye amekatwa mkono kwa kupigwa risasi na askari wa polisi na mpaka saa hii kijana huyo amezunguka akienda kwa IPOA Garissa. Mara anazungushwa akirudi na mpaka saa hizi hajapata haki yake. Kwa hivyo kama watakuwa wanaongezwa pesa hizi ili wapate kula mishahara minono minono kwa nyumba zao na wananchi wanadhulumika mimi hata sioni faida yake. Lakini ninaunga mkono wapatiwe pesa hizo wazidi kutudhulumu. Ahsante.
Ahsante Mhe. Naibu Spika kwa kunipa hii fursa ili niweze kuchangia Hoja hii. Kabla ya hapo ningependa kuleta suala la kisheria mbele yako. Kama Wabunge kifungu cha Saba cha Katiba ya Kenya kinasema kuwa lugha ya taifa ni Kiswahili. Lugha rasmi ya Kenya ni Kiswahili. Unapoangalia Kanuni za Bunge kifungu cha 77 kinasema kuwa maongezi yote yanayoongewa hapa yaongewe kwa Kiswahili. Sisi tunaoenzi lugha hii tuna matatizo wakati tunafanya utafiti kwa Hoja ambazo zinaletwa mbele yetu. Tumeomba Bunge mara kadha wa kadha itupe Kanuni za Bunge kwa lugha ya Kiswahili ili tuchangie Hoja zinazoletwa hapa Bungeni. Kuzungumza kwa Kiswahili si ujinga. Tunaweza kuzungumza kimombo. Hoja hii ina sehemu mbili. Sehemu moja ni ya wale wanaovamia watu kuiba na kuua. Sehemu ya pili ni wale walioathiriwa. Hoja hii inazungumzia juu ya wale walioathiriwa. Hoja hii haizungumzii juu ya hatua itakayochukuliwa dhidi ya wale wanaovamia watu. Maana ya hii Hoja ni nini basi? Maana yake ni kwamba sisi kama Bunge tuunge mkono mila ya dhuluma na ushenzi wa wafugaji. Tukitangaza wizi wa mifugo kama janga la kitaifa Bunge linaunga mkono hatua ya wezi wa mifugo. Mimi najua athari za wizi wa mifugo. Wizi wa mifugo ni mchanganyiko wa jinai kuu zaidi ya kumi. Kuna uuaji ubakaji ujeruhi wa watu na wizi wa mali. Najua ni jinai aina kumi lakini kuitangaza kama janga la kitaifa na kuwapa pesa waathiriwa ni kuwaambia wezi waende kesho asubuhi kuiba ng'ombe wengine. Hoja hii haina maana. Inaunga mkono wizi wa mifugo. Ili kama Bunge tulaani hicho kitendo hii Hoja haistahili kupitishwa. Ni hatari. Tunapoteza lengo. Najua athari. Najua vile watu wameathiriwa. Najua athari ya mtu akikosa mali yake. Najua vile mtu aliyeuawa anasikia lakini kutangaza wizi wa mifugo janga la kitaifa ni kupoteza njia. Ningependa kumwambia Mhe. Cheptumo aangalie Uganda iliyokuwa na matatizo kama hayo. Mhe. Museveni alituma jeshi kule. Matatizo haya mengi yamezidi katika eneo la Elemi Triangle katika Bara Afrika. Elemi Triangle inamilikiwa na jamii moja. Ikiwa ni sehemu ya Ethiopia South Sudan au Kenya watu wanaoishi Elemi Triangle ni jamii moja. Haya ni masuala ya mila. Mila ya kishenzi; mila ya dhuluma na mila isiyotambua mali wala maisha ya mwanadamu. Tutachukua hatua gani kama Serikali kuhakikisha mila hii ya dhuluma na ushenzi imesimamishwa? Ukisema tuitangaze na tutoe rasilimali tulinde wale watu walioathiriwa hayo matatizo hayataisha. Kesho asubuhi yataendelea. Mimi kama Mbunge sitaunga mkono sheria yoyote inayoendeleza dhuluma ya maisha ya mwanadamu na unyang'anyaji wa mali. Ukiangalia hii sheria upande wa pili unaendeleza wizi wa mifugo. Kwa nini Uganda imefaulu kutatua matatizo ya wizi wa mifugo katika eneo la Karamoja? Kwa nini Ethiopia imefaulu? Ni nini kama nchi hatujaweza kushugulikia ipasavyo kuitangaza janga la taifa? Je kesho asubuhi itazuia wale wavamizi wasiende kuvamia? Hapana. Tunasema tu wale waliovamiwa wapewe pesa na kulipwa fidia lakini wale wanaoenda kudhulumu bado sheria haijachukua hatua juu yao. Kwa hivyo mimi nimesimama kupinga Hoja hii kwa sababu inaendeleza hiyo dhuluma ya wizi wa mifugo uuaji wa watu na ubakaji wa wanawake. Lazima tuisimamishe leo; si kesho. Ahsante.
Ahsante Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii nichangie mjadala huu wa jinsia ya kike. Nakubaliana na mnenaji ndugu yangu Mheshimiwa aliyeongea kuhusu Mswada huu ulioletwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Kisheria. Kama kiongozi katika Bunge hili natumai wenzangu kule nje wananisikiliza ndiposa tuwaambie nini kinachoendelea. Jumamosi iliyopita nilikuwa Bungoma kwa hafla ya mazishi mahali fulani. Mama mmoja aliamka akasema kwamba wale akina mama ambao wako Bungeni hawataki kushughulikia masuala ya akina mama kule nje. Alisema kwamba tuwe na akina mama wengi ndiposa sauti zetu zisikilizwe katika Bunge. Niliwahakikishia wananchi kwamba viongozi ambao tuko Bungeni haswa akina mama tutahakikisha kwamba masuala ya akina mama ama jinsia ya jamii moja yatashughulikiwa. Nimesikiliza wenzangu wakisema kwamba iwapo tutaongeza idadi ya akina mama katika Bunge huenda Bajeti itakuwa juu na nchi yetu itagharamika sana. Wakati walipobuni Maeneo Bunge 290 hawakuangalia mambo ya bajeti. Lakini tukizingatia kuwa na akina mama katika Bunge wanaongea kuhusu bajeti. Ningependa kumshukuru Mhe. Millie Odhiambo kwa kusema kuwa akina mama pia wanafaa kuja Bungeni na vile vile kuwakilisha nchi yetu katika nyadhifa mbalimbali. Ningependa kuwashukuru kwa sababu walihakikisha kuwa tuna akina mama 47 katika Bunge hili. Tumeshikana na wale wenzetu ambao walichaguliwa - ukiwa mmoja wao - kuhakikisha kuwa tunapigania masuala ya akina mama nchini. Ningependa kumshukuru Mhe. Rais kwa kumpendekeza Waziri Amina Mohamed kwa Muungano wa Afrika. Tungependa kuwaambia ndugu zetu wa kiume kuwa iwapo wanasema kuwa masuala haya yatatusaidia sisi kama akina mama na viongozi basi lazima wafikirie pia ndugu au dada zao ambao wanaweza kuwa kwenye nafasi kama hizi zetu. Ningependa kumuunga mkono dadangu Nyokabi kuhusiana na suala la idadi ya wanawake katika Kamati zetu. Amesema kuwa Kamati yao ina wanawake watano tu ilhali wanaume ni 25. Itakuwa vigumu sana kuzungumzia mambo ya jinsia moja katika Kamati zetu. Ningependa kumwambia Naibu Spika kwamba aende apiganie kiti cha ugavana katika eneo la Bomet. Ningependa pia kuwaambia Millie Odhiambo na Rachel Shebesh kuwa wasiogope kutafuta viti vya kisiasa kwa sababu tutawaambia akina mama wawachague. Tumeelezwa kuwa kuna mtu ambaye alienda mahakama kutaka kujua kwa nini tumechelewa kutekeleza Katiba hii. Nimeshangaa sana kusikia wenzetu wakisema kuwa Katiba hii ni mbaya kwa asilimia 20. Kwa nini waliipitisha Katiba hiyo na makosa hayo bila kuangalia uongozi wa wanawake? Wanawake lazima wawe na nyadhifa mbalimbali katika nchi yetu. Ni lazima tuwatendee haki akina mama ambao ni viongozi nchini. Katika eneo langu akina mama ambao ni viongozi ni wachache sana. Nilikuwa diwani lakini sikubaki hapo kwa sababu nilihakikisha kuwa nimepigania kiti na nikachaguliwa kama mwakilishi wa akina mama katika kaunti. Tusilale bali tuhakikishe kuwa masuala yetu yanatekelezwa. Tukiwa kule nje tunaweza kueleza wenzetu kuwa masuala yao yanawakilishwa vizuri hapa Bungeni. Napinga Mswada huu.
Ahsante Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii ili nijaribu kuiunga mkono Mswada huu. Nikizungumzia mambo ya misitu kisheria ingekuwa muhimu kujua njia barabara na mipaka ya misitu. Katika kaunti ya Samburu tuko na shida sana kwa sababu kuna watu wengi ambao wanaishi kwenye misitu. Ukiangalia rai utaona kwamba wako nje ya msitu. Lakini kwa sababu mpaka wa msitu huo haujulikani wananchi wanahangaika. Hawajui mpaka wa msitu na mahali ambapo wanaishi. Mara kwa mara wananchi husumbuliwa na kuambiwa wako ndani ya msitu. Wananchi hao wako na shida sana. Hata mimi na miaka yangu yote nilizaliwa ndani ya msitu huo. Watu hawana shule hospitali ama maji na wanateseka. Mara kwa mara wanaambiwa wahame kutoka kwa msitu. Kwa hivyo ni muhimu mipaka ya misitu ijulikane ili wananchi pia wapate kujua iwapo wanaishi msituni ama la. Hii ni kwa sababu tumesumbuka sana katika Kaunti ya Samburu. Katika baadhi ya sehemu hizo shule zilijengwa miaka 40 iliyopita na watu sasa hivi wanambiwa wahame kwa sababu makazi yao yako katika sehemu ya msitu. Kwa hivyo ni muhimi mipaka katika makazi ya wananchi na misitu ijulikane. Kuna mpaka ambao umechorwa mara mingi. Kila mwaka huo mpaka uko kwa rai nyingine. Rai zinatolewa kila wakati. Wananchi wanaishi kwa njia ambayo haistahili na watoto wao hawaendi shule. Nikiwa mwakilishi wa Kaunti ya Samburu nimesema kuwa hapo wanapoishi watakuwa na shule. Tumeagana na gavana wetu tukasema lazima tuweke shule na hospitali ili watu wapate njia ya kujisaidia. Mara kwa mara wanaambiwa wako kwa msitu na hawako msituni. Kwa hivyo ni vizuri mpaka ujulikane. Asante kwa kunipatia nafasi hii. Tutazidi kufuata njia ya kutafuta mpaka wa msitu.
Ahsante Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii nami nitoe mchango wangu kuhusu sekta hii ya boda boda. Kama uelewavyo shughuli za boda boda zimeenea kila pembe ya nchi yetu. Huwezi kwenda pahali popote na kukosa vijana wakifanya biashara ama shughuli za boda boda. Kwa hivyo tunakubaliana sote kuwa ni biashara ni sekta ambayo inakua na inahitaji kupatiwa msaada ama kutiwa shime ili ipate kukua zaidi. Imeongeza uchumi wa nchi imetoa ajira; vijana wanafanya kazi wao wenyewe bila kung'ang'ana au kuzozana na watu wakitafuta ajira. Kitu kinachohitajika ni kuboresha sekta hii ili hao vijana wawe wanaweza kutoa huduma kwa umma huduma ambayo ni nzuri huduma ambayo haitaumiza watu huduma ambayo ni rahisi na itarahisisha usafiri. Vijana ambao wanashughulika na kazi ya boda boda mara nyingi wana shida. Moja ya shida wanazokumbana nazo ni ukosefu wa mafunzo ya kutosha. Kama wangekuwa wamefunzwa uwajibikaji na kujua sheria za barabarani kulingana na sheria za usafiri bila shaka ajali tunazoziona nchini mwetu zingekuwa zimepungua. Jambo lingine ni kuhusu vifaa. Utakubaliana nami kuwa mara nyingi hawa vijana wanabebana bila kuvaa kofia ambazo zinaweza kuwasaidia wakati wa ajali. Abiria ambao pia wanabebwa nao hawawezi kuvaa hizo kofia. Hawana nguo ambazo zinaweza kuonyesha mtu usiku kuwa hapo mbele kuna boda boda. Mara nyingi ukosefu wa vifaa unachangia kuweko kwa ajali. Kuna sehemu nyingine za nchi ambapo unaweza kwenda hospitalini ukakuta pahali pametengwa pa watu ambao wamepata ajali ambazo zimetokana na boda boda. Hiyo haimaanishi kuwa biashara si nzuri. Inaweza kuboreshwa na tunaomba serikali ije na shughuli mwafaka za kuweza kuboresha sekta hii ya boda boda. Mna kitu ambacho kinaendelea inchini mwetu kuhusu hawa vijana wetu wa boda boda na polisi. Polisi ambao wamejitoa badala ya kuangalia wezi huko mitaani wamekuwa ni kuamka asubuhi na kujipanga kwa barabara ili kuwanyanyasa hawa vijana. Unaweza kuona kuwa kijana amesafirisha na kupewa Kshs.200 ama Kshs.300 akikutana na polisi bila shaka hakuna kosa litakalo patikana katika gari lake la usafiri. Mara nyingi utakuta analazimishwa atoe hongo kwa polisi; polisi hua hawana haya kuona kijana amerauka asubuhi amepigwa na baridi angalau ajitafutie ajira na hizo fedha kidogo amepata kama Kshs200 pia wanamnyanganya. Kuna mambo mengi tumeyashuhudia hata katika sehemu ambayo nawakilisha Wundanyi. Utakuta boda boda zinazotoka Mgange kwenda Mgange-Dawida polisi wamejipanga njiani kuwanyang'anya hawa vijana pesa. Wundanyi kwenda Wesu ni hivo hivo; Viruga kwenda Wesu hivo hivo Viruga kwenda Mgambonyi ni hivo hivo. Kwa hivyo tunawaomba polisi nao watusaidie kuboresha sekta hii badala ya kuwa tayari kila wakati kuwanyanyasa hawa vijana. Serikali pia ingetoa hundi kuwasaidia hawa vijana. Hawa vijana mara nyingi wanaendesha magari njiani ambayo mara nyingi si yao; hua kuna watu ambao wameyanunua na wakawaajiri vijana ili jioni angalau wajipatie riziki zao. Sasa hawa vijana wataendesha hizi boda boda mpaka lini? Tunatarajia nao pia watapata nafasi ya kuweza kuinuka kimaisha na kutoka katika hiyo sekta ya boda boda na kununua magari kama matatu ; lakini wanaanza chini na boda boda. Litakuwa ni jambo la busara kwamba kwa vile Serikali ilitenga hela ama fedha za akina mama na vijana sasa ifikirie kama inaweza kutenga hela za vijana wa boda boda. Bunge hili lina mamlaka ya kuweza kutoa pesa ambazo zinaweza kutumiwa kuwafadhili vijana ambao wanashughulika katika sekta hii ya boda boda ili iweze kuboreshwa. Hizi pesa za CDF ambazo tunazitumia wengine wetu tumezitumia kuhakikisha kuwa vijana wamepata mafunzo wameelimishwa kuhusu uendeshaji magari na boda boda. Lakini haitoshi. Mara nyingi fedha tulizo nazo ni chache na hazitoshi. Litakuwa jambo la busara Bunge lifikirie kukaa chini na kuona kama tunaweza kuweka kiwango fulani katika kila eneo bunge ambacho kitatumiwa kuwafadhili hao vijana; fedha hizo zitatosha kuwapatia mafunzo na hata mikopo ya kunua pikipiki ili wazitumie kufanya biashara yao. Kwa haya machache naunga mkono Hoja hii ili ipate kuwasaidie vijana wetu huko mashinani.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kuniokoa hapo. Ninaunga mkono Hoja hii. Kule ninakotoka ni shida kubwa sana mtu kuoa. Hii ni kwa sababu watu wengi hawawezi kupata vyeti vya ndoa. Zai vyeti hivyo viligharimu Ksh100. Hivi leo nafikiri vinagharimu Ksh500. Kuna mahali kwingine vinagharimu Ksh1200. Kwa hivyo imekuwa shida kubwa sana. Kama inawezekana vile mheshimiwa mwenzangu amesema ni muhimu watu wapelekewe hivi vyeti kule mashinani. Jambo lingine ni kwamba siku hizi sisi wanaume tuna taabu sana ya kuoa akina mama. Ukisoma magazeti kila siku utaona kwamba akina mama wamekuwa wakiwapiga na hata kuwaua wanaume. Kuna wanaume ambao wanatafuta pesa kwa taabu sana. Wakati umepata pesa mwanamke atasema eti lazima ufe ndio abaki na mali. Kwa mfano angalia mambo yanayotendeka huko Nyeri ambayo yamesimuliwa katika magazeti. Sisi wanaume tuna taabu. Ni lazima tutafute kufuli na mabati ili tujikinge kwenye nguo zetu ndiposa vitu vyetu visiende - imekuwa shida. Ona sasa huko Nyeri mtu aling'olewa "mizigo" yake na hali hiyo "mizigo" ndiyo inasaidia mama. Hiyo "mizigo" imesaidia kila mtu. Hiyo "mizigo" ndiyo inainua mtu. Hiyo "mizigo" ndio umetoka hapo lakini hawana heshima.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii na vile vile kuunga mkono Hoja hii. Ni muhimu sana kuhakikisha watoto wetu wamepata misingi ya kidini na kielimu. Kuna mambo mengi ambayo watoto wanajifunza kutoka kwa mitandao na kwenye runinga. Wakikosa kuwa na misingi ya kidini utapata wanapotea kimaisha. Ni kweli katika masomo tunayosoma tuna masomo ya kidini kama Christian Religious Education (CRE) na Islamic Religious Education (IRE). Lakini ni vizuri ya kwamba watu ambao watakua wanaendesha masomo hayo wawe ni watu ambao wako tayari katika misingi iliyosimama kwa kidini kama vile mashehe ama waliosomea theologia. Umuhimu wa kuwa na misingi ya kidini ni kuwa inaleta uwezo wa kuwapatia watoto mwelekeo katika maisha. Vile vile kuna watoto wanaopoteza ii kwa sababu ya mambo yanatokea yumbani mwao. Kwa wengine wazazi wao wana matatizo ya ulevi ama mama zao wanapitia hali ngumu katika ndoa. Wakienda shuleni watoto hawa hawatulii na kuangazia masomo. Kwa hivyo wakiwa na walimu wa dini watoto hao watapata matumaini na misingi ya kuweza kusimama wakijua kuwa mbeleni kuna maisha bora na vile vile wataweza kutia bidii katika masomo yao. Hoja hii ni ya maana na ni vizuri tume ya kuajiri walimu - Teachers Service Commission (TSC) - wakati wanaajiri walimu wasiangalie mtu aliyepata shahada ya chuo kikuu lakini wazingatie wale ambao wamesomea theologia na wawape nafasi za mbele. Naunga mkono Hoja huu. Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ya kuchangia Hoja hii. Vilevile ningependa kumpongeza Mheshimiwa ambaye ameleta Hoja hii baada ya kuzingatia pakubwa suala la afya katika nchi yetu. Kwa kweli hii ni Hoja ambayo inaonekana ni kama imeletwa Bungeni kama Hoja nyingine za kawaida lakini ukweli ni kwamba suala la afya katika nchi hii limeachwa nyuma sana na limekuwa katika hali ya kutothaminiwa. Mjadala uliopo ni baina ya kauli mbili: Je huduma hii ipatikane katika kaunti au katika maeneo Bunge? Kwa kweli ni jambo la kusikitisha. Hivi sasa huduma hii haiwezi kupatikana katika baadhi ya kaunti hata ingawa tuna miaka 52 ya Uhuru. Hilo ni jambo la kusikitisha. Kuna umuhimu mkubwa nchi hii kuzingatia suala hili kwa sababu kifo kimewekwa na Mwenyezi Mungu. Sababu kubwa ya watu kufariki ni kutokuwa na huduma bora katika sehemu nyingi katika nchi hii. Tukizungumzia huduma hizi kuwepo katika kaunti hata zikiweko katika kaunti mgonjwa anapotolewa mahali anapotoka kukimbilia mahali huduma hii inapatikana kuweza kufikia huduma hii kulingana na hali ya barabara zetu wengi wanakufa katika magari ya kubebea wagonjwa kwa sababu ya misongao ya magari katika barabara zetu. Suala hili lahitaji kuzingatiwa pakubwa. Kuna umuhimu mkubwa kila mwananchi katika nchi yetu ya Kenya kuhakikisha ya kwamba amepata huduma ya kawaida. Watu wengi sana hawawezi kujimudu kwa sababu ya matatizo ambayo tuko nayo. Ni muhimu kuhakikisha kwamba kila mwananchi anayeishi katika Kenya hii amehudumiwa. Wakenya wengi wanasafiri nchi za nje kwa sababu suala hili la afya huonekana ni kama halina thai ama halitiliwi juhudi katika nchi yetu. Siyo kwamba hatuna watu wa kuhudumia wagonjwa. Mipangilio katika Serikali yetu ya kuliendesha jambo hili ndiyo inaleta pingamizi kubwa katika kulifanikisha jambo hili. Uwajibikaji ni jambo muhimu sana. Leo hii tunazungumza kuhusu kuweka huduma hizi katika maeneo yetu ya Bunge lakini ikiwa hakutakuwa na uwajibikaji itakuwa ni kama vile Waswahili husema kumpigia mbuzi debe. Kuna dharura kubwa ya kuwajibikia masuala haya. Wakenya wanaumia. Ni lazima iwapo tumekubaliana kupitisha mambo kama haya ufuatilizaji na uwajibikaji ni lazima upatikane kwa sababu tunaweza kuyapitisha mambo haya lakini yakabaki vilevile kwamba hayana maana yoyote kama inavyosemwa na wenzangu. Inaonekana ni kama ndoto tunajaribu kupanga hivi sasa. Lakini ninaamini pakubwa hakuna jambo ambalo haliwezekani. Utapata kwamba kwa mfano hapa tulipo wakati mmoja palikuwa ni kiwanja tu. Waliofikiria kujenga Jumba hili walikuwa na mpango wakalijenga. Hivi sasa tukisema tutatoa huduma hizi sharti tuhakikishe kwamba kila mmoja amewajibika katika kulitekeleza jambo hili. Hivi sasa tumepeana majukumu ya afya kwa serikali za kaunti. Ingawa hivyo kuna malalamishi mengi.Ni kwa nini? Tatizo liko wapi? Limesababishwa na nini? Tatizo kubwa ni kutowajibika. Je hakuna pesa za kuendesha shughuli hii? Katika kaunti yangu ya Lamu hakuna huduma hizi. Tujiulize kosa liko wapi. Matatitzo yako wapi? Ikiwa ni pesa Serikali kuu inapeana pesa kwa Kaunti ya Lamu. Je ni viongozi walioko pale hawajawajibika kuliangalia suala hili? Anayeumia ni nani? Mwananchi wa kawaida anaenda sehemu nyinginezo kutafuta hizi huduma. Tukisema kwamba tutaweka katika kituo kimoja katika kaunti
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuunga mkono sera hii. Ni kwa nini naiunga mkono? Nchi ya Kenya kama nchi zingine zinazoenedelea katika Bara la Afrika tulipopata Uhuru tulizipa kipaumbele sekta za uzalishaji uwekezaji na biashara kuliko sekta ya haki na sheria. Maswala ya demokrasia na haki za binadamu yamekuwa matukio ya kigeni katika nchi ya Kenya. Ukilinganisha uwekezaji wa rasilimali katika sekta za biashara na uzalishaji na sekta ya sheria ni kama uwekezaji katika sekta ya sheria umeanza juzi. Kwa sababu hiyo dhuluma dhidi ya jamii na wananchi wa Kenya imeenda juu sana. Ni furaha yangu kubwa kusimama hapa kuzungumzia sera itakayoangalia haki za binadamu itakayoboresha demokrasia na itakayoleta sekta tofauti tofauti pamoja ili kushughulikia usalama wa taifa la Kenya. Naiunga mkono na inanifurahisha zaidi. Sehemu kame za Kenya kama dera Wajir Garissa Lamu na Tana River zimeshuhudia mauaji mengi tangu tulipopata Uhuru. Kwa nini? Ni kwa sababu taasisi za sheria zinazohusika na haki za binadamu zimekuwa duni katika sehemu hizo. Hii sera inatupa fursa ya kurekebisha sheria za kitaifa. Kuna jamii tofauti tofauti ambazo katika mila zao zina mahakama za kitamaduni. Mfano ni Njuri Ncheke . Hizo mahakama zinakaa kutatua matatizo baina ya jamii hizo. Jamii ya Oromo iko na mahakama yao ambayo inakaa kusikiliza na kuhukumu makosa baina yao. Hii sera itaipatia jamii ya Oromo fursa ya kuendeleza sheria zao za kutatua matatizo na mizozo katika jamii. Tukiongea kuhusu sekta ya uongozi na haki tusiangalie tu kitaifa ama vile mahakama za Kenya zinafanya kazi vile Idara ya Polisi inavyoendelea au hali ya jela za Kenya. Turudi nyuma kidogo tupeane fursa kwa taasisi za kimila ili ziweze kuinuka na kuchangia maswala ya uongozi bora. Tutakapotoa rasilimali za kutosha kwa sekta ya sheria itaboresha pakubwa maswala ya sheria na uongozi bora. Mwisho kabisa ningependa kugusia maswala ya magereza ya Kenya chini ya sekta hii. Kulikuwa na jitihada za kuboresha magereza ya Kenya. Kunao wazee wakongwe katika jela zetu. Wengine wamekaa ndani ya jela kwa zaidi ya miaka 20. Lengo la jela ni kurekebisha mtu aliyefanya makosa. Mtu akishakaa kwa jela miaka 20 na ni mtu amefikisha miaka 80 atafika umri gani ndiyo Serikali iamini atajirekebisha? Kwa hayo machache naiunga mkono sera hii.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii hata mimi nimshukuru Mhe. Wangamati kwa kuleta Hoja hii. Nafikiri tunazungumzia mambo ya wazungu wakoloni. Nafikiri kila mahali katika Kenya ilipata shida kwa sababu watu waliteswa. Mahali nimetoka kama Samburu Wakenya wote wanajua wakati Jomo Kenyatta aliletwa huko kufungwa. Watu wanajua yale mateso Wasamburu walipata wakati huo. Ni mateso hata babu zetu wakituambia leo tunatoa machozi hata kama hutukuona. Maajabu yalifanyika. Haikujulikana vile wananchi walifanyiwa wakati huo. Haswa ukienda Samburu kuna mzee mmoja kwetu anaitwa Leaduma. Ukitaka kumpiga mwanamke au mtoto unamwambia: "Nitakupeleka mahali Leaduma alipelekwa." Lakini hatujui Leaduma alipelekwa wapi. Kwa hivyo wale wenzetu waliopigania Uhuru wa Kenya nafikiri ni Wakenya wote. Hakuna pembe haikuteswa ama kuwa na waliopigania Uhuru na kuteswa. Tuna mzee mmoja marehemu alikuwa anaitwa Lekalja. Ndiye alimlisha marehemu Jomo Kenyatta katika Samburu. Wakati alikuwa anaenda kupeleka maziwa ama nyama yake ile taabu alipata ilikuwa ni ya maajabu sana. Hadi sasa familia ya Lekalja ama familia ya Leaduma tunavyosikia bado wanafuata historia ya baba zao walivyofanyiwa. Wakenya wengi au wazee waliopigania Uhuru wamekufa na familia zao bado wanafuatilia historia za familia zao. Serikali yetu ingeangalia hizo familia na kuona vile zitasaidiwa. Ama wakoloni - sisi tunawaita makaburu - wasaidie hizo familia . Ukiangalia mambo ya ardhi kutoka kwetu hadi Laikipia hao mabeberu bado wameisimamia. Bado hayo mashamba ni yao. Hata sasa tukitaka nyasi hatupati. Ile taabu tunayo sasa ni kuwa wamechukua ardhi yote katika Laikipia. Hata nyasi hatupati. Bado wanawatesa watu wetu wakienda kutafuta nyasi. Bado wanawatesa watu wetu hata wakienda kutafuta maji kwa sababu wamechukua ardhi yote. Kwa hivyo haya mambo ya Mau Mau yalikuwa ya Wakenya wote. Wote walipigania Uhuru wetu. Kwa hivyo Serikali ingeangalia wale mabeberu wamebaki hapa - hata kama wanasema wao ni Wakenya - bado wanawaona Wakenya ni kama wako katika ukoloni. Hii ni kwa sababu tunaona watoto wetu wakipigwa wakipatikana wakifuga ng'ombe katika mashamba ya wazungu. Bado unapigwa unateswa na unapigwa risasi. Hakuna kitu hatufanyiwi wa wale walibaki. Kwa hivyo ningetaka kusema warudishwe kwao. Bado tuna uchungu sana. Yangu ni kusema tu tunaunga mkono na tunamshukuru Mhe. Wangamati kwa kuleta Hoja hii. Napendekeza kamati iundwe kutoka Bunge ili izunguke na kuyachukua majina ya familia ya wale waliopigania Uhuru. Pia wale waliopigana katika Vita vya Pili vya Dunia wangewekwa pamoja kwa sababu hawajulikani. Wakati wa Mashujaa Day ingefaa wale wamebaki wapewe nafasi ili wapate kujulikana hasa na watoto wa kisasa kwamba ndiyo walipigania Uhuru wetu. Mhe. Naibu Spika wa Muda naunga mkono. Ahsante.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia Hoja hii. Kabla niseme jambo ningependa kusema kuwa mmesalimiwa na watu wangu wa Ruiru na wakaniambia muendelee kushikilia Serikali ya Jubilee ambayo ni ya kusema na kutenda. Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningetaka kuunga mkono lakini kabla nifanye hivyo ningependa kusema watu wengi wana bunduki. Ni vizuri kuongea juu ya bunduki lakini mwananchi akisikia bunduki anaona kifo ama madharau. Hiyo ni kwa sababu wakati mwingi hata wale wana bunduki za halali wanafikiria ni nguo ya kitenge ama koti ya pesa nyingi. Wanaonyesha kila mtu kuwa wana bunduki. Tumefika mahali hata mtu akienda kula kwa hoteli pale mashinani halipi! Mwenye hoteli akimudai pesa anatoa bunduki na kuiwekea mezani. Kwa hivyo hata kama tunataka kujua mahali bunduki ziko ningeomba kwa heshima hata wale wako nazo kihalali waweze kuzitumia kwa njia nzuri. Kuna wengi ambao wako nazo na wanazitumia vibaya. Wengine wanaibia wale walionazo kihalali. Ningeomba ikiwa tutajua mahali ziko ni vizuri kwa sababu tukiweka mashini ile kila mtu atajua. Hii itasaidia polisi wetu kwa sababu wakati mwingi katika maeneo Bunge yetu wakati kumekuwa na ukora kwa nyumba fulani ni vigumu sana kujua kama mtu ako na bunduki halali ama amejitengenezea ile ya mbao ya kupiga ngeta. Kwa hivyo nikiunga mkono ni vizuri tuweze kujua bunduki ngapi tulizonazo ni halali. Tukiendelea hivyo usalama utaweza kuwa katika nchi yetu ya Kenya. Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii nami nichangie. Mwanzo ningependa moja kwa moja niunge mkono Kamati. Tunapouliza maswali ama tunapoleta petitions huwa kuna sababu za kutufanya tufanye hivyo. Baada ya kuleta maombi haya ikiwa hakuna linalofanyika basi huwa zile sababu zetu hazijapata suluhisho. Kwa hivyo ni muhimu tunapouliza maswali yanapojibiwa yawe yenye kufuatiliwa ili shida zilizoko mashinani ziweze kutatuliwa ama huduma kwa mwananchi iweze kupatikana. Pia ingawaje wakati mwingine shughuli hiyo hufanyika huwa inachukua muda kufanyika. Wakati mwingine inapofanyika inakuwa imepitwa na wakati. Kwa mfano tunapouliza Swali tuseme msimu wa matikiti maji kabla swali hilo lishughulikiwe ule msimu umeisha kabisa! Sasa ni kama lile swali ulilouliza halikuwa na maana. Sitaki kuchukua muda mwingi kwa sababu nilisikia kuwa ni watu watatu wanaostahili kuzungumza ili tumpe nafasi Mwasilishi Hoja aendelee. Sitaki kuchukua muda mwingi. Wacha nikomee hapa ili tupate kuendelea. Ahsante.
Ahsante mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia mjadala ulioko mbele yetu. Kwanza kabisa ni vizuri kila mtu ambaye anaongea mbele ya Bunge hili ajue kwamba heshima inahitajika. Tukija hapa ni lazima tukumbuke kwamba Rais ambaye tunaongea kumhusu amechaguliwa na nchi nzima ya Jamhuri ya Kenya. Hatupaswi kumwambia vile anavyostahili kufanya. Kwa mfano kusema kwamba Rais anafanya hivi kwa sababu kuna mgeni anakuja ni kumkosea heshima. Samahani kwa sababu naona Mbunge ambaye amesema hivyo ameondoka. Hatuwezi kusema kwamba katika nchi ya Kenya tutakuwa tukifanya kazi kwa sababu mtu fulani anakuja nchini. Kila mtu alifurahia mambo yaliyoendelea siku hiyo. Sisi tunasema kwamba hatuna shaka na Rais kuhusu yale aliyotuambia hapa Bungeni. Tuko na uhakika kwamba ataendelea kusaidiana na sisi katika mambo yote aliyoyasema. Nashukuru sana kwa sababu ukienda katika maeneo bunge yetu utaona kuna kazi nyingi sana zinazoendelea. Sisi tunasema kwamba akina mama na vijana wamefurahia kubuniwa kwa Hazina ya Uwezo. Wameanza kuitumia na wanaendelea. Miradi inayowahusu akina mama imenigusa sana. Akina mama wakiingia katika chumba cha kuzalia watazaa watoto na kupewa neti bila malipo. Siku hizi kuzaa hakulipishwi. Mimi nimewaomba wakazi wa Ruiru na waheshimiwa wenzangu watie bidii sana tuzae watoto wengi kwa sababu ni vizuri tukiwa na watoto. Mimi tayari ukiniangalia nimejitayarisha na niko karibu kwa sababu najua kuzaa kutanisaidia. Tafadhali hayo nimesema ni yangu. Kwa sababu mimi ni mama kujifungua ni kawaida. Naona akina mama wengine watanifuata nyuma ili katika miaka ya mbeleni tuwe na kura nyingi. Wazee wamepata pesa kidogo za kuwasaidia maishani mwao. Tusiseme kwamba Rais anaangalia upande mmoja wa nchi kwa sababu hata sisi tukiwa hapa Bungeni utasikia mtu akisema tunapendelea wadi moja kuliko nyingine. Hayo ni maoni ya watu. Yale ambayo mimi najua ni kwamba Rais anaangalia pembe zote za Jamuhuri ya Kenya. Simtetei lakini sio vizuri sana kusema kwamba Rais anaangalia kabila fulani. Nimesikia wengine wetu hapa wakisema Rais anaangalia Kiambu peke yake. Kuhusu vitambulisho kila mtu anapaswa ajipange na watu wake awasaidie kuchukua vitambulisho kwa sababu ni shughuli ambayo inaendelea. Nasema kwamba tumshike Rais wetu mkono ili sisi sote tuendelee mbele. Tumefurahi vile Rais alisema asamehewe. Mkubwa wa nchi nzima akisema: "Mnisamehe" sisi tunajua ina maana nzito. Kama vile Mbunge mwenzangu amesema pale hadi nikafikiria anataka kuchukua kiti changu cha pasta ni kwamba hata kama ni mtu mwenye dhambi tunafaa kumsamehe. Kila mtu ana dhambi ya aina yake na hivyo basi tusiseme eti tuendelee kumkanyaga Rais ili aendelee hivyo na hali amesema "pole". Binadamu ni binadamu na anaweza kuwa na makosa. Hatujui ni nini kinachoweza kufanyika tukiwa katika huu uhai. Kwa hiyo naunga mkono na nauliza Wabunge wenzangu tumuunge mkono Rais wetu ndio aendelee kusaidia nchi yetu. Ahsanteni.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Karibu niulize pia tukiwa watatu sipati nafasi? Ningependa kuunga mkono Hoja hii lakini ningependa kusema kwamba hakuna kiasi cha pesa kinachoweza kulipa uhai wa mwanadamu ama kumlipa mwanadamu aliyeathiriwa na ajali. Hata hivyo ni bora kufikiria kwamba tuko na shida na ni lazima tuitatue shida hiyo. Tukiangalia tutaona kwamba watu wengi wanaumia kutokana na kutolipwa fidia wanapopata ajali. Hata hizo hela kidogo wanazostahili kulipwa ndiyo waweze kujisaidia zinapotelea mikononi mwa watu wengine. Ninaamini kwamba mtu anapoumia inafaa ajijulie hali yeye mwenyewe. Katika maeneo Bunge watu wanalia sana. Unapata muathiriwa akisema kwamba kesi yake imemaliza miaka 20 na mwingine akisema kwamba kesi yake imemaliza miaka kumi lakini unapofuatilia unagundua kwamba fedha za fidia za waathiriwa hao zimelipwa na kupotelea kwa mikono ya watu wengine. Kwa hivyo hili ni jambo muhimu. Ikiwezekana inafaa waathiriwa walipwe pesa ambazo zitawasaidia katika mambo ambayo watakua wakifanya ingawaje hawataweza kufurahia fedha hizo. Mtu hufurahia akiwa na afya njema na uhai. Ni jambo la kuhuzunisha sana familia inapozunguka tu kortini ikifuatilia fidia ya mpendwa wao aliyeaga dunia kwenye ajali pasi na mtu yeyote kuwaonyesha njia. Kwa hivyo hii ni njia nzuri sana itakayowasaidia watu wetu. Kwa hayo machache ninaunga mkono.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Nilikua nafikiri sionekani kwa maana niko mbali. Kumbe niko karibu sana. Nataka kuunga mkono Mswada huu. Ni vizuri sana kufikiria mambo ya wafungwa. Wengine wako katika nchi za nje na wengine wako katika nchi yetu. Ni vizuri mtu akiwa na shida awe karibu na nyumbani. Nataka kuunga mkono. Mtu akipatikana na hatia akiwa katika nchi za nje ni vizuri arudishwe nyumbani angalau atembelewe na familia yake. Hii ni kwa sababu hapa Kenya wengi wanatembelewa. Ni vizuri kujua ya kwamba hata mtu akiwa na makosa anawezwa kurekebishwa. Wale ambao wako nje waje hapa ili waweze kuhukumiwa wakiwa karibu. Ukiwa nje haujihisi ya kwamba unataka kukaa katika nchi hiyo tena. Unataka kurudi nyumbani. Kwa hivyo yangu ni kuunga mkono Mswada huu ili tuweze kuwasaidia watu wetu ambao wako nje. Hata wakirudi Mhe. mwenzangu amesema ya kwamba mahali pa kulala katika magereza ya huku kwetu yako katika hali mbaya. Lazima magereza yetu yawe katika hali nzuri ili kuwafaa wale ambao wanaenda huko. Pia magereza yanaweza kuwa katika hali nzuri lakini ile tabia wanaofanyiwa huko ni mbaya zaidi. Kwa hivyo ni lazima tuangalie pande zote ili wakiingia huko wakae kwa njia ambayo inafaa kwa Mkenya yeyote. Asante Mhe.Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Yangu ni kupongeza Kamati ya Mazingira na Mali ya Asili na hasa zaidi Mwenyekiti wake. Swala la maji ni muhimu sana.Kulikuwa na mvutano mwingi sana kati ya serikali za kaunti na Serikali ya Kitaifa kuhusu ni nani atabaki na mambo ya maji. Kama ingekuwa ni kaunti inasimamia kila kitu watu wengi wetu wangepata shida sana kwa sababu ya kuongezewa ada. Pengine unaambiwa: "Mara hii utapewa pesa hii." Na kesho unarudishwa. Lazima kuwe na bodi ya kusimamia masuala ya maji. Sio rahisi kufikia hapa. Ni kwa sababu ya bidii ya Kamati ya Mazingira na Mali Asili ambayo inaongozwa na Mheshimiwa Amina
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Yangu ni machache na ningependa kumuunga Rais mkono kwa kazi nzuri aliyoifanya. Ningependa kusema kwamba uchaguzi unapofanywa nchini Kenya nchi nzima inafaa kuangaliwa kwa sababu watu wote ni wa Mungu. Kutoka wakati wa enzi ya Rais Moi Tigania Mashariki na Magharibi hawajawahi kupata Katibu Mkuu au Waziri. Lakini naunga Hoja hii mkono kwa sababu imetoka kwa Rais. Kama viongozi Bungeni pia sisi tunafaa kuitwa na kumshauri Rais maeneo ambayo yanafaa kupewa nafasi kusimamia ofisi mbalimbali katika Serikali. Rais amefanya kazi nzuri. Katika Bunge hili mtu anapokosoa Serikali inasemekana kuwa anapinga Serikali. Sijapinga Serikali lakini watu wote lazima wachukuliwe sawa. Wanatigania tuko wengi. Wakati wa kupiga kura Mlima Kenya huwa na nyasi na mtu wa Mlima Kenya huambia Wanatigania anawapenda wampe kura. Lakini ikifika wakati wa kula na kugawa Mlima Kenya humea nyasi na Mtigania haonekani tena. Wakati umefika bendera ya Mtigania ipande juu ili aweze kuonekana nchini Kenya. Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi kuunga mkono Hoja hii. Wenzangu wamezungumzia ugonjwa huu na kwa kweli umeathiri watu wengi. Tunaomba Serikali iangalie njia zinazoweza kutumika kuzuia ugonjwa huo. Watu wengi nchini Kenya hawaelewi chanzo cha ugonjwa huo. Watu wengi wamekufa. Wakati watu wanaenda kutafuta matibabu wanaambiwa kuwa hakuna njia ya kutibiwa kwa sababu ugonjwa umeenea sana. Kwa sasa HIV/AIDS ni afadhali kwa sababu kumepatikana madawa ya kusaidia watu kwa muda mrefu. Ingefaa tuwe na njia ya kupima watu mapema ili waanze kutibiwa. Tumeleta watu wetu wengi Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta lakini mara nyingi madaktari wanasema kuwa hakuna njia ya kutibiwa kwa sababu saratani imeenea sana mwilini. Madaktari wanafaa wapime watu mapema kabla saratani haijaenea sana mwilini. Mhe. Naibu Spika wa Muda vile vile kuna ugonjwa wa figo ambao pia umezidi. Unaathiri hata watoto wadogo wa miaka mitatu na mine. Unapata kwamba figo zote zimeathiriwa. Ningependa kushukuru dadangu Mhe. Wanga kwa kuleta Hoja hii. Magonjwa yamekuwa mengi sana. Kwa mfano kuna ugonjwa wa figo ugonjwa wa kisukari na ugonjwa wa shinikizo za damu. Tunafaa kufanya uchunguzi wa magonjwa haya kwa sababu labda yanatokana na vyakula ambavyo tunavila. Mwanzoni hakukuwa na magonjwa kama haya. Lakini wakati huu hata mtoto mdogo wa miaka sita 10 na hata 15 anaweza kupatikana na ugonjwa wa moyo. Serikali inafaa kuchunguza magonjwa hao yanatokana na nini. Sisi ni wafugaji na siku hizi tunaambiwa kule mahospitalini kuwa kuna magonjwa ya nyama na maziwa. Watu wamekuwa wakinywa maziwa kutoka zai. Kwa hivyo tuunge mkono Hoja hii ya saratani ili watu waanze kupimwa na kujua hali yao mapema. Zahanati pia zijengwe katika kila mahali ili watu wahudumiwe. Pia naunga mkono masomo ya wataalamu wa saratani. Hii sheria ipitishwe kwa sababu ugonjwa huo umetatiza watu wengi sana. Nashukuru na naunga mkono.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi nichangie Hoja ya Hotuba ya Rais tunayempenda. Katika mambo yaliyonifurahisha la kwanza ni kuhusu kupambana na ufisadi. Lau litafuatilizwa kisawa sawa Kenya yetu itafika mbali. Nampongeza Rais kwa sababu ameleta matumaini. Awali hungeweza kuona Waziri akienda kuhojiwa mbele ya Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) lakini sasa hivi tunaona Mawaziri kadhaa wakienda mbele ya tume hiyo kuhojiwa. Kwa mfano sasa hivi mitandaoni tunaona Waziri Prof. Magoha akienda kwa EACC pamoja na wengine waliomtangulia kwenda. Kwa hivyo tunampongeza Rais kwa kuleta haya matumaini. Kupitia kwa Utaratibu wa Utendaji No.2 ya 2020 Rais aliamurisha mfumo wa utendakazi na uwajibikaji wa matayarisho ya kupambana na COVID-19. Hata hivyo mpaka sasa ni masikitiko. Tunasikia kuwa kwa afya bado kaunti hazijajitayarisha vilivyo. Sasa sijui kama sisi Wakenya itabidi tuwekwe fimbo jela kwa sababau mambo yameelezwa lakini watu hawayafanyi. Pesa zinapelekwa kwa magatuzi kwa matayarisho lakini watu hawawajibiki. Tutamlaumu nani? Rais ameshatoa njia na utaratibu wa kufuatwa lakini watu hawazifuati kisha watamlaumu Rais. Itabidi mujifundishe Mheshimiwa. Kiswahili kitukuzwe kwani ni lugha ya Taifa. Leo mchana itabidi watu wazungumze Kiswahili. Kwa hivyo tuanze kujifundisha. Hata sisi kuna mambo mengine ambayo hutushinda na sisi hujitahidi kujua mambo hayo yana maana gani.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili niweze kuchangia Mswada huu ambao ni mzuri. Ninampongeza Mhe. Martha kwa kuweza kuleta Mswada huu Bungeni. Kama akina mama tunahusika sana kutetea masuala kama haya kwa sababu mara nyingisisi ndio hukaa na watoto na tunajua ni muda gani unahitajika kukaa nao ili waweze kuwekwa katika hali iliyo sawa. Ninaunga mkono Suala la kuweza kuwa na muda unaofaa na mtoto mdogo kwa sababu muda huu ndio utakaoruhusu kuweza kumjua mtoto vizuri naye akujue na utaweza kumfundisha maadili yanayofaa. Mara nyingi tunawakuza watoto bila ya kuwa na muda nao na wanakosa maadili na kuwa na tabia za ajabu ajabu. Utastaajabu ikiwa hiyo ni jamii yako uliyoweza kuikuza ama sivyo. Itatokea hivyo kwa sababa ya kukosa kuwa na muda unaofaa na jamii hiyo. Kwa hivyo ninaliunga mkono suala hili. Muda unastahili uwe wa kutosha kati ya mtoto. Hata ikiwa ni baba familia husika sharti iwe na muda wa kutosha na huyo mtoto wanaomchukua ili iweze kumpa maadili. Hivyo watakuwa na wakati mzuri wa kujuana na kuelewana vizuri. Ahsante sana.
Ahsante mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii niichangie Hoja hii. Ninaiunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na dada yetu. Mimi ni mwanachama wa Kamati ya Utekelezaji wa Katiba.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia hii nafasi ili niweze kuunga mkono Mswada huu ambao haswa ni Mswada No. 26 wa mwaka 2019 na unaosomwa kwa Mara ya Pili. Juu ya jambo kama hili pia mimi naunga mkono viongozi wenzangu akiwemo Mhe. Ruweida Obo ambaye amezungumza sasa hivi juu ya shida za Lamu. Vile vile naunga mkono kwa sababu Lamu na Mombasa siyo mbali. Naamini ni kweli kuwa pia wao wawekwe katika hazina hii ili waweze kusaidiwa kama watu wengine ambao wanasaidiwa. Leo ni jambo la kutamausha sana kuwa kutoka Kenya ipate Uhuru mpaka leo ni miaka mingi sana ilhali bado tunazungumzia suala la ukame. Lakini juu ya yote nataka kuunga mkono Mswada huu kwa sababu wakati huu wetu ambapo sisi ndio viongozi tunashukuru kwa maana halmashauri hii ya kupambana na makali ya ukame itaweza kufanya kazi kikamilifu kulingana na yale mapendekezo ambayo wametoa. Jambo la muhimu sana ambalo nimeweza kuliona katika Mswada huu ni kuletwa kwa zile fedha ambazo itabidi ziweze kuangalia makali ya ukame ambayo yatakuwa yanakumba sehemu mbalimbali katika nchi yetu ya Kenya. Kwa hivyo hata mimi naungana na wenzangu wengi sana ambao walisema kuwa kaunti zao pia ziweze kuangaliwa na kuwekwa kati ya zile ambazo zaweza kufikiriwa kupata ufaa kupitia hazina hii. Kwa maana hiyo nasema Kaunti ya Mombasa ambapo ninatoka pia ni muhimu kuangaliwa katika hazina hii ili nasi tufaidike. Namwona Mhe. Obo pale hafurahi kwa sababu watu wengi waliozungumza hapa kutoka Kirinyaga Turkana Kitui Machakos Makueni na sehemu mbali mbali wanachukulia kwamba makali haya yatawaathiri wao pekee yao ambao wanafanya ukulima. Lakini mimi na wewe Mhe. Naibu Spika wa Muda tumekuwa pale Mombasa na tukatembea sehemu mbali mbali za Mombasa hasa kwenye mahoteli makubwa makubwa na majumba ambamo watu wanakula kamba ambacho ni chakula kizuri sana. Chakula hiki hakiwezi kupatikana baharini bila kuwepo mikondo ya mito kuelekea baharini. Kamba huzaana kwa wingi kwenye hiyo mikondo. Kwa hivyo mkondo huu hauwezi kuwepo ikiwa kiwango cha maji kitakuwa chini. Na kiwango cha maji kuwa chini hakiwezi kuletwa hivi hivi isipokuwa kitaletwa na kiangazi. Kwa hivyo kitaalamu nimezungumzia jambo hili ili kujitetea kuwa sisi watu wa Mombasa huenda ukulima wetu sio sana wa kushika jembe lakini ukulima wetu pia ni ile bahari na wale viumbe ambao wanapatikana katika bahari. Kwa hivyo naona ni muhimu zaidi Serikali kuu inapoangazia mambo haya kaunti yangu ya Mombasa nayo ifaidike. Jambo la pili ambalo nataka kulisema ni kuwa viwango vya maji vikiwa chini huwa ni sababu ya ukame. Ni huo ukame unaosababisha watu kukosa maji ya kunywa. Leo hii nikizungumza hapa kuna shida kubwa ya ukosefu wa maji ya kunywa Mombasa. Hii ni kwa sababu maji ambayo yanatumika katika sehemu za Mombasa yanatoka Mzima Springs na Marere. Ukame unapozidi viwango vya maji huwa chini na watu hupata shida. Lakini kulingana na hazina hii kuna utaalamu ambao unaweza kufanyika. Nasema hivi kwa sababu kule Pwani kuna sehemu inayoitwa Mtwapa ambapo kuna Mjerui anayetengeneza maji mazuri kutokaa na maji ya bahari. Maji yale yanaitwa Dutch Water. Maji yale ndiyo wengi wanatumia katika nyumba zao na kwa njia tofauti tofauti. Kwa hivyo fedha hizi zikitumiwa vizuri. Ikiwa mwekezaji mmoja ameweza kujiletea faida katika bishara yake kwa nini pesa hizi zisitumiwe na Serikali ili kuwawezesha wananchi wa Pwani kuishi wakiwa na maji safi katika nyumba zao? Sharti kila mmoja apate haki hii ambayo ni ya kisheria kulingana na Katiba. Tulipopata Uhuru katika nchi yetu tulisema tunataka tuondoe umaskini baa la njaa na matatizo ya vitu muhimu kama hivi ambavyo vinastahili kutumika. Naamini ikiwa fedha hizi zitafanyiwa mipango mizuri basi zitaweza kutumika na hali Mombasa mjini na hata Jomvu ninakoongoza itaimarika. Taaluma hii ikifanyika wananchi watasaidika. Kule Mikindani kuna mkondo wa bahari. Miritini kuna mkondo wa bahari katika sehemu inayoitwa Mkupe. Jomvu Kuu kuna mkondo wa bahari Jomvu Kuu yenyewe na Misheni. Kwa hivyo taaluma hii itawasaidia wananchi wetu pakubwa. Amesema hapa Mhe. Sophia kuwa pesa zatumika nyingi sana karibu KSh8 bilioni ama hata kuzidi. Wakati matatizo yanapotokea ndipo utaona watu wakikimbilia Red Cross World Vision na mashirika mengine yasiyo ya Serikali. Serikali ambayo ina uhuru kamili na inajali maslahi ya watu wake ni serikali ya kujipanga. Kwa hivyo hivi sasa tunasema kuwa kuundwa kwa halmashauri hii na kuwekwa pesa za kudhibiti makali ya ukame. Tunatumai mambo haya yatasimamiwa vizuri. Kabla matatizo hayajatokea watu huwa na mipango mizuri. Huwa kuna fedha zakutumika kusaidia waathiriwa. Kwa hivyo naunga mkono mapendekezo haya. Vile vile katika mapendekezo haya tumeunga mkono kuwa kuwekwe pesa ambazo zitasimamiwa na halmashauri hii. Lakini vile vile nasema na nataka ninukuliwe katika Bunge hili kuwa pesa hizi lazima zitumiwe kwa njia ambayo ni ya sawasawa na sio sisi tuidhinishe pesa hapa kumbe tunawawekea watu wengine pesa hizo kula badala ya kusaidia wananchi wa Kenya katika masuala yale. Kwa hivyo viongozi ambao watasimamia halmashauri hii lazima wawe waadilifu na watumikie Wakenya. Wajue Wakenya wote wako na haki ya kuishi vizuri. Kwa hayo asante kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia. Naunga mkono mapendekezo haya. Asante sana na Mungu atubariki.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Hoja hii.Ninatoa kongole kwa Mhe. K'oyoo kwa kuleta Hoja hii. Mafuriko yanaathiri sehemu nyingi za Kenya Lamu ikiwa mojawapo. Kabla ya kutoa lawama ningependa kushuru Serikali kwa jitihada zake lakini ukweli ni kwamba kazi ya ziada inafaa kufanyika. Maeneo ya Moa na Chalaluma huko Lamu yameathirika pakubwa na mafuriko. Mwaka jana mafuriko yalitokea nakulikuwa na mipango ya waathirika kulipwa. Kamati ilipendekeza lakini mpaka leo hawajalipwa. Yale yaliyotokea sasa yametokea zaidi mengine. Kila mwaka sasa yamekuwa yakitokea. Hawa wafugaji wanapata matatizo sana kwa sababu hali ya hewa imebadilika. Ikiwa si mafuriko ni ukame. Ukame unatokea na ninashukuru Serikali. Ilikuwa na jitihada kutumia shirika la Kenya Meat Commission (KMC). Ninashangaa kama hili Shirika linajua rai ya Kenya kwa sababu walienda kaunti zingine zote wakaokoa wafugaji wakachukua ile mifugo wakachinja wakasaidia wale ambao hawana chakula lakini Lamu hawakufika. Sijui rai ya Lamu inakaa vipi ni watu hawaielewi ama wanaona hawa ni wanyonge wazidi kukandamizwa maanake wafugaji wa Lamu hawakupata kusaidika na hili shirika la KMC. Wengine wengi wamesaidika lakini hao hawakusaidika. Saa hii watu wengine wanalipwa kwa ile mifugo waliotoa wakati wa ukame ilhali watu wangu wa Lamu wametatizika. Ukweli ni kwamba Lamu ni kaunti ambayo ina wafugaji. Sehemu ya Witu kuna upande mkubwa jamii ya Orma wako hapo na wana mifugo wengi. Ukienda Hindi majirani zetu nasisi wenyewe kuna jamii ya Somali na ni wengi. Na hata wa Ijara wanatoka kule wakija kwetu kutafuta malisho. Lakini wakati wa mavuno wanasahau sisi watu wa Lamu. Nataka hili Shirika lijue Lamu ni Kenya na inahitaji huduma zote zile zinapeanwa kwa Wakenya wengine. Hata kama namba za kura ni kidogo na hizi hesabu zimezidi kutuumiza sisi ni Wakenya na kama vile inavyosemekana kila kura inahesabiwa haiwezi kwenda mbili kama haijaanza na moja. Sisi ni Wakenya kule na matatizo yako. Naomba Serikali itutambue ili tusiseme tu watu waliotengwa siku zote. Naomba Serikali ipeleke misaada mbali na chakula kama vile blanketi na mambo mengine. Yatasaidia sana. Kuna watu wameathirika na ikiwa hawasaidiwi inaongeza umaskini. Wenyeji wanajitahidi. Wanafanya kazi mwaka mzima. Lakini ikifika wakati wa mafuriko vitu vyao vyote vinaenda. Umaskini unazidi. Ni muhimu Serikali iongeze bidii isaidie na wasisahau Lamu kaunti ina wafugaji. Ahsante.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie. Suala hili linatuathiri hata sisi Wabunge. Kuna wale waliogombea viti vya ubunge lakini hawakufanikiwa kupata. Ingekuwa vyema wapate huduma za ushauri nasaha kwa sababu wamebaki tu kwenye Facebook wakitutukana. Nafikiri kuna ugonjwa fulani ambao umewaingia. Inafaa washauriwe kwa nasaha. Hata sisi tukitoka hapa na tusifanikiwe kurudi tena inafaa tushauriwe ili tujue namna ya kuwahudumia watu wetu. Pia inastahili ushauri upatiwe wanaotafuta kura au wale ambao hawakupata kiti chochote ambacho walikuwa wakiwania. Wao hupata shida sana wanapokosa ushindi ama kuteuliwa. Pia watu wengi hupata shida wakati wanatarajia jambo fulani lakini halitokei. Wanafaa wapate ushauri nasaha. Katika depression kuna viwango tofauti kama vile kutokubali. Kuna viwango vingi ambavyo mtu hupitia kabla ya kufikia depression . Haya yanatokea zaidi kule Lamu kwa maafisa wa Serikali. Kwa mfano polisi wakikaa pahali kama Kiunga kwa muda mrefu wanasumbuka akili hadi wengine hutatizika kwa utenda kazi wao. Wanasumbua wananchi kusudi washtakiwe ili wapate faida ya kutolewa mahali hapo kwa sababu wamekaa kwa muda mrefu kwa mfano miaka saba. Wanahitaji ushauri nasaha ili wasaidike. Hata walimu wanahitaji huduma hizi. Walimu wanaofanya kazi kule Kiongwe Boni Forest wanastahili wapate huduma hizi kwa sababu sehemu hii ni ya kutisha. Inawasumbua akili hadi familia zao zinatatizika. Saa nyingine wanafanya vitendo vya kushangaza hadi unajiuliza kama wao ni binadamu au la. Kumbe huwa ni matatizo yanayotokana na ile hali wako nayo kule Lamu. Maafisa wengine wa Serikali wanaohitaji ushauri nasaha ni wale wanaofanya kazi katika Huduma Centre. Lamu inastahili kuwa ya kwanza kupata huduma hizi. Tunazihitaji sana kwa sababu watu wengi hupigana wao kwa wao. Hata wenyenji wa Lamu East wanakatana kwa mapanga kwa sababu ya kukosa ajira. Imewaharibu akili. Wengine wanaenda sehemu ambazo hazifai. Wengi wao wamevuka mpaka na kwenda hadi Somalia kwa sababu wana shahada lakini hawana kazi. Wakipata ushauri nasaha utawasaidia sana. Wengine wanaingilia mambo ya kusikitisha. Tumefanya assessement ya vijana na tukapata hivi: katika wadi ya Faza asilimia 20 ya vijana wana maradhi ambayo wao hawajasema wako nayo. Hawajawambia bibi zao. Wengine wameengia kwa mihadarati. Utasikitika kwamba huko Lamu hasa wadi za Faza na Mkoi depression imewaingia watu na hawana la kufanya. Kwa hiyo wameingilia matumizi ya mihadarati sana. Vijana wetu Lamu wameisha. Hatuna vijana Lamu. Vijana ambao wameingilia matumizi ya mihadarati na kwa mambo mabaya ni asilimia 57 kwa makadirio ya daktari. Haya yote yametokea kwa sababu wamekosa huduma za ushauri nasaha. Wangeitwa wakalishwe chini na waelezwe hali ilivyo wangekuwa faida kwa Serikali Lamu na Kenya nzima. Nakubaliana na haya na mwenzangu aliyependekeza Mswada huu. Ingekuwa vizuri utiliwe mkazo utusaide sote. Akina mama wanaona vibaya watoto wao wakipotea. Ahsante.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii kuchangia. Ninaheshimu sana walimu kwa sababu wao ni kioo katika jamii. Tukiwa shuleni huwa tunaigiza walimu. Nimeshangazwa sana na mwalimu huyu. Sijui ni mfano gani anaonyesha wanafunzi. Najua Kenya tuna Wakristo na Waislamu wanaopendana. Haya mambo ambayo yametukia hayamo humu nchini. Huyu ni mwalimu na hilo kosa alilofanya ni yeye mwenyewe anafaa kuchukuliwa hatua za kisheria. Ikiwa kuna mwingine anachezea na kukosea heshima Biblia naye pia achukuliwe hatua za kisheria. Hapa ametuudhi. Mimi naona hivi: Wanaiga mambo wanayoona katika mitandao. Huu ni ukoloni mamboleo. Mambo haya huku kwetu Afrika hayako. Wanaiga nchi za kizungu. Mambo hayo yanafanyika huko lakini Afrika hayafanyiki. Itakuwa vizuri awe mfano kwa wengine maana ni uhalifu amefanya. Ni kama wale wahalifu wa kigaidi wanaoharibia Uislamu jina. Nimefurahi kwamba watu wa Ijara hawakuchukua hatua mikononi mwao. Naomba mwalimu huyu achukuliwe hatua za kisheria maana si mfano mzuri analeta na huenda ikaleta matatizo zaidi. Ikiwa kuna mtu pia amekosea heshima Biblia naye pia achukuliwe hatua za kisheria. Asante.
Ahsante mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Ninataka kwanza kumshukuru mhe. Millie sana kwa kuleta huu Mswada hapa. Sisi kama viongozi ambao tumechaguliwa kuja katika Bunge hili kazi yetu ni kuwakilisha wale ambao hawawezi kufika hapa. Tunajua wakati mwingi kuna watu ambao wanateseka. Mhe. Naibu Spika wa Muda Waheshimiwa ambao wako nyuma yangu wana mkutano mwingine. Ninakuomba uwakanye. Bi. Naibu Spika wa Muda kuna watu tunaowawakilisha ambao wanateseka. Shida iliyoko ni kwamba hawana nafasi ya kujitetea; hawajui pa kuelekea ili kupata usaidizi. Ningependa kusema hivi: Ikiwa wewe ama mimi tutanajisiwa hakuna mtu atajua katika nchi nzima kwa sababu sisi ni wabunge. Kuna wengi ambao wamepata shida lakini wamenyamaza kwa sababu hawajui wataambia nani. Kuna visa vingi vya mama na watoto wake wasichana kunajisiwa na kuporwa mali. Hawa ni watu hawana watu wa kuwafariji na kwa hivyo wanasumbuka. Tunashukuru sana kwa ajili ya huu Mswada kwa sababu hii sheria itawasaidia watu kama hawa. Wapo wale wanaosumbuliwa na wenye pesa. Mtu akipigwa ama auliwe na mwenye pesa humu nchini huwa ni shida kubwa kwa sababu mnyonge hana lake. Kutokana na huu Mswada tutaweza kuwakumbuka wanyonge na kuwasaidia. Pakitokea maafa kama yale yanayojulikana kama " bomb blast " na mengineyo sharti tukumbuke kwamba kuna Wakenya wasio na sauti. Itakuwa ni furaha yetu sisi sote ikiwa sauti zao zitasikika kwa sababu ya huu Mswada. Tusiwachukulie polisi kana kwamba si wanadamu. Kuna visa ambapo polisi wanajeruhiwa ama wanauwa wakiwa kazini. Huu Mswada unagusia kila Mkenya. Sisemi kwamba polisi wasifanye kazi yao lakini nao wachukuliwe kama Wakenya wanaohitaji kufanyiwa haki. Ukitembea kortini utaona waathiriwa ambao hawana watu wa kuwatambua. Utapata kwamba hawana watu wa kuwatetea na hawajui haki zao. Huwa hawana namna ya kuendelea. Tutapitisha huu mswada ndiposa tusimamie watu wetu ambao wamefinyika humu nchini. Ningependa kuwaambia watu wa Ruiru constituency "hi" na ninawapenda. Godbless.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Ningependa kuchangia Mswada huu kwa lugha ya taifa kwa sababu jambo hili ni muhimu sana hasa kwa akina mama wa Makueni na wengine katika nchi ya Kenya. Nimesimama kuunga mkono Mswada huu ambao unahusu Maji. Ningependa kusema kwamba ukosefu wa maji kama Waswahili husema ni kidonda ndugu ambacho kimekuwa katika nchi yetu ya Kenya kwa muda mrefu au tangu tujinyakulie Uhuru. Pia ni jambo ambalo limezungumziwa katika sehemu mbali mbali lakini inaonekana bado hatujapata suluhisho la ukosefu wa maji katika nchi yetu ya Kenya. Ni jambo ambalo si la kupendeza. Hii ni kwa sababu tangu tupate Uhuru mpaka leo yapata miaka 51 bado tunazungumzia mambo haya ya maji hasa katika sehemu za Ukambani kaskazini mashariki na sehemu nyingine. Sehemu nyingi za nchi zina ukame na watu wengi wanaosumbuka ni akina mama. Ni kwa nini tunazungumza juu ya maji wakati Kenya bado inapata mvua na tunaweza kukusanya haya maji kwa njia mbalimbali? Ni kwa sababu labda mikakati iliyopo yakukusanya haya maji ndiyo imechangia kuweko ukosefu wa maji ya kunyunyizia mimea maji na kupatia wanyama maji. Hii ndiyo sababu ninasema Serikali inafaa kuhakikisha kwamba kila Mkenya ama kila mwananchi anapata maji safi ya kutumia. Inafaa Serikali iweke mikakati mizuri. Wakati mwingi shida inayochangia ukosefu wa maji ni kamati ambazo zinateuliwa wakati maji yamechimbwa. Kamati inapata mafunzo lakini baada ya miaka michache mashine za maji zinaharibika na hasiwezi kutengenezwa na watu wanakuwa na shida iliyokuwako hapo mwanzoni. Hili ni jambo la kusikitisha. Kwanza kamati zingine ni fisadi kwa sababu zinauza maji na hakuna uwajibikaji au pesa wanazouza maji hazionekani zimeenda wapi. Kwa hivyowatu wanarudi mahali walipoanzia. Ningependekeza sheria iwekwe ili wanachama wengi wa kamati hizi wawe ni akina mama. Hii ni kwa sababu wanaume hawatumii maji mengi. Mwenye kuumia ni mama. Akina mama wanajua uchungu wakutafuta maji kutoka mbali. Ninakumbuka nilipoenda huko Makindu Makueni nilimpata mama mmoja ambaye alikuwa amejifungua na alikuwa amekaa siku nne bila kupata maji ya kuoga. Mnajua jinsi mama anavyokuwa anapojifungua. Inafaa Serikali iangalie sana sehemu ambazo ni kame hasa sehemu za Ukambani ambazo hazina maji na tumeongea juu ya jambo hili sana. Pia inafaa Serikali iangalie ni wapi itachimba maji. Kuna vidimbwi vya maji ambavyo vimechimbwa lakini inafaa tuangalie ni vipi tunaweza kupata maji nyumbani. Kweli kuna njia nyingi za kupata maji. Tunaweza kupata maji ya mvua inaponyesha kwa kuyakusanya katika matangi. Ningependekeza haya matangi yapeanwe kwa watu na walipie kama bili ya maji kila mwezi. Hii itawasaidia watu kukusanya maji na kila familia itakuwa na maji. Mhe. Naibu Spika wa Muda ninaunga mkono Mswada huu. Ningependa jambo hili la maji liangaliwe sana hasa katika bajeti ya Kenya. Inafaa kiwango kikubwa cha fedha za Kenya kitumike kumpatia mwananchi maji ili tatizo la maji lisuluhishwe kabisa. Ahasante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda na kongole kwa kuchaguliwa kuwa Naibu Spika wa Muda. Kama wenzangu ningependa kuchukua fursa kumpongeza Mhe. Sang. Licha ya ugumu wa nyakati tulioko za kufanya uchaguzi yeye ameweza kuleta Mswada ambao nina ii utakapopita utatatua matatizo yanayokumba sekta ya afya katika nchi hii. Maafisa wa kliniki wa Kenya katika nchi ya Kenya wana wajibu mkubwa sana. Mimi natoka katika sehemu kame ya Kenya; sehemu ambayo ni nadra kupata madaktari. Mengi ya matatizo ya kiafya yanayowakumba watu wetu yanashughulikiwa na maafisa wa kliniki wa Kenya. Kwa hivyo sisi kuunda taasisi itakayowasajili itakayoweka nidhamu itakayowapa uwezo wa kisheria maafisa wa kliniki wa Kenya kuweza kuhudumia wagonjwa wetu itatatua matatizo ya kiafya yanayokumba nchi ya Kenya katika sehemu nyingi. Nasikitika kwamba miaka 50 baada ya Uhuru wafanyikazi wetu wa afya wako barabarani kufanya maandao. Ni nyakati ambazo wangepewa kipao mbele na washughulikiwe; maanake wewe huwezi ukatibu mtu ukiwa hujui utapata chakula wapi. Uko Nairobi gharama ya nyumba ndiyo hiyo na matatu zinaongeza bei. Huyo maafisa wa kliniki wa Kenya ama nesi atafanya vipi aende atoe huduma bila kuomba deni? Ni masuala ya haki. Ni masuala ya kuboresha mapato yao ili waweze kutoa huduma inayohitajika kwa Wakenya. Kuwaweka jela na kuwakimbiza barabarani haiwezi kuwa suluhu ya shida zinazowakumba maafisa wa kliniki wa Kenya na nesi wa Kenya. Sessional Paper No. 2 ya 1965 iligawanya Taifa la Kenya katika mapote mawili. Pote ya sehemu za rotuba na pote moja ya sehemu ya Kenya isiokuwa na rotuba. Sehemu za Kenya isiokuwa na rotuba ni kama Tana River dera na Wajir. Katika sehemu hizo yule daktari wa hakika utakayepewa katika hizo kaunti zai alikuwa anitwa Medical Officer of Health (MOH). Kwa hakika utapata huyo. Huna hakika ya kupata daktari wa pili. Wale wako na maafisa wa kliniki wa Kenya. Hawawezi kutekeleza wajibu wao kwa sababu sheria haiwaruhusu. Sheria ambayo tunajadili leo inawapa uhuru na uwezo wa kisheria waweze kutatua matatizo ya matibabu yanayokumba Wakenya. Mhe. Naibu Spika wa Muda tunazungumza juu ya mafunzo na usajili wa maafisa wa kliniki. Hapa tumepewa aina ya matatizo wanayoweza kutatua ili waweze kufungua mahospitali yao ya kibinafsi ili waweze kuhudumia Wakenya. Kiwango ambacho wamefika wako na ujuzi na wanaweza kuwahudumia Wakenya katika hicho kiwango chao. Sio lazima daktari awepo mtu anapougua malaria na homa ya kawaida lakini ni lazima mtu atafute mtaalamu wa kutibu magonjwa hayo. Nimesimama kumuunga mkono Mhe. Sang kwa kazi nzuri aliyofanya na kuleta pendekezo hili la sheria ili maafisa wa kliniki wa Kenya waweze kutambulika na kupewa heshima na haki wanayostahili ili waweze kutekeleza kazi yao. Tukiangazia masuala ya migomo ya wafanyikazi kuna mgomo ambao unatawala katika taifa hili. Tunaweza kuketi chini na kusikiliza malalamiko ya wafanyikazi. Hakuna mgomo ambao utawala hauwezi kuketi chini. Hii migomo inahatarisha maisha ya Wakenya. Suluhu ya matatizo yanayowakumba madaktari ingepatikana jana. Ninamuomba Rais wa Kenya aamke aingilie kati na awaondoe madaktari kutoka barabarani awarudishe hospitalini ili waweze kuwahudumia Wakenya. Kwa hayo machache ahsante Mhe. Spika.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ahsante ndugu yangu Mhe. Mohamed Ali. Nataka kulikumbusha Bunge hili kuwa katika Bunge lililopita kuna Mswada nilioleta kubadilisha sheria na kuifanya Coast General Hospital ijulikane kama Pwani Referral Hospital. Nataka kutoa sababu. Wengi wametaja kuwa hospitali kuu zenye kusimamiwa na serikali ni mbili. La si mbili. Ni nne. Ya kwanza ni Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta yenye wafanyakazi 6000 na vitanda 800 lakini mpaka watu 3000 wanaweza kulala katika hospitali hiyo. Ya pili ni Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Moi ambayo ilipandishwa ngazi mwaka 2010. Wakati inafanyiwa census wafanyakazi wake walikuwa 3066. Nataka kutoa hesabu. Katika hesabu ya fedha ya Bajeti ya mwaka 2014/2015 Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta ilipewa Ksh6.5 bilioni. Mwaka wa 2015/2016 ilipatiwa Ksh6.6 bilioni. Katika mwaka wa 2014/2015 Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Moi ilipewa Ksh4.3 bilioni na mwaka wa 2016/2017 ikapewa Ksh 4.7 bilioni. Mathare Hospitali ni hospitali ya watu wenye akili punguani. Hospitali ya mwisho ilijengwa wakati wa ukoloni mwaka wa 1945. National Spinal Injury Hospital ina vitanda 25 pekee. Kwa hivyo sio hospitali mbili mbali ni nne ambazo Serikali kuu inaweza kuangalia. Baada ya kuweka Hoja hii Mhe. Spika wa Muda niliitwa na kongao la magavana wa Kenya nzima. Walikuwa na mkutano wao pale Mombasa. Walielezea wazi ya kuwa hawana furaha na hili jambo la
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Baraza La Mitihani Nchini linaajiri wasimamizi wa mitihani siku ya mitihani. Mbali na hawa wasimamizi wanaosimamia mitihani kuna askari ambao wanapelekwa kuangalia usalama wa watoto. Kutambuliwa kwa makosa au kuibiwa kwa mitihani hufanyika siku ya mitihani au ni baada ya kuchunguza ile mitihani? Hii ni kwa sababu wale wanaosimamia mitihani ndio wangesema jambo kama hili likitendeka. Mara nyingi ripoti huja baada ya ile mitihani kukaguliwa. Wale wanaolipwa kusimamia hii mitihani ikiwa jambo la wizi wa mitihani limetendeka Baraza linawachukulia hatua gani?
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kama anavyosema Mhe. Ken Okoth ahadi zilikuwa kima cha ndovu lakini kilichotendeka ni kima cha sungura. Sawa hicho kima cha sungura hakikuwepo mbeleni. Unastahili kuwa na shukrani. Ieleweke kwamba kuanza jambo si kazi rahisi. Huwa kuna changamoto nyingi unapoanzisha jambo. Kuna uwezekano kwamba yote yaliysajiliwa hapa yalitendeka. Lakini kufikia hivi sasa tunapozungumza hali imerekebishika. Nimesema kutoka mwanzo kwamba naunga mkono Ripoti hii na ningependa hatua za kisheria zichukuliwe kwa waliohusika. Pamoja na hayo ninasisitiza kwamba mabadiliko yale ambayo yameletwa na huduma hii ya vijana kwa taifa sharti tuyapongeze. Kazi yao inaonekana kote nchini. Ningependa kuzungumzia unga. Baa la njaa halikuanza jana ila mtu aliona mapema hali ambayo iliwapata Wakenya kisha akachukua hatua. Eti mahindi yaliyoagizwa juzi yalifika jana kwenye bandari yetu ya Mombasa! Kuna shida gani na hilo? Lililo muhimu ni lipi? Watu wetu wapate kupona ama waendelee kuangamia kwa njaa? Sharti Wakenya wajifunze kushukuru kwa mambo mazuri yanayotendwa. Sasa hivi ifahamike kwamba NYS haikuanza wakati wa Jubilee. Imekuweko hata katika serikali za hapo awali. Kwa hivyo yale yote ambayo yametendeka ni mabadiliko. Yameonekana wazi. Ni wajibu wetu kuboresha hii huduma. Ninaamini kwamba wale ambao wamechaguliwa hivi sasa kuongoza ugatuzi watawajibika na watafuatilia matumizi mazuri ya pesa za NYS. Hilo likitendeka sote tutashukuru. Kila mtu abebe msalaba wake. Atakayepatikana na hatia basi sharia ichukue mkondo wake.
Ahsante mhe. Naibu Spika wa Muda. Kiswahili ni lugha ambayo ina umuhimu kwetu sisi Wakenya. Ni lugha ambayo inatuelekeza katika shughuli zetu za kila siku. Kwa hakika idadi kubwa ya Wakenya hutumia Kiswahili katika kila jambo wanalolifanya kwa sababu hiyo ndiyo lugha ambayo inafahamika vyema. Kwa hivyo tunapotunga sheria na kufanya jambo lolote ni lazima tufahamu kwamba wakenya ndio muhimu. Tunafaa kuhakikisha kwamba jambo hili limefahamika. Kwa hivyo ninaiunga mkono Hoja hii.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kutegemeana kwa lugha ya kimombo ni high dependency ratio ambayo ni asimila 75 katika Kenya. Idadi ndogo ya wale watu ambao wameajiriwa inawabidi wasaidie wale wengine ambao hawana kazi. Mhe. Naibu Spika wa Muda naomba uniongezee muda kwa sababu dakika zangu zimechukuliwa. Hoja hii itawapatia vijana ii na matumaini. Tutawasaidia hao vijana wawe tofauti katika miaka ijayo.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwa kweli swala hili kuzungumzia kwa dakika mbili hata sijui niache kuzungumza ama nizungumze vipi kwa sababu sisi ni miongoni mwa wale ambao tumeathirika pakubwa katika swala hili. Lakini pengine moja ama mawili ambayo nitazungumzia ni kwamba hivi sasa nafikiri sote twafahamu ya kwamba hata wale wachezaji katika mpira wakiwa ni wazuri lakini wanapofanya makosa lawama zote zinaenda kwa coach . Hali halisi ilivyo katika Kenya yetu kwa maswala ya usalama imekua ni swala ambalo lazungumzwa kila siku lakini halionekani kupata suluhisho. Ni vyema tukiwa kama viongozi kama wajumbe tulitafutie suluhisho jambo hili. Kwa kweli tulitafutie suluhisho jambo hili. Iwapo tutaliacha kuendelea namna hivi na kulijadili ama kupeana lawama hapa na pale hatutafika katika zile suluhisho ambazo tuko nazo. Matatizo yapo. Watu wanauawa. Hivi sasa tunavyozungumza katika Jimbo la Lamu watu hawana ruhusa ya kutoka nje usiku kwa sababu hakuna usalama. Haya yote yamechangia kuzorota kwa uchumi katika sehemu zetu. Kuna umuhimu mkubwa kwa swala hili kuangaziwa pakubwa na sisi viongozi na viongozi wote katika nchi hii. Tukianza kulaumiana hatutapata suluhisho. Ni wajibu wetu sote kuhakikisha kwamba tumeliangalia swala hili. Watu wote waliopewa majukumu katika maswala haya ni lazima tuangalie kwa sababu hawa ambao wanafariki leo na kesho ni ndugu zetu na tunawajibika kuhakikisha kwamba tumekomesha haya. Hivi sasa watu wanaumia na kuteseka kwa sababu ya tatizo hili la kutokuwa na usalama.
Ahsante mhe. Naibu Spika wa Muda. Moja kwa moja ninaiunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na mhe. Lay. Kabla sijaendelea ningependa kumpa Mbunge wa Kisauni mhe. Bedzimba dakika moja na nusu ya. Mhe. Naibu Spika wa Muda Wakenya wengi wanaitambua lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo ni muhimu kama viongozi kutambua umuhimu wa Hoja hii. Mfano nzuri ambao nitauzungumzia leo ni tofauti zinazoibuka wakati tunapoleta Bungeni Miswada iliyobuniwa kwa Kiswahili na ile iliyobuniwa kwa Kiingereza. Kwa hakika kule mashinani wananchi hutiririka kwa wingi kutazama runinga mjadala unapofanywa kwa Kiswahili. Kwa hivyo ninawaomba viongozi wenzngu; tuipe kipa umbele Hoja ili tuhakikishe kwamba Kiswahili kimeimarishwa humu nchini. Kwa hayo machache ninaiunga mkono Hoja hii na kumpa fursa mhe. Bedzimba.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii ambayo dada yangu Mhe. Mishi wa Likoni ameleta Bungeni. Maswala haya tunayoyaongelea hapa kama Bunge la Taifa ni maswala mazito. Tunaongelea swala la mmoja wetu na mtoto wake kupoteza maisha. Kwanza naomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za hao watu wawili mahali pema peponi. Aibu kubwa imetupata kama nchi. Mimi nimekuwa nikipiga mtazamo kuwa mambo haya yangetokea katika nchi zilizoendelea taifa jirani kama Tanzania ama mahali ampapo kuna vijana ambao dada yangu kutoka Lamu amewataja na wapewe ruhusa ya kufanya kazi mahali kama pale leo hii hatungepoteza roho hizo mbili. Asubuhi kulikuwa na Mswada hapa wa kuongeza hukumu ya wale ambao wanafanya ufisadi. Mswada ule kwa mtazamo wangu ni Mswada uliokuja wakati mzuri. Haya tunayoyajadili ni mazao ya ufisadi nchini Kenya. Tumwekuwa wafisadi kufikia kiwango cha kwamba hata kifo hatukiogopi. Ufisadi umetufikisha pale ambapo watu wafa maji ilihali kuajiri mpiga mbizi ni rahisi kwa malipo yake kuliko kupeana zabuni kwa kampuni zinazoweka usalama pale Feri. Ukienda kule Feri utapata kuna wanaume waliokula wakashiba. Wako pale wakijitapa. Mkasa huu umetuonyesha kuwa hawana kazi pale. Badala ya kuandika kazi watu ambao wanaweza kuokoa maisha Feri na Bodi yake yote imeona ni vyema ipeane zabuni na kandarasi kwa vitu ambavyo si vya msingi. Maisha ni kitu ambacho ni lazima tukilinde. Juzi nilimwona Mkurugrnzi akisema kwamba hawana wapiga mbizi. Mara wanasena hawana gesi ya kushuka chini ya maji kizitoa zile miili. Ufisadi umemaliza nchi hii. Ni wakati mwafaka kwa Bunge hili la Taifa kusema ni lazima tupigane na ufisadi kwa njia zote tukianza na Kenya Ferry na kwingineko. Hata mahospitalini watu wafa kwa sababu ya ufisadi. Wapiga mbizi wanajeshi walioko pale Mtongwe kama kilomita moja ama mbili kutoka pale Feri wana tajiriba. Wanatambulika dunia nzima. Lakini hakukuwa na mawasiliano baina ya Kenya Ferry na wao kuwatoa waje kuokoa maisha. Hili ni jambo la kusikitisha. Leo tumewapoteza watu wawili katika janga lile. Si mara ya kwanza tumepoteza watu pale. Pale ni eneo Bunge la Mhe. Mishi Mboko. Ni lazima tupatiwe ripoti kamili ya kile kinachoendelea ndani ya Kenya Ferry. Tumechezewa ya kutosha. Kila mara kinachofanyika pale ni njia ya watu kujitajirisha. Tulitarajia wakati kama huu Waziri... Ingelikuwa ni maswala mengine yametendeka kwingineko Waziri wa Uchukuzi angekuwa amefika mahali pale. Leo hatujamwona Waziri. Tumemwona Mwenyekiti tu Mwazo...
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ni masikitiko kwamba aliyeshiba hajui mwenye njaa. Ujenzi wa sehemu ya pili ya kituo hiki ni muhimu sana. Nasimama kuunga mkono kwa sababu kwanza ni kituo ambacho kitaongeza nafasi za kazi kwa watoto wetu. Vijana wetu hawana kazi na kwa wakati huo ambapo ujezi utakuwa ukiendelea wataajariwa na pia vile vile ukikamilika kuna wengine wengi ambao wataajariwa. Hivyo pia itakuwa ni nafasi kwa nchi kujiongezea mapato yake. Kufikia hivi sasa Bandari ya Mombasa inachangia hela nyingi kwa uchumi wa taifa. Kwa hivyo kupinga Hoja hii ni hatua ya kurudisha nyuma maendeleo. Tukisema kwamba hata vile vilivyoko bado havijatumika kikamilifu ni sawa na kusema ya kwamba kwa sababu mwaka ujao tutajenga shule zingine hakuna haja tupanue zile shule zilizoko. Hayo ni mawazo duni na siyatazamii kuzungumziwa na waheshimiwa katika Bunge hili. Kwa hayo machache naunga mkono Hoja hii.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nimechukua amri yako. Lakini ningekuomba uwaangalie walioketi mpaka saa tatu ili kuwe na njia ya kuwapa nafasi kwa sababu wamengoja sana.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kwa heshima kuunga mkono Mswada huu. Kumekuwa na shida kubwa sana katika eneo la Pwani haswa karibu na Bahari Hindi. Kwa hivyo najulisha Wakenya kwamba Mswada huu ungeletwa mapema zaidi ili tupate njia ya kulinda maziwa yetu. Kwa upande wa usalama watalii wamekuwa wakisumbuliwa na magaidi. Mtalii mmoja alitekwa nyara na magaidi wakampeleka Somalia. Baadaye Serikali ilijaribu kumtafuta na baadaye Rais Kibaki aliyekuwa madarakani alituma wanajeshi Somalia kwa sababu ya huyo mgeni kutekwa nyara akiwa eneo la Pwani. Kwa hivyo Mswada huu utasaidia sana kuangalia vile eneo letu la Pwani na maziwa mengine yataangaliwa kiusalama. Tumekuwa na shida ya kuchafuliwa kwa Bahari Hindi na Ziwa Victoria . Tukipitisha Mswada huu uwe sheria tutapata njia ya kulinda maziwa yetu ili watu wasiyachafue na wadhuru mazingira. Tuko na vijana nchini ambao hutumia madawa ya kulevya. Tukipitisha Mswada huu uwe sheria utazingatia jinsi tutalinda eneo letu la Pwani ili madawa ya kulevya yasiletwe nchini Kenya. Kwa hivyo naunga wenzangu mkono ambao wamechangia na wakasema ya kwamba Mswada huu upitishwe uwe sheria. Naunga mkono na naeleza Wakenya wenzangu ya kwamba tukiwa na Mswada huu tutakuwa na nafasi nyingi za kazi kwa Wakenya. Tukiwa na hiyo sheria na zinginezo tutapata ujuzi kutoka nchi ambazo zimejaribu kulinda pwani yao kama vile nchi za Ujerui Uhisipania na Japani. Kwa hayo machache naunga mkono Mswada huu na naomba Wabunge wenzangu wauunge mkono pia. Ahsante sana.
Ahsante mhe. Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kwa Hoja ya nidhamu nikijua kwamba una uwezo wa kuamua ni nani anafaa kuongea. Ninaona kwamba kuna upendeleo humu ndani. Nimekuja Bungeni mbele ya mhe. Ramadhani lakini amepewa nafasi nami bado sijaongea. Kwa hivyo ninaomba kwamba iwapo kuna Waheshimiwa wengine ambao hawaruhusiwi kuzungumza tuambiwe tujue ndiyo tukae mpaka muda uishe twende zetu. Ninaomba majina ya wanaongojea kuzungumzwa yawekwe mahali ambapo tutayaona ndiyo kila mtu ajue ni nani anafuata mwingine. Ahsante.
Ahsante mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninachukua fursa hii kumpongeza mhe. Mbadi kwa kuuleta Mswada huu Bungeni. Kwanza kabisa ningependa kusema kwamba ninauunga mkono Mswada huu. Mimi ni Mbunge anayeegemea upande wa Serikali. Sitoshawishika kuunga mkono kupitishwa kwa sheria yoyote ambayo ni kinyume na Katiba ya nchi hii. Ninasema hivi kwa sababu nimebahatika kusoma kumbukumbu ya aliyekuwa Rais wa Zambia mhe. Kenneth Kaunda. Mhe. Kaunda ni miongoni mwa viongozi ambao hawajawahi kufungua akaunti ya benki nje ya nchi zao. Alihudumia taifa lake na kuhakikisha kwamba ameliboresha. Alistaafu akiwa maskini. Sitofurahia leo kuwaona wale ambao walijitolea mhanga kuhakikisha kwamba taifa la Kenya limepiga hatua kwenda mbele wamerudi katika umaskini kufikia kiwango cha kutoweza kujitibu wanapoathirika na maradhi. Hii ndiyo sababu ninaiunga mkono Hoja hii. Pili kuna neno moja nililolisoma katika Biblia. Nino hilo linasema kwamba wale wakwanza watakuwa wamwisho na wamwisho watakuwa wakwanza. Pengine tunafanya hivi kwa sababu tuko kwenye mrengo wa Serikali. Tutaweka vishawishi. Tutafunga barabara ili fulani na fulani asifaidi. Naomba tuangalie taifa na taasisi; tusiangalie watu. Ikiwa tutaangalia watu basi tutatunga sheria ambazo zitawatatiza watoto wetu siku za usoni. Ningependa kulinganisha wabunge wa hapa Kenya na wabunge kutoka nchi za nje. Tuchukulie mfano wa Afrika Kusini na tuseme kwamba familia ya dela imesemekana haitalipwa hela kwa sababu dela alihusika na kampeni za ANC. Ama tuchukulie mfano mwingine wa nchi jirani Tanzania na tuseme kwamba familia ya Mwalimu Kabarage Nyerere isilipwe malipo ya uzeeni kwa sababu alihusika kwenye kampeni za CCM. Kwa kweli haya mambo hayataingia akilini. Kipengele cha tatu katika Mswada huu kinakwaruzana na Kipengele 38(1). Mimi nitakuwa wa kwanza kuleta marekebisho ili kuhakikisha Kipengele hicho cha tatu kimetolewa. Hii ni kwa sababu ni sheria ambayo inadhulumu na inakwaruzana na Katiba ya nchi hii. Kwa nini tutunge sheria kama hizi? Naunga mkono Mswada huu. Ahsante Bwana Naibu Spika wa Muda.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninaomba nichangie Hoja hii. Kwanza ninatoa shukrani kwa Mhe. Alhaji Omar Mwinyi Mbunge wa Changamwe kwa kuleta Hoja hii Bungeni ili tuichangie ili watu wa Kenya wapate afueni kutokana na haya masaibu wanayoyapata kwa sababu ya mwenendo wa Shirika la Ndege la Kenya. Ningependa Wakenya wafahamishwe kwamba wanamiliki theluthi moja ya Shirika la Ndege la Kenya. Wamombo wanasema 30 per cent. Hisa zingine si za Wakenya wala Serikali ya Kenya bali ni za Wadachi. Kwa hivyo hili shirika si mali ya watu wa Kenya lakini anga ambayo wanaitumia vile watakavyo ni ya Kenya. Mhe. Naibu Spika wa Muda ukiangalia mwongozo wa Shirika la Ndege la Kenya utagundua kwamba unatolewa na Wadachi. Hii ndio sababu kuna njia zingine ambazo Shirika la Ndege la Kenya limeachia Wadachi. Hizi ni safari ambazo zinaweza kuletea shirika hili pesa. Kwa mfano kuna njia ya kutoka Nairobi kwenda Roma. Njia hii ilikuwa inaletea hili shirika pesa lakini kwa sababu Wadachi waliitaka waliambia Shirika la Ndege la Kenya waache hiyo njia na ikawa yao. Walipokonya Wakenya hiyo njia. Nauli za Shirika la Ndege la Kenya zinakera. Pia zinapatia watu wengi masaibu. Kwanza ni ghali. Utaketi kiti na mwenzako vile nilivyokaa hapa na Mhe. Omar Mwinyi na utakuta umelipa nauli tofauti kabisa na mwenzako ambaye ameketi nawe. Kisa na maana ni nini? Ni kwa sababu wewe aidha ulikata tiketi yako mapema na mwenzako amekata tiketi yake baadaye. Nimeona mambo haya katika Shirika letu la Ndege. Pili ukisema unabadilisha masaa yakusafiri; labda ulikuwa usafiri jioni na useme unataka kuongeza masaa mara nyingi utaambiwa kwamba nauli imebadilika. Kwa nini nauli ibadilike? Ninaposafiri kwenda Mombasa kwa basi nikisema ninaenda huko nikitumia basi ya saa tatu na nibadilishe nisafiri na basi ya saa tano nauli haibadiliki. Lakini katika Shirika la Ndege la Kenya utakuta kwamba unalipishwa ada. Mhe. Naibu Spika wa Muda ukipatikana na mkosi na uamue unabadilisha safari yako labda ulikuwa umetafuta nafasi ya kusafiri kutoka Nairobi kwenda Mombasa nakurudi ikiwa hukuchukua safari ya kwanza yakuenda na unatumia nauli yakurudi pia utalipishwa kwa kutosafiri. Ni mara ngapi tumesafiri na ndege ya shirika hili na unakuta viti viko bure? Ndege inapaa juu na inaenda bure lakini watu wameachwa chini na wanaambiwa kwamba ndege imejaa. Tunaomba kwamba Shirika la Ndege la Kenya lipatiwe changamoto na njia yakulipatia changamoto ili liamke ni kuruhusu mashirika mengine ya ndege kutumia anga yetu ya Kenya. Tuko na Mkenya mmoja anayeitwa Rubani Musa Bulhan. Huyu alikuwa ni mmoja wa Wakenya wa kwanza kununua ndege kubwa lakini amenyimwa nafasi ya kutumia hizi ndege kutoka Nairobi hadi Kisumu ama Nairobi hadi Mombasa. Ameamua ndege zake zitoke Nairobi ziende Jeddah na kama si Jeddah ziende Somalia. Je hili anga ni la Kenya Airways peke yake? Tukiwapatia changamoto wafanyikazi wa shirika la Kenya Airways watageuza mienendo yao na tabia zao na kuanza kuwajibika. Mara nyingi wafanyikazi wa shirika hilo ni wazembe wafidhuli na mahanithi. Siwezi kusema mengine lakini wafanyikazi wa Kenya Airways wamekuwa wajeuri kiasi kwa sababu wanajua kwamba hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kupatiwa nafasi ya kuleta ndege zake humu nchini. Bi. Naibu Spika wa Muda mara nyingi unapoenda kwenu kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Eldoret hutumia ndege gani? Utaona kwamba ni shirika moja tu ambalo limepewa nafasi - Kenya Airways. Kampuni nyingine inayoruhusiwa kupeleka ndege huko ni Flight 540. Mimi na mhe. Mwinyi tukichukua mkopo kutoka kwa benki na kununua ndege hatuwezi kuruhusiwa kutumia anga ya nchi hii kwa sababu imetengewa Kenya Airways. Kwa hivyo ninatoa changamoto kwa Serikali iweke anga yetu wazi kwa wale watu ambao wangependa kushiriki katika biashara ya usafiri wa ndege ili nauli za ndege zishuke. Kwa hayo machache ninatoa ombi langu kwa mara nyingine na kumshukuru ndugu yangu Alhaj Omar Mwinyi kwa kuuleta Muswada huu Bungeni.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuandaa na wenzangu kuunga mkono huu Mswada ambao uko mbele yetu leo. Jambo muhimu ambalo nataka tujiulize ni kwamba umuhimu wa huu Mswada ni nini katika nchi yetu ya Kenya? Ni yapi ambayo tumeweza kuyafaidi ama tumeyaona katika nchi yetu ya Kenya kuhusiana na Mswada huu? Kwa kweli kumekuwa na tatizo kubwa katika suala la umeme katika nchi yetu. Tunajua vizuri kwamba kampuni ya Kenya Power and Lighting Company ndiyo iliyokuwa ikishughulika sana na suala hili na wao ndio washikadao katika suala la kusambaza umeme katika nchi yetu ya Kenya. Wachache ndio walikuwa wakipata huduma hii na wengi hawakuwa wakiipata. Kumekuwa na matatizo makubwa sana kwa sababu ukilinganisha na matumizi utaona kwamba malipo ya huduma hiyo yako juu. Kutokana na hali hii kumekuwa na utata mkubwa lakini nimeshukuru pakubwa kwamba jambo hili limeweza kusambazwa kwa njia nyingine kiasi kwamba kumekuwa na mashirika mengine ambayo yanasambaza umeme. Jambo ambalo tunahitaji kulizingatia ni kwamba ni lazima kuwe na mwelekeo wa kupunguza umaskini katika nchi yetu. Naamini kwamba umeme utakapokuwepo viwanda vingi ambavyo vinatumia umeme vitalipa pesa kidogo ili bidhaa kutoka kwa viwanda hivyo ziweze kuuzwa kwa bei nafuu na wananchi wapate huduma ambazo zitawasaidia kujitoa kutoka kwa umaskini. Bidhaa nyingi hivi sasa zimekuwa na bei ya juu kwa sababu zinatumia umeme ambao ni wa bei ya juu sana. Hayo ndiyo matarajio makubwa ambayo tunahitaji kuwa nayo tunapolizingatia suala hili. Ukweli ni kwamba hivi sasa katika nchi yetu suala la stima linaonekana kuwa afadhali. Nikizungumzia eneo la Bunge langu la Lamu Mashariki kwa mara ya kwanza tangu tupate Uhuru wananchi wa sehemu hii sasa watafurahia kuwa na umeme. Huduma hiyo imepelekwa kule na Serikali ya Jubilee kupitia shirika la Rural Electrification Authority. Hivi karibuni tutapeana huduma hii kwa wananchi na KP watachukua usukani. Hili ni jambo ambalo Serikali ya Jubilee imeweza kulipea kipaumbele. Hakuna lolote linaloweza kufanyika katika nchi hii ikiwa kutakuwa na matatizo ya stima. Maendeleo mengi yanayofanyika katika nchi yetu na kwote ulimwenguni yanatokana na kuwepo kwa stima. Iwapo tutafanya hivyo basi ninaamini kwamba tutaweza kuendelea sana. Vilevile kuna kampuni ya Amu Power ambayo iko Lamu ambayo hivi karibuni itaanza kutumia mtambo unaotumia makaa ya mawe kuzalisha umeme. Amu Power ni kampuni imeenda Lamu kuwekeza katika sekta ya umeme. Naamini kwamba kampuni hii itakapoanza kutoa huduma vijana wengi watapata kazi na gharama ya umeme katika eneo la Lamu itapungua. Ni lazima Serikali pia iwajibike pakubwa kuhakikisha kwamba wananchi wamelindwa. Utapata mashirika mengi ya umeme yanapata hasara fulani ama kunatokezea mambo ambayo yanaleta kutokua na mwelekeo katika suala hili. Ningependa Serikali iwe na tahadhari kubwa kwa sababu kuna malalamishi mengi juu ya suala hili kutoka kwa wananchi. Mara nyingi wananchi hulalamika kuhusu huduma duni wanazopata kutoka mashirika kama haya. Wakati mashirika kama hayo yanapokwenda kwenye sehemu kama hizo kuna mambo fulani ambayo wananchi wanatarajia yazingatiwe pakubwa haswa masuala ya ajira. Watu kutoka sehemu nyingine hupelekwa kufanya kazi katika sehemu hizo lakini wenyeji ndio wanaostahili kupewa kipaumbele kwenye masuala ya ajira. Vilevile kuna masuala mengine. Wakati huduma hiyo inapofika katika eneo hilo wenyeji wanastahili kuzingatiwa zaidi kuliko wageni. Ningependa kutoa tahadhari na kuwaomba wahusika wahakikishe kwamba mipango yote imetekelezwa vizuri ili huduma hii iweze kumfikia kila mmoja wetu kikamilifu bila ya kumsahau mwananchi wa kule mashinani ambaye hakutarajia kuipata huduma hii. Zaidi ningependa wananchi waelimishwe jinsi ya kutumia umeme kwa sababu tunajua kwamba umeme ni hatari. Kuna watu ambao hawajawahi kutumia umeme. Serikali inastahili kuwaelimisha watu hao kuhusu uzuri na madhara yanayotokana na umeme. Mhe. Naibu Spika wa Muda bila ya kupoteza wakati ninaunga mkono Mswada huu. Ninawaomba Wabunge wenzangu tuungane ili tuweze kurekebisha pale ambapo panahitaji kurekebishwa na tuuunge mkono Mswada huu.
Ahsante mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua fursa hii kuunga mkono Mswada huu. Kwa hakika wanyamapori wanaleta faida kubwa katika taifa hili lakini pia inastahili tufahamu kwamba mwanadamu yuko na thai kubwa zaidi kuliko mnyama. Hata Mwenyezi Mungu alipoumba mbingu na ardhi alimuamuru mwanadamu aje ardhini kuwatawala wanyama na awe mwenye mamlaka juu yao. Inatupasa pia tuzingatie kwamba binadamu anathai zaidi kuliko mnyama. Pendekezo kwamba ridhaa kwa mtu ambaye ameuawa na mnyamapori iwe Ksh3 milioni halijatosheleza. Tuchukulie kwamba mtu huyu ndiye anayeitafutia riziki jamii yake. Mtu huyo anapopotea kwa ghafla ridhaa hiyo ya Ksh3 milioni haiwezi kukidhi mahitaji ya jamii yake kwa muda mrefu haswa tukizingatia jinsi shilingi inavyopoteza thai yake siku baada ya nyingine. Kwa hivyo wakati wa kupendekeza marekebisho utakapowadia nitajaribu kuleta pendekezo la kuibadilisha hali hiyo na kuongeza ridhaa kwa mtu atakayeuawa na wanyamapori kutoka Ksh3 milioni hadi Ksh10 milioni. Hata ikibidi jamii ya mwendazake wagawane pesa hizo kila mmoja atakuwa na kiwango cha fedha kitakachomusaidia. Tuchukulie kwamba aliyeuawa ni mwanamume ambaye amejimudu na kuweza kuoa mabibi 10 alafu uwapatie Ksh3 milioni. Ukiwagawanyia fedha hizo mabibi 10 na watoto wao kila mmoja anapata kiwango ambacho hakistahili kamwe. Ni pesa ambazo anaweza kuzimaliza kwa mwezi mmoja halafu wabaki wakihangaika. Miongoni mwa wanyama walioorodheshwa kuna wanyama kama vile nyani na tumbili ambao wameachwa nje licha ya kwamba hao ndio wanyama waharibifu zaidi wa mimea na haswa mumea wa mahindi. Inafaa wanyama hao pia wajumuishwe kwenye orodha ya wanyama waharibifu. Vile vile kuna wavuvi ambao huenda kuvua samaki. Wakati mwingine hukumbana na papa na kupambana nao. Wakati mwingine utapata yule mvuvi amekatwa vipande viwili naye hupoteza maisha yake. Wanyama kama papa inafaa waorodheshwe ndiposa atakayepata hasara ya kuuliwa na papa alipwe ridhaa. Kuna samaki mwingine hatari sana tunamwita pweza. Huyu samaki akikupata katika mwamba utabaki pale pale mpaka bahari ijaye tena upya; utakufa maji. Yule pweza pia angeorodheshwa kama mojawapo wa wanyama ambao wakimwathiri binadamu basi alipwe ridhaa. Ridhaa inayolipwa kwa ajili ya mimea kuharibiwa kiwango chake ki chini sana. Pana haja wakati wa marekebisho tulete marekebisho mwafaka. Kwa mfano mnazi unafaida chungu nzima.Hakuna sehemu moja ya mnazi ambayo utaitupa.Kila sehemu inayo faida. Ukipata mnazi umeharibiwa na hali kiwango kimetengwa kulipa mnazi ni duni kabisa Inapaswa hili lizingatiwe ili pawekwe kiwango kinachostahili na kinachoweza kukimu hali ya maisha ya mkulilma. Wenyeji wanaoishi karibu na sehemu zilizotengewa wanyama pori sharti wapate kiwango fulani kutoka kwa mapato ya utalii. Baadhi ya jamii pia ziruhusiwe kubuni mashamba ya wanyama.Hivyo watawaalika watalii kutembelea mbuga hizo zilizobuniwa. Hii ni njia ya kupata mapato ya kukimu hali yao ya maisha. Kuna sehemu nyingi ambazo ni kame na zinaweza kutumika kuhifadhi wanyama. La ziada sina. Nawapa nafasi wenzangu nao wachangie.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua fursa hii kwanza kumpongeza Mhe. Kaluma kwa kuleta Mswada huu ambao utaleta mwongozo na uuwiano baina ya taasisi tofauti humu nchini. Bunge lina wajibu wa utunzi wa sheria. Mahakama hutafi sheria na utawala hutekeleza sheria. Ni lazima kuwe na uwiano baina ya taasisi tatu za Serikali zinazohusika katika utekelezaji wa sheria. Iwapo hakuna heshima maanake sisi kama BungeKatika Kanuni za Bunge ambazo zinatuongoza hazituruhusu kujadili maswala ambayo yako mbele ya mahakama. Kwa bahati nzuri au mbaya kanuni kama hizo haziko katika upande wa mahakama. Wakati mwingine mahakama huingilia shughuli za utunzi wa sheria na jambo hili huwa na athari kubwa. Kwa mfano kura ya kutokua na ii kwa Gavana wa Embu. Sheria inatoa mchakato vile kura ya kutokua na ii juu ya gavana au Rais inavyostahili kupigwa. Inaanza kwa bunge la ugatuzi halafu Senate linampa fursa. Kuna kipengele ambacho kinapeana mamlaka mahakama kusimamia maswala haya. Ile kura ya kutokua na ii kwa Gavana wa Embu imebadilishwa na mahakama ya Kenya. Sasa tunajiuliza kama tunastahili kuwa na Bunge hili Bunge litakuwa na kazi gani? Kuna sheria ambayo inasema wakati Kamati ya Bunge inakaa ina mamlaka sawa na mahakama kuu. Sasa mahakama itasimama kulia kushoto na kuingilia maswala ya Bunge. Ili taasisi hizi ziweze kushirikiana na kuheshimiwa ni vyema mahakama itoe fursa kwa Bunge Bunge litekeleze kazi yake hata kama ni kuimpeach mtu. Wale ambao hawajaridhika na uamuzi wa Bunge waende kortini. Lakini sio kusimamisha shughuli za Bunge katikati na mahakama kuchukua hatua ambayo haistahili. Kwa hayo machache ninaunga mkono Mswada huu.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuongeza sauti yangu katika kuupinga Mswada huu ambao umewasilishwa hapa na Mhe. Chepkong'a. Inafaa ifahamike kwamba Katiba hii inayowapatia akina mama nafasi zaidi katika Bunge haikupitishwa na akina mama peke yao bali ilipitishwa na wananchi wa nchi tukufu ya Kenya. Iwapo Katiba itatupatia kwa mkono wa kulia na Bunge itunyang'anye kwa mkono wa kushoto itakuwa aibu fedheha na dhuluma. Sisi kama akina mama ambao tumehesabika katika Bunge hili la kumi na moja tutaingia katika vitabu vya historia kama akina mama waliohudumu katika Bunge ambalo lilinyanyasa na kudhulumu akina mama. Mimi nikiwa Mbunge kutoka Laikipia nimeingia Bunge hili kupitia uteuzi. Iwapo nisingepata fursa ya kuingia katika Bunge hili nisingekuwa nazungumzia eno ya kugombea kiti cha ubunge cha Laikipia Kaskazini mwaka wa 2017. Tunasema kwamba mtoto akizaliwa ni sharti umpe chakula ili akue. Jinsi akina mama waliwezeshwa kuingia humu Bungeni ni njia mojawapo ya kutayarisha miundo misingi ili kukuza maazimio yao ya kugombea viti na kuhesabika katika uongozi wa nchi hii tukufu ya Kenya. Mswada ambao umeletwa na Mhe. Chepkong'a unaturudisha nyuma. Mswada huo unadhulumu na kunajisi Kenya. Sote tunajua kunajisi ni kitendo chafu. Ni dhambi na hata hakitajiki. Hatuwezi kukubali Mswada ambao unanajisi Katiba ya Kenya ambayo sisi wenyewe tulipigia kura na ikawa sheria kuu inayoongoza nchi hii. Mwisho ningependa kusema kwamba mimi ninakienzi chama cha Jubilee. Ninajivunia kuwa mmoja wa wanajubilee. Nakienzi kwa sababu hii: Ni chama ambacho kimesifika na kina umaarufu wa kutetea haki za wanawake. Chama hiki kinawatambua akina mama na kuwaheshimu. Ifikapo hiyo 2017 ninataka kuwarai wanawake wa Kenya nzima wasije wakauliza chama ni gani. Waangalie chama kinachoheshimu na kutetea akina mama. Katika upande ule wa Upinzani wa ODM tumemwona mama mmoja peke yake ambaye ni Millie Odhiambo ambaye amechaguliwa katika Eneo Bunge la Mbita. Yeye hupigwa vita kila mara. Hata tunapozungumza hapa Mimi si mwanachama wa ODM lakini ninajua Mhe. Millie Odhiambo anapigwa vita na wale mabwanyenye ambao wanajiita vigogo wa ODM. Kwa hivyo ninawarai akina mama wavuke na kuungana na chama cha Jubilee ili tulete akina mama hapa Bungeni na tupunguze mzigo aliobeba punda ambaye wanasema amechoka. Tuchague akina mama mimi nikiwa mmoja wao kutoka idadi ya 60 kuendelea. Ninapinga.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuungana na wenzangu katika kuwapongeza wanakamati kwa kazi yao nzuri ambayo wamefanya kuhusiana na Ripoti hii ambayo imeletwa Bungeni. Kwa kweli wengi wamechangia kuhusiana na masuala haya na haswa kuhusu pesa za NG-CDF - Hazina ambayo imekuwepo kuanzia mwaka wa 2003. Ni vyema Wakenya wafahamu utaratibu wa NG-CDF na mabadiliko ambayo yamefanyika katika NG-CDF. Ukweli ni kwamba fedha hizi kuanzia mwaka wa 2003 zimeleta mabadiliko makubwa nchini Kenya. Leo kuna mengi yanayozungumziwa kuhusiana na maendeleo na mengineo lakini ukweli ni kwamba fedha hizi zimeonekana katika sehemu za mashinani. Fedha hizi zimeleta maendeleo makubwa katika maeneo Bunge. Faida ambayo imepatikana kutokana na matumizi ya NG-CDF ni nyingi sana ukilinganisha na hazina nyingine zilizoanzishwa na Serikali ya Kitaifa na serikali za kaunti. Hizi sitaki ziwe ni sifa ambazo twajipa sisi Wabunge. Ni lazima Wakenya wafahamu kwamba sisi kama Wabunge hatuhusiki kwa namna yoyote kwenye utendakazi wa NG-CDF. Fedha hizi zimeweza kutumika kwa mipangilio yake na Wakenya wanaziona. Huu ni ushahidi kamili. Tatizo ambalo bado lipo mpaka sasa ni kwamba Wakenya bado wanahitaji maendeleo. Changamoto ni nyingi. Ni lazima Serikali ifahamu kikamilifu. Miongoni mwa mbinu zilizotumika kugawanya fedha hizi katika maeneo Bunge hapo ni idadi ya watu na hali ya umaskini katika sehemu hizo. Utakubaliana nami kwamba baadaye mbinu hiyo ilibadilishwa na kila eneo Bunge likawa linapokea kiwango sawia cha fedha kutoka NG-CDF. Hakuna eneo Bunge linalopata pesa nyingi kuliko lingine. Ukweli ni kwamba maeneo Bunge hayafanani. Kuna sehemu ambazo zimeendelea na kuna sehemu ambazo bado kuna udhaifu na umasikini mkubwa. Mbali na kusema kwamba tuangalie idadi ya watu sidhani ni kiegezo kizuri kwa sababu utapata idadi ya watu ni ndogo lakini matatizo na umaskini ni mwingi. Kwa hivyo naunga mkono lile pendekezo au mwongozo wa kila eneo Bunge lipewe fedha zile. Ukweli ni kwamba fedha hizi zinazopelekwa kwa maeneo Bunge ni fedha ambazo zinahitajika. Naunga mkono waheshimiwa ambao wamechangia swala hili. Wanahitaji kuongezeka. Kuna uwezo na njia za kuongeza fedha hizi. Kwa mfano fedha hizi zimewekewa mipangilio ya kwamba zitatumika katika maswala ya elimu ama ulinzi. Utapata kuwa katika Serikali ya Kitaifa kuna pesa ambazo zinatengwa kupewa wizara inayohusika na maswala ya elimu ama ulinzi wakati Bajeti ya Kenya inapangwa. Ni kama kusema kuwa fedha hizi zinazopelekwa katika Wizara ya Elimu matumizi yake ni yale ambayo yamepangiwa miongoni mwa matumizi ya NG-CDF. Kwa maoni yangu ningesema kwamba Serikali izingatie pakubwa. Ni kama kutumia pesa kwa njia moja. Leo utapata kwamba eneo Bunge linahitaji kujengewa madarasa. Baada ya pesa zile kupatiwa NG-CDF zingine zinapatiwa wizara katika kuifanya kazi hiyo hiyo. Fedha hizi mwishowe hazionekani dhai yake katika wizara hizi. Kila mmoja wa Wabunge hawa anaweza kutoa ushahidi mkubwa kuwa zile pesa tunazoziona ni zile zinazotumika kwa NG-CDF. Zile ambazo zinaenda katika wizara halafu wizara inapendekeza kuwa kujengwe madarasa hatuelewi zinagawanywa vipi. Ni lazima tuzingatie haya pakubwa. Nchi yetu iko na malengo na maono katika kuendeleza elimu lakini changamoto ni nyingi. Sisi Wabunge ndio ambao tunapambana na changamoto hizi katika maeneo Bunge yetu mashinani. Serikali imepanga kwamba watoto wasome bure na madarasa yajengwe. Lakini utapata kwamba mipangilio hii Serikali imependekeza haijakamilika. Utapata kwamba katika shule moja darasa moja lina watoto kati ya mia moja na mia mbili kwa sababu elimu ni bure. Hii ni hali ya kusikitisha. Ingekua ni vyema kwamba kabla hawajakuja na mipangilio hii wangefanya utafiti kikamilifu katika maeneo Bunge yote katika kaunti zote na kujua yale yanayohitajika kukamilishwa au kutekelezwa kwa mapendekezo yao ya watoto kusoma bure. Swala la kutaka kufanya mambo na wakenya halafu baadaye kuona wanadanganywa sioni kama yatatatua matatizo yetu. Kuna dharura kubwa ya Serikali kuzingatia. Ndio kwa sababu tunataka wanafunzi au watoto wetu wa kila sehemu waende shule. Tunataka wazazi wasaidiwe mizigo ya kulipa karo shuleni. Ningependa kuambia Bunge hili kwamba hadi tunavyozungumza hivi sasa mipangilio hii haijaweza kuwa na mwongozo kikamilifu kwa sababu matatizo mengi hayajaweza kusuluhika. Ningependekeza kama wenzangu walivyotoa maoni kuhusu fedha za NG-CDF. Nina ii kwamba utafiti huu umefanyika na umeonekana kuleta mabadiliko makubwa. Fedha hizo ziongezwe katika kuendesha maswala haya ya maendeleo katika maeneo Bunge yote ya Kenya hii ili tuweze kuhakikisha kuwa matatizo ya jamii katika swala nzima la elimu na mengineyo yamesuluhishwa. Ningependa kuunga mkono Ripoti hii ambayo imeletwa Bungeni.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuzungumzia Hoja hii kwa huzuni sana haswa tunapoona kwenye magazeti na televisheni vifo vya watu kila siku. Kama alivyosema Mhe. Shebesh ni lazima Serikali ichukue jukumu la kumaliza janga hili la watu kuwaua wengine kule Baringo Turkana Elgeyo Marakwet na Trans Mara. Kama kundi la Mungiki liliangamizwa basi inawezekana kumaliza janga hili. Rais Kibaki alimkubalia mwendazake Waziri Michuki kumaliza kundi la Mungiki lililokuwa likiwahangaisha wakazi katika eneo la Kati mwa Kenya. Michuki hakujali kama Wakikuyu watamlaani. Janga la wizi wa mifugo linafanyika katika eneo la Bonde la Ufa sehemu ambako Gen. Nkaissery na Naibu wa Rais wametoka. Ni lazima wasimamishe vifo vya watu. Gen. Nkaissery afuate nyayo za Michuki. Naibu wa Rais yuko Serikalini na ni lazima asimamishe vifo vya watu. Serikali tu ndiyo inaweza kumaliza wizi wa mifugo kwa sababu iko na ripoti kuwahusu watu ambao wanahusika na vitendo hivyo. Hatuwezi kumwambia Mhe. Ng'ongo Kamama na Cheptumo wawakamate wale wanaohusika. Lakini inafaa Serikali itekeleze jukumu la kumaliza janga hili. Hatutashinda tukiwaambia watu wajisajili kama wapiga kura ilhali kuna wale ambao wanakufa. Je wale wanaouwawa watapiga kura? Tunaiambia Serikali ichukue jukumu hili. Hata katika Eneo Bunge langu kuna mtu yuko hospitalini ambaye amepigwa risasi sijui ngapi. Juzi tulizika kijana aliyeuawa kwa kukatakatwa mara kumi. Watu kutoka jamii za Maasai na Kipsigis wanakufa na hakuna mtu anayejali. Nkaissery na Naibu Rais hawajakanyanga kule. Hawa watu watakufa mpaka lini? Lazima tuiambie Serikali iamka imalize ukosefu wa usalama nchini. Kama hawatafanya hivyo uchaguzi utakuwa wa bure. Kama watu wetu wamekufa nani atapiga kura na watapigia nani kura? Watapiga kura ya nini kama Serikali yenyewe haiwezi kuamka na kumaliza tatizo la ukosefu wa usalama. Ndugu zangu naiambia Serikali kwamba wakati umefika wa kumaliza ukosefu wa usalama. Tunataka kuishi kwa ai na mipaka yetu iwe na ai. Naomba Serikali ichukue jukumu lake.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Protect me from the other . Nataka kusema ya kwamba ni aibu kama viongozi tukijadiliana mambo ya mazingira mtu analeta siasa na uongo wa kibinafsi hasa Mheshimiwa ama kiongozi. Sio vizuri watu wa Mau wangoje wakuwe na shida kama vile Mhe. Kutuny ametaja Kisumu ndio wajue ni vibaya kukata miti na kuharibu mazingira. Mhe. anapotosha Bunge la Kitaifa.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Sitaki kumjibu Mhe. Pamela Ochieng lakini amejaribu. Sipotoshi Bunge la Kitaifa. Mimi si mtu wa kawaida bali ni Mhe. Kwa hivyo ni vyema kujifahamisha wakati mwingine. Licha ya kuzungumzia hayo mimi nataka kukashifu viongozi kutoka Bonde la Ufa ambao walienda kule Mau na kumkashifu Rais na kumpatia ilani juu ya suala hili. Kwa mazungumzo ambayo yanaendelea sasa ni kwamba ubomoaji wa nyumba umekwama. Tunashukuru Serikali kwa hilo. Lakini watu wapewe makao. Hayo ndiyo mimi naomba kwa sasa. Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Swala la barabara si swala la Githunguri na Ruiru pekee. Tulipitisha Hoja hapa kuhusu kilomita 20 za barabara katika kila eneo-wakilishi la Bunge. Pengine Mwenyekiti angetuelezea ni lini mipango hiyo itaanza katika kila eneo-wakilishi la Bunge ili barabara zipitike vyema. Wizara ina mipango gani ili miradi hiyo ianze mara moja kwa sababu mwaka wa kwanza umepita na hakuna chochote kimeanza? Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Unavyofahamu hawa ni watu ambao wana familia. Wakitoka kufanya kazi hizi wako na majukumu ya kulea familia zao. Wako na watoto ambao wanaenda shule na vile vile wana mahitaji. Kwa hivyo ni vema sisi kama viongozi tuwasaidie ili waweze kujisikia kama Wakenya wengine. Ni vigumu kuwa katika viatu vyao. Kwa mfano ukitoka kwa nyumba kwenda kujenga nchi na unaporudi nyumbani uwe huna hata mkate uliobebea wanao hilo ni jambo baya. Ni vema sisi kama Bunge tulichukulie hili jambo kuwa la dharura na kuhakikisha kuwa hawa wazee tunawasaidia ili waweze kupata mshahara kama wafanyikazi wengine nchini. Kwa hayo machache naunga mkono hoja hii.
Ahsante Mhe. Naibu Spika. Awali ya yote naomba kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwenye wingi wa rehema kwa kutujalia afya njema na kutufikisha siku ya leo. Mwenyezi Mungu anaendelea kuitikia dua ya kuliombea Bunge hili kwa kutuongezea hekima na maono kwa ajili ya kuwatumikia Wakenya. Nachukua fursa hii pia kukushukuru wewe binafsi Naibu Spika wenye viti Bungeni pamoja na Wabunge wote kwa uteuzi wayo. Mighairi na hayo nachukua fursa hii pia kuwapongeza na kuwashukuru wana Nyali kwa kuamua kwenda kinyume na itikadi na siasa chafu za pesa vyama na ukabila na badala yake kunichagua mimi kama mgombea huru katika eneo Bunge la Nyali. Nawapongeza pia Wakenya wote waliojitolea na kuchangia katika mkoba wangu wa Kampeni pamoja na ushauri walionipa. Sina la kuwapa ila nawaahidi kuwa nitazidi kuwapigania na kuwakilisha sauti zao katika Bunge la 12. Kwa ufupi nasema Mungu awabariki wote kwa kuamini kuwa hakuna lisilowezekana mbele ya macho ya Mungu. Fauka na hayo naomba hili Bunge la 12 liwe kielelezo na tofauti kabisa na Bunge za hapo awali kwa kujadili na kupasisha Miswada itakayo wakinga Wakenya dhidi ya udhalimu ukiukaji wa haki za binadamu ufisadi na mambo mengine ya kuchukiza. Mhe. Naibu Spika mengi yalitajwa wakati wa Hotuba ya Rais huku kukiwa na matumaini ya mambo kuwa sawa katika siku za usoni. Nchi inayoongozwa na demokrasia hufanya mambo yake kidemokrasia. Nchi inayoongozwa na demokrasia ya kijambazi hubaka demokrasia ya wananchi wa taifa hilo na kuwakandamiza. Ni matumaini yangu kuwa sote tutakuwa mamoja pasi na misingi ya dini kabila rangi au vyama kuilinda Katiba na taifa letu zuri. Letu kuu kama viongozi waliochaguliwa na Wakenya ni kuhakikisha kuwa safari hii hatutazalisha tena umaskini. Tuhakikisheni kuwa kupitia sura hizi ninazoziona Bungeni - sura za Wabunge maprofesa wanahabari madaktari wahandisi miongoni mwa wengine wengi - tutashikaa na kujenga Kenya kwa kutumia taaluma zetu na wala sio kuwa vibaraka wa kuabudu miungu binadamu. Kwa ufupi tusikubali akili ndogo kutawala akili kubwa. Mhe. Naibu wa Spika licha ya Hoja zote zilizotajwa majuzi na Rais - Hoja za Kenya na Ukenya ndani yetu - ningelipenda pia kuchukua fursa hii kuomba Bunge hili chini ya uangalizi wako katika siku za usoni kuwa makini na kutunga sheria kali dhidi ya walanguzi wa dawa za kulevya. Hakika sisi Wapwani tumeathirika pakubwa na watu wachache wanaojipiga kifua na kujiona kama miungu midogo huku wakiangamiza kizazi chetu. Safari hii tunaujumbe kwa walanguzi wa dawa za kulevya Pwani. Tunasema kama noma naiwe noma . Wakenya wote ni mashahidi kwamba vijana wetu wengi wameendelea kudhoofisha afya zao kutokana na matumiza ya dawa za kulevya. Dawa za kulevya ni hatari sana kwa usalama wa ustawi wa taifa letu. Vita hivi ni vita vikubwa dhidi ya uagizaji uzalishaji usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya. Sote tunapaswa kuunga mkono jitihada hizi. Nikimalizia nihitimishe hotuba yangu kwa kuombea waheshimiwa Wabunge-wenza pamoja na Wakenya wote waliotutuma katika Bunge hili kama watumishi na wala si waheshimiwa Mwenyezi Mungu atujalie sote nasiha njema katika kipindi chote tutakachokuwa mashinani kuwatumikia Wakenya waliotuchagua kwa kuchukua maoni yao na kuwawakilisha ipasavyo katika hili Bunge la 12. Mungu ibariki Kenya.
Ahsante mhe. Naibu Spika. Kifungu cha 94 (5) kinasema hivi:- Hakuna mtu chuo au taasisi ambayo itatunga sheria bila kupewa fursa ya Kikatiba na Bunge hili. Sasa mimi nauliza: Kwani hii Tume ya Sarah Serem imetoa mamlaka hiyo wapi? Kifungu 41 cha Katiba kinasema: Kila mfanya kazi apewe huduma aki na usawa. Naibu Spika nilikuwa katika Bunge la Tisa na najua mshahara wangu ulikuwa wa pesa ngapi. Nimekuja katika Bunge la Kumi na Moja. Ni nini kimebadilika kwa wajibu wangu kama Mbunge au wajibu wa Bunge hili? Tofauti ni nini? Ni nini inaongoza Tume hiyo kukata mshahara wangu kwa asilimia 57 bila kunihusisha mimi kama mfanyi kazi. Kipengele 41 cha Katiba kinamwambia: Umekosea sheria. Mhe. Naibu Spika ukiangalia vile walivyofanya ranking Kipengele cha 3 cha sheria za Kenya kimefanya ranking na kimemaliza eno. Kipengele cha 3 kimetoa
Ahsante Mhe. Naibu Spika. Kwa niaba yangu na kwa niaba ya wananchi wa Taita Taveta nachukua fursa hii kutuma rambirambi kwa jamaa na marafiki wa Mhe. Grace. Nilipata fursa ya kumjua kidogo tu. Siku yetu ya kuapishwa hapa Bungeni nilikuwa nimeketi karibu naye na tuka.
Ahsante mhe. Naibu Spika. Kwanza ningependa kumpongeza mhe. Lay kwa kuileta Bungeni Hoja ambayo tunaizungumzia kwa sababu ya kufikiria sana kuhusu lugha yetu tukufu ya Kiswahili. Nimesimama kuunga mkono Hoja hii kwa sababu ya Kipengele cha 7 cha Katiba ambacho kinasema: - "(1) Lugha ya taifa ya Jamhuri ni Kiswahili. (2) Lugha rasmi za Jamhuri ni Kiswahili na Kiingereza. (3) Serikali- (a) itazikuza na kuzilinda lugha tofauti za wanainchi wa Kenya; na (b) italinda na kustawisha matumizi ya lugha za kiasili lugha ishara ya Kenya breli na njia nyingine za mawasiliano na teknologia zinazoweza kufikiwa na watu wenye ulemavu." mhe Naibu Spika ukiviangalia hivi vipengele katika Katiba yetu utaona kwamba sisi kama Wakenya tumekubali kwamba lugha ya Kiswahili ndiyo lugha ya kitaifa. Hiyo ni kumaanisha kwamba lugha hii ina maana zaidi kushinda hata lugha ya Kiingereza ambayo imetujia sisi kutokana na historia yetu - tulikuwa koloni la Uingereza. Jambo la kushangaza ni kwamba lugha ya Kiswahili bado haijatiliwa maanani kama inavyopaswa. Ndiposa namshukuru mhe Lay kwa kufikiria jinsi hii. Tukianzia hapa kwetu Bungeni kanuni za Bunge haziko katika lugha ya Kiswahili. Kamati ya Kanuni Itifaki na Mienendo ya Bunge inafaa kuangazia umuhimu wa kutafiwa kwa kanuni za Bunge kwa lugha ya Kiswahili. Mhe Lay amethibitisha kwamba unapotunga Hoja na Miswada kwa madhumuni ya kuileta Bungeni ni lazima uandike kwa lugha ya Kiingereza. Hilo ni jambo la kufedheesha. Mimi mwenyewe nimejaribu kubuni Hoja kwa lugha ya Kiswahili lakini maafisa wa Bunge wanaopaswa kutusaidia kufanya hivyo hawaielewi lugha ya Kiswahili. Hili ni jambo ambalo tunapaswa kuliangazia ili tuweze kuwa na wafai ambao wanaweza kutusaidia sisi Wabunge kujieleza rasmi katika Bunge hili. Jambo lingine la kushangaza ni kwamba hata nakala ya Katiba ambayo nimetumia niliponukuu Kipengee cha 7 ni nakala rasimu; siyo ile ambayo tayari imefaiwa rasmi kama Katiba ya nchi hii. Hii ni kumaanisha kwamba tangu tulipopitisha Katiba hii mwaka wa 2010 hakuna juhudi zozote zilizofanywa na Serikali kuhakikisha kwamba Wakenya wanaweza kupata katiba hii rasmi katika lugha ya kitaifa. Ni fedheha iliyoje? Kiswahili ni lugha ambayo ina mashiko makuu sana katika historia ya Kenya. Kiswahili ni lugha ya kiafrika. Wengi watakubaliana nami kwamba Kiswahili kimetiririka kutoka kwa lugha za kiafrika. Ukitembea katika nchi nyingi za kiafrika utapata eno mengi ambayo yanawiana na lugha yetu ya Kiswahili. Kwa mfano lugha ya Kizulu kule Afrika Kusini lugha za kizambia kule Zambia na hata humu nchini zinawiana na Kiswahili. Mimi mwenyewe nikiiangazia lugha yangu asilia kuna eno mengi sana ambayo yanawiana na Kiswahili. Sembuse kusema kwamba jina "Swahili" limetokana na jina la kiarabu 'sawahil' - watu ambao wanaishi katika ufuo wa bahari. Jambo muhimu ni kwamba ukiitizama lugha hii utaona kwamba haina watu ambao unaweza kusema haswa ndio watu ambao wanaweza kuienzi kama lugha zingine za Kikuyu Kiluo Kiluhya na kadhalika. Kwa hivyo ni lugha ambayo inaweza kutujumuisha sisi kama Wakenya bila ya watu wengine kuhisi kwamba wao kwa sababu ya lugha hii wako sawa zaidi kuliko watu wengine. Ukiangazia changamoto ambayo sisi kama Wakenya na pengine watu ambao wametumia lugha za kigeni kama lugha zao za kitaifa ni kwamba kunakua na kukanganya kidogo wakati dhana zako ziko katika lugha ile halafu wewe mwenyewe unajieleza katika lugha yako ya Kiswahili. Mara nyingi watu wanakataa kuzungumza Kiswahili hususa kwa sababu za kilahaja. Hakuna shule yoyote ambako watu hufundishwa lahaja ama lafudhi. Ni muhimu Wakenya tuelewe kwamba jinsi unavyoizungumza lugha ya Kiswahili haijalishi; hata kama umeathiriwa na lugha yako ya asili. Mhe Naibu Spika lahaja ya Kiswahili tunayotumia ni ya kizanzibari. Kuna lahaja nyingine za Kiswahili kama vile Kimvita Kimtang'ata Kipemba na kadhalika. Hata kule pwani lugha ya Kiswahili ambayo inazungumzwa kule Mombasa ni tofauti sana na lahaja ya Kiamu ambayo inatumika kule Lamu. Kwa hivyo hii njia ni ya kuweza kusema kwamba watu hawawezi kujieleza kwa lugha ya Kiswahili kwa sababu katika kufundisha lugha hii kule shule kuna mtazamo wa kuisanifisha lugha - mtazamo ambao unawafanya watu kuhisi kwamba hawawezi kuizungumzia lugha hii kwa misamiati. Kwa hivyo wanaogopa. Lakini la hasha! Ninaikataa dhana hiyo. Mara nyingi sisi kama wanasiasa tunapoenda mashinani tusiwe tukizungumzia wananchi wetu kwa Kiingereza. Mara nyingi tunazungumza kwa lugha ya Kiswahili. Kiwe Kiswahili sambamba ama Kiswahili kombokombo la muhimu ni kwamba Wakenya wengi wanaweza kutuelewa vilivyo wakati tunazungumza katika lugha ya Kiswahili. Mhe. Naibu Spika hili ni jambo ambalo kama tunaweza kuitumia lugha hii tunaweza kuzifungua fikra na dhana za watu wengi. Watu wengi hawawezi kuzungumza kwa lugha ya Kiingereza kwa ufasaha. Kwa hivyo wanaogopa kujieleza kwa lugha ya Kiingereza. Wanaonekana kama ni wajinga ilhali ukiwasikiza katika lugha za mama na katika Kiswahili wana Hoja nzuri na wanaweza kuchangia katika maendeleo hususan ukiangazia kwamba watu wetu wengi hawajasoma vilivyo na ni wa kipato cha chini na hawajaweza kuwa na ule upana wa kujua vile mambo yanaweza kuendeshwa katika nyanja tofauti tofauti.
Ahsante Mhe. Naibu Spika. Nachukua fursa hii kutuma rambirambi zangu kwa jamaa na marafiki wa Mhe. Grace. Nilifanya kazi naye katika kamati ya uchukuzi. Najua ni kiongozi anayepaswa kuigwa. Kifo kitakwenda na kila mmoja wetu. Tenda wema kabla hujakufa. Ahsante.
Ahsante mhe. Naibu Spika. Nasimama kuunga mkono hoja hii. Hali ya kumudu uchafu nchini si sawa. Hii ni kwa sababu wale waliopatiwa hayo majukumu wamezembea. Sehemu hii ya Dandora ina uchafu mwingi. Mimi nimewahi
Ahsante mhe. Naibu Spika. Naunga mkono haya mambo ya miraa . Hii kamati sharti ichunguze miraa ina sections ngapi. Hii ni kwa sababu kuna ile inaitwa kangeta muguka giza na kadhalika. Hii ambayo inaitwa kata ndiyo inakata wanaume. Tungependa tujue gani kati ya hizo ndiyo mbaya. Miraa ni kama ngombe kwa Wameru kwa sababu wanaitumia kusomesha watoto wao. Sharti tujue gani mbaya na gani nzuri. Miraa sasa inatumika na Wakenya wote. Watoto wote wanakula hii miraa . Kamati itupatie habari kamili.
Ahsante Mhe. Naibu Spika. Ningependa kuchukua fursa hii kukushukuru kwa kunipatia nafasi hii niweze kuichangia Hoja hii. Vile vile ningependa kumshukuru mhe. John Mbadi kwa kuileta Bungeni Hoja hii muhimu sana inayotuhusu sana sisi watu wa Pwani. Masikitiko makubwa ni kwamba sekta ya uvuvi katika eneo la Pwani imedharauliwa sana na Serikali kwa sababu tunazoshindwa kuzielewa. Hivi sasa ukienda kuulizia katika afisi za uvuvi utapata kwamba licha ya kwamba Pwani ni eneo kubwa sana la uvuvi kwa sababu ya Bahari Hindi kiasi cha samaki wanaopatikana ni kidogo sana ukilinganisha na kiasi cha samaki wanaopatikana katika Ziwa Victoria na kwingineko. Kusema kweli hili ni jambo la kushangaza sana. Tukiangazia zaidi watu wanaofanya kazi hii katika maeneo ya Lamu na kwengineko na haswa tukiangazia suala la vifaa vya kuhifadhia samaki kama lilivyozungumziwa; huwezi kuvipata vifaa hivyo katika sehemu hiyo. Vifaa hivyo vikiweko vitawasaidia wavuvi kuendeleza kazi hiyo kwa njia bora zaidi. Mhe. Naibu Spika maskitiko makubwa ni kwamba tatizo kubwa linaloikabili jamii ya wavuvi katika maeneo ya Lamu na sehemu nyingine za Pwani ni kwamba jamii hiyo haijawahi kusaidiwa ili iweze kujiendeleza. Utapata watu kutoka nchi zingine kama vile Indonesia na China wanakuja kuvua samaki katika maeneo ya nchi yetu kwa sababu wako na vifaa vya kisasa yakiwemo maboti mazuri yanayowawezesha kufanya kazi hiyo kwa njia bora zaidi. Wanakuja kuvua samaki katika sehemu ya nchi yetu na kuwapeleka samaki hao kwao kwa faida ya nchi zao na faida zao binafsi. Chombo kinachotumiwa na watu wetu kwa shughuli ya uvuvi hakiwezi kumudu na kuwawezesha wavuvi wafaidike. Ni maskitiko makubwa kwamba ndugu zetu wavuvi wana ujuzi kamili wa kuwawezesha kuifanya kazi hiyo lakini hawajapata usaidizi kikamilifu kutoka kwa Serikali yetu kama walivyosaidiwa Wakenya kwenye sekta ya kilimo na sekta nyinginezo. Hivi sasa samaki wanatoka sehemu ya Lamu na kupelekwa kuuzwa Mombasa. Kuna sehemu inayoitwa Majengo. Huko ndiko wanakouzwa samaki hao
Ahsante Mhe. Naibu Spika. Ningependa kuchukua nafasi hii kurudisha shukrani kwa Waheshimiwa waliopata nafasi kufika kwa mazishi ya magu na wale ambao walinyoosha mikono yao. Mwenyezi Mungu awabariki. Mhe. Naibu Spika ukweli wakati mwingine ni mchungu lakini haina budi usemwe. Zote tulikosea tulipochukua kitengo cha afya na kukiweka kwenye ugatuzi na tukakisambaza kwenye kaunti. Tunapolalamika kwamba madaktari hawako ni muhimu tukumbuke kwamba sio jukumu la Serikali ya Kitaifa kuhakikisha kuwa hospitali zote zina madaktari. Kaunti zimepewa pesa na ni wajibu wao kuhakikisha kwamba madaktari wanalipwa vyema na kuona kwamba kitengo hicho cha afya kinatiliwa maanani vilivyo. Wale ambao walipigania ugatuzi ni kidonda hivi sasa kwa Serikali ya Kitaifa na hawataki kukubali kwamba zote tulikosea. Ukweli usemwe na uongo ujitenge. Ningependa kuwaomba magavana wote wawajibike na kuhakikisha ya kwamba wanawalipa madaktari vyema. Si vyema kaunti zingine zilipe madaktari vizuri na wanaendelea na kazi na wengine wapo nyumbani kwa sababu ya kutolipwa vyema. Wale wanaolipa vizuri wanatoka Kenya ipi na wale ambao hawalipi vizuri wanatoka Kenya ipi? Naunga mkono Hoja hii ya kuahirisha Bunge kwa muda mfupi kwa sababu nitakuwa na nafasi ya kumpokea Rais akiendeleza shughuli zake za maendeleo kwa upanuzi wa barabara kutoka Sabaki kuelekea Marafa na kusambaza maji kwa wananchi. Hilo si jukumu la Serikali ya Kitaifa bali ni kazi ya kaunti. Serikali ya Kitaifa imejitolea mhanga kupitia Rais Uhuru Kenyatta kusambaza maji kwa wananchi. Ningependa kushukuru Serikali na kuwaomba wakaze mshipi na waendelee kusambazia wananchi maendeleo na waache wanaopiga mdomo waendelee.
Ahsante Mhe. Naibu Spika. Unajua lugha ya taifa kwa ndugu yangu Mhe. Wamalwa ni dhaifu sana. Haelewi lakini tutakuwa tukimsaidia kila wakati ili ajaribu kuelewa na awe akikizungumza katika Bunge hili. Ningependa kumuunga mkono ndugu yangu Mhe. Limo. Maswala nyeti ambayo tungependa yazungumziwe katika kikao maalum cha kamukunji ni maswala yanayowahusu wafanyikazi wetu. Wengi wao hawajapata mshahara zaidi ya miezi minane. Kuna maswala tungependa tukae na Parliamentary Service Commission tuwaulize maswali kwa sababu kuna mambo ambayo tungependa watupe majibu. Tuliambiwa wiki iliyopita kwamba tutakutana nao wiki hii. Lakini wiki hii imepita. Ningependa ikiwa inawezekana utoe uamuzi wako kama Naibu Spika tukutane wiki ijayo ama siku fulani - hata kama ni kesho - ili tujaribu kujadili mambo yanayohusu maswala ya matakwa ya wafanyakazi wetu na wale ambao wanatushughulikia ili tuje kufanya mambo hapa. Jambo lingine ni hili. Sisi kama Wabunge tuna jambo ambalo tungependa Kamati ya Bajeti ituambie ilifanya nini. Tuliitisha na kusema tungependa tuwe na kikao maluum cha kamukunji ili watueleze vile walivyofanya mambo yao. Ahsante Naibu Spika.
Ahsante Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii ili nami nichangie Mswada huu. Kwanza ningependa kumpongeza mhe Odhiambo-Mabona kwa kujifikiria yeye mwenyewe na wengine ambao hawana uwezo wa kupata mimba. Hivyo Mswada huu ukiwa sheria utawasaidia wale tasa kupata watoto kwa kutumia njia ya yai kutoka kwa mtu mwingine likichanganywa na mbegu za kiume kisha kuweza kuwekwa katika tumbo lake. Kwa hakika wengi huwa wanagadhabika kwa kutopata watoto hasa akina mama. Kama tunavyofahamu wakati mwingi watu huwa katika hali ya kuwafyolea wale wengine wasiokuwa na uwezo wa kupata watoto. Watoto ni Baraka kutoka kwa Mungu na ndiyo maana wakati wote tuna wachukua watoto kama wasaidizi wetu. Vile vile tunajivunia kwamba wao ndio viongozi wa kesho. Ijapokuwa mara nyingi wengi walio mamlakani husema vijana ndio viongozi wa kesho hiyo kesho huwa haifiki. Hata hivyo ni jambo la busara. Ningehimiza wenzangu waunge mkono zaidi Mswada huu. Utakapofika katika kamati itafaa tuweze kufanya mabadiliko yatakayozidi kuongezea nguvu sheria hii. Kwa hayo machache naunga mkono.
Ahsante Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia Mswada huu ambao ni wa kuzuia watu kuteswa kwa njia ambazo hazifai. Tunajua kwamba miaka ya 1990 Wakenya wangeshikwa na Special Branch na kuhusishwa na mambo ya siasa. Walimu wa vyuo vikuu na wanafunzi pia walishikwa kwa tuhuma za kupindua Serikali. Waliitwa "Mwakenya". Hayo mateso yaliendelea hata katika sehemu zingine. Ndiposa sisi kama Wakenya tunaleta sheria za kuangalia kwamba wale wanaoteswa kwa namna moja ama nyingine wanapata ridhaa. Kwa mfano kule Endebess kuna jamii ambayo ilidhulumiwa miaka ya sabini na theini. Ikiwa unatoka jamii ya Sabaot wanasema wewe ni Mganda. Unashikwa unawekwa kwa gari na unabebwa mpaka Malaba. Wanasema wewe ni mtu wa Uganda na unakosa namna ya kurudi nyumbani. Unaenda unapitishwa kule sehemu za Mbale unarudishwa na wewe ni mtu wa kutoka Endebess. Ndiposa ninaposikia viongozi wengine wakisema kuna jamii ambao siyo Wakenya inapewa vitambulisho inatukumbusha kwamba tunarudi kwa yale mateso jamii ya Sabaot ilipata miaka ya sabini. Waliitwa Waganda na kupelekwa Uganda kwa mateso. Nafikiri kiongozi kama huyo hana kichwa sawasawa. Mateso yanapoingia katika jamii inaendelea kwa vizazi vijavyo. Ni lazima tujaribu kuheshimu uongozi na raia ya Wakenya. Huu Mswada unatupa nafasi ya kuangalia kwamba mtu anapoteswa kwa namna moja ama nyingine na apelekwe hata nchi nyingine tunaweza kupata ridhaa. Huyo mtu anaweza kulipwa kwa njia gani wakati anaporudi hapa. Kwa hivyo mimi niko tayari hii sheria itakapokuwa tayari wale watu wetu ambao waliteswa kwa namna moja au nyingine na kupelekwa sehemu zingine tutakusanya majina yao ili walipwe ridhaa. Tunapoongea mambo ya mateso kuna wale ambao wameteswa sana. Pengine ilikuwa jamii inayoishi sehemu fulani na ikahamishwa kwa lazima. Sisi kule Trans Nzoia katika miaka ya sabini katika sehemu moja ambayo inaitwa Kaptegat na juzi juzi katika sehemu kama Timboroa watu walifurushwa kutoka msituni wakateswa yumba yao yakachomwa na wakapigwa na askari wa Serikali ya wakati huo. Mhe. Spika tutaiangalia kwa makini sheria hii ili tutakapoipitisha tujue wale walioumia miaka iliyopita watafidiwa namna gani. Kwa hayo machache naunga mkono.
Ahsante Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii nichangie Ombi ambalo limeletwa na jirani yangu Mhe. Caleb Amisi. Wakazi wengi wa Matisi ambao wako kando ya barabara wamejenga majumba ya biashara. Hao ni watu wenye biashara ndogo ndogo. KeNHA iliposema kuwa inataka kujenga barabara hiyo kutoka Kitale hadi Endebess mpaka kule Suam ili kutuunganisha na majirani zetu ni vizuri waangalie malalamishi ya wakaazi. Serikali huwa na compulsory acquisition . Sio Matisi tu peke yake lakini ningependa Kamati inapoangalia iangalie barabara hiyo kwa ujumla kwa sababu wako wakazi wa Endebess pia ambao wameathirika na ujenzi wa barabara hiyo. Barabara imepitia huko na hawako kwa orodha ambayo ilitolewa na KeNHA. Kwa hivyo ninaungana na mwenzangu ili tufike mbele ya Kamati hiyo na watu wetu wa Matisi mpaka Endebess ili barabara ijengwe lakini wananchi pia wapate haki yao. Ahsante Mhe Spika.
Ahsante Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii ili nami nitoe maoni yangu kuhusu uteuzi wa Daktari Muraguri. Dunia hii ni duara na rangi rangile. Naomba nikimuunga mkono huyo daktari wakumbuke waliyonitendea wakati tulipewa fedha - Shilingi milioni mia moja katika hospitali ya Wesu Taita. Mhe. Spika wamenizungusha huku na kule wakiniambia nilete orodha ya vifaa na mashine ambazo nahitaji. Niliwakabidhi lakini mpaka leo Dr. Muraguri na wenzake wameshindwa kueleza vile walivyotumia fedha hizo na vifaa walivipeleka wapi. Hayo yalifanyika katika Bunge la Kumi. Ni ombi langu kwa sababu amepewa nafasi ya kuchukua wadhifa wa kuendesha Wizara ya Afya. Kwa yale madhambi aliyonifanyia nimemsamehe. Nafikiri ataanza upya kufanya kazi ninavyomtarajia. Daktari Muraguri amekuja wakati ugatuzi umeingia. Nina ii ataweza kufanya kazi sawasawa. Nina ii ataweza kuangalia madaktari wale ambao wana sifa na ambao wanahitajika kufanya kazi katika sehemu zote za nchi. Wakati huu Daktari Muraguri anachukua nafasi hii ni wazi kuwa kuna matatizo chungu nzima katika Wizara ya Afya. Ni matumaini na matarajio yangu kuwa Daktari Muraguri akishirikiana na Daktari Cleopa watafanya kazi ambayo inahitajika na kuwa hawatawaaibisha watu ambao wamewapatia kazi hii. Kila wakati tunakemea Serikali kuhusu ufisadi. Ukiangalia mara nyingi wagonjwa wameenda mahospitali makubwa wakaambiwa: "Msipotoa mlungula hampati chochote. Usipotoa hiki hutibiwi." Nina ii Daktari Muraguri atachukua nafasi hii kuhakikisha kwamba yale yote yaliyokuwa yakitendeka katika Wizara yamerekebishwa. Naunga mkono.
Ahsante Mhe. Spika kwa kunipatia fursa hii. Naunga mkono Hoja hii iliyoletwa na Mhe. Kimunya Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi hapa Bungeni. Naunga mkono Hoja ya kuhifadhi Miswada. Zaidi ya miaka miwili iliyopita nilipendekeza Mswada unaohusu sukari kwa kimombo unaitwa "Sugar Bill" ambao uliamrisha uende kwa Kamati inayoshughulika na mambo ya kilimo ili iweze kufanya public participation yaani kusikiliza na kuchukua maoni ya wananchi. Mswada huu umekaa kwa Kamati hiyo zaidi ya mwaka moja na nusu. Nilitoa lalama kwako kuwa kamati za Bunge hazifai kuweka Miswada Binafsi iliyoletwa na Waheshimiwa kwa muda mrefu sana mpaka ilazimike ziokolewe na HouseBusiness Committee . Naomba Wenyekiti wenzangu na Wabunge katika kamati za Bunge wawe wakitekeleza wajibu wao muhimu wa kuhakikisha wanajadili na kupitisha Miswada na kuwasilisha ripoti zao Bungeni ili zifanyiwe legislation inayofaa. Kwa hayo machache naunga mkono Hoja hii. Naamini tukirudi baada ya likizo au wakati wowote tutakapoitwa kwa special sitting tutaomba tukubaliwe kuleta hii Miswada iliyokaa siku nyingi. Ahsante.
Ahsante Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii ili niomboloeze na familia ya mwendazake Rais wa Pili Mzee Toroitich arap Moi. Kuna mambo mawili ambayo tumesoma kutokana na hayati mzee. Alikuwa na filosofia ya ai upendo na umoja ambao tunapaswa kama Wakenya kuiga. Ya pili Mzee Moi alituambia kila wakati kwamba siasa mbaya maisha mabaya. Kwa hivyo sisi kama wanasiasa na viongozi ni vizuri tuyaige yale mambo mazuri ambayo tulionyeshwa. Ya mwisho ni kwamba tulikuwa na nyimbo nyingi za kizalendo na tunazikumbuka na kuzienzi. Mhe. Spika kabla hujaingia nyimbo hizo zilikuwa zinaimbwa hapa na Wabunge. Nyimbo hizi zilikuwa zinatuleta pamoja kama Wakenya. Tunapaswa kuziiga hizo nyimbo ili tulete Kenya pamoja. Kwa hayo machache kwa niaba yangu ya familia na watu wa.
Ahsante Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi ya kuchangia. Suala la ardhi ni suala tata sana na ni donda sugu. Limetatiza kaunti nyingi. Inatatiza sana kuona watu ambao wameishi katika ardhi kwa muda wa zaidi ya miaka 200 wakifurushwa. Kwenye ardhi hiyo kuna nyumba na visima. Serikali inakuja na kufanya gazettement bila ya wakazi kujua. Barabara inapitishwa hapo. Kule Lamu watu wamekatiwa mnazi na kufidiwa Kshs3000 ilhali mnazi huo kwa mwaka mmoja unakupatia zaidi ya hizo Kshs3000. Kwingineko kwenye kaunti hiyo hiyo gogo la stima kupitia shambani mwake amelipwa Kshs500000. Kwa hivyo unashangaa ni njia gani zinatumika ndiyo watu wengine walipwe zaidi na watu wengine wanyanyaswe. Ahsante Mhe. Spika.
Ahsante mhe. Spika kwa mwongozo huo. Nilikuwa nikieleza kwamba maafisa wa usalama wanapofika kwenye maeneo kulikofanywa ugaidi badala ya kutafuta ukweli wa mambo ili waweze kuwafuata wahalifu vilivyo wao huwavamia watu wasio na hatia kama vile wakulima na hata watoto wa shule. Ninasema hivi nikizingatia kitendo kilichofanyika Malindi wakati Casino ilipovamiwa. Watoto wa shule katika sehemu za mashambani walivamiwa na maafisa wa polisi wakatandikwa na baadhi yao kukamatwa na kufungiwa korokoroni. Vijana hao waliwekwa korokoroni kwa muda wa siku nane na kuachiliwa bila ya kufunguliwa mashtaka yoyote. Kwa hivyo ninamwomba kiongozi wa chama cha walio wengi Bungeni kulieleza Bunge hili mikakati iliyonayo Serikali kuhakikisha kwamba wananchi wanaweza kutoa habari kwa polisi bila ya kushurutishwa ama kuhangaishwa. Polisi wa sasa wanatarajiwa kuzingatia utendakazi na uadilifu wanapotoa huduma kwa wananchi na siyo kutumia nguvu na kuwahangaisha wananchi kama walivyokuwa wakifanya polisi hapo zai. Ahsante Bw. Spika.
Ahsante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kuchangia Hoja hii. Kabla sijaendelea ningependa kukupongeza kwa kupewa kiti ambacho ni muhimu. Hiki ni kiti ambacho kinasimamia kila mtu. Tunajua tutaendelea vizuri tukiwa na wewe. Tunaongea kuhusu Hoja ya maji katika shule za msingi. Katika eneo bunge langu kupata maji ni shida. Kuna Shule ya Msingi ya Mwiki ambayo iko na watoto 3000. Ningependa Wabunge wa eneo hilo na marafiki wangu waje waone shule ambayo iko na watoto wengi zaidi katika nchi yetu ya Kenya. Maji yakikosekana katika Shule ya Msingi ya Mwiki sisi huomba watoto wetu warudi nyumbani. Ninashukuru kwa sababu wakati Rais wa Jamhuri ya Kenya alitembelea Kaunti ya Kiambu alituelezea kwamba tutapata maji. Katika eneo bunge langu kuna soko ambalo sisi sote hununua vyakula ambavyo hupikwa nyumbani mwetu. Tumejenga vyoo na bafu. Tulijenga bafu kwa sababu watu wakitoka kuchukua vyakula vyao vya kutuuzia kutoka mashamba badala ya kwenda nyumbani wanatumia bafu hizo kuoga ndio waende kazini. Kama hakuna maji sokoni inakuwa shida kwa sababu inabidi mtu apeleke bidhaa sokoni halafu arundi nyumbani kuoga na kwa hivyo anapoteza wakati. Kwa sababu hii mimi ninaunga mkono Hoja hii. Ninajua mambo mengi ya maji yako katika serikali za ugatuzi. Tukishikana mikono kama viongozi tutasaidia watoto wetu shuleni na watu wengi masokoni na kwingineko ndio tuweze kusaidiana katika kuleta usafi humu nchi. Ahsante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia hii nafasi.
Ahsante Mhe. Spika wa Muda. Kwanza ninataka kumshukuru ndugu yangu Mheshimiwa aliyeleta Hoja hii hapa. Tunafahamu vyema kwamba wazee wetu ni watu ambao wanahitaji kuzingatiwa sana. Hii ni kwa sababu hatungefika hapa leo au hatungefikisha umri huu bila wazee wetu. Hata sisi tutakuwa wazee. Hoja hii inafuatana na Katiba yetu ambayo tuliipitisha kwa kusema kwamba tutawasimamia na kuwasaidia wazee. Jambo hili liko katika Kipengee cha 57 cha Katiba ya Kenya. Kipengee hiki kinasema: The State shall take measures to ensure the rights of older persons. Kipengee cha 57(d) kinasema: to receive reasonable care and assistance from their family and the State. Mheshimiwa ameelezea usaidizi ambao wazee wetu wanaweza kupata. Moja ni kuwa wazee wa umri wa miaka 60 na zaidi wahudumiwe katika hospitali zetu bila malipo yoyote. Hii ni kwa sababu mzee ataenda hospitalini aambiwe alipe shilingi mia mbili na hajui atoe hizo pesa wapi. Ningeomba tulizingatie suala hili sana. Vile vile zile Kshs.4000 ambazo Serikali inawapatia wazee itakuwa vyema kama tutahakikisha kwamba zinamfikia kila mzee popote alipo. Hii ni kwa sababu
Ahsante Mhe. Spika. Kwa niaba yangu na wakaazi wa eneo Bunge la Rabai natoa rambirambi kwa familia na marafiki wa Mstahiki Gavana Gakuru. Tunatoa rambirambi pia kwa wakaazi wa Nyeri. Tunajua kwamba ni wakati mgumu kwa sababu ni miezi minane tu iliyopita mliachwa na Gavana mliokuwa mmechagua na sasa imetokea tena. Letu ni kufanya maombi pamoja nanyi. Msimame na mungu. Tuna ii kwamba mungu atawapatia nguvu wote ambao wamesumbuka. Pia nataka niungane na wenzangu kuwaambia wale wahusika wa mabarabara... Tumeambiwa hapa kwamba katika sehemu ya Makenzi Salgaa na hata kule Bonje katika Rabai ajali zinatokea kila wakati. Ombi langu kwa shirika husika la Kenya National Highways Authority (KeNHA) ni kwamba wahakikishe kwamba hatungoji maisha yamalizike kila wakati mahali pale. Kama barabara ile haiko sawa basi shirika hili la KeNHA lifanye kazi yake ili tusiwe tunashuhudia tu ajali. Ikisemekana mahali ni black spot shirika la Kenya National Highways Authority (KeNHA) linatakikana lituambie mikakati linalofanya ili maisha yasiendelee kupotea hapo. Kwa yote hayo letu ni kumuombea mstahiki gavana kwamba Mungu aipokee roho yake peponi na wote ambao wameachwa pia Mungu awe nao na akawafariji. Asante Mhe. Spika.
Ahsante Mhe. Spika. Kwa niaba yangu na ya watu wa Taita Taveta tunatoa pole zetu kwa familia ya aliyekuwa Rais wetu wa pili Rais Daniel Toroitich arap Moi. Tunamshukuru kwa kuongoza kwa ai upendo na umoja. Tunamshukuru pia kwa shule nyingi ambazo alijenga Kenya nzima. Tunafurahia sana kwa kuwa alisimama na elimu haswa elimu ya watoto wa kike. Tunatoa pole zetu kutoka Taita Taveta kwa familia na Kenya yote nzima. Ahsante Mhe. Spika.
Ahsante Mhe. Spika. Kwanza ningependa kuchukua nafasi hii kabla ya kuunga mkono Hoja hii kuwatakia Waheshimiwa wote mwaka mpya mwema na wenye mafanikio. Ninaunga mkono Hoja hii kwa sababu unapoandaliwa chakula si lazima ule chakula hicho chote kama kimekuzidi. Kwa hivyo si lazima utumie wakati wote mwingi ambao umepewa. Unaweza kutumia dakika moja kusema hoja zako na uachie wakati mwingine watu wengine. Hivyo ilivyo inastahili kabisa kwa sababu mwenye kuwasilisha Hoja anahitaji wakati wa kutosha ili aweze kujieleza na aweze kueleweka ndipo wengine wapate fursa ya kumuunga mkono au kumpinga baada ya kuelewa Hoja hiyo. Kwa hayo machache ninaunga mkono Hoja hii vile ilivyo bila mabadiliko.
Ahsante Mhe. Spika. Nachukua nafasi hii ya kutoa rambirambi kama Mjumbe wa Bahati kwa niaba ya watu wa eneo Bunge la Bahati pamoja na familia yangu kusema pole kwa familia. Yangu ni machache. Kama kuna mtu anayemjua Rais mstaafu aliyetuacha ni mimi Mhe. Kii Ngunjiri. Nilikuwa Mwenyekiti wake wa chama cha KANU kwa miaka kumi. Kwa hivyo nilimjua kwa undani. Ninajua uzuri wake kwa sababu alikuwa mzee wa heshima na alijua kuwasaidia maskini na kuunganisha watu wote. Alikuwa na msimamo. Ikiwa mtakumbuka yeye ndiye rais wa pekee aliyemaliza siasa na chama alichochaguliwa nacho bila kubadilisha na kujiunga na chama kingine. Pengine kwenda kwake kutakuza.
Ahsante Mhe. Spika. Naomba kuunga mkono Hoja hii ya mabadaliko ya Wabunge katika nyadhifa mbalimbali za kamati. Kama unavyoelewa imebidi mara nyingine tuje mbele ya Bunge tuombe kibali cha kupatia Wabunge kamati mbalimbali kulingana na uzito wa kazi vile ulivyo. Kama tunavyoona tuko na Mhe. Opiyo Wandayi ambaye kama mnavyojua kuna wakati alikuwa na tatizo. Kwa hivyo tunamrudisha maana tulikuwa tumekwishapeana nafasi katika kamati mbalimbali. Imebidi basi tufanye mabadiliko na ukarabati ili angalau nafasi zipatikane ndiposa kila moja apate nafasi yake. Tumejadiliana na ikatubidi tufanye mageuzo yanayowahusu wenzetu katika kamati mbalimbali ili wapate kupelekwa kufanya kazi katika kamati nyingine. Wapo wengine walioomba ruhusa wabadilishiwe kamati kwa sababu labda kazi zimewazidi ama wangependa wapate kuelewa zaidi kazi katika kamati nyingine. Kwa hivyo imebidi tufanye mageuzo haya na ni ombi langu kwenu Wabunge wenzangu mwapatie kibali ili wapate nafasi ya kuhudumu katika kamati hizi. Iwapo itabidi tutarudi hapa Bungeni tena kuleta mageuzo mengine ili kila Mbunge apate nafasi ya kuchangia kikamilifu katika shughuli za Bunge. Naunga mkono.
Ahsante Mhe. Spika. Naomba kuunga mkono Kamati hii ya Uteuzi vile ilivyosomwa na mwenzangu ili ikaanze kufanya kazi yake haraka iwezekanavyo. Uteuzi wa Kamati hizi saa zingine unachangamoto zake. Ni ombi langu kwa Waheshimiwa wahakikishe wamebainisha ni akina nani wanaweza kuwa kwa Kamati hizi. Mara nyingi inabidi uangalie vile utakavyosambaza wenzako katika Kamati mbalimbali. Kamati ya Ratiba za Bunge ilionelea haya majina yaletwe mbele ya Bunge hili ili Wabunge wafikirie na kuyaweka maanani ili yaidhinishwe na uteuzi huu uweze kufanya kazi. Kwa hayo machache Mhe. Spika naomba kuunga mkono uteuzi wa Kamati hii.
Ahsante Mhe. Spika. Naomba nami nichukue nafasi hii kupeana rambirambi zangu kwa familia ya kaka yetu ndugu yetu mpendwa Prof. Ali Mazrui. Wengi wetu tulimfahamu Prof. Ali Mazrui tukiwa chuoni kama wanafunzi wakati alikuja kupeana mijadala kadha wa kadha ijapokua wakati huo ilikua vigumu sana kwa mtu msomi mwenye fikira tofauti na za uongozi kukubaliwa kuendelea kupeana mijadaala. Ilibidi mara nyingi Prof. Ali Mazrui awe nje ya nchi kwa kueneza na kufunza watu ambao walikua wanahitaji elimu yake na ufasaha wake. Tutakubali kuwa Prof. Ali Mazrui alikua amesifika. Alikua ana sifa za hali ya juu. Prof. Mazrui alikua ametukuzwa na watu kwa ule ufasaha wake na vile alivyo kuwa anawajibika katika shughuli zake za kila siku. Prof. Ali Mazrui alikua ametamba katika shughuli za elimu. Nani angeweza kutamba mbele ya Prof. Ali Mazrui kwa kisomo alichokua nacho? Baada ya kutamba kimasomo alikua ameheshimika kwa sababu ya maadili yake. Ufisadi kama wenzangu walivyotangulia kusema ulikuwa si mmoja wa ngao zake katika maisha. Mara nyingi alikosana na wengi kwa sababu ya kuzungumza kwa undani kuhusu ufisadi. Aliwakemea wote ambao walikua wanajaribu kuendesha ufisadi. Tutakubaliana kuwa kifo cha Prof. Ali Mazrui kimepokonya nchi hii na ulimwengu mzima na wasomi wote kwa ujumla Mwanakenya shupavu; shujaa. Nina ii atawekwa katika kumbukumbu zetu nchini kuwa mmoja wa watu wa Kenya ambao wamejibidisha iwezekanavyo katika mrengo wa elimu. La mwisho naomba wenzetu ambao pia nao wamesoma wajaribu wawezavyo kuiga mfano wa Prof. Ali Mazrui. Si mtu ambaye alikuwa anataka kujilimbikiza mali ya ulimwengu. Sote tunajua tunaiacha bali aliishi kama mtu mnyenyekevu mpole mwenye hekima na busara na mstaarabu. Yote haya ni maadili ambayo yalikua na Prof. Ali Mazrui. Kwa hayo machache naomba kutoa pole zangu kwa familia na nchi nzima kwa ujumla. Ahsante Mhe. Spika.
Ahsante Mhe. Spika. Naomba niunge mwenzangu mkono. Jambo la kwanza ningependa kuwatakia Wabunge wote wakati mwema kwa kikao hiki na kuwatakia mema wakati huu wote tutakapokuwa tukizungumza ama kujadiliana Bungeni. Mhe. Spika naomba niunge Hoja hii mkono kwani Kamati hii ya Bunge ni kamati muhimu inayotoa mipangilio yote ya Bunge na kuhakikisha kuwa shughuli za Bunge zinaendelezwa vilivyo. Ukiangalia orodha hii tumeangalia kwa utaratibu tuone kama kuna wengine ambao hawashughuliki sana na shughuli za Bunge na wengine wakaamua kuwa hawangependelea kuendelea katika hivi vikao kwa sababu kila siku ya June wakati shughuli za Bunge zimemalizika lazima Kamati hii iende ikutane na ijadiliane. Unakuta wakati mwingine wanakamati wengine ambao wako katika orodha hii ama walikua katika orodha ya awali hawakuwa wakishughulika na mambo ya Kamati. Hapo ndipo ilipobainika wazi kuwa itakua ni jambo la busara kwa haya majina yabadilishwe. Hii ndio maana mwenzangu katika Hoja yake katika utangulizi wake ameomba kuwa mabadiliko yawepo na tunaomba na kuwasihi Wabunge wenzangu wakubali hayo mabadiliko na orodha hii ambayo tumepeana iwe ndio tutakayokubalia iwe orodha ambayo itakuwa katika Kamati hii ambayo inashughulika sana na mambo ya Bunge. Mhe. Spika nikimalizia la muhimu ni kuwa Wabunge waelewe kuwa bado kuna kamati zingine ambazo lazima zifanyiwe marekebisho kama itahitajika. Ni muhimu kuwa wakati huu tuangazie umuhimu wa kamati za Bunge. Kuna Wabunge ambao sitawataja majina hapa ambao wamepewa nafasi za kuhudumu katika kamati na hawajahudhuria mkutano hata mmoja.
Ahsante Mhe. Spika. Nasimama kuunga mkono Ripoti iliyo mbele yetu ya kuwachagua Makamishina Bi. Kagwiria Mbogori kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu pamoja na wenzake. Pia naunga mkono kukataliwa kwa Bw. Lempaa. Kwa hakika tuna matarajio kwamba Tume hii itafanya kazi yake vyema. Nimepitia Ripoti hii na nikaona kwamba baadhi ya wahusika hawa wamefanya kazi nzuri sana hasa kwa kuzingatia dhuluma za kihistoria. Hivi tunavyozungumza natoka kwa Kamati ambayo imeweza kufuatilia Ripoti ya NEMA lakini ni dhuluma tupu ambayo imeendelea pale ndani. Mashamba ambayo kwa hakika yanastahili kuwa ya wenyeji yamechukuliwa na hivi sasa badala ya kuwachiliwa kwa kilimo yanatumika kupanda miti ilhali wawekezaji hawakuyaitisha mashamba hayo kwa kupanda miti. Waliyaitisha kwa kutengeneza chumvi. Watu wamepigwa risasi katika maeneo hayo wakitetea haki zao. Basi ni matumaini kwamba Tume hii itaweza kuangazia hasa Ripoti ambayo imeandikwa na Tume iliyotangulia kulingana na mashamba yale ya chumvi na mapendekezo yake yatekelezwe kikamilifu ili watu wa eneo lile la Marereni Kanagoni na Msumarini waweze kupata mashamba yao. Mhe. Spika naunga mkono Hoja iliyo mbele yetu ili walio mbele yetu wakaweze kuhudumu katika Tume hiyo. Asante.
Ahsante Mhe. Spika. Nilipokuwa nikija Bunge siku ya leo nilikuwa nimejitayarisha kuipinga Hoja hii kwa sababu hivi majuzi tuliletewa majina ya watu ili tuyakubali au tuyakatae lakini tuliyakubali. Hayo yalikuwa majina ya walioteuliwa katika Tume ya Huduma ya Walimu. Siku ya leo nilipoangalia Ripoti ambayo Kamati imetuletea niliona kuwa Serikali imeleta jina la mtu ambaye amestaafu. Sisi wenyewe na hata Rais wetu na Naibu wake tumekuwa tukiongea juu ya ukosefu wa kazi katika nchi hii. Zaidi ya asilimia 70 ya wale ambao wamekosa kazi ni vijana wetu. Kila wakati tunapoletewa majina ya watu ambao wamepatiwa kazi ni watu ambao wamestaafu - wenye wamezidisha miaka 55 au 60. Nilipoongea na Mwenyekiti wa Kamati hii niliambiwa kuwa wale ambao wamekuwa mabalozi katika Somalia miaka kadhaa iliyopita wamekuwa wamekatalia hapa Nairobi kwa sababu ya kuogopa ukosefu wa usalama katika Mogadishu na nchi ya Somalia. Kwa sababu huyu Generali amekubali kuenda kutuwakilisha katika nchi ya Somalia kukaa huko badala ya kukaa katika Jumba la National Social Security Fund (NSSF) hapa Nairobi nitaunga mkono uteuzi huu. Tuko na shida sana katika nchi hii. Ningependa kumwambia Rais wetu Naibu wake na Tume zote ambazo zitaleta majina ya watu ambao wameteuliwa ili wapitishwa na Bunge hili kuwa tutapiga kampeni katika Bunge hili ikiwa watu hao hawatakuwa na miaka ya chini kidogo. Iwapo watu ambao watakuwa wakichaguliwa hivi karibuni hawatakua watu wenye umri mdogo kukiletwa watu ambao wamestaafu kama Bunge tunafaa kukataa. Sisemi kwamba watu ambao wamestaafu ni wabaya lakini ni lazima tuzingatie maslahi ya wafanyikazi wa nchi hii. Katika nchi hii kuna vijana ambao wamehitimu. Kupitia Hoja ambayo ilikuwa hapa tuliongezea muda Kamati ya Haki na Masuala ya Sheria ikamkague mtu ambaye ameteuliwa kujiunga na JSC. Iwapo watatuletea watu ambao wamestaafu nawaomba waheshimiwa tukatae. Jambo lingine ambalo ningependa kulitaja ni kwamba Kaunti yangu ya Nyandarua imesahaulika kabisa katika mambo ya uteuzi. Sisi hatuna mtu ambaye ameteuliwa kuwa Balozi ama Waziri. Pia miongoni mwa Makatibu kwenye Wizara za Serikali hakuna hata mmoja kutoka Kaunti ya Nyandarua ingawaje kuna wanaojihusisha tu na Kaunti hiyo. Kwa hivyo ninamuomba Rais; anapoteua wafanyikazi wengine wakuu wa Serikali aikumbuke Kaunti ya Nyandarua. Mhe. Spika kuna shida kubwa kwenye mpaka wa nchi hii na Somalia. Kuna watu wanaofikiria kwamba magaidi wa Al Shabaab wanatushambulia kwa sababu tulipeleka majeshi yetu kule Somalia. Uhalifu unaofanyika katika Kaunti za dera Garissa na Wajir umekusudiwa kuwafukuza wafanyikazi wa Serikali ambao wanazuia kuingizwa kwa bidhaa haramu humu nchini. Nilipokua kwenye Bodi ya KRA tulijua kwamba ukosefu wa usalama katika mipaka yetu ulikuwa unasababishwa na watu wanaoingiza bidhaa haramu humu nchini. Lengo lao ni kuhakikisha kwamba hakuna maafisa wa polisi ama maafisa wa KRA ama maafisa wa Idara ya Uhamiaji kwenye miji ya mipakani. Kama kuna biashara ambayo inailetea Kenya hasara ni ile ya kuingiza bidha humu nchini kupitia Somalia. Wengi miongoni mwetu hatutaki kuamini kwamba wanajeshi wetu walioko Somalia wanafanya biashara hiyo. Hatutaki kuamini kwamba hilo ndilo linalofanyika. Tunawaomba marafiki zetu wanaotoka kwenye kaunti hizo tushirikiane tuweze kuisaidia Serikali. Wafanyi biashara kutoka kaunti hizo wakishirikiana na wengine ambao wako hapa Nairobi wanafadhili makundi yanayohusika kwenye uhalifu unaochangia kutokuwepo kwa usalama. Ukiona Serikali imefikia kiwango cha kusema itajenga ukuta kati ya Kenya na Somali - jambo ambalo halistahili kufanyika kabisa - ni kwa sababu ya huo ukora. Mhe. Spika kwa sababu Gen. Tumbo ambaye ameteuliwa na Rais amekubali kwenda Mogadishu nitaiunga mkono Hoja hii. Lakini iwapo uteuzi wa baadaye hautazingatia sehemu zote za Kenya na haswa Kaunti ya Nyandarua kukumbukwa nitakuwa miongoni mwa Wabunge ambao wataupinga eteuzi huo. Kwa hayo machache naunga mkono Hoja hii.
Ahsante Mhe. Spika. Nimeshukuru kwa jawabu lililotoka kutoka kwa Mwenyekiti wa Ardhi. Lakini niko na maoni kwa baadhi ya majibu. Jibu la kwanza (b). Serikali ibadilishe vyeti vya wale watu walio kodisha Arthi kwa muda murefu na hawaitumii na haswaa katika maeneo ya makaazi. Jawabu la pili serikali iharakishe utoaji wa vyeti vya umiliki unaoendelea pwani. Jibu la tatu serikali imetoa hakikisho ya kuto furusha watu kwenye ardhi ya serikali. Pia imetoa hakikisho ya kwamba wako mbioni kubuni sheria na mwongozo wa ufurushaji na utatuzi wa mizozo kama hiyo. Je ni lini muongozo huu utakua tayari?
Ahsante Mhe. Spika. Ninamatatizo mawili na tetesi iloyoletwa mbele yako na Mhe. Mwadime. Kwanza inafaa ibainike na Wakenya kwamba asilimia 90 ya mbuga za wanyamapori ziko katika sehemu za wafugaji. Pili kuna sheria katika Kenya ambayo inasema ukipatikana ndani ya mbuga ya wanyamapori utatozwa faini au ufungwe jela kwa muda fulani. Sasa kama sheria hiyo tayari inatekelezwa tetesi hii itatatua nini leo? Kazi anayotaka kufanya Mhe.Mwadime imefanywa kupitia sheria hiyo. Hata ukipatikana ndani ya mbuga ya wanyamapori utashtakiwa kisha utozwe faini ama ufungwe gerezani. Kuna sheria tayari. Ni nini mpya Mhe. Mwadime anatuambia katika hii Petition ? Pili sehemu nyingi za national parks ziko katika sehemu ya wafugaji. Inafaa tutafute njia mwafaka kama hiyo sheria haitoshi kutatua matatizo hayo. Hii Petition haileti mambo mapya kwa hili Bunge leo. Ahsante Mhe. Spika.
Ahsante Mhe. Spika. Ninaona Mwenyekiti ana wasiwasi. Nilikuwa nikitafuta tafi ya Kiswahili ya Ripoti hii lakini ninashukuru imeandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Nitachukua nafasi hii kuwatafia wale ambao labda lugha ya kimombo inawaletea shida. Tumeisoma na kuielewa Ripoti hii. Ninaomba nichukue nafasi hii kuwapongeza Wanachama wa Kamati husika. Hii inaonyesha wazi kwamba ukichukua fimbo na kuwachapa watu fulani wanaamka. Tulipomwambia Mwenyekiti hapa kwamba wanazembea katika kazi yao walifanya bidii na kuhakikisha kwamba ripoti hizi zimeletwa Bungeni na hivi sasa zinashughulikiwa. Ninaomba ripoti kama hizi zinapofika Bungeni na kujadiliwa Kamati Tekelezi - ambayo inahitajika kutekeleza maamuzi ya Bunge - iyatekeleze maamuzi hayo. Sioni maamuzi ya Bunge yakitekelezwa. Ninasema hivi kwa sababu niko na ushahidi kuhusu ripoti nyingi ambazo zimepitishwa na Bunge hili lakini mpaka sasa hakuna pendekezo lolote ambalo limetekelezwa. Kamati ambayo inahusika na masuala ya sukari imetueleza na kufafanua jinsi hali ilivyo duni katika sekta ya sukari humu nchini. Tunasubiri tuone iwapo Kamati Tekelezi itafuata maagizo ya Bunge ambayo yameandaliwa na kila mtu ameyasoma na kuyatilia maanani ili tuyafuatilie. La muhimu ni kwamba sukari inatumika kwa njia ya kawaida na takriban watu wote humu nchini. Tukiwa na upungufu wa sukari utasikia kelele kutoka pembe zote za nchini hii. Tukiwa na mapendekezo yanayoweza kuiboresha sekta ya sukari nchini ni bora kuyatoa. Inastaajabisha kwamba hata fedha zikitengewa shughuli ya kuboresha viwanda vya sukari punde tu zinapowasili kwenye kampuni husika pesa hizo hupotea. Kampuni ambayo ilikuwa maarufu wakati nilipokuwa chuoni na wakati nilipoanza kufanya kazi ni kampuni ya Sukari ya Mumias. Kampuni hiyo ilikuwa imebobea enzi hizo; kila mtu alikuwa akiisifu. Hivi leo kila mtu anastaajabu ni kitu gani kimetokea katika kampuni hiyo ndiyo ikajikuta katika hali yake ya hivi sasa. Sababu ni ufisadi na wizi ama ni utendakazi duni? Sababu ni sukari yenye bei rahisi inayoingizwa nchini? Wakati umefika wa kujiuliza ni lini tutahakikisha kwamba viwanda vya sukari ambavyo tumevianzisha humu nchini vimeimarika na kutimiza malengo na matakwa ya wananchi. Mhe. Spika utakumbuka kwamba humu nchini kulikuwa na viwanda vya makonge bixa korosho na nyama miongoni mwa viwanda vingine ambavyo hivi sasa haviko. Kwani nchi yetu ina nini? Aidha tunaanzisha viwanda tukiwa na nia ya kuvipora baadaye ama utendakazi wetu ni hafifu. Wakati umefika wa kujiuliza: "Jai tunaenda wapi Wakenya na ni kitu gani tunachohitaji kufanya ili tuiboreshe hali hii?" Katika sehemu ya magharibi ya nchi wananchi wengi wanategemea sukari katika maisha yao ya kila siku. Wakulima hupanda miwa ambayo wanaitegemea kuwaelimisha watoto wao na kupata ajira zinazowawezesha kulea familia zao. Ni kitu gani kimetokea hivi sasa? Hivi sasa watu wamefadhaika na kukata tamaa. Hawana mbele wala nyuma kwa sababu ya mambo ambayo tumeyaona kwenye Ripoti hii. Ripoti hii imeeleza kwamba kuna ufisadi wa hali ya juu katika sekta ya sukari humu nchini. Kuna masuala ambayo hayajatekelezwa vizuri. Mara nyingi Serikali huleta kampuni kutoka nje kusimamia utendakazi katika viwanda vyetu vya sukari lakini punde wasimamizi wa kampuni hizo wanapowasili humu huangalia na kuona kwamba kuna nafasi ya kujitengenezea fedha. Mhe. Spika kwa sababu tumeisoma Ripoti hii na kuielewa ninaiomba Kamati Tekelezi ya Bunge iyafuatilie mapendekezo yote kwa uangalifu angalau tuweza kugeuza sura ya sekta ya sukari na kuihifadhi. Kwa hayo machache ninaunga mkono Ripoti hii.
Ahsante Mhe. Spika. Ninatumaini sote tumesikia ombi ambalo limetolewa kwa sababu ya mazishi na vile hali ilivyo kwenye familia ya Mheshimiwa Shitanda. Kwa hivyo ni ombi letu kwa Wabunge wenzetu kuwa tukubaliane kuwa viongozi ama vinara wa Bunge wakuandikie barua kwamba kila Mbunge atoe Ksh5000 ili ziweze kusaidia shughuli za mazishi na kusaidia kama kuna lolote la kulipia hospitali ili familia ya Mheshimiwa Shitanda iweze kupata afueni. Mheshimiwa Spika hili ni ombi nzuri. Tunaliunga mkono na bila shaka Wabunge wenzetu watakubaliana nasi kama viongozi tumuandikie Mhe. Spika barua ya kumuwezesha kutoa Ksh5000 kutoka kwa mshahara wa kila Mbunge. Ninatumaini kwamba ombi hilo limekuwa na Wabunge wenzangu.
Ahsante Mhe. Spika. Ningeomba nitumie lugha fasaha ya Kiswahili ili tuweze kufahamikiana. Kabla ya Kenya kuwa na mfumo wa serikali ya vyama vingi na katiba mpya ambayo tunaitumia sasa hivi kulikuwa na kipengele katika sheria ya State Corporations Act. Kipengele hicho cha 5(a) kilikuwa kinampatia ruhusa Rais wa Kenya ya kuwa licha ya masuala yote yaliyoko pale Rais akiweza kupeleka ilani katika gazette notice anaweza kuinua sehemu yoyote katika sheria hii isipokuwa vipengele 17 peke yake. Sasa tuangalie sarakasi ya marekebisho ambayo yanahitajika kufanywa kutumia Mswada huu kumba kwa lugha ya Kiingereza Miscellaneous Amendments Bill . Hii inajaribu kumpatia uwezo na nguvu Waziri. Wakati ule ilikuwa Rais wa Kenya baada ya kuingia Katiba mpya na mfumo mpya wa Kenya inavyoendeshwa Bunge hili hili likaamua kutoa kipengele kile kuwa hakuna yeyote anayeweza kuinua sheria yoyote ya Bunge isipokuwa Bunge lenyewe. Lakini huu Mswada kisawasawa - lau hawana nia mabaya na hakuna nia chafu katika masuala haya - ilikuwa iletwe kwa kupitia Mswada wa maana si Mswada kumba ambayo kuna uwezekano wa watu kutoweza kuona na kujua ni kitu gani kinachoendelea. Bunge hili lilikataa ilhali tunaletewa Mswada ili tukubali ya kuwa Waziri akiamua licha ya mambo yaliyopitishwa Bungeni anaweza kuinua sheria ambayo imewekwa na Bunge hili kwa kalamu yake. Kuna mambo mengine tutayahisi. Ndugu yangu Mhe. Duale anasema kuwa hafahamu lugha yangu lakini ningeomba zile dakika zilizobaki niweze kutoa duku duku langu nisije nikazungumza kwa lugha ambayo pengine ni ya haa nikaambiwa ni saumu. Ni zile hisia za hawa watu wanaojaribu kutuchukua sisi. Ukienda katika maeneo anapotoka Mhe. Duale ni mfano wa kuuziwa mifugo kwa kuonyeshwa wayo wa wale mifugo waliopita. Unaambiwa kwa kuangalia mfugo ule amepita hapa amewanda na ukiangalia zile kato vile alivyoweza kupita pale. Kule kwetu mfano mwingine unaoweza kutumiwa ni kupelekwa katika bahari kisha uone yale mawimbi yanavyopigwa mvuvi aanze kukuuzia samaki akuambie hapa kuna sulisuli kolele papa na nyangumi nitakuuzia kwa kuangalia tu jinsi yale mawimbi yanavyopiga. Ni muhimu sana Kiongozi wa Walio Wengi.
Ahsante Mhe. Spika. Ningeomba tu kuwe na usawa kwa sababu inaonekana unalalia upande mmoja.
Ahsante Mhe. Spika. Ningependa kuchangia hoja hii. Mheshimiwa Chelagat Mutai alikuwa ameheshimika na alikuwa amesoma vizuri. Kazi aliyofanya akiwa Mbunge ilikuwa ya heshima mno. Kama mwanafunzi wa awali wa
Ahsante Mhe. Spika. Ningependa kuchukua nafasi hii kuunga mkono Hoja hii. Ningependa pia kuwatakia Wabunge wenzangu kila la heri muhula huu kwa sababu watakuwa wanakunja jamvi wakijiandaa kwa uchaguzi ambao utafanyika hapo mwakani. Tunakubaliana kwamba Bunge limejaribu kufanya lile ambalo lingeweza kufanya. Nina ii kuwa katika zile kazi ambazo zimebaki Wabunge watajitolea kikamilifu kuhakikisha kuwa wameifuata ratiba yao ambayo tutaizungumzia leo jioni ili waweze kukamilisha. Kama ilivyosemwa na mwenzangu uongozi wa Bunge umeonelea kuwa haina haja kubadilisha viongozi ambao wanahudumu katika Kamati hii inayoshughulikia masuala ya Bunge. Tumeiacha vile vile ili iweze kuwajibika na kumaliza muhula huu ili tuendelee na kazi ambazo tumepatiwa za Bunge. Ninaomba nichukue wakati huu kuwaomba Wabunge wenzangu kuwa tujibidishe tuwezavyo ili tujumuike na wenzetu wakati huu wa kujiandikisha ili wakati wa kupiga kura utakapofika mwezi wa Agosti kila mtu awe amejiandaa vilivyo ili kuhakikisha kuwa amerudi. Lakini ningependa pia kutoa tahadhari. Kulingana na takwimu tulizonazo asilimia 80 ya Wabunge huwa kawaida hawarudi. Kwa hivyo hapa huenda ikawa kuna wengine ambao watakuwa wanakunja jamvi lao na kuondoka Bungeni baada ya muda wao kuisha. Kwa hivyo ni muhimu Wabunge wajiandae kwa vyovyote vitakavyotokea. Wengine wetu kama mimi tushaamua kuwa hatutaki kurudi kwa maana nitaomba kiti cha ugavana. Kwa hivyo ninaagana na wenzangu polepole. Ninawatakia kila la heri katika kazi hii ambayo mtakuwa mnaifanya ili tuweze kujumuisha nchi yetu vile ilivyo. Mhe Spika ninaweka tamati kwa kusema kuwa kulingana na takwimu tulizo nazo Bungeni asilimia 80 ya Wabunge huwa kawaida hawarudi. Kwa hivyo wengine watakuwa wanakunja jamvi lao wakiwa wanaondoka na kuaga Bunge. Mimi ni mmoja wa Wabunge ambao watakuwa wanakunja jamvi lao kama Mbunge wa Wundanyi maana nitakuwa ninaomba kiti cha ugavana katika Kaunti ya Taita Taveta. Kwa hivyo wenzangu ninawaaga polepole wakati huu ambao nimewatumikia. Kwa muhtasari ninawatakia Wabunge kila la heri katika kazi yao. Kwa heshima na taadhima kumbwa ninawaomba Wabunge waunge mkono majina haya ili tuendelee na kazi. Kwa haya mengi ninaomba kuunga mkono majina haya ili yaratibiwe na Bunge na tuendelee na kazi. Asante Mhe. Spika.
Ahsante Mhe. Spika. Ningependa kumwambia Mhe. Cheboi kwamba tuna wachekeshaji kama Churchill na Nyambane humu nchini ambao wanaongea kama "Nyayo". Mugambi anajulikana Tigania East na huwa anapelekwa kwenye sherehe ambako huongea kama "Nyayo" Kibaki Muturi na Raila na watu wanafurahia. Nilimtambulisha kama mtoto wa nyoka kule kwa Mhe. Kiraitu. Alizungumza na watu wakafurahia sana. Alisema kwamba anaweza kumtemea yule anayecheza na Mhe. Kiraitu Murungi mate na afe. Mugambi alikuwa tu anafurahisha watu. Hakukuwa na uchawi wowote. Mhe. Mwiti na Mhe. Cheboi ndio wachawi. Pili mimi ni Mkristo.
Ahsante mhe. Spika. Ningetaka kiongozi wa chama cha walio wengi Bungeni atueleze kinaga ubaga mipango ya Serikali ya kuhakikisha kwamba wananchi wanaweza kutoa habari kwa polisi kwa njia mwafaka na bila ya kushurutishwa. Mara nyingi vitendo vya ugaidi vinapoibuka kwenye maeneo ambako kuna makundi kama vile Mombasa Republican Council (MRC) uhalifu huo husingiziwa MRC mara moja. Hata hivyo huwa hakuna wa kusingiziwa uhalifu unapofanywa na
Ahsante mhe. Spika. Yangu si mengi kwa sababu nimekaa na Njee Muturi kwa miaka mingi na wana-CORD ambao wako katika Bunge hili walimjua mwaka wa 2001 wakati wa muungano wa NDP na KANU. Njee alikuwa mratibu wetu. Tulitembea na Njee sambamba mpaka dakika ya mwisho. Halafu mwaka wa 2005 wakati wa kura ya maoni ya chungwa na ndizi Njee alikuwa mratibu wa taifa. Tulimpigia makofi kwa sababu aliweza kutueleza vizuri na tukaenda vizuri na ilikuwa nzuri. Na chama changu cha CORD pia mimi najua ya kwamba kiliendelea vizuri. Yangu si mengi. Nataka kuwaeleze wenzangu ya kwamba hakuna maana tunaita mtu wakati wa vita na vita vikiisha wakati wa kula tunampiga makofi. : Toboa. Toboa
Ahsante mhe. Spika. Yangu si mengi kwa sababu nimekaa na Njee Muturi kwa miaka mingi na wana-CORD ambao wako katika Bunge hili walimjua mwaka wa 2001 wakati wa muungano wa NDP na KANU. Njee alikuwa mratibu wetu. Tulitembea na Njee sambamba mpaka dakika ya mwisho. Halafu mwaka wa 2005 wakati wa kura ya maoni ya chungwa na ndizi Njee alikuwa mratibu wa taifa. Tulimpigia makofi kwa sababu aliweza kutueleza vizuri na tukaenda vizuri na ilikuwa nzuri. Na chama changu cha CORD pia mimi najua ya kwamba kiliendelea vizuri. Yangu si mengi. Nataka kuwaeleze wenzangu ya kwamba hakuna maana tunaita mtu wakati wa vita na vita vikiisha wakati wa kula tunampiga makofi. : Toboa. Toboa Namuunga mkono Njee kwa sababu nambari ya simu alionipatia mwaka wa 2001 hajabadilisha. Lakini nasema ya kwamba nina ii na wenzangu. Naunga mkono kama vile wengine wamefanya na hii ni mambo ya nchi yetu ya Kenya. Sio jambo la mtu moja. Nasema kwamba sipingi. Nasema kwamba Njee ako sawa kwa sababu namjua.
Ahsante Mheshimiwa Naibu Spika kwa kunipa fursa hii niweze kuunga mkono Kiongozi wa Walio Wengi katika Bunge kwa Mswada aliyoleta Bungeni siku ya leo. Mswada wa Halmashauri ya Kuchunguza Hali ya Ukame ulisomwa mara ya kwanza tarehe 2/5/2019. Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge mia mbili kumi na sita (g) wajibu wa kusimamia halmashauri hii uko chini ya Kamati ya Utendakazi na Ustawi. Leo nimepata fursa ya kuweza kuunga mkono Kiongozi wa Walio Wengi katika Bunge. Mswada huu umeletwa kwetu baada ya Karani wa Bunge kutangaza magazetini na Wakenya wengi kuleta maoni yao. Katika maoni hayo wengi wameunga mkono pendekezo lililoletwa mbele ya Bunge. Sio hivyo tu hii Kamati imeweza kutayarisha ripoti ya kujadili kipengele baada ya kingine na kutathmini faida na hasara ya pendekezo la kuibadilisha hii sheria. Lengo kubwa la kubadilisha hii sheria ni nini? Ilivyo hali kwa sasa jambo la kuchunguza hali ya ukame liko katika sheria za halmashauri hiyo. Lakini kuna pendekezo la washikadau na wafadhili ambao wanataka rasilimali wanazotoa zisimamiwe na PFM Act. Huu ndio msukumo mkubwa ili wafadhili wapate hakikisho kwamba usimamizi wa rasilimali zao uko chini ya PFM Act badala ya sheria ya Halmashauri ya Taifa ya Kuchunguza Hali ya Ukame. Kwa uchache hili ndilo lengo au maudhui ya pendekezo la leo. Yangu kama mwenyekiti tumechukua maoni na Wakenya wengi wameunga mkono. Kabla sijakaa chini ningependa kusema kwamba ninatoka Tana River na upande wa Tana North kuna ukame mkubwa. Upande wa Garsen South na Lamu kunanyesha mvua. Wengi wa wafugaji wamelazimika kwa sababu ya ukame watoke Tana North Bura an Galole waelekee upande wa Lamu na Garsen. Idadi ya wafugaji walioteremka huko ni kubwa. Kufuatia jambo hili kukawa na mzozo baina ya wenye mashamba na wenye mifugo. Kwa bahati mbaya walinda usalama badala ya kutatua mzozo uliotokea na kuchukua hatua wanachoma nyumba za wafugaji na kupiga watu kiholela bila kuangalia haki na sheria ya taifa. Nalaani vikali tendo hilo! Taifa na watunzi wa sheria wanastahili kutambua ufugaji. Mifugo ni rasilimali ya taifa. Kwa hayo machache naunga mkono Mswada huu na ninakushukuru pia Mheshimiwa Naibu Spika. Ahsante.
Ahsante Mheshimiwa Naibu Spika kwa kunipatia fursa hii ili nami nichangie Hoja hii. Ni dhahiri kwamba wengi wamedhulumika kwa sababu ya kutofahamu sheria kwa sababu sheria zimeandikwa katika lugha ya kigeni Kiingereza. Kwa hivyo watu wengi wanapata ugumu kufahamu sheria za nchi. Nikikumbuka vyema kuna wakati ambapo kulikuwa na mapinduzi ya Serikali kwa masaa machache mnamo mwaka wa 1982. Wale ambao walishikwa walisomewa mashtaka na kuambiwa wayajibu. Walidhani waliyajibu mashtaka hayo sawa lakini walishtukia wameyajibu visivyo kwa kudai kwamba hawakuhusika wala hawakiri mashtaka yote. Mmoja wa watuhumiwa hao alisema: " I am not guilty of all those ". Hii ina maana kwamba siyo yote anayoyakiri lakini baadhi ya hayo anayakiri. Hiyo ni hali ya kwamba hakuwa anaelewa ni nini kilichomkabidhi hapo mahakai. Hivyo basi kuna madhara mengi ambayo wananchi wa Jamhuri ya Kenya wanayapata
Ahsante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii. Kwanza kabisa ninasimama kuiunga mkono Hoja hii. Pili Kenya ilipopata Uhuru kulikuwa na SessionalPaper No.2 . Sera hii iligawanya Kenya katika sehemu mbili; sehemu ya rotuba na sehemu isiyokuwa na rotuba. Huduma katika taifa imegawanywa kwa msingi wa sera hii. Wakenya wengine wanapozungumza kuhusu utoaji wa kitambulisho mimi nahisi kulia. Kule kwangu utapata mama amezaa watoto watano na mpaka leo hana kitambulisho na hawezi kutembea barabarani kwa sababu Kenya Defence Forces (KDF) wako katika kila kona. Kitu cha kwanza watamuuliza ni atoe kitambulisho na si makosa ya yule mama kutokuwa na kitambulisho. Lakini wale wanaowasajili Wakenya kwa furaha yao au uwezo wao wanakufanya Mkenya au usiwe Mkenya. Wamemnyima yule mama fursa ya kupata kitambulisho. Swala la pili ni muda ambao unahusika katika utoaji wa kitambulisho. Kuna mtu ambaye amebeba kadi ya kusubiri kwa miaka mitatu au minne. Masuala ya utoaji wa vitambulisho ni masuala ya dhuluma dhidi ya binadamu. Unamnyima mtu haki yake ya kuwa Mkenya. Unaambiwa kuwa Cheti cha Kuzaliwa hakithibitishi uraia wako. Kitambulisho na hati ya kusafiria ndizo zinathibitisha uraia wako. Huwezi kupata hati ya kusafiria kama huna kitambulisho. Wakati umefika wa kuwanasua Wakenya kutoka kwa dhuluma ya Sessional Paper No.2 na kutoa uhuru wa kila Mkenya kumiliki kitambulisho. Kwa sababu uraia wako rasilimali yako na biashara yako haziwezi kuwepo kama huna kitambulisho. Kuweka usalama ni jukumu la Serikali ya kitaifa lakini kaunti zinafanya kazi nzuri. Hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge ni jukumu la Serikali ya kitaifa lakini kaunti zinafanya kazi nzuri. Kwa nini vitambulisho visitolewe katika kaunti? Ile huduma itakuwa rahisi kwa Wakenya. Nikimaliza kuunga mkono ninatoa kongole kwa Mhe. Wamalwa kwa kuileta Hoja hii. Hii Hoja ingekuja jana leo vitambulisho vingetolewa katika Kaunti ya Tana River. Ninasema hivyo kwa sababu mtu anatoa nauli kuja Nairobi na kulipa hoteli kutafuta kitambulisho ambacho angeletewa kule aliko. Kwa hayo machache ninaunga mkono Hoja hii. Asante.
Ahsante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ya kuzungumzia Hotuba ya Rais. Mwanzo ningependa kumpongeza Rais. Alizungumza kama watu 100 hata zaidi ya 1000. Alizungumza kama kiongozi. Alizungumzia mambo ambayo yatatuleta pamoja. Nchi nyingine Afrika zinatutaja vibaya kwa sababu ya mambo mawili ambayo Rais alizungumzia. Wenzetu wanatusengenya. Hapa Afrika Mashariki wanasema shida yetu Wakenya ni kwamba baada ya uchaguzi tunagombana kisha tunarudi nyuma. Ikiwa majirani wanatuona Rais akizungumza kwa nini watu wasione amezungumza jambo zuri. Jambo la pili majirani wetu wanatuzungumzia vibaya ni ufisadi. Kupata uwiano na nchi nyingine inakuwa vigumu kwa sababu wanatuogopa. Ikiwa Rais ametambua na kuzungumzia hilo suala tunafaa tumuunge mkono mia kwa mia. Rais amefanya kazi. Mimi na Mheshimiwa Mishi hatukuweza kuangaliana kwa macho kwa sababu ya mirengo ya kisiasa. Saa hii tumefanya Harambee. Nilimwita Katibu wa COTU Atwoli akaja akanifanyia Harambee ambayo haijawahi kufanywa kwa miaka yote tangu tupate uhuru. Akina mama kule Lamu hawajafanyiwa Harambee kama hiyo. Vita ambavyo tumepata leo kutoka kwa Mheshimiwa Duale ni kwa sababu ameona kina mama wa Lamu wameinuliwa na kuwa sawasawa na kaunti nyingine. Hilo limeanza kuwakera. Kina mama wa Lamu wameinuliwa kwa kuwa wamepata pesa kima cha Kshs10700000. Hilo ndilo muhimu. Na hata wakija tena kufanya Harambee nyingine tunawakaribisha. Waje tushindane kwa mazuri pesa ziingie Lamu Kaunti nayo iwe sawasawa na kaunti nyingine. Ninataka kuwatahadharisha wale ambao watakuja Lamu wahakikishe kuwa wakija wasishikane na walanguzi wa madawa ya kulevya. Tatizo kubwa tulilonalo kule Lamu ni ulanguzi wa madawa ya kulevya. Vita vinavyotokea kwa wingi Lamu ni kwa sababu ya madawa ya kulevya. Wanaouza wanajulikana. Katika eneo Bunge la Lamu East watu ambao wanauza dawa za kulevya ni wawili. Mmoja ni Hamza As Ali. Anaharibu watoto wa watu wa Lamu na anajulikana. Serikali pia inamjua mpaka imempatia bunduki kumaliza watoto wetu. Kwa hivyo ninamtahadharisha Mhe. Duale akija Lamu asiunge mkono walanguzi wa dawa za kulevya. Watoto wetu wameisha Lamu na tunataka suluhisho. Ninaomba Serikali.
Ahsante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Kwanza ningependa kusema kuwa ni heshima kubwa sana kujadili hapa hii Hoja ambayo ni muhimu sana kwa nchi yetu ya Kenya. Ukiangalia pengine wengine wetu hatujaliangalia hili jambo vilivyo kwa sababu hatujaelewa kuwa mjadala huu uko kwa hii nyumba yetu ya Bunge kwa sababu ya Katiba yetu ambayo ilisema kuwa jambo lolote ambalo ni la ulinzi ama mkataba wowote ambao Serikali itakuwa imetia sahihi lazima ujadiliwe hapa na viongozi wa wananchi wa Kenya. Ningependa kuunga mkono Hoja hii ya Kamati ya Ulinzi na Mashauri ya Nchi za Kigeni. Mimi ni mmoja wa Kamati hiyo. Ningependa kutoa heshima zangu kwa Mwenyekiti wangu Mheshimiwa Gethenji. Pia ningependa kutoa shukrani zangu kwa Waziri Amina na Katibu Mkuu wake Dr. Kibicho. Tena ningependa pia kutoa shukrani zangu kwa wale maofisa katika idara ya ulinzi katika nchi yetu na Serikali ya Kenya ambao walijihusisha na kujadiliana na kuyaangalia masuala nyeti ambayo yangetusumbua na kuhakikisha kuwa hii Hoja imeletwa hapa Bungeni. Nina uhakika kuwa Wabunge wataipitisha Hoja hii kwa sababu haina tashwishi kabisa. Ukiangalia Hoja hii mkataba huu ukitiwa sahihi nchi za Africa Mashariki zote zitakuwa zinaungana na kufanya kazi pamoja. Zitapashana habari kuhusu mambo ya ujasusi. Ikiwa kutakuwa na msiba ama shida yoyote - hata kama kutakuwa na ugonjwa kama vile Ebola - nchi zote za Afrika Mashariki zitakuja pamoja na tutaungana na kujaribu kutatua shida hiyo. Jambo lingine ningependa kusema ni hili: Ukiangalia Jumuia ya Afrika Mashariki tangu 1962 hadi 1963 wakati nchi za Afrika Mashariki zilikuwa zinapata uongozi kutoka kwa wakoloni tumekuwa tukisema ingekuwa vizuri sisi tuwe na eneo moja la kiuchumi. Tutakuwa na ushirikiano katika mambo ya ulinzi kwa sababu sisi ni Waafrika kutoka eneo la Afrika Mashariki na sisi ni kitu kimoja. Imefikia kiwango cha lazima tuanze kufanya kazi pamoja tuheshimiane na tuangalie eno ya mipaka yetu ili tusiwe na tashwishi kabisa. Kama kuna shida ambayo inatokea lazima tuwe na njia ambazo sisi wenyewe tunazungumzia masuala hayo. Lazima tukubaliane kuwa lazima tuyazungumzie tuwe na ai ili tujaribu kuendeleza eneo letu kiuchumi na tuhakikishe kuwa wananchi wetu ndio wanafaidika. Nawasihi ndugu zangu hapa Bungeni kwa kupitisha Hoja hii kwa sababu jeshi hilo litakuwa la dharura. Kabla hilo jeshi la dharura halijaenda kuvamia nchi yoyote kikao kitakuwa kimesimamiwa kule Jumuia ya Afrika kule Ethiopia na watajadiliana vile jambo hilo litatatuliwa. Jambo la pili ni kuhakikisha kwamba kila nchi itakuwa imetoa msimamo wake. Hili ni jambo lazima likubalike katika nchi zote ambazo zimehusika. Tukubali Mkataba huu ili kuhakikisha kuwa tumesuluhisha shida iliyoko. Nina uhakika kuwa wakati ambao Rwanda ilikuwa na shida zake kama tungekuwa na jeshi la dharura lingekuwa limeenda Rwanda na yale mauaji ambayo yalifanyika yangesimamishwa. Kwa hivyo ningependa kuwasihi ndugu zangu kuwa tupitishe Hoja hii kwa sababu ni nzuri. Kumalizia ningependa kusema kuwa nilisikia ndugu yangu mmoja akizungumza na kusema kuwa pengine hii Hoja isipitishwe kwa sababu nchi kama Burundi wakati huu ina shida na tuna shida yetu na Uganda kuhusu Migingo. Ningependa kumwambia ndugu yangu Mwenyekiti wa chama changu cha Orange Democratic Movement (ODM) kuwa shida ambayo iliyoko Burundi kama kungekuwa na mkataba kama huu Rais wa Burundi angefikiria mara mbili kabla yeye kuamua kuwa angependa kupigwe kura ama la. Angekuwa anaangalia sheria vile iko na angekuwa anawauliza marais wengine: "Mnaona aje na nifanye vipi?" Kwa hivyo mimi naonelea tukiwa na huu Mkataba ni vizuri. Kuhusu eneo la Migingo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Mashauri ya Nji za Kigeni amesema kuwa hili ni jambo ambalo Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Mawaziri wale wanahusika na Kamati ya Ulinzi na Mashauri ya Nchi za Kigeni wamekuwa wakilijadili. Hivi karibuni tutakuwa na suluhu ili tujaribu tusiwe na hii shida. Sisi kama viongozi na wananchi wa Afrika Mashariki ni lazima tuendelee kuishi pamoja tupendane na tuheshimiane. Kwa hayo mengi ningependa kusema kuwa mimi naunga mkono Hoja hii. Ni nzuri na itafanya Kenya iendelee kama nchi ambayo ni ya heshima na sheria. Ahsante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda.
Ahsante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Naomba nami nichangie Hoja hii kuhusu gharama za ndoa na vile ndoa zimekuwa haziwezi kufanyika hivi sasa kwa sababu ya matatizo ambayo yameletwa hasa na Serikali. Tulipopitisha Mswada wa Ndoa wakati mwingine hatukutarajia kuwa baadaye Serikali itageuka iseme kuwa itaweka sheria ya kusema kuwa yule ambaye anataka kufunga ndoa lazima asafiri hadi makao makuu ambayo yamepangwa na Serikali. Nikitoa mfano watu wangu wa Taita watoke Taita waende Mombasa ama waje Nairobi ndio waweze kupata cheti cha ndoa. Utakubaliana nami kuwa cheti cha ndoa ni muhimu na kila mtu anakihitaji ili kuthibitisha kuwa amefunga ndoa na mtu na kuwa wale watoto ambao Mungu amewajalia mkapata wametokana na ile ndoa mliofunga. Tatu mmoja wenu akiwa hayupo na ameaga ndunia mali mtaigawanya namna gani ama ni nani ataachiwa mali? Mkiwa mnamiliki mali nani ataweza kumiliki hiyo mali? Lakini hivi sasa imekuwa ni kero kubwa kwa mtu yeyote anayetaka kuoa mwenzake ama kuolewa na mwenzake. Inambidi licha ya kutoa mahari agharamie usafiri kwenda kutafuta cheti na asajiliwe. Badaye ndio arudi tena kanisani kuja kufunga ndoa. Swali tunalouliza ni: Kwa nini tumeweka sheria kama hizi ambazo zinafanya watu washindwe kufunga ndoa ama kuoana? Je nia yetu tulipokuwa tunapitisha Sheria ya kuoana ilikuwa kuleta gharama ambazo binadamu ama wananchi hawawezi kuzigharamia na baadaye kuanzisha mipango ya watu tu kuungana? Binti atoke nyumbani kwao aende akae na mwanaume. Wazungu wanasema ni " Come let us stay" Hiyo sio nia yetu. Nia ilikuwa kutafuta taratibu ambazo zinaweza kukubaliwa ili watu wakiamua wakae pamoja waweze kuenda pahali ambapo wanahitaji wapatiwe cheti na mtu ambaye amethibitishwa kuwa amehitimu kufunganisha ndoa. Hivi sasa tumeshindwa kuheshimu kanuni za ndoa kwa sababu tumeifanya iwe ghali mno. Watu wameamua tu wataondoka yumbani mwao waje wakae kwa sababu wanaogopa zile gharama. Ombi letu ni hili: Katika kila kaunti kuwe na ofisi ambayo imesajiliwa na ina msajili ambaye anaweza kuandikisha kufunga ndoa na kupeana cheti. Nakubaliana na mawazo ambayo yalitolewa hapo awali kuwa mara nyingine kulikuwa na watu bandia ambao walijitokeza wakaanza kufunga watu ndoa na kuwapatia vyeti. Lakini hilo halimaanishi watu wote waadhibiwe kwa ujumla. Tunaomba irudishwe pale ilipokuwa na makanisa yakubaliwe kutoa vyeti vya ndoa pale pale ambapo watu wanaamua waoane ama wafunge ndoa. Ndugu zetu waislamu wana bahati. Hawakuhusishwa na sheria hii kwa sababu makadhi kokote walipo wanaweza kufungisha ndoa zao. Lakini sisi wakristo tuna shida kubwa sana kwa vile watu lazima wasafiri ndio waende kupata vyeti. Halafu ile ilani ambayo inahitajika ni kubwa. Unatakiwa kutoa ilani siku 21. Katika wakati huo hauwezi kupanga kitu chochote kwa sababu haujui ikiwa ilani italeta kero na mtu mwingine ataenda asimamishe hiyo ndoa. Kwa hivyo tunaomba kuwa gharama za ndoa zirudi chini. Tuhakikishe kuwa ofisi zimetengwa katika kila sehemu ya kaunti. Watu waweze kufungishwa ndoa na wale ambao watasajiliwa kuweza kupeana vyeti wawe ni watu wa kuaminika wamehitimu na wanaheshimika. Kwa haya machache naomba kuunga mkono Hoja hii. Asante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda.
Ahsante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Nimesikia ombi la mwenzangu ambaye ni wakili na namheshimu sana. Nashukuru kwa kuwa haujakataa hilo ombi ila umelichukulia maanani. Vile alivyosema kuwa anaona kweli nafaa kuwa gavana namshukuru na naomba kuwa Mungu azidi kulirehemu na kulibariki ombi lake. Tutakutana wakati mwingine. Ni muhimu tuangalie kuwa hizi sheria ambazo tumezipitisha hapa na ambazo tutazipitisha tukipata nafasi Inshallah Mungu akipenda ziwe sheria ambazo zitaendesha nchi yetu isije ikapata matatizo kwa sababu ya ardhi. Langu la muhimu ni kuangalia vipi tutakavyofanya na ile rasilimali tulionayo. Vile ilivyo itabidi wale watu ambao wamefanyiwa maovu tangu hapo awali watafute mbinu zingine za kufuata jopo ambalo ni la ardhi ili waweze kuhakikisha kuwa malalamishi yao na zile dhuluma ambazo wametendewa zimefikishwa. Malalamishi hayo ni kama yale nilioyanukuu mwanzo. Kwa mfano maovu ambayo yametendewa watu wa Taita ambao ardhi yao yote iko katika mbuga ya kuhifadhia wanyama. Hatukuweka mikakati mwafaka ambayo ingehakikisha kuwa hali waliojikuta inarekebishika kivipi. Namshukuru Mwenyeketi wa Kamati ya Ardhi alivyoifafanua Sheria tuliyofikiria itakuja inayobainisha watu watachukua kiasi kipi cha ardhi. Alieleza kuwa haitakuwa busara kusema tunaweka vipimo kuwa mtu awe na ekari tano kumi au elfu moja ya shamba kwa sababu inalingana na sehemu aliyoko. Tuliona haifai kuweka viwango vya ardhi ambayo mtu anaweza kukaa nayo. Lakini tukisema hivyo haimaanishi kuwa sasa watu wanapata ruhusa ya kunyang'anya wenzao ardhi ili wawe ni wao pekee yao ndio watachukua ardhi. Settlement schemes ni za wale watu ambao wako katika eneo hilo lakini sheria ilivyo inasema kuwa watu wanaweza kuja wakagawanya hiyo ardhi na kuishi hapo -ilhali wenyeji wanakosa ardhi hiyo. Hizo ndizo dhuluma ambazo lazima zitafutiwe mbinu ya kuzirekebisha. Nikielewa umuhimu wa ardhi tutajibidiisha tuwezavyo kuhakikisha kuwa haya marekebisho yote ambayo watu wameyaomba na Wabunge wanayaomba yachangiwe kwa undani ili sheria hizi ziwe mwafaka. Marekebisho haya yakipitishwa hizi sheria zitakuwa za kuungwa mkono na yasipopitishwa basi tutakuwa na shida. Kama nilivyosema tangu hapo awali mimi ni mmoja wa wanakamati wa Kamati ya Ardhi na naelewa kinachoendelea. Kwa hivyo naunga mkono Mswada huu nikijua marekebisho yanakuja. Naomba mnitakie kila la heri kwa malengo yangu ya baadaye.
Ahsante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Ningependa kusema kuwa namuunga mkono Mheshimiwa Chris Wamalwa kwa kuleta Hoja hii katika Bunge hili. Watoto wengi katika yale maeneo tumetoka
Ahsante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Sijui ni kwa nini Mheshimiwa Mbadi anaona ni kama sina Hoja ya Nidhamu. Lakini nakuomba kwa heshima Mheshimiwa Mwenyekiti Mbadi ya kwamba sisi hatutaki kujua zaidi vile uenyekiti wako unaendelea. Tunataka kujua yale tunaongea siku ya leo. Tafadhali mambo yako na Mheshimiwa Ken Obura na chama yasijadiliwe hapa bali kwa chama. Ahsante.
Ahsante Mheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi hii ya kusema katika hilo Ombi Ombi hili ni muhimu na naliunga mkono Kwa hakika watu wengi wanapata shida pande zote za Kenya Lamu sisi ndio tuna shida zaidi Kuna hiyo park ambayo iko hapo lakini haitusaidii bali hutuumiza Afadhali sehemu zingine kama Maasai Mara angalau wanasaidika kwa upande mwingine Sisi kwetu katika pesa ambazo zimetolewa za malipo zaidi ya miaka kumi saa hii zimetolewa milioni sita peke yake na kuna watu wengi wameathirika na wanyama Kisha wanatuumiza zaidi Sisi ni watu wa bahari Wanyama karibu wote wa bahari waliwatoa kwenye orodha ya malipo Ukienda ukifika baharini ukipigwa na mnyama anayeitwa yeda haulipwi Ukipatikana na papa hulipwi Na kule tuna wanyama msituni na wanyama baharini Na saa zingine wanaenda baharini na wanapata hata mamba ndani ya bahari kwa sababu wako karibu na maji ya mto Kwa hivyo sisi tuna shida nyingi Lakini huyu Waziri naye anatoka Coast huko lakini hata sijui ni kwa nini huko Lamu amekusahau Sijui ni kwa sababu vile kuko mbali Watu wanalipwa na ikibakia kidogo ndio inarushwa Lamu Nataka Waziri Balala ajue kwamba Lamu ni Kenya na Lamu ni Pwani Ahsante Bw Spika
Ahsante Mheshimiwa Spika kwa nafasi hii ambayo nimepewa ya kuunga mkono Ratiba ya Bunge na mpangilio ambao umewekwa waziwazi vile Bunge itakavyoendesha kazi zake. Naomba nichukue nafasi hii kuwatahadharisha Wabunge wenzangu. Mmekaa hapa karibu miaka minne na mpaka sasa hamjaelewa shughuli za Bunge. Mara nyingi nimeona Mheshimiwa Spika amesimama na naona Mbunge anatembea tembea ndani ya Bunge. Inamaanisha mpaka sasa hawajachukua nafasi ya kuelewa shughuli na mpangilio wa Bunge. Naomba wakati huu Mheshimiwa Spika hawa Wabunge ambao wamekaa hapa miaka minne na mpaka leo hawajaelewa Mmoja alikuwa anasimama mbele yangu wakati nilikuwa ninazungumza akikuzuia usinione.
Ahsante Mheshimiwa Spika kwa ruhusa yako. Ninachukua fursa hii kumpongeza mwenyekiti wa Kamati hii kwa kazi nzuri alioifanya. Kabla sijampa sifa sheria iliyoko mbele yetu ni mchanganyiko wa mazuri na mabaya. Tutakaposimama pamoja kukosoa yale mabaya yalioko mbele yetu bila shaka hii itakuja kua sheria nzuri sana. Nasema hivyo kwa nini? Juzi Mhe. Halima Ware alizungumzia kuhusu mauaji ya mtoto katika sehemu inayopakana na Tsavo West. Maafisa wa KWS walimuua mtoto. Wakati ripoti ilifika nyumbani watu kuenda kuchukua maiti walikuta ilikua imechukuliwa na KWS. Sasa swala nzito tunajiuliza ni; watu hawa wanawala watu? Mtoto huyo walimpeleka wapi? Hakuna mama mzazi anaweza kulia akibingirika akisema mtoto wake ameuawa pale bila jambo hili kuwa la kweli. Damu ilionekana pale lakini maiti haikupatikana. Pengine Mswada huu utaleta uso wa ubinadamu katika uwindaji wa wanyama na kusimamia mbuga za wanyama. Mwenyekiti alipokua akizungumza jana alizungumzia faida nyingi ikiwemo faida ya utalii GDP na faida aina mbali mbali. Ukumbusho wangu kwa Bunge hili ni kuwa tuwe na sheria bora. Faida haipatikani mpaka tutakapotambua haki ya wale wanaoishi karibu na mbuga za wanyama. Kwa nini niseme hivyo? Wema hulipwa na wema. Mtu amekupa ardhi mifugo wake hawatoki shamba lake hawezi kulima na KWS wanaua watoto na kuwaficha! Hapa unalipa wema wetu sisi tunaokupa ardhi kwa ubaya. Kule kwetu tuna Mbuga ya Wanyama ya Kora Mto Tana Mbuga ya Wanyama ya Tsavo West na Tana River Primate Reserve. Ardhi yote imeenda na KWS. Pengine sheria iliyoko mbele yetu itapitisha kwamba kila kaunti iwe na mbuga ya wanyama moja na national reserve kadhaa ambazo zitasimamiwa na serikali ya kaunti. Usimamizi wa mbuga za wanyama umewekwa chini ya Serikali ya taifa. Ni vizuri tukubaliane nyingi ya hizi mbuga za wanyama na reserves ziko katika kaunti. Serikali ya taifa ikisimamia usimamizi mwingine utafanywa na nani? Kuna maswala nyeti ambayo yanastahili kuamuliwa na serikali za kaunti. Hivyo basi rasilimali hizi zisimamiwe na serikali ya kaunti. Kama tunazungumza juu ya ukame ni vigumu kwa waziri kutafakari Tana River iko wapi na ina matatizo gani. Lakini serikali ya kaunti inatambua kweli sehemu ya kusini ya Tana River inastahili kupewa ruhusa walishe mifugo katika mbuga ya wanyama. Lakini itakuwa vigumu kwa Serikali ya Taifa kufahamu haya. Ningependa kusema pia kuwa mchakato wa kuifanya sehemu yoyote hifadhi ya wanyama unafaa uhusishwe mwananchi kutoka siku ya kwanza mpaka siku ambayo hiyo sehemu itatangazwa kuwa hifadhi ya wanyama. Nilipokuwa katika Bunge la Tisa Kola ilikuwa national reserve. Hatukuhusishwa kwa mkutano wowote na leo Kola ni national park. Mchakato huu ni lazima uhusishwe mwananchi wa kawaida. Ninaambiwa ya kwamba kupitia Kifungu cha 38(1) (a) (b) and (c) Waziri ana uwezo wa kuamka na kutangaza sehemu kuwa national park au marine park. Uwezo huyoni lazima upitishwe na Bunge ili Waziri asiwe na mamlaka kama hayo. Kwa nini asipewa mamlaka kama hayo? Kwa sababu Kifungu cha Katika cha 63(2)(d)(i) mpaka (iii) kinazungumzia juu ya ardhi ya wafugaji na ardhi ya umma ambayo haiwezi kutangazwa na Waziri kutumiwa kwa matumizi mengine. Ili sheria hii ambayo tunaitunga isigongane na Katiba mamlaka ya kutangaza sehemu kuwa national park ipitishwe na Bunge. Isipopitishwa na Bunge hivi ilivyo inafaa kubadilishwa na haifai kupita hapa ndani. Ukiangalia sehemu ya hatia na faini inanichekeza. Naona mkono wa wakoloni ndani ya hii sheria. Nasema hivyo kwa sababu kuna wanyama katika kifungu cha (a) ambao ukiwaua utatoa faini ya Kshs20 milioni au kufungwa milele gerezani. Lakini wale wanyama wakiuwa wewe utalipwa Kshs1 milioni au Kshs3 milioni. Baina ya hao wanyama na wanadamu nani anastahili kulipwa Kshs20 milioni? Nikiua ndovu nitafainiwa Kshs20 milioni au nifungwe milele gerezani.Ndovu akiua mtu familia yake italipwa Kshs1 milioni au Kshs3 milioni kuambatana na hali ilivyo. Jee wanyama ni muhimu kuliko wanadamu? Je swali hili tukiulizwa na wananchi ambao wanatutegemea sisi kuwatungia sheria tutawapa jawabu gani? Hapa naona mkono wa wakoloni. Ili tutoe huu mkono wa wakoloni ni lazima tuseme kuwa ndovu akiua mtu familia yake ilipwe Kshs20 milioni au ndovu akiuawa faini iwe Kshs3 milioni ili kuwe na usawa baina ya sheria na utekelezaji. Kifungu cha 89(f) kinasema kuwa ukipatwa ukilisha ndani ya uhifadhi ya wanyama hata kama ni mbuzi kumi utafainiwa Kshs200000. Pengine dhaa ya wanyama wako haifiki Kshs200000. Sheria hii itaumiza wafugaji. Ukisoma ukurasa wa mwisho hifadhi za wanyama ambazo zinahesabiwa hapo ziko katika sehemu za wafugaji. Ni lazima tutambue kwamba kuna haki baina ya mifugo na wanyama hao. Nikimalizia juzi maafisa wangazi za juu katika KWS ambao wote wanatoka katika sehemu ya wafugaji walisimamishwa kazi. Lakini kabla ya muda wao wakufutwa kufika ofisi yao ilibadilishiwa watu wengine. Hiyo ni dhuluma. Sisi ardhi yetu imechukuliwa na KWS na tunataka nafasi za kazi kwa watoto wetu. Wale ambao wako katika ngazi za juu wahifadhiwe. Kwa hayo machache tukirekebisha nitaunga mkono.
Ahsante Mheshimiwa Spika nimesimama kwa hoja ya nidhamu. Natumaini umesikia Mheshimiwa aliyezungumza mbele yangu akisema mwenendo wa mataifa ya Kiafrika umeongozwa na nchi za Kiafrika zisizokuwa na rekodi nzuri ya haki za binadamu. Je Mh. Spika Bunge hili au mwanachama yeyote wa Bunge hili anaruhusiwa kuzungumzia ubaya wa nchi jirani yetu? Ahsante Mhe. Spika.
Ahsante Mheshimiwa Spika. Naomba nichukue nafasi hii kupongeza Bunge la Kitaifa wakati huu ambalo linatarajia kwenda likizo kwa kazi ambayo imefanyika vile imeelezwa hapo na mwenzangu ambaye ametangulia kusema. Mheshimiwa Spika wakati kama huu Waheshimiwa Wabunge wanatarajiwa kwenda katika maeneo yao wanayowakilisha ili wakae na wananchi wao wapate kuwaeleza yale ambayo wamekuwa wakifanya kwa muhula huu wote Bungeni. Ni ombi langu kuwa tutaweza kujistili na tufanye kazi ile ambayo tumepatiwa na wananchi. Hivi leo mchana tumechukua muda mwingi sana tukiangalia vipengele kadha wa kadha kutokana na Mswada huu ambao ni wa sheria za ulinzi. Imebainika wazi kuwa Mswada huu unahitaji marekebisho kadha wa kadha. Nashukuru Mwenyekiti wa Kamati. Amekubali kuwa marekebisho haya yataletwa. Ameyaweka maanani na kuwa yataletwa hapa yajadiliwe na Wabunge. Mheshimiwa Spika si nia yangu kuchosha kila mtu hapa jioni ya leo. Nashukuru Kamati ya Bunge ambayo inahusika na wale wanakuja mbele yake wakiomba uwaajiri kama Mheshimiwa Nkaissery ambaye amepewa wadhifa ama amependekezwa apewe wadhifa na hivi leo amepitia kwa Kamati. Ni ombi langu kuwa
Ahsante Mheshimiwa Spika. Naomba nichukue nafasi hii pia kuunga mkono yote ambayo yamewasilishwa na Kamati ya Uwekezaji ambayo inazungumzia juu ya kubinafsishwa kwa Shirika la Simu la Kenya; uwekezaji ambao ulifanywa umeleta tashwishi. Vile tunavyojua Serikali ililazimika itoe billioni mbili nukta tano fedha ambazo tumepoteza na nchi hii itakuwa imepata hasara kubwa na hatujui ni wakati gani tutakuwa tumepata fedha hizi. Inasikitisha kuwa wakati wowote watu wakitaka kubinafsisha mashirika ya Serikali kila wakati lazima hasara iingie na moja yao ndio hii. Ndio maana tunapendekeza kuwa shirika ambalo linahusika na kuangalia kuwa ufisadi haupo linahusishwa kikamilifu ili likapate kuchunguza kashfa hii kwa undani sana. Naunga mkono Kamati.
Ahsante Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii ambayo umenipa nami niweze kutoa maoni yangu kuhusu Hoja hii. Kwanza naunga mkono Hoja hii kwa dhati. Ni jambo la kushangaza kuwa wenzangu wanasema ni vibaya kuorodhesha shule ama wanafunzi ambao wamehitimu vyema katika mitihani ya taifa. Tunaorodhesha shule ambazo zimefanya vyema ili umma upate kujua ni wapi matokeo yamekuwa mazuri. Watu watajiuliza ni kwa nini matokeo yamekuwa mazuri. Huenda ikawa ni kwa sababu ya vifaa vizuri vya shule walimu mazingara nakadhalika. Tusipoorodhesha shule na wanafunzi ni lini umma utajua sehemu fulani inafanya vyema kuliko sehemu nyingine? Tusipofanya hivyo fedha za serikali zitapelekwa mahali fulani peke yake. Basi itakuwa rahisi kwamba ni sehemu fulani za nchi ambazo zitatoa vinara na wanafunzi shupavu. Si kwamba wao wamejaaliwa akili kuliko wenzao bali ni kwa sababu ya kuwa na vifaa bora. Mheshimiwa wa Rarieda ananiambia kwamba katika eneo lake kuna wanafunzi ambao hawana viatu. Anasema kwamba shule zao hazina mijengo wala maabara. Ingawa hivyo wamefanya vizuri. Walipata alama nzuri za "A" "B" na "C". Hii ni kwa sababu wanafunzi wenyewe wanaweza kusoma. Wanafunzi wanakosa vifaa vya kutosha. Tunaomba waorodheshwe ili watu wajue ni vipi wanafanya mitihani. Hata wabunge ambao wako Bungeni wameorodheshwa. Mbona sisi tukatae shule ziorodheshwe? Nakubaliana na wenzangu kuwa mara nyingi watu wamechukua nafasi hii ili kutengeneza hela katika zile shule zinazofanya vizuri kwa sababu ya kuorodheshwa. Serikali lazima ichukue jukumu la kuhakikisha kwamba tabia kama hiyo imekomeshwa. Tusiseme kwamba kwa sababu tabia hiyo ipo basi ni kwa sababu ya kuorodheshwa. Lazima shule ziwe na mpangilio. Sharti ziorodheshwe ndipo tutajua sehemu fulani inafanya vyema kwa sababu fulani na fulani. Nimesikia mwenzangu akisema kuna kamati ambazo zimeteuliwa kufanya utafiti na zimependekeza kwamba shule zisiorodheshwe. Mimi nafikiri hii ni kwa sababu Serikali imeshindwa kutekeleza majukumu yake hasa kwa kuhakikisha kwamba vifaa vya shule vimesambazwa nchini kote. Sharti Serikali ihakikishe kwamba wanafunzi wanashindana katika mazingara ambayo ni sawia. Shule za hapa jijini Nairobi zina vifaa. Kwa hivyo walimu wanakimbilia huku. Wale waliobaki mashinani wana shida zao. Shule huko hazina vifaa. Kama Serikali itahakikisha imesambaza vifaa na walimu wazuri wanabaki mashinani basi wanafunzi watakuwa wakishindana katika mazingara sawasawa. Kwa hivyo naunga mkono Hoja hii. Nawasihi Wabunge wenzangu wafikirie ni nini wanachotaka kufanyia wanafunzi wetu wanaposema shule zisiorodheshwe. Juzi hatukupata hiyo orodha. Nini kimetokea? Orodha ziko. Hata katika kaunti yangu najua zile shule ambazo zimefanya vyema na zile ambazo hazikufanya vema. Nimejua upungufu uko wapi. Tunajua ni wapi tunatelezea. Hii ni kwa sababu shule zimeorodheshwa hata huko mashinani katika kaunti. Mnataka kuficha ukweli na hali tunaomba huo ukweli ujitokeze waziwazi ili tujue fedha zinapelekwa wapi. Kwa hayo machache naunga mkono Hoja huu.
Ahsante Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii nichangie Hoja hii. Moja kwa moja nataka kuipongeza Kamati kwa Ripoti yao nzuri. Lakini Kamati hii imeangazia sana upande wa Magharibi. Kwa hakika sio upande wa Magharibi peke yake ambako miwa inapatikana. Miwa inaweza kupatikana kwa wingi upande wa Tana River na Lamu hata kushinda upande wa Magharibi. Kunaweza kutoka miwa nyingi eneo la mto Tana. Kilomita chache kutoka Mto Tana kunaweza toka miwa nzuri zaidi kushinda upande wa Magharibi. Utafiti uliofanywa unaonyesha kwamba miwa ya upande wa Magharibi inavunwa baada ya mwaka mmoja na nusu. Lau ingefanyika upande wa Tana River na Lamu sana sana Lamu miwa hiyo inawezavunwa baada ya miezi kumi. Utafiti tena ukaonyesha kwamba tunaweza kuzalisha miwa na kupata tani 100 kwa kila ekari moja. Upande wa Magharibi mwa Kenya ekari moja huzalisha tani 80. Lamu inaweza kupatikana tani 360 kwa siku. Tunajua kwamba kila tunapokwenda tunaliliwa mambo ya kazi. Watu wanatafuta kazi. Hizi ndizo nafasi za kazi. Kamati hii ikitia akilini jambo hili inafaa kufikiria kaunti nyingine pia; sio upande wa Magharibi peke yake. Sekta hii itatoa kazi nyingi. Pia tutakuwa tumechangia katika zile Agenda Nne za Rais. Tutakuwa na uzalishaji mwingi. Tunaweza mpaka kusafirisha. Na sisi Lamu tuna bandari ambayo iko karibu. Twaweza kuitumia ile bandari kwa faida ya Wakenya na wakazi wa Lamu pia. Tusingojee kutoa miwa au sukari kutoka huku. Twaweza pia kutumia bandari ya Lamu kusafirisha. Pia itakuwa ni faida kwa Serikali. Mhe. Naibu Spika wa Muda ndio tunasema pesa zipelekwe mashinani ndio tuweze kuzalisha mashinani na watu watoke kwenye miji waende wakatafute kazi mashinani. Tukisema pesa ipelekwe tu kwenye watu wengi basi tutasababisha kuwe na idadi kubwa ya watu katika miji. Naiomba Kamati hii au Bunge tafadhali lipitishe hii Ripoti au mtaandika nyingine na mhakikishe mmeiweka Lamu ndani ili tuweze kuzalisha sukari. Watoto wenu watakuja kufanya kazi kule. Haimaanishi mkipeleka pesa Lamu ni watu wa Lamu tu ndio watafaidi. Hapana! Bandari iko Lamu au Mombasa lakini wanaofanya kazi kule ni Wakenya wote. Narejelea: Pelekeni pesa mashinani ili tutoe watu kwenye miji waende wakafanye kazi mashinani. Mkiweka pesa huku watu watajaa huku. Kwa mfano pesa zikiwekwa Nairobi zaidi watu watatoka Lamu waje wakae Nairobi kutafuta kazi. Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Ahsante Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Nachukua nafasi hii kuwapa hongera wanariadha wetu ambao walikuwa Rio. Tunasema ni ahsante kwa walivyofanya. Kweli wametufanya kuwa na furaha kubwa. Ningependa pia kumrudishia shukrani mwanariadha Rudisha ambaye aliweza kufanya jambo la kipekee ambalo tulilifurahia sana kama Wakenya. Kwa wote walioweza kushiriki pongezi. Sisi kama viongozi hatukupenda mambo ya ufisadi yalioendelea na kuwatesa watoto walioenda kule Rio.
Ahsante Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Nasimama kuunga mkono Mswada huu. Naelewa kwamba Mswada huu pia utapelekwa kwa Bunge la Seneti na urudishwe hapa na hivyo basi tukakuwa na nafasi ya kuuzungumzia zaidi. Ningetaka tu kuwaunga mkono wenzangu waliozungumzia mambo ya kuhifadhi misitu. Katika Serikali ya Rais mstaafu mzee Moi nilikuwa mwenyeketi wa KANU katika Wilaya ya Nakuru. Wakati huo misitu yote ilikuwa imefungwa ili watu waweze kulima ndani. Niliweza kunyenyekea kwake na nikajua kitu kimoja. Hakuna wakati juhudi za kuhifadhi misitu zitafaulu bila ya kuwahusisha wananchi. Hapo mbeleni uharibifu wa misitu ulikuwepo kwa sababu wananchi walifurushwa kutoka kwa misitu. Misitu haiwezi kulindwa kwa njia ya haki bila kuwahusisha wananchi. Ni lazima wafahamu kwamba misitu in mali yao na ni muhimu kuichunga. Siku hiyo nilipata nafasi hiyo na nikawa mtu wa kwanza - kabla nichaguliwe kuwa Mbunge - kurudisha mambo ya kulima ndani ya misitu. Imetufaidi sana kwa sababu Serikali haikuwa na pesa za kupanda miti na kulimia katika misitu. Wananchi wakihusishwa itakuwa ni jambo rahisi sana. Hata sasa ni rahisi kwa sababu wananchi watapewa sehemu fulani ambako watalima. Kawaida msitu hufukuza wakulima baada ya miaka mitatu kwa sababu miti ikifika miaka mitatu hauwezi kupanda kitu kingine ndani. Kwa hivyo tulijaribu sana. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu yale tunayoyazungumzia leo hii ni mambo nyeti ambayo tunastahili kusukuma ili yapite. Baada ya wananchi kulima na kupanda miti bila kulipwa kuna mambo machache ambayo yataleta mabadiliko. Hii ni kwa sababu baada ya wananchi kuilinda miti hiyo kuna shida ambazo zinawapata. Kuna watu kutoka Nairobi ambao hupewa vibali vinavyowaruhusu kuikata miti hiyo. Wananchi hao hawapewi hata kuni kutokana na mabaki baada ya miti kupasuliwa mbao licha ya kwamba wao ndio walioipanda miti hiyo. Uhusiano wa wakazi na misitu unaanza kuharibikia hapo. Wananchi wakikosa ii na kuona kwamba hawahusishwi kwenye juhudi za kuhifadhi misitu uharibifu wa misitu unaanza. Lakini sheria ambayo tunaipendekeza hivi sasa itawawezesha wananchi ambao wanalinda misitu kupewa nafasi wakati wa kuvuna miti ili nao wafurahie. Serikali ikipata pesa kutokana na bidhaa za misitu wananchi pia watafurahia kuni na malipo mengine. Sisi kama Wajumbe tunahitaji kuziendeleza juhudi za kuwafunza wananchi ili wapate kwamba hakuna utajiri mkubwa kama misitu. Tukiichunga misitu yetu kwa njia nzuri tunaweza kuweka nyuki na watatusaidia. Kule kwetu Nakuru tunapanda pareto ambayo inawawezesha wananchi kupata kiasi kizuri cha pesa kila wiki kutokana na mazao yao. Kwa hivyo Mhe. Naibu Spika wa Muda nimeshukuru. Kama ulivyosema Mswada huu utapelekwa kwenye Bunge la Seneti alafu urudishwe hapa tena na tutaendelea kuuangazia. Kwa hayo machache naunga mkono.
Ahsante Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Ningependa mwanzo kuchukua nafasi hii kumshukuru Mheshimiwa Oluoch kwa Hoja hii. Ni kweli vijana wetu wengi hawajaajiriwa. Kulingana na utafiti wa United Nations Development Programme (UNDP) asilimia 39 ya vijana wa Kenya hawajaajiriwa. Ukipima hicho ni kiwango kikubwa ukilinganisha na majirani wetu kama Tanzania Uganda na wengine. Nawakilisha Kaunti ya Lamu. Kenya National Bureau of Statistics walisema asilimia 68 ya vijana wetu hawajaajiriwa. Ni kiwango kikubwa sana. Kutoajiriwa huleta uhalifu. Kwa mfano utaona ya kwamba kaunti nyingi ambazo watu hawajaajiriwa uhalifu uko juu zaidi. Mfano ni Lamu ambapo uhalifu uko juu zaidi. Vijana wetu wameingia kwenye mihadarati sana. Hii inachangia matatizo zaidi. Kwa mfano ugonjwa wa ukimwi umekuwa juu zaidi. Ugonjwa huu na mihadarati ni janga kubwa katika Kaunti ya Lamu. Tunapambana na mihadarati. Tunapeleka vijana waende wakajikomboe na mihadarati lakini wakirudi wanarejelea. Kwa hivyo kukosa kazi kwa vijana wetu kumechangia shida nyingi. Serikali pia kwa mipango yake saa zingine husababisha watu kukosa kazi zaidi. Kwa mfano katika Kaunti ya Lamu wakati Lamu Port -South Sudan-Ethiopia Transport (LAPSSET) Corridor Project ilipoanza wavuvi wengi hawangeweza kwenda baharini. Kwa hivyo imechangia ukosefu wa ajira. Kuna kiwanda ambacho kinataka kuwekwa cha makaa. Sehemu hiyo ilikuwa na wakulima ambao walikuwa wamekaa hapo miaka mitatu wakingojea walipwe. Hawalimi sasa. Hii imeleta ukosefu wa ajira na wengi ni vijana. Pia kuna mpangilio wa Serikali uliyowekwa wa kutokata mikoko. Hii imechangia pakubwa ukosefu wa ajira kwa familia 3000 katika Kaunti ya Lamu. Mipango hii ambayo iko katika Hoja hii itasaidia pakubwa. Kitu kingine ambacho kinachangia zaidi pia ni kutegemeana. Kuna ukosefu wa ajira. Wale ambao wana kazi wanategemewa na familia.
Ahsante Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ili nichangie Hoja hii ya kupitisha majina ya wanakamati ambao watatusaidia kama Wabunge katika malipo baada ya kustaafu. Kwanza kabisa ningependa kusema kuwa hili jambo limechelewa kidogo kwa sababu kuna wenzetu ambao walipoteza viti vyao na wanateseka kule nje. Kwa hivyo sina pingamizi lolote. Naunga mkono ili majina haya yapitishwe. Siwajui waheshimiwa hao kwa kukutana nao lakini naamini kwamba wale wamechagua majina hayo wanawajua na wanajua kwamba watatekeleza majukumu yao kwa njia ambayo itafaidi waheshimiwa. Katika hili Bunge wale ambao tumekuja kwa mara ya kwanza tumefika karibu asilimia 60. Tunaambiwa kwamba kurudi hapa ni vigumu sana. Tungeomba sana haya mambo ya malipo baada ya kustaafu ianze baada ya muhula wa kwanza wala siyo baada muhula wa pili. Ianze baada ya Mbunge amefanya kazi katika muhula wa kwanza. Jambo lingine ni kwamba hakuna haja ya kuita mtu Mheshimiwa na unamnyima malipo baada ya kustaafu halafu anaanza kuzunguka katika Bunge kuomba hayo malipo. Kama mtu ni mheshimiwa basi apewe heshima yake. Kama hajafaulu katika kura apewe malipo yake ya baada kustaafu na mshahara wake wa mwisho. Jambo la waheshimiwa kuja na kuanza kuzunguka hapa si zuri. Jambo hili kuhusu malipo baada ya kustaafu halifai tu kuongelewa Bungeni. Hii ni shida ambayo kila Mkenya ako nayo. Nikirudi katika eneo langu la Bunge la Butere niko na wale watu waliostaafu na wanauliza kwa nini Serikali haijawalipa malipo yao baada ya kustaafu. Nikienda katika hiyo ofisi naambiwa nitoe stakabadhi nyingi. Ningependa kusihi Serikali na hii kamati malipo baada ya kustaafu yachukuwe muda mfupi kutayarishwa. Mambo ya kuzungushwa huku na huku haifai kabisa katika nchi yetu ya Kenya. Nikimalizia ningependa kutuma risala za rambirambi kwa familia ya Gavana Wahome Gakuru aliyetuacha. Nilimjua kama rafiki. Tumejuana kidogo. Angebadilisha maisha ya Wanyeri. Kwa hayo machache ningependa kuunga mkono Hoja hii inayopitisha majina ya waheshimiwa watakaounda kamati ya kushughulikia malipo ya baada ya kustaafu. Ahsanteni.
Ahsante Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuwapa shangwe Wakenya ambao walihudhuria michezo ya Olimpiki katika nchi ya Brazil. Tunasema asanteni sana na pongezi kwa kazi nzuri mliyofanya. Sisi kama wanaspoti katika Bunge letu la Kitaifa la Kenya na nikiwa Mwenyekiti katika ule mchezo wa voliboli tunasema pongezi sana. Tunaoimba Serikali yetu iiangalie mambo ya wachezaji wanapoenda kutuwakilisha katika zile nchi za mbali. Ni vizuri tuangalia hali yao vile watakaa kule wanaenda na vile watarudi baada ya kuhudhuria hiyo michezo ili walete sifa katika nchi yetu.
Ahsante Naibu Spika wa Muda. Nataka kumpa kongole Mheshimwa K'oyoo kwa kuleta Hoja hii ya muhimu kwa Wakenya wote. Mafuriko hapa Kenya yamekuwa ni janga kuu haswa kwa wale tunaotoka sehemu tambarare. Nasema kwa Serikali kuwa shida zingine zinaweza tatuliwa. Kwa mfano sehemu ninaotoka ni tambarare kweli lakini kule Tana River tuna barabara za maji. Barabara hizo zinaezajengwa ili maji yasipite huko kwa wengi. Kwa mfano katika eneo la Madogo sehemu ya Ziwani iko ng'ambo ya mto sehemu ya Garissa barabara ya maji ni ndogo sana sehemu hiyo. Serikali ikichukua hatua inaweza kuzuia maji yasiingie kwa miji. Kiswahili chasema kuwa ni heri kuziba ufa kuliko kujenga ukuta. Yatakikana tuwe tunayapangilia mambo kama hayo kama mitigation. Ni muhimu sana. Tunajua mapema kuwa hadhari hizi ziko miaka nenda miaka rudi. Lazima tujipange. Saa hii sehemu kubwa ya Tana River iko ndani ya maji. Mimea iko ndani ya maji na nyumba zimebomoka. Pia naomba wasamaria wema waende kwa sehemu zimehadhirika kama Tana River Pokot na zingine wapeane misaada kwa watu wanaoumia. Kuna watu wanalala kwenye nyumba ambazo wamezifunika na nguo zao. Hawana hema. Ni vizuri wafikishiwe hema chakula na hata madawa. Kwa hayo machache naunga mkono. Ahsante.
Ahsante Naibu wa Spika kwa kunipa nafasi ili nichangie pia hali ilivyo leo. Kwanza nataka kushukuru na kupongeza watu wa Kapenguria na West Pokot kwa jumla. Nawatakia kila la heri Wakenya na Wajumbe wakati wanarudi nyumbani. Nataka niseme kwa ufupi kwamba watu wamelalamika na kulia sana juu ya suala la usalama. Leo tumejadili kuhusu jinsi ya kurekebisha sheria na kutengeza hali ambayo itasaidia kudumishwa kwa mambo ya usalama. Lakini nataka kuwaeleza Wajumbe wenzangu kwamba hata tukitengeneza karatasi nzuri namna gani hakuna kitu ambacho kitafanyika. Lazima tuanze kusafisha nyumba ya wale ambao wanasimamia mambo ya usalama. Bwana Kimaiyo na Bwana ole Lenku wameumia kwa sababu wanatoka jamii ndogo. Wale wanaotoka katika jamii kubwa Mimi niko katika kamati ya usalama. Wakati mwingi hawa maafisa wakija katika mikutano yetu huwa pana shida. Hii ni kwa sababu mkuu wa polisi anaweza kusema jambo lakini wale wenzake wawili wanakanyagia hilo jambo. Sharti tuanze kutengeneza mambo. Kwa sababu ya ukabila ambao umejaa katika Kenya hii hakuna mahali tutafika. Wakati tutaanza kujadili vizuri suala hili kama nyumba nzima lazima tuangalie vitu kama hivyo kuhakikisha kwamba hatufanyi mambo ambayo hayasaidii.
Ahsante sama Mhe. Naibu wa Spika kwa kunipa nafasi hii ili nami nichangie Hoja hii. Naunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa mara nyingi humu Bungeni. Hoja hii imejadiliwa katika Kamati mbali mbali za Bunge na katika mikutano tofauti tofauti kwa miaka mingi hapa nchini. Hili jambo linaudhi kwa sababu viongozi ambao wamepewa nafasi kuwasaidia wananchi hawaonyeshi wana kusudia kuwasaidia wananchi. Mbinu zote ziko. Ripoti zimeandikwa. Pesa ziko katika nchi ya Kenya. Haya yote yanatuwezesha kuwa na chakula cha kutosha na maji ya kutumika hata pakiwepo ukame lakini viongozi ambao wamepewa mamlaka wamekataa kufanya hivyo. Kuna ukame katika Kaunti ninayotoka. Inasikitisha. Inatubidi sisi Wabunge kufanya mengi zaidi. Unataka kama Mbunge kufanya zaidi lakini hauna hizo nguvu. Kuna mashirika kama Msalaba Mwekundu na mengine ambayo yanashugulikia wananchi. Vile vile vijana wamekuja na miradi mbalimbali kujaribu kusaidia wananchi wapate chakula na maji. Lakini kwa ukweli hiyo haiwezi kusaidia kwa sababu Serikali peke yake ndiyo iko na pesa nyingi za kusaidia. Wakati mwingine ninashangaa nikiona wananchi wanakunywa maji ambayo rangi yake ni kama ya kahawa. Kuna watu hawajaoga miezi mitatu imepita. Watoto wadogo wa miaka miwili na mitatu wanakaa njaa na hukula mara moja tu kwa siku. Wanakunywa uji peke yake bila sukari ama maziwa kuanzia saa tisa mpaka kesho yake saa tisa ndiyo wanakula tena. Hatuwezi kuamini watoto wetu wakipitia shida kama hiyo. Pia kuna ripoti kwamba kuna watu katika hizi sehemu za ukame ambao wanaenda kwenye sehemu ambazo ni nafuu ama zina maji ya mifereji na kupeana watoto wao waangaliwe kwa sababu hawana chakula na wanaweza kuaga dunia. Pia kuna habari za wasichana wadogo ambao wanauziwa wanaume kwa shillingi mia tano elfu moja au mbili kwa sababu familia zao zimeshindwa kuwalisha na pia kuna hatari ya hao wasichana kuaga dunia. Hili ni jambo la kusikitisha sana. Hebu fikiria sisi hapa tukiwa na msichana wetu na hatuwezi kumlisha na inabidi tumuuze kwa mwanaume. Kuna wale ambao wanafurahia jambo kama hilo. Ni jambo la kusitikisha na haya yote si kwa sababu ya wananchi kuwa wajinga ama Kenya kuwa nchi maskini sana. Kenya ni nchi tajiri yenye mali ya kutosha kuhakikisha kwamba wananchi hawafikii hali kama hii. Kitu kingine cha kuudhi ni kuwa viongozi hawa ambao wanapewa majukumu ya kuhakikisha kuna maji na chakula kwa wananchi wanatumia njaa kama kitega kura. Wanaenda kwa wananchi wakijisifu sana na kugawanya kilo moja au mbili za maharagwe na mahindi ama maji kidogo na kuwaambia wananchi wawapigie kura. Unashangaa sana kama hii ni nchi ambayo tumemweka Mwenyezi Mungu mbele. Hapa Bungeni kabla tuanze kuzungumza tunaomba Mwenyezi Mungu. Kweli Mungu yuko ndani ya mioyo yetu ama ni jina tu ambalo tunataja? Katika mafunzo ya Kikristo na Kiislamu tunaambiwa tupende majirani wetu kama tunavyojipenda wenyewe na zaidi kwa kiongozi ambaye ameapishwa na kuuamua kuwasaidia wananchi. Mwaka jana tulikuwa na Mswada huu na tukazungumza haya haya lakini hakuna jambo ambalo limefanywa huko nyanjani. Kwa hivyo naomba kama Bunge tuwe tukiangalia tukipitisha mambo ya Bajeti na vile pesa zinavyofuatiliwa kuhakikisha kuwa pesa zinaenda kule zinastahili. Asante Naibu Spika.
Ahsante sana Bi Naibu Spika wa Muda kwa kunipa wakati huu. Kwa sababu muda umeyoyoma sana hatutazungumza sana kama chiriku. Ningelipenda kusema yafuatayo. Kwanza nasimama kupinga Mswada huu ambao umependekezwa na upande wa Serikali kwa hoja zifuatazo: Kwanza itakuwaje Waziri-Katibu kupewa nguvu za kuwateua aibu Chancellor wa vyuo vikuu baada ya bodi ya seneti na Council kuwachagua katika nyadhifa hizo? Nafikiri hilo ni jambo ambalo silo la muhimu. Jambo la pili ambalo linanifanya nipinge ni kwa sababu ukiangalia ile bodi ya vijana ambayo inafaa kuwa imeteuliwa na Waziri-Katibu inapatiwa jukumu la kuweza kufanya makadirio ya bajeti na pia kupitisha mipango ya vijana ilhali vijana wale wamechaguliwa na vijana wenzao kote nchini. Napinga huu Mswada kwa sababu utapata Msajiri Mkuu wa Vyama vya Kisiasa Rais anapatiwa mamlaka ya kuteu mtu aweze kufanya ile kazi kabla ya Bunge kupitisha. Hilo silo jambo nzuri kwa sababu linaweza kutumiwa kuchelewesha kuchaguliwa Msajiri Mkuu wa Vyama vya Kisiasa. Jambo hilo litaadhiri sana mambo ya vyama vya kisiasa. Jambo lingine ambalo linafanya nipinge Mswada huu ni kuhusu ile Tume ya Mishahara na Marupurupu. Utakuta Makamishina wengine pamoja na Mwenyekiti wanatakikana kufanya kazi mfurulizo na wengine waje kwa muda. Hilo si jambo nzuri. Ikiwa tutapitisha Mswada huu basi watapatiwa muhula mwingine wa miaka sita. Hivyoni kinyuma na Katiba yetu. Ningependa kuangazia Mswada huu kwa sababu kuna mbinu za kichini chini za kuhakikisha kwamba wale Mawaziri-Katibu wanajilimbikizia mamlaka ambayo hata Rais mwenyewe hana. Utakuta vipengele vingi ambavyo vinapendekezwa hapa vikisema kwamba Waziri-Katibu aweze kuwa na nafasi ya kuteua bila idhini ya Bunge hili la Kitaifa. Hilo si jambo la busara.
Ahsante sana Bi. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nami niweze kuizungumzia Ripoti ya Rais. Ninaiunga mkono Ripoti hii. Ninakubaliana na Rais kwamba watu wote wanatakiwa kuishi kwa umoja. Usalama wa nchi huadhirika kwa njia nyingi. Ndiposa tunazungumzia usalama juu ya lishe bora. Tunazungumzia usalama juu ya elimu. Pia tunazungumzia usalama juu ya uadui wa nje na ndani ya nchi. Bi. Naibu Spika wa Muda juzi wewe ulikuwa mkali sana ulipokuwa ukizungumzia hali ilivyokuwa kule Baringo. Bado pia tunasema vilevile; kwamba ni jukumu la viongozi walioteuliwa katika sehemu zile kuona jinsi watakavyowajibika ili kudumisha usalama katika maeneo yao wakishirikiana na viongozi wengine. Hata hivyo kunyoosha kidole cha lawama kwa mtu mmoja haiwezekani kwa sababu Rais pekee hawezi kupigana vita hivi pasipo na ushirikiano. Baadhi ya watu katika nchi hii tunaona kuwa mambo mengi ambayo yanasababisha shida ni kusahaulika kwa baadhi ya sehemu za nchi hii tunapoweka miundo musingi muhimu. Mhe. Nyenze alizungumzia shida za maji katika sehemu kadhaa za Kenya. Mimi leo ninazungumza kwa uchungu kwa sababu katika eneo langu la Jomvu katika Kaunti ya Mombasa muda huu wote kuanzi wakati tulipopata Uhuru mwananchi kupata maji ni kama kuona dhahabu. Katika sehemu nyingi watu hupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya uhaba wa maji. Maji ni bidhaa adimu. Watu hupigana kwa ajili ya maji ndiyo wanyama wao waweze kupata maji ya kunywa na wao wenyewe waweze kupata maji yatakayowawezesha kujikimu. Je inakuwaje binadamu anakosa maji katika sehemu anakoishi? Ninazumgumza nikiwa Mbunge. Mbali na kuiunga mkono taarifa ya Rais kuna vitengo kadhaa kama vile Coast Water Services Board na Mombasa Water and Sewerage Company ambavyo viko katika Serikali ya Taifa. Tukiangalia kuna ufadhili mkubwa sana ambao ulipatikana kutoka World Bank ili kuweza kupitisha mabomba kutoka chemichemi ya Mzima Spring kuleta maji mpaka sehemu za Mombasa lakini mpaka leo tunayaona mabomba yale yakitembea barabarani. Yamekuwa mabomba ya rangi ya kibichi. Yamekaa sana hakuna kazi yoyote ambayo imefanyika katika muda wa mwaka mmoja na nusu kufikia sasa ilhali hali haijabadilika na watu wanaendelea kupata shida. Ninamsihi Mhe. Rais kwamba tulifuatilie jukumu hili muhimu ili tuweze kuona kwamba wananchi wanaweza kupata bidhaa hii adimu. Ni muhimu Serikali ishughulikie hali hii kwa sababu wananchi wanaendelea kuumia. Hatuwezi kuumauma eno tukisema kwamba kila kitu kiko sawa ilhali mambo mengine hayako sawa. Ni muhimu tuwajibike na kuona kwamba maji yanapatikana katika sehemu zetu. Nikiwa kwenye Bunge la Taifa ninataka ninukuliwe nikisema kwamba hali hii imenitamausha mimi binafsi nikiwa Mbunge wa Jomvu. Ninaisihi Serikali tushirikiane pamoja ili maeneo ya Miritini Jomvu Kuu na Mikindani yaweze kupata maji ndiyo wakazi wa sehemu zile waweze kuishi vizuri. Ninamuona Mhe. Sakaja akipiga chini vizuri kwa kuashiria kuwa anakubaliana nami kwa sababu mkwewe na mke wake wanatoka Miritini ambayo iko katika sehemu yangu ya uwakilishi Bungeni. Leo mama mkwe wa Mhe. Sakaja hana maji. Kwa hivyo ninataka Serikali ya Mhe. Uhuru Kenyatta ijue kwamba mimi niliyoko katika muungano wa National Super Alliance (NASA) ambao imeshanaswa; na ndugu yangu Mhe. Sakaja ambaye yuko katika muungano wa Jubilee sote tunapata shida katika sehemu hiyo. Ninaomba Rais aingilie kati aone jinsi wananchi watakavyoweza kupata maji. Mwisho ufisadi hauwezi kuisha ikiwa vita hivi tutamwachia Rais pekee. Ni lazima tupigane vita hivi pamoja. Ni lazima tushirikiane. Tusingojee kumumwagia Rais lawama na kusema ameshindwa kumaliza ufisadi. Hatuwezi kusema Rais amefeli kama mwenye kupewa na mwenye kuchukua hongo hawatashirikiana kwenya kitendo cha ufisadi. Kwa hivyo ni lazima tuhakikishe kwamba tunaidhibiti hali hii pamoja; kama kunavyofanywa katika nchi nyingine ambako ufisadi ni kama donda sugu ambalo haliwezi kukubalika. Nilitembea katika nchi ya Rwanda ambako mambo ya ukabila hayaruhusiwi kabisa. Katika nchi ya Rwanda ukiwa ndani ya gari na uvute sigara halafu urushe ncha ya sigara chini dereva wa texi anaweza kukuripoti kwa polisi. Hilo jambo linamaanisha wote wameungana pamoja kuweka nchi yao safi na kuweka kando kwa ufisadi. Ni muhimu Wakenya tuige huo mfano ili tuweze kumkosoa Rais kwa mambo mengine lakini si kuhusu mambo ya ufisadi. Ni jukumu letu sote kwa pamoja kuijali nchi yetu. Ni jukumu la Serikali iliyoko na wale walioko upande wa Upinzani pamoja na wananchi kuhakikisha kwamba nchi yetu iko katika hali nzuri. Kwa hayo machache ninarudisha shukrani kwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili namimi niweze kuchangia mjadala juu ya Ripoti ya Rais.
Ahsante sana Bi. Naibu Spika wa Muda. Hoja hii imekuja wakati unaofaa lakini ni lazima kwanza tuangalie chanzo cha matatizo haya. Alipokuwa Waziri wa Kilimo Makamu wa Rais William Ruto wakulima katika eneo la Pwani walivuna chakula kingi mpaka wakakosa mahali pa kukihifadhi na kikaoza. Kuna shida katika Wizara ya Kilimo. Tunaomba Waziri wa Kilimo wa sasa aige mfano wa Mheshimiwa Ruto. Tunaomba asikae ndani ya ofisi bali aende mashambani akajionee na awasikize wananchi. Halmashauri ya nafaka nchini imejitweka majukumu yakuleta mbolea ambayo si majukumu yake. Kama halmashauri hiyo imeshindwa kutuletea mbegu italeta mbolea? Tumeipitisha Katiba ambayo imeanzisha serikali za majimbo. Sielewi ni kwa nini mpangilio wa ugavi wa mbegu ama mbolea umebaki katika Serikali Kuu. Inafaa kila kaunti inayofanya shughuli za kilimo ipelekewe pesa inunue mbolea na kuwapatia wakulima. Mamlaka ya kununua mbegu yatakapopewa kaunti na taasisi iliyopendekezwa kuundwa bodi ndogo katika kaunti zitapatiwa hayo mamlaka na tutaweza kupata mbegu na mbolea kwa wakati unaofaa. Wakati huo itakuwa rahasi kuwatambua wale ambao watakuwa wanazembea katika kazi zao kinyume na hali ilivyo sasa ambapo uzembe uko katika Serikali Kuu. Wakenya wanalia kwa sababu mbegu na mbolea haziwafikii kwa wakati unaofaa. Ninakumbuka kwamba katika miaka ya 90 kule kwetu Pwani kuliletwa mbegu iliyoitwa "Coast Composite". Mbegu hiyo ilizaa ajabu lakini kulipoonekana kwamba Wapwani walianza kupata chakula mbegu hiyo iliangamizwa. Sasa tunaletewa mbegu ndani ya mifuko. Tunaambiwa ndiyo mbegu inayofaa lakini tukipanda mahindi yanazaa yakiwa futi moja. Tutapata vipi chakula sisi Wapwani? Bi. Naibu Spika wa Muda wakati umefika wa haki kutendeka kupitia kwa majimbo yetu. Nina ii kwamba Serikali hii itaweza kutilia maanani kwamba bila ya chakula hatuwezi kufika popote. Kilimo ni njia moja ya kuleta ajira. Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza mbolea ni njia moja ya kuleta ajira. Nchi kama Israel inaweza kutengeneza mbolea yake. Unapoingia Mombasa na sehemu nyingine za Nairobi unashindwa hata pa kupitia. Kunanuka uvundo. Uchafu umeenea kila mahali licha ya kwamba uchafu huo unaweza kugeuzwa na kufanywa mbolea. Tunaomba shirika lililopendekezwa liundwe lihakikishe kwamba katika kila eneo kutakuwa na kiwanda cha kutengeneza mbolea. Tukifanya hivyo tutaweza kuisafisha miji yetu na kuwa na mazingira masafi. Tutakuwa tumeua ndege kumi kwa jiwe moja. Kwa hayo machache ninaiunga mkono Hoja hii.
Ahsante sana Bi. Naibu Spika wa Muda. Kwa hakika hata ukiangalia eno yaliyotoka katika kinywa changu hauwezi kuwa umeandika eno kama hayo. Nimeyazungumza yakitoka katika akili yangu. Nilikuwa nikiangalia tu kama ninataka kufanya reference ya kuonyesha kifungu fulani ambayo inaruhusiwa kulingana na Kanuni za Bunge. eno kama hayo siwezi kuyaandika na kuweza kuyasoma. Huu ni mtiririko wa eno ambayo yametoka katika kinywa changu na akili yangu.
Ahsante sana Bi. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii kwa sababu ni moja kati ya zile nguzo ambazo zinasimamia taifa hili katika upande wa afya. Kusema ukweli tuna upungufu mkubwa sana katika nchi hii. Nikiongea hususan katika upande wa Pwani kuna masikitiko makubwa sana wakati akina mama wanatembea zaidi ya kilomita ishirini kutafuta matibabu. Hata wakifika huko wanapata kwamba huduma ni duni kwa sababu hatuna wauguzi wa kutosha maabara hayana wasimamizi wa kutosha na hata hakuna vifaa vya kutosha. Bi. Naibu Spika wa Muda pia ningependa ieleweke vizuri sana kwamba ijapokuwa tunapigania hao watu waajiriwe ili tupata hiyo huduma kuna upendeleo katika uajiri. Tarehe nne mwezi wa nne hadi tarehe kumi na sita watu walikuwa wakisajiriwa ili waweze kupata ajira katika sekta ya afya. Bi. Naibu Spika wa Muda ni ajabu kwamba tuna majimbo lakini watu wanaitwa Nairobi kuja kuhojiwa. Kwa nini hiyo huduma haiwezi kufanyika katika makao makuu
Ahsante sana Bi. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua nafasi hii kusema kwamba utovu wa usalama nchini Kenya umekuwa jambo la kuhuzunisha. Umeumiza watu wengi katika jamii nyingi. Hivi tunavyozungumza tumepoteza watu wengi kwenye visa vya wizi wa mifugo hali ambayo imesababisha kudorora kwa usalama katika nchi hii. Tunapozungumzia Kerio Valley na haswa maeneo ya Tot Marakwet Pokot Tiaty na Pokot Magharibi tunafaa kufahamu kwamba haya ni maeneo ambako usalama umedorora. Nimeishi katika sehemu hiyo na ninaelewa jinsi hali vilivyo. Kuuawa kwa watu kiholelaholela ni jambo la kuhuzunisha sana. Kifo ni tukio la kawaida. Kifo kinapowatembelea kulingana na mpango wa Mwenyezi Mungu hatuna uwezo; lakini kifo kinachosababishwa na binadamu wenzetu kwa sababu ya kuzorota kwa usalama huwaumiza waathiriwa zaidi. Watu wengi nchini Kenya wamepoteza maisha yao kwa sababu ya kutokuwepo kwa ulinzi wa kutosha. Kwa mfano jana watu wengi walipoteza maisha yao mjini dera. Hili ni jambo la kuhuzunisha sana. Ni jambo ambalo linafaa kutusukuma tuchukue hatua ya dharura. Ukosefu wa usalama nchini humu ni jambo ambalo linafaa kuzungumziwa. Hatufai kuketi chini tukiangalia tu huku watu wetu wakiuawa. Jambo hili pia linasababisha watoto wetu kuacha kwenda shuleni. Kuhusu mzozo unaoendelea kati ya jamii zinazoisih katika sehemu za Marakwet Magharibi na Baringo tumezungumzia jambo hili kwa muda mrefu. Ni lazima tuchukue hatua kwa sababu wakazi katika Kaunti hizo mbili ni Wakenya. Mimi ni mkaaji wa Chesegon. Kwa muda mrefu sasa akina mama wamekuwa wakijifungua wakitembea na kwa sababu hiyo tumepoteza watoto wengi. Tunaishi nje ya nyumba zetu kwa sababu ya kudorora kwa usalama. Tumepoteza watoto wengi kutokana na magonjwa yanayosababishwa na baridi. Huu ni msimu wa mitihani ya kitaifa ya Kidato cha Nne na Darasa la Nane. Watahiniwa katika shule kama vile Chesegon Tot na Liter watafanya mtihani namna gani kama usalama haupo? Matokeo ya mitihani ya wanafunzi katika shule za Tot na Chesegon yatalinganishwaje na matokeo ya mitihani ya wanafunzi katika sehemu nyingine humu nchini? Hakuna atakayekumbuka kwamba watoto wengine walifanya mitihani kwenye mazingira ambayo hayakuwa na usalama. Matokeo ya mitihani ya watoto kote yatasawazishwa kutumia vigezo sawia bila ya kujali kwamba watoto wengine waliathirika kwa sababu ya kukosekana kwa usalama. Tunaomba usalama uimarishwe katika sehemu hizo kwa sababu wakazi hawana utulivu ama usalama. Hatuwezi kukosa suluhu. Ninaamini ya kwamba tuna uwezo wa kumaliza shida hiyo. Watu wengi wameuchangia mjadala huu wakiwemo wakazi wa sehemu hizo wenyewe. Kwa hivyo tunaomba sheria ichukue mkondo wake. Ningependa maafisa wa polisi na wananchi katika sehemu hizo washirikiane ili waweze kuleta suluhu kwa jambo hili.
Ahsante sana Bi. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kusimama na kuunga mkono Hoja hii ambayo inaweza kuhakikisha kwamba akina mama na vijana wanapata nafasi ya kuweza kutumia fedha ambazo zimetengwa na Bunge hili na Serikali kwa miradi ya biashara. Jambo ambalo linafurahisha ni kwamba watu walemavu pia wataweza kuakilishwa katika ile bodi ya kitaifa kupitia baraza la kitaifa kuhusu watu walemavu na pia katika eneo Bunge ambapo mojawapo wa wale ambao watakuwa ni wanakamati atakuwa ni mtu mlemavu ambaye atateuliwa na mashirika ya watu walemavu katika kiwango hicho. Hili ni jambo la kufurahisha kwa sababu ukiangalia maeneo yetu kila gatuzi linajaribu kuwekeza ndiposa kuwe na watu ambao wataweza kushiriki katika masoko yao. Lakini jambo ambalo pengine ni la kushangaza ni kwamba watu wetu hawana hela mifukoni. Watu wetu bado ni fukara hawajaweza kujihusisha katika biashara kwa sababu imekuwa ni vigumu sana kupata fedha za kuendeleza zile ajenda ambazo wako nazo yale mawazo ambayo yataweza kuwafaidi. Naunga mkono Hoja hii kwa sababu inaimarisha vile ambavyo tunaweza kujiendeleza ukianagalia vizuri kabisa. Lakini pia kuna dosari kwa sababu sijui kwangu mimi kama ingelikuwa bora Hoja hii ipendekeze ule mfuko wa fedha wa akina mama na ule wa vijana uweze kujumulishwa. Wale ambao wamekuwa wakiendesha mifuko hiyo wamekuwa na ujuzi na wamepata maarifa kutokana na vile ambavyo wamekuwa wakiendesha shughuli hizo. Ndiposa tusifanye yale makosa pengine ambayo waliyafanya. Kwa mfano wanaweza kueleza kinaga ubaga zile changamoto ambazo vijana akina mama na watu walemavu wanapitia katika shughuli zao za kibiashara. Ninatumaini kwamba kama Bunge tutahakikisha kwamba haya maarifa yanaweza kusaidia ili kuimarisha utekelezaji wa mfuko huu. Pia ni muhimu kuangazia kwamba kumekuwa na vijana wengi ambao wamekuwa na maarifa ya kuweza kuanzisha kampuni naku
Ahsante sana Bw. Mwenyekiti wa Muda nasimama kuunga mkono hoja hii. Kwa hakika pesa hizo ni za vijana na kuna umuhimu wa kwamba zikaweze kutawaliwa na vijana wenyewe. Kwa hivyo hakika ni vyema tuwape nafasi vijana. Haijalishi itakuwa ni vijana wa aina gani lakini pia kwa kuwa inasimamiwa ama imewalenga akina mama ni sawa huyo achaguliwe na akina mama. Kwa hakika hela hizi zimewalenga vijana na akina mama
Ahsante sana Bw. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Ninasimama kuunga Hoja hii mkono vile ilivyoletwa na mhe. Shukra. Naunga mkono kwa sababu tumetoa nafasi zote ambazo ni nyingi zinazosimamiwa na Wabunge wa maeneo ya uwakilishi Bungeni; tano ama zaidi ya tano zitakuwa mikononi mwenu. Kwa hivyo kuomba hii nafasi moja si kioja! Hii nafasi inapaswa kuwa itachukuliwa na mwakilishi wa wanawake na itakuwa ya mwanaume ama mwanamke kijana.
Ahsante sana Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Kifungu 94(1) cha Katiba ya nchi yetu kinatoa uwezo na mamlaka ya utunzi wa sheria kwa watu wa Kenya na hili Bunge. Kwa hivyo yeyote mwenye ndoto ya kubeba taka na kutuletea na sisi tusifungue kuingalia hiyo ni ndoto iliyopitwa na wakati. Mimi nina wajibu na Bunge lina wajibu. Kifungu 95(2) kinasema kuwa Bunge ni lazima lijadiliane juu ya matatizo yanayowakumba Wakenya na ipitishe na itafute suluhu. Kwanza kabisa naunga mkono Hoja hii. Pili pengine ripoti iliyoletwa hapa ina mapendekezo mazuri na mabaya. Bunge itayachukua mapendekezo mazuri na itarekebisha mapendekezo mabaya ili yawe ya ufaa kwa watu wa Kenya. Kuna watu ambao wamedhulumiwa. Ripoti inasema kinaga ubaga kuwa kuna Wakenya ambao wamedhulumiwa. Wale Wakenya wanastahili malipo. Je malipo hayo yanatosha? Kwa mujibu wa Ripoti hii kama hatutaifungua na kuirekebisha pengine malipo yanayopendekezwa ni madogo kuliko dhuluma waliofanyiwa Wakenya. Ni lazima Bunge liangalie mapendekezo hayo na fidia watakayolipwa wale waliodhulumiwa ili kuona ikiwa inatosha. Ni juu yetu sisi Wabunge kuangalia na kukubaliana. Kama kuna msamaha ni mikakati gani ambayo tumeweka na ni mchakato gani ambao tumetayarisha ili wale waliodhulumiwa kwa roho safi waweze kusamehe? Siyo tu kupendekeza msamaha kusema kuwa Wakenya wemekubaliana Ripoti imepita na eno yameisha. Ni lazima Bunge liangalie jambo hilo. Nikimalizia rafiki yangu na Mwenyekiti wa Wabunge Wafugaji Mhe. Gen. Nkaissery amesema kuwa ametajwa. Wale ambao wametajwa ni haki yao kupewa fursa ili kujulikane kama ni kweli wamehusika ama wametajwa tu. Tume yenyewe ya Ukweli Haki na Maridhiano ilikuwa na matatizo mengi; mara mwenyekiti achunguzwe mara naibu wake amejiuzuru na matatizo mengine. Kwa hivyo hata hatujui walitulia lini na wakaja na Ripoti hili. Je Ripoti hii ikitaja mtu mtu yule alipewa fursa ya kujisafisha? Sheria inahitaji kuwa ukimtaja mtu ni lazima umpe fursa ya kujieleza. Kwa hayo machache Bunge lina wajibu na naunga mkono.
Ahsante sana Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kuiunga mkono Hoja hii. Kwanza ningependa kutuma rambirambi na pole zangu kwa jamaa na marafiki waliopoteza wapenzi wao katika kaunti ya Tana River na kule Baragoi na hasa wale
Ahsante sana Bw. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchangia Hoja hii ya kuwapa Wabunge likizo ya muda ili tuweze kwenda mashinani na tuweze kuwa na wenzetu kule. La muhimu zaidi ni kuhusu fedha za CDF ambazo kwa hakika mahali pake sio kwenye benki bali zinafaa zitolewe. Tayari tumeshapata zile fedha. Ziweze kutolewa na kuwafikia wananchi. Miradi yote kule ambayo imepewa pesa ni wakati wa kwenda kutoa zile hundi za pesa ili miradi yote ambayo iko kule iweze kuendelea barabara. Vile vile ningependa kusema kwamba wakati huu ambao tunaenda likizoni tumepitisha Ripoti ya kuwa na halmashauri za kusimamia maendeleo katika kaunti. Hili ni jambo nzuri sana na litawezesha kuweko na uwajibikaji ili maendeleo yafike kule mashinani na kuzuia ufujaji wa pesa. Wakati ambao hatukuwa na halmashauri tuliweza kupata kwamba fedha hazikutumika kwa njia mwafaka. Fedha nyingi zilitumika vibaya. KERRA ilikuwa inafanya barabara moja na ile barabara pia kaunti nayo ilikuwa inazingatia kuijenga. Kukiwa na jambo kama hilo ni kuonyesha kwamba kuna fedha fulani ambazo hazikutumika vizuri. Tukiwa na mikakati kama hiyo kwa hakika tutaweza kupata maendeleo ya hali ya juu. Mwaka uliopita wa fedha za Serikali kulikuwa na fedha ambazo zilitengwa za kuwaajiri wauguzi na wafanyi kazi wa afya. Sijaona jambo kama hilo likifanyika kule kwetu. Nadhani katika nchi yote hakuna mahali wauguzi waliajiriwa. Tunashangaa hela ambazo zilitengwa zilienda wapi. Inafaa tuwe na ai tunapoelekea likizoni kwa sababu ai ni muhimu sana. Hata ndugu zetu wakitaka kwenda katika Uwanja wa Uhuru Park wapewe nafasi. Lakini nao wakifika pale wahubiri ai kwa sababu mambo yakuchezea shari ai ya nchi yetu ni jambo ambalo halitaruhusiwa na halifai kuruhusiwa. Lakini kama
Ahsante sana Bw. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kusema kwamba sauti ya Bunge hili ni sauti ya Wakenya. Rai yangu kwa wakuu wa elimu ni kwamba wazibebe sauti zetu wakijua kwanba wamebeba maoni ya Wakenya na sauti ya kila mmoja alioko hapa ambaye amezungumza kwa bughutha kuhusu hali ya elimu ilivyo; hususan masuala ya karo katika shule za upili. Serikali ilikaa na ikatengeneza Ripoti ambayo ilipeana. Ripoti ya Jopo lililoongozwa na Kilemi Mwiria iliandika kwa umakinifu kwamba: Kama sekta ya elimu nchini ingepewa Kshs11 bilioni basi kila asomaye katika shule ya upili atasoma bure isipokuwa wale wasomao katika shule za malazi ambao watalipa Kshs38969. Naikumbusha nchi hii na Serikali kwamba Kshs11 bilioni ni asilimia 0.55 ya Bajeti ya Kenya ya trilioni mbili. Ikiwa hatuwezi kusema kuwa tunachukua asilimia 0.55 ya Bajeti ya Kenya kwa sababu ya kujali masomo ya watoto wetu basi tutakuwa tunaelekeza nchi hii kwenya mrengo usioeleweka. Kenya iko katika hali ya kipekee katika dunia hii ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu wanalipa gharama za chini kuliko wanafunzi katika shule za upili. Nataka tuweke wazi kuwa kama Serikali haitahakikisha kwamba ahadi iliyowekwa na viongozi wa zai na wa sasa - kwamba fedha hizo zitawekwa - na ikiwa Bunge hili halitaweza kutenga Kshs11 bilioni ili wanafunzi wetu wasome basi tutakuwa tunapitisha mabilioni ya kujenga majumba ya mahabusu zaidi kwa sababu tutakuwa badala ya kujenga wanafunzi
Ahsante sana Bw. Naibu Spika. Ninaitwa Haika Mizighi kutoka Taita Taveta. Ninatangulia kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipatia nafasi ya kuwa hapa siku ya leo. Pili wacha niwashukuru wananchi wote wa Taita Taveta County kwa kunipatia kura zao kwa wingi kwa kuniwezesha kuwa mwakilishi wa akina mama katika Bunge hili la kitaifa nikiwa katika chama cha Jubilee. Hili si jambo la kawaida kule kwetu Taita Taveta lakini wananchi waliniamini na wakanipatia fursa hii. Ninasema ahsanteni sana na mimi niko hapa kuwawakilisha bila uoga. Naungana na wananchi wengine naungana pia na wenzangu hapa Bungeni kulijadili suala hili ambalo ni Hotuba ya Rais wetu iliyosomwa hapo jana na yeye mwenyewe. Ninaungana na akina mama wenzangu wengi. Kwa kweli tumefurahi sana. Tunamshukuru Rais wetu kwa kuwa ametutambua sisi kama akina mama na uongozi. Ametambua juhudi zetu nyingi ambazo tumefanya na bidii tuliofanya kwa ajili ya kuweza kupata nafasi hizi za uongozi. Tunasema ahsante sana kwa Rais wetu. Natumai akina mama wote wa Kenya wameliona hilo. Tunapoelekea kwenya uchaguzi tarehe 17 wanamjua rais ambaye anasimama na akina mama na ambaye anawatambua na kuwaheshimu akina mama kama viongozi. Jambo lingine pia ni kumpongeza sana Rais wetu kwa kuwa mstaarabu. Jana alipokuwa akitoa Hotuba yake Bungeni hakuchukua nafasi hiyo kuuza sera zake bali alituomba tuendelee na kazi na akasisitiza umuhimu wa kudumisha ai nchini Kenya. Kwa sababu hiyo pia ninampongeza sana. Sisi tunasema tuko pamoja na yeye. Hata tarehe 17 tutasimama nayeye. Ahsante sana.
Ahsante sana Bw. Spika kwa kunipa nafasi nitume risala zangu za rambirambi kwa familia ya marehemu Gavana wa Nyeri. Tunapotafakari kuna sababu kubwa sana ambayo ilifanya wakaaji wa Nyeri kumchagua Dkt. Gakuru kama kiongozi wao. Kama wakaaji wa Jimbo la Nakuru tunawaombea sana kwamba wakati huu wa majonzi Mungu aweze kuwasimamia kulisimamia Jimbo la Nyeri na kuisimamia familia hasa kijana wake ambaye anakalia mtihani wake. Mungu aweze kusimama naye na kumpa nguvu ili aweze kustahimili shida ambayo imeipata familia yake. Pia natoa risala za rambirambi kwa watu waliotoka katika kijiji changu na Jimbo la Nakuru ambao walipoteza maisha yao katika ajali ambayo ilitokea katika barabara ya Salgaa inayojulikana sana kama barabara mbaya ambapo tumepoteza watu wengi sana. Pia natoa risala zangu za rambirambi kutoka Jimbo la Nakuru kwa wale wote ambao walipoteza maisha yao katika ajali ya ndege ambayo ilitumbukia ndani ya Ziwa la Nakuru. Watu wawili walipatikana lakini watatu hawajapatikana mpaka sasa. Ni maombi yetu kwamba Mungu aweze kuzisimamia familia zao na kuwapa nguvu. Ninawaza kwamba Bunge hii pia iangalie vile tutatatua ama kuchunguza mambo ya ajali ambazo hutokea kila mara. Nafikiri tukifanya uchunguzi kuhusu ajali zinazotokea itakuwa ni njia moja ya kupunguza ajali katika nchi yetu. Kama Bunge bado tutarudi hapa tuongee tena na kuona vile ambavyo mambo ya ajali yanaweza kutatuliwa katika nchi yetu. Poleni sana kwa wale wote ambao walipatwa na ajali na familia zao.
Ahsante sana Bwana Spika kwa kunipa fursa hii ya kuongea juu ya suala hili la Hazina ya Uwezo. Ni kweli kwamba Wakenya wamengojea kwa muda mrefu. Nasimama kumuunga mkono kiongozi ya walio wengi hamu Bungeni. Wakati umefika; chelewa chelewa utakuta mtoto si wako. Bwana Spika tumengoja kwa muda mrefu sana. Wakati tumengojea hivi kuna umuhimu tukubali kwamba Kenya imebadilika na katika Bunge hili hatuko peke yetu bali tuna wenzetu. Yale ambayo wametaka tubadilishe ni machache tu. Mimi nimeyapendelea hayo mabadiliko kwa sababu kuna umuhimu Serikali kuu ihusishwe wakati tunafanya hizi kazi. Nimependa pale walipotaja kuwa mwenye kusimamia masuala ya maendeleo ambaye ni mfanyikazi wa Serikali kuu na Msimamizi wa Pesa ambaye pia ni mfanyikazi wa Serikali kuu wataweza kuileza Serikali kuu yale yanayoendelea. Kina mama vijana na wazee ambao wamejiunga kwenye vikundi hivyo wataweza kufanya kazi kutumia pesa hizi taslimu Ksh6 bilioni ambazo zinatakikana kutumika humu nchini ili kuleta maendelea. Muda unakwenda na kwa vile mwaka uko karibu kuisha naomba wenzangu wamuunge mkono kiongozi wa walio wengi humu Bungeni ili tupitishe hii mara moja na tufanye kazi pamoja na wananchi kuhakikisha kuwa maendeleo mashinani yamewawezesha watu wetu kuishi na kukabili matatizo yaliyoko. Hii ni kwa sababu kutafuta hela kwenye mabenki inahitaji kuwa na vyeti vya kumilki ardhi na mambo mengi ambayo Wakenya wengi hawana hasa akina mama na vijana. Ahsante sana Bwana Spika. Naunga mkono.
Ahsante sana Bwana Spika kwa kunipa nafasi au fursa hii ili nichangie jambo hili ambalo ni la kuleta raha furaha basheshe na bashasha. Hiyo ni lugha ya Kiswahili. Nataka kukupongeza kwa sababu utakuwa katika kumbukumbu za vitabu vya Bunge kama aliyeleta mabadilisho - that is reforms - ambayo tumeyaona katika Bunge hili la 12. Nakushukuru kwa sababu lugha ya Kiswahili ina lahaja mbali mbali. Mimi kama Mkalenjin kutoka Nandi tuko na lahaja za Kinandi. Mjaluo pia ako na lahaja zake za Kijaluo. Wale ambao wanaongea lugha ya Kiswahili kutoka Pwani si kwamba hawana lahaja katika lugha hii. Nashukuru kwa sababu tumezindua Hoja ya Kanuni za Kudumu za Bunge ili sisi sote tupate kujumuika katika hali ya kuchangia na kukuza lugha hii ili ikubalike Afrika Mashariki na ya Kati. Ndugu wapenzi Wabunge wenzangu lugha hii si ngumu kuelewa. Siku ikitengwa maalum ya kuchangia katika lugha ya Kiswahili sisi sote tutaenda maabarani kuangalia vizuri ni lugha gani na msamiati gani tutatumia. Niko na kitabu ambacho Waswahili na wale ambao wanaongea lugha ya Kiswahili na ya King'eng'e wamejaribu kuidhalilisha ili tuipate katika lugha ambayo inafaa. Inaitwa Istilahi za Kiswahili. Hapo ndipo tunaweza kupata mambo yanayohusiana na Kizungu ili tuchangie Miswada na Hoja ambazo tutapata hapa Bungeni. Nashukuru sana kuona Mheshimiwa Junet anajikakamua kabisa kuelewa lugha ya Kiswahili kwa njia zote. Kupotea njia ndio kujua njia. Kutoka leo tukianza kuongea lugha hii ambayo tunaienzi na kuipenda wakati tunapata nafasi ya kuchangia Miswada na maono yetu tutaongea kwa wepesi na kuizoea zaidi. Kumalizia ni kwamba lugha ya Kiswahili inakua. Kuna eno ambayo tutaazima kutoka lugha nyingine kama Kizungu na lugha inayohusiana na kitaalamu. Wataalamu wengine kama madaktari wako na lugha yao. Tunaweza kuchukua kutoka kwa lugha yao katika ile hali ya kujieleza. Nashukuru kwamba mwaka huu tutaongea lugha ambayo itakuwa rahisi kwa wananchi ambao tunawaongoza kuelewa ni nini ambacho tunasema kama Wabunge. Sheria ikitungwa katika lugha ambayo wananchi wanaelewa ni rahisi kwao kufuatilia maelezo matukio na maendeleo hapa Bungeni. Ili nisichukue muda mrefu nachukua nafasi hii kukupongeza na kushukuru wenzangu na wale wote ambao wamefanya ukalii na kutafi hizi Kanuni za Kudumu katika lugha ya Kiswahili. Nawapongeza sana. Tukae tukijua kwamba lugha ya Kiswahili inakua siku baada ya siku. Kwa hayo machache nashukuru kwa nafasi na fursa ambayo nimepata kuchangia wazo hili.
Ahsante sana Bwana Spika. Kwa niaba ya wakaazi wa Eneo Bunge la Imenti Kusini familia yangu na mimi mwenyewe nachukua fursa hii kuomboleza kuachwa na Baba Moi. Rais Moi alifanya mambo mengi sana hapa nchini Kenya kwa mfano elimu na hasa kusimamia demokrasia kwa kukubali kuondolewa kwa Kifungu cha 2A cha Katiba yetu pamoja na vile alivyopeana uongozi. Wakenya wengi walifikiria hataachilia uongozi sababu alikuwa Rais kwa miaka 24 na Naibu wa Rais kwa miaka minane. Sisi kama viongozi tunaiga mfano wake na kuombea familia yake na Wakenya wote wakati mwema tunapomlaza Rais Moi wiki hii.
Ahsante sana kwa kuniongezea muda Ningeomba Kamati iwape adhabu kali zaidi kwa sababu hawajaonyesha nia ya kutekeleza lolote Ni muhimu kwetu sisi kutetea haki za wafanyikazi hawa kwa sababu hawako kwenye muungano wa wafanyikazi wowote Licha ya kazi iliyofanywa na Kamati kampuni hii imeonyesha kuwa haina nia ya kutekeleza lolote na ningependa vitengo vya Serikali vichukue hatua na kufuatilia zaidi kuhakikisha kuwa haki ya wafanyikazi wa Kenya inalindwa Ahsante sana
Ahsante sana kwa nafasi hii umenipa niweze kuchangia Hoja hii inayoendelea wakati wa sasa kuhusiana na wale watu ambao wako na changamoto ya miili yao jinsi ambavyo wako na ulemavu. Jambo hili linaguza kila mtu. Ni jambo ambalo kila mtu anahitaji kulitilia maanani. Katika nchi hii tunapopanga kazi na ratiba zetu kila wakati ni vyema tuwe tukiwakumbuka wale wenzetu wanaoishi na ulemavu. Hata tunapoongea mambo ya ulemavu ni kweli kwamba huduma za afya nchini humu zimegatuliwa. Kule mashinani katika kaunti zetu wangeweza kuweka bajeti ya kuhudumia watu hao. Wakati tunaposema BBI itaweka fedha nyingi kwa kaunti zetu ningependa kaunti zitilie jambo hili maanani maanake kule ndiko wanaweza kujua idadi ya watu walioko katika wadi zao na wale walemavu. Itafaa wapitishe bajeti wakiwa na idadi hiyo ndio watu wapate huduma kwa njia ambayo inafaa binadamu. Wakati mwingine tunachukulia hao watu kama kwamba hawafai. Hata unakuta kwamba wanafichwa nyumbani mwetu. Kama vile kila mtu amesema hapa huu ni mtihani ambao kila mtu anaweza pita. Lakini wakati mwingine jinsi ambavyo tunawachukulia walemavu si kama binadamu ama njia ambayo inamfurahisha Mwenyezi Mungu. Tukiongea hapa kuhusu vifaa ambavyo wanatumia kuna jambo moja huko kwetu Baringo ambalo limenisumbua na nataka kulitatua. Nashangaa kama Kenya nzima iko na hiyo shida. Katika kaunti zetu tukiangalia sehemu za biashara ni ngapi zinavyoo vinavyo ambavyo vinawafaa walemavu? Hii ni kuonyesha hatuwakumbuki. Walemavu pia wanafanya biashara lakini hawana vyoo vinavyo wafaa. Wamama ndio wameathirika zaidi kutokana na hii shida. Kwa sababu mama akiwa na mtoto ambaye hawezi kutembea hiyo ni shida yake. Huyu mama hubaki nyumbani na haendi shambani. Wakati mwengine unapata mama yule bado ana umri mdogo lakini amezeeka kwa sababu ya mawazo. Hana fedha za kulisha mtoto ama kununua bidhaa za kumsaidia. Sisi kama viongozi wa nchi hii tuwape kibao mbele walemavu ili waweze kuiishi kama watu wengine. Mheshimiwa ambaye ameongea mbele yangu amesema kwamba kwa muda mfupi alikuwa na ulemavu lakini sasa ako sawa. Bado anakumbuku kwa ugumu na ndio anahitaji sisi kuwasaidia walemavu. Nashukuru kwa kupata nafasi kuchangia Hoja hii kwa sababu ni nzuri. Pia nimeona wenzangu wanachangia kwa njia inayofaa. Naunga mkono mia kwa mia. Serikali ya Ugatuzi pamoja na Serikali kuu wanapaswa kuketi pamoja na kuangalia vile walemavu wataishi vyema hapa nchini. Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Ahsante sana Mhe Naibu Spika wa Muda. Kwanza nataka kumshukuru Mhe. Odanga kwa kukubali maoni yangu kwamba alete Hoja hii na akafanya hivyo. Hoja hii ni muhimu sana kwa sababu hali ilivyo hivi sasa ni kwamba nchi yetu inaelekea mahali pabaya sana. Vijana wanachoma mashule wazee wanafanya mapenzi kiholela bila ya kujali vijana wanafanya mapenzi wakati usiofaa watu wengine wanaiba na kufanya mambo chungu nzima ambayo hayana maana na ambayo yanamuudhi Mwenyezi Mungu. Hii yote ni kwa sababu watu hawana elimu ya kidini ya Kikiristo Kiislamu Kibudha na kadhalika. Haya yote ni kwa sababu Serikali haijashugulika kuhakikisha ya kwamba inaweka masheikh makasisi na watu wengine wa kidini ambao wangeweza kuwafanya vijana wawe na maadili ya kidini kutoka awali. Hii ni muhumi sana na inataka kufuatiliwa. Ikiwa tunataka hali hii iwe sawa ni lazima tuirekebishe Katiba ya nchi hii haraka inavyowezekana ili shida hizi ziweze kuondoka. Nilikuwa nije huku siku ya Jumatatu lakini ilibidi nije June kwa sababu shule mbili katika sehemu yangu ya uwakilishi Bungeni zilichomwa na vijana na hayo yote ni kwa sababu hawataki kufuata maadili ya kidini. Namuunga mkono kikamilifu Mhe. Odanga kwa kuleta Hoja hii Bungeni. Nawaomba Wabunge wenzangu waipitishe haraka iwezekanavyo. Kwa hayo machache naunga mkono.
Ahsante sana Mhe Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hii kuhusu mtoto wa kike. Sisi tunaoishi katika sehemu kame sio kwamba tuliomba kuishi kule bali ni maumbile ya Mwenyezi Mungu. Serikali zilizopita zilitutenga ndio maana tumeamua kuwa na Hoja kama hii. Namuunga mkono Mhe. Dukicha kwa kuleta Hoja hii. Kwa kweli hakuna shule katika sehemu kame. Hata kama mtazungumzia CDF tunafahamu kwamba imekuja juzi tu. Miaka ya nyuma shule hazikujengwa. Kuna sehemu za wafugaji wanaotafutia wanyama wao lishe. Wao hata hawana nafasi ya kusoma. Ndiposa tunaonelea kuwe na shule ambako watoto watalala na kusoma. Mimi nazungumzia watoto wote wa kike na wa kiume wanaoishi katika sehemu hizi kame. Mwenzangu amesema kuwa nchi nzima inafaa kuangaliwa kupitia Hoja hii. Lakini kuna kule ambako ni Kenya na kule ambako ni Kenya nusu. Kwa hivyo Kenya nusu nayo ivutwe angalau ifike karibu na Kenya nzima ndio tujihesabu kuwa katika nchi moja. Hii haitafanyika mpaka mambo ya elimu yaangiliwe na yatekelezwe kwa wakati unaofaa. Kwa sababu ya ukosefu wa elimu katika maeneo kame ile hesabu inapoletwa kwamba watu waajiriwe kwa kiwango fulani sisi tunakosa hizo nafasi. Kwa upande wa kuwaajiri askari au wauguzi tunakosa nafasi. Tunaletewa watu kule kwetu ambao hawako tayari kufanya kazi kule. Mtu anaajiriwa kazi leo na baada ya miezi mitatu anaomba kuhamishwa. Anasema huko kuna shida nyingi. Kwa hivyo tupewe hizi nafasi. Serikali inafaa kutoa pesa za kutosha na kutujengea mashule ili watoto hawa wasome na kuwa watu ambao watatuhudumia kule kwetu ambako wengine hawataki kufanya kazi. Kama alivyosema mhe. Shaban wengine wanapatiwa pesa za kuwsaidia katika sehemu ambazo zina uzito wa utendaji wa kazi lakini hawastahili kupewa hizo pesa na
Ahsante sana Mhe Spika Jambo hili ambapo wanyama wa pori wanavamia na kukula mimea ya wananchi ni jambo ambalo tumelizungumzia sana katika Bunge hili Hasa mimi nimezungumza kuhusu eneo Bunge langu la Endebess ambapo tuko na Mbuga ya Wanyama ya Mount Elgon Jambo ambalo limeniguza katika hii Petition ni kwamba wamesema askari wanapiga wananchi Hiyo ni ukweli kabisa Kwa hivyo nataka Kamati inayoongozwa na Mjumbe wa Maara itakapochunguza hili jambo tunataka kujua kwa nini askari wa hifadhi za wanyama pori wanashambulia wananchi Kwa nini wanapiga wananchi? Hilo ni jambo ambalo ni nzito sana Askari hao hata kule Endebess wamehusika katika kupiga wananchi hata wamama ambao huenda kuokota kuni wanapigwa Kwa hivyo ni jambo ambalo linatakikana kushughulikiwa Tunataka kujua ni hatua gani Wizara itachukua kwa wale askari wanaopiga wananchi Sijui kama hiyo pia ni kati ya kazi za kuchunga wanyama ama namna gani Kamati itakapokaa tungependa sisi ambao tunaishi karibu na hifadhi za wanyama watuite Ahsante Mhe Spika
Ahsante sana Mhe Spika Kupitia Kanuni ya Kudumu Nambari 44 (2) (c) naitisha jawabu kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama kuhusu upigaji risasi uliosababisha kuumia kwa Bw Sadat Salim Abdallah mwenye umri wa miaka 42 Bw Fahal Salim Abdallah mwenye umri wa miaka 35 na kuuawa kwa Amur Ahmed Salim kijana mdogo aliyekuwa na umri wa miaka 24 risasi zilipomiminwa kwenye miili yao Alhamisi iliyopita tarehe 11 Sadat Fahal na Amur walipigwa risasi kadhaa na watu wanaosemekana kuwa polisi katika hali isiyoeleweka Walikuwa nje ya duka dogo la M-PESA eneo la Kaloleni Mvita Yaliyotokea ni kifo cha Amur na majeraha makubwa kwa Fahad na Sadat Mhe Spika la kushangaza kusikitisha na kutia wasiwasi zaidi ni kuwa polisi hawajafanya uchunguzi wowote hadi leo Hawajarudi kwenye eneo ambako uhalifu huo ulitokea Hawajaongea na majirani ama watu ambao waliona tukio hilo wala hawajaitisha rekodi za CCTV katika maeneo ya karibu mahali pale Juzi nikiwa hospitali nilithibitisha kuwa polisi hawajawafuatilia wale walioumizwa ili kuweza kuchukua kauli zao Nimeongea na familia ya marehemu na hadi leo hawajajulishwa chochote wala kuambiwa waende waandike maelezo yoyote Mhe Spika kupitia haya twastahili jawabu kupita kwa Mwenyekiti wa Usalama kuhusu mambo matatu yafuatayo: (i) Serikali imeweka mikakati gani kuhakikisha kwamba uchunguzi unafanywa ili wale waliosababisha madhara na kifo wapelekwe mbele ya haki? (ii) Ni mikakati gani Serikali inaweka kuhakikisha kwamba familia za walioathirika kwenye mkasa huu wamepewa fidia ikiwemo kulipa malipo ya hospitali na ni lini jambo hili litaweza kufanyika na kumalizika? (iii) Serikali ni lazima iwe wazi na kutuelezea imeweka mikakati gani kuhakikisha kwamba kuna hali ya usalama haswa wakati huu tulioko wa dijitali Wameweka mikakati gani ili mambo kama haya yakitokea tuweze kujua bila ya kuchelewa wahalifu ni akina nani? Ahsante Mhe Spika
Ahsante sana Mhe Spika wa Muda lakini mimi nilikuwa nimeweka ombi kwa Hoja iliyopita Ahsante
Ahsante sana Mhe Spika Wakati ambao ulinihitaji sikuwepo kwa sababu ya sherehe ya Eid-ul-Fitr lakini leo nina furaha kwa sababu umenipatia nafasi ya kujitetea Kwanza kabisa sijui mlalamishi ni nani na singelipenda kuwa mwingi wa eno ila niseme kwamba mambo hayo yamepitwa na wakati Mhe Moses Kuria alitoa ushahidi kwa kusema kwamba yeye ni miongoni mwa Wabunge waliopokea hongo Sijui nitamjibu nani kwa sababu aliyeleta haya malalamishi simjui ni nani Ni vile tu alitaja jina langu bila sababu zinazofaa kuhusishwa nami Fauka ya hayo Mhe Moses Kuria alisimama ndani ya Jumba hili na akatoa hongo ya Kshs100000 pesa ambazo aliziweka wazi na akasema alikuwa miongoni mwa wale waliopokea hela hizo Nadhani huo ni ushahidi tosha Singelipenda kupoteza wakati mwingi kwa mambo ambayo yamewekwa wazi na Mbunge mwenzetu Hili si jambo la kwanza kuwahi kutajwa katika Bunge hili Utakumbuka Mhe Spika nikikurudisha nyuma wakati ambapo kulikuwa na masuala ya sukari Baadhi ya Wabunge walisema kwamba wapo wenzao waliopokea baina ya Kshs10000 na Kshs30000 ndani ya choo ili wapitishe masuala fulani katika Bunge hili Kwa hivyo kwa Mbunge mwenzangu kusimama na kunitaja mimi Mohamed Ali bila ushahidi tosha inaonekana kwamba ni kupelekwa katika Kwanza sijui ni nani alisema mimi Mohamed Ali nilizungumza katika hili Bunge na kusema mambo hayo Ningependa kujua Ndiyo maana nilipokuandikia barua nilitoa ombi la kusema itakuwa vyema nikijua ni nani ili niweze kujibu kulingana na masuala aliyouliza Ingawa hivyo muda umeyoyoma Ni wakati muhimu kusonga mbele Tugange yajayo ili tuendeleze nchi hii Tuwasaidie wananchi kwa kutunga sheria Kwa hivyo Mhe Spika siwezi kusema nitaomba msamaha kwa jambo ambalo silijui Watu huomba msamaha kwa mambo ambayo wanayajua Kwa kumalizia ushahidi uliotelewa na mwenzangu Moses Kuria wa Kshs100000 ni ushahidi tosha katika Bunge hili Kwa hivyo Mhe Spika naomba
Ahsante sana Mhe. Mwenyekiti. Kusema kweli tuko hapa kuhusisha wakenya wote. Kama kuna jambo lolote la kutenga wengine basi hatutendei Wakenya haki. Kwa hivyo ni vyema kufanya mambo haya yote kwa uwazi na tuandike maandiko yatakayosomwa na wote kwa sababu hakuna Mkenya nusu; Wakenya wote tuko sawa na tunastahili kuheshimika sawa. Naunga mkono.
Ahsante sana Mhe. Naibu Mwenyekiti Wa Muda. Katika nchi yetu ya Kenya kumekuwa na ukora mwingi. Ukiingia ofisi za Serikali wakati wanataka kupeana zabuni unasikia mtu mwingine kwa mfano. Stephen amepewa stakabadhi kumi kwa mtu moja. Ni kwamba ikiwa hiyo kazi ilikuwa ya Kshs.100 milioni yeye anasema ya kwamba kwa sababu mtu mmoja ndiye amepewa kazi hiyo wacha niweke iwe Kshs300 milioni. Kama ni ya Kshs300 milioni anafanya iwe Kshs500 milioni. Kama ni ya Kshs500 milioni anafanya iwe Kshs600 milioni. Lakini usisahau hiyo kazi ni ya Kshsh100 milion. Hiyo kazi
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika kwa fursa hii. Ningependa kumpongeza Mhe. Gatobu kwa kuleta Hoja hii hapa. Ilivyozungumziwa mara nyingi Kifungu 53(1)(b) kinatoa kwa uzito haki kwa kila mtoto kupata elimu na kinasema kwamba ni lazima. Bunge litakapopata fursa ya kutekeleza Kifungo hicho cha Katiba ni bora itafute ni vipi itawasaidia wale watoto. Katika Hotuba ya kwanza ya Rais wa Taifa hili Baba wa Taifa Mzee Jomo Kenyatta alitoa changamoto tatu kubwa ambazo ni umaskini kutojua kusoma na kuandika na maradhi. Ni kwa nini kutoka miaka 50 iliyopita mpaka leo hatujapata zuluhisho la matatizo haya? Tunapozungumzia kuhusu elimu ya watoto elimu ya watoto wanaoishi katika sehemu kame ni nadharia. Ikiwa watoto wa Kenya wana matatizo watoto wa kutoka sehemu kame ya Kenya au watoto wa wafugaji wana matatizo mara kumi ukilinganisha na watoto wale wengine. Kwa nini nasema hivyo? Ni kwa sababu watoto wa wafugaji ni watoto ambao wanategemea mazingara. Ikiwa kumenyesha na kuna nyasi ya kutosha wanapata fursa ya kusoma. Kukiwa na ukame inabidi watoto hao watoke wanapoishi ili watafute malisho ya mifugo. Watoto hao wanaathirika. Hoja hii inazungumza juu ya mtoto mwelevu. Watoto welevu ni tegemeo la taifa lolote. Kama watoto welevu ni tegemeo la nchi hii katika siku za uzoni lazima kuwe na mikakati. Tuna pesa ngapi katika kila sehemu ya uwakilishi Bunge kuwawezesha watoto hao kusoma? Nasikitika kwamba katika sehemu ninayotoka hasa Boka Ilii na Asa mpaka leo watoto hawapati fursa ya kupata ufaa ya elimu ya kawaida. Kwa hivyo naunga Hoja hii mkono ilivyorekebishwa ili watoto kutoka jamii maskini waweze kupata elimu kama watoto wengine.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika kwa hii fursa ambayo umenipatia. Ninasimama kumuunga mkono Mbunge wa Igembe ya Kati kwa haya malalamishi ambayo ameleta kwa niamba ya wananchi wake. Ni kweli Wizara inayohusika na wanyama pori ina tabia ya kuchukua ardhi ya wananchi. Ombi langu pia lipo njiani. Kuna malalamishi kutoka watu wa Taita Taveta. Walikuwa na malumbano kwa sababu Wizara inayohusika imechukua ardhi yao kama vile Mhe. aliyenitangulia wa Wundayi amesema. Kutoka Maungu Voi Tsavo Taveta na sehemu za Mwatate KWS imechukua ardhi kubwa sana ya wananchi. Tuliuliza Wizara inayohusika itengeneze jopo ambalo linahusisha wananchi wa hapo na maafisa wa Serikali ili wajaribu kutatua mzozo huo. Lakini jambo hili limechukua muda. Ni vyema Kamati ya Bunge inayohusika ijaribu kuyatatua maswala kama haya ambayo yameletwa na Mbunge wa Igembe ya Kati. Pia inafaa kuangalia maswala katika mbuga za wanyama nchini na kuyatatua kwa haraka iwezekanavyo. Kwa hayo machache nakushukuru kwa hii fursa ya kujadili kuhusu hili swala tata la ardhi baina ya mbuga za wanyama na wananchi.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Hakuna taifa duniani ambalo litajigamba kujimudu kibiashara kijamii na kiuchumi. Ndiposa mataifa duniani ikiwemo Ushirikiano wa Nchi za Ulaya (European Union) wanatafuta ni vipi watashirikiana kuboresha hali ya maisha ya watu wanaoishi katika sehemu hizo. Ndiposa pia Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imeungana ili tufungue soko na tushirikiane kibiashara kijamii na kisiasa. Leo itifaki iliyowekwa mbele ya Bunge hili inatupatia ushirikiano wa kijeshi. Kwa nini wanajeshi washirikiane? Kuna masuala ya mafunzo ya kijeshi na kuna ushirikiano baina yao. Dunia ya leo inakumbwa na ugaidi. Tatizo la ugaidi si tatizo ambalo taifa moja linaweza kusimama na kutatua. Hivyo basi ni lazima Afrika Mashariki ije pamoja. Ni lazima wanajeshi wa Afrika Mashariki waweke sahihi itifaki hii ili tuweze kupambana na kushinda adui anayekumba taifa la Kenya leo. Mhe. Naibu Spika nimesikia matatizo kama yale ya kisiwa cha Migingo. Hayo ni matatizo ya kawaida. Katika mwili wa mwanadamu kuna ulimi na meno ambayo hushirikiana sana katika kufanya kazi. Hata hivyo saa zingine viungo hivi hukwaruzana. Licha ya tatizo la kisiwa cha Migingo Uganda inatoa biashara kubwa kwa taifa la Kenya. Kwa hivyo ni vipi tutakuja pamoja tutatue matatizo haya yanayokumba Afrika Mashariki? Nimesimama kuunga mkono Hoja hii ili tushirikiane kijeshi kisiasa na kibiashara katika eneo la Afrika Mashariki. Ahsante Mhe. Naibu Spika.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Hili ni jambo ambalo ni sugu sana. Kusema kweli dakika 15 zitakuwa chache sana. Hivi tunavyozungumza kuja kwa SGR ni maendeleo lakini sasa hivi kulingana na maelekezo kuwa kasha lolote linalokuja lazima libebwe na SGR mbali na lile kasha ambalo latakikana libakie Mombasa watu wengi wamefunga maduka. Ukiangalia barabara ya kutoka Nairobi hadi Mombasa kumekuwa na vitongoji na vijiji kadhaa wa kadhaa ambavyo miaka yote viko na shughuli nyingi. Lakini kutoka shughuli hii ianze kazi zote zimekufa. Haya si makosa yetu. Kazi ya SGR ilipofanywa mategemeo ni kuwa ilikuwa ijilipe yenyewe. Lakini kulingana na mipango ile ipo imeshindwa kujilipa. Haiwezi kulazimisha wawekezaji waingie katika hasara ya kupoteza pesa. Wengine wamechukua pesa katika mabenki. Naomba hili suala lipewe muda mrefu kama vile wenzangu walizungumza ili tuweze kulichangia kisawasawa. Ahsante.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii ili nami nichangie Hoja hii. Namshukuru mhe. Ganya kwa kuleta Hoja hii katika Bunge hili ili tuizungumzie. Mambo ya wanyama wa pori yanafaa tuyazungumzie kwa sababu sisi ndiyo tunaishi nao. Tulizaliwa na kuishi na hao wanyama na tumewachunga kama vile tunawachunga ngombe na mbuzi wetu. Lakini ajabu ni moja. Wale wanaowachunga na wale wanaoangalia hakuna faida wanayopata kutokana na wanyama hao. Kuua ndovu ama mnyama yeyote wa pori Wenzangu wamepata soko kubwa na ingefaa ijulikane ni ya nani. Sheria ingewekwa ili tujue soko hiyo ni ya nani. Hiyo ni kwa sababu soko ya meno ya ndovu imewaangamisha watu wengi. Soko hilo linafanya wenyeji wa eneo letu la Samburu Wamaasai na wafugaji wote kuumia kwa sababu ndovu wanauliwa na kutolewa meno. Wakazi kama sisi hatukuli nyama ya ndovu. Kwa hivyo unapata ndovu kama 20 wameuawa na wenye wanaowachunga. Hujui wanauliwa namna gani. Kwa hivyo ningesema kwamba sisi wengine tunaumia kwa sababu vifaro pia wameisha. Wamebaki kwa wazungu na katika mashamba makubwa. Ukienda katika hifadhi za wanyama wa pori kama vile Hifadhi ya Wanyama ya Samburu hutapata ndovu. Ukipata labda mbili au tatu ukibahati. Mhe. Naibu Spika mashamba ya ranches siku hizi hayafugi ngombe. Yanahifadhi wanyama wa pori. Ningeomba Serikali ilipishe mashamba hayo kodi kwa sababu ya kuhifadhi wanyama. Wanyama wanapatikana katika mashamba hayo peke yake. Katika biashara hiyo pia tunasikia kuna mashini ya kusaga meno ya ndovu. Yanabebwa kama unga na kusafirishwa. Kwa hivyo usalama katika viwanja vya ndege lazima uimalishwe kwa sababu ndovu wamekwisha. Kuna pahali pengine hapa nchini ambako hakuna ndovu. Wamebaki tu katika pande za Wamaasai na Taita. Ni sehemu chache ziko na ndovu na wanyama wengine wa misitu.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii kuzungumzia sheria hii kuhusu wanyama wetu. Kwa sababu wenzangu wameongea zaidi kuhusu mambo ya wafugaji wa mbuzi na ng'ombe kwa kweli hizo ndizo shida zinazowakumba wachungaji. Ni muhimu sana kuwe na sheria hii ili tupate bodi ya kuangalia mambo hayo. Mara kwa mara wafugaji wanapata shida kwa sababu hawana namna nyingine. Wanategemea wanyama wao pekee. Hakuna sheria katika Kenya yetu ya kulinda wanyama wao. Ndio unaona shida zote za ukame maji na zingine zinawakaba wanaochunga wanyama wetu. Ni ukweli tukipata hiyo bodi tutakuwa na sheria ya kuchunga wanyama wetu. Sheria imewekwa kwa kila kitu kinachotengenezwa katika Kenya yetu. Kuna bodi ya sukari bodi ya kahawa bodi ya majani na bodi ya kila kitu. Tunaomba tuipitishe hii sheria kwa sababu itasaidia wafugaji wote katika Kenya nzima. Tumetembea na tukaona vile wafugaji wanachunga wanyama wao na vile sheria imewekwa. Tukipitisha hii sheria itawasaidia wafugaji na wanyama wao. Sheria hii itatusaidia hasa katika wakati wa ukame kama huu. Mwenzangu amesema hajui mahali Kshs450 milioni zimeenda na hiyo pesa inaendelea kununua wanyama katika kila pembe ya Kenya ambayo imeathiriwa na ukame. Ningeomba pesa ipitishwe ili isaidie pande za wanyama yetu. Wafugaji wanaumia sana katika uchungaji wao. Ndio maana kila mtu anasema wafugaji wamehama wamepeleka ng'ombe na mbuzi zao kwa mashamba ya watu. Wameenda kulisha mifugo yao huko. Wametoka upande huu wanaenda tena upande mwingine. Nafikiri sheria hii ya kulinda wanyama ikipitishwa itasaidia kila mtu. Pia tunaomba ile idara inasimamia wanyama iangalie ni njia gani itaweza kusaidia kwa sababu pesa nyingi sana zinaitishwa hata kwa mashirika yasiyo ya Kiserikali kuhusu wanyama wetu na hazisaidii. Utakuta tu zinaitishwa na haziwezi kusaidia. Tukipata bodi tunaomba iangalie mambo ya maji zaidi katika pande za wafugaji kwa sababu hiyo ndiyo shida nyingine mbaya zaidi wakati wa ukame. Pia mambo ya ugonjwa vile wenzangu wamesema. Magonjwa mengi sana hudhuru wanyama.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii nichangie Mswada huu wa Mahakama Kuu. Mwanzo nataka kusema kwamba naunga mkono Mswada huu. Nafurahi kuwa Mswada huu umeweza kuja hapa Bungeni hususan kwa sababu napenda sana kutetea haki za wanyonge. Wakenya wengi wako katika hali hiyo. Pia Wakenya wengi hawana njia ya kupata haki katika nchi hii. Wananchi wengi sana huteseka sana kwa kukosa haki hapa nchini. Kitu cha kwanza ambacho ningetaka kuangazia ni kwamba Mswada huu unaongeza idadi ya mahakama kuu humu nchini. Hivi sasa mahakama kuu nchini ni 20 pekee. Zikiongezeka huenda kila kaunti itapata mahakama kuu moja au zaidi kutegemea ukubwa wake. Mhe. Naibu Spika sheria hii kama nilivyosema itapeleka haki karibu na mwananchi. Mara nyingi walala hoi huwa wanashindwa kwenda katika mahakama kwa sababu ya ukosefu wa pesa za usafiri wa mara kwa mara. Kwa hivyo mabwenyenye ama wenye kudhulumu watu wengine ama wenye pesa ndio wana nguvu za kwenda mahakai. Wakenya wengi hukosa kupata haki katika mahakama kuu za humu nchini. Kwa hivyo hili ni jambo ambalo limenifurahisha. Jambo lingine ni kwamba kutokana na kuongezeka kwa mahakama itabidi tuongeze bajeti za mahaka humu nchini ili tuweze kujenga mahama kuu nyingine ili wananchi waweze kufaidika kama sheria hii inavyosema. Licha ya maswala tofauti ya kisiasa nawaomba Wabunge wenzangu kuwa wakati wa kutayarisha Bajeti tusaidiane ili senti ziweze kupatikana ili mahama nyingi yaweze kujengwa ndio Wakenya wengi waweze kufaidika hususan walala hoi. Mhe. Naibu Spika watu wengi huteseka kutokana na masuala kama ubakaji wa watoto wadogo na wanawake na kudhulumiwa kwa wanawake mabwana zao wanapofariki. Mara nyingi watoto mayatima hunyang'anywa urithi wao na kadhalika. Kwa hivyo hili ni jambo la busara. Jambo lingine ni kwamba mwananchi ataweza kupeleka kesi yake katika mahakama kuu na akishindwa anaweza kukata rufaa hapo hapo - si lazima asafiri kwingineko. Mimi nimeleta Miswada mingi hapa Bungeni kuhusu watoto wa Kiislamu waliodhulumiwa katika baadhi ya shule za upili za umma humu nchini. Kwa mfano hivi sasa kuna kesi katika Kaunti ya Isiolo lakini kukata rufaa imebidi kesi hiyo ipelekwe Kaunti ya Meru. Hii inamaanisha kwamba ni lazima mashahidi wasafiri na walale mahotelini. Kwa hivyo sheria hii itawasaidia mwananchi. Mhe. Naibu Spika kuongezeka kwa mahakama kuu kutafupisha muda wa kusikilizwa kwa kesi na mahakama. Kuna kesi ambazo zimekuwa mahakai kwa miaka kumi ama zaidi. Katika hali ilivyo sasa mmemfanya mwananchi mlala hoi kutumia pesa nyingi - pesa ambazo hana - kufuatilia kesi hiyo. Kwa hivyo wanaoshinda kesi mara nyingi ni wale watu ambao wana pesa. Kifungu cha 26 kinazungumzia mbinu zingine za kutatua mizozo. Kwa kweli hili ni jambo nzuri sana - ni jambo nzuri kuliko yale ambayo nimeshayazungumzia. Kupitia mbinu hiyo mwananchi anapokuwa na kesi hatohitaji kuwa na wakili. Kama tunavyojua mawakili huitisha pesa nyingi sana kuanzisha kesi yoyote. Mara nyingi inabidi mtu alipe angalau Ksh50000 kuanzisha kesi. Mwananchi wa kawaida hawezi kuwa na hela hizo. Kwa hivyo kifungu hiki kinachozungumzia mbinu hiyo kitamuwezesha mwananchi kwenda kujiwakilisha mwenyewe mbele ya mpatanishi ili aweze kueleza kesi yake. Kesi yake iweze kusikilizwa bila yeye kutumia pesa nyingi kuajiri wakili. Mhe. Naibu Spika sheria hii itaongeza nafasi za kazi katika Mahakama Kuu. Wazazi waliuza ardhi na rasilmali nyingine za familia zao na kuwaelimisha vijana wao katika vyuo vikuu. Nafasi za kazi zitakapopatikana vijana hao watapata ajira. Hivi sasa wengi wa vijana ambao wamehitimu katika vyuo vikuu hawana kazi. Vijana hao wanaishia kufanya kazi ya kusukuma mikokoteni na kazi nyingine ndogo ndogo. Baadhi yetu wanaweza kusema kwamba kama nchi hatuwezi kulipa wafanyikazi zaidi kwa sababu gharama ya ajira katika sekta ya umma iko juu lakini tukiwa na wafanyikazi wengi na ikiwa haki itapatikana kwa wepesi na kwa haraka tutaweza kuokoa fedha nyingi zinazopotea kutokana na kucheleweshwa kwa utendaji haki na mahakama zetu - hali ambayo inaumiza uchumi wetu. Kwa hivyo badala ya kuendelea kupoteza pesa kupitia hali hiyo nchi yetu itaokoa pesa. Mwisho ningependa kuwahimiza wale ambao watakuwa wanawaajiri mahakimu wakuu wahakikishe kwamba watu kutoka makabila tofauti humu nchini wameajiriwa pale nafasi za ajira zitakapotokea. Hususan wananchi katika eneo la Pwani ambako nimetoka wanaona kwamba wanatengwa katika masuala ya kitaifa. Mara nyingi tunasingiziwa kwamba hatujasoma. Lakini ningependa kulihakikishia Bunge hili kwamba vijana wengi katika eneo la Pwani hususan katika Kaunti ya Kwale sasa wamesoma. Wazazi wamejizatiti kuwaelimisha vijana wao. Kwa hivyo kuna vijana wa kutosha nchini kote waliohitimu kutoka vyuo vikuu. Vijana hao wanafaa kuajiriwa nafasi za kazi zitakapopatikana. Kwa hayo machache naunga mkono Mswada huu.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii. Naunga mkono.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii ili nami pia niwaunge wenzangu mkono kwamba tunahitaji halmashauri ya jiji la Nairobi ili tupate usafiri wa kitaifa. Ukweli ni kwamba jiji la Nairobi ni letu sisi sote. Si la watu fulani. Ni la Wakenya wote. Jiji la Nairobi ndilo sura ya Kenya na pahali ambapo pesa nyingi ambazo zinatumika humu nchini hupatikana. Vile vile nikiwapeleka nyuma kidogo kihistoria ukiangalia wakati wa Rais Moi utaona kwamba alijaribu kuweka usafiri kutumia mabasi ya Nyayo. Watu hawakumwelewa. Lakini leo hii watu wakikaa wanakumbuka kuwa Rais Moi alikuwa amefikiria kuwa na usafiri wa kitaifa. Rais Kibaki naye alitutengenezea barabara ya kwenda Thika na hata akataka kupanua barabara ya kuelekea Mombasa lakini siasa iliingizwa hapo. Nataka kuwakumbusha wenzangu: Kilio kilikuwa; kwa nini Nairobi? Sisi tunaoishi Nairobi tunajua matatizo yaliyoko Nairobi kuhusu usafiri. Ukweli ni kwamba Roma haikujengwa kwa siku moja. Ni lazima tuanzishe mahali kabla hatujaenda kwingine. Rais Uhuru Kenyata alivyoanza kazi yake aliangalia kwa kina sana usafiri wa Mombasa hasa barabara ya Dongo Kundu ambayo ilizungumziwa kwa muda mrefu. Sasa hivi inajengwa. Vile vile barabara ya kutoka uwanja wa ndege inapanuliwa. Barabara ya kutoka Mariakani hadi Mazeras ambapo kulikuwa na tatizo kubwa inapanuliwa. Ukienda jiji la Kisumu vile vile barabara zinapanuliwa. Tukubali Nairobi ikae hivi hivi na tuwe na matatizo milele ama Nairobi iwe ya kwanza kuangaliwa alafu huko kwingine kufuatie. Miaka iliyopita nikiwa Waziri niliwahi kusafiri kwenda Beijing China. Nilikuta magari mjini ni zaidi ya milioni tano. Niliporudi baada ya miaka kadha nilikuta wakijenga usafiri wa kitaifa. Nilipoenda tena niliuliza: "Haya imekuaje?" Sasa hivi hakuna msongao wa magari. Sasa usafiri wa kitaifa upo na watu wengi wanaowacha magari nyumbani na kusafiri kwa reli. Vile vile Serikali ambayo inasimamia jiji la Beijing imeamua kuwa kuna siku ambazo magari fulani hayataruhusiwi mjini. Ukifika huko unaona tofauti kubwa sana. Katika jiji la London kuna usafiri mzuri sana. Serikali imewataka watu wasafiri na usafiri ule lakini wakati mwingine watu wengine wanapendelea kuendesha magari yao na kwenda mjini. Wanalipa ridhia pesa nyingi wakiingia mjini bila sababu nzuri. Wanalipa karibu Kshs1000 pesa taslimu za Kenya. Ukienda miji mingine mingi utaona kuwa kuna tofauti kubwa sana kupata usafiri wa kitaifa. Kuna wasiwasi kuwa kazi za Kaunti ya Nairobi zinachukuliwa na Serikali Kuu. Swali ni kuwa je wakiachiwa wataweza kutatua tatizo hili?" Ukweli ni kwamba haiwezekani. Kwa hivyo ni lazima Serikali ya Kitaifa ifanye kazi na serikali ya kaunti ili kutatua matatizo haya. Mhe. Naibu Spika Kenya yetu pale imefika sasa ni lazima tubadilishe. Tusiweke siasa katika kila kitu. Tubadilishe mwenendo. Tubadilishe kuwa miradi muhimu inayofanywa na Serikali ambayo inafaidisha Wakenya wote iweze kufanyika. Nafikiria tulikuwa na wewe hapa katika Bunge la Tisa. Wakati tukiwa hapa kulizungumziwa sana upanuaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Ikaleta hisia mbaya na ikacheleweshwa mpaka sasa bei zilibadilika zikawa juu sana kwa sababu ya mradi ule kucheleweshwa. Ninawaomba wenzangu wajue kuwa jiji la Nairobi ni letu sote. Kila siku kuna pahali utaanzia na nina ii kuwa mwanzo ni Nairobi ili kwenda kwengine nchini Kenya kupanua usafiri wa maeneo yale. Jina hili la Nairobi linatia watu wasiwasi lakini ukweli ni kwamba suala hili lilianzishwa wakati wa wizara ya kusimamia masuala ya Nairobi. Ukienda nchi nyingi utakuta kuwa miji mikuu ya nchi hizo yako na wizara ambayo inasimamia kila kitu. Hata ukienda Nigeria Lagos ilishindikana na wakaenda Abuja. Wako na wizara inayosimamia masuala ya Abuja. Suala hili lilianzishwa na Raisi Kibaki wakati wa serikali ya mseto wakiwa na Waziri Mkuu kuwa kuna umuhimu wa kuwa na wizara ambayo inasimamia jiji la Nairobi. Sasa kwa sababu wizara zimepunguzwa haiwezekani kuwa na wizara ikisimama kivyake. Kuna umuhimu wa halmashauri hii iweze kusimamia masuala ya usafiri. Ndugu zangu na waheshimiwa wote nawaomba tuunge mkono suala hili ili tuweze kuanzisha mradi huu ambao utaokoa hali ya usafiri na kuongeza hali ya uchumi. Pia utawezesha wageni wanaokuja Kenya kutaka kuja zaidi na kuwekeza hapa ili watu wetu waweze kupata kazi. Asante sana Mhe. Naibu Spika. Naunga mkono.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie. Kwa yale yote ambayo yamekuwa yakiendelea mimi ni Mbunge ambaye ameadhirika kwa hali ya juu. Kwa mwezi mzima kumetokea vifo vya watu 12 kwa jumla wakiwemo watoto wa shule. Mtoto wa kwanza akiwa wa kidato cha pili wapili ni wa kidato cha tatu na wa mwisho ambalo ni jambo la kusitikisha ni ya kwamba jumapili hii waliua mtoto wa miaka mitatu. Ni jambo la huzuni kwa sababu eneo hili la Matungu kuna shida. Shida ya kwanza ni kwamba OCPD anayesimamia police station ya Harambee sub-county hana gari. Ni kama jeshi akitumwa vitani bila silaha. Panapotokea hali kama hii askari hawana namna ya kusafiri. Ni jambo ambalo sijui lilitokea kwa nini. Sijui kama Waziri anajua kwa sababu ili askari wafanye kazi yao kwa njia ambayo inastahili wanafaa kupata gari la kuzungukia. Hawana gari. Gari lililoko limeharibika. Inasemekana kwamba wakati walikuwa wanapeana magari kituo cha polisi cha Harambee hakikuwa gazetted. Kwa hivyo hakikupata gari walipokuwa wakipeana magari ya contract yale serikali ilikuwa inapena kwa kila kituo cha polisi. Jambo la pili eneo hili ni kubwa na linahitaji askari wa kutosha. Nilipoenda kukutana na wasimamizi wa sub-county ilionekana kwamba askari ni wachache. Swali ambalo liko katika akili yangu ni sijui kama Waziri mhusika anajua kwamba eneo hili ni kubwa na idadi ya askari ni ndogo. Kwa sasa tunapoongea katika Bunge hili wananchi wa sehemu husika wako na haa. Chochote kinaweza kutokea na ningependa Bunge hili tukufu.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii. Ijapokuwa umenipunguzia muda kwa dakika tano nitazitumia vilivyo. Kwanza ninaunga mkono Mswada huu kwa kusema kuwa mambo ya ufisadi sio mambo mazuri kufanyika katika nchi yoyote. Ni vizuri sana kuona kile kitengo cha kupambana na ufisadi kuwa kimeweza kufanya kazi yake bila kuogopa na vilevile kutumia fursa kuona kuwa watoto wa shule wanaweza kufundishwa kuhusu mambo ya ufisadi ili waweze kujua kuwa hii si tabia nzuri katika nchi inayoendelea. Nikitoka kwenye mambo ya ufisadi ninaingia katika hii mada ya economic crimes yaani uhalifu wa kiuchumi. Mswada uko sawa kabisa kwa sababu nikiwa Mbunge kutoka Mombasa kuna mambo ambayo yamenigusa. Tukiangalia mambo ya kiuchumi kama watu wa Mombasa tumeumizwa sana kulingana na hali ilivyo kwa wakati huu. Tukiangalia mambo ya SGR mambo ya kubeba makasha wafanyibiashara wetu hivi sasa hawawezi kufanya biashara kwa njia huru. Kwa maana hiyo inakuwa hujuma ya kiuchumi. Nikiwa Mbunge wa Jomvu ninasema hatutakubali jambo hili. Lazima Serikali iweke huru ufanyaji wa biashara. Watu watumie njia yoyote ile wanataka kutumia. Ikiwa mtu anataka kutumia malori atumie malori. Ikiwa mtu anataka kutumia SGR atumie lakini kulazimishana isifanyike katika nchi hii. Serikali imesema kuwa imesimamisha mambo haya lakini tunaona mambo haya bado yanaendelea. Juzi kuna watu waliofanya maandamo na wameshikwa. Nikiwa Mbunge wa Jomvu ambapo wafanyibiashara wa malori wengi wapo ninasema leo sisi watu wa Mombasa tutaichukulia hatua Serikali ya Kenya ikiwa haitaki kutusikiza. Tutapeleka mashtaka katika Korti ya Afrika Mashariki. Afrika Mashariki ina haki ya kusikiza shida yetu ikiwa nchi yetu haiwezi kutusikiza. Kando na Afrika Mashariki hata International Criminal Court (ICC) tunaweza kuenda kwa sababu hii ni hujuma. Hatuwezi kuishi katika hujuma ya kiuchumi. Watu hawana kazi. Watu hawawezi kusomesha watoto sasa. Hivi sasa watu hawawezi kuishi katika nyumba zao. Kwa hivyo ninachukua fursa hii kusema ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu utawezesha kuona kuwa mambo ya economic crimes yamechukuliwa kwa hali ya sawasawa. Ahsanteni sana.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Bunge kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie yale yaliyozungumziwa na kiongozi wa nchi alipotutembelea hapa Bungeni. La muhimu ni kuwa kiongozi wa nchi alitambua ugatuzi kama njia mwafaka ya kuleta maendeleo katika maeneo mengi nchini. Tayari Serikali kuu imepatia serikali za ugatuzi Kshs1.7 trilioni. Hii inamaanisha kuwa kuna shida kwa sababu asilimia 67.5 imetumika kwa mambo ya kawaida na si maendeleo. Ni vizuri serikali za ugatuzi ziangalie na kuona kiwango kikubwa kimetumika katika maendeleo na si mambo ya kawaida. Rais alizungumzia kuhusu mambo ne muhimu kama vile usalama makaaji bora viwanda na kilimo. Alisema kuwa huo ndio utakuwa mwelekeo wa kujimudu kama Wakenya wakati tunaongea juu ya maendeleo. Vile vile aliongea kuhusu mambo ya afya. Alisema kuwa kumekuwa na majaribio katika kaunti za Kisumu Garissa Isiolo na Nyeri kuona vile wanaweza kujimudu kiafya. Jambo hili linafaa kutiliwa mkazo kwa sababu nchi hii haiwezi kuendelea kama sekta ya afya haijapewa kipaumbele. Eneo langu la Ruiru liko na kiwango kikubwa cha watu ambao wanakadiriwa kuwa laki sita na maeneo ambayo yametengwa kwa sababu ya afya ni ne pekee. Itabidi Serikali itilie uzito mambo ya afya katika maeneo yaliyo na watu wengi ili waweze kufanya kazi. Kazi haiwezi kufanywa ikiwa watu ni wanyonge. Hilo ni jambo ambalo sisi kama Wabunge lazima tulizingatie na kuhakikisha maeneo yaliyo na watu wengi yamehudumiwa kiafya ili kuwe na maendeleo. Vile vile Rais aliguzia mambo ya kilimo na akaongea juu ya kahawa. Alisema kitengo maalum kimebuniwa ili kiweze kusaidia wakulima wa kahawa kuendelea kushughulikia kahawa. Kwa maoni yangu ni vizuri tuangalie mambo mengine yanayohusu kilimo. Kwa nini tunakubali mayai kutoka nje ilhali sisi wenyewe tunaweza kufuga kuku wa mayai? Ni vizuri sisi kama viongozi tutenge kiwango fulani cha fedha ili tusaidie wanachi wanaofuga kuku ili tuweze kukabiliana na watu wanaoleta chakula kutoka nje. Inawezekana kuwa nchi zinazotupatia chakula zimetenga fedha za kuwasaidia wakulima. Pia Rais aliguzia mambo ya masomo. Hakuna maendeleo yanayoweza kufanyika bila masomo. Katika eneo Bunge la Ruiru masomo yako chini kwa sababu hakuna vifaa vya kutosha vya masomo. Kuna madarasa ambayo yana wanafunzi mia mbili. Waalimu watafundisha vipi? Inafaa kile kitengo katika Wizara ya Elimu kiangalie yale maeneo ambayo yametatizika zaidi ndiyo tuweze kujimudu kimaendeleo. Ninaunga mkono na ninafurahia vile Rais aliongea juu ya mambo ya uwiano; Wakenya wote kufanya mambo kama kikundi kimoja. Ninaunga mkono Hoja hii.
Ahsante sana mhe. Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii. Mwanzo kabisa ninaunga mkono hii Hoja ambayo imeletwa na mwenzetu mhe. Njenga. Ukweli kabisa ni kwamba vijana wetu haswa wale wa shule wakati wako likizo huwa ni hatari sana kwa sababu hivi vijibwasha haviko tu mijini mikubwa ya Kenya bali viko katika kila sehemu ya Kenya. Ni tatizo kubwa na sugu kwa sababu mambo ya pombe na madawa mihadarati ni hatari sana kwa vijana wetu. Hata Serikali hupoteza vijana wengi kwa sababu ya kutupatupa mikebe na vibwasha kila mahali. Ni vyema kabisa kuzidhibiti na ikiwezekana mashirika kama NACADA yawezeshwe angalau kuzuia utupaji wake mapema maanake tukiziona mapema ni vyema zaidi kuliko kuzuia baadaye. Nikiongea kuhusu eneo la Bunge la Mwatate ni tatizo sugu maanake vijana wadogo ingawaje amesema wa kiume hata pia wa kike wako katika hali hiyo hiyo. Kwa hivyo ingekuwa ni vyema tuzuie hili tatizo mapema kwa kudhibiti na kuzuia kabisa mpaka wakati hawa vijana wamefika wakati unaofaa ndio waweze kujishughulisha na vinywaji. Suala hili kwanza limeenea zaidi katika maeneo ya Kenya ambako hakuna kazi. Nikiangazia sana eneo Bunge la Mwatate utakuta kwamba hatuna kiwanda hata kimoja. Mvua hakuna na maji ni tatizo. Tuko tu na wale ndovu wakubwa ambao wanakula chakula kingi na wanatumalizia chakula chetu shambani. Basi hao vijana kwa sababu hawana shughuli nyingi mambo ya pombe na madawa ndio hujishughulisha nayo. Ingekuwa ni vyema tutafute njia mwafaka ya kuwezesha haya mashirika angalau wadhibiti utupaji wa vitu hivi. Hata kile kiwango tumefikia kwa sasa hivi nchini ingewezekana tungetengeneza mahala pia pa kuwezesha hawa vijana kutibiwa maanake wengine wako katika hali mbaya sana. Tungekuwa na rehabilitationcentres katika kila jimbo ingekuwa ni vyema zaidi. Nampa pongezi mhe. Njenga kwa kuleta hii Hoja maanake hili ni swala tata sana; vilevile ni swala ambalo linatutatiza sana sisi viongozi. Mambo ya pombe na madawa yako kila mahali Kenya nzima. Utawakuta watu hata mchana katika hali ya kujiburudisha ingawaje ni kujiharibu. Ingekuwa ni vyema kabisa hili swala lishughulikiwe kikamilifu na liwe ni kitu ambacho tumemalizana nacho. Vijana wetu ndio viongozi wetu wa miaka ijayo. Tukishughulikia hili swala itakuwa ni vizuri . Sina mengi zaidi bali ni naunga mkono hii Hoja. Ahsante sana.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa hii nafasi. Ningetaka kuunga mkono hii Hotuba ya Rais ambayo ilikuwa ni ya kusisimua na imejaa mawaidha. Kwanza nilimwangalia Rais; nilikuwa nimeketi hapa na yeye pale. Nilipata wazo kwamba yeye ni kama Yesu ambaye alikuwa ni mtoto wa Mungu lakini akajishusha hadhi na kuwa mwanadamu. Tulikuwa na Rais ambaye alichukuwa kiapo kuongoza hii nchi lakini mwisho wa Hotuba yake akasema anampa msaidizi wake Mhe. William Ruto uongozi. Hilo lilikuwa tendo ambalo lilitufanya kama Wakenya kufikiria mara mbili na kuona kwamba Rais ambaye anatuongoza wakati huu ni mtu tofauti sana. Aliporudi juzi alinena kwamba haijalishi ni nani anakalia kiti. Kilicho cha maana ni nani aliyekalia kiti hicho na anafanya nini. Hayo ni eno niliojifunza. Najua kuna wenzangu ambao wako Bunge leo ama wametoka lakini walisikia jambo la maana. Mhe. Naibu Spika wa Muda tumeongea kuhusu mambo mengi na sitaki kuyarudia. Najua kwamba kuna wale waliathirika na shida za mwaka wa 2007/2008. Kuna wengine ambao walidhulumiwa hasa na maafisa wa Serikali. Pesa zilipotumwa kule mashinani kuwasaidia zilipotelea katika mashimo ya panya na waathiriwa hawakupata fedha hizo. Nawatetea watu hao. Napendekeza kwamba Serikali ifuatilie tena ili tujue wale ambao hawakupata pesa ili waweze kupatiwa hata kama tumefunga hiyo sura. Mhe. Naibu Spika wa Muda ni uchungu kuona watu wengine ambao hawakuathirika wakipewa pesa hizo. Pesa hizo zilitolewa na Serikali kuwasaidia wale walioathirika. Lakini hawakupata pesa hizo. Naomba kwamba tufuatilie jambo hilo ili walioathirika wapatiwe haki yao. Katika upande wa Upinzani wa Bunge hili nilishangaa waliposema kwamba hawatahudhuria Kikao kilichoitishwa na Rais wa Nchi. Hiyo ni kuonyesha tabia mbaya. Ikiwa ni wakati ule ambao nchi yetu ilikuwa taabani ingebidi sisi sote tushikane mkono tuonyeshe wale tunaowakilisha katika Bunge
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa jicho lako zuri lililoniona na kunipatia fursa hii. Kabla sijaongea lolote ningekuomba unipatie fursa niweze kuomboleza na jamaa na marafiki wa Daktari Gakuru ambaye alikuwa rafiki yangu. Hata alinialika nihudhurie sherehe za Mashujaa Day kule Nyeri. Tulikuwa na yeye kule Nyeri na tukaongea mengi kuhusu maendeleo ya Kenya yetu tunayoipenda. Jamaa wa Ruiru wote wanaomboleza na familia yake pahali popote walipo. Hilo ni pigo kubwa kwa nchi yetu ya Kenya. Kama watangulizi wangu walivyoongea ni vizuri tuwaheshimu viongozi wetu wakati wanapopata majanga kama haya. Nikigusia mjadala wa leo ningependa kusema kuwa ni mjadala mwafaka zaidi hasa katika eneo ninalotoka la Ruiru. Katika nchi nyingi za Afrika kuna uhamiaji wa watu kutoka mashambani kuelekea mijini. Haraka ya kwenda mjini inakuwa ya mwendo wa kasi kuliko haraka ya kutengeneza mazingira ya wale watu wanaokuja mjini. Hii ni hasa wakati tumetengeneza barabara kuu kama hii ya Thika na barabara nyingine za kando. Watu wanatoka mijini na kuhamia karibu na barabara zile. Kama wengi walivyosema hapa unakuta kwamba hatuwekei uzito mambo muhimu katika maisha ya binadamu kwa sababu labda hatuna mjadala kama huu wa kuweka utaratibu mwafaka wa kuleta maendeleo ya watu waliokuja pale. Mambo kama ya usalama yamekuwa yakizorota kwa sababu watu wamekuja wengi na hakuna polisi na utaratibu wa maji taka. Unaona kwamba tunapata janga la magonjwa makali kama kipindupindu na mengineyo. Tukichukua mwelekeo mpya wa kuweka utaratibu katika uhamiaji wa watu kutoka mashambani kwenda katika miji mikuu utakuta kuwa maeneo ya mashambani yatakuwa yamehusishwa katika maendeleo kutokana na ugatuzi. Kwa nini nimesema hivyo? Mhe. Naibu Spika wa Muda unajua tumepata ugatuzi na miji sio ile miji mikuu kiongozi wa mjadala huu ametaja bali hata maeneo ya ndani. Vile sasa tuko na kaunti na kaunti ziko na fedha zake utakuja kukuta kuwa hata huko kutakuja kuwa na miji mikuu. Kwa hivyo wakati tunajadiliana na kutafuta mwelekeo wa mjadala huu ni vizuri tukumbuke ugatuzi na kujua kuwa maeneo kama Turkana yatakuwa na miji mikuu na ni vizuri tuweke uzito katika maendeleo ya watu watakaokuwa katika miji ile. Mengi yatasemwa yatakayogusia utaratibu wa kuishi kwa watu lakini bila mikakati kuwekwa tutakuwa tunaongea jambo moja likifuatwa na lingine na tutakuwa tunajirudia. Kuna mambo ambayo yamekuwa yakijirudia katika miji. Kuna shida ambazo zimekuwa zikijirudia. Kukinyesha unakuta tunakimbia kujaribu kutafuta mwelekeo wa kuishi lakini tukiweka mikakati haya yatakuwa mambo ya kupita na sisi tutaendelea mbele na tutakuwa na misimamo itakayotufanya tuonekane tumekomaa kama wanasiasa waliochaguliwa na wananchi. Majukumu yetu yatakuwa ya kufaa wakati tumepewa kazi na tuje Bungeni na kutekeleza yale yametufanya tuje hapa. Tunaweza sema haya yote lakini tusipochukua jukumu la kuyatimiza itakuwa ni eno tu ya bure na mwelekeo hautapatikana. Mjadala huu uko na uzito na upatiwe kipaumbele.
Ahsante sana mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunihurumia. Nimeshindwa kwenda kula chakula cha mchana ili niwe wa kwanza kuzungumza lakini sikupata nafasi kwa sababu kadi yangu haifanyi kazi. Ninataka pia nichangie kuhusu Hotuba ya Rais. Nitaanzia masuala ya usalama.Ukweli ni kwamba Rais ni mtu mzuri lakini kwa sababu haambiwi ukweli eno yanaharibika na watu kila wakati ni kusifu mahali ambapo hapastahili. Usalama umezorota Kenya nzima. Watu wanauawa na wengine wanapata shida. Mpaka hivi sasa njaa imezidi kwa sababu utalii umekufa. Utalii umekufa kwa sababu watalii wanasema Kenya haina usalama. Leo mtu anasimama na kusema kwamba usalama umeimarika kisawasawa. Tafadhalini nawaomba wabunge na Wakenya wote haswa wale walio karibu na Rais wamweleze eno ya ukweli ili tuweze kufaulu katika maisha yetu. Usalama si mzuri. Usalama huenda ukazidi kuharibika kwa sababu hali ya unyakuzi wa ardhi umepita kiasi. Kama kule kwangu Matuga ardhi imenyakuliwa na hata kama tunasema kwamba title deeds zinatolewa mimi ninasema hata heri zisije kwa sababu ukiangalia waliopata karibu theluthi moja ya watu sio wenyeji. Katika hali hii kule kwangu haswa kuna fujo na tunataka Serikali ihakikishe kwamba wanaohusika kupata ardhi ndio wale wenyewe. La si hivyo usalama utazidi kuzorota kwa sababu watu hawawezi kukubali kunyakuliwa ardhi kiwaziwazi ilhali wanaona. Kwa hivyo masuala ya usalama hayajakuwa mazuri na lazima Rais aambiwe ukweli ili tuweze kufaulu katika hili suala. Masuala ya pesa za wazee ninaona hata badala ya pesa za wazee kutujenga sisi zinatuharibu kwa sababu ndani ya kata moja ambayo ina wazee karibu 200 wanapata wazee 15. Sisi tunajulikana kwamba tunatoa pesa hizo. Sasa mara kwa mara tunaambiwa tutawaachia watu wenu 15 wawapigie kura kwa sababu wale wazee wengi hawajapata pesa hizo. Ikiwa pesa za wazee zinataka kutujenga sisi basi Rais aongeze pesa hizo kwa wingi ili kila mzee aweze kupata. Hapo majina yatakuwa yamejengeka na mambo yatakuwa yameenda barabara. Bila ya hivyo tutaendelea kumsifu na hali eno yanaharibika sawasawa na kusuka kamba ilhali huku nyuma inachomeka. Mambo mengine ambayo ningependa kuyazungumzia ni mambo ya kutajana katika hizo orodha za wale ambao wamefanya ufisadi. Sijapinga lakini ni lazima kuwe na ushahidi mkali. Kwa wale ambao walikuwa hai zama za akina Njonjo kulikuwa na usaliti. Wakati huo watu walipata nafasi ya kuanza kuwataja watu wengine ambao walikuwa wapinzani. Tukiendelea katika hali hii mimi ninaona kwamba hali itakuwa vilevile; watu kutajana mtu kama anakupinga unamtaja mradi tu wewe uwe karibu na Serikali. Unajitajia yeyote ili mtu aweze kupata shida pengine kwa sababu ni mpinzani wako ambaye unaona kwamba anakupatia taabu. Najua kwamba Rais siye aliyeenda kuangalia yale majina ni watu wanapeana majina na majina hayo mara nyingi huwa yanaleta shida kwa sababu wale maadui huwa wanataka kuhakikisha kwamba wenzao wamepata shida. Kwa hivyo masuala ya kutajana ni lazima tuwe waangalifu au sivyo chuki itazidi kuendelea katika nchi hii yetu ya Kenya. Mhe. Naibu Spika wa Muda napongeza masuala ya pesa za mashujaa lakini nasema kwamba pesa hizi ni lazima ziongezwe mara kumi ili ziweze kufidia kila shujaa. Mara kwa mara tunapata mambo kama haya na kwamba kuna watu wanatajwa mashujaa lakini utaona kwamba mashujaa wanatoka sehemu fulani. Kule Pwani nakumbuka nilipokuwa kijana hayati Jomo Kenyatta alikuwa akija kule anakaa kwa Mzee Bambaulo Mzee Mbonze Mbonze au kwa Mzee Mwamgunga. Hawa ni watu ambao walipigania uhuru kikamilifu lakini watu wao hivi sasa wanateseka na orodha ya mashujaa ikiletwa wao hawamo. Kwa hivyo hili jambo la kuchagua watu wa sehemu fulani kwamba ati wao ndio walipigania Uhuru sisi hatuwezi kukubaliana nao. Ikiwa walikuwa wanapigania mashamba yao ni sawa lakini Uhuru ulipiganiwa na Wakenya wote na kwa hivyo mashujaa waangaliwe kutoka kusini mpaka kaskazini; kutoka magharibi mpaka mashariki. La sivyo hali hii itakuwa haileti maana na ukweli ni kwamba utakuwa ni ubaguzi wa mwaka ambao sisi hatuwezi kukubaliana nao. Mhe. Naibu Spika wa Muda hiyo ndio hali nilikuwa naifikiria kwamba si hali nzuri. Narudia ya kwamba wale walio karibu na Rais wamshauri kisawasawa. Mambo ya kuunga mkono lolote linalokuja na japo suala la maana hayatatusaidia bali yatatutia katika mashimo. Mambo ya kusimama hapa kwamba huyu ni wa muungano wa CORD au Jubilee na sasa lolote baya linalozungumzwa na CORD mtu wa CORD anaunga mkono likizungumzwa baya na Jubilee watu wa Jubilee wanaunga mkono; hatutafika popote isipokuwa tutamaliza nchi hii. Asante sana.
Ahsante sana mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili niwe katika orodha ya wale wenzangu ambao watachangia ama kudadisi Hotuba ya Rais ambayo aliisoma hivi majuzi. Nakubaliana na Ripoti yake kulingana na yale masuala aliyoyazungumzia kama vile umeme katika mashule. Shule zetu za sehemu tunazowakilisha hazijakuwa na umeme kwa muda mrefu. Lakini kwa sasa hivi
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika Wa Muda kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia Hoja hii. Nikitanguliza ningependa kutoa shukrani kwa Mhe. Odanga kwa kuja na wazo kama hili. Kusema kweli ni changamoto ambayo imekua katika Jamhuri yetu ya Kenya. Watoto wetu wamekuwa katika hali ambayo haieleweki. Wazo kama hili la kuwaleta walimu wa kidini ili wazungumze na watoto wetu ili wawe na maadili ni kuwatayarishwa kifikra na kimipango ili wafanikiwe katika maisha yao ya usoni. Mbali na hayo mipango kama hii huwa inataka iwe na mawazo ya kuangalia ni watu gani watapewa shughuli hizi. Tunavyojua somo la dini liko katika mitihani yote. Sisi kama watengenezaji wa sheria tunafaa kuangalia ni mbinu gani tunaweza kuweka kuhakikisha kuwa wale watakaochukuliwa kusomesha dini katika shule zetu ni mashehe ama wale chaplains ? Watu hao wanastahili kuwa watu walio pande mbili - dunia na dini - ili waweze kuwapa watoto wetu mazungumzo mazuri. Mhe. Naibu Spika wa Muda suala la watoto kufanya mapenzi na kupata mimba za mapema ni changamoto iliyo juu sana katika maeneo yetu. Ningeomba Wabunge wenzangu tuiunge mkono Hoja hii ili tuweze kubadilisha mipango ya watoto wetu. Hii isiwe mwisho kwa sababu Hoja hii itakua bora zaidi kama itafanywa sheria ili tuhakikishe katika shule zetu tumepata watu ambao wanaweza kuelekeza watoto wetu kwa njia ya kuwa na mawazo sawa sawa katika maisha yao. Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naunga Mkono.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili niweze kupenyeza sauti yangu hasa katika Hoja hii ya ushirikiano baina ya Serikali yetu ya Kenya na Uingereza kupitia muungano wa majeshi. Mimi nitaunga mkono Hoja hii ikiwa taratibu fulani zitafuatwa. Kwanza wahakikishe kuwa mahali ambako jeshi hili litakuwa likifanyia mazoezi zile silaha zote ambazo hazikulipuka zilipuliwe ili mahali pale pawe salama. Wakenya wengi sana wamepata ulemavu kwa ajili ya silaha ambazo Waingereza walitumia na kuchimbia chini ya ardhi yetu. Nazungumza haya kwa sababu nilikua askari kwa miaka tisa. Tumetembea sehemu nyingi ambako kambi za Waingereza ziko. Mabomu mengi sana ambayo hayakulipuka bado yako ardhini. Watu wanaoishi katika sehemu hizo ni wafugaji na mara kwa mara wanalipuliwa wakiwa katika shughuli zao za kulisha mifugo. Waingereza pamoja na serikali nyingi za ulaya zilitukoloni kabla tupate uhuru wetu. Walichukua rasilmali zetu nyingi sana. Sasa tuko huru. Tusipeane nafasi katu ya rasilmali zetu kuchukuliwa tena. Ikiwa tutakubalia waje wafanyie mazoezi katika ardhi zetu ili kwamba wazoee mazingara ya Afrika basi ni lazima kuwepo na taratibu wa kuhakikisha kwamba mambo fulani yanatekelezwa mwanzo ili kufaidi jamii zinazoishi mahali pale. Kwanza wakija lazima waje na bajeti ambayo itaonyesha kwamba watajenga shule za msingi shule za sekondari na hosipitali kubwa ili wakaazi wa maeneo hayo waweze kufaidika. Silaha ambazo zinatumika zina madhara. Hakuna silaha ambayo baada ya kutumika inakosa madhara. Kuna vitu ambavyo tunaweza kuona na vile hatuwezi kuona. Lazima wajenge hospitali kubwa na iwe na madawa ya kutosha ili watu wetu waendele kupata matibabu kama ambavyo jeshi lao hufaidika na matibabu mazuri. Ni aibu kwamba kambi ya wanajeshi wa Uingereza ina vitu vingi vinavyohusiana na jamii kuliko zile jamii zinazoishi katika haya maeneo tuliyowatengea kufanyia mazoezi ya kivita. Zile jamii maskini kwa kukosa maji na chakula huenda kuishi karibu na kambi hizo ili kutafuta misaada. Hii ndiyo sababu wale wanajeshi wanachukua nafasi ya kuwadhulumu kimapenzi watoto wetu wa kike. Wanadhulumiwa na kufanyiwa mambo hayo bila hiari yao. Ni kwa sababu ya umasikini na kukosa mambo muhimu kama maji ndiposa wanakwenda kule kukubaliana na wanajeshi. Ilionyeshwa wakati mmoja kwenye runinga watoto wengi wakizungu. Hawa watoto waliachwa humu nchini nao hao wanajeshi Waingereza. Itakuwa vema mazingira maalum yakitengenezwa karibu na kambi zile ili kuwezesha kimaisha jamii zinazoishi mahali pale. Ni muhimu jamii hizo ziwe na maji hospitali na shule. Ni muhimu pia watu katika jamii hizo wawe na kazi za kufanya ili isiwe mazoea kwao kwenda kuomba vitu kwenye kambi za wanajeshi. Mwenyekiti wa kamati inayohusika na ulinzi sharti asisitize kwamba kuwepo na taratibu za kuwaruhusu wanajeshi hawa kufanya mazoezi yao humu nchini. Isiwe kwamba tu wakisema wanakuja sisi hao tunawapokea eti kwa sababu wametuahidi watatufundisha kupambambana na shida tuliyonayo ya ugaidi. Huenda wao ndio watazidisha matatizo! Wanakuja kutufundisha kumpambana na ugaidi. Wanazidisha matatizo kwa sababu hata wale magaidi hawakuwa na haja na sisi Wakenya. Wamekuja hapa wakati fulani kwa sababu Serikali za Marekani na Uingereza ziko hapa. Kwa hiyo madhara yanakuja kuliko faida. Kwa hivyo tuwe na utaratibu na msimamo kama Serikali kwamba taratibu fulani zifuatwe ili tuweze kuwakubalia. Kwa hayo machache nakubali na nakataa. Ikiwa taratibu zitakuwepo nitakubali. Ikiwa hakuna nitakataa. Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja hii. Kwanza kabisa ninapeana rambirambi zangu pamoja na familia yangu na wana Lungalunga vilevile na Kwale kwa jumla. Haya ni masuala ambayo yamejiri kwa muda mrefu. Janga la kwanza likitokea Likoni bado nilikuwa shuleni. Tulipoteza watu zaidi ya 200. Lamu ilitokea habari kama hii. Familia nzima ikapotea isipokuwa mzazi wa kiume aliyeweza kuogelea kwa masaa matano bila kupata usaidizi wowote kutoka kwa kitengo chochote cha kuangalia hali ya usalama katika nchi hii. Hili suala la kupeana kidole kwa Serikali naliona si suala sawa kwa sababu kila anayepewa nafasi ya kuongoza katika shirika lolote yeye kama mkurugenzi anatakikana apange mikakati ya kisawasawa na kuangalia vitengo ambavyo haswa vinatakikana vipewe kipaumbele katika mipango yake ya kuhakikisha anaendesha shirika lile. Lile gari ambalo lilizama pale lilichukua karibu dakika 30. Wale wanajeshi wa Navy waliokuwa wakifanya mazoezi waliona likizama. Kama baharia - mimi uogelea - na ikiwa hujazoea hata kama wajua huna vifaa hauwezi kuruka kwenda kusaidia. Kwa hivyo mimi kama Mbunge nilizungumza na wenzangu kule Vanga na hii leo tunavyozungumza katika timu ambayo inazunguka na imeruka kule chini kuhakikisha wametoa miili ni vijana wanne ambao hawakusoma hawana elimu lakini kazi yao ni kuruka ndani ya maji na kuhakikisha wametoa vilivyo kule chini. Kwa hivyo suala la kuajiri wafanyakazi haswa katika hivi vivuko ambavyo vinatumia madau ni lazima tuweke katika sheria kuwa katika hivi vivuko lazima kuwe na watu wawili au watatu ambao wana tajiriba ya kisawasawa na ile ari ya kuingia kule ndani kusaidia wakati wowote. Hili ni swali ambalo sisi tunajiuliza kama wakenya: Basi sisi kama Wakenya ikiwa hatuwezi kubuni basi kuiga pia hatuwezi? Ukiangalia nchi za kuendelea ambazo tunategemea kuiga mipango yao katika kila sehemu hata zile sehemu ambazo vijana wetu wanakwenda kujivinjari za bichi huwa tumeweka walinda usalama. Kukitokea janga lolote wanaweza kuingia pale na kusaidia kwa haraka. Kwa hivyo ombi langu mbali na kuwa hili suala limekuwa suala nyeti wale wote ambao wanahusika sio kuhusika kwa kuwa walitenda lakini kuhusika kuweka mipango kabambe wajiuzulu ama Rais wa Jamhuri ya Kenya aseme kila mmoja ambaye amezembea kikazi ni sharti kukitokea jambo kama hili ajiuzulu. Hii italeta heshima katika haya mashirika ambayo yamepewa nafasi ya kuongozwa na watu. Vilevile nikienda upande wa usimamizi leo ukiangalia sehemu kama ile unakuta wakati feri inatakikana kushukisha kabla gari halijatoka wananchi hupita. Leo ni baharini kesho utasikia kuna wananchi wamepandiwa na magari. Hii yote ni kwa sababu ya ukosefu wa usimamizi bora. Ikiwa hakuna usimamizi bora majanga yataendelea kutokea. Vilevile ukiangalia uajiri wa watu ukiajiri mkurugenzi lazima awe na tajiriba ya usimamizi. Ukichukua mkurugenzi ambaye ni mhasibu au mhandisi lazima awe na tajiriba ya usimamizi ili ajue kuna masuala kama inventory masuala ya kuangalia spares za hiyo meli zinatoka wapi. Tulitoa shillingi billioni 1.8 kununua feri mbili. Ile feri ya kwanza ambayo ililetwa azimio lilikuwa ni feri mpya lakini iliyoletwa ilikuwa ishatumika. Kwa nini tutumie vifaa ambavyo vimeshatumika katika nchi zingine na hali tunaweka pesa za kisawasawa kuhakikisha tumepata feri za kisawasawa na zile pesa tumetoa ziwe ni haki kwa mwananchi ili apate huduma ya kisawasawa? Pili hadi wa leo hizo feri hazijafika hatujui pesa zimeenda wapi. Kama Bunge la Kitaifa hayo ni maswala ambayo ni muhimu tuyaangalie kwa undani.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Hotuba ya Mhe. Rais. Kwa kweli taifa nzima lilikuwa linatarajia mengi kutoka kwa kinywa cha Mhe. Rais kuliko hata yale ambayo aliyazungumza. Kwanza Wakenya walikuwa wanataka yeye kama Amiri Jeshi Mkuu atueleze hali halisi ilioko nchini Somalia ambako vijana wetu wa kike na wa kiume katika sare rasmi wanapoteza maisha yao. Pia tulikuwa tunatarajia atakuja kuzungumzia idadi ya wanajeshi waliopoteza maisha yao kule ni wangapi na wale ambao wameachwa bila waume wao wanasaidiwa namna gani. Vile vile tulikuwa tunatarajia atueleze ameelekea vipi na Wizara ya Mambo ya Nje kuhusu suala ambalo Wabunge wa Bunge la Somalia wakati fulani walipitisha kuwa hawataki wanajeshi ya Kenya wawe kule. Kwa hivyo tulitaka pia atueleze Wizara yake imekaa na wale Wabunge wa taifa la Somalia na atueleze sasa wamefikia mpango gani na wamekubali wanajeshi wetu wafanye nini. Bila hivyo sisi tunafikiria kama Wakenya kwamba kulingana na vile Wabunge walikataa Jeshi la Kenya kuwa kule wao ndio wanafanya mipango wanajeshi wetu wavamiwe katika makambi yao. Kwa hivyo sisi tunategemea kwamba wanajeshi wetu wataendelea kupoteza maisha yao ikiwa Serikali haitakuwa na makini kufuatia suala hilo.
Ahsante sana mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa ningependa kutoa shukurani kwa ndugu na rafiki yangu Chris Wamalwa kwa kuileta Hoja hii Bungeni. Mimi nilijikuta kwenye ulingo wa siasa kwa sababu ya marehemu Kijana Wamalwa. Nikiwa naibu mwenyekiti wa chama cha FORD(K) na kwa sababu marehemu Kijana Wamalwa alikuwa mwanzilishi wa chama chetu ninamushabikia zaidi. Ninawaomba Wabunge wenzangu tuipitishe Hoja hii ili tuweze kumtambua kama kiongozi aliyechangia kuwepo kwetu Bungeni. Kwa hayo machache ninaiunga mkono Hoja hii.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa ili niweze kujadili Mswada huu. Ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu ufisadi katika nchi yetu ya Kenya umekithiri sana. Hivyo basi mambo mengi yamekuwa hayaendi ipasavyo. Mambo mengi hayaendi vizuri kwa sababu ya suala hili la ufisadi. Mahospitali hayana madawa na watu wanakufa ovyo ovyo. Ukifuatilia sana unapata ni kwa sababu ya ufisadi. Kuna kisa kimoja cha ufisadi kilichonishangaza sana. Kilinisababisha kutambua ufisadi umefanya watu kupenda mali zaidi hata utu umewatoka. Dereva wa ambulance alienda kuchukua mgonjwa ambaye alikua ni mama mja mzito aliyekuwa karibu kujifungua. Lakini kufika pale akasema kwanza anataka afungiwe kitu chake kidogo ambacho hakina risiti wala hakijulikani mahali popote akiweke mfukoni ndiposa waende. Ni huzuni kwa maana tulimpoteza huyo mama. Nilimshughulikia yule dereva vilivyo kwa sababu nilivyofahamishwa hali hiyo sikufurahi. Hiki ni mojawapo ya visa vya ufisadi nchini. Visa kama hivi vinawafanya sisi viongozi kudharauliwa. Tazama kisa kilichotokea pale Likoni Ferry Mombasa. Ni siku tatu sasa na hali haieleweki. Kumekuwa na mauti pale na mpaka sasa watu wanakaa katika hali wasiyoifahamu. Kuna utepetevu ambao haueleweki. Tukiangalia kwa mtazamo tunaona ni kwamba kuna ufisadi ambao unaendelea pale. Kenya nzima hakuna watu wa kuokoa hali kama hiyo? Mhe. Naibu Spika wa Muda ndio maana ninaunga mkono suala hili kwamba kuwe na hukumu kali kwa mambo ya ufisadi. Tumeona watu wengi na majina tajika yakihusishwa na ufisadi.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa ya kuuchangia Mswada huu ambao unahusu ugavi wa pesa kwa vyama vya kisiasa. Ningependa pia kuchukua fursa hii kumshukuru Mhe. Chris Wamalwa kwa kuuleta Mswada huu Bungeni kwa sababu kama Naibu Mkuu wa Chama cha FORD (K) natambua jinsi mambo yalivyokoseka katika sheria ya vyama. Vyama vya kisiasa katika nchi yetu ya Kenya viliundwa kudumisha demokrasia. Tunataka kiwango ambacho yatakikana chama kifikie ili kipate sehemu ya pesa kishukishwe. Hii ni kwa sababu kama FORD(K) hatukuweza kufikia kiwango hicho na tuna Wabunge 11 magavana wawili na wawakilishi 85 katika mabunge ya kaunti. Kama si maelewano na Chama Kikuu cha Orange Democratic Movement (ODM) sisi tungekuwa katika hali mbaya kwa sababu ni muhimu uwakilishi ufike mashinani. Na kufikisha uwakilishi mashinani ni lazima kuwe na pesa za kuwalipa maafisa na wale ambao wanasambaza jina la chama. Mhe. Naibu Spika wa Muda naunga mkono Mswada huu ili pesa hizi ziwafaidi Wakenya wote. Vile vile hizi ni pesa za umma ambazo zinafaa kufika kwa wananchi wote nchini Kenya. Pesa hizi za umma zina haki kutambulika na kujulikana jinsi zinatumika. Ikiwa zitakwenda katika vyama tunaweza kubuni sheria mwafaka na vile vile kuandikisha vyama vipya. Nitapinga yale eno ambayo yamezungumziwa - kwamba iwapo tutayapitisha marekebisho hayo basi vyama vingi zaidi vitaandikishwa. Kuna tetesi kwamba vyama vitakavyosajiliwa vitakuwa vingi kushinda vile vilivyoko hivi sasa. Sioni kama tetesi hiyo ni sawa kwa sababu tayari sheria ya kuandikisha vyama iko na imeweka mikakati ili kuchuja vile chama ambavyo vitakuwa na mwelekeo wa kisawasawa. Kwa hayo machache naunga mkono Mswada huu.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa ya kuzungumzia suala hili la ardhi ambalo ndilo lenye utata kwa taifa nzima. Nimeona ni vyema sana nipenyeze sauti yangu katika suala hilo. Kwanza ninakubaliana na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi kwamba ni lazima tuheshimu hati miliki. Ni vyema sana kuziheshimu. Lakini vilevile tuangalie uzito ulioko kuhusu watu wetu kwa sababu hao maskwota walioingia katika shamba hilo ni watu ambao hawana makao na ndiyo sababu wakaingia katika lile shamba kujiwekea makao. Ikiwa waliingia kuuza hapo ni makosa. Lakini kama walienda kwa makao yao ni kwamba walikuwa na utata. Vile vile unakuta kuwa kinachochangia watu kuingia katika ardhi hizo huwa lile shamba limekaa wazi halilimwi na hakuna shughuli inafanyika. Inavutia mtu mwingine ambaye anapata shida na pale pako wazi panakaa nyoka na wanyama. Hii ndiyo sababu wanaenda pale. Kwa upande wangu ningeomba Kamati ya Ardhi ishughulikie suala hili. Inafaa Serikali inunue lile shamba ili wale walio pale wasiondolewe. Tatizo hili lipo katika upande wa Kisauni. Wengi wameingia katika mashamba ambayo yako wazi. Kama wale watu wangekuwa wameyatumia mashamba yale hata kwa kulima na kuleta mapato hakuna mtu angeingia. Lakini kwa sababu shamba halina mtu lipo wazi na panaishi nyoka ambao wanakaribia zile nyumba wananchi wanaingia pale kujisaidia wenyewe. Kwa hivyo ningeomba Kamati ya Ardhi ishughulike na ihakikishe kwamba Serikali imenunua mashamba hayo na wale maskwota wapewa vipande hivyo vya ardhi ili wakae huko. Naiunga mkono lakini hilo ndio suala ambalo ninalitilia uzito. Asante.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa hii nafasi. Nataka kujiunga na wenzangu kwa ajili ya Mswada huu. Ningependa kumshukuru Mhe. Keynan kwa ajili ya Mswada huu. Hapo awali tulikuwa na Wabunge katika Bunge hili na niliona kwamba kuna wengi ambao walikuwa wanasumbuliwa sana haswa na mambo ya korti. Nakumbuka tulikuwa na Mbunge kutoka kule Saboti Mhe. Davis Nakitare ambaye kule nje hangepata nafasi ya kukaa vizuri kwa sababu korti ilikuwa inamsumbua sana. Kwa sababu yeye mwenyewe hangeweza kujisimamia ilimbidi atafute wale ambao walimpigia kura wamsimamie katika korti. Naunga mkono Mswada huu kwa ajili utatupa sisi mamlaka ya kuhahikisha kwamba tunaheshimiwa kule nje na tunaheshimiwa pamoja na wale ambao wametuchagua. Kama vile wenzangu wamesema tukiwa na mambo yoyote kortini kama vile kushikwa ama unatakikana kutoa ushahidi kwa mambo ambayo yametendeka utasukumwa na askari bila kujali kama wewe ni Mheshimiwa. Watasema: "Hii sheria ambayo ni nyinyi wenyewe mmeunda inafanya hivi na vile". Tunaposhikwa na polisi kwa barabara zetu ukisema kuwa wewe ni Mheshimiwa wanakwambia kuwa uheshimiwa wako uko Bungeni wala si huko nje. Naunga mkoni ili tuwe na mamlaka ama sheria kama hii ya kuturuhusu sisi kama viongozi kuheshimiwa katika taifa letu. Naunga mkono.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa mwanya kuchangia Hoja hii muhimu kuhusu kazi ya askari wetu hapa nchini. Sitasema mengi kwa vile wenzangu Waheshimiwa wamegusia. Nitagusia mawili matatu ili niwape wengine nafasi kuchangia pia. La muhimu ni kwamba ukiangalia idadi ya wale askari wanatufanyia kazi haswa viongozi wanakaa maeneo duni sana. Isitoshe idadi ya askari wanaotufanyia kazi ni haba mno. Nimesema hapa mara kwa mara kwamba tuko zaidi ya watu 500000 katika eneo langu la Ruiru. Idadi ya askari wanaotuchunga Ruiru ni 153. Ukiangalia hicho kitengo utapata askari mmoja anachunga watu zaidi ya 3000. Hata kama anataka kufanya kazi itakuwa vigumu kufanya kazi vilivyo. Ndiposa tunawalaumu. Lawama kwa askari iko juu kuliko kazi yao. Pili kwa sababu ya uhaba wa hawa askari itabidi watumikie wananchi utakuta askari anafanya kazi usiku na mchana. Wakati anafanya hii kazi hatembei mikono mtupu; huwa amebeba bunduki ya kilo kumi au zaidi. Naskia wengine wanasema amesomeshwa kufanya hivyo. Lakini mwili ni wa binadamu. Tuheshimu hiyo. Hata kabla hatujaongea juu ya makazi ya askari wetu wacha kwanza tuangalie wanafanya kazi wakitumia kiwango kipi cha utu. Hilo ni jambo litaleta usawa wa hawa askari kutufanyia kazi na sisi kufanyiwa kazi na wao. Labda hilo ndilo jambo linagusia hawa askari kutumia bunduki kiholela. Nafikiria imetokana na haa. Hawa ni binadamu.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii angalau pia nichangie Mswada huu unaonuia kuzuia visa vya udanganyifu wa mitihani katika nchi yetu. Wenzangu wameongea kuhusu changamoto ambazo watoto wetu hupitia na pia shida ambazo watangulizi wetu walizipitia hapo awali. Ni kweli vile wenzangu wamechangia. Kuna wengine wametoka katika maisha duni ama wamesoma kwa shule ambazo hazijajengwa vizuri katika maeneo yao. Mhe. Moroto amesema kwamba ukiona West Pokot mahali anatoka wanafunzi walikuwa wakisomea chini ya miti. Sasa unaona katika maisha kama haya wengine wakifika wakati wa kufanya mitihani yao halafu mwishowe isemekane kwamba mitihani imefutiliwa mbali hiyo inaleta shida hata kwa jamii na wazazi wa watoto hao. Na siyo hiyo tu. Vile wenzangu wamesema zile changamoto walimu wanapitia katika sehemu kama hizo za ukame na sehemu zinginezo ambazo hazina barabara ama hazina vifaa vya kutosha ni nyingi. Shida hizo pia zinachangia katika mambo haya ya mitihani. Hapo awali tulikuwa tunafanya mitihani ya darasa la saba. Kutoka darasa la saba mtu akienda katika shule ya upili wanafanya mtihani katika kidato cha pili. Ilikuwa inapatia mtu nafasi angalau kuona anaendelea mbele ama ako na nafasi ya kurudia hicho kidato. Hiyo ilikuwa inatupatia ufaa mazuri sana. Tukipata wale wamehitimu vizuri kutoka hapo walielekea kidato cha nne na baadaye wakamalizia kidato cha sita kule mbele. Walikuwa wakiendelea vizuri sana. Lakini kulifika mahali tukawa na udanganyifu kwa sababu baadhi ya walimu na wazazi wale wanajitosheleza katika jamii wanatafuta njia za kuhonga walimu ama walimu wakuu na hao walimu pia wanapata nafasi ya kutembea katika Mtihani House kuhakikisha kwamba watoto wao wanafanya vizuri katika shule zao ama wanafanya vizuri kuhitimu katika madarasa waliokuwa wakifanya mitihani yao. Cha kushangaza ni kwamba tulikuwa na mwenda zake Mheshimiwa katika Bunge hili Mhe. Mutula. Mliona kwamba baada ya kukuwa waziri alihakikisha kwamba amepatia mtoto wake shahada ya degree ilhali hakumaliza ile miaka inahitajika katika chuo kikuu. Sasa unaona hao ni baadhi ya viongozi miongoni mwetu - wale walikuwa wakichangia mambo kama haya katika nchi yetu ya Kenya. Mtoto wa tajiri ama mtoto wa kiongozi anafaidika. Huyo kiongozi anapata nafasi ya kuhakikisha ya kwamba mtoto wake anapita mtihani bila hata kupitia masharti yale yanayotakikana katika sekta ya elimu katika nchi yetu. Na haya mambo ya ufisadi ndio huwa tunapinga sana katika nchi yetu kwa sababu yanatuletea madhara. Unapata mtu amehitimu lakini ukimpa kazi afanye hafanyi kwa njia sawa kwa sababu hakutumia njia mwafaka ya kuhakikisha kwamba anafika penye amefika. Ninataka kuunga mkono Mhe. Agoi kwa kuleta huu Mswada katika Bunge hili wa kuhakikisha kwamba tuko na jopo kazi la kuhakikisha kwamba kuna usawa. Iwapo kutakuwa na matatizo ama iwapo tutakuwa na mambo yale yasioeleweka katika nafasi ya mtu kuhitimu ama ya kupewa cheti chake - tunafahamu yaliyompata Mhe. Joho - hilo jopo kazi litasaidia wananchi ambao hawana nafasi ya kujitetea. Tena ni aibu kubwa sana kwa sababu ikifika uchaguzi jopo kazi la uchaguzi na mipaka linaingilia kati na kusema kwamba wanatafuta hiki na kile. Jambo kama hili linaelekea kutumua vibaya ushuru wa wananchi katika nchi yetu. Hatuna barabara na maji sehemu zingine ilhali tunatumia ushuru vibaya. Badala ya matumizi mabaya ya hizi pesa ni heri zipelekwe kule mashinani zilete maendeleo katika nchi yetu. Namshukuru Mhe. Agoi kwa kuleta Mswada huu ili sisi kama viongozi katika Bunge hili tuuchangie na kuona kwamba sekta ya elimu katika nchi yetu imeendelea mbele na inaleta usawa. Bila elimu watoto wetu na vizazi vijavyo havitapata nafasi ya kuwa viongozi. Usipokuwa na elimu watu wanasema kuwa Serikali haijapeana kazi ya kutosha. Lakini mtoto akihitimu akipata cheti chake licha ya kwenda katika chuo kikuu anaweza kwenda katika chuo cha kiufundi. Hiyo inaendelea kuongeza maarifa zaidi na inawapatia nafasi ya kupata kazi katika sekta mbalimbali katika nchi yetu. Ahsante sana. Naunga mkono Mswada huu.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili nami nitoe mchango wangu kwa Ripoti hii ya Kamati ya Uwekezaji. Kiwanda hiki ambacho kuanzia mwaka wa 2007 - katika mahojiano na makubaliano ya Baraza la Mawaziri - ilikubalika wazi wazi kuwa kinahitaji kuboreshwa ili Serikali ya Kenya iwe na zile hisa zake theluthi hamsini na mwekezaji mpya aje achukue nafasi ya BP Shell na Chevron ambao ndio walikuwa wanashikilia hisa hizo nyingine. Jambo la kushangaza ni kuwa ombi lilipotumwa kwa mashirika mbalimbali ya ulimwengu kati ya mashirika yaliyoomba kuingia na kumiliki hizo hisa ilikuwa kampuni ya Essar kutoka Mauritius. Madhumuni ya Essar kutoka Mauritius kupatiwa nafasi ya kuingia na kuchukua hisa za yale makampuni mengine ya mafuta yalikuwa kwanza kuboresha kiwanda hicho ili kiwe kinasafisha mafuta ndio tupate kiwango ambacho kinahitajika cha mafuta na cha kuridhisha. Mhe. Naibu Spika wa Muda utaelezwa na hii Ripoti ukiisoma kwa undani kuwa waliohusika na ubinafsishaji wa kiwanda hicho waliweka mikakati ya vile hiyo kampuni itaingia ianze kazi ichukue hisa na ihakikishe kuwa kiwanda kimeboreshwa kabisa na shida ya mafuta imeisha. Ilikuwa pia ihakikishe kuwa usafishaji ulikuwa mzuri Serikali itapata faida na wafanyikazi wa kiwanda cha mafuta nao pia watakuwa wamepata nafasi. Suala likawa US$15 milioni ndizo hela kampuni hiyo ingelipa Serikali. Baadaye kwa sababu ambazo hazikueleweka na mpaka sasa hakuna mtu ambaye ameeleza ikawa hawatalipa US$15 milioni bali watalipa US$2 milioni. Hata hundi hiyo ya US$2 milioni ilipotolewa ilizungushwa kati ya Wizara ya Fedha na kiwanda hicho cha mafuta kwa muda wa miezi sita bila ya kujua ni nani aliyepaswa kuipokea hundi hiyo mpaka muda wake wa kulipwa ukaisha. Kwa hivyo inabainika wazi kwamba kampuni hiyo ya Mauritius haikulipa chochote kukibinafsisha kiwanda hicho. Mhe. Naibu Spika wa Muda katika mikataba ambayo waliweka walikubaliana kwamba muda ukifika na watu hao washindwe kukiboresha kiwanda hicho watalipwa US$5 milioni na Serikali. Swali ambalo unapaswa kujiuliza ni: Kwa nini Serikali ilipe US$5 milioni kwa mtu ambaye alikuja kununua asilimia 50 za hisa za kiwanda ambacho kinafanya kazi? Kwa nini mtu huyo ambaye aliahidi kukiboresha kiwanda hicho alipwe fedha hizo na kuondoka anaposhindwa kukiboresha kiwanda hicho? Hii inamaanisha kwamba nchi hii imepoteza hisa zake US$15 milioni na ikapoteza muda tukitarajia kuwa kiwanda kitaboreshwa. Tunavyozungumza wafanyikazi hawana chochote. Kiwanda kimefungwa; hakifanyi kazi. Wafanyikazi wamepoteza ajira yao. Wakazi wa Pwani tumekuwa tukijivunia kwamba tulikuwa na mtambo wa kusafisha mafuta kule Changamwe. Mtambo huo haupo tena. Sasa imebaki fedheha. Kimekuwa kitu cha kuangalia tu. Zai kulikuwa na mtambo wa mafuta. Sasa kilichobaki ni vyuma vinavyoshika kutu. Ardhi yenyewe inaelekea kuuzwa; ina utata. Lililobaki ni kujiuliza je wale waliohusika walikuwa na madhumuni gani? Nia yao ilikuwa ni nini? Je nia yao ilikuwa ni kukiboresha kiwanda hicho ama nia yao ilikuwa kwanza kwenda Muritius na kuanzisha kampuni ya kununua hisa za kiwanda hicho? Kwa nini Mauritius? Kwa sababu Mauritius ni nchi ambayo inaficha i za wahusika wa makampuni. Pili Serikali ya Mauritius haitozi kodi. Tatu wafisadi wakuu ulimwenguni huenda kujificha huko. Wahusika ni wakuu serikalini wanaoshikilia nyadhifa mbali mbali haswa wakuu wa kitengo cha uboreshaji na ubinafsishaji wa mashirika ya umma nchini na wakuu katika kiwanda hicho ambao baadhi yao wao wameondoka baada ya kukipora kiwanda hicho. Baada ya kufanya hizo mbinu zote baadhi yao wakaenda kuchukua nyadhifa za kisiasa. Je tutaendelea na mambo kama haya nchini kwa muda gani? Mhe. Naibu Spika wa Muda Wizara ya Kawi ilikuwa imetuahidi kuwa kiwanda hicho kikiboreshwa bei ya mafuta ingepungua na tungekuwa na bidhaa za mafuta za kutosha. Kama unakumbuka kuna wakati watu walianza kupiga foleni kununua mafuta kwa sababu ya uhaba wa mafuta. Washikadau katika sekta ya mafuta nchini walikuwa wakibishana na Serikali wakiulizana ni nani aliyepaswa kuleta mafuta yaliyosafishwa na ni nani aliyepaswa kuleta mafuta ambayo hayakuwa yamesafishwa ili yasafishwe kwenye kiwanda hicho. Kukawa na shida ya mafuta. Wamiliki wa Kampuni ya Essar ya Mauritius walipokuja walisema kwamba shida ile ingeisha kwa sababu wangekiboresha kiwanda hicho ili kiweze kutoa mafuta masafi na nchi itafaidika. Tunashangaa ni masaibu gani ambayo yameikumba nchi hii? Jambo la kushangaza ni kwamba watu wote wanaokuja nchini kushiriki kwenye mpango wa ubinafsishaji wa viwanda na makampuni yetu nia yao ni kupora mali ya nchi hii. Kwa mfano ni nani ambaye hajui kwamba Telkom Kenya lilikuwa shirika kubwa ambalo halikuwa linatingisika? Lakini limeuzwa na ukiangalia jinsi lilivyouzwa utaona kwamba hisa zimeporwa na hivi sasa wafanyikazi wa shirika hilo hawana ajira. Shirika limechukua mkondo huo. Hivi sasa wameshikana na shirika la Wareno ambao wanasema wanaliboresha shirika na ndege nchini. Wamenunua ndege lakini madhumuni yao ni nini? Mhe. Naibu Spika wa Muda tunakioomba Kitengo cha Ufisadi kiwachunguze watu wote waliohusika na kuwachukulia hatua. Tunawajua watu hao. Hatutalala mpaka wote wanaohusika wachukuliwe hatua ya kupelekwa kortini na wanapopatikana na hatia warudishe pesa za hicho kiwanda na pia wafungwe jela. Kwa hayo machache naiunga mkono Ripoti hii.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili nami pia nichangie Hoja hii ya Mhe. Mohamed Ali ambaye kwa umaarufu anaitwa "Jicho Pevu." Hii ni Hoja ya maana sana. Katika nchi hii yetu miaka 54 tangu tujinyakulie uhuru suala la afya bado linatuchanganya. Tunatumia pesa nyingi sana kupeleka wagonjwa katika nchi za nje kutafuta matibabu. Hizi pesa zinaweza kutumika katika nchi hii kujenga hospitali ambazo zinaweza kuwa na vifaa maalum.Tuko na madaktari ambao wamehitimu katika nchi yetu wanaoweza kufanya kazi katika hizi hospitali. Ukienda Hospitali Kuu ya Kenyatta utapata kwamba haina vifaa vya kisasa. Hii ni aibu kubwa. Madaktari wapo lakini wale wanafanya upasuaji wanafanya kazi katika mazingira duni kabisa. Lazima tuweke maanani mambo ya afya kwa sababu nchi ambayo haina afya haiwezi kuendelea. Nchi ambazo zimeendelea zimetilia mkazo sana mambo ya afya. Kitu kingine ni kwamba matibabu katika nchi yetu ni ghali sana. Watu wanalipa pesa nyingi. Ndiyo maana unapata watu wanakufa kwa magonjwa ambayo yanaweza kutibiwa. Wagonjwa wengi hawawezi kufika hospitali ama wakifika hospitali huwa hakuna madawa. Lazima Serikali iekeze pesa katika mambo ya afya ili tulipe madakdari vizuri tununue vifaa tuweke madawa katika hospitali na tujenge hospitali za kisasa katika kila kaunti vile Mhe. Mohamed amesema. Tuko na kaunti 47. Kaunti nyingi hazina hospitali za kiwango cha 4 yaani Level 4. Nyingi ni hospitali ndogo ambazo hazina vifaa vya kisasa. Karibu miaka 20 iliyopita nilipopata ajali nilipelekwa Brussels Ubelgiji kwa matibabu. Nikienda huko nilifikiria ninaenda kupata matibabu ambayo hayawezi kupatikana hapa Kenya. Nilipofika huko niliona mambo ya kawaida ambayo yanafanywa hapa Kenya. Kwa sababu hatuna hospitali ya kiwango cha juu singepata hayo matibabu huku kwetu. Mimi ninajua kuna wakenya wengi ambao wanapata ajali katika barabara zetu na hawawezi kufika hospitalini kwa sababu ni ghali na hakuna vifaa vya kusaidia wagonjwa ambao wamepata matatizo ya uti wa mgongo ama wale wa saratani. Ukienda hospitali za kibinafsi kama Aga Khan ama Nairobi utapata wako na vifaa vya kisasa ambavyo vinaweza kutibu aina yote ya magonjwa lakini ni wakenya wangapi wanaweza kufika katika hizo hospitali? Kwa hivyo hii Hoja itawezesha kujengwa hospitali ambazo zitafikiwa na wananchi wa kawaida. Vile vile Serikali inatakikana iangalie gharama ya matibabu kwa sababu matibabu katika zile hospitali za umma inashinda watu. Watu wakienda huko daktari anawaandikia dawa ama vifaa vya kununua ili warudi kutibiwa. Hiyo haiwezekani kwa sababu wananchi wengi wana matatizo mengi. Kuna umaskini na tunatakikana tuangalie kwamba watu wanapata matibabu badala ya kuambiwa waende watafute matibabu pahali pengine. Tukijadili hii Hoja tunatakikana tuifanye sheria katika nchi yetu ili tuanze kufikiria ni namna ipi tutainua viwango vya mahospitali ili tuwe na hopitali ya Level 5 katika kila kaunti; iwe na vifaa vya kisasa dawa na ile huduma ya madaktari kutumwa huko. Kila wakati tuna migomo ya madaktari. Madaktari wa Hospitali ya Kenyatta wamefanya upasuaji hivi juzi na kutibu mtoto ambaye mkono wake ulikuwa umekatika lakini hakuna mtu anawatambua . Wakifanya kosa kidogo utaona kila mtu anawaelekezea kidole cha lawama. Madaktari wanang'ang'ana kufanya kazi katika mazingira duni. Lazima tuangalie ni vipi tutafanya bidii tuweke kiwango cha hospitali zetu kiwe katika hali nzuri. Nashukuru sana Muwasilishi wa Hoja hii Mhe. Mohamed. Naomba Wabunge wenzetu wachangie na kuunga mkono. Mhe. Naibu Spika wa Muda naomba kusema asante kwa Hoja hii na kunipa nafasi kuchangia; asanteni sana.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Hoja hii. Mwanzo ningependa kumpongeza Mhe. Gs Wanga kwa kuja na Hoja hii. Nataka niwe kwa rekodi kuwa nimeunga mkono Hoja hii. Mambo ya saratani ni mambo ambayo yamesumbua wananchi wengi wa Kenya. Ninavyozungumza mimi binafsi katika ofisi yangu pale mashinani nina mmoja wa wafanyikazi wangu anayeugua saratani ya matiti. Ilituchukuwa karibu miaka miwili kumfanyia Harambee mpaka akatolewa lile titi na akawekwa lile titi bandia. Jambo hili ni la kusikitisha kwa sababu yeye aliwapata watu wa kumfanyia Harambee lakini wengine wasio na uwezo wa kufanyiwa mambo kama hayo inakua ni shida. Mhe. Naibu Spika wa Muda tunaona athari ya ugonjwa wa saratani kwa watu wengi katika sehemu nyingi nchini. Watu wakitaka kupata matibabu mpaka waje kwa Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta Nairobi. Kwa Serikali yetu ya Kenya tunasema kuwe na vifaa vya kuangalia mambo ya ugonjwa wa saratani na viwekwe katika kila sehemu na nyanja ya nchi yetu ya Kenya. Mhe. Naibu Spika wa Muda zaidi tunaona ugonjwa wa saratani unasababishwa na mambo ya vyakula. Kupitia kwa wizara inayohusika na mambo ya afya ni vizuri kuona kuwa vyakula vinavyoingia nchini vimethibitishwa kuwa sawa. Isiwe vyakula vinavyowachiliwa kuingia nchini na kusababisha magonjwa kwa wananchi wetu. Tukiangalia hali ya kutibu magonjwa ya saratani imekuwa hali ngumu kwa sababu wagonjwa waathiriwa wanapokuja Nairobi inabidi watafute pesa za kutibiwa kwa kila hatua ya matibabu. Wengi wao hufuata viongozi kama sisi na kuwaambia wanatakiwa kufanyiwa matibabu hospitali fulani kwa wakati fulani. Hivyo wao hutaka pesa za matibabu na makaazi katika sehemu ya hospitali. Naomba Serikali iwe na hazina. Kwanza ingetangaza mambo ya saratani kuwa janga la kitaifa kama ilivyotangaza Ukimwi. Vile vile Serikali iweke pesa fulani zitakazosaidia kiwango fulani cha waathiriwa wa saratani kujikimu. Hii ni kwa sababu wengi wameharibu maisha yao kwa kugharamia matibabu. Watu wanafanya kazi ili wasomeshe watoto waweze kujikimu maishani na kwa mambo mengine mbali mbali. Lakini utamuona mtu anafanya kazi na pesa zote zinaenda kwa matibabu kwa miaka mitano 10 ama 20. Kwa hivyo twatakikana twende mbele. Kwa sababu ya ugonjwa wa saratani maisha ya binadamu ni kama wasemavyo Waswahili: "kiribagoji-gojikiriba." Yaani huendi mbele. Mtu huwa yuazungukia hapo hapo. Naiomba Serikali itilie maanani mambo haya ya kutibu saratani. Sisi kule mashinani katika hazina ya Ustawi wa Maeneo Bunge ni vizuri kuwe na kiwango fulani cha kusaidia kwa matibabu kama hayo. Mwisho nataka kumpongeza dadangu Mhe. Gs kwa kuja na jambo kama hili. Tutamuunga mkono kama Wabunge kuona kuwa tumepitisha Hoja hii kwa njia ya sawa ili wananchi wetu wawe sawa. Ahsante sana kwa kunipa nafasi Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii kuchangia mjadala huu ambao umeletwa na dadangu Mhe. Gs Wanga. Hoja hii imekuja wakati mzuri sana kwa sababu katika eneo langu la Trans Nzoia watu wanaumia kwa ajili ya ugonjwa wa saratani. Wiki mbili zilizopita nilimpoteza mtoto Purity. Mwenzangu ambaye aliwania kiti katika eneo la Endebes Jenipher Masis pia ameathirika na ugonjwa huo wa saratani. Tunapojadiliana katika Bunge hili lazima tuhakikishe kwamba Serikali imetekeleza kulingana na vile sisi viongozi tunataka katika Bunge hili. Tunaweza kuongea hapa na baada ya kuongea hakuna kitu chochote kinachotendeka. Najua kwamba Serikali imesikia na itahakikisha kwamba imetilia maanani maoni yetu na inatekeleza eno haya ya saratani katika nchi yetu ya Kenya. Namshukuru dadangu Mhe. Wanga kwa sababu watu wanalia katika nchi yetu ya Kenya hasa akina mama ambao wanakatwa matiti yao wakiwa bado wangali wachanga. Hawawezi kuwanyonyesha watoto wao kwa ajili ya ugonjwa wa saratani ya matiti. Wenzangu wengi wameongea kuhusu ugonjwa wa saratani. Watu ambao wanakufa ni karibu 18000 na wale wameathirika kwa sasa ni 82000. Hii ni idadi kubwa sana. Tunaomba Serikali ihakikishe kwamba inawahamasisha watu kuhusu ugonjwa wa saratani katika nchi yetu ya Kenya. Namuunga mkono Mhe. Wanga aliposema kwamba tunatakikana tuwe na afisa mmoja katika kaunti. Afisa mmoja hatatosha. Tunapaswa tuwe na afisa katika kila wodi katika nchi yetu ya Kenya ili wahamasishe watu kuhusu ugonjwa wa saratani. Sio hayo tu kuna magonjwa mengi ambayo Wabunge wenzangu wameyasema hapa. Kuna ugonjwa wa Ukimwi. Siku hizi wengi wakiambukizwa ugonjwa wa Ukimwi au saratani wanafikiria wamerogwa. Nataka kuwaambia wale walioathirika na hata wale ambao bado hawajaathirika wahakikishe kwamba wametafuta matibabu kwa wakati unaotakikana. Kuna wagonjwa tuliowachangia lakini kuna wengi ambao hatujawachangia kwa sababu hawajatufikia sisi kama viongozi. Tunawachangia wale ambao wameangaziwa. Asilimia kubwa sana hawatufikii sisi viongozi au hata hospitali kuhakikisha kwamba wamepata nafasi ya kupata matibabu. Pesa ambazo zimeenda katika kaunti zetu na haswa zile ambazo zimeenda upande wa afya hazijwasaidia watu mashinani. Ndiposa viongozi wa kutoka eneo langu tulikuwa tunawaza kwamba sekta ya afya inapaswa kurudishwa katika Serikali kuu ili kuhakikisha kwamba watu wanapata nafasi ya kufikia matibabu kwa wakati unaotakikana. Heko dadangu Mhe. Wanga kwa kuleta Hoja hii katika Bunge hili. Nawaomba Wabunge wenzangu tuipitishe.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii kuchangia Mswada huu. Ningependa kumshukuru Mhe. Wamunyinyi kwa kuleta Mswada huu. Wakulima wa miwa kutoka upande wa magharibi wanaumia sana. Ushuru hutozwa kwa wale watu ambao wanapeleka sukari viwandani. Sukari kutoka nchi zingine hutozwa ushuru mdogo lakini wakulima wa humu nchini wanatozwa ushuru mkubwa. Ningependa kuunga mkono wenzangu kuwa ni lazima Serikali inafaa kuwa na mikakati mwafaka kuhakikisha kuwa wakulima wa miwa wamepewa nafasi ya mazao yao na wapate haki yao kwa wakati unaofaa. Mhe. Naibu Spika wa Muda Mhe. Chris Wamalwa alisema kuwa kiwanda cha mbolea kinachotarajiwa kufunguliwa Eldoret kifunguliwe haraka ili wakulima wa miwa pia wapate mbolea hiyo. Viwanda kama Nzoia Butali na Mumias vimeajiri watu wengi ambao hivi sasa wanajimudu kimaisha. Katika kaunti yangu ya Trans Nzoia wakulima wengi wameacha kupanda mahindi na hivi sasa wanapanda miwa kwa sababu bei ya mahindi imeenda chini. Ni sharti Serikali ijikakamue kutoa ushuru kwa wale wanaosafirisha miwa na wale wanaopanda ili wapate haki yao kwa sababu maisha yao na ya watoto wao inategemea faida kutoka kwa miwa. Natumai Wabunge wataunga mkono Mswada huu ili wakulima wa miwa wapate haki yao. Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii kuunga mkono Hoja ya Mhe. (Dkt.) Ottichilo ambaye ameona umuhimu wa sisi kuzungumzia suala la mazingira. Suala hili limekuwa donda sugu ambalo Wakenya wote wanatakikana kuliangazia. Suala hili limetajwa kwenye Katiba katika Vipengele vya 42 69 na 70 japo kama Wakenya tumechukulia mazingira kama jambo la dhihaka na mchezo na wala sio jambo la kulindwa na kutunzwa. Wakenya wengi wanaugua magonjwa tofauti. Kule mashambani mifugo wetu wanakula karatasi zinazotupwa na wanakufa. Mbuzi wengi wamekufa kwa sababu ya kutafuna karatasi badala ya nyasi. Ni jambo la kusikitisha kuwa kama Wakenya tunafikiria kwamba inatosha tu kufagia nyumba na kutupa takataka hapo nje. Tukisafiri ulimwengu mzima tunaona na kufurahia usafi tunaouona kule. Lakini tunaporudi nyumbani hatujali usafi wa mazingira na maeneo tunayoishi. Sio mara ya kwanza kwa Mhe. (Dkt.) Ottichilo ambaye anaelewa masuala ya mazingira kuleta Hoja kuhusu mazingira. Lakini mara nyingi ametaka kubadilisha sheria ili kutekeleza yale ambayo yako kwenye Katiba yetu ili kuhakikisha kuwa Wakenya wanaishi kwenye mazingira yanayofaa na kudumisha mazingira haswa wakati huu ambapo masuala ya mazingira yameharibu mambo mengi hapa duniani. Ufagio ni chombo kinachotumika kwa usafi na unatakikana kuwa rafiki wa kila mtu. Ufagio pia ni mti ambao hauwezi kukuzwa kwenye maeneo ambayo hayafai. Hivyo basi Hoja hii ya kuwa siku moja kwa mwezi Wakenya wote wajitokeze kusafisha miji yetu ili tuishi kwa mazingira mazuri ni Hoja muhimu na ningependa kuwaomba wenzangu kuipitisha haraka iwezekanavyo ili suala liweze kutekelezwa. Rais alipopata kiti kwa mara ya kwanza alionyesha umuhimu wa kuweka mazingira yetu safi kwa kufagia wakiwa na Gavana wa Nairobi. Lakini hatukufuatia kufanya yale ambayo aliyafanya. Huyu Gavana Kidero ambaye ndiye anasimamia mji wa Nairobi ni kama alisahau suala kubwa analopaswa kuliangalia. Mhe. Spika wa Muda naunga mkono Hoja hii. Nahimiza kuwa vipengele 42 69 na 70 vya Katiba vitekelezwe vilivyo ili tuweze kuweka mazingira yetu yawe masafi. Naunga mkono Hoja hii. Ahsante sana Mhe. Ottichilo kwa kuleta Hoja hii.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii nichangie Mswada huu. Jambo la kwanza nataka kuunga mkono Mswada huu kwa sababu swala la ardhi hasa kwa sisi ambao tunatoka Pwani takribani karibu watu asilimia 80 wanakumbwa na jambo hili kwa njia moja ama nyingine. Vile vile kwa wenzetu katika jamii ya wafugaji jambo hili linawakumba. Ningependa kusema ya kwamba Mswada huu umetambua walemavu akina mama na jamii ya watu wadogo wadogo yaani marginalised community kuwa ni lazima wapate haki sawa sawa. Katika kipengele cha 31 cha Mswada huu kinasema kuwa kila mmoja ana haki sawa ya kumiliki ardhi katika ardhi za kijamii. Kwa hivyo Mswada huu unawapatia nguvu wale wakaaji ama wenyeji ambao wako katika ardhi hizo katika maamuzi yoyote yanayotaka kufanyika katika ardhi hizo. Vile vile tunaona kuwa ikiweza kufanya hivyo itaweza kutoa nguvu kuwa jambo lolote hata likiwa ni la kuekeza watu wenyewe washauriwe halafu kisha baada ya kuweka maamuzi ndio tuone kwa namna gani mipangilio ile itaweza kufanywa. Jambo kama hili mimi binafsi limenifurahisha nikiwa Mbunge wa Jomvu kwa ajili kuna sehemu kadhaa katika sehemu yangu kama vile Aldina Maganda na sehemu nyingine za Bangladesh KCC na Ganahola. Tukiangalia katika sehemu ya Aldina wenyeji walikaa hapo takribani tangu Kenya haijapata Uhuru. Vile vile Tume ya Kuchunguza Mambo ya Ardhi - National Land Commission - ilikwenda pale. Waliweza kuweka jopo na wakasema yule anayedai kuwa mahali pale ni pake ajitokeze. Hawakujitokeza. Huu Mswada unatupa nguvu kuona kuwa wale mabwenyenye ambao wanakuwa na makaratasi ya kumiliki ardhi na wenyeji wakiwa wanaishi mahali hapo hapo itaweza kuwapokonya nguvu. Pia nikiangalia hali hii ya wenyeji ni lazima wahusishwe. Ni muhimu kwa shauri nikiangalia mradi mkubwa sana wa reli unaofanyika watu katika sehemu yangu ya Maganda ambapo inapitia walipewa makaratasi yaani allotment letters kusubiri hati miliki zao. Unaona mradi ule unafanyika mtu anapigiwa hesabu za nyumba yake lakini hapigiwi hesabu ya ardhi. Jambo kama hilo si jambo la sawa sawa. Ni muhimu sana watu watambue wenyeji na wawapatie hati miliki za ardhi ili ziwafanye kuwa na nguvu ya kudai haki yao katika sehemu hiyo. Tukiangalia jambo kama hili limetuadhiri Pwani nzima. Watu wengi katika jamii zao wanasongezwa kando na wale wawekezaji. Hatimaye watu kama hao hawapati haki yao. Naunga mkono Mswada huu na nampongeza ndugu yangu Mhe. Alex Mwiru na Kamati yake yote ya Ardhi kwa kufanya kazi na kuleta mambo ambayo tunayazungumzia katika Bunge hili leo. Kwa sababu zai tulikuwa tunawaita "walala hoi" sasa tutawaita "walala hai" kwa shauri watakuwa na ukweli wa kuona watakuwa na haki ya kumiliki ardhi katika seheme zao. Tukiangalia kuna wale wa jadi. Kama sehemu yangu kuna sehemu inaitwa Kwa Shehe. Wenyeji wa pale walitoka sehemu ambazo hazijapimwa na mpaka leo wanalipa malipo ya ardhi katika kaunti. Jambo hili si la sawa sawa. Ni muhimu wenyeji kupewa hati miliki za ardhi. Mhe. Naibu Spika wa Muda ningependa kuunga mkono Mswada huu lakini kuna mambo ambayo nayapinga. Napinga Kipengee cha 35 ambacho kinasema kwamba mtu akiwa amechukua ardhi ya mtu mwingine kabla ya kupitishwa kwa Mswada huu mtu yule ndiye atakayetambuliwa baada ya kupitishwa kwa Mswada huu kuwa mwenye ardhi hiyo. Nasema vizuri sana kwamba tutaupiga msasa Mswada huu ili tuone kwamba waliochukua ardhi za wenyewe kabla ya Mswada huu
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia huu Mswada. Mwanzo namshukuru Mhe. Kamket kwa kuleta huu Mswada. Mwenyezi Mungu atakubariki. Ningependa kuwaelezea Wabunge wenzangu kwamba huu Mswada ni muhimu kwa sababu kuna watu wengi wanateseka huko ndani ndani. Tusiwe sisi Wabunge ndiyo sababu ya wao kuteseka. Kama mwenzetu alivyosema sisi wengine tumezaliwa katika haya maeneo ambayo yametengwa. Si kuchagua kwetu; ni kwa sababu ya mipango ya Mwenyezi Mungu. Leo nitazungumza kwa kihemko. Kwa wale hawaelewi Kiswahili labda nitasema niko emotional kwa sababu nimetoka Lamu jana. Kwa bahati nzuri tumetoka maeneo ya Kiangwi ambayo ipo Wadi ya Basuba. Iko ndani ya Msitu wa Boni. Kabla niwaeleze yale niliyoyaona kule - ambayo yatawasikitisha - tukipitisha Mswada huu utasaidia haya maeneo. Mwanzo ni muhimu tuunge Mswada huu mkono ili mambo yaende vizuri. Vile ilivyo wengine wametengezewa barabara na kupelekewa maji. Tunasaidia lakini hatumalizi hizo shida. Kuna vijiji vilivyo na shida ya kutokuwa na hivi vitu vyote kama vile maji na elimu. Ningeomba wahusika ikiwezekana wachague vijiji ambavyo vimeathirika kabisa nchini ili visiseme vimetengwa. Kuna vijiji vidogo kama Kiangwi vyenye matatizo yote hapa duniani. Tuzisaidie mpaka ionekane kwamba tumeziinua ili siku zijazo ziwe zimepiga hatua nyingine. Wenzangu wamechangia elimu. Ningependa kushukuru Wizara za Elimu na Usalama. Kwa miaka mitano shule za Kiangwi na Basuba zimefungwa. Jumatatu ya wiki hii tumekwenda na tukakubaliana shule hizo zifunguliwe baada ya mimi kufuatilia na kupiga kelele. Nashukuru maana walisema shule zote zitafunguliwa baada ya miaka mitano. Hakuna Mbunge yeyote ambaye sehemu yake shule zimefungwa hata kwa mwaka mmoja. Tukizungumza kuhusu kutengwa tunajua tunazungumza nini. Hatujipendekezi tu. Ni baada ya miaka mitano shule hizi zinaenda kufunguliwa. Nashukuru wamefanya hivyo. Nilikuwa na wenzetu kutoka idara mbali mbali tulipoenda kujionea mambo ya pale Kiangwi. Tulipokuwa kule kuna mmoja wa wahudumu wa Kenya Red Cross amabaye katika mazungumzo yake aliwaambia watu wa Kiangwi kuwa kwa sasa mvua inanyesha wahakikishe wameficha vyeti vyao vya kuzaliwa hata ikiwa watazipeleka kwa majirani wao ili zisinyeshewe. Usemi kama huu utakueleza hali ilivyo. Watu walio kule wananyeshewa kutokana na shida zilizoko. Ni vizuri sisi kama Bunge tupange Wabunge watembee waone zile hali. Tulipoenda kama kamati Lamu tuliaambiwa mbona tunasema tumetengwa na Lamu Town iko sawa. Kuna sehemu ndani ya Lamu County ambazo ukienda zitakusikitisha. Elimu haipo. Kuna jamii ambazo mpaka sasa hazijapata mtu aliyehitimu na shahada ya digrii hata mmoja. Pia hazina barabara na maji. Tukipewa hizo pesa wale watakaozishughulikia wamakinike kwa kuwa watawajibika kwa Mwenyezi Mungu. Kwa mfano kuna pesa ya Equalization Fund zilizopelekwa kwa mradi wa maji unaoitwa Kigai-Kiunga. Mradi huo haupo. Pesa hizo zilipelekwa kwingine. Watu wa sehemu hizi ni fukara sio maskini. Maskini ni afadhali. Wale ni fukara; hawana hata chakula ilihali pesa za mradi kama huo zinapotolewa zinapelekwa kwingine. Nilipiga kelele kwa wahusika na wakasema watapeleka mradi mwingine kule. Mradi huo wa Kigai-Kiunga sasa haupo kwa watu maskini ambao hawawezi kujitetea. Tulipoenda Kiangwe hata nguo za kuvaa watu hawana. Ilibidi nimwambie mhudumu mmoja wa ofisi yangu aivue T-Shirt yake amvalishe mtoto aliyekuwa na vazi la aibu lililo chanika. Matatizo yako. Hatutaki kuwa hivo siku zote. Tunataka siku moja hili tusemalo kuwa sisi ni jamii iliyotengwa lisiwe. Tuinuliwe ili wengine kutoka county zingine waje waangalie makwetu. Hatupendi kujiita hivyo. Kwamba siku zote tunalalamika tumetengwa. Hatupendi kuitwa hivyo; ni hali zimetuwia tu. Wanaofanya kazi Kiangwe hawatoki Lamu County peke yake. Kuna wafanyikazi kutoka county zote. Kwa mfano kuna watu wanaofanya kazi kwa Jeshi. Kwa hivyo wanaofanya kazi kule wana matatizo mengi kwa sababu ya ukosefu wa vitu kama barabara maji na hospitali. Wanaofanya kazi kule ni wenu pia; wateteeni maana wanapoenda kule pia wao wanapata shida hizo. Nilienda kuona Jeshi kule. Wana shida. Zile sehemu ni ngumu. Ukienda kuwaona askari wanaokaa kule na kulipwa sawa na walio kwingineko pia nao wanapata shida. Kuna sheria zimewekwa kwamba walimu wapelekwe kokote kwa sababu Serikali inataka tujumuike pamoja kama Wakenya. Walimu wakitolewa Lamu kupelekwa sehemu zingine imekuwa sawa. Lakini wa sehemu zingine wakipelekwa Lamu wanakimbia. Hawawezi kuishi katika yale mazingira. Tunaomba serikali inapopanga policies sehemu kama Lamu iangaliwe. Mhe. Naibu Spika wa Muda ukiniruhusu hiyo delocalisation haifanyiki Lamu ingawa inalazimishwa. Sisi wakati mwingine tunaenda extra mile kusomesha wanafunzi wa kule Kiangwe ili waweze kufundisha sehemu yao ya Waboni na pakitokea shida wasikimbie. Utapata kuwa wale waliokubali tukawasomesha hukubali kuchukuliwa kupelekwa sehemu zingine ilhali wengine wakipelekwa Kiangwe hawataki kwenda. Sera hii ni nzuri lakini haiwezi kutekelezwa Lamu. Tunataka tufikiriwe katika swala hili. Nimelalamika kuwa walimu wameandikwa lakini wanapelekwa kaunti jirani na wale wa county jirani wanaletwa kwetu. Watafanya kazi kivipi na shida ya Boni imekuwepo kwa miaka mitano? Ukiwaleta walimu watakimbia na shida zetu zitasalia kuwa vile vile. Kwa hivyo kabla ya sheria hii kupitishwa watufikirie maana kila wanapobandika sheria hizi kwa nguvu na hazitekelezeki wanazidi kutusukuma chini. Ninaunga mkono Mswada huu na ninaomba Mhe. Kamaket na Waheshimiwa wenzangu watuunge mkono. Kama hamuamini ninayosema naomba mtembee Basuba Ward mujionee; mtalia. Sizungumzi kuhusu sehemu zingine za Lamu. Watu hawana hata nguo za kuvaa. Sasa nina mobilise nipate guo nipeleke kule. Sikatai kuwafanyia haya lakini hatuna ule uwezo wa kuwafanyia haya. Ahsante.
Ahsante sana mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Mimi pia ningependa kuchukua nafasi hii nimshukuru Rais kwa Hotuba yake na yale aliyotupatia wiki iliyopita. Nilifurahishwa sana na mambo; Rais alisema kwamba hatutalipa pesa za mtihani wa kidato cha nne na pia darasa la nane. Hiyo ilinifurahisha sana kwa sababu kuna watoto wengi ambao wameishi katika maisha magumu ama wanaishi katika maisha yasiyo sawa na hawangeweza kulipa pesa za mtihani. Pili nataka kumshukuru Rais kwa kuongea juu ya umeme. Ni kweli tusipokuwa na umeme katika nchi yetu ya Kenya utaona kwamba hakutakuwa na kazi nyingi zakufanya katika sehemu zetu. Wengi wa watu wa jua kali akina mama wa kuuza mboga ama vijana wale wanaendesha piki piki Kwa kweli ni lazima tuwe na umeme ndiposa mambo ya usalama yaende sambamba. Tatu ningependa kumshukuru Rais kwa sababu aliongea kuhusu matibabu na kuwa na kadi za NHIF ndiposa jamii zinazotoka katika maisha ya umaskini wapate matibabu katika hospitali zinazostahili. Pia namshukuru Rais kwa sababu ya hazina ya Uwezo Fund. Imewafikia akina mama kule mashinani na pia vijana wetu; hatukuwa na hizi pesa na vijana na akina mama wetu walikuwa wakiangamia. Lakini sasa ninafurahi sana kwa sababu akina mama wanaweza kufanya biashara zao vijana wetu si kwamba ni piki piki pekee ama baiskeli peke yake ila wana njia nyingine za kujiendeleza kimaisha. Ningependa pia kumshukuru Rais kwa sababu ya pesa za wazee. Zile pesa zimeweza kuwafikia wazee kule mashinani. Kuna pesa za watoto mayatima. Hizi pesa pia zimeweza kuwafikia watoto mayatima katika sehemu tunakotoka. Kile pia ningependa Rais asisitize ni mambo ya mashamba. Kweli tumekuwa na ufisadi kuhusu mambo ya mashamba kwa sababu kuna matapeli wanaojaribu kupata vyeti ama title deeds vya mashamba yasiyo yao. Kama hivi juzi nilikuwa Cherangany. Kuna shule moja iliyokuwa imenyakuliwa shamba lake. Halikuwa jambo zuri kwa sababu unyakuzi wa mashamba umezidi sana katika nchi yetu ya Kenya. Ningependa Rais aorodheshe majina ya wafisadi ama watu wanaojaribu kunyakua mashamba yasiyo yao. Unaona kwamba shule nyingi hazijapata title deeds lakini ninataka kumshukuru Rais kwa sababu amesema kwamba ifikapo mwaka 2017 title deeds milioni tatu ziwe zimetolewa kwa watu wanaostahili. Ningependa hiyo iharakishwe sana kwa sababu katika Trans Nzoia kuna mashamba kama Matunda na Cherangany. Haya mashamba hayajatolewa title deeds; kama moja ya haya mashamba litapata title deeds tutafurahi sana. Nikimalizia ningesema kwamba mambo ya ufisadi katika nchi yetu ya Kenya Ni lazima sisi Wabunge tumuunge Rais mkono ili tuhakikishe kwamba mambo ya ufisadi yanaisha. Katika hii orodha ambayo imeletwa tunaka kuona uchunguzi utakavyofanyika ndiposa tujue huyu amefanya nini na yule amefanya nini. Ninaomba kwamba sisi kama viongozi tuunge mkono Rais na naibu wake ili tuhakikishe kwamba tunapata maendeleo katika miaka mitano tuliyochaguliwa kuhudumu. Ahsante sana.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu hata vyama vidogo vinachangia katika uchumi wa nchi hii. Ukiwa na watoto na uanze kuwabagua na kusema: "Huyu anatambaa hastahili kupata huduma kutoka kwangu; nitahudumia yule ambaye tayari yuko mbio kujitafutia" hapo husaidii. Itakuwa ni busara kwetu ikiwa wakati wa marekebisho ya mwisho tuseme kwamba chama chochote kitakachokuwa na mwakilishi Bungeni kifadhiliwe kwa sababu kimeweza kuweka kiongozi Bungeni kupitia kwa wanachama na wananchi ambao pia wanachangia hela za kuendeleza hivi vyama na hata nchi. Tukisema hivi vyama vidogo havistahili kupata huu mgao tunajaribu kuvunja demokrasia. Tunataka uwazi na nafasi kubwa ya demokrasia ionekane katika nchi hii kwa kuvipa nafasi vyama vidogo vidogo fedha. Nakumbuka mwaka wa 2002 nilikuwa Mbunge wa pekee wa Chama cha Shirikisho. Ni hali ngumu kwa mtu mmoja kufadhili chama mpaka kifikie wakati wa uchaguzi mwingine. Ni shida kukifadhili chama. Hivyo basi ni vyema kwamba chama chochote kilicho na Mbunge kifadhiliwe. Kwa hayo machache Mhe. Naibu Spika wa Muda naunga mkono Mswada huu.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Ningependa kuchangia wazo hili ambalo linahusiana na ulipaji wa wakulima wa miwa katika viwanda vyetu. Jambo hili linashangaza sana. Ukulima umekuwa ni hasara. Hasara hii si kwa sababu ya mkulima bali ni kutokana na usimamizi mbaya wa viwanda vya sukari. Viwanda ambavyo vimefungwa kwa sababu moja ama nyingine ni Miwani Muhoroni Ramisi Chemilil na Nzoia. Ni sababu gani viwanda hivi vya kusaga miwa vinafungwa? Je ni uongozi mbaya ama ni gharama kubwa ya uzalishaji wa miwa? Sababu ni nini? Serikali imekuwa ikisimama na mkulima Miswada imewekwa Bungeni sheria zote zimepitishwa lakini ni kwa nini mkulima hapati haki yake? Mimi kama Mbunge wa Mosop naona wananchi wangu wameanza kuchukua mashamba yao ya kukuza mahindi na wameanza kupanda miwa. Kampuni ambayo kwa sasa inanunua miwa yetu ni kampuni ya Butali. Kwa sasa tunaona kwamba kuna faida. Lakini swali ni hili: Kama wale ambao walianza mbeleni viwanda vyao vimefungwa sababu na kisa ni nini? Vile wenzangu wamesema ni kwamba kuna ufisadi mkubwa katika wizara na usimamizi wa viwanda hivi. Jambo lingine ambalo ningependa kuongelea ni hali ya anga inayochangia katika sehemu zetu. Tunajua kwamba ulimwengu mzima hali ya anga na hali ya kutokuwa na mvua inaharibu na inachangia pia katika mazao ya mkulima; kwamba ekari moja haitaweza kutoa mazao yanayowezesha mkulima yule kupata faida. Jambo hili ni la maana. Inatubidi sisi kama Wabunge tuangalie ni nini tunahitaji kufanya. Kama ni unyunyizaji wa maji katika sehemu zile ziko na maji ili tupate mazao tupitishe sheria kama hizo. Wakulima wa miwa wanatakikana kusaidiwa na Serikali wapate mbolea kupitia subsidy. Kusaidiwa mbolea na Serikali ili kuimarisha matokeo ama mapato yao. Ni jambo la kushangaza kuona kwamba mkulima ako na miwa na hawezi kumpeleka mtoto wake shule hawezi hata kulipia mahitaji yake kama binadamu kwa sababu kupanda miwa kwake ni kutoka mwezi wa kwanza mpaka mwezi wa kumi na nane ambao ni muda mrefu sana kwa mtu yeyote ambaye anafanya biashara ya ukulima. Sisi kama viongozi na watunzi wa sheria lazima tuwajibike na tuone kwamba mtu yeyote ambaye amekuza chochote ambacho ni cha kumsaidia kwa ukulima apate faida yake na malipo yake apate siku kumi na nne baada ya kupeana mazao yake. Nachukua nafasi hii kumuunga mkono Mhe. Melly kwa wazo hili kwamba wakulima wote wa miwa na hata wa mahindi - Nashukuru kwamba katika ile orodha ya pesa tumepitisha siku ya leo wakulima wa mahindi na wa kufuga mifugo watafaidika kwa kuwa na pesa za kununua mahindi yao. Hili ni jambo muhimu. Lazima tuweke kwamba mkulima yeyote akipeana mazao yake kwa halmashauri ya miwa ama kwa kiwanda chochote alipwe baada ya siku kumi na nne. Naunga mkono kwa dhati.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Ningependa kuongeza sauti yangu na kuunga wenzangu mkono. Kuna umuhimu kwa Wakenya kufahamu kuwa mhasibu ni mtu ambaye ana kisomo cha shahada ya juu. Hawa ambao wamepatiwa sheria hii kuwalinda ni aibu ama wasaidizi wa wahasibu. Hivyo basi ni muhimu kwa watu kujua tofauti ya aina mbili za wafanyakazi. Wale ambao watakuwa wasaidizi wakitaka kuitwa wahasibu basi ni sharti warudi vyuo vikuu wakasome kazi ya uhasibu. Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Pia namshukuru Mhe. Okoth kwa kuleta Hoja hii kwa sababu ni jambo ambalo limetutatiza sana. Wakati umefika ambapo elimu yetu ya Kenya iweze kupigiwa msasa kamili kwa sababu kunayo matatizo mengi yameikumba kuanzia wanafunzi mpaka wale ambao wanawaangalia kama vile wazazi au wale ambao wanawachunga. Kuanzia mambo ya kulipa karo na vilevile kuangazia mambo ya vile uchaguzi unaofanywa watoto wakienda katika kidato cha kwanza unapata kwamba kuna kuwa na ubaguzi sana wakati wa kuchagua wanafunzi ambao wataenda katika kidato cha kwanza na hii imeleta kero sana kwa wazazi ambao wanataka elimu bora katika maisha ya watoto wao. Tukiangazia mambo ya kulipa karo ni kwamba jambo hili limekuwa jambo zito sana haswa kwa wananchi wa kawaida wa Kenya. Pesa ambazo tunalipa kama wazazi ni nyingi mno. Mimi kama kiongozi anayesimamia kaunti yote nzima sina kitengo ambacho kimetengwa kama CDF ama"bursary" lakini kila mwaka lazima niandike cheki ya Kshs.800000 ili watoto waweze kusoma. Unapata kwamba wanaopata mzigo huu sana sana ni wanawake. Wanawake wanaumia katika mambo ya kulipa karo za watoto. Ni kitu ambacho kinaumiza sana wakati pia akina mama wanatukanwa wakiambiwa: "Kwani hawa walimu ni wa mama yako". Hilo ni jambo la kushangaza - kwamba hata sisi akina mama hatupatiwi heshima na sisi ndio tunaumia na kubeba mzigo wa wanafunzi ili waweze kusoma. Tukiangazia pia katika mambo ya walimu wamekuwa kila mwaka wanaandaa.Wakati umefika sasa kwa Serikali viongozi na wanaoshughulika mambo ya elimu kuketi ili jambo hili liweze kutatuliwa mara moja ili watoto waweze kusoma. Hii ni kwa sababu tunawanyima watoto haki yao ya kupata elimu. Kwa hivyo katika mambo ya karo ni lazima tuketi tuweke vichwa pamoja na tuhakikishe kwamba wanafunzi wanaweza kupata haki yao ya kusoma. Vile vile naangazia pia wanafunzi ambao hawapati zile alama za kuweza kwenda kidato cha kwanza. Kama mwaka jana kuna watoto 2000 ambao hawakuweza kwenda kidato cha kwanza kwa sababu hawakuweza kupata ile alama ya 200. Ni lazima tuketi chini tuangazie jambo hilo hili tusiwanyime watoto haki yao. Watoto wa miaka 13 tunasema waende "polytechnic". Hakuna mikakati tumeweka ya kuhakikisha kwamba watoto wameenda "polytechnic". Wengi wanaingilia mambo ya madawa ya kulevya na kufanya ukahaba. Kwa hivyo ni lazima tuweke vichwa vyetu pamoja ili tuweze kulitatua jambo hili. Ahsante sana.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Ugonjwa wa saratani ni shetani kwa sababu uliuwa mama yangu. Mimi niliweza kuzunguka na yeye Kenya nzima. Hakuna mahali sikuenda na yeye. Tulikuwa na uwezo wa kumnunulia dawa lakini baadaye pesa ziliisha kwa sababu ya huo ugonjwa. Kule mashinani watu wengi hawana uwezo wa kuja huku Nairobi kutibiwa. Saa hizi mtu akipatikana na huo ugonjwa anajua ya kwamba yeye anaenda kufariki. Kama ingewezekana tungekuwa na madaktari kule kwenye kaunti ambao watawasaidia wananchi ambao hawana uwezo wa kuja Nairobi. Ukiangalia mwaka huu kuanzia Januari wake wa magavana wa serikali za kaunti wamekuwa wakitembea kule mashinani na magari wakiwashughulikia wagonjwa wa saratani. Zile pesa ambazo serikali za kaunti zimepewa za kuwashugulikia watu hao hawangepatiwa. Pesa hizo zingebaki kwa Serikali Kuu. Serikali Kuu ingeweza kuwachagua madaktari ambao wangewashugulikia watu hao. Tungefanya hivyo kuliko kutuma hizo pesa za ugonjwa wa saratani kwa serikali za kaunti. Serikali za kaunti siku hizi zimekuwa za "wanyama" ambao hata hawajali mambo ya watu. Wanajali mifuko yao. Namuunga mkono Bi. Wanga kwa kuleta Hoja hii hapa Bungeni. Watu wengi sana wanahangaika kule mashinani. Nikimalizia ningependa kusema ya kwamba ugonjwa huo ni mbaya sana na kila mtu anauogopa. Nimemsikia Mheshimiwa akisema watu wengi wanaogopa kwenda kupimwa. Ndani ya Bunge hili tuko Wabunge wengi. Hatuwezi kukosa wawili ama watatu ambao wako na ugonjwa huo. Hata mimi naweza kuwa nao. Lakini naogopa kwenda kupimwa na nipatikane na saratani kama ile ya mama yangu halafu nife. Kama inawezekana tuwe na madaktari kule mashinani wa kuwashughulikia watu hao. Nikimalizia nawaeleza Wakenya ambao wanatusikiliza tukiongea kwamba pesa ambazo zinapelekwa kwa serikari za kaunti zinapitia katika Bunge hili kama Bajeti. Kwa mfano tunajua pesa za Kajiado Kilifi Mombasa Nairobi Kericho na Meru ni ngapi. Hizo pesa ni nyingi na zimepewa kaunti ili washughulikie hospitali lakini zikifika huko hazishughulikii mwananchi wa kawaida aliye na taabu nyingi sana. Ukienda Hospitali ya Meru haiko vile ilivyokuwa wakati wa Rais mstaafu Kibaki au "Nyayo". Ilikuwa safi sana na haikuwa na harufu yoyote. Hivi sasa watu wanaoishi karibu na chumba cha kuhifadhia maiti cha Meru wameanza kuhama. Pesa hizo ambazo Serikali kuu inapatia serikali za kauti ili zishughulikie hospitali za kaunti huenda kwa hospitali za kibinafisi au kwenye mifuko yao. Naunga mkono Hoja hii ya Bi. Wanga. Itawezesha kuwa na madaktari kule mashinani.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi kutathmini Ziara ya Rais wa Marekani Obama. Kwanza kabisa natoa pongezi kwa Serikali ya Kenya ikiongozwa na Mhe. Uhuru pamoja na Serikali ya Marekani kwa kufanikisha ziara hiyo. Ziara hiyo ilikuwa ya kihistoria. Kwanza kabisa Obama ni Rais wa Marekani wa kwanza kuja Kenya. Rais Obama pia ana asili ya Kenya kwa sababu ana mizizi yake Kogelo. Pia tunatoa pongezi kwa Rais Obama kwa sababu anajua "mwacha asili ni mtumwa." Hajaacha asili yake. Ningependa kutoa pongezi kwa Rais Obama kwa kuzungumzia uimarishaji wa uwezo wa kiuchumi wa akina mama na vijana haswa alivyozungumzia fedha ambazo zitatolewa kuhakikisha ya kwamba akina mama na vijana wameimarika katika biashara. Kwa hivyo sisi kama Wakenya na viongozi tuhakikishe kwamba fedha hizo zitafika mashinani kusaidia wale ambao wameanzisha kampuni miradi ama biashara. Hizo fedha zisibakie tu kwa wale ambao tayari wameimarika ama wamebobea katika biashara. Tukifanya hivyo tutaona shabaha yetu imefika. Rais Obama alisema kwamba sisi kama Wakenya ama kama Afrika tunaendelea lakini lazima tufanye maamuzi magumu. Maamuzi magumu aliyoyazungumzia ni kama kupigana na ufisadi. Lazima tuseme ukweli na tuwe tayari kusema kwamba tumechoshwa na ufisadi na wafisadi wapate adabu. Pia alizungumzia jambo la ukabila ambalo ni donda sugu na limekithiri katika nchi yetu ya Kenya. Alisema lazima tuache ukabila na mtu asitambulike kwa jina lake la mwisho. Kwa mfano nikisema naitwa Mishi mtu ataniuliza Mishi nani? Nikisema jina lingine la Kiarabu bado ataniuliza jina jingine. Nikisema Mboko atajua natoka Pwani. Katika misingi kama hiyo tunaweza kuhujumiana. Kwa hivyo inafaa tumalize ukabila kabisa. Rais Obama alisema kwamba kuna mapengo ambayo yamekuwa katika Jamhuri yetu katika hali ya kuendeleza usawa. Alipeana mfano wa tofauti kati ya mtoto wa Bonde la Ufa na mtoto wa Nairobi kwa kupata haki za elimu. Pia akazungumzia ukosefu wa usawa kati ya mtoto wa eneo la kati na mtoto wa Nyanza kwa kupata huduma za afya. Jambo hili sio jambo la uchochezi. Ni jambo ambalo sisi kama viongozi wa nchi lazima tulitathmini na tuhakikishe ya kwamba yale mapengo ambayo yaliwekwa kuanzia utawala wa ukoloni ambayo yalichangia sehemu fulani kuendelea kimiundo msingi kiafya na kielemu sasa tuendeleze sehemu ambazo zina umaskini na sehemu ambazo hazijawahi kustawi kimaisha na kiuchumi ili ziwe sawa na sehemu zingine za Kenya. Rais Obama alitambua mashirika yasiyo ya kiserikali na akakuwa na kongao nayo. Walizungumzia changamoto ambazo wameziona katika utawala na katika mipango mingi ya nchi inayoendelea ikiwemo haki za wanyama pori na haki za watoto wa kike katika kupata masomo. Rais Obama alisema kwamba mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ni mashirika ambayo yanatetea wananchi. Hivyo basi kama Wakenya tusihujumu mashirika ambayo yanafanya kazi kihaki kutetea haki za Wakenya. Kwa mfano hilo Shirika la Haki Afrika liloko Mombasa na Pwani kwa jumla lilikuwa limepokonywa kibali kwa sababu za kiholela sizizokuwa na msingi. Lakini shirika hilo lilitambuliwa na Mheshimiwa Rais Obama na lilikuwa katika kongao lile. Pia nataka kusema kwamba Mheshimiwa Rais Obama hakuweza kuwasahau viongozi wa upinzani. Alijua katika demokrasia kuna Serikari na pia kuna uongozi wa upinzani. Aliwapatia masikio yake na wakakaa chini na kujadili
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi kuzungumzia Mswada huu ambao unazungumzia taratibu za shule za chekechea. Masomo ya shule za chekechea ndiyo nguzo ya masomo katika zile ngazi zote mpaka chuo kikuu. Kwa muda mrefu sana nchi yetu ilikuwa imepuuza masomo hayo ya chekechea. Hivyo basi watoto wengi wamekosa kupata masomo ya chekechea. Ni muhimu sana na nimefurahi kwamba Mswada huu unazungumzia miundo misingi ya kuwezesha kuwepo katika hii Jamuhuri yetu ya Kenya shule za chekechea. Ingekuwa vizuri zaidi iwapo tunajenga shule mpya tujenge hapo hapo shule ya chekechea shule ya msingi na shule ya upili. Tukifanya hivyo tunawapatia fikra watoto wetu kwamba masomo ni mtiririko wa ngazi fulani mpaka kufikia ngazi fulani. Hivyo basi tutaweza kuzuia watoto wengi kuacha shule katika chekechea ama katika shule ya msingi bila kuendelea hadi chuo kikuu. Nashukuru kuletwa kwa Mswada huu kwa sababu unazungumzia elimu bora. Utatuwezesha kuhakikisha kwamba elimu inayopeanwa katika shule za chekechea inaambatana na ratiba ya kitaifa. Kuna shule nyingi za chekechea ambazo zimefunguliwa na watu binafsi. Ukipitia katika shule zile unapata kwamba yale masomo yanayosomeshwa hapo ni tofauti sana na masomo katika shule za chekechea za umma. Tatizo hapa ni kwamba watoto wetu wanakuwa na mbinu tofauti za kielimu. Kunatokea mtafaruku katika mitaala ama "syllabus" katika lugha ya Kiingereza. Tunapozungumzia hili suala la shule za chekechea tunatakikana tufikirie zile sehemu kame - yaani sehemu za wafugaji ambazo zina umaskini sana. Sharti tuweke mipango ya chakula hata kama ni kuwapa watoto vitafunio. Wakati wanapopumzika shuleni wapatiwe angalau chakula kidogo ili waweze kuhimili hali ngumu. Tunatakikana kuwa na takwimu ili tujue shule za chekechea ni ngapi. Utapata katika eneo Bunge fulani kuna zaidi ya shule za msingi 20 lakini shule za chekechea labda ni tano ama sita. Sijui ni hesabu gani ambayo itawezesha wale watoto wa chekechea waweze kupanda hadi daraja la pili la elimu. Kwa hivyo tunapojenga shule za msingi basi tujenge shule za chekechea sambamba ili hesabu iwe sawa. Vile vile nimefurahi kwamba kutakuwa na ushirikiano wa Serikali kuu serikali ya kaunti na watu binafsi ambao wanajenga shule za chekechea. Ninayo furaha kwa sababu Mswada huu unapendekeza kushirikishwa kwa washikadau wengine. Hili ni suala ambalo lazima litiliwe uzito. Waswahili wanasema: "Samaki mkunje angali mbichi." Lazima watoto wetu tuwafunze maadili mema katika shule za chekechea ndiposa waweze kuwa na maadili mema. Kwa sababu sasa tuna ugatuzi lazima Serikali za ugatuzi katika kaunti zetu ziweze kuongeza bajeti ili shule nyingi za chekechea zijengwe na hata kuboresha zile ambazo ziko. Zile ziliopo zinatupatia masikitiko sana. Nyingine watoto wanasoma kwenye uwanja. Wanapata maradhi na hata funza. Tumezungumzia katika Mswada huu kuwa elimu hii ya chekechea iwe lazima na bure. Pindi tunapopitisha mambo kama haya lazima tuhakikishe kwamba hata yule aliye chini kabisa kwa mfano katika sehemu ya North Horr Hayo maeneo yana ukame na shida nyingi. Kwa hivyo sharti tuweke miundo misingi ambayo itahakikisha kwamba walimu watapatikana na vifaa vinavyohusika vitapatikana ili watoto hao waweze kupata masomo mazuri. Mafunzo ya walimu wetu wa shule za chekechea lazima tuyapige darubini. Kuna taasisi nyingi ambazo zinafundisha watu elimu ya chekechea lakini utakuta zina tofauti. Nyingine ziko pale kwa kujibinafsisha ama kwa sababu ya kujipatia pesa. Unapata wengine wanaambiwa watahitimu baada ya miezi mitatu ama miezi sita ama mwaka moja. Inakuwa hakuna kanuni ya kitaifa inayoshikilia kwamba ili mtu afuzu kutoka taasisi ya kuwafunza walimu wa shule za chekechea sharti awe amesoma kwa muda fulani ndiposa apate shahada. Kwa hivyo mikakati hii lazima tuiangalie ndiyo tujue kwamba watoto wetu watapata mafunzo yaliyosawia na kanuni zetu. Tukifanya hivyo tutaboresha elimu ya watoto wetu. Vilevile lazima tuwaangalie watoto ambao wana ulemavu. Ama kwa kweli sisi kama Wakenya hapa tumeanguka mtihani. Hii ni kwa sababu hata katika shule zetu za msingi bado hatuna miundo misingi ya kuwawezesha watoto walemavu kupata elimu bora kama wale watoto wasio na ulemavu wowote. Kwa hivyo ni lazima serikali za kaunti - kwa sababu tumeambiwa tumefanyiwa ugatuzi - zishirikiane na Serikali kuu katika kushughulikia watoto walemavu. Hao ni watoto wetu pia na lazima wapatiwe haki zao. Zile shughuli ambazo tunaona ni za kimsingi kwa mfano kuhamasisha kueneza na kutoa habari kuhusu masuala ya shule za chekechea lazima tuzifanye. Nakubaliana na Mswada huu kwa sababu umezungumzia mambo haya yote. Mswada huu pia umezungumzia suala la ukaguzi wa kijamii katika kuangalia matakwa ya shule za chekechea. Hili litatuwezesha kujua takwimu kuhusu asilimia ya watoto ambao wanapaswa kuhudhuria masomo katika shule za chekechea. Tukiangalia watoto wengi wanakaa nyumbani na kwenda tu kuanza darasa la kwanza. Inakuwa vigumu kwa mtoto kama huyo kufanya vizuri darasani kwa sababu atakuwa amekosa nguzo ambayo ingemwezesha kuwasiliana na mwalimu kwa njia rahisi akiwa kidato cha kwanza. Vile vile ili shule hizi ziendeshwe vizuri na kuwe na utekelezaji kulingana na kanuni na sheria ni lazima kuwe na bodi ya utekelezaji. Tusichukulie kuwa hii ni elimu ndogo kwa sababu tunasema kuwa kila kitu ni lazima kiwe na nguzo. Ni lazima tuwe na bodi ambayo itaangalia shughuli zote husika na kuboresha elimu hiyo. Serikali za kaunti sharti zichukue hatamu na kubidiika kuonyesha kwamba hili ni jambo muhimu. Ni sharti waweke mikakati zaidi ya kuboresha elimu ya chekechea. Tukiangalia usalama wa watoto wetu ni masikitiko makubwa kuwa kuna pahali ambapo shule za chekechea zimejengwa karibu au pembezoni za barabara na hakuna vigezo vyovyote vya kuwasaidia watoto wale kupita huko. Hayo ni matatizo makubwa. Kiafya chekechea nyingi hazina sehemu za kujisaidia ama kupumzika wala watoto kujivinjari kimichezo. Katika elimu vitu hivi ni msingi na tusiache kwa kusema kuwa ni vitu vidogo. Majanga hutokea na ni muhimu tujue vigezo ambavyo vitasaidia kukitokea moto na kuhakikisha kwamba watoto watakuwa salama. Mhe. Spika najua wenzangu wangependa kuzungumzia suala hili lakini ni vizuri tujue jinsi tutashirikiana kuimarisha shule za chekechea. Ni lazima pia tuwaboreshe walimu kwa kuwapa mishahara.
Ahsante sana mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili kuchangia Mswada huu. Kwanza ninataka kuunga mkono Mswada huu kwa ajili naamini kuwa ni muhimu kuwa na mkaguzi wa hesabu kwani itawezesha Serikali kutumia fedha kwa njia ya sawa sawa na njia ambayo itakuwa ya kujulikana. Inatakikana pia kuona kuwa mkaguzi wa hesabu hataegemea upande wowote katika kufanya kazi yake. Inatakikana kazi yake kubwa kuona kuwa anakagua hesabu za fedha ama rasilimali za pesa za wananchi na kuona kuwa hesabu hizo ni sawa sawa. Katika kipengele cha 25 cha Mswada huu ningependa kuunga mkono kwani nimeona kimependekeza kuundwa kwa bodi ya ushauri ambayo itakuwa ikimshauri mkaguzi wa hesabu katika kufanya maamuzi. Vilevile naona kuwa katika Mswada huu kazi ya bodi hii imeweza kuonyeshwa katika kipengele cha 27 na kazi yake kubwa itakuwa kutoa ushauri kwa mkaguzi wa hesabu ili kuona kazi hii itafanyika sawasawa. Ni lazima pia ofisi ya mkaguzi wa hesabu ipewe uwezo wa kuchukua hatua kwa wafujaji wa rasilimali kwa sababu tumeona kuwa ofisi hii ya mkaguzi wa hesabu hutoa hesabu zake na ikasema watu kadhaa ama kitengo fulani wamefuja mali ama rasilimali. Haya yamekuwa ni maoni tu yametolewa na hakuna hatua yoyote imechukuliwa. Kwa hivyo ningependa kuona kuwa ofisi hii imepewa nguvu pamoja na bodi yake wakati wowote ambao itaona kuna ufujaji was pesa ama hesabu hazikuenda sawa sawa ichukulie hatua watu ambao watakuwa wamefanya mambo yasiyo ya sawa. Mwisho kabisa nataka kuunga mkono Mswada huu kwa sababu umekuja kwa wakati mwafaka. Tumeona mambo mengi kama ya Anglo Leasing Goldenberg na mengine ambayo yalitokea lakini kwa vile hakukuwa na kitengo ambacho kilikuwa kimethabitiwa vizuri tunaona ni mazungumzo yamezungumzwa halafu baadaye rasilimali ya wananchi ikapotea katika mikono ya watu wengine. Kwa hivyo bodi ikiwako pamoja na ofisi hii nina hakika zitaweza kuchukua hatua ambayo itaweza kulinda rasilimali zetu sisi kama wananchi wa Kenya. Kwa hivyo ninaunga mkono Mswada huu na kusema kuwa ni muhimu tuweze kuupitisha. Ahsante.
Ahsante sana mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kuunga mkono na haswa pia kulizungumzia suala hili ambalo dada yangu mhe. Lay ameweza kulileta hapa Bungeni - kuhusu umuhimu wa kuzitafi sheria zetu kwa lugha ya taifa. Ninampongeza Bi. Lay kwa kuileta Hoja hii ambayo ni ya muhimu sana. Ukiangalia Kipengele cha 7(2) ambacho kinazungumzia masuala ya jamuhuri yetu ya Kenya ni wazi kwamba Kiswahili ni lugha ya taifa. Kipengele cha 7(2) kinabainisha kwamba lugha rasmi za taifa letu ni mbili; Kiswahili na Kiingereza. Utaona kwamba Kiswahili kimetangulia Kiingereza kwenye mpangilio huo. Hii inamaanisha kwamba Kiswahili kina umuhimu mkubwa nchini Kenya. Kipengele cha (7) hakikuwekwa kwenye Katiba yetu kuwa pambo bali kimewekwa kwenye Katiba kuonyesha wazi umuhimu wa Kiswahili kwa nchi yetu. Kwa hivyo kama alivyopendekeza Bi. Lay Kiswahili kitumike rasmi kwenye sheria zetu zote. Ninapendekeza Serikali ilazimishwe kutekeleza suala hili. Suala hili halikuwekwa kwenye Kipengee cha 7 bure. Kuna umuhimu wa kuzitafi sheria zote za Kenya kwa lugha ya Kiswahili. Kiswahili kimepatiwa kipa umbele kwenye jumuiya ya Afrika Mashariki pia katika Bunge la Afrika nzima ambako kinatumika rasmi. Lugha hii haikuwekwa pale kama mapambo. Inatakikana sisi tunaofahamu lugha ya Kiswahili kuwa muhimu tusukume gurudumu hili ili wengine watufuate. Lugha inatakikana iwawezeshe watu kuelewana. Lugha hutumika kuelimisha watu. Kwa hivyo tutumie Kiswahili kuwaeleza wananchi masuala yanayowahusu. Mara nyingi watu wengi huwa na uoga wa kuzungumza lugha hii ya Kiswahili wakifikiria kuwa kuna yule ambaye labda ana ujuzi kushinda mwingine. Nafikiria lugha huwa inazidi kukuzwa kama watu wataitumia. Ukienda Rwanda utakuta kuwa Kiswahili kinatumika kila mahali kwa sababu pia wao wameamua kuwa Kiswahili ni lugha yao ya taifa. Kama Rwanda ambayo ni nchi ilikuwa na matatizo inatumia lugha hii sembuse sisi Wakenya ambao tulianzisha suala hili kitambo?
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii kuchangia Hotuba ya Mheshimiwa Mtukufu Rais wa Jamhuri ya Kenya. Kwanza lazima nishukuru Maulana. Pili niangazie yale aliyoyazungumzia ikiwa mojawapo ni lile suala la kusalimiana ambalo limewezesha nchi hii kama wenzangu walionitangulia walivyosema kuwa na ai na mioyo kutulia. Lakini mikono hiyo isiwe tu ni ya watu wawili kwa sababu ukweli ni kwamba tukienda nyanjani hasa kwetu sisi wanasiasa. Leo tulikuwa na mkutano na Mhe. Naibu Rais kule Kwale na tumeona bado wale walioko chini hawajakubali kwamba watu wanaweza kufanya kazi pamoja ama wanaweza kuwa na maono pamoja na wakasaidia watu kwa kauli moja. Jambo lingine ambalo ningetaka kuchangia ni suala la viwanda. Ukweli ni kwamba nchi hii haitaweza kuendelea ikiwa viwanda havitanawiri. Kule kwetu Kaunti ya Kwale kwa saa hii ndiko kuna madini ambayo yanachimbuliwa kwa wingi zaidi nchi nzima. Lakini la kushangaza ni kwamba katika karne hii bado tunachimbua yale madini na kuyapeleka Ulaya bila kuyafanyia kazi hapa. Hii inamaanisha faida kubwa haitufaidi sisi hapa nchini. Inamaanisha pia kazi ambazo zingetokea na kusaidia vijana wetu bado tunazipeleka Ulaya. Kwa hivyo kuhusu viwanda ni lazima kuwe na mikakati maalum ya kuhakikisha kwamba sio tu kusema tutakuwa na viwanda wakati rasilmali zetu na mali ghafi bado tunapeleka katika nchi nyingine. Tuhakikishe usafishaji wa mali unafanyiwa hapa ili kuongeza faida na vijana wetu kupata ajira. Jambo lingine ambalo pia ni la msingi kwa viwanda ni bei ya kawi ilivyo hivi sasa. Ukweli ni kwamba katika nchi zote za Afrika Mashariki na Kati Kenya ndiyo ina bei ya juu zaidi ya umeme. Huwezi kuzungumzia viwanda bila kugusia umeme. Ni jukumu la Serikali na washikadau wote kuona kwamba kiwango cha bei ya umeme kimeregeshwa chini ikiwa ni kweli viwanda vinatakikana vinawiri. Mwisho ni suala ambalo kila kiongozi analizungumzia ufisadi. Ukweli ni kwamba tuna tatizo. Mojawapo ya shida zetu ni mishahara ambayo wafanyajikazi wa Serikali wanapatiwa. Niliona tangazo wiki iliyopita kuhusu kazi fulani ya Serikali. Mtu anatakikana awe na shahada ya kwanza ama ya pili lakini mshahara wake wa kuanza kazi ni Ksh30000. Ukweli usemewe. Je mtu kama huyo ukimlipa Ksh30000 unatarajia achunge mabilioni ya pesa? Hakika humtarajii atakuwa na maadili mema. Huwezi kumpatia fisi ambaye ana njaa nyama aibebe eti kwa sababu labda ni mcha Mungu ama umemwombea. Kwa hivyo tukitaka kupambana na ufisadi ni lazima pia Serikali iwapatie wafanyakazi hasa wale ambao wamesomea taaluma mbalimbali mishahara ambayo itawasaidia. Kwa hayo machache nakushukuru Mhe. Naibu Spika wa Muda. Pia natoa pongezi kwa Rais wetu kwa Hotuba yake aliyoitoa hivi karibuni.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ya kuzungumzia likizo hii tuliyopatiwa. Tumetoka hivi juzi kwenye kinyaganyiro cha uchaguzi na bado uchaguzi wa urais upo ambao utaendelea tarehe 26 mwezi ujao. La muhimu ni kwamba tunatakiwa kuzungumzia ai. Twende makwetu kujulisha wananchi umuhimu wa kupiga kampeni bila kupigana wala kugombana. Watu watofautiane kisera lakini sio kwa ngumi. Kuna umuhimu sote twende tukazungumze na wananchi tuwaeleze yaliyojiri na yatakayotufikisha wakati wa uchaguzi. Vile vile kwa wenzetu ambao wamechaguliwa kwa mara ya kwanza watumie fursa hii kuwaeleza wananchi waliowachagua mipangilio yao haswa. Mimi ninaona tutakuwa katika pilkapilka za kutafuta ni nani atakayeshikilia Serikali yetu ya Kenya. Ningependa tu kuwajulisha wenzangu katika Bunge hili la Kumi na Mbili kwamba tumekuja hapa kwa sababu tumetumwa na wale waliotuchagua. Hilo ni jukumu na nafasi kubwa sana. Tusisahau kuwa wengi tuliowashinda wangali wana uwezo wa kuja hapa na kupigania yaliyotuleta hapa. Lakini la muhimu ni kukumbuka lililotuleta hapa. Tunapoelekea kwenya kinyaganyiro kijacho tukumbuke kuwa Kenya ni muhimu kutuliko sisi sote. Kwa hiyo tudumishe ai. Tusiwapiganishe wananchi kwa misingi ya kisiasa ama kwa misingi ya kikabila ila tuwaunganishe. Naunga mkono hii Hoja. Ahsante sana.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza ningependa kumshukuru dada yangu mhe. Millie Odhiambo kwa kutuletea Mswada huu ambao unazungumzia maswala nyeti na muhimu sana yakusaidia waathiriwa katika jamii yetu. Mswada huu unasema kwamba waathiriwa watatoa habari ambazo zitawasaidia ili wapate huduma na fidia kutoka kwa wale ambao wamewaathiri. Sura ya Pili Aya ya Tatu inazungumzia mambo yamaridhiano katika kesi fulani na pia katika kuleta ai. Tukiangalia katika nchi ya Rwanda tunaona kwamba kitambo walikuwa na vita vya kikabila lakini kwasababu ya maridhiano baina ya zile jamii mbili tunaona hii nchi ikiwa na ai na umoja. Kwa hivyo Mswada huu utaangalia mambo ya maridhiano kwa sababu kesi nyingine huwa ni kesi ambazo mwathiriwa na mwathiri wanapowekwa pamoja na jamii na familia huwa kunapatikana ai ya kudumu na haki itakayowaridhisha wote wawili. Pia Mswada huu unazungumzia ushirikiano baina ya vitengo vya Serikali vinavyoangalia mambo ya waathiriwa kutokana na majanga ya uhalifu. Kwa mfano kuna kitengo cha polisi na kitengo cha mahakama. Mara nyingi watoto wetu ambao wameathiriwa kwa sababu ya kubakwa ama kwa kufanyiwa mambo machafu na mabaya kama vile ya ngono huwa wanakosa kupata haki kwasababu vitengo hivi havina ushirikiano dhabiti. Unapata polisi katika uchunguzi wao na ushahidi unakuwa na utata na mahakama inapata ripoti ambayo haitaweza kumsaidia mtoto yule. Lakini wakati vitengo hivi vitakuwa na ushirikiano dhabiti basi mtoto huyu atapata haki yake na anapopata haki basi hata sisi Wakenya tunatoa shukrani sana. Vile vile Mswada huu umezungumzia maadili ambayo yako katika Katiba yetu. Mswada huu unasema kwamba waathiriwa wasibaguliwe kwa misingi ya kikabila kijinsia dini au umri. Hivyo basi tunasema Mswada huu umezingatia Katiba yetu ambayo inatupatia haki nasisi Wakenya tunasema "haki iwe ngao na msingi wetu". Sisi kama viongozi tunaiomba Serikali izingatie mambo yaliyozungumziwa katika Mswada huu kwa mfano mambo yamaridhiano. Kwa hivyo ripoti ya TJRC ambayo inaongea juu ya ukweli haki na maridhiano inafaa itekelezwe ili tusiwe na matukio ya vita vya kijamii kama vile vilitokea kule kwetu Pwani Kaya Bombo na Molo. Mambo haya hutokea kwasababu hatuna miundomisingi au mikakati ambayo inaweza kuzuia mambo kama haya kuweza kutokea tena. Ninaunga mkono huu Mswada kwa kusema tutakuwa na hazina itakayoitwa "Victim Protection Trust Fund". Hazina hii pia itaweza kumsaidia yule mwathiri aweze kupata huduma zitakazo mwezesha kupata haki. Nikiangalia katika Mswada huu ninaona kwamba huduma zimezungumziwa kwa utaratibu unaofaa. Hakika tukifuata mtiririko wa huduma hizi basi haki itakuwa ngao na msingi wetu kama Wakenya. Mhe. Naibu Spika wa Muda jambo lingine ambalo ninaunga mkono na ninatoa kongole sana kwa mhe. Millie linahusu kuweka mtoto katika hali ya usalama wakati ameathirika. Tumeona mifano katika nchi yetu. Unapata baba wa kambo anambaka mtoto wa mkewe. Wakati anatenda kitendo hiki anaenda mahakai anapewa bond na anatoka nje. Akiwa nje na akina mama ni sisi wengine tunawapenda waume wetu unaona kwamba huwezi kuwa kando na mme wako. Unaendelea kuishi na mme wako na mtoto huyu anapolegeshwa katika familia kuishi na mama na baba wakambo aliyembaka hawezi kupata haki. Huyo mtoto ataendelea kuathiriwa zaidi na mambo mengine. Basi ikiwa tutawapeleka katika taasisi za usalama ambapo watawekwa sawa wapate chakula makao na matibabu basi watoto hao watajua haki zao zitapatikana katika njia ambayo inahitajika. Pia Sura ya Nne Aya 13 inazungumzia wale ambao ni walemavu katika kupata haki zao. Inasema kuwa miundomisingi lazima iwawezeshe walemavu ambao wameathiriwa kupata haki yao. Tunaona katika mahakama zetu mwathiriwa ambaye ni mlemavu anashindwa kufika katika kizimbani ama kuingia katika mahakama na hii ni kwasababu ya vile imejengwa miundo misingi yake haikuzingatiwa. Pia kuna mambo mengi sana ya wale watu ambao wana ulemavu. Uhalifu unaofanyiwa mtu aliye sawa kimaumbile na ule unaofanyiwa mtu ambaye ni mlemavu ni tofauti. Ninaona Mswada huu pia umewazingatia hao ndugu zetu. Hivyo basi tunasema kwamba huu ni Mswada ambao lazima tuupigie debe sisi kama Wakenya na sisi kama viongozi katika Bunge hili la Kumi na Moja ili haki itendeke. Tumeona wengi wameuwawa kwa njia hii. Kwa lugha ya Kiingereza tunasema " mob justice ". Unaweza kuwa na chuki na mtu fulani unapiga nduru na kusema huyu mtu ni mwizi ama huyu mtu amefanya jambo fulani. Huyo mtu anauwawa na tunakosa haki kwa watu kama hao. Jambo la mwisho ambalo ninatoa kongole kwasababu limenifurahisha sana katika Mswada huu ni lile la kuzungumza katika lugha ambayo utaielewa ama lugha ambayo umeichagua. Tunafahamu kwamba lugha za taifa ni mbili nazo ni lugha ya Kiingereza na lugha ya Kiswahili lakini unapata watoto na akina mama wengi katika mashinani wanapenda kuzungumza katika lugha yao. Hii pengine ni lugha yake ya Kikuyu Kidigo au Kiluhya ili aweze kuzungumzia yale mambo ambayo yamemvika yeye kama Mkenya. Hivyo basi kukiwa na mkalii tunaweza kusikia yaliyojili katika mikasa kama hiyo. Mhe. Naibu Spika wa Muda ninashukuru sana na ninaunga mkono Mswada huu. Ninatoa kongole kwa mhe. Millie.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Nimesimama kuunga mkono Hoja ambayo imeletwa na ndugu yangu Ali ambaye anatoka eneo la Pwani. Hospitali ya rufaa ya kiwango cha sita huko Pwani imechelewa kufika. Mimi ningependa kuongea kwasababu hospitali hii ya Mombasa iwekwe kama hospitali ya rufaa. Kwanza kuna magonjwa mengi hapa duniani ambayo huathiri watu wanaoishi Pwani. Ni magonjwa ambayo hayawezi kufanyiwa utafiti katika maeneo mengine. Matibabu yake yanafanyika vizuri yakifanyiwa pale Pwani. Saa hii pale Mombasa kuna ugonjwa wa Chikungunya ambao unaathiri wapwani peke yao. Kuna magonjwa mengine kama vile tende guu ambayo yako katika eneo la Pwani peke yake na matibabu yake hayawezi kupatikana mahali pengine popote humu nchini. Kwa hivyo kama tunataka kuwasaidia watu wa Pwani na kuhakikisha kwamba wamepata haki yao ya kikatiba kulingana na Kipengee 43 cha Katiba ni haki kwamba hospitali ya Mombasa ifanywe hospitali ya rufaa. Pili hospitali ya Mombasa imekuwa pale muda mrefu kabla hospitali nyingine hazijajengwa humu mchini. Pengine Hospitali Kuu ya Kenyatta peke yake ndiyo inatoshana na hospitali ya Mombasa ki-umri. Hospitali ile imesahaulika licha ya kwamba ni hospitali ambayo wakati wa ukoloni na baada ya kupata Uhuru ilitiliwa maanani sana. Hospitali hiyo ilikuwa ikopewa kila kitu lakini ikafika wakati ikaachiliwa. Sasa tuko na wakati mwafaka kwa sababu ya kile ndugu yangu Sankok alichokitaja kuwa handshake. Sasa tunataka ile handshake pia ifike kule Pwani ili tuone matunda yake.Tunataka ile hospitali ya Mombasa iwe tunda la kwanza la ile handshake. Sisi Wapwani tutafurahi. Pengine ningefanya ukarabati wa hii Hoja kusema kwamba haya mambo yawekwe katika Bajeti ya mwaka huu wa kifedha ili tuhakikishe kwamba hospitali ya rufaa ya Mombasa inatimilika. Tatu hospitali ile inasaidia kaunti karibu nane za Kibwezi Lamu Tana River Taita Taveta Kilifi na maeneo mengine. Watu wote huteremka Mombasa kutafuta matibabu. Zaidi ya watu milioni kumi nchini huenda kwenye hospitali ile kutafuta matibabu lakini ukiangalia ambulensi ambazo zinaenda Mombasa zote huelekea kwenye hospitali za kibinafsi ambazo zina gharama kubwa kwa watu wetu. Jambo lingine ambalo ningependa kusema ni kwamba kuna ugonjwa wa saratani ambao umekithiri zaidi Mombasa na sehemu ya Pwani kwa jumla kwa sababu ya madini mazito ama heavy metals yanayopatikana katika eneo lile. Utafiti unaonyesha kwamba watu wengi katika Kaunti yaKwale wameathirika kutokana na ugonjwa wa saratani. Katika kaunti ya Kilifi kwa sababu ya kuweko kwa madini mazito aina ya iron ore na titanium ambayo yako na carbon wakazi wanaathirika kutokana na ugonjwa wa saratani kwa urahisi kuliko wakazi katika sehemu zingine za Kenya. Kwa sababu hiyo na kwa sababu ya uchafuzi wa hewa unaofanyika Mombasa tunahitaji usaidizi wa haraka ili hospitali ya Mombasa iweze kupandishwa cheo na kuwa hospitali ya rufaa. Nikimalizia kwa sasa kuna utafiti ambao unafanywa. Pale kwetu kilifi kuna kitengo kinaitwa Kenya Medical Research Institute (KEMRI) ambacho kinafanya utafiti wa tropical diseases. Ule utafiti kwa sasa umeonyesha kuwa watu wengi wa Pwani wanaathirika na tropical diseases ambazo matibabu yake hayapatikani humu nchini. Tukifanya hospitali ya Mombasa kuwa ya rufaa na kuweka vyombo ambavyo vitatuwezesha kupata matibabu ya magonjwa hayo itakuwa tumefanya jambo la busara. Kwa sasa kuna vyuo vikuu viwili kule Pwani ambavyo vinajaribu kutoa mafunzo ya udaktari - Chuo Kikuu cha Pwani kilichoko pale Kilifi na Chuo Kikuu Cha Teknolojia cha Mombasa. Hivyo vyuo vimeshindwa kutoa mafunzo ya matibabu kwa sababu hakuna hospitali ya rufaa na mafunzo. Kama tunataka kuvikuza vyuo hivyo ili viwe taasisi za elimu zinazoheshimika ni lazima tuhakikishe kwamba mafunzo ya udaktari hayapatikani Nairobi peke yake bali yanapatikana katika vyuo hivyo pia. Kwa hivyo tuna wajibu wa kuhakikisha kwa haraka sana kwamba hospitali ya Mombasa imefanywa hospitali ya rufaa na mafunzo kama hospitali za Edoret na Kenyatta. Ni matumaini yangu makubwa kwamba Hoja hii itatiliwa maanani na Serikali. Kabla sijasahau miongoni mwa maono ne makubwa ambayo Rais Uhuru Kenyatta ametangaza ni matibabu bora kwa kila Mkenya. Ndiyo tuweze kuyafikia malengo hayo inatubidi sisi Wakenya na Serikali kuhakikisha kwamba hospitali za rufaa pia zimepewa kipaumbele. Rais hawezi kutimiliza ile ndoto ya universal healthcare ambayo iko kwa ile Big Four Agenda yake; hawezi kuafikisha haya maono yake kama ile hopitali ya Mombasa itabakia vile na zile hospitali ndogo ndogo pia zitabakia vile. Ni matumaini yangu hospitali ya Mombasa ikukuzwa kuwa ya rufaa zile hospitali ndogo ndogo katika Mkoa wa Pwani zitafanya mabadiliko makubwa katika kuhakikisha kwamba watu wa Pwani na Kenya wanapata matibabu yanayofaa ambayo Serikali inatumainia kuyapata.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi name nichangie Hoja hii inaopendekeza kuwekwa kwa kamera katika shule za upili. Naona kuweka kamera hizo ni jambo la muhimu sana. Zitasaidia sana kuzuia uhalifu tofauti tofauti katika shule.Itasaidia kaunti pia. Kwa mfano itasaidia Lamu katika wadi ya Basuba. Najua hata wakiniona nachangia mambo ya kamera wanashangaa sana. Wadi ya Basuba haina hata shule moja ya upili. Mtu akizungumzia mambo ya kamera nashangaa sana kwa sababu kule Basuba hatuna hata walimu katika shule za msingi. Shule tano zimefungwa. Wanafunzi wanaenda kusoma huko Hindiwood. Nasisitiza kuwa kamati ya elimu iliangalie suala hili zaidi. Inasikitisha kwamba watu wanazungumzia mambo ya kwenda mbele ilhali wengine wanazungumzia kamera na mambo mengine. Mahali kama Kiangwi Milii Basuba na kwingineko shule zote zimefungwa na hatujui walimu watarudishwa lini. Ni lazima waangalie suala hili kwa kina. Tunaambia Wakenya eti ni sawa lakini bado hatujajua ni sawa kivipi. Bado watu wa wadi ya Basuba wanaona haijakuwa sawa. Sitaki kuchaingia zaidi. Nangojea Mswada wa Korosho. Naona wakati umeisha. Twende kwa Mswada mwingine. Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Ahsante sana mhe. Naibu Spika wa Muda kwa nafasi hii. Naunga mkono hoja hii inayohusu masuala ya usalama. Ni jambo la huzuni kuona mambo yaliyofanyika huko Bungoma. Vile vile ni jambo la aibu kuona kwamba sisi Wakenya tunauana wenyewe. Haifai hata kidogo. Inatupasa kuangalia hili jambo kwa njia nyingi. Tusilaumiane. Sisi kama Wabunge sharti tuangalie jambo hili kwa makini. Rais alisema kwamba atahakikisha kwamba kuna askari mmoja kwa raia 450. Nisingesema tunamlaumu Rais wetu kwa sababu kuna mpangilio wa mambo. Ukisema utaoa si kwamba utamaliza kufanya mambo yote. Huwa kuna utaratibu. Kusema kwamba askari wataajiriwa lazima pawepo na bajeti ambayo italetwa hapa. Tunaingojea kwa hamu sana ili tupitishe jambo hilo la fedha ndiposa tutimize lengo la Rais wetu. Hata kama tunalaumu Serikali sisi Wabunge tunalo jukumu kubwa sana kuhusu usalama wa maeneo bunge yetu. Katika eneo langu la Bahati pakitokea jambo sharti niwe mstari wa mbele kuita Mkuu wa Wilaya na maafisa wakuu wa usalama. Tunao huo uwezo.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Hata mimi nilikuwa hapa kitambo sana dada yangu Mhe. Fatuma. Kwanza nataka kumshukuru Mhe. Wanga kwa kuleta Hoja hii ambayo ni muhimu sana kwa nchi yetu ya Kenya. Maradhi ya saratani ni sugu sana. Ni maradhi ambayo yamechukuwa maisha ya Wakenya wetu wengi hasa akina mama kupitia saratani ya matiti na ya kizazi. Pia kwa wanaume saratani ya kibofu imekuwa mbaya sana na imewapoteza akina baba wetu. Pia vile vile watoto wetu wengi wameweza kuangamia na kupoteza maisha yao kupitia saratani ya damu. Tatizo hili la maradhi haya limekuwa kwa sababu nchi yetu bado haijaweza kuwa na taasisi ama zahanati zinazoweza kupigana na maradhi hayo na kuweza kukimu wakenya wengi ambao wamepata hayo matatizo. Inabidi Wakenya wengi wasafiri kutoka sehemu mbali mbali za Kenya kwenda kwa hospitali yetu kuu ya Kenyatta ili waweze kupata matibabu na zile huduma ambazo zinafanyiwa wagonjwa walio na saratani sampuli tofauti tofauti. Kuyatambua maradhi ya saratani imekuwa tatizo sugu kwa sababu madaktari wengi hawana taaluma ya kuyatatua. Hivyo basi wagonwa wengi wanaotembea kwa hospitali ama zahanati zetu wanakumbana na utata. Kwa mfano kwa akina mama saratani ya matiti mwanamke anaweza kupata jipu au uvimbe mdogo. Mara nyingi anapokwenda kwenye hospitali zetu za kawaida anaambiwa pengine in jipu au uvimbe wa kawaida. Baadaye muda mchache inapatikana ya kwamba ilikuwa ni saratani wakati ambapo imeshaenea na kumletea madhara makubwa sana. Nataka nitoe mapendekezo machache ambayo yanaweza kutusaidia sisi kama Wakenya kupigana na janga hili la maradhi ya saratani. Kwanza kabisa lazima Serikani ishirikiane na mashirika yasio ya kiserikali ambayo yanapigana na maradhi ya saratani. Kwa mfano kuna hili shirika la wagonjwa mahututi la Hospitali ya Pwani. Shirika hilo linawachukua wagonjwa takribani 2000 kila mwaka ambao wana matatizo ya saratani. Matatizo ya saratani si tiba peke yake. Wagonjwa wa saratani lazima wapate ushauri na huduma zingine ambazo ni tiba-kemikali na tiba-redio; chemotheraphy and radiotherapy . Ikiwa Serikali ingeweza kusambasa huduma kama hizo kwa hospitali za kaunti pale mashinani basi hata wagonjwa hao wangeweza kupata afueni. Itakuwa vizuri kuliko kuwalazimu kusafiri hadi Hospitali ya Kenyatta ama kufanya Harambee kuchangisha fedha nyingi ili kwenda nchi za nje kutibu maradhi hayo. Maradhi kama hayo pia yanasababishwa na ndoa za haraka. Wasichana wetu wanapoozwa wakiwa bado mili yao haijakuwa tayari kuweza kuzaa ama kufanya ngono na wanaume pia huleta matatizo kama hayo ya saratani ya kizazi. Hivyo basi sisi kama viongozi pia lazima tuzungumzie swala la ndoa za haraka ili watoto wetu waweze kuiva na kuwa na uwezo wa kuolewa na kuzaa bila matatizo. Vile vile pia mambo ya ubakaji na kunajisi watoto wadogo pia inasababisha saratani ya kizazi. Hivyo basi swala hili pia lazima tuliangalie sisi kama viongozi ili tulitatue. Maradhi ya saratani lazima yachukuliwe kama ya Ukimwi. Hayo maradhi yamekuwa ni janga na Serikali imeweza kuweka bajeti ya kitaifa kushughulikia watu ambao wana matatizo ya Ukimwi. Hivyo basi wanaweza kupata madawa bure na wauguzi ambao
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Hata mimi pia ningependa nizungumzie suala hili la ukuzaji wa sukari. Kila sehemu katika Jamhuri ya Kenya iko na uti wa mgongo wa uchumi wake. Hakika kwa watu wa Magharibi na Nyanza sukari imekuwa uti wa mgongo katika uchumi wao. Suala hili la sukari ni suala nyeti kwa sababu viwanda hivyo vya sukari vilikuwa vimeajiri zaidi ya watu 40000. Pia vilikuwa vinafaidisha watu zaidi ya laki moja ambao ni wakulima wa miwa na hivyo basi kuweza kufaidisha zaidi ya watu milioni mbili katika taifa letu la Kenya. Ni masikitiko makubwa ya kwamba viwanda hivi vyote vilikufa na hivyo basi tukapoteza ajira na maisha kwa Wakenya wenzetu. Hivi sasa Rais wetu amezungumzia ajenda zake nne. Katika ajenda moja amezungumzia mambo ya viwanda. Basi iwapo ako na ajenda kama hio ni wazi kabisa Ripoti kama hii itekelezwe ili tufufue viwanda hivi. Tumeona ya kwamba changamoto nyingi zilikuwa katika sera. Kumekuwa na sera duni ambazo zimesumbua sana wakulima wetu kuendelea na kilimo kwa njia ilio sawa. Vile vile kumekuwa na ushindani. Wakulima wetu hawana uwezo wa kushindana na wakulima kutoka nchi za nje katika biashara ya sukari. Vile vile soko ilikuwa changamoto kwa sababu nchi yetu iligeuka ikawa ni sehemu ya kutupia sukari kutoka nchi za nje. Sukari ile inahujumu juhudi za wakulima wetu na kufanya sukari inayokuzwa na wakulima wetu kukosa soko hata hapa kwetu Kenya mbali na zile nchi zingine za nje. Kwa hivyo jambo kama hilo kama tunataka kuenda mbele kama taifa la Kenya lazima tulizingatie sana. Vile vile tunafaa kujenga taaluma zaidi kwa wakulima wetu katika ukuzaji wa sukari. Hivi sasa tuna lengo na madhumuni ya kufufua viwanda kama hivi. Hilo litakuwa suala muhimu sana. Vile vile lazima kuwe na fedha na hazina maalum kwa sababu hivi ni viwanda vilivyokuwa vizuri na vimeboresha maisha ya Wakenya na kuboresha uchumi wa taifa la Kenya. Hivyo basi katika harakati za kuvifufua lazima kuwe na hazina maalum ambayo itahakikisha ya kwamba Ripoti hii na yale ambayo sisi tumeyapendekeza yanatekelezwa bila taswishi yoyote. Suala lingine ni kuwa wafanyakazi walikosa mishahara. Swali ni: Je mishahara ilikosekana kwa nini? Katika Ripoti tunaona kuna ufisadi ambao ulikithiri kwa kiwango ambacho hata wakulima walishindwa kupata mapato yao. Hata wafanyakazi walishindwa kupata mishahara yao. Hayo yalihujumu ukuzaji wa miwa na kuhujumu viwanda vyetu vilivyokuwa wakati ule. Jambo lingine ambalo nataka kuzungumzia ni utekelezaji wa sheria. Yale ambayo kama Bunge la Taifa tumezungumzia lazima tuyachukulie kwa upeo wa juu sana. Tusiwe tu tutazungumza kisha ripoti inawekwa kando bila utekelezaji. Sasa ni wakati wa Bunge kuhesabika katika kufufua ukuzaji wa viwanda vya sukari. Leo tunaona katika miji yetu watu wengi wamejaa; kumekuwa na msongao kwa sababu kule nyanjani kule mashambani hakuna ajira yoyote wala viwanda vyovyote. Wakenya wote wanakimbilia mijini. Kwa hivyo iwapo tunataka kukabiliana na mambo kama hayo lazima kuwe na viwanda mashinani na viboreshwe kwa hali ya juu kwa tekinolojia.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Hoja ambayo iko mbele yetu ni muhimu. Nashukuru Mhe. Chris Wamalwa kwa kuileta. Ombi langu ni moja. Kwa sababu kila Mbunge anayesimama anaongea kuhusu shida zilizoko katika sehemu yake wa Uwakilishi Bungeni ni kama hii shida iko kila mahali. Sijasikia mtu akisema ya kwamba kuna watu ambao wako maeneo ya Bunge ya mijini ambao wanaambiwa waende kwao wakachukue
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ingawa nilikuwa nimebonyeza kwa ile ya makavazi ya hayati Mzee Jomo Kenyatta nitaendelea na hii pia ambayo imenifikia sasa. Ni vyema sana tupeleke viongozi wa dini katika shule zetu kwa sababu kulingana na hali ilivyo sasa wanafunzi wanakua bila ii ya dini kwa sababu muda mwingi wanautumia wakiwa shule. Ni vigumu kwao kwenda katika madrassa au sehemu ambazo watafundishwa Biblia. Ni vyema sana viongozi wa dini zote wapelekwe katika shule. Wenye ii ya Kiislamu wapelekewe walimu wa Kiislamu kama maimamu ama masheikh. Wenye ii ya Kihindu na ya Kikristu pia wepelekewe walimu wao ili watoto wetu wakue katika mazingira ya dini kupendana na huruma. Huo ndio wakati pekee ambapo mtoto akiwa shuleni aone dini imewekwa katika somo atachukua na uzito. Kulingana na mazingira yaliyoko sasa mitaani ni vyema sana watoto wetu wapate mafunzo ya kidini. Wanafunzi wakue katika maadili ya kidini kuanzia shule za chekechea shule za msingi na zile za sekondari. Ikiwezekena wakati mitihani inapotungwa wawekewe maswali hayo ili wakifanya mtihani waone umuhimu wake. Kila siku kabla hawajaingia madarasani wawekwe katika sehemu za ii zao ili wafundishwe hali halisi jinsi dini inavyosema aina ya upendo na jinsi ya kuishi pamoja ili wakue katika mazingira hayo na tubadilishe taifa letu. Taifa letu sasa limebadilika. Watu wanagawanyika kikabila na kidini. Wanahitaji neno la Mungu na kuelezewa hali zilivyo ili watoto wetu wainukie katika mazingira mazuri. Nilikuwa nimebonyeza kuhuzu suala la makavazi ya hayati Jomo Kenyatta. Itabidi nipenyeze neno moja ambalo halikuzungumziwa hapa. Katika makavazi hayo kuwekwe taratibu za watu watakaoenda pale wasiwe wataenda kumuomba kwamba awasaidie. Itakuwa kinyume na ii. Iwekwe sehemu ambayo watu wataomba Mungu kwa sababu hata tukiwaruhusu watalii waingie kikubwa ambacho marehemu aliyetangulia mbele zake anahitaji ni maombi. Kwa hivyo kuwe na sehemu ya maombi ambapo watu watakuwa wanamuombea. Kwa hayo mengi ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kabla sijaendelea ningependa kuwafahamisha kwamba sisi ndio tunatengeneza Bajeti na sisi tuko katika Serikali ya kitaifa. Ni jambo la kusitikisha kwamba walio katika serikali za majimbo wanaweza kuangalia watu wao huko ilhali ni sisi ndio tunaowagawanyia pesa. Sisi tunaowagawanyia pesa watu wetu ambao wako katika Serikali ya kitaifa ambao ni wazee wa vijiji wanapata matatizo na shida nyingi mno. Hili ni jambo ambalo sisi wenyewe tungeliangazia kwanza kabla hatujaangalia serikali za majimbo. Ukweli ni kwamba wazee wa vijiji wanaojulikana kama village elders wanafanya kazi ngumu mno na wanaifanya katika umri wowote bila kupoteza hata dakika moja. Mwenyekiti wa kijiji anaanza kazi kutoka asubuhi hadi kesho asubuhi. Akiishi miaka 60 basi atakua amefanya kazi hiyo kwa takriban miaka 60 ilhali watu wengine ambao wanafanya kazi masaa ane kwa siku wanapata mishahara minono. Nataka kuwaunga mkono wale wenzangu ambao wamesema kwamba wazee wa vijiji ndio wazee ambao wanaweza kuleta shida katika usalama na ni wao tu ndio wanaoweza kuleta nafuu kubwa katika usalama. Kila kitu kinamwangalia yeye. Ikiwa kila kitu kinamwangalia kule kwetu wengi sana wamepigwa risasi wakionekana kwamba wanatoa i za watu ni watu ambao wamepata matatizo makubwa. Wanachukiana na watu kwa sababu ya kufanya kazi nzuri kwa Serikali. Lakini Serikali imewaacha nyuma. Hawajui la kufanya. Kwa hivyo ni wajibu wetu sisi hapa tupitishe waweze kupata mshahara na sio mambo ya kupata eti kiinua mgongo baada ya mwaka. Hapana! Tunataka wazee wa vijiji waangaliwe mapema wapate mishahara minono. Ikiwa haiwezekani basi Wabunge wajitolee kutoa mishahara ili wazee wa vijiji waweze kufaidika pia. Leo hii imekuwa vigumu wakati mwingine kwenda kukutana na wazee wa vijiji kwa sababu ukifika pale kwa sababu ya kukosa mshahara na unataka wafanye kazi fulani ambayo itakusaidia wewe katika kampeni zako wanasema kwamba wao wana njaa. Sasa inatubidi sisi Wabunge tutoe pesa kutoka mifuko yetu ili tuwapatie mapeni ya kujisitiri ilhali kazi wanayoifanya ni ya Serikali. Serikali hii yetu ninajua kwamba ina uwezo wa kuwalipa wazee wote wa vijiji ndani ya taifa hili. Ikiwa wanaweza kulipa wazee kwa mwezi Kshs2000 au kitu kama hicho sioni sababu yoyote wasiweze kuwalipa. Wao ndio walio juu ya wale wazee ambao wamekaa majumbani na wanalipwa kila mwezi. Ninakumbuka Mhe. Mwadime hapa akisema kwamba yeyote atakayekataa Hoja hii achukuliwe hatua. Watu wamecheka na kuona kwamba labda anazungumza utani. Mimi ninarudia kwamba yeyote ambaye hataki kuunga mkono Hoja hii ni adui wa maendeleo na ukweli anastahili kuchukuliwa hatua ya kufaa. Mwaura awe mfano mzuri wa kuchukuliwa hatua hiyo. Kwa hayo machache ninataka kukushukuru kwa kunipatia wakati huu japo wengine waliokuja nyuma wamepewa mapema kuliko mimi. Asante.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kabla sijazungumzia kalenda ya Bunge ningependa kuchangia Hoja iliyokuwa ikizungumziwa hapo awali kuhusu Kenya na ukenya ndani yetu. Naweza kuwa mchanga au mdogo katika Bunge hili kisiasa lakini jana nilipokuwa nimeketi na kujituliza nilisikiliza Hoja za Wabunge mbalimbali wakijadili masuala ya taifa hili. Kutathmini tu kwa ufupi niliona kwamba katika Bunge hili hapo jana mada ilikuwa ni Raila-Uhuru NASA-Jubilee na tutunge sheria-tusitunge sheria. Watu wengi pia walijaribu kuzungumzia mifano mbalimbali na kufanya nchi mbalimbali kama mifano ikiwemo Ujerii huku wakilitaka taifa hili lisonge mbele kisheria ambayo labda sheria yenyewe imependekezwa na vile mtu binafsi anavyoiona. Kwa ufupi mimi nasema kwamba iwapo hatutakuwa waangalifu kama viongozi taifa hili litakwenda katika hali mbaya sana. Mwaka wa 2007 baada ya uchaguzi nchi hii ilitumbukia katika ghasia za baada ya uchaguzi. Tunachoona sasa ni dalili ya mambo mengine mabaya kuzidi kushamiri. Waswahili wanasema kwamba mimba ya mwanaharamu huingia mara ya kwanza. Ya pili ni kusudi. Mimba ya Kenya iliingia mwaka wa 2007 wakati ambapo tuliwapoteza watu zaidi ya 1000 na jinsi ambavyo tunajadili katika Bunge hili huenda kukachangia zaidi maana watu wengi wanajadili kwa misingi ya chama kabila dini na chaguo la kiongozi wanayemtaka. Mhe. Naibu Spika nilipokuwa katika kampeni zangu nilikuwa nikiomba kura nikiwarai na kuwasihi wananchi wanilete katika Bunge hili ili tujadili taifa hili na njia sawa ya uongozi wa taifa hili but I am afraid.
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza kabisa nataka nichukue